Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu
amemkusudia kila mwanadamu kuwa na uwezo wa kufanya mambo ya kushangaza,
Mwanadamu hakuumbwa kama kiumbe kingine cha kawaida, wanadamu sio viumbe wa
mchezo mchezo, wanadamu sio tu viumbe vya kijamii lakini inaonekana kuwa
mwanadamu ni kiumbe kilichobarikiwa uwezo mkubwa sana wa kubuni mambo na
kutengeneza vitu na vingine vikadumu kwa muda mrefu sana, Mwanadamu ni kiumbe
wa kushangaza, Nyani wanaweza kushangaza namna wanavyoruka toka tawi moja hata
lingine lakini hakuna jipya wanaloweza kulifanya, sivyo ilivyo kwa wanadamu ni
kiumbe wa ajabu Mungu amaemuumba kwa ajabu mno mno.
Matendo 6:8 Biblia inasema “Na Stefano, akijaa
neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.”
Biblia inatuambia kuwa Stefano
alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu, maana yake Mungu anaweza
kumtumika kila mtu kwa karama yake kufanya mambo makubwa ya kutisha na
kushangaza
·
Maana ya neno Kushangaza
·
Mifano ya watu waliofanya mambo makubwa ya
kushangaza
·
Siri ya kufanya mambo ya kushangaza
Maana ya neno Kushangaza.
Neno Maajabu tunalolizoma katika
Matendo 6:8 limatokana na neno la Kiyunani “TERAS” Kiebrania “PALA”
ambalo kiingereza husomeka kama “WONDERS”,
“MARVELLOUS”, au “ TREMENDUS” Kwa hiyo kufanya maajabu
maana yake ni kufanya mambo ya kushangaza, kila mmoja anaweza kuushangaza
ulimwengu kwa kadiri ya neema na uwezo aliopewa na Mungu.
Mifano ya watu waliofanya mambo makubwa ya kushangaza
Dunia imakuwa na historia ya watu
wengi waliofanya mabo makubwa ya kushangaza na wengine wanakumbukwa hata leo,
kutokana na mambo makubwa waliyoyafanya
Muda hauwezi kutosha kuelezea
Jinsi wamisri walivyojenga Pyramid zaidi
ya miaka 2500 kabla ya Kristo ni majengo ya ajabu sana hawakuwa na cranes wala
winch lakini katika ujuzi mkubwa wa kihesabati waliweza
1. Huko
ufaransa katika jiji la Paris uko mnara mkubwa sana unaojulikana kama Iron Lady
wenyewe wanauita “La Dame de Fer” yaani mwanamke wa chuma mnara huu unavutia
maelfu ya watu kila mwaka kwenda kuuangalia mnara huo wa chuma mzuri na wa
kuvutia lakini jambo la kushangaza mnara huu pia ujulikanao kama “Eiffel Tower” umejengwa mwaka 1889 na
ulibuniwa na Enjinia “Gustave Eiffel” inaweza kukushangaza mnara wa siku nyingi
hivyo unamvuto mkubwa mpaka leo duniani
2. Empire states Mimi niliwahi kufika
mahali hapa katika jiji la New York Jengo hili lilikuwa ndio jingo refu zaidi
katika jiji la New York na lilikuja kupitwa baadaye na Trade towers
zilizojengwa mnamo miaka ya 1931-1975, kwa miaka zaidi ya 40 kabla ya 1931
Jengo hili limekuwa ni la aina yake.
3. Stature of Liberty ni Sanamu
iliyoshikilia Mwenge iko katika lango la bandari ya jiji la New York ni moja ya
sanamu yenye mvuto mkubwa sana hata leo lakini ilizinduliwa tarehe 28 October
1886 na mbunifu wake aliitwa Fredrick
Berthold
4. Ikulu
ya marekani WHITE HOUSE ni ikulu
yenye mvuto mkubwa sana ilianza kukaliwa na maraisi wote walioko Marekani tangu
rais Adam ni nzuri naya kifahari watu wengi hutembelea hapo mimi pia nilipata
nafasi ya kupiga picha hapo, pamoja na mvuto mkubwa wa nyumba hiii ya kifahari
na yenye kupendeza huwezi kuamini kuwa ilijengwa kati ya mwaka 1792 – 1800.
Tukiwa White House kutoka kushoto Athur Chikoka, Rev. Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi mwenye hekima, William Boniventure Kifutumo Nyadili, Yohana Martin Komba, Imani Peter Mngazija, Onstard Mashauri, Hubert Gumbo na baraka kolombo tulipotembelea Marekani mwezi Juni 2014
5. Kwa
nini mifano hii yote? Ni kuonyesha kuwa wanadamu wanauwezo mkubwa sana wa
kufanya maajabu wa kufanya mabo ya kutisha na kushangaza, tunaweza kufanya
katika, masomo yetu, katika kuimba, katika kucheza soka katika kufundisha
katika kupika na kila eneo Mungu analotupa tunaweza kulifanyia kazi kwa bidii
na juhudi na kwa maarifa makubwa na tukaonekana watu wa tofauti
Mungu ndi ye
mfanya maajabu makubwa zaidi duniani na Mbinguni kwa uwezo wake neema yake na
roho wake anaweza kabisa kutusaidia kufanya mamnbo makubwa ya kupita kawaida ya
kutisha na kushangaza
Siri ya kufanya mabo ya kushangaza
1.
Jiunganisha na Mungu kwa wokovu
2.
Jaa Roho Mtakatifu
3.
Omba neema na uweza Matendo 5:12, 6:8, 19:11
4.
Muombe Mungu Ishara na maajabu vifanyike Matendo
4:43
5.
Mwambie Mungu akujalie Matendo 14 :3
6.
Uwe na Bidii katika kila unalolifanya
Ukiyajua hayo Heri wewe
ukiyatenda.
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni