Jumapili, 25 Oktoba 2020

Na utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake !

 

Mwanzo 27:38-40 “Esau akamwambia babaye, Una mbaraka mmoja tu, babangu? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia.  Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia, Angalia, penye manono ya nchi patakuwa makao yako, Na penye umande wa mbingu unaotoka juu. Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo; Na itakuwa utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake katika shingo yako.

 


Utangulizi:

Wengi wetu tutakuwa tunafahamu habari za Yakobo na Esau kwa sababu tumezisoma mara kadhaa katika Biblia na pengine tumezijadili mara kadhaa na pia kuzihubiri, kwa ujumla watu wengi sana wanaposoma kisa hiki, humsikitikia sana Esau na hata kumuona Esau kama mtu mjinga na aliyedanganywa mara kadhaa na kukandamizwa na Ndugu yake pamoja na mama yake, na tumesahahu kuwa uko upande mwingine ambao Esau ana jambo lake na linaweza kutufundisha kitu.

Kama tunavyoielewa habari hii yenye kusisimua na kusikitisha, Tunasoma kuwa Isaka anamjibu Esau alipouliza kama kuna mbaraka wowote japo mmoja umebaki kwaajili yake, Majibu anayopewa Esau hayaonyeshi kuwa amepata Baraka kwa sababu Isaka alikusudia kumwaga Baraka zote kwa Mwanaye mkubwa na bahati mbaya amebariki Baraka hizo kwa yakobo mwanaye mdogo ambaye alikuja kwa hila baada ya mpango mkakati wa Rebeka ona

Mwanzo 27:1-10 “
Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa. Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu. Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo; ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa. Na Rebeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe. Basi Esau akaenda nyikani awinde mawindo, ayalete. Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, akisema, Angalia, nimemsikia baba yako akisema na Esau, ndugu yako, akinena, Niletee mawindo, ukanifanyie chakula kitamu ili nile, na kukubariki mbele za BWANA kabla ya kufa kwangu. Basi, mwanangu, sikiliza sauti yangu kama nitakavyokuagiza. Enenda sasa kundini ukanitwalie wana-mbuzi wawili walio wema, nami nitawafanya chakula kitamu kwa baba yako, namna ile aipendayo. Kisha utampelekea baba yako, apate kula, ili akubariki kabla ya kufa kwake.

Unaweza kuona kwa njama za
Rebbeka na Yakobo waliweza kuchukua Baraka zote alizokusudiwa Esau, wakati wote wakimfanya Esau kuwa mjinga  na pamoja na baba yake hata kumbariki mtu mwingine 

Mwanzo 27:26-29 “
Isaka, baba yake, akamwambia, Njoo karibu sasa, ukanibusu, mwanangu. Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba alilolibariki BWANA. Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo. Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe.”


Kulikuwa na tatizo kubwa sana katika familia hii, wazazi walikuwa wamegawanyika mama akiwa na Yakobo na Isaka akiwa na Esau kila mmoja alikuwa na jambo lake moyoni  Isaka alikuwa amekusudia kumbariki Esau kweli kweli na nduguye anngekuwa mtumwa wake tu, na hakukuwa na vinginevyo, Isaka anagundua kuwa amemwaga mibaraka yote kwa Yakobo wakati alikuwa ahajkusudia kumuachia yakobo chochote sasa kumbe amembariki Yakobo na jambo hili lilimpa kutetenmeka san asana Isaka lakini angefanya nini alikuwa amekwisha kutamka

Mwanzo 27:32-33 “
Isaka, baba yake, akamwuliza, U nani wewe? Akasema, Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza. Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa.”Lilikuwa ni tukio la kusikitisha na kutisha sana katika maisha ya Isaka na Esau na Isaka alisema japo mtu huyu amekuja kwa hila atabarikiwa  sasa ni mbaraka gani umebakia Esau alihoji kwa nguvu zake zote kuwa endapo uko mbaraka umebaki tafadhali basi baba unibariki na mimi!

Na itakuwa utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake katika hingo yako!

Ndipo Isaka akatamka mbaraka huu Hebu tuuangalie vizuri Mwanzo 27:38-40 “Esau akamwambia babaye, Una mbaraka mmoja tu, babangu? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia.  Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia, Angalia, penye manono ya nchi patakuwa makao yako, Na penye umande wa mbingu unaotoka juu. Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo; Na itakuwa utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake katika shingo yako.

Esau alipokea mbaraka mmoja tu lakini mbaraka huu ulikuwa na masharti, ni kweli Mungu alimuandalia penye umande na unono, lakini ili aweze kuyapata lazima afanye vita lazima apambane haitakuwa rahisi, na nduguye atamtawala lakini lazima aponyoke na kulivunja kongwa yaani nira ya utumwa na kuwa huru,  

Kongwa ni nini?

Kongwa ni neno la kiswahili lenye jina lingine liitwalo Nira, kwa kiingereza Yoke, chombo hiki huvalishwa wanyama kazi shingoni kwa kusudi la kuwatumikisha na kuwafanyisha kazi kwa lazima, Katika biblia hutumika kama alama ua utumwa, au ukoloni, chombo hiki kinapovalishwa kwa mnyama mnyama huyo hutekeleza matakwa ya Bwana wake tu na kutumikishwa kwa muda na majira na nyakati kama atakavyo bwana wake hivyo mnaya hupoteza uhuru na uwezo wa kufanya mambo yake ayatakayo, Mtu yeyote anayetaka kuwa huru katika jambno lolote linalomtumikisha bila kupenda ni lazima aponyioke na kujivua Kongwa ndipo aweze kuwa Huru! Mbaraka aliopewa Esau na baba yake ulihusisha unono na umande kutoka kwa Mungu lakini ulikuwa unahusisha nguvu zake yaani ilikuwa ili Esau awe huru kutoka kwa nduguye atumie nguvu, apigane akatae kuwa mtumwa kama nchi nyingi za afrika zilivyojipatia uhuru ni chache sana zilipata uhuru bila kumwaga damu, Esau alitamkiwa kuwa mtumwa wa Israel lakini sio milele, alitakiwa kujitetea alitakiwa kupigana alitakiwa kujichomoa na kulivunja kongwa la nduguye ili aweze kuwa huru!

