2Nyakati 24:23 - 25 “Ikawa mwisho wa mwaka, wakakwea juu yake jeshi la Washami;
wakafika Yuda na Yerusalemu, wakawaangamiza wakuu wa watu wote miongoni mwa
watu, wakamletea mfalme wa Dameski nyara zao zote. Maana wakaja jeshi la
Washami watu haba; Bwana akatia mikononi mwao jeshi kubwa mno, kwa sababu
wamemwacha Bwana, Mungu wa baba zao. Hivyo wakamfanyia Yoashi hukumu. Hata walipoondoka
kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi,) watumishi wake mwenyewe
wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua
kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika
makaburi ya wafalme.”
Utangulizi:
Yosia alikuwa mfalme wa Yuda aliyetawala kati
ya mwaka wa 640-609 Kabla ya Kristo, jijini Yerusalem, Ni mtawala aliyeingia
madarakani akiwa kijana mdogo sana, Yeye ni mwana wa Amon Mwana wa Manase ambao
kimsingi walikuwa wafalme waovu mno katika wafalme waliowahi kutawala Israel ya
Kusini, Lakini hata hivyo Yosia alikuwa mfalme mwema sana na aliyemcha Mungu!
Yeye alitawala akiwa na miaka 8 baada ya kuuawa kwa baba yake. Mfalme huyu
alikuwa mcha Mungu na alitenda yaliyo haki mbele za Mungu!
2Wafalme 22:1-2 “Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala;
akatawala miaka thelathini na mmoja katika Yerusalemu; na jina la mama yake
aliitwa Yedida, binti Adaya wa Bozkathi. Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana,
akaenda katika njia yote ya Daudi baba yake, wala hakugeuka upande wa kuume
wala wa kushoto.”
Wakati wa utawala wake alifanya kazi kubwa
sana ikiwa ni pamoja na kuchangisha fedha za ujenzi na ukarabati wa Hekalu
nyumba ya Mungu ambayo ilikuwa na nyufa kutokana na kutokujaliwa na watu wakati
wa utawala wa babu yake na baba yake, Kuhani Hilikia aligundua vilevile kitabu
cha torati ambapo alipomsomea mfalme alirarua mavazi yake na kutubu, kisha
kuwaita watu wote wapate kuitubu na kumgeukia Mungu, walifanya agano kuwa
watamtumikia Mungu kwa mioyo yao yote kwa ujumla kulikuwa na uamshi mkubwa sana
wakati huo
2Wafalme 23:1-25
“Kisha, mfalme akatuma wajumbe, nao wakamkusanyia
wazee wote wa Yuda na wa Yerusalemu. Mfalme akapanda kwenda nyumbani kwa Bwana,
na watu wote wa Yuda, nao wote waliokaa Yerusalemu, pamoja naye, na makuhani,
na manabii, na watu wote, wadogo kwa wakubwa; akasoma masikioni mwao maneno
yote ya kitabu cha agano kilichoonekana katika nyumba ya Bwana. Mfalme
akasimama karibu na nguzo, akafanya agano mbele za Bwana, kumfuata Bwana, na
kuyashika maagizo yake, na shuhuda zake, na amri zake, kwa moyo wake wote, na
kwa roho yake yote, na kuyathibitisha maneno ya agano hilo yaliyoandikwa katika
kitabu hicho; nao watu wote wakalikubali agano lile. Kisha, mfalme akamwamuru
Hilkia, kuhani mkuu, na makuhani wa daraja ya pili, na walinzi wa mlango,
kwamba watoe katika hekalu la Bwana vyombo vyote vilivyofanywa kwa ajili ya
Baali, na kwa ajili ya Ashera, na kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni;
akavipiga moto nje ya Yerusalemu, katika mashamba ya Ridroni, akayachukua
majivu yake mpaka Betheli. Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao
wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya
miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia
waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la
mbinguni. Naye akaiondoa Ashera katika nyumba ya Bwana, nje ya Yerusalemu,
mpaka Kidroni, akaipiga moto penye kijito cha Kidroni, na kuiponda-ponda iwe
mavumbi, akayatupa mavumbi yake juu ya makaburi ya watu. Akaziangusha nyumba za
mahanithi, waliokuwamo nyumbani mwa Bwana, wanawake walipofuma mapazia ya
Ashera. Akawatoa makuhani wote katika miji ya Yuda, akapanajisi mahali pa juu,
makuhani walipokuwa wamefukiza uvumba, tangu Geba hata Beer-sheba; akapavunja
mahali pa juu pa malango, palipokuwapo penye kuingia lango la Yoshua, liwali wa
mji, palipokuwa upande wa kushoto wa mtu langoni pa mji. Walakini hao makuhani
wa mahali pa juu hawakupanda madhabahuni kwa Bwana katika Yerusalemu, bali
wakala mikate isiyo na chachu katikati ya ndugu zao. Naye akainajisi Tofethi,
iliyomo katika bonde la wana wa Hinomu, ili mtu asipitishe mwana wake au binti
yake motoni kwa Moleki. Akawaondoa farasi ambao wafalme wa Yuda waliwatoa kwa
jua, hapo pa kuingia nyumbani mwa Bwana, karibu na chumba cha Nathan-Meleki,
towashi, kilichohuwako kiungani; akayapiga moto magari ya jua. Nazo madhabahu
zilizokuwako darini juu ya chumba cha juu cha Ahazi, wafalme wa Yuda
walizozifanya, nazo madhabahu alizozifanya Manase katika behewa mbili za nyumba
ya Bwana, mfalme akazivunja, akazitelemsha huko nje, na kuyatupa mavumbi yake
katika kijito cha Kidroni. Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya Yerusalemu,
palipokuwa upande wa kuume wa mlima wa uharibifu, alipopajenga Sulemani, mfalme
wa Israeli, kwa Ashtorethi, chukizo la Wasidoni, na Kemoshi, chukizo la Moabu,
na Milkomu, chukizo la wana wa Amoni, mfalme akapanajisi. Akazivunja-vunja
nguzo, akayakata-kata maashera, akapajaza mahali pake mifupa ya watu. Tena
zaidi ya hayo, ile madhabahu iliyokuwako Betheli, na mahali pa juu alipopafanya
Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyewakosesha Israeli, madhabahu hiyo aliibomoa;
na mahali pa juu alipateketeza, akapaponda-ponda hata pakawa mavumbi,
akaiteketeza ile Ashera. Naye Yosia alipogeuka, aliyaona makaburi yale
yaliyokuwako huko, juu ya mlima; akatuma watu, akaitoa ile mifupa katika yale
makaburi, akaiteketeza juu ya madhabahu, akainajisi, sawasawa na lile neno la
Bwana, alilolinena yule mtu wa Mungu, aliyetamka mambo hayo. Kisha akasema, Ni
kumbukumbu la nani, hili ninaloliona? Na watu wa mji wakamwambia, Ni kaburi la
yule mtu wa Mungu, aliyetoka Yuda, akayanena mambo hayo uliyoyatenda wewe juu
ya madhabahu ya Betheli. Akasema, Mwacheni; mtu awaye yote asiiondoe mifupa
yake. Basi wakaiacha mifupa yake, pamoja na mifupa ya yule nabii aliyetoka
Samaria. Na nyumba zote pia za mahali pa juu palipokuwa katika miji ya Samaria,
wafalme wa Israeli walizozifanya, ili kumkasirisha Bwana, Yosia aliziondoa,
akazitenda kwa mfano wa mambo yote aliyoyatenda katika Betheli. Akawaua na
makuhani wote wa mahali pa juu waliokuwako huko, juu ya madhabahu, akateketeza
mifupa ya watu juu yake; kisha akarejea Yerusalemu. Naye mfalme akawaamuru watu
wote, akasema, Mfanyieni Bwana, Mungu wenu, pasaka, kama ilivyoandikwa katika
kitabu hiki cha agano. Hakika yake haikufanyika pasaka kama hiyo, tangu zamani
za waamuzi waliowaamua Israeli, wala katika zamani za wafalme wa Israeli, wala
za wafalme wa Yuda. Bali katika mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yosia
ilifanyika pasaka hii kwa Bwana ndani ya Yerusalemu. Tena wenye pepo wa
utambuzi, na wachawi, na vinyago, na sanamu, na machukizo yote yaliyoonekana
katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu, Yosia akayaondoa yote, ili apate
kuyathibitisha maneno ya torati yaliyoandikwa katika kile kitabu alichokiona
Hilkia kuhani ndani ya nyumba ya Bwana. Kabla ya huyo hapakuwa na mfalme mfano
wake, aliyemwelekea Bwana kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kwa
nguvu zake zote, sawasawa na sheria zote za Musa; wala baada yake hakuinuka
mmoja mfano wake yeye.”
