Mithali
31:4-5 “Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme,
hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo? Wasije wakanywa na
kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.”
Utangulizi:
Ni muhimu
kufahamu kuwa moja ya swala ambalo lina mjadala mpana sana miongoni mwa
wanazuoni wa Kikristo kwa karne nyingi ni pamoja na kuwepo kwa mijadala na
maoni tofauti tofauti kuhusu unywaji wa mvinyo au Pombe, Kila dhehebu na
wanatheolojia wanaweza kuwa na mitazamo yao kuhusu unywaji wa Pombe, Lakini
kupitia kulichunguza neno la Mungu vema utaweza kuona kuwa Biblia ina majibu ya
moja kwa moja kuwa Pombe/ulevi ni moja ya dhambi yenye madhara makubwa sana kwa
wanadamu. Na inazungumza kwa upana sana matokeo mabaya ya matumizi ya mvinyo
kuliko mvinyo wenyewe. Na kuhitimisha kuwa hakuwafai watu wa Mungu.
Ni muhimu
kufahamu kuwa watu walioitwa na Mungu yaani watu waliookoka yaani waliompokea
Yesu na kumuamini wanafanyika kuwa wana wa Mungu ona
Yohana1:11-12 “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;“
kwa kuwa Yesu anaitwa mfalme wa wafalme na Bwana wa Mabwana hii ni wazi kuwa waliookoka au waliomuamini moja kwa moja wanakuwa wafalme au wana wa ufalme kutokana na kumuamini Yesu, Mungu amekusudia tuwe watawala pamoja naye, wafanya sheria pamoja naye, makuhani pamoja naye, waamuzi pamoja naye, waalimu pamoja naye na ndio maana unaweza kuona katika maandiko wanaitwa uzao mteule,Ukuhani wa kifalme,taifa takatifu na watu wa miliki ya Mungu, kwa msingi huo kila amwaminiye Mungu ni Mfalme, Na Yesu Kristo mwenyewe ndio mfalme mkuu yaani mfalme wa wafalme ona katika
Ufunuo 19:16 “Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.”
Kwa msingi huo kila Mkristo pia ni mkuu yaani mtawala ni watu ambao Mungu amewakusudia kuwaweka katika kiwango kikubwa na cha juu sana hivyo watu wa aina hii Mungu hakukubali kuwaruhusu wanywe Pombe.
1Petro 2:9 “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;”
Katika maandiko watu wenye kujiheshimu, na waliotaka kujiweka karibu na Mungu, viongozi na wafanya sheria watawala, makuhani walitakiwa kuishi maisha ya kiwango kikubwa na cha juu kuliko watumwa hawa ndio wanaotajwa kuwa hawapaswi kutumia mvinyo, Watu ambao Mungu ameyaweka maisha ya watu wake katika mikono yao kila mtu aliye katika ngazi ya kufanya maamuzi na kuongoza na kufundisha watu wa Mungu, hapaswi kutumia mvinyo kwa mujibu wa maandiko matakatifu.
Yohana1:11-12 “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;“
kwa kuwa Yesu anaitwa mfalme wa wafalme na Bwana wa Mabwana hii ni wazi kuwa waliookoka au waliomuamini moja kwa moja wanakuwa wafalme au wana wa ufalme kutokana na kumuamini Yesu, Mungu amekusudia tuwe watawala pamoja naye, wafanya sheria pamoja naye, makuhani pamoja naye, waamuzi pamoja naye, waalimu pamoja naye na ndio maana unaweza kuona katika maandiko wanaitwa uzao mteule,Ukuhani wa kifalme,taifa takatifu na watu wa miliki ya Mungu, kwa msingi huo kila amwaminiye Mungu ni Mfalme, Na Yesu Kristo mwenyewe ndio mfalme mkuu yaani mfalme wa wafalme ona katika
Ufunuo 19:16 “Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.”
Kwa msingi huo kila Mkristo pia ni mkuu yaani mtawala ni watu ambao Mungu amewakusudia kuwaweka katika kiwango kikubwa na cha juu sana hivyo watu wa aina hii Mungu hakukubali kuwaruhusu wanywe Pombe.
1Petro 2:9 “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;”
Katika maandiko watu wenye kujiheshimu, na waliotaka kujiweka karibu na Mungu, viongozi na wafanya sheria watawala, makuhani walitakiwa kuishi maisha ya kiwango kikubwa na cha juu kuliko watumwa hawa ndio wanaotajwa kuwa hawapaswi kutumia mvinyo, Watu ambao Mungu ameyaweka maisha ya watu wake katika mikono yao kila mtu aliye katika ngazi ya kufanya maamuzi na kuongoza na kufundisha watu wa Mungu, hapaswi kutumia mvinyo kwa mujibu wa maandiko matakatifu.
Kunywa mvinyo hakuwafai Wafalme wala wakuu:
Kama
tulivyoona katika utangulizi na Mstari
wa Msingi wa somo hili Mungu katika mpango wake alikataza watu wote muhimu,
hususani wafalme na watawala na waamuzi
wanadhiri, walimu wa sheria (rabbis)
na makuhani kutokutumia mvinyo kabisa, Sababu kubwa ya kuwakataza watu hawa ni
kwamba wao ni wahudumu wa ngazi ya juu kabisa katika kazi za Mungu na
wanaopaswa kufanya maamuzi kwa mujibu wa sheria za Mungu, wao ni watu
wanaopaswa kuhesabika kama watu wenye hekima na kielelezo hivyo hawapaswi
kujiingiza katika maswala ya unywaji wa pombe, Mungu aliona Pombe kwao itakuwa
ni yenye kuwavunjia heshima na kuwaharibu katika utendaji wa Maamuzi yao ya
kila siku na kuipotosha sheria ya Mungu kwa msingi huo Mungu aliwatarajia kwamba
wataishi kwa viwango vya juu zaidi vya mamlaka ya kifalme na hivyo hawakupaswa
kutumia mvinyo, Biblia inayataja makundi kadhaa ya watu wa Mungu wanaopaswa
kujihadhari na kujitenga na Divai au mvinyo kuwa ni Pamoja na wafalme,
watawala, wakuu,wanadhiri, waamuzi yaani mahakimu na majaji, watu safi, manabii
wakubwa wenye heshima, Maaskofu, waangalizi, mashemasi, wakristo na wanawake
wakubwa wanaotarajiwa kuwa walimu wa wanawake wachanga hawa wote walipaswa
kujihadhari na mvinyo:-
Mfano
a. Wafalme na
wakuu Mithali 31:4-5 “Ee Lemueli, kunywa
mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi
kileo? Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye
taabuni.” Wafalme na watawala Mungu alikiwakataza kutumia mvinyo au
kujihusisha na unywaji wa Pombe kwa sababu Pombe ingewaongoza katika kuvunja
uadilifu na kupotosha hukumu ya Mungu. Moja ya mambo ambayo Isaka aliweza
kujuta sana ni pamoja na kugundua kuwa hakutenda haki kwa mwanae Esau kwa
kumbariki Yakobo badala ya Esau, Tunajua mapenzi ya Mungu na mpango wake kwa
Yakobo, tunajua pia kuwa Esau alikwisha kuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza,
tunajua pia kuwa Isaka alikuwa haoni vizuri, tunajua pia kuwa Rebeka alifanya
mpango yeye na mwanaye Yakobo kupata mbaraka ule lakini Mvinyo unatajwa kuwa
ilikuwa ni mojawapo ya sababu ya Isaka kutokuamua mambo vema
Mwanzo 27:24-29 “Akamwuliza, Wewe ndiwe kweli mwanangu Esau? Akasema, Ndimi. Akasema, Niletee karibu nami nipate kula mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki. Akamsogezea karibu, naye akala; kisha akamletea MVINYO, AKANYWA. Isaka, baba yake, akamwambia, Njoo karibu sasa, ukanibusu, mwanangu. Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba alilolibariki BWANA. Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo. Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe”
unaweza kuona kuwa Isaka baada ya tukio hili aliogopa na kutetemeka mno kwani alijua kuwa hakutenda haki hakunyoosha hukumu na kuwa hakukuwa na namna ya kutengua yeye alikuwa amevunja sheria za utamaduni wa kumbariki mwana mkubwa kama mzaliwa wa kwanza hivyo alitetemeka sana na kuogopa mno lakini tayari Yakobo alikuwa amekwisha barikiwa
Mwanzo 27:33 “Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa.” Mungu anataka wafalme wasiwe walevi ili waweze kufanya maamuzi ya haki na kutokupotosha hukumu, kila mtawala, au mtu mkubwa au mtu aliye katika ngazi ya kufanya maamuzi hapaswi kutumia mvinyo kwa sababu anaweza kupindisha haki ya Mungu anayopaswa kuitoa kwa wanaostahili na kwa wanyone anaowaongoza. Kwa msingi huo wana wa kifalme na mabinti wa kifalme watawala wa familia ya ufalme wa Mungu hawapaswi kutumia mvinyo!
Mwanzo 27:24-29 “Akamwuliza, Wewe ndiwe kweli mwanangu Esau? Akasema, Ndimi. Akasema, Niletee karibu nami nipate kula mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki. Akamsogezea karibu, naye akala; kisha akamletea MVINYO, AKANYWA. Isaka, baba yake, akamwambia, Njoo karibu sasa, ukanibusu, mwanangu. Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba alilolibariki BWANA. Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo. Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe”
unaweza kuona kuwa Isaka baada ya tukio hili aliogopa na kutetemeka mno kwani alijua kuwa hakutenda haki hakunyoosha hukumu na kuwa hakukuwa na namna ya kutengua yeye alikuwa amevunja sheria za utamaduni wa kumbariki mwana mkubwa kama mzaliwa wa kwanza hivyo alitetemeka sana na kuogopa mno lakini tayari Yakobo alikuwa amekwisha barikiwa
Mwanzo 27:33 “Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa.” Mungu anataka wafalme wasiwe walevi ili waweze kufanya maamuzi ya haki na kutokupotosha hukumu, kila mtawala, au mtu mkubwa au mtu aliye katika ngazi ya kufanya maamuzi hapaswi kutumia mvinyo kwa sababu anaweza kupindisha haki ya Mungu anayopaswa kuitoa kwa wanaostahili na kwa wanyone anaowaongoza. Kwa msingi huo wana wa kifalme na mabinti wa kifalme watawala wa familia ya ufalme wa Mungu hawapaswi kutumia mvinyo!
b. Makuhani
Walawi 10:8-11 “Kisha BWANA akanena na Haruni, na kumwambia,
Usinywe divai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo
mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni
amri ya milele katika vizazi vyenu; kisha, mpate kupambanua kati ya yaliyo
matakatifu na hayo yaliyo ya siku zote, na kati ya yaliyo najisi na hayo yaliyo
safi; tena mpate kuwafundisha wana wa Israeli amri hizi zote ambazo BWANA
amewaambia kwa mkono wa Musa.” Kutokunywa mvinyo au Pombe lilikuwa
moja ya agizo la viongozi wa Kiroho katika agano la kale yaani makuhani, wao
walikuwa wamewekwa wakfu kama vyombo vitakatifu vya kumtumikia Mungu na
kufundisha watu neno la Mungu, kufanya kosa hili kungepelekea wao kupata adhabu
ya kifo, kwa Mungu kiwango chochote cha ulevi kwao kulihesabika kuwa ni kinyume
na viwango vya uadilifu, Hekima na utii wa kiongozi wa kiroho, Mtu hawezi kuwa
mlevi na pia wakati huo huo akajazwa Roho Mtakatifu kwa hiyo makuhani hawakujihusisha
na pombe. Kutokana na tafasiri ya
andiko hili Marabi wa kiyahudi
hawakuruhusu muamuzi “Jugde” au Hakimu kuendesha kesi ikiwa itabainika kuwa
amekunywa hata glasi moja ya pombe, aidha
walimu (Rabbis) katika Israel
hawaruhusiwi kufundisha endapo watabainika kuwa wamekunywa pombe!, Ni mfano gani
ataonyesha kwa anaowafundisha, na anawezaje kupambanua mema na mabaya na
kuonyesha kuwa anamuheshimu Mungu akiwa na ulevi, mwilini mwake hiyo hata leo
Marabi katika Israel hawatumii mvinyo hata kidogo.
c.
Wanadhiri Hesabu 6:1-5 “Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Nena na watu wa
Israeli, uwaambie, Mtu mume au mtu mke atakapoweka nadhiri kubwa, nadhiri ya
Mnadhiri, ili ajiweke wakfu kwa Bwana; atajitenga na divai na vileo; hatakunywa
siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yo yote ya zabibu, wala
asile zabibu, mbichi wala zilizokauka.
Siku zote za kujitenga kwake asile kitu cho chote kilichoandaliwa kwa
mzabibu, tangu kokwa hata maganda.Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, wembe
usimfikilie kichwani mwake; hata hizo siku zitakapotimia, ambazo alijiweka
wakfu kwa Bwana, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele za kichwani mwake zikue
ziwe ndefu.” Wanadhiri ni
watu waliojifunga kwa Mungu, ili kujitunza katika uwepo wake hawa nao iliagizwa
wasijitie unajisi ikiwa ni pamoja na kutokusogelea au kukaribia ulevi au kunywa
Pombe. Mtu anayeweka nadhiri maana yake amejitenga kwa makusudi ya kutembea na
uwepo wa Mungu, anajitenga ili awe karibu na Mungu, Mungu ni mtakatifu sana ni
wazi kuwa mtu hawezi kumkaribia Mungu au kutunza uwepo wa Mungu kama atakuwa
mlevi, hivyo wote waliojifunga kwa nadhiri katika maandiko sheria ya kwanza
kabisa katika maisha yao ilikuwa ni kutukutumia, mvinyo au pombe ya aina yoyote
ile.
d.
Waamuzi Waamuzi 13:3-5 “Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama,
wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume.
Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu
kilicho najisi; kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na
wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu
tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.” Waamuzi katika agano la kale walikuwa ni
viongozi wa kijeshi waliowaongoza waisrael kupigana vita dhidi ya adui zao
wakati wa vita, lakini vilevile waliwaamua watu wakati wa amani, walitegemea
uhodari wa Roho Mtakatifu katika maongozi yao walikuwa ni wakombozi wa uonevu
dhidi ya watu wa Mungu kwa wale waliowaonea, Mungu hakutaka wanywe mvinyo wala
kileo, Ni wazi kuwa hata kamanda wa majeshi hawezi kutimiza wajibu wake vema
vitani kama atakuwa amelewa, Mungu aliwataka waamuzi wasinywe na muamuzi
maarufu zaidi Samsoni Mungu hakuruhusu anywe!
e. Watu safi
“Devoted” Yeremia 35:1-8,14 “Neno hili ndilo lililomjia
Yeremia, kutoka kwa Bwana, katika siku za Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa
Yuda, kusema, Enenda nyumbani kwa Warekabi, ukanene nao, ukawalete nyumbani kwa
Bwana, katika chumba kimoja, ukawape divai wanywe. Basi nikamtwaa Yaazania,
mwana wa Yeremia, mwana wa Habasinia, na ndugu zake, na wanawe wote, na nyumba
yote ya Warekabi; nikawaleta ndani ya nyumba ya Bwana, ndani ya chumba cha wana
wa Hanani, mwana wa Igdalia, mtu wa Mungu, kilichokuwa karibu na chumba cha wakuu,
nacho kilikuwa juu ya chumba cha Maaseya, mwana wa Shalumu, bawabu; nikaweka
mabakuli yaliyojaa divai, na vikombe, mbele ya wana wa nyumba ya Warekabi,
nikawaambia, Nyweni divai. Lakini wakasema, Hatutakunywa divai; kwa maana
Yonadabu, mwana wa Rekabu, baba yetu, alituamuru, akisema, Msinywe divai, ninyi
wala wana wenu, hata milele; wala msijenge nyumba, wala msipande mbegu, wala
msipande mizabibu, wala msiwe nayo; bali siku zenu zote mtakaa katika hema;
mpate kuishi siku nyingi katika nchi ambayo mtakaa ndani yake hali ya wageni. Nasi
tumeitii sauti ya Yonadabu, mwana wa Rekabu, baba yetu, katika yote
aliyotuamuru, kwamba tusinywe divai siku zetu zote, sisi, na wake zetu, na wana
wetu, na binti zetu; 14. Maneno ya Yonadabu, mwana wa Rekabu, aliyowaamuru
wanawe, kwamba wasinywe divai, yametimizwa, na hata leo hawanywi; maana waitii
hiyo amri ya baba yao; lakini mimi nimesema nanyi, nikiamka mapema na kunena,
bali ninyi hamkunisikiliza mimi.” Hii
ni Familia ya wakeniz jamii ya watu walioambatana na Israel kutoka Jangwani ni
wana wa ukoo wa Kalebu na ukoo wa Yethro kuhani mkuu wa Midian, walishika sana
mausia ya wazazi wao na Mungu aliwabariki na kuwatumia kama mfano wa utii
akiwafundisha wana wa Israel, kutokana na maisha yao ya uadilifu wamekuwa
kielelezo na mfano wa kuigwa katika kushika maagizo, kutokana na wana wa Rekabu
kuyashika sana maagizo ya baba yao hususani kutokunywa mvinyo Mungu aliibari familia hii na kusema kuwa
siku zote hata milele Yonadabu mwana wa rekabu hatakosa mtu wa kusimama mbele zake
yaani wa kumtumikia milele ona Yeremia
35:18-19 “Naye Yeremia akawaambia watu wa nyumba ya
Warekabi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa sababu mmeitii
amri ya Yonadabu, baba yenu, na kuyashika maagizo yake yote, na kutenda
sawasawa na yote aliyowaamuru; basi, kwa
sababu hiyo, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Yonadabu, mwana wa
Rekabu, hatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu hata milele.”
f.
Viongozi wakubwa katika Israel ambao walikuwa kielelezo kikubwa cha imani
ya wayahudi waliokuwa uhamishoni huko Babeli hawa ni Daniel, na Hanania , Mishael na Azaria ambao pia walijulikana kama Shedrak, Meshack na Abednego, walipata
vyeo vikubwa sana, walikuwa na hekima mno na walikuwa mashujaa wa imani na watu
wenye msimamo mkali hawa hawakuruhusu kuwa najisi kwa kunywa, Na matokeo yake
waoa wakawa na akili mno na maarifa na ujuzi mkubwa sana na Daniel akawa hodari
wa kujua ndoto na maono Divai ona Daniel 1:8-16 “Lakini
Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme,
wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa
asijitie unajisi. Basi Mungu alimjalia Danieli kupata kibali na huruma machoni
pa huyo mkuu wa matowashi. Mkuu wa matowashi akamwambia Danieli, Mimi namwogopa
bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa
nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi
kwa kufanya hivyo mtahatirisha kichwa changu mbele ya mfalme. Ndipo Danieli
akamwambia yule msimamizi, ambaye mkuu wa matowashi amemweka juu ya Danieli, na
Hanania, na Mishaeli, na Azaria, Tafadhali utujaribu sisi watumishi wako muda
wa siku kumi; na watupe mtama tule, na maji tunywe. Kisha nyuso zetu zitazamwe
mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula chakula cha mfalme; ukatutendee
sisi watumishi wako kadiri ya utakavyoona. Basi akawasikiliza katika jambo
hilo, akawajaribu siku kumi. Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa
nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote
waliokula chakula cha mfalme. Basi yule msimamizi akaiondoa posho yao ya
chakula, na ile divai waliyopewa wanywe, akawapa mtama tu. Basi, kwa habari za
hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima;
Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.” Unaweza
kuona habari ya Daniel, Shedrack, Meshack na Abednego hawakuwa watu wa kawaida
walikuwa watu maalumu mno wenye kuheshimiwa sana Ujuzi, Elimu na hekima
viliwakalia, kumbe ukitaka kuwa mlevi umechagua daraja la chini sana! Hawa
wanahesabika kama watu waliomuheshimu Mungu kwa kiwango cha juu sana na kuwa
mashujaa wa imani waliozima miali ya moto, moja ya siri yao kuu ni kuwa mbali
na Mvinyo.
g.
Mtu mkuu kama Yohana Mbatizaji. Luke 1:15 “Kwa sababu
atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho
Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.” Kuna sababu kubwa mbili kwa nini Yohana
atakuwa mkuu mbele za Bwana na kwanini hakuruhusiwa kunywa divai/ mvinyo? Ni kwa
sababu alijazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mamaye na pili alikuwa na
wajibu wa kuwaongoza wengi au kuwarejeza wengi kwa Bwana Mungu wao Luka 1:16 “Na
wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao”. Kwa kazi ya
kufundisha na kuwaelekeza wengi kwa Mungu hakupaswa kutumia mvinyo. Malaika
anasema kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana, Hatakunywa divai wala kileo
unaona kumbe kama unataka kuwa na heshima kwa Mungu ni vema na wazi ukajiepusha
na pombe au kile, usinywe mvinyo wa aina yoyote.
h.
Maaskofu au waangalizi 1Timotheo 3:1-3 “Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani
kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja,
mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si
mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana,
wala asiwe mwenye kupenda fedha;” Neno
askofu kwa kiyunani linasomeka kama
“EPISKOPOS” neno hili maana yake ni mtu mwenye huduma ya uangalizi, au
uchungaji, Uangalizi wa roho za watu ni uchungaji, watu wa namna hii ni watu
wanaopaswa kuwa vizuri kiroho na kiuadilifu, Neno la Mungu limeweka sifa kadhaa
na viwango wanavyotakiwa kuwa navyo wachungaji waangalizi na maaskofu na katika
viwango walivyowekewa kimaandiko
kimojawapo ni kutokuzoelea ulevi,
wao ni watu wanaopaswa kuwa kielelezo ni watu ambao wanaangalia na jamii na wanapaswa kuishi kwa viwango vya
juu mno kwa msingi huo hawapaswi kusogelea mvinyo wala kunywa pombe 1Timotheo 4:12 “Mtu
awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika
usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.” Maandiko
yanamchukulia kiongozi mchungaji, mwangalizi askofu kuwa ni mtu anayepaswa kuwa
safi katika usemi, mwenendo, upendo imani na usafi Hiwezekani kuwa kielelezo
katika mwenendo, usemi, upendo, imani na usafi kama anatumia Pombe haiwezekani 1Petro 5:2-3 “lichungeni
kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa
hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. Wala si
kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile
kundi.” Mungu hatarajii kundi hili kuwa hawatajihusisha na unywaji
wa mvinyo kwa sababu wao ni viongozi wa kiroho na wana wajibu mkubwa wa kuwa
kielelezo kwa jamii. Neno hili “SI MTU WA KUZOELEA ULEVI” Biblia ya
kiingereza Amplified Bible inasomeka
“NOT A DRINKER”NIV inasema “NOT
GIVEN TO DRUNKENNESS” Biblia ya kiyunani inatumia “ne- Parainon” likimaanisha kutokukaa karibu na mvinyo au
kutokusogelea mvinyo, au kula na kunywa pamoja na walevi Mathayo 24:45-51 “Ni nani basi yule mtumwa
mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape
watu chakula kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo
atamkuta akifanya hivyo. Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote.
Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; akaanza
kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; bwana wake mtumwa
huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na
kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.”
Unaweza kuona kwa msingi huo
maandiko yanaweka wazi kuwa mjoli, mtumwa mwaminifu mtu wa Mungu mwangalizi,
askofu, Mchungaji na wenye hekima hawapaswi sio kusogelea ulevi lakini hata
kula na kunywa pamoja na walevi, kwa wachungaji hiki ni kiwango kikubwa na cha
juu zaidi kwetu
i.
Mashemasi 1Timothy 3:8 “Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli
mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana,si watu wanaotamani fedha ya aibu.”
Ni Muhimu kufahamu kuwa neno “Si watu wa kutumia mvinyo sana” kwa
kiingereza “not given to much wine”
kwa kawaida neno hilo katika biblia ya kiyunani linasomeka “NOT PAYING ATTENTION TO WINE” kwa
msingi huo andiko hili linakataza sio kunywa tu lakini kutokukaribia kabisa
mvinyo, Kama maandiko yanaagiza kutokuifuatisha ni wazi kuwa mojawapo ya njia
iliyo bora zaidi ya kujilinda na uovu ni pamoja na kutokuikaribia pombe Yakobo 1:27, 1Petro 5:8 Tito 2:12.
j.
Wakristo 1Thesalonike 5:6-8 “Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na
kiasi. Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku. Lakini
sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo,
na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.” Ona pia
Waefeso 5:18 “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna
ufisadi; bali mjazwe Roho;” Wakristo wanaaswa kuwa wasilewe kwa
mvinyo ambayo ndani yake ina ufisadi neno hilo ufisadi katika biblia ya
kiingereza ya NIV linasomeka kama “DEBAUCHERY”
ambalo tafasiri yake ni “immoral
behaviour” na Biblia ya kiingereza
ya Aplified Bible imetumia neno “DISSIPATION”
ambalo maana yake “disapproving
behaviour” yaani inasababisha moyo uharibike, inasababisha ufanye matukio
yasiyopaswa, inasababisha ujiingize kwenye uasherati au ulevi na madawa ya
kulevya na tabia zisizofaa ndio maana Biblia ya Kiswahili imetumia neno ufisadi
yaani ni mjumuiko wa matendo yasiyofaa,
k. Wanawake
watu wazima Tito 2:3-5 “Vivyo hivyo na wazee wa kike
wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo
nyingi, bali wafundishao mema; ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume
zao, na kuwapenda watoto wao; na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi
nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu
lisitukanwe.” Wanawake
watu wazima walitarajiwa kuwa walimu wa kuwafunza adabu wanawake vijana kwa
msingi huo hawakupaswa kabisa kujihusisha na mvinyo au ulevi au pombe. Nyakati
za agano la kale kama mwanamke angekuwa mlevi aliitwa mwanamke Baradhuli au
asiyefaa kitu, Mwanamke mwenye kujiheshimu alipaswa vilevile kuwa mbali na
ulevi, Mama wa nabii Samuel yaani Hanna, hakuwahi kutumia mvinyo ona katika 1Samuel 1:13-16 “Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo
yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli
alimdhania kuwa amelewa. Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia
mbali divai yako. Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke
mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho
yangu mbele za Bwana. Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa kitu;
kwa kuwa katika wingi wa kuugua kwangu na kusikitika kwangu ndivyo nilivyonena
hata sasa. Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli
akujalie haja yako uliyomwomba.” Anna amekuwa mwanamke aliye
kielelezo katika subira, maombi na kama mwanamke aliyeteseka kutokana na kuwa
tasa lakini alimtegemea Mungu, aliomba na kujiweka karibu na Mungu akijifunga
katika nadhiri na kujitoa huku akijiepusha na Divai na kileo yaani hakunywa
pombe.
l.
Awaye yote anayetaka kutembea katika uwepo wa Mungu na miujiza yake lazima ahakikishe
kuwa anajiweka mbali na divai na pombe, Ni
muhimu ikakumbukwa wazi na kila mwanazuoni kuwa kama mtu anataka kuufurahia
uwepo wa Mungu na kushuhudia matendo yake makuu hapaswi kunywa divai wala
pombe, Mungu alitembea na wana wa Israel miaka 40 jangwani ni wazi kuwa Israel
walitembea katika uwepo wake moja ya vitu ambavyo kizazi kile walikuwa mabli
nacho ni pamoja na Divai na kileo yaani Mvinyo na Pombe ona Kumbu kumbu la torati 29:1-6 “Haya ndiyo maneno ya agano Bwana alilomwamuru Musa alifanye na
wana wa Israeli katika nchi ya Moabu, pamoja na agano alilofanya nao Horebu.
Musa akawaita Israeli wote akawaambia, Mmeyaona yote Bwana aliyomfanya Farao
katika nchi ya Misri mbele ya macho yenu, yeye na watumwa wake wote, na nchi
yake yote; yale majaribu makuu yaliyoyaona macho yako; hizo ishara, na ile
miujiza mikuu; lakini Bwana hakuwapa moyo wa kujua, wala macho ya kuona, wala
masikio ya kusikia, hata leo hivi. Nami miaka arobaini nimewaongoza jangwani;
nguo zenu hazikuchakaa juu yenu, wala kiatu chako hakikuchakaa katika mguu
wako. Hamkula mkate, wala hamkunywa divai, wala kileo; ili mpate kujua kwamba
Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”
Kwa nini kunywa mvinyo hakuwafai Wafalme na
wakuu!
1.
Inadhihaki au kuwavunjia heshima wale
wanaotumia Mithali 20:1 “Mvinyo hudhihaki, kileo huleta
ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.” Katika maandiko Biblia inaonyesha matokeo ya
pombe kivitendo zaidi, Ni jambo la kusikitisha kuwa Nuhu aliyekuwa mtu
aliyapata neema kutokana na uadilifu mkubwa aliokuwa nao yaya na uzao wake hata
Mungu akamuokoa na gharika, aliheshimika kama nabii aliyeweza kutabiri na
unabii wake ukatimia, lakini ni jambo lenye kusikitisha kuwa Nuhu anatajwa
katika maandiko kuwa alikuwa mtu wa kwanza kulima zabibu na ambaye alitengeneza
juisi yake na aidha kwa kujua au kwa kutokujua alikunywa pombe akalewa na
kujiaibisha sio hivyo tu aliweza kutoa laana kwa mjukuu wake mkubwa kutokana na
mwanae kumuona akiwa hana nguo kutokana ana kulewa Pombe Mwanzo 9:20-27 “Nuhu akaanza kuwa mkulima,
akapanda mizabibu; akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. Hamu,
baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili
waliokuwa nje. Shemu na Yafethi wakatwaa
vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika
uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba
yao.Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
Akasema, Na alaaniwe Kaanani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake. Akasema, Na
atukuzwe BWANA, Mungu wa Shemu; Na Kaanani awe mtumwa wake. Mungu akamnafisishe
Yafethi, Na akae katika hema za Shemu; Na Kaanani awe mtumwa wake.” Ni
wazi na kweli kabisa kuwa pombe ina dhihaka, inaweza kumfanya mtu
anayeheshimika sana akapoteza heshima kutokana na vitendo vitakavyofanywa akiwa
katika hali ya ulevi.
2.
Inaharibu tabia njema! (Behaviour changes)
Maandiko yanamtaja Lutu kuwa mtu
mwenye haki ambaye Mungu alimuokoa katika miji ya watu walioharibika kwa dhambi
miji ya sodoma na Gomorah ona katika 2 Petro 2:7-8 “akamwokoa
Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi wa hao
wahalifu; maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa kuona na kusikia,
alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na
sheria;” Ni jambo la kusikitisha sana kuona kuwa mwisho wa maisha ya
Lutu haukuwa mwema, bindti zake walikuwa na hatia ya kufanya ngono na baba yao,
na Lutu alikuwa na hatia ya kukubali kunywa mvinyo kiasi cha kulewa na
kushiriki ngono zembe iliyoleta matokeo ya kuweko kwa mataifa ya kipagani
baadaye, Biblia inatuonyesha mfano wa mtu huyu muadilifu ambaye aliweza kunyweshwa
mvinyo na kujikuta akifanya mapenzi na binti zake ona Mwanzo 19:30-38 “Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake
wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika
pango, yeye na binti zake wawili. Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni
mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia
yote. Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie baba
yetu uzao. Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa
akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Ikawa siku ya
pili, mkubwa akamwambia mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe
mvinyo tena usiku huu, ukaingie ukalale naye. Wakamnywesha tena baba yao mvinyo
usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala
alipoondoka. Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao.
Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi,
hata leo. Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye
baba wa Waamoni hata leo.” Ngono mbaya zaidi ya baba kufanya mapenzi
na binti zake inatajwa hapa katika maandiko ambayo inaonyesha kuwa japo
maandiko yalimtaja Lutu kuwa mtu mwenye haki, lakini hakukuwa na uadilifu wa
kutosha katika nyumba yake ikiidhinishwa na ushahidi wa mkewe kuangalia nyuma
na kugeuka nguzo ya chumvi lakini kuhurumiwa kwa binti zake na yeye mwenyewe
kunaifanya dhambi ileile waliyoikimbia huko Sodoma kujitokeza tena kwa kiwango
kingine ikichangiwa na ulevi na pombe au mvinyo aliyoipewa na binti zake hii ni
aibu na fedheha kubwa! Ni ni dhahiri kuwa mtu na heshima zake mbele za Mungu na
wanadamu anaweza kujivunjia heshima hiyo endapo ataendekeza ulevi na unywaji wa
mvinyo kweli mvinyo hauwafai wakuu wala wafalme.
3.
Mvinyo inaleta madhara makubwa na hatari za
aina nyingi Mithali 23:29-34 “Ni nani apigaye, Yowe? Ni
nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na
jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu? Ni wale wakaao sana
kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika. Usiitazame mvinyo iwapo
ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu; Mwisho wake huuma
kama nyoka; Huchoma kama fira. Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako
utatoa yaliyopotoka. Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye
asinziaye juu ya mlingoti.”mwisho wa
ulevi una maumivu makali sana mwenye hekima anaifananisha na kugongwa na nyoka
mwenye sumu kali kama Fira.Wakati mwingine kwa sababu ya ulevi kumetokea
magomvi makubwa sana katika familia, watu wengi wenye wazazi walevi
wameshuhudia hali ya kukosekana kwa utaratibu katika familia nyingi kufuatia
unywaji wa Pombe, watru wana majeraha ya mwili nay a kiroho kutokana na ulevi
uliokithiri.
4. Biblia
inasema huwezi kuwa mtu mkubwa na tajiri kama utatumia mvinyo Mithali 21:17 “Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; Apendaye mvinyo na mafuta
hatakuwa tajiri.” Kutokana na
kujihusisha na ulevi watu wengi sana wamajikuta kwenye umasikini mkubwa sana,
nimewahi kushuhudia baba mmoja mlevi, akiwa amerejea nyumbani akiwa mgomvi sana
kutokana na ulevi, aliamua kuvunja kabati la vyombo na kulibwaga huko, aidha
alivunja TV na kuwajeruhi mke wake na watoto na yeye mwenyewe asubui wakati
napita nilimuona rafiki yangu ambaye ni mtoto wa ile familia akiwa amejaa damu
na kuumia kwa vioo nilipomuuliza ndio akanielezea habari ya yaliyowakuta Pombe
inaleta umasikini na maandiko yanakubali hilo na kutoa ushauri kuwa tusiwe
miongoni mwa wanaokunywa mvinyo Mithali 23: 20-21 “Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni
mwao walao nyama kwa pupa. Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na
utepetevu humvika mtu nguo mbovu” Ni wazi kuwa Mungu anataka
tufanikiwe na kustawi sana lakini moja ya kikwazo kikubwa cha ustawi wetu ni
pamoja na kujihusisha na ulevi, bwana ampe neema kila mmoja wetu kuwa mbali na kileo.
5. Ulevi
unahatarisha usalama wako. Biblia
inaonyesha kuwa ulevi unaweza kusababisha maadui zako ama watu wabaya
wakaitumia nafasi yako ya kuwa umelewa na wakakuangamiza, ilhali kama ungekuwa
hujalewa ungeliweza kuokoa maisha yako 2Samuel
13:28-29 “Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake,
akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami
nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, ndipo mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru?
Iweni hodari, iweni na ujasiri. Basi watumishi wa Absalomu wakamfanyia Amnoni
kama alivyoamuru Absalomu. Ndipo wakaondoka wana wote wa mfalme, wakapanda kila
mtu nyumbu wake, wakakimbia.” Watu wengi sana duniani wameuawa kwa
sababu ya mvinyo, Bibi yangu mzaa mama alikuwa mwanamke mzuri sana alikuwa na
umbile la kisomali, kwa kuwa ni mzigua mwenye asili ya Somalia, alikuwa mzuri
sana Joyce na alikuwa mwenye maringo kutokana na uzuri aliokuwa nao watu
waliomuonea wivu walimletea chupa ya pombe mchana alipokuwa anasonga ugali, kwa
kumwamini mtu huyo alikunywa na akafa ugali ukiwa unaungua na mtot wake mdogo
akiwa mgongoni, Adui zako na watu waovu wanaweza kukufanyia mamboi mabaya
unapokuwa umelewa, watu wenye kisa na wewe wanaweza kukufanyia mambo mabaya
unapokuwa umelewa ona pia 1Wafalme
16:8-10 “Katika
mwaka wa ishirini na sita wa Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha alianza
kutawala juu ya Israeli huko Tirza, akatawala miaka miwili.Na mtumwa wake
Zimri, jemadari wa nusu ya magari yake, akamfanyia fitina; alipokuwako Tirza
akinywa hata kulewa nyumbani mwa Arsa, aliyekuwa juu ya nyumba huko Tirza; Zimri
akaingia akampiga, akamwua, katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa
Yuda, akatawala mahali pake”. Wafalme zamani wao wenyewe pia
walikuwa Majemadari Ela angeweza kujiokoa au kujihami au kujilinda kama askari
jemadari lakini kwaajili ya ulevi, aliweza kuuawa kirahisi, kwaajili ya usalama
wako vilevile usinywe, Madereva wengi sana wamesababisha ajali na kupoteza
maisha au kusababisha vifo kwa sababu ya ulevi.
6. Walevi
hawataurithi ufalme wa Mungu 1Wakoritho 6:9-10 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme
wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu
sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala
watukanaji, wala wanyang'anyi.” Ni ukweli usiopingika kuwa ni vigumu
kwa wadhalimu au watenda dhambi wote wa kila aina hawataingia katika ufalme wa
Mungu, lakini hata hivyo unaweza kuona maandiko yanawataja walevi pia, kwa
msingi huo kama mtu ataendekeza ulevi ni anajiweka katika njia mbaya ya
kuurithi ufalme wa Mungu.
7. Ulevi ni
moja ya matendo yasiyo ya Kiroho Wagalatia 5:19-21 “Basi
matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya
sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda,
ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama
nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo
hawataurithi ufalme wa Mungu.”
8. Ulevi
unaongoza katika maovu mengine Hosea 4:10-11 “Nao
watakula, lakini hawatashiba; watafanya zinaa, lakini hawataongezeka; kwa
sababu wameacha kumwangalia Bwana. Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu
za wanadamu.” Moja ya jambo ambalo biblia inalielezea hapa ni kuwa
ulevi una tabia ya kuambatana na dhambi nyingine, Katika ulevi kuna kamali,
michezo ya kubahatisha, lakini vilevile zinaa huambatana na ulevi pamoja na
maovu ya aina nyingine haribiko la kitabia la mtu anavyokuwa mlevi ni tofauti
na anapokuwa na akili timamu, kwaajili ya ulevi mtu anaweza kufanya ujinga
mwingi sana hata kutukana mtu, bila kufikiri, Ulevi unaondoa fahamu, ulevi
unaharibu mahusiano na kuondoa heshima hata katika ndoa.
9.
Ulevi unaweza kuvunja mahusiano.
Katika maandiko tunapewa mifano kadhaa ya
watu walivuruga mahusiano yao kwa sababu ya ulevi uliopindukia, Mwanadamu
ambaye yuko vizuri kiroho na kiakili anapaswa kuwa na na uhusiano mzuri na
wanadamu wengine Lakini bibliainaonyesha kuwa ulevi uliokithiri umeweza
kuharibu mahusiano ya watu wengi na moja ya mifano ya kibiblia ni pamoja nah ii
angalia Esta 1:1-12 “Zamani za Ahasuero;
naye huyu Ahasuero alimiliki toka Bara Hindi mpaka Kushi, juu ya majimbo mia na
ishirini na saba; siku zile mfalme Ahasuero alipoketi katika kiti cha enzi cha
ufalme wake, huko Shushani ngomeni; mwaka wa tatu wa kumiliki kwake, ikawa
aliwafanyia karamu maakida wake wote na majumbe wake; wakuu wa Uajemi na Umedi,
watu wenye cheo na maakida wa majimbo, wakihudhuria mbele zake. Akawaonyesha
utajiri wa ufalme wake mtukufu, na heshima ya enzi yake bora siku nyingi, maana
siku mia na themanini. Hata siku hizo zilipotimia, mfalme akawafanyia karamu
watu wote waliokuwapo huko Shushani ngomeni, wakubwa kwa wadogo, muda wa siku
saba, katika behewa la bustani ya ngome ya mfalme. Palikuwa na mapazia ya
bafta, nyeupe na samawi, yamefungiwa kamba za kitani safi za rangi ya zambarau
kwa pete za fedha na nguzo za marumaru; pia na vitanda vilikuwa vya dhahabu na
fedha juu ya sakafu ya marumaru, mawe mekundu, na meupe, na ya manjano, na
meusi. Wakawanywesha kileo katika vyombo vya dhahabu, na vile vyombo vilikuwa
mbalimbali, na divai tele ya namna ya kifalme, sawasawa na ukarimu wa mfalme;
kunywa kulikuwa kama ilivyoamriwa, bila sharti; maana ndivyo mfalme
alivyowaagiza watumishi-wa-nyumbani, kila mtu afanye apendavyo. Tena Vashti,
malkia, naye akawafanyia karamu wanawake ndani ya nyumba ya kifalme ya mfalme
Ahasuero. Hata siku ya saba, mfalme alipofurahiwa moyo wake kwa divai,
aliwaamuru Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari, na Karkasi,
wale wasimamizi-wa-nyumba saba waliohudumu mbele za mfalme Ahasuero, wamlete
Vashti, malkia, mbele ya mfalme, amevaa taji ya kifalme; ili kuwaonyesha watu
na maakida uzuri wake, maana alikuwa mzuri wa uso. Bali Vashti, malkia,
alikataa kuja kwa amri ya mfalme kwa mkono wa wasimamizi-wa-nyumba; kwa hiyo
mfalme akaghadhibika sana, na hasira yake ikawaka ndani yake.” Unaweza
kuona katika kisa hicho hapo Juu, Mfalme Ahasuero anaachana na mkewe kutokana na ulevi
uliokithiri, yeye alikuwa amelwa sana pamoja na watu wake wote na sasa anataka
mkewe aletwe mbele ya watu wote iliawaonyeshe watu jinsi mkewe alivyo mrembo,
Malkia mke wa mfalme aliyeitwa Vashtiinaonekana anakataa kutii amri hiyo ya
kuitwa mbele za watu na kufanywa kituko, kutokana na kitendo hicho uhusiano wao
ulivunjika, Ulevi unavunja mahusiano, umevuruga mahusiano ya watu wengi sana
katika jamii, Sio tu mahusiano katika ndoa lakini vilevile hata na watu
tuliopaswa kuheshimiana nao ona mfano mwingine katika Biblia ambapo mtu mmoja
aliyeitwa Nabal alikuwa na maneno ya jeuri sana yaliyopelekea kuharibu uhusiano
wake na Daudi na sababu kubwa ya mtu huyu ilikuwa ulevi uliokithiri 1Samuel 25:5-17 “Daudi akatuma vijana kumi, Daudi naye
akawaambia hao vijana, Kweeni mwende Karmeli, na kumwendea huyu Nabali ili
mnisalimie; na hivi ndivyo mtakavyomwambia huyu aishiye salama, Amani na iwe
kwako, na amani nyumbani mwako, na amani kwao wote ulio nao. Nami sasa
nimesikia ya kuwa una watu wanaokata manyoya kondoo zako; haya! Wachungaji wako
wamekuwa pamoja nasi, wala hatukuwadhuru, wala hawakukosa kitu wakati wote
walipokuwako huko Karmeli. Waulize
vijana wako, nao watakuambia; basi na wakubaliwe vijana hawa machoni pako;
maana tumekujia katika siku ya heri; uwape, nakusihi, cho chote kitakachokujia
mkononi, uwape watumwa wako na mwanao Daudi. Basi walipofika vijana wake Daudi,
wakamwambia Nabali sawasawa na maneno hayo yote kwa jina la Daudi, kisha
wakanyamaza. Naye Nabali akawajibu wale watumishi wa Daudi, akasema, Huyu Daudi
ni nani? Na mwana wa Yese ni nani? Siku hizi kuna watumwa wengi wanaomtoroka
kila mtu bwana wake! Basi mimi je! Nitwae mkate wangu, na maji yangu, na
machinjo yangu niliyowachinjia hao watu wangu wakatao manyoya kondoo zangu, na
kuwapa watu ambao siwajui wametoka wapi? Basi vijana wake Daudi wakageuka,
wakaenda zao, wakarudi, nao wakaja wakamwambia sawasawa na maneno hayo yote.
Kisha Daudi akawaambia watu wake, Haya! Jifungeni kila mtu upanga wake. Nao
wakajifunga kila mtu upanga wake; Daudi naye akajifunga upanga wake; nao
wakapanda nyuma yake Daudi, wapata kama watu mia nne; na watu mia mbili wakakaa
na vyombo vyao. Lakini kijana mmojawapo alimpasha habari Abigaili, mkewe
Nabali, kasema, Tazama, Daudi alituma wajumbe kutoka nyikani waje ili kumsalimu
bwana wetu, naye akawatukana. Walakini watu hawa walitutendea mema sana, wala
hatukupata dhara, wala sisi hatukupotewa na kitu cho chote, wakati wote
tulipofuatana nao, tulipokuwako mavueni; watu hao walikuwa boma kwetu usiku na
mchana, wakati wote tulipokuwa nao tukiwachunga kondoo. Basi sasa ujue na
kufikiri utakayotenda; kwa sababu yamekusudiwa mabaya juu ya bwana wetu, na juu
ya nyumba yake yote; kwa kuwa yeye ni mtu asiyefaa kabisa, hata mtu hawezi
kusema naye.” Ni kutokana na majibu haya mabovu Daudi alikusudia
kumfutilia mbali Nabali na jamii yake yote lakini kupitia mkewe Nabal aliyeitwa
Abigaili ambaye alikuwa na akili sana aliweza kumzuia Daudi asimuue Nabali,
Hata hivyo baadaye Mungu alimuua Nabali, utaweza kuona aidha katika kisa hiki
pia tunaona Abigaili akijiombea kuolewa na Mwanaume asiyetumia mvinyo na
kuachana au kutamani mwanaume wake mlevi afe, hii ni wazi kabisa kuwa kutokana
na ulevi uliokithiri Mwanamke huyu alikuwa hafurahishwi na mwenendo mzima wa
kuwa na Mume mpumbavu ona 1Samuel
25:32-38 “Naye
Daudi akamwambia Abigaili, Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye
amekuleta hivi leo kunilaki; na ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe,
uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu
mwenyewe. Kwa kuwa ni kweli, aishivyo Bwana, Mungu wa Israeli, aliyenizuia
nisikudhuru, kwamba hungefanya haraka kuja kunilaki, hakika huyu Nabali
asingaliachiwa hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi. Basi Daudi
akapokea mkononi mwake vitu vile alivyomletea; akamwambia, Haya! Kwea kwa amani
kwenda nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimeukubali uso
wako. Kisha Abigaili alimjia Nabali; na tazama, alikuwa amefanya karamu
nyumbani mwake, kama karamu ya kifalme; na moyo wake huyo Nabali ukafurahiwa
ndani yake, kwa maana amelewa kabisa. Kwa sababu hiyo hakumwambia neno, dogo
wala kubwa, hata kulipopambazuka. Ikawa asubuhi, divai ilipokuwa imemtoka
Nabali, mkewe alimwambia mambo hayo, na moyo wake ukafa ndani yake, akawa kama
jiwe. Tena ikawa, yapata siku kumi baadaye, Bwana alimpiga huyo Nabali, hata
akafa.” Unaweza kuona sasa jinsi ambavyo mvinyo na ulevi uliokithiri
unavyoweza kuathiri mahusiano katika jamii.
10. Ulevi
husababisha vijana kuwa wakaidi kwa wazazi wao!
Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la vijana
kutokuwatii wazazi wao na kuwa wakaidi, Biblia imeagiza watoto kuwatii wazazi
wao katika bwana na tunaambiwakuwa hii ni amri ya Mungu yenye ahadi ya vijana
kupata heri na maisha marefu ona katika maandiko katika Kutoka 20:12 “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa
nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.” Na unaweza pia kuona katika Waefeso 6:1-3 “Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana,
maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya
kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.”
Unaweza kuona kumbe mpango wa Mungu ni kuwabariki watoto pale wanapowaheshimu
wazazi wao na sio kuwabariki lakini pia kuwapa maisha marefu, Lakini kutokana
na hali ya ukaidi unaosababishwa na ulevi ni jambo lakusikitisha kuwa katika
maandiko Mungu aliagiza kuwa kama wazazi watakuwa na mwana mkaidi asiyetaka
kutii wala kusikiliza maagizo yaokwa sababu ya ulevi walipaswa kumtoa katika
baraza la wazee na angehukumiwa kifo ona Kumbukumbu
21:18-21 “Mtu
akiwa na mwana mkaidi, mshupavu, asiyetii sauti ya baba yake, wala sauti ya
mama yake, nao wajapomwadhibu hawasikizi, ndipo babaye na mamaye na wamkamate,
na kumpeleka kwa wazee wa mji wake, katika lango la mahali pake; wawaambie
wazee wa mji wake, Huyu mwana wetu ni mkaidi, mshupavu, hasikizi sauti yetu; ni
mwasherati, tena ni mlevi. Waume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo
utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa.”
Unaweza kuona ni wazi kabisa kimaandiko kuwa kama ulevi lingekuwa ni swala la
uadilifu na linalokubalika mbele za Mungu basi Mungu asingeliweka adhabu kali
namna hii, Maandiko ynaonyesha wazi kuwa ulevi unaleta ukaidi na kuharibu
baraka ambazo mungu alikuwa amezikusudia kwa watoto.
11. Nchi ambayo
viongozi wake sio walevi imebarikiwa, Kwa kujibu
wa Muhubiri mwana wa daudi katika kitabu cha Muhubiri 10:17 “Heri kwako, nchi, mfalme wako
akiwa mtoto wa watu, Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate
nguvu, wala si kwa ajili ya ulevi.” Yaani
imabarikiwa nchi ile ambaye mfalme wake anakula kwa wakati ili apate nguvu na
wakuu wake hawana muda na ulevi unaweza kuona
12. Ulevi
unaharibu mwili wa Mwanadamu
Biblia iko wazi kabisa kuwa miili yatu ni
hekalu la Mungu aliye hai, Ni hekalu la Roho Mtakatifi 1Wakoritho 6:19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu
ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si
mali yenu wenyewe;” Mungu anajihusisha sana na namna tunavyoitumia
miili yetu, Matumizi ya pombe katika mwili huufanya mwili kuchakaa haraka kuna
madhara mengi ya aina mbalimbali yatokanayo na pombe katika miili yetu, yako
madhara ya muda mfupi yasababishwayo na pombe katika miili yatu lakini vilevile
yako madhara ya Muda mrefu
Madhara ya
muda mfupi ni pamoja na
a. Kutokuona vizuri kwa vile ulevi unasababisha
uoni hafifu
b. Kuyumba wakati wa kutembea au kushindwa
kutembea sawa sawa
c. Kuharibu hali ya mtazamo na hali ya kihisia,
na hivyo kuweza kujinyea kujitapikia, kujikojolea na hata kuwa mgomvi, na
kuropoka hovyohovyo
d. Kutokuweza kupambanua vema jambo jema na
jambo baya
e. Kupumua kwa shida na kukoroma pamoja kuamka
ukiwa na maluweluwe, haya ni Madhaya yasababiswayo na ulevi kwa muda mfupi mara
baaba ya kunywa pombe
Madhara ya
Muda Mrefu
Matatizo mengine yanayoweza kushababsihwa na
ulevi endelevu ni Pamoja na Kuzeeka
haraka, Magonjwa ya Moyo, matatizo ya kansa, matatizo ya Kongosho au
bandama, na kuharibika au kuungua ini,
kwa ujumla haya ni baadhi ya matokeo ya ulevi, kitaalamu kama wanawake watakuwa
wanatumia ulevi wanaweza kuwa na matatizo makubwa zaidi ya kiafya kuliko
wanaume na hata kama wanakunywa kiasi tu, Pombe huathiri karibu kila kiungo cha
mwili endapo itatumika kwa muda mrefu na pia inamueweka mtumiaji katika
uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na magonjwa mbalimbali
a.
Kusinyaa kwa Ubongo -
shrinking brain kisayansi matumizi ya muda mrefu ya Pombe hupelekea
tatizo la kusinyaa kwa Ubongo, ubongo ni moja ya sehemu muhimu sana yenye
maamuzi yote ya kimwili na kiroho, kuathiriwa kwa kiungo hiki muhimu ni
uharibifu mkubwa sana wa uumbaji wa Mungu katika mwili wa Mwanadamu.
b.
Kuathiriwa kwa mfumo wa fahamu – Njia nyepesi nya kujua kuwa Pombe
inaathiri mfumo wa fahamu ni namna mlevi anavyozungumza hii maana yake ni
kwamba pombe inaathiri utendaji wa Ubongo na hivyo kuharibu mpangilio wa meneno
yaani kunakuwa na mwasiliano mabovu yati ya uzungumzaji wako na ubongo, Pia
unakuwa na wakati mgumu jinsi na namna ya kutembea na ndio maana inashauriwa
kuwa kama unaendesha gari au mitambo ni vema kuacha au kuizia kama umekunywa,
Pombe ina madhara makubwa katika mfumo wako wa fahamu, Pombe ina uwezo wa
kukufanya usiweze kukumbuka vema na uwezo wako wa kutunza kumbukumbu unakuwa wa
Muda mfupi, uwezo wako wa kufikiri unaathiriwa, utendaji wa ubongo wa mbele FRONTAL LOBE unaathiriwa ubongo huu
ndio unaohusika na hisia, na kumbukumbu
za muda mfupi, na uwezo wa kufanya
maamuzi. hivyo matumizia endelevu ya pombe
yanaweza kupelekea kuharibika kwa ubongo.
c.
Tabia tegemezi -
Baadhi ya watu wanaokunywa pombe huweza kutengeneza tabia tegemezi ya
kihisia na kimiwli kwa pombe, yaani kwao kuja kuiacha Pombe linakuwa swala gumu
sana “alcoholic addiction”
d.
Magonjwa ya Moyo – Imethibitika kisayansi kuwa unywaji wa
Pombe una mchango mkubwa sana katika kusababisha magonjwa ya moyo kama vile
shambulio la Moyo, Pressure, na strok yaani kupooza
e.
Kuathiriwa kwa ini – Nchini Marekani zaidi ya watu milioni
mbili wanateseka na ugonjwa wa kuathiriwa kwa ini kunakotokana na ulevi, walevi
wa pombe wanaweza kuharibu maini yao, aidha wanaweza kuendeleza kuungua kwa
ini, kisukari, homa, ngozi kuwa ya njano, kuathiri njia ya mkojo na maumivu na
pombe ikiendelezwa inasababisha kifo, kifo kitokananacho na pombe na madhara
yanaweza kuepukika tu mtu akiacha kunywa
f.
Bandama
– Ni moja ya kiungu muhimu ambacho kazi yake ni kurekebisha mwenendo wa sukari
mwilini kwa kuzalisha kemikali iitwayo INSULIN
aidha bandama pia ina kazi ya kuchakata chakula tunachokula, unywaji wa
muda mrefu unywaji endelevu hupelekea bandama kuungua na kuanza kusababisha maumivu ya chembe cha
moyo, kiungulia na maumivu mengine
makali, kuhara na hatimaye kupunua uzito, aidha pombe iingiapo kwa wingi katika
bandama, huongeza uzaliswhaji mkubwa wa Enzymes ambazo ndio zenye uwezo wa
kuunguza bandama.
g.
Kuhara
- Matumizi ya pombe kupita kiasi
hupelekea kuharibiwa kwa utumbo mdogo na hivyo kupelekea kuwa na tatizo la
kuharisha mara kwa mara, na maumivu makali ya tumbo au vidonda vya tumbo
h.
Ugumba na utasa – Matumizi ya pombe kwa muda mrefu huweza
kupelekea watu wanaume kwa wanawake kupoteza uwezo wa kuzaa, na pia kuzalisha
homoni inayoweza kumfanya mwanaume kuwa kama mwanamke au kuwa na hamu ya
kuingiliwa kinyume na maumbile.
i.
Kupoteza nguvu za kiume – kwa kawaida wanaume wengi sana wanywaji
huwa wanajidanganya kuwa pombe huwaongezea mashamu shamu katika tendo la Ndoa
lakini ni ukweli unaokubalika kitaalamu kuwa matumizi endelevu ya pombe
hupelekea walevi kuwa watu dhaifu zana katika utekelezaji wa tendo la ndoa na
ulevi kupindukia huweza kupelekea kupoteza nguvu za kiume.
j.
Athari za mfumo wa chakula – unywaji wa Pombe unaathiri mfumo wa
usagaji wa chakula, matumizi ya Pombe endelevu yanaweza kusababisha utumbo
mwemabamba ushindwe kunyonya chakula kinachohitajika mwilini na matokeo yake
hupelekea kuwa na “Kwashakoo” “Malnutrition” na ndio maana wakati
mwingine utaweza kuona afya ya walevi ni kama haipendezi na wanakuwa na kitambi
fulani kisichi cha kiafya!
k.
Tatizo la Kiwango cha sukari –Bandama
inasaidia mwili uweze kutengeneza Insulin na kutumia vema glucose yaani
sukari inayotakiwa kuingia mwilini sasa pale Bandama na ini linaposhindwa
kuifanya kazi yake vema kutokana na pombe unaweza kuingia katika tatizo la
kupungua kwa sukari mwilini “Low blood
sugar” aidha kuharibika huko kwa bandama kunaweza kulifanya bandama
kutokuzalisha insulin ya kutosha kutengeneza sukari na inaweza kupelekea
kuruhusiwa kwa sukari nyingi sana kuingia katika damu, na mwili wako ukishindwa
kuweka uwiano wa sukari inayotakiwa mwilini kinachofuata sasa ni kupata ugonjwa
wa kisukari kwa hiyo watu wenye kisukari wanapaswa kuwa mbali na pombe.
l.
Tabia mbaya
– ulevi huweza kusababisha hata mtu mwenye akili timamu, na anayeheshimika
katika jamii kufanya jambo lisilotarajiwa kutokana na kulewa anaweza kujinyea,
kutapika, kujikojolea, kukojoa mahali ambapo sio chooni na hata au kutaka
kufanya mapenzi na mtu anayestahili heshima.
m.
Maluweluwe
– walevi wengi kutokana na unywaji wa pombe huwa wanaona maluweluwe au kuota
ndoto za mchana na ndio maana wakati mwingine unaweza kuona wakizungumza
wenyewe njiani ilhali hakuna mtu wa kumuitikia, wengine huimba pambio au
kuzungumza kiingereza wakichanganya na kikabila chao
n.
Lugha isiyoeleweka – walevi wakati mwingine kutokana na uwepo
wa Pombe wanashindwa kutamka vema maneno yakaeleweka kwa hiyo wanaropoka ropoka
tu
o.
Kansa
- Unywaji wa pombe kwa muda mrefu
unamuweka mtumiaji katika uwezekano mkubwa wa kupata aina fulani ya kansa kama
Kansa ya koo, uharibifu wa kisanduku cha sauti, kansa ya ziwa, kansa ya utumbo
mpana na sehemu ya kutolea haja kubwa
p.
Maambukizi katika Mapafu – watu wanaotumia pombe mvinyo wakao katika
hatari kubwa sana ya kupata matatizo ya mapafu na kuingiliwa na virusi au
bacteria wanaopelekea kupata pneumonia au Tb na matatizo mengine ya kifua
q.
Uchovu
– hisia za kuchoka sana huwa zinawapata walevi na hata kupelekea kupata
upungufu wa damu, ambao kwa vyovyote unaweza kuwa umesababishwa na ulevi
r.
Vidonda vya tumbo – Kunywa mvinyo kupita kawaida hupelekea
kujawa na gesi tumboni na kupelekea uwepo wa vidonda vya tumbo.
s.
Athari kwa mtoto aliyeko tumboni – unywaji wa Pombe unaweza kusababisha mtoto
aliyeko tumboni kuwa katika hatari kubwa sana, anaweza kuzaliwa njiti au kufia
tumboni au kufa muda mfupi tu mara baada ya kuzaliwa
t.
Kusinyaa kwa mifupa – unywaji wa pombe hupelekea tatizo la
kusinyaa kwa mifupa
u.
Kuyumba
yumba – kutokana na ulevi mwendo wa mnywa pombe unaweza kubadilika na kuwa
wenye kuyumba yumba
v.
Athari kwa afya ya uzazi – Walevi wengi huwa wanajidanganya wakidhani
kuwa Pombe huwa inawaongezea burudani wakati wa tendo la ndoa, Lakini ilivyo ni
kwamba wanaume wanaokunywa pombe sana wanapoteza uwezo wa nguvu za kiume,
unywaji wa pombe unaweza kuathiri, uzwalishaji wa homones zinazochechea tendo
la ndoa na pia inaua kabisa hamu ya tendo hilo, wanawake wanaokunywa sana
huacha kuona siku zao za hedhi na hivyo
kuwa katika uwezekano mkubwa wa kuwa tasa, wanawake wanaokunywa sana wakati wa
ujauzito wanaweza kuharibu mimba au
kuzaa watoto njiti, au mtoto mfu. Aidha kama watazaa mtoto atakuwa na ugumu
katika kujifunza, matatizo ya kiafya, matatizo ya kihisia uwezekano wa kuwa na
ulemavu.
Kwa hiyo sasa unaweza kuona kwa unywaji wa
Pombe tunasaidia kwa kiwango kikubwa kuharibu maisha yetu na ya wengine Pombe
ina madhaya Kimwili, kiakili na kiroho na ndiomaana haishangazi kuona kuwa
Biblia inaonya watu wasitumie mvinyo, aidha vyanza vongi vya ajali za
barabararani pia vimebainika kuwa moja ya sababu zinazopelekea kutokea kwa
ajali hizo ni pamoja na ulevi Mungu anataka kutuepusha na swala hili.
Mvinyo au
Divai Katika Maandiko.
Tunapoendela kujifunza somo hili sasa ni
muhimu kwetu tukaendelea kuangalia kwa undani hasa neno Divai au mvinyo katika
maandiko lilimaanisha nini, hii itatusaidia kuweza kutambua ni aina gani ya
mvinyo ulitumiwa wapi na kwa sababu gani kwa mfano unaposoma
Luka 7:33-34 “Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo. Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa; nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi.”
Hapo unaweza kuona jinsi neno la Mungu linavyoonyesha kuwa Yohana hakutumia divai na Yesu anakiri kuwa alitumia alikunywa, kwa hivyo watu wengi wasio na akili timamu hufikiri kuwa Yesu alikunywa mvinyo
Luka 7:33-34 “Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo. Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa; nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi.”
Hapo unaweza kuona jinsi neno la Mungu linavyoonyesha kuwa Yohana hakutumia divai na Yesu anakiri kuwa alitumia alikunywa, kwa hivyo watu wengi wasio na akili timamu hufikiri kuwa Yesu alikunywa mvinyo
Maana ya neno Divai – Kwa kawaida neno Divai
au mvinyo lilipotumiwa katika biblia lilitumika kumaanisha aina kubwa mbili za
Divai au mvinyo, neno hili kwa kiibrania linatumika neno “YAYIN” na kiyunani “OINOS”
Maneno hayo yalimaanisha Divai au mvinyo
wa aina kubwa mbili
1.
Divai ya mzabibu iliyochachwa – Fermented grape juice
2.
Divai ya mzabibu isiyochachwa – Unfermented grape juice
Ni muhimu kufahamu kuwa neno hilo la kiyunani
Oinos lilitumika kwa aina zote mbili
za juisi ya mzabibu, Kwa hiyo neno oinos lilikuwa neno la jumla la juisi za
aina zote mbili, kama vile matumizi ya Mikate iliyochachwa na mikate
isiyochachwa, Kwa msingi huo waandishi wa Biblia walijitahidi sana kuonyesha
matokeo ya juisi iliyotumika kivitendo ili kusaidia watu waweze kujua ni aina
gani ya Divai ilitumika katika tukio husika, Lakini Biblia pia hutumia neno Nzuri, au njema, au tamu au tunda la
mzabizu au uzao wa mzabibu kwa divai siyoyochahwa na kuitofautisha na ile
iliyochachwa kwa mfano
a.
Waefeso 5:18 “Tena
msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;” unaweza kuina katika neno hili biblia ya
kiyunani inatumia neno Oinos lakini
mwandishi anaonyesha kwamba hii ina ufisadi kwa hiyo hapo ni wazi kuwa mvinyo
unaotajwa hapo ni ule wenye kulewesha ambao sio sahihi kutumiwa na watu wa
Mungu
b.
Ufunuo 19:15 “Na
upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye
atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu
ya hasira ya Mungu Mwenyezi.” Hapa sasa
tunaweza kuona tena mvinyo ukitajwa na katika kiyunani neno linalotumika tena
hapa ni Oinos sasa tofauti kubwa
iliyoko hapa ni kuwa Yesu atakanyaka shinikizo la mvinyo unajua maana yake?
Neno shinikizo katika biblia ya kiingereza wanatumia neno “winepress” yaani ni mashine
ya kukamulia zabibu kwa hiyo hapa inazungumziwa mvinyo au divai isiyo na kilevi
unaweza kuona ! sasa basi zabibu ile iliyo safi ilipatikana pale shinikizoni inapotengenezwa
kabla ya michakato mingne Isaya 16:10 “Na furaha imeondolewa, na shangwe toka mashamba yaliyozaa
sana; hapana kuimba katika mashamba ya mizabibu, wala sauti za furaha;
akanyagaye hakanyagi divai katika mashinikizo; nimeikomesha sauti ya furaha
yake akanyagaye.” Unaweza kuona kwa msingi huu kwamba hata ile
iliyokuwa ikikamuliwa na haijachachushwa bado iliitwa Divai au mvinyo kwa lugha
ileile kwa aina zote mbili za mvinyo au Divai
c.