Maandiko haya yalitimizwa kwani wazao wa Yakobo na Esau walikuja kuutimiza unabii huu kwa dhahiri, Wazao wa Esau ambao ndio Edomu walikuja kutawaliwa wakati wa Daudi kupitia jemadari wake Yoabu ambaye aliwatenda vibaya sana na kuwakatilia mbali na kuwapoteza wanaume wote ona  

1Wafalme 11:15-16 “
Kwa maana ikawa, Daudi alipokuwako Edomu, naye Yoabu, mkuu wa jeshi, amepanda awazike waliouawa, akiisha kumpiga kila mwanamume wa Edomu, (kwa kuwa Yoabu alikaa huko miezi sita pamoja na Israeli wote, hata alipompoteza kila mwanamume wa Edomu);”  

Kutokana ana ushindi huu wa Daudi wana wa Esau walikuwa watumwa wa Israel kwa muda Fulani  na walilipa kodi na kutawaliwa, Lakini Biblia inasema baadaye  waklikataaa na kujilipia kisasi na kutangaza uhuru wao na kujitawala ona

2Wafalme 8:20-22 “
Zamani zake, Edomu wakaasi mkononi mwa Yuda, wakajifanyia mfalme. Basi akaenda Yehoramu mpaka Sairi, na magari yake yote pamoja naye. Akaondoka usiku, akawapiga Waedomi waliomzunguka yeye na maakida wa magari; na watu wakakimbilia hemani kwao. Hivyo Edomu wakaasi mkononi mwa Yuda hata leo. Na Libna wakaasi zamani zizo hizo.” 

Biblia inaonyesha kuwa Esau alikataa kuwa mtumwa wa Israel hata leo  na hivyo unabii wa Isaka ulitimizwa, Edomu ukawa ni utawala huru na wakawa watu hatari sana kwa
Yuda na wakati wa utawala wa Ahazi Edomu waliipiga Yuda vibaya sana na kuwachukua Mateka ona

2Nyakati 28:16-17 “
Wakati ule mfalme Ahazi akatuma wajumbe kwa mfalme wa Ashuru ili amsaidie. Kwa kuwa Waedomi walikuwa wamekuja tena, na kuwapiga Yuda, na kuwachukua wafungwa.”

Nisikilize mpendwa ziko haki zako na Baraka zako nyingine huwezi kuzipata hivihivi, huwezi kuzipata kwa maombi pekee huwezi kuzipata kwa kufunga na kuomba ziko Baraka zako zingine zinapatikana kwa kupambana kwa kukataa kuwa mtumwa kwa kuvunja kongwa la nduguyo kongwa ni  chombo anachovalishwa mnyama wa kazi shingoni ili kumtumikisha na kumfanya afanye kazi ngumu tena si kwa hiyari yake mwenyewe. ziko haki nyingine huwezi kuzipata mpaka uende mahakamani. Ziko haki nyingine huwezi kuzipata bila kutumia nguvu au kutumia upanga, waulize wapigania uhuru wengi kama unadhani uhuru luilikuwa jambo rahisi hata kidogo, wazunghu hawangetaka kuachia unono wa rasilimali za Afrika kirahisi au kwa maneno tu, waulize kina Keneth Kaunda, Kwame Nkuruma, Julius Nyerere, Haile Sellasie, Jomo Kenyatta, Abeid Karume, Samora Machel, Martin Luther King na wapoigania haki wa kweli kama ilikuwa rahisi kuwa huru na kuliacha kongwa la kitumwa na kikoloni? Kutokana na upole wetu na ukarimu wetu, Sfrika ilipoteza uhuru wake, rdhi nzuri zilichukuliwa, mashamba mazuri yakawa ya wazungu, Eaafrika waligeuzwa vibarua kwa ujira mdogo, mazao yaliyolimwa walilzazimishwa ya kibiashara, walilipishwa kodi na walipaswa kutumia mamlaka za kifedha za kikoloni Afrika walijikuta wamepotea uhuru wao, Ukombozi wa kweli na uhuru wa kweli ungekuja kwa kupigana tu na si vinginevyo:-

Yako mambo hata kama umeokoka vipi huwezi kuyapata bila mapambano ya dhati Kama hunielewi vizuri Rais wa  sasa wa Malawi anaweza kunielewa vizuri, Yeye alikuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Assemblies of God Malawi kwa miaka 24, kisha aliingia kwenye siasa na chama cha Malawi congress Part, aligombea urais mara kadhaa na mara ya mwisho alipambana na  chama tawala cha DPP ambao walijitangaza kuwa washindi kwa hila  na Rais Peter Mutharika aliapishwa kuwa rais wa malawi haki ikiwa imepotioshwa na uchaguzi ukiwa uimegubikwa na hila na udanganyifu wa kila aina, Askofu huyu Mstaafu haki yake aliipata mahakamani, ambapo mwaka huu 2020 uchaguzi ulipoamuriwa urudiwe na mahakama alishinda kwa asilimia 59% ya kura zote zilizopigwa na kuapishwa kuwa rais wa Malawi akiwa na miaka 65 sasa  lazarous Askofu Chakwera ni rais  wa sita wa Malawi aliyeapishwa mwaka huu june 28 2020, Inawezekana alifunga na kuomba lakini haki yake ilipatikana mahakamani!

Yako mambo mengine ni lazima upambane, yako mambo mengine hayaondoki kwa kuwa mpole yako mambo mengine hayarekebishiki kirahisi, lazima upambane , lazima uvunje kongwa la utumwa, lazima ukatae ushenzi na ujinga na dharau na ukandamizwaji, hivi ndio nchi nyingi za Afrika zilivyojikomboa haikuwa rahisi, shetani hawezi kuruhusu uhuru kwa njia rahisi, hawezi kuruhusu furaha wa njia rahisi, hawezi kuachia mateka kwa njia rahisi  lazima upambane, Isaka akamwambia Esau mwanangu unono upo na umande upo Mungu amekupa lakini wewe utakula kwa upanga  wako na nduguyo amekusudiwa kukutawala lakini ukiponyoka na kulivunja kongwa lake utakuwa huru, Ponyoka kutoka katika ukandamizwaji na maumivu na mateso tangaza uhuru wako mwenyewe  shetani asikuonee tena sio lazima ufie hapo, sio lazima ufie kwenye ndoa hiyo iliyojaaa masimango ugomvi, mikwara ubabe na kutokupatikana kwa suluhu utumwa na udhalilishaji kunyimwa tendo la ndoa, kukosa maamuzi yako, wakeo na ndugu wamekuwa na sauti kuliko wewe mwenye nyumba,  sio lazima ufie kwenye kazi hiyo iliyojaa ukandamizwaji, mateso posho ndogo kuibiwa na kuonewa na kutukanwa, wakati mwingine ili uwe na mbele njema ni lazima upambane, yako mambo ni mpaka ukasirike ndio yanawezekana !, sio lazima ufie kwenye dhehebu hilo unaweza kuanza hata huduma yako, uwezo wa kujikomboa u katika mikono yako wewe mwenyewe jikomboe wewe na ndugu zako! Sio lazima umsamehe mtu aliyedhulumu shamba lako sio kila kitu kinahusu kumuachia Mungu, vingine vinahitaji mapambano pigana weka upanga wako vunja Kongwa la utumwa utakuwa huru na uko sahihi

Wakati wa Uhuru wa zimbabwe Robert Nesta Maley aliimba maneno ya Muhimu sana kwamba wakati mwingine ni sahihi kupigana kwaajili ya Maisha yako yajayo, pata muda sikiliza  maneno yake kuhusu Zimbawe hapa naweka kiasi tu nanukuu

Every man gotta right to decide his own destiny,
And in this judgement there is no partiality.
So arm in arms, with arms, we'll fight this little struggle,
'Cause that's the only way we can overcome our little trouble.

Brother, you're right, you're right,
You're right, you're right, you're so right!
We gon' fight (we gon' fight), we'll have to fight (we gon' fight),
We gonna fight (we gon' fight), fight for our rights!

Natty Dread it in-a (Zimbabwe);
Set it up in (Zimbabwe);
Mash it up-a in-a Zimbabwe (Zimbabwe);
Africans a-liberate (Zimbabwe), yeah.

Na. Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Alhamisi, 15 Oktoba 2020

LENGO KUU LENYE FAIDA KUU!

Wakati huu tulio nao ni wakati wa mwisho 1Yohana 2;18. “Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. “ Mwisho wa mambo yote umekaribia 1Petro 4;7. “Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.” bado kitambo kidogo Yeye ajaye yaani Yesu Kristo anakuja, wala hatakawia Waebrania 10;37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.” katika wakati huu wa mwisho ni muhimu kwa kila mmoja wetu kujifunza na kutafakari kwa makini somo letu la leo ‘Lengo kuu lenye faida kuu ”Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele sita vifuatavyo.:-

*      Malengo mbalimbali ya wanadamu katika maisha

*      Tatizo kubwa la malengo ya kawaida ya wanadamu

*      Lengo kuu lenye faida kuu

*      Mifano ya watu wenye Busara waliokuwa na lengo kuu lenye faida kuu maishani mwao

*      Mifano ya watu wapumbavu ambao hawakuzingatia lengo kuu lenye faida kuu

*      Yatupasayo Kufanya




Malengo mbalimbali ya wanadamu katika maisha

     Ukimuuliza mtu awaye yote maswali haya Je ni kitu gani unachotamani kuwa nacho maishani mwako? ukipata nini utakuwa na furaha isiyo na kikomo? wanadamu mbalimbali watakuwa na majibu Tofauti katika kujibu maswali haya au kwa Maneno mengine watakuwa na malengo mbalimbali. katika Biblia tunawaona watu waliokuwa na malengo mbalimbali katika maisha yao 


Luka 12;13 “Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu” 

tunaona juu ya mtu mmoja aliyelenga tu kupata urithi. Ina maana hata mzazi wake alipokuwa hai aliwaza moyoni kwamba siku ya kugawiwa urithi itafika lini, Lengo lake ilikuwa ni mali za baba yake mbaya sana 


Luka 12 16-19 “Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.” tunaona mtu moja mkulima aliyekuwa tajiri sana yeye lengo lake lilikuwa kujenga ghala kubwa na kuweka nafaka zake na vitu vyake ili apumzike, kula kunywa na kufurahia. Maandiko yanatupa habari za mtu mwingine  aliyekuwa na cheo kikubwa sana huko Shamu huyu aliitwa Naaman yeye alikuwa jemedari wa jeshi la mfalme wa Shamu,alikuwa mtu mkubwa mwenye Kuheshimiwa wa pili kutoka kwa mfalme huyu Tofauti na waliotangulia alikuwa na lengo la kupona ukoma 


2Falme 5;1-3. Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake Bwana alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma. Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani.  Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake.” 


Wako watu vilevile hali kadhalika wanaweza kuja kwa Yesu Kristo lakini malengo yao yakiwa ni kupokea miujiza yao, kuponywa magonjwa yao ama wanaweza kumfuata Yesu kwa sababu kadhaa wa kadhaa Mwanamke Hana, pamoja na kupendwa sana na mumewe na kupata kila kitu lakini aliwaza moyoni mwake wakati wote kupata mtoto 


1Samuel 1;1-11 “Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu  naye alikuwa na wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto. Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea Bwana wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa Bwana, walikuwako huko. Hata siku ile ilipofika Elkana alipotoa dhabihu, kumpa mkewe Penina sehemu, akawapa na watoto wake wote, waume kwa wake, sehemu zao; lakini Hana humpa sehemu mara mbili; maana alimpenda Hana, ingawa Bwana alikuwa amemfunga tumbo.  Ila mwenzake humchokoza sana, hata kumsikitisha, kwa sababu Bwana alikuwa amemfunga tumbo. Tena mumewe akafanya hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke alipokwea kwenda nyumbani kwa Bwana, ndivyo yule alivyomchokoza; basi, kwa hiyo, yeye akalia, asile chakula. Elkana mumewe akamwambia, Hana, unalilia nini? Kwani huli chakula? Kwa nini moyo wako una huzuni? Je! Mimi si bora kwako kuliko watoto kumi? Ndipo Hana akainuka, walipokwisha kula na kunywa huko Shilo. Naye Eli, kuhani, alikuwa akiketi kitini pake penye mwimo wa hekalu la Bwana.  Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba Bwana akalia sana.  Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe.” watu wengine katika 


Yakobo 4;13 “Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida;” 


wao walikuwa na lengo kuu  la kufanikiwa kibiashara na kupata utajiri,hata hivi leo kama ilivyokuwa kwa watu hawa lengo lao kuu ni kupata mchumba, kuolewa au kuoa, kuwa na digrii tatu, kuwa na cheo cha rais n.k Mtu aliye na lengo kuu la kupona au kupata mtoto anaweza hayo tu wakati wote na kwake mengineyo hayana uzito mkubwa kwake, wengine watakuja Kanisani kama hapa lakini lengo lao ni kupona tu, kuolewa au kuwa na mtoto na wokovu au kumtumikia Mungu kwake havina uzito mkubwa kila mmoja hana budi kujiuliza lengo lake kuu alilonalo ni nini? Wengine watatamani kuwaombea maelfu ya watu na kuwaona wanapokea miujiza yao n.k.

Tatizo kubwa la malengo ya kawaida ya wanadamu

Tatizo lililopo ni kwamba hata kama malengo waliyo nayo wanadamu yanatimia bado hayawapi furaha isiyo na kikomo. Mtu akipona ugonjwa wake au mateso yake kwa miujiza mkubwa bado hatimaye atakufa tu Lazaro aliyefufuka katika 


Yohana 11;38-44 “Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.  Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.  Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake”.          


hatimaye alikufa tena,na wengine wengi walioombewa na Yesu wakapata miujiza yao kama kipofu Bartimayo aliyepata kuona,hatimaye alikufa,mtu hata akipata utajiri na mali iwe ni mamilioni ya mapesa, magari mengi, nyumba na kadhalika akifa haondoki navyo anaviacha vyote Zaburi 49;16-19 “Usiogope mtu atakapopata utajiri, Na fahari ya nyumba yake itakapozidi. Maana atakapokufa hatachukua cho chote; Utukufu wake hautashuka ukimfuata. Ajapojibariki nafsi yake alipokuwa hai, Na watu watakusifu ukijitendea mema, Atakwenda kwenye kizazi cha baba zake Hawataona nuru hata milele”. katika yote haya na malengo mengineyo mengi  hakuna cha kudumu  yote haya ni ya kupita wafalme wengi waliokuwa maarufu na wengi waliokuwa maarufu hapa duniani wamepita wamekufa na imebaki historia tu. Wanasiasa wengi, wakubwa na maarufu duniani, waimbaji, wachezaji, wasanii, matajiri na wanasayansi na wenye umaarufu wa kila aina wote wamepita duniani na historia zao zimehifadhiwa hakuna cha kudumu, wahubiri maarufu waliotikisa dunia na kila mwenye mafanikio ya kila namna duniani wamepita hakuna jipya chini ya jua mambo yote ni ubatili tu kila kitu kina mwisho na hakuna cha kudumu kwa msingi huo malengo yetu duniani ni ya muda mfupi tu na sio ya kudumu wala hayana faida za kudumu!

Lengo kuu lenye faida kuu.

Lengo kuu lenye faida kuu ni kupata uzima wa milele au kuingia mbinguni mtu anapokuwa na lengo hili moyoni mwake wakati wote na kulipa uzito mkubwa kuliko malengo mengine yote mtu huyu anakuwa ameigundua siri, kukosa uzima wa milele kunaitwa kupotea katika Biblia 

Yohana 3;16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele       

Mtu Yeyote mwenye Busara atawaza kwanza juu ya uzima wa milele kuliko uzima huu wa Muda tu katika miili yetu wakati wote atawaza kama mtu mmoja aliyekwenda mbio akitafuta juu ya jambo hili wakati wa Yesu 

Marko 10;17 “Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? “ 


unaona swala kubwa sana na la msingi kuliko yote ni kuwa kuna maisha baada ya kufa, Je utakuwa wapi baada ya maisha yako duniani kuisha?  Iko jehamnamu ya moto milele na milele na uko uzima peponi milele na milele! Mtu anayekusudia kuupata uzima wa milele ndiye mtu mwenye akili kubwa kuliko wote, wako watu katika Biblia ambao licha ya Mungu kuwabariki kwa Baraka mbalimbali walikuwa na mawazo ya ufalme wa Mungu! Nahii ilikuwa ndio busara kubwa sana!

Mifano ya watu wenye Busara waliokuwa na lengo kuu lenye faida kuu maishani mwao.

Biblia inasema Ibrahamu alikuwa tajiri sana kwa mifugo,kwa Fedha na dhahabu Mwanzo 13;2, Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu.hata hivyo wakati wote lengo lake kuu lilikuwa kuingia mbinguni, aliacha kila kitu na kuwaza juu ya mbinguni  tunaelezwa katika 

Waebrania 11;8-10, kwamba “Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.  Sara, Habili, Henoko na Nuhu na wengine wengi walitamani wakati wote kuingia mbinguni kuliko kupata mtoto,kupona n.k 

Waebrania 11;16  Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.” Ayubu pamoja na utajiri wake yeye pia aliwaza juu ya kuingia mbinguni ukuu na utajiri kwake havikuwa na uzito mkubwa kuliko wokovu na kumuona Yesu 

Ayubu 1;1-3, Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti watatu.  Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.          

Mtume Paulo hakuwaza tu kuifanya kazi ya Mungu au kufanya miujiza mikubwa mingi, lakini pamoja na kutumiwa sana na kupewa mafunuo makubwa Matendo 19;11-12, Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida; hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka.” 2Petro 3;15-16  Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;  vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.” 


Paulo mtuma alikuwa ni mtume aliyafanya kazi kubwa kuliko mitume wote, aliyetumiwa na Mungu kwa miujiza ya kupita kawaida na kutumiwa kuandika Nyaraka na agano jipya karibu nusu na robo alihubiri njili na kuupoindua ulimwengu wa wakati wake hata hivyo hakusahau kuwa na lengo kuu  wakati wote lengo lake lilikuwa kwenda Mbinguni kuikaa na Kristo,Jambo hili alilitamani upeo ona  Wafilipi 1;23,” Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana;” hatuna budi kukumbuka kwamba tunaweza kufanya miujiza mingi lakini tukajikuta miongoni mwa watu wa kupoteza, ikiwa tutakuwa na maisha yaliyo jaa dhambi na tukajikuta kuwa sisi ni watu wa kukataliwa  


Mathayo 7;21-23 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.  Tunaweza tukawahubiri wengine na kuwafundisha lakini sisi tukashindwa kuingia mbinguni Paulo mtume alikataa kuwa mtu atakayewahudumia na kuwahubiri wengine kisha yeye kuwa mtu wa kukataliwa ona 

1Koritho 9;26-27, Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.”  Yusufu wa Armathaya, masatahiki yeye aliwaza mbinguni Marko 15;43. “akaenda Yusufu, mtu wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza ya mashauri, naye mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu.”

Mifano ya watu wapumbavu ambao hawakuzingatia lengo kuu lenye faida kuu

Mtu yule mkulima tajiri aliyekuwa na lengo kuu la kujenga ghala kubwa la kuweka nafaka na vitu vyake ili apumzike ale kunywa na kufurahia badala ya kuwaza kwanza juu ya uzima wa milele anaitwa na Mungu “mpumbavu” 

Luka 12;16-21. “Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.”  Mtu mwingine tajiri Yeye aliwaza tu kula kwa anasa siku zote na kuvaa kwa anasa lakini hakuwaza juu ya uzima wa milele Tofauti na masikini lazaro matokeo yake alipokufa alikwenda kwenye mateso ya milele motoni 

Luka 16;19-30.” Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.

Yatupasayo kufanya .

·         Kuwa na lengo hili kuu la kuingia mbinguni na kuliweka kuwa la kwanza ya yote mengine Mathayo 6;33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”

·         Kuhakikisha tumetubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha ili tupate rehema ya kuingia Mbinguni Mithali 28;13 “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”

·         Kuangalia tusianguke dhambini tena 1Koritho 10; 12 ”Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.” na kuhakikisha lolote lile jingine mbali na lengo kuu lenye faida kuu yaani kuingia mbinguni halichukui nafasi ya kwanza, tunaweza tukaitenda kazi ya Bwana lakini tukasahau utakatifu kwanza kutenda kazi huko hakutatusaidia kuiona mbingu.

Preached by Bishop Zachary Kakobe 15 October 1995 my Spiritual Father

Composed by Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

0718990796

Ikamote@yahoo.com

Jumanne, 13 Oktoba 2020

Hapa yupo Aliyemkuu Kuliko Sulemani


Mathayo 12: 38-42 Biblia inasema “38. Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. 39. Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona. 40. Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi. 41. Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona. 42. Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.

 


Kifungu hicho hapo juu cha maandiko ni cha muhimu sana na tunapokifanyia uchambuzi yakinifu itatupa mwanga wa kumfahamu Yesu Kristo kwa kina na upana na urefu zaidi, kifungu hiki ni matokeo ya mjadala uliokuweko kuhusu Yesu Kristo, Baada ya Wayahudi hasa jamii ya  mafarisayo kumnenea Yesu maneno mabaya zaidi, Baada ya kuwa Yesu amemponya mtu aliyekuwa ana pepo, kipofu na ni Bubu,
Mathayo 12:22-23. Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona. Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi?  Muujiza huu uliwashangaza watu na kumfanya Yesu aanze kukubalika miongoni mwa jamii kuwa “MWANA WA DAUDI” hii ilikuwa ni wazi kuwa walikubali kuwa Yesu ndiye MASIHI, ni wazi kuwa kwa kazi hii na nyinginezo alizozifanya Yesu zilipelekea watu kumuamini na kuondoa shaka kuwa ndiye mfalme ajaye kwa JIna la Bwana, Hata hivyo kwa sababu ya wivu wa Mafarisayo ambao waliona Yesu anaheshimika zaidi na kuwa gumzo kuliko wao waliamua kwa makusudi kuharibu kibali cha Yesu kwa kusema kuwa anatoa pepo kwa nguvu za mkuu wa Mapepo Belzebuli Mathayo 12:24 “Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo. “

Yesu Kristo akitambua hilo alitoa hutuba kali sana ya maonyo dhidi ya watu wanaopinga kazi ya Mungu Roho Mtakatifu, na zaidi ya yote aliwaonya watu kuhusu kuzungumza maneno yasiyo na maana kwa vile watatoa hesabu kwa kila neno lisilo na maana wanalolitoa katika vinywa vyao,

Mathayo 12:33-37. Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana. Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya. Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa

Baada ya hutuba hii ya Yesu ambayo ilikuwa kali na yenye maonyo baadhi ya Mafarisayo waliogopa sana Lugha “Hapo” inatumika kuonyesha kuwa iliwalazimu sasa waombe ishara ya kumfahamu Yesu vema kuwa yeye ni nani, Tupe ishara itakayotusaidia kukutambua wewe ni nani? Ndipo Yesu aliwajibu kwamba watamtabua kupitia Ishara kuu mbili.

1. Ishara ya Nabii Yona.

Yesu aliwaeleza kwa uwazi kuwa Ishara ya kumtambua Masihi iko wazi, ishara hii ndiyo iliyowavutia watu wa Ninawi wakatubu na kumgeukia Mungu kupitia mahubiri ya Yona, Mathayo 12:38-41, Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona. Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi. Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona.”

Kimsingi Yesu alitaka kukazia kuwa kile kilichomtokea Yona kilikuwa ni ishara halisi, na kilikuwa ni kivuli cha kumtambua Masihi, ambaye Yesu alikazia kuwa ni mkuu kuliko Yona, Yesu alikazia kuwa namna njema ya kumtambua yeye ni pale atakapokufa na kufufuka siku ya tatu, hii ndio kazi kubwa ya ukombozi itakayowavuta wengi katika ufalme wa Mungu. Nguvu kubwa ya masihi ni kukishinda kifo, kuishinda mauti, hii ni ishara kubwa waliyopewa watu.

 

2. Ishara ya Malkia wa Sheba.

Yesu aliwapa Mafarisayo Ishara nyingine ya muhimu. Ambapo sasa anaeleza kuhusu Malkia wa kusini yaani Sheba kwamba alitoka mbali sana pande zamwisho wa Nchi kuja kusikiliza Hekima ya Sulemani, Yesu ni kama alikuwa anakazia kuwa njia nyingine ya kumtambua ni kumsikiliza, usikivu ungeliwasaidia kujua kuwa hakuna mwingine anayeweza kunena au kutenda katika kiwango kama cha Yesu, Mathayo 12:42 “ Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.”

 hata hivyo  mahali hapa ndipo paliponisukuma zaidi kufanya Uchambuzi hususani Yesu alipohitimisha kuwa malikia huyu alisafiri kutoka mbali kusikiliza Hekima ya Sulemani, hata hivyo Yesu alitamka wazi kuwa Yeye ni mkuu kuliko Sulemani.

Suleimani ni mfalme aliyeishi kwa anasa na ufahari wa hali ya juu, mfalme huyo alikuwa na Hekima na ufahamu na maarifa ya hali ya juu sana kuliko wafalme wote ambao wamepata kuweko, Biblia inasema kabla yake hajakuweko na badala yake hatokuweko 1Wafalme 3:9-13, Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi? Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili. Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu; basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe. Na mambo yale usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika wafalme kama wewe, siku zako zote.

1Wafalme 4;29-34 “Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani.Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri.Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka. Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano. Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki. Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya Sulemani, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake.

 unaweza kuona!, wengi waliosikia Hekima ya Suleimani katika enzi zake walisafiri kutoka mbali ili kwenda kumsikiliza, Lakini ziara ya kifahari na maarufu sana na iliyoelezewa kwa kina ni safari ya Malkia wa Sheba au Ethiopia ambaye alikwenda kwa mikogo mingi na mikubwa  1Wafalme 10:1,Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Sulemani juu ya jina la Bwana, alikuja ili amjaribu kwa maswali ya fumbo. 2Nyakati 9:1-6 Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Sulemani, alikuja ili amjaribu Sulemani kwa maswali ya fumbo huko Yerusalemu, mwenye wafuasi wengi, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikilia Sulemani, akamwambia mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake. Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala halikuwako neno alilofichiwa Sulemani, asimwambie. Naye malkia wa Sheba alipoona hekima ya Sulemani, na nyumba aliyoijenga, na vyakula vya mezani mwake, na kikao cha watumishi wake, na usimamizi wao wangoje wake, na mavazi yao; na wanyweshaji wake, na mavazi yao; na daraja yake ya kupandia mpaka nyumba ya Bwana; roho yake ilizimia. Akamwambia mfalme, Ndizo kweli habari zile nilizozisikia katika nchi yangu za mambo yako na za hekima yako. Lakini mimi sikuyasadiki maneno yao, hata nilipokuja na kuona kwa macho yangu; wala, tazama, ukuu wa hekima yako sikuambiwa nusu; wewe umezidi kuliko habari nilizozisikia. 

Biblia inasema malkia huyu alikwenda akiwa na maswali magumu sana  The Amplified Bible inasema kwa lugha ya kiingerezaShe came to Jerusalem to test him with Hard Questions  na Biblia ya kiingereza ya NIV “she came to Prove Solomon with Hard Questions pamoja na ziara yake ya kifahari na zawadi kibao alizozibeba alipofika Yerusalem kwa Suleimani alijibiwa maswali yake yote na mambo yake yote hata aliyokuwa ameyaficha sirini, hakuna kilichofichika kwa Suleimani, alitosheleza mahitaji yake yote na hisia zake zote zilijibiwa na kuzidi.

Dunia ya leo ina maswali magumu mengi yasiyo na majibu, pamoja na kuendelea na kukua kwa maarifa na uvumbuzi wa kisayansi na Teknolojia, Watu wanazidi kuharibikiwa dunia imejawa na hekima ya uharibifu, wizi, ufisadi, uchochezi, uchoinganishi, majungu na fitina, kuliza wengine, kutoa mimba udanganyifu, na hakuna majibu ya maswala muhimu katika matatizo ya watu, Sulemani alikuwa na ujuzi zaidi ya wa kibailojia, Chemistry, Physics, aliishi kwa anasa kuliko mtu yeyote, mwisho aliona hekima na maarifa bila ya Mungu ni upuuzi au ubatili, alishauri watu kumkumbuka Muumba wao siku za ujana wao, Muumba huyu ndiye mkuu kuliko Sulemani, Yesu Kristo anatajwa kama Hekima yetu

1Wakoritho 1:30 “Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;”

 kwa kiyunani Epignosis sofia, Full of wisdom Knowledge and Understanding, Yesu aliposema Hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani alimaanisha Yeye ndiye aliyemuumba huyo Sulemani, Yeye ndiye mwenye majibu yote hata ya mambo magumu, Yeye ndiye Masihi, ni zaidi ya mfalme Sulemani, watu watatoka kila pande za dunia kumjia yeye, na atawahukumu wote waliomkataa yeye atakuwa na majibu ya kutosha na kushangaza ulimwengu kwa hao wanaomjia

Hapa yupo aliye mkuu Kuliko Sulemani.

Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Rev. Innocent Kamote.
0718990796
ikamote@yahoo.com

Jumapili, 27 Septemba 2020

Bwana ni Mtu wa Vita!

Kutoka 15:2-3 BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake.


 

Bwana ni Mtu wa Vita.

Ni muhimu kufahamu kuwa moja ya ufunuo mkubwa zaidi wa Mungu kwa wana wa Israel ukiacha kujitambulisha kama NIKO AMBAYE NIKO Mungu vilevile alijifunua kama Bwana wa vita au Mtu wa vita! Katika Biblia ya Kiebrania mara zote jina Yahweh, na jina Elohim wakati wote huambatana na neno tzevaotao Sabaothambayo maana yake ni Majeshi kwa hiyo jina la Mungu katika israel husomeka YHWH Elohe Tzevaot kwa kiingereza Jehova Lord of Host kwa kiswahili Bwana Mungu wa majeshiNeno hili Bwana wa Majeshi limejitokeza mara 300 katika biblia, Ufunuo huu kuhusu Mungu ulikuwa dhahiri hasa pale wana wa Israel  walipokuwa wamekwama katika eneo ambalo kushoto kulikuwa na mwamba mkubwa sana na kulia kulikuwa na mwamba mkubwa sana na mbele yao ilikuweko bahari ya shamu, wakati huu wakiwa katika kona hii, Farao aliwaamuru majeshi yake kuwafuatia wana wa israel na kuwaangamiza kabisa majeshi yake yalitii na kuwafuatia wana wa Israel ambao wakati huu walikuwa hawajajifunza vita na hawana wa kuwapigania

Kutoka 14:9-10
Wamisri wakafuata nyuma yao, farasi zote na magari yote ya Farao, na askari zake wenye kupanda farasi, na jeshi lake, nao wakawapata hali wamepanga pale karibu na bahari, karibu na Pi-hahirothi, kukabili Baal-sefoni. Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia BWANA.

  
Kwa Mujibu wa mwana historia wa kiyahudi wa nyakati ya karne ya kwanza Flavious Josephus anasema kwamba Majeshi yaliyokuwa yakiwafuatia Israel yalikuwa ni majeshi katili ya makomandoo hodari waliokuwa na Magari ya farasi 600, wapiganaji wa juu ya farasi 50,000 na askari wa miguu 200,000. kwa hiyo unaweza kupata picha kwa taifa hili changa ilikuwa ni haki yao kupiga kelele na kuhitaji msaada wa Mungu, Musa kama Nabii wa Bwana alisema kwa niaba ya Mungu kuwa Israel hawapaswi kuogopa badala yake wanatakiwa kusimama na kuuona wokovu wa Bwana!  Na kuwa hawa wamisri wanaowaona leo hawatawaona tena milele! Bwana atawapigania nao watanyamaza kimya 

Kutoka 14:13-14
Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.

Ni ukweli usiopingika kwamba Jeshi hili kali lingewamaliza Vibaya Israel bila huruma, lakini hata hivyo Bwana aliwapigania kwa jinsi ya ajabu mno, Kumbuka ya kuwa unaposikia Bwana anampigania mtu ni muhimu kufahamu kuwa huwa hapigani yeye, Yeye hutumia malaika wake

Mathayo 26:52-56
Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga. Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?  wanauwezo mkubwa sana na wanapiga vibaya mno, Jambo kubwa ambalo Mungu alilifanya kwanza ni kumtuma malaika aliyesimama kuwatenga Israel na Majeshi ya wamisri

Malaika wa Bwana ndio hufabya kazi ya kupigania watu wa Mungu, Mungu hawezi kupigana na yoyote wala hawezi kupigana na kiumbe chake Yeye ni mwenye nguvu sana uwezo wake ni mzito mno ukimuona tu unakufa mwenyewe hata kabla ya lolote kwa hivyo yeye hutumia malaika ni malaika wa Bwana aliyekwenda kusimama katikati ya wana wa Israel na wamisri ona
 

Kutoka 14:19
Kisha malaika wa Mungu, aliyetangulia mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akaenda nyuma yao; na ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao, ikasimama nyuma yao;

Hapa Malaika wa Bwana alikuwa anatenganisha kwanza kwa ulinzi wake kwa kawaida Mungu anapotulinda hutumia malaika lakini pia hutumia ukuta wa moto ona
 

Zekaria 2:5
Kwa maana mimi, asema Bwana, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.”  

kuna hatua kadhaa hapa ambazo Mungu alizifanya na hatimaye Bwana akawapigania Israel ona
 Kutoka 14:19-28 Kisha malaika wa Mungu, aliyetangulia mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akaenda nyuma yao; na ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao, ikasimama nyuma yao; ikafika kati ya jeshi la Misri na jeshi la Israeli; napo palikuwa na lile wingu na lile giza, lakini lilitoa nuru wakati wa usiku; na hawa hawakuwakaribia hawa usiku kucha. Musa; akanyosha mkono wake juu ya bahari; BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika. Wana wa Israeli wakaenda ndani kati ya bahari katika nchi kavu; nayo maji yalikuwa ukuta kwao mkono wa kuume, na mkono wa kushoto.  Na wale Wamisri wakawafuatia, wakaingia ndani kati ya bahari, farasi zote za Farao, na magari yake, na wapanda farasi wake. Ikawa katika zamu ya alfajiri, BWANA akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri. Akayaondoa magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa uzito; na Wamisri wakasema, Na tukimbie mbele ya Israeli; kwa kuwa BWANA anawapigania, kinyume cha Wamisri. BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao. Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na BWANA akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari. Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja.

ni baada ya israel kushuhudia tukio hili kubwa la kushangaza na utaratibu ambao Mungu aliutumia kuwapigania israel, Waliimba nyimbo za furaha na sasa walianza kumtambua Mungu kama Mtu wa vita , watu wengi wanamjua Mungu kama Mwingi wa rehema na fadhila, wanamjua kama Mungu wa upendo lakini hawajui pia kuwa Bwana ni Mtu wa vita  A man of war” “warriorsasa basi kwanini linatumika jina Mtu kwa kawaida Mungu sio mtu lakini kwanini hapa linatumika neno Mtu? Biblia ya kiebrania inatumia neno Iyshlinasomeka ishi ambalo maana yake ni Mwanaume, kwa hiyo kiebrania Mwanaume wa Vitalakini vilevile mwanaume ni mtu na neno Mtu linapotumika kwa Mungu linamaanisha Yesu Kristo ambaye yeye ni jemadari wa vita ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Mbinguni, Yesu ana nguvu dhidi ya taifa lolote linalompinga yeye, anauwezo dhidi ya yeyote anayesimama kinyume na kusudi lake anauweza na nguvu za kupigana kinyume na yeyote anayeshindana kinyume na agano lake, hakuna mtu, wala mfalme wala rais, wala taifa, wala mamlaka wala wakuu wa giza wala majeshi ya pepo wabaya yanayoweza kupambana naye yeye ni Mtu wa vita israel waliona hili alipowapigania

Farao alifanya ujinga kuamuru majeshi yake kusonga mbele alipaswa kuwaonya mapema warejee nyumbani lakini kwaajili ya kiburi na ubishi aliendelea kupambana na kuwafuatia israel Mungu alimuonyesha uwezo wake wa ajabu wa kupambana Mungu alimtia fadhaa, mungu alichomoa magurudumu yao Mungu alirejesha maji ya bahari mungu aliwafutilia mbali

Jinsi Bwana anavyopigana vita

Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu hapigani au hapiganii mtu au watu hovyo hovyo tu, kama watu wengi wanavyofikiri Mungu hupigania watu wake katika medani ya uadilifu na haki kwa njia ya  juu sana  Kumbukumbu 32:4 Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.kwa msingi huo ili Mungu akupiganie kwanza ni lazima uzingatie maswala kadhaa yafuatayo;-

1. Lazima ujue Bwana yuko upande wa nani!

Maandiko yanasema Bwan akiwa upande wetu Ni nani aliyejuu yetu? Warumi 8:31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?kwa hiyo swali kubwa unapohitaji msaada wa Bwana kwanza ni lazima ujue uko upande gani na Bwana yuko na nani Joshua 5:13-15 Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu? Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana. Yoshua akapomoka kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake? Huyo amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo.”  Hapa Yoshua anatokewa na yule mtu mume yule mtu wa vita amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Bwana na Yoshua anauliza swali la Muhimu sana uko upande gani, kwanini swali hili ni la Muhimu kwa sababu watu wote ni mali ya Mungu Mungu ni Mungu wa wote wenye mwili, kwa hiyo unaweza kudhani yuko na wewe kumbe hayuko nawe, ni hatari kupigana upande ambao Bwana yuko kisha wewe ukawa kinyume naye kwa hiyo ili uweze kushinda ni lazima uwe upande wake na Bwana awe pamoja nawe hii ni kanuni muhimu sana Kumbukumbu 1:42-45 Bwana akaniambia, Uwaambie, Msiende, wala msipigane; kwani mimi si kati yenu; msije mkapigwa mbele ya adui zenu. Basi niliwaambia, msinisikize, bali mliasi amri ya Bwana, mkajikinai, na kukwea mlimani. Na Waamori waliokuwa wakikaa katika mlima huo, waliwatokea juu yenu, wakawafukuza, kama wafukuzwao na nyuki,

wakawapomoshea Seiri mpaka Horma. Mkarudi mkalia mbele za Bwana; Bwana asiisikize sauti yenu, wala hakuelekeza masikio yake kwenu.

 unaweza kuona unapomtaka Bwana akupiganie kanuni ya kwanza Lazima Bwana awe upande wako na ndio maana watu wengi waliokuwa hodari wa vita kama Daudi mara kadhaa kabla ya kupigana vita ya aina yoyote waliuliza kwa Bwana kutaka kujua kuwa yuko na nani ona 2Samuel 2:1 Ikawa baada ya hayo, Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Niupandie mji wo wote wa Yuda? Bwana akamwambia, Haya! Panda. Daudi akasema, Niupandie mji upi? Akasema, Hebroni.

 na 2Samuel 5:19 Basi Daudi akauliza kwa Bwana, akisema, Je! Nipande juu ya Wafilisti? Utawatia mkononi mwangu? Naye Bwana akamwambia Daudi, Panda; kwa kuwa hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako.

unaweza kuona kwa msingi huo kila mtu ambaye anataka Mungu ampiganie ni lazimaahakikishe kuwa Mungu yuko upande wake na ili Mungu awe upande wako ni lazima uishi maisha matakatifu, na yanayompendeza yeye nhuku ndiko kupigana katika mapenzi yake vinginevyo kichapo kitakuhusu.

