Warumi 1:26-29 “Hivyo Mungu
aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili
kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume
nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa,
wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao
yaliyo haki yao. Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu
aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na
tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia
mbaya, wenye kusengenya,”
Utangulizi:
Ni
muhimu kufahamu kwamba tunaishi katika Nyakati wa Mwisho sana; Maandiko
Matakatifu yanatuonya kwamba katika nyakati hizi za mwisho tunapaswa kuwa na
akili na kukesha katika sala, yaani kudumu katika kuomba na tunaonywa kuwa nyakati
hizi ni nyakati za hatari, Moja ya matukio Mabaya ambayo yataongezeka katika
nyakati hizi za mwisho ni pamoja na kuongezeka kwa uovu na mmomonyoko mkubwa wa
kimaadili, zikiwemo dhambi za ushoga au mapenzi ya jinsia moja, Dhambi hizi
zilikuweko tokea awali lakini katika nyakati za leo zimeongezeka na kuenea kwa
kasi zaidi kuliko kawaida kutokana na kukua kwa teknolojia na kupanuka kwa
utandawazi.
2Timotheo
3:1-4 “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati
za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha,
wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na
shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu,
wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye
kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;”
Katiika
nyakati hizi za hatari duniani Moja ya dhambi inayoashiria kuharibika kwa
kiwango kikubwa cha mwanadamu ni pamoja na kuongezeka kwa dhambi ya ushoga na kwa bahati mbaya Dunia imelikalia kimya
suala hili, Mataifa viranja wanalifanyia kampeni za makusudi ili swala la
mapenzi ya jinsia moja liweze kuenea na kukubalika kwa ulimwengu ili yamkini,
lionekane kuwa ni swala la kawaida na wanaolifanya waweze kujisikia
kutokuhukumiwa na dhamira zao kwa vile kilio cha wengi ni harusi; Lakini watumishi wa kweli ya Mungu hawawezi
na wala hawataweza kulinyamazia swala hili kwani Bwana ametupaka mafuta
tuwaambie watu Njia za bwana zilizonyooka!
Swala
la Mapenzi ya jinsia moja liko kinyume na maandiko na utamaduni wa kibinadamu,
lakini limeenea limeingia katika kila dini na madhehebu, limekaliwa kimya na
baadhi ya watu wameanza kulipitisha kisheria na hata kukubaliana na kuozesha
watu wa jinsia moja: Lazima tuseme wazi kuwa hapa Dunia imepotoka mno,Dunia
imelewa Dunia imewayawaya kama mlevi, Dunia imepinduka kama machel, Dunia
imeoza, hapa hatuwezi kupakalia kimya, wala ahtuwezi kuwapaka watu mafuta kwa
mgongo wa chupa ni lazima tujikumbushe msimamo wa Kibiblia kuhusu swala hili. Hii
ni dhambi na ni hatari kwa afya na maisha ya mwanadamu, Kiroho, Kimwili,
kiakili na kisaikolojia.
Wengine
wanadai kuwa wamezaliwa wakiwa namna hii, wanaamini kuwa ni tatizo la
kimaumbile, au mvurugiko wa homoni katika miili yao na kuwa swala hili ndio
limepelekea wao kuwa na uhitaji wa mapenzi ya jinsi moja, swali kubwa la
kujiuliza je kuna ukweli kuwa watu huzaliwa Shoga? Wengi sasa wanadai kuwa
wamezaliwa hivyo na ndio maumbile yao na wako tayari kudai haki ya kutambuliwa
kama watu wengine katika jamii, Lakini je Neno la Mungu linasema nini juu ya
swala hili? Neno la Mungu liko wazi kuwa swala hili ni dhambi na linatokana na
tamaa na kutaka kufanya majaribio kunakotokana na mgandamizo wa kufikiriwa kuwa
swala hili ni zuri kutoka katika jamii, marafiki, ndugu na kadhalika lakini
swala hili sio mpango wa Mungu na ni wazi bila kupaka mafuta kuwa liko kinyume
na mapenzi ya Mungu na hakuna utetezi wa kisayansi wala kisaikolojia Neno la
Mungu linatutaka tujiepushe na jambo hili tuliangalie neno:-
Msimamo wa Neno Kuhusu
Mapenzi ya jinsia moja.
Neno
la Mungu ndio mamlaka ya mwisho, na ya juu zaidi ya mwanadamu, Neno la Mungu
ndio taa ya miguu yetu, neno la Mungu ndio Muongozo wetu, Neno la Mungu lina
maelekezo yote yatupasayo wanadamu namna na jinsi ya kuenenda na ni Katika neno lake Mungu hufunua mapenzi yake,
katika neno lake Mungu hutupa maelekezo sahihi, na namna ya kuishi na kuenenda Biblia inasema
hivi:- tunapozungumzia dhambi ya ushoga au mapenzi ya jinsia moja ni muhimu
kwanza tukawa na ufahamu kuhusu misamiati inayotumiwa na dunia kulizungumzia
swala hili
·
Homosexuality - the quality or
characteristic of being sexually attracted solely to people of one's own sex,
Hali yoyote ya kujisikia au kuvutiwa kimapenzi na mtu wa jinsia kama yako au mtu
jinsia moja (Ushoga)
·
Bisexuality is - romantic attraction, sexual attraction, or
sexual behavior toward both males and females, or to more than one sex or
gender. Hali yoyote ya kujisikia kuvutiwa kimapenzi na mtu wa jinsia yoyote ya
kiume au ya kike (hawani watu wanaochanganya kotekote)
·
Heterosexual - sexually attracted to people
of the opposite sex, Hali ya kuvutiwa au kujisikia kufanya mapenzi na
mtu wa jinsia tofauti na yako hii ndio ngono ya kawaida.
·
Asexual - (‘ace’ for short) is someone
who does not experience, or experiences very little, sexual attraction
Hali ya kutokujisikia wala kuvutiwa kufanya ngono kabisa au kutokuvutiwa kabisa na maswala ya
ngono
Katika aina hizo za matumizi ya kingono
tutaangalia zaidi aina hizo kubwa mbili za ngono ambazo ziko kinyume na mapenzi
ya Mungu na ndizo ambazo tunatumia neno ushoga kuzitaja japo lugha ya kibiblia
inakazia mapenzi ya jinsia moja, yaani mwanamke kwa mwanamke au mwanaume kwa
mwanaume hii ndio dhambi ambayo Maandiko yanaikemea na kuikataza kwa kiwango
kikubwa sana! Tuliangalie sasa neno la Mungu katika swala
hili!
Walawi 18:22, 24-25 “Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.
Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa
nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote; na hiyo nchi
imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi
yatapika wenyeji wake na kuwatoa”.
Unaweza
kuona kuwa mojawapo ya sababu ya kufutiliwa mbali kwa mataifa
yaliyoimiliki kanaani ni kwasababu ya dhambi za aina hii, Mungu anawaonya
Israel kuwa inchi itawatapika watu watendao mambo mfano wa hayo, taifa
linalotenda mambo ya jinsi hii au kuruhusu mambo ya jinsi hii linajiweka katika
wakati mbaya na mgumu wa hukumu ya Mungu,
Mungu hulifuta au kumfuta mtu awaye yote anayetenda machukizo ya kiwango hiki
cha kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Mapenzi ya jinsia moja ushoga huitia nchi
unajisi na kuiharibu! Ardhi au nchi ikilaaniwa inawatapika watu wake yaani
inawakataa inawaua kwa sababu iliumbwa kwaajili ya utukufu wa Mungu, wakati
wowote dunia inapo hukumiwa ni lazima tuelewe insababishwa na aina hii ya uovu
pamoja na maovu mengine.
Mwanzo 19 inatupa habari za miji ya Sodoma na Gomora namna Mungu
alivyoweza kutuma malaika wakaihukumu miji hii kwa moto kutokana na kukithiri
kwa aina hii ya dhambi, Watu wa miji ya Sodoma na Gomora waliharibika kiasi cha
kutokutamani tena kulala na mwanamke na walitamani sana kufikia ngazi ya
kutamani wanaume wapya na wageni waliotembelea nchi yao! Akili zao zilikuwa
zinawaza ni mwaume gani hajabikiriwa bado wambikiri, bikira za wanawake kwao
hazikuwa tena na maana, wanawake kwao hawakuwa na maana wao walikuwa wanatamani
mwanaume mpya wamfundishe mambo ya kisodoma, Mungu alipothibitisha kuwa uovu
umefikia kiwango hiki alikusudia kuwaangamiza wote kwa moto na salfa kutoka
mbinguni kwa kutumia malaika zake ona:-
Mwanzo 19:1-13 “ Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na
Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda
kuwalaki, akainama kifudifudi. Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie
nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na
mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha.
Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu,
akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala. Hata kabla hawajalala, watu wa mji,
wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka
pande zote. Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako
usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua. Lutu akawatokea mlangoni, akafunga
mlango nyuma yake. Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi.
Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu
mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa
wamekuja chini ya dari yangu. Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu
mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi
tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu,
wakakaribia wauvunje mlango. Lakini wale watu wakanyosha mikono yao,
wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango. Kisha wakawapiga hao watu
walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta
mlango. Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao,
na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa; maana
tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za BWANA;
naye BWANA ametupeleka tupaharibu.”
Ni
jambo la kusikitisha kuwa Mungu aliwatuma wageni Malaika kule katika Mji wa
Sodoma na Gomora, Lutu kama mtu mwenye haki alikuwa mwenyeji wa wageni hao,
watu wa mji yaani wenyeji walikuwa wamejawa na tamaa kubwa ya ngono za jinsia
moja waliwataka wageni hao ili wafanye nao mapenzi ya jinsia moja lilikuwa ni
jambo lenye kushangaza, kwani hata Lutu alipokataa kutoa ushirikiano wa kuwatoa
wageni wake walimuahidi kumfanyia yeye kitu mbaya kuliko hao wageni wake, Hali
ilikuwa mbaya Malaika waliingilia kati na kumuokoa Lutu na walieleza kuwa Mungu amewatuma waweze
kupaharibu mahali hapo kutokana na uovu wake.
Ni
jambo lenye kushangaza sana kwamba ulimwengu wa leo umefikia kiwango cha aina
hii cha uharibifu ambao hata wanyama hawajawahi kufikia, Ndoa za jinsia moja ni
kielelezo cha juu zaidi cha uharibifu wa Mwanadamu, Ushoga ni uharibifu wa juu
zaidi wa uadilifu wa mwanadamu, Leo hii watu wa mataifa yenye nguvu ndio wanaoshawishi
dunia ifikie huko kwa madai ya kivuli cha haki za binadamu na haki za mashoga,
tunaweza kuheshimu mambo mengine kuhusu haki za binadamu, lakini hatuwezi
kukubali kutoa kipaumbele kwa jambo lolote lile ambalo liko kinyume na na Neno
la Mungu, swala la Mapenzi ya Jinsia moja Mungu amelikataza na analichukulia
kwa uzito mkubwa mno, na pia analishughulikia kwa uzito pale inapobidi, na
ameiweka dhambii hii kuwa ni kilele cha uharibifu wa juu zaidi wa mwanadamu.
Warumi 1:26-32 “Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu,
hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi
ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata
nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Na kama walivyokataa kuwa
na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa,
wayafanye yasiyowapasa. Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na
ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya,
wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye
kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio
na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu,
ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu,
bali wanakubaliana nao wayatendao.”
Mungu
hangeweza kuweka katazo la aina hii kama angekuwa anakubaliana kuwa kuna watu
amewaumba au wamezaliwa na mfumo wa aina hii, kuna uwezekano wa kisayansi wa
mtu kuzaliwa akiwa na homoni nyingi za kike au za kiume lakini uko uwezekano wa
kutumia dawa zenye kuleta, uwiano wa homoni na kumfanya mtu awe sawasawa, sio hivyo tu mwanadamu wa asili yoyote ile na wa
jinsia yoyote ile anapaswa kuishi kwa kiasi na hivyo ni lazima itambulike wazi
kuwa swala la Ushoga ni dhambi kama ilivyo dhambi ya ukahaba kwa vile ni matumizi
mabaya ya makusudi ya tendo la Ndoa ambalo Mungu alikusudia lifanyike katika
utaratibu uliokusudiwa
Neno la Mungu katika torati
lilikataza tabia ya umalaya na tabia ya ushoga, Mungu hakutaka iwe hivyo kwa
wayahudi (Israel ) na kwa taifa lolote lile. Aidha kila mzazi na wana jamii
wanapaswa kuwafundisha vijana mapema kuwa na ufahamu sahihi kuhusu NGONO “sex
orientation” na kuwahimiza kujitambua mapema kuwa wao ni wajinsia gani na wanatakiwa
kuishi vipi na kuwa na tabia zipi, Wazee wetu zamani walikuwa na tabia za
kukuza sana uanaume na kuupona uanawake kwa sababu za misingi za kujaribu
kuwatofautisha au kuwasaidia kujitambua kuwa wao ni nani:- maandiko yanakataza
kuweko kwa mashoga au Makhanisi miongoni mwa watu wa Mungu!
Kumbukumbu la Torati 23:17 “Pasiwe na kahaba katika binti za Israeli, wala
pasiwe na hanithi katika wana wa Israeli wanaume.”
Mungu anataka kulilinda tendo la
Ndoa lifanyike katika usafi na utaratibu, hawezi Mungu kuachia swala la ngono
lifanyike hovyohovyo na ndio maana utaweza kuona kuna makatazo makali sana
kuhusu swala hili, shetani anajua namna anavyoweza kuwaangamiza wanadamu kiafya
na kiroho na kisaikolojia na ndio maana nyakati za leo Maelfu kwa maelfu ya
watu wanavutwa kwa wingi kuingia katika ngono hizi zilizo kinyume na maumbule
ya asili, na zisizo salama shetani ana wajumbe wake ambao wanaitetea ili
iaonekana ni ya kawaida huku watu wote hasa watu wa Mungu wakiwa wamenyamaza
kimya, wakati biblia inakataza sio tu kutenda bali hata kukubaliana na
wanaotenda hayo ni machukizo kwa Bwana Mungu wetu na jambo hili ni lazima
lieleweke wazi hivyo.
Paulo mtume anapowataja watu ambao
hawataingia katika ufalme wa Mungu kwa uzito kabisa hajaacha kuwataja watu
wanaoshiriki ngono ya jinsia moja au wanaowafanyia wenzao aina hii ya ngono,
sio hivyo tu bali onyo limetolewa pia kwa wale wanaowafanyia wake zao kinyume
na maumbile, angalia jinsi neno la Mungu lilivyo wazi kuhusu swala hili!
1Wakoritho 6:9-10 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu?
Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu,
wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala
walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.”
Kumbe basi maandiko katika agano la
kale na agano jipya yamerejea kwa wingi kwa kina na kwa upana na urefu katazo
la Neno la Mungu kuhusu aina hii ya uovu!
Mapenzi ya jinsia moja ni dhambi
Ni muhimu kufahamu kuwa mapenzi ya
jinsia moja kwa mujibu wa maandiko ni dhambi, Mungu yuko kinyume kabisa na
mapenzi ya jinsia moja kwa sbabau ni kinyume na mapenzi yake na mpango wake wa
uumbaji, Mapenzi ya jinsia moja yanaharibu kabisa Mfumo wa mwanadamu kimwili,
kiroho na kiuadilifu lakini pia unaharibu kabisa mpango mzima wa Mungu kuhusu
tendo la ndoa ambalo Mungu amelikusudia lifanyika katika utakatifu na utaratibu
uliowekwa na Mungu chini ya baraka ya kuizaliana na kuongezeka, Kwa mujibu wa
maandiko dhambi ya Ushoga inachukua nafasi ya juu kabisa ya dhambi ambazo ni
machukizo kwa Mungu Biblia inakemea kwa ukali zaidi swala hili katika maandiko
kadhaa yafuatayo:-
1. Mambo ya walawi 18:22-24 “Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke;
ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala
mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko. Msijitie
unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa
mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote;”
2. Mambo ya walawi 20:13 “Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama
alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao
itakuwa juu yao.”
3.
Warumi
1:22-32 “Wakijinena kuwa
wenye hekima walipumbazika; wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa
mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya
vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao,
waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili
kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba
anayehimidiwa milele. Amina. Hivyo Mungu
aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili
kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya
mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata
nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Na kama walivyokataa kuwa
na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa,
wayafanye yasiyowapasa. Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na
ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya,
wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye
kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio
na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu,
ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu,
bali wanakubaliana nao wayatendao.”
4.
1Timotheo 1:9-11 “akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu
wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na
wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na
wauaji, na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa
uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye
uzima; kama vile ilivyonenwa katika Habari Njema ya utukufu wa Mungu
ahimidiwaye, niliyowekewa amana.”
5.
1Wakoritho
6:9-10 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu?
Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu,
wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala
walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. “
6.
Wagalatia 5:19-21 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati,
uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu,
uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi,
ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama
nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo
hawataurithi ufalme wa Mungu.’’
7.
1Wafalme 14:21-24 “Naye Rehoboamu mwana wa Sulemani akatawala katika
Yuda. Rehoboamu akaanza kutawala alipokuwa mwenye miaka arobaini na mmoja,
akatawala miaka kumi na saba huko Yerusalemu, mji aliouchagua Bwana miongoni
mwa kabila zote za Israeli, ili aliweke jina lake huko. Na jina la mamaye
aliitwa Naama, Mwamoni. Basi Yuda wakafanya maovu machoni pa Bwana; wakamtia
wivu, kwa makosa yao waliyoyakosa, kuliko yote waliyoyafanya baba zao. Maana
hao pia wakajijengea mahali pa juu, na nguzo, na maashera, juu ya kila kilima
kirefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi. Na mahanithi walikuwako
katika nchi, wakafanya sawasawa na machukizo yote ya mataifa Bwana aliowafukuza
mbele ya wana wa Israeli.”
8.
Kumbukumbu 22:5 “Mwanamke asivae
mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana
kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.”
9. Kumbukumbu 23:1 “Aliyejeruhika
konde, au aliyekatika tupu yake, asiingie mtu huyo katika mkutano wa Bwana.” Mstari huu katika biblia ya kiingereza NIV
unasomeka hivi “ No one who has been emasculated m by crushing or cutting may enter the assembly
of the LORD. Neno EMASCULATED maana yake katika iingereza linasomeka hivi -
Emasculation
of a human male is the removal of both the penis and the testicles, the
external male sex organs. Depending on the context, this may be seen as
consensual body modification, or non-consensual genital mutilation ni tendo la kuondoa sehemu za kiume za
nje ni mtindo wa kuasi au wa kubadilisha
maumbile Transgender na kumfanya mtu aliyekuwa na maumbile ya kiume kuwa ya
kike wengine huwaita “SHEMALES” au “LADYBOYS” katika
nyakqati hizi za uwepo wa dhambi hii sasa dunia imefikia hatua ya kuwa na
majike dume shemales au ladyboys
waliongeza jinsia ya tatu ukiacha mbili alizoziumba Mungu.
10.
Yuda 1:7 “Kama vile Sodoma na
Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na
hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili,
wakiadhibiwa katika moto wa milele.” Unaona maandiko yote
hayo hapo juu ni makatazo kuhusu dhambi hii ya kushiriki mapenzi ya jinsia
moja, ukaka poa au u dada poa katika maandiko haukubaliki
Kwa nini Biblia iko kinyume na ushoga?
Biblia inaonyesha kuwa ushoga ni dhambi ya kiwango cha juu
zaidi kuliko kuabudu miungu, ulevi na anasa, kutokumcha Mungu na kadhalika Biblia
inaonyesha wazi kuwa Walawiti na wafiraji hawataurithi ufalme wa Mungu, Dhambi
ni dhambi lakini inapofikia wanadamu wakaanza kufanya dhambi hii ambayo maandiko
huiita machukizo Maana yake ni kwamba mwanadamu ameharibika kwa kiwango cha
ngazi ya juu mno, inapofikia ngazi yoyote maandiko yakakuonyesha kuwa watu wameharibika
lazima neno la Mungu litagusia kuwepo kwa dhambi ya ulawiti na ufiraji unapoona
hili limetajwa mahali maana yake ni kuwa mwandishi anataka kukuonyesha kiwango
cha juu zaidi cha uharibifu, kwa nini neno la Mungu linatuonye dhidi ya
kushiriki mapenzi haya ya jinsia moja?;-
1. Ufiraji na
ulawiti au usagaji na ushoga unaashiria kiwango cha juu zaidi cha uharibifu wa
mwanadamu.
Nyakati za kitabu cha waamuzi zinaitwa
nyakati za giza katika israel kwa sababu Israel wakikuwa hawana wafaklme wala
viongozi wenye nguvu ya kuwaongoza kama ilivyokuwa Musa na Yoshua hivyo watu
walijifanyia mambo yoyote waliyoyaona kuwa mema machoni pao katika mlango wa 19
wa kitabu hiki mwandishi anaonyesha kuwa Pamoja na Mungu kuwainulia waamuzi
wana wa israel lakini uovu katika israel ulikuwa umefikiwa kiwango cha juu sana
cha uharibifu na stori hii inaonyesha wakati wote wanadamu wanapofikia kiwango
cha juu cha uharibifu utaweza kuina dhambi za kiwango cha juu na uharibifu
mkubwa wa uvunjifu wa maadili ukijitokeza ona mfano huo katika mstari wa 16-30
Waamuzi
19:16-30 “Kisha, tazama, akatokea mtu mume mzee, atoka kazini kwake shambani,
wakati wa jioni; mtu huyo alikuwa ni wa ile nchi ya vilima vilima ya Efraimu,
naye alikuwa anakaa katika Gibea hali ya ugeni lakini wenyeji wa mahali hapo
walikuwa Wabenyamini. Naye alipovua macho yake, akamwona huyo mtu msafiri
katika njia kuu ya mji; huyo mzee akamwuliza, Waenda wapi wewe? Nawe watoka
wapi? Akamwambia, Sisi twapita hapa kutoka Bethlehemu-yuda, twaenda huko upande
wa mbali wa nchi ya vilima vilima ya Efraimu; ndiko nilikotoka nami nilikwenda
Bethlehemu-yuda; nami sasa naiendea nyumba ya Bwana wala hapana mtu anikaribishaye
nyumbani mwake. Walakini nyasi tunazo, na chakula cha hawa punda zetu; mkate
pia tunao na divai kwa mimi na huyu kijakazi wako, na kwa huyu kijana aliye
pamoja nasi watumishi wako; hapana uhitaji wa kitu cho chote. Kisha huyo mzee
alisema, Na iwe amani kwako; lakini na haya yaliyokupungukia na yawe juu yangu
mimi lakini usilale njiani. Basi akamtia
ndani ya nyumba yake, akawapa punda chakula; nao wakaosha miguu, wakala na
kunywa. Hapo walipokuwa wakifurahisha mioyo yao, tazama, watu wa mji huo, watu
mabaradhuli wakaizingira hiyo nyumba pande zote, wakagonga mlango; wakasema na
huyo mwenye nyumba, huyo mzee, na kumwambia, Mlete nje mtu yule aliyefika nyumbani
kwako, ili tupate kumjua. Naye mtu mwenye nyumba akawatokea hapo nje, na
kuwaambia, La, sivyo, ndugu zangu nawasihi msifanye uovu jinsi hii; kwa kuwa
mtu huyu ameingia ndani ya nyumba yangu, msifanye upumbavu huu. Tazama, binti
yangu yupo hapa, ni mwanamwali, na suria wake huyo mtu; nitawaleta hapa nje
sasa nanyi watwezeni, na kuwatenda hayo myaonayo kuwa ni mema; lakini mtu huyu
msimtende jambo la upumbavu namna hii. Lakini hao watu hawakukubali kumsikia;
basi mtu huyo akamshika suria wake, na kumleta nje kwao; nao wakamjua, na
kumtenda uovu usiku kucha hata asubuhi kisha kulipoanza kupambauka wakamwacha
aende zake. Ndipo huyo mwanamke akaja alfajiri, akaanguka chini mlangoni pa
nyumba ya mtu yule alimokuwamo bwana wake, hata kulipokucha. Bwana wake
akaondoka asubuhi, akaifungua milango ya nyumba, akatoka nje ili aende zake, na
tazama, huyo mwanamke suria yake alikuwa ameanguka pale mlangoni pa nyumba, na
mikono yake ilikuwa i pale kizingitini. Akamwambia, Haya ondoka, twende zetu;
lakini hakuna aliyemjibu; ndipo akamwinua akamweka juu ya punda; mtu huyo
akaondoka, akaenda mahali pake mwenyewe. Naye alipokwisha kuingia nyumbani
mwake, akatwaa kisu, kisha akamshika huyo suria yake, akampasua kiungo kwa
kiungo, vipande kumi na viwili akampeleka katika mipaka yote ya Israeli. Basi
ikawa, wote walioliona jambo hilo wakasema, Jambo kama hili halijatendeka wala
kuonekana tangu siku hiyo wana wa Israeli walipokwea kutoka katika nchi ya
Misri hata leo; haya, lifikirini, fanyeni shauri, mkanene.”
2. Ushoga uko
kinyume na tendo la ndoa
Tendo la ndoa lilianzishwa na Mungu kwa
makusudi ya ustawi wa jamii duniani ili wanadamu wazaliane na kuongezeka Mathayo 19:4-6 “Akajibu, akawaambia,
Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili
mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.” Yeye aliyewaumba mwanzo aliwaumba mtu mume
na mtu mke unaona hii ni wazi kuwa tendo la ndoa lilikusudiwa na Mungu kuwa
tendo la kipekee litakalohushisha wanandoa na sio vinginevyo Biblia inakataza
hata zinaa na uasherati, matendo haya yakifanyika hivyo na bila ya utaratibu
yanaweza kusababisha watu walee watoto wasio wao kwa asili, ndio maana Mungu
aliweka utaratibu tamaa inayokusudiwa kibiblia ni tamaa ya mtu kuwa na mkewe na
mumewe na wameamuriwa kupeana bila amri ona
1Wakoritho 7:2-5 “Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe
na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo
mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe;
vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane isipokuwa
mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije
akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu”. Kimsingi unaweza kuona mkazo wa kibiblia kuhusu
ndoa na umuhimu wake na jinsia imewekwa wazi kuwa tendo linalopaswa kufanyika
kwa mume na mke au mke na mume na sio vinginevyo, Jambo hili hata kwa asili
utaweza kuona viumbe vyote vinakubaliana na agizo hili la kimungu
3. Ushoga uko
kinyume na baraka za Ndoa.
Mwanzo
1:27-28 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba,
mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni,
mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na
ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.” Mungu alipomuumba mtu mke na mtu mume
aliwabariki akitaka wakazaliane na kuongezeka watu wanaoshiriki mapenzi ya
jinsia moja yaani wanawake kwa wanawake na wanaume kwa wanaume hawawezi
kutimiza kusudi hili la kimungu na hivyo wanafanya machukizo makubwa hawawezi
kuiongeza dunia na kwa matendo yao wanafanya machukizo na swala ambalo liko
kinyume na mapenzi ya Mungu tendo la ushoga kwa uwazi linaashiria mwisho wa
dunia kwa sababu wiote wanaotenda haya watakufa bila kuacha uzao duniani.
4. Mashoga
hawawezi kuwa na ndoa halali.
Mungu aliikusudia Ndoa kuwa jambo lenye
kuheshimika sana Waebrania 13:4 “Ndoa na
iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi
Mungu atawahukumia adhabu.” Ndoa inayoweza kuheshimiwa kwa mujibu wa maandiko ni ndoa ya
mke na mume ni ndoa ya watu wa jinsia zisizofanana, wakati biblia ikiagiza
kuheshimika kwa ndoa ya aina hii ni muhimu kukumbuka kuwa Biblia haijawahi
kutaka mwaname kulala na mwanaume mwenzake kama kulala na mwanamke swala hili
ni machukizo na haliwezi kuwa la kuheshimika Mambo ya walawi 18:22-24 “Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala
usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame
mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko. Msijitie unajisi katika mambo
hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa
najisi kwa mambo hayo yote;”
5. Ndoa ya mashoga haiwezi kumwakilisha
Kristo.
Ndoa zimekusudiwa
kuwa kielelezo cha uhusiano ulioko kati ya Kristo na Kanisa ona katika
Waefeso 5:23-25 “Kwa maana mume ni
kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa
mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume
zao katika kila jambo. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye
alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;” Katika kielelezo hiki ndoa na uhusiano wake inafananishwa na uhusiano
ulioko kati ya Yesu na kanisa , ni wazi kuwa tabia za ushiga na ndoa ya jinsia
moja ni uasi na kufuru kubwa kinyume na kielelezo hiki, ushoga unamkana Mungu,
ushoga naharibu na kuvunjilia mbali kweli ya Mungu na haiwezi kupakwa mafuta
kwa jinsi yoyote ile.
6.
Ushoga
unaashiriki kiwango cha juu kabisa cha matatizo ya akili.
Utafiti wa
kisayansi umebaini kuwa katika viwango vya juu kabisa vya matatizo ya
kisaikolojia yaani matatizo ya akili ambayo ni pamoja na msongo wa mawazo,
matumizi ya madawa ya kulevya, kujiua na usagaji na ushoga ni mojawapo ya alama za kiwango cha juu zaidi
cha matatizo ya akili aidha kukubaliana na maswala ya ushoga duniani kuwa ni
jambo la kawaida pia ni ishara ya kuhari9bika kwa akili za mwanadamu ushoga ni
haribiko la juu zaidi ambalo ni gumu kulirekebisha na hivyo dawa yake ni
kuharibu kabisa au kuwaacha watu hao waangamie katika hasira za Mungu Biblia
inakubaliana na na tafiti hizi za kisayansi
Warumi 1:22-32 “ Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; wakaubadili utukufu wa
Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na
ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha
katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili
yao.Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na
kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. Hivyo Mungu aliwaacha
wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa
matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke,
ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini
mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Na kama walivyokataa kuwa na Mungu
katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye
yasiyowapasa. Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya;
wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye
kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye
kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio
na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; ambao
wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili
mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.” Unaona Biblia
haielezi tu wale wanaoshiriki uchafu bali hata wanaokubaliana na uchafu huo nao
ni wenye matatizo makubwqa sana Mungu anachukizwa na jambo hili kwa kuwa
linaharibu kabisa akili ya mwanadamu na kumfanya asiwe na akili, unakuta
mwanaume kwa sababu ya kuathiriwa na tabia za kishoga anavaa Heleni, analegeza
suruali, anavaa chupi za kike anajichubua, anapaka wanja, anapaka lipstiki,
anakunywa soda za kike kama mirinda au fanta, anajisikia kama ana mimba, kama
anaweza kuzaa akama anataka kunyonyesha, ana joto anahisikia kuingiliwa marafiki
zake ni wanawake, analegeza vidole, kila wanachokifanya wanakifanya kama
wanawake hili ni haribiko la akili na saikolojia mlinalotokana na mtu
kuharibika na kuvurugwa!
7.
Ushoga ni
kubadili matumizi ya asili
Kwa asili Mungu aliuumba unyeo “Anus” kwaajili ya kutolea kinyesi na
sio kwaajili ya kuingiliwa, njia ya haja kubwa rectum ni tofauti kubwa
kimaumbile na uke vigina na hazifanani vigina umeandaliwa tayari kwa kuingiliwa
na uume lakini sio ilivyo kwa upande wa pili, uke una maji maji maalumu yanayoangaa
kuingiliwa na uume lakini sivyo ilivyo kwa utumbo mkubwa , uke una misuli
maalumu ya asili unayoweza kustahimili lakini sivyo milivyo kwa unyeo, uke
unauwezo wa kustahimili msuguano wowote lakini sivyo ilivyo kwa unyeo, Unyeo
umeumbwa na misuli midogomidogo na maalumu kwaajili ya utoaji wa kinyesi nje na
sio kupokea kitu kutoka nje na kama kutafanyiwa tendo hilo baada ya muda Fulani
misuli yake italegea na kushindwa kustahimili kuuzia kinyesi, aidha uwezekano
mkubwa wa kusababisha michubuko utakuwepo na kuruhusu magonjwa mabaya ya
kuambukiza ikiwemo UTI kwa sababu hili sio tukio la asili na biblia inalitamka
hivyo Warumi 1:26-27 “Hivyo Mungu
aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili
kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya
mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata
nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.”
8. Ushoga
unaharibu nafsi.
Nasfi ya mwanadamu ina nafasi kubwa sana
katika maisha yetu ya kiroho, vita vyote vya kiroho hufanyika katika nafsi
nasfi ikishindwa anguko la kiroho hutokea na nafsi ikishinda ushindi mkubwa wa
kiroho hutokea na ndio maana maandiko
yanatutaka tulinde moyo wetu yaani nasfi zetu kwani huko ndiko ziliko chemichemi
za uzima Mithali 4:23. “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana
ndiko zitokako chemchemi za uzima.” Ni muhimu kufahamu
kuwa neno Moyo au mwili katika Biblia ya Kiibrania hutajwa kwa kutumia neno “NEPHESH” neno hili maana yake ni “NAFSI, AU AKILI AU NIA” Maandiko yanajua
umuhimu wa nia au nafsi au akili akilia au nafsi au nia ikishikwa na kitu
kingine au ikitekwa inakubali kuwa mateka kule ilikotekwa Neno la Mungu
linatuagiza tuijaze akili yetu neno la Kristo ona Wakolosai
3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote,
mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku
mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.” Kwa nini maandiko yanatutaka neno la Kristo likae kwa wingi
ndni yetu maana yake tuijaze mioyo yetu au nafsi zetu na akili zetu kwa neno la
Mungu, Ni neno la Mungu na utii kwa neno la Mungu linaloweza kutugeuza nia zetu
na kutufanya kwa upya Warumi 12:2 “Wala msiifuatishe
namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika
mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” Unaweza kuona jinsi neno na Mungu
linavyotoa kipaumbele katika kujaa neno lake na kuzielekeza nasfi zetu
kumtukuza na kumuhimidi Bwana Mungu wetu! Daudi alijiambia nafsi yake na
kuiimbisha zaburi ili imhimidi bwana ona Zaburi
103:1-5 “Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau
fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako
yote,Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema, Aushibisha
mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai;” kwa hiyo nasfi ni moja ya sehemu muhimu sana, akili na nia ni
moja ya sehemu muhimu sana kwa mustakabali wa maisha yetu, sasa basi Mapenzi
nayo yana tabia ya kushika nafsi na kuiharibu, zinaa ina tabia ya kushiika
nasfi na kuiharibu uasherati nao una tabia ya kushika nasfina kuiharibu lakini
kwa bahati mbaya dhambi ya ushoga, ulawiti na ufiraji zina uwezo wa kiwango ca
juu cha uharibifu na kuweza kuishika nafsi na kuiharibu na ndio maana Mungu katika hekima yake anajua kuwa watu wakifikia
kiwango hicho cha tabia chafu ni vigumu sana kuacha mwenendo wa aina hiyo kwani
unakamata sana nafsi na kuiteka kabisa kwa hiyo watu wa aina hiyo wanastahili
hukumu Warumi 1:26-27 “Hivyo Mungu
aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili
kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya
mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, WAKAPATA
NAFSINI MWAO malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.”
9. Ushoga
unaharibu mwili.
Watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja
wanajitahidi sana duniani kulifanya tendo hili lionekane kama tendo la kawaida
na lisilo na madhara yoyote, lakini ukweli unabaki wazi kuwa swala hili lina
madhara makubwa sana katika mwili wa mwanadamu, Mungu aliuumba mwili wa
mwanadamu kwa heshima kubwa sana kwa
matumizi ya utukufu wa Mungu, Mwili umeumbwa kwaajili ya Mungu na sio kwaajili
ya zinaa
1Wakoritho
6:12-13 “Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni
halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote. Vyakula
ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili,
tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni
kwa mwili.” Watu wa
Mungu na dunia nzima inapaswa kuelewa kuwa tukiitoa miili yetu kwaajili ya
zinaa ni dhambi maana Mungu aliuumba mwili kwa utukufu wake na hivyo ni mbaya
zaidi tukiinajisi miili yatu kwa kufanya ngono ya jinsia moja , ushoga na
usagani una madahara makubwa sana katika maisha ya mwanadamu na unaharibu kwa
kiwango kikubwa mfumo wa utendaji wa mwili na maumbile Mungu atatuadhibu kwa
kuharibu miili yetu 1Wakoritho 6:18-20
18. “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili
wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au
hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu,
mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa
thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.” Ni jambo
la kusikitisha kuwa kwa dhambi ya ushoga ni vigumu kumtukuza Mungu, kama
wanadamu wataruhusu tamaa ya ushoga kuchukua nafasi na kuitawala dunia ni
lazima ieleweke wazi kuwa tutaharibu kabisa jamii ya aina buinadamu duniani
Ushoga hasa ulawiti na ufiraji ni moja ya
sababu kuwa sana ya magonjwa ya zinaa au ngono magonjwa ya zinaa au ngono ni
pamoja na :-
·
Kisonono (Gonorrhea) ni mojawapo ya magonjwa
najisi ya ngono,Mtu anapokuwana kisonono nyakati za biblia alitengwa kusudi
asiwaambikize wengine lakini ni ugonjwa ambao mtu aliweza kupona (Walawi 15;1-15)
·
Clamidia Huu dalili zake haziko wazi lakini zina
usaha mweupe unao natanata uumeni au ukeni.
