Jumatano, 20 Mei 2020

Vita kali dhidi ya ndoa katika Mpango wa Mungu!


Malaki 2:14-16 “Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako. Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.”



Utangulizi:
Mojawapo ya changamoto kubwa zinazoukumba ulimwengu wa leo ni pamoja na changamoto kali katika ndoa, kila kunapokucha na katika kila mazungumzo, mafundisho na mijadala swala la ndoa na changamoto zake haliwezi kukosekana swala hili linasumbua wengi katika jamii masikini kwa matajiri, wenye cheo kwa wasio na cheo, wenye elimu na wasio na elimu wakristo na wasio wakristo na kadhalika; Kuna tatizo kubwa sana katika swala la ndoa, hata kwa wataalamu wa saikolojia, walimu na hata watumishi wa Mungu wenye kuzijua ndoa kwa kina na mapana na marefu bado linapokuja swala la ndoa watu wote huingia katika malalamiko ya changamoto hii! Walimu wengi wa Ndoa na mahusiano wamejaribu kutoa ufahamu wa aina mbalimbali katika ndoa ili ndoa ziweze kuwa na amani na zinaweza kufanya kazi kwa kiwango flani lakini huwa wanasahau kuzungumzia swala moja la muhimu kuhusu VITA VYA KIROHO DHIDI YA NDOA! Wengi watafundisha kuhusu ndoa, majukumu ya mwanamke na mwanaume, wajibu wa mke na mume, maswala ya mahaba na staili na mitindo, vyakula muhimu vya wana ndoa sijui nini sijui nini lakini wanasahau kuzungumzia kwamba kuna vita vya kiroho dhidi ya ndoa hili ni muhimu kujulikana kwa kila mwana ndoa vinginevyo hakuna kitakachoweza kufabnya kazi, masomo yote ni ya muhimu lakini kama changamoto bado ziko hapa linabaki swala la mapambano ya kiroho kwa ajili ya ndoa yako! Ndoa ina vita zake hii ni muhimu kufahamu.

2Wakoritho 2:11.”Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.” Ni muhimu kufahamu kuwa ziko mbinu za utendaji wa ibilisi zinazopambana na ndoa sahihi ili isiweze kufanya kazi, na shetani anaweza kukupa amani ambayo unaweza kudhani kuwa ni amani ya kweli kwa kukubali kuweko kwenye ndoa bandia baada ya kushindwa vita katika ndoa Halisi, watu wengi sana wanadhani kuwa wana amani sasa kwa kuweko kwenye ndoa ambazo sio mpango wa Mungu na huko wanaweza kusema kuwa ndoa ile sio mpango wa Mungu, labda mwanzoni nilikosea au pale nimeingia cha kike swali kubwa la kujiuliza kwanini ile ndoa yako ya awali ilikuwa na vita kiasi kile ? na sasa je unadhani una amani ya kweli kwa kuwa sasa uko katika ndao ya pili? Je hujawahi kujiuliza kuwa amani hiyo sio ya Kristo? Imetokana na kuwa shetani hawezi kukupiga vita tena kwa sababu umeshashindwa vita na umekuwa mateka wake ukijifariji katika ndoa isiyokuwa ya halali hata kama imefungwa na mchungaji flani! Angalia!

Shetani anaitwa mungu wa dunia hii  na moja ya kazi yake ni kupofusha fikra uwezo wa kufikiri au kumgundua na kupata upenyo, anapofusha fikra za watu wa ulimwengu huu wasiijue kweli ambayo itawaweka huru 2Wakoritho 4:4 “ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.” Yeye ni muongo ni mwenye hila na kwa kutumia hila zake anauwezo mkubwa sana wa kuudanganya ulimwengu ona pia Ufunuo 12:9 “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Unaona maandiko yanamuita shetani joka Mkubwa, joka la zamani anaujuzi wa kupanga mambo, ana ujuzi wa kushambulia ana ujuzi wa kutenda kwa hila ili audanganye ulimwengu ana vita dhidi ya kanisa ana vita dhidi ya taasisi inayoitwa ndoa, kabla ya kupigana na kanisa zamani sana alianza kupigana na ndoa, ndo ndio taasisi yake ya kwanza kupambana nayo, fikiria leo alivyofanikiwa kusambaratisha maneno ya Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai leo ynaonekana kama maneno yasiyotekelezeka na yaliyojaa uongo je ni ili shetani aonekane kuwa mkweli? Tujikumbushe maandiko kuhusu kile alisema Yesu hapa Mathayo 19:3-10 “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.  Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.” Kutokana na uongo wa ibilisi kifungu hiki kimewashinda wengi kukitii na kukifanyia kazi katika ulimwengu wa leo, kumbuka hata Dunia na mataifa makubwa na makanisa makubwa yanapofikia ngazi ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja leo hii ni muhimu kwetu kukumbuka kuwa hii ni mojawapo ya dalili ya kiwango cha juu cha shetani kupambana na kitu kinaitwa ndoa, wengi wamekivunjilia mbali kifungu hicho cha maandiko wakijihalalishia ndoa zisizo sahihi chini ya amani ya muda mfupi ya shetani, Sheatani anachukizwa na ndoa shetani anachukizwa zaidi na ndoa ya Kikristo, shetani anapiga vita ndoa sahihi, kwa sababu anajua kuwa kwa kufanya hivyo anaizuia injili isiwafikie walengwa na watu hao wakakokolewa kwa sababu kwenye ndoa kuna siri kubwa sana inayofananana na siri ya kuwepo kwa kanisa Waefeso  5:32-33 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.Ni kwaajili ya jambo hili ni muhimu kwetu kuangalia kwa undani kuhusu vita vya kiroho katika ndoa ili kujiepusha na kuangalia upande mmoja wa shilingi ikiwemo swala la mahusiano, mawasiliano, taili, uongozi, wajibu na majukumu,  malezi  na kadhalika na tusisahau kuwa pamoja na umuhimu wa haya yote ndoa inapigwa vita kali sana !

Ndoa katika mpango wa Mungu!

Mungu alimuumba mwanadamu katika sura na mfano wake Mwanzo 1;27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” Mwanamke na mwanaume wanapofunga ndoa wanafunua mpango maalumu wa Mungu neno kuumbwa kwa Mfano wa Mungu kwa kiyunani linatumika neno “imago dei”  ambalo kwa kiingereza ni intellectual ability, Moroal decision and the ability to make wilful choice, purity and ruling, uwezo wa kiakili, maamuzi ya kimaadili, uwezo wa kuchagua usafi na utawala kwa hiyo mwanadamu aliumbwa awe mwakilishi wa Mungu na Mungu alimuamuru mwanamke na mwanaume kuitawala Dunia kueneza utukufu wake kumfanya yeye asifiwe huu ndio ulikuwa msingi wa mwanzo kabisa wa Ndoa Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Kuzaa na kuongezeka hapa ni kuendeleza uzao wa Mungu duniani kwa jamii ya watu wanaomtii na kumuheshimu Mungu na kutangaza utukufu wake Kwa kupitia ndao hii ya kwanza tunauona wazi kabisa Mpango wa Mungu ni kuzalisha watu watakaomtukuza yeye Duniani, watu watakaodhihirisha uhodari wa kutembea na uwepo wa Mungu na Biblia katika fundisho hili inaonyesha wazi kupitia uumbaji huu Mungu alikusudia kwamba

·         Ndoa iwe ya mke mmoja Mume mmoja
·         Ushirikiano wa tendo la Ndoa uwe ni wa jinsia ya kiume na ya kike
·         Kiongozi katika ndoa aliwajibika kuwa Mwanaume kutokana na kuumbwa kwanza
·         Ndoa ilikusudiwa iwe ya kudumu na yenye umoja usioweza kutenganishwa maneno ya Adamu huyu ni Mfupa katika mfupa wangu na nyama katika nyama yangu yanatumika kuonyesha umoja usioweza kutenganishwa yaani Adamu na Eva walikuwa kitu kimoja na umoja wao ulikuwa wa kudumu na msikamano wao ulikuwa ukitenganishwa ni kifo ndio kingetokea kwao wote Neno Mfupa wangu na nyama yangu katika agano la kale lilitumika kumaanisha Undugu ambao kwa namna yoyote ile hauwezi kukanushika ona Mwanzo 29:14 “Labani akamwambia, Ndiwe kweli mfupa wangu na nyama yangu. Naye akakaa kwake muda wa mwezi mmoja.” Ona pia Waamuzi 9:2 “Haya, neneni tafadhali masikioni mwa waume wote wa Shekemu, mkaulize, Je! Ni lipi lililo jema kwenu, kwamba hao wana wa Yerubaali wote, ambao ni watu sabini, watawale juu yenu, au kwamba mtu mmoja atawale juu yenu? Tena kumbukeni ya kwamba mimi ni mfupa na nyama yenu.” Linganisha pia 2Samuel 5:1 “Ndipo kabila zote za Israeli wakamwendea Daudi huko Hebroni, wakasema naye, wakinena, Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako.” Tungalie pia 2Samuel 19:12 “Ninyi ni ndugu zangu, ninyi ni mfupa wangu na nyama yangu; mbona basi ninyi mmekuwa wa mwisho wa kumrudisha tena mfalme. 1Nyakati 11:1 “Ndipo Israeli wote wakamkusanyikia Daudi huko Hebroni, wakisema, Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako.” Unaona neno Mfupa wangu na Nyama yangu lilitumika kumaanisha umoja usioweza kutenganishwa kamwe, muunguno usioweza kukanushwa sasa ukaribau anaokuwa nao mke na Mume na muungano wao wa kimapenzi na uwezo wao wa kushirikiana tendo la ndoa na Baraka za Mungu huwafanya wao wawe karibu zaidi kuliko ndugu wa kawaida kwa lugha nyingine unapoacha mumeo aende au mkeo aende zake yaani mnapoachana unaacha uchi wako uende zake, mwili wako uende zake, mifupa yako iende zake, na mwili wako uende zake, na kuanza kutumiwa na watu wengine, Mungu alikusudia Ndoa ibebe huduma ya kuongezeka duniani na kuitawala dunia chini ya mamlaka ya uungu kwa kumtii, kwa kulitambua kusudi hili kila ndoa iliyo sahihi iliyo katika mapenzi na mpango wa Mungu itaanza kupigwa vita kali na ibilisi kwa sababu Shetani anajua wanando wasichokijua kwa hiyo anawataka wasumbuke wapigane wagombane wafarakane waachane watendane mambo ya hiyana wasemane vibaya wanyimane unyumba wasimtii Mungu atawasumbua mpaka wakimbie na atawapa nafuu wanapokuwa katika ndoa ya pili isiyokuwa mapenzi ya Mungu

Shetani atafanya hivi kwa sababu yupo na yuko tayari kupingana na Muumba wake, atawadanganya wanadamu atawavuruga ili wamuasi Mungu wasitii neno lake akitumia hila na ujanja mwingi sana hatimaye aweze kuharibu na atakupa amani bandia kwa sababu anajua umeshaasi na kifo kinakuhusu yaani utakwenda katika ziwa la moto wa milele kwa sababu sasa unazini milele wewe ni mali yake hawezi kukuvuruga tena amefanikiwa kukupata na ndio maana utaona wale walioachana na wake zao na waume zao wa awali unaweza kukuta sasa wanaamani ya kutosha huko UZINZINI kwa mtu asiye Mfupa wake wala nyama yake kwa sababu amekuwa mtumwa wa dhambi na chombo cha ibilisi hata kama mambo yanakwenda “smoothly” yaani shwari usifikiri wewe ni mjanja kwamba umeshinda vita hapana umeshindwa vita wewe ni mali ya ibilisi hii ndio mbinu yake tangu awali ona Mwanzo 3:1 anasifiwa kwa uhodari wake ujanja na udanganyifu au werevu Mwanzo 3;1 “Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?neno mwerevu hapo katika kiingereza linatumika neno “crafty” ambalo maana yake ni Clever at achieving one’s aims by indirect or deceitful methods  Yaani mwerevu ni mwenye ujanja wa kufikia malengo yake kwa kutumia njia isiyo ya wazi moja kwa moja au kwa kutumia njia za udanganyifu kwa kutumia hila hizo sasa Shetani alifanikiwa kumdanganya Eva na kisha kummalizia Adam na kuwafanya waasi na kwa njia hii kufanikiwa kuleta mauti duniani na uharibifu mkubwa na kupitia wao wanadamu wote wamekuwa wavunjifu wa sheria ya Mungu namaanisha neno lake kama ilivyokuwa kwa Adamu Hosea 6;7 “Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu; huko wamenitenda mambo ya hiana.” Ona pia Warumi 5:12-21 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja. Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi. Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki. Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.  Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.  Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi; ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.” Unaona sasa hasara kubwa sana imaupata ulimwengu mzima kutokana na kazi ya ibilisi kwa Adamu na Eva na nikwambie kuwa hasara kubwa inaupata ulimwengu kupitia wewe na mimi kwa kuasi kwetu na kuvunja amri na maagano na Mungu wetu, ndoa sasa haiwezi kuwa kamilifu duniani na ikiwa ni ya watu wa Mungu inakuwa na vita kubwa sana na wapiganaji wakiwa hawaelewi zitavunjika sana na watapewa ndoa ambazo zina amani ya muda mfupi lakini zinawapeleka Motoni kimya kimya vita ilitangazwa kati ya shetani na uzao wa mwanamke  kwa mtazamo mpana uzao wa mwanamke ni Yesu Kristo lakini kwa mtazamo rahisi sisi wanadamu wote ni uza wa mwanamke kwa hiyo mafarakano katika ndoa ni vita ileile alioianza shtani katika bustani ya Edeni, kwa hiyo kama vile mtu akiokoka tunamfundisha kuwa imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi yaani vita nyingi ni muhimu vile vile wana ndoa wakaelewa kuwa pamoja na sarakasi zote mtakazofanikiwa au mtakazojifunza iwe uwazi katika maswala ya fedha, mahusiano, ndugu, staili, kujituma, vyakula, majukumu ya mke na mume, malezi na kuchekeana na kadhalika lazima ujue shetani na mapepo yako kazini kuhakikisha kuwa yanapambana na ndoa yako mpaka mwisho wa dahari kwa hiyo 1Petro 5:8 “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.“ shetani anazunguka zunguka popote palipo na kusudi la Mungu ili awaharibu wana ndoa.

Ndoa katika mpango wa Ibilisi

Unapoyachunguza maandiko utaweza kuona sasa Shetani kama mpinzani wa Mpango wa Mungu naye ana mipango yake inayolenga kuleta uharibifu katika ndoa, Ni muhimu kukumbuka sasa wakati dhambi inaingia ulimwenguni kupitia kazi za shetani taasisi ya kwanza kushambuliwa na vita ya ibilisi ilikuwa ni ndoa kwa haraka sana tunaona sasa katika kitabu cha Mwanzo wanadamu wakiondoka katika mapenzi ya Mungu kuhusu ndoa na kujiingiza katika mapenzi ya ibilisi na matakwa yao au tamaa zao.  Hapa ziko aina nyingi za uharibifu wa ndoa ambao maandiko yanaonyesha kuwa shetani aliufanya kwa ulimwengu hatua kwa hatua na kuwapeleka wanadamu kwenye uharibifu mkubwa sana wa ndoa iliyokusudiwa na Mungu, Dalili zifuatazo ni Ishara ya kazi za shetani kutokomeza mapenzi ya Mungu katika ndoa.

1.      Ndoa ya mke zaidi ya mmoja.

Moja ya dalili kubwa kabisa ya matokeo ya dhambi ilikuwa ni ndoa ya wake wengi ona katika Mwanzo 4:19 “Lameki akajitwalia wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila.Wakati huu kutoka katika ndoa ya mke mmoja ambaye ni mfupa katika mfupa na nyama katika nyama kuelekea kwenye wanadamu kutekeleza tamaa zao kuoa wake wengi ilikuwa ni sihara ya uharibifu wa uadilifu katika ndoa, ndoa hizi zimeonyesha na kuashiria kutokuwepo kwa haki, kuwepo kwa mafarakano, visa na mikasa katika biblia tumeona kuwa hata pale ndugu wa familia moja walipoolewa na mtu mmoja kama Leah na Raheli bado mapungufu makubwa yaliashiria kuwa ndoa hizi hazikuwa mpango wa Mungu, sio hivyo tu wanadamu waliondoka katika ndoa ya mke mmoja kuelekea wake wengi, shetani aliendelea kuwatoa wanadamu kutoka hatua ya kuoa wanawake kwa kujitakia bila kufuata utaratibu.

2.      Ndoa za watu wasiofuata utaratibu.

Ukiyachunguza maandiko hapo katika Mwanzo 4:19 kuna neno KUJITWALIA neno hili laonyesha wazi kuwa Lameki alikuwa mtu wa kwanza wa uzao ule wa Kaini ambao ulijitenga na uso wa Mungu na kwa matakwa yake mwenyewe alijitwalia wake zaidi ya mmoja tofauti na mpango wa kwanza wa Mungu ambao ulikuwa mke mmoja na mume mmoja Mwanzo 2:24 “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.Tabia hii ya lameki baadaye ilienea hata miongoni mwa uzao wa watu waliokuwa wanamcha Mungu na hivyo watu walianza kujiolea bila kufuata utaratibu ona Mwanzo 6:1-2 “Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.” Unaweza kuna maana yake sasa watu waliingia katika kujitwalia wake wowote waliowachagua neno kujitwalia maana yake ni bila kufuata utaratibu, uchafu wa tendo la ndoa na kutokuheshimiwa kwake na watu kujifanyia vyovyote watakavyo bila kufuata utaratibu ulikuwa ni mpango wa ibilisi kuvuruga mpango wa Mungu kadiri dunia inavyoharibika leo, hizi vurugu za shetani zitaonekana ni kitu cha kawaida katika jamii, watu hawatafuata utaratibu, kwa nini Mungu anataka utaratibu ufuatwe? Tusipofuata mpango wake itafikia hatua watu watazaa watoto wakiwa hawajui baba wa watoto hao ni nani, wanaume watakanusha watoto kwa nsababu hawana uhakika kuwa mimba hiyo ni yake au ya mwanaume mwingine ni jambo la kusikitisha Mungu alihukumu kizazi hiki cha watu wasiofuata utaratibu

3.      Ndoa ya watu wa jinsia moja.

Baada ya ndoa za watu wasiofuata utaratibu biblia inatuonyesha uharibifu mwingine huu ni wa ndoa za jinsia moja  yaani wanaume kwa wanaume na au wanawake kwa wanawake  mifano ikiwa ni miji ya Sodmoma na Gomora  ona Mwanzo 19: 1-25 “Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi. Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha. Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala. Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote. Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua. Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake. Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi. Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu. Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje mlango. Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango. Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango. Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa; maana tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za BWANA; naye BWANA ametupeleka tupaharibu. Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze. Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu. Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi BWANA alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji. Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea. Lutu akawaambia, Sivyo, bwana wangu! Tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha rehema zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia mlimani nisipatwe na yale mabaya, nikafa. Basi mji huu u karibu, niukimbilie, nao ni mdogo, nijiponye sasa huko, sio mdogo huu? Na nafsi yangu itaishi. Akamwambia, Tazama, nimekukubali hata kwa neno hili, kwamba sitauangamiza mji huo uliounena. Hima, ujiponye huko, maana siwezi kufanya neno lo lote, hata uingiapo humo. Kwa hiyo jina la mji ule likaitwa Soari. Jua lilikuwa limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari. Ndipo BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa BWANA. Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile.Ndoa zinapofikia kuwa ni za jinsia moja hapo ndio huwa ni kilele cha juu kabisa cha uharibifu wa ndoa katika mipango ya shetani, Shetani alifanikiwa kuharibu Ndoa kwa kiwango hiki Mungu alitaka Ibrahimu alishuhudie tukio hili ili iwe fundisho kwa wana wa Israel na wale wote wanaomuamini Mungu wa Ibrahimu kuwa wasifanye mambo kwa mfano wa watu wa Sodoma.

4.      Ndoa ya Ndugu wa damu au ndugu wa karibu sana.

Muda mfupi sana mara baada ya tukio hili la kuangamizwa kwa miji nya Sodoma na Gomora  Biblia inatupa kisa kingine tena namna na jinsi shetani alivyoendelea na jitihada zake za kuhakikisha kuwa kila aina ya uchafu na mambo yanayovuruga na kuleta uharibifu  katika ndoa yanastawi sasa hata tunaona Lutu na binti zake wakilala na kuzaa hii ni aina nyingine ya mipango ya ibilisi katika kuchafua na kuharibu ndoa angalia sasa Mwanzo 19:30-38 “Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili. Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote. Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao. Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena usiku huu, ukaingie ukalale naye. Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo. Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo.” Hili lilikuwa ni tukio la kushangaza sana namna na jinsi shetani alivyoweza kuharibu Familia hii ambao walikuwa wameokolewa kutoka Sodoma sasa wanaingia katika uchafu huu, dhambi ya aina kama hii inaonekana kufanyika pia katika kanisa la Koritho wakati wa kanisa la Kwanza 1Wakoritho 5:1-2 “Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo.Unaweza kuona kuwa tabia za uchafu wa aina hii unaweza kufanywa hata na watu walioko kanisani kama hawatasimama na kushindana na ibilisi katika kupingana na uharibifu anaokusudia kuufanya katika ndoa ni kwaajili ya haya Musa alitangaza laana kubwa sana kwa watu wanaoweza au kuthubutu kutaka kufanya mapenzi ngono au tendo la ndoa na jamii ya watu waliokaribu nao na ambao ni ndugu zao ona Mambo ya walawi 18:1-24 “BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena wewe na wana wa Israeli, uwaambie, Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mliyokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msiende katika amri zao hao. Mtazifanya hukumu zangu, nanyi mtazishika amri zangu, ili mwenende katika hizo; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi BWANA. Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi BWANA. Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake.  Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako. Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue. Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe. Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake. Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu. Usifunue utupu wa umbu la mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya karibu.Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi lako. Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo. Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo.  Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu. Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu hai. Nawe usimkaribie mwanamke kufunua utupu wake wakati wa kutengwa kwa ajili ya unajisi wake. Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye. Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapitisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA. Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko. Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote;Mungu aliweka sheria hizi zote kwa kusudi la kulinda uadilifu na kuweka utaratibu miongoni mwa watu wake kwa sababu mataifa na dini zile za kanaani zilifanya haya hawakuishi kwa utaratibu wa kimungu bali wa kishetani na Mungu akliwataka watu wake kutunza uadilifu, Hata hivyo sheatani aliendelea na vita byake dhidi ya ndoa hata kufikia utaratibu wa ndoa kuwa utaratibu wa mikataba yaani ndoa zenye talaka, Mpango wa talaka ni ishara nyingine ya kuharibiwa kiuadilifu kwa ndoa je inawezekanaje mtu ambaye ni mfupa wako na nyama yako sasa ikafikia ngazi ya kuachana kwa karatasi na wino?

5.      Ndoa ya mikataba kupeana talaka.

Talaka haina tofauti na ndoa za mikataba tu, watu wanaingia makubaliano wanaishi kwa muda flani halafu wanaachana huu haukuwa mpango wa Mungu, Kisheria Musa aliruhusu hati ya talaka katika torati, hii ni kwaajili ya maswala ya kimahakama au kimaamuzi kwa vile Musa pia alikuwa mwamuzi wa Israel Judge, Lakini katika uadilifu na mpango wa Mungu, Mfupa wako na Nyama yako haviwezi kutenganishwa kamwe, watu ambao wamekuwa mwili mmoja wanatenganishwaje ? lakini kutokana na uharibifu wa kimaadili hati ya talaka ilikubalika ona maandiko Kumbukumbu 24:1-4 “Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake.  Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine. Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe; yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za Bwana; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi. Yesu Kristo nabii mkuu au mkuu wa manabii au mwenye kutuma manabii ambaye manabii wote walizungumza habari zake yeye ndio kiongozi mkuu wa wokobvu wetu alipokuja Duniani katika mafundisho yake hakukubaliana na swala zima la hati ya talaka, kwani hili halikuwa msingi wa mwanzo wa mpango wa Mungu kupeana talaka ni kutoka nje ya mapenzi ya Mungu Mungu alonyesha wazi kuchukizwa na tabia ya kuachana na hata kunyimana unyumba ambako kuliitwa kutendana mambo ya hiyana ona Malaki 2:14-16 “Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako. Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.” Ni wazi kuwa Mungu anachukia kuachana Yesu alionyesha wazi kuwa watu waadilifu na wale wanaomfuata yeye wanapaswa kukubali kuwa kutoa talaka ni ngazi ya juu kabisa ya ugumu wa moyo uliokosa msamaha mapenzi ya Mungu kamili kwetu ni kuwa ndoa zidumu mpaka kifo kiitenganishe ona Mathayo 19:3-10 “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?  Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?  Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.  Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.” Kutokana na kifungu hiki ndio maana utasikia usemi kama ule Ndoa ni pingu za maisha, au utasikiwa wamefunga pingu za maisha usemi huu una maana gani? Wanafunzi wa Yesu (Mitume) walimuelewa sana  Yesu alipozungumzia  Maswala ya ndoa hasa pale alipokuwa akijibu maswali ya mafarisayo kuhusu ndoa, Mafarisayo walimuuuliza Yesu kwa kumjaribu kama Ni halali mtu kumuacha mkewe kwa kila Sababu,Majibu ya Yesu yalionyesha kuwa hakuna sababu  ya mtu kumuacha mkewe hata kama mmojawapo wa wanandoa amefanya zinaa! Wanafunzi kwa kulielewa hili walisema mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivi haifai kuoa.

Najua utakuwa umeshitushwa sana na Mtazamo huu hapo juu lakini nataka nikupeleke katika msingi wa mafundisho ya Kristo kuhusu ndoa na Kuachana, Ni muhimu ikaeleweka wazi kuwa wakati mafarisayo wakimuuliza Yesu maneno hayo walikuwa tayari wameathiriwa na shule kuu Mbili za marabi maarufu waliofundisha theolojia za kiyahudi Rabi wa kwanza aliitwa Rabi Shimney huyu alikuwa na msimamo mkali alipinga Kuachana akisimamia vilivyo mafundisho ya Musa na rabi wa pili aliitwa Rabi Hilel huyu alikuwa na mrengo wa kushoto na msimamo wa wastani yeye alikazia kuwa waweza kumuacha mkeo kwa sababu zozote na ukaoa mwingine akisimamia Sheria ya Musa, Kimsingi Mafarisayo wengi walipendezwa na msimamo wa Hilel katika maswala ya ndoa na kwakuwa walimuona Yesu kuwa Kama rabi mwenye msimamo wa wastani  walitaka kujua kuwa angelielemea katika Eneo gani kati ya haya Mawili;  katika namna ya kushangaza sana Yesu alionekana kuwa na Msimamo mkali katika Eneo la ndoa kuliko Hilel, Shimney na Hata Musa Mwenyewe Yeye alionyesha kuwa hakuna sababu yoyote ambayo inakubalika katika Mungu kuwa Inaruhusu Mtu kumuacha mkewe au kuachana na ya kuwa hata Musa aliruhusu talaka kama matokeo ya ugumu wa mioyo waliyokuwa nayo wayahudi kwa vyovyote ugumu huu ni ile hali ya kutokusamehe.

Watu wengi sana leo wamewaacha wake zao au hata waume zao kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao ugumu wa kutokusamehe wamekuwa wakiwaona kuwa wenye dhambi sana ni wangapi ambao wamefanyiana mambo ya hiyana lakini leo wako pamoja inashangaza leo hii kuona hata wapendwa (watu waliookoka) wakiingia katika  hali hizi za kuvunja ndoa na kushindwa na watu wasio mjua Mungu na huku wakiungwa mkono na viongozi wao wa dini kwa nini watu waachane kama Yesu yupo? Yeye alikuwa na msimamo thabiti wa kutokupenda watu waachane je leo tunamfuata Yesu au tunaona kuwa alipitwa na wakati maana wakati wake hakukuwa na Magonjwa na changamoto kama hizi zilizoko leo? Kuachana ni kumvunjia Mungu Heshima na kudhalilisha mafundisho mazuri ya Kristo na kuvunja kanuni zake za uumbaji na utaratibu wake tangu mwanzo acha mawazo ya kuachana katika jina la Yesu, tafuta kutengeneza nyumba yako na sio kuibomoa Yesu alionyesha wazi kuwa hakuna sababu za kuachana. Hii ina maana gani?  Hakuna sababu ya Kuachana. Kifungu kile tulichosoma katika Mathayo 19;3-10. Kimsingi katika mistari hii Yesu alifafanua kuwa hakuna sababu ya Kuachana isipokuwa kifo tu  ni muhimu kufahamu msingi wa Mungu kuwa Yeye anachukizwa na kuachana tangu zamani Kama tulivyoona pia katika kitabu cha nabii malaki hapo juu Malaki 2;16. Hata hivyo kuna utata wa kitheolojia kuhusu Mathayo 19;3-10 kwamba Yesu alisema Mtu anaweza kumuacha mkewe kwa sababu ya Uasherati ni muhimu kuchambua Maana halisi ya Mistari hii ili kupata maana halisi ya kile anachokisema Bwana Yesu, Kwanza ni muhimu kwetu kuchanganua Maneno haya Mawili Uzinzi na Uasherati huku ukitilia maanani kuwa Yesu alitumia neno uasherati.

Tofauti ya Uzinzi na Uasherati;

Katika tafasiri za kawaida za Kiswahili uasherati ni tendo la kujamiiana linalofanyika nje ya watu waliooana au tendo la ngono linalofanywa na watu au mtu ambaye hajaoa au kuolewa mtu wa jinsi hii anapofanya hayo huitwa Muasherati, Uzinzi ni tendo la ndoa linalofanywa na wanandoa nje ya ndoa.
Kwa msingi huu Yesu alipotumia neno Uasherati alimaanisha watu ambao hawajaoana bado isipokuwa wana uhusiano wa kutaka kuoana yaani ni wachumba, hii ni kwa sababu katika jamii ya Kiyahudi hawakuwa na neno mchumba kama tulilonalo sisi, Hivyo Binti bikira ambaye anatarajiwa kuolewa au amelipiwa mahari huyu aliitwa mke na huyu angeweza kuachwa kama angebainika kuwa amefanya uasherati kabla ya ndoa basi uhusiano huu ungevunjika, Mfano mzuri ni ule wa Yusuphu na Mariam walikuwa ni Mtu na mchumba wake ambaye alikuwa amemposa, Hivyo kwa tendo la Yusuphu kumuona Mariam akiwa na Mimba alikusudia kumuacha kwa siri Hata hivyo katika Kumuasa asimuache Malaika na Biblia  inatumia Neno  Usimuache Mkeo” Unaona! Mathayo 1;18-25 “Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.  Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.  Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe; asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.kwa Msingi huu basi Yesu alimaanisha kuwa anayeweza kuachika ni Mchumba na si mke, Yesu anasemaje kwa Wanandoa? Kwa wanandoa endapo wataachana kwa sababu ya zinaa wote aliyeacha na aliyeachwa watakaa bila kuoa au kuolewa tena, na endapo watafanya hivyo yaani mume ataoa na mke ataolewa tena “Remarried” watakuwa wanazini milele yaani wanaishi katika maisha ya dhambi. Yesu anatoa ushauri gani? Wanaweza kumaliza tofauti zao na kupatana tena na kurudiana angalia 1Wakoritho 7; 10 “Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;” kwa nini kwa sababu watu wanapooana wanakuwa mwili mmoja na kinachoweza kuwatenganisha ni kifo tu kama vile ambavyo ndugu wanakuwa ndugu siku zote za maisha yao duniani mpaka ndugu huyo anapofariki Dunia ona   Warumi 7;2-3 “ Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume. Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.” Unaona kwa hivyo ni kifo tu ndicho kinachoruhusiwa kutoa upenyo wa mtu kuoa au kuolewa tena!  Na hakuna kosa lolote linalohalalisha ndoa kuvunjwa na kama ikitokea wanandoa wakaachana wanapaswa kukaa hivyo hivyo maisha yao yote au kurudiana kinyuime cha hapo wanafanya uzinzi  Ni kwa sababu hii wanafunzi wa Yesu walisema Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivi haifai kuoa, Kimsingi Yesu alionyesha wazi kuwa wale walioachana wakati wa Musa waliachana au Musa aliruhusu wafanye hivyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yaani hali ya kutokutaka kusameheana, Hakuna dhambi isiyosameheka hivyo kimsingi kama tunashindwa kusamehe ni Ngumu nasi kupokea msamaha kutoka kwa Mungu. Aidha katika agano la kale wazinzi walipigwa kwa mawe hata kufa na jambo hili lilimfanya mtu mwenye haki awe mume au mke aliyebaki kuoa au kuolewa tena hivyo kanuni inabaki vilevile kuwa kifo tu ndicho kingetenganisha wanandoa Adamu angeamua kumuacha Hawa ingekuwa sawa na kujiharibu mwenyewe je mtu aweaza kujikata sehemu ya mwili wake na kujitupa? Kama watu wakioana wanakua mwili mmoja unadhani kuna usalama watu wanapoachana rudi kwenye msingi wa neno, sasa tunapoona watu wanaachana leo na wanaolewa tena tujue kuwa shetani yuko kazini anafanikisha kazi yake ya kuharibu mpango wa Mungu kwa wanadamu na wote waliotengana na kuamua kuolewa tena wameshindwa vita na kama wana amani ni amani ya bandia, na kama wanamtumikia Mungu sijui ni kwa Biblia gani lakini msimamo wa bwana Yesu uko wazi zaidi ndoa nyingi sana zimepigwa leo, na watu wameoa tena na wengine ni wachungaji kama msimamo huu umekushinda ni vema ukauza nyanya, kwa sababu kama ndoa imekushinda unapoteza sifa ya kusimamia ndoa nyingi zilizoko kanisani, kama ndoa imekushinda huna sifa ya kuhubiri msamaha, huna sifa ya kuhubiri uvumilivu, huna sifa ya kufungisha ndoa, huna sifa ya kuwa kiongozi, maana umeshindwa hata kujisimamia mwenyewe!, huna sifa ya kuwa kiongozi wa maombi na mapambano ya kiroho kwa sababu umeshindwa vita na mapambano dhidi ya ndioa yako mwenyewe!

6.      Ndoa ya binadamu na mnyama.

Kama maswala ya uharibifu wa ndoa kwa talaka na mikataba hautoshi shetani ameshambulia sana ndoa na kuifikisha katika hatua ya wanadamu kutokutamani kuwa na binadamu wenzao sasa watu wanahangaika na kuzini na wanyama, katika karne hizi maswala haya yamezidi watu wanafikia hatua hata ya kufanya ngono na farasi, mbwa, nguruwe na kadhalika haya pia ni machukizo na machafuko ambayo Mungu aliyakemea ona Kutoka 22:19 “Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa.” Kwa nini haya yote yanatokea huu ndio mpango wa ibilisi katika kutaka kuharibu kabisa mpango wa Mungu kuhusu Ndoa, Muda usingeweza kutosha kuelezea kila kitu kibaya ambacho kinaashiria uharibifu mkubwa wa ndoa kwa aina binadamu, lakini hili ndio kusudi kubwa la shetani kuharibu na kushindana na kupambana na kupigana na ndoa kwa wanadamu wote, ndoa hizi zote za aina hii ni mpango wa ibilisi katika kushambulia na kuharibu kusudi kubwa la Mungu kutukuzwa kupitia uadilifu wa watu wake na ndoa zao.

7.      Ndoa ya watu wa Imani tofauti.

Mpango mwingine wa ibilisi katika kuharibu kusudi la Mungu katika ndoa yeye pamoja na majeshi yake ya pepo katika ulimwengu wa roho watataka watu waoane na watu wa imani tofauti kumbuka hapa sio kabila bali imani tofauti, Mungu alipowakataza wayahudi kuolewa na au kuoa mataifa wengine sababu kubwa haikuwa kabila zao bali imani zao, walikuwa wanaabudu miungu mingine na hivyo mpango na makusudi ya Mungu yangeharibika kwa shetani kulazimisha watu wa Mungu waolewe au waoe watu wasiokuwa na imani au wasioamini katika Mungu wa Ibrahim na Isaka na Yakobo  mtego mkubwa wa ibilisi kwa watu wa mungu ni kuwa wao na watoto wao waabudu miungu mingine jambo ambalo ni machukizo kwa Mungu Kumbukumbu 32:16 “Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa machukizo”.  Imani hizi ni mbaya na zina ushetani mwingi na uovu mkubwa sana Zaburi 106:37 “Naam, walitoa wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani.” Mungu hataki kwa namna yoyote watu wake kushirikiana na mashetani 1Wakoritho 10:20-21 “Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.Mungu alipowakataza wana wa Israel wasioane na watu wa mataifa yale yanayowazunguka sababu kubwa ilikuwa ni kuzilinda imani zao, kuwalinda wasiingie kwenye wimbi kubwa la kuabudu miungu na kushiriki ibada za kishetani, Mungu aliwaonya kuwa ndoa ni moja ya kwa watu hao wa imani tofauti ni moja ya mtego wa ibilisi atakaoutumia kuwaingiza katika ibada hizo na tabia mbaya isiyo ya kiadilifu na itakayoharibu utukufu wa Mungu duniani Kutoka 34:11-16 “Liangalie neno hili ninalokuamuru leo; tazama, mbele yako namtoa Mwamori, na Mkanaani, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.  Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako. Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao. Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa BWANA, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu. Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake. Ukawaoza wana wako binti zao, nao binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakawavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao.”  Unaona hakuna hekima unaweza kuitumia hapa kuwavuta wao kwa Mungu, wewe ndio utakayevutwa kuelekea upande wao na kujikuta ukiingia katika mtego wa ibilisi ni kwa kutumia ndoa shetani atajitahidi kuwanasa watu wa Mungu waingie katika mtego wa ibilisi ndoa na watu wa imani tofauti nay a Mungu wa kweli iko mifano kadhaa katika biblia ambapo muda usingeweza kutosha kuiona ya watu ambao walioa wanawake wa aina hiyo na baadaye wakajikuta wanaabudu miungu moja ya mifano hii ni Mfalme Sulemani aliyegeuzwa moyo na kumuacha Mungu wa baba yake kwa sababu ya kuoa binti za wanawake wa falme za kipagani 1Wafalme 11:1-6 “Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda. Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni. Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.Wewe huwezi kudai kuwa una hekima kama Suleimani lakini hata pamoja na kupewa hekima kubwa aligauzwa moyo na kuabudu miungu kwa sababu ya mtego wa ndoa, wakristo hawana budi kuvumilia na kusubiri kuolewa na mtu mcha Mungu wa jamii ya Kikristo, usikubali kuingia katika mtego wa ibilisi na kusukumwa kuoa au kuolewa na mtu wa imani tofauti na yako, unaweza kudhani kuwa mtazamo huu ni wa gano la kale tu hapana katika agano jipya pia Paulo mtume alikazia vikali kutokufungiwa nira na watu wasioamini ona 2Wakoritho 6:14-18 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.  Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,” andiko hili linakataza sio tu kuoana lakini hata kushirikiana katika maagano au vutu vyenye kutufunga pamoja na wasioamini, kwa kuwa tunazungumzia ndoa hapa nataka kukazia kuwa Mungu hajaruhusu ujiolee tu mtu wa imani tofauti  na ya Mungu wa kweli n ukioana na mtu awaye yote ambaye yuko nje ya ushirika na Yesu umeingia katika mtego wa ibilisi katika ndoa yako wewe na watoto wako, unapooa mtu wa imani tofauti na yako maana yake unaunganisha mwili wako na mtu anayetokea katika chanzo kingine cha kiroho jambo hili litazuia kuendelea kuenezwa kwa utukufu wa Mungu duniani Kumbukumbu 22:10 . “Usilime kwa ng'ombe na punda wakikokota jembe pamojamwenye masikio ya kusikia na asikie

8.      Ndoa ya watu waovu.

Ni muhimu kufahamu kuwa shetani akitaka kuleta uharibifu katika kanisa hutumia ndoa mbovu ya watu waovu, kama katika kanisa kutakuwa na ndoa mbovu ni rahisi kuwa na kanisa bovu au kuwa na viongozi waovu, Tangu kanisa lilipoanza kwa nguvu siku ya Pentecost tunaona Shetani hajawahi kutajwa tena mpaka katika Matendo 5:1-11 1. “Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali, akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?  Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya. Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika. Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo.Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe. Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe. Hofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya.Hapa shetani anatajwa kwa mara ya kwanza katika kanisa la kwanza akiwa amewatumia wana ndoa Anania na Safira wao ni wana ndoa walioshindwa kumpinga shetani ili kusudi wasitumbukie katika mtego wa dhambi, kutokana na tabia yao na mwenendo wao waliliathiri kanisa kwa kumpa ibilisi nafasi na wakapatana pamoja ili walidanganye kanisa hii inatufundisha nini kwamba Shetani anaweza kuzitumia ndoa kupinga mpango wa injili, kuna wanadoa wengi wanaotaka kujitoa kwaajili ya kanisa lakini shetani anaweza kuwazuia wenzi wao wasitoe, kuna wahubiri wengi wazuri wameanguka na kushindwa kuwa Baraka kwa kanisa kwa sababu ya ndoa mbovu, unasikia muhubiri mkubwa sana anayetumiwa na Mungu kwa mamlaka ya ajabu sana, mkewe anavunja maagizo ya neno la Mungu la kutokunyimana agizi ambalio liko wazi msinyimane wao wanawabania waume zao na kuharibu huduma zao katika karne hii haya tumeyaona sana Petro aliona ni afadhali hawa wafe lakini Kanisa liendelee, watu wengi kwaajili ya ubinafsi, choyo, ujinga na kutokuelewa hawafikiri kuwa wao ni wa muhimu sana katika huduma za kanisa kupitia ndoa zao, kupitia uovu wa wana ndoa kazi ya Mungu inakataliwa, mabinti wengi na wamama wamekwaza katika huduma zao kwaajili ya mama wachungaji wenye wivu mkali wa kimapenzi, eti mumewe anapofanya huduma yeye anawaza kuwa mumewe ataibiwa, mabinti wanapotaka kumtumikia Mungu wao wanawaza ujinga, shetani amepata nafasi sana ya kulishambulia kanisa kupitia ndoa za watu waovu. Watu wengi wameingia katika mtego wa ibilisi kupitia wake zao akiwemo Adam kwa msingi huo ni muhimu kwa kila mwanandoa kujua na kutambua kuwa usafi wake wa moyo una umuhimu mkubwa kwa kanisa na kuwa tabia zao zina umuhimu mkubwa kwa kanisa fikiria kama Mariamu na yusufu wangekuwa hawana msimamo katika ndoa yao Je wangeweza kuwa Baraka kwa ulimwengu kwa kumlea Masihi!

9.      Kukataza watu wasioe wala kuolewa.

Paulo alimuonya Mwangalizi askofu Timotheo kuwa awe makini kwa sababu wengine watamfuata shetani na kufuata roho zidanganyazo nyakati za mwisho kutakuwako na aina nyingi sana za mafundisho na ni mafundisho ya mashetani na yatakuwa na nguvu sana katika kanisa na hivyo watu wa Mungu wanapaswa kuwa makini katika maonyo hayo yote utaweza kuona shetani hataacha kutumia ndoa angalia katika 1Timotheo 4:1-3 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.Unaona hapa shetani analishambulia kanisa kwa njia muhimu, halishambulii kanisa kwa kukanusha kuwa hakuna utatu, au Kuwa Yesu sio Mungu hapa shetani anaingiza kwa werevu mafundisho yenye kukataza watu kuoa au kuolewa, katika nyakati hizi kulikuwa na mafundisho kuwa kutokuoa ndio kujitoa kwa viwango vya juu sana katika maswala ya wokovu na huko Coritho walifundisha wazi kuwa unaweza kuoa lakini tendo la ndoa ni najisi na hivyo kujiepusha nalo ni kwa muhimu sana katika kujitoa kwako kwa Mungu kiasi ambacho wakristo walinyimana sikiliza nikuambie ni wazi kabisa haya ni mashambulizi ya nshetani na ni muhimu ikaeleweka wazi kuwa kukataza Wakristo kuoa au kuolewa ni sawa na kukataza injili isihubiriwe.

10.  Ndoa ya watu Kunyimana unyumba

Ndoa inaimarika kwa kushirikiana kwenye tendo la ndoa la mara kwa mara au ikiwezekana kila siku na kila saa nafasi ipatikanapo na kama afya zinaruhusu, 1Wakoritho 7:2-5 “Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.”        

Kushirikiana katika tendo la Ndoa kwa wana ndoa mara kwa mara ni jambo zuri na linakubalika sana mbele za Mungu, katika kanisa la Koritho kulikuwa na tatizo la watu kufikiri kuwa huenda tendo hili ni dhambi, kwa hiyo watu walikosa kiasi na kujitoa kwa Mungu katika kufunga na kuomba wakishindwa kuwa na kiasi katika kukumbuka ndoa zao, Paulo mtume aliwakumbusha wajibu wa kila mwana ndoa kuhakikisha kuwa wanashirikiana tendo la ndoa 1Wathesalonike 4:3  Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;” jambo au wazo la kufikiri kuwa tendo la ndoa ni dhambi lingeharibu hali ya utakatifu wao lakini tendo hili linapofanyika ndio linaimarisha utakatifu miongoni mwa wanandoa, swala la kujinyima tendo la ndoa kwa kufikiri kuwa ndio kujitoa kwa Mungu yalikuwa ni mafundisho potofu kwa kanisa la Korintho, Paulo mtume alieleza kwa uwazi kwamba mke na mume wanapaswa kushirikiana tendo la ndoa bila vikwazo kwa hiyo aliwaamuru wasinyimane (Mst5) Kumpa mwenzi wako tendo la ndoa ilikuwa ni moja ya wajibu ambao uliamuriwa katika Torati Kutoka 21:10 “Kwamba ajitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia.” Kumpa mkeo ngono au mumeo ngono ni wajibu kwa kuwa ni haki ya mwenzi wako iwapo mtu hatatoa haki hiyo kimaandiko Mungu atakuja kumuhukumu kwa kosa la kutokutoa haki na kutokumuogopa yeye angalia Malaki 3:5 “Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi.Lugha aliyoitumia Paulo mtume kuhusu kupena haki inafanana na lugha inayotumika kudhulumu au kutoa haki kwa mtu aliyeajiriwa na kutokumpa au kumpa  haki yake au ujira wake au mshahara wake ona katika Yakobo 5:4 “Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi.” Kwa msingi huo kitendo cha kumnyima mwezi wako kinafanana na kuzuia haki ya mtu au mshahara wa mtu au kumdhulumu kwa hiyo kilio cha mwezi wako kuhusu tendo la ndoa au kunyimwa hali yake kitaingia masikioni mwa Bwana na Bwana atahukumu! Sasa Paulo mtume sio tu anaonya na kuwataka wanandoa kupeana haki lakini vilevile anaonya kuwa kunyimana huko kutampa ibilisi nafasi yaani watu wanaonyimana tendo la ndoa au kukosa kiasi kwa visingizio vya kujitoa kwa Mungu na kumnyima mwezi wako tendo la ndoa ni kumkaribisha shetani kuingilia ndoa yenu, shetani akifanikiwa kuwaangusha au kumuangusha mwanandoa mmoja mnakuwa mmewapa nafasi maadui wa Yesu Kristo kukufuru 2Samuel 12:14a “Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za Bwana nafasi kubwa ya kukufuru,  kwa hiyo jina la Bwana litadhaulika watu wanaofundishwa na kuhubiriwa injili watakuwa na moyo mgumu na unasababisha kikwazo kwa injili ya Mungu kusambaa ulimwenguni kote, njia sahihi ya kutatua tatizo hili ni kuhakikisha kuwa wana ndoa wanapeana tendao la ndoa kila wakati, na wote mnalifurahia tendo hilo, kinyume cha hayo mnakaribisha mashambulizi ya shetani kwenye maisha yenu na huduma zenu. Baraka kubwa na mafanikio makubwa ya mwanadamu yamefungwa katika ndoa kama wanadamu wataharibu ndoa wataondoa baraka zote ambazo Mungu amezikusudia acha kuzuia baraka zako, acha kuharibu mpango na kusudi la Mungu kwa mwenzi wako kwa kumnyima au kwa kunyimana kumbuka shetani yuko kazini kukuharibia ndoa yako na ndoa yako ikiharibika umeingia dosari.

Jedwali hapa chini linaonyesha ndoa katika mpango wa Mungu na ndoa katika mpango wa ibilisi

NDOA KATIKA MPANGO WA MUNGU
NDOA KATIKA MPANGO WA IBILISI
Mwili mmoja
Iwe njema
Mke na mume
Mke mmoja
Enye utaratibu
Bila zinaa
Hakuna kuachana
Ya kudumu
Yenye amani na utulivu
Yenye utakatifu
Yenye kupeana
Imani moja
Binadamu kwa binadamu
Nnia sahihi

Mali ya kila mmoja
Watu wanyimane
Jinsia moja
Wake wengi
Isiyo ya utaratibu
Enye zinaa
Yenye talaka
Ya mikataba
Mafarakano na kero
Yenye uchafu
Yenye kunyimana
Imani ya mashetani
Binadamu na wanyama
Njia isiyosahihi

Jinsi ya kupambana na kuitetea ndoa yako
Sheatani pia ataishambulia ndoa ya Kikristo kwa mashambulizi ya aina mbalimbali yakiwemo magonjwa na  mateso mengine yakiwa na uhusiano na uzazi au viungo vya uzazi moja kwa moja ili Ndoa ya Wakristo iweze kuwa imara na yenye kusimama kama lilivyo kanisa wanandoa wanapaswa kuvaa silaha zote za Mungu ili waweze kuzipinga hila za shetani
Waefeso 6:10-20 10. “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.  Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu
kitabu cha waefeso ndio kimezungumzia kwa undani zaidi mapambano ya vita vilivyopo katika ya shetani na kanisa kuliko kitabu kingine chochote, ni kweli tunafahamu kuwa shetani ameshindwa pale Msalabani, lakini ni muhimu kukumbuka sehemu ya hukumu yake haijalkamilika mpaka mwisho wa dahari kwa msingi huo akiwa bado ni mungu wa dunia hii yeye na majeshi yake anapambana na kanisa lakini vilevile anapambana na wana ndoa kwa msingi huo basi ni muhimu kwa wanandoa kusimama imara na kupambana kiume dhidi yake ili waweze kushinda kama ningekuwa natumia English ningeweza kutumia neno  you must be very aggressive” ndio maana biblia inasema tuwe Hodari hii ni lugha ya kivita tuwe hodari katia uweza wa nguvu zake, wanandoa wana nguvu kubwa sana ya kumsabaratisha shetani kama ndoa yao itasimama imara  Kumbukumbu la torati 32:230 “Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana asingaliwatoa?unaweza kuona pia katika Muhubiri 4:9-12 “9. “Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!  Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto? Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.” Biblia inaonyesha kuwa wawili hii ni wale walioshikamana walio na umoja wana nguvu kubwa sana wana uwezo mkubwa sana wa kusambaratisha adui katika ulimwengu wa roho na ndio maana shetani hupigana na wana ndoa ili kuondoa umoja na mshikamano na wakati mwingine ugomvi vita na mafarakano, kinyongo na kutokusameheana ili yamkini hata wana ndoa wasiweze kuomba pamoja  na kama wana ndoa wakifarakana kisha mmoja aakaomba peke yake hawezi kufanikiwa na kupenya 1Petro 3:7 “Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

Ili wanandoa waweze kuwa na ushindi dhidi ya vita kali dhidi ya Shetani wanapaswa kuishi kwa amani wanapaswa kuitafuta sana amani ili kusudi maombi yao yasizuiliwe, kumbuka tunapambana na shetani hivyo tunapaswa kuwa makini sana tunapaswa kuvaa silaha zote za Mungu ili tuweze kuzipinga hila zake asili ya vita yetu hii ni ya kiroho lakini matokeo yake ni ya kimwili, shetani atataka kutushambulia na kutuvuruga akitaka kuhakikisha kuwa mke anakuwa kinyume na mumewe na mume anakuwa kinyuma na mkewe au watoto kinyume na wazazi, aidha vita hii itaathiri wote wanaowazunguka likiwemo kanisa.

Mkiyajua hayo heri ninyi mkiyatenda!

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Jumanne, 12 Mei 2020

Mtego wa shughuli Nyingi!

1Petro 4:15 “Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine.  

Utangulizi:
 Ni muhimu kufahamu kwamba ili mtu wa Mungu aweze kuwa imara kiroho anahitaji muda mwingi wa kukaa katika uwepo wa Mungu, kuomba, kujisomea neno na kutafakari na kuimba na kujizatiti kiroho kuliko tunavyoweza kufikiri, maandalizi yetu ya kiroho binafsi ni muhimu kwa ushindi dhidi ya ibilisi kuliko hata huduma, Mojawapo ya mbinu kubwa sana anayoitumia ibilisi ili kuwamaliza watu wengi kiroho na hatimaye ili aweze kuwaangusha ni kuwaingiza katika MTEGO WA SHUGHULI NYINGI kwa msingi huo ni muhimu kwetu kuijua mbinu hii ili shetani asipate kutushinda kwa kutokuzijua mbinu zake angalia  2Wakoritho 2:11 “Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake Biblia ya kiingereza inatumia maneno “Let Satan should get advantege of us – yaani asije akapata faida, akapata kitu kwetu, akafaidika, kwa mbinu “Fikra” zenye hila zenye kuumiza zenye ujanja cunning strategies mbinu anazitumia adui ili aweze kutushinda, Biblia inatutahadharisha kuwa wajuzi na wajanja katika mbinu za ibilisi ili asitunase, moja ya mbinu hii ni mtego wa shughuli nyingi!
Shetani anajua nguvu zako na uweza wako ulio nao, anajua wazi kuwa asili ya nguvu zako iko katika chanzo cha ngubu za Roho Mtakatifu unachokitegemea, ambacho kimeungwa katika kujityoa kwako binafsi kwa Mungu self devotional kwa msingi huo hataki na wala hatakubali upate nafasi ya kurudi magotini na katika kulisoma neno la Mungu na badala yake atakupa kitu mbadala ili akutumie kwenye hilo na baada ya muda flani aje na mbinu zilezile za kukuangusha ukiwa mtupu kabisa, mtego huu na mbinu hii anayoitumia shetani ni Mtego wa shughuli Nyingi.
Ni muhimu kufahamu kuwa unaweza kuwa unampenda Mungu sana na unapenda sana uwe na Muda wa kuomba na kububujika katika uwepo wa Mungu, unapenda upate nafasi ya kufunga na kuomba na kutafakari neno na kuhudhuria ibada na kufanya mambo yote yatakayokuweka karibu na Mungu na kuna uwezekano kabisa umekomaa kiroho na umefikia ngazi ambayo hakuna jaribu jipya litakuja kwako usilibaini, Shetani akiisha kufahamu hilo hatakuwa na Majaribu ambayo anajua kuwa utashituka kwa haraka bali atakuja na Mtego wa shughuli nyingi, kwa mtego huu atakutumia kwa muda mrefu uwe unashughulika na mambi mengi sana ambayo yanaweza kuwa kama ya kiroho hivi lakini baada ya Muda utagundua kuwa umepungukiwa sana na uwepo wa Mungu na katika wakati huu anaweza kukusambaratisha atakavyo akihakikisha kuwa hauna na wala haupati nguu ya kuinuka tena!  
Binafsi Kuna jambo nimekuwa nikimuomba Mungu sana, kuhusu maisha yangu katika siku za karibuni ili kwamba Mungu aweze kuingilia kati na kunisaidia, nampenda sana Mungu, napenda sana neno lake na napenda sana kuomba na pia kuandaa jumbe za neno la Mungu kwa kusudi la kuwasaidia watu wake, napenda kukaa uweponi mwake,  hiyo ni kazi yangu, ni wajibu wangu ndio kazi niliyoitiwa, nimeitwa kuujenga mwili wa Kristo na hili nalifanya kwa uaminifu, Lakini nahisi kuna kitu kimepungua kwangu, nahisi kiu ya kumuhitaji Mungu, nafanya kazi yake lakini nahisi nimemmisi Mungu, sio yeye tu nimemisi pia baadhi ya watu, ndugu zangu jamaa zangu na hata marafiki zangu nahisi kama kuna jambo ninapoteza sio kiroho bali na hata kimwili, kwa sababu hata ratiba ya kula haiko sawasawa nimekuwa na shughuli nyingi mno mno nikiwa natafakari hilo siku moja nikaelewa kuwa ni mtego wa Ibilisi!
Fikiaria kama unaweza kuwa na shughuli nyingi, kiasi cha kutokuwa na Muda na marafiki, jamaa, familia, mkeo, wanao, na hata muda wa kula au ahata kufanya mazoezi na unarejea nyumbani ukiwa umechoka mno, hata kula kwenyewe unaona uvivu! Kumbuka shughuli ulizokuwqa ukizifanya sio dhambi hata kidogo ni shughuli zilizoko katikati yako na huduma yako, kwa hiyo ni kama za huduma yako, wale watu waliofikia ngazi ya kuwa viongozi, Maasskofu, waangalizi, mitume na manabii watakubaliana nami katika hili kuwa kadiri unavyokuwa na majukumu haya makubwa na shughuli zionaongezeaka mno ni shughuli za kati kati katika ya uwepo wa Mungu na uwepo wa dunia hapa ndipo shetani anapokuweka kwa kusudi la kukuingiza katika mtego huu ninaouzungumzia shetani anaogopa sana akuachie mtu kama wewe ukae katika uwepo wa Mungu anajua utampa shida sana angalia mistari ifuatayo:-

Luka 4:1-2 “Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa

Luka 4:14-15 “Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando. Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote.”

Katika maandiko hayo hapo juu Yesu alikaa katika uwepo wa Mungu kwa muda wa kutosha alikuwa anafunga na kuomba alishinda majaribu yote makubwa ya ibilisi, na sasa anaingia katika jamii akiwa na NGUVU ZA ROHO nguvu hizi ndio zinazomfanya Yesu anakuwa maarufu kil a mahali habari zake zinaenea kila sehemu na watu wote wanamsifu na kumtukuza, Kukaa katika kuutafuta uwepo wa Mungu ni jambo la muhimu na lenye kumuogopesha sana shetani kuliko jambo lolote lile shetania anajua ni vigumu kumshinda mtu anayekaa katika uwepo wa Mungu lakini ni rahisi sana kumpata mtu kwa kumfanya ashighulike na mambo ya wengine kuliko kushughulika na yeye binafsi

Jambo hili hunitokea na mimi bila kupenda unakuwa busy unakuwa na shughuli nyingi tu zenye kuchosha  nikitafakari wakati mwingine naingia shaka kama yanafanana na kile Mungu ameniitia au nimeingia katika metgo wa ibilisi? Siku moja nikiwa nimechoka majira ya saa tatu usiku nikiwa nimevaa suti niliyoivaa tangu asubuhi, na nikiwa sijachukua mazoezi wala kuoga nikiwa nawasubiri watu fulani ambao nilikuwa na kikao nao tangu asubuhi mpaka saa sita nikaenda kunywa chai ya mchana, kisha wao wakenda mjini na kuniahidi watarejea na hivyo nikawa nawasubiri warejee mpaka ilipofika saa tatu usiku waliniahidi wanakuja nikaendelea kusubiri sikubadilisha nguo sikutaka kuondoa nguo nzito mwilini mwangu nawasubiri watu wa Mungu niwahudumie, nilipompigia simu mmoja akaniambia ndio yuko mezani anakula ameshindwa kurudi kha mimi nilikuwa sijaweza kufanya jambo lolote namshubiri yeye, nilimweleza mke wangu naye akaniambia omba ili kwamba roho ya Masumbufu ikuachie unakuwa busy sana lakini ni ubize ambao ni kama unakutesa wewe, ratiba za kula hazikai vizuri, ratiba za mazoezi huzifuati sawasawa, kukaa na familia na hata muda wako wa kuandaa neno la Mungu kaa sawa alinieleza mke wangu!

Nikaomba na kumuuliza Mungu mbona maswala yasiyo ya muhimu lakini yanayoonekana kama ni ya muhimu sana yananiandama maisha yangu  naona nashughulika nayo kuliko yale niyapendayo kuyatenda? Ndipo Roho Mtakatifu akaniambia “UMEINGIA KATIKA MTEGO WA SHUGHULI NYINGI”

Nilifikiri ninamtumikia Mungu na ninafanya kazi zake sasa nimeingiaje kwenye mtego washughuli nyingi? Nilikuwa najiuliza mbona kazi zimeongezeka sana nyingine njema ni za kazini, na taasisi yetu ni ya kimungu tunamtumikia Mungu sasa nimeingiaje kwenye mtego wa shughuli nyingi? Ni Mungu ndiye aliyeniita nilidhani kuwa wakati huu nimekuwa na shughuli nyingi kwa sababu nimekuwa mtu mzima kwa hiyo majukumu yananipeleka nisikokutaka nilijipa moyo kwa neno la Mungu Yesu alimwambia Petro ulipokuwa kijana ulikwenda kokote ulikotaka wewe utakapokuwa mtu mzima mtu mwingine atakufunga na kukupeleka usikotaka, Yesu alikuwa anaongelea juu ya mauti ya Petro katika Yohana 21:18 “Akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka.” Tafasiri ya Maneno haya ya Yesu ipo katika mstari wa 19 Yesu alitabiri namna Patro atakavyokufa akimtukuza Yesu, Mimi niliutumia mstari wa 18 pekee kukubali tu ukweli kuwa ukiwa kijana unakuwa na uhuru mkubwa wa kujifanyia lolote ulipendalo nafasi inakuwa nyingi mno na  unaweza kwenda kokote utakako ukiisha kuwa mtu mzima na mwenye majukumu shughuli zinakufunga kiasi ambacho huwezi kufanya utakalo, bali majukumu yanakulazimisha uyafanye nilitumia maandiko haya kujipa moyo kuwa huenda ndio mambo yalivyo lakini Roho Mtakatifu alisisitiza tu “UMEINGIA KATIKA MTEGO WA SHUGHULI NYINGI” UMEINGIA KATIKA MTEGO WA SHUGHULI NYINGI?

Sasa niliamua kuwa mpole na kumsikiliza Roho Mtakatifu, lakini pia safari hii nilimsikiliza mke wangu, ni nadra sana kwangu kusikiliza mwanamke narudia tena ni nadra sana kwangu kumsikiliza mwanamke hii niachie mwenyewe labda yatokana na athari zangu za kimaandiko na kimaisha huwa simsikilizi mwanamke  aaa huwa namsikiliza sana lakini kwa vile niko  na shughuli nyingi (busy) na huwa anazungumza habari nyingine za kwenye mitandao ya kujamii huwa nahesabu kama mtu anayeweza kunipotezea Muda lakini safari hii alichoniambia “omba ili kwamba roho ya Masumbufu ikuachie u nakuwa busy sana lakini ni ubize ambao ni kama unakutesa wewe,” akili ilinijia kuwa nachoka sana na kufadhaika sana kwa shughuli nizifanyazo kila siku nikihangaikia watu na taasisi  nimekuwa  na shughuli nyingi kweli kweli busy mno hakuna wakati wakupumzika,  shughuli zenyewe ukizitafakari sio dhambi ila ziko katikati ya shughuli za kimungu ni shughuli za kanisa kabisa lakini hazikupi nafasi ya kuukaribia uwepo wa Mungu hizi ndio zinaitwa Mtego wa shughuli nyingi, Mtego huu ndio Ibilisi anautumia kulikamata kanisa la leo, chunguza kwa undani makanisani kila idara ina shughuli, kanisa lina shughuli wachungaji wanashughuli, kuna shughuli za VIJANA, Kuna shughuli za WAMAMA, kuna shughuli za WABABA, kuna shughuli za UJENZI, kuna shughuli za UINJILISTI, kuna shughuli za Vikao vywa WACHUNGAJI, Kuna shughuli za WAANGALIZI, kuna shughuli za MAASKOFU kuna shughuli za UMOJA WA MAKANISA, kuna shughuli, Kuna mipango kadhaa ya maswala kadhaa, kuna shughuli nyingi mno, siku moja nilifika kwenye kituo Fulani cha Polisi kwenye shughuli nikamuona rafiki yangu mmoja ASKOFU wa kanisa Fulani aliwa pale POLISI mimi nilikwenda kutoa taarifa ya mhasibu wetu alikuwa amechukua fedha nyingi za taasisi yetu zilizotakiwa kwenda TRA na tulipokuwa tunambana azirudishe akawa hato maelezo yaliyonyooka kwa hiyo nilimpeleka POLISI na ilinipasa kufika hapo kuandikisha maelezo sikuwa na nania ya kumfunga lakini nilitaka pesa zirudi tu zilikuwa milioni 16, sikuwahi kufikiri kuwa nitafika Polisi hata siku moja, Nilishangaa kumuona Askofu yuko pale, Nilimuuliza Mchungaji Vipi mbona uko hapa akaniambia kuna Mchungaji wangu yuko Ndani amefungwa nimekuja kumletea chakula tulikaa sana pale kituoni wakati huu somo hili lilikuwa ndio linafunuliwa kwangu upesi nikajisemea Moyoni ni “ULE MTEGO WA SHUGHULI NYINGI” ulimwengu umekuwa wa shughuli nyingi, ninasimamia shule ya Seminary mahali ambapo injili inahubiriwa wanafunzi wetu ni wa kiume tu baadhi ya wanafunzi watatu walijihusisha na dhambi ya USHOGA tukawafukuza, wazazi wao wakapingana nasi vikali, wakitaka vijana wao warudishwe shuleni, Afisa Elimu wilaya na Mkoa pia walisimama na wazazi ili kuwatetea warejee shuleni, Msimamo wetu ni kuwa hatuwezi kuwarudhisha shuleni wanafunzi waliokiuka maswala ya uadilifu kwa kiwango kama hiki, ilikuwa shughuli kubwa sana, vikaoa kadhaa vilikaliwa, vikao vya Kamati ya nidhamu, vikao vya walimu, vikao vya bodi ya shule, vikaoa na wazazi vikao na maafisa Elimu, vikaoa na watu wa usalama wa taifa  ilichukua miezi mitatu kuumaliza mgogoro huo wa kuvutana sisi HAWARUDI maafisa Elimu wanasema WATARUDI lilikuwa jambo la kushangaza viongozi wakubwa wanaotakiwa kusimamia uadilifu katika maswala ya Elimu wakitetea ujinga na uchafu, tena wakisema haifai Mchungaji kuwa mkuu wa shule? Nilikuwa naumia moyoni nilitamani Mungu afanye kitu flani na Mungu alifanya lakini mapambano hayo dhidi ya uovu yalichukua miezi mitatu kumalizika na kumbuka maafisa Elimu wote walikuwa wakristo na wazazi wa watoto walioshiriki uovu ule walikuwa wakristo kwa nini shetani alikuwa akitusumbua hivi dunia imeharibika ibilisi alikuwa anataka tuwe na shughuli nyingi tujiumize na kujichosha kwa jambo rahisi la walioshiriki vitendo viovu kinyume na sheria za shule na imani yetu na neno la Mungu walitakiwa kuondoka mara moja lakini tulitumia miezi mitatu kuvutana shetani alitaka kuleta usumbufu na kutuingiza katika mtego wa shughuli nyingi. Sasa basi ni muhimu kujihoji basi mtego wa shughuli nyingi ni nini?
Maana ya Mtego wa shughuli Nyingi.
Nilijiuliza kwanza huu mtego wa shughuli nyingi ni upi? Katika moja ya mafunzo ya awali sana ya wokovu tulijifunza kuhusu kuwa na shughuli nyingi kunavyozuia ukuaji wa mtu kiroho hasa kupitia mfano wa Mpanzi ambapo zile mbegu zilizoangukia katika miiba humaanisha watu wanaolipokea neno la Mungu, lakini kwa sababu ya kusongwa na shughuli za ulimwengu wanashindwa kukua vizuri na hatimaye kushindwa kuzaa matunda! tujikumbushe maana za mfano ule


Mathayo 13:18-23 “Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi.Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.  Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha; lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa. Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai. Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini.”


Nilitafakari sana kifungu hiki cha maandiko kwamba je inawezekana kwamba nimegeuka kuwa kundi la wale waliopandwa kwenye miiba? Ambao shughuli za dunia na udanganyifu wa mali hulisonga neno lisikue?au lisizae, sitaki kujihesabia haki sitafuti vitu vya dunia nimeridhika Mungu amenipa kila kitu ambacho mwanadamu wa kawaida anatakiwa kuwa nacho sitaki mambo makubwa kwa hiyo udanganyifu wa mali hauwezi kunisumbua lakini naweza kukiri kuwa shughuli za dunia zimenifunga, shughuli za dunia ni nyingi na sio lazima ziwe dhambi, lakini ni kazi za kawaida lakini hili silo lile ambalo Roho Mtakatifu alimaanisha.


Kwa hiyo nilitafakari kifungu kingine Katika wimbo uliobora 1:6 “Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.“


Kifungu hiki pia sio tatizo kubwa sana huyu ni mtu ameajiriwa na au amefanywa mtumwa maisha yake yamemlazimisha kuwa mtumishi wa wengine kiasi ambacho ameshindwa kutimiza wajibu wa kuangalia mambo muhimu yanayiomuhusu yaani shamba lake mwenyewe la mizabibu, huu sio mtego wqa shughuli nyingi  ni mazingira flani tu ya kuajiriwa na kutokufanya maswala yako mwenyewe, hili halikuwa lile ambalo Roho Mtakatifu alikuwa analikemea kwangu “UMEINGIA KATIKA MTEGO WA SHUGHULI NYINGI”
Kwa hiyo nilitafakari kifungu kingine tena kuhusu siku ile Yesu alipomtembela Martha na Mariamu ona 


Luka 10:38- 42 ”Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie. Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.”


Hichi alichokisema Yesu kwa Martha kilikuwa ni cha Muhimu sana angeweza kuketi kama Mariam na kumsikiliza Yesu ambaye anauwezo hata wa kushusha chakula kutoka mbinguni, Yeye alikuwa akisumbuka kwaajilya kumpikia Yesu hakikuwa tatizo kama Martha  angepika na kuleta chakula  kwa Yesu angekula yeye ni mwanadamu kwa wakati ule angekula lakini tatizo la Martha alinung’unika na kushitaki kuhusu Mariamu Hivyo Yesu alitaka kuonyesha ubora wa Mariamu kwa upande mwingine kumsikiliza Yesu na kukaa minguuni pake ni shughuli muhimu sana, Kuliko alichokuwa anakifanya Martha,  Martha alikuwa  na shughuli nyingi (busy) lakini hili halikuwa tatizo isipokuwa kama tu amenung’unika lakini shughuli yake ilikuwa ni sahihi kimila na kitamaduni kushughulika kwaajili ya Yesu  aliyekuwa mgeni wao haikuwa tatizo kama tutakuwa na shughuli nyingi bila kuwanu;gunikia wengine sio tatizo, mimi ninashughulika kwaajili ya Yesu na sitaki kumlaumu Mtu lakini hili sio lile ambalo Roho Mtakatifi analikemea kwetu Mungu anatuonya na kutukemea kuhusu hili  “UMEINGIA KATIKA MTEGO WA SHUGHULI NYINGI”


Andiko la msingi hasa linasema hivi 1Petro 4:15 “Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au KAMA MTU AJISHUGHULISHAYE NA MAMBO YA WATU WENGINE.


Nitalinukuu andiko hili pia kwa lugha ya kiingereza uweze kuliona vizuri kile kinachomaanishwa hapa 1Peter 4:15 “If you suffer, It should not be as a murderer or thief or any other kind of criminal or EVEN AS A MEDDLER” Neno Meddler – maana yake mwenye kujishughulisha na mambo ya watu katika njia isiyo sahihi, au yenye kuingiliana na shughuli muhimu za kazi, au kujishughulisha ma maswala yasiyopaswa au yasiyotakiwa toleo lingine la kiingereza linatumia neno “Busybody” mtu anayeteseka kwa kujishughulisha na mambo ya wengine yanayoonekana kama mambo yake  au ya Mungu lakini sio ya Mungu KJV inasema hivi  1Peter 4:15But let none of you suffer as a murderer, or as a thief, or as an evildoer, or as a busybody in other men's matters.”



 

Mtu aliyeingia katika mtego wa shughuli nyingi ni mtu anayejishughulisha na maisha ya wengine lakini mtego huu ni mtego wa dhambi isiyokusudiwa, hili ni tatizo kubwa sana unajishughulisha na mambo ambayo sio kazi ya wito wako Mungu aliokuitia na hili pekee ni tatizo tosha na mbaya zaidi mtu mwenye kujishughulisha na mambo ya wengine ana muda mchache au hana muda kabisa wa kushughulikia mambo yake, hawafanyi dhambi lakini wakati wote hufukiri kuhusu wengine hawana muda wa kutubu husaidia wengine kutubu, hawana muda wa kusoma neno husaidia wengine kuelewa neno, hawana Muda kuomba huhamasisha watu kuomba, hawana muda hata wa kula huhudumia watu walioshiba huku yeye akiwa na njaa, hutatua matatizo ya wengine huku yake hakuna anayeyajali kwa ujumla wanapoteza lengo na hawana muda hata wa kujitathimini, wanaweza kunyoosha kidole kwa wengine huku vitatu vikiwarejea wenyewe ikiwa ni ishara ya Mungu Baba Mwana na Roho Mtakatifu wakitusihi kujiangalia wenyewe zaidi kujitathimini na kujilinda na kujihami



 

Huu ni mtego wa Ibilisi anatufanya tupeleke mawazo yetu kwenye kitu vitu ambavyo havitaweza kubadilika ili kwamba tusiweke mawazo yetu katika mabadiliko yetu wenyewe, ni kwaajili ya haya Shetani anataka tuangalie mambo ya wengine ambao ni vigumu kuwabadilisha ili kwamba tusijiangalie wenyewe ambao tunauwezo wa kubadilika kwa haraka kumbuka mtu aliyebadilika yeye mwenyewe ndio mwenye uwezo mkubwa zaidi wa kuwabadilisha wengine, shetani haogopi mtu anayeshughulikia mambo ya wengine bali anaogopeshwa zaidi na mtu anayetumia muda mwingi kwa mabadiliko yake mwenyewe



 

Kwa hiyo utaweza kuona kuwa na shughuli nyingi sio sifa bali ni wazi kuwa ni mtego wa Ibilisi, kukaa kwetu katika uwepo wa Mungu na kubadilika kwetu ndio kwa muhimu zaidi na kunakoweza kubadilisha wengine kuliko shughuli zetu za kushughulika katika kubadilisha mambo!

 



Shetani amefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana kulipa kanisa kuwa na shughuli, makanisa mengi  leo yana mipango na shughuli na watumishi wengi wa Mungu leo wanashughulikia mipango na shughuli, vijana wako kwenye mipango na shughuli, wamama wako kwenye mipango na shughuli, wababa wako kwenye mipango na shughuli, waangalizi wa makanisa wako kwenye mipango na shughuli, maaskofu na viongozi wako kwenye mipango na shughuli, Muda mwingi unaotumika ni wa vikao vya mipango na shughuli wajkati mwingine vikao vya mipango na shughuli ndio huwa vinakuwa virefu kuliko hata ibada yenyewe leo washirika wanakwenda katika ibada lakini wakiwa wamejaa mawazo ya mipango na shughuli, penginepo watatakiwa kutoa taarifa ya mipango na shughuli sasa haya nyanapozidi kuliko yale tutakayoyatolea Hesabu atakapokuja mwana wa Adamu ndio yanaitwa mtego wa Ibilisi na mtego huu una madhara yake angalia kisa kifuatacho:-



 

Baba Mtakatifu Gregory the great (Pichani hapo Juu) wakati wa mwisho wa huduma yake ya kichungaji alikuwa akitafakari kuhusu swala zima na kujishughulisha na mambo ya wengine yeye alitumia mfano wa stori ya Dina katika Biblia hakutumia neno Mtego wa shughuli nyingi bali alifananaisha na kile kinachomtokea mtu aliyenaswa na mtego wa shughuli nyingi, alisema kwanza shetani hutoa mawazo yenye ushawishi kwa mtu ili kumuhakikishia ulinzi na usalama wa uongo kwa kusudi la kumbomoa mtu huyo polepole na mfano huu ni sawa na yake yaliyomtokea Dina.
Mwanzo 34:1-3Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kuwaona binti za nchi. Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri. Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri.” 


Dina alitoka kwenda kuwaona mabinti wa nchi, kila mara mtu anapoacha kuifikiri nafsi yake na kuanza kujishughulisha na wengine Shekemu mtawala wa dunia ataiwinda nafsi hiyo na kuibikiri au kuitia unajisi, shetani nwakati wote huitia unajisi nafsi ya mtu inayojishughulisha na mambo ya nje wakati mwingine bila yeye kujua na shetani atazungumza na wewe kwa maneno mazuri, kwa sababu shetani anatufikiri sisi kuwa watu wenye kufaa kwake  shetani wakati wote atatupa tumaini la uongo lakini hatima yake ni kututia unajisi tu, habari ya Dina ni sawa na mtu anayeingizwa taabuni na shetani, Shetani ataendelea kuzungumza vizuri na mtu anayejishughulisha na mambo ya wengine ili aweze kumnasa katika mtego wake (Binti Bikira wakati wote huwakilisha Kanisa, Binti za nchi huwakilisha wana wa dunia hii na Mfalme wao huwakilisha Mungu wa dunia hii yaani Shetani)


Inawezekana tukawa hatufanyi dhambi, lakini tukanaswa katika mtego wa shughuli nyingi, tukionana  na kukutana na watu wa dunia hii wenye dhambi na wakatutia unajisi kwaajili ya kushughulika nao, tunapaswa kulinda nafsi zetu zisiondoke katika ushirika na Mungu, shetani anataka tuwe na shughuli nyingi (busy) na shughuli za dunia tushughulike na wenye dhambi na kujisahau taratibu, anataka atunase duniani taratibu tutapungua katika kusimamia neno la Mungu, tutapungua katika kuomba, tutapungua katika kuhudumu, kuhudhuria ibada, kutenda mema kuona wagonjwa, kuhudumia yatima, kujenga ushirika, kujenga umoja, kukuza familia kuimarisha ndoa, kukuza ndugu kuonyesha kuwajali baba na mama na washirika weengine, tutakuwa na shughuli nyingi kiasi cha kushindwa kusimamia watoto wetu na malezi yao na masomo yao, tutakuwa na shughuli mno mpaka tunachoka na kushindwa kuona umuhimu wa wa kuwa karibu na Mungu, Kumbuka Dunia haibadilishwi na watu wanaobadilisha wengine bali inaweza kubadilishwa na watu waliobadilika wao wenyewe kwanza, “unapojaribu kubadilisha wengine utayeyuka mwenyewe kama sabuni” tunaposhughulika na wengine tunaweza kuingia vilevile katika mtego wa kujilinganisha nao na kuona aaa mimi sio mbaya sana ukilinganisha na hawa na shetani anaweza kutunasa kijanja sana na kuzungumza lugha nzuri na sisi bila sisi kuelewa kuwa tumeingia katika mtego wa shughuli nyingi,


Mtu aliyechoka kwa shughuli nyingi anapoteza uwezo wa kuona mambo ya Msingi ya kiroho, Kutokana na kuchoshwa kwa shughuli nyingi tunapoteza kujitambua kuwa sisi ni nani kwa Mungu, tunaweza kujikuta tunapuuzima mambo ya msingi kwa sababu tu shughuli nyingi zimetuzinga, mtu mwenye utulivu wa nafsi anaweza kuina kwa jicho lingine na kuyapima mambo kwa uzito unaiostahiki kuliko mtu aliyechoka, Shetani anajua nguvu zako na uwezo wako wa kiroho anajua kuwa unatambua mbinu zake zote kwa kiwango kikubwa anajua uzoefu wako hivyo hawezi kukupata tena vilabuni, hawezi kukupata tena kwa zinaa, hawezi kukupata tena kwa majaribu na mateso lakini anajua akikuacha ufanye shughuli nyingi sana utachoka na kwa urahisi sana atakubembeleza wakati umechoka na kukuchukulia kitu chako cha thamani kile ambacho Mungu amekupa ni wakati gani Esau aliuza urithi wake wa Mzaliwa wa Kwanza ni wakati amechoka na uwezo wa kufikiri umepungua 

Mwanzo 25:29-34 “Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana. Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu.Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza. Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi? Yakobo akamwambia, Uniapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza. Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.”


Jinsi ya kujitoa katika Mtego wa shughuli nyingi!.


Ni lazima tuchukizwe na hali ya kudhalilishwa na kubakwa na na kunajisiwa na ibilisi na kukataa kumuacha azungumze nasi lugha nzuri ya kutupendezesha, Lazima uamke na kujipima na siku za mwanzoni mwa wokovu wako tulipokuwa tunaomba sana na kusoma neno la Mungu sana mambo yalirahisishwa na wala hatukuwa na shughuli nyingi, sasa angalia tuna shughuli nyingi lakini je tunaomba kama zamani je haujihisi kupungukiwa na kitu? Sasa basi tufanye nini lazima tukubali kujipima sawa na neno la Mungu!


Ni lazima tujishughulishe sana katika kuomba ili Mungu atuepushe na mtego wa shughuli nyingi na kuhakikisha kuwa hatukubali kuwa washirika wa shughuli  nyingi na kumpa Ibilisi nafasi, jambo moja la msingi la kukumbuka ni kuwa mtu mwenye shughuli nyingi ni mawindo rahisi sana ya ibilisi, kwa kuwa tunaangalia sana mambo ya wengine kiasi cha kusahau kuangalia mambo yako mwenyewe, ni rahisi kunajisiwa na kuingia katika taabu kwa sababu ya kushughulika na mambo ya wengine, unaweza tu kusahaulishwa na ule mpango wa ibilisi wa kukulinganisha kuwa hata hivyo mimi sio mbaya sana ukilinganisha na wengine, unaweza tu kujifikiri kuwa wewe ni bora sana ukijilinganisha na wengine kumbuka kuwa kiwango cha ubora wetu si watu wengine bali ni Yesu Kristo yeye ndio kielelezo chetu na kiwango cha ubora wetu na ni kupitia neema na rehema tunaweza kufikia kiwango chake tatizo kubwa la watu walioingia katika mtego wa shughuli nyingi ni kuwa wanajishughulisha sana na mambo ya wengine na wanasahau kujihukumu wenyewe kwa msingi huo basi ni muhimu kwanza


1.       1Wakoritho 11:31 “Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa.”  Kila mtu aliyeokoka anapaswa kujipima mwenyewe na kujiangalia mara kwa mara kwamba yuko katika kiwango gani cha kumpenda Mungu na kuacha shughuli nyingi na kujitoa zaidia katika dua na sala na maombi na kulia sana machozi


2.       Tunapaswa kujilinda na kujihami na sifa tunapofanya kazi ya Mungu wakati mwingine watu watatusifu na wenye mahitaji yao wengi watatujia tutajikuta tunawahudumia sana wao na kusahau kuwa nguvu za kuwahudumia hazitokani na nafsi zetu tuuige mfano wa Yesu ambaye mara kadhaa alijitenga na umati wa watu waliokuja kwa nia njema ili awahudumie lakini yeye alikumbuka kwenda kuomba angalia Luka 5:15-16Lakini habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao. Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba.” Leo hii wako watu wanafanya huduma na kushinda wakishughulika na watu kuanzia asubuhi mpaka jioni wanasahahu kuwa ni mtego wa shughuli nyingi Yesu alikumbuka mara kwa mara kujiepusha na kwenda kuomba


3.       Kila unapojiandaaa na jukumu kubwa ni muhimu kutanguliza maombi, Dr David Yong Cho wa kanisa la Full Gospel of Yoido kule Korea kusini huomba masaa matatu asubuhi kabla ya kuingia katika shughuli za kila siku, Martin Luther aliomba masaa matatu asubuhi kabla ya kuingia katika shughuli za kila siku Yesu mwana wa Mungu kwa maandalizi ya huduma yake alifunga na kuomba kwa siku 40 Luka 4:1-2, 14-15 “Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa.” “Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando. Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote.” 


4.       Ni muhimunpia kuwaamini wengine na kugawa majukumu si vema kila kitu ukakifanya wewe, kwa mamlaka uliyonayo unaweza kuwapa majukumu wengine na kuwaelekeza wakafanya kama ambavyo wewe ungefanya  Yesu aliwatuma wale 12 na wakafanya kazi nzuri wakamletea ripoti na akawaagiza wapumzike ona Marko 6:30-32 “Na mitume wakakusanyika mbele ya Yesu; wakampa habari za mambo yote waliyoyafanya, na mambo yote waliyoyafundisha. Akawaambia, Njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokuwa na watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hata haikuwapo nafasi ya kula.Wakaenda zao faragha mashuani, mahali pasipokuwa na watu.” Unaona Yesu alitambua kuwa watu wanaofanya hduma wabahitaji muda wa kuwa faragha na kupumzika 


5.       Kunapokuwa na mambo ya kuhuzunisha au habari ngumu pia huna budi kuhakikisha kuwa unajitenga na shughuli nyingi upate nguvu mpya Mathayo 14:1-13 “Wakati ule mfalme Herode alisikia habari za Yesu, akawaambia watumishi wake, Huyo ndiye Yohana Mbatizaji; amefufuka katika wafu; na kwa hiyo nguvu hizo zinatenda kazi ndani yake. Maana Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodia, mke wa Filipo nduguye. Kwa sababu Yohana alimwambia, Si halali kwako kuwa naye. Naye alipotaka kumwua, aliwaogopa watu, maana walimwona Yohana kuwa nabii. Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode. Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lo lote atakaloliomba. Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe; akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani. Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule kijana; akakichukua kwa mamaye. Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari. Naye Yesu aliposikia; hayo, aliondoka huko katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, faraghani. Na makutano waliposikia, walimfuata kwa miguu kutoka mijini mwao.”


6.       Hatuwezi kufanya maamuzi muhimu huku tukiwa katika shughuli nyingi ni muhimu kukumbuka kuwa kila maamuzi muhimu yanahitaji maombi ili kwamba Mungu aweze kuingilia kati, viongozi nwengi sana wamefanya maamuzi mengi mabaya bila kufikiri wala kuwaza kwa sababu wako kwenye mtego wa shughuli nyingi kisha linawajia jambo linalohitaji maamuzi na wanaamua bila kuwa katika uwepo wa Mungu  Yesu alipotaka kuamua hata kuchagua viongozi aliomba usiku kucha Luka 6:12-13 “Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume;” 


7.       Tunapokuwa na Msongo wa mawazo inatupasa kuomba kwa masaa ya kutosha na hasa tunapotambua kuwa kuna mambio magumu mbeleni yanatukabili Luka 22:39-44 “Akatoka akaenda mpaka mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa desturi yake; wanafunzi wake nao wakafuatana naye. Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni. Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba, akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu. Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]” 


8.       Kumbuka wakati wote Maombi ndiyo yanayotuweka karibu na Mungu, kusoma neno la ke na kulitafakari na kumtii yeye hutupa nguzu za rohoni kwa hiyo ni muhimu sana kwetu kuhakikisha kuwa tunaufurahia uwepo wa Mungu zaidi ya kukubali kuwa na shughuli nyingi Luka 5:16 “Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba."  

         
Kama tutakuwa na shughuli nyingi na Mungu, Mungu ataweka wepesi katika yale tunayoyashughulikia kwa hiyo tusikubali kuingia katika mtego wa shughuli Nyingi

Mchungaji: Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima