Ijumaa, 14 Februari 2020

Kunywa mvinyo hakuwafai wafalme wala wakuu!


Mithali 31:4-5Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo? Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.”


 


Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kuwa moja ya swala ambalo lina mjadala mpana sana miongoni mwa wanazuoni wa Kikristo kwa karne nyingi ni pamoja na kuwepo kwa mijadala na maoni tofauti tofauti kuhusu unywaji wa mvinyo au Pombe, Kila dhehebu na wanatheolojia wanaweza kuwa na mitazamo yao kuhusu unywaji wa Pombe, Lakini kupitia kulichunguza neno la Mungu vema utaweza kuona kuwa Biblia ina majibu ya moja kwa moja kuwa Pombe/ulevi ni moja ya dhambi yenye madhara makubwa sana kwa wanadamu. Na inazungumza kwa upana sana matokeo mabaya ya matumizi ya mvinyo kuliko mvinyo wenyewe. Na kuhitimisha kuwa hakuwafai watu wa Mungu.
Ni muhimu kufahamu kuwa watu walioitwa na Mungu yaani watu waliookoka yaani waliompokea Yesu na kumuamini wanafanyika kuwa wana wa Mungu ona

Yohana1:11-12 “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;“
 
kwa kuwa Yesu anaitwa mfalme wa wafalme na Bwana wa Mabwana hii ni wazi kuwa waliookoka au waliomuamini moja kwa moja wanakuwa wafalme au wana wa ufalme kutokana na kumuamini Yesu, Mungu amekusudia tuwe watawala pamoja naye, wafanya sheria pamoja naye, makuhani pamoja naye, waamuzi pamoja naye, waalimu pamoja naye na ndio maana unaweza kuona katika maandiko wanaitwa uzao mteule,Ukuhani wa kifalme,taifa takatifu na watu wa miliki ya Mungu, kwa msingi huo kila amwaminiye Mungu ni Mfalme, Na Yesu Kristo mwenyewe  ndio mfalme mkuu yaani mfalme wa wafalme ona katika

Ufunuo 19:16
Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.

Kwa msingi huo kila Mkristo pia ni mkuu yaani mtawala ni watu ambao Mungu amewakusudia kuwaweka katika kiwango kikubwa na cha juu sana hivyo watu wa aina hii Mungu hakukubali kuwaruhusu wanywe Pombe.

1Petro 2:9Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
Katika maandiko watu wenye kujiheshimu, na waliotaka kujiweka karibu na Mungu, viongozi na wafanya sheria watawala, makuhani walitakiwa kuishi maisha ya kiwango kikubwa na cha juu kuliko watumwa hawa ndio wanaotajwa kuwa hawapaswi kutumia mvinyo, Watu ambao Mungu ameyaweka maisha ya watu wake katika mikono yao kila mtu aliye katika ngazi ya kufanya maamuzi na kuongoza na kufundisha watu wa Mungu, hapaswi kutumia mvinyo kwa mujibu wa maandiko matakatifu.

Kunywa mvinyo hakuwafai Wafalme wala wakuu:

Kama tulivyoona katika utangulizi  na Mstari wa Msingi wa somo hili Mungu katika mpango wake alikataza watu wote muhimu, hususani wafalme na watawala na waamuzi  wanadhiri, walimu wa sheria (rabbis) na makuhani kutokutumia mvinyo kabisa, Sababu kubwa ya kuwakataza watu hawa ni kwamba wao ni wahudumu wa ngazi ya juu kabisa katika kazi za Mungu na wanaopaswa kufanya maamuzi kwa mujibu wa sheria za Mungu, wao ni watu wanaopaswa kuhesabika kama watu wenye hekima na kielelezo hivyo hawapaswi kujiingiza katika maswala ya unywaji wa pombe, Mungu aliona Pombe kwao itakuwa ni yenye kuwavunjia heshima na kuwaharibu katika utendaji wa Maamuzi yao ya kila siku na kuipotosha sheria ya Mungu kwa msingi huo Mungu aliwatarajia kwamba wataishi kwa viwango vya juu zaidi vya mamlaka ya kifalme na hivyo hawakupaswa kutumia mvinyo, Biblia inayataja makundi kadhaa ya watu wa Mungu wanaopaswa kujihadhari na kujitenga na Divai au mvinyo kuwa ni Pamoja na wafalme, watawala, wakuu,wanadhiri, waamuzi yaani mahakimu na majaji, watu safi, manabii wakubwa wenye heshima, Maaskofu, waangalizi, mashemasi, wakristo na wanawake wakubwa wanaotarajiwa kuwa walimu wa wanawake wachanga hawa wote walipaswa kujihadhari na mvinyo:-

Mfano

a.       Wafalme na wakuu Mithali 31:4-5Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo? Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.” Wafalme na watawala Mungu alikiwakataza kutumia mvinyo au kujihusisha na unywaji wa Pombe kwa sababu Pombe ingewaongoza katika kuvunja uadilifu na kupotosha hukumu ya Mungu. Moja ya mambo ambayo Isaka aliweza kujuta sana ni pamoja na kugundua kuwa hakutenda haki kwa mwanae Esau kwa kumbariki Yakobo badala ya Esau, Tunajua mapenzi ya Mungu na mpango wake kwa Yakobo, tunajua pia kuwa Esau alikwisha kuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza, tunajua pia kuwa Isaka alikuwa haoni vizuri, tunajua pia kuwa Rebeka alifanya mpango yeye na mwanaye Yakobo kupata mbaraka ule lakini Mvinyo unatajwa kuwa ilikuwa ni mojawapo ya sababu ya Isaka kutokuamua mambo vema

Mwanzo 27:24-29Akamwuliza, Wewe ndiwe kweli mwanangu Esau? Akasema, Ndimi. Akasema, Niletee karibu nami nipate kula mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki. Akamsogezea karibu, naye akala; kisha akamletea MVINYO, AKANYWA. Isaka, baba yake, akamwambia, Njoo karibu sasa, ukanibusu, mwanangu. Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba alilolibariki BWANA. Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo. Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe

unaweza kuona kuwa Isaka baada ya tukio hili aliogopa na kutetemeka mno kwani alijua kuwa hakutenda haki hakunyoosha hukumu na kuwa hakukuwa na namna ya kutengua  yeye alikuwa amevunja sheria za utamaduni wa kumbariki mwana mkubwa kama mzaliwa wa kwanza hivyo alitetemeka sana na kuogopa mno lakini tayari Yakobo alikuwa amekwisha barikiwa

Mwanzo 27:33 “Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa.” Mungu anataka wafalme wasiwe walevi ili waweze kufanya maamuzi ya haki na kutokupotosha hukumu, kila mtawala, au mtu mkubwa au mtu aliye katika ngazi ya kufanya maamuzi hapaswi kutumia mvinyo kwa sababu anaweza kupindisha haki ya Mungu anayopaswa kuitoa kwa wanaostahili na kwa wanyone anaowaongoza. Kwa msingi huo wana wa kifalme na mabinti wa kifalme watawala wa familia ya ufalme wa Mungu hawapaswi kutumia mvinyo!

b.      Makuhani Walawi 10:8-11Kisha BWANA akanena na Haruni, na kumwambia, Usinywe divai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu; kisha, mpate kupambanua kati ya yaliyo matakatifu na hayo yaliyo ya siku zote, na kati ya yaliyo najisi na hayo yaliyo safi; tena mpate kuwafundisha wana wa Israeli amri hizi zote ambazo BWANA amewaambia kwa mkono wa Musa.Kutokunywa mvinyo au Pombe lilikuwa moja ya agizo la viongozi wa Kiroho katika agano la kale yaani makuhani, wao walikuwa wamewekwa wakfu kama vyombo vitakatifu vya kumtumikia Mungu na kufundisha watu neno la Mungu, kufanya kosa hili kungepelekea wao kupata adhabu ya kifo, kwa Mungu kiwango chochote cha ulevi kwao kulihesabika kuwa ni kinyume na viwango vya uadilifu, Hekima na utii wa kiongozi wa kiroho, Mtu hawezi kuwa mlevi na pia wakati huo huo akajazwa Roho Mtakatifu kwa hiyo makuhani hawakujihusisha na pombe. Kutokana na tafasiri ya andiko hili Marabi wa kiyahudi hawakuruhusu muamuzi “Jugde” au Hakimu kuendesha kesi ikiwa itabainika kuwa amekunywa hata glasi moja ya pombe, aidha walimu (Rabbis) katika Israel hawaruhusiwi kufundisha endapo watabainika kuwa wamekunywa pombe!, Ni mfano gani ataonyesha kwa anaowafundisha, na anawezaje kupambanua mema na mabaya na kuonyesha kuwa anamuheshimu Mungu akiwa na ulevi, mwilini mwake hiyo hata leo Marabi katika Israel hawatumii mvinyo hata kidogo.

c.       Wanadhiri Hesabu 6:1-5 “Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Nena na watu wa Israeli, uwaambie, Mtu mume au mtu mke atakapoweka nadhiri kubwa, nadhiri ya Mnadhiri, ili ajiweke wakfu kwa Bwana; atajitenga na divai na vileo; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yo yote ya zabibu, wala asile zabibu, mbichi wala zilizokauka.  Siku zote za kujitenga kwake asile kitu cho chote kilichoandaliwa kwa mzabibu, tangu kokwa hata maganda.Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, wembe usimfikilie kichwani mwake; hata hizo siku zitakapotimia, ambazo alijiweka wakfu kwa Bwana, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele za kichwani mwake zikue ziwe ndefu.” Wanadhiri ni watu waliojifunga kwa Mungu, ili kujitunza katika uwepo wake hawa nao iliagizwa wasijitie unajisi ikiwa ni pamoja na kutokusogelea au kukaribia ulevi au kunywa Pombe. Mtu anayeweka nadhiri maana yake amejitenga kwa makusudi ya kutembea na uwepo wa Mungu, anajitenga ili awe karibu na Mungu, Mungu ni mtakatifu sana ni wazi kuwa mtu hawezi kumkaribia Mungu au kutunza uwepo wa Mungu kama atakuwa mlevi, hivyo wote waliojifunga kwa nadhiri katika maandiko sheria ya kwanza kabisa katika maisha yao ilikuwa ni kutukutumia, mvinyo au pombe ya aina yoyote ile.

d.      Waamuzi Waamuzi 13:3-5 “Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume. Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi; kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.Waamuzi katika agano la kale walikuwa ni viongozi wa kijeshi waliowaongoza waisrael kupigana vita dhidi ya adui zao wakati wa vita, lakini vilevile waliwaamua watu wakati wa amani, walitegemea uhodari wa Roho Mtakatifu katika maongozi yao walikuwa ni wakombozi wa uonevu dhidi ya watu wa Mungu kwa wale waliowaonea, Mungu hakutaka wanywe mvinyo wala kileo, Ni wazi kuwa hata kamanda wa majeshi hawezi kutimiza wajibu wake vema vitani kama atakuwa amelewa, Mungu aliwataka waamuzi wasinywe na muamuzi maarufu zaidi Samsoni Mungu hakuruhusu anywe!


e.      Watu safi “Devoted” Yeremia 35:1-8,14 “Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, katika siku za Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, kusema, Enenda nyumbani kwa Warekabi, ukanene nao, ukawalete nyumbani kwa Bwana, katika chumba kimoja, ukawape divai wanywe. Basi nikamtwaa Yaazania, mwana wa Yeremia, mwana wa Habasinia, na ndugu zake, na wanawe wote, na nyumba yote ya Warekabi; nikawaleta ndani ya nyumba ya Bwana, ndani ya chumba cha wana wa Hanani, mwana wa Igdalia, mtu wa Mungu, kilichokuwa karibu na chumba cha wakuu, nacho kilikuwa juu ya chumba cha Maaseya, mwana wa Shalumu, bawabu; nikaweka mabakuli yaliyojaa divai, na vikombe, mbele ya wana wa nyumba ya Warekabi, nikawaambia, Nyweni divai. Lakini wakasema, Hatutakunywa divai; kwa maana Yonadabu, mwana wa Rekabu, baba yetu, alituamuru, akisema, Msinywe divai, ninyi wala wana wenu, hata milele; wala msijenge nyumba, wala msipande mbegu, wala msipande mizabibu, wala msiwe nayo; bali siku zenu zote mtakaa katika hema; mpate kuishi siku nyingi katika nchi ambayo mtakaa ndani yake hali ya wageni. Nasi tumeitii sauti ya Yonadabu, mwana wa Rekabu, baba yetu, katika yote aliyotuamuru, kwamba tusinywe divai siku zetu zote, sisi, na wake zetu, na wana wetu, na binti zetu; 14. Maneno ya Yonadabu, mwana wa Rekabu, aliyowaamuru wanawe, kwamba wasinywe divai, yametimizwa, na hata leo hawanywi; maana waitii hiyo amri ya baba yao; lakini mimi nimesema nanyi, nikiamka mapema na kunena, bali ninyi hamkunisikiliza mimi.” Hii ni Familia ya wakeniz jamii ya watu walioambatana na Israel kutoka Jangwani ni wana wa ukoo wa Kalebu na ukoo wa Yethro kuhani mkuu wa Midian, walishika sana mausia ya wazazi wao na Mungu aliwabariki na kuwatumia kama mfano wa utii akiwafundisha wana wa Israel, kutokana na maisha yao ya uadilifu wamekuwa kielelezo na mfano wa kuigwa katika kushika maagizo, kutokana na wana wa Rekabu kuyashika sana maagizo ya baba yao hususani kutokunywa mvinyo  Mungu aliibari familia hii na kusema kuwa siku zote hata milele Yonadabu mwana wa rekabu hatakosa mtu wa kusimama mbele zake yaani wa kumtumikia milele ona Yeremia 35:18-19 “Naye Yeremia akawaambia watu wa nyumba ya Warekabi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa sababu mmeitii amri ya Yonadabu, baba yenu, na kuyashika maagizo yake yote, na kutenda sawasawa na yote aliyowaamuru;  basi, kwa sababu hiyo, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Yonadabu, mwana wa Rekabu, hatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu hata milele. 
           

f.        Viongozi wakubwa katika Israel ambao walikuwa kielelezo kikubwa cha imani ya wayahudi waliokuwa uhamishoni huko Babeli hawa ni Daniel, na Hanania , Mishael na Azaria ambao pia walijulikana kama Shedrak, Meshack na Abednego, walipata vyeo vikubwa sana, walikuwa na hekima mno na walikuwa mashujaa wa imani na watu wenye msimamo mkali hawa hawakuruhusu kuwa najisi kwa kunywa, Na matokeo yake waoa wakawa na akili mno na maarifa na ujuzi mkubwa sana na Daniel akawa hodari wa kujua ndoto na maono  Divai ona Daniel 1:8-16 “Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi. Basi Mungu alimjalia Danieli kupata kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi. Mkuu wa matowashi akamwambia Danieli, Mimi namwogopa bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi kwa kufanya hivyo mtahatirisha kichwa changu mbele ya mfalme. Ndipo Danieli akamwambia yule msimamizi, ambaye mkuu wa matowashi amemweka juu ya Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria, Tafadhali utujaribu sisi watumishi wako muda wa siku kumi; na watupe mtama tule, na maji tunywe. Kisha nyuso zetu zitazamwe mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula chakula cha mfalme; ukatutendee sisi watumishi wako kadiri ya utakavyoona. Basi akawasikiliza katika jambo hilo, akawajaribu siku kumi. Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme. Basi yule msimamizi akaiondoa posho yao ya chakula, na ile divai waliyopewa wanywe, akawapa mtama tu. Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.” Unaweza kuona habari ya Daniel, Shedrack, Meshack na Abednego hawakuwa watu wa kawaida walikuwa watu maalumu mno wenye kuheshimiwa sana Ujuzi, Elimu na hekima viliwakalia, kumbe ukitaka kuwa mlevi umechagua daraja la chini sana! Hawa wanahesabika kama watu waliomuheshimu Mungu kwa kiwango cha juu sana na kuwa mashujaa wa imani waliozima miali ya moto, moja ya siri yao kuu ni kuwa mbali na Mvinyo.

g.       Mtu mkuu kama Yohana Mbatizaji.  Luke 1:15 “Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.Kuna sababu kubwa mbili kwa nini Yohana atakuwa mkuu mbele za Bwana na kwanini hakuruhusiwa kunywa divai/ mvinyo? Ni kwa sababu alijazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mamaye na pili alikuwa na wajibu wa kuwaongoza wengi au kuwarejeza wengi kwa Bwana Mungu wao Luka 1:16 “Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao”. Kwa kazi ya kufundisha na kuwaelekeza wengi kwa Mungu hakupaswa kutumia mvinyo. Malaika anasema kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana, Hatakunywa divai wala kileo unaona kumbe kama unataka kuwa na heshima kwa Mungu ni vema na wazi ukajiepusha na pombe au kile, usinywe mvinyo wa aina yoyote.


h.      Maaskofu au waangalizi 1Timotheo 3:1-3 “Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;Neno askofu kwa kiyunani linasomeka kama “EPISKOPOS” neno hili maana yake ni mtu mwenye huduma ya uangalizi, au uchungaji, Uangalizi wa roho za watu ni uchungaji, watu wa namna hii ni watu wanaopaswa kuwa vizuri kiroho na kiuadilifu, Neno la Mungu limeweka sifa kadhaa na viwango wanavyotakiwa kuwa navyo wachungaji waangalizi na maaskofu na katika viwango walivyowekewa kimaandiko  kimojawapo ni kutokuzoelea ulevi,  wao ni watu wanaopaswa kuwa kielelezo ni watu ambao wanaangalia  na jamii na wanapaswa kuishi kwa viwango vya juu mno kwa msingi huo hawapaswi kusogelea mvinyo wala kunywa pombe 1Timotheo 4:12 “Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.” Maandiko yanamchukulia kiongozi mchungaji, mwangalizi askofu kuwa ni mtu anayepaswa kuwa safi katika usemi, mwenendo, upendo imani na usafi Hiwezekani kuwa kielelezo katika mwenendo, usemi, upendo, imani na usafi kama anatumia Pombe haiwezekani 1Petro 5:2-3 “lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi.Mungu hatarajii kundi hili kuwa hawatajihusisha na unywaji wa mvinyo kwa sababu wao ni viongozi wa kiroho na wana wajibu mkubwa wa kuwa kielelezo kwa jamii. Neno hili “SI MTU WA KUZOELEA ULEVI” Biblia ya kiingereza Amplified Bible inasomeka “NOT A DRINKER”NIV inasema “NOT GIVEN TO DRUNKENNESS” Biblia ya kiyunani inatumia “ne- Parainon” likimaanisha kutokukaa karibu na mvinyo au kutokusogelea mvinyo, au kula na kunywa pamoja na walevi Mathayo 24:45-51 “Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.”  Unaweza kuona kwa msingi huo maandiko yanaweka wazi kuwa mjoli, mtumwa mwaminifu mtu wa Mungu mwangalizi, askofu, Mchungaji na wenye hekima hawapaswi sio kusogelea ulevi lakini hata kula na kunywa pamoja na walevi, kwa wachungaji hiki ni kiwango kikubwa na cha juu zaidi kwetu

         
i.        Mashemasi 1Timothy 3:8 “Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana,si watu wanaotamani fedha ya aibu.” Ni Muhimu kufahamu kuwa neno “Si watu wa kutumia mvinyo sana” kwa kiingereza “not given to much wine” kwa kawaida neno hilo katika biblia ya kiyunani linasomeka “NOT PAYING ATTENTION TO WINE” kwa msingi huo andiko hili linakataza sio kunywa tu lakini kutokukaribia kabisa mvinyo, Kama maandiko yanaagiza kutokuifuatisha ni wazi kuwa mojawapo ya njia iliyo bora zaidi ya kujilinda na uovu ni pamoja na kutokuikaribia pombe Yakobo 1:27, 1Petro 5:8 Tito 2:12.

j.        Wakristo 1Thesalonike 5:6-8 “Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi. Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku. Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.” Ona pia Waefeso 5:18 “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;” Wakristo wanaaswa kuwa wasilewe kwa mvinyo ambayo ndani yake ina ufisadi neno hilo ufisadi katika biblia ya kiingereza ya NIV linasomeka kama “DEBAUCHERY” ambalo tafasiri yake ni “immoral behaviour” na Biblia ya  kiingereza ya Aplified Bible imetumia neno “DISSIPATION” ambalo maana yake “disapproving behaviour” yaani inasababisha moyo uharibike, inasababisha ufanye matukio yasiyopaswa, inasababisha ujiingize kwenye uasherati au ulevi na madawa ya kulevya na tabia zisizofaa ndio maana Biblia ya Kiswahili imetumia neno ufisadi yaani ni mjumuiko wa matendo yasiyofaa,


k.       Wanawake watu wazima Tito 2:3-5 “Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.” Wanawake watu wazima walitarajiwa kuwa walimu wa kuwafunza adabu wanawake vijana kwa msingi huo hawakupaswa kabisa kujihusisha na mvinyo au ulevi au pombe. Nyakati za agano la kale kama mwanamke angekuwa mlevi aliitwa mwanamke Baradhuli au asiyefaa kitu, Mwanamke mwenye kujiheshimu alipaswa vilevile kuwa mbali na ulevi, Mama wa nabii Samuel yaani Hanna, hakuwahi kutumia mvinyo ona katika 1Samuel 1:13-16Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa. Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai yako. Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za Bwana. Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa kitu; kwa kuwa katika wingi wa kuugua kwangu na kusikitika kwangu ndivyo nilivyonena hata sasa. Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.” Anna amekuwa mwanamke aliye kielelezo katika subira, maombi na kama mwanamke aliyeteseka kutokana na kuwa tasa lakini alimtegemea Mungu, aliomba na kujiweka karibu na Mungu akijifunga katika nadhiri na kujitoa huku akijiepusha na Divai na kileo yaani hakunywa pombe.

l.        Awaye yote anayetaka kutembea katika uwepo wa Mungu na miujiza yake lazima ahakikishe kuwa anajiweka mbali na divai na pombe, Ni muhimu ikakumbukwa wazi na kila mwanazuoni kuwa kama mtu anataka kuufurahia uwepo wa Mungu na kushuhudia matendo yake makuu hapaswi kunywa divai wala pombe, Mungu alitembea na wana wa Israel miaka 40 jangwani ni wazi kuwa Israel walitembea katika uwepo wake moja ya vitu ambavyo kizazi kile walikuwa mabli nacho ni pamoja na Divai na kileo yaani Mvinyo na Pombe ona Kumbu kumbu la torati 29:1-6 “Haya ndiyo maneno ya agano Bwana alilomwamuru Musa alifanye na wana wa Israeli katika nchi ya Moabu, pamoja na agano alilofanya nao Horebu. Musa akawaita Israeli wote akawaambia, Mmeyaona yote Bwana aliyomfanya Farao katika nchi ya Misri mbele ya macho yenu, yeye na watumwa wake wote, na nchi yake yote; yale majaribu makuu yaliyoyaona macho yako; hizo ishara, na ile miujiza mikuu; lakini Bwana hakuwapa moyo wa kujua, wala macho ya kuona, wala masikio ya kusikia, hata leo hivi. Nami miaka arobaini nimewaongoza jangwani; nguo zenu hazikuchakaa juu yenu, wala kiatu chako hakikuchakaa katika mguu wako. Hamkula mkate, wala hamkunywa divai, wala kileo; ili mpate kujua kwamba Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”  

            

Kwa nini kunywa mvinyo hakuwafai Wafalme na wakuu!

1.      Inadhihaki au kuwavunjia heshima wale wanaotumia Mithali 20:1 “Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.” Katika maandiko Biblia inaonyesha matokeo ya pombe kivitendo zaidi, Ni jambo la kusikitisha kuwa Nuhu aliyekuwa mtu aliyapata neema kutokana na uadilifu mkubwa aliokuwa nao yaya na uzao wake hata Mungu akamuokoa na gharika, aliheshimika kama nabii aliyeweza kutabiri na unabii wake ukatimia, lakini ni jambo lenye kusikitisha kuwa Nuhu anatajwa katika maandiko kuwa alikuwa mtu wa kwanza kulima zabibu na ambaye alitengeneza juisi yake na aidha kwa kujua au kwa kutokujua alikunywa pombe akalewa na kujiaibisha sio hivyo tu aliweza kutoa laana kwa mjukuu wake mkubwa kutokana na mwanae kumuona akiwa hana nguo kutokana ana kulewa Pombe Mwanzo 9:20-27 “Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.  Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea. Akasema, Na alaaniwe Kaanani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake. Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa Shemu; Na Kaanani awe mtumwa wake. Mungu akamnafisishe Yafethi, Na akae katika hema za Shemu; Na Kaanani awe mtumwa wake.” Ni wazi na kweli kabisa kuwa pombe ina dhihaka, inaweza kumfanya mtu anayeheshimika sana akapoteza heshima kutokana na vitendo vitakavyofanywa akiwa katika hali ya ulevi.

2.      Inaharibu tabia njema! (Behaviour  changes)  Maandiko yanamtaja Lutu kuwa mtu mwenye haki ambaye Mungu alimuokoa katika miji ya watu walioharibika kwa dhambi miji ya sodoma na Gomorah ona katika  2 Petro 2:7-8 “akamwokoa Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi wa hao wahalifu; maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sheria;” Ni jambo la kusikitisha sana kuona kuwa mwisho wa maisha ya Lutu haukuwa mwema, bindti zake walikuwa na hatia ya kufanya ngono na baba yao, na Lutu alikuwa na hatia ya kukubali kunywa mvinyo kiasi cha kulewa na kushiriki ngono zembe iliyoleta matokeo ya kuweko kwa mataifa ya kipagani baadaye, Biblia  inatuonyesha mfano wa mtu  huyu muadilifu ambaye aliweza kunyweshwa mvinyo na kujikuta akifanya mapenzi na binti zake  ona Mwanzo 19:30-38 “Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili. Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote. Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao. Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena usiku huu, ukaingie ukalale naye. Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo. Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo.” Ngono mbaya zaidi ya baba kufanya mapenzi na binti zake inatajwa hapa katika maandiko ambayo inaonyesha kuwa japo maandiko yalimtaja Lutu kuwa mtu mwenye haki, lakini hakukuwa na uadilifu wa kutosha katika nyumba yake ikiidhinishwa na ushahidi wa mkewe kuangalia nyuma na kugeuka nguzo ya chumvi lakini kuhurumiwa kwa binti zake na yeye mwenyewe kunaifanya dhambi ileile waliyoikimbia huko Sodoma kujitokeza tena kwa kiwango kingine ikichangiwa na ulevi na pombe au mvinyo aliyoipewa na binti zake hii ni aibu na fedheha kubwa! Ni ni dhahiri kuwa mtu na heshima zake mbele za Mungu na wanadamu anaweza kujivunjia heshima hiyo endapo ataendekeza ulevi na unywaji wa mvinyo kweli mvinyo hauwafai wakuu wala wafalme.

3.      Mvinyo inaleta madhara makubwa na hatari za aina nyingi Mithali 23:29-34 “Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu? Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika. Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu; Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira. Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka. Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.”mwisho wa ulevi una maumivu makali sana mwenye hekima anaifananisha na kugongwa na nyoka mwenye sumu kali kama Fira.Wakati mwingine kwa sababu ya ulevi kumetokea magomvi makubwa sana katika familia, watu wengi wenye wazazi walevi wameshuhudia hali ya kukosekana kwa utaratibu katika familia nyingi kufuatia unywaji wa Pombe, watru wana majeraha ya mwili nay a kiroho kutokana na ulevi uliokithiri.

4.       Biblia inasema huwezi kuwa mtu mkubwa na tajiri kama utatumia mvinyo Mithali 21:17 “Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; Apendaye mvinyo na mafuta hatakuwa tajiri.Kutokana na kujihusisha na ulevi watu wengi sana wamajikuta kwenye umasikini mkubwa sana, nimewahi kushuhudia baba mmoja mlevi, akiwa amerejea nyumbani akiwa mgomvi sana kutokana na ulevi, aliamua kuvunja kabati la vyombo na kulibwaga huko, aidha alivunja TV na kuwajeruhi mke wake na watoto na yeye mwenyewe asubui wakati napita nilimuona rafiki yangu ambaye ni mtoto wa ile familia akiwa amejaa damu na kuumia kwa vioo nilipomuuliza ndio akanielezea habari ya yaliyowakuta Pombe inaleta umasikini na maandiko yanakubali hilo na kutoa ushauri kuwa tusiwe miongoni mwa wanaokunywa mvinyo  Mithali 23: 20-21Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa. Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu” Ni wazi kuwa Mungu anataka tufanikiwe na kustawi sana lakini moja ya kikwazo kikubwa cha ustawi wetu ni pamoja na kujihusisha na ulevi, bwana ampe neema kila mmoja wetu kuwa mbali na kileo.

5.       Ulevi unahatarisha usalama wako. Biblia inaonyesha kuwa ulevi unaweza kusababisha maadui zako ama watu wabaya wakaitumia nafasi yako ya kuwa umelewa na wakakuangamiza, ilhali kama ungekuwa hujalewa ungeliweza kuokoa maisha yako 2Samuel 13:28-29Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake, akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, ndipo mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru? Iweni hodari, iweni na ujasiri. Basi watumishi wa Absalomu wakamfanyia Amnoni kama alivyoamuru Absalomu. Ndipo wakaondoka wana wote wa mfalme, wakapanda kila mtu nyumbu wake, wakakimbia.” Watu wengi sana duniani wameuawa kwa sababu ya mvinyo, Bibi yangu mzaa mama alikuwa mwanamke mzuri sana alikuwa na umbile la kisomali, kwa kuwa ni mzigua mwenye asili ya Somalia, alikuwa mzuri sana Joyce na alikuwa mwenye maringo kutokana na uzuri aliokuwa nao watu waliomuonea wivu walimletea chupa ya pombe mchana alipokuwa anasonga ugali, kwa kumwamini mtu huyo alikunywa na akafa ugali ukiwa unaungua na mtot wake mdogo akiwa mgongoni, Adui zako na watu waovu wanaweza kukufanyia mamboi mabaya unapokuwa umelewa, watu wenye kisa na wewe wanaweza kukufanyia mambo mabaya unapokuwa umelewa ona pia 1Wafalme 16:8-10Katika mwaka wa ishirini na sita wa Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha alianza kutawala juu ya Israeli huko Tirza, akatawala miaka miwili.Na mtumwa wake Zimri, jemadari wa nusu ya magari yake, akamfanyia fitina; alipokuwako Tirza akinywa hata kulewa nyumbani mwa Arsa, aliyekuwa juu ya nyumba huko Tirza; Zimri akaingia akampiga, akamwua, katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, akatawala mahali pake”. Wafalme zamani wao wenyewe pia walikuwa Majemadari Ela angeweza kujiokoa au kujihami au kujilinda kama askari jemadari lakini kwaajili ya ulevi, aliweza kuuawa kirahisi, kwaajili ya usalama wako vilevile usinywe, Madereva wengi sana wamesababisha ajali na kupoteza maisha au kusababisha vifo kwa sababu ya ulevi.         

6.       Walevi hawataurithi ufalme wa Mungu 1Wakoritho 6:9-10Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,  wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.Ni ukweli usiopingika kuwa ni vigumu kwa wadhalimu au watenda dhambi wote wa kila aina hawataingia katika ufalme wa Mungu, lakini hata hivyo unaweza kuona maandiko yanawataja walevi pia, kwa msingi huo kama mtu ataendekeza ulevi ni anajiweka katika njia mbaya ya kuurithi ufalme wa Mungu.

7.       Ulevi ni moja ya matendo yasiyo ya Kiroho Wagalatia 5:19-21 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.”   

8.       Ulevi unaongoza katika maovu mengine Hosea 4:10-11 “Nao watakula, lakini hawatashiba; watafanya zinaa, lakini hawataongezeka; kwa sababu wameacha kumwangalia Bwana. Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.” Moja ya jambo ambalo biblia inalielezea hapa ni kuwa ulevi una tabia ya kuambatana na dhambi nyingine, Katika ulevi kuna kamali, michezo ya kubahatisha, lakini vilevile zinaa huambatana na ulevi pamoja na maovu ya aina nyingine haribiko la kitabia la mtu anavyokuwa mlevi ni tofauti na anapokuwa na akili timamu, kwaajili ya ulevi mtu anaweza kufanya ujinga mwingi sana hata kutukana mtu, bila kufikiri, Ulevi unaondoa fahamu, ulevi unaharibu mahusiano na kuondoa heshima hata katika ndoa.