Unaona ni wakati wa Yosia kwa kweli kulikuwa
na uamsho mkubwa sana kila kitu cha kipagani kiliharibiwa na kila aina ya
miungu iliyoabudiwa iliharibiwa, alifukuza na kuharibu wenye pepo wa utambuzi,
makhanithi na wachawi, anasifika kuwa alikuwa mfalme mwema ambaye kbla yaka na
baada yake hakuwahi kutokea!
Sababu kubwa ya
mafanikio ya Yosia
Uwezo mkubwa na uadilifu mkubwa alioupata
Yosia ulitokana na malezi mazuri na thabiti kutoka kwa kuhani mkuu maarufu sana
aliyeitwa Yehoiada kuhani huyu alikuwa mwaminifu na aliweza kutumika kwa miobgo
kadhaa chini ya wafalme wa Yuda, Kuhani huyu alioa dada wa Mfalme Ahazia, mwaka
mmoja kabla mfalme Ahazia hajauawa, Athalia mama wa mfalme alishikwa na tamaa
ya madaraka na kuamua kuua watoto wote wa kifalme na kila mtu aliyeonekana na
ushawishi wa kiutawala, baada ya adhima yake hiyo kufanikiwa alijitangaza kuwa
mtawala ona
2Wafalme 11;1-3 “Na Athalia, mama yake Ahazia, alipoona ya kuwa mwanawe
amekufa, akainuka, akawaharibu wazao wote wa kifalme. Ila Yehosheba, binti wa
mfalme Yehoramu, umbu lake Ahazia, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia, akamwiba
miongoni mwa hao wana wa mfalme waliouawa, yeye na mlezi wake, na kuwatia
katika chumba cha kulala; wakamficha usoni pa Athalia, basi kwa hiyo hakuuawa.
Alikuwako pamoja naye, amefichwa nyumbani mwa Bwana, miaka sita. Naye Athalia
akaitawala nchi.”
Yehosheba na Mumewe Yehoiada walimficha kijana
pekee aliyeponyoka katika sakata hilo ambaye ni Yosia na walimlea vizuri na
ilipotimia miaka sita yaani ya kufichwa kwake hii ikiwa na maana alifichwa
akiwa na miaka miwili sasa Yehoiada alifanya mpango wa kumtyawaza Yosiah kuwa
Mfalme wa Yuda ona
2Wafalme 11:4-17.
“Hata mwaka wa saba Yehoyada akatuma, na kuwaleta
wakuu wa mamia, wa Wakari, na wa walinzi, akawaleta kwake ndani ya nyumba ya
Bwana; akapatana nao, akawaapisha nyumbani mwa Bwana, akawaonyesha huyo mwana
wa mfalme. Akawaamuru, akasema, Hili ndilo neno mtakalolifanya; theluthi yenu,
mtakaoingia siku ya sabato, mtayalinda malinzi ya nyumba ya mfalme; na theluthi
mtakuwapo mlangoni pa Suri; na theluthi langoni nyuma ya walinzi; hivyo
mtayalinda malinzi ya nyumba, kuzuia watu wasiingie. Na sehemu mbili zenu,
yaani, wote watokao siku ya sabato, mtayalinda malinzi ya nyumba ya Bwana
kumzunguka mfalme. Mtamzunguka mfalme pande zote, kila mtu mwenye silaha zake
mkononi; naye awaye yote aingiaye ndani ya safu auawe; mkafuatane na mfalme,
akitoka na akiingia. Nao wakuu wa mamia wakafanya sawasawa na yote aliyowaamuru
Yehoyada kuhani; wakawatwaa kila mtu watu wake, hao watakaoingia sabato, nao
watakaotoka sabato, wakaja kwa Yehoyada kuhani. Naye yule kuhani akawapa wakuu
wa mamia mikuki na ngao zilizokuwa za mfalme Daudi, zilizokuwamo nyumbani mwa
Bwana. Walinzi wakasimama, kila mtu na silaha zake mkononi, kutoka pembe ya
kuume ya nyumba mpaka pembe ya kushoto ya nyumba, kando ya madhabahu na nyumba,
wakimzunguka mfalme pande zote.Ndipo akamleta nje mwana wa mfalme, akamvika
taji, na kumpa ushuhuda; wakamfanya mfalme, wakamtia mafuta; wakapiga makofi,
wakasema, mfalme na aishi. Na Athalia alipoisikia sauti ya walinzi na ya watu,
aliingia kwa watu nyumbani kwa Bwana; akatazama, na tazama, mfalme amesimama
karibu na nguzo kama ilivyokuwa desturi, nao wakuu na wapiga baragumu karibu na
mfalme; na watu wote wa nchi wakafurahi, wakapiga baragumu. Ndipo Athalia
akararua mavazi yake, akalia, Fitina! Fitina! Naye Yehoyada kuhani akawaamuru
wakuu wa mamia, majemadari wa jeshi, akawaambia, Mtoeni kati ya safu; naye ye
yote amfuataye mwueni kwa upanga. Kwani kuhani akasema, Asiuawe nyumbani mwa
Bwana. Basi wakampisha njia; akaenda kwa njia ya kuingia kwa farasi nyumbani
mwa mfalme; akauawa huko. Kisha, Yehoyada akafanya mapatano kati ya Bwana na
mfalme na watu, ili wawe watu wa Bwana; tena kati ya mfalme na watu.”
Unaona chini ya uangalizi wa Yehoiada, Mfalme
Yosia aliweza kutawala vema na kwa mapenzi ya Mungu, kumbuka kuwa ni yeye na
mkewe ndio waliomsaidia na kumuongoza na kuuondoa utawala wa malikia na
kumrudisha mfalme katika kiti cha Enzi cha baba zake kama ilivyokuwa kwa
mapenzi ya Mungu kwa Daudi, kupitia kuhani mkuu huyu inchi ikawa na amani na
watu wakamcha Mungu mno, Yosiah katika wakati wote wa kuhani mkuu aliweza
kufanya vizuri, Mfalme alikuwa na ushawishi mkubwa, aliwaongoza watu kumrudia
Bwana kila mtu aliitii sharia ya Mungu, jambo hili lilimfurahisha Mungu sana na
klilikuwa Baraka kubwa sana kwa kila mtu, maandiko yalikuwa yamepuuzwa kabisa
lakini alipokuwa mfalme Heshima ya kimaandiko ilirejea, watu wote wenye kutoa
dhabihu mbaya za watoto na kila aina ya uovu iliharibiwa kabisa kwa ujumla
alikuwa mfalme ambaye aliushawishi moyo wa Mungu na Mungu alimsikiliza ona
2Wafalme 22:19 “kwa kuwa moyo wako ulikuwa mwororo, nawe ukajinyenyekesha
mbele za Bwana, hapo ulipoyasikia maneno niliyoyanena juu ya mahali hapa, na
juu ya wenyeji wake, ya kwamba watakuwa ukiwa na laana, nawe ulizirarua nguo
zako, ukalia mbele zangu; basi, mimi nami nimekusikia wewe, asema Bwana.”
Ikawa mwisho wa
Mwaka!
Pamoja na uzuri aliokuwa nao Mfalme huyu
ambaye aliifanya kazi nzuri wakati wote wa uongozi wa kuhani mkuu Yehoiada
ambaye aliishi miaka 130 kuhani huyu mkuu aliheshimika na watu wote kutokana na
ushauri wake mzuri kwa Mfalme na watu wake alikuwa amejaa hekima ya kiungu hata
hivyo jambo la kusikitisha ni kuwa baada ya kifo chake Yosia alibadilika moyo
na kuanza kuwa na washauri wabaya ambao walirudisha tena ibada ya baali na
maashera ona
2Nyakati 24:17-20
“Hata baada ya kufa kwake Yehoyada, wakuu wa Yuda
wakamwendea mfalme, wakamsujudia. Naye mfalme akawasikiliza maneno yao.
Wakaiacha nyumba ya Bwana, Mungu wa baba zao; wakatumikia maashera na sanamu;
ghadhabu ikawajia Yuda na Yerusalemu kwa sababu ya hiyo hatia yao. Hata hivyo
akawapelekea manabii, ili kuwarudisha kwa Bwana; nao wakawashuhudia; lakini
hawakukubali kuwasikiliza.”
Mungu alipeleka manabii mbalimbali kwaajili ya
kuwaonya hata hivyo hawakukubali, wala hawakuwasikiliza, Hata hivyo Kuhani mkuu
Marehemu Yehoiada alikuwa na kijana aliyeitwa Zekaria ambaye Roho Mtakatifu
alikuja juu yake ili aweze kuwaonya, Nabii Zekaria bin Yehoiada aliwaonya kuwa
kama wanamuacha Bwana ni dhahiri kuwa Bwana naye atawaacha hata hivyo hawakutaka
kusikia maonyo na badala yake walipanga mpango wa kumuua ona Na mfalme Yoashi
alimuua zekaria akasahau wema wote ambao mama yake na baba yake walimfanyia
hili lilikuwa jambo la kusikitisha sana ona
2Nyakati 24:20-22
“Na roho ya Mungu ikamjia Zekaria, mwana wa
Yehoyada, kuhani; naye akasimama juu ya watu, akawaambia, Mungu asema hivi,
Kwani ninyi kuzihalifu amri za Bwana, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa
mmemwacha Bwana, yeye naye amewaacha ninyi. Basi, wakafanya shauri juu yake,
wakampiga kwa mawe kwa amri ya mfalme katika ua wa nyumba ya Bwana. Basi hivyo
mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake, alimfanyia, bali
alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, Bwana na ayaangalie haya, akayatakie
kisasi.”
Wakati Zeakaria anauawa alikumbuka wazi mema
yote ambayo baba yake alimfanyia mfalme Yosia ni ukweli usiopingika kuwa Yosia
alikuwa mtu asiye na shukurani hakulipa mema na badala yake alilipa mabaya
Zekaria alimuomba Bwana wakati anauawa akasema BWANA AYAANGALIE HAYA
AKAYATAKIE KISASI, ni ukweli usiopingika kuwa Mungu wetu hujilipia kisasi
wakati watu wanapokutendea yasiyopaswa wewe uwe na uvumilivu tu kwa dhambi hii
aliyoifanya Yosia ukweli haikuchukua muda tangu wakati ule iluipofika mwisho wa
Mwaka Bwana akajilipizia kisasi ndio maana tunasoma IKAWA MWISHO WA MWAKA ona
2Nyakati 24:23-25.
“Ikawa mwisho wa mwaka, wakakwea juu yake jeshi la
Washami; wakafika Yuda na Yerusalemu, wakawaangamiza wakuu wa watu wote
miongoni mwa watu, wakamletea mfalme wa Dameski nyara zao zote. Maana wakaja
jeshi la Washami watu haba; Bwana akatia mikononi mwao jeshi kubwa mno, kwa
sababu wamemwacha Bwana, Mungu wa baba zao. Hivyo wakamfanyia Yoashi hukumu.
Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi,) watumishi
wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani,
wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika
katika makaburi ya wafalme.”
Hitimisho
Inawezekana wako watu umewawaidia lakini
wamekugeuka, inawezekana umedhulumiwa, na watu hawataki kukulipa inawezekana
umetukana, inawezekana umeonewa, leo nataka nikupe habari njema ya kuwa yuko
Mungu anayelipa kisasi, kama
maandiko yasemavyo ni haki mbele za Mungu kuwaluipa kisasi wale wanaowaonea
ninyi
2Wathesalonike 1:6
– 9 “Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa
mateso wale wawatesao ninyi; na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi;
wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa
uweza wake katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu,
na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya
milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;”
Mungu anao wakati wake wa kujilipizia kisasi
dhidi ya wale wote wanaokuonea na kukutesa, kila unapopitia uonevu unayo haki
ya kumwambia Mungu liangalie na hili ukalitakie kisasi na Mungu mwenyewe
atausbiri wakati wake na wakati mwingine itakuwa mwisho wa Mwaka, ikawa nmwisho
wa Mwaka, ikawa mwisho wa Mwaka, ikawa mwishio wa Mwaka Mungu alijilipizia kisasi
dhidi ya Yosia aliyemuua Zekaria ili hali baba yake alimtendea mema hakuna
sababu ya kuogopa kila aina ya uonevu katika maisha yako italipwa mwisho wa
mwaka, umeonewa wewe kumbuka ikawa mwisho wa mwaka, umekopwa hujalipwa wewe
kumbuka ikawa mwisho wa Mwaka, umekataliwa, mumeo au mkeo ameibiwa, ikawa mwiho
wa Mwaka, umedhulumiwa paka kumbuka ikawa mwisho wa Mwaka IKAWA MWISHO WA MWAKA
Na Rev. Innocent
Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi
mwenye hekima!