2. Mungu hupigania mtu mwenye kusudi lake

Wako watu ambao wanabeba kusudi la Mungu, na umuhimu wao unakuwa ni mkubwasana katika macho ya Mungu kutokana na lile kusudi wanalolibeba, kama utapigana na mtu mwenye kusudi la Mungu, haraka sana Mungu atakuondoa wewe na atamuacha mtu mwenye kusudi lake aendelee kuwepo Matendo 5: 38-39 Basi sasa nawaambia, Jiepusheni na watu hawa, waacheni; kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa imetoka kwa binadamu, itavunjwa, lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu.unaona Mungu hupigania mtu au watu ambao ana kusudi nao na kama utapambana na mtu mwenye kusudi la Mungu Mungu haoni vibaya kukushughulikia vikali yeye makusudi yake hayawezi kuzuilika hata kidogo ona Ayubu 42:2 Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika.kwa msingi huo kama mtu anapigana na Kanisa au israel au mtu mwenye kusudi la Mungu ni wazi kuwa unaweza kujikuta unapamba ana Mungu na ukasambaratika vibaya watu kama Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Daudi na kadhalika ambao walikuwa wanabeba kusudi la Mungu ndani mwao, Mungu huingilia kati na kuwatetea sio kwa sababu wao ni wema sana bali kwa sababu wanakusudi lake ndani yao.

3. Mungu hupigania watu wanyonge wasioweza kujitetea

Mtu awaye yote ambaye ni masikini, mjane au yatima Zaburi 140:12 Najua ya kuwa Bwana atamfanyia mnyonge hukumu, Na wahitaji haki yao.Wanyonge masikini na wajane na yatima hutetewa na Mungu kwa msingi huo neno la Mungu linaahidi kuwa awaye yote atakayewadhulumu atapata hasara kubwa sana Mithali 22:16 Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato, Naye ampaye tajiri, hupata hasara. Mungu anachukizwa sana na dhuluma na uonevu hususani dhidi ya masikini unapoingia katika vita na watu wa namna hii ambao hawana uwezo wa kujitetea kutokana na unyonge wao basi ujue unapambana na Bwana ! Mithali 22:22-23 Usimnyang'anye maskini, kwa kuwa ni maskini; Wala usimdhulumu mtu mnyonge langoni; Kwa sababu Bwana atawatetea; Naye atawateka uhai wao waliowateka.Mungu hawezi kuvumilia uonevu wa mtu mnyonge hata kama Mtu huyo yuko mikononi mwa mtu wa Mungu, Kuna wakati Sara alimtesa hajiri sana mpaka hajiri akakimbia jangwani, Sara alikuwa tajiri na hajiri alikuwa mtumwa wake kwa msingi huo sara alifikiri ya kuwa ana hati miliki ya Mungu, Kumbe Mungu huweza kujali na kutetea yoyote amtakaye ona Mwanzo 16:1-10 Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri. Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai. Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe. Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake. Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi na wewe. Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake. Malaika wa BWANA akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri. Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai. Malaika wa BWANA akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake. Malaika wa BWANA akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.

4. Mungu hupigania watu wanyenyekevu /wapole.

Ogopa sana Mtu anayejishusha au mtu mpole ambaye yeye anamuachia Mungu tu kila kitu ili Mungu aingilie kati na kumtetea, Katika neno lake Mungu ameahidi kumwangalia mtu mnyonge ona Isaya 66:2 Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.Mungu hana muda na mtu mwenye kiburi, unapokuwa na kiburi haraka sana unanyimwa neema na kupingana na Mungu ona Yakobo 4:6 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. mtu mnyenyekevu au mpole sana unapoingilia kati na kumsumbua Mungu ndiye atakayejibu kwa niaba yake ona Hesabu 12:1-10 Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao. Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. Bwana akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje. Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili. Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, Bwana, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa? Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.

5. Mungu hupigana kwaajili ya Jina lake takatifu

Kuna mambo Mungu anaweza kuyafanya katika maisha yetu kwa sababu tu tunabebajina lake Zaburi 23:1-3 Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.”  Kama ikitokea kuwa Mungu anaona jina lake linachafuliwa, Yeye amejikuza sana Duniani na jina lake amelitukuza mno Walawi 22:32 Wala msilinajisi jina langu takatifu; lakini nitatakaswa mimi katika wana wa Israeli; mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi,Inapotokea mtu anafanya mambo ya ajabu ajabu kisha anajivunia upuuzi wake kuliko jina la Mungu aliyehai Mungu husimama na mtu amabaye anajua kupitia yeye jina lake litatukuzwa ona 1Samuel 17:45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.

6. Mungu hupigana kwaajili ya masihi wake.

Watu waliotengwa kwa kusudi la kumtumikia Mungu huwa wanapakwa mafuta kwa kazi hiyo na maandiko huwa yanasema mtu akimtumikia Mungungu atamuheshimu ona Yohana 12:26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.wote wanaomtumikia Yesu, baba huwaheshimu sana Mungu hataacha heshima ya watumishi wake ivunjwe kwani kuvunjwa heshima ya watumishi wake ni kuvunjiwa hehsima yeye  ona Zaburi 105:14-15 Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao. Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.unapopambana na mtu wa Mungu na hasa aliyepakwa mafuta mwisho wa siku wewe ndiye utakayepondwa na kupigwa radi kisha Mungu ataitukuza pembe ya masihi wake 1Samuel 2:10 Washindanao na Bwana watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; Bwana ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.

Muhimu.
Mungu anaupendo mwingi na mkubwa sana na wala hapigani pasipo sababu, awaye yote akipigana na Mungu atakufa haraka sana, Na ndio maana Mungu sio mwepesi wa hasira wala hahesabu maovu yaya anatoa mwaliko kwa kila mtu kumjia kwa dhati na kumtegemea na kumtumainia kwa moyo wa dhati na yeye atakuwa pamoja nasi wakati wote tutakapomuomba Mungu atatusikia kama tutakuwa pamoja naye na kuishi kwa mujibu wa kanuni zake, Yeye ni Mtu wa vita lakini hapendi vita lakini uko wakati Mungu hupigana au hupigania watu wake kwa sababu kadhaa wa kadhaa zaidi ya zile zilizotajwa hapo juu hivyo kaa katika kusudi la Mungu uweze kutetewa na Mungu!

Na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Rev. Innocent Samuel Kamote

0718990796.