Namna walivyohifadhi Divai isiyochachwa – Katika Israel kulikuwa na namna ya kuhifadhi
divai isiyochachwa. Maji ya zabibu yalipokamuliwa waliyahifadhi chini ya nyuzi
joto 10 Centgrade, walitengeneza
chombo na kuiweka divai humo kisha walikiziba chombo kile ili hewa isiingie na
maji mengine yasiingie na walikizamisha
chombo hicho ndani ya maji au chombo chenye maji ya baridi kwa kuhakikisha kuwa
hakuna sehemu inachungulia nje au kutokea juu waliweka hivyo kwa siku 40 na
ukiitia kutkka hapo hakuna uwezekano tena wa juisi hiyo ya mzabibu kuchacha na
itaendela kuwa na utamu uleule kwa mwaka mzima
d.
Njia
nyingine ya kuhifadhi zabibu ilikuwa ni kuzichemsha.
Je Yesu alitumia Divai au mvinyo wa aina
gani?
Yesu na
wanafunzi wake walitumia juisiya mzabibu isiyochahwa! Na hakutumia mvinyo wenye
kulkevya kabisa Mathayo 26:26-29 “Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki,
akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu
Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; kwa
maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo
la dhambi. Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa
mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba
yangu.”
Marko 14:22-25 “Nao
walipokuwa wakila, alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa, akasema,
Twaeni; huu ndio mwili wangu. Akatwaa
kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote. Akawaambia, Hii ndiyo damu
yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. Amin, nawaambia ninyi, Sitakunywa
tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa
Mungu.”
Luka 22:17-18. “Akapokea
kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi; Maana
nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu
utakapokuja.”
Unaweza kuona
kile Yesu alikuwanywa na wanafunzi wake kinaitwa mzao wa mzabibu au tunda la
mzabibu hii inamaamisha nini? Yesu na wanafunzi wake hawawezi na wasingeliweza
kutumia mvinyo uliochwachwa kwa sababu
katika Biblia chachu ilikuwa ni sihara ya dhambi na kwa msingi huo wayahudi
walipaswa kuwa mbali na chachu yoyote katika mikate na katika divai mtu ambaye
angekuwa na chachu ya aina yoyote hususani wakati wa Pasaka alipaswa kufa kwa
mujibu wa Torati ona
Kutoka 12:14-20 “Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba; siku hiyo ya kwanza mtaondoa chachu yote isiwe katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula mkate uliochachwa tangu siku hiyo ya kwanza hata siku ya saba, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na Israeli. Siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yo yote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu. Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele. Mwezi wa kwanza, siku ya mwezi kumi na nne, wakati wa jioni, mtakula mikate isiyochachwa, hata siku ya mwezi ishirini na moja jioni. Muda wa siku saba isionekane chachu katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula hiyo iliyotiwa chachu, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli, akiwa mwenye kukaa hali ya ugeni, au akiwa mtu aliyezaliwa katika nchi. Msile kitu chochote kilichochachwa; mtakula mikate isiyochachwa katika makao yenu yote.”
Kutoka 12:14-20 “Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba; siku hiyo ya kwanza mtaondoa chachu yote isiwe katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula mkate uliochachwa tangu siku hiyo ya kwanza hata siku ya saba, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na Israeli. Siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yo yote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu. Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele. Mwezi wa kwanza, siku ya mwezi kumi na nne, wakati wa jioni, mtakula mikate isiyochachwa, hata siku ya mwezi ishirini na moja jioni. Muda wa siku saba isionekane chachu katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula hiyo iliyotiwa chachu, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli, akiwa mwenye kukaa hali ya ugeni, au akiwa mtu aliyezaliwa katika nchi. Msile kitu chochote kilichochachwa; mtakula mikate isiyochachwa katika makao yenu yote.”
Neno la
Mungu lilikuwa limepiga marufuku matumizi ya chachu ya aina yoyote yaani “SEOR” au hamira kwa Kiswahili
haikupaswa kuwa karibu kabisa nyakati za Pasaka kwa sababu SEOR au chachu iliashiria uharibifu au dhambi Luka 12:1 “Wakati huo, makutano walipokutanika
elfu elfu, hata wakakanyagana, alianza kuwaambia wanafunzi wake kwanza,
Jilindeni na chachu ya Mafarisayo, ambayo ni unafiki.”
1Wakoritho 5:6-8 “Kujisifu
kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima? Basi,
jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile
mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka,
yaani, Kristo; basi na tuifanye
karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa
yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.”
Kumbe chachu
au hamira katika maandiko humaanisha dhambi, kama Yesu na wanafunzi wake
wangetumia mvinyo wenye kilevi ni dhahiri kuwa Yesu hangefaa kuwa Pasaka wetu,
hangefaa kuwa Sadaka ya ukombozi wa mwanadamu hata kidogo kama Yesu ndiye
Pasaka wetu na wakati wa Pasaka chachu haikuruhusiwa kabisa ni dhahiri kama
Yesu angetumia chahu yoyote hangefaa kuwa Pasaka yetu Kutoka 13:7 “Mikate isiyochachwa italiwa katika hizo siku saba mkate uliotiwa chahu
usionekane kwako ndani ya mipaka yako yote”
Je Yesu aligeuza maji kuwa Divai?
Mojawapo ya hoja kubwa sana ya watu wanaotetea pombe au mvinyo kwa kutumia maandiko hujengwa pia katika muujiza wa kwanza alioufanya Yesu wa kugeuza maji kuwa divai huko Kana- Galilaya katika arusi ambayo yeye alialikwa na andiko linalotumika ni
Yohana 2:1-11 “. Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni. Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu. Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi, akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa. Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.”
Je Yesu aligeuza Maji kuwa Divai jibu ni ndio, Lakini ni muhimu kwetu kuwa na ufahamu wa kutosha kuwa ni aina gani ya divai Yesu aliifanya katika muujiza huu, kwa sababu ni ukweli usiopingika kuwa kama Yesu alitengeneza Divai au mvinyo wenye kulewesha basi ni halali kwa watu kunywa mvinyo, ni halali kuuzalisha, ni halali kuuuza, na ni halali kuuhifadhi na sio uvunjifu wa maadili kuunywa na Yesu angekuwa na Mchango mkubwa sana katika uharibifu wa maisha ya Mwanadamu tofauti na tulivyoona hapo juu, Katika vipengele vilivyotutangulia
Balasi moja lilikuwa lina uwezo wa kuingia kati ya ndoo 20-30, na kama utazidisha mara sita maana yake Yesu alitengeneza Divai ndoo kati ya 120-180, na kama hii ilikuwa ni Pombe basi katika harusi ile kulikuwa na ulevi uliopindukia ambao haujawahi kutokea katika harusi yoyote ile
Aidha katika mstari wa 10 tunaambiwa kuwa Divai ile ilikuwa njema sana, hii ina maana kuwa kama kile alichikitengeneza Yesu ilikuwa mvinyo wenye pombe basi kwa ndoo kati ya 120-180 Yesu alikuwa amechangia kiwango kikubwa mno cha pombe katika muujiza wake wa kwanza na hivyo hangeweza kuwa kiongozi asiye na dhambi.
Divai njema aliyotengeneza Yesu katika biblia ya kiyunani hapa linatumika neno “TYROSH” yaani toka kwenye zao la zabibu. ni kama ambavyo “crude oil” ikipitia refining process hutoa petrol, diesel, kerosene etc vivyo hivyo zao la zabibu hutoa divai kileo, divai pure juice, divai dawa, zabibu kavu etc
haya ni majina yanayotofautisha aina hizo kama yanavyoonekana kwenye hebrew bible(tanakh) na greek bible(septuagint)
· tyrosh pure juice of cana (john 2) yaani ile aliyoifanya Yesu kwa muujiza ilikuwa ni Juice ya mzazbibu isiyochachwa’
· yayin the most common wine in the bible
· chekar
· mamchak
· gath
Yesu alitengeneza Divai njema yaani Mzao wa mzabibu usiochachwa ! yaani hakukuwa na Pombe pale Kana ya Galilaya, Yesu mwenyewe katika mahubiri yake alikemea ulevi Luka 12:45-46 “Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini”
Hakuna andiko lolote linalohalalisha mtu kutumia Pombe katika agano jipya na msingi wa kimaandiko umeonyesha na shuhuda za kibinadamu zimeonyesha kuwa Pombe ni tatizo
Hitimisho:-
1.
Warumi 14:21 - Ni
vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lo lote ambalo kwa
hilo ndugu yako hukwazwa.
2.
1Wakoritho 6:9-10, Au
hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike;
waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi,
wala wafiraji, wala walawiti,. wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala
watukanaji, wala wanyang'anyi.
3. Warumi
13:13 - Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa
ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.
4. Mtu
anawezaje kuacha Pombe?
a.
Kwa
kumuamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake, my akiokoka anaweza
kubadilishwa maisha na kuwa mbali na pombe
b.
Kwa kuomba
kama kuna jambo lolote hulipendi mwambia Mungu omba funga na kuomba na Mungu
atakusaidia kuwa mbali na pombe
Na Rev.Innocent Kamote.
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima’
0718990796
Maoni 1 :
Your Affiliate Profit Machine is ready -
And making money online using it is as easy as 1, 2, 3!
Follow the steps below to make money...
STEP 1. Input into the system which affiliate products you want to push
STEP 2. Add some PUSH BUTTON traffic (it LITERALLY takes 2 minutes)
STEP 3. Watch the affiliate products system explode your list and sell your affiliate products on it's own!
Are you ready to make money automatically?
Check it out here
Chapisha Maoni