Mstari wa Msingi: Yohana 16: 23 -24
“Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia,
Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba
neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; FURAHA YENU IWE TIMILIFU.”
Je wewe hutegemea hali ya nje kama chanzo cha Furaha maishani mwako? Angalia kwamba Mungu ndio chanzo kikubwa cha furaha timilifu na sio vinginevyo
Utangulizi:
Maisha ya mwanadamu yanategemea sana kuwa na furaha ili yawe maisha, na
mwanadamu siku zote anafanya kila kitu kwaajili ya furaha yake tuu.
Furaha ndio kilele cha maisha ya mwanadamu, kila analolifanya mwanadamu
lengo lake kuu ni kupata furaha.
Mathalani ukitoa msaada kwa mtu
moyo huwa na furaha, ukipongezwa au kusifiwa kwa jambo fulani moyo huwa
na furaha, ukiwa mshika ibada moyo huwa na furaha, ukiwa na mke mwema au
mume mwema moyo huwa na furaha vilevile, ukiwa na watoto wazuri na
wenye adabu na kujiheshimu, ukifanya kazi kwa ufanisi, ukipata malipo ya
kazi yako au mshahara moyo huwa na furaha kadhalika, ukisikiliza mziki
au filam ama picha na hata kusoma vitabu moyo huwa na furaha pia, Ukiwa
na mafanikio makubwa, ukijenga nyumba, ukiwa na mashamba, ukinunua gari,
ukipandishwa cheo, ukichumbiwa, ukiolewa, ukizaa mtoto, ukiwa na afya
njema moyo huwa na furaha, ukipewa tuzo, ukishinda uchaguzi, ukimiliki
kampuni na kufanikiwa Moyo huwa na furaha Lakini pamoja na hayo yooote
bado utaweza kuona kuwa hakuna furaha iliyo timilifu, Je ni wapi
tunaweza kuona na kuwa na furaha timilifu?
Furaha nini?
Ni vigumu sana kuielezea furaha zaidi ya neno lenyewe furaha, Katika
kiingereza neno linalotumika kuelezea furaha ni “JOY” ambalo katika
lugha ya kiyunani ni “CHARA” linatamkwa “KHA-RAH” ambalo maana yake ni
Hali ya kujaa raha katika nafsi kutokana na kufikia au kufanikiwa katika
jambo fulani, hali ya kuwa na raha isiyo na mipaka kutokana na
kutoshelezwa kwa nafsi.
Katika imani ya Kikristo tunaweza kusema
ni Raha ya nafsi ndani ya mwamini anayopipata kama matokeo ya Neema na
upendo wa Roho Mtakatifu kumuwezesha mtu huyo, kufurahia kuwa na
uhusiano na Mungu na kumjua Yesu Kristo, Neno lake na makusudi yake na
tumaini lililo ndani yake.
Je ni watu wangapi wana furaha?
Ukiulizwa swali je una furaha je unaweza kulijibu vipi? Ni swali gumu
sana, kwani unaweza ukawa una furaha lakini unafahamu kuwa furaha hiyo
haidumu milele. Labda una furaha kutokana na kuwa una familia nzuri,
lakini kwa kina utaona kuwa furaha hiyo inategemea uwepo wa familia
nzuri, na uwepo huo ukitenganishwa kwa vifo, maisha, mabadiliko
mbalimbali basi furaha yake nayo inaisha. Hivyo kuna furaha za milele na
furaha ya muda mfupi.
Kila mtu anapenda kuwa na furaha, na lengo
kuu la maisha ni kuwa na furaha. Hata hivyo furaha ya watu wengi sana
sio furaha timilifu kwa sababu furaha zao zinatawaliwa na hali ya nje ya
maisha yao angalia mfano huu:-
Mtu moja alikuwa anamiliki nyumba
nzuri sana ni nyumba ya thamani na ilikuwa yenye kupendeza na yenye
mvuto mkubwa sana katika mji aliokuwa anaishi, na jamaa huyu aliipenda
nyumba yake sana watu wengi waliwahi kumuendea na kumuomba awauzie hata
kwa bei kubwa mara mbili ya thamani yake lakini alikataa, wakati fulani
bwana huyu alisafiri na aliporejea aliikuta nyumba yake ikiwa inawaka
moto mkubwa sana na hivyo alipatwa na huzuni kubwa mno! Mamia ya watu
walikusanyika kwaajili ya kuangalia namna ya kusaidia kuuzima moto ule,
lakini hakuna walichofanikiwa kukiokoa katika moto ule
Mara
mwanae mkubwa alimjia na kumnongoneza sikioni, Baba usiogope, “Niliiuza
nyumba hii jana na niliiuza kwa bei nzuri sana, bei ilikuwa nzuri kiasi
ambacho nisingeliweza kukusubiri au kukutaarifu, Hivyo unisamehe bure tu
baba”
Baba yule alivuta pumzi na kuzishusha akimshukuru Mungu kwani sasa amekuwa moja ya washuhudiaji wa ajali ile kama walivyo wengine,
Mara mwanae wa pili alikuja mbio akimkimbilia na kumbwambia baba
unafanya nini uangalia nyumba yetu ikiwa inaungua? Baba alimjibu kijana
yule kuwa tulia kwani kaka yako aliiuza tayari kwa bei nzuri, Kija ayule
alimwambia baba yake kuwa tulichukua kiwango fulani tu cha fedha na sio
zote hivyo nina mashaka kama yule aliyenunua atakubali kumalizia
ilihali nyumba imeungua!
Yule baba alianza kulia tena, machozi
ambayo mwanzoni alikuwa ameshasahau,Moyo wake ulianza kwenda mbio sana
na nguvu zikaanza kumuishia alikuwa mwenye huzini kubwa sana, Mara mtoto
wake wa tatu akaja na kumwambie Baba yule mtu aliyenunua nyumba yetu ni
mtu mwema na mwaminifu na mwenye kutunza sana ahadi kwani nimetoka
kuongea naye sasa na ameniambia “ Haijalishi kwamba nyumba imeungua au
la Nyumba ni yangu na nitalipa kiwango chote cha fedha tulichopatana,
kwa kuwa hakuna aliyejua kuwa nyumba itaungua, Kisha wote wakasimama
wakiwa wametulia kama washuhudiaji wengine wakiangalia nyumba inayoungua
bila wasiwasi wowote!
Tunajifunza nini kutokana na kisa hiki?
Watu wengi sana wanajisikia kuwa wenye furaha kutokana na hali ya nje ya
mambo na sio ya ndani na kwa sababu hiyo hawawezi kuwa na furaha ya
kweli, furaha ya kibinadamu ya ya dunia hii ni yenye kuyumba kutokana na
hali halisi ya kubadilika badilika kwa mambo, aidha furaha ya kweli
haipatikani kwa kuwakosea wengine.
Wako watu wengine wanafikiri
kuwa watakuwa wenye furaha kwa sababu ya kukandamiza wengine, kuwatesa,
kuwatendea vibaya, kuwashitaki, kuwasengenya, na kuwakosea ni muhimu
kufahamu kuwa watu wote wanahitaji furaha kwa sababu hiyo kama huwezi
kuwasaidia wengine kuwa wenye furaha basi jitahidi usiwe sababu ya
huzuni zao, furaha ya kweli hua kwa kuhakikisha kuwa wengine wana furaha
kama wewe na sio kuwakosea.
Faida za kuwa na furaha timilifu
Kwa mujibu wa wataalamu wa maswala ya saikolojia wanaeleza kuwa furaha ina faida kubwa sana
Zikiwemo
Zikiwemo
a. Inakulinda na magonjwa ya Moyo
b. Inaimarisha kinga za mwili
c. Inatupilia nje mikandamizo ya mawazo katika maisha
d. Inakulinda dhidi ya Magonjwa
e. Inarefusha maisha
b. Inaimarisha kinga za mwili
c. Inatupilia nje mikandamizo ya mawazo katika maisha
d. Inakulinda dhidi ya Magonjwa
e. Inarefusha maisha
Kitaalamu hata utungiswaji wa Mimba hutokea siku ambayo wana ndoa wote wamefurahi
Unawezaje kuwa na Furaha timilifu?
Kaa katika uwepo wa Mungu Zaburi 16:11 “Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.” Unaweza kuona maneno Mbele za uso wako ziko furaha tele
yanamaanisha mbele za uwepo wa Mungu “Presence” kuna furaha tele, Musa
alikuwa ni mtu aliyependa kukaa katika uwepo wa Mungu, alikaa uweponi
mwa Munngu kiasi ambacho hakusikia njaa kwa siku 40 na hata aliporejea
uso wake ulikuwa unangaa’ kiasi ambacho watu walishindwa kumtazama
Kutoka 34:29-35 “Hata ikawa, Musa aliposhuka katika mlima Sinai, na zile
mbao mbili za ushuhuda zilikuwa mkononi mwa Musa, hapo aliposhuka
katika mlima, Musa hakujua ya kuwa ngozi ya uso wake iling'aa kwa sababu
amesema naye. Basi Haruni na wana wote wa Israeli walipomwona Musa,
tazama, ngozi ya uso wake iling'aa; nao wakaogopa kumkaribia. Musa
akawaita; Haruni na wakuu wote wa kusanyiko wakarudi kwake; Musa akasema
nao. Baadaye wana wa Israeli wote wakakaribia; akawausia maneno yote
ambayo BWANA amemwambia katika mlima Sinai. Na Musa alipokuwa amekwisha
kusema nao, akatia utaji juu ya uso wake. Lakini desturi ya Musa ilikuwa
alipoingia mbele za BWANA kusema naye, kuuvua huo utaji mpaka atoke;
akatoka akawaambia wana wa Israeli maneno yote aliyoambiwa. Wana wa
Israeli wakauona uso wa Musa ya kuwa ngozi ya uso wake Musa iling'aa;
naye Musa akautia utaji juu ya uso wake tena, hata alipoingia kusema
naye.”
Usitawaliwe na hali ya nje.
Habakuki 3:17-18 “Maana
mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya
mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa
na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng'ombe; Walakini
nitamfurahia Bwana Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.” Kwa mujibu wa
Habakuki ni kuwa yeye atamfurahi Mungu bila kujali kuwa mtini
haujachanua maua, au zabibu hazina matunda aku mzaituni haukuzaa au
mashamba hayakutoa chakula au mazizi mifugo kutokuwa na kitu, Yeye bado
atafurahi, hii ni wazi kuwa Mungu ndio chanzo cha furaha yetu na sio
vinginevyo.
Dumu katika kuomba.
Kwa mujibu wa Yesu Kristo
ukweli ni kuwa maombi yanasaidia kwa kiwango kikubwa sana kuketa firaha
timilifu, kila amtu anapaswa kuomba, maombi ni muhimu sana, usiache
kuomba Yohana 16: 23 -24 “Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin,
amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.
Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; FURAHA
YENU IWE TIMILIFU.”
Mwamini Mungu na Kumtegemea.
Warumi 15:13
“Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika
kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho
Mtakatifu.”, Imani katika Mungu na kumtegemea yeye kunaweza kutupa
furaha timilifu.
Watumikie wengine Watu wanaowatumikia wengine huwa na furaha sana Duniani.
Na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.
Rev. Innocent Kamote