Wakolosai 2:16-17 “Basi,
mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au
mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili
ni wa Kristo.”
Waebrania 10:1 “Basi
torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo
hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo
wote kuwakamilisha wakaribiao.”
1Wakorintho 10:11 “Basi
mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi,
tuliofikiliwa na miisho ya zamani.”
Utangulizi:
Leo tutachukua muda kujifunza kwa kina
kuhusu kivuli cha mambo yajayo, ambayo ni picha kivuli cha picha halisi
tunazokutana nazo katika agano la kale zikimzungumzia Yesu Kristo kwa kina na
mapana na marefu, likiwemo kwa mfano tukio la Abrahamu kutaka kumtoa kijana
wake Isaka kama sadaka ya kuteketezwa baada ya kupewa maagizo hayo na Mungu na
kisha Malaika wa Bwana kumzuilia Abraham, na badala yake alimuonyesha kondoo aliyetolewa
kwa niaba ya Isaka tunaangalia kwa kina kuwa swala hili lina maana gani na
linatufundisha nini ukiacha tu kuwa Mungu alikuwa anamjaribu Abrahamu, Lakini
tunajifunza pia kumbe tukio hili kiunabii linamuhusu Yesu Kristo kuyafuatilia
matukio hayo kwa undani tutajifunza somo
hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-
·
Ufahamu
kuhusu alama za kinabii
·
Mifano
kadhaa ya alama za kinabii
·
Ishara ya Abraham kumtoa Isaka
Ufahamu
kuhusu alama za kinabii.
Ni muhimu kwa kila mwanafunzi wa neno
la Mungu kuwa na ufahamu kuwa katika agano la kale kulikuweko na matukio ambayo
kimsingi yalikuwa pia ni alama za kinabii, ambazo licha ya kutokea katika
maisha halisi ya wahusika lakini pia yalikuwa yanatabiri maswala kadhaa yajayo
katika maisha ya wahusika halisi kinabii, Mwalimu mkuu wa alama za kinabii
kimsingi alikuwa ni Yesu Kristo mwenyewe alama hizi kitaalamu zinaitwa TYPOLOGY ambalo limetokana na neno la
asili la kiyunani TYPOLOGIA neno hilo typology maana yake katika kiingereza ni – The study and interpretation of types and symbol or events,
originally especially from within the Bible. (TYPOLOGIA two Greek terminology Types and
Logos which means Studies about symbols) Kwa Kiswahili tunaweza kusema ni
somo linalohusu tafasiri ya alama, ishara na matukio ya kinabii, yenye asili ya
kibiblia hususani agano la kale ambayo yanahusu mambo yajayo kinabii. Kwa mfano
Israel walimuasi Mungu Jangwani na Mungu akaleta hukumu ya nyoka za moto yaani
nyoka wenye sumu kali na walianza kuwauma watu ona katika
Hesabu
21:6-9 “Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu,
wakawauma, watu wengi wakafa. Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi
kwa sababu tumemnung'unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa Bwana, atuondolee nyoka
hawa. Basi Musa akawaombea watu. Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya
shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.
Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma
mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.”
Unaona kimsingi hili ni tukio ambalo
lilikuwa tukio halisi kwa wana wa Israel walifanya dhambi walingung’unika Musa
na Mungu akatuma nyoka kama adhabu na watu wengi wakafa lakini walipomlilia
Musa Mungu alimuagiza Musa kutengeneza nyoka wa shaba na kumtundika juu ya
msalaba na kila aliyeumwa na nyoka alipomwangalia yule nyoka alipona, sasa
ingawa tukio hili ni halisi lakini Yesu analitafasiri kama ni alama ya kinabii
kumuhusu yeye ona :-
Yohana
3:14-15 “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka
jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye
awe na uzima wa milele katika yeye.”
Kwa msingi huo tunapata ufunuo kutoka
katika mtazamo wa Yesu kuwa kuna matukio katika maandiko hususani agano la kale
ambayo yalizungumza kumuhusu yeye au
kuhusu mambo yajayo japo yalikuwa ni matukio ya kawaida kutoka katika agano la
kale lakini yalikuwa yanazungumza jambo kuhusu masihi Yesu, mwenyewe na matukio
mengine muhimu ya kinabii, mfano mwingine tunajifunza kutioka kwa Yesu tena
kuhusiana na tukio la Nabii Yona (Yunus)
kumezwa na nyangumi ona tukio halisi na ona namna Yesu alivyokuja kulitumia
Yona
1:17 “Bwana akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze
Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana
na usiku.”
Tunaona hapa tukio halisi la Nabii
Yona (Yunus) kumezwa na nyangumi na
kuweko ndani ya samaki mkubwa kwa siku tatu usiku na mchana kwetu sisi ni tukio
halisi na la kawaida lakini tukio hili ni alama za kinabii linazungumza kuhusu
kufa na kufufuka kwa Yesu Msalabani siku ya tatu na ni Yesu mwenyewe ndiye aliyezungumza swala
hilo ona
Mathayo
12:39-41 “Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha
zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona. Kwani
kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi,
hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo
wa nchi. Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi
hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya
Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona.”
Mpaka hapo tunajifunza kuwa ingawa
manabii na watu maarufu katika agano la kale waliishi maisha yao ya kawaida na
kukatukia matukio ya kawaida kama stori tu za maisha yao, lakini kumbe kwa vile
walikuwa ni manabii, Roho Mtakatifu alikuwa akiwatumia kutabiri au kutupa
matukio na ishara muhimu kuhusu matukio muhimu yajayo na mengi kati ya hayo
yalikuwa yanamuhusu Yesu Kristo, kwa hiyo ukishaweka hili akilini utagundua
kuwa tukio la Ibrahimu Kumtoa Isaka kama sadaka ya kutekeketezwa na kisha
kukatokea Kondoo akatolewa kama mbadala wa Isaka vilevile uko ujumbe katika
shule za kinabii ya kuwa swala zima licha ya kuwa tukio la kawaida pia lilikuwa
ni tukio la kinabii linalo muhusu Yesu Kristo. Kama tutakavyoweza kuliona tukio
hilo kwa kina katika kipengele cha tatu;
Mifano
kadhaa ya alama za kinabii.
Kwa hiyo kama tulivyojifunza ya kwamba
kuna alama vivuli ambazo zinafunua mambo muhimu yajayo ni muhimu kufahamu ya
kuwa kuna Unabii, manabii na alama vivuli na hizi zote zilitumiwa na Mungu Roho
Mtakatifu ambaye ndiye mwasisi na msimamizi wa uandishi wa Biblia kufunua
maswala kadhaa muhimu ya kinabii na mengi yakiwa na uhusiano na ujio wa Masihi
Yesu Kristo ambaye ndiye wa Muhimu kuliko mambo yote, kwa hiyo watu, alama na
unabii unaweza kuletwa kwetu kutoka katika agano la kale kutupa picha hizo za
kinabii kama ninavyotaka kuonyesha baadhi ya nhizo hapa ambazo zote kitaalamu
tunaziita alama vivuli (Typology) na
maandiko yameweka wazi alama hizo na maana zake, Hata hivyo ni muhimu kufahamu
kuwa katika alama hizo vivuli zimegawanyika katika makundi makuu mawili yaani
Kivuli chanya na kivuli hasi (Type and
Antitype) :-
Mfano:-
1. Sikukuu za mwandamo wa mwezi (Iddi) - Katika tamaduni za kiyahudi kulikuwa na
sikukuu za kusheherekea mwezi mpya ambazo ziliitwa Rosh Chodesh au Rosh Hodesh
ambazo tafasiri yake kwa kiingereza ni new moon, yaani mwezi mpya ni sikukuu
walizozitumia kusheherekea mwanzo wa mwezi mpya katika kalenda ya kiyahudi na
zilisheherekewa kwa siku moja au mbili kutokana na kuandama kwa mwezi kama
mwezi ulikuwa na siku 29 au 30 sikukuu
hii inatajwa katika
Hesabu 28:11 “Tena
katika mianzo ya miezi yenu mtamsongezea Bwana sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng'ombe
waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa
kwanza, wakamilifu, saba;”
2Wafalme 4:22-23 “Kisha
akamwita mumewe, akasema, Tafadhali, uniletee mtu mmoja wa watumishi, na punda
mmoja, ili nimwendee yule mtu wa Mungu kwa haraka, nikarudi tena. Akasema, Kwa
nini kumwendea leo? Sio mwandamo wa mwezi, wala sabato. Akasema, Si neno.”
Kwa hiyo
utaweza kuona kuwa sikukuu hizo za mwandamo wa mwezi zilikuwepo, lakini sikukuu
hizi zilikuwa na maana ya kinabii kuhusu ujio wa masihi na ndio maana Yesu
alipokuja alijitambulisha kuwa yeye ndiye NURU
YA ULIMWENGU
Yohana 8:12 “Basi
Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye
hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”
Kimsingi
hapo Yesu alikuwa anaonyesha wazi kuwa mwandamo wa mwezi (Iddi) ilikuwa ni
alama kivuli cha ujio wa masihi, mwezi uliingia gizani na watu walifurahia kuiona
nuru kwa msingi huo basi Mwezi na mwandamo wa mwezi ni kivuli cha jambo halisi
na jambo hilo ni Yesu Kristo mwenyewe, jambo hilimlinawekwa wazi na vizuri
Zaidi na Paulo mtume akiwataka wakristo wasishituke watu wanapoandama mwezi na
sikukuu nyingine kwani zote zilikuwa ni unabii kumuhusu masihi ona
Wakolosai 2:16-17 “Basi,
mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au
mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili
ni wa Kristo.”
Unaona kwa
msingi huo mwandamo wa mwezi kwa wakristo hauna maana tena kwa sababu Nuru
halisi ni Yesu, na sabato haija maana tena kwa sababu pumziko halisi ni Kristo
kwa hiyo kupitia alama vivuli unapata neema ya kuuelewa ukristo katika agano
jipya kwa namna njema Zaidi, kwa namna hiyo sharia nyingi, sikukuu, na baadhi
ya stori au matukio katika agano la kale zilikuwa ni kivuli cha kumuhusu
masihi, zilikuja kwa kusudi la kuwandaa wana wa Israel kuna na ishara
zitakazosaidia kumtambua mwana wa Mungu ajaye ulimwenguni ambaye ni Bwana wetu
Yesu Kristo.
Waebrania 10:1 “Basi
torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo
hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo
wote kuwakamilisha wakaribiao.”
2.
Adamu – Adamu huyu
ndiye baba wa wanadamu wote kwa hiyo alikuwa ni kiongozi mkubwa sana duniani,
ni mwanadamu wa kwanza kuwa na uhusiano wa karibu sana na Mungu, lakini yeye
alisababisha dhambi na mauti kuingia ulimwenguni, ni nabii mkubwa sana lakini
Yesu tofauti na Adam yeye aliishinda dhambi na mauti na kufanikiwa kuwaongoza
wanadamu wote kuishi maisha ya haki na kuurithi uzima wa milelekwa hiyo Adamu
ni kivuli kisicho na ukamilifu cha ujio wa Yesu Kristo aliye mkamilifu, kwa
hiyo katika maandiko mitume wanamfananisha Adamu na Kristo katika mfanano
kinzani (Antitype). Adamu asiye
mkamilifu na Adamu aliye mkamilifu, adamu aliyesababisha mauti na adamu
aliyesababisha uzima, Adamu mwenye asili ya udongo na Adamu mwenye asili ya
mbinguni, Adamu aliyeleta mauti na Adamu aliyeleta Ufufuo.
1Wakorintho 15:45-48 “Ndivyo
ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni
roho yenye kuhuisha. Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye
huja ule wa roho. Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili
atoka mbinguni. Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na
kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni.”
1Wakorintho 15:21-22 “Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu,
kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu wote
wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.”
Warumi 5:14 - 17 “walakini
mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya
dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja. Lakini
karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja
wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake
mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi. Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya
dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja
ikaleta adhabu; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta
kuhesabiwa haki. Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa
sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa
cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.”
Kwa hiyo
Adamu ni alama kivuli –hasi, (Antitype)
cha Yesu Kristo sio katika ulinganifu wa mfanano bali katika ulinganifu
unaokinzana kutufundisha ya kwamba kama tutaishi kwa kumfuata mtu wa mwilini
tutakufa na kama tutaishi kwa kumfuata mtu wa rohoni tutaishi na kuwa na uzima
wa milele kimsingi Yesu ni Bora Zaidi kuliko Adamu.
3.
Abel –
Abel naye ni moja ya alama kivuli kizuri sana kumuhusu Yesu Kristo,
yeye ni mwana wa Adamu na aliuawa na ndugu yake aitwaye Kaini, kimsingi Yesu
Kristo alipokuwa akijitaja kama Mwana wa Adamu kinabii alikuwa akimaanisha yeye
ni mwana mpendwa wa Adamu atakayeuawa na ndugu zake na kumwaga Damu isiyo na
hatia, Habili aliuawa na ndugu yake kwa sababu tu ya wivu na husuda lakini
hakuwa ametendo kosa lolote Zaidi ya kutenda jema na kupata kibali kwa
Mungu ona
Mwanzo 4:9-11 “BWANA
akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi
wa ndugu yangu? Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia
kutoka katika ardhi. Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua
kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;”
Tunaona
mfanano mkubwa sana ulioko kati ya mwana wa Adamu Abeli na Mwana wa Adamu Yesu
Kristo, tofauti ni kwamba Damu yake Abeli ilipomwagika ilikuwa inadai haki
yaani kisasi, wakati Yesu Kristo ambeye ni bora Zaidi kuliko Kaini, yeye
tunaelezwa ya kuwa damu yake ilipomwagika ilidai Msamaha, rehema na kuleta
wokovu badala ya laana
Waebrania 12:24 “na
Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya
Habili.”
Waefeso 1:6-7 “Na
usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa. Katika
yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na
wingi wa neema yake.”
Kwa hiyo
unaweza kuona na kuthibitisha kimaandiko kuwa Mwana wa Adamu Abel ni alama
kivuli cha unabii cha Mwana wa Adamu Yesu Kristo ambao wote waouawa na ndugu
zao na kumwaga damu zao na damu zao
kunena maswala tofauti kwa jamii ya wanadamu.
4. Safina ya Nabii Nuhu – Safina
hiii nayo inatajwa katika maandiko kama ishara ya mwokozi Masihi Yesu Kristo,
yaani kama safina ile ilivyotumiwa na kumuokoa Nuhu na familia yake wakati
Mungu alipouhukumu ulimwengu kwa gharika, sasa Mungu anawaokoa watu wote
wanaomuamini Yesu Kristo, nje ya Yesu Kristo watu wote watashuhudia hasira ya
Mungu ya milele ona katika
1Petro 3:20-21 “watu
wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu,
safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane,
waliokoka kwa maji. Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku
hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za
Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.”
Neno mfano
wa mambo hayo ni ubatizo linamaanisha kuwa kilichotokea ni mfano kwa maana ya
safina iliyowaokoa ni Yesu Kristo na maji yaliyotumika kuwahukumu watu ni
ubatizo kwa mambo yajayo, na hapa Petro anazungumzia ubatizo unaohusiana na
kusafishwa kwa dhamiri, kwa wote wanaomuamini Yesu Kristo na kazi aliyoifanya
Msalabani, wote wanaomuamini wamebatizwa katika kazi aliyoifanya Kristo kwa
kufa na kufufuka.
1Wakorintho 12:12-13 “Maana
kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule,
navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. Kwa maana katika Roho
mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu
Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.”
Warumi 6:3-5 “Hamfahamu
ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti
yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi
kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo
na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyounganika naye
katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;”
5.
Melchizedeki
– Melkizedeki anajitokeza katika maandiko kama Mfalme wa salem (jina la zamani
la jiji la Yerusalem) na alikuwa kuhani wa Mungu aliyekutana na Abraham katika
Mwanzo 14 na Ibrahimu alimuheshimu na kumpa sehemu ya kumi (Zaka) ya mateka
yake
Mwanzo 14:17-20 “Abramu
aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye,
mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme.
Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa
Mungu Aliye juu sana. Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye
juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia
adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.”
Moja ya
kitu kinacholeta upekee wa mfalme huyu Malkizedeki ni kuwa alikuwa Mfalme na
kuhani wa Mungu aliye juu sana, katika tamaduni za Israel majukumu hayo
yalitenganishwa, Mfalme hakuwa kuhani na kuhani hakuwa mfalme, Wafalme wa
Kiyahudi walitoka katika ukoo wa Daudi tu, na Makuhani walitoka katika ukoo wa
Haruni pekee, aidha maana na jina Melkizedeki tafsiri ya jina lake kwanza ni
mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; hana baba,
hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake,
bali amefananishwa na Mwana wa Mungu. Na Roho mtakatifu anaruhusu kuhani huyu
katika agano la kale atokee tu bila kuelezea historia yake kwa undani maandiko
pia yana maneno ya unabii wa kuja kwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki
Zaburi 110:1-4 “Neno
la Bwana kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui
zako Kuwa chini ya miguu yako. Bwana atainyosha toka Sayuni Fimbo ya nguvu
zako. Uwe na enzi kati ya adui zako; Watu wako wanajitoa kwa hiari, Siku ya
uwezo wako; Kwa uzuri wa utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao umande wa
ujana wako. Bwana ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano
wa Melkizedeki.”
Unabii huo
unamuhusu Yesu Kristo ambaye ana cheo cha Ufalme na ukuhani kwa pamoja, na
unabii huo tafasiri ya jina la Melkizedeki na kitendo cha Abrahamu kumpa zaka
kunathibitisha ya kuwa kuhani huyu ni wa ngazi ya juu sana na hivyo kinabii
Malkizedeki ni alama kivuli cha Yesu Kristo ambaye ni kuhani mkuu aliyebora
Zaidi ya Melikizedeki ona
Waebrania 7: 14-17 “Maana
ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena
neno lo lote juu yake katika mambo ya ukuhani.Tena hayo tusemayo ni dhahiri
sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki; asiyekuwa
kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio
na ukomo; maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa
Melkizedeki.”
Roho
Mtakatifu hajatupa tena historia ya Melkizedeki kuzaliwa kwake na mwisho wake ili
asimame kama alama ya kivuli cha kinabii kumuhusu Yesu kristo ambaye ni kuhani
mkuu milele na mfalme kwa mfano wa Melkizedeki
6.
Ngazi ya
Yakobo – Ngazi ya Yakobo nayo inasimama kama alama kivuli cha kinabii
kumuhusu Yesu Kristo nah ii ni kwa mujibu wa ufafanuzi wa Yesu Kristo mwenyewe,
awali tunaona katika maandiko kwamba Yakobo alipokuwa akienda Haran njiani
alipokuwa amepumzika aliona maono kuwa kuna ngazi kubwa ambayo imeegamizwa
mbinguni na katika ardhi aliyokuwa amepumzika na malaika walikuwa wakipanda na
kushuka ona katika
Mwanzo 28:10-15 “Yakobo
akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulani akakaa huko usiku
kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale
akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. Akaota ndoto; na
tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena,
tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, BWANA
amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na
Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako
utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki,
na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za
dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako,
nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata
nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.”
Unaweza
kuona katika tulio ili iko ngazi iliyokuwa imesimamishwa juu ya nchi na ncvha
yake inafika mbinguni, na malaika
walikuwa wakipanda na kushuka kama Yesu asingelisema lolote kungekuwa na
tafasiri nyingi sana kuhusu ngazi ya Yakobo lakini kumbe Yesu alikuwa Mwalimu
mzuri sana wa alama vivuli yeye alisema maneno haya
Yohana 1:47-51 “Basi
Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli
kweli kweli, hamna hila ndani yake. Nathanaeli akamwambia, Umepataje
kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini
ya mtini nilikuona. Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe
Mfalme wa Israeli. Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona
chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya. Akamwambia, Amin,
amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na
kushuka juu ya Mwana wa Adamu.”
Kitendo
cha Yesu kunukuu kuhusu tukio lile na kuwahakikishia wanafunzi wake hususani
Nathanael kuwa Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na
kushuka juu ya mwana wa Adamu hii ilikuwa ni Dhahiri kuwa Yesu alikuwa akiweka
wazi kuwa ngazi ile ilikuwa ni alama kivuli kuhusu ngazi halisi ambaye ni
Kristo unaona! Nathaniel na wanafunzi wengine wamekuzwa wakiwa wanafahamu stori
za agano la kale na labda walielewa kuhusu hii ngazi kwa hiyo kwa haraka
wanapata ujumbe kuwa Yesu ndiye njia ya mbinguni
Yohana 14:6 “Yesu
akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa
njia ya mimi.”
7. Yusufu - hakuna mtu amewahi kumtaja Yusufu,
kama alama kivuli cha Yesu Kristo lakini kutokana na uzoefu wetu wa kujifunza
neno la Mungu sasa unaweza kuelewa alama kivuli zote ambazo ziko katika
maandiko hata kama hakuna mtu amezitaja mahali kwengineko katika maaandiko,
unapoyachunguza maisha ya Yusufu utaweza kuona kuwa kuna maswala kadhaa ambayo
yanafanania, Yusufu alichukiwa na Ndugu zake, na aliuzwa kule Misri, na
alipokuwa Misri alisingiziwa mambo ya uongo na kufungwa, baada ya kutafasiri
ndoto ya farao kuhusu maswala yajayo ndipo Farao akampandisha kuwa msaidizi
mkuu wa mfalme, ambapo baadaye alikuja kuwa mwokozi wa familia yake unawezaje kujua kuwa Yusufu alikuwa pia ni
alama kivuli cha Yesu Kristo?
o
Alikuwa ni
wa Uzao wa Ibrahimu ambaye kupitia yeye mataifa mengine walibarikiwa Mwanzo
41:53-57 “Miaka ile saba ya shibe ikaisha katika
nchi ya Misri, ikaanza kuja miaka ile saba ya njaa, kama vile Yusufu
alivyosema. Kukawa na njaa katika nchi zote, bali katika nchi yote ya Misri
palikuwa na chakula. Na nchi yote ya Misri ilipoona njaa, watu walimlilia Farao
awape chakula. Farao akawaambia Wamisri wote, Enendeni kwa Yusufu;
atakavyowaambia, fanyeni. Njaa ikawa katika dunia yote pia. Yusufu akazifungua
ghala zote, akawauzia Wamisri. Njaa ikawa nzito katika nchi ya Misri. Watu wa
nchi zote wakaja Misri kwa Yusufu; ili wanunue nafaka; kwa sababu njaa imekuwa
nzito katika dunia yote.”
Mwanzo
22:16-18 “ akasema,
Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala
hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika
kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko
pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa
yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.”
Leo hii Yesu mwana wa Ibrahimu amekuwa Baraka kubwa kwa mataifa
yote, Yusufu alikuwa mwana mpendwa wa Yakobo baba yake, Yesu naye ni mwana
mpendwa wa pekee Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata
akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa
milele.”
Yusufu alifanyika masikini, kama Kristo naye 2Wakorintho 8:9 “Maana mmejua neema ya
Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa
tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake”.
Yusufu alichukiwa na ndugu zake kwa sababu ya ndoto zake ya kuwa
atawatawala na kuwa watamsujudia
Mwanzo
37:4-8 “Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao
anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia, wala hawakuweza kusema naye kwa
amani.Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia;
akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. Tazama, sisi tulikuwa
tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama,
miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. Ndugu zake wakamwambia,
Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa
ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake.”
Ilitokea hivyo kwa Yesu, Wayahudi walimchukia ili asiwatawale Luka 19:14 “Lakini
watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki
huyu atutawale.”
Hatimaye ndugu wa Yusufu walikuja kumsujudia ingawa hapo awali
walimkataa na kumdhuru, hali kama hiyo ilimtokea Yesu Kristo ambaye wayahudi
walimtoa mikononi mwa wenye dhambi ili auawe lakini maandiko yanasema wazi kuwa hatimaye siku moja watamkubali na kumuabudu
wakiamini kuwa ndiye masihi wao
Zekaria
12:10 “Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi,
na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye
walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa
pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa
ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.”
Warumi
11:26-27 “Hivyo Israeli wote wataokoka; kama
ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia
yake.Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao.”
Yusufu na Yesu wote walisalitiwa na ndugu zao (Wayahudi) na wote
waliuzwa kwa vipande vya fedha
Mwanzo
37:28 “Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi
wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika, wakamwuza Yusufu kwa
Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri.”
Mathayo
26:15 “akasema,
Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya
fedha.”
Yusufu
aliinuliwa sana huko Misri na kila kitu kiliwekwa chini ya utawala wake
isipokuwa Farao tu
Mwanzo
41:40 “Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na
kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu
kuliko wewe.”
Tunaelezwa katika maandiko pia ya kuwa Yesu Kristo kama yanenavyo
maandiko ameinuliwa juu ya kila kitu na kila kitu kimewekwa chini ya utawala
wake
1Wakorintho 15:27 “Kwa
kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote
vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.”
Yusufu alilia kwaajili ya ndugu zake Mwanzo 45:2 “Akapaza sauti yake akalia,
nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia.” Yesu
Kristo naye alilia kwaajili ya Wayahudi Luka
19:41 “Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia,”
Yusufu aliokoa maisha ya wote waliomjia kwa msaada ikiwemo watu wa
mataifa mengi ya dunia waliokutwa na njaa,
Mwanzo
41:57 “Watu wa nchi zote wakaja Misri kwa Yusufu;
ili wanunue nafaka; kwa sababu njaa imekuwa nzito katika dunia yote.”
Yohana
3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali
awe na uzima wa milele.”
Kwa hiyo tunaweza kukubaliana kuwa Maisha ya Yusufu yaakisi kuwa
ni alama kivuli cha maisha yanBwana Yesu kwetu hata kama hakuna nukuu ya aina
hiyo katika maandiko, hizi alama vivuli zimekuwepo na kadhaa zimefunuliwa ili
kutusaidia kutufunulia aina nyinginezo kwa sababu unabii wote ulimuhusu Yesu
Kristo.
8. Musa nabii – Musa naye ni alama kivuli cha Yesu
Kristo, yeye ni mjumbe wa agano la kale
wakati Yesu Kristo ni mjumbe wa agano jipya na neno la Mungu linaweka wazi kuwa Mungu
angeinua nabii mwingine mfano wa Musa na Mungu aliamuru asikilizwe
Kumbukumbu 18:15-19 “Bwana,
Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi;
msikilizeni yeye.Kama vile ulivyotaka kwa Bwana, Mungu wako, huko Horebu, siku
ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya Bwana, Mungu wangu, wala
nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa. Bwana akaniambia, Wametenda vema
kusema walivyosema. Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano
wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote
nitakayomwamuru. Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule
kwa jina langu, nitalitaka kwake.”
Kwa kuwa
nabii huyu alitabiriwa ni wazi kuwa wayahudi walikuwa wakimtazamia kama masihi
na kumgojea kwa hamu kubwa sana
Yohana 6:14 “Basi
watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule
ajaye ulimwenguni.”
Katika
ulinganifu wa ubora wa Musa na Yesu Kristo mwandishi wa kitabu cha Waebrania
anamfananisha Musa kama mtumishi mwaminifu katika nyumba ya Mungu na Yesu kama
Mwana mwaminifu katika nyumba ya Mungu
§ Musa alikuwa
kama mtumishi mwaminifu katika nyumba ya Mungu wakati Yesu Kristo ni Mwana muaminifu katika nyumba ya Mungu. Waebrania 3:5-6 “Na
Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe
ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye; bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba
ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu
na fahari ya taraja letu mpaka mwisho.”
§ Musa
kulinganishwa na Kristo ni sawa na kulinganisha
nyumba na mjenzi wa Nyumba Yesu ndiye mjenzi wa nyumba na ni Mungu Waebrania 3: 3-4 “.Kwa
maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile
yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba. Maana kila
nyumba imetengenezwa na mtu; ila yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu.”
§ Musa alikuwa
ni kiongozi mkuu mwenye kuheshimika sana mwenendo wake na mapito ya maidha yake
ni alama kivuli cha maisha halisia na unabii halisia kumuhusu Yesu Kristo:-
§ Ukuu wa Nabii Musa.
Ø Alikuwa mtoto
wa kifalme (Nyumbani kwa Farao Misri)
Mrithi
mtarajiwa wa Farao
Aliishi kama
mtu maalumu (Prince) miaka 40 ikulu
Ø Alikuwa
mchungaji wa kondoo jangwani
Alijinyenyekeza
Alipata mateso
magumu ya jangwani, upweke na kuwa mbali na ndugu
Aliishi kama
tu duni miakla 40 jangwani
Ø Alikuwa
kiongozi wa taifa la Israel
Aliishi kama
Mtumishi wa Mungu miaka 40.
Alionyesha
njia,Nguvu za Mungu
Aliandika neno
la Mungu (Sheria) Mungu ana tumia mtu duni.
§ Ukuu wa Yesu Kristo.
Ø Alikuwa mtoto
wa kifalme Mbinguni
Mrithi wa
Mungu
Alikuwako
tangu milele na milele
Ø Alijinyenyekeza
Duniani
Aliteswa Msalabani,alikuwa
mpweke mpaka msalabani
Aliishi kama mtu duni
Ø Amekuwa kichwa
cha Kanisa
Ametunukiwa
jina lipitalo majina yoote
Ametupa Neno
la uzima wa milele (Injili)..
Kufanana Kwa Musa na Yesu Kristo Kihuduma na kimapito
1. Woote walikuwa
viongozi
2. Woote
walikataliwa na watu wao Kutoka 2: 14 “Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na
mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa
akaogopa, akasema, Kumbe! Jambo lile limejulikana., Yohana 1:11 “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.”
3. Woote
walijaribiwa jangwani Hesabu 20: 3-4 “Watu wakashindana na Musa, wakanena, wakisema,
Ingalikuwa heri kama tungalikufa wakati ule ndugu zetu walipokufa mbele za
Bwana! Mbona mmewaleta kusanyiko la Bwana hata jangwa hili ili tufe huku, sisi
na wanyama wetu?” Luka 4:1-2 “Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi
kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, akijaribiwa
na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa.”
4. Woote waliitwa
Manabii na walifananishwa kinabii Torati
18:18 “Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa
ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye
atawaambia yote nitakayomwamuru.” Luka 24:19 “Akawauliza, Mambo gani?
Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo
katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote;”
Pamoja na kuwa
Yesu ana maswala yanayofanana na Musa kihuduma ama kimapito Bado mwandishi wa
kitabu cha waebrania anawaonyesha wakristo wa kiebrania kuwa Yesu ni Bora zaidi
ya Musa ambaye ni nabii kivuli cha Kristo..
9. Kondoo wa Pasaka
- Mwana kondoo wa Pasaka aliyekuwa anachinjwa na jamii ya wayahudi pia
alikuwa ni alama kivuli cha Yesu Kristo, hususani siku ile Wayahudi walipokuwa
wanatolewa Misri, Mungu aliwahukumu wamisri kwa kuua kila mzaliwa wa kwanza
kama tu hakukuwa na Damu ya mwana kondoo katika miimo ya malango yao, na wale
waliokuwa wameweka alama ya damu ya mwana kondoo Malaika wa kuharibu alipoiona
alama ya damu hakuleta madhara katika nyumba hiyo Angalia
Kutoka 12:3-14
“Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku
ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya
baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja; na ikiwa watu wa nyumba ni
wachache kwa mwana-kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake
na watwae mwana-kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji
wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana-kondoo.
Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo
au katika mbuzi. Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na
kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni. Nao watatwaa baadhi ya
damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika
zile nyumba watakazomla. Watakula nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni,
pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena pamoja na mboga zenye uchungu. Msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini, bali
imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani. Wala
msisaze kitu chake cho chote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata
asubuhi mtakichoma kwa moto. Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu,
mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa
haraka; ni pasaka ya BWANA. Maana
nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza
wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu
ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.
Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami
nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu,
nitakapoipiga nchi ya Misri. Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi
mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu
vyote, kwa amri ya milele” Mwana kondoo huyu alikuwa ni alama kivuli cha ujio wa
Yesu kristo ona
Yohana 1:29 “Siku ya pili
yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu,
aichukuaye dhambi ya ulimwengu! ”
Katika siku
ile ya pasaka wana wa Israel
hawakutakiwa kula au kupika au kuingiza chochote chenye chachu, Na Paulo mtume
anaeleza moja kwa moja kuwa Yesu ndiye Kondoo wa pasaka aliyechinjwa kwa niaba
yetu na kuwa tunapaswa kuondoa chachu yote chahu hapa inasimama kwa niaba ya
dhambi
1Wakorintho 5:7 “Basi,
jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile
mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka,
yaani, Kristo;”
10. Mana (Mkate ushukao kutoka juu) - Wote tunakumbuka jinsi ambavyo Mungu aliwalisha nwana
wa Israel kwa mikate au keki maalumu kutoka mbinguni walipokuwa safarini
jangwani, baada ya malalamiko kuwa hawana chakula, Mungu aliwapa chakula hicho
cha ajabu ambacho walikihoji kuwa hiki ni nini MANHU kwa kiebrania au MANNA
maana yake hiki nini mkate huu ulioshuka kutioka mbinguni ulikuwa ni alama
kivuli kumuhusu Yesu kristo
Kutoka 16:4 “Ndipo BWANA
akamwambia Musa, Tazama, mimi nitawanyeshea ninyi mvua ya mkate kutoka
mbinguni; na hao watu watatoka nje na kuokota kila siku sehemu ya siku; ili
nipate kuwajaribu, kwamba watakwenda katika sheria yangu, ama sivyo.”
Yohana 6:31-35 “Baba zetu
waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili
wale. Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa chakula
kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho
mbinguni. Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na
kuupa ulimwengu uzima. Basi wakamwambia, Bwana, sikuzote utupe chakula hiki.
Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa
kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.”
Kama wana wa
Israel walivyoishangaa mana ndivyo walivyoshangaa kuhusu Yesu Kristo awezaje
nabii kutoka Galilaya? Aidha mana ilikuwa inafundisha kuwa ni Mungu ndiye
anayeweza kuwapa watu mahitaji yao na kutunza maisha yao na ni kupitia Mungu
tunapata wokovu na uzima wa milele kama tutamwamini Bwana Yesu, mana ilikuwa ni
alama kivuli tu Yesu ndiye mkate wa uzima.
11.
Kuhani mkuu - Kuhani mkuu katika agano la kale naye alikuwa
ni picha au alama kivuli kumuhusu Yesu Kristo, makuhani katika agano la kale
ndio waliokuwa wakifanya kazi ya upatanishi kati ya Mungu na wanadamu,
waliwaombea watu, walitoa sadaka za kuteketeza, na miongoni mwa makuhani mmoja
alikuwa nachaguliwa kuwa kuhani mkuu kutoka ukoo wa Haruni, Maandiko ynatuambia
kuwa Yesu ndiye kuhani wetu mkuu na ndiye mpatanishi kati ya Mungu na wanadam,
ingawa tofauti na makuhani wengine yeye alikuwa mkamilifu na hakutenda
dhambi, na Zaidi ya yote anaishi milele
Waebrania 4:15-16 “Basi,
iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na
tuyashike sana maungamo yetu. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana
nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi
katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa
ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.”
Waebrania 7:26-27 “Maana ilitupasa sisi tuwe
na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na
waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu; ambaye hana
haja kila siku, mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa
ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za hao watu; maana
yeye alifanya hivi mara moja, alipojitoa nafsi yake.”
12. Pazia la Hekalu - Pazia la patakatifu pa
patakatifu ambalo lilitenganisha patakatifu pa Hekalu na mwanzio katika hema ya
kukutania pia ni alama kivuli kumuhusu Yesu Kristo, Pazia hili lilipatenga
patakatifu na Patakatifu pa patakatifu, yaani eneo ambalo kulikuwa na uwepo wa
Mungu au mahali ambapo palikuwa na uwepo wa Mungu, kuhani mkuu angaingia mara
moja kwa mwaka kutoa dhabihu ya dhambi siku ya upatanisho, Lakini siku
aliyokufa Yesu Kristo moja ya jambo la kushangaza ni kuwa Pazia lile la Hekalu
lilipasuka, kuashiria kuwa kizuizi cha kuufikia uwepo wa Mungu kimeondolewa,
Mathayo 27:51-54 “Na
tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi
ikatetemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya
watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka
kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi. Basi yule akida, na hao
waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo
yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
Kwa mujibu wa
mwandishi wa kitabu cha Waebrania Pazia lile la Hekalu ni Mwili wa Yesu Kristo
ambao uliposulubiwa ulitoa nafasi ya watu kuufikia uwepo wa Mungu ambao
ulizuiwa katika nyakati za agano la kale
Waebrania 10:19-20 “Basi,
ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile
aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake;”
Unaona kwa
hiyo Pazia ni Alama kivuli cha kinabii kuhusu Mwili wa Kristo.
13. Kiti cha Rehema - Kiti cha rehema
ambacho kilikuwa juu ya sanduku la agano kimsingi nacho ni alama kivuli kumhusu
Yesu Kristo, Kiti cha Rehema ndicho ambacho kilikuwa kinatoa rehema na
upatanisho kati ya Wanadamu na Mungu
Warumi 3:25 “ambaye Mungu
amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe
haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote
zilzotangulia kufanywa.”
Katika kiti
cha Rehema kuhani mkuu angenyunyiza Damu ya Mwanakondoo na Mungu angeiona damu
hiyo na angetoa ruhusa na kumkubali kuhani mkuu kuomba kwaajili ya watu, Yesu
ndiye kiti cha rehema klwa sababu Mungu anapoiona damu yake aliyoimwaga pale
Msalabani anatupa neema ya kukaribia katika kiti chake cha enzi na katika uwepo
wake!
14. Siku ya sabato. - Sabato nayo ni moja ya
alama kivuli kumuhusu Yesu Kristo na kazi yake aifanyayo kwa wanadamu na katika
mioyo ya wanadamu, Sabato inaadhimishwa kuanzia ijumaa jioni na kuisha siku ya
jumamosi jioni, Sabato iliwataka wayahudi wote kupumzika na kuacha kufanya kazi
zao na kumuabudu Mungu
Kutoka 20:8-11 “Ikumbuke
siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini
siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote,
wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako,
wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa
siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo,
akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.”
Lakini kwa
habari ya sabato Paulo Mtume anasema hivi Wakolosai
2:16-17 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula
au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo
hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.”
Kulikuwa na
walimu wa uongo katika kanisa la Kolosai ambao waliwataka waamini kuendelea
kuishika sabato, Paulo anawajulisha kuwa Sabato ilikuwa ni kivuli tu cha Yesu
Kristo ambaye yeye ni pumziko la kweli la wanadamu na kwa kuwa Kristo amekuja
ambaye ni picha halisi, wakristo hawahitajiki tena kusihika sabato, Sabato
inatukumbusha kuwa sisi sio Mungu na hivyo hatuwezi kufanya kazi siku zote na
tunahitaji mapumziko, na hivyo hatupaswi kuwa watumwa wa sabato
Marko 2:27-28 “Akawaambia,
Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato.
Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.”
Kwa hiyo ni
ndani ya Yesu Kristo ndiko ambako wanadamu wanaweza kupata pumziko halisi Mathayo 11:28-30 “Njoni
kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa
moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo
wangu ni mwepesi.”
15.
Miji ya
makimbilio.
Miji ya
makimbilio katiika agano la kale ilikuwa pia ni alama kivuli cha Yesu Kristo,
Kwa mujibu wa Torati ya Musa, Mungu alimuelekeza kuwa atenge miji sita ili
kwamba kama mtu ameua mtu mwingine kwa makusudi au kwa kutokukusudia akimbilie
kwenyo moja ya mji wa makimbilio kwa usalama wake ili asije akauawa na watu
wanaotaka kujilipizia kisasi cha damu kwa sababu maelekezo ya Mungu ni kuwa mtu
atakayemwaga danu ya mwanadamu naye atauawa
Mwanzo 9:5-6 “Hakika damu
yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa
mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu.
Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana
kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.”
Kwaajili ya
kuwalinda watu hao kabla kesi zao hazijajulikana kuwa waliua kwa bahati mbaya
au kwa kukusudia iliwekaa miji ya makimbilia ambako mtu angekaa humo angekuwa
salama na sii ryhusa kumuua isipokuwa kama atakuwa ametoka nje ya mji huo wa
makimbilio
Hesabu 35:6 “Na hiyo miji
mtakayowapa Walawi, itakuwa miji sita ya makimbilio, mtakayoweka kwa ajili ya
mwenye kumwua mtu, ili akimbilie huko; pamoja na hiyo mtawapa miji arobaini na
miwili zaidi.”
Hesabu 35:11-13 “Ndipo
mtajiwekea miji iwe miji ya makimbilio kwa ajili yenu; ili kwamba mwenye kumwua
mtu, pasipo kukusudia kumwua, apate kukimbilia huko. Na hiyo miji itakuwa kwenu
kuwa makimbilio, kumkimbia mwenye kutwaa kisasi, ili asiuawe mwenye kumwua mtu,
hata atakaposimama mbele ya mkutano ahukumiwe. Na hiyo miji mtakayowapa itakuwa
kwenu ni miji sita ya makimbilio.”
Mwandishi wa
kitabu cha waebrania anakuja kuweka wazi kuwa miji hiyo ya makimbilia ilikuwa inamwakilisha Yesu
kristo, kwamba usalama wetu unategemea sisi kuwa ndani ya Yesu na sio
vinginevyo, nje ya Kristo ni rahisi kupatwa na madhara na ni rahisi kuuawa ona
Waebrania 6:18-20 “ili kwa
vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema
uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale
yawekwayo mbele yetu; tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye
nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia, alimoingia Yesu kwa ajili yetu,
mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.”
Mwandishi wa
kitabu cha weaebrania anaonya hatari ya
kukengeuka na kuwa mbali na neema ya Mungu, na kisha baadaye anajadili
ujasiri tulio nao endapo tutamkimbilia Bwana Yesu ambaye ni bora Zaidi ya mji wa makimbilio,
wote tunafahamu kuwa mshahara wa dhambi ni mauti bali karama yaani zawadi atoayo
Mungu kama tunamuamini Yesu ni uzima wa milele
Warumi 6:23 “Kwa maana
mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika
Kristo Yesu Bwana wetu.”
16. Ule Mwamba 1Wakorintho
10:1-4 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose
kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya
bahari; wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; wote
wakala chakula kile kile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho;
kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni
Kristo.”
Paulo mtume
anapoelezea kuhusyu mwamba wa roho uliowapa kinywaji cha roho wana wa Israel
kule jangwani katika habari hii ambayo ilijulikana vizuri sana na wayahudi,
kwamba Musa aliwapa wana wa Israel maji kutoka katika mwamba kwa maelekezo ya
Mungu baada ya kuugonga mwamba
Kutoka 17:1-7 “Mkutano
wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama
BWANA alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe. Kwa
hiyo hao watu wakateta na Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia,
Kwani kuteta na mimi? Mbona mnamjaribu BWANA? Watu wakawa na kiu huko; nao
wakamnung'unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi
na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu? Musa akamlilia BWANA, akisema,
Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe.BWANA akamwambia
Musa, Pita mbele ya watu, ukawachukue baadhi ya wazee wa Israeli pamoja nawe;
na ile fimbo yako ambayo uliupiga mto kwayo, uitwae mkononi mwako, ukaende.
Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe
utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo
mbele ya wazee wa Israeli. Akapaita mahali pale jina lake Masa, na Meriba; kwa
sababu ya mateto ya wana wa Israeli, na kwa sababu walimjaribu BWANA, wakisema,
Je! BWANA yu kati yetu au sivyo? ”
Hesabu 20:2-13 “Na hapo
hapakuwa na maji kwa ule mkutano; wakajikusanya juu ya Musa na juu ya
Haruni.Watu wakashindana na Musa, wakanena, wakisema, Ingalikuwa heri kama
tungalikufa wakati ule ndugu zetu walipokufa mbele za Bwana! Mbona mmewaleta
kusanyiko la Bwana hata jangwa hili ili tufe huku, sisi na wanyama wetu? Na
mbona mmetupandisha kutoka Misri ili kutuleta hata mahali hapa pabaya? Si mahali
pa mbegu, wala tini, wala mizabibu, wala makomamanga; wala hapana maji ya
kunywa. Musa na Haruni wakatoka pale palipokuwa mkutano, wakaenda hata mlangoni
pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa Bwana ukawatokea. Bwana
akasema na Musa, akinena, Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni
ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe
utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama
wao. Musa akaitwaa hiyo fimbo kutoka mbele za Bwana kama alivyomwamuru. Musa na
Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi
waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu? Musa akainua mkono wake akaupiga
ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na
wanyama wao pia. Bwana akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi,
ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo,
hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa. Maji haya ni maji ya
Meriba; kwa sababu wana wa Israeli waliteta na Bwana, naye alijionyesha kuwa
mtakatifu kati yao.”
Unaona ingawa
wana wa Israel walikunywa maji halisi kutoka katika mwamba ule kwa muujiza
uliofanywa na Musa baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Mungu, Paulo mtume
anasema mwamba ule ni Yesu, Mwamba huu uliowafuta na kuwapa Maji ulipigwa ili
kutioa maji yaliyowapa uzima wana wa Israel ilikuwa ni Picha ya kusulubiwa Kwa
Yesu Kristo ambako kumeleta ukombozi wa mwanadamu, Kwa hiyo ni wazi kuwa wakati
wana wa Israel wanapewa maji kutioka katika mwamba huo uliokuwa ukiwafuata
mwamba ule ulikuwa ni Yesu Kristo ambao wao walikuwa wakimtazamia kinabii,
mwamba ni picha ya maandalizi ya ujio wa masihi.
17.
Daudi. - Daudi naye anasimama kama alama kivuli cha
kinabiii kumuhusu Yesu Kristo, Maandiko
yanaonyesha wazi kuwa Yesu alitabiriwa kuwa mwana wa Daudi na anaitwa hivyo
ilitabiriwa kuwa ni Mwana wa Daudi atakayetawala katika kiti cha Enzi cha Daudi
baba yake katika Israel na ulimwengu mzima kwa ujumla, hata hivyo wakati
mwingine katika maandiko pia Bado Yesu anaitwa Daudi ona Ezekiel 37;24 “Na mtumishi wangu, Daudi,
atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja; nao wataenenda
katika hukumu zangu, na kuzishika amri zangu, na kuzitenda.”
Kwaajili ya
unabii huu wanatheolojia wengine wanadhani ya kuwa labda Mungu atamfufua Daudi
aje atawale wakati wa utawala wa miaka 1000 duniani milemium, ingawaje hapa
Mungu anatumia jina Daudi akimaanisha Masihi Yesu Kristo ambaye ni Mwana wa
Daudi
Yeremia 23:5-6
“Tazama siku zinakuja, asema Bwana,
nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa
hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi.Katika siku zake Yuda
ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana
ni haki yetu.”
18. Sulemani – Sulemani naye
anasimama kwa niaba ya Yesu Kristo kama alama kivuli, mapema Mungu alikuwa
amefanya agano na Daudi kwamba hatakosa
mtu wa kukaa katika kiti chake cha enzi milele
1Wafalme 8:24-25 “Umemtimizia
mtumishi wako, Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidia; naam, ulinena kwa kinywa
chako, ukayatimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo. Na sasa, Ee Bwana, Mungu wa
Israeli, umfikilizie mtumishi wako, Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidia,
ukisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli
machoni pangu, kama watoto wako wakiangalia njia zao, ili kuenenda mbele zangu
kama wewe ulivyoenenda.”
1Nyakati 17:11-14 “Hata
itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende na babazo, nitainua mzao wako nyuma
yako, atakayekuwa wa wana wako; nami nitaufanya imara ufalme wake. Yeye ndiye
atakayenijengea nyumba, nami nitakifanya imara kiti cha enzi cha ufalme wake
milele. Nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; wala sitamwondolea fadhili
zangu, kama nilivyomwondolea yeye aliyekuwa kabla yako; ila nitamstarehesha
katika nyumba yangu na katika ufalme wangu milele; na kiti chake cha enzi
kitathibitishwa milele.”
Kimsingi mwana
wa Daudi aliyeketi kwenye kiti cha enzi cha Daudi ni Sulemani katika namna
nyembamba au fikira finyu lakini katika namna pana Mwana wa Daudi aliyeketi
kwenye kiti cha Enzi milele ni Yesu Kristo, na nyumba ambayo suleimani
aliijenga ni hekalu la na Hekalu halisi
ni watu waliookolewa yaani kanisa ambalo Mwamba na msingi wake ni Yesu Kristo
1Wakorintho 3:16 “Hamjui
ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani
yenu? ”
1Petro 2:5 “Ninyi nanyi,
kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe
dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.”
Hili ni hekalu
la kiroho ambalo wanatheolojia wanaamini kuwa Kristo amelijenga na ingawa wako
wanaoamini kuwa pia atajenga Hekalu halisi wakati wa utawala wa miaka 1000
duniani kama alivyotabiri Ezekiel katika Ezekiel
40-43 na Ufunuo 20, Yesu ni bora
Zaidi kuliko Suleimani.
19.
Maombi ya Musa - Israel walipokuwa jangwani kulitokea vita
kati yao na wana wa amelekikatika vita hii Joshua ndiye alikuwa jemadari
mpiganaji kiongozi wa vita na Musa na Haruni ha Huri wao walipanda mlimani na
kumuombea Yoshua Maandiko yanaonyesha kuwa wakati mikono ya Musa ikidhoofika
wakati anaomba aliinua mikono yake miwili kuelekea Mbinguni, mikono ikichoka
amaleki walikuwa wanapata ushindi, lakini mikono yake ilipokuwa imara Yoshua na
Israel walipata ushindi, picha au alama kivuli cha mUsa kupanua mikono yake na
kusaidia na haruni na Huri inatupa alama ya kinabii ya siku aliposulubiwa
Kristo ambapo alisulibiwa pale Golgotha na wahalifu wawili mmoja mkono wake wa
kuume na mwingine mkono wake wa kushoto, haimaanishi kuwa Huri na haruni
walikuwa waovu kama wale wanyang’anyi waliosulubiwa pamoja na Kristo lakini
katika alama vivuli tunapata picha ya kinabii ya tukio husika ona
Kutoka 17:8- 13 “Wakati
huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu. Musa akamwambia
Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya
kilelekile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Basi Yoshua
akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na
Huri wakapanda juu ya kile kilima. Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli
walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. Lakini mikono ya
Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia.
Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu;
mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Amaleki na
watu wake kwa ukali wa upanga.”
Luka 23:32- 43 “Wakapelekwa
na wawili wengine, wahalifu, wauawe pamoja naye. Na walipofika mahali paitwapo
Fuvu la Kichwa, ndipo walipomsulibisha yeye, na wale wahalifu, mmoja upande wa
kuume, na mmoja upande wa kushoto.Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa
hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura. Watu wakasimama
wakitazama. Wale wakuu nao walikuwa wakimfanyia mzaha, wakisema, Aliokoa
wengine; na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye Kristo wa Mungu, mteule wake. Wale
askari nao wakamfanyia dhihaka, wakimwendea na kumletea siki,huku wakisema,
Kama wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi, ujiokoe mwenyewe.Na juu yake palikuwa na
anwani; HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI. Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa
alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi. Lakini yule
wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika
hukumu iyo hiyo? Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo
tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa. Kisha
akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. Yesu akamwambia,
Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.”
Ushindi wetu
unapatikana kwa kazi iliyofanyika pale Msalabani, kwa Yesu aliyewambwa mikono
yake msalabani akituombea ushindi kama Musa alivyomuombea ushindi Yoshua.
20. Maombi ya Samsoni.
Samsoni ni
moja ya watu ambao wanamwakilisha Yesu Kristo kwa namna nyingi sana huyu
alikuwa mwamuzi katika Israel anawakilisha mtu mwenye nguvu nyingi sana nguvu
kutoka Mbinguni, Mwanadamu huyu mwenye nguvu za kupita kawaida za kiasi cha
kutosha sio kuongoza jeshi tu bali yeye pake yake kuwa na uwezo mkubwa sana wa
kukabiliana na adui, yeye naye ni alama kivuli cha Kristo japo hakuna mtu
ametaja hili lakini mimi nataja
-
Kuzaliwa kwa
Samsoni kulitangazwa na malaika Waamuzi
13:3-5 3 “Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke,
akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe
utamzaa mtoto mwanamume. Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala
kileo, wala usile kitu kilicho najisi; kwani tazama, utachukua mimba, nawe
utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo
atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na
mikono ya Wafilisti.”
-
Kuzaliwa kwa
Yesu Kulitangwazwa na malaika Luka
1:26-31 “Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa
na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali
bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina
lake bikira huyo ni Mariamu. Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa
neema, Bwana yu pamoja nawe. Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake,
akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Malaika akamwambia, Usiogope,
Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.Tazama, utachukua mimba na kuzaa
mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.”
-
Wote
walisalitiwa na ndugu zao Wayahudi wakawafunga na kuwatia mikononi mwa wenye
dhambi – Waamuzi 15:9-13 “Basi Wafilisti wakapanda
wakapiga kambi yao katika Yuda, wakajieneza katika Lehi. Watu wa Yuda wakasema,
Mbona mmekuja kupigana nasi? Wakasema, Tumepanda ili kumfunga Samsoni, kumtenda
yeye kama alivyotutenda sisi. Ndipo watu elfu tatu wa Yuda wakatelemka hata ule
ufa wa jabali la Etamu, wakamwambia Samsoni, Je! Hujui ya kuwa Wafilisti wanatutawala?
Ni nini hii, basi, uliyotutenda? Akawaambia, Kadiri ile walivyonitenda mimi,
ndivyo nilivyowatenda wao. Wakamwambia, Tumeshuka ili kukufunga, tupate kukutia
katika mikono ya Wafilisti. Samsoni akawaambia, Niapieni ya kwamba ninyi
wenyewe hamtaniangukia. Wakamwambia, wakisema, Vema, lakini tutakufunga sana,
na kukutia katika mikono yao; lakini hakika hatutakuua. Basi wakamfunga kwa
kamba mbili mpya, wakamchukua kutoka huko jabalini.”
-
Yesu Krito
naye alisalitiwa na wayahudi na kukamatwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi –
Mathayo 20:17-19 “Hata Yesu alipokuwa akipanda
kwenda Yerusalemu, aliwachukua wale wanafunzi kumi na wawili faraghani; na
njiani akawaambia, Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemu; na Mwana wa Adamu
atatiwa mikononi mwa wakuu wa makuhani na waandishi; nao watamhukumu afe; kisha
watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi, na
kumsulibisha; na siku ya tatu atafufuka.”
-
Wote
hawakuheshimika sana walipokuwa hai, lakini waliheshimika siku ya maziko yao
Waamuzi 16:31 “Ndipo ndugu zake, na watu wote wa
nyumba ya baba yake wakatelemka, wakamtwaa wakamchukua, wakamzika kati ya Sora
na Eshtaoli, katika kiwanja cha kuzikia cha Manoa baba yake. Naye alikuwa
mwamuzi wa Israeli muda wa miaka ishirini.” Unaona miaka yote ya
uhai wa Samsoni hakuonekana kuwa wa maana sana hakna mtu alimjali lakini siku
ya kuzikwa kwake alizikika kadhalika Yesu alipata Heshima kubwa wakati wa
maziko watu wakubwa wastahiki ndio waliokuja kumzika ona
Mathayo
27:57-60 “Hata ilipokuwa jioni akafika mtu tajiri
wa Arimathaya, jina lake Yusufu, naye mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu; mtu
huyu alimwendea Pilato akauomba mwili wa Yesu. Ndipo Pilato akaamuru apewe.
Yusufu akautwaa mwili, akauzonga-zonga katika sanda ya kitani safi, akauweka
katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe
kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.”
Kuna kufanana kwingi kwa namna ya picha ya kinabii kati ya Samsoni na
Yesu lakini picha kubwa Zaidi ni kuwa wmisho wao wote walikuwa wakiwa wamekunjua
mikono katika nguzo mbili, Samsoni akisukuma nguzo mbili muhimu zilizokuwa
zimeshikilia jingo la hekalu la Mungu Dagoni wa wafilisti na kuwafutilia mbali,
na Yesu alikufa akiwa katika nguzo mbili za mti, yaani msalaba na hapa ndio
kila mmoja akawa amekufa kifo cha ushindi dhidi ya adui zake
Waamuzi
16:26-31 “Samsoni akamwambia yule kijana
aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate
kuzitegemea. Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote
wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume
kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza. Samsoni akamwita
Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba,
mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili
ya macho yangu mawili. Kisha Samsoni akazishika nguzo mbili za katikati ambazo
nyumba ile ilikaa juu yake, akazitegemea, moja kwa mkono wake wa kuume na moja
kwa mkono wake wa kushoto. Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti.
Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote
waliokuwa ndani yake. Basi wale watu aliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa
wengi kuliko wale aliowaua wakati wa uhai wake. Ndipo ndugu zake, na watu wote
wa nyumba ya baba yake wakatelemka, wakamtwaa wakamchukua, wakamzika kati ya
Sora na Eshtaoli, katika kiwanja cha kuzikia cha Manoa baba yake. Naye alikuwa
mwamuzi wa Israeli muda wa miaka ishirini.”
Hivyo unaweza kukubaliana name kwamba Samsoni na maisha yake sehemu
kadhaa wa kadhaa anamwakilisha Yesu kama kivuli cha Picha Halisi.
Ishara ya Abraham kumtoa Isaka.
Ishara ya Abraham kumtoa Isaka – Isaka naye
anasimama kama kivuli cha kinabii cha Yesu Kristo kwa namna pana Zaidi, kuna
maswala mengi sana yanayofanana kumuhusu Isaka kumwakilisha Bwana Yesu, Isaka
alikuwani mwana wa ahadi ambayo Mungu aliitoa kwa Abraham. Isaka alizaliwa kwa
muujiza, wakati Abrahamu alipokuwa na umri wa miaka 100 na Sara akiwa na miaka
90. Baada ya tukio la kuzaliwa kwake tunaona Mungu akimjaribu ili kwamba
Abrahamu amtoe mwanae huyu wa kipekee kuwa sadaka ya kuteketezwa, na Abrahamu
alipokuwa katika kulitekeleza hilo tunaona kwa njia ya muujiza Mungu akiingilia
kati na kumuokoa Isaka kwa namna ya kipekee, Mungu alimpa Abraham mwana kondoo
ambaye alikuwa ni mbadala, tunaelezwa sababu kubwa ya Abrahamu kutii kufanya
hivyo ni kwa sababu alimuamini Mungu kuwa anaweza kumfufua mwanae Isaka kutoka
kwa wafu,
Waebrania 11:17-19 “Kwa
imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea
hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee; naam, yeye aliyeambiwa,
Katika Isaka uzao wako utaitwa, akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata
kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.”
Kuna
maswala mengi ya kujifunza kutoka katika kisa hiki cha Abraham na Isaka, ambayo
yanatupa picha za kinabii katika tukio zima la kwenda kutolewa sadaka kwa
Isaka.
a. Abrahamu
kukubali kumtioa mwana wake wa Pekee kuwa dhabihu – ni alama kivuli cha unabii
wa Mungu baba kumtoa mwana wake wa Pekee Yesu Kristo kufa Msalabani kwaajili wa
watu wote watakaomwamini.
b.
Kitendo cha Isaka kukubali baba yake amtoe
sadaka – ni alama ya kukubali kwa Bwana Yesu kuyatoa maisha yake kwaaji ya watu
akimtii Mungu
c.
Kitendo cha Isaka kubeba kuni ili akatolewe
dhabihu juu ya kuni hizo ni alama kivuli cha kinabii cha Yesu kuubeba Msalaba
ambao atakwenda kusulubiwa juu yake.
d.
Kitendo cha Isaka kuokolewa kwa Ibrahimu
kupewa kondoo ni alama kivuli cha kinabii ya kwamba Yesu Kristo ndiye mwana
kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu ona
Yohana
1:28-29 “Hayo yalifanyika huko Bethania ng'ambo ya
Yordani, alikokuwako Yohana akibatiza.Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja
kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”
e.
Kitendo cha yule mwana kondoo kwamba pembe
zake zilikuwa zimenasa kwenye kichaka ona
Mwanzo
22:13. “Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na
tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi
Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala
ya mwanawe.”
Unaona AMENASWA PEMBE ZAKE
KATIKA KICHAKA – kitendo cha mwana kondoo huyu kunaswa pembe zake katika
kichaka ni alama kivuli cha Kristo aliyesulubiwa akiwa amevikwa taji ya miiba
kichwani ona
Yohana 9:2
“Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia
kichwani, wakamvika vazi la zambarau.”
f.
Katika ujumla wake tendo hili zima la Isaka
kutaka kutolewa na Abraham kama Sadaka lilikuwa ni unabii wa kazi nzima ya
ukombozi ambayo Mungu baba na mwana wake wa peke Yesu Kristo waliifanya
kwaajili ya ukombozi wa mwanadamu, najua wako waislamu ambao wanaamini kuwa
tukio hili lilikuwa ni kati ya Abraham na Ishimael vyovyote vile mtu anavyoweza
kudai lakini unabii huu ulikuwa una
uhusiano na ukombozi wa mwanadamu uliofanywa na Bwana Yesu pale Msalabani,
Mungu alimtaka mwana wa pekee wa ibrahimu ona
Mwanzo
22:1-2 “Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu
Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Umchukue
mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya
Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.”
Ibrahimu tunaambiwa kuwa alikuwa na wana wengi, lakini Mungu
alikuwa maalumu sana kiuchaguzi, alikusudia wazi kabisa kuwa mtoto huyu awe ni
Isaka, jumla ya watoto wa Ibrahimu walikuwa ni naneo ngoja nikuonyeshe na
wengine
Mwanzo
25:1-2 “Ibrahimu alioa mke mwingine jina lake
akiitwa Ketura. Akamzalia Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na
Ishbaki, na Sua.”
Unaona watoto wa Ibrahimu
ZIMRANI, YOKSHANI, MEDANI, MIDIANI, ISHBAKI NA SUA NA WENGINE NI ISHMAEL NA
ISAKA, Upekee wa Isaka unakuja kwa sababu yeye alizaliwa kwa muujiza
alizaliwa kwa ahahdi alizaliwa kwa mapenzi ya Mungu na sio kwa mapenzi ya
kibinadamu, Ibrahimu alimpenda sana Isaka kuliko watoto wengine kwa sababu hawa
wengine walikuwa ni wana wa Masuria na sio watoto wa ndoa halali ya Ibrahimu na
Sara na maandiko yako wazi ona
Mwanzo 25:5-6.
“Ibrahimu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo. Lakini
wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu akawapa zawadi, naye akawaondoa
katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za
mashariki, mpaka nchi ya Kedemu.”
Wana wa Masuria hawezi kuwa wana wa pekee, wala hawawezi kuwa
wanawapendwa kwa hiyo Mungu aliposema Mwana wako wa pekee alikuwa anamamisha
Isaka na sio wana wa Masuria
Na Kama ilivyo kwa Isaka
Mungu ana watoto wengi lakini mwana wake wa Pekee anayependezwa naye ni Bwana
wetu Yesu Kristo
Yohana
3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali
awe na uzima wa milele.”
Alitabiriwa na maandiko mara baada ya uumbaji, alizaliwa kwa
Ahadi, alizaliwa kwa muujiza, zlizaliwa na mwanamke bikira, alikuwa ndiye
sadaka halisi iliyochaguliwa na Mungu kwaajili yetu ndiye mwanakondoo halisi wa
Mungu ambaye kwa kupigwa kwake sisi tumepona, kwa hiyo Isaka ni alama kivuli
iliyo bora Zaidi ikimzungumia Kristo ambaye ni mwana pekee wa Mungu.
Muda usingeliweza
kutosha kuangalia alama vivuli vyote vilivyomo katika agano la kale ambavyo
vinatupa picha kamili ya shughuli mbalimbali alizokuja kuzitimiza bwana wetu
Yesu Kristo, lakini tunapopitia alama vivuli ambavyo vinatoa picha ya kinabii
tunapata picha kubwa sana ya namna Roho Matakatifu alivyoikatibu Biblia hata
ikatiokea ya kuwa matukio na matendo na maneno ya manabii yalitabiri sasawa
kabisa na matukio yote yaliyitimizwa na Bwana wetu Yesu, kumbuka hata mitume
hawakumaliza alama vivuli vyote lakini wewe unaweza ukaongezea kwa jicho lako
la mwanafunzi wa Biblia kumuona kristo katika matukio mbalimbali lakini
tunajifunza kuwa
1.
Mungu ni Mungu wa Matukio na Historian a kuwa kupitia
matukio na Historia ametuelekeza kumjua Kristo kwaajili ya utukufu wake
2.
Inatukumbusha kuwa Kweli Biblia ni neno la Mungu na
kuwa kweli Mungu alichagua Yesu Kristo kuwa mkombozi wetu
3.
Unabii wote katika maandiko unamuhusu Yesu Kristo.
Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!
+255 718 99 07 96