Yeremia 23:28-29 . “Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na
neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano?
Asema Bwana. Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo
mawe vipande vipande?”
Askari wa Israel pamoja na mbinu za kimapigano pia hutumia neno la Mungu kwa vita
Utangulizi:
Ni
muhimu kufahamu kuwa kama tunataka kufanikiwa katika maisha yetu na kusitawi,
Hatuna budi kuhakikisha kuwa tunaliangalia neno la Mungu, siri zote za
mafanikio yote ya mwanadamu zimefungwa katika neno la Mungu, nje ya kanuni na
njia za Mungu hatuwezi kufanikiwa, kwa nini tunapaswa kuliangalia neno la Mungu
ni kwa sababu nje ya neno la Mungu hatuwezi kuzijua Nguvu zake, Yeremia alikuwa
ni nabii aliyetumwa kuwaonya wayahudi kwa miaka mingi kuhusu hukumu itakayokuja
kwa sababu ya dhambi yakuabudu sanamu na dhuluma, hata hivyo watu walimdharau,
walimpinga na kumtesa, na hata manabii wa uongo waliojichagua wenyewe waliamka
na kuhubiri kintume na Yeremia wakiwaahidi watu kuwa kutakuwa na amani na
Mafanikio, Mwitikio wa Yeremia ulikuwa “Kila nabii na aeseme alichopewa kama ni
ndoto zungumza ndoto zako lakini mimi nitalizungumza neno la Mungu kwa sababu
Yeremia alijua kuwalina nguvu, lina uweza, ni Neno la kweli la Mungu
linalozungumzwa kwa uaminifu ndilo linaloweza kuleta Mabadiliko makubwa kwa
wanadamu na nguvu yake kuonekana. Historia ilionyesha kuwa Maneno ya Yeremia
yalikuja kutimia kwa sababu alikuwa akizungumza neno la Mungu sawa na jinsi
Mungu alivyotaka. Ni kweli ya neno la Mungu pekee inayoweza kutupeleka kwenye
ujuzi na uelewa wa nguvu zake.
·
Ujuzi
wa kisayansi hauwezi kutusaidia
·
Ujuzi
wa dini mbalimbali hauwezi kutusaidia
·
Ujuzi
kuhusu Mungu hauwezi kutusaidia
·
Kwenda
vyo vya biblia na kuwa na madegree ya Kitheolojia hayawezi kutusaidia
Ni
ujuzi wa neno la Mungu uliokaa katika ufunuo wa kweli yake ndio unaoweza
kutusaidia kumjua Mungu na Nguvu zake,
Hivyo neno la Mungu ni la Muhimu sana kama Mungu mwenyewe anavyoliheshimu na
kutushauri.
Yoshua 1:8 “itabu hiki cha
torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku,
upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo
utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.”
Hakuna
siri nyingine yoyote ya mafanikio ya maisha yetu kama sio kuliangalia neno la
Mungu, Yoshua alipewa siri hii na Mungu mwenyewe kwamba ili aweze kufanikiwa na
kusitawi sana hana budi kuliangalia neno la Mungu, kulitafakari, kulisoma,
kulielewaq, kulijadili, na hapo ndipo tukilifanyia kazi tutaweza kuona
mafanikio makubwa sana katika maisha yetu, Daudi alikuwa ni mfalme aliyepata
mafanikio makubwa sana wakati anakaribia kufa alimuhusia Daudi kwamba ili aweze
kufanikiwa hana budi kuliangalia neno la Mungu, na wakati ule neno la Mungu
lililokuweko ilikuwa ni torati iliyoandikwa na Musa.
1Wafalme 2:3 “3. uyashike
mausia ya Bwana, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na
amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika
torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;”
·
Mafanikio ya kila mtu mmoja mmoja
·
Mafanikio ya Kifamilia
·
Mafanikio ya kijamii
·
Mafanikio ya kitaifa
·
Mafanikio ya kijeshi
·
Mafanikio ya kiafya
Yote
yamefungwa katika neno la Mungu, Mtu awaye yote anayetaka kufanikiwa katika
jambo lake lolote hana budi kujiweka katika mazingira ya kujifunza na kulielewa
na kulitafakari neno la Mungu.
