Alhamisi, 26 Januari 2017

Mfano wa tai ayashukiaye Mawindo!


Andiko: Ayubu 9: 25 -26 Biblia inasema “ Basi siku zangu zina mbio kuliko Tarishi; Zakimbia wala hazioni mema, Zimepita kama merikebu ziendazo mbio; Mfano wa tai ayashukiayemawindo.”



Leo tutachukua muda kutafakari kwa kina somo kuhusu Mfano wa tai ayashukiaye Mawindo, Ni muhimu kuwa na ufahamu kuwa Mungu aliviumba viumbe vingi duniani kwa makusudi mbali mbali lakini mojawapo ya kusudi kuu ni kutufunza mambo mbalimbali ya msingi, Tai ni moja ya Ndege au kiumbe ambaye biblia imezungumza sifa zake kwa kina na mapana na marefu na tunaweza kujifunza mambo kadhaa ya muhimu kutoka kwa kiumbe hiki.
Kuna usemi wa wahenga kuwa ndege wa aina moja huruka pamoja, Usemi huu kwa Tai ni tofauti tai wanaruka pekeyo na wanafurahia kuruka juu sana, sifa zake zinawekwa katika Biblia kwa vile ni ndege mwenye sifa za kipakee ni ndege asiyeshindwa na ukubwa wa mawindo yake.
Kwa nini Biblia inampa Tai sifa za hali ya juu sana ni muhimu kwetu kujifunza sifa zake na kuzilinganisha na maisha yetu.

1.       Tai ni wenye uwezo mkubwa wa kuona mbali.



Ayubu 39:27-29 Biblia inasema hivi “ Je! Tai hupaa juu kwa amri yako, Na kufanya kioto chake mahali pa juu?  Hukaa jabalini, ndiko kwenye malazi yake, Juu ya genge la jabali, na ngomeni. Toka huko yeye huchungulia mawindo; Macho yake huyaangalia toka mbali.”

Tai kama utamfanyia uchunguzi na kumchungulia kwa mbali ni ndege makini sana Biblia inamsifia kuwa “macho yake huyaangalia mawindo toka mbali” ndi ndege hodari katika kuwinda macho yake amebarikiwa uwezo wa kuona mbali sana na anaona kwa uwazi kabisa inasemekana anauwezo wa kumuona mwenzake akiwa Maili 50 kwa uwazi kabisa! Jambo hili linatufundisha nini? Naamini unaweza kupata picha Fulani

Mamia ya watu hodari wamewahi kuishi duniania na kupita wakiwemo watu maarufu sana duniani na viongozi wakubwa

Ili dunia iweze kuwa na Mafanikio makubwa sana inahitaji watu na viongozi wenye uwezo wa kuona mbali sana, Abraham Lincoln rais wa 16 wa Marekani aliongoza katika wakati mgumu sana wenye matatizo mengi na inchi ikiwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini ndiye aliyefanikiwa kuweka misingi ya umoja na kukomesha utumwa na kuifanya Marekani iwe kama ilivyo leo,

Ili dunia iweze kuwa na mafanikio ni lazima iwe na watu wenye uwezo wa kuona mbali, wanaoangalia faida za mbeleni za kwao na za kizazi kinachokuja badala yao
·         Watu wasio na maono ya mbali wanaweza kutugawa kupitia dini na ukabila
·         Watu waioona mbali hawajali kutunza Mazingira
·         Watu wasioona mbali hawaogopi kuharibu mahusiano
·         Watu wasioona mbali hawaogopi kuua wanyama kama tembo kwa faida yao
·         Watu wasioona mbali hawaogopi kufanya Ufisadi kwa kuifilisi nchi
·         Watu wasioona mbali hawafikiri kujisomea kwa bidii
·         Watu wasioona mbali hawafikiri kujiwekea akiba
·         Watu wasioona mbali hawafikiri kuhusu maisha yao baada ya kufa duniani
Awaye yote aliye kama tai atakuwa na ujuzi wa kuona mbali na kuzingatia faida za siku zijazo kuliko kuangalia leo. Unayaona mwindo yako kwa mbali. Ni lazima tuwe na maono makubwa yaliyopimwa kwa kina na yatakayoleta faida kubwa na matokeo makubwa katika jamii.

2.       Tai ni ndege wasioogopa Mawindo.


Tai ni ndege asiyeogopa hata kidogo, wakati wote anapambana kuhakikisha anashinda, atapambana kuhakikisha anapata mawindo yake au anatawala,unapoangalia sinema za maisha ya tai utaweza kuona  hawaogopi mawindo haijalishi mawindo yao ni makubwa kiasi gani hata kama ni mbuzi ambaye anaonekana kuwa mkubwa kuliko uwezo wake tai ni lazima atabeba, wana ujuzi mkubwa wa kuwinda na ni mahodari, tai haogopi
Ni muhimu kufahamu kuwa kama unataka kufanikiwa katika maisha haya usiogope kufanya jambo gumu, usiogope kukabiliana na watu wakubwa au waliokuzidi umri, hakikisha kuwa unakipigania kile unachokipenda,
·         Usiogope kupigania unachokipenda
·         Usiogope kusimama katika kweli hata kama itakuletea madhara
·         Usiogope ukubwa wa tatizo unalopambana nalo pigania mpaka kieleweke
·         Usiogope ugumu wa masomo unayosoma
·         Usiogope au kuonea aibu aina ya kazi unayoifanya
·         Lengo lako kuu ni kuhakikisha unafanikiwa
·         Usiogope mateso utakayoyapata kwaajili ya imani au kile unachokipigania
·         Usiogope kuanzisha huduma au kufungua kanisa, usiogope kuwa mmisionary, usiogope kugombea urais kama Mungu anataka ufanye jambo kwa faida yako lifanye
·         Uisogope kufanya lolote ili kufafikia malengo yako, Tai hawaogopi mawindo yao hata kama anachokiwinda ni kikubwa kuliko umbile lake.

3.       Tai ni Hodari hawaogopi Dhuruba.


Ukitaka kujua uhodari wa Tai utaweza kuuona wakati wa dhoruba, wakati huu ndege wengine wote hukimbia na kujificha kwa kuogopa dhoruba , kwa tai mambo ni tofauti anafunua mbawa zake na kuzitanua na kupaa kwenda juu zaidi, taia wanatabia ya kutumia dhoruba kwa faida, wakati ndege wa kawaida wakiogopa, ni muhimu kufahamu kuwa watu wanaolinganishwa na tai hawakimbii changamoto zozote bali huzitumia changamoto kusimama na kuongeza viwango, Mungu anataka watu wasiokimbia changamoto bali wenye uwezo wa kukabiliana nazo huku wakisimama katika kusudi au kuelekea juu zaidi

4.       Tai wanaruka juu sana.



Ndege huyu ndiye anayejulikana kama mfalme wa ana inasemekana tai wanauwezo wa kuruka juu kiasi cha fiti 10,000, katika kiwango hicho hutaweza kumuona ndege mwingine na ukimuona ni lazima atakuwa tai, Tai haruki wala kutafutiza chakula pamoja na njiwa, alisema Dr, Myles Munroe Marehemu, alisema wakati njiwa wakiwa ardhini wanacgakuachakua siku nzima na kulalamika, Taia hawanung’uniki, hawapigi kelele, wanapaa juu sana wakisubiri mawindo wakisubiri nafasi waweze kuitumia, watu wakuu duniani ni wale wanaotatua matatizo na sio wanaolalamika, wanatumia nafasi na changamoto yoyote kama tai dhoruba inapotokea.

5.       Tai hawali kibudu
Ni muhimu kufahamu kuwa sifa nyingine ya tai ni pamoja na kutokula kibudu tai hawali wasichokiua wenyewe, siku zote wanakula nyama ya mawindo yao wenyewe, wanakula nyma safi na mpya hivi ndivyo watu wakuu katika dunia wanavyopaswa kuwa
Watu wakubwa duniani hukaa na watu wenye mawazo mapana na wenye kufikiri na wenye uwezo wa kuamua, watu hodari wasiokata tamaa, hawa ndio watu wanaoweza kulete mabadiliko makubwa Duniani, watu wenye uwezo wa kuleta badiliko unapowasikiliza au kukaa nao karibu, watu wenye ushawishi
Kamwe usipoteze muda na watu wanaopoteza muda
Kamwe usipoteze muda na watu wenye kusengenya
Kamwe usipoteze muda na watu wasio na imani
Kamwe usipoteze muda na watu wenye kuzungumzia wengine
Kamwe usipoteze muda na watu wenye kupiga majungu na fitina
Kamwe usipoteze muda na watu ambao kuanguka kwa wengine ndio furaha yao
Kamwe usipoteze muda na watu wenye kuhukumu
Kamwe usipoteze muda na watu wenye mitazamo hasi wenye kujihusisha na rushwa na uovu hivyo ni vibudu, tafuta vya kwako mwenyewe mawindo yako mwenyewe.



Tai anayekula Mizoga!
Ni muhimu kufahamu kuwa tai tunayemzungumzia hapa  mwenye sifa tulizozitaja anaitwa Eagle huyu hali mizoga na taia anayetajwa katika Mathayo 24:28 huyu ndiye taia anayekula mizoga huyu anaitwa VULTURE
§  Mathayo 24:28Kwa kuwa popote ulipo mzoga ndipo watakapokusanyika tai”
§   Matthew 24: 28 "Whenever there is carcass, there the VULTURE will gather” NIV.
§  Matthew 24: 28 "For wheresoever' the carcase  is there will eagles be gathered together KJV
Tai anayekula Mizoga haitwi “Eagle” anaitwa  “Vulture”
Huyu ni aina nyingine ya tai ambaye hupatikana mashariki ya kati nyikanani na katika mbuga za wanyama Afrika tai huyu ndiye anayekula mizoga kiingereza sahii anaitwa VULTURE huyu ndiye ambaye Yesu anazungumza katika injili ya Mathayo  

Tai aina ya Vulture ndiye anayekula Mizoga na sio Tai aina ya Eagle

6.       Tai wanauwezo wa kujitia nguvu mpya
Zaburi 103:4-5 “ Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,  Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai;”


Isaya 40:31 “Bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”
 
Moja ya tabia ya tai ya kushangaza sana ni uwezo wake wa kujitia nguvu kwa upya ukiacha kuwa wanauwezo wa kuona mbali lakini wana maisha marefu inasemekana Tai anapofikisha miaka 30 anakuwa anachakaa na manyoya yake yanakuwa yamezeeka hivyo kuathiri uwezo wake wa kiutendaji, inapofikia hivyo tai hakati tamaa ya kuishi badala yake hutafuta kilele kikubwa cha mlima na kutulia kwa miezi mitano anagonga mdomo wake katika mawe ya miamba na kungoa ngozi ya juu, hujinyonyoa manyoa nyake yote wakati huu ajajigomoa na kuanza kuwa na manyoya mapya mdomo mpya na magamba mapya jambo hili humfanya tai awe na uwezo wa kurejexza uhai wake kwa miaka mingine 30-40, Ndo maana biblia inasema ujana wako utarejezwa kama tai
 Watu wenye akili ni watu wanaoweza kujitafakari na kuangalia yote waliyoyafanya katika maisha yao liwe jema au baya linapokuwa baya unaachana nalo  wanatafuta nini lililo jema na lipi wanaweza kuliendeleza na jipya gani wanaweza kuenda nalo, na kujifunza jambo jipya la kufanya siku hadi siku.
Kamwe sukubali kudumaaa
Usikubali kubaki vilevile siku zote

7.       Tai wanatoa mafunzo kwa vifaranga vyao


Amini usiamini tai wanaotoa mafunzo kwa vijana wao, tai wanafikiriwa kuwa ni ndege katili sana wakati wa kutoa mafunzo na kama hujui makusudi yao unaweza kukubaliana kuwa ni ndege wakatili, jambo moja la kushangaza kuhusu tai ni uwezo wake wa kutoa mafunzo kwa vifaranga vyake, utafiti unaonyesha kuwa hakuna aina ya ndege mwenye mvuto na mpole kama tai kwa watoto wake kushinda tai
Mama wa tai anapogundua kuwa wakati umefika kwa vifaranga vyake kujifunza kuruka, anawabeba vifaranga wake mgongoni na kupanua mbawa zake anaruka juu sana kisha anajiondoa kutoka kifaranga chake na kukiachia kiangukekinapoanguka kinajifunza kuruka akiona kinaogopa na kinataka kuanguka anakidaka na kukirejeza katika kiota chake, atafanya hivyo mpaka kimejifunza kuruka.

Watu wakubwa sana duniani sio mabosi, wakati wote wanawafanya wengine kukua katika jamii na wanawapa changamoto lakini wanawasaidia kukua na kujiamini na kuendelea kuwapa maelekezo wengine mpaka wameweza kufanya vilevile kama wao wafanyavyo.

Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima
0718990796

Maoni 3 :

Unknown alisema ...

Nimebarikiwa sana na Mahubiri ya tai Mungu akuinue mtumishi

Bila jina alisema ...

Njmebarikiwa mno💪💪

Bila jina alisema ...

Ata Mimi nimefurahia sana mafundisho ya tai. Ubarikiwe sana