Jumanne, 25 Julai 2023

Jinsi ya kuwashinda Pepo wa Mahaba! - Incubus and Saccubus


Waefeso 6:10-13. “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.  Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.”


Utangulizi:

Tuko vitani, uwe unapenda au hupendi lakini ni muhimu kwako kuwa na ufahamu kuwa tuko vitani, hii sio vita kama zile za kawaida za dunia hii, ni muhimu wote kukumbuka kuwa tunazungukwa na maadui wa aina mbalimbali kila siku na kila wakati katika ulimwengu wa roho kila mmoja kulingana  na kiwango chake cha kiroho, uwe umeona au hujawahi kuona lakini uko katikati ya vita, uchaguzi ni wako uweke silaha chini na ukimbie au uvae silaha na kupambana, kwa wale ambao wako tayari kupambana, ufahamu kuhusu somo hili utakusaidia kuweza kufahamu yale yanayokukabili na ukajipatia ushindi, kule kuwa na ujuzi tu kuhusu adui zako unaopambana nao ni nusu ya ushindi kwa sababu kunatusaidia kujua namna shetani na malaika zake wanavyofanya kazi katika ulimwengu wa roho 2Wakorintho 2:11 “Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.” Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele kadhaa vifuatavyo:-

 

·         Ufahamu kuhusu kuwepo kwa pepo wa mahaba.

·         Makusudi ya utendaji wa pepo wa Mahaba.

·         Namna tunavyokaribisha pepo wa mahaba.

·         Jinsi ya kuwashinda Pepo wa Mahaba.

 

Ufahamu kuhusu kuwepo kwa pepo wa Mahaba.

Maandiko yanatueleza wazi juu ya kuwepo kwa Pepo wabaya, shetani na mamlaka zake, jambo hili ni halisi, na sio dhana na ndio maana Yesu alitupa mamlaka ya kushughulika na pepo wabaya Luka 10:18-20 “Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.”

Kama uwepo wa shetani na pepo ungekuwa sio halisi Yesu asingelisema lolote kuhusu hao wala asingetupa mamlaka dhidi yao, lakini kitendo cha kutajwa na Kristo na huduma nzima ya Masihi ilijihusisha pia na kutoa pepo ni swala lililowazi kuwa Pepo wapo na wanafanya kazi katika Nyanja mbalimbali, jambo la kumshukuru Mungu ni kuwa ukimuamini Yesu na kutokumpa ibilisi nafasi ushindi dhidi yao ni Dhahiri. Sitaki kuchukua Muda mwingi leo kuzungumzia uwepo wa shetani na mapepo na namna wanavyofanya kazi,  na historia yao lakini leo nataka tuchukue muda kuzungumzia kuhusu pepo wa mahaba wakiwepo pepo wa mahaba wa ngazi ya juu wajulikanao kama Incubus and Succubus ambao mimi nitawaita Inkubi na Sakubi kwa Kiswahili pepo hao ni wabaya zaidi katika aina ya pepo hao wa kawaida wa mahaba.

Pepo wa mahaba ni roho maalumu wachafu wanaohusika na kuwatesa wanadamu kwa tamaa ya kingono, wakipandikiza mawazo machafu ya zinaa na kuathiri maswala kadhaa katika maisha na utendaji wa kila siku wa wanadamu pamoja na kuwafanya waishi maisha dhaifu ya kiroho, wadumae kiroho na hata kushindwa kuendelea na tabia ya uchaji wa Mungu kwa sababu tu ya tamaa ya ngono. roho hawa wachafu wanaweza kumuingia mtu mwanaume na mwanamke kwa kujificha na kukaa katika akili zao na kuwasumbua kwa tamaa ya ngono, pepo hao wako katika makundi makuu mawili wako wanaofanya kazi kama wanaume na wako wanaofanya kazi kama wanawake na kusababisha ndoto za kingono, tamaa ya kingono, na mashambulizi ya kingono, watumishi wengi wa Mungu wanaojihusisha na utoaji wa Pepo watakuwa wanaufahamu wa kutosha kuhusu kuwepo kwa pepo hao wa mahaba.

Lakini hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa Pepo hao wachafu wa mahaba pia wako kwenye ngazi mbalimbali za kiutendaji na ngazi ya juu zaidi ambao wao huweza kushambulia na kuondoka zao wakiacha athari kubwa sana katika maisha ya mwanadamu huitwa Inkubi na Sakubi kwa kiingereza [Incubus and Succubus] wenyewe hujulikana sana kama pepo wa usiku wa mapenzi ambao hushambulia wanadamu wakiwa wamejitokeza katika umbile la kiume au umbile la kike na kuwanajisi kwa kuwafanyia vitendo vya kingono vilivyo na msisimko mkubwa kuliko wa binadamu.

Inkubi [Incubus] – hawa ni roho wachafu wa mahaba wanaomtembelea mtu wakati wa usiku hususani wanawake na kufanya nao mapenzi.

Sakubi [Succubus] – hawa ni roho wachafu wa mahaba wanaomtembelea mtu wakati wa usiku hususani wanaume na kufanya nao mapenzi.

Pepo hawa hufanya mapenzi na wanadamu hususani wanapokuwa usingizini au katikati ya usingizi na kuamka hawa ni pepo wa ngazi ya juu wa mahaba wanaofanya ngono na wanadamu na wanajulikana kama pepo wa usiku, tofauti ya pepo wa mahaba wa kawaida inkubi na sakubi wao wanahusika zaidi ya upotoshaji wa kingono huo ndio msingi wao mkubwa, tunapozungumzia upotoshaji wa kingono maana yake pepo hawa ni wakali na ni wabakaji lakini hupenda kuhakikisha kuwa wamekuacha umekasirika na kukosa amani ya kiakili na utulivu, pia husababisha mgandamizo mkubwa na mateso ya kisaikolojia, pepo hawa pia wanaweza kuleta tamaa ya kufanya ngono kinyume na maumbile, wanaweza kuwa na majina tofauti tofauti kulingana na jamii mbalimbali duniani, sehemu nyingine hujulikana kama popo bawa na kadhalika, pepo hawa wamepewa majina mbalimbali kutokana na namna wanavyojidhihirisha katika jamii mbalimbali duniani, Pepo hawa sio wa kawaida wako katika ngazi ya juu zaidi na ni wenye nguvu tofauti na pepo wa kawaida wa mahaba, wakorofi na wakali na wanaweza kuchukua nguvu zako! Wao ndio viongozi wa ngazi ya juu zaidi katika maswala yote ya ngono.

Pepo hawa wanauwezo wa kuvaa mwili [Incarnation] sio lazima uwe mwili wa kibinadamu lakini hawa wana kiwango Fulani kinachowaruhusu kuvaa mwili wa kiume au wa kike na kufanya ngono na wanadamu sawa tu na shetani ambaye ni roho lakini aliweza kujitokeza kwa Eva katika umbile la nyoka kama unavyoweza kuona katika kitabu cha:-

Mwanzo 3:1-4 “Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,”

Nyoka huyu maandiko yanamtambua kama Shetani (Joka) Ambaye yeye pamoja na pepo wengine wachafu yaani malaika zake walitupwa duniani baada ya kufukuzwa huko mbinguni, kwa hiyo katika lugha ya kinabii Nyoka na nge humaanisha Shetani na malaika zake, katika pepo wenye gazi inayowaruhusu kutwaa mwili kwa muda na kutekeleza jambo Fulani Sakubi na Inkubi wana ngazi ya aina hiyo kwa hiyo ndio maana wanapofanya uhalifu wa kingono utaweza kuona au kuhisi kuwa unapata hisia za kuhisi kuwa kuna kiumbe kisicho cha kawaida kimefanya jambo linalofanana na uhalisia katika mwili wako na kuacha athari za kisaikolojia, kiroho na mateso. Pepo hawa pia wanahusika na swala zima la kupooza kwa wanadamu [impotance] and [inability of an erection] pamoja na kuua shauku ya kimapenzi kwa wanawake na wanaume.

Ufunuo 12:7-10 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.”

Inaweza kuwa ngumu kuelewa namna roho hawa wachafu wanavyoweza kujipachika mwili lakini wale ambao wamewahi kushambuliwa nao wanajua ukweli halisi wa namna roho hawa wanavyofanya kazi yao, akili yako na nafsi yako itakuhakikishia tukio lisilokuwa la kawaida la kukandamizwa na msisimko mkali na halisi, watakaokuachia au utakaojisikia wakati wamekuingilia. Lakini wakati mwingine wengi huwa wasiri wanaficha yanayowakuta na ni ngumu kuelezea yaliyokukuta kwa sababu Pepo hawa wanabaka au kukuingilia bila ridhaa yako.

Pepo hawa hujidhihirisha wakati wa usiku, ingawa wanaweza pia kujitokeza wakati mwingine hata mchana, wengi wanaeleza kuwa wakati mwingine unawahisi pepo hawa wakiwa na miili yao ya kiroho wanakuja na kufanya nao mapenzi, lakini inkubi na sakubi,  mara nyingi ni wakorofi na waasi na wanavamia na kukukandamiza na kukubaka, wanaweza kukupiga, na kukuzuia wanaweza pia kusumbua na hata kuvunja vitu, unapofikiri kuhusu wao na utendaji wao hauna tofauti na mpenzi mwenye fujo anayebaka au kulazimisha kufanya mapenzi na anayetumia nguvu nyingi katika ngono tofauti tu ni kuwa hali ya hisia kali za ngono yao utakaousikia unazidi ule wa wanadamu wa kawaida.

Pepo hawa watakuachia mbegu mbaya ya kuitamani kufanya ngono kupita kawaida, au wataucha mwili wako ukiwa na athari za kutaka sana ngono na utajua kabisa kuwa umepata mashambulizi ya pepo hao, uhitaji wako wa kingono unakuwa wenye nguvu ya kupita kawaida na unatawala akili yako hali hii itatokea wakati wowote lakini zaidi sana unapokuwa mwenyewe, au unapokuwa peke yako au unapokuwa umelala, au kupumzika, unaweza kujisikia kutokufanya lolote, au kufikiri lolote, unapatwa na uzito hujisikii kuoga, kwenda kazini, au hata kuchangamana na watu utaona tu kuwa unachokitaka wewe ni ile testi ladha ya ngono waliokuachia hawa viumbe, wakati mwingine utasikia hamu na tamaa ya kufanya ngono ambayo ni kali zaidi kuliko ya kawaida ya kibinadamu, mahitaji yako ya kingono hayawi ya kawaida wakati mwingine uhitaji wako wa ngono unakuwa mkubwa kupita kawaida, ni muhimu tu kufahamu sio kila uhitaji mkubwa wa kingono na wa nguvu unatokana na pepo hawa, kwani unaweza kuwa na uhitaji mkubwa wa kingono, kihisia na ukashiriki ngono hiyo kwa nguvu tu lakini na mpenzi wako au mkeo halisi au mumeo halisi, kwa wakati halisi, hii inakuja tu bila kujali ni wakati gani na wakati mwingine hata bila msisimko kutoka nje na ni tamaa ambayo huwezi kuidhibiti, hii ndio nguvu na athari inayosababishwa na pepo hao na ni rahisi kuijua kwa sababu sio ya kawaida! Kama umeokoka na ikatokea ukavamiwa na roho hizi utatambua kuwa pepo hawa ni halisi, na utajua wazi kabisa kuwa umepatwa na shambulizi, kwa ujumla Inkubi na Sakubi wanawasumbia na kuwashambulia waamini pia  katika nyakati Fulani Fulani.  

Inkubi na Sakubi pia hujihusisha na ndoto  zinazohusisha kulowa mbegu au majimaji ya kutoka via vya uzazi au ndoto zinazohusisha kuleta mwamko mkubwa sana wa kingono yaani nyege za kupita kawaida na inapokutokea usiku kama ndoto hizo utaweza kuona umeamka ukihisi uhalisia wa tukio kupoteza usingizi, moyo kwenda mbio na wakati mwingine kuachwa katika hali ya hofu.         

Makusudi ya utendaji wa pepo wa Mahaba.

Incubi na Sakubi ni pepo ambao kazi yao ni kuharibu uzao wa kiungu, wote tunakumbuka habari ya wana wa Mungu na wana wa wanadamu iliyotokea katika Mwanzo 6 ambapo wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu kuwa ni wazuri wakajitwalia wake wowote waliowachagua na kukazaliwa majitu hodari, hii sio lazima kuwa andiko hili liendane na kazi ya inkubi na sakubi kwani wao ni viumbe wa kiroho na hawana uwezo wakuzaa na wanadamu lakini matokeo yao yanafanana na tukio lile la Mwanzo 6 yaani kubadili kabisa mwenendo wa watu wachamungu na kuharibu mwenendo mzima wa kifikra na kiutendaji  na kitabia wa binadamu.

Mwanzo 6: 2-4. “wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu, wakazaa nao wana; hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.”    

Kama ilivyo katika tukio hilo wana wa Mungu walipooa binti za wanadamu kukazaliwa watu hodari ambao kimsingi walianzisha tabia nyingine tofauti na kawaida za kibinadamu na ikalazimu Mungu kuleta gharika, ni katika mtazamo kama huo Mapepo ya mahaba sakubi na inkubi wanapofanya ngono na wanadamu, hawawezi kuzaa nao watoto lakini wanazaa nao watoto wa kiroho,yaani kuna matokeo mabaya sana ya kiroho yanayotokana na athari za pepo hawa,  watoto hao wa kiroho ni nini ni tabia chafu za kingono ambazo ziko nje ya asili ya tabia ya kawaida ya kibinadamu, wao wanataka kuzalisha hali mbaya ya kiroho kwa mtu, wanaamsha hitaji la kingono na kuiharibu dhamiri yako na kuvunjilia mbali ukuta wa kingono na kuzalisha uovu katika ubongo wako wakikuachia mbegu ambayo wanaamini itakuja kuota au kujitokeza, kwa hiyo wanapokuingilia wanaacha athari kubwa sana, kama vile mwanamke mwenye hisia kali za kimapenzi anavyojiachia kwa mwanaume na kumruhusu mwanaume huyo kumtawala kila eneo na kupandikiza lolote analolitaka linalotokea kwake,  au kama mwanamke anayesumbua akihitaji ngono anavyoweza kujiachia kwa mtu aliyemsumbua, mbegu zinapoingia hajui zinaenda wapi zitafanya nini na hajui kama zitambadilisha,au kumpa mimba au magonjwa na yanaweza kujitokeza kwa sasa au baadaye.

Inkubi na Sakubi halikadhalika watakuacha ukiwa na hisia kali sana za kingono na hali ya ukavu wa kiroho, baada ya kukuibia tabia njema na kukupandia mimba ya tamaa mbaya, lengo kubwa ni kutaka kukuchepusha, kukutawala la kukuacha ukijiona hufai, pepo hawa wana ujuzi mkubwa sana wa kukuachia msisimko mkubwa sana wa utamu wa kingono lakini watakuachia hali ya kujiona duni usiyefaa kwa vyovyote vile, raha watakayokuachia hawa roho wabaya kwa kawaida inazidi sana ile ya kawaida na inakufanya uwe teja wa hiyo raha, hali hii inaleta hatia, kwa sababu ya raha ambayo mwili wako umeisikia na inashusha chini nguvu yako ya kukataa jambo hilo tena, kama utaumbiwa tamaa ya kuwataka pepo hao wakutembelee tena na tena utakuwa mshirika na mashetani.

Jambo lingine wanalotaka kuliingiza kwa kazi za pepo hawa wa usiku ni kuchepusha Imani, wanakuachia mgandamizo wa mawazo utakaokupa nguvu ya kutafuta faraja, watakuingiza kwenye shughuli za kingono, kupiga punyeto, kujipa raha zizizo halisi, kuangalia mikanda ya ngono, sinema na picha za ngono, kwa ujumla kila aina ya jambo la kingono linalokupa raha na zaidi ya yote kupoteza uadilifu na Imani kwa Mungu na kujikuta umeacha kumpendeza Mungu, pepo hawa watafanya kila juhudi na bidii ya kuhakikisha unaikana Imani kivitendo:-

Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.”

Wakifanikiwa kukupandikizia hayo maana yake wamefanikiwa kuharibu uhusiano wako na Mungu na unapoteza kusudi la kuishi kwako,  kama kila kitu kinawezekana kwake aaminiye kinyume chake ni kuwa kila kitu hakiwezekani kwake asiyeamini, kwa msingi huo kila kitu kinaanza kuharibika, watu wanaoathiriwa na pepo hawa huanza kuharibikiwa akili, lakini kila kitu katika maisha yao huanza kwenda kombo na unaweza kudhani umerogwa au umelaaniwa, au u mtu mwenye bahati mbaya sana lakini ukweli ni kuwa mfumo wako wa kiimani umeingiliwa na kuharibiwa na kunajisiwa  kwa kuchepushwa na pepo hawa inkubi na sakubi. Sakubi na Inkubi wanajihusisha pia na maswala ya migogoro katika ndoa, ugomvi hasa unaotokana na tendo la ndoa kutokujitosheleza, wanakausha raha ya ndoa, wanaleta ukavu na kuondoa nyege kwa wanawake na wanaume, wanaiba nguvu za kiume na nguvu za kike, wanaiba hata mbegu za kiume, wanazuia watoto wasizaliwe, wanazuia ndoa zisifungwe, na ikifungwa ni kivumbi kwa migogoro, wanapandikiza mawazo machafu unapofanya tendo la ndoa na mkeo au mumeo mawazo yako yanakuwa kwa mwanaume mwingine au mwanamke mwingine, kusudi likiwa lilelile la kukutoa katika wazo la kiungu kukuchepusha, wanajihusisha na kusinyaza uume na uke,  wanaweza kusinyaza uke au uume hata kati kati ya tendo la ndoa, wanajihusisha na kuzuia uzazi,  yaani ugumba na utasa, au idadi ndogo ya watoto usiowatarajia, unaweza kupata watoto wachache sana au ukakosa au ukapata wa aina moja tu kusudi likiwa lilelile la kukutoa nje ya ndoa na nje ya Mungu,  pale unapotaka kupata mtoto au watoto wa aina nyingine, unaweza kuumbiwa wazo la kutafuta mtoto unayemaka nje ya ndoa yako, wanajihusisha na kupiga punyeto za aina zote ikiwa ni pamoja na kutumia vifaa vya ngono kama uume wa bandia, na aina nyingine za vifaa au nyenzo zinazofanana na hizo, mizozo na mafarakano, na zinaa zinazolenga wake za watu na waume za watu watoto wadogo, ndugu na kadhalika vitendo hivi vyote na hata ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia na vinavyofanana na hivi vina ushawishi wa uwepo wa pepo wa mahaba na pepo wa usiku na hasa hawa majini makubwa Sakubi na inkubi, aidha Inkubi pia anauwezo wa kumuingilia mwanaume kinyume na maumbile na Sakubi kujihusisha na maswala ya usagaji yaani kumuingilia mwanamke mwenzake kwa namna ya kusagana, na inkubi pia anaweza kumuingilia mwanamke kinyume na maumbile wakati wote huo watasababisha msisimko mpya na mkubwa usiokuwa wa kawaida ili kukupandia mbegu ya kukuchepusha kutoka katika mapenzi ya Mungu, wanaweza kusababisha kununiana na kugombana sana bila sababu hata kwa vitu vidogo vidogo, kuharibika kwa mahusiano unashangaa tu kama ulichumbia mchumba wako anakukimbia au anavunja uhusiano bila sababu ya msingi, kutokushika mimba, au kutokuweza kumpa mtu mimba, kukosa hamu ya kufanya tendo la ngono na mkeo au mumeo, wakati mwingine kwa muda mrefu tu, kulala mzungu wa nne au kuhama chumba, au kuamua kulala mbali na mwenzako, kwa ujumla wao wanailenga sana ndoa ili iweze kuharibika bila kujali ni mwaka gani watafanikiwa kufanya hilo, na wakati mwingine kuota unaoa au unaolewa, kutokuolewa, au kutokuoa huku ukiwa na umri ambao watu wanatarajia utaoa au kuolewa, wanawafanya vijana wanaume kuogopa kuoa na kubaki mabachela kwa muda mrefu huku maisha yao ya ndoa yakiwa hayaeleweki, pia wanasababisha watu kuachana na kupeana talaka, hii ni kwa sababu pepo hao pia wana wivu, na hawapendi uwe na uhusiano mzuri na mwenzi wako mwanadamu, wanaleta hamu za ngono zisizoweza kutoshelezeka, lengo kuu la pepo hawa ni lazima kukuchepusha ili kutoka katika njia za kawaida za kingono za uumbaji na sheria za Mungu, Katika maandiko pepo hawa wanaitwa kiebrania LILITH AU LILIT ambayo tafasiri yake ni  viumbe wa usiku kwa kiingereza “night creatures

 Isaya 34:14 “Na hayawani wa nyikani watakutana na mbwa-mwitu, na beberu anamwita mwenziwe; naam, BABEWATOTO anakaa huko na kujipatia raha.”  

Ukitazama vizuri mstari huo kwa makini utaweza kuona neno BABEWATOTO nadhani ni Kiswahili ambacho hakitumiki sana siku hizi lakini Biblia ya kiingereza imetumia neno NIGHT CREATURE mfano mzuri unapoangalia katika biblia ya kiingereza ya New International Version yaani NIV maneno hayo yanasomeka hivi:-

Isaiah 34:14 “Derset creature will meet with hyenas, and wild goats will bleat to each other; there the NIGHT CREATURE will also respose and find for themselves places of rest.”

Unaona kimsingi hapa anazungumzwa mnyama mweusi mkubwa kama bundi au popo lakini kwa kiebrania anaitwa “LIYLIYTH” Kwa kiingereza NIGHT SPECTRE yaani mzushi wa usiku au mnyama wa usiku kwa kawaida hapa yanazungumziwa majini ya usiku yaani Majini mahaba au mapepo wa mahaba au inkubi na sakubi ambayo ndio majinamizi ya usiku. Kwa kawaida biblia ina tabia ya kujitafasiri yenyewe kama kuna sehemu imetumia neno gumu eneo lingine linakusaidia kuweka sawa  na hivyo ni rahisi kuelewa kile ambacho kilikuwa andiko hilo limekusudia kupitia andiko lingine ona sasa:-

Isaya 13:19-21 “Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza. Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko. Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na MAJINI WATACHEZA HUKO.”

Andiko hili sasa linatusaidia kufafanua andiko lile la mbele kwamba viumbe wanaozungumziwa hapo ni majini, ndio maana huitwa jini mahaba, au pepo la mahaba, na ngazi ya juu zaidi ya pepo hao ndio sakubi na inkubi, pepo hawa licha ya kuonekana kuchochea raha ya kingono kwa wanadamu lakini wana madhara makubwa sana na maudhi makubwa sana kwa wanadamu kiujumla sio wazuri hata kidogo, unaweza kufurahia utamu wa ngono unaoshirikiana nao lakini unaweza kuwajibika kulipa gharama kubwa sana kwa uharibifu mkubwa watakaosababisha katika maisha yako, shetani hana urafiki na wanadamu ni adui wa wanadamu kwa hiyo ni muhimu kukataa hali hiyo vinginevyo athari watakazozisababisha au wanazozisababisha zimewatesa wanadamu wengi sana na kuwafanya watafute msaada baadaye na kama utakwenda kwa waganga wa kienyeji utasababisha majanga makubwa zaidi hizi ndio athari zinazoweza kusababishwa na majini hawa au pepo hawa wa mahaba:--

-          Pepo hawa huwa wanaharibu sana uhusiano kabla ya ndoa chumba kadhaa zinaweza kuvunjika kama mtu analo pepo hili halitaki mahusiano hata kama mpenzi wako hujamkosea lolote unaweza tu kushangaa amesitisha uhusiano na wewe na labda akabaki anakula tu pesa zako, hata kama ishu sio kula pesa zako lakini ni pepo hawa wamesababisha uhusiano huo ufe bila sababu na baada ya ndoa kama watashindwa kuvunja uchumba wanaleta mafarakano na chuki ya kufa mtu ili mahusiano hayo yaharibike, unaweza kushangaa unamchukia mumeo au mkeo kana kwamba ndiye adui namba moja duniani wakati ulimpenda mwenyewe mtagombana na kususiana na kulala mzungu wanne na wakati mwingine kuvunjiika kwa ndoa.

-          Kama ni kwa mtumishi anayemtumikia Mungu hasa waliotoa mwanya Fulani kushambuliwa na Inkubi au Sakubi basi ujue majini haya yanaharibu kiwango cha upako na huduma ya utumishi wako usishangae wahubiri wengi sana waliokuwa na upako mkubwa sana wamejikuta wakiangukia pua kwani kadiri unavyoongeza kiwango cha upako nao wanaiongeza tamaa ya zinaa mpaka ugundue na kufunguliwa au kufanya kazi ya kujikomboa wewe mwenyewe, kumbuka inkubi na sakubi hawaogopi ngazi yako ya kitumishi, watakuacha utumike na kutoa pepo lakini watahakiklisha unakuwa dhaifu sana linapokuja swala la ngono, huwezi kabisa kufurukuta, utafunga na kuomba, utahubiri, utatoa unabii, utatoa pepo lakini utajikuta u mzinzi mzuri sana na unaweza usielewe sababu zake lakini ni kama uliwapa mwanya sehemu fulani jambo hili litakufanya ukataliwe na Yesu wakati wa hukumu ona;-

   Mathayo 7:21-23 "Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu."

 (Kama wewe ni mtumishi wa Mungu na una tatizo hilo husika nipigie au tuma ujumbe kwa namba 0718990796 Rev. Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima Nitakupa maelekezo ya kuondoka katika changamoto hii ili uweze kuhudumu na kuwahudumia watu lakini uweze pia kwenda Mbinguni)

Inkubi na Sakubi pia ;-

-          Wanaharibu Baraka za Mungu ambazo zimekusudiwa kwako, wanaweza kupandikiza roho ya kukataliwa

-          Wanasababisha kufilisika na kuleta umasikini mkubwa na wa hali ya juu, kila unavyopambana na kuinua kiwango chako cha kiuchumi wao huharibu na kukushusha kwa kasi ili uwe masikini wa kutupwa!

-          Wanapandikiza chuki kubwa mnashangaa unamchukia mkeo au mumeo kwa chuki kubwa sana kana kwamba ulilazimisha kumuoa hii inatokea baada ya muda mfupi tu wa kufurahia ndoa yenu na kuendelea mfululizo mpaka ufunguliwe, au wanaweza kusababisha talaka katika umri wowote wa ndoa yenu.

-          Wanasababisha kutokewa na matukio mabaya yasiyoeleweka elewekaeleweka, kama mikosi, kuharibikiwa kazini nk.

-          Wanasababisha utasa kama yako kwa mwanamke na ugumba kama yako kwa mwanaume mayai hayakomai na mbegu hazizalishi, au kiwango kidogo cha mbegu za mwanaume na kusababisha kukosekana kwa watoto

-          Wanasababisha mimba kuharibika kama zinashika, au kutokushika kabisa, au kuzaa watoto wawili au mmoja ama watoto kadhaa wa kike tupu au kadhaa wa kiume tupu.

-          Wanafunga siku zako za kuona mwezi na kusababisha ugomvi mkubwa katika siku za hatari au za kufurahi tendo la ndoa, wanasababisha kuweko kwa maumivu makali wakati wa tendo la ndoa na uvimbe katika kizazi

-          Wanaleta mawazo mabaya ya kutoa mimba, kuikataa na hata kuharibika, kwa ujumla hali ya uzao inakuwa ngumu. Pepo hawa pia wanaweza kuleta mvurugiko wa mzunguko wa siku zako za mwezi kwa wanawake.

-          Wanavuruga sana tendo la ndoa na hawataki mtu aoe au aolewe unaweza kushangaa mtu wa miaka 40 mwanaume wala hana mpango wa kuoa, au dada mwenye sifa za kuolewa lakini haolewi.

-          Wanasababisha maumivu makali sana wakati wa tendo la ndoa kiasi cha kuhatarisha ndoa na sababu mbali mbali za hovyo hata kununiana na kunyimana bila sababu mtu anaweza kupoteza hamu ya kulala na wewe, maumivu chini ya kitovu na kwenye mji wa uzazi, wakati mwingine kuwa na uvimbe unaohatarisha uzazi.

-          Wanaleta fadhaa kubwa, hali ya kujiona duni, kudhalilisha, kukataliwa na hata kujiona hufai au kutaka kujiua na kukuumbua kuchukiwa na ndugu, jamaa na marafiki, kukufanya ukasirike kasirike na kuharibu mipango yako yote na mambo yako hasa ya maendeleo na kushindikana kwa kila unalolifanya hata kama utasaidiwa.

-          Wanaharibu nguvu za kiume na za kike na kuwafanya washindwe kufanya tendo la ndoa na wenzi wao na hatimaye wanaweza kufunga ndoa na wewe ya kiroho jambo ambalo ni baya  zaidi kwani litaongeza kifungo, Inkubi anaweza kuchukua nguvu za mwanaume mara baada ya kumuingilia kinyume na maumbile na kufunga nguvu zake za kiume kwa kusudi la kumuharibu na kumuingilia mwanamke kinyume cha maumbile ili kumuharibu pia 

-          Ukiota ndoto za kufunga ndoa kuna uwezekano wakawa wamekuoa katika ulimwengu war oho, na ukiota unanyonyesha mtoto kuna uwezekano umezaa nao katika ulimwengu war oho, lakini kimwili hutapata watoto, wala ndoa na kama ikiwepo itakuwa ni ndoa iliyo kwenye mashaka makubwa sana ni ndoa ya moto

-          Kuwakwa sana na tamaa ya ngono ma mambo machafu unapokuwa peke yako, lakini unapokuwa na mwenzi wako unakuwa huna hamu ya ngono kabisa, na unaweza kupoteza nguvu, mwenzio akiwa mbali unatamani sana awepo lakini akiwepo, unachukizwa naye bila sababu za msingi na unatamani asingekuwepo!

-          Pepo hawa wanaweza kuwapo ndani yako kwa muda mrefu na usigundue tatizo, kama wapo ila dalili zake na majanga yote niliyoelezea hapo juu, ufunuo wa juu kabisa kuwa wako nawe ni siku inkubi na sakubi watakapo fanya shambulio la kimapenzi litakalokupa wakati mgumu sana hii ndio dalili mbaya na ya juu zaidi ya kujidhihirisha kwao, na ukiifurahia watakutembelea tena na tena!

Kuna maswala mengi yanayoweza kuonyesha utendaji wa pepo hawa lakini mengi yanapatikana kupitia watu waliowahi kukutana na hali hizo na wakamua kuweka wazi. Sasa ni namna gani pepo hawa wanapata nafasi za kupita na kuwasumbua wanadamu katika maisha yao tunaliangalia hilo katika kipengele kifuatacho:-      

Namna tunavyokaribisha pepo wa mahaba.

Inkubi na Sakubi pamoja na pepo wote wa mahaba kama ilivyo kwa shetani hawatuwezi kibinadamu, kama umemuamini Bwana Yesu na kumfanya kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, pepo wa mahaba huondoka haraka au mara moja tu mtu anapookoka, lakini inkubi na sakubi wanaweza kushambulia kutoka nje sio lazima wawe wamekupagaa, hata hivyo kama ilivyo desturi ya pepo huwa kuna vitu vinawavutia kuja na kusababisha waweze kutushambulia;-

Mathayo 12:43-45 “Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.”

Pepo hupata nafasi kama mioyo yetu iko tupu, imefagiwa na kupambwa, kama hatutaruhusu Roho Mtakatifu kuwapo katika mioyo yetu, kama hatutaruhusu maombi na maisha matakatifu kama hatutaruhusu kujaa neno la Mungu na kama tutaruhuru uasi na ukiukwaji wa amri za Mungu watapata nafasi ya kutushambilia lakini inkubi na sakubi huvutiwa Zaidi na maswala yafuatayo:-

1.       Tamaa ya raha ya zinaa na uasherati

Pepo hawa ni pepo wa tamaa ya ngono na hivyo moja ya pambo lao kubwa wanalovutiwa nalo ni tabia ya kutamani kupenda ngono na misisimko ya kingono isiyokuwa ya kawaida, kwa kawaida iko haja ya kawaida ambayo mwili wa kibinadamu unahitaji lakini inapotokea kuwa haja hiyo inazidi mipaka inakuwa dhambi, mfano kula sio tatizo lakini kula kupita kawaida kwa ulafi ni dhambi, Hakuna shida wala tatizo kuwa na hamu ya ngono ambayo Mungu ametujalia lakini kutimiza mahitaji hayo ya kingono kwa kupiga punyeto, kujitia vidole, kutumia vifaaa vya kujitimizia raha ya kingono kwa vifaa vya bandia, na kila aina ya maasi ya kingono hayo ni mapambo yanayowapa pepo nafasi ya kuichezea miili yetu na kuitumia, wokovu haufanyi kazi na uasi.

Kama unataka kweli kuwa mbali na pepo hawa basi lazima uwe umekasirishwa na tabia mbaya za kwako mwenyewe na kufanya maamuzi ya kutubu na kuacha viashiria ngono vya iana zote ambavyo vitawavutia hawa pepo na hivyo unawajibika kwa uzembe wa kuwaruhusu kukufikia na hata kukudhaklilisha na kukushambulia kupitia matendo yako, kwa hiyo ni lazima ujiangalie moyo wako na kujipima katika mtindo wako wa maisha sawa na neno la Mungu kama uko mlango ulifungua unapaswa kuufunga na kujiweka huru kupitia jina la Yesu

Milango ambayo inaweza kuruhusu pepo wa usiku inkubi na sakubi ni pamoja na

a.       Uzinzi na Uasherati – kila tendo la kingono lisilo halali ikiwemo zinaa, zinaa na ndugu, ushoga, usagaji, na mambo yote yanayofanana na tendo hilo yanafungua mamlaka ya pepo hao kukufanyi lolote.

b.      Kupiga punyeto – Punyeto ni mlango mzuri sana wa kuwaruhusu pepo wabaya wa usiku hususani inkubi na sakubi kutuvamia, kwa sababu kupitia punyeto unafanya dhambi dhidi ya mwili wako mwenyewe na kuutoa ushughulikiwe na pepo wabaya, hata hivyo tendo la punyeto lenyewe linatawaliwa kwa kiwango kikubwa na pepo hawa wa mahaba kutokana na tamaa inayokuwa imepandikizwa ndani yako na wao.

c.       Kuangalia picha za ngono – Ni mlango mzuri sana unaotuharibu akili na kutoa kibali cha kushughulikiwa na pepo wa usiku, picha na sinema za ngono zimeundwa maalumu kufanya kazi sawasawa na utendaji wa pepo wa usiku inkubi na sakubi na hivyo kile ambacho wangekupandikizia kinapandikizwa vema na sinema hizo na hivyo wao kutengenezewa njia nzuri ya kukushughulikia na kutawala na kukudhoofisha na kujiweka katika nafasi dhaifu ya kuupinga uovu huo unapokuja ki halisia, chochote tunachoingiza akilini mwetu wakati wa mida ya kawaida kinaweza kutawala wakati wa usiku  na kuzalidha uovu ndani yetu , usikubali kuingiza uchafu katika ubongo wako pepo wa ngono wako karibu na kila picha ya ngono.

 

Zaburi 101:3-4 “Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami. Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu, Lililo ovu sitalijua.”

 

d.      Kuwa na hisia kali za kingono (Tamaa) –  Moja ya mambo ynayowavitia sana pepo hawa inkubi na Sakubi ni pamoja na kuweko kwa hisia kali za kingono, uhitaji wako mkubwa wa kingono na nguvu kubwa ya uhitaji wa kingono aliyonayo mtu huwavuta pepo hawa na kuja kuweka jiwe la msingi, wana wanavutiwa na mtu mwenye hisia kali za kingiono na wanataka kuja kumsaidia mtu mwenye hisia kali za kingono ambazo hazijatoshelezwa au kutimiziwa mahitaji yake, hisia kali za kimapenzi zinatumika kama sumaku ya kuwavutia maviumbe haya na kukuza uwepo wao na uhitaji wao. Wito wa Mungu na mapenzi yake ni kila mmoja aishi maisha matakatifu na kujihadhari na uasherati hata katiika hatua ya mawazo na kujifunza kuiweza miili yetu katika nnjia ya utakatifu na heshima ona 1Wathesalonike 4:3-5 “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.

 

e.      Mtu aliye katika hali ya upweke – Inkubi na Sakubi pia wanapendelea au kuvutiwa na mtu ambaye ana hisia kali lakini anayezungukwa na mazingira ya upweke huku akiwa na uhitaji wa kingono, yaani ni kama mtu aliyepeke yake anayetamani mtu Fulani atokee, wanamuwinda mtu wa namna hiyo mtu anayehitaji ngono  anayetamani apate mwanaume au mwanamke wa kushirikiana naye ngono, au aliye katika hali ya kusumbuka kwaajili ya ngono, au aliyevunjika moyo, au upweke watu wa aina hii huwavutia viuomba hawa wa kiroho kuja kumshambulia

 

f.        Watu walioumizwa sana kihisia – watu waliumizwa mioyo kihisia wako katika nafasi kubwa sana ya kuwavutia inkubi na sakubi, hususani watu wenye histiria ya kupoitia majanga mazito kama kukataliwa kisaikolojia maumivu makali ya kihisia na kujeruhiwa moyo kunaitwa (Trauma) yaani watu waliopita mateso, vitisho na matukio ya kukataliwa na yenye kuwakandamiza kihisia, changamoto za kisaikolojia zilizokosa majibu, hofu na mateso ya kiakili yaliyodumu kwa muda mrefu, mawazo mabaya, tabia haribifu, au kuvutiwa sana na maswala ya kiroho, watu wa namna hii wanaweza kutengeneza mazingira yenye nguvu za kuruhusu kuja kwa viumbe hawa.

 

g.       Mazingira yenye giza na yenye nguvu – Mazingira yenye giza na nguvu yanaweza pia kutengeneza uwanja mzuri kwa inkubi na sakubi kuweza kuvamia, yaani mazingira ambayo yana historia kali za kihisia kama vile nyumba zulizojengwa na kuwachwa kwa muda mrefu, mapagala, Majengo ya zamani, au eneo linalohusika na matambiko, au mawasiliano ya rohoni, yanaweza kuwavutia hawa pepo, au eneo lenye mabaki ya kale  na eneo lenye rutuba au uwanja ambao unatumika kwa dua na maombi, au mazungumzo na viumbe wa kiroho eneo hilo linaweza kuwa na mvuto mzuri kwa viumbe hao pia

 

h.      Watu waliowahi kupambana na maswala ya rohoni – watu waliowahi kupambana na ulimwengu wa kiroho wa mzizimu, roho, au watu wa rohoni mara nyingi wao wenyewe wanakuwa ni mawindo makubwa ya inkubi na sakubi, madhara ya kirpoho yanayoachwa na viumbe hivi vya rohoni yanaweza kuwa sababu ya viumbe vingine jirani navyo kujihusisha, kwa hiyo ni muhimu kutambua na kupambana na uzoefu huo wa zamani ili kujikinga na uvamizi na mashambulizi ya haya majamaa.

 

i.         Kuwaalika kwa kujua au kwa kutokujua – Yako mazingira ambayi kway yanaweza kuwapoa nafasi pepo hawa kufanya uvamizi, kupitia mawazo yako na matendo yako, hii inaweza kutokea endapo mtu Fulani kwa kujua au kwa kutokujua anatamani viumbe hao wakutane nae au kuzalisha nguvu zenye kutengeneza mazingira ya kuwavutia, kwa hiyo ni muhimu wakati wote kuwa na dhamiri safi na mawazo masafi

Zaburi 19:14 “Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.”        

 

2.       Uchungu na kutokusamehe – uchungu na kutokusamehe unafunga kabisa mlango wa neema ya Mungu kwetu na hivyo kutuondolea ulinzi na hivyo kila iana ya pepo anaweza kupata nafasi ya kulivamia hekalu na maisha yako yakaharibikiwa Yesu alionya ya kuwa kutokusamehe humweka mtu kifungoni

 

Mathayo 18:21-34 “Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi. Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni. Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.  Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia akamkamata, akamshika koo,akisema Nilipe uwiwacho. Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni. Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote.”

 

Unapoacha kusamehe unaachiwa kwa watesaji gerezani maana yake pepo wanapewa kibali cha kukutesa kwa msingi huo ni lazima usamehe, ili kutoa mlango wa wewe kuwa huru mbali na mashambulizi na mapepo yote wakiwepo pepo wa mahaba na sakubi na inkubi maandiko yanasemaje linapokuja swala la mtu kuwa na uchungu na kupaswa kusamehe ni kuhakikisha unaachia kabla jua halijachwa ona Waefeso 4:26-27 “Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi.” Uchungu, hasira hali ya kutokusamehe inapaswa kumalizwa mapema kabla jua halijachwa vinginevyo shetani atapata nafasi wakiwemo pepo hawa hatari wa mahaba inkubi na sakubi.

 

3.       Kufuata kawaida ya ulimwenguWaefeso 2:1-3 “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.” 

 

Ni jambo la hatari sana kuishi kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, yaani kuishi maisha ya kawaida unaweza kuwa uliokoka lakini ukawa huna hata haja ya kuendeleza hali yako ya kiroho badala yake unaishi maisha ya kawaida sana unatumia muda mwingi sana kwenye maswala ya kawaida na yasiyo ya kiroho, inaweza ikawa sio dhambi lakini yanakunyima muda wa kujijenga na kujikuza kiroho au kukuza uhusiano wako na Mungu, kumbuka kuwa tunajiweka katika mazingira magumu katika wakati wa usiku akili zetu na miili yetu inapokuwa imechoka, huu ni wakati ambapo tunategemea sana nguvu za roho zetu kutulinda dhidi ya uovu, kama hatujamjenga mtu wa ndani yaani roho zetu na zikawa dhaifu na kama hatujampa Roho Mtakatifu nafasi roho wabaya wanaweza kuifikia miili yetu na kufanya wayatakayo. Kwa msingi huo ni muhimu kujiendeleza kiroho, wako watu ambao wanampenda Mungu lakini hawaombi, hawasomi neno, hawasikilizi hata kwaya, wanaishi maisha ya kawaida tu, hawana utumishi wa aina yoyote kanisani na wakati mwingine hata hawahudhurii ibada yaani wanaishi kawaida hali kama hiyo inahatarisha ustawi wako wa kuwa mtu wa rohoni na hivyo ibilisi na malaika zake wanaweza kukukushambulia watakavyo kwa sababu wao wako kazini na hawana muda wa kupoteza kosa lako moja tu wao wanajitengenezea ushindi.

 

4.       Msinyimane – 1Wakorintho 7:2-5 “Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.”

 

Moja ya kazi kubwa sana ya pepo wa mahaba wakiwepo inkubi na sakubi ni pamoja na kuharibu ndoa, wote tunajua kuwa moja ya lengo kubwa la pepo hawa kuchepusha, kupotosha kuwaondoa watu katika kusudi na mpango wa Mungu, kuwafanya watu hawa waende mbali kabisa na mpango wa Mungu, sasa jaribu kuwaza kuwa ninyi ni waamini waaminifu na mnamcha Mungu lakini mnanyimana tendo la ndoa au mnakomoana katika tendo hili kwa vyovyote vile kama Paulo mtume alivyosema ngono ni hitaji mojawapo la muhimu la mwanadamu, na mpaka mtu anaoa au kuolewa moja ya kusudi kuwa ni ili aweze kutimiziwa mahitaji yake ya kimwili, na sasa anakutana na hali ya kukosa tendo hilo, jambo hili linafungua mlango wa tamaa ya zinaa, linafungua mlango wa mawazo mabaya, linafungua mlango wa mafarakano, linafungua mlango wa kuvunja agano la ndoa maana kila mmoja aliapa kuwa atampa mwenzi wake haki yake,tendo la kunyimana  linapoteza umaana wa ndoa, nadhani umewahi kuwasikia wakristo wanaosema afadhali ndoa za mitala, au afadhali wenzetu waislamu wanaona kama ndoa ya mke mmoja ambayo ndio mpango wa Mungu unaonekana mpango huo kama ndio wa hovyo zaidi na hivyo kuwafikisha watu kwenye hali ya kulidharau neno la Mungu, tendo la kunyimana unyumba ukiacha tu kuwa linamchukiza Mungu lakini linampa shetani nafasi ya kuharibu na pepo wa mahaba hufanya kazi hiyo lakini inkubi na sakubi wanapata mlango wa kuidhalilisha miili yenu na kuongeza mpasuko mkubwa na uharibifu mkubwa katika ndoa, pepo hawa pia hufanya usimamizi huu wa kunyimana ili kuwachepusha kwenye neno la Mungu lililoagiza msinyimane na hivyo zinaa inaweza kutokea, watu wengi wanajua kuwa ndoa ni agano na agano hili kabla ya talaka linavunjwa na kukiukwa pale watu wanapoanza kunyimana. Kama ulimyima mwenzi wako mpaka akatioka nje ya ndoa fahamu na kukumbuka kuwa kabla hujamlaumu wewe ndio unawajibika kwa kuvunja agano:-

 

Malaki 2:14-16 “Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.  Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.”

 

Kwa msigi huo kama hakuna sababu za msingi zinazosababisha usimtimizie mwenzi wako haja zake za kimwili basi ni vema kuhakikisha kuwa hatuendi na uchungu kitandani na kuhakikisha kuwa wanandoa wanapeana huduma sahihi na toshelevu za kindoa ili kutokumpa ibilisi nafasi kumbuka maneno yale ya mtume PauloMsinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu ni kwambie shetani na mapepo yanapata nafasi aidha kwa kusababisha mnyimane au kwa sababu wewe umeamua kumnyima mwenzi wako na kutokujali hali yake ya kutaka kutimiza hitaji lake kupitia wewe.

 

5.       Hofu na Mashaka – Kuwa na hofu na Mashaka katika maisha yako kunafungua mlango wa pepo wabaya wakiwepo inkubi na sakubi na pepo wengine na pepo wa usiku au pepo wa mahaba kushambulia maisha yako kwa kusudi la kuongezea hofu na mashaka katika maisha yako, wanataka uwe na hofu, ukiondoa hofu na mashaka kwa kawaida utakuwa mbali na kuonewa lakini ukiruhusu hofu na mashaka ukaogopa utaonewa Isaya 54:14 “Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia.” Ukikubali kuogopa na ukajaza moyo wako hofu na mashaka pepo hawa huja kuongezea hali hiyo ili kuchepusha Imani yako na kuidhoofisha kwa kusudi la kuiba uhusiano wako na Mungu.

 

6.       Uchawi na kutokutii au uasi – Uchawi na kutokutii au uasi katika maandiko vinawekwa katika kiwango kimoja kwa sababu uchawi na kutikutii vyote vinahusisha uasi, au kwenda kinyume na njia za Mungu, lakini kwa ujumla kujihusisha na unajimu, kupiga ramli, kuangalia nyakati mbaya, kuwaendea wenye pepo wa utambuzi, na aina zozote za uchawi hata mawasiliano na wafu ni maswala yanayoweza kuharibu kabisa uhusiano wetu na Mungu

 

1Samuel 15:22-23 “Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.”      

 

Mambo ya walawi 19:31Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu

 

Kumbukumbu 18:10-14 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako. Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo.”

 

Tunaweza tusijihusishe na maswala yaliyoidhinishwa hapo juu lakini kama hatuwatunzi vema na kuwatendea haki watu tunaoishi nao, na kuwonea watoto, wenzi wetu na wote wanaoishi katika nyumba zetu, na wote waliokaribu nasi yaani kutokuwa na amani na watu wote kunaweza pia kufungua mlango kwa pepo wa usiku kutushambulia.

 

7.       Unyanyasaji – Unyanyasaji ni moja ya mlango mzuri sana wa kuwaruhusu Pepo wabaya wa usiku kutushughulikia, kwa kuwa pepo wenyewe ni wanyanyasaji, unaponyanyasa watu unajiweka katika njia yao ya kukuingia, lakini pia unaiweka akili yako kuwa chini ya mashambulizi ya pepo, kumbuka kuwa pepo wa usiku Sakubi na inkubi ni wanyanyasaji kwa msingi huo ukiwa na tabia ya unyanyasaji unawapa nafasi ya kukunyanyasa nawe usiku, mtu mnyanyasaji ni mtu asiyejiamini, uko unyanyasaji wa aina nyingi sana, kunyanyasa mke, kunyanyasa mume, kunyanyasa wafanyakazi, na unyanyasaji wa kijinsia, Unyanyasaji huu unahusisha tabia ya kuwaingilia watoto wadogo kingono na vitendo vya aina hii huwaacha watoto walioingiliwa kimwili katika hali ya aibu, hatia na msongo wa mawazo sawa kabisa na utendaji wa pepo wa usiku Dini iliyo safi ni dini inayohusisha kujali “Caring” watu wanyanyasaji huwa hawajali angalia

 

Yakobo 1:26-27 “Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.”

 

Neno kuwatazama kwa kiyunani ni episkeptomai yaani hali ya kwenda kutafuta nafuu ya wengine caring au go to see relieve.  Hali ya kuhakikisha wengine wananufaika kinyume cha hapo ni unyanyasaji, Pepo wa usiku huvutiwa sana na matukio ya upweke, unyanyasaji, msongo wa mawazo, hatia, huzuni mtindo wao wa kimateso unafanana na mwanadamu anayefanya unyanyasaji hivyo kufanya unyanyasaji kunawapa wao mlango wa kuja kuchochea jambo hilo na kukunyanyasa. Swala hili pia linahusisha kujeruhiana mioyo kimsingi kila aina ya udhaifu pepo hawa huititumia kama nafasi ya kufanya wayatakayo.

 

8.       Kuchokana – hii inahusiana zaidi na wana ndoa watu wanapoishi muda mrefu sana katika ndoa hufikia wakati wakazoeana sana na kama ndoa yao ilipita katika majaribu mbalimbali hasa ya kugombana  nasfi zao zinachokana  na hivyo wanandoa hutamani kujaribu mfumo mpya wa kujipatia raha ya nafsi kwa mtindo huu unaweza kufikia ngazi ya kuamua kuchepuka, jambo hili nalo linaweza kufungua mlango wa Pepo hawa wa usiku kukuvamia mawazo yako yatakuwa yanatamani kujaribu jambo jipya, penzi jipya changamoto mpya mwanaume mpya au mwanamke mpya na kadhalika  hali na mna hii inapendwa na pepo hao.

 

9.       Miungu ya kifamilia – Miungu ya kifamilia yaani Mizimu nayo inamchango mkubwa sana katika kusababisha uvamizi wa pepo wakiwepo pepo wa usiku, miungu ya kifamilia ina usumbufu mkubwa sana miungu hii au mizimu ni miungu ya mababa iliyokuwa ikimilikiwa na viongozi wa ukoo fulani zamani ambao hufanya mawasiliano kwa njia ya ndoto na ramli au maono na kupanda kwa pepo ni pepo wa ngazi ya juu miongoni mwa pepo ambao hujihusisha na kutoa taarifa kuhusu sababu ya janga fulani, au ugonjwa, kifo, na majanga mengineyo na wakati mwingine hutoa maelekezo yanayoweza kusaidia kuleta ufumbuzi wa aina fulani katika familia, Pepo hawa kama wako kwenye ukoo basi wataweza kurithiwa kutoka kizazi hata kizazi, Mjomba wa Yakobo Labani alikuwa na miungu na Raheli alipokuwa anaondoka na Yakobo mumewe aliiba miungu ya baba yake ona

 

Mwanzo 31:19 “Basi Labani alikuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo zake, na Raheli akaviiba vinyago vya babaye.”

 

Watoto waliozaliwa na Raheli ni Yusufu na Benjamini, tunafahamu kuwa Yusufu alikuwa mcha Mungu lakini siku za mbeleni watoto wa Yusufu yaani Eframu na Manase, hasa Efraimu alijihusisha sana na kuabudu sanamu kuliko kabila zote katika Israel Hosea 4:17 “Efraimu amejiungamanisha na sanamu; mwache.”

 Athari za kuabudu miungu hata pamoja na kuwa ilitekeketezwa na Yakobo lakini ilikuja kujitokeza katika wana wa Yusufu miaka mingi baadaye hii ni athari ya miungu ya kifamilia roho hizi zinaweza kuwafuatilia hasa wale ambao watakuja kuwa watu wa rohoni na kuwasumbua na kuwatesa ziko familia nyingine shangazi alikuwa tasa na baadhi ya watoto wa ndugu zake wanakuja kuwa tasa hizi ni dalili zinazoashiria kuwa huko nyuma kuna mtu alikuwa na roho wachafu aliokuwa akiwafuga kwa niaba ya familia sasa Pepo wa mahaba wanaweza pia kuingia na kushambulia kwa njia hii hii ya kufuata hali kiroho ya familia  na ndio maana utaweza kuona kuwa kuna familia nyingine wanaathiriwa na maswala kadhaa wa kadhaa yanayofanania kutoka mababu mpaka mababu wakati unapotafuta ukombozi ni muhimu kuhakikisha kuwa unakata kitovu za kiroho cha familia yako kutoka pande zote upande wa baba na mama babu na bibi wa pande zote na kujitangaza kuwa huru huku ni kukata kitovu kwa jinsi ya rohoni yaani kuvunja makataba wa mambo mabaya ya kifamilia na kuruhusu yale mazuri tu.

 

Ezekiel 16:2-4 “Mwanadamu, uujulishe Yerusalemu machukizo yake, useme, Bwana MUNGU auambia Yerusalemu hivi; Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti. Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa.”          

 

Kitovu ndicho kinachohusika kuunganisha mtoto tumboni mwa mama yake na kuumbika na kumkuza muunganiko huo hukatwa mara baada ya mtoto kuzaliwa huu ni muunganiko wa kimwili, lakini uko muunganiko wa kiroho ambao nao unatakiwa kushughulikiwa ili roho za kifamilia zisiweze kukuandama na kukuonea na kukutesa wakiwepo pepo hawa wa usiku inkubi na sakubi kama waliwahi kuwa na umiliki dhidi ya mtu katika familia yenu, zamani. Kata kwa kutumia maombi na kukataa mabaya na kukubali mazuri.

 

10.   Kujihusisha na mambo ya kiroho au nguvu za giza – kujiingiza katika maswala ya kufanya mambo ya kiroho ua ya kichawi pasipokuwa na ufahamu wa kutosha kunaweza kukaribisha mambo yasoyohitajika katika maisha yako, mfano unafanya tambiko au jaribio la kuwasiliana na ulimwengu war oho bila kufuata maelekezo kwa usahihi au bila kuchukua tahadhari, kuna uwezekano mkubwa ukafungua mlango wa inkubi na sakubi, kwa hiyo ni muhimu kufuata maelekezo ya kiroho kwa tahadhari, au kutafuta muongozo kutoka kwa watu wenye uzoefu, ili kukulinda au kujilinda na roho wasiotakiwa na ukajikuta unanaswa nao. Pepo hawa pia wanaweza kutumwa kwa nguvu za giza za kichawi au za kiganga kwa kusudi la kumdhuru mtu au kumuharibia, kwa sababu ya wivu wa mfumo wa maisha yako.

 

11.   Vita vya kiroho – kunaweza kukawa na sababu nyingi lakini kwa wale wenye kiwango cha utumishi ikitokea unashambuliwa na pepo wa usiku ufahamu kuwa ni vita vya kiroho, Pepo hawa kwa kawaida wanatumia nafasi yoyote ile ya kutaka kuathiri  na hivyo inapotokea umelala ni lazima ukumbuke kuwa tunavita, vita vya kiroho tulivyo navyo katika maisha yetu ya kiola siku wakati mwingine vinadhoofisha hali yetu ya Rohoni na ndio maana wakati mwingine wanaweza kupata nafasi ya kushambulia ili walete uharibifu wa kiroho ikiwa ni pamoja na kukuingizia roho ya uzinzi na ndio maana wakati mwingine unaweza kuona sio jambo la kushangaza kuona watoaji pepo waombaji  manabii na wainjilisti watu ambao wako Mstari wa mbele katika vita vya kiroho na huduma unashangaa wanaingiziwa tamaa kubwa Zaidi  ya kingono n ahata kuathiriwa Zaidi kwa sababu ya vita za kiroho kusudi kubwa ni ili wakataliwe na kwenda motoni.

 

Mathayo 7:21-23. “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”

 

Kila muhubiri wa injili na watu wote wanaojihusisha na maswala ya kuimarisha wengine kiroho wako katika ngazi ya juu Zaidi ya kushambuliwa na pepo wa ngazi ya juu Zaidi, kwa msingi huo kwaajili ya ulinzi lazima kanisa lijifunze kuomba na kuwaombea watu walioko katika ngazi za utumishi, lakini sio hivyo tu nao hawana budi kuhakikisha kuwa wanajitahidi kutokujiachia lakini waweke bidi ya kutokufanya kazi ya kuwahubiri wengine kisha wao wakawa wakukataliwa

 

1Wakorintho 9:25-27 “Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.

 

Wimbo uliobora 1:5-6 “Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani. Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.”

 

Ni wajibu wa kila mkristo na wakristo, watumishi kuhakikisha kuwa wanajilinda wanapolinda hali ya kiroho ya wengine wasisahau kulinda na mioyo yao wenyewe ili wasishambuliwe na mapepo haya ya usiku na aina nyingine za pepo ili wao wawe mstari wa mbele katika kuwasaidia.

 

12.   Dhambi yoyote isiyotubiwa kwa haraka – Pepo hawa wanaweza kuitumia nafasi yoyote ya dhambi isiyotubiwa kukuadhibu, maandiko yanasema wala msimpe ibilisi nafasi Waefeso 4:27 “wala msimpe Ibilisi nafasi.” Kumbuka kuwa kazi za shetani ni kuharibu kuchinja na kuua tendo la kumpa ibilisi nafasi linaweza kuleta majuto makubwa sana katika maisha yetu, tunaweza kupata shambulizi la ghafla, haichukui muda mrefu kwa Inbubi na sakubi kusababisha majuto na huzuni katika maisha yako kwa msingi huo tunajua kuwa kila mkristo aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, yaani hadumu katika dhambi, lakini ukikosea na ukatenda kosa moja tu lisilotubiwa hata hasira na uchungu wa muda mrefu unaweza kuleta haribiko kubwa sana katika maisha yetu. Hivyi ukihisi hauko sawa hakikisha kuwa unatubu haraka na usilale na dhambi ambayo hujaitubia hasa wakati wa usiku, hakikisha unatubu, unaishi maisha matakatifu, unafunga na kumuomba Mungu akusaidia na kukuokoa na pepo hawa wa mahaba kwa maelekezo mengine tuzingatie kipengele kinachofuata jinsi ya kuwashinda pepo wa mahaba.   

Jinsi ya kuwashinda Pepo wa Mahaba.

Ni muhimu kufahamu na kukumbuka kwamba moja ya funguo muhimu sana ya kufunguliwa kutoka katika changamoto yoyote ile ya adui kwanza ni maarifa au ujuzi Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.”

2Wakorintho 2:11 “Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.” Kama tumepata uelewa wa kutosha  na ufahamu wa kutosha kuhusu utendaji wa pepo hawa na jinsi adui yetu shetani anavyotenda kazi katika kiwango hicho sasa tunaweza kutumia mbinu za ushindi ambazo maandiko yanatupa ili pepo hawa wawe mbali nasi na tukaishi kwa ushindi, furaha na amani

Lengo kuu la inkubi na sakubi ni kutuchepusha kutoka katika mapenzi ya Mungu, kutuumiza na kutuletea fadhaa, lakini hawa huacha mimba au mbegu ambayo wanaamini itaona katika akili zako na mawazo yako, kwa msingi huo lazima kuhakikisha kuwa tunavunja mkataba nao kwa jina la Yesu na kung’oa kabisa mbegu zao na mimba zao kuzitoa na kuua kila kitu kibaya wanachokikusudia lazima kuhakikisha kuwa kila aina ya kazi za kipepo ambazo zimeainishwa kufanywa ndani yetu zinaharibiwa na kusambaratishwa na kuondolewa na kuuawa kabisa katika maisha yetu, na kuhakikisha kuwa tunakuwa vizuri kiroho ili hayo yatendeke ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo:-

1.       Kama hujaokoka hakikisha ya kuwa unamkubali Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozo wa maisha yako, hakikisha kuwa umesamehewa dhambi zako na unaanzisha uhusiano mwema na Mungu naye atakuhamisha katika nguvu za giza na kukuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake jambo litakaloleta usalama katika maisha yako ya kimwili na kiroho ona Waefeso 2:1-6 “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;”

 

2.       Hakikisha unafunga milango yote ya dhambi ambazo pepo hawa huzitumia kama nafasi ya kupita na kutushambulia  - baada ya kuwa umeokolewa usiruhusu mlango wa dhambi hata kwenye mawazo dhambi zishughulikiwe kwenye nia na mawazo hata kabla hayajakomaa na kuzaaa dhambi na dhambi kuzaa mauti  kila mtu aliyeokolewa anapaswa kujua wazi kanisa kuwa usalama wake ni kukaa ndani ya mji wa makimbilio ambao ni Yesu nje ya Kristo utaumizwa, kushuka kiwango cha kiroho kunakuweka katika hatari ya kuumizwa usitende dhambi tena Yohana 5:14 “Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.”

 

3.       Watangazie pepo wote na mapepo yote ya mahaba na inkubi na sakubi kuwa unakataa kazi zao katika maisha yako na huwezi kuwa na ushirika na mashetani- kama walikuvamia  au kukushambulia au wako ndani yako kwamba kazi zao zinavunjwa na kuharibiwa na kusambaratishwa katika jina la Yesu, kila mbegu waliyoipanda ndani yako na kusababisha madhara iharibiwe na wakome kabisa kukufuatilia tumia jina la Yesu na damu yake kuharibu roho na kujikinga, endapo wamekutokea mara moja anza kushughulika nao mara moja kabla hawajakurudia tena na tena, usikubali roho hawa wakutawale bila kuwakatalia kwa nguvu na kuwaamuru kuacha mambo yao katika jina la Yesu. Kama hutafanya dhambi tena na kuwafungulia mlango basi hawatapata nafasi ya kukushambulia tena 

 

4.       Hakikisha kuwa unamuomba Mungu na kuwakemea kabla hujalala na kama utaota ndoto zao tena unapoamka anza mara moja na usiruhusu mbegu zao kuota katika maisha yako, kumbuka kutamka yale usiyoyataka kwa sababu mauti na uzima uko katika uweza wa ulimi wako, kuitamka kuna nguvu kubwa sana maneno utakayoyasema yatakupa uzima na kuua kila kitu kilichopandwa na usijaribu kuikumbuka ndoto ile hata kama ilikuwa na mvuto kiasi gani. Angusha mawazo yote mabaya kwa jina la Yesu!. Mithali 18:21 “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”

 

5.       Hakikisha ya kuwa unajitakasa na kujiweka wakfu, na kuharibu kila roho chafu iliyopata nafasi katika maisha yako, na usikubali kujihusisha tena na matendo yoyote yasiyo ya kiungu, na ikitokea umekosea hakikisha ya kuwa unatubu haraka, haimaanishi kuwa wewe ni mkamilifu wala hakuna mtu mkamilifu lakini kumbuka kuwa kila aina ya dhambi na tendo lolote lisilotokana na imani lazima lishughulikiwe kwa kiwango cha juu, hii lazima iwe hivyo hawa wakati unashughulika kujikomboa kutoka kwa pepo hawa. Wakati mwingine husisha kufunga na kuomba lakini hakikisha unajiokoa na kila ushawishi, wa aina yoyote wenye uhusiano na maswala ya ngono na dhambi nyinginezo.

 

6.       Kumbuka kila udhaifu na uovu ndani yako unawaalika hawa pepo kukushambulia, lazima ujifunze na kuwa na ufahamu kuwa pepo hawa pia wanaweza kukushambulia kwa njia ya zinaa, hivyo kila unapofanya zinaa uwe na uelewa kuwa unajiungamaisha nao, pia pepo hawa wanapofanya ngono na wewe ni kama unakuwa mwili mmoja nao.hivyo usikubali kuchepushwa kifikra na majini haya

 

7.       Kumbuka pepo hawa ni pepo wa tamaa mbaya na tamaa yao huwa sio ya kawaida na nitamaa isiyo ya kidunia kwa hiyo huwezi kusema kuwa hutajaribiwa tena utajaribiwa kila mmoja hujaribiwa na shetani katika tamaa mbalimbali Shetani yeye ni mungu wa dunia hii atatujaribu tu kwa kusudi la kudhoofisha roho zetu hivyo kumbuka kuishi maisha matakatifu na usikubali kulegea uwe mwenye nguvu.

 

8.       Omba kwa kutumia zaburi za ukombozi kila siku tumia Zaburi 9, 31, 38, 39, 68, na 46 zaburi hizi zitaimarisha misuli yako ya kiroho utakayoitumia kuvunja daraja la uovu na kupandisha Imani huku ukiomba dua za kushughulikiwa kwa adui zako wakiwepo pepo hawa, katika maisha yetu ni Imani yangu kwamba pamoja na maombezi utakuwa huru kutoka katika mashambulizi ya roho hawa wabaya

 

9.       Waone watumishi wa Mungu – watumishi wa Mungu wenye uzoefu wa kukemea pepo hawa na weka ahadi ya kupata maombezi kwa kusudi la kufunguliwa, tubu, omba, kemea, funga, jitoe kwa Mungu, ishi maisha ya kumpendeza Mungu utaelewa kwanini Mungu anatoa wito wa kila mmoja wetu kuishi maisha matakatifu na kuwa makini au kukesha kwaajili ya umakini dhidi ya adui, Mungu ni mwingi wa rehema atafanya.

Endapo utakuwa umesumbuliwa na pepo hawa na wamesababisha madhara kadhaa katika mwili, nasfi na roho yako usisite kunitafuta kwa namba zangu za Whatsapp nitakusaidia, nitakupa maelekezo ya kufanya, kama ni wewe na mkeo msiogopa nitawapa maelekezo hukohuko mliko na mtakuwa huru Mungu ni mwema kwa sababu kwa kila jaribu ameweka na mlango wa kutokea!

 

Na. Rev. Innocent Mkombozi Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.

Whats’app +255 718 99 07 96