9.      Ulevi unaweza kuvunja mahusiano.

Katika maandiko tunapewa mifano kadhaa ya watu walivuruga mahusiano yao kwa sababu ya ulevi uliopindukia, Mwanadamu ambaye yuko vizuri kiroho na kiakili anapaswa kuwa na na uhusiano mzuri na wanadamu wengine Lakini bibliainaonyesha kuwa ulevi uliokithiri umeweza kuharibu mahusiano ya watu wengi na moja ya mifano ya kibiblia ni pamoja nah ii angalia Esta 1:1-12Zamani za Ahasuero; naye huyu Ahasuero alimiliki toka Bara Hindi mpaka Kushi, juu ya majimbo mia na ishirini na saba; siku zile mfalme Ahasuero alipoketi katika kiti cha enzi cha ufalme wake, huko Shushani ngomeni; mwaka wa tatu wa kumiliki kwake, ikawa aliwafanyia karamu maakida wake wote na majumbe wake; wakuu wa Uajemi na Umedi, watu wenye cheo na maakida wa majimbo, wakihudhuria mbele zake. Akawaonyesha utajiri wa ufalme wake mtukufu, na heshima ya enzi yake bora siku nyingi, maana siku mia na themanini. Hata siku hizo zilipotimia, mfalme akawafanyia karamu watu wote waliokuwapo huko Shushani ngomeni, wakubwa kwa wadogo, muda wa siku saba, katika behewa la bustani ya ngome ya mfalme. Palikuwa na mapazia ya bafta, nyeupe na samawi, yamefungiwa kamba za kitani safi za rangi ya zambarau kwa pete za fedha na nguzo za marumaru; pia na vitanda vilikuwa vya dhahabu na fedha juu ya sakafu ya marumaru, mawe mekundu, na meupe, na ya manjano, na meusi. Wakawanywesha kileo katika vyombo vya dhahabu, na vile vyombo vilikuwa mbalimbali, na divai tele ya namna ya kifalme, sawasawa na ukarimu wa mfalme; kunywa kulikuwa kama ilivyoamriwa, bila sharti; maana ndivyo mfalme alivyowaagiza watumishi-wa-nyumbani, kila mtu afanye apendavyo. Tena Vashti, malkia, naye akawafanyia karamu wanawake ndani ya nyumba ya kifalme ya mfalme Ahasuero. Hata siku ya saba, mfalme alipofurahiwa moyo wake kwa divai, aliwaamuru Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari, na Karkasi, wale wasimamizi-wa-nyumba saba waliohudumu mbele za mfalme Ahasuero, wamlete Vashti, malkia, mbele ya mfalme, amevaa taji ya kifalme; ili kuwaonyesha watu na maakida uzuri wake, maana alikuwa mzuri wa uso. Bali Vashti, malkia, alikataa kuja kwa amri ya mfalme kwa mkono wa wasimamizi-wa-nyumba; kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, na hasira yake ikawaka ndani yake.  Unaweza kuona katika kisa hicho hapo Juu, Mfalme Ahasuero  anaachana na mkewe kutokana na ulevi uliokithiri, yeye alikuwa amelwa sana pamoja na watu wake wote na sasa anataka mkewe aletwe mbele ya watu wote iliawaonyeshe watu jinsi mkewe alivyo mrembo, Malkia mke wa mfalme aliyeitwa Vashtiinaonekana anakataa kutii amri hiyo ya kuitwa mbele za watu na kufanywa kituko, kutokana na kitendo hicho uhusiano wao ulivunjika, Ulevi unavunja mahusiano, umevuruga mahusiano ya watu wengi sana katika jamii, Sio tu mahusiano katika ndoa lakini vilevile hata na watu tuliopaswa kuheshimiana nao ona mfano mwingine katika Biblia ambapo mtu mmoja aliyeitwa Nabal alikuwa na maneno ya jeuri sana yaliyopelekea kuharibu uhusiano wake na Daudi na sababu kubwa ya mtu huyu ilikuwa ulevi uliokithiri 1Samuel 25:5-17Daudi akatuma vijana kumi, Daudi naye akawaambia hao vijana, Kweeni mwende Karmeli, na kumwendea huyu Nabali ili mnisalimie; na hivi ndivyo mtakavyomwambia huyu aishiye salama, Amani na iwe kwako, na amani nyumbani mwako, na amani kwao wote ulio nao. Nami sasa nimesikia ya kuwa una watu wanaokata manyoya kondoo zako; haya! Wachungaji wako wamekuwa pamoja nasi, wala hatukuwadhuru, wala hawakukosa kitu wakati wote walipokuwako huko Karmeli.  Waulize vijana wako, nao watakuambia; basi na wakubaliwe vijana hawa machoni pako; maana tumekujia katika siku ya heri; uwape, nakusihi, cho chote kitakachokujia mkononi, uwape watumwa wako na mwanao Daudi. Basi walipofika vijana wake Daudi, wakamwambia Nabali sawasawa na maneno hayo yote kwa jina la Daudi, kisha wakanyamaza. Naye Nabali akawajibu wale watumishi wa Daudi, akasema, Huyu Daudi ni nani? Na mwana wa Yese ni nani? Siku hizi kuna watumwa wengi wanaomtoroka kila mtu bwana wake! Basi mimi je! Nitwae mkate wangu, na maji yangu, na machinjo yangu niliyowachinjia hao watu wangu wakatao manyoya kondoo zangu, na kuwapa watu ambao siwajui wametoka wapi? Basi vijana wake Daudi wakageuka, wakaenda zao, wakarudi, nao wakaja wakamwambia sawasawa na maneno hayo yote. Kisha Daudi akawaambia watu wake, Haya! Jifungeni kila mtu upanga wake. Nao wakajifunga kila mtu upanga wake; Daudi naye akajifunga upanga wake; nao wakapanda nyuma yake Daudi, wapata kama watu mia nne; na watu mia mbili wakakaa na vyombo vyao. Lakini kijana mmojawapo alimpasha habari Abigaili, mkewe Nabali, kasema, Tazama, Daudi alituma wajumbe kutoka nyikani waje ili kumsalimu bwana wetu, naye akawatukana. Walakini watu hawa walitutendea mema sana, wala hatukupata dhara, wala sisi hatukupotewa na kitu cho chote, wakati wote tulipofuatana nao, tulipokuwako mavueni; watu hao walikuwa boma kwetu usiku na mchana, wakati wote tulipokuwa nao tukiwachunga kondoo. Basi sasa ujue na kufikiri utakayotenda; kwa sababu yamekusudiwa mabaya juu ya bwana wetu, na juu ya nyumba yake yote; kwa kuwa yeye ni mtu asiyefaa kabisa, hata mtu hawezi kusema naye.” Ni kutokana na majibu haya mabovu Daudi alikusudia kumfutilia mbali Nabali na jamii yake yote lakini kupitia mkewe Nabal aliyeitwa Abigaili ambaye alikuwa na akili sana aliweza kumzuia Daudi asimuue Nabali, Hata hivyo baadaye Mungu alimuua Nabali, utaweza kuona aidha katika kisa hiki pia tunaona Abigaili akijiombea kuolewa na Mwanaume asiyetumia mvinyo na kuachana au kutamani mwanaume wake mlevi afe, hii ni wazi kabisa kuwa kutokana na ulevi uliokithiri Mwanamke huyu alikuwa hafurahishwi na mwenendo mzima wa kuwa na Mume mpumbavu ona 1Samuel 25:32-38Naye Daudi akamwambia Abigaili, Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye amekuleta hivi leo kunilaki; na ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe, uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu mwenyewe. Kwa kuwa ni kweli, aishivyo Bwana, Mungu wa Israeli, aliyenizuia nisikudhuru, kwamba hungefanya haraka kuja kunilaki, hakika huyu Nabali asingaliachiwa hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi. Basi Daudi akapokea mkononi mwake vitu vile alivyomletea; akamwambia, Haya! Kwea kwa amani kwenda nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimeukubali uso wako. Kisha Abigaili alimjia Nabali; na tazama, alikuwa amefanya karamu nyumbani mwake, kama karamu ya kifalme; na moyo wake huyo Nabali ukafurahiwa ndani yake, kwa maana amelewa kabisa. Kwa sababu hiyo hakumwambia neno, dogo wala kubwa, hata kulipopambazuka. Ikawa asubuhi, divai ilipokuwa imemtoka Nabali, mkewe alimwambia mambo hayo, na moyo wake ukafa ndani yake, akawa kama jiwe. Tena ikawa, yapata siku kumi baadaye, Bwana alimpiga huyo Nabali, hata akafa.” Unaweza kuona sasa jinsi ambavyo mvinyo na ulevi uliokithiri unavyoweza kuathiri mahusiano katika jamii.

10.   Ulevi husababisha vijana kuwa wakaidi kwa wazazi wao!

Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la vijana kutokuwatii wazazi wao na kuwa wakaidi, Biblia imeagiza watoto kuwatii wazazi wao katika bwana na tunaambiwakuwa hii ni amri ya Mungu yenye ahadi ya vijana kupata heri na maisha marefu ona katika maandiko katika Kutoka 20:12Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.”  Na unaweza pia kuona katika Waefeso 6:1-3Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.” Unaweza kuona kumbe mpango wa Mungu ni kuwabariki watoto pale wanapowaheshimu wazazi wao na sio kuwabariki lakini pia kuwapa maisha marefu, Lakini kutokana na hali ya ukaidi unaosababishwa na ulevi ni jambo lakusikitisha kuwa katika maandiko Mungu aliagiza kuwa kama wazazi watakuwa na mwana mkaidi asiyetaka kutii wala kusikiliza maagizo yaokwa sababu ya ulevi walipaswa kumtoa katika baraza la wazee na angehukumiwa kifo ona Kumbukumbu 21:18-21Mtu akiwa na mwana mkaidi, mshupavu, asiyetii sauti ya baba yake, wala sauti ya mama yake, nao wajapomwadhibu hawasikizi, ndipo babaye na mamaye na wamkamate, na kumpeleka kwa wazee wa mji wake, katika lango la mahali pake; wawaambie wazee wa mji wake, Huyu mwana wetu ni mkaidi, mshupavu, hasikizi sauti yetu; ni mwasherati, tena ni mlevi. Waume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa.” Unaweza kuona ni wazi kabisa kimaandiko kuwa kama ulevi lingekuwa ni swala la uadilifu na linalokubalika mbele za Mungu basi Mungu asingeliweka adhabu kali namna hii, Maandiko ynaonyesha wazi kuwa ulevi unaleta ukaidi na kuharibu baraka ambazo mungu alikuwa amezikusudia kwa watoto.

11.   Nchi ambayo viongozi wake sio walevi imebarikiwa, Kwa kujibu wa Muhubiri mwana wa daudi katika kitabu cha Muhubiri 10:17 “Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto wa watu, Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate nguvu, wala si kwa ajili ya ulevi.” Yaani imabarikiwa nchi ile ambaye mfalme wake anakula kwa wakati ili apate nguvu na wakuu wake hawana muda na ulevi unaweza kuona

12. Ulevi unaharibu mwili wa Mwanadamu
Biblia iko wazi kabisa kuwa miili yatu ni hekalu la Mungu aliye hai, Ni hekalu la Roho Mtakatifi 1Wakoritho 6:19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;Mungu anajihusisha sana na namna tunavyoitumia miili yetu, Matumizi ya pombe katika mwili huufanya mwili kuchakaa haraka kuna madhara mengi ya aina mbalimbali yatokanayo na pombe katika miili yetu, yako madhara ya muda mfupi yasababishwayo na pombe katika miili yatu lakini vilevile yako madhara ya Muda mrefu

Madhara ya muda mfupi ni pamoja na
a.      Kutokuona vizuri kwa vile ulevi unasababisha uoni hafifu
b.      Kuyumba wakati wa kutembea au kushindwa kutembea sawa sawa
c.       Kuharibu hali ya mtazamo na hali ya kihisia, na hivyo kuweza kujinyea kujitapikia, kujikojolea na hata kuwa mgomvi, na kuropoka hovyohovyo
d.      Kutokuweza kupambanua vema jambo jema na jambo baya
e.      Kupumua kwa shida na kukoroma pamoja kuamka ukiwa na maluweluwe, haya ni Madhaya yasababiswayo na ulevi kwa muda mfupi mara baaba ya kunywa pombe
Madhara ya Muda Mrefu

Matatizo mengine yanayoweza kushababsihwa na ulevi endelevu ni Pamoja  na Kuzeeka haraka, Magonjwa ya Moyo, matatizo ya kansa, matatizo ya Kongosho au bandama,  na kuharibika au kuungua ini, kwa ujumla haya ni baadhi ya matokeo ya ulevi, kitaalamu kama wanawake watakuwa wanatumia ulevi wanaweza kuwa na matatizo makubwa zaidi ya kiafya kuliko wanaume na hata kama wanakunywa kiasi tu, Pombe huathiri karibu kila kiungo cha mwili endapo itatumika kwa muda mrefu na pia inamueweka mtumiaji katika uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na magonjwa mbalimbali



a.       Kusinyaa kwa Ubongo -  shrinking brain kisayansi matumizi ya muda mrefu ya Pombe hupelekea tatizo la kusinyaa kwa Ubongo, ubongo ni moja ya sehemu muhimu sana yenye maamuzi yote ya kimwili na kiroho, kuathiriwa kwa kiungo hiki muhimu ni uharibifu mkubwa sana wa uumbaji wa Mungu katika mwili wa Mwanadamu.

b.       Kuathiriwa kwa mfumo wa fahamu – Njia nyepesi nya kujua kuwa Pombe inaathiri mfumo wa fahamu ni namna mlevi anavyozungumza hii maana yake ni kwamba pombe inaathiri utendaji wa Ubongo na hivyo kuharibu mpangilio wa meneno yaani kunakuwa na mwasiliano mabovu yati ya uzungumzaji wako na ubongo, Pia unakuwa na wakati mgumu jinsi na namna ya kutembea na ndio maana inashauriwa kuwa kama unaendesha gari au mitambo ni vema kuacha au kuizia kama umekunywa, Pombe ina madhara makubwa katika mfumo wako wa fahamu, Pombe ina uwezo wa kukufanya usiweze kukumbuka vema na uwezo wako wa kutunza kumbukumbu unakuwa wa Muda mfupi, uwezo wako wa kufikiri unaathiriwa, utendaji wa ubongo wa mbele FRONTAL LOBE unaathiriwa ubongo huu ndio unaohusika na hisia,  na kumbukumbu za muda mfupi,  na uwezo wa kufanya maamuzi. hivyo matumizia endelevu  ya pombe yanaweza kupelekea kuharibika kwa ubongo.

c.       Tabia tegemezi -  Baadhi ya watu wanaokunywa pombe huweza kutengeneza tabia tegemezi ya kihisia na kimiwli kwa pombe, yaani kwao kuja kuiacha Pombe linakuwa swala gumu sana  alcoholic addiction

d.       Magonjwa ya Moyo – Imethibitika kisayansi kuwa unywaji wa Pombe una mchango mkubwa sana katika kusababisha magonjwa ya moyo kama vile shambulio la Moyo, Pressure, na strok yaani kupooza

e.       Kuathiriwa kwa ini – Nchini Marekani zaidi ya watu milioni mbili wanateseka na ugonjwa wa kuathiriwa kwa ini kunakotokana na ulevi, walevi wa pombe wanaweza kuharibu maini yao, aidha wanaweza kuendeleza kuungua kwa ini, kisukari, homa, ngozi kuwa ya njano, kuathiri njia ya mkojo na maumivu na pombe ikiendelezwa inasababisha kifo, kifo kitokananacho na pombe na madhara yanaweza kuepukika tu mtu akiacha kunywa

f.        Bandama – Ni moja ya kiungu muhimu ambacho kazi yake ni kurekebisha mwenendo wa sukari mwilini kwa kuzalisha kemikali iitwayo INSULIN aidha bandama pia ina kazi ya kuchakata chakula tunachokula, unywaji wa muda mrefu unywaji endelevu hupelekea bandama kuungua  na kuanza kusababisha maumivu ya chembe cha moyo, kiungulia na  maumivu mengine makali, kuhara na hatimaye kupunua uzito, aidha pombe iingiapo kwa wingi katika bandama, huongeza uzaliswhaji mkubwa wa Enzymes ambazo ndio zenye uwezo wa kuunguza bandama.

g.       Kuhara -  Matumizi ya pombe kupita kiasi hupelekea kuharibiwa kwa utumbo mdogo na hivyo kupelekea kuwa na tatizo la kuharisha mara kwa mara, na maumivu makali ya tumbo au vidonda vya tumbo

h.       Ugumba na utasa – Matumizi ya pombe kwa muda mrefu huweza kupelekea watu wanaume kwa wanawake kupoteza uwezo wa kuzaa, na pia kuzalisha homoni inayoweza kumfanya mwanaume kuwa kama mwanamke au kuwa na hamu ya kuingiliwa kinyume na maumbile.

i.         Kupoteza nguvu za kiume – kwa kawaida wanaume wengi sana wanywaji huwa wanajidanganya kuwa pombe huwaongezea mashamu shamu katika tendo la Ndoa lakini ni ukweli unaokubalika kitaalamu kuwa matumizi endelevu ya pombe hupelekea walevi kuwa watu dhaifu zana katika utekelezaji wa tendo la ndoa na ulevi kupindukia huweza kupelekea kupoteza nguvu za kiume.