Neno
la Mungu lina uhai kama Mbegu kwamba ikipandwa inaongezeka,mbegu ikitulia
mahali na kuhifadhiwa haiwezi kuonekana kuwa na maana lakini ikitumiwa na
kupandwa huleta mazao makubwa sana ndivyo lilivyo neno la Mungu, Luka 8:11 “Na huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno
la Mungu”., Yohana 12:24
“Amin, amin, nawaambia,
Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake;
bali ikifa, hutoa mazao mengi.”
Kama
tukikaa hivi hivi katika maisha yetu bila kulitendea kazi neno la Mungu,
Hatutaweza kuona uweza wa Mungu ukitenda kazi katika maisha yetu, ili tuweze
kuona matokeo chanya katika maisha yetu hatuna budi kuhakikisha kuwa
tunalifanyia kazi neno, lazima tulisome, lazima tulijadili, lazima tujifunze,
lazima tulitafakari na kulitendea kazi, nguvu za Mungu na utendaji wake
utadhihirika kwa uwazi katika maisha yetu.
Yesu
alimuita mtu anayesikiliza neno la Mungu na kulifanyia kazi kama mtu mwenye
akili na mtu asikilizaye kisha asilifanyie kazi kama mtu mpumbavu Mathayo 7:24-27 “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na
kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya
mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile,
isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo
maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake
juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga
nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa” Kama tunataka
kuishi maisha ya ushindi na mafanikio kamwe tusimlaumu Mungu maelekezo yote Mungu
ameyaweka katika neno lake, hatuna budi kuhakikisha kuwa tunajisomea neno la
Mungu kila mara tunalikariri,tunalielewa, tunajifunza, tunalijadili kwa kusudi
la kulielewa na tutaweza kuona mafanikio makubwa sana katika kupitia neno la
Mungu.
Nguvu ya neno la Mungu
Ni
muhimu sasa kujiuliza kwamba, kwa nini neno la Mungu ni ni muhimu sana katika
maisha yetu? Je tunawezaje kufanikiwa na kufaidika kwa neno la Mungu,
nikilisoma na kulielewa na kulikariri itanifaidia nini?
1. Neno
la Mungu linafaa kwa Mafundisho
2Timotheo
3:14-17“Bali wewe ukae
katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina
nani ambao ulijifunza kwao; na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko
matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo
katika Kristo Yesu. Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na
kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika
haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.”
Nyakati hizi tulizo nazo watu wanapata shida sana na namna na jinsi tunavyoweza
kuwalea watoto wetu katika ustahivu, dunia ya leo inaonekana kama kuna tatizo
kubwa sana la uadilifu! Unajua ni namna gani tunaweza kuwasaidia watu, ni namna
gani tunaweza kuwaongoza watu, ni namna gani tunaweza kuwakemea watu ni namna
gani tunaweza kuwaonya watu na ni namna gani watu wanaweza kuwa wakamilifu ni
kwa kuwajuza neno la Mungu hakuna njia ya mkato, Zaburi 119:9 “Jinsi gani kijana aisafishe njia
yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.” Kila kijana na jamii itakuwa
safi kama watu watafundishwa neno la Mungu na kujifunza kulitii, wat7u wakilipa
kipaumbele neno la Mungu watafaa kwa kila tendo jema , watu wengi leo hawafai
sehemu mbalimbali kwa sababu hawajaandaliwa katika neno la Mungu, Bwana amope
neema kila mmoja wetu kulitii na kulifanyia kazi neno la Mungu.
2. Neno
la Mungu ni upanga wa roho.