·
Chankroid sijapata jina zuri la
Kiswahili lakini ugonjwa huu wa zinaa mtu huwa na vidonda sehemu za siri na
maumivu makali hususani wakati wa kujisaidia,kuvimba tezi sehemu za siri na
wakati mwingine kupasuka na kutoa usaha
na kuwa na utando mweupe mdomoni.
·
Ukimwi/HIV – Ukosefu wa kinga ya mwili
ni moja ya magonjwa ya zinaa lakini kwa njia iliyowazi mtu anaweza kuambukizwa
kirahisi zaidi kama ataingia kwenye mapenzi ya jinsia moja hususani ya wanaume
kwa wanaume, na tabia za ushoga
·
Kubadilika kwa maumbile – kutokana na tendo
la kumwagiwa shahawa kwenye utumbo mkubwa shahawa hizo hufanyiwa digestion
yaani husagwa tena kama chakula na kurejeswa mwilini japo nyingine zinaweza
kumwagika kitendo hiki hupelekea, Mabadiliko ya mwili wa mwanaume kuwa kama
mwanamke, aidha kutokana na kuwepo kwa chemikali ya Lactic acid ambayo katika
mbegu za kiume ina milgram 2.11 kati ya mils 3 za mbegu za kiume acid hii ina
nbakteria wanaotumika kuchachusha kitu kwa hiyo bakteria hao huchahusha na kujijenga
katika eneo la utumbo mkubwa na hivyo kusababisha miwasho itakayopelekea
mfirwaji kujisikia kuingiliwa tena na tena , aidha kutokana na michubuo ya uume
kuingia sehemu ya haja kubwa kunasababisha kutokea
kwa uvimbe mdogo mdogo wenye usumbufu, muwasho usiokuwa wa kawaida, kulegea kwa
njia ya haja kubwa, kuharibika kwa uwezo wa utumbo mkubwa kuzuia choo,
kuharibika kwa mfumo wa nguvu za
kiume ambazo kwa kwaida zinategemea sana uimara wa mishipa ya nyuma, kulegea
kwa maumbile na maumbile kuanza kuwa ya kike, na mabadiliko ya sauti ambayo
huanza kuwa nyembamba na mabadiliko ya homoni na maumbile ya kisaikolojia na
kumfanya mtu aliyeingiliwa kuanza kuwa kama mwanamke, kujificha kisaikolojia na
kuanza kutunisha misuli ili kujazia ili mtu aonekane kuwa ni mwanaume kweli,
kushituka kihisia kunakotokana na kujikausha ili watu wasijue kuwa unaingiliwa
hivyo ubongo huwa unakandamiza hisia kwa kusudi la kujikausha ili usijulikane
kuwa unafanya jambo hilo na hivyo ikitokea ukijambishwa unaathirika kiakili! Na
kushituka sana kwa kufikiri kuwa aliyekujambisha amejua kuwa wewe ni shoga. Kwa
ujumla ya kishoga ni mabaya Matukio haya yote husababishwa na hali hii ya
kumkataa Mungu na kukataa kutawaliwa na Mungu na hivyo kuutia mwili uchafu
yaani unajisi Mungu atahukumu mageuzi ya aina hii yanayofanywa na wanadamu
dhidi ya uumbaji wake Yuda 1:5-8 “Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya
yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri,
aliwaangamiza baadaye wale wasioamini. Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe,
lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele
chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu. Kama vile Sodoma na Gomora na miji
iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda
kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa
katika moto wa milele. Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili
uchafu, hukataa kutawaliwa, na kuyatukana matukufu.”
·
Kwa kawaida kitaalamu Mbegu za
kiume shahawa kwa mujibu wa lugha ya kitaalamu zinaitwa Spermatozoa kwa kifupi
Sparm zinabeba viluwiluwi vinavyotarajiwa kuwa binadamu kati ya milioni 200-
milioni 500 kwatika ujazo mmoja wa shahawa zenye ujazo wa milgram 5 na ndani
yake kuna Lactic acid, vulume ya
mils 2;11, magnesium 0.374. Potassium 3.71 na Protein 0.171
10. Mashoga
hawana sifa ya kumtumikia Mungu.
Nyakati za Biblia kulikuwa na sifa maalumu
za watu waliotakiwa kumtumikia Mungu, katika sifa hizo za kimwili na kiroho
Mungu hakuwahi kuruhusu Mashoga wawe watumishi wake na sio tu kumtumikia yeye
bali hata kusogelea mkutano wa watu wa Mungu
ona Kumbukumbu
23:1 “Aliyejeruhika konde, au aliyekatika tupu yake, asiingie mtu huyo
katika mkutano wa Bwana.” Mtu ambaye amehasiwa asiye na uume au ambaye uume umelegea
au hasimamishai hakupaswa kuingia katiia mikutano wa watu wa Mungu na sio hivyo
tu hakupaswa kumtumikia Mungu ona Mambo
ya Walawi 21:17-21 “Nena na Haruni, umwambie, Mtu awaye yote wa kizazi
chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kusongeza chakula
cha Mungu wake. Kwa kuwa mtu awaye yote aliye na kilema hatakaribia; mtu
kipofu, au kiwete, au mtu aliye na pua iliyoharibika, au aliye na kitu
kilichozidi vimpasavyo mwili, au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono,
au aliye na kijongo, au aliye kibeti, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye
na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu; mtu awaye yote wa kizazi cha
Haruni kuhani aliye na kilema asikaribie kuzisongeza sadaka za BWANA kwa njia
ya moto; ana kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.” Mungu hakukubali walemavu wamtumikie Mungu, lakini zaidi pia
alikazia kuwa hata mtu aliyevunjika mapumbu yaani mwauame khanithi ambaye
anaingiliwa kama mwanamke huyu hapaswi kabisa kumtumikia Mungu,
Katika agano jipya utaweza kuona sifa za mtu anayetakiwa kumtumikia Mungu
zinatajwa kwamba ni lazima awe mwanaume au mume wa mke mmoja 1Timotheo 3:2 “Basi imempasa
askofu awe mtu asiyelaumika, MUME WA MKE MMOJA, mwenye kiasi na busara, mtu wa
utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;” Unaona mkazo huo Mume wa mke mmoja unamaana ni lazima awe
mwanaume rijali, mwanaume mwenye kujihusisha na ushoga hawezi kuwa mwenye kufaa
katika kumtumikia Mungu.
Sababu zinazopelekea kuweko kwa mapenzi ya
jinsia moja duniani
Ushoga ni hali ya kuvutiwa kimapenzi kwa mtu watu wa jinsia
inayofanana, ni mtindo wa maisha ya kimapenzi wa kati ya watu wa jinsia moja
yaani mwanaume kwa mwanaume au mwanamke kwa mwanamke, hii ni hali inayowatokea
watu kihisia, na kimvuto na kitamaa kwa watu wa jinsia moja inaweza pia kuelezewa
kama mtazamo wa mtu wa kimapenzi au tabia ya mtu au watu fulani katika jamii
ambao wanavutiwa kushirikiana kimapenzi na watu wa jinsia kama yao, Biblia
imepiga marufuku aina hii ya tamaa au mvuto au hisia au hata kujihusisha na
mapenzi ya jinsi hii, lakini hakuna anayeeleza kuwa ni sababu gani zinapelekea
jambo hili kujitokeza au kuwepo, hata wanasayansi wanapata taabu sana na bado
hawajagundua sababu za moja kwa moja zenye uhakika zinazopelekea kuwepo kwa
aina hii ya mapenzi miongoni mwa jamii ya aina buinadamu.