j.         Athari za mfumo wa chakula – unywaji wa Pombe unaathiri mfumo wa usagaji wa chakula, matumizi ya Pombe endelevu yanaweza kusababisha utumbo mwemabamba ushindwe kunyonya chakula kinachohitajika mwilini na matokeo yake hupelekea kuwa na “Kwashakoo” “Malnutrition” na ndio maana wakati mwingine utaweza kuona afya ya walevi ni kama haipendezi na wanakuwa na kitambi fulani kisichi cha kiafya!

k.       Tatizo la Kiwango cha sukari –Bandama  inasaidia mwili uweze kutengeneza Insulin na kutumia vema glucose yaani sukari inayotakiwa kuingia mwilini sasa pale Bandama na ini linaposhindwa kuifanya kazi yake vema kutokana na pombe unaweza kuingia katika tatizo la kupungua kwa sukari mwilini “Low blood sugar” aidha kuharibika huko kwa bandama kunaweza kulifanya bandama kutokuzalisha insulin ya kutosha kutengeneza sukari na inaweza kupelekea kuruhusiwa kwa sukari nyingi sana kuingia katika damu, na mwili wako ukishindwa kuweka uwiano wa sukari inayotakiwa mwilini kinachofuata sasa ni kupata ugonjwa wa kisukari kwa hiyo watu wenye kisukari wanapaswa kuwa mbali na pombe.

l.         Tabia mbaya – ulevi huweza kusababisha hata mtu mwenye akili timamu, na anayeheshimika katika jamii kufanya jambo lisilotarajiwa kutokana na kulewa anaweza kujinyea, kutapika, kujikojolea, kukojoa mahali ambapo sio chooni na hata au kutaka kufanya mapenzi na mtu anayestahili heshima.

m.    Maluweluwe – walevi wengi kutokana na unywaji wa pombe huwa wanaona maluweluwe au kuota ndoto za mchana na ndio maana wakati mwingine unaweza kuona wakizungumza wenyewe njiani ilhali hakuna mtu wa kumuitikia, wengine huimba pambio au kuzungumza kiingereza wakichanganya na kikabila chao

n.       Lugha isiyoeleweka – walevi wakati mwingine kutokana na uwepo wa Pombe wanashindwa kutamka vema maneno yakaeleweka kwa hiyo wanaropoka ropoka tu

o.       Kansa -  Unywaji wa pombe kwa muda mrefu unamuweka mtumiaji katika uwezekano mkubwa wa kupata aina fulani ya kansa kama Kansa ya koo, uharibifu wa kisanduku cha sauti, kansa ya ziwa, kansa ya utumbo mpana na sehemu ya kutolea haja kubwa

p.       Maambukizi katika Mapafu – watu wanaotumia pombe mvinyo wakao katika hatari kubwa sana ya kupata matatizo ya mapafu na kuingiliwa na virusi au bacteria wanaopelekea kupata pneumonia au Tb na matatizo mengine ya kifua

q.       Uchovu – hisia za kuchoka sana huwa zinawapata walevi na hata kupelekea kupata upungufu wa damu, ambao kwa vyovyote unaweza kuwa umesababishwa na ulevi

r.        Vidonda vya tumbo – Kunywa mvinyo kupita kawaida hupelekea kujawa na gesi tumboni na kupelekea uwepo wa vidonda vya tumbo.

s.        Athari kwa mtoto aliyeko tumboni – unywaji wa Pombe unaweza kusababisha mtoto aliyeko tumboni kuwa katika hatari kubwa sana, anaweza kuzaliwa njiti au kufia tumboni au kufa muda mfupi tu mara baada ya kuzaliwa

t.        Kusinyaa kwa mifupa – unywaji wa pombe hupelekea tatizo la kusinyaa kwa mifupa

u.       Kuyumba yumba – kutokana na ulevi mwendo wa mnywa pombe unaweza kubadilika na kuwa wenye kuyumba yumba

v.       Athari kwa afya ya uzazi – Walevi wengi huwa wanajidanganya wakidhani kuwa Pombe huwa inawaongezea burudani wakati wa tendo la ndoa, Lakini ilivyo ni kwamba wanaume wanaokunywa pombe sana wanapoteza uwezo wa nguvu za kiume, unywaji wa pombe unaweza kuathiri, uzwalishaji wa homones zinazochechea tendo la ndoa na pia inaua kabisa hamu ya tendo hilo, wanawake wanaokunywa sana huacha kuona siku zao  za hedhi na hivyo kuwa katika uwezekano mkubwa wa kuwa tasa, wanawake wanaokunywa sana wakati wa ujauzito  wanaweza kuharibu mimba au kuzaa watoto njiti, au mtoto mfu. Aidha kama watazaa mtoto atakuwa na ugumu katika kujifunza, matatizo ya kiafya, matatizo ya kihisia uwezekano wa kuwa na ulemavu.

Kwa hiyo sasa unaweza kuona kwa unywaji wa Pombe tunasaidia kwa kiwango kikubwa kuharibu maisha yetu na ya wengine Pombe ina madhaya Kimwili, kiakili na kiroho na ndiomaana haishangazi kuona kuwa Biblia inaonya watu wasitumie mvinyo, aidha vyanza vongi vya ajali za barabararani pia vimebainika kuwa moja ya sababu zinazopelekea kutokea kwa ajali hizo ni pamoja na ulevi Mungu anataka kutuepusha na swala hili.

Mvinyo au Divai Katika Maandiko.

Tunapoendela kujifunza somo hili sasa ni muhimu kwetu tukaendelea kuangalia kwa undani hasa neno Divai au mvinyo katika maandiko lilimaanisha nini, hii itatusaidia kuweza kutambua ni aina gani ya mvinyo ulitumiwa wapi na kwa sababu gani kwa mfano unaposoma

Luka 7:33-34 “Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo. Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa; nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi.”
          
Hapo unaweza kuona jinsi neno la Mungu linavyoonyesha kuwa Yohana hakutumia divai na Yesu anakiri kuwa alitumia alikunywa, kwa hivyo watu wengi wasio na akili timamu hufikiri kuwa Yesu alikunywa mvinyo
Maana ya neno Divai – Kwa kawaida neno Divai au mvinyo lilipotumiwa katika biblia lilitumika kumaanisha aina kubwa mbili za Divai au mvinyo, neno hili kwa kiibrania linatumika neno “YAYIN” na kiyunani “OINOS” Maneno hayo yalimaanisha Divai au mvinyo  wa aina kubwa mbili

1.       Divai  ya mzabibu iliyochachwa – Fermented grape juice
2.       Divai  ya mzabibu isiyochachwa – Unfermented grape juice

Ni muhimu kufahamu kuwa neno hilo la kiyunani Oinos lilitumika kwa aina zote mbili za juisi ya mzabibu, Kwa hiyo neno oinos lilikuwa neno la jumla la juisi za aina zote mbili, kama vile matumizi ya Mikate iliyochachwa na mikate isiyochachwa, Kwa msingi huo waandishi wa Biblia walijitahidi sana kuonyesha matokeo ya juisi iliyotumika kivitendo ili kusaidia watu waweze kujua ni aina gani ya Divai ilitumika katika tukio husika, Lakini Biblia pia hutumia neno Nzuri, au njema, au tamu au tunda la mzabizu au uzao wa mzabibu kwa divai siyoyochahwa na kuitofautisha na ile iliyochachwa kwa mfano
a.       Waefeso 5:18 “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;” unaweza kuina katika neno hili biblia ya kiyunani inatumia neno Oinos lakini mwandishi anaonyesha kwamba hii ina ufisadi kwa hiyo hapo ni wazi kuwa mvinyo unaotajwa hapo ni ule wenye kulewesha ambao sio sahihi kutumiwa na watu wa Mungu
b.       Ufunuo 19:15 “Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.” Hapa sasa tunaweza kuona tena mvinyo ukitajwa na katika kiyunani neno linalotumika tena hapa ni Oinos sasa tofauti kubwa iliyoko hapa ni kuwa Yesu atakanyaka shinikizo la mvinyo unajua maana yake? Neno shinikizo katika biblia ya kiingereza wanatumia neno “winepress”  yaani ni mashine ya kukamulia zabibu kwa hiyo hapa inazungumziwa mvinyo au divai isiyo na kilevi unaweza kuona ! sasa basi zabibu ile iliyo safi ilipatikana pale shinikizoni inapotengenezwa kabla ya michakato mingne Isaya 16:10 “Na furaha imeondolewa, na shangwe toka mashamba yaliyozaa sana; hapana kuimba katika mashamba ya mizabibu, wala sauti za furaha; akanyagaye hakanyagi divai katika mashinikizo; nimeikomesha sauti ya furaha yake akanyagaye.” Unaweza kuona kwa msingi huu kwamba hata ile iliyokuwa ikikamuliwa na haijachachushwa bado iliitwa Divai au mvinyo kwa lugha ileile kwa aina zote mbili za mvinyo au Divai
c.       Namna walivyohifadhi Divai isiyochachwa – Katika Israel kulikuwa na namna ya kuhifadhi divai isiyochachwa. Maji ya zabibu yalipokamuliwa waliyahifadhi chini ya nyuzi joto 10 Centgrade, walitengeneza chombo na kuiweka divai humo kisha walikiziba chombo kile ili hewa isiingie na maji mengine yasiingie  na walikizamisha chombo hicho ndani ya maji au chombo chenye maji ya baridi kwa kuhakikisha kuwa hakuna sehemu inachungulia nje au kutokea juu waliweka hivyo kwa siku 40 na ukiitia kutkka hapo hakuna uwezekano tena wa juisi hiyo ya mzabibu kuchacha na itaendela kuwa na utamu uleule kwa mwaka mzima

d.        Njia nyingine ya kuhifadhi zabibu ilikuwa ni kuzichemsha.

Je Yesu alitumia Divai au mvinyo wa aina gani?
Yesu na wanafunzi wake walitumia juisiya mzabibu isiyochahwa! Na hakutumia mvinyo wenye kulkevya kabisa Mathayo 26:26-29 “Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.”

Marko 14:22-25 “Nao walipokuwa wakila, alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa, akasema, Twaeni; huu ndio mwili wangu.  Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote. Akawaambia, Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. Amin, nawaambia ninyi, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu.”

Luka 22:17-18. “Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi; Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja.”

Unaweza kuona kile Yesu alikuwanywa na wanafunzi wake kinaitwa mzao wa mzabibu au tunda la mzabibu hii inamaamisha nini? Yesu na wanafunzi wake hawawezi na wasingeliweza kutumia mvinyo uliochwachwa  kwa sababu katika Biblia chachu ilikuwa ni sihara ya dhambi na kwa msingi huo wayahudi walipaswa kuwa mbali na chachu yoyote katika mikate na katika divai mtu ambaye angekuwa na chachu ya aina yoyote hususani wakati wa Pasaka alipaswa kufa kwa mujibu wa Torati ona

Kutoka 12:14-20 “Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele  Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba; siku hiyo ya kwanza mtaondoa chachu yote isiwe katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula mkate uliochachwa tangu siku hiyo ya kwanza hata siku ya saba, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na Israeli. Siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yo yote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu.  Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele.  Mwezi wa kwanza, siku ya mwezi kumi na nne, wakati wa jioni, mtakula mikate isiyochachwa, hata siku ya mwezi ishirini na moja jioni.  Muda wa siku saba isionekane chachu katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula hiyo iliyotiwa chachu, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli, akiwa mwenye kukaa hali ya ugeni, au akiwa mtu aliyezaliwa katika nchi. Msile kitu chochote kilichochachwa; mtakula mikate isiyochachwa katika makao yenu yote.”

Neno la Mungu lilikuwa limepiga marufuku matumizi ya chachu ya aina yoyote yaani “SEOR” au hamira kwa Kiswahili haikupaswa kuwa karibu kabisa nyakati za Pasaka kwa sababu SEOR au chachu iliashiria uharibifu au dhambi Luka 12:1 “Wakati huo, makutano walipokutanika elfu elfu, hata wakakanyagana, alianza kuwaambia wanafunzi wake kwanza, Jilindeni na chachu ya Mafarisayo, ambayo ni unafiki.”

1Wakoritho 5:6-8 “Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima? Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;     basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.”
Kumbe chachu au hamira katika maandiko humaanisha dhambi, kama Yesu na wanafunzi wake wangetumia mvinyo wenye kilevi ni dhahiri kuwa Yesu hangefaa kuwa Pasaka wetu, hangefaa kuwa Sadaka ya ukombozi wa mwanadamu hata kidogo kama Yesu ndiye Pasaka wetu na wakati wa Pasaka chachu haikuruhusiwa kabisa ni dhahiri kama Yesu angetumia chahu yoyote hangefaa kuwa Pasaka yetu Kutoka 13:7 “Mikate isiyochachwa italiwa  katika hizo siku saba mkate uliotiwa chahu usionekane kwako ndani ya mipaka yako yote

Je Yesu aligeuza maji kuwa Divai?

Mojawapo ya hoja kubwa sana ya watu wanaotetea pombe au mvinyo kwa kutumia maandiko hujengwa pia katika muujiza wa kwanza alioufanya Yesu wa kugeuza maji kuwa divai huko Kana- Galilaya katika arusi ambayo yeye alialikwa na andiko linalotumika ni

Yohana 2:1-11 “. Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni. Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.  Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi, akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa. Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.

Je Yesu aligeuza Maji kuwa Divai jibu ni ndio, Lakini ni muhimu kwetu kuwa na ufahamu wa kutosha kuwa ni aina gani ya divai Yesu aliifanya katika muujiza huu, kwa sababu ni ukweli usiopingika kuwa kama Yesu alitengeneza Divai au mvinyo wenye kulewesha basi ni halali kwa watu kunywa mvinyo, ni halali kuuzalisha, ni halali kuuuza, na ni halali kuuhifadhi na sio uvunjifu wa maadili kuunywa na Yesu angekuwa na Mchango mkubwa sana katika uharibifu wa maisha ya Mwanadamu tofauti na tulivyoona hapo juu, Katika vipengele vilivyotutangulia

Balasi moja lilikuwa lina uwezo wa kuingia kati ya ndoo 20-30, na kama utazidisha mara sita maana yake Yesu alitengeneza Divai ndoo kati ya 120-180, na kama hii ilikuwa ni Pombe basi katika harusi ile kulikuwa na ulevi uliopindukia ambao haujawahi kutokea katika harusi yoyote ile

Aidha katika mstari wa 10 tunaambiwa kuwa Divai ile ilikuwa njema sana, hii ina maana kuwa kama kile alichikitengeneza Yesu ilikuwa mvinyo wenye pombe basi kwa ndoo kati ya 120-180 Yesu alikuwa amechangia kiwango kikubwa mno cha pombe katika muujiza wake wa kwanza na hivyo hangeweza kuwa kiongozi asiye na dhambi.

Divai njema aliyotengeneza Yesu katika biblia ya kiyunani hapa linatumika neno “TYROSH” yaani toka kwenye zao la zabibu. ni kama ambavyo “crude oil” ikipitia refining process hutoa petrol, diesel, kerosene etc vivyo hivyo zao la zabibu hutoa divai kileo, divai pure juice, divai dawa, zabibu kavu etc

haya ni majina yanayotofautisha aina hizo kama yanavyoonekana kwenye hebrew bible(tanakh) na greek bible(septuagint)

·         tyrosh pure juice of cana (john 2) yaani ile aliyoifanya Yesu kwa muujiza ilikuwa ni Juice ya mzazbibu isiyochachwa’

·         yayin the most common wine in the bible

·         chekar

·         mamchak

·         gath

Yesu alitengeneza Divai njema yaani Mzao wa mzabibu usiochachwa ! yaani hakukuwa na Pombe pale Kana ya Galilaya, Yesu mwenyewe katika mahubiri yake alikemea ulevi Luka 12:45-46 “Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa;  bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini

Hakuna andiko lolote linalohalalisha mtu kutumia Pombe katika agano jipya na msingi wa kimaandiko umeonyesha na shuhuda za kibinadamu zimeonyesha kuwa Pombe ni tatizo

Hitimisho:-

1.       Warumi 14:21 - Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lo lote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa.
2.       1Wakoritho 6:9-10, Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,. wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.
3.      Warumi 13:13 - Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.
               
4.      Mtu anawezaje kuacha Pombe?
a.       Kwa kumuamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake, my akiokoka anaweza kubadilishwa maisha na kuwa mbali na pombe
b.       Kwa kuomba kama kuna jambo lolote hulipendi mwambia Mungu omba funga na kuomba na Mungu atakusaidia kuwa mbali na pombe

Na Rev.Innocent Kamote.
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima’
0718990796