Waefeso
6:17 “Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho
ambao ni neno la Mungu;” Katika fungu la silaha za kiroho zinazotajwa katika Waefeso 6:10-18, Neno la Mungu ni moja
ya silaha kali za mashambulizi, silaha nyingi zinazotakwa kwa mkristo ni za
kujilinda, na silaha chache sana ni za mashambulizi, Neno la Mungu ni silaha ya
mashambulizi, katika vita ka katika michezo kujihami sana hakusaidii, kujilinda
na kujihami ni kuzuri lakini hakuwezi kumfukuzia mbali adui, nafikiri kama
ningelikuwa mwalimu wa vita au kocha wa Mpira ningewafundisha watu wangu
kushambulia zaidi, kushambulia ndiko kutakako mfanya adui akimbie na kwenda
mbali sana au afanye kazi ya kujihami na kujilinda, ushindi wetu katika
maandiko unatajwa kuwa katika neno la Mungu na Damu ya Yesu, Ufunuo 12:10-11 “Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa
kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake;
kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za
Mungu wetu, mchana na usiku. Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa
neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.” Wote tunafahamu kuwa Yesu wakati wa Majaribu
aliweza kumshinda shetani kwa sababu alikuwa na ujuzi wa ajabu kuhsu neno la
Mungu, ujuzi kuhusu neno la Mungu na kujaa kwake maandiko kulimfanya ibilisi
kumkimbia, kushindwa kwa Eva katika Bustani ya Edeni ni wazi kunaonekana
kulitokana na kushindwa kuhifadhi na hata kulielewa agizo la Mungu na neno la
Mungu kwamba wasile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, Lakini hali
hiihaikuwa hivyo kwa Yesu yeye alikuwa amejaa nneno na ufahamu kuhusu neno la
Mungu ulikuwa juu yake naye alifanikiwa Luka
4:1-13 “Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi
kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, akijaribiwa
na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa.
Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate.
Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. Akampandisha
juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia,
Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami
humpa ye yote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa
yako. Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu
yeye peke yake. Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha
hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; kwa maana
imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde; na ya kwamba,mikononi mwao
watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Yesu akajibu akamwambia,
Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi
akamwacha akaenda zake kwa muda.” Watu wengi wanashindwa na hali
zinazowazunguka leo kwa sababu hawana ujuzi wa neno la Mungu katika vita vyao, Neno
la Mungu lina nguvu unapolisema na kulitaja kazi za adui zinashambuliwa vibaya
na shetani anapata tabu sana, unawezaje kuwa mshindi katika maisha yako uwe na
neno la Mungu kwa kila hali inayokuzunguka, uwe na neno la Mungu kwa kila vita
inayokuzunguka, mkumbushe Mungu hali unayokutana nayo na mtamkie shetani hali
anayokujaribu nayo na hapo ndipo utakapoona uweza mkubwa wa neno la Mungu.
3. Neno
la Mungu lina Nguvu ya kuhekimisha (power to make you wise)
Mithali
3:13 “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye
ufahamu.”
Biblia ya kiingereza inasema “Blessed is the man who finds wisdom, the man who
gains understanding” kwa Kiswahili kizuri tungeweza kusema heri mtu yule
atafutaye hekima, na mtu yule apataye ufahamu”
Ni muhimu kufahamu kuwa kuna ujuzi na hekima kubwa
sana katika neno la Mungu kuliko katika maandiko mengine yoyote yale, mtu
anayejisomea neno la Mungu hata asiposoma vitabu vingine anauwezo wa kuitambua
Hekima ya kweli kuliko wenye hekima wa dunia hii Katika macho ya Mungu hekima
ya dunia hii ni upuuzi 1Wakoritho 1:20 “Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja
wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu?” 3:19
“Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa
maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao.” Katika
historia ya ulimwengu watu ambao wameweza kuutikisha ulimwengu, watu ambao
wameweza kuupindua ulimwengu, watu ambao wameweza kusimamia uadilifu na
kusimamia mafundisho sahihi ya biblia ni watu ambao wanalijua neno la Mungu,
watu wasio na tamaduni zozote na wakaweza kufaidika kwa ujuzi ni wale ambao
wallifahamu neno la Mungu wale wanaoisoma na kuijua Biblia, ujuzi katika neno
la Mungu, Kaka zangu dada zangu kama tunataka kuwa na uelewa wa kupita kawaida
katika maswala ya ulimwengu huu suiache kujifunza neno la Mungu, Hekima
inajenga Nyumba inaimarisha Mithali 14:1
“Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake;
Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.”
4. Neno
la Mungu hupandisha Imani
Warumi
10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia
huja kwa neno la Kristo.” Ni muhimu kukumbuka kuwa hatuwezi kuwa na imani kamwe kwa kuomba pekee,
wala imani haiji kwa kujitahidi, Imani inakuja kwa kusikia, kwa kusoma kwa
kuliamini neno la Mungu, Mkuu wa Gereza pale Filipi aliuliza afanyeje ili aweze
kuokoka na Mtume Paulo alimjibu kuwa lazima amuamini Bwana Yesu Matendo 16:30-31,32 na hawakuishia hapo
bali aliendelea kumueleza neno la Mungu na ndipo alipoweza kuokoka yeye na
nyumba yake yote Matendo 16:30-32 “kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye
nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na
nyumba yako. Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani
mwake.” Maombi yetu nili
yaweze kuwa na nguvu vilevile yanahitaji imani Marko 11:24 “Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote
myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” Yohana 20: 31 Neno la Mungu
liliandikwa ili tupate kusadiki ya kuwa Yesu ni mwana wa Mungu Yohana 20:31 “Lakini
hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu;
na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.” Unaweza kuona kama sasa
tunahitaji imani katika kila eneo na katika maisha yetu hatuna budi kulisoma
neno la Mungu, hatuna budi kuliamini, iliimani zetu ziweze kupanda na
kutusaidia kutuletea wokovu, kuleta majibu ya maombi yetu na kutusaidia kumjua
Yesu na kumuamini tunahitaji neno la Mungu na ni neno la Mungu pekee linaloweza
kutusaidia kuwa na imani.
5. Neno
la Mungu lina Nguvu.
Ni muhimu kufahamu kuwa Neno la Mungu lina nguvu na
uweza wa ajabu, wakati ambapo tunapitia haki ngumu mno na haki za kukata tamaa
au magumu ya aina yoyote tusisite kulitamka neno la Mungu kwa sauti, litamke
neno kwa mamlaka kila hali inayokukabili kinyume na neno la Mungu itawekwa
sawa, Isaya 55:10-11 “Maana kama vile
mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha
ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye
chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu;
halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika
mambo yale niliyolituma”
Neno la Mungu lina Nguvu kama mstari wa
msingi usemavyo, Lina nguvu kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande, lina
nguvu kama moto, lolote na hali yoyote inayoonekana kuwa ngumu katika maisha
yetu, inaweza kusambaratishwa kupitia neno la Mungu, Yeremia 23:28-29 . “Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na
neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano?
Asema Bwana. Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo
mawe vipande vipande?”
6. Neno
la Mungu lina nguvu ya kusafisha.
Yohana
17:17 “Uwatakase kwa ile kweli;
neno lako ndiyo kweli.” Mungu
husafisha na kutakasa kupitia neno lake Waefeso
5:26-27. “ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa
maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi
wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa”, Yohana 15:3 “Ninyi
mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.” Neno
lina uwezo wa kusafisha maisha yetu, ikiwa tuna tatizo lolote neno la Mungu
linatuagiza kutubu kuungama na kuacha maovu yetu 1Yohana 1;9, “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni
mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu
wote.” na hali
kadhalika tunapaswa kuruhusu neno la Mungu kutusafisha na kututakasa.
7. Neno
la Mungu lina nguvu ya kujenga (the power to build up).
Matendo
20:32 “Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na
kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao
wote waliotakaswa.” Tunajifunza
hapa kuwa kumbe neno la Mungu lina uwezo mkubwa sana wa kutujenga, neno la
Mungu linanguvu ya kutujenga katika tabia na mwenendo wetu, Mungu anataka watu
wake wajengwe kupitia neno lake na ndio maana ametoa karama mbalimbali katika
kanisa ili kila mmoja ajengwe, kujengwa kwetu kuna mpango wa kutupeleka katika
ukamilifu “Maturity” hata tuweze kumfikia
Yesu Kristo Waefeso 4:11-13 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na
wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la
kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;
hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa
Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu
wa Kristo; ili tusiwe tena watoto
wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa
hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike
kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa,
Kristo.” Mungu anataka tuondoke katika hali ya uchanga na kufikia
ngazi ya kuwa walimu wa neno la Mungu, kamwe sio mpango wa Mungu sisi tudumae Waebrania 5: 12-14 “Ambaye tuna
maneno mengi ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa
mmekuwa wavivu wa kusikia. Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati
mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya
Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. Kwa maana kila
mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. Lakini
chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa
kupambanua mema na mabaya.” Tunawezaje kuondoka katika uchanga na
kuelekea katika ukomavu ni kwa kukubali kujifunza neno la Mungu, tukiwa wavivu
kujifunza neno la Mungu tutadumaa na hatutaweza kujengeka.Kwa msingi huo
tunapaswa kulitamani neno la Mungu kama tunavyotamani maziwa ili tuweze kukua 1Petro 2:2 “Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa
yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;”
ili tuweze kukua na kujengeka vema tunapaswa kulitamani nenola Mungu,
Mkristo wa kweli anapaswakujua kuwa hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno
litokalo katika kinywa cha Mungu, Neno la Mungu lina virutubisho vya kutosha
kutufanya kukua na kujengeka na kufikia kiwango ambacho Mungu amekusudia katika
maisha yetu.
8.
Neno la Mungu lina Nguvu ya kitupa furaha na amani.
Maisha yetu duniani yana changamoto nyingi sana,
kama hakungekuwa na neno la Mungu watu nwengi wangeweza kukata tamaa na
wasingeliweza kupata faraja ya aina yoyote, lakini ni kupitia neno la Mungu tunakuwa na amani na furaha, ya kweli
ujuzi wa kweli katika neno la Mungu unaweza kutusaidia na kutufanya tuwe na
amani wakati wote Yeremia 15:16 “Maneno yako
yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe
ya moyo wangu; maana nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana, Mungu wa majeshi.”
Neno la Mungu liliandikwa ili kutupa Matumaini kutufunza uvumilivu na
kutuletea faraja Warumi 15:4 “Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili
kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini”.
Unaona ndani ya maandiko kuna faraja na matumaini, tunapopita katika wakati
mgumu na wenye kukatisha tamaa tunaweza kukubaliana wazi kuwa Mungu hufanya
mambo yote katika kutupatia mema sisi tumpendao Warumi 8: 28 “Nasi twajua ya kuwa katika mambo
yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani,
wale walioitwa kwa kusudi lake.” Zaburi 85:8 Biblia inasema “Na nisikie atakavyosema Mungu Bwana, Maana atawaambia watu
wake amani, Naam, na watauwa wake pia, Bali wasiurudie upumbavu tena.”
9. Neno
la Mungu li hai tena lina nguvu (the word of God is alive and active)
Moja ya sifa kubwa
na ya kipekee kuhusu neno la Mungu ni pamoja na kuwa na uhai na tena
lina nguvu, Kwa wayahudi ilikuwa inaeleweka wazi kwamba ukitaja neno la Mungu
ni sawa na kumtaja masihi mwenyewe Yohana
1;1 “Hapo mwanzo kulikuwako
Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu” Neno la Mungu lina uhai maana yake ndani yake
kuna uwezo wa kumfanya mwanadamu aishi, maisha yetu na kuwepo kwetu hakutegemei
tu nguvu ya chakula bali tunaweza kuishi kwa neno la Mungu Mathayo 4:4 “Naye akajibu akasema, Imeandikwa,
Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.” Neno la Mungu halitakuja kufa wala
halitachakaa kila kitu kitapita lakini neno la Mungu halitapita kamwe Mathayo 7:24 “Mbingu
na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.” Ni neno la
Milele, ndani yake iko pumzi ya Mungu na hivyo linafanya kazi ndani ya
walioamini 1Wathesalonike 2:13 “Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa
kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si
kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli;
litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.” Neno la Mungu lina
uhai, lina nguvu, lina na lina uwezo wa kuponya Zaburi 107:19-20 “Wakamlilia Bwana katika dhiki
zao, Akawaponya na shida zao. Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika
maangamizo yao.” Kwa sababu hiyo kuna umuhimu mkubwa sana kwetu,
kulitegemea, kuliamini, kulisoma na kulitumia litumie katika hali yoyote na
mazingira yoyote kwa changamoto zozote zinazokukabili.
10. Neno la Mungu lina Nguvu ya kutufunulia siri kuu za
ulimwengu (Reveal philosophical question)
Mtaifahamu
kweli nayo itawaweka huru Yohana 8:32
“tena mtaifahamu
kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”
Neno la
Mungu lina nguvu ya kutufunulia na kutujuza maswala makubwa ya kifalsafa ambayo
tusingeweza kuyajua kwa akili za kawaida za kibinadamu, Maswali makubwa ya
ki-falsafa ni kama vile
a. Ulimwengu
uliumbwa na nani (Mwanzo 1-2, Waebrania
11:3)
b. Kwa nini
wanadamu wako hivi walivyo (Zaburi
146:6, Isaya 45:12)
c. Mungu ni
nani
d. Nini
kinatokea baada ya kifo (Waebrani 9:27)
e. Kwa nini mwanadamu
yuko Duniani
f.
Mwanadamu anawezaje kuishi duniani (Kumbukumbu la Torati 10:12)
Maswali
haya ya kifalsafa tungeweza kusoma na kusoma miaka na miaka, na mawazo mengi
yangetengenezwa kama “EVOLUTION THEORY”
na nyingine nyingi lakini zoyte zingebaki kuwa upuuzi kwa sababu zinashindwa
kutujulisha ukweli, Ni neno la Mungu tu linaloweza kutusaidia kujua na kujibu
maswali yote ambayo ulimwengu wa kawaida.
11. Neno la
Mungu lina nguvu ya kufuta Makosa (the
Power to refute).
Dunia
imaejaaa utetezi mwingi wa kijinga, wako wanaotetea Pombe, wako wanaotetea
zinaa, wako wanaotetea ushoga, wako wanaotetea uongo, wako wanaotetea, dhuluma,
wako wanaoona mambo yasiyo sawa kuwa yako sawa, katika ulimwengu hu tulio nao
wa sasa kamwe hatupasi kukubaliana na kila kinachopendekezwa na ulimwengu, ni
lazima tuliangalie neno la Mungu linasema nini na kukemea na kukaripia na
kuvunjialia mbali kila kinachoonekana kuwa sio tatizo wakati ni tatizo 2Timotheo 4:1-4 “Nakuagiza
mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na
waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; lihubiri neno, uwe tayari,
wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu
wote na mafundisho. Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye
uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi,
kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na
kuzigeukia hadithi za uongo” Mitume walilitumia neno la Mungu
kuilinda na kuitetea imani na kuwakemea kwa nguvu kubwa manabii au walimu wa
uongo, pia walilitumia kung’oa falsafa na imani potofu dhidi ya kanisa 2Petro 1:19-21 “Nasi
tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa
ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota
ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu. Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna
unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana
unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena
yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” Unaweza kuona
hivyo wanafunzi wa Yesu wana kila sababu ya kuliangalia neno na kuyatatuta
mapenzi yake na kilitafasiri kwa halali baada bya kulijifunza kwa kina ili
hatimaye waweze kuishindania imani Yuda
1:3-4 “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana
kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu
kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu
mara moja tu. Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa
tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi,
nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo”.
12. Neno la Mungu lina nguvu ya kutuandaa kwa wakati ujao
“get us ready for the feature
Maandiko
yana nguvu ya kutuandaa kwa wakati
ujao Yesu Kristo mwenyewe alisema ni
lazima tujiweke tayari Luka 12:40 “Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo
Mwana wa Adamu.” Neno la Mungu linaelezea wazi kuwa kuna siku
tutasimama mbele za nkiti cha hukumu ya Mungu, na kwa sababu hiyo hatuna budi
kuwa na ufahamu wa namna gani tunaweza
kujiandaa kukutana na Mungu, kwa hukumu,
tunawezaje sasa kujiandaa vema ni kwa kuliangalia neno, ni neno la Mungu
pekee lenye uwezo wa kutusaidia katika maandalizi yetu
Neno la
Mungu linaonyesha mpango wa Mungu wa ukombozi kupitia mwana wa Mungu Yohana 3:16
Neno la
Mungu linatuonyesha namna tunavyoweza kuwa na uzima wa milele na kuhukumiwa Yohana 3:17-18
Neno la
Mungu linatuelekeza namna tunavyoweza kumrudia Mungu kwa toba Matendo 2:37-38
Neno la
Mungu linatuandaa kwa kifo na ufufuo
Ni neno la
Mungu pekee linaloweza kutusaidia kutuandaa katika hali zote za maisha yetu,
swala kubwa la msinhgi na la muhimu sasa ni jinsi gani tunaweza kufurahia nguvu
za Neno la Mungu?
1. Ni lazima
tulisome Yoshua 1:5-8
2. Ni lazima
tulitii Zaburi 119:9
3. Ni lazima
tulihubiri na kulieneza Warumi 1:16
Neno la
Mungu lina nafasi pana ya kutusaidia na kutufanikisha katika maisha yetu
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!.