Wataalamu wa utafiti wa swala la kwanini watu wanajihusisha
na mapenzi ya jinsi moja wanasema kuna dhana kubwa mbili zinazotolewa na
watafiti wa swala hili
1.
Kuna wanaosema
kuwa swala hili watu huzaliwa nalo
2.
Kuna wanaodai
kuwa swala hili ni tatizo la kisaikolojia na kimazingira
Kuhusu swala la kuzaliwa na hali hii wataalamu wa uchunguzi wa mfumo wa ubongo
wakishirikiana na Simon Leyay, mtaalamu wa mapacha J Michael Bailey na Richard
c Pillard na mtaalamu wa geneology dean H Hamer wamesema katika utafiti waoa
kuwa hakuna mtu anazaliwa shoga, hivyo dhana pekee inayobaki kuwa inaweza kuwa
sababu ya ushoga ni swala la kisaikolojia na kimazingira, kwa msingi huo neno
la Mungu lisingeweza kuwa kali kwa jambo ambalo liko nje ya uwezo wa kibinadamu
au ka ma wanadamu wangekuwa wanazaliwa na ushoga kwa msingi huo uko uwezekano
wa mtu kuchagua kuwa awe ni mtu wa namna gani. Sababu za kimazingira zinazoweza
kupelekea mtu kuwa shoga ni kama ifuatavyo:-
Hapa ziko sababu ambazo zinaweza kukubalika kisaikolojia
kusaidia kujua kwa nini watu hujihusisha na mapenzi ya jinsi moja:-
a.
Sababu za
Msongo wa mawazo depression mawazo yanayosababisha mtu kuwa jna huzuni na
kuanza kuona hana uthamani kwa jamii yake rafiki zake na watu wa jinsia yake,
b.
Urithi wa
vichocheo vingi homons kutoka kwa mama na malezi ya kudekezwa, hii huchangiwa
kuanzia mimba hasa mzazi anapotarajia mtoto wa kike zaidi
c.
Kunyanyaswa
“bulled” kwa Maneno au vitendo tangu
utoto wako
d.
Msukumo wa
kukataa au kutaka kubadilisha jinsia yako
e.
Kujilinganisha
na wengine kimaumbile
f.
Kuogopa kukataliwa
na kutengwa au kuwa npeke yako
g.
Kukusa msaaada
wa kujielewa
h.
Kulelewa katika
sheria kali sana zinazokukataza kuchangaana na sex tofauti
i.
Vifungo vya
muda mrefu
j.
Kuangalia
picha na mikanda ya ngono
k.
Kuwa na
makundi mabaya na marafiki wabaya
l.
Kukosa
mafundisho sahihi ya neno la Mungu tyangu utoto
m.
Mashambulizi
ya ibilisi kwa watu wenye akili na vipawa ili akuharibu mapema
Jinsi ya
kuishinda dhambi ya ushoga!
1. Amini kuwa
Mungu anasamehe
Kwa kawaida kwa vile dhambi ya ushoga ni ya ngazi ya juu sana
na maandiko pamoja na jamii wanaipinga sana wengi wanadhani kuwa dhambi hii ni
sawa na kumkufuru Roho Mtakatifu na hivyo haisameheki, Biblia inaonyesha nwazi
kuwa Mungu anauwezo wa kusamehe dhambi hii na kuwabadilisha wale wanaomjia kwa
imani ona 1Wakoritho 6:9-11 Biblia
inasema hivi “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi
ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala
waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,wala wevi, wala
watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi yenu
mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa
haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu”.
Kama watu walioshiriki mapenzi ya jinsia moja yaani usagaji na ushoga
wakimuamini Yesu na kutubu na kuacha njia zao mbaya kwa imani wanweza kabisa
kubadilishwa mstari wa 11 katika kifungu hicho ni wa muhimu wakati huu kwa
sababu unaeleza hivi “Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini
mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu
Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu”. Kwamba kule Koritho Mungu aliokoa watu wa aina zote
wakiwemo watu waliofanya ulawiti na ufiraji, kwa msingi huo hatuwezi kuizuia
neema ya Mungu inayookoa watu wote, lakini hata hivyo tunaweza kuona ugumu
mkubwa sana na madhara makubwa sana yanayotokana na mtu kujiingiza katika
dhambi hii labda tukinena kiwazimu afadhali dhambi nyingine, Lakini hata hivyo
hatuwezi kumuwekea Mungu mipaka kwani mwaliko wa Mungu kwa msamaha unaonyesha
kuwa anasamehe dhambi ya kiwango chpchote kile ona Isaya 1:18 “Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu
zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu
kama bendera, zitakuwa kama sufu.” Andiko hili lamaanisha kuwa Mungu yuko tayari kusamehe dhambi
bila kujalia dhambi hiyo ilikuwa mbaya kiasi gani mara mtu anapotubu na kukiri
mbele za Mungu, Mungu husamehe hii ndio tabia yake yeye ni mwaminifu katika
kusamehe 1Yohana 1;9 “Tukiziungama
dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na
kutusafisha na udhalimu wote.” Unaweza kuona ni wazi kuwa neno la Mungu linafungua mlango
kwa kila mtu kama tukiziungama dhambi zetu bwana ni mwenye rehema
anasamehe na kuosha kabisa na kukufanya
upya hasa kama utaendelea kuitegemea neema yake na kukaa kwa imani kila kitu kitakuwa
kipya 2Wakoritho 5:17-21 “Hata imekuwa, mtu
akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa
mapya.” Ndani ya
Kristo ya kale yanapita na kila kitu kinakuwa kipya Mungu anauwezo wa kusamehe
na uwezo wa kubadilisha na anauwezo wa kuweka dhambi zako mbali nawe kabisa Zaburi 103:10-13 “Hakututenda
sawasawa na hatia zetu, Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu. Maana mbingu
zilivyoinuka juu ya nchi, Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. Kama vile baba awahurumiavyo watoto
wake, Ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao.”
2. Kubali
kugeuzwa nia yako!
Warumi
12:1-2 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili
yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu
yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa
upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza,
na ukamilifu.” Mapambano
makubwa na vita kubwa ya mwanadamu hupiganwa katika nia yaani katika akili kwa
msingi huo ni muhimu kumuomba Mungu aihuishe nia yako na kuifanya upya roho
iliyotulia ndani yako ili kwamba usimtende Mungu dhambi Zaburi 51:9-10 “Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute
hatia zangu zote. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia
ndani yangu” Kila mtu
aliyeokolewa alikuwa na dhambi zake ambazo alipokuwa duniani zilikuwa zinamtesa
au kumtawala na kumtumikisha ni muhimu kufahamu kuwa tunapokuwa tumeokolewa
dhambi zileziole tulizokuwa tukiziednea zamani ndio zitakuwa mtego mkubwa wa
adui kuzitumia kututega tena ili turejee dhambini kwa hiyo nia zetu
zinapogeuzwa na sisi kukubali kugeuzwa nia zetu tunaifungia dhambi mlango wa
kutupata tena na ndio maana ni muhimu sana kumuomba Mungu atufanyie upya nia zetu na zaidi sana
atulinde na tujilinde na ile dhambi ituzingayo kwa haraka yaani ile dhambi
tuliifanya sana kabla ya kukutana na Yesu hiyo katika maandiko huitwa dhambi
ituzingayo kwa haraka Waebrania 12:1-3”Basi na sisi pia,
kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando
kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi
katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye
kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau
aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. Maana mtafakarini
sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu
ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu” Mtu aliyetoka katika ushoga dhambi
imzingayo kwa upesi ni ya ushoga na anapaswa kujilinda nao.
3. Jiingize
katika kuomba sana .
Maombi ni silaha yenye nguvu kubwa sana
hatuna budi kuhakikisha kuwa tunaomba na kujisomea neno la Mungu, na kumuabudu
Mungu jambo hili litatutengenezea mfumo mpya wa tabia na hofu ya Mungu ndani
yetu jambo hili litabadilisha kabisa maisha yetu, Katika kumuomba Mungu lazima
tumuombe Mungu atuchunguze mioyo yetu ili kuondoa njia zenye kuleta majuto Zaburi 139:23-24 “Ee Mungu,
unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu; Uone kama iko
njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele.” Mungu anauwezo wa kubadili mitazamo ya
mioyo yetu na kuondoa kabisa mambo yanayotuudhi na hatimaye atatupa amani na
nguvu ya kutusaidia kushinda kila aina ya tamaa mbaya Wafilipi 4:6-7 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila
neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na
Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia
zenu katika Kristo Yesu.” Tegemea nuwezo wa Mungu na nguvu zake, usijitumainie
mwenyewe wewe huwezi kujibadili tabia kwa nguvu zako jiachilie
katika neema ya Mungu madamu tu moyoni unachukizwa na jambo hilo kutoka moyoni
2Wakoritho 4:7 . “Lakini tuna
hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala
si kutoka kwetu.”
4. Hakikisha unaujaza moyo wako kwa mawazo yenye kujenga .
Achana na marafiki
wabaya wahubiri wa ushoga wana maneno mazuri sana yenye kuvutia kuelezea jambo
hili kana kwamba ni jambo jema sana watakuingizia kwenye akili yako kuwa nhili
swala ni jema wakati ni swala baya katika njia za Mungu1Wakoritho 15:33 “Msidanganyike; Mazungumzo
mabaya huharibu tabia njema” Biblia ya kiingereza inaita “bad
company” hakikisha kuwa unaepuka kila aina ya mazungumzo au unavunja urafiki na
watu wabaya wanaozungumzia maswala ya ushoga, badala yake ijaze akili yako kwa
neno la Mungu Zaburi 119:9-11 “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata
neno lako. Kwa moyo wangu wote
nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka
neno lako, Nisije nikakutenda dhambi” hakikisha kuwa unajisomea neno
la Mungu na kulitii yaani kufuata masharti yake, na wakati wote kutafakari na
kujadili au kutafakari mambo yaliyo mema Wafilipi
4:8 “Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya
kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo
yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo
sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.” Ni neno la Mungu pekee lenye
nguvu ya kubadilisha maisha yetu kwa sababu lenyewe lina uwezo wa kutambua
mawazo ya mioyo yetu na kututengeneza
Waebrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina
nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata
kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li
jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.” 1Wakoritho 6:9-11 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu?
Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu,
wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala
walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa
namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika
jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.” Waefeso 5:3 “Lakini
uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama
iwastahilivyo watakatifu;”
5.
Jilinde moyo wako na
picha chafu.(pornography)
Hakikisha kuwa
unajilinda na kitu chochote kinachohusika na kuinua hisia za mwili wako, iwe ni
picha magazeti na stori za mapenzi au vipindi katika televisheni, vitabu na
majarida na vijiwe vya stori zinazochochea ngono, Wakolosai 3:5-6 “Basi, vifisheni viungo vyenu
vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na
kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya
Mungu.
6. Pigana vita kali kwaajili
ya mabadiliko yako !
Kama unapambana na tamaa ya mapenzi ya jinsia moja ni lazima ufahamu
kuwa vita uliyonayo sio nyepesi, lazaima upambane “ Nimemuomba sana Mungu
anisaidie, nimesoma maandiko, nimefunga lakini sielewi nitashindaje” alisema kijana mmoja anayepamba
na ushoga, vita dhidi ya dhambi inayotuzinga kwa harapa au upesi sio nyepesi,
ni vema kutokujiingiza kabisa na kama umejiingiza ni lazima upambane, huwezi
kupigana vitanhii kwa nguvu zako mwenyewe hakuna tiba rahisi, kila mtu
anayetaka kumpendeza Mungu lazima apambanae na nlolote lile linalokushusha
kutoka kwenye kiwango ambacho Mungu amekikusudia, Mungu anajua mapambano
tuliyonayo 1Yohana 3:19-20 “Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, nasi
tutaituliza mioyo yetu mbele zake, ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana
Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote.” Unapomtii Mungu
unafungua mlango wa kupokea baraka na kuna thawabu kubwa za kumtii yeye Zaburi 19:8-11 “Maagizo
ya Bwana ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya Bwana ni safi, Huyatia macho
nuru. Kicho cha Bwana ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za Bwana ni kweli,
Zina haki kabisa. Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu
safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali. Tena mtumishi wako
huonywa kwazo, Katika kuzishika kuna thawabu nyingi.” Ni muhimu
kumtegemea Mungu na kupambana na tamaa mbaya katika mioyo yetu tusichoke Wagalatia
6:9 “Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna
kwa wakati wake, tusipozimia roho.” Kadiri tutakavyoendelea
kupambana na tamaa hii mbaya hatimaye tutajikuta tuko katika uhusiano ulioimara
sana na Mungu
7.
Hakikisha unautiisha mwili kwa kufanya mazoezi.
ITimotheo 4:8 “Kwa
maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa
mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.” Maandiko yanatukumbusha nkuwa tunapaswa
kufanya mazoezi japo kwa kiasi, na kuishi maisha matakatifu, kila kitu Duniania
ambacho tunajiandaa kukifanya kinahitaji mazoezi, na wakristo pia wanapaswa
kufanya mazoezi kufanya mazoezi sio dhambi, mazoezi yana umuhimu mkubwa katika
mkaisha yetu ya kimwili na kiroho, lakini pia katika kuzitiisha tamaa za mwili.
Kwa nini Biblia inatutaka tufanya mazoezi kwa kiasi? Kwa sababu mazoezi yana tambia ya kuwa ikama
ibada ya sanamu, ukitapenda sana yanakuwa kama ibada kwa hiyo tunapaswa kuwa na
kiasi, pia Wakrito hawapaswi kufanya mazoezi kwa kusudi la kubadili maumbile
yao yaani Bodybuilding na pia kwa kusudi la kuongeza uzito weightlifting,
wakristo wanapaswa kufanya mazoezi kwa kusudi la kujiweka imara na kuiondoa
katika miganamizo ya mawazo na kuruhusu akili zetu kufanya kazi zizuri, kujenga
kuiamini na kujiweka sawa, kwa hiyo tufanye mazoezi lakini tusiyageuze mazoezi
kuwa kama ibada, Tunaweza kumuheshimu Mungu kwa kuituza miili yetu 1Wakoritho 6:19-20 “Au hamjui ya kuwa
mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu?
Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana
mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”
Angalia pia 1Wakoritho 10:31 “Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni
yote kwa utukufu wa Mungu.” Warumi 12:1 “Basi,
ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu
iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.”
Na Mchungaji Innocent
Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye
Hekima!
0718990796.