UTANGULIZI:
Katika
moja ya kazi zilizongumu kitheolojia ni kumwelezea kibinafsi Yesu Kristo huu ni
mzigo mkubwa mno, Wasomo wengi sana wamekubali kwa haraka kuwa kuna mipaka ya
kibinadamu inayotosheleza kabisa kuwafanya wasimuelezee Kristo katika namna
inayofaa na inapofikia hatua ya kutaka kumweleza inakuwa ni Shughuli ngumu,
Hasa pale inapokupasa kumuelezea mtu huyu mwenye utukufu mkubwa unaozidi
kawaida zaidi sana katika uhusiano wake wa kazi nzima ya ukombozi wa wanadamu
tuliokuwa tumepotea,Kwa msingi huo Basi ingawaje hatuwezi kuelezea au kujibu
kila kitu kumhusu Yesu Kristo lakini kujifunza kuhusu Yesu Kristo kazi zake ndio msingi wa Mambo yote ya
kitheolojia na ndio kiini cha Biblia nzima kutoka Mwanzo hata Ufunuo, Kwa
msingi huo kusudi la somo hili ni kukuhabarisha swala zima kuhusu Yesu Kristo
kama anavyelezwa Kibiblia na kujaribu kufafanua maeneo magumu ili kuyaelezea
upate kumfahamu Bwana Yesu katika upana wake.
Vitabu
vingi sana vimeandikwa kumuhusu Bwana Yesu lakini kozi hii au somo hili
limeandaliwa ili kukupa wewe kuelewa ukweli wa kitheolojia kumuhusu Yesu ili
awe rafiki wa karibu sana unayeweza kufahamiana naye Vizuri na utaona jinsi
Mungu alivyofunua Neno lake la ukombozi wa mwanadamu na kulitimiza kupitia Yesu
Kristo maswala ambayo yatakusaidia si tu kumuelewa bali pia kumueleza Vema kwa
wengine
Kuzaliwa
kwake kunaadhimishwa dunia nzima na kifo chake na habari za kufufguka kwake
zinzsimuliwa na kuutikisa ulimwengu mzima na kila anga Huyu Ni nani? Swali kama
hili litakuwa linajaribiwa kujibiwa katika somo hili ,Mapema katika maisha yake
Bwana alipokuwa anakaribia mwisho wa Maisha ya kidunia aliuliza swali kama Hili
Watu husema kuwa mwana wa Adamu ni nani? Wanafunzi walijaribu kutoa maoni
mbalimbali kumhusu, wengine walisema Huyo ni Eliya, au Yohana mbatizaji
amefufuka kutoka kwa wafu au moja ya Manabii wa kale na kadhalika swali
liligeuka kwa wanafunzi wenyewe Je ninyi nanyi mwaninena mimi kama nani? Ni
Petro pekee aliweza kujibu Kuwa “wewe
ndiwe Kristo mwana wa Mungu aliye hai”na hata hivyo Yesu alimwambia Petro
kuwa Damu na nyama havikukufunulia hili Bali baba yangu aliye mbinguni, Kumbe
tunawezakuwa tumeokolewa,tumemtumikia Mungu na kutembea naye Lakini tukiwa bado
hatuja mfahamu, ndio hii inaonekana wazi pale wanafunzi wengine wanapokuwa
kimya na kushindwa kujibu swali lile na Hata huyu aliyejibu alijibu kwa msaada
wa Mungu hili lina tupa picha ya kwamba Kujibu kuwa Yesu Kristo ni nani sio
swala dogo na kumbe linahitaji Mwangaza maalumu kutoka kwa Mungu. Swali hili
linabakia kwetu leo na wanadamu wengi wanajaribu kulijibu Lakini jibu halisi
tunalipata kutoka katika Biblia hususani agano jipya ambalo limeandikwa na watu
waliomjua Vema na kwa msaada wa Roho Mtakatifu walihesabu mambo yote kuwa kama
mavi ili kumtumikia Kristo hawa walimuelewa Vema ni imani yangu kuwa Bwana
atampa neema kila mmoja wetu kuweza kujua Mungu na Kumjua Yesu Kristo kupitia
kozi hii sala hii ni Muhimu kabla ya kuendelea
“Eee
Nafsi yangu umfahamu Mungu wangu,Eee ngome yangu uufunulie moyo wangu ee Roho
wa Mungu wangu Uufunulie moyo wangu kwa damu yangu na kwa akili zangu siwezi
kumjua mwokozi wangu, lakini kwa kiu yangu Mungu ukajifunue kwangu nimjue mwana
wa Mungu wangu Yesu Kristo mwokozi wangu wewe ndiwe kimbilio langu sikuzote
maishani mwangu jufunue moyoni mwangu ”
UFAHAMU
KUHUSU KRISTO (CHRISTOLOGY)
Neno
Christology lina asili ya Kiyunani na ni muunganiko wa Maneno mawili Christ
ambalo maana Yake Kristo na o logy au logos
ambalo maana yake ni Elimu au ufahamu kuhusu, kwa msingi huo basi
Christology maana yeke Ni Elimu kuhusu Kristo au ufahamu kuhusu Kristo katika
somo hili tunajifunza kwa undani kile ambacho Biblia inakifundisha kuhusu Yesu
Kristo kwa msingi huo tunajifunza kwa
undani na kwa mpangilio kuhusu utu wa Yesu Kristo Milele wakati uliopita ulioko
na kazi zake za wakati ujao somo hili litakusaidia wewe kama Mwanafunzi wa
Biblia kuweza kukanusha dhana zozote zisizo sahii kuhusu Kristo zitolewazo na
watu wenye kuipinga imani yetu , ndani ya somo kuna mambo mengi kuhusu Yesu na
tutayajifunza kwa makini ili kupata Ufunuo wa kimaandiko wa kutosha kuhusu
Kristo na kuitetea imani,tutamuona Yesu katika Agano la kale na kumfahamu
anavyozungumzwa katika agano jipya lakini kusudi la somo hasa ni Kujua kuwa
Maandiko yanasema nini kuhusu Yesu Kristo somo hili ni la kitheolojia zaidi
Theology ni Elimu kuhusu Mungu Theo ni Mungu o logy au logos ni Elimu au
ufahamu kwa msingi huo kwa kuwa Yesu ni Mungu si kitu rahisi sana kueleweka
kirahisi inahitajika neema maalumu ya kiungu ili kujua somo hili vizuri na ni
maombi yangu kuwa Mungu atatusaidia kumfahamu Bwana vema.
Somo
hili ni tofauti na somo la Maisha ya Yesu Kristo ambalo huzungumzia Yesu na
maisha yake na kazi zake kama zinavopatikana katika injili, ambapo utajifunza
mafundisho yake mifano n.k somo hili la ufahamu kuhusu Kristo lina lengo la
kumjua Kristo mwenyewe kuliko kuelezea alifanya nini? Kwa msingi huo tofauti ya
Masomo haya tunaweza kuiweka hivi
Life of Christ (Maisha ya Kristo)
tunajibiwa kuwa Yesu Kristo alifanya nini?
Christology (Ufahamu kuhusu
Kristo) tunajibiwa kuwa Yesu Kristo ni nani?
Mwanafunzi
atakapomaliza somo hili angalau awe na uwezo wa kufanya mambo ya msingi na ya
muhimu yafuatayo;-
1. Kujua kwa usahii na
kufundisha kwa usahii Yesu Kristo ni
nani na kupinga dhana potofu
2. Kujua mawazo ya wasomi mabimbali
na michango yao waliyochangia kuhusu Yesu Kristo
3. Kuweka uwiano wa ufahamu kuhusu
Kristo na Shughuli za wokovu na utatu wa Mungu katika imani yetu na mafundisho
ya kibiblia
4. Kutambua na kufundisha kwa ujasiri
maswala mengi kumhusu Yesu Kristo na kazi zake kuanzia agano la kale na mpaka
jipya
5. Kujua ukweli mbalimbali kuhusu
Kristo, kama Kuzaliwa kwake na Bikira na faida zake, Kuteseka kufa na kufufuka
na uhusiano wake na mpango wa Mungu
6. Kufundisha ukweli wa kibiblia
kuhusu uungu wa Yesu na ubinadamu wake kupitia incarnation yaani tendo la Mungu
kuutwaa mwili wa kibinadamu
7. Kufahamu vema na kwa undani na
kufurahia tendo la Kristo kuutwaa mwili na kuwako duniani na faida
zilizopatikana kwa matendo yake kufa na kufufuka kwake
8. Kutumia mafundisho sahii na
mahubiri sahii tunapomzungumzia Kristo katika huduma zetu
9. Kufundisha na kuhubiri kwa usahii
maana ya kurudi kwa Yesu mara ya pili na huduma yake ya baadaye ya kimbinguni
MITAZAMO MBALIMBALI KUHUSU
UFAHAMU KUHUSU KRISTO (CHRISTOLOGY)
Swala
kuhusu Yesu kristo lilichanganya wasomo wengi sana katika ulimwengu wa
kitheolojia na hivyo iko mitazamo mbalimbali ya kimafundisho kuhusu Yesu Kristo
ambayo ni muhimu kuipitia pia kabla ya kujifunza kuwa Yesu Kristo ni nani jamaa
hawa waliokuwako enzi hizo waliamini hivi kuhusu Yesu
Ebonites
Waebonait
Hili lilikuwa kundi la wakristo
wenye msimamo mkali wa kiyahudi (Extreme Judaizing Christianity) hawa
walifundisha kuwa ni mwana wa Mariamu na Yusufu na aliitimiza Sheria ya Musa kwa
ukamilifu kiasi kwamba Mungu alimchagua awe masihi na walikataa kabisa kuwa
yeye ni Mungu, hivyo pamoja na kukubali wazi kuwa alizaliwa na Bikira waliona
kuamini katika uungu wa Yesu ni kwenda kinyume kabisa na imani ya kuwa Mungu ni
mmoja tu (monotheism)
Gnosticism
Wanostiki
Hawa waliamini kuwa kila kitu
pamoja na mwili ni kiovu tu isipokuwa roho na kwa msingi huo basi Mungu hawezi
kukaa katika mwili na hivyo wao hudai kuwa Kristo alikuja juu ya mwili wa Yesu
wakati wa Ubatizo na kuondoka Muda Mfupi kabla ya Yesu kufia msalabani kwa
msingi huo imani hii ilienea sana wakati wa Nyakati za kanisa la kwanza na
hivyo mitume walipambana na mafundisho ya aina hii katika
Wakolosai,wathesalonike na 1Yohana na
ufunuo vinagusia Kuweko kwa mafundisho hayo 1Yohana 4;1-3 Wapenzi, msiamini kila roho,bali zijaribuni hizo
roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea
ulimwenguni. Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho
inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu. Lakini
kila roho ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu. Hii ndiyo roho ya mpinga
Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni.
Arians
Waariyani
Jamii hii ilitokana na mwana
theolojia maarufu wa karne ya nne aliyeitwa Arius wa Alexandria huko Misri Yeye
alikuja na hoja ya kuwa ingawa Yesu anaitwa Mungu au amepewa heshima ya kuitwa Mungu Hakuwa Mungu kwa asili wala hakuwa Mungu
tangu milele bali alikuwa mzaliwa wa kwanza aliumbwa kabla ya vitu vingine
Ufunuo 3;14c “… Mwanzo wa kuumba kwa Mungu” kwa hivyo yeye alikuwa wa kwanza
kuumbwa na alishiriki kazi ya uumbaji kwa hivyo Kristo hakuwa Mungu kamili wala
mwanadamu kamili Marko 13;32, Yohana 5;19,14;28 na 1Korotho 15;28 mistari hiyo
aliitumia kuunga mkono hoja zake imani hii ilipingwa vikali wakati wa baraza la
Nikea lililofanyika mwaka 325 na kuitangaza imani hii kuwa potofu
Nestorians
Wanestori
Mwana theolojia huyu alikataa
dhana ya kuwa na asili mbili na kudai kuwa haiwezekani uungu na ubinadamu kukaa
katika hali moja inawezekana je mtu akawa Mungu na huku akawa mwanadamu? Dhana
hii haikuingia kichwani mwake
Apollinarians
Waapolonari
Mafundisho ya huyu bwana yalikuwa
na lengo la kuharibu kabisa ubinadamu wa Yesu Kristo kwa kweli Baraza la
Constantinople lililofanyika mwaka 381 AD lilihukumu mawazo ya waapolonari na
kuyatangaza kuwa ni mafundisho potofu
Eutychians
Waeutiko
Jamaa hawa walipinga hali ya
Kuweko kwa asili mbili za Yesu na kudai kuwa kulikuwa na asili moja tu na hivyo
Yesu alikuwa Mungu tu na hata alipokuwa katika mwili, mwili wake ulikuwa Mungu
dhana hii ilikuja kupingwa vikali na baraza la Chalcedon mwaka wa 451 na
kulihukumu fundisho hilo kuwa ni potofu
Mawazo
ya wa Orthodox
Waorthodox maana yake wenye imani
sahii hawa walifundisha kuwa Yesu Kristo ni mmoja bali ana namna mbili za asili
Ni Binadamu kamili na ni Mungu kamili hii iliungwa mkono katika baraza la Chalcedon
mwaka wa 451 AD wakiliwekea msimamo mkali hata leo
Mambo
kama haya yanatupelekea sisi kuwa tayari kujifunza kwa makini habari kuhusu Yesu
Kristo ili tuweze kuelewa vema kile ambacho Biblia inakisema kumhusu jambo hili
litatusaidia kumjua vema Kristo na siri hii ya ajabu kumhusu
SURA
YA KWANZA; KUWEKO KWA YESU KRISTO KABLA YA ULIMWENGU
Yesu Kristo ni
nani?
Yesu
Kristo ni muungano wa majina mawili Yesu Kristo. Jina Yesu ni jina lenye asili
ya kiyunani ambalo kwa asili limetokana na jina la Kiebrania Yoshua ['Wv¢/hy“ , [~'vŸu/hy“, au WvyE, ambalo maana yake Yahweh
anaokoa, jina linalobebwa na moja ya Viongozi maarufu katika agano la kale
Yoshua, hili lilikuwa jina la kawaida miongoni mwa majina ya kiebrania na
nyakati za ulimwengu wa agano jipya na
ili kulitofautisha na majina hayo ya kawaida Jina YESU KRISTO lilitumika na
wakati mwingine lilijumuishwa na eneo alilokulia Nazareth na ndio maana angalau
katika mistari ya Mwanzo ya vitabu vya injili jina hili liliwekwa na ingawa
hawarudii kila wakati ndani ya vitabu hivyo lakini kule kuliweka mwanzoni
ilimaanisha kuwa ni Yesu yupi wanaye mzungu mzia Mathayo 1;1,Marko 1;1 na 9 kuonyesha
kuwa wanamzungumzia Yesu Kristo wa Nazareth, Ingawaje si kila wakati
watayaunganisha majina hayo yote sehemu nyingine jina Yesu pekee hutumika
lakini katika msisitizo wa mistari ile ya msingi katika kitabu cha Matendo ya
mitume wanalitumia jina hilo kwa kuchanganya
Katika Mathayo 1; 21 Uthamani wa jina la Yesu unaonekana kuwekewa
wazi zaidi kwanza si jina ambalo lilichaguliwa na mwanadamu ni jina ambalo
Mungu mwenyewe alimchagua lakini linaonekana linatoka katika mzizi uleule wa
maswala ya wokovu “Maana yeye ndiye atakayewaokoa watu watu wake na dhambi zao”
na ni baadaye baada ya kazi ya ukombozi wa Msalabani ndipo dhana ya jina hili
ilifahamika wazi zaidi
Kwa habari ya jina linguine Kristo hili ni la muhimu kwani ndilo
linalo mtofautisha Yesu na wanadamu wengine wanaotumia jina hilo. Kuna makristo
wengi wa uongo lakini yuko Yesu Kristo mmoja tu wa kweli jina hili
linawakilisha jina la kiebrania Masihi j'yvim;,
ambalo maana yake ni mpakwa mafuta lakini limekuja kutumika zaidi kwa Mpakwa
mafuta mmoja tu ambaye alikuja kwa ajili ya kuutimiza unabii katika agano jipya
kwa msingi huo jina hili linapounganishwa Yesu Kristo ndipo tunapopata maswala
mengi ya kitheolojia ya kujifunza kumuhusu Yesu Kristo, kwa hivyo hatupaswi
kufikiri tu kuhusu Historia ya Yesu Kristo bali na kweli zinazobebwa na msingi
katika jina hilo.
Asili ya Yesu Kristo
Swali letu bado linabaki palepale kuwa Yesu Kristo ni nani
kumbuka kuwa hapo juu tulikuwa tunafafanua maana ya Jina Yesu Kristo lakini ili
tumfahamu Bwana Yesu inatupasa kujua majina yake jinsi anavyojulikana na
kutumika lakini lazima tujue asili yake
Kristo Yesu Kuweko kabla ya
ulimwengu kuumbwa
Yesu Kristo aliishi duniani takribani
miaka 2000 hivi iliyopita lakini kwa asili alikuwako kabla ya ulimwengu kuwako
kimsingi Yeye hakuwa mwanadamu wa kawaida au nabii tu au kama mtumishi yeyote
wa Mungu yeye ni zaidi ya kawaida hivi leo Yesu Kristo anawafuasi wengi zaidi
kuliko kiongozi yeyote duniani na hutajwa mara milioni kwa siku tu habari zake
zimeandikwa katika Vitabu vingi vinavyoelezea Maisha au Matendo yake kuliko mtu awaye yote duniani, amehubiriwa
katika mamilioni ya jumbe amenukuliwa na Viongozi, wasomi, wasio wasomi,
wanasayansi.wana historia na vyombo vingi vya habari kuliko mtu yeyote zaidi ya
yote mafundisho yake Yamebadili maisha ya watu wengi kwa karne nyingi na jina
lake limetumika kuponya na kufanya miujiza mingi zaidi na ni mwenye sifa nyingi
zaidi kuliko mtu awaye yote duniani
Kwa
msingi huo basi ni muhimu sana kujua habari zake kwa kina na mapana na marefu
na kwa utafiti wa kibiblia au kitheolojia unaonyesha maisha ya Kristo hayakuanzia duniani mara
baada ya Kuzaliwa na Mariam bali inaonekana kuwa alikuwako katika ulimwengu wa
roho kabla ya kudhihirika ulimwenguni humu na kujulikana na watu hata leo
·
Yohana 8;56-58 “…. Wayahudi
wakamwambia, “Wewe hujatimiza hata miaka hamsini, Wewe wasema umemwona
Abrahamu?’’ Yesu akawaambia, ‘‘Amin, amin, nawaambia, kabla Abrahamu
hajakuwako, ‘Mimi niko. Hii ni kauli ya Yesu Kristo mwenyewe akijitambulisha
kuwa alikuwako kabla ya Ibrahimu jambo hili ni moja ya misingi inayoonyesha
kuwa Kuzaliwa kwake haukuwa ndio Mwanzo wa maisha yake.
·
Yesu
Kristo alikuwako Tangu milele, milele ni muda mrefu usio na Mwanzo wala mwisho,
malaika,wanyama ,pepo na kadhalika ni viumbe tu
na viliumbwa na Mungu na havina sifa ya kuwako tangu milele mwenye sifa
ya kuwako tangu milele ni Mungu peke yake, tunawezaje kulijua hili Biblia
inatufundisha katika Yohana 1;1,14 “Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno
alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 14Neno alifanyika
mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi takauona utukufu Wake, utukufu kama wa Mwana
pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.Ushahidi huu mwingine wa kimaandiko
unathibitisha ya kuwa Yesu alikuwako tangu milele
·
Wakolosai 1;15-18 Kristo anaelezwa kuwa
amekuwako kabla ya vitu vyote kuwako ni wazi kuwa si tu kuwa Yesu aliumba vitu
vyote na kuwa kila kilichoumbwa kiliumbwa kwa ajili yake lakini amekuwako kabla
ya vitu vyote naye ndiye Mwanzo ni wazi tu kwamba kuja kwake duniani na kuutwaa
mwili kulikuwa kwa ajili ya kusudi linguine la ukombozi wa mwanadamu lakini
Yesu alikuwa ana asili ya Uungu
·
Wafilipi
2;5-8
“ Iuweni na nia ile ile
aliyokuwa nayo Kristo Yesu. Yeye ingawa alikuwa sawa na Mungu, hakuona kule
kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho, bali alijifanya si kitu,
akajifanya sawa na mtumwa, akazaliwa katika umbo la mwanadamu. Naye akiwa na
umbo la mwanadamu, alijinyenyekeza hata mauti, naam, mauti ya msalaba! Andiko
hili linasaidia kuweka wazi habari za Kristo kwamba yeye alikuwa sana na Mungu
na alikuja duniani katika mfumo wa Kuzaliwa tu na alijinyenyekeza sana
·
Hakuna
andiko lolote linalothibitisha kuwa Yesu ni kiumbe au aliumbwa hapana Kwa kweli
hana Mwanzo wa siku zake wala mwisho wa siku zake Waebrania 7;3 “Hana
Baba wala mama, hana ukoo, hana mwanzo wala mwisho wa siku zake, kama Mwana wa
Mungu, yeye adumu kuhani milele.na Waebrania 13;8 inasema Yesu Kristo ni Yeye
yule jana, leo na hata milele. Unaweza kuona pia Ufunuo 1;8,17-18 maandiko
yanathibitisha kuwa Yesu ni wa milele
·
Penginepo
inaweza kuonekana kana kwamba labda waandishi tunataka kumfagilia Yesu na
kumtukuza sna kuliko anavyopaswa kutukuzwa na hivyo tunampa sifa hii lakini
Yesu mwenyewe anasema Maneno haya katika Yohana 17; 4-5 “Mimi nimekutukuza
Duniani hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye, Na sasa Baba unitukuze
mimi pamoja nawe kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu
kuwako. Unaona! hii ni wazi katika
Maandiko kuwa Yesu alikuwako kabla ya ulimwengu kuwako alikuwako tangu milele
·
Nabii
Mika aliyeishi miaka 750 hivi kabla ya Kristo ni moja ya Manabii waliotabiri
mji atakaozaliwa masihi kuwa ni Bethelehemu lakini pamoja na hayo anaonyesha
kuwa mtawala huyo ana asili ya milele Mika 5;2 “Lakini wewe, Bethlehemu Efrata,
ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda, kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu
yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli, ambaye asili yake ni kutoka zamani,
kutoka milele.’’
·
Yohana
mbatizaji amabaye ni Nabii aliyetangulia kumuelezea Kristo au kumtambulisha
Kristo kwa dunia alieleza kuwa asili ya Kristo sio Duniani ni juu Yohana 3;31 “Yeye
ajaye kutoka juu yu juu ya yote, yeye aliye wa dunia asili yake ni ya dunia,
naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye
kutoka mbinguni, yu juu ya yote.” Sio tu yuko juu ya Yote lakini ametoka
mbinguni.
Majina
aliyopewa Yesu Kristo alipokuwa Duniani
Ni muhimu kufahamu kuwa Swali yesu
Kristo ni nani halitoshi kujibiwa tu na kwamba alikuwako kabla ya ulimwengu
kuwako kwani hii inaweza kuwachanganya wanadamu lakini namna watu
walivyomueleza na majina anavyopewa au aliyopewa akiwa duniani na heshima
anazopewa katika Maandiko ni msaada mkubwa katika kulijibu swali Yesu ni nani?
1. Yesu anaitwa mwana wa Mungu
Wako watu ambao
wanakubali kuwa Yesu ni moja ya mitume wa Mungu lakini wanakataa kuwa si mwana
wa Mungu, Mashahidi wa Yehova wanaamini kuwa Yesu ni mtu mkuu zaidi aliyepata
kuishi lakini wanakataa kuwa yeye ni Mungu huku wakiamini kuwa amepewa heshima
ya kuwa juu ya malaika na kuwa chini au msaidizi wa Mungu lakini sio Mungu.
Kila mtu anaweza kuwa na jibu lake
kuhusu Yesu lakini Biblia pekee inayo majibu sahii kuwa Yesu ni nani nasi
tutaiangalia Biblia kuwa inatuambia nini?
Yesu Kristo kama mwana wa Mungu Neno mwana wa
linamaanisha asili kama ni Mwana damu maana yake ni aliyezaliwa na mwanadamu na
Mwana wa Mungu maana yake aliyezaliwa kutokana na Mungu, Yesu anapoitwa mwana
wa Mungu maana yake ana asili ya Mungu wala yeye haitwi mwana wa Mungu katika
dhana ile ya mwana wa Mungu kama inayotajwa kwa malaikaAyubu 2;1 ,Adamu.Israel
na wanadamu wa kawaida Yeye anatajwa kama mwana wa Mungu katika namna ya pekee
sana
·
Malaika
huitwa wana wa Mungu (Created sons of God) Ayubu 1,;6,2;1-3,8;7,Zaburi 89;7,Daniel3;25)
wana wa mungu kwa kuumbwa
·
Adamu
aliitwa mwana wa Mungu Luka 3;38 (Created son of God) kwa kuumbwa
·
Wakristo
huitwa wana wa Mungu Yohana 1;12,Warumi 3;14,19,9;26 (adopted sons of God)
·
Wana
wa Israel wanaoitwa wana wa Mungu (Elected sons of God) kwa kuchaguliwa
·
Yesu
anaitwa mwana Pekee wa Mungu Yohana 1;1, 3;16,Matahyo3;17,17;5 (Monogyny means
of the same nature) yaani wa asili moja
na Mungu kwa msingi huo Yesu alipojitambulisha kwa kumuita Mungu baba yake
wayahudi walielewa Yesu alikuwa akimaanisha ana asili moja na Mungu au yuko
sawa na Mungu Yohana 5;17-18 “Yesu akawajibu,
“Baba yangu anafanya kazi yake daima hata siku hii ya leo, nami pia ninafanya
kazi. Maneno haya yaliwaudhi sana viongozi wa Wayahudi. Wakajaribu kila njia
wapate jinsi ya kumwua, kwani si kwamba alivunja Sabato tu, bali alikuwa
akimwita Mungu Baba Yake, hivyo kujifanya sawa na Mungu.ni Muhimu pia kufahamu
kuwa katika ulimwengu wa tawala za kifalme kama mtawala mranyingi hufuata ukoo
na hivyo mtoto wa kifalme Prince huwa na heshima sawa na ile ya Mfalme kwa
msingi huo Kristo ni mwana wa kifalme He is the Prince
Yesu
anasema nini kwa habari ya nafsi yake?
Akiwa kijana mdogo tu hivi mwenye umri kati ya miaka 12 Yesu
alikuwa na ufahamu wa kutosha kujihusu kwanza alijitambua kama Mwana wa Mungu
kwa kumuita Baba yangu Luka 2; 49 Yesu akawaambia, “Kwa nini
kunitafuta? Hamkujua kwamba imenipasa kuwa katika nyumba ya Baba Yangu?” hii ni
wazi kuwa mapema sana alitambua kuwa Yeye ni mwana wa Mungu aliwezaje kujua
jambo kama hili mapema sana katika umri mdogo kama huo? Hii inabaki kuwa siri
kwetu
Alipokuwa akibatizwa katika mto wa
Yordani Yesu aliisikia sauti ya Baba yake ikithibitisha Mbele ya watu kuwa Yeye
ni mwana wake mpedwa anayependezwa naye Mathayo 3; 17 “Nayo
sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ambaye ninapendezwa
sana naye.’’
Mapema kabisa Shetani alipokuwa
akimjaribu Yesu kule Jangwani alitambua kuwa Yesu alikuwa mwana wa Mungu
Mathayo 4; 3 “Mjaribu akamjia
na kumwambia, “Kama Wewe ndiye Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.’’
Yesu alimsifia Petro kuwa
aliweza kumtambua kuwa yeye ni mwana wa Mungu kwa kuwezeshwa na Mungu baada ya
Petro kwa uweza wa Mungu kugundua kuwa Yesu alikuwa ni mwana wa Mungu Mathayo
16;15-17 “Akawauliza,
‘‘Je, ninyi, mnasema mimi ni nani?’’Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye
hai.’’ Naye Yesu akamwambia, ‘‘Heri wewe, Simoni mwana wa Yona, kwa maana hili
halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni. Usemi huu
wa Kristo unathibitisha kuwa yeye mwenyewe alijitambua kuwa ni mwana wa Mungu.
Jambo linguine la kushangaza
kabisa lilijitokeza Pale Yesu alipokuwa hukumuni mbele ya kuhani mkuu ambapo
angeweza kuepuka hukumu ya kifo kama tu angekubali kuwa Yeye sio mwana wa Mungu
lakini akiulizwa kwa kuapishwa aseme kama kweli yeye ni mwana wa Mungu Hivi
ndivyo ilivyokuwa Mathayo 26;62 - 65 “Kisha Kuhani Mkuu akasimama na kumwambia
Yesu, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi wa namna gani hawa watu wauletao dhidi
yako?” Lakini Yesu alikuwa kimya. Ndipo Kuhani Mkuu akamwambia, “Nakuapisha
mbele za Mungu aliye hai, tuambie ikiwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.”
Yesu akajibu,“Wewe umenena. Lakini ninawaambia nyote, Tangu sasa mtamwona Mwana
wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu na akija juu ya
mawingu ya mbinguni.’’
Semi
za Yesu zinazomweka katika ngazi ya uungu au mwana wa Mungu
·
Alieleza
wazi kuwa anatenda kazi kama baba yake wa Mbinguni Yohana 16;28
·
Alieleza
kuwa ametumwa na baba yake Yohana 20;21
·
Alikiri
kuwa ana ushirika na Mungu Mathayo 11;27 Yohana 17;25
·
Alikiri
kuwa amekuja kumfunua Baba aliye ndani
yake Yohana 14;9-11
·
Alionyesha
ya kuwa yuko mahali kote Mathayo 18;20
·
Alionyesha
mamlaka ya kusamehe dhambi marko 2;5-10
·
Alionyesha
ya kuwa ana mamlaka ya kuhukumu na kuamua mwisho wa mwanadamu Yohana
5;22,Mathayo 25;31-46
·
Alionyesha
kuwa anahitajika kupendwa zaidi kuliko chochote sawa na Mungu Mathayo
10;37,luka 14;25-33
Hizi
nisemi za Yesu mwenyewe zinazodhihirisha kuwa yeye ni mwana au Mungu Kwa msingi
huo hatumsingizii Yesu kuwa ni mwanqa wa Mungu yeye mwenyewe amethibitisha mara
kadha na kwa msingi huo basi ni muhimu kufahamu kuwa yesu alikuwa ni mwana wa
pekee wa Mungu na kwakuwa hakuwahi kutenda dhambi hakuwa na sababu ya
kutuongopea
Jinsi mamlaka
aliyokuwa nayo inavyomtambulisha
Katika
mafundisho yake Bwana Yesu hautaweza
kuona Maneno yenye mashaka kama “kwa maoni yangu” au “inawezekana” au “nafikiri…”n.k wayahudi wenyewe
waliomsikia walisema alizungumza kwa
mamlaka ya kuonyesha ndiye Mungu mwenyewe hili lilidhihirika kwa wazi kabisa
kwa mfano katika hutubva yake ya mlimani na neno la Mungu alilolifundisha
aliweka wazi kabisa kuwa lilikuwa neno lake pia matumizi ya Neno amini
nawaambieni Mathayo 7;24,Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na
kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba.na
Mathayo 7;28-29 “ Yesu alipomaliza kusema maneno haya, makutano ya watu
wakashangazwa sana na mafundisho yake, kwa sababu alifundisha kama yeye aliye
na mamlaka, wala si kama walimu wao wa sheria.Mathayo 6;38-39 Mmesikia kwamba
ilinenwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ Lakini mimi nawaambia,
msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume,
mgeuzie na la pili pia, semi hizi zenye mamlaka ambazo ni tofauti hata na za manabii
waliosema asema Bwana wa majeshi zinadhihirisha kuwa Kristo alikuwa na mamlaka
ya kiungu
Maisha yake ya
kutokutenda dhambi.
Hakuna
mwalimu yeyote aliyeweza au anayeweza kuwaambia watu watubu na kuishi maisha ya
haki anayeweza kuepuka kuwa hana dhambi au mapungufu katika wanadamu wote Yakobo
3;1-2Sisi sote tunajikwaa katika mambo mengi. Ikiwa mtu ye yote hakosei kamwe
katika yale anayosema, yeye ni mkamilifu, naye anaweza kuuzuia pia na mwili
wake wote. ni Yesu pekee ambaye aliishi bila kufanya
dhambi na kwa Maneno na kwa Matendo yeye pekee alikuwa na ujuzi wa ndani sana
kuhusu ubaya wa dhambi wakla dhambi haijawahi kuukaribia hata moyo wake na kwa
ujasiri kabisa huku akiwa mnyenyekevu aliwauliza wayahudi kuwa ni nani
anishuhudiaye kuwa nina dhambi? Yohana 8;46 “Je, kuna ye yote miongoni mwenu
awezaye kunithibitisha kuwa nina dhambi? Kama nawaambia yaliyo kweli, mbona
hamniamini? Kwa msingi huo hakuna mwanadamu aliye mkamilifu ila Mungu peke yake
na hivyo kwa uwezo wa Yesu kuishi duniani Bila kufanya dhambi ni utambulisho
ulio wazi kuwa Yeye alikuwa na asili tofauti na kibinadamu.
Ushuhuda wa
wanafunzi wake
Wayahudi
hawajawahi kufanya makosa ya kufikiri hata siku moja kuwa Musa ni mwana wa
Mungu na wala wanafunzi wa Yesu hawakuwahi kufikiri kubatiza watu kwa jina la
Baba na Musa na Roho Mtakatifu sawa na Matahayo 28;19 na sababu kubwa ni kwamba
Musa hajawahi kusema kuwa yeye ana ushirika na Mungu au ametoka kwa Mungu,
Badala yake wanafunzi wa Yesu walumuhubiri Yesu walifanmya miujiza kwa jina
lake na walimuabudu wao walikuwa na uelewa tofauti na jamii nyingine za watu
·
Walimuhusisha
na kazi ya Uumbaji na hivyo Yesu ni Muumba Yohanma 1;1;3
·
Thomasi
alimuabudu na kutamka Maneno Bwana wangu na Mungu wangu Yohana 20;28
·
Petro
ambaye alikula naye na kutembea naye katika mitaa mbalimbali ya Israel alieleza wazi kuwa Yesu yuko mkono wa Kuume
wa Mungu Matedno 2;33,36 na ya kuwa huyu ndio njia ya pekee ya wokovu Matendo
4;12 ndiye anayesamehe dhambi Matendo
5;31 na ndiye atakayehukumu wafu Matendo 10;42 na alimuabudu katika waraka wake
kwa kumpa yeye utukufu hata milele 1Petro 3;18
·
Hatuna
habari kuwa Paulo aliwahi kumuona Yesu katika mwili ingawa amewahi kumuona
baada ya ufufuko wake akiwa ametukuzwa lakini katika namna ya kushangaza Paulo
ambaye alikuwa na wivu kwa ajili ya Mungu tangu utoto wake alimtambua Yesu kama
Mungu mkuu Tito 2;13 “Tukilitazamia tumaini lenye Baraka na mafunuo ya utukufu
wa Kristo Yesu,Mungu mkuu na mwokozi wetu;anamtambua kama ukamilifu wote wa
Mungu wakolosai 2;9 muumba wa vitu vyote wakolosai 1;17 na kulijumuisha jina
lake katika Maombi 1Koritho 1;2 na Matendo 7;59 na kuyatumia majina ya Baba na
Roho pamoja na la Bwana Yesu katika salamu za neema
·
Nyakati
za kanisa la kwanza hakuikuwa na ubishi kuwa Yesu ni Mungu na wakristo wote
walimuabudu na waandioshi wa kipagani wa karne ya kwanza waliandika hivi kuwa
wakristo wanamuabudu kiongozi mkubwa sana aliyesulubiwa huko Israel na wengine walisema wanaimab wimbo wa kumopa
sifa Yesu kama wanampa Mungu kwa hiyo wapagani walijua kuwa watu wa karne ya
kwanza walimuabudu Bwana Yesu
·
Wanafunzi
wa Yesu walikuwa wayahudi na ndio waliotuletea habari za Kristo kumbuka ni
ngumu sana kwa myahudi aliyejifunza sheria Tangu utoto kuabudu miungu au kumpa
mtu sifa ya Mungu kwa msingi huo sisi tumepokea habari hizi njema kutoka kwao
na wokovu watoka kwa wayahudi Yohana 4;22“Ninyi (Wasamaria) mnaabudu
msichokijua. Sisi (Wayahudi) tunamwabudu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu
unatoka kwa Wayahudi.
·
Imani
ya Nikea mababa walipokuwa wakitengeneza ukiri wa imani yetu waliemndelea
kumuheshimu Yesu kama Mungu “Twamwamini Yesu Kristo mwana wa pekee wa Mungu
mwana wa azli wa baba,wenye uungu moja na Baba,mwana wa azli asiyeuumbwa,Mungu
kutoka katika Mungu Nuru kutoka katika Nuru …..”
2.
Yesu anaitwa Neno la Mungu
Mwana
damu anapozungumza Maneno ndipo anapoweza kujiweka wazi mwenyewe ama kueleweka
anapowasiliana na wengine na kwa Maneno anaweka wazi hisia zake na mawazo yake
kujulikana na anatoa amri na kuonyesha mapenzi yake na hivyo tunaweza kumjua au
kumfahamu na kujua nguvu zake uwezo wake wa ufahamu na matakwa yake. Mungu naye
amejifunua kwetu kupitia mwana wake Waebrania 1;1-3 kwa msingi huo yeye ni neno
la Mungu na mtu akijiuliza swali Mungu yukoje jibu ni kuwa yuko kama Kristo
Yeye ni neno ni wazo la Mungu Yeye ni mng’ao wa utukufu wa Mungu asiyeonekana
3.
Yesu ni Bwana
Jina
hili Bwana ni moja ya majina yanayotumika kuweka wazi kuwa Yesu Kristo ni
Mungu, ametukuka na ni mtawala wa Ulimwengu wote Jina Bwana linapotumika Kabla
ya jina husika huwa linawakilisha dhana ya uungu hii ilikuwa wazi kwa wayahudi
na wayunani,Jina Bwana kwa kiyunani ni “Kurios”
ambalo hutumika sawa na Yehova katika tafasiri ya kiyunani ya agano la kale kwa
msingu huo kwa wayahudi unaposema “Bwana Yesu” ilikuwa wazi kwamaba huyo ni
Mungu, sote tunakumbuka kuwa mtawala wa kirumi Kaisari alipotawala alitaka pia
kuabudiwa alitaka kuitwa Bwana Kaisari
ambalo ni sawa na kusema kuwa Kaisari ni Bwana na mataifa walielewa madai ya
Mtawala huyo na kwa sababu hizi wakristo waliteswa sana kwa sababu hawakutaka
kumtambua Kaisari kuwa ni Bwana Badala ya Yesu
·
Jina
Bwana katikaagano la kale Septuagint lilitumika kumaanisha mambo makuu matatu
a.
Bwana
maana yake kuwa sawa na Mungu Yehova
b.
Mrithi
wa Mungu adonai
c.
Heshima
ya kibinadamu inayotolewa kwa Mungu Yoshua 3;11,Zaburi 97;5
·
Katika
agano jipya tunaona maana zinazo fanana na hizo zikielekezwa kwa Yesu
a.
katika
hali ya heshima kubwa na unyenyekevu mkuu Mathayo 8;2,,20;33
b.
katika
kuonyesha mamlaka na nguvu za kitawala Mathayo 21;3,24;42
c.
Katika
mamlaka iliyo kuu sawa na Mungu Marko 12;36-37,Luka 2;11,3;4,Filipi
2;111Koritho 12;3.
4.
Yesu ni mwana wa Adamu.
Kwa
mujibu wa matumizi ya Maneno ya kiebrania: “Neno mwana wa” huwa linahusu
uhusiano au ushiriki mfano wana wa
Ufalme Mayhayo 8;12 ni wale wanaoshiriki katika kweli na Baraka za ufalme wa
Mungu au washirika wa ufalme wa Mungu, au neno Mwana wa Amani Luka 10;6 maana
yake mwenye kuonyesha ushiriki au kumiliki Amani, au neno mwana mpotevu Yohana
17;12 Ni mwenye kushiriki au kushirikiana na upotevu, Kwa msingu huo Kristo
anapoitwa mwana wa adamu maana yake ni mwenye kusushiriki ubinadamu,au mwenye
kuushiriki udhaifu wa wanadamu wasio na msaada Neno hili lilitunmiwa na Mungu
sana karibu mara “80” katika Ezekiel kuonyesha udhaifu wa Ezekiel aliyekuwa mwanadamu
Hesabu 23;19,Ayubu 16;21,25;6 Linapotumika kwa Yesu Kristo lina maana ya mwenye
kuushiriki Ubinadamu kwa ubora,Yesu alipotumia jina hili mwana wa adamu yaani
mwanadamu angeweza kuleta hoja kuwa ndio tunajua kuwa wewe ni mwanadamu sasa
kuna haja gani tena ya wewe kutangaza kuwa u mwanadamu? Hivyo katika midomo ya
Yesu hii ilikuwa ina maana ya Mwenye asili ya Mbinguni au uungu anashiriki Ubinadamu
na hii inakamilisha ule unabii Mungu pamoja nasi Mathayo 1;23, Kwa msingi huo
jina hili linatumika kuonyesha maswala kadhaa kumhusu Yesu Duniani
·
Linaonyesha
maisha ya Kristo duniani Marko 2;10
·
Linaonyesha
kuwa ni mwana wa Mungu pia ni mwana wa adamu anashiriki uungu na ana shiriki
ubinadamu
·
Yohana
5;17-18 Kwa msingi huo Mtu aliposema kuwa Yeye ni mwana wa Mungu maana yake
anashiriki uungu na hivyo yuko sawa na Mungu Maandiko hayakanushi kuwa Yesu ni
Mungu Wafilipi 2;5-7
·
Baadhi
ya wanatheolojia walijaribu kufikiri kuwa neno mwana wa pekee “Monogyny” ni kuwa labada aliumbwa lakini neno hili
maana yeke mwenye asili moja na Mungu Yohana 1;14,18kuitwa kwake mwana wa adamu
kunakuja tu kwa sababu
1.
Alishiriki
ubinadamu kwa Kuzaliwa hapa duniani Mathayo 2;1-2,1;21,Yohana 18;37
2.
Alifufuka
toka kwa wafu Matendo 13;33
·
Muhubiri
mashuhuri John Wesley anachangia vizuri
wazo lake juu ya Matendo 13;33 ambayo yanaleta msaada wa kitheolojia anasema
Yesu aliitwa mwana wa Mungu tangu milele hivyo hakuwa mwana wa Mungu baada ya
kufufuka wala hakujiita mwana wa Mungu baada ya kufufuka hata katika eneo
ambalo Paulo anaeleza hivyo Warumi 1;4 Yesu ni wa aina moja na Mungu Baba tangu
milele
·
Wasomi
wengine wanahoji kwanini Yesu anaitwa mzaliwa wa Kwanza kama ni Mungu?
Ni kweli kuwa watu wengi
wamefikiri na kudhani kuwa Yesu aliumbwa kwa sababu ya neno mzaliwa wa kwanza
kutumika kwake kwa hivyo ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote Mashahidi wa
Yehova wanaamini kuwa Yesu ndio kiumbe wa kwanza kuumbwa na Mungu kisha
akashirikishwa katika uumbaji na Mungu mwenyewe, ni muhimu kufahamu kuwa kwa
wayahudi Neno mzaliwa wa kwanza halikumaanisha kuwa alizaliwa au kuumbwa kwanza
kabla ya viumbe vingine Neno mzaliwa wa kwanza linapotumika kwa wayahudi
humaanisha Heshima kubwa au heshima maalumu kuliko wengine Neno mzaliwa wa
Kwanza katika kiyunani ni “Prototokos”
Prototokos ambalo maana yake ni “Wa kwanza
katika cheo” kwa msingi huo kwa Waebrania mzaliwa wa kwanza ni cheo na kinaweza
kuhama kutoka kwa mkubwa na kwenda kwa mdogo kwa mfano Esau na Yakobo Esau
alikuwa mzaliwa wa kwanza lakini aliokiuza cheo hicho kwa Yakobo na haki ya
mzaliwa wa kwanza ikampata Yakobo
5.
Yesu ni Kristo
Yesu pia anaitwa Kristo Neno
Kristo maana yake mwenye kutiwa mafuta ili awe kuhani, au nabii au mfalme na
hujitokeza mara ya kwanza kwa ufafanuzi katika
1Samuel 2;10 na mafafanuzi chini ya Biblia ya Kiswahili Neno hilo Kristo
kwa kiebrania ni Masihi au mpakwa mafuta
kwa msingi huo mtu alipochaguliwa na Mungu kufanya kazi fulani kati ya
hizo alitiwa mafuta kama ishara ya Kuchaguliwa na Mungu na hivyo mtu huyo
angekuwa anamwakilisha Mungu katika ngazi aliyowekwa ,kupakwa mafuta
kuliambatana na hali halisi ya kiroho ili kwamba mpakwa mafuta huyo awe mpakwa
mafuta halisi katika kuishi kwake,2Samuel 1;14 1Samuel 10;1,6,16;13.Kwa hivyo
anapopewa Yesu Kristo ambaye ndiye masihi mkuu ni kwa ajili ya kumwakilisha
Mungu na kufanya kazi Ya nabii, mafalme na kuhani wa kipekee sana kwani wote
waliopakwa mafuta kwa ngazi hizo walikuwa na mapungufu Yesu alitabiriwa maalumu
kama masihi halisi na ndio maana jina Kristo kwa Yesu ni maalumu sana Isaya
11;1-3,61;1 Yeye kama mwana wa Daudi pia wakati huo huo anagekuwa mwana wa
Mungu akiwa na sifa za Mungu Isaya 9;6-7,Yeremia 23;6 na tofauti na Daudi yeye
utawala wake ni wa milele na wa ulimwengu mzima na yeye ndiye tumainai la
Israel
Nyakati za Agano la kale mtu
alipochaguliwa kushika wadhifa wa viti vile vyenye kutiwa mafuta aliwekwa
mafuta hayo kama kuteuliwa au kutawazwa rasmi kuwa mfalme mpaka mafuta
alitakiwa kutangaza wazi sababu za kumpaka mafuta mtu huyo Yesu alitangazwa
wazi pale Yordani kuwa mwana wa Mungu 1Samuel 10;1 Marko 1;11, 9;7,Luka 3;22
6.
Yesu ni mwana wa Daudi
Yesu Kristo kuitwa mwana wa Daudi
haina tofauti na ile ya kuitwa Masihi hii ni kwa sababu masihi alittabiriwa
kuwa mwana wa Daudi ni kwa sababu ya uaminifu wa Daudi mungu alimuahidi kuwa
atampa kiti cha ufalme milele au hatakosa mtu wa kutawala katika kiti chake cha
enzi milele 2Samuel 7;16 kwa hivyo hilo lilikuwa agano la milele la Mungu kwa
Daudi na kwa msingi huo tangu wakati huo watu walikuwa wakitazamia kutokea kwa
kiongozi wa aina hiyo si hivyo tu bali manabii pia walikuwa wakiwakumbusha watu
juu ya ujio wa kiongozi wa jinsi hiyo ambaye ni mwana wa Daudi ambaye atakuwa mfalme mkuu Yeremia
30;9,23;5Ezekiel 34;23,Isaya 55;3-4,Zaburi 89;34-37, Isaya 11;1
KRISTO YESU NDANI YA AGANO
LA KALE.
Kwa kuwa tunakubali kuwa Yesu
alikuwako tangu milele na pia kabla ya uumbaji ni muhimu kufahamu kuwa
alihusika kutenda kazi ndani ya agano la kale katika namna iliyofichika
Indirect katika namna isiyokuwa ya kawaida alijulikana kama malaika wa Bwana Hii
ni kwa sababu zifuatazo
·
Wengi
tunafahamu kuwa malaika hawakubali kuabudiwa au kusujudiwa na hii iko wazi hata kama malaika huyo ni
malaika mkuu Ufunuo 19;10,22;8-9 kwa kawaida heshima ya kuabudiwa hupelekwa kwa
Mungu tu na kwa msingi huo malaika wanajua kuwa heshima ya kuabudiwa na
kusujudiwa ni heshima ya Mungu pekee na katika utii na unyenyekevu walio
nao wao hawakubali kuipokea ibada hata
kidogo
·
Malaika
wa Bwana anayetajwa katika agano la kale
na ambaye ameonekana kuipokea ibada ana sifa zifananazo na zile za
Kristo
Anaitwa
Mungu wa Ibarahimu Isaka na Yakobo kutoka 3;2-6
Huapa
kwa nafsi yake Mwanzo 16;7
Huongea
kwa mamlaka kamili kama Mungu Waamuzi 2;1
Ana
uwezo wa kusamehe au kutokusamehe dhambi na jina la Mungu liko ndani yake
Kutoka 23;20-23
Anakubali
kusujudiwa na ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Bwana Yoshua 5;13-15
Ana
uwezo wa kubariki na walipomuona walimuona kama Mungu Mwanzo 32;30,48-16
Hajaumbwa
na ana sifa nyingine nyingi.
·
Ni
kwa sababu hizo wanatheolojia wengi wameshindwa kuepuka kuhitimisha kwa kusema
kuwa huenda malaika huyu ni Masihi mwana wa Mungu na mwokozi wa ulimwengu na
hivyo huitimisha kwa kusema huyu ni Yesu Kristo mwenyewe akiwa kazini nyakati
za Agano la kale kabla ya Kuzaliwa duniani maalumu (Incarnation) kwa hivyo hii
ni wazi kuwa Yesu alikuwa akafanya kazi katika agano la kale katika namna hii
na kwa Ufunuo mdogo aliokuwa nao Nebukadreza kumhusu Masihi mwana wa Mungu Yeye
alisema huyu ni mafano wa mwana wa Miungu Daniel 3;22-25 Kama Mungu Kristo
alitenda kazi na Mungu baba yake Bega kwa bega Mwalimu wa somo hili Mchungaji
Innocent Kamote anahitimisha kwa kuwasaidia wanafunzi kugundua utendaji wa
utatu kwa migawanyo ya kazi zao kwa Mukhutasari huu kwamba popote pale
utakapoona kazi hizi zinafanyika basi moja ya nafsi ya Mungu inahusika sana na
swala hilo japokuwa wote hufanya kazi pamoja lakini hizi huwatambulisha zaidi
Kazi
ya Mipango na majira au Muda ni kazi
ya Mungu Baba
Kazi
ya ukombozi na wokovu Shughuli
zozote zinazo husiana na ukombozi au wokovu na uponyaji ni kazi za Mungu Mwana
Yesu Kristo
Kazi
zozote zinazohusiana na maongozi au
kuweka Viongozi au kuongoza ni kazi za Roho Mtakatifu
Aidha
ndani ya agano la kale Kristo sasa anapewa majina ambayo yanadhiohirisha kazi
nzima ya ukombozi aliyokuwa akiifanya kwa mfano sasa kila utakapoona kazi za
ukombozi zikifanyika zinafunua utendaji wa Yesu Kristo ulio wazi katika agano
la kale chukulia sasa mfano jina
Yehova
Biblia ya kiingereza ya KJV inatafasiri
jina hilo Yehova kama Bwana na Adonai Jina
Bwana lilitumika Badala ya jina Yehova {JHVH} kwa sababu
wayahudi waliliheshimu sana jina hili na kuogopa hata kulitaja sasa
unapofuatilia kwa makini jina Hili Yehova utagundua kuwa halina tofauti na kazi
atakazo zifanya Kristo mwenyewe katika ulimwengu wa agano jipya angalia kwa
mfano katika unabii wa Zekaria 12;1-10
“Hili
ni neno la BWANA kuhusu Israeli. BWANA, Yeye azitandaye mbingu, awekaye misingi
ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake, asema: ‘‘Nitakwenda kufanya
Yerusalemu kuwa kikombe cha kulewalewa kwa mataifa yote yanayoizunguka. Yuda
utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia.Katika siku hiyo, wakati mataifa yote ya
dunia yatakapokusanyika dhidi yake, nitaufanya Yerusalemu kuwa jabali
lisilosogezwa kwa mataifa yote. Wote watakaojaribu kulisogeza watajiumiza
wenyewe. Katika siku hiyo nitampiga kila farasi kwa hofu ya ghafula, naye
ampandaye kwa uenda wazimu,’’ asema BWANA. Kisha viongozi wa Yuda watasema
mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa sababu BWANA Mwenye Nguvu ni
Mungu wao.’ “Katika siku hiyo nitawafanya viongozi wa Yuda kuwa kama kigae cha
moto ndani ya lundo la kuni, kama mwenge uwakao kati ya miganda. Watateketeza
kulia na kushoto mataifa yote yanayowazunguka, lakini Yerusalemu utabaki salama
mahali pake. “BWANA atayaokoa makao ya Yuda kwanza, ili heshima ya nyumba ya
Daudi na wakazi wa Yerusalemu isiwe kubwa zaidi kuliko ile ya Yuda. Katika siku
hiyo, BWANA atawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba aliye dhaifu kupita
wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama
Malaika wa BWANA akiwatangulia. Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote
yatakayoushambulia Yerusalemu. “Nami nitamiminia roho ya neema na maombi juu ya
nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma,
nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika
kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.” Kwa msingi
huo Zekaria anatumia neno Bwana ambalo ni mbadala wa Yehova lakini kazi hii
kinabii ni ya Yesu kwa msingi huo utaona kuwa kazi za ukombozi ni za Yesu na
jina la Yehova hutumika pamoja na shughuli za wokovu au ukombozi.
Elohim
Jina Elohim limetumika
mara nyingi sana katika agano la kale kiasi kuwa baadhi ya wasomi hulitafasiri
maana yake ni Mwenye nguvu au wa kuogopwa jina hili kwa asili ni jina linalowakilisha
wingi kwa msingi huo wasomi huamini kuwa jina hili lilikuwa likihusisha utatu
mzima wa Mungu hata ingawaje jina hilo hutumiwa
wakati mwingine kama kumaanisha maana moja
Adonai
Adonai ni jina
lililotumika kwa Mungu ambalo lilitafasiriwa pia kama Bwana katika agano la
kale kuonyehs ubwana wake au uwezo wake wa kiutawala, kumiliki na pia
linatumika kuonyesha mabwana wa kibinadamu
Muonekano wa Yesu Kristo katika agano la kale
(Theophany)
Muonekano wa Yesu Kristo
katika agano la kale katika matedno fulani ya muda mfupi kitheolojia unaitwa Theophany
katika hali kama hizi Yesu alijitokeza kama malaika wa Bwana laki tofauti na malaika wengine malaika huyu
alikuwa akikubali ibada neno malaika
maana yake ni mjumbe malaika wa Bwana pia Ni malaika wa Yehova huyu alitokea
katika Matukio kadhaa na akakubali kuabudiwa
Alimtokea Musa kutoka 3
Aliwatembelea Israel kutoka 19
Musa na Haruni na Nadabu na wakuu sabini wa wana wa Israel walimuona
katika namna ya kibinadamu Kutoka
24;9-11,kutoka 33;17-33
Alitambuklika kama malaika wa bwana au wa Mungu Mwanzo 16;13,Kutoka
3;2,5-7
Alimtokea hajiri Mwanzo 16;7-13
Sehemu nyingine katika agano la kale malaika huyu anakotokea ni pamoja
na Mwanzo 22;11-18, 24;7, 40, 31;11,32;24-32, 48;15-16, Hosea12;4, Kutoka
3;2.13, 21, 14;19, 23;20-23, 32;34,33;2, Hesabu 20;16,22,22-35, Waamuzi
2;1-4,5;23,6;11,13;3-23, Samuel 14;17-20, Muhubiri 5;6, Isaya 37,63, Zekaria
1;9,2;3,3;1-10,4;1-7,5;5-10,6;4-5,12;8.
Aidha ni muhimu kukumbuka kuwa Yesu Kristo anatajwa kama mwokozi katika
agano la kale wanatheolojia hutimia
unabii wa Maandiko kama Ayubu 19;25 na Mwanzo 3;15 na maeneo mengi
yanayohusiana na kazi za ukombozi kuonyesha Yesu kuwa ni mwokozi kupitia agano
la kale Yeye anaonekana kama Mowkozi kwa umoja,kwa watu binafsi na kwa siku
zijazo.
KRISTO
YESU KATIKA ALAMA VIVULI TYPOLOGY
Typology
ni Elimu inayohusu Picha au kiwakilishi au mfano au kivuli cha kitu fulani halisi
kitakachokuja kwa lugha za kinabii hii inahusisha tukio la uhakika la
kihistoria linaloweza kusimamia kama mfano wa kweli fulani za kiroho kwa msingi
huu ndani ya agano la kale kuna mifano zaidi ya 50 hivi inayomwakilisha Kristo
au iliyokuwa ikitoa Picha ya uhalisi wa Yesu Kristo katika uhalisia wa kutimiza
unabii huo Mifano hii inaweza kujumuisha watu, Matukio,vitu,sherehe za kidini, ibada
na kadhalika
Umuhimu
wa typology
·
Zinatusaidia
kuelewa kwani uhalisi kuwa kazi ya ukombozi na wokovu halikuwa swala lililozuka
tu bali lilikuwa katika mpango wa mMngu.
·
Zinatusaidia
sana katika kuelewa kazi ya Kristo ya wokovu na kutupa picha iliyo wazi ya sifa
zake,kazi na tabia
·
Zinatusaidia
katika kuwasilisha kweli za kibiblia kwa mafundisho au mahubiri kumuhusu Yesu
Kristo
·
Zinawakilisha
kweli halisi zijazo kumuhusu Kristo.
Mifano
ya watu Typical Person
o
Adamu
- ni kiongozi wa uumbaji wa kwanza wenye anguko, Yesu ni kiongozi wa
utii unaoleta utu mpya Mwanzo 2;7,1Koritho
o
Habili –mchungaji wa kweli aliyetoa
dhabihu ya damu yenye kukubalika na Mungu
katika utii
o
Haruni - aliwekwa na Mungu kuwa kuhani
Waebrania 5;4 kama Kristo Waebrania 8;6
o
Musa – alichaguliwa kufanya kazi ya
ukombozi kutoka 3;7-10;Matendo 7;25 wote walikataliwa na ndugu zao kutoka
2;11-15 Yohana 1;11Matendo 7;23-28;18;5-6
o
Malkizedeki- Kuhani mkuu wa Mungu Mwanzo
14,Zaburi 110;4 Kristo ni kuhani mkuu milele kwa mfano wa Melkizedeki maana ya
jina hilo ni uhalisia wa jina na tabia za Kristo na ukuhani wao ulitoka nje ya
kabila ya Lawi Waebrania 5;6,6;20,7;12,21
o
Boazi Kinsman redeemer- Kinsman
redeemer maana yake ni Mkombozi ambaye kwa mujibu wa agano la kale na tamaduni
za wakati ule kama mtu alifiwa na mume na mume alikuwa na ndugu ndugu huyo
aliyekaribu alitakiwa kufanya kazi ya ukombozi ya kumkomboa na kumuoa Mwanamke
aliyeachwa hali ya ujane ili kumuinulia nduguye uzao Walawi 25;48-49,Ruthu 3;12
Waebrania 2;14-15 Kristo alifanyika kwa njia ya kufanyika mwanadamu na
kutukomboa na kulipa gharama Walawi 25-27, Warumi 3;24-26,1Petro
1;18-19,Wagalatia 3;13
o
Yoshua- jina lake maana yake Yohova
anaokoa ni jina sawa na la Yesu aliwapa raha ya kanaani Waisrael Yesu atatoa
raha ya mbinguni Waebrania 7;19-29
o
Yusufu- alisalitiwa na ndugu zake na
baadaye kuja kuwa mtawala wao Yesu alisalitiwa na wayahudi nduguze na baadaye
atakuja kuwa mtawala wao,walinyang’anywa mavazi Mwanzo 37;23,Mathayo
27;35,waliuzwa kwa Fedha Mwanzo 37;2814-15.
o
Isaka – wote ni wana wa pekee Yohana
3;16;Waebrania 11;17 maisha yote ya Isaka
yanaonyesha mfano ulio kamili
zaidi wa nafasi na kazi ya Kristo kuliko wote waliotangulia alibeba kuni
ili kutolewa sadaka juu ya kuni hizo, alibeba Msalaba ili kutolewa sadaka juu
ya Msalaba huo
o
Daudi – Mchungaji na mfalme Kristo
ndiye Mchungaji mwema kwa mamlaka kama ya Daudi
o Benjamin kwa jina lake – majina yote
mawili ya Benjamin huonyesha mateso ya
Yesu Kristo na utukufu utakaofuata aliitwa jina Bennon yaani mwana wa huzuni
kutoka kwa mamaye Rahel na Yakobo alimpa jina Benjamin maana yake mwana wa
mkono wangu wa kuume
o Yona
– alikuwa tayari
kuyatoa maisha yake kwa ajili ya wengine, pia alikaa katika tumbo la nyangumi
kwa siku tatu na umisheni katika jamii ngeni
o Samsoni
– Alitiwa
mikononi mwa wenye dhambi na nduguze, hakuheshimika, lakini aliheshimika baada
ya kufa alikufa akiwa ametanua mikono yake katika Nguzo mbili
o Esta
– alikuwa Tayari
kufa kwa ajili ya taifa lake, alijitoa sadaka kwa mfalme ili awakomboe ndugu
zake
o Abrahamu
– rafiki wa
Mungu Isaya 41;8 na Mathayo 17;5
Mifano
ya vitu Typical things
o Kondoo aliyechukua nafasi ya
Isaka – Mwanzo 22;13,Isaya 53;6,1Korithians 15;3
o Ngazi aliyoiona Yakobo Mwanzo
28;12, Yohana 14;6
o Manna Kutoka 16;14,15,Yohana
6;31-63
o Mwamba wa Herobu kutoka
17;6,1Koritho 10;4 na Yohana 7;37-39
o Hema ya kukutania Kutoka 40;33,34,Kolosai
2;9
o Sanduku la agano Kutoka
25;16,Zaburi 40;7,8,Yohana 15;10,Luka 22;20
o Kiti cha rehema Kutoka
25;21,22,Warumi 3;25,Waebrania 4;16
o Pazia la hema na hekalu Kutoka
40;21,2Nyakati 3;14 Waebrania 10;9,-10
o Madhabahu ya kufukizia uvumba ya
dhahabu kutoka 40;26,27 Waebrania 13;15
o Meza ya mikate ya wonyesho Kutoka
25;23-30 Yohana 6;48
o Taa ya vinara saba kutoka
25;31,Yohana 8;12
o Madhabahu ya shaba Kutoka
27;1-2Waebrania 13;10
o Nyoka wa shaba Hesabu 21;9 Yohana 3;14,15
o Miji ya makimbilio Hesabu 35;6 Waebrania
6;18
Mifano
ya sikukuu typical feast
o Malimbuko Walawi 23;10-11
1Koritho 15;20
o Sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi
na jioni Kutoka 29;38-39 Yohana 1;29
o Siku ya upatanishi walawi
16;15-34,Waebrania 9;11-13
o Sadaka ya dhambi walawi 14;6,7
waebrania 13;11-13
o Sadaka ya amani walawi 3;1-2
Efeso 2;14-18
o Pasaka 1Koritho 5;7 1Petro
1;15-19
Mifano
ya kimatukio typical events
o Kuvikwa vazi kwa Adamu na
Hawa Mwanzo 3;21
o Nuhu kuhifadhiwa katika safina
2Petro 2;5,9
o Ukombozi wa wana wa Israel kutoka
Misri kielelezo cha kazi ya ukombozi wa Kristo
o Kuingia kanaani ni mfano
kielelezo cha kuingia mbinguni halisi itakavyokua
KRISTO
YESU KATIKA UNABII WA AGANO LA KALE
Yesu
Kristo alitabiriwa katika maisha Shughuli kazi na utendaji wa aina mbalimbali
kuhusu maisha yake katika agano la kale hata kabla ya Kuzaliwa kwake yako
maeneo mengi yaliyotabiriwa kumhusu masihi Yesu jambo hili ndilo lililopelekea
wayahudi kuwa na mtazamo wa kumtazamia masihi Yesu Kristo
Unabii kuhusu
Mtangulizi wa masihi
Masihi
alitabiriwa kutanguliwa na mtangulizi na ambaye angepiga kelele nyikani kuwa
watu watengeneze njia huyu alikuwa Yohana mbatizaji na unabii ulitimizwa
Ø Isaya 40;3-5 Luka 3;2-6 Isaya
40;9-10 Mathayo 3;1-3
Ø Malaki 3;1,Malaki 4;5 Marko
1;2-3,Luka 7;24-27Mathayo 11 ;10,13-14 Luka 1;17
Ø Ezekiel 29;21 Luka 1;68-69,76-79
Unabii kuhusu ukoo
wa masihi na Nafsi ya Masihi
Ø Ni uzao wa mwanamke Mwanzo
3;15,Galatia 4;4
Ø Ni mwana wa Daudi Mathayo
1;1,Yohana 7;42
Ø Amekuwako tangu milele Mika 5;2
Ø Ni Mungu mwenye nguvu Isaya 9;6-7
Unabii kuhusu
Kuzaliwa kwake
Ø Atazaliwa Bethelehemu Mika
5;2,Mathayo 2;1-6
Ø Kuzaliwa na Bikira Isaya 7;14
Ø Ndiye atakaye miliki Mwanzo 49;10
Ø Ni Mtawala aliyepakwa mafuta
Daniel 9; 25
Unabii kupakwa
kwake mafuta
Ø Utawala wake ni wa milele na
milele Zaburi 102;25-27,Waebrania 1;8-12
Ø Roho wa Bwana atakuwa juu yake
Isaya 61 ; 1-3 Luka 4;16-21,Yohana 3;34
Ø Ni chipukizi katika shina la Yese
Roho atakua juu yake Isaya 11;1-4, 42;1.Luka 3;21-22,
Unabii kuhusu
huduma yake
Ø Kiongozi toka miongoni mwao
Yeremia 30;21,Marko 6;1-4
Ø Huduma atakayoifanya Isaya 61;1-4,Mathayo 4;17,Marko
1;14-15,Luka 4;17-21
Ø Miji itakayofaidika na huduma ya
masihi Luka 9;1-2,Mathayo 4;12-17
Ø Kufundisha kwake kwa mifano
Zaburi 78;2-4, Mathayo 13;34-35
Ø Kushangiliwa na wanafunzi na watu
na watoto Zaburi 8;2, Mathayo 21;15
Ø Kufukuza watu Hekaluni wivu wa
Bwana Zaburi 69;9,119;139 Yohana 2;13-17
Unabii kuhusu kifo
chake
Ø Nitampiga Mchungaji wa kondoo na
kondoo watatawanyika Zekaria 13;7, Yohana 10;11,15
Ø Kuinuliwa kwake msalabani Yohana
3;14,12;32
Ø Mateso yake, kujitoa kwake kwa
ajili yetu, kuchukua dhambi zetu kupatwa na adhabu itakayoleta amani yetu Isaya
53.Zaburi 22
Ø Masihi kukatiliwa mbali Daniel
9;26
Unabii kuhusu
kufufuka kwake
Ø Nafsi yake haitaachwa kuzimu,
Zaburi 16;8-10
Ø Nafsi yake haitaachwa kaburini, Zaburi
30; 3, 41;10
Ø Nafsi yake haitaachwa katika
nguvu za kaburi Zaburi 49;15
Unabii kuhusu kupaa
kwake
Ø Kukaa kwake mkono wa kuume wa
Mungu Zaburi 16;10-11
Ø Kupaa kwake juu na kutoa vipawa
Zaburi 68;18
Unabii kuhusu
Ufalme wake
Ø Utakua ufalme wa amani Isaya
9;6-7,
Ø Utakua ufalme wa milele 2Samuel
7;16-17,Luka 1;32-33
Ø Fimbo ya ufalme haitaondoka
katika Yuda Mwanzo 49;10 Ufunuo 19;15-16
Ø Adui zake wote watawekwa chini ya
miguu yake Zaburi 110;1 Matendo 2;34-35
Ø Atalijenga hekalu la Bwana Zekaria
6;12,9;9-10
Ø Ufalme wake hautaondoshwa Daniel
7;14
SURA
YA PILI; YESU KRISTO KATIKA MWILI WA KIBINADAMU
KRISTO YESU
KUUTWAA MWILI
Kristo Yesu kuwa
katika mwili wa kibinadamu tendo hili kitheolojia huitwa Incarnation dhana hii imekuja kutokana na ukweli kuwa
ukiichunguza injili kweli hii inadhihirika wazi kuwa Yesu alikuwa Mungu na
aliamua kuchukua asili ya kibinadamu ili kwamba apate kuwakomboa wanadamu huku
alipokuwa mwanadamu hakuutumia uwezo wake wa kiungu bali aliishi kama mwanadamu
wa kawaida Tendo la kiumbe cha kiroho
kuutwaa mwili wa kibinadamu huitwa Incarnation kwa msingi huo basi Yesu
alikuwa Mungu kamili na Mwanadamu kamili tendo hili linaungika mkono kama
sehemu ya utatu wa Mungu kwamba nafsi moja ya Mungu ilichukua umbile la
kibinadamu kwa ajili ya kutimiza Makusudi fulani maalumu neno akafanyika mwili
Mathayo 1;20, Luka 1;35, Yohana 1;13-14, Matendo2;30, Warumi 8;3, Wagalatia 4;4,
Wafilipi 2;7
Swala hili katika karne ya kumi na tisa
katikati lilichukua sura mpya ya aina mpya ya ufahamu kuhusu Kristo na kuundwa
kwa fundisho maalumu lililoitwa Doctrine of Kenosis au kenotic Theory
fundisho hili lilipata kibali miongoni mwa jamii ya kilutheri na baadhi ya
waprotestant na hivyo kulileta kanisa
pamoja mwanzilishi wa fundisho hili au mgunduzi wa fundisho hili aliitendea
haki nafsi ya Yesu kuwa Ni mwanadamu halisi na pia ni Mungu halisi isipokuwa
Yesu alijinyenyekeza na kujitoa sadaka kuwa mwanadamu
Neno kenosis hutumika
katika maana kuu mbili ya kwanza ni self limitation yaani hii ni
hali ya kujiwekea mipaka kujidhili au kujishusha na kujiondoa katika uhalisia
na kuweka kando tabia za kiungu na kutumia uanadamu wake hali hii Ina
faida kwetu kama zinavoonekana chini.
Faida za Yesu kuutwaa mwili wa kibinadamu
Incarnation?
- Alimshinda
yeye aliyekuwa na nguvu za mauti shetani.na kuziharibu kazi zake 1Yohana 3;8;Waebrania
2;14
- Alizuhubiri
roho zilizokuwa kifungoni (1Petro 3;18-19), neno linalotumika katika Petro
kuhusu kuzihubiri roho zilizokuwa kifungoni katika biblia ya kiyunani ni “Kerussen” ambalo maana yake ni
kutangaza announce na sio
kuhubiri kule tunakofikiri au tulikozoea.
- Kwa
kuuvaa mwili amefaa kuwa kuhani mkuu mwenye rehema na mwaminifu katika
mambo ya Mungu (Waebrania 2;17-18).Yeye anawajua wanadamu na anamjua Mungu
hivyo yu afaa kuwa kuhani mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu.kwa kuwa anawajua wote kwa
asili
- Alijaribiwa
sawa na sisi katika mambo yoote bila kufanya dhambi na kwa sababu ya
ukamilifu wake tunaweza kuyategemea maombi yake, msaada wake na tunapata
ujasiri wa kumuendea maana anatujua vizuri,mara nyingi tumewaeleza
wanadamu shida zetu na hisia zetu na wakaishia kutuumiza zaidi kuhani
anayefaa zaidi na mtu wa kumueleza shida zetu na hisia zetu ni Yesu Kristo
pekee yake.
- Aliweza kuzichukua dhambi za
wanadamu na kufanya upatanishi kwa Mungu na kumfanya awe hakimu wa haki
utawahukumuje wanadamu huku wewe hujawahi kuonja uanadamu?
- Aliweza kufanya matayarisho ya
kuja kwake mara ya pili Waebrania 9;28
Ubinadamu wa Yesu Kristo
1.
Kuzaliwa kupitia kwa Bikira.
Unapozungumzia Yesu kama mwana wa
Adamu yaani Mungu anayeshiriki ubinadamu lazima kwanza utafikiri juu ya
Kuzaliwa kwake na Bikira.maandiko yanafundisha kuwa Yesu alizaliwa kwa Muujiza
katika tumbo la Mariamu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu wala sikwa uwezo wa
kibinadamu Mathayo 1; 18, 20, 24-25 Luka 1; 35, 3; 23 ni nini maana ya tukio
hili la Yesu kuizaliwa na Bikira kuna mafundisho makuu kama matatu tuyapatayo
kupitia Tendo la Yesu Kuzaliwa kwa njia hii
1.
Kuonyesha
kuwa Wokovu unatokana na Mungu mwenyewe kama Mungu alivyoahidi kupitia uzao wa
mwanamke Mwanzo 3;15.Wokovu ni matokeo ya kazi ya Mungu na sio ya wanadamu ni
kwa miujiza wa kiungu ndipo tunapata wokovu kwa msingi huo tendo hili ni wazi
kabisa kuwa kazi ya ukombozi ni juhudi ya Mungu kwa hivyo alizaliwa chini ya sheria ili
awaokoe wale walio chini ya sheria na kufanywa wana wa Mungu Wagalatia 4;4-5
2.
Kunaonyesha
Muungano sasa wa asili ya uungu na asili ya ubinadamu na hii ndio maana neno
Mungu alimtumia mwana wake hutumika Yohana 3;16,Wagalatia 4;4 Hapa ndipo Yesu
alichukua Ubinadamu na ili aje ulimwenguni kama mwanadamu na ingekuwa ni vigumu
kwetu kuamini kuwa Yesu ni mwanadamu kamili kama angelikuja moja kwa moja
kutoka Mbinguni na sio hivyo tu bali ilibidi achukue asili ya Adamu na pia
ingekuwa ni vigumu ketu kuamini kuwa Yesu ametoka kwa Mungu kama kwa upande
mwingine angeruhusu Yesu Kuzaliwa na wazazi wa kibinadamu wawili kwa msingi huo
kwa kuwa wokovu ni kazi kamili ya Mungu ilibidi asili mbili ziungane kwa hivyo
tunampata Yesu Mwanadamu kamili na Mungu kamili kwa msingi huo Mungu katika
Hekima yake aliamua kufanya hivi hivyo tunaamini Yesu alikuwa Mungu kwa sababu
kutungwa kwake katika tumbo la Mariam ni kazi ya Roho Mtakatifu na Kuzaliwa
kwake na mariam kunatupa uhakika kuwa ni mwanadamu
3.
Kitendo
hiki pia ndicho kinachomfanya Yesu Kristo kama mwanadamu kamili pia lakini
asiye na dhambi, wanadamu wote wana asili ya Dhambi na tuna hatia na hatuko
sawa kimaadili kwa sababu ya Baba yetu wa kwanza Adamu Kwa msingi huo kwa kuwa
kua na ukweli kuhusu Yesu kutokuwa na baba wa kidunia kuna mfanya Bwana Yesu asiwe na asili kama
ile tuliyo nayo sisi ya dhambi na hii ndio maana Yesu huitwa mwana wa Mungu
Luka 1;35 kwa msingi huo miujiza huu unamfanya Yesu asiwe na asili ya dhambi ya
Adamu huku akiwa mwanadamu na kwa kule kuwa mwana wa Mariam Yesu hakuweza
kuchukua asili ya dhambi kwa sababu Roho wa Mungu aliingilia kati Kuzaliwa kwa
Kristo na pia kulinda asili ya ubinadamu ya dhambi ndani ya Mariamu isiweze
kuleta athari kwa Yesu Kristo rejea Luka 1;35
2.
Udhaifu wa kibinadamu na Mipaka
ya kibinadamu
a.
Yesu
alikuwa na mwili wa kibinadamu. Ukweli kuwa Yesu alikuwa na mwili wa kibinadamu
kama tulio nao sisi unaonekana katika
Maandiko yenyewe ,
·
Alizaliwa
kama wanadamu wengine yaani kwa miezi kamili tisa tumboni Luka 2;6-7,
·
Alikuwa
na kuongezeka katika kimo Luka 2;40
·
Alikua
kiakili yaani katika Hekima, kimo na
maadili na yaani akiwapendeza Mungu na wanadamu Luka 2;52
·
Wakati
mwingine alichoka kama wanadamu wengine
Yohana 4;6
·
Aliona
kiu kama watu wengine Yohana 19;28
·
Alisikia
njaa na kutamani kula Mathayo 4;2
·
Alikuwa
dhaifu baada ya kufunga kwa siku kadhaa Mathayo 4;11
·
Alichoka
Baada ya kupigwa mijeledi na hatimaye kushindwa kuubeba nsalaba na kuhitaji
kusaididwa Luka 23;46
·
Alikufa
kama wanadamu wengine wawezavyo kufa pale msalabani Yesu alikufa Luka 23;46
·
Alikuwa
na mifupa na majeraha baada ya kufufuka kuonyesha alikuwa mwanadamu Luka 24;39
·
Walimpa
samaki wa kuo9kwa na alikula mbele yao Luka 24;42,30,Yohana 20;17,20,27,21;9,13.
·
Kisha
Bwana Yesu alipaa kwenda mbuinguni huku wakimshuhudia Matendo 1;9
Mistari yoote hiyo hapo juu
inatuthibitishia kuwa Yesu alikuwa na mwili wa Kibinadamu na hivyo alikuwa
mwanadamu kamili akiwa na nyama na mifupa na ule ukweli kuwa alipaa mbinguni
akiwa na mwili huu wa kibinadamu ni wazi kuwa Yesu ameendelea kuwa na mwili wa
kibinadamu hata huko mbinguni mwili huu haukubadilika hata baada ya kufufuka isipokuwa
ulikuwa katika hali ya kutokuharibika tena na kuwa mwili wa kimilele ambao ni
mortal
b.
Yesu
alikuwa na akili za kibinadamu. Ukweli kuwa Yesu alikuwa katika kimo na Hekima unatuthibitishia
kuwa alikuwa na akili za kibinadamu Luka 2;52, alijifunza kama wanadamu wengine
Luka 2;46,alijifunza kula,kutembea.kusoma na kuandika na kuwatii wazazi Waebrania
5;8 hali hizi zote za kujifunza zilikuwa ni za kibinadamu na akiwa na akiliza
kibinadamu kama wanadamu wengine hakuweza kujua siku atakayo rudi duniani mara
ya pili Marko 13;32
c.
Yesu
alikuwa na Nafsi ya kibinadamu na hisia za kibinadamu, tunaona dalili nyingi za
kuonyesha kuwa Yesu alikuwa na Nafsi au roho ya kibinadamu
·
Alifadhaika
rohoni Yohana 12;27
·
Alisikitikia
usaliti Yohana 13;21 neno la kiyunani kufadhaika linasomeka Tarasso
Tarasso Neno ambalo hutumika kwa wanadamu
wanapokuwa katika hali ya kuteseka au kufadhaishwa na kukabiliwa na hali ya
hatari.
·
Alisikia
huzuni kiasi cha kufa Mathayo 26;38
·
Alistaajabia
imani ya akida Mathayo 8;10
·
Alilia
wakati wa msiba wa Lazaro Yohana 11;35
·
Alimlilia
Mungu amtoe katika wafu Waebrania 5;7
Lakini
pamoja na haya yote hukufanya dhambi bali alijifuza kuwa mtii Waebrania 5;8-9
4;15 ukweli kuwa alijaribiwa sawa na sisi katika mambo yote ni wazi kuwa
alikuwa na Nafsi ya kibinadamu na hisia ya kibinadamu
d.
Watu
waliokuwa karibu naye walimuona kama mwanadamu wa kawaida Mathayo 4;23-25 Yesu
alifanya miujiza mingi sana lakini alipokuja kwao Nazarethi watu hawakumpokea kwani walimjua na kuona kuwa alikuwa mtu wa
kawaida Mathayo 13;53-58 maandiko haya yanafunua kuwa wale watu walipomuona
yesu majirani zake eneo alilokulia akitengeneza fanicha na ndugu zake
wakijulikana wao walimuona Yesu kuwa Binadamu wa kawaida
·
Walimuona
kama mwana wa Seremala Mathayo 13;55
·
Walimfahamu
yeye mwenyewe kama Seremala marko 6;3
·
Alikuwa
wa kawaida hata wakamuuliza amepata wapi haya Mathayo 13;56
·
Hata
ndugu zake walimuona wa kawaida kiasi cha kutomuamini Yohana 7;5
Kwamaaana hii Yesu alikuwa wa
kawaida kiasi kuwa wale walipomuona akikua katika yao kwa muda wa miaka 30
kabla ya kuanza huduma walimuona mtu wa kawaida mwema tu na sio vinginevyo
e.
Yesu
Kristo hakutenda dhambi
Ingwaje
mafundisho ya kibiblia pia huonyesha ya kuwa Yesu alikuwa mwanadamu wa kawaida
lakini yanatuhakikishia kuwa yeye hukufanya dhambi na hii ndio tofauti yake na
wanadamu wengine ni wazi kuwa wanadamu wote hutenda dhambi lakini sivyo ilivyo
kwa Yesu
·
Alikuwa
na Hekima na alimpendeza Mungu na wanadamu Luka 2;40
·
Shetani
alimshawishi ili atedne dhambi na alishindwa Luka 4;13
·
Wayahudi
walishindwa kushuhudia kuwa alitenda dhambi Yohana 8;46
·
Semi
zake zinathibitisha kuwa aliishi maisha ya ushindi alisema mimi ni Nuru ya
ulimwengu Yohana 8;12
·
Alighakikisha
kuwa wakato wote anafanya mapenzi ya baba yake Yohana 8;29
·
Alizishika
amri zote za baba yake Yohana 18;38
·
Aliitwa
mtakatifu mwenye haki Matendo 2;27,3;14,4;30,7;52,13;35
·
Mitume
walishuhudia kuwa asiyejua dhambi 2koritho 5;21
·
Mwandishi
wa kitabu cha Waebrania anasema kuwa yeye alijaribiwa katika mambo yote bila
kufanya dhambi Waebrania 4;15-16
·
Ni
kuhani mkuu aliye mtakatifu Waebrania 7;26
·
Ni
mwanakondoo asiye na waa 1Petro 1;19
·
Hukufanya
dhambi wala kunena uovu 1Petro 2;22
·
Ni
mwenye haki aliyekufa kwa ajili ya wasio haki 1Petro 3;18 1Yohana 2;1
·
Ndani
yake hakuna dhambi 1Yohana 3;5
Je
Yesu angeweza kutenda dhambi?
Kuna
mijadala ya kitheolojia kuhusu Yesu kama angeweza kutenda dhambi au la na hii
huzaa makundi maalumu mkauu mawili kundi la kwanza husema ndio Yesu asingeweza
kufanya dhambi na kundi jingine linasema kama asingeweza kutenda dhambi gasi
hakukuwa na sababu za kujaribiwa au majaribu yake hayakuwa majaribu ya kweli
utakijaribu vipi kitu amabacho unajua kuwa hakiwezi kufanya dhambi? katika
kulijibvu swala hili vema ni lazima kwanza kusema hivi
1. Maandiko yanaonyesha kuwa Yesu
hakutenda dhambi hii ieleweke hivyo kuwa hakutenda dhambi
2. Maandiko yanaonyesha wazi kuwa
kweli Yesu alijaribiwa na kuwa majaribu haya yalikuwa halisi kabisa Luka 4;2 na
kama tunayaamini maaandiko basi nilazima tukubali wazi kuwa majaribu ya Yesu
yalikuwa majaribu halisi na alijaribiwa kila eneo Waebrania 4;15 kwa hivyo
swala la kusema kuwa majaribu ya Yesu hayakuwa dhahiri ni wazi kuwa ni
hitimisho lisilo la kimaandiko na la uongo
3. Lazima pia tukubali wazi kuwa
Mungu hajaribiwi kwa uovu sawa na Yakobo 1;13 na kama hivyo ndivyo basi je
kwanini kama Yesu ni Mungu anajaribiwa?ndio Yesu ni Mungu lakini pia ni
mwanadamu na hakuna Maandiko yanayothibitisha kuwa Yesu hajaribiwi kwa uovu
kama yesu angekuwa na asili ya kibinadamu inayosuimama mpeke yake kama ile ya
adamu basi kulikuwa na uwezekano ulio halisi wa Yesu kufanya dhambi, lakini kwa
kuwa Yesu alikuwa na asili zote mbili kwa wakati huu basi uwezekano wa
kutotenda dhambi kwa Kristo ulikuweko na katika hali kama hii basi Yesu
angetenda dhambi basi pia ilikuwa ni wazi kuwa Mungu ametenda dhambi
4. Kwa msingi huu tunapo jiulize je
Yesu angeweza kutenda dhambi jibu ni moja tu hangeweza kutenda dhambi lakini
swali linaweza kubakia Je majaribu yake yalikuwa halisi
5. Jibu ni kuwa kama Yesu angekubali
kugeuza mawe kuwa mkate wote tunajua kuwa utendaji wa Yesu wa miujiza ulikuwa
ni sehemu yake ya kazi za kiungu hivyo angefanya hivyo basi angekuwa ameitumia
sehemu yake ya uungu na kukana ubinadamu na hivyo angekuwa ameanguka kama Adamu
tu
Umuhimu wa Yesu
kuwa mwanadamu
a. Kwa ajili ya kutufundisha utii
uliotimia
b. Kwa ajili ya kuwa sadaka halisi
ya ukombozi wa dhambi zetu
c. Ili awe mpatanishi kati ya Mungu
na wanadamu
d. Kutimiza kusudi la Mungu la asili
la mwanadamu kuutawala uumbaji
e. Kuwa mafano wa kuigwa wa maisha
ya mwanadamu
f. Kuwa sehemu ya miili yetu
itakayokombolewa
g. Ili kusudi aweze kuchukuliana
nasi kama kuhani mkuu
Yesu ataendelea
kuwa Mwanadamu?
Ni
muhimu kufahamu kuwa Yesu hakuacha kuwa mwadamu hata baada ya kufufuka katika
wafu alikuwa akiwatokea wanafunzi wake akiwa na alama za misumari kuonyesha
mwili wake uliojeruhiwa kwa kusulubiwa Yohana 20;25-27 alikuwa na mifupa na
nyama Luka 24;39 alikula chakula Luka 24;41-42 na hata baada ya kufufuka
alipokuwa akipaa Malaika waliahidi kuwa kama alivyopaa ndivyo
atakavyokujqa matedno 1;11 Stefano
alisisitiza kua alimuona ameketi mkono
wa kuume wa Mungu Matedno 7;56 alimtokea
Paulo huko dameski matedno 9;5 na alitokea wengine wengi kwa jinsi hiyo
Ikorotho 9;1 ,15;8 na katika Ufunuo Yohana anamuona kama mwana wa kuibinadamu
Ufunuo 1;13 pamoja na kuwa alikuwa amefunikwa na utukufu mwingi kiasi cha kumfanya Yohana kuanguka
kumsujudia Ufunuo 1;13-17 Yeye mwenyewe alihaidi kuwa siku moja atakula na
kunywa pamoja na wanafunzi wake katika ufalme wake Mathayo 26;29 Ufunuo 19;9
hii ni wazi kuwa Yesu ataendelea kuwa mungu mwanadamu milele.
MAISHA
YA YESU KRISTO DUNIANI
Hatutakuwa
tena na Muda wa kutosha kujadili kuhusu Kuzaliwa kwa masihi maana hilo
tumeligusa katika maeneo mengi ya kutosha katika eneo hili tutazungumzia zaidi wajibu alio kuwa nao au ofisi za Kristo
yesu alipokuwa duniani , Nyakati za agano la kale kulikuwa na ofisi kuu tatu
amabazo zilikuwa ni ofisi zenye kufanya kazi ya upatanishi kati uya Mungu na
wanadamu hawa wal;ikuwa wafalme makuhani na amanabii Yesu kama Mpatanishi
mkamilifu nawa pekee alikuwa na ofisi hizo zote tatu kwa wakati moja (1Timotheo
2;5) Yeye alikuwa nabii, Kuhani na mafalme na alitimiza nyadhifa hizo katika
maisha yake duniani kwa namna hii tunayoichambua chini
Kristo Yesu kama
Nabii
Yesu
Kristo kama Nabii ni wazi kuwa Manabii katika agano la akle waliifanya kazi ya
kumwakilisha Mungu na kusema kwa niaba ya Mungu
wakifunua mapenzi yake kwa wakati uliopo na wa baadaye nao walitabiri
wazi kuwa Masihi pia atakuwa nabii mkuu mwenye kusubiriwa kwa hamu na Israel wote Isaya 42;1 na Warumi 15;8 na ndivyo Yesu
alivyochukuliwa katika injili Marko 6;15,Yohana 4;14,9;17marko 6;4 1;27 kote
huku anachukuliwa kama nabii Yesu kama Nabii alifanya mambo ya msingi yafuatayo
a.
Alihubiri wokovu mara nyingi katika Israel
ilipotokea kuwa Viongozi wa kisiasa na makuhani na wengine wamefikia mahali pa
kushindwa kujua nini cha kukifanya Ndipo nabii hutokea na kuonyesha njia kuwa
hili ndilo jamabo la kufanya au kufuata Yesu alikuja katika wakati kama huo
watu wakiwa katika hali ya kukosa amani na kutokujua nini cha kukifanya na kuwaonyesha njia aidha wale waliokataa njia na kutaka kufanya
mapinduzi kwa njia zao Yesu alikwisha kuwaonya kama nabii kuwa nini kingewapata
Luka 19;41-44 na Mathayo 26;52 mwaka wa 70 Ad. Hivi walijaribu kujitafutia
uhuru tofauti na ujumbe wa Kristo na hivyo damu nyingi ilimwagika na matokeo
yake walitawanywa duniani
b.
Yesu alitangaza ufalme wa Mungu Manabii wote waliopita walikuwa
wakiwakumbusha watu yaliyo wajibu wao kwa sheria za Mungu hii ina maana ya
kujitia katika utawala wa Mungu yaani ufalme wake Yesu alihubiri watu watubu kwa kuwa ufalme wa
Mungu umekaribia Mathayo 4;17 na alimtumia muda mwingi kufafanua namna ufalme
huo unavyofanya kazi
c.
Alitabiri mambo yajayo Unabii hautegemeani na kanuni za
kakwaida za kihistoria wenyewe unakwenda kutokana na mpango wa Mungu kwani yeye
anajua mwisho kabla ya Mwanzo Mathayo 24-25 ni mfano wa Matukio ya kinabii
amabayo Yesu alitabiri na pia anaendelea na kazi hii ya unabii hata baada ya
kupaa kwake kupitia mwili wake yaani kanisa Yohana 14;26;16;13 hii hainja maana
kuwa wakristo wanapaswa kuongezea katika Maandiko ya kinabii hapana lakini ziko
karama za kinabii 1Koritho 12;0 lakini unabii huo unapimwa kulingana na
Maandiko na unabii huo lazima uwe kwa kusudi la kujenga 1koritho 14;3
Kristo Yesu kama
Kuhani
Kristo
Yesu kama kuhani alitimiza mambo makuu ya msingi yafuatayo
·
Alifaa
katika ofisi ya ukuhani Waebrania 1;3-6
·
Aliwekwa
na Mungu kuwa kuhani Waebrania 5;1-10
·
Alikuwa
na ukuhani bora zaidi kuliko ukuhani ule wa Haruni Waebrania 5;6,10
·
Alifanya
kazi zote za ukuhani Waebrania 7;23-28,9;11-28,10;5
·
Ukuhani
wake ni wa milele usio na kikomo
Kristo Yesu kama
Kuhani
·
Yesu
Kristo alikuwa ni kuhani mafalme na nabii na kwakuwa na ofisi hizi zote
kumemfanay awe kiongozi mkamilifu kwa mfano wa Melkizedeki Mwanzo 14;18-19
waebrania 7;1-3, na kwa mujibu wa agano la kale masihi alitabiriwa kuwa mfaqlme
mkuu wa uzao wa Daudi Isaya 11;1-9 zaburi 72 na Yesu alikubali kuwa yeye ndiye
mfalme huyo mbele ya Pilato Yohana 18;36
·
Baada
ya Ufufuo Yesu alikiri kuwa mamlaka yote Mbinguni na duniani amepewa yeye
Mathayo 28;18, hivyo kupitiqa Ufufuo Yesu alivikwa taji na kuketishwa katika
kiti cha enzi cha Mungu na baba byake Ufunuo 3;21,sawa na Waefeso 1;20-22 haya
yote ni sahii katika mtazamo wa Mungu lakini kwa wanadamu bado wengi hawajatambua
kuwa yeye ni mafalme ingawa amekwisha kupakwa mafuta kuwa mafalme Matendo
2;30Yohana 1;11,19;15
Kristo Yesu kama
Mwalimu mkuu
Ni
wazi pia kuwa Yesu Kristo alikuwa mwalimu mwema na mwenye mafanikio makubwa
kuliko waaalimu wote duniani aliyefanikiwa sana alikuwa “Rabi”
·
Amekuwa
na mafundisho Bora zaidi kuliko mtu awaye yote
·
Mafundisho
yake yanauwezo mkubwa wa kubadili maisha ya watu kwa karne nyingi
·
Alimtumia
njia bora zaidi za ufundishaji ikiwamo mifano na hadithi alieleweka kwa wasomi
na wajinga
·
Amepata
matokeo mazuri kuliko yeyeote katika historia ya dunia mwenye kuweza
kubadilisha maisha ya watu na wanafunzi wake kupitia neno lake
·
Alikuwa
na sifa zote kuu tano za mwalimu mwema, aliwapenda wanafunzi wake Mathayo
9;35,marko 6;34,aliwajua wanafunzi wake
na wanadamu Yohana 2;24-25 alilijua vizuri somo lake na kile alichokuwa
akikifundisha Luka 2;42-47,52, Mathayo 7;28-29 alijua namna za njia za
kufundisha na kuzitumia aliongoza alishirikisha alidhibiti na kuweka mipango
·
Aliishi
kile alichokuwa akikifundisha matedno 1;1 1Koritho 1;11 mwalimu mwema anaishi
kile anachokifundisha
KAZI ZA YESU KRISTO DUNIANI
MATESO YA YESU KRISTO NA KIFO CHAKE
Yesu
Kristo alifanya kazi nyingi sana lakini kazi moja ya mughimu ilikamilishwa
klatika kifo chake cha mateso pale msalabani ambapo aliklufa kwa ajili ya
dhambi za ulimwengu Mathayo 1;21, Yohana 1;29 hii ni kazi iliyoleta upatanishi
wa wanadamu kwa Mungu na pia kufufuka kwake na kupaa kwake Mbinguni
kunawakilisha utendaji endelevu wa kazi nyingine anazo zifanya Kristo huko
anatuombea kama kuhani Warumi 8;34,4;25,5;10
Kufa kwa Yesu
Msalabani
a.
Umuhimu wa kifo cha Yesu
Msalabani
Kiini kikubwa cha injili na mafundisho
yote ya agano jipya kinaweza kuhitimishwa kwa neno Kristo alikufa kwa ajili
yetu 1Koritho 15;3, Martin Luther alisema hii ndiyo tofauti kati ya ukristio na
imqani nyingine zote duniani na kiini
cha uprotestant ni katika fundisho la akzi ya msalabani hivyo kuelewa fundisho
sahii la Msalaba ni huruma za Mungu kwa wanadamu ili wapate Msamaha
b.
Maana ya kifo cha Kristo
msalabani
Kuna uhusiano wa Muumba na
uumbaji wake yaani mwanadamu ambaye aliumbwa na Mungu wana mahusiano lakini
mahusiano hayo yaliharibika na hivyo kulihitajika upatanishi kwa njia ya damu
ya mwadamu mwenye kumtii Mungu kwa asilimia zote asiye na doa mwenye ujuzi
kumhusu Mungu na mwanadamu ili afanye upatanishi kwani kwa juhudi za kibinadamu
ni muhimu kufahamu kuwa mwanadamu hawezi kamwe kufuta historia yake kuhusu
dhambi na hatia wala kuiondoa au kuizuia na hivyo ilikuwa ni lazima Kristo
mwenye sifa za kiungu na kibinadamu afe kwa ajili ya kazi ya kuwapatanisha
wanadamu kwa Mungu Yohana 1;35
c.
Yesu aliteseka na alikufa pale
msalabani
Mazingira
ya kifo cha Msalabani kwa Yesu.
Yako madai kutoka kwa wanaharakati wa
kiislamu kuwa Yesu alikuwa na afya nzuri na ndio maana aliweza kufunga siku
arobaini na kutembea kwa miguu sehemu mbalimbali, na kutokana na mazingira ya
hukumu ya kifo cha msalabani kilikuwa ni kifo cha polepole isingekuwa rahisi
Yesu kufa msalabani mapema na ushahidi ni kwa wale wahalifu wengine
waliolazimika kukatwa miguu ili wafe mapema.
Nataka kuwajibu waislamu hoja hii kwa
ufupi kuwa wahalifu wale wengine wawili walibeba misalaba yao na kwenda
kusulubiwa moja kwa moja bila mateso ya aina yoyote mbadala. Lakini kwa Bwana
Yesu yeye alikamatwa Mapema alfajiri katika siku hii hatuambiwi kama
alihudumiwa kwa chakula au la? lakini bila shaka wafungwa wale wengine
walihudumiwa gerezani kama kawaida, akiwa hajala kitu alianza kuteswa (Mathayo 26;67),Tunaambiwa kuwa alipigwa
makonde na makofi,hatuambiwi ni kwa kiasi gani,Pia tunaambiwa kuwa alipigwa
mijeledi ambayo kwa mujibu wa Historia Enzi za Warumi, Mtuhumiwa
alivuliwa nguo zote na kuwambwa
kwenye nguzo au kuinamishwa kwenye nguzo fupi na kufungwa mikono yake na
kuchapwa na kifaa maalumu,Kifaa hiki cha kuchapia yaani mjeledi kilikuwa ni
kifaa chenye Mpini mfupi wa mbao ambapomikanda kumi na mbili ya ngozi
iliambatanishwa ikiwa na vipande vya chuma au mifupa iliyofungwa kama shanga
kwenye kila mkanda,vipigo vilifanywa na wanaume wawili mmoja upande huu na
mwingine upande huu,Kipigo hicho kilipelekea nyama ya mwili kupurwa au ku katwa
katwa kiasi cha kuweza kuathiri mishipa ya fahamu,vena na ateri na hata kuumiza
viungo vya ndani vya vya tumbo na wakati mwingine vilitoka nje jambo hili pekee
lilifanya watuhumiwa wengi kufa wakati
wa kupigwa mijeledi,Mijeledi ilikuwa inaharibu kabisa sura ya Mtu ukweli
ilikuwa ni adhabu yenye kutisha sana,Inawezekana kabisa kushindwa kwa Yesu
kuubeba msalaba wake na kuanguka mara tatu na hatimaye kusaidiwa na Simon
mkirene kulitokana na kuchoshwa na kipigo cha mijeledi alichopata (Math 27;32, ),Achilia mbali kule
kusimikwa kwa taji la miiba kama mfano wa taji kichwani ambapo kulitoboa maeneo
ya kichwa na mishipa,kubeba ule msalaba,Na baadae kugongomelewa masumari mazito
ya chuma yenye umbo la mraba miguuni na kusimamishwa na kuchuruzika madamu kwa
masaa masaa tkribani sita hivi,misuli inavutwa Ngozi inaharibika,huku kukiwa na
dhihaka na matusi na shutuma ili kuteswa kiakili katika hali kama hii hata kama
ulikuwa unalia huwezi kulia tena ni
rahisi kuhisi kuwa Mungu amekuacha! Acha kiu ya maji ambayo kwa mateso kama
haya mtu alalamika kua ana kiu maana yake kutokana na kumwagika kwa damu nyingi
akiomba maji akinywa anakufa(Yohana
19;28).hivyo kuomba maji kwa Yesu
kunaashiria alikuwa amefikia hatua ya kukata roho na kwakweli ALIKUFA!. Mateso haya kwa kweli
yalichangia Yesu kufa mapema kuliko wale wengine.
Pamoja na mateso hayo yoote aliyoyapata
Masihi ambayo yalichangia kufa kwake mapema kabla ya wale wawili,Inashngaza eti
kuona wahubiri wa kiislamu wanakosa shukurani na kugundua Upendo mkuu aliokuwa
nao Yesu kwa ajili ya ulimwengu na wao pia
badala yake wandhihaki kazi hii ya huruma kwa wanadamu na wanafanya
jitihada za kuipinga kazi hii kwa makusudi hii ndio shukurani wanayomlipa Mungu
kuupinga msalaba jaribu kuwaza ni hukumu gani itawapata watu wa jinsi kama hii
kwa kushindwa kumuamini Yesu na kushikamana na marehemu Muhamad na kusahau kuwa
mateso ya Kristo yalikuwa ni kwa ajili yao.
(Isaya 53;2b-5). “…Yeye hana umbo wala
uzuri, Na tumuonapo hana uzuri hata tumtamani, Alidharauliwa na kukataliwa na
watu; Mtu wa huzuni nyingi ajuaye sikitiko; Nakama mtu ambaye watu humficha
nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu,Hakika ameyachukua
masikitiko yetu,Amejitwika huzuni zetu, Lakini tulimdhania ya kuwa
amepigwa,amepigwa na Mungu na Kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu.
Alichubuliwa kwa Maovu yetu, Adhabu ya amani Yetu ilikuwa juu yake na kwa
kupigwa kwake sisi tumepona….”
Pichani
Mchoro kuonyesha jinsi Yesu alivyopigwa mijeledi
Isaya nabii alitabiri vema na
kuonyesha wazi kuwa ni kifo cha namna gani Masihi angekufa soma aya hizo hapo
juu za unabii wa Isaya kumhusu masihi, Hivi karibuni wataalamu wa biblia
walifanya utafiti wa kutosha kuhusu Mateso yaliyompata Masihi na kujaribu
kuyaigiza katika filamu iitwayo “The
passion of Christ”Tunaweza kusema kuwa lile kilichoigizwa katika filamu ile
ni sahihi kabisa na kuna uwezekano kuwa mateso hayo yalikuwa zaidi ya kile
kilichoigizwa,Lakini lile wazo la nabii Isaya limeweza kufikiwa kwa aslimia
zaidi ya themanini!
Pichani juu ni
muigizaji maarufu wa filamu “The passion
of the Christ” akiigiza kwa karibu sana aina ya Mateso aliyoyapata kristo
ndugu huyu amejipatia sifa kubwa kwa uigizaji unaokaribiana na kile Biblia
inachosema.(Picha na Maelezo Na Rev. Innocent Samuel Kamote Mwandishi wa somo hili. 2007.)
Ufufuko
wa Yesu Kristo ni miujiza mkubwa sana
kwa ukristo miujiza mingine yote katika
injili ingekuwa haina maana kama miujiza huu haungelifanyika na kwa sababu hii imani yetu ya ukristo
inasimamama katika kufufuka kwake Yesu Kristo
·
Kifochake
kisingekuwa kinafaa kwa upatanishi
·
Ukristo
ungekuwa ni uongo na wahubiri wangekuwa
wamehubiri makosa
·
Lakini
ashukurtiwe Mungu kuwa Yesu Kristo amefufuka na kuna ushahidi mwingi katika
Maandiko lakini muda usingeweza kutosheleza kuyapitia 1Koritho 15;14-20
·
Uko
ushahidi wa Maandiko kadhaa ya kinabii na yaliyotimizwa kuhusu kufufuka kwa
Yesu zaburi 16;8-10,zaburi 30,3,41;10 marko 16;6-7matedno
2;27-31,13;33-35,zaburi 49;15,Hosea 6;2,118;17,Mathayo 28;5-7,Luka 24;36-48
Yohana 20;19,24-29 !koritho 15;17,20,Wafilipi 3;21
Pichani juu ni kaburi alilozikwa Bwana
Yesu kisha akafufuka,liko wazi hata leo,Watu wengi huenda mahali hapo kwa
shughuli za kutalii tu .Eneo hili huitwa Garden Tomb,Yaani Bustani ya
Kaburi,Mungu amepatunza mahali hapa hata leo hii ili watu wapate kusadiki kuwa
Yesu yu hai.Picha na Maelezo kwa hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Samuel
Kamote,
Kupaa kwa Yesu Kristo
·
Kupaa kwake mbinguni
kulikuja kwa sababu wakati wake ulikuwa umewadia
Kule mbinguni Yesu
ametukuka sana
·
Aliridi kule alikokuwa
Yohana 17;5 ni bwana na matawala mwenye mamlaka yote
·
Ushahidi wa kimaandiko
kuwa Yesu alipaa zaburi 16;10-11,Marko 16;19,Yohana 20;16-17.Mathayo 28;9 , 1Koritho
15;4, Zaburi 68;18, Luka 24;50-51 Matendo 1;9-11Zaburi 24;1-10, Efeso 4;8, Yohana
6;62,7;33,13;33,14;28-29, Zaburi 118;17-20, Waebrania 4;14,9;24
·
Kupaa kwake
kumemuwezesha kufanya kazi ya kutuombea na kuandaa makao
SURA YA TATU; WAKATI HUU NA KUJA KWA YESU KRISTO
MARA YA PILI
Kazi za sasa za Yesu Kristo
Ule
ukweli kwamba Yesu alipaa mbinguni ambao umethibitishwa katika injili na
Matendo ya mitume na nyaraka ni wazi kuwa kuna kazi anazozifanya Yesu kwa sasa,
Yesu aliacha ulimwenfu huu na kurudi kwa baba yake kwa wakati alirudi katika
ulimwengu amabao kwamba alikuweko kama alivyokuja kwa njia ya miujiza wa
kimungu pia alipaa kwa miujiza wa kiungu tedno hili linatufundisha mambo kadhaa
yafuatayo
A. Yesu ametukuzwa Mno
Yesu kupaa mbinguni zinatumika
lugha mbili kuu kwanza alipaa mbinguni
na pili akachukuliwa juu mbinguni Lugha hizi zinatumika kwanza kuonyesha kuwa ilikuwa ni kwa mapenzi
yake yeye mwenyewe alipaa na pili ilikuwa ni mapenzi ya baba yake yeye kupaa si
kuwa mbingu kilikuwa ni kitu kipya kwake lakini ametukuzwa kwa maana ya kuwa amerudi
katika utukufu ule aliokuwa nao kwanza Yohana 17;5 si hivyo tu bali akiwa
ametimiza Jukumu kubwa la kiungu la kumkomboa mwanadamu Waebrania 12;2 jambo
amabalo limeleta furaha kubwa sana mbinguni na ni kwa ajili ya furaha hii
tunasema Kristo ametukuzwa mno huko mbinguni, Kristo alirudi katika hali ya
matumizi ya mamlaka kamili ya kiungu yote ya mbinguni na duniani Mathayo
28;18,Efeso 1;20-23,1Petro 3;22,Wafilipi 2;9-11,Ufunuo 5;12
B. Yesu amekuwa Bwana juu ya yote
Kwa kupaa kwake Mbinguni amekuwa
kichwa cha kila Mwanadamu 1Koritho 11;2,amekuwa juu ya falme na mamlaka kolosai
2;10 amekuwa juu ya mamlaka zote zisizoonekana 1Petro 3;22,Warumi 14;9 na
Wafilipi 2;10-11 huko anamiliki ubwana wa ulimwengu mzima na Mungu ameweka kila
kitu chini ya miguu yake na pia amekuwa
Kichwa cha kanisa
C. Yesu anaandaa makao
Kujitenga kwa Yesu Kristo na
kanisa lake kulikotokea baada ya kupaa kwake sio mwisho wa kila kitu au sio kwa
kudumu lakini huko qanaandaa makao ili
kwamba kule atatkakokuwako na watumishi wake wawezekuweko Yohana 12;26 na pia
anakuwa kama Bwana harusi ambaye yuko kwenye maandalizi ya kuja kumchukua bibi
harusi ambaye ni kanisa
D. Yesu anafanya kazi za kikuhani
Kwa kuopaa kwake Mbinguni Yesu
Kristo kama kuhani mkuu ameingia patakatifu pa kimbinguni ili kutuombea na
kufanya upatanishi wa dhambi kwa ajili yetu yeye sasa ndiye mpatanishi pekee
kati ya Mungu na wanadamu 1Timotheo 2;5, Kutuomea ni kazi muhimu sana
anayoifanya Kristo huko mbinguni Warumi 8;34 kwa msingi huo hata kupaa kwake
mbinguni ni kwa ajili yetu ,Shetani ni mshitaki wetu kwa msingi huo tunapotenda
dhambi hupeleka hoja za kuonyesha madai kuwa hatufai tena kwa Mungu lakini kwa
ushirikiano wetu na Kuhani mkuu tunapomueleza kwa njia ya Toba yeyey hufanya
upatanishi kwa kutuombea anagalia 1Yohana 2;1-2 “Watoto wangu wapendwa,
nawaandikieni haya ili msitende dhambi. Lakini kama mtu ye yote akitenda
dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo Mwenye haki. Yeye ndiye dhabihu
ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu,
bali pia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote.”
E. Yesu Kristo anakuwa na sifa ya kuwako mahali kote kwa wakati mmoja
Alipokuwa duniani Yesu Kristo
alikuwa na mipaka ya kibinadamu iliyomlazimu Kuweko kule Israel tu Yohana 14;12
Yeye anapokuwa Mbinguni kwa baba sasa anaweza Kuweko mahali kote kwa wakati
mmoja Omnipresent kwa hivyo kwa kupaa kwake sio tu amepewa Nguvu zote lakini
amekuwa na uwezo wa Kuweko mahali kote Mathayo 28;18,20
KAZI
ZA BAADAYE ZA YESU KRISTO
Kristo
Yesu atakuja tena Fundisho kuhusu kuja tena kwa Yesu Kristo limetajwa mara 300
hivi katika agano jipya pekee, Paulo mtume pekee amahitimisha katika nyaraka
zake mara 50 hivi akitaja kuhusu kuja kwa Yesu mara ya pili duniani, kuja kwake
mara ya pili kuetajwa mara 80 hivi na kumerudiwa kwa uwazi kzaidi katika
Wathesalonike 1&2 Mathayo 24, na Marko 13 ni vitabu vinavyowekwa wakfu kwa
habari ya kuja kwake mara ya pili kuja kwa Yesu mara ya pili kimegawanyika
katika sehemu kuu mbili
1. Kunyakuliwa kwa kanisa Rapture au
Parousia “
Parousia”
2. Kuja mara ya pili duniani
Revelation
Kunyakuliwa kwa kanisa
Rapture.
·
Kristo
atakapokuja kwa ajili ya kanisa hatakanyaga ardhi ataishia hewani au mawinguni
na kulinyakua kanisa yaani watu wake wanaomcha yeye kutoka kila pembe ya dunia
na dhehebu
·
Ujio
huu ni wa ghafla kama mwivi na si kila jicho litamuona swala hili litafanyika
kabla ya gharika kwa mujibu wa imani Orthodox hata hivyo wako watu wengine
wanaoamini tofautina hivyo kufanya Kuweko kwa dhana kama nne hivi za ungakuo
amabazo ni
1.
Kunyakuliwa
baada ya dhiki (PostTribulation View)
2.
Kunyakuliwa
wakati wa dhiki au katikati ya dhiki (Midtribulation view)
3.
Kunyakuliwa
kwa awamu (Partialtribulation View)
4.
Kunyakuliwa
kabla ya dhiki kuu (Pretibulation view)
·
WaOthodox
wenye imani sahii wana amini kuwa kanisa litanyakuliwa kabla ya dhiki ile kuu
kwani ndicho tunachosubiri kwa sasa 1Thesalonike 4; 13-18,5;1-7, 1Koritho 15;52,
tukio la unyakuo litakuwa la ghafla ni kama kufumba na kufumbua ,litaambatana
na kufufuliwa kwa wafu watakatifu na kuungana na watakatifu walio hai
watakaobadilishwa mioyo na kumlaki Kristo mawinguni na tutakuwa naye mawinguni na kupewa tahwabu
na kusha kualikwa kwenye karamu ya mwana kondoo Baada ya kupewa taji za haki
huku duniani dhiki kuu itakuwa ikiendelea na mwishoni ndipo Kristo atarudi na
watatkatifu wake duniani hapo itakuwa dhahiri na sio kwa wizi
Kuja Mara ya pili
kwa Yesu duniani Revelation
Hili
ni tukio litakalokuwa waziwazi kwani kila jicho litamuona Kristo atarudi na
kukanyaga ardhi mahali pale alipopaa kwenda mbinguni katika mlima ule wa
mizeituni tukio hili ni la Kristo kuja na watakatifu wake kwa ajili ya utawala
wa miaka 1000 hapa duniani kuja kwake huku kutaambatana na kuuawa kwa Mpinga
Kristo na nabii wa uongo pia kutiwa kifungoni kwa Ibilisi miaka 1000 ufunuo 19;
20 ujio huu utakuwa na sifa nyingi kama zifuatazo
·
Utakuwa
ni halisi Kriosto mwenyewe ataonekana
Yohana 14;3,Matendo 1;10-11,1Thesalonike 4;16,Ufunuo 1;7 Zekaria 14;4
·
Haitakuwa
kwa wizi itakuwa waziwazi Waebrania 9;28,Wafilipi 3;20,Zekaria 12;10
·
Itakuwa
kwa utukufu mkubwa sana Mathayo 16;27,2Thesalonike 1;7-9,Kolosai 3;4Mathayo
25;31
Mahali
hapa ndipo ambapo Inasadikiwa Yesu alipaa kwenda Mbinguni Pale Yerusalemu
katika mlima wa mizeituni,mahali hapa Yesu aliacha nyayo zake na zimetunzwa
kitaalamu hata leo kachumba haka katikamlima wa mizeituni ndiko kanakotunza
nyayo hizo za mwisho Yesu alipopaa kwenda Mbinguni atakaporuidi atakuja katika
mlima huu wa mizeituni Picha na maelezo kwa hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Samuel Kamote.
Siku ya kurudi kwa
Yesu
Wako
watu waejaribu kuweka sawa hesabu zao kujaribu kujua kuwa Yesu anakuja
lini lakini waliaibika vinaya kwani
Maandiko yanaeleza kuwa siku ya kuja kwake imeficha katika Hekima ya mungu Mathayo 24;36-42,Marko 13;21,22, hakuna mtu
ajuaye siku ya kuja kwa Bwana kimsingi hata mitume waliokuwa na mafunuo makubwa
hawajawahi kujidfai kuwa wanajua kuwa Yesu anakuja lini lakini tumepewa dalili
za kuja kwake ikiwa Hata Yesu kama Mwanadamu na Nabii mkuu alisema haijui siku
hiyo kujifanya unaijua siku hiyo ni kiburi cha wazi cha kujifanya unajua kuliko
mitume siku hiyo itakuwa ghafla 1Koritho 15;52,Mathayo 24;27 na haitategemewa
2Petro 3;4Mathayo 24;48-51Ufunuo 16;15
Kristo
alitoa dalili nyingi sana za ujio wake hizi ndio za muhimu kwetu kuziangalia na
kujiandaa mioyoni mwetu
Injli
itahubiriwa kwa mataifa yote kuwa ushuhuda Luka 19;11-27Mathayo 24;14
Atachelewa
kiasi ambacho kanmisa watashangaa kwanini amechelewa Luka 18;1-8
Wengine
watajiandaa na wengine watapuuzia na kukata tamaa Luka 12;45Mathayo 25;19,6
Hakuna
ajuaye siku wala saa atakayokuja mwana wa Adamu Mathayo 24;36,42,50
Atakuja
ghafla na kuhukumu watumishi wake kulingana na kazi zao Mathayo 25;19 na
2Koritho 5;10
Watu
watakuwa wakila na kunywa wakioa nakuolewa kama siku za Nuhu Mathayo 24;37-39
na siku za sodoma Luka 17;28,29
Atakuja
kwa utukufu mkubwa na nguvu na hukumu kuja kuutawala ulimwengu na mataifa yote
ya Dunia Mathayo 25;31-46
Makusudi ya kuja
kwake
1. Kwa ajili ya kanisa lake
atawanyakua kabla ya ujio kamili wa kuja kuitawala dunia
2. Kwa ajili ya mpinga Kristo kumuhukumu kwa ajili ya uovu dhidi ya Israel
na ulimwengu na dini potofu pia kujitukuza kwake juu kama Mungu na kwa ajili ya
mateso makubwa jkwa wanadamu na hasa wale wanaoamini katika Mungu wa kweli
1Yohana 4;3,2;18,2;22,2Thesalonike 2;3Ufunuo 13;1,Daniel 7;8,25,Ufunuo
13;16-17,17;1-15
3. Kwa ajili ya kuhukumu mataifa
,kila taifa la dunia litahukumiwa na
kila mtu atawajibika kwa mfalme wa wafalme Daniel 2;44,Mika 4;1,Isaya
49;22-23,Yeremia 23;5,Luka 1;32,Zekaria 14;9,Isaya 24;23,Ufunuo 11;15
4. Kwa ajili ya kutwawala dunia
miaka 1000 wakati wa millennium Zaburi 2;7-9,72,Isaya 11;1-9 Ufunuo 20;6.
YESU
KRISTO KATIKA MITAZAMO TOFAUTI YA KITHEOLOJIA
Ziko
dhana mbalimbali ambazo muda susingeweza kutosha za watu na wanatheolojia
mbalimbali kumhusu Yesu Kristo ni muhimu kuwa na ufahamu na kujua namna na
jinsi ya kuitetea imani yako baada ya kuwa umejifunza mafundisho haya ya muhimu
kuhusu Yesu Kristo
Wako
wanaoamini kuwa Yesu akishindwa kama watu wengine pale alipokubali kusulubiwa
Msalabani kwa msingi huo tunaweza
kujifunza kutoka kwake maisha safi aliyoishi na wema wake lakini tendo la
kukubali kudhalilishwa msalabani ni kushindwa vibaya kwa Yesu
Wako
wengine wanamuona kama mwana siasa,mwana jamii na mwanauchumi
Wengine
wanamuona mwanadamu wa kawaida tu aliyewahi kuishi duniani au mwana Filosofia
au rabi mkubwa aliyepata kutokea katika Israel ambaye wengine walimkubali na
wengine walimkataa
Apolonarianism
hii ni jamii iliyotokana na Apolliaris ambaye alikuwa ni Askofu wa Laodekia
kati ya mwaka 361 Yeye alifundisha kwamba Yesu alikuwa na mwili wa kibinadamu
lakini akili za kiungu na roho ya kiungu hivyo Kristo alikuwa na mwili wa
kibinadamu na akili za kiungu na roho ya kiungu
Mwili wa kibinadamu
akili na roho za Kimungu
Nestorianism hawa walifundisha kuwa kuna aina mbili za utu
wa Yesu Kristo zilizo tofauti Kristo wa kimwili na Kristo wa kiroho kwa hivyo
Yesu alikuwa Mwanadamu na pia alikuwa Mungu
fundisho hili liko tofauti na mtazamo wa kibiblia kumhusu Yesu Kristo
ambao humuona Yesu kuwa ni nafsi moja kamili
Imani ya wanestorian Kristo ni nfsi mbili
Mwanadamu na Mungu
Monophyisitism
au Eutychianism walifundisha kuwa Kristo
ni mwenye asili moja kwa msingi huo
asili ya kiungu iliungana na asili ya kibinadamu na kufanuya asili mpya moja
Asili Mpya
Asili ya kimungu
Asili ya kibinadamu
Eutychianism wana amini kuwa Yesu
ni muungano wa asili mbili uliozaa asili mpya.
SURA
YA NNE; UUNGU WA YESU KRISTO
Kwa
kumalizia somo letu la Christology ni muhimu kwetu kuhitimisha kwa kusema kuwa
Yesu sio tu alikuwa mwanadamu kamili lakini pia ni Mungu kamili ingwa hakuna
andiko linalothibitisha moja kwa moja lakini neno lile Incarnation limetumiwa
na kanisa kwa Muda mrefu kuonyesha wazi kuwa Yesu ni mwanadamu na ni Mungu au
ni Mungu katika mwili tunaweza kugundua kuwa Yesu ni mungu kwanza kwa kuangalia
mambo ya msingi yafuatayo
Ana sifa zote
ambazo kwa kawaida ni sifa za Mungu peke yake
1.
Ni mwenye nguvu zote His
Omnipotence (He is all Poweful).
Sifa hii ya kuwa na nguvu zote sio ya
kibinadamu ni sifa ya Mungu tu viko vitu vingi duniani vina nguvu hata shetani
ana nguvu ,miungu ina nguvu,mapepo na wachawi wana nguvu na vitu mbalimbali
vina nguvu lakini havina nguvu zote Yesu alitabiriwa kuwa na nguvu zote na
alitimiza sifa ya kuwa na nguvu zote, Zaburi 110;3,Nahumu 1;3,Luka
4;14-15,8;54-55,Isaya 40 ;10,Waefeso 1;20-23,Isaya 50;2-3,mathayo 28;18,Ayubu
42;2,Mwanzo 18;14 Mathayo 19;26,zaburi 107;25,Mathayo 8;26-29.
2.
Ni mwenye kujua yote His
Omniscience (He is all Knows).
Hakuna mwanadamu mwenye kujua yote sifa ya
kujua yote ni sifa ya Mungu pekee lakini Maandiko yanamuonyesha Yesu kuwa
anajua yote unaweza kuulizwa kwanini Yesu alipoulizwa siku ya kuja kwake
alisema siku ya kuja kwake hakuna aijuaye? Yesu alijibu kwanza kama mwanadamu,
lakini siku ya kuja kwa bwana Mungu katika Hekima yake aliamua kuifanya kuwa
siri na hatupaswi kuhoji kwa nini lakini kama Yesu alikuwa haijui siku hii
angewezaje kutupa dalili za kuja kwake kama mtu anaweza kukupa dalili kamili za
ujio wake ni wazi alikuwa anajua siku ya kuja kwake kama Mungu, aida ifahamike
pia kuwa nilisema mwanzoni katika somo hili Nafsi zote za Mungu zina wajibu
wake Mungu baba hushughulika na majira na nyakati na mipango na kwa sababu hizo
Yesu kila mara alikwepa kujibu maswali yanayohusiana na majira na nyakati au
mipango Mathayo 24;36,Matendo 1;6-7, Yesu majukumu yake ni ya ukombozi na
wokovu, na Roho majukumu yake ni maongozi na nguvu kwa msingi huu basi hayo
hayamaanishi kuwa yesu hajui yote Yesu anajua yote Mithali 8;14,Isaya
11;2,Mathayo 9;4,12;25,Luka 6;8,22;10-13,Yohana 6;64,18;4,Ayubu 37;16,Zaburi
145;5 1Yohana 3;20 kolosai 2;3Mithali 15;3,Yohana 1;48,zaburi 139;2-4,Yohana
4;16-19,28-29,Yeremia 17;9-10,Yohana 2;24-25.
3.
Yuko kila mahali kwa wakati mmoja
His Omnipresence (He is Everywhere in one time).
Hakuna mwanadamu mwenye sifa ya
kuwa kila mahali kwa wakati mmoja wala malaika ghata shetani mwenyewe hana
uwezo wa kuwa kila mahali kwa wakati mmoja bali huzungukazunguka, Kristo
alipokuwa Duniani hakuwa na uwezo wa kuwa kila mahali kwa wakati mmoja kwa
sababu alikuwa mwanadamu lakini kwa kupaa kwake mbinguni na kuirudia enzi
ameweza kuwa na sifa ya kuwa kila mahali kwa wakati mmoja hii ni sifa ya Mungu
pekee na Yesu alikuwa nayo Zaburi139;7-10,Mathayo 18;20,Yeremia 23;23-24, Mathayo
28;20,Ufunuo 21;2,3,10,22-23, Mika 5;2Yohana 14;20,1;1Kolosai 1;1
4.
Yesu ni wa milele He is eternal
Waebrania 13;8, Ufunuo 1;17, Ni
muhimu kufahamu kuwa viumbe vyote vina Mwanzo na vina mwisho hata shetani ana
mwisho kwani atatupwa jehanamu ya moto lakini sivyo ilivyo kwa Yesu Kristo yeye
amekuwako tangu milele Yohana 1;1 sifa ya umilele ni ya kimungu pekee na siyo
ya kibinadamu wala malaika kwani wao walikuwa na mwanzo Mungu hana Mwanzo wala
mwisho yeye yuko siku zote milele nyuma na milele mbele Mika 5;2, Yeye ni alfa
na omega Ufunuo 1;11
5.
Yesu Kristo habadiliki He is
Unchangeble
Waebrania 13;8 pia humaanisha
kuwa yesu ni yeye yule jana leo na hata milele si kuwa andiko hili linaonyesha
kuwa Yesu ni wa milele lakini pia linaonyesha tabia ya Mungu ya kutokubadilika
badiliko Mungu alipojifunua kwa Musa na
Musa kumuuliza jina lako ni nani Yeye alijibu mimi Niko ambaye Niko maana yake ni kuwa atakuwa kama atakavyokuwa
au yeye ambaye kweli yuko kutoka 3;15 hii ni sifa ya Mungu wanadamu hubadilika
badiliko hata malaika walibadilika na kuacha kumtii Mungu wakawa mapepo kwa
msingi huu tabia ya kubaki kuwa mkeli na ya Mungu pekee na Yesu anayao.
Anauwezo wa
kusamehe dhambi
Kwa
kawaida mwanadamu anapotenda dhambi huwa hamkosei mwanadamu mwenzake tu hayta
pale inapotokea kuwa kosa hilo amelifanya kwa mwanadamu mwenzake lakini kama
Mungu alikataza kosa hilo lisifanyike kwa wanadamu wenzake unakuwa umemkosea
Mungu Daudi alionyesha wazi kuwa alimkosea Mungu pekee Zaburi 51; 4 “
Nimekutenda dhambi wewe peke yako na kufanya uovu mbele ya macho yako” Kwa msingi huo dhambi hutendwa
kumuelekea Mungu peke yake na hivyo kama tunahitaji Msamaha lazima Msamaha huo
utoke kwa Mungu pekee soma Mathayo 6;12a “utusamehe makosa yetu” hii ni sehemu
ya sala ya bwana kumuomba Mungu atusamehe kwa msingi huo Msamaha wa dhambi
hutolewa na Mungu tu na wayahudi walilielewa hilo Vizuri Luka 5;18-24 Ni wazi
kuwa mwenye uwezo wa kusamehe dhambi ni Mungu pekee Yesu husamehe dhambi hii
inamaanisha kuwa yeye ni Mungu
Anakubali kuabudiwa
Wanafunzi
wa Yesu walikuwa ni wayahudi na wayahudi walikuwa waeonywa kuwa wasiabudu kitu
kingine chochote isipokuwa Bwana Mungu wako peke yake hii hata Kristo mwenyewe
alisema Pale shetani alipotaka ibada kutoka kwake Luka 4;5-8 lakini katika
namna ya kushangaza Yesu alikubali kusujudiwa na kuabudiwa hii ni wazi kuwa
alikuwa Mungu
·
Alisujudiwa
na kuabudiwa na mamajusi Mathayo 2;10-12 pia walitoa matoleo
·
Alisujudiwa
na wenye ukoma Mathayo 8;1
·
Alisujudiwa
na mapepo yaliyokuwa ndani ya mgersi Marko 5;1-15
·
Thomasi
alimkiri kuwa Ni bwana na Mungu Yohana 20;26-29
·
Alisujudiwa
na kuabudiwa na wanafunzi wake Mathayo 28;9,16-20
·
Anaabudiwa
na malaika wote Ufunuo 14;1-5
Kristo ni Mungu
kamili
Kwa
ujumla agano jipya katika Maandiko mengi sana limemuita Yesu kuwa ni Mungu au Bwana kwa mamia ya aya na kwa majina
mengine mengi yanayoonyesha uungu wakeuemi wake maisha na matedno yake yote
yanaonyesha uungu wake na kuwa Yeye
alikuwa Mungu kweli au Mungu wa kweli
wakolosai 1;19 inasema hivi Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu
wote wa Mungu ukaye Biblia nyingine za Kiswahili zimeruka neno hilo Mungu na ujio wake duniani ni kwa ajili yetu ili
kuwa Mungu akae au apatane na sisi na kurudisha uhusiano wake kwetu ili
kutimiza unabii ya kuwa yeye ni Immanuel uyaani Mungu pamoja nasi Mathayo 1;23
‘Tazama bikira atachuikua mimba naye atazaa mwana nao watamwita jina lake Immauel yaani Mungu
pamoja nasi’Paulo mtume alimwita Yesu Mungu mkuu na mwokovu wetu Tito 2;13 kwa
msingi huo ni muhimu kuhitimisha somo hili kwa kusema kuwa Yesu ni Mungu!
Na
kama tunakubali kuwa Yesu ni Mungu basi ni muhimu kulikumbuka hili kuwa
hatuwezi kumfahamu Mungu kwa asilimia 100 tukiwa na akili hizi za kibinadamu
kwani Mungu ni mkubwa kuliko akili zetu take care!
somo na Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima!