Mwanzo 16:1-13 “Basi Sarai mkewe Abramu
hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri. Sarai
akamwambia Abramu, Basi sasa, BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie
mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.
Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu
katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe. Basi
akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba,
bibi yake alikuwa duni machoni pake. Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata
na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba
amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi
na wewe. Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako,
mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele
yake. Malaika wa BWANA akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa,
chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri. Akamwambia, Hajiri, wewe
mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi
kutoka mbele ya bibi yangu Sarai. Malaika wa BWANA akamwambia, Rudi kwa bibi
yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake. Malaika wa BWANA akamwambia, Hakika nitauzidisha
uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi. Malaika wa BWANA
akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina
lake Ishmaeli, maana BWANA amesikia kilio cha mateso yako. Naye atakuwa kama
punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu
wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote. Akaliita jina la
BWANA aliyesema naye, Wewe U Mungu uonaye, kwani alisema, Hata hapa nimemwona
yeye anionaye?”
Ni muhimu kwa kila mwanadamu kuwa
na ufahamu kwamba kila wakati tunapopitia Mateso na mambo magumu ya kukatisha tamaa, kukumbuka kuwa
hatuko wenyewe, Mungu aonaye “Jehoha
Rohi” anaona kila tunalolipitia na kila kinachotokea katika maisha yetu,
Mungu anajali sana na anajishughulisha
sana na mambo yetu, Yeye sio mwepesi wa hasira, wala sio Mungu aliye mbali, au
asiyejali yeye anajali, anatamani sana tuwe na mambo mazuri na kila kitu
kituendee vizuri katika maisha yetu, anataka kila mmoja wetu aweze kuwa na
maisha ya ushindi na furaha, sisi ni watoto wake ni kondoo wa malisjo yake
anawajibika kututunza na kushughulika na mahitaji yetu Bila upendeleo.
Mungu anajua na anaona kila unachopitia.
Mwanzo 16:1-6 “Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na
mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri. Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, BWANA
amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa
yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai. Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri
Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi,
akampa Abramu mumewe, awe mkewe. Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba.
Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake.
Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi
wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni
machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi na wewe. Naye Abramu akamwambia
Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako.
Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.”
Katika kifungu cha maandiko wote
tunaweza kuoina hali halisi, iliyojiyokeza katika familia ya Ibrahimu na Sara a
mjakazi wao Hajiri, kwamba japo jambo hili lilikuwa sawa katika mila na desturi
za kikaldayo, lakini haikuwa sawa katika macho ya Mungu, ziko mila na desturi
ambazo watu baada ya kuwa na urafiki na Mungu wakizifuata zinaweza kuharibu
mtiririko wetu wa imani katika kuonyesha kuwa tunamtegemea Mungu, Sara alikuwa
amechoka kwa mapito aliyokuwa akiyapitia, Mungu alikuwa amemuona Sara na
alikuwa amekwisha kumuahidi kuwa atamkumbuka lakini Sara alikuwa ameelemewa na
huzuni na maumivu:-
·
Maumivu yamatumaini yaliyokuwa yakitarajiwa
lakini yamechelewa
·
Maumivu yanayoashiria kana kwamba Mungu hajajibu
mamombi au amechelewa kujibu maombi
·
Maumivu kwamba mikono yake haijawahi kushika
mtoto wake mwenyewe
·
Maumivu ya aibu kujulikana kama mwanamke aliye
tasa au mgumba na asiyezaa katika jamii
·
Maumivu ya kumlaumu Mungu kama asiyejali maumivu
yake na mateso yake
Hali hii inampelekea Sara kuamua
kutumia akili na njia za kibinadamu kutatua tatizo walilonalo katika familia
yake, Usahwishi wake kama ilivyokuwa kwa Eva na Adamu unasikilizwa na Ibrahimu,
wanaamua kuongeza mke ambaye ni Hajiri, Bila shaka ni moja ya watumwa
(Kijakazi) wa Sara aliyepewa huko Misri
na Farao, Matumizi yao ya akili katika kutaka kutatua tatizo lao nje ya mfumo
wa njia za kimungu kunaleta tatizo kubwa zaidi, Hajiri anashika Mimba, lakini
yeye sasa anapoteza kutii, kule kushika Mimba kunampa kiburi, anasahaku kuwa
aliinuliwa kwa mawazo ya Sara, mgogoro unakuwa mkubwa sara anaona Abrahamu kuwa
pia ni sehemu ya tatizo, Abrahamu anamuonyesha sara kwamba hajiri bado ni
mtumwa wake ni mjakazi wake anaweza kumfanya anachokitaka, sasa sara anamtesa
Hajiri, huku Ibarahimu akiwa ameridhia kuteseka kwa Hajiri, mwanamke huyu
mnyonge, na masikini sasa hana namna kibano kimezidi kuwa kikali sana na sasa
anakimbia jangwani, Ni safari ngumu, ni safari ndefu, bila shaka alikuwa
akijaribu kurejea kwao Misri lakini bila msaada wa wowote, hakuna anayejali
wala hakuna anayetaka kubeba lawama kila mtu amechoka. Ni mwanamke mjamzito,
anataka kiujaribu kurudi kwao, kupitia Jangwani, hana msaada kuna wanyama
wakali, kilichoko kwenye kichwa chake “NI
HERI KUFA KULIKO MATESO NINAYOYAPITIA KWA SARA” Biblia haijaeleza kuwa sara
alimfanya nini lakini mwanatheolojia mmoja ametumia neno la Kiingereza “Sarai attacked Hagar with disproportionate
cruelty,” Neno hilo “DIS-PRO-POR-TIONATE”
maana yake ukatili usiopimika, na maneno mengine ya kiingereza “Harshly, Cruel, severe, Mistreated” ni aibu kwa mwanamke bosi kama Sara kuwa na
ukatili wa aina ile ni aibu, japo haikuwa vema pia kwa Hajiri kuwa asiyetii,
lakini hali hizi zote ziliweza kufikisha katika hatua hii, wako watu duniani
wanajua kutesa, wako watu duniani wanajua kunyanyasa mpaka inapofikia hatua ya
mtu kuchagua kujiua kuliko mateso unayoyapata, Mungu sio mjinga, Mungu sio kipofu,
Mungu sio Mungu asiyejali, Mungu sio Mungu wa Upendeleo, Mungu ni Mungu aonaye,
Hajiri anakuwa ni Mwanamke wa kwanza Duniani kumuona malaika wa Bwana, Hajiri
anajulikana Mbinguni, Mungu anamtaja kwa jina lake… Munguanamjua anakotoka na
anakokwenda Hajiri ni mwanamke wa Kwanza kumpa Mungu Jina “YEHOVAH ROHI” alishuhudia kuwa Mungu alimuona.
Mungu ataingilia kati hali unayoipitia.
Mwanzo 16:7-13 “Malaika wa BWANA akamwona kwenye chemchemi ya maji katika
jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri. Akamwambia, Hajiri,
wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia
mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai. Malaika wa BWANA akamwambia, Rudi kwa
bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake. Malaika wa BWANA akamwambia,
Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa
mwingi. Malaika wa BWANA akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa
kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana BWANA amesikia kilio cha mateso
yako. Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya
watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu
zake wote. Akaliita jina la BWANA aliyesema naye, Wewe U Mungu uonaye, kwani
alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye”
Unaweza kuona tayari hali ya
Hajiri ilishaanza kuwa mashakani, ashukuriwe Mungu alikuwa amekwama kwenye kisima
cha maji jangwani, kwa vyovyote vile hapo alipumzika kama angeendelea mbele
hali ya hatari ilikuwa ikimkabili, Jangwa la shuri ni jangwa pan asana unapoliangalia
huwezi kuna mwisho waka ukigeuka huwezi kuona utokako hii ilikuwa ni muelekeo
wa kuangamia sasa kwa mwanamke kijana tena mwenye mimba alihitaji msaada na
sasa Bwana mwenyewe anamtokea angalia maneno ha malaika wa Bwana:-
-
Wewe Hajiri Mjakazi wa Sarai
-
Unatoka wapi nawe unakwenda wapi
-
Rudi kwa bibi yako ukanyenyekee chini ya mikono
yake
-
Nitauzidisha uzao wako wala hautahesabika kwa
jinsi utakavyouwa mwingi
-
Utazaa mtoto wa kiume nawe utamwita Ishamel
maana Bwana amesikia kilio cha Mateso yako
-
Atakuwa kama punda mwitu, atakaa mbele ya ndugu
zake wote
-
Mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa
watu wote utakuwa juu yake.
Malaikia wa bwana alionyesha kuwa
anamjua Hajiri vizuri sana kwa jina lake na kwa kazi yake, Malaika wa bwana
alitaka kupima unyenyekevu ndani ya hajiri kwamba anajisikiaje kuitwa Mjakazi
wa Sarai, Swali unatoka wapi na unakwenda wapi lilikuwa lina kusudi la
kumrejesha Hajiri,katika toba na kuacha kiburi, kisha kurudi panapopaswa na
kuwa Mnyenyekevu , kwa sababu kwa mila na tamaduni alikuwa na mtoto wa watu hao
tumboni, na hivyo alipaswa kumrejesha, alimuakikishia kuwa uzao wake utakuwa
mwingi, maneno haya huenda yalikuwa ni maneno aliyozoea kuyasikia katika
familia ya Ibrahimu kuhusu ahadi za Mungu, ni wazi maneno hayo na ahadi hizo
zilimfanya hajiri awe na utambuzi kuwa huyu hakuwa malaika wa bwana tu bali
alikuwa ni Mungu mwenyewe alikuwa na ujuzi kuwa Mungu anaona, ujuzi huu una
umuhimu mkubwa kwetu, Mungu mwenye kuhusika na mahitaji ya wanadamu anaona na
anajua kila kitu na kila njia na aina ya mateso tunayoyapitia.
Hakuna mtu mwenye hati miliki ya
Mungu, Mungu sii wa Ibrahimu na Sara tu, wala Mungu si wa matajiri peke yao,
Mungu ni wa kila mtu, anajali na anamuhurumia kila mtu bila kujali kabila wala
rangi yake, inapofikia ngazi ya kukata tamaa yuko Mungu anayesikia na kuona mateso
yetu, yuko Mungu anayejua sida na mateso na changamoto unazozipitia, yeye
atahusika na maisha yako, hana dini wala ukabila hana upendeleo, kila mtu
anayemwendea na kuliitia jina lake anasikiwa, anaweza kumuongeza na kumzidisha
awaye yote, hakuna mtu maalumu kwa Mungu, Mungu ni wa watu wote, Mungu anataka
kumponya na kumganga na kumuhudumia kila mmoja wetu, Unaweza kuteswa,
kunyanyaswa, kuonewa na kufanyiwa mabaya lakini liko Jicho lenye nguvu linalochungulia
ulimwenguni na kuitafuta haki ili kuona ikitendeka na kama haitendeki,
huingilia kati na kutokezea njia yeye ni Mungu aonaye
Kutoka 3:7-9 “BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko
Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua
maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe
kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata
mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. Basi,
tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso
ambayo Wamisri wanawatesa.”
Mungu aonaye Jehovah Rohi macho yake yako kila mahali hawