Jumamosi, 5 Machi 2016

Ushauri wa Kichungaji !



UTANGULIZI
 
A.      Umuhimu wa Kozi ya Ushauri wa kichungaji

*      Itakusaidia kufahamu historia na Ufahamu kuhusu ushauri nasaha

*      Itakusaidia kufahamu mbinu za kishauri ili kwamba uanze kufanya ushauri nasaha


B.      Maeneo muhimu ya kozi ya ushauri wa kichungaji

*      Katika kozi hii kuna mambo ya msingi makuu matatu ambayo yanahusu

*      Watu ambao tutawafanyia ushauri

*      Mbinu za kufanya ushauri

*      Aina za ushauri wa kichungaji


C.      Kwa ni nini ni muhimu kujifunza ushauri wa kichungaji?

*      Kwa sababu kuna watu ndani na nje ya Kanisa wanaokuzunguka ambao wana matatizo wanayokumbana nayo

*      Watu wana shida  katika maeneo makuu manne


1.       Matatizo ya kihisia Emotional problems au matatizo ya kisaikolojia Psychological Problems

2.       Matatizo ya kiroho Spiritual Problems

3.       Matatizo ya kiuchumi Economic Problems

4.       Matattizo ya kimwili Physical Problems

D.      Kazi yako au jukumu lako kama mchungaji ni pamoja na

*      Kutafuta njia za kuwasaidia watu kuchukuliana na matatizo yao na kutafuta kuyatatua kwa mafanikio

*      Kuhakikisha kuwa hatimaye wanayaona matatizo yao madogo na yasiyotishio.



 Ushauri wa Kichungaji "Pastoral counseling"

SOMO LA KWANZA: UFAHAMU KUHUSU USHAURI COUNCELING
A.      Ushauri Nasaha ni nini?
·         Usahauri ni uhusiano baina ya pande mbili zenye mahusiano ambapo mmoja wa wenye mahusiano hayo yaani mshauri (The counselor) anatafyuta kutoa ushauri, kutia moyo na kumsaidia muathirika (The counselee) kukabiliana na tatizo alilo nalo katika maisha yake kwa ufanisi.
·         Jambo la msingi hapa ni kuwa Mshauri nasaha anapaswa kufahamu kuwa hatoi tu ushauri tu na kutia moyo lakini pia unapaswa kuvaa kiatu cha Yule unaye msahuri yaani kuumia pamoja naye ,
·         Jambo kuu la msingi katika kushauri ni kutafuta wazo lenye uifanisi litakalosaidia katika kumfanya msauriwa kufanya maamuzi na kumsaidia kurudi katika hali ya kawaida kiakili na kisaikolojia
·         Kwa kawaida kulingana na mtazamo huu hata kama mtu hana tatizo ambalo ni kubwa sana bado anaweza kuja kutafuta wazo lenye busara litakalo msaidia kufanya maamuzi mazuri na kupata mafanikio katika maisha kwa ujumla

B.      Mchungaji kama msahauri

·         Ushauri wa kichungaji ni moja ya njia za hali ya juu ya njia za uponyaji na njia ya kusaidia watu kubeba matatizo yao na magumu wanayaokutana nayo hivyo kusababisha ukuaji ulio bora na uponyaji wa mioyo iliyovunjika, si kila wakati mahubiri ya madhabahuni yanaweza kuyafikia matatizo ya ndani sana ya wanadamu wakati mwingine inahitaji kuwasikiliza watu na ushauri nasaha ndio njia ya uponyaji huo.
·         Huduma hii pia ni hatua ya kuwafikia walio karibu na walio mbali kimisheni hasa kwa kuwafikia wenye shida  na taabu jambo hili hujumuisha mbinu ya kuwafikia watu kwa kuitikia mahitaji yao ya kishauri ndani ya kanisa na nje ya kanisa

C.      Lengo la ushauri wa kichungaji.

·         Lengo kuu la ushauri wa kichungaji ni kuhakikisha kwamba muathirika yaani mwenye kuhitaji ushauri anafikia kilele cha uponyaji wa kiroho na ukomavu
·         Mshauri anakuwa ni njia ya kusaidia kukua kiroho kwa wahusika washauriwa anakuwa ni mwezeshaji na njia ya uponyaji na mchakato mzima wa ukombozi.
·         Washirika wa kanisa husika wafikie hatua ya kumuona mchungaji wao kuwa Baba mwenye kuaminika , Mchungaji anapojishughulisha na  mahitaji ya kondoo anajiweka katika nafasi ya kuonekana kuwa ni muhusika wa kundi na sio polisi katika kundi Matendo 20;28. Biblia ina sema hivi “

D.      Mbinu kuu mbili zinazohitajika katika ushauri wa kichungaji
1.       Kijihusisha (Relating) – Ili kutia moyo kwa uwazio kabisa  uponyaji na ukomavu mshauri lazima akubali kuwa na na uhusiano na watu au kujihusisha na watu, ushauri wa kichungaji ni  njia nzuri ya kupeleka habari njema  katika lugha ya mahusiano lugha itakayo ruhusu mshauri kuwasilisha ujumbe wa uponyaji kwa mshirika mwenye kusumbuliwa  na hatimaye kuweza kumfanya aone mambo yako sawa.
2.       Mawasiliano (Communicating) – Mchungaji mshauri  ni njia ya kupitisha taarifa na njia ya kuhakikisha kwamba wazo lenye Busara litakalomfganya msauriwa kuchukua uamuzi kwa msingi huo ni muhimu mchungaji kuwasiliana au kujifunza namna ya kuwasiliana kwanza kwa kuonyesha upendo wake binafsi na upendo wa Mungu kwa Mshauriwa.
           
UHUSIANO WA USHAURI WA KICHUNGAJI NA UCHUNGAJI.

        Uchungaji ni jukumu moja la muhimu na pan asana kuliko tunavyoweza kufikiri na ni zaidi ya kuhubiri,Huduma ya uponyaji na makuzi katika kanisa na jamii katika mzunguko wa maisha haya basi ushauri wa kichungaji ni moja ya majukumu ya ndani nay a muhimu sana ya kichungaji. Kwa ujumla kuna majukumu  makubwa muhimu kama matatno hivi katika shughuli za kichungaji

1.       UPONYAJI – Moja ya majukumu ya muhimu ya kichungaji ni uponyaji ambapo mchungaji anafanya kazi ya kuweka malengo ya watu wake au wateja wake kushinda matatizo ya aina mbalimbali kwa kupitia
a.       Kuhakikisha kuwa mtu anakombolewa kwa ujumla
b.      Kumuongoza katika malengo yaliyo zaidi ya mahitaji yake ya mwanzoni
2.       KUWEZESHA – NI wajibu wa mchungaji kumsaidia muathirika kuweza kuvumilia na kuchukuliana na Mazingira hata pale inapoonekana kuwa kuna mazingira ya kutokuwezekana au pale ambapo uponyaji uko katika mchakato au haiwezekani.
3.       KUONGOZA -  mchungaji atamsaidia muathirika ,kufanya uamuzi sahii kwa ujasiri
4.       KUPATANISHA – Ni wajibu wa mchungaji kustawisha uhusiano ulio haribika kati ya mtu na mtu  au kati ya mtu na Mungu hivyo wakati wa kufanya ushauri wa kichungaji , Mchungaji pia atakuwa anaifanya kazi ya kumpatanisha mtu husika na Mungu
5.       KUFANYA MALEZI – huu ni uwezeshaji wa kumtia moyo mtu kuweza kuendeleza kipawa au karama aliyopewa na Mungu.
6.       Kumbuka kuwa kuna nafasi za kufanya mambo nmengi yahusianayo na huduma za kichungaji endapo nafasi hiyo itatumika zaidi ya nafasi zilizoorodheshwa hapo juu.       

A.  BIBLIA NA MASWALA YA USHAURI

Umuhimu wa kutumia maandiko wakati wa kufanya ushauri.

Biblia ni kitabu cha ushauri wa Kikristo , Kila msahuri wa kikristo hususani Mchungaji ni muhimu kukumbuka kuwasaidia watu kuwa na uwezo wa kuchukuliana na maisha ya kila siku kupitia neno la Mungu, ushauri wowote ambao hautaruhusu Biblia kufunuliwa huo sio ushauri wa kichungaji au hauwezi kuwa ushauri wa kikristo
     Kuna matatizo mengi ambayo yanaweza kutatuliwa au kutiwa moyo kupitia vifungu Fulani vya kimaandiko, ndani ya hayo kuna majibu yaliyo wazi na yaliyo elezewa vizuri, ingawaje inaweza kuwa ngumu kutafuta maandiko kwa ajili ya kila aina ya tatizo lakini hutakosa muongozo au kanuni zinzoongoza ndani ya biblia ambazo zinahusiana na maisha ya kila siku kwa ajili kujifunza namna ya kuchukuliana na hali halisi.




MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUWA NA UTUMIAJI WENYE MATOKEO MAZURI WAKATI WA USHAURI
·         Ni muhimu uwe mtandaji wa neno Yakobo 1; 22-25,2Timotheo 2;15.
·         Soma biblia kila mara kwa utaratibu maalumu ili uweze kuwa na ufahamu wa kutosha wa kanuni hizo zenya kuongoza maswala Fulani ya maisha Wakolosai 3; 16-17,2Timotheo 3;16-17.
·         Hakikisha kuwa unakariri baadhi ya maandiko, kwa mfano unajua kuwa utashauri watu katika maeneo kadhaa ya kimaisha basi ni muhimu kuandaa maandiko yanayoendana na tatizo husika utakalokuwa ukishugjhulika nalo weka orodha ya matatizo unayotaka kuyashughulikia kwamfano
-       Woga andaa Zaburi ya 34;4
-       Kukosa amani andaa Yohana 14;27
-       Kutokusamehe Mathayo 6;12
-       Zinaa andaa Mathayo 15;19, 1Koritho 6;9-10 n.k.
-       Majaribu andaa 1Petro 1; 6-7n.k.
-       Ulevi na madawa ya kulevya andaa 1Koritho 6;15,19-20Luka 21;34
-       Utaweka orodha ya matatizo unayokutana nayo katika jamii na majibu ya kimaandiko kwa shida za aina mbalimbali
·         Tumia toleo zuri la Biblia na itifaki ili kujaribu kusaidia kukusanya maandiko yanayohusiana katika na matatizo husika
·         Muombe Roho wa Mungu akupe  maandiko yenye kufaa ambayo yatavuvia utumiaji wako wa neno wakati wa kufanya ushauri wa kikristo
B. MASWALA YA USHAURI WAKATI WA AGANO LA KALE
      Nyakati za agano la kale tunaona kuwa kulikuwa na aina nyingi sana za maswala ya ushauri pamoja na kusaidia watu kishauri, nyingine kati ya vifungu vya kishauri katika agano la kale vilikuwa vilikuwa vikilenga tatizo moja kwa moja ili kulishughulikia na shauri nyingine zilikuwa zenye kuzunguka

Maneno yanayotumika kuonyesha ushuri katika agano la kale ni pamoja na
a.       Mithali 12 ; 15 Yeye atafutaye ushauri ni mwenye hakima
b.      Mithali 11 ; 14 Katika wingi wa mashauri kuna usalama
c.       Zaburi 25 ; 9 Wanyenyekevu  wataongoza
d.      Zaburi 23 ; 2 Kando ya mito ya maji ya utulivu huniongoza
e.      Yeremia 23;3-4,Mwanzo 29;7, Isaya 40;11,1Nyakati 17;6 Mungu anatajwa kama mchungaji ambaye analisha kundi lake

*      Nabii Kama Mshauri
Manabii wote wa agano la kale walikuwa ni washauri,Hususani  kwa wafalme na pale ushauri unapokuwa ni wa taifa zima Mfalme angeutoa kwa watu wote mfano 2Falme 21; 1-14, Damuel 12;1-15.
*      Waamuzi kama washauri
Kutoka 18;13-26  Musa alikuwa aki waamua watu na kuwashauri kutoka aubuhi hata jioni,lakini kuna wakati nay eye alishauriwa namna ya kuwaamua watu ili asichoke na watu wasichoke alishauriwa kuweka makuindi ya viongozi kubeba kazi ile pamoja naye.
Debora alifanya kazi ya kiushauri waamuzi 4-5
Samueli alikuwa nabii na mwamuzi
*      Mifano mingine ya kiushauri katika agano la kale
1. Mordekai alikuwa akimsauri Esta Esta 4;1-14
2. Samuel alikuwa akimsahuri Sauli 1Samuel 15;10-12
3. Suleimani aliwashauri wanawake wawili 1Falme 3;16-28
4. Rehoboamu alikataa ushauri mzuri na kuchukua mbaya 2 Wafalme 10;1-13.

C. MASWALA YA USHAURI WAKATI WA AGANO JIPYA
- Neno ushauri katika agano jipya lina asili ya kiyunani “Symboleuo” ambalo maana yake kutoa wazo, kutoa au kuwaza kwa pamoja Matendo 20; 27
- Maandiko mengi katika agano jipya yanayohusu wachungaji au uchungaji yana wazo lihusulo ushauri Matendo 20; 28.
- Katika agano jipya Neno la kiyunani Koinonia lilitumika kuonyesha uponyaji wa kikanisa katika kuibadilisha jamii wakilenga maswala ya kiroho, Koinonia ilimaanisha kustawisha ushirika miongoni mwa waamini kwa ajili ya kusaidia na kutia nguvu Matendo 2; 42-47 kwa msingi huo mshauri anaweza kumjumuisha mwenye kuhitaji na kupitia ushirika unaotolewa na waamini unaleta uponyaji na ushindi unajitokeza
- Injili zinazo fanana zinaonyesha kuwa ingawa Yesu alihubiri injili kwa umati mkubwa wa watu lakini pia alikuwa na muda na kutoa uthamani kwa mtu mmoja mmoja, mafano wake wa kondoo aliyepotea, shilingi iliyopotea na ule wa mwana mpotevu unaonyesha kielelezo chake cha kujihusisha na kujali maisha ya mtu mmojammoja na furaha inayowakilishwa katika mifano hiyo inaonyesha mafanikio ya kujihusisha na mtu mmojammoja mifano hiyo iko katika Luka 15.
- Katika injili ya Yohana pia tunaona jinsi Bwana akijihusisha na maisha ya mtu mmoja mmoja binafsi kama Nikodemo Yohana 3;1-17 na hatimaye kumshauri kuhusu kuzaliwa mara ya pili,na Yohana 4;1-30 alijihusisha na mwanamke msamaria na kumuhubiri kuhusu uzima wa milele  na katika Yohana 20;27-28,alimshauri Thomasi kuhusu kuamini.


SOMO LA PILI: MBINUMBALIMBALI ZA KUFANYA USHAURI.
     Kuna njia mbalimbali za kufanya ushauri hizi ni njia zinazowakilisha falsafa mbalimbali za kuelewa ipi ni njia ifaayo katika kufanya ushauri (Theories of counseling).

A.      PSYCHOANALYSIS
     Falsafa ya njia hii ni imani kwamba kila mtu ana baadhi ya maumivu aliyoyapitia mapema tangu utoto wake maumivu hayo kamwe hayawezi kusahaulika isipokuwa yanakandamizwa tu chini sana katika ubongo wa kumbukumbu bila kudhamiria, Ubongo unaitunza kumbukumbu hiyo isiyopendeza na kutokutaka ikumbukwe na pale inapochochewa na kukumbukwa inasababisha matatizo ya kihisia kwa hiyo kupitia njia hii ya Psychoanalysis tatizo lililokuwa limekandamizwa linaweza kugunduliwa na likiisha kugundulika ndipo sasa muhusika anapoweza kujisikia vizuri
     Njia hiyo ya Psychoanalysis hufanywa na Psychoanalyst ambapo mtaalamu huyu humruhusu muhusika kujieleza kwa uhuru kuhusu historia yake ya huko nyuma, mambo aliyojihusisha nayo na kumbukumbu zake na kadhalika. Theory hii au falsafa hii iligunduliwa na mtaalamu wa Psychology Bwana Sigmund Freud daktari kutoka Austria.

Sigmund Freud 1856-1939
     Hili jamaa lilikuwa daktari katika maswala ya madawa na utabibu alikuwa ni mtaalamu wa maswala ya akili aliamini kuwa tabia ya binadamu inasukumwa na misukumo “Drives” isiyozuilika kidhamiri au isiyokusudiwa kuelekea kwenye hitaji husika la kistarehe kama tendo la ngono na endapo halitatimizwa basi linamuacha mwanadamu huyu katika migogoro wa mtu na mazingira yake .




B.      CLIENT – CENTERED THERAPY
     Falsafa hii inaamini kuwa kama muathirika akipewa nafasi salama ambapo anaweza kuzungumza kwa uhuru kuhusu tatizo lake anapata ahueni na hatimaye anaweza kupona ahueni hii inaletwa na upatikanaji wa wazo jipya au ufahamu mpya kuhusiana na tatizo alilo nalo ufahamu huu huja baada ya kuwa mgonjwa amepewa nafasi salama ya kuzungumza na kujadili nini kiko moyoni mwake aina hii ya tiba iligunduliwa na kuendelezwa na mtaalamu Carl Rogers ambaye alikuwa na shahada ya udaktari wa falsafa katika maswala ya saikolojia huko U.S.A.

C.      REALITY THERAPY. (Dawa ya kweli)
     Tiba hii inahusiana hasa na tatizo ambalo limejitokeza hivi karibuni na sio nyakati zilizopita, aidha tiba hii hufanya kazi katika maeneo ya mahusiano zaidi hususani pale mtu anapowajibika kitabia kuliko maswala ya hisia
     Kiini kikuu cha tiba hii ni kuwajibika mara moja hapa au sasa hivi na sio kusubiria mpaka baadaye kabla ya kusubiri muhusika azalishe hisia zenye kujirekebisha kitabia
Aidha lengo linguine kubwa la tiba hii “Reality therapy” Kumpa mtu vidonge vyake kwa lugha za mtaani au kumwambia mtu ukweli ili aamue kupona au kufa hapohapo, na kumpa fundisho ili asiruydie tena baadaye
      Njia hii ina faia kwamba inampa mtu kujitambua na kujielewa anapokosea kujua makosa yake anapofanya vema kujua uwezo wake  na hii itasaidia katika kumfanya mtu kuwa na uwezo wa kujirekebisha mwenyewe, inamfundisha mtu kutokukwepa kuwajibika na kujengeka mwenyewe kitabia njia hii iligunduliwa na Dr.William Glasser.

D.      MINIMUM CHANGE THERAPY (hata badiliko dogo ni badiliko)
     Tiba hii au falsafa hii inalalia katika wazo la kuleta mabadiliko yaliyo mazuri hata kama ni kwa kiasi kidogo, bado inasadikiwa kuwa ni muhimu, kwa hiyo muhusika anaachiwa ateseke kwa muda wowote atakao uchukua kwani hatimaye atatulia na kupokea mabadiliko
Tiba hii imegunduliwa na Bwana Leona Tyler ambaye alikuwa ni Professor wa chuo kikuu na mtaalamu wa mambo ya ushauri

E.       BEHAVIORISM
     Kwa mujibu wa tiba hii ambayo ni falsafa ya bwana B.F.Skinner ambaye anaamini kuwa mwanadamu ni zaidi ya mbwa asiyeeleweka na kwa ujumla anaathiriwa na mazingira yanayoamuliwa na shughuli za kila siku na aina za mawazo, hisia, na matendo na hivyo anaweza kufundishwa na kudhibitiwa kama mnyama mwengine yeyote kwa sababu ya kuharibu hali ya mazingira yake.
     Tiba hii inasema kwamba hakuna mtu muahalifu, Bali kuna mazingira yanayopelekea uhalifu wakati bwana Freud anatafuta namna ya kuufanya utu wa ndani wa binadamu ukae sawa bwana Skinner anataka kuboresgha mazingira ambayo yatapelekea badiliko la kitabia katika muelekeo utakaochaguliwa na mchongaji wa tabia yaani msahuri
     Kwa hiyo kila kilichoko na mwanadamu ni tabia na kwa haraka tunajifunza kuwa bora zaidi na sayansi ndio jibu la swala hilo

F.       EXISTENTIALISM
     Falsafa hii inaamini kuwa mwanadamu ni kiumbe kisichotabirika na huwezi kuhusisha swala Fulani na ujuzi kuhusu tabia Fulani hii ni kwa sababu maswala yake mengine hutokea kama ajali na hakuna sababu inayokubalika kuweza kumzungumzia
     Kwa msingi huo suluhisho pekee ni kutokuhusisha hali yake na jambo lolote bali kujaribu kumfanya awe na furaha, mfanya afurahi bila kutafuta sababu na anapopata furaha itatupilia mbali matendo na tabia zilizokuwa zimejitokeza na jambo hili litaleta maana kuliko kutafuta sababu

G.     GROWTH COUNSELING APPROACH
     Kulingana na falsafa hii ushauri wenye matokeo ni moja ya njia ya kutafuta kumtia nguvu mashauriwa na kumfanya Yeye kwa ujumla wake atiwe nguvu katika maeneo yote muhimu ya maisha hii inaonekana kuwa mwanadamu anafunguka katika mfumo mzima na ukuaji unachukua nafasi katika mahusiano ambayo yanalenga maeneo makuu sita ambayo ni
*      Uhusiano wake na Mungu unaimarika
*      Akili zake zinakaa sawa
*      Mwili wake unaponywa na kuwa na afya nzuri
*      Uhusiano wake katika ndoa unakomaa vema
*      Uhusiano wake na mazingira ya asili unastawi
*      Ukuaji wenye kuhusiaha umuhimu wa kujifunza maswala kadhaa katika maisha

Growth counseling approach ndiyo mbinu ya ushauri inayopendelewa sana na wasomi wengi katika mpango mzima wa maswala ya ushauri wa kichungaji
 
SOMO LA TATU: MCHUNGAJI KAMA MSHAURI
A.      Wachungaji wote ni washauri

     Kila mtumishi hususani mchungaji ni mshauri mara unapokuwa umeitwa kwa ajili ya kumtumikia Mungu basi wakati huohuo umeongia katika kazi ya ushauri kwa msingi huo kushauri kwako linakuwa sio swala la kuchagua kuwa nishauri au nisishauri, kwa sababu uwe umejifunza ushauri au hukujifunza unakuwa umeingia katika kushauri hii ni kwa sababu katika kila kanisa wako watu ambao wana maumivu ya ndani sana ya uhitaji wanahitaji mchungaji awashauri ili kwamba wajue ni namna gani wanaweza kuepukana na matatizo yao lakini sio kushauri tu kwani kuna nidhamu na mbinu za stadi za kufanya ushauri hivyo kama kuna mchungaji atazikosa stadi hizo mtu mwenye uhitaji anakuwa na moyo wa jiwe kwa kukata tama kwa kawaida ni mchungaji pekee ambaye ana nafsi kubwa ya kuingia katika moyo wa maisha binafsi ya mtu na ushauri ni sehemu muhimu ya kukutana na maswala ya aina hiyo

B.      Moja ya silaha za muhimu za ushauri kwa mchungaji

     Kuishi maisha yaliyo kielelezo ni moja ya silaha yenye nguvu sana ya Ushauri wa kichungaji Mshauri hususani mchungaji anawajibika kuwa na maisha yaliyo ya maadili ambayo yatakuwa ni kielelezo katika jamii swala kama hili linamsaidia muathirika, kwa msingi huo unaweza kufisha tabia ambazo zinawadhuru unaotaka kuwahudumia na kujijengea tabia zitakazo wafanya wengine wakuamini.
     Ni jambo gani tunapaswa kulifanya wote tunajua kuwa Matendo yanasema kuliko maneno na ndivyo ilivyo kwa watu wanaotuzunguka tabia zetu zinaleta athari, Biblia ina mafundisho mengi yanayotukumbusha kuwa kielelezo kwa wengine kwa msingi huo maisha yako ni moja ya mtaji mkubwa sana wa kufanya ushauri kumbuka
·         Ni maisha Yesu aliyoyaishi yaliyoweza kuleta changamoto kubwa kwa wanafunzi wake maisha yao yalibadilika kadiori walivyokuwa wakimkaribia na kuwa na muda naye soma injili
·         Paulo mtume aliishi maisha ambayo kwayo aliweza kuwahamasisha wafuasi wake kuufuata mfano wake 2Thesalonike 3;7-9,Maisha ya Paulo yalikuwa yamejaa mafundisho yenye nguvu kwaajili ya ushauri kwa msingi huo hata anapotoa ushauri kwa watumishi kama Timotheo na Tito ushuri huo unaweza kufanya kazi kupitia mfumo wa maisha ya mfano aliyoishi

C. Mipaka na faida za ushauri wa kichungaji

*      Mipaka
1. Kila shughuli itamgharimu mtumishi nguvu na muda, ukiachia mbali swala la kuandaa jumbe, kuna maongozi ya kanisa zima kwa ujumla nah ii huwafanya wachungaji wengi kushauri kati ya masaa 5-10 kwa wiki bila kuacha shughuli nyingine ziharibike

2. Mshauri ambaye amesomea kitaalamu anatakiwa atumie miaka 8-10 ukiachia elimu ya sekondari kujifunza swala zima la kufanya ushauri hivyo kwa mchungaji sio lazima atumie muda wote huo kwa ajili ya mafunzo ya kushauri lakini anapaswa kufanya kila liwezekanalo kujizoeza na kujifunza mbinu za kufanya ushauri

3. Wajibu wa mchungaji mara nyingi umekuwa ukichanganya watu, Wengine humuona mchungaji kama polisi na wengine huwaona wachungaji kama majaji wakali sana wasio na huruma  kwa msingi huo ni muhimu sisi wachungaji kuondoa upolisi na kukubali na kujaribu kuwasiliana na watu kwa sababu watu ndio sehemu ya utumishi wetu inatupasa kuwapenda na kuwapa kipaumbele bila kujali wako vipi

4. Wachungaji wengi hawashiki malipo ya kazi zao za kiushauri lakini wataalamu wa maswala ya ushauri Psychologists waligundua kuwa kuna watu ambao hawawezi kuithamini huduma hii mpaka uwatoze fedha yaani inapowagharimu basi inaleta maana kwao

5. Majaribu wakati mwingine hutokea kuwa mshauriwa akaweza kuendeleza hisia kali kwa mshauri na hii inaweza kusababisha, hisia za upendo au chuki, hii inaweza kutokea hususani katika ushauri unaochukua muda mrefu na maswala ya aina hii husababisha wakati mwingine kashfa za ngono kwa wachungaji na chanzo kikiwa ni maswala ya ushauri

Faida za ushauri wa kichungaji.

1.  Kuaminika mara nyingi moja ya faida za ushauri wa kichungaji ni pamoja na kuaminiwa na washirika na watu washauriwa watakuja kwako.

2.  Kustawisha uhusiano ukweli kuwa wewe ni mchungaji ni rahisi kwa jamii na washirika kuwa na uhusiano na wewe kwa msingi huo unaweza kustawisha uhusiano na jamii na familia katika kanisa na hivyo kuwa na mahusiano yenye nguvu mahusiano haya yanaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika maswala ya kiushauri kuwa na mafanikio makubwa sana na hivyo kumfanya mchungaji kuweza kutoa ushauri pale inapobidi.

3.   Upatikanaji, Kwasababu ya upatikanaji wa mchungaji inakuwa ni rahisi mwenye mahitaji kuja mara moja au mchungaji kuwatembelea

4.   Imani  moja ya faida kubwa ya mchungaji kama mshauri ni pamoja na  watu kumuendea mara wanapokuwa na matatizo kwa sababu ya maswala ya imani na kutoa uthamani kwa kiongozi wa kiroho.

5.     upekee wa kuwa mshauri wa kichungaji ni kuwa ni lazima angalau uwe na ujuzi wa kitheolojia na Saikolojia, kwani mchungaji sio tu kuwa ni mshauri wa kawaida anaye shauri kwa kutumia mbinu za kiushauri tu lakini anakuwa ni msomi mwenye ujuzi wa falsafa, elimu kuhusu Mungu, maadili, ujuzi wa kibiblia, historia ya kanisa na dini za ulimwengu kwa msingi huo ana elimu pana zaidi inayoweza kumpa uwezo mpana katika kushauri

7.       Hali ya kutokuweko kwa Malipo ushauri wa kichungaji ni ushauri unaotolewa bure tu pasipo malipo faida yake ni kuwa inaruhusu mtui awaye yote hata masikini asiye na uwezo anaweza kumuona mchungaji hata bila ya kusubiri kwa siku kadhaa au wakati mwinguine hata pasipo mapatano maalumu appointment


SOMO LA NNE: WATU TUNAOWASHAURI
A.      Maelezo;
Msingi mkubwa wa somo hili ni kukusaidia wewe kufahamu zaidi watu kwa ujumla na hatimaye mtu utakayekuwa unamfanyia ushauri, Lengo la ushauri ni kumfanya mtu awe katika hali yake ya kawaida na kuweza kuchukuliana na mazingira yake katika hali iwayyo yote lengo la kushauri sio kuwa fanya watu wote wafanane hapana lakini ni kutunza utu huku ukimsaidia mtu huyo kuishi kwa ajili ya mungu kwa usahii zaidi.
Kuna mambo ambayo ni ya msingi yanayoweza kuwafanya binadamu wote wafanane au wasifanane mmoja wa wanasaikolojia maarufu alisema
·         Kila mtu ni kama mtu mwingine
·         Kila mtu ni kama watu wengine
·         Kila mtu si kama kila mtu au watu wengine
Kwa sababu kila mtu kwa mfano ni mwanadamu na kwamba Yesu alikufa kwa ajili yake kwa msingi huo tunaweza kuwa na kanuni ambazo zinafanana na kanuni kwa watu wengine lakini si kila wakati, na tunaweza kutatua matatizo kwa kutumia kanuni ya msingi inayolingana lakini pia sio kila wakati, lakini wakati wote ni muhimu kujikumbusha wenyewe kwamba si kila watu wawili wanaweza kuwa sawa kabisa na kuwa lazima tuheshimu kila mmoja kama mtu tofauti.

B.      Utu wa mtu Binafsi
Kwa ujumla utu wa mtu binafsi ndio unaomfanya kila mtu kuwa tofauti kutoka mtu mmoja na mtu mwingine utu huo wa mtu unatofautiana katika mazingira yafuatayo
·         Tofauti ya kiakili
·         Tofauti za kimwili
·         Tofauti za kitabia
Mambo hayo matatu muhimu hapo juu ndio yanayoamua Kuweko kwa tofauti za msingi nne zifuatazo

Tofauti za msingi nne
1.           Tofauti za kurithi
Kila binadamu ana tofauti zake za kurithi ambazo kwa kawaida huanza mara tu baada ya kutungwa mimba tofauti hizi huamuliwa na chromosomes na genes yaani Kromoson na jins, hizi ndizo zinazoamua mtu awe mwanamume au mwanamke awe na rangi gani na macho ya nmna gani, urefu gani na aina ya mwili, akili, aina Fulani za uwezo na vipawahivi vyote huamuliwa na GENES
-       Hizi ndizo tofauti za kurithi zinazoweza kusababisha kuweko kwa hisia tofauti kwa njia tofauti kwa mfano
·         Kama kijana mfupi sana aliandamana na marafiki ambao wana urefu wa kawaida anaweza akajikuta anachekwa au kudharauliwa na kutaniwa  au kukataliwa
·         Na wakati msichana anapoishi katika jamii ambayo wanawake ni wachache ni warefu nay eye pakee ni mrefu sana anaweza kuepukwa na watu na akaonekana sio mwenye kuvutia kwa vijana

2.       Tofauti za ukuaji
     Ukuaji ni moja ya tofauti ambazo nazo ni sehemu ya urithi ni maswala ya kuzaliwa yaani hili linahusu maeneo mbalimbali ya ukomavu na makuzi hii ni kuanzia aina ya meno, utembeaji wetu wa upesi au kuchelewa kutembea,usomaji,sauti ya kivulana wakati wa kukua, ukuaji wa mwanamke na kubalehe kwao yote huamuliwa na tofauti za ukuaji zinazotokana na kurithi

3.       Tofauti za kujifunza
    Tabia ya mwanadamu piua huathiriwa na namna anavyojifunza, kujifunza ni kubadilika na kunabadilisha tabia nba mwenendo kulingana na namna tunavyoyafanyia kazi yale tuliyojifunza kuna falsafa mbili za nman ya kujifunza
a.            Drive-Reduction theory wazo hili linaamini kwamba kila tendo linalotokea la kitabia hasa litokanalo na misukumo yaani maswala ya kiu ya maji, Chakula, na hewa yanaweza kupungua au kutoshelezwa kwa tabia ya kujirudia rudia, yaani mambo haya mtu anajifunza kupitia kurudiarudia tendo Fulani linalokamilisha hitaji hii ndio maana mtoto hujifunza kunyonya tena na tena.
b.            Reinforcement theory wazo hili ni imani ya kuwa kama tendo fulani linaambatana na hisia nzuri basi muhusika ataendelea kulifanya tendo hilo hii inaitwa kuendeleza tabia chanya
Lakini kama mtu huyo atafanya tendo Fulani likaambatana na maumivu mtu huyo ataacha kufanya tendo hili hii inaitwa kuendeleza tabia hasi

Kwa mfano;-
i.                     Kama mtoto anapochukua hatua ya kwanza akasifiwa kwa kujaribu kutembea na kuimbiwa basi atajaribu tena na tena kutembea na kujenga tabia chanya katika kutembea
ii.                   Kama mtoto atagusa jiko la moto na akaungua basi ataogopa kugusa tena kwa sababu ameungua na hivyo kuendeleza tabia hasi
4.       Mambo mengine yanayoendeleza tabiia ni pamoja na

1.           Tabia ya kuambukizwa INTERNALIZED VALUES hii ni hali inayotokea tunapoambatana na mtu na kumpa uthamani Fulani bila kutumia akili tunaambukizwa tabia zake mambo anayoyapa uthamani na anayo yapendelea
2.            Kuchukuliana au kutokuchukuliana CONFORMITY AND NON-CONFORMITY halii hii hutokea kwa mfano mtoto au kujana anapokuwa anakubalika au kutokukubalika katika jamii kwa sababu kadhaa kwa mfano labda ni mbunifu na hufanya mambo vema kuliko jamii anayoishi sasa ili akubalike na jamii ambayo inaishi chini ya kiwango anaanza kufanya kama kila mtu wa eneo hilo anavyofanya ili akubalike na jamii au anaweza kuiasi jamii hiyo na kutokuchukuliana nayo.

3.           Tatizo la kutokujitambua IDENTITY CRISIS Baadhi ya watu wanashindwa kabisa kujitambua kuwa wao ni nani kwa sababu ya tatizo la kushindwa kujitambua na kwa sababu hiyo wanaweza kutumia miaka mingi wakibadilisha uthamani wa mambo hii huwapata sana vijana anaweza kujiingiza katika makundi  au kujiunga na kundi linguine tofauti akijaribu kujijibu swali yeye ni nani na anapaswa kufanya nini ?
     Mtu anastawisha utu wake vema baada ya kujitambua na kujijua kuwa yeye ni nani na ni nini anapaswa kukifanya
     Kanisani mara nyingi tatizo la kutojitambua linaweza kubainika wakati mtu anapofikia hatua ya kuchagua mchumba, au wakati wa kufanya uamuzi fulani, wakati wa kuhudumu na hata wakati wa kuamua namna ya kumtumikia Mungu, wapi na jinsi gani wakati huu utaweza kuona kuwa huenda wazazi wake walikuwa na mpango mwingine tofauti kabisa na ule aliouchagua matatizo kama ya usagaji na ushoga wakati mwingine pia hutokana na hali ya tatizo la kutojitambua.

4.            Ndoto iliyovunjika BLOCKED MOTIVATION hakuna mwanadamu awaye yote   anayeweza kufanya jambo bila kusukumwa na nguvu fulani ya uhitaji kuna nguvu za aina hizo mbili mahitaji ya kimwili nay a kisaikolijia mahitaji ya kimwili hujumuisha hewa, chakula, maji, na kwenda haja.
Mahitaji ya kisaikolojia ni pamoja na
a.       Kuhitaji muitikio mfano kama ukiwapenda watu unatarajia nao watarudisha upendo kwako
b.      Kuhitaji kutambuliwa kila binadamu anahitajim kutambuliwa kama hujaliwi unajiona hufai au mahali usipojaliwa hapakufai
c.       Kuhitaji usalama hili ni hitaji la vyote kimwili na kisaikolojia kila mtu anahitaji usalama hususani unaotokana na jamii husika unayoishi
Sasa inapotokea kuwa ndoto hizo za kimsukumo zinavunjwa kunakuweko matokeo mfano kama mtu amepata pancha hamu yake itakuwa ni kulikarabati tairi au kulibadilisha sasa wakati anajaribu kufanya hivyo na vifaa vya kufanyia kazi hiyo vikawa havipo basi anakuwa na shauku au ndoto iliyovunjika na hivyo kusababisha mgandamizo wa mawazo au msongo

5.       Hali za kujihami DEFENSE MECHANISMS
     Katika hali ya kujaribu kuchukuliana na hali ya kidhamiri hasa mwanadamu anapokuwa na ndoto iliyovunjwa au shauku iliyokwazwa basi kutazaliwa hali za kujihami hali hizo za kujihami ni pamoja na
i.                     Ndoto za mchana DAY DREAMING: mtu anapokuwa na ndoto ya mchana maana yake ni kuwa akili zake au mawazo yake yana wayawaya anakuwa hayuko kanisani au kazini au shuleni na anaanza kufikiria kuweko mahali pengine pasipokuwa na shida ili kujipendezesha na kupata raha katika kufikiri kwake lakini tatizo linakuja kuwa kufikiri kwake au kuwaza kwake hakuwezi kumsaidia kitu na matatizo yake yanabakia kuwa kweli vilevile.

ii.                   Hali ya kutafuta visingizio RATIONALIZATION: mtu anapokuwa na hali hii hutafuta visingizio ili kujikidhi kisaikolojia kwa mfano mchungaji anaweza kuwa anatamani kupewa kanisa Fulani kubwa ili aliongoze na anapokuwa hajateuliwa yeye kuliongoza basi anaweza kusema “Ah! Hata hivyo hawako kiroho Pele”Hiki ni kisingizio.

iii.                  Kusukuma lawama kwa wengine PROJECTION; Mtu anweza kuwa na tatizo lakini akatafuta kumsingizia mtu mwengine ili kukwepa kuwajibika kwa makosa yake mfano Mwanzo 3 adamu alilaumu kuwa Eva kuwa ndio chanzo cha tatizo na kasha Eva akamlaumu Nyoka.

iv.                 Kukandamiza wengine kwa ajili ya maslahi yako COMPENSATION: hali hii hutokea pale mwanadamu anapofanya jambo kwa ajili ya usalama wa maslahi yake tunaiyona hali hii kwa Farisayo katika Luka 18;10-14 anajaribu kumponda mtoza ushuru na kujiinua mwenyewe ili kujipendekeza kwa Mungu, watu wengi wenye tabia hii hutaka kufanikiwa kwa kuumiza wengine kwa mfano meneja aliye mfupi anaweza kuwa mkali sana,au mume asiye na elimu anaweza kuwa mkali samna kwa mkewe mwenye elimu ili kuziba ufa wa tatizo lake

v.                   Kujifichia au kujifananishia IDENTIFICATION: Hii ni tabia ya mwanadamu kukimbia hali Fulani ya matatizo aliyo nayo kwa kukaa karibu na mtu mwenye hali nzuri au maisha mazuri au cheo kizuri au tabia nzuri ili kufunika madhaifu aliyo nayo anaweza kuwa yuko karibu sana na muhubiri mkubwa au mchungaji ili kuficha uovu alionao au kuonyesha kuwa ni rafiki wa mkubwa Fulani au mtoto wa raisi

vi.                 Kukanusha DENIAL; Katika hali hii mwanadamu anakanusha kabisa kwamba ana tatizo au amekosea anakubali kujidanganya mwenyewe kuwa hakuna kitu kilichotokea kwangu.

vii.                Kutafuta sifa ATTENTION-GETTING: Hii ni jamii ya watu wanaojaribu kutafuta sifa na kuvuta hisia za watu kuwaelekea marko 12;38-40 mafarisayo walivaa mavazi marefu sana , au kusalimia kwa upendo na kusali sala ndefu sana  na kuketi katika masinagogi na masokoni ili waonekane na watu kuwa ni watu wema sana kwa watoto ili aweze kusikika hutumia njia ya kulia na kusagasaga miguu ili watu wahusike nay eye zaidi, wengine huchelewa ibada na kuingia na kiatu kirefu sana chenye mlio ili watu waone anavyoingia, makahaba huitumia hii kwa kuvaa nguo maalumu zenye mvuto wa kuonyesha mapaja, makalio au mahips waliyo nayo kwa lengo la kuwapata wanaume n,k

viii.              Kutafuta makosa na kukosoa NEGATIVISM: Ni hali ya kutafuta makosa kwa watu na kuzungumza kwa hali ya kutafuta kuwadhuru au kuwakosoa kinyume na watu au vitu, yaani hawa kila kitu kwao hakiko salama

ix.                 Enzi ya zilipendwa REGRESSION: Hii ni hali ya watu kujaribu kurudi nyuma na kukumbuka enzi hizo au wakati wa ujana au utoto katika maisha yao ambapo walifurahia maisha kwa hivyo katika kanisa utawasikia watu wakisema “enzi zile bwana”  hili ni tatizo la kisaikolojia la kujilinda kinyume na hali halisi ambayo kwayo inatutaka tusonge mbele kwa maswala ya mkondo ulioko

x.                    Kukandamiza REPRESSION: Ni hali ya kukandamiza chini hasa hali zozote zenye kuumiza, za huko nyuma au za karibuni hali hii hutokea bila kukusudia na ingawaje kumbukumbu za jambo hilo zinabakia pale pale na bado zinatuudhi.kwa wahubiri wengi hujikuta wakikemea hali hizo hata katika mahubiri yao kwa nguvu sana kumbe wamekandamiza hali zao wenyewe wakati mwingine.

xi.                 Kuhamisha matatizo kwa wengine DISPLACED AGGRESSION: Hali hii hutokea hata kwa kupiga au kudhuru mtu aliyekukosea na inapotokea kuwa hatuwezi kumduru mtu huyo aliyetusababishia matatizo kama bosi au rafiki au wazazi basi tatizo hilo linahamishiwa kwa mwengine, kama umekemewa kazini na Bosi basi unamalizia hasira zako nyumbani kwa mkeo na mke naye anahamishia kwa mtoto na mtoto anamalizia kwa paka na hivo paka anakuwa na wakati mgumu
C.      Hitimisho

1.            Ili kuwa wazi kabisa ni muhimu kufahamu hususani sisi washauri kuwa wanadamu wanatofautiana kabisa katika hali na utu kila tukio linaweza kutubadilisha katika hali Fulani kwa hiyo utu ni hali tete inayoweza kubadilika wakati wowote
2.            Hali hizo hapo juu zinamsaidia mshauri kujua kitu Fulani kuhusu Yule anayemsahuri na utu wake  ili kumsaidia katika hali kubwa mbili

a.       Kufikia hatima yaani kukupa mwanga kuwa mshauriwa anaweza kuwa anapitia hali ya namna gani ili kwamba kwa msaada wa Mungu na maongozi haya kumfikisha panapohusika

b.      Kuchukuliana  yaani kukupa mwanga jinsi gani mshauriwa anaweza kuchukuliana na hali halisi iliyoytukia katika maisha , kwa mfano kifo cha mpenzi aliye karibu na hivyo kumfanya hata kama amehuzunika sana bado aweze kuchukuliana na ukweli kuwa mwenzi wake hayuko naye kimwili tu lakini ameenda kukaa na Bwana 1Koritho 5;8 na hali hii ya kuweza kuchukuliana pia inaweza kuwa tofauti kati ya mtu na mtu


SOMO LA TANO: MBINU ZA KUFANYA USHAURI

1.       Stawisha uhusiano; ESTABLISHING A RELATIONSHIP.

-       Ushauri wa kichungaji wenye mafanikio siku zote unategemea jambo moja kubwa ni kustawisha uhusiano kati ya mashauri na mshauriwa lazima kuweko na upendo wa kimungu Agape na kukubalika hzi ndio funguo za kifundi katika maswala ya ushauri na mbinu zake.
-       Uhusiano kati ya mshauri na watu wengine lazima uongozwe na upendo wa kimungu agape, ambao ni upoendo unaotokana na nguvu za kimungu za kupenda hata kile kisichopendeka bila sababu.
-       Mshauri pia lazima  awe mwenye kukubalika na kuaminika  kwa watu wengine akikubalika pia kupitia tabia zake ni hiyari kumruhusu mtu kuwa tofauti kwa njia iwayo yote, Kukubalika kunahusisha pia swala zima la kuheshimu kila mtu yaani kama mtu amezaliwa mara ya pili tutamuhesabu kuwa ndugu katika Bwana, na kama hajazaliwa mara ua pili tutamuhesabu kama mmoja wa watu ambao Yesu alikufa kwa ajili yao
-       Ni muhimu kufahamu kuwa kama humkubali mshauriwa wanakuwa na uwezo wa kujua au kuhisi kuwa hakubaliki na atahisi kupwekeka na kutokujihusisha na kutokujaliwa na mshauri kwa msingi huo kujali ni muhimu sana.

2.       Stawisha mazingira yenye kufariji; ESTABLISHING RAPPORT.

-       Neno rapport maana yake ni faraja, katika maswala ya ushauri ni lazima ustawishe mazingira yanayoleta ujasiri na  faraja kwa kawaida mshauriwa hupenda mtu na eneo ambalo anajisikia amani  na hivyo inamsaidia kuwa wazi na kujiamini machoni pa mshauri  
-       Amani hiyo inapatikana kutokana na muda muafaka uliopangiliwa kwa maswala ya mashauri na matumizi ya sauti hususani kwa mjadala wa mara ya kwanza mazingira hayo yataamua ni namna gani utaweza kufanikiwa kulingana na mtu husika.
-       Baadhi ya maswala yanayoweza kusaidia katika kustawisha mazingira mazuri ya ushauri ni pamoja na ;-

Ø  Onyesha uaminifu jambo ambalo linaweza kusomeka katika uso wako
Ø  Anza wakati mwingine na mazungumzo ya taratibu yanayoweza kumfanya mshauriwa kujisikia salama mfano unaweza kumsifia kuwa unaonekana smart sana leo, au unafikirije kuhusu radii le ya usiku wa leo, na vinginevyo
Ø  Pia unaweza kuzungumzia swala ambalo unajua kuwa linamvutia sana mshauriwa kama maswala ya siasa na kadhalika.

-       Kumbuka kuangalia alama bubu za mshauriwa non vebal cues yaani alama ya uso wa mshauriwa kama anaonekana kuwa na huzuni,au mchangamfu,mkao wake katika kiti na pia kama kuna ishara za kuumizwa
-       Wakati mwingine  unaweza kuanza na kile unachofikiri kuwa ndio tatizo njia hii inaitwa “Shock approach” njia ya kustukiza  kwa mfano unaweza kumwambia umekasirika sana leo,Hebu tuzungumze ni kwa nini unaonekana hivyo leo n.k.

Mifano ya kibiblia ya mazingira ya amani ya kiushauri
Ø  Yesu alistawisha mazingira ya amani ili kuzungumza na mwanamke msamaria Yohana 4;7-15 alianzia na swala la kutaka maji swala ambalo msahauriwa ndio alikuwa na lengo nalo

3.        Stawisha hali ya kuchukuliana; SUSTAINING EMPATHY

-       Hali ya kuchukuliana na tatizo Emphathy ni hali ya ndani sana ya kuliona tatizo la muhusika kama tatizo lako, kuna usemi unaosema kuvaa kiatu cha mwingine au
o    kuona kama yeye anavyoona
o   Au ni hali ya kuliona tatizo la muhusika kama tatizo lako ni hali ya
o   Kuhurumia na kusukumwa na pendo la kweli kuhusu tatizo la mwingine
-       Mshauri anayejali hujihusisha sana na tatizo la msahauriwa yaani anakuwa tayari kwa muda kuyaachia maisha yake kwa ajili kufikiri maswala ya wengine na hii sio hali ya kuigiza lazima uwe mkweli na mwaminifu kwani mshauriwa ataona mwanga kupitia wewe, unatakiwa kutenda na kuhisi kana kwamba tatizo analolipitia mwengine ni kana kwamba ni la kwako, usijaribu kuigiza jambo hili na usijali matatizo yako.
-       Mwitikio wa mshauri kivitendo kwa maneno na kwa ishara bubu vinawasilisha ujumbe kwa unayemshauri iwe ni wenye kukubaliana naye au ulio kinyume naye na yote yatakubaliana na hisia zake
-       Huruma za Bwana yesu zilionekana alipokufa Lazaro Yohana 11; 33-36 na alipomuona mama mjane aliyefiwa na mwanaye Luka 7; 11-17.       

4.       Stawisha hali ya kuuliza maswali; QUESTIONING TECHNIQUES.

-       Moja ya njia za muhimu Sana za kumsaidia mshauri na mshsuriwa ni kustawisha hali ya kuuliza maswali na ziko namna mbili kuu za kuuliza maswali
i.                     Maswali mepesi kwa ajili ya kupata taarifa simple-Information question - mfano unatokea wapi,mumeo anaitwa nani, unafanya kazi wapi na kadhalika
ii.                   Maswali ya kufungua yaliyofichika kwa ajili ya kutatua tatizo Open-end” question – Kwa mfano unafikiria nini sasa juu ya hili, je unaweza kurudia tena namna ambavyo utamwambia? Kusudi kubwa la maswali namba mbili ni kumfanya mshauriwa ajieleze mwenyewe ili kwamba uweze kumfahamu vema au kumsaidia kufumua vitu na kujitambua

5.       Stawisha hali za kujadili pamoja ; THE INTERVIEW

-       Namna ya kustawisha mijadala
a.       Mahali (Location).Ushauru unaweza kufanyika mahali popote mahali pa siri ndipo pa muhimu zaidi, ni muhimu kutafuta mahali ambapo kuna utulivu na ambapo hapaytakuwa na mwingiliano, kiti pia ni lazima kiwe chenya kumfanya mshauriwa kujisikia salama na mahali hapo pasiwe na picha zenye mvuto.
b.      Tabia ya Mshauri au mtazamo (Counselor’s Attitude) Mshauri mwenyewe ni mtu wa muhimu sana  na sehemu muhimu sana ya ushauri,kama msahuri mwenyewe anajiweka katika hali ambazo zinamfanya mshauriwa ajisikie kutokukubalika au kutokujaliwa mshauriwa anaweza asijisikie vema
-       Vikwazo vya kustawisha mijadala.
1.       Njia unayoitumia- Unaposisitiza matumizi ya mbinu fulani zaidi itumike kuliko au kukazia mambo fulani kunaweza kusababisha kutokuweko kwa usikivu na hatimaye kuvunja mawasiliano, kwa msingi huo ni muhimu kukumbuka kuwa njia za mawasiliano ziko kwa ajili ya kutusaidia tu katika maswala ya ushauri ili uweze kufanyika vema na kwa sababu hiyo tunahitaji kujifunza kwa undani zaidi ili kwamba hatimaye ziweze kuwemo ndani yetu kwa kusudi la kuwasaidia watu na sio kuonyesha kuwa sasa ndo tunazitumia hususani wakati wa kufanya ushauri
2.       Usijaribu kutafuta suluhu mapema jambo hilin kitaalamu tunaliita Pre-mature seeking of solutions usijaribu kujionyesha kuwa una majibu tayari ya tatizo la mtu hii ndio shida ya wachungaji wengi wanaposikia shida ya mtu hujaribu kuyatumia maandiko mapema ili kusuluhisha tatizo kabla ya kuwa amemsikiliza mshauriwa na kuhakikisha kuwa je anaweza kubeba hali yake na kuchukuliana na hali yake.
3.       Usionyeshe kushangaa hali hii inaweza kusababisha mshauriwa kutokuwa makini kujisikilizia kihisia na hata wewe kumsikiliza vizuri unayemshauri hali hii kwa kawaida inaweza kuondoa usikivu na hisia za mshauri kujihusisha na hisia za mshauriwa kwa msingi huo ni muhimu sana kusikiliza kwani ndiko kutakakokuongoza katika kuelewa vema.
4.       Jihadhari na maneno au maswali kwanini aina hii ya maswali katika mjadala inaweza kumfanya mshauriwa kujiondoa katika kuelekea kujibu maswali kwa sababu inaweza kusababisha aijibu maswali ya aina hiyo kwani swali kwanini limekuwa likitumika kwaajili ya kuhukumu kwa muda wote wa maisha kwa hivyo mshauriwa anaweza kudhani kuwa anahukumiwa kwa msingi huo ni muhimu sana kujihadhari na maswali
i.                     Kwanini ulimpiga mkeo?
ii.                   Kwanini hukukabidhi ile kazi?
iii.                  Kwanini hukufika kanisani kwa siku zote hizo tatu?

-       AINA ZA MWITIKIO WA MSHAURI WAKATI WA KUFANYA MJADALA.(FATUKA)
Zifuatazo ni aina tano za mwitikio ambazo zinaweza kuwakilishwa na msahuri wakati wa kazi ya kushauri
i.                     Fanya tathimini - jaribu kuanza kumuonyesha unayemshauri kama ambaye unampeleka katika kukubali hitimisho la shida yake kwa mfano unaweza kuanza kumshauri kwa maneno kama Hili no wazo zuri sana, au huu ni mwanzo mzuri, au Biblia inasema kuwa jambo hilo ni dhambi,au hivyo haikupaswa kufanyika au natarajia utaonyesha mabadiliko
ii.                   Anza kutafasiri mambo - kwa mfano Mwitikio unaoonyesha kutaka kufundisha au mtu kufafanua jambo kwa nguvu ili kubadilisha tabia Fulani badala ya kuuliza swali kwanini unaweza kutengeneza sentesi isemayo Inaonekana unataka kusema kuwa…, au Inaonekana unategemea kuwa…
iii.                  Tumia uwezo wa kutegemeza – Hapa mshauri anapaswa kuanza kumuinua mshauriwa, kwa kumtia moyo ili ushauri uweze kueleweka na mshauriwa aweze kuwa na uhakika au kuchochewa, hapa unaweza kutumia misemo kama Oh! Watu wengi hupatwa na mambo kama hayo, au naamini watakuelewa, au mambo yatakuwa mazuri
iv.                 Uliza maswali yenye lengo la kufanya uchunguzi zaidi kwa mfano Je mkeo analichukuliaje hili? Na ilikuwaje baada ya hapo? Ahaa! Ok! Sijui kama nimekuelewa vema, Hebu nifafanulie zaidi swala hili.
v.                   Kuwa na uelewa hii ni hali ya kuwa na ufahamu unaotaka kuonyesha kuwa una mwitikio na kuwa unamuhurumia mshauriwa na hapa unaweza kutumia misemo kama hii inaweza kuwa ni ngumu sana …au kwa hiyo umesema , kwa kweli ulikuwa na wakati mgumu sana mtu mmwingine asingeweza!.
vi.                 Anza kutoa ushauri hii hutokea baada ya kuwa umemsoma  na kumuelewa mshauriwa kuwa anafikiri ni jambo gani linaweza kujenga au kuondoa tatizo kwa hiyo hapa utakuwa na semi kama mimi naona au hebu na mimi nichangie  kwa nini usijaribu kuzungumza na mumeo kuhusu hisia zako n.k

Kwa msingi huo basi endapo utakuwa umeitumia kanuni hiyo hapo juu (FATUKA).bsi utakuwa na nafasi nzuri ya kuwa na uwezo wa kushauri kulingana na tatizo husika

-       Namna ya kuandaa mjadala STRUCTURING INTERVIEWS

o   Kuandaa mjadala kunajumuisha
1.       Jiandae kuwa na ujuzi wa tatizo la mteja wako
2.       Amua kama mshauriwa anaweza kurudi kwa ajili ya ushauri
3.       Amua namna ya ratiba ya mjadala na muda utakaotumika
4.       Weka mazingira yenye uhakika kwa mshauriwa kuwa mazungumzo yenu yatakuwa siri yenu
5.       Fafanua kanuni za kuonyesha ushirikiano na ile kweli kuwa anawajibika kuwa muwazi kwa faida yake
6.       Na mdhihirishie kuwa hakuna tiba ya kichawi inayoweza kuleta suluhu ya matatizo yake isipokuwa kuyakabili

6. Stawisha hali ya usalama wa kihisia EMOTIONAL CATHARSIS.

-       Usalama wa kihisia ni hali ya kumfanya mshuriwa kujiachia kuwa huru na kuweza kuachilia hisia zake ili kusafisha akili inasemekana moja ya mambo muhimu sana katika kufanya ushauri ni pamoja kumuachilia mtu kuwa wazi kimawazo na kihisia kuzunguka tatizo alilo nalo hii inaponya kutoka katika shida binafsi individual conflicts.
-       Hali ya mtu kujiachia kihisia inatokea tu pale kunapokuwa na mazingira mazuri yanayoruhusu mshauriwa kujiachia kihisia na mshauri kuichochea hali ya kumfanya ajiachie kihisia hili linaweza kufanyika mahali salama na hapa mtu atajisikia huru kuzungumza na kujiachia kihisia Hapa mshauriwa anweza hata kulia machozi kwa sauti kubwa bila kuhofia kusikiwa na watu na kujieleza kwa uhuru

Matokeo mazuri ya ya usalama wa kihisia POSITIVE OUTCOMES OF EMOTIONAL CATHARSIS
-       Mtu anapojiachia kihisia anaondoa sumu ya maumivu yaliyoumiza nafsi ya mtu hali ya kujiachia kihisia inaondoa hali ya kupooza, kukata tama na inakuwa ni msaada wa ndani wa kuondoa hukumu na matatizo ambayo hayangeweza kutibika

SOMO LA SITA: AINA MBALIMBALI ZA USHAURI

1.      Ushauri wenye kutia moyo; SUPPORTIVE COUNSELING

-       Lengo kuu , Lengo kuu la ushauri wenye kutia moyo  ni pamoja na kumsaidia mshauriwa katika maisha yake  ya kila siku na hivyo mchungaji atatumia njia inayoongoza ,inayolea inayotia nguvu hata wakati wa matatizo

Ø  Kuongoza – ni kumpeleka mtu katika uelekeo ulio sahii, ni kumuonyesha njia
Ø  Kulea – Ni kuonyesha kujali na kujihusisha na maisha ya kila siku ya mshauriwa
Ø  Kutia nguvu – ni kumfanya mtu aimarike
Ø  Kuhamasiha – ni kumfanya mtu atende katika hali Fulani
Ø  Kuhakikishia – ni kumuwekea mtu hali yenye usalama.
A.       Njia ya kufanya ushauri wenye kutia nguvu METHODS OF SUPPORTIVE COUNSELING
1.       Tengeneza mazingira ya kufariji, Gratifying Dependency Needs kutia moyo kulisha, kuhamasisha kuongoza, kufundisha na kuweka mipaka
2.       Tengeneza mazingira ambayo mshauriwa atakuwa na uwezo wa kujieleza Emotional Catharsis kiasi cha kuweka matatizo yake nje akiamini kuwa kuna usalama
3.        Ni muhimu kiufahamu mtu huyo ameumizwa kiasi gani Objective Review of the stress situation Mtu aliyeumizwa  anakuwa karibu sana na tatizo alilo nalo kuliko kawaida na hivyo anashindwa kuielewa hali yake kuwa iko vipi na kujisahiisha kwani anaiona kwa ndani yeye mwenyewe  kwa hivyo mshauri yuko pale ili kumsaidia kuona uhalisi wa mambo wazi na kuona uzito wake katika namna inayofaa
4.        Hudumia hali ya kujilinda nafsi Aiding the Ego Defenses: mwanadamu anapokuwa anapitia hali Fulani ngumu akili zake zinajiandaa kujilinda lakini kujilinda huko sio sababu ya kupata suluhisho la kudumu baadhi ya hali za kujilinda huwa zinahitajika kwa ajili ya kutatua matatizo ya ghafla na mchungaji anapaswa kumsaidia muhusika  kuchukuliana na tatizo na kumpa muda wa kuondoka katika mshituko kisha kushughulika naye baadaye badala ya kumshambulia mara nyingi watu wengi wanapokuwa wametoka katika hali za kujilinda kwa sababu ya mshituko wanarudi katika hali ya kawaida  na kutambua tatizo lao na kisha kukubali kuwajibika na kubeba hatia na hapa ndipo ambapo mchungaji sasa anaweza kuwajibika kumjenga muhusika na kushughulikia tatizo lake
5.        Kubadilisha hali halisi ya maisha Changing Life Situation msaada wa kivitendo unaweza kutolewa na mchungaji kama sehemu ya ushauri ni pamoja na kumsaidia muhusika, aidha kupata kazi au kusaidia kupatikana kwa makazi ya muhusika na familia yake na kutoa msaada wenye kujenga.
6.        Tia moyo hali ya kuchukua hatua mahususi Encouraging Appropriate Action: wakati mwingine mtu anpopatwa na tatizo kunakuweko hali ya kupooza na kushindwa,kuanguka na kujidhuru au kujiua ni wajibu wa mchungaji basi kuwapa baadhi ya watu jukumu la kushughulika na muhusika ili kustawisha uhusiano na mtu huyo na kumfanya asijisikie mpweke au aliyetengwa njia hii huitwa kitaalamu Action Therapy hapa kinachofanyika ni kumfanya mshauriwa atende wakati njia ya kjuu inataka mshauri atende
7.        Tumia vyanzo vya kidini Using Religious/Spiritual Resources hapa inahusisha maswala ya maombezi, kujitoa, kufundisha na vijarida au tracts maandiko njia za kutia moyo na ushauri wa kichungaji.
B.      Aina za ushauri wenye kutia nguvu TYPES OF SUPPORTIVE COUNSELING

Ø  Ushauri wa kushughulika na mgogoro CRISIS COUNSELING
Hu ni ushauri wa kushughulika na matatizo yanayojitokeza katika maisha ya kila siku kivitendo bila kutarajia au katika namna isiyopendeza na ambayo hali zetu za kujilinda zinakuwa bado hazija jiandaa na kama mgogoro au tatizo ni kubwa au baya sana hisia zinakuwa kali sana na hali ya kukosa faraja kwa namna isiyotegemewa hujitokeza na wakati mwingine hata tatizo la ugonjwa mkubwa unaweza kutokea.
Kuna aina kuu mbili za matatizo ya Kimgogoro.
a.       Mgogoro endelevu DEVELOPMENTAL CRISES
     Migogoro hii ni ya kawaida na hutokea kwa mtu awaye yote kadiri tunavyokua, ni migogoro inayojumuisha namna tulivyozaliwa, tunavyoishi nyumbani, tunavyokwenda masomoni, tunavyochumbia, maswala ya ndoa, maswala ya ujauzito, namna ya malezi, miaka ya ujanani, kufiwa na wazazi, kustaafu, kifo cha umpendaye, haya yote yanaweza kusababisha migogoro ambayo inaweza kusababisha hali zetu za kuweza kubeba au kuchukuliana kuathiriwa

b.      Migogoro inayotokea kama ajali ACCIDENTAL CRISES
Hii ni migogoro inayojitokeza katika hali isiyo ya kawaida na katika hali isiyoweza kutegemewa  na kwa kawaida hutokea pale mtu anapopoteza  kile ambacho kwake ni cha muhimu sana au anaamini ni chanzo kwa utoshelevu wake, hii inaweza kuwa kupoteza kazi, kupoteza fedha, kuvunjiwa heshima, au kupata ajali au matukio ya vita na maswala ya ukimbizi

Mchungaji kama mshauri ambaye yuko makini kwa mahitaji ya watu waqliosumbuka na matatizo ya aina mbalimbali atachukua muda mwingi kushughulika na migogoro hii ya kimaisha iliyojitokeza na kutoa ushauri

Njia zisizo za kiafya za kuchukuliana na Migogoro ya kimaisha.
i.                     Kukataa tatizo lililojitokeza Denial that a problem exist
ii.                   Kukataa au kujaribu kufunika tatizo kwa nia mbadala kama vile kunywa sana Pombe
iii.                  Kukataa kutafuta au kukubali Kusaidiwa
iv.                 Kushindwa kujielezea au kuona kinyume cha hali halisi Inability to express or master negative feelings
iv.                 Kushindwa kulifanyia au kulipitia au kutafuta chanzo cha tatizo
v.                   Kushindwa kutafuta suluhu
vi.                 Kutafuta visingizio, kukwepa kuwajibika au kumalizia hasira kwa wengine
vii.                Kujitenga na marafiki aun kwenda mbali na familia

Mshauri anayeshughulika na migogoro anapaswa kuwa makini  na kujihadhari na kudhuriwa au kuumuzwa kamamatokeo ya kushughulika na hali halisiya muathirika kwa msingi huo ili kumsaidia unaweza kuwa mbali na muhusika na kuanza kutumia njia bora za kuweza kuchukuliana na migogoro katika njia zilizo za kiafya za kuchukuliana na mgogoro.

Njia zilizo za kiafya za kuchukuliana na mgogoro ya kimaisha
i.                     Kukubali kukabiliana na tatizo
ii.                   Kukubali kupanua ufahamu wa mtu mwenye tatizo mfano 1Thesalonike 3;13-18
iii.                  Kujieleza na kuzifanyia kazi mawazo yaliyokinyume na ghisia kama njia ya kukubali hatia na kujirekebisha
iv.                 Kuwajibika kuchukuliana na tatizo Daniel 9;4-11
v.                   Kujaribu kutafuta njia za kulibeba tatizo na kuchukuliana nalo
vi.                 Kutenganisha kinachobadilika na kisichobadilika
vii.                Kukubali kuwa umeshindwa na kukubali kuchukuliana na mzigo huo na kujiona mwenyewe kujichunguza
viii.              Kufungua njia za kuwasiliana na wengine miongoni mwa ndugu jamaa au marafiki au watu wanaoweza kutoa msaada wa kitaalamu Yakobo 5;14
ix.                 Kuchukua hatua hata kama ni ndogo katika kushughulika na tatizo kwa namna ya kuhakikisha kuwa unajenga
                Uzuri wa nia bora za kushughulika na mgogoro
Ni muhimu kufahamu kuwa migogoro hii ya kimaisha ni rahisi lakini ni hatari ina maumivu ina migandamizo,haibebeki na lakini inabadilisha tabia zetu na utu wetu na inatusaidia kukua na kumpelekea mtu kuwa na hatua kubwa za uvumilivu na nguvu yakobo 1;3-4,warumi 5;3-4.

Ø  Vunja kizuizi cha kufanya ushauri STOP GAP COUNSELING

Jambo hili linahusiha swala zima la kutumia njia za kumtia nguvu mshauriwa aliyesumbuliwa mpaka afikie hatua ya kukaa sawa, Kwa bahati mbaya wachungaji wengi wanafikiri kuwa kumsaidia mtu ni mpaka akubaliane na tatizo lakini ukweli ni kuwa wachungaji wengi hawana muda katika huduma zao za kichungaji na kwa sababu hiyo wanasisitiza jambo lifanyike tu kwa maslahi ya faida zao wanashidwa kuwa na muda wa kutafuta kujua matatizo ya ndani sana ya jamii zao ili kwamba wajishughulishe kutatua au hata kujifunza kutoka kwa wataalamu wa maswala ya ushauri na watumishi wenzao ambao wangeweza kuwasaidian hata mawazon Fulani ni namna gani wanaweza kubeba mizigo na kuwasaidian wahusika wanaopatwa na shida na hivyo hujikuta wakiwa mbali na wanaowashauri na kutokujua matatizo yao kwa undani.

Ø  Ushauri wenye kutianguvu ulio endelevu  SUSTAINING COUNSELING

§  Ni uhsuri ambao kwamba unaendeleza ushirikiano na mshauriwa ambao utachukua muda mrefu kabala ya kuzungumza neye
§  Aina hii ya ushauri imekuwa ikitumika na mtu ambaye ana hisia zisizo kali sana ambaye haumizwi kwa haraka au mwenye tatizo sugu au mzee
§  Lengo la aina hii ya ushauri ni kumtia nguvu mshauriwa na kumpatia namna mbalimbali za kufanyia kazi hata kufikia kuwa katika hali yake ya kawaida

Ø  Ushauri wenye kuchochea ukuaji. SUPPORTIVE GROWTH COUNSELING

§  Ni ushauri wenye kuchochea hali ya ukuaji kwa kutumia mbinu za kisaikolojia kulingana na maeneo ambayo mtu huyo amekulia au anaishi
§  Kwa mafano kama una kundi la watu waliokomaa ambao wana tatizo kama la kwake basi kuna mambo makuu matatu amabayo yanaweza kufanyika
-       Hali ya mtu kuweza kuchukuliana na tatizo lake inachochewa anapokuwa nao
-       Hali ya kutiwa moyo na wengine inamsaidia mshauriwa kuvunja hali ya kukata tama na kuwa na uwezo wa kuchukuliana na tatizo alilo nalo
-       Inamsaidia muhusika kuondoa upweke
2.       Ushauri wenye kuelimisha EDUCATIVE COUNSELING

A.       Maelezo;

Ushauri wenye kuelimisha ni ushauri unaojumusha mawasilianao yenye aina Fulani ya maarifa au imani na njia mbalimbali za stadi za kiushauri ndani ya shughuli nzima ya kufanya ushauri kama sehemu ya mchakato wa kufanya ushauri kwenyewe.
Ushauri elimishi ni tofauti na aina nyingine za ushauri kwa sababu unathamani ya kutoa elimu na ujuzi mkubwa wa kugundua tatizo kutimiza malengo kuwasiliana na kusaidia

C.      Malengo ya ushauri Elimishi .THE GOALS OF EDUCATIVE COUNSELING.

§  Kumfanya mshauriwa agundue Kweli, apate wazo aone uthamani, aamini aongozeke ashughurike aelewe mahitaji ya ya mtu nini mtu napenda na namna gani mtu naweza kuchukuliana na hali ya halisi ya matatizo yake.

§  Kuwasilisha kweli moja kwa moja ni kumsaidia mshauriwa kugundua kweli anazopaswa kuzifahamu hata kama ni kwa kupitia kusoma n.k.

§  Kumsaidia mtu kuwasilisha taarifa ili kusaidia uelewa na hii inapanua ufahamu wake  na kumpa kufanya uamuzi wenye busara kukabiliana na hali ngumu na zenye kujenga

§  Kwa ufupi hatua hii ina mambo ya msingi katika swala la kugundua na kuwasiliana  na kutoa maarifa yanayohitajika kwa mshauriwa kusaidika kwa hekima
Mambo matano ya kuwasiliana kuhusu mahitaji ya mshauriwa
1.       Mpe kweli na taarifa zinazomuhusu
2.       Mpe mawazo au ushauri na namna ya kufanya uamuzi ibaki kwake
3.       Mshauri kutumia vyanzo vinavyoweza kutumika na kumuhusu kulingana na hali yake
4.       Msaidie kukutana na hali halisi.
5.       Mpe shuhuda zinazoweza kumtia nguvu kulingana na hali zake         

D.      Hatari ya ushauri Elimishi DANGERS OF EDUCATIVE COUNSELING.

§  Hatari ya kukubali kushawishika kwa mshauriwa
Unapotoa ushauri unaoelimisha ni rahisi sana kutoa msukumo kwa mshauriwa na kumsababishia kuchukua mawazo yako yatokanayo na ushawishi wa msukumo huo na hivyo kuweza kumfanya achukue uamuzi ulio kinyume na matakwa yake
§  Kunakuweko hatari ya kuikosea mamlaka
Hatari hii ni ile inayoweza kusababishwa na kutoka katika kuwa mwenye mamlaka kuelekea katika kutumia mamlaka yaani unaacha sehemu yako kama mshauri na kuiingilia hali ya mshauriwa na kumuamuru kidikteta kwa ajili ya ushawishi wako Yesu aliwafundisha watu akiwa Kama yeye aliye na mamlaka lakini hakuwa dikteta Marko 1;22.
§  Taarifa zenye kuhukumu vibaya
Kuna hatari ya kufikiri kuwa taarifa pekee inaweza kutosheleza kumfanya mshauriwa kukubali kirahisi rahisi kwa kufikiri labda kwa sababu nimesema basi iatasaidia bila kujali kuwa ni wazo gani tumelitumia haijalishi wazo hilo likoje na lina hekima kiasi gani ni muhimu kufahamu kuwa si sehemu ya mshauriwa mpaka amelikubali wazo baada ya kulichuja na hatimaye kulikubali kwa ajili yake.
§  Kutia moyo utegemezi.
Katika aina hii ya ushauri kuna uwezekano wa kumfanya mshauriwa kuwa tegemezi katika maisha,ni kweli unaweza kumsaidia kiushauri yaani ni ushauri wenye kutia moyo sana na wenye kuonyesha kujali hususani kwa watu wenye migandamizo na tunarizishwa na hali zao tegemezi lakini hili linapoongoza katika hali kubwa tegemezi Mchungaji anapaswa kujitoa taratibu katika aina hii ya ushauri kwa kutoa ushauri wa aina nyingine wenye kuongoza kwenye kujitegemea.
§  Hatari ya kuhukumu vibaya mafunzo
Kuna hatari hatari ya kupeleka mafunzo Fulani na taarifa Fulani ambazo ni wazi kuwa ni njema kwa mshauriwa kwa sehemu, kunaweza kujitokeza ujifunzaji wa kweli kabisa kuhusu wazo fulani kwa msingi huo ili mtu awe na wa kujifunza lazima kuna wazo linguine litagongana na wazo jipya na kama uhitaji ni lazima basi mtu atahitaji wazo jipya kama kuna kitu kipya kimejitokeza

3.       Ushauri wenye kukabibliana  CONFRONTATIONAL COUNSELING

A.      Ushauri wenye kukabiliana ni nini?
Huu ni ushuri wa moja kwamoja wenye kumleta mshauriwa kukabiliana na tatizo lake moja kwa moja
B.      Lengo la ushauri wenye kukabiliana
i.                     Ni ushauri unaomlazimisha mshauriwa kukabiliana na tatizo lake kama ni dhambi au hali yoyote ngumu
ii.                   Ni kumsaidia muhusika kuweza kuendeleza nguvu ya kimaadili na kuepuka kufanya tatizo kama hiulo tena wakati mwingine baadaye ni kama unakomesha kuwa muhusika akome kufanya aina hii ya kosa tena ni njia yenye maumuvu haina kupaka mafuta
C.      Aina za matatizo yanayohitaji ushauri wenye kukabiliana
i.                     Tendo lolote lisilo la kimaadili au kitendo cha kikatili
ii.                   Aina yoyote ya tendo ambalo mtu binafsi au jamii au kanisa la mahali pamoja au kile ambacho maandiko yanafundisha kuwa si sahii.
iii.                  Jambo lolote lile ambalo linasababisha hatia au hali ya kujisikia hatia kihisia
iv.                 Kukabiliana na mafarakano ya kundi au migawanyiko, au kutokuelewana na migomo katika kanisa.
D.      Ufunguo wa Ushauri wa wenye Kukabiliana.
§  Ufunguo mkubwa wa aina hii ya ushauri ni KIBALI
-       Hapa maana yake ni kuwa Mshauri lazima awe ni mtu anayekubalika sana kwa mshauriwa ili ieleweke kwamba kinachokataliwa ni tabia mbaya lakini mtu Yule bado tunampenda vilevile
-       Mshauriwa ni lazima akubali kuwajibika kwa ajili ya tatizo alilolifanya sio swala la kujua tun bali aelewe kuwa amefanya makosa.

E.       Mbinu zinazotumika katika kufanya ushauri wenye kukabiliana.

i.                    Mkabili CONFRONTING
Hii ni njia mojawapo ya kushughulika na mtu mwenye tatizo  na ni moja ya njia za kichungaji katika ushauri wa kichungaji mara nyingi hujumuishwa uangalifu katika kutumia mamlaka ya mtumishi ingawaje mchungaji anapaswa amkubali mahsuriwa na ikumkabili ikiwezekana na mkabiliwa ni lazima akubali kukabiliwa.

ii.                   Kuungama CONFESSION: Mchungaji ni lazima ahakikishe kuwa muhusika anakubali kukiri makosa yake au ahatia yake.

iii.                Msamaha  FORGIVENESS
Ni muhimu sana kumuhakikishia mshauriwa kwa habari ya msamaha kutoka kwa mungu na kuwa pia ni lazima ajisamahehe mwenyewe.

iv.                 Malipizi RESTITUTION:
Ni lazima mchungaji umsaidia muhusika kufanya uamuzi ulio sahii, afanya mambo mema yenye kujenga ,aonyeshe wema kwa mtu aliyemkosea yaani kama kunauwezekano wa kwenda kwa mtu aliyemkosea na kufanya mapatano na wahusika ni muhimu wakikubali kwa vile walivyiokwazwa wao pamoja na wengine.

v.                   Upatanishi RECONCILIATION: baada ya hatua kadhaa ni muhimu sana kwa mchungaji kuhakikisha kuwa upatanishi unafanyika kati ya muhusika na Mungu kisha muhusika na wale aliowakosea na kuhakikisha kuwa kama ni uarafiki unarudia katika hali yake ya kawaida ,amani inakuwepo na mawasiliano yanaendelea na kusababisha mtu huyo kukubalika au kujikabidhi tena kwa Mungu.

vi.                 Ukuaji wa kiroho SPIRITUAL GROWTH:
Ujenzi wa kiroho katika njia mbalimbali ikiwemo maombi, uisomaji wa neno la Mungu Biblia na kumtegemea Roho mtakatifu kutachangia ukuaji wa kiroho baada ya kutokea kwa amtatizo.

F.       MAANDIKO NA USHAURI WENYE KUKABIBLIANA.

Kukabiliana katika agano jipya kunazungumzwa kama kuelezana ukweli katika upendo sawa na Waefeso 4;15 kupeana ukweli ni kuzuri sana kama kutafanyika kwa uangalifu na kwa njia ya upendo, mshauri ambaye anazungumza ukweli asipokuwa anajali au kuonyesha upendo atazalisha hisia za kukataliwa au hakli za kujitetea kutoka kwa mshauriwa

WAGALATIA 2:11 Tunaona Paulo mtume akimkabilia Petro ambaye kwakweli alistahili kulaumiwa

2SAMUEL 12:1-12 Tunamuona nabii Nathani akimkabili Daudi kuanzia na kuufunua ukweli kuhusu matendo ya Daudi na kumafanya asikie hatia ya kile alichokifanya na hatimaye kukubali toba na kukiri kisha kupokea mshamaha na badiliko huu ni mafano mzuri wa ushauri wenye kukabiliana.


G.     HATARI WAKATI WA KUKABILI
Kukabili ni kama dawa kali sana inapotumika bara bara inaweza kuleta uponyaji lakini pia kuna hatari kubwa sana inapotumika vibaya
i.                     Hatari ya kutumia Udikteta - halii hii inapoptumika vibaya hususani kwa wachungaji inaweza kupelekea hali ya wao kujisahau na kujiona kama watu wengine ambao hufikiri kuwa wakati wote wao wako sawa na wengine tu ndio wakati wote wanakosea, kwa ujumla watu namna hii ni wale wanaoamini kwamba wakatui wote unapaswa uitii mamlaka na wanatarajia kuwa mshauriwa atafanya kila wanachokitaka swan a jinsi wanavyotaka.
Udikteta hauwezi kuwa na matokeo endapo kutakosekana uvumilivu na upendo na kumbuka kuwa funguo muhimu hapa ni kukubalika
ii.                   Swala la maadili - Mtu anapoishi juu ya kiwango cha maadili kule tu kuishi kwake ni hukumu kw2a watu wasio na maadili, kwa hiyo unapotaka kufanya ushauri wenye kukabili ni muhimu sana kwako kuhakikisha kuwa unaishi sawa na maadili ili uwe na mamlaka ya kuwambia wengine nini cha kufanya utawezaje kuelekeza wengine wafanya kile ambacho wewe hukifanyi huo ujasiri unautoa wapi, lengo kuu likiwa kumfanya mshuriwa kutambua makosa yake na kugundua kuwa anawajibika juu ya hilo.
iii.                Mshambulizi mageni.
Baadhi ya watumishi wanaweza kuwakabili watu kwa mashambulizi mageni kwa hiyo ni muhimu kutofautisha kati ya ushauri wa kukabili na Hasira zako, kwa hiyo pale unapokemea uovu usimwage hasira zako juu ya mshauriwa kwani matokeo yake inaweza kuwa ni kudhuru badala ya matokeo kuwa mazuri au yanayokusudiwa.

4.        USHAURI KATIKA MASWALA YA NDOA NA FAMILIA.

A.      MAMBO YANAYOCHANGIA KUMFANYA MCHUNGAJI KUWA MSHAURI MZURI WA MASWALA YA NDOA NA FAMILIA

1.       Mkao wenye faida STRATEGIC POSITION
Wachungaji wana nafasi nzuri sana ya kuwa washauri wazuri wa maswala ya ndoa na familia kuliko aina nyingine za washauri, ana nfasi kwa maswala ya vijana, wanaojiandaa kwa aajili ya kuoana, wakati wa harusi, kwa ajili ya kujihusihsha na maswal aya furaha na huzuni katika matukio mbalimbali ya kifamilia na hivyo kumfanya mchungaji kuwa na nafasi nzuri za kuweza kushauri familia na ndoa za jamii

2.       Mkao wa kimafundisho STRATEGIC INSTITUTION
Wachungaji wana nafasi ya kuifundisha jamii katika mkakati wa kimafundisho kwa sababu kimsingi wana nafasi ya kuzifikia familia kwani katika ngazi hii ndiko watu wanako kulia, wanakoharibika na wanakoweza kubadilishwa, Kupitia ndoa ambao ndio msingi wa kila familia, mchungaji ana nafasi ya kuchangia kiakili, kiroho,na kimwili ukuaji wenye afya kuaznia na wanandoa wenyewe na hata , wadhamini,watoto wao na hata wajukuu wao.

3.       Matatizo ya kindoa MARRIAGE CRISIS:
Yafuatayo ni baadhi ya changamoto za ndoa na familia ambazo hujitokeza kwa wingi katika nyakati za leo na kuonyesha wazi kuwa kweli ndoa hiyo iko katika wakati mgumu au ina mgogoro.
·         Kutishiana ama kupeana talaka
·         Kutawanyika au kufarakana kwa familia
·         Uchungu wa kupita kawaida wa mke
·         Watoto kuwa na tabia mbaya au kubakwa
·         Tabia mbaya za kipindi cha mpito kwa watoto
·         Swala la mtu kutaka kujiua
·         Hali ya kutokufurahiana tendo la ndoa au kunyimana, maumivu au kukosekana kwa furaha
·         Kuweko kwa ukimwi n.k.
·          
4.       Kubadilishana wajibu ROLE CHANGES.

Katika nykati za leo kumekuweko na wimbi kubwa la wanawake na wanaume kubadilisha na wajibu na kufikia hqali ya kutokutambua wajibu wa kila mmoja na hivyo kusababisha mtikisiko wa mahusiano na kutikisa misingi ya mahusiano katika ndoa nyingi, hali ya wanawake kutaka au kudai kuwa wana haki sawa na wanaume na kuwa wanaweza kushiriki sawa katika kila kitu ikiwemo hata kufanya maamuzi kumepelekea familia nyingi na ndoa kuwa katika hali ya migogoro

B.                  ASILI YA MIGOGORO KATIKA NDOA
Migogoro katika ndoa imejengeka katika msingi wa mahitaji ya aina mbili ya kibinadamu, misingi inayomvutia mwanaume na ile inayomvutia mwanamke katika kila aina ya mahitaji kwa ajili ya kujiridhisha, kuridhika kimahitaji kunategemeana nguvu ya ndoa yenyewe na kutokuridhishwa katika kila sehemu ya hitaji la kibinadamu la wana ndoa linaweza kupelekea kuweko migogoro katika ndoa.

Aina kuu mbili za mahitaji.
1.       Mahitaji ya kiutu PERSONALITY NEEDS.
i.                     Hali ya kustahili
ii.                   Uhuru wa ndani
iii.                  Hali ya kumaanisha mambo
iv.                 Uhusiano wenye uaminifu
v.                   Hitaji la kupendwa
vi.                 Jitaji la kiulinzi
Hali yoyote inayopelekea mahitaji ya kiutu kuingia katika matatizo inaweza kusababisha migogoro.

2.       Hitaji la kingono SEXUAL NEEDS
Mahitaji ya kingono ya kike au ya kiume yana aina zake za changamoto kisaikolojia, kuna uhitaji wa ndani sana uliofichika unaohitaji kuridhishwa au kutoshelezwa na kama hautoshelezwi katika jinsia hizo mbili zinapokutana pamoja katika ndoa basi kuna uwezekano wa mwanamke au mwanaume kutafuta utoshelevu huo kwa mwingine na kwa kweli ni jambo lisilokanushika kuwa kuna hitaji kubwa la kingono linalohitaji kutimizwa ambalo hatuwezi kulikana.

C.                  BAADHI YA VYANZO VYA MATATIZO KATIKA NDOA.
1.                   MAWASILIANO MABAYA NEGATIVE INTERACTION:
Mawasiliano yanaweza kumaanisha ni kitu gani kila mmoja anakifanya katika mchakato mzima wa kuonyesha mwitikio kwa mwenzake, wanasaikolojia wametumia swali hili katika kujaribi kutafiti ni namna gani watu wanaingiliana katika ndoa Je unakunywa kwa sababu mkeo ana kelele, au ana kelele kwa sababu wewe unakunywa?

2.                   Mawasiliano mabaya huweza kusababishwa na maswala kadhaa yakiwemo yafuatayo
a.       Kukosekana kwa mawasiliano au mawasiliano kuwa duni
b.      Hali ya kukataliwa
c.       Hali ya kutokuwa sawa na majibu ya mkato
d.      Hali za kushambuliana
e.      Hali za kukosoana kila wakati

Kazi kuu za mshauri hapa ni
·         Anapaswa kisimama kama mpatanishi
·         Anapaswa kuwa kama nguzo ya mawasiliano
Wajibu huo unaweza kumsaidia yeye kuingiliana vema na watu waliokosana na kusaidia wao wanandoa kupatana na kuacha kuumizana na kuacha kuchochea mgogoro unoweza kuwapeleka pabaya

                                       NAMNA YA KUPANUA WIGO WA MAWASILIANO







Ili kuruhusu muingiliano Mchungaji kama mshauri anapaswa kuhakikisha kuwa anapanua wigo wa kuvunjika kwa mawasiliano,kuvunja hali za kuumizana kihisia,kuondoa hali za kukataana, na mgogoro wa kihisia , kuachwa kwa majibu ya mkato na kukosoana

3.                   KUANGALIWA WAJIBU WA NDANI INTERNALIZED ROLE IMAGES:
Kila mwanandoa ana aina ya mtazamo namna gani mwenzake anapaswa kuwa mtazamo huu hauko nje uko ndani huu unajengeka kutokana na wazazi wa kila mmoja walivyokua, na kile watu walichokiona mama yake akikifanya anatarajia mke wake naye akifanye, na kile mke alichokiona baba yake akikifanya anatarajia kukiona mume wake akikifanya , kazi ya mshauri itakuwa ni kupanua wigo wao wa kimtazamo ili uweze kuwa matazamo wa hali halisi jambo hili linawezekana tu pale inapotumika njia ya kuelimisha yaani ushauri elimishi kwa kuwafundisha upekee alio nao kila mmoja  na kuwa kama wana ndoa wanapaswa kuchukuliana

4.                   Kukosekana kwa maarifa LACK OF KNOWLEDGE.
Baadhi ya wana ndoa hawana maarifa na matatizo mengine katika ndoa zao husababishwa na hali hiyo na maarifa hayo yamo katika maswala makuu matatu hivi mfano
a.       Maswala ya fedha.
b.      Maswala ya tendo la ndoa
c.       Maswala ya malezi na mipango ya kifamilia.
Ni wajibu wa mshsuri kuwasilisha ujuzi kulingana na eneo linalohusika au lenye tatizo.

5.                   Dhambi. SIN
Hili ni moja ya Sababu ya matatizomakubwa sana katika ndoa na kwa kawaida hujumuisha
·         Zinaa
·         Hali ya kinafiki
·         Kukosekana kwa uaminifu
·         Ubinafsi

Kwa msingi huo kukabiliana kunakoongoza katika toba, Msamaha na upatanisho ni muhimu kunapokuweko na matatizo makubwa na kujadili sababu muhimu za kuzitendea kazi baadaye

6.                   Misukumo kutoka nje EXTERNAL PRESSURES.
Wakati mwingine maswala ya matatizo ya ndoa huweza kuwa mabaya au husababishwa kuwa mabaya kwa sababu ya misukumo kutoka nje au kutokana na hali za migandamizo hali hizi ni pamoja na
·         Wahusika kutoka nje yaani mawifi, n.k ambao huwa na matakwa kadhaa dhidi ya wana ndoa
·         Watoto ambao mahitaji yao na kuweko kwao kunaleta mwingiliano wa ndani kati ya mwanaume na mwanamke na wakati mwingine wanaweza kuwa ukuta kati ya wana ndoa.
·         Marafiki ikiwa ni pamoja na marafiki wa jinsia tofauti ambao huchukua muda kati ya wanandoa aidha mmoja wao au wote kwa pamoja au kwa nyakati toafauti.
·         Kazi ambazo zinahitaji mume au mke kuchukua muda na kurudi akiwa amechoka na hivyo kuwafanya wana ndoa wakiwa na muda usiotoshelezana

D.                  JINSI YA KUDHIBITI MATATIZO YA KINDOA.

1.       Fundisha kanuni za Kibiblia kuhusu ndoa
Mungu ndiye mwanzilishi wa ndoa na ndiye aliyemuumba mwanaume na mwanamke na ametoa muongozo wa kibiblia ni namna gani wanapaswa kuishi na majukumu waliyo nayo kila mmoja, miongozo hiyo ni lazima ifundishwe kwa uwazi majumbani na makanisani na kuonyeshwa mfano kutoka kwa kiongozi kanisani ni moja ya maswala ya muhimu sana. Hivyo mshauri mchungaji anapaswa kuwa mfano huo wa kuigwa vinginevyo itakuwa ngumu kushauri.

2.        Sisitiza umuhimu wa ndoa, utajiri uliomo katika ndoa na kujitoa katika tendo la ndoa.

§  Ni muhimu kusisistiza umuhimu wa ndoa kwa muda wakutosha na kuwa juhudi kubwa ionyeshwe katika kushughulika na matatizo hayo aidha tia moyo watu kuipa ndoa uthamani wa hali ya juu na kuipa kipaumbele zaidi ya kitu chochote
§  Watie moyo wana ndoa kujihusisha na
-       Semina mbalimbali za ndoa
-       Kusoma vitabu mbalimbali vyenye kutoa msaada wa maswala mbalimbali ya ndoa na kusikiliza kaseti zinazohuso maswala ya ndoa
-       Watie moyo kufanya mambo pamoja  na kwa ajili ya kila mmoja
-       Wasaidie kustawisha  kipaumbele chao katika maisha na kufanya kazi kuelekea katika kutimiza malengo hayo
3.       Wafundishe kanuni za mawasiliano na namna ya kutatua matatizo.
§  Wafundishe namna ya kuchukuliana kila mmoja kwa madahaifu ya mwenzi wake.
§  Wafundishe umuhimu wa kila mmoja kumsikiliza mwenzake na kujifunua kumkubali mwenzi wake na kumuelewa isha kuchukuliana naye kama alivyo.
§   Wafundishe umuhimu wa kuhurumiana na kuchukuliana kuwa wazi kwa kila mmoja na mwenzi wake
4.       Wafundishe kuhitaji ushauri pale inapobidi.
§  Kwa baadhi ya wanandoa kutafuta ushauri kwao inakuwa kama aibu na inaonekana kwao ni kama wameshindwa au wanatoa nje maswala yao ya ndani, lakini inaweza kusisitizwa hata kupitia madhabahuni kuwa kuna umuhimu wa kuwaona ashauri kama sehemu ya kutia nguvu hali yao ya kindoa Mtu mmoja alisema hivi njia mojawapo ya kujua nguvu ya mtu ni kujua udhaifu wako
§  Hata hivyo ushauri ni muhimu kama utatolewa mapema kabla ya kusubiri matatizo yatokee na kurundikana na hatimeye kushughulikiwa wakati hali ikiwa mbaya.
E.                   BAADHI YA MASWALI MUHIMU UNAYOWEZA KUYAULIZA WAKATI WAUSHAURI WA MASWALA YA NDOA
§  Kwanza jiulize kama wanandoa hao wanaweza kuwa pamoja au kwanza kila mmoja peke yake?
-       Ndoa ni uhusiano na matatizo ya ndoa hujumuisha watu wawili kama mijadala inaweza kufanyika  pamoja basi mapatano yatakuwa ni matokeo makubwa nay a haraka
-       Ingawaje wakati mwingine unaweza kugundua kuwa miongoni mwa hao wanaohitaji ushauri mmoja anataka ushauri na mwingine hataki  na kuna maeneo ambayo mmoja aun wote wana matatizo ambayo ni ya siri na yanaweza kuwa faida kutatua tatizo endapo watatsikilizwa tofauti tofauti.
-       Kumbuka kuwa hata kama unawaona labda mwanandoa mmoja ndiye tatizo kubwa zaidi ni muhimu kuwa katikati usionyeshe kukosoa mmoja na kumkandamiza mwingine



§  Je inakuwaje unapomshauri mtu wa jinsia tofauti?

-       Kadiri iwezekanavyo ni muhimu kufahamu kuwa kumshauri mtu wa jinsia tofauti na yako ni swala la hatari sana hivyo hakikisha kuwa kunakuweko watu wengine hata kama ni mbali kidogo lakini wawepo.
-       Kama n I muhimu sana kufanya hivyo basi ni lazima uwe na maarifa ya kutosha, na maombi ya kutosha au uwe na mkeo, ama kiongozi wa kanisa kwani nao wana wajibu mkubwa wa kujua nani anamsaidia nani nini, hata kama hawajui kwa undani yale mnayoshauriana lakini ni muhimu kwa usalama wenu wako na mshauriwa na kama kuna uwezekanao basi aina hizo za ushauri zifanyike katika eneo lililo wazi ofisini au maeneo mengine ambayo watu wanapita.

§  Je kuna haja ya kuwa na Muda maalumu kwa ajili ya ushauri?

Kumekuwako na utafitu unaobainisha kuwa ushauri unaofanyika ndani ya muda mfupi umekuwa na matokeo mazuri sana kuliko ule unaochukua Muda mrefu hasa wa majuma kwa majuma.

§  Je kuna umuhimu wa kutunza siri za ushauri?

Kwa kweli mshauriwa anahitaji kuwekewa uhakika kwamba kila kinachozungumzwa kitakuwa ni siri na kuwa itabaki kuwa hivyo
Kama mshauri anamuhusisha mkewe kwa undani sana maswala ya mshauriwa basi hilo linapaswa kuwa wazi sana kwa muhusika kuwa maswala hayo yatakuwa bayana kwa mke/mume wa mshauri.
Maswala ya ndani ya ushuri hayapaswi kamwe kuchukuliwa kwenye bomba yaani madhabahuni na kutolewa mifano katika mahubiri ama vinginevyo usinukuu jina la mshauriwaa au dalili zinazoweza kudhihirisha

5.       Ushauri wa jumla au ushauri wa kimakundi

A.  Maana ya ushauri wa kimakundi Group Counseling.
·         Ni ushauri unaohusu kushirikishana ain a za hisia, mawazo na uzoefu katika hali ya heshima na Ufahamu.
B.      Kikundi fulanmi katika kanisa kinaweza kujihusisha na ushauri wa kimakundi
·         Kikundi kidogokatika kanisa kinaweza kikaandaliwa kushughulika na watu wenye upweke na hatimaye wakafaidika kuona uzuri wa ukristo kupitia  mahusiano yanayofanyika kupitia uhusiano huo ulioundwa  na hivyo kupitia wengine Mungu anatumia kikundi kuleta uponyaji makundi ambayo Mungu huweza kuyatumia ni pamoja na
o   Makanisa ya nyumbani
o   Makambi ya kanisa hisika
o   Makundi ya wazazi kwa ajili ya kuelimishana
o   Vyama vya vijana
o   Vikundi vya kujifunza Biblia
o   Familia rafiki
o   Kundi la wataalamu
o   Makundi ya waajiriwa
o   Vyama vya akina mama
o   Vikundi vya wasiooa na wajane. N. K.

C.      Shughuli za Vikundi hivyo  ni pamoja na
§  Maombi ya pamoja
§  Usomaji wa Biblia wa pamoja
§  Kushirikiana kwenye kujali
§  Huduma kwa jamii.

-       Kama kundi linaloongozwa na Mchungaji au kiongozi mwingine  aliyeteuliwa  waamini wanaelekeza utendaji wao katika maeneo makuu matatu
§  Juu Kumuabudu Mungu
§  Nje kuwafikia wasiofikiwa
§  Ndani kuwajenga washirika kupitia kubebeana mizigo na mafundisho na ushirika.
D.      Maandiko na ushauri wa kimakundi.
1.       Wanafunzi wa Yesu (Katika injili)
-       Yesu alizungumza na mtu mmoja mmoja kuhusu mahitaji binafsi na alikutana na vikundivikundi baadhi yao wakiwa ni wanafunzi wake ambao alikuwa akiwandaa kwa ajili ya kufanya utumishi baada ya yeye kurudi Mbinguni.
-       Yesu aliweza kuwafundishwa wanafunzi wake alipokuwa akiingiliana nao kimazungumzo kimaisha na kupitia mafundisho maalumu.
               
2.       Nyakati za kanisa la kwanza (Katika Matendo na Nyaraka)
-       Nyakati za kanisa la kwanza wakristo waliyaendeleza mafundisho ya Kristo na huduma kwa kufundisha na kuhubiri, na kutoa ushauri Matendo 2
-       Maswala haya hayakuwa yanaonekana kama jukumu maalumu la mtu maalumu au kiongozi wa kanisa ziliweza kufanyika kupitia wakristo wa kawaida tu walifanya kazi,walishirikiana, na kujaliana kila mmoja na mwenzake na hakuna mtu aliyetengwa nje ya kanisa
-       Kama utasoma kitabu cha matendo ya mitume ni wazi kuwa hawakuwa wanaifanya kazi ya kuhubiri tu bali na kufundisha na kuitiisha jamii na kushughulika na uponyaji wa jamii
                               
E.       Faida zitokanazo na ushauri wa kimakundi.
§  Kunakuwa na uponyaji wa ujumla kupitia mazingira ambayo watu wanakutana nayo katika familia, kazini, shuleni, na mahusiano yatokanayo na jinsia zao na katika jamii na kupitia hali hiyo basi kunatokea uponyaji na kupitia watu waliokutana na changamoto mbalimbali kunakuweko uzima hivyo kunakuweko uponyaji kuna usemi usemao kwa makundi walivunjika moyo na kwa makundi walitiwa moyo.
§  Kunakuweko na kuokoa Muda wakati mwingine ni ngumu kumzungukia kila mtu na kumshauri na kukutana na mahitaji yake lakini ushauri wa kimakundi unasaidia  kuokoa Muda na huku tunakuwa tumewafikia wengi walioumizwa kwa wakati mmoja.
§  Kufundisha wasaidizi wengi watu waliosumbuliwa watapata nafasi ya kujifunza na kusikia njia au mbinu mbalimbali zinazotumiwa na wahusika katika kuwasaidia watu na hivyo baada ya muda unapata wengine wenye uwezo wa kusaidia wengine.
§  Kuponya tatizo la upweke. Uzoefu mmojawapo wa kufanya ushauri wa kimakundi ni pamoja na kuondoa upweke, haliza kuvunjika moyo na kupata shuhuda kama Da nafikiri nilikuwa mtu mbaya sana, lakini sasa naweza kuona shida yangu ilikuwa wapi au naona tatizo kumbe ni dogo sana ukilinganisaha nay a wengine.

§  Kurudisha uaminifu, watu ambao walipoteza uaminifu wanaweza kurudisha uaminifu sasa kupitia wale walio walioponywa kwa ushauri wa kimakundi.

Kanuni ya kuwa na ushauri wa kimakundi wenye mafanikio.
                                                                           i.      Kuweko kwa vigezo vyote vyenye kuwavutia watu.
§  Unda kundi lenye malengo ya kuyafikia matatizo ya kihisia ya mahitaji ya watu aumtu Fulani katika kundi.
§  Elezea wazi kwa kundi kusudi la kundi hilo kwa jamii
§  Lipe kundi hilo jina lisilotishia watu
§  Mchungaji anaweza kumuweka mtu aliyemuamini au kiongozi wa kawaida au mtu Fulani anaweza kualikwa kwa ajili ya mada Fulani
                                                                         ii.      Hakikisha kuwa unaunda kundi dogo linaloweza kutosheleza na kuruhusu muingiliano na uwezo wa kuonana uso kwa uso wakati wa mawasiliano na wahusika wote
                                                                        iii.      Katika wakati Fulani ni muhimu sana kwa kiongozi kuwauliza washirika kueleza kile wanachokitazamia na kupata kutokana na uzoefu wao
                                                                       iv.      Mnaweza kuandaa vitabu au mada au mistari ya muongozo ni namna gani mijadala itaongozwa ili kuondoa hofu na kupata mtiririko unaokwenda kwa mpango na utaratibu.
                                                                         v.      Kiongozi anapaswa kutengeneza mazingira yanayokubalika na kutoa nafasi ya kusikiliza kila mmoja anasema nini, kisha kutia moyo hali ya kuwa wazi na kuwasiliana
                                                                       vi.      Kiongozi ni muhimu kujaribu kupata mwangwi feed back na kujaribu kulisaidia kundi kuwa waangalifu katika mchakato mzima wa muingiliano na mawasiliano.

Jinsi hali ya mambo inavyopaswa kuwa.kwa mfano wakati wa kushughulikia tatizo la ktokukubali kubadilika.
Luka 12; 16-19, na Yohana 5; 1-9.
§  Mada izungumzwe katika hali inayoashiria tatizo linashughulikiwa sasa au tatizo lilioko leo
§  Au inaweza kupangiliwa katika hali inayoonyesha kuwa una tatizo sasa na ukilijumuisha katika mtazamo wa kikristo leo na kuonyesha kama sababu ni za kiroho au udhaifu wa wakristo na kuonyesha kama mkristo anaweza kukubali mabadiliko au hapana.

Njia kuu mbili za kuonyesha hali ya mambo katika maisha tuliyo nayo
1.       Kuridhika na hali hjalisi tulizo nazo leo mfano mafanikio Luka 12;16-19 tajiri huyu aliridhika na kila alichokipata na hakujua kuwa kulikuwa na jambo muhimu zaidi ya hilo
2.       Kuna wakati tunaweza kuufikia tukadhani kuwa tumafika na hatuhitaji kwenda zaidi ya hapo na hatufany bidii zaidi ya ile
Paulo alishinda tatizo kama hili kwa kuwa na tabia ya kutokukubali kuwa amefika Wafilipi 3;12-14.
3.       Hali ya kutokuwa na matumaini ya kubadilika. Yohana 5;1-9.
-       Mlemavu huyu aliyepooza alikuwa amekwisha kupoteza tumaini la kuwa angekuja apone
-       Kuna watu huwa wanasubiri mabadiliko mpaka wanakata tama ya kuweza kutokea kwa mabadiliko
-       Kume njia za mabadiliko ziko na kwa Mungu hakuna lisilowezekana.
3.       Mambo makuu matatu yanayosababisha watu kutokukubali mabadiliko au kufikiri wamefika
1.       Kujilinganisha na wengine Luka 18;9-12 Farisayo na mtoza ushuru.
Ni muhimu kukumbuka kuwa“hatujaitwa kuwa bora kuliko wengine bali tumeitwa ili tuwe bora kwa kadiri itakavyowezekana.”
2.       Kukosa imani Mwanzo 28;10-14 Mungu naweza kufanya zaidi ya tunavyofikiri Waefeso 3;20.
3.       Kuwa na maonao madogo. Weka mawazo yako juu sana gfanya malengo yako katika maisha kwa nguvu na kutumia uwezo wako ,uvumilivu wako na kujipa moyo ili uyafikie na Anthony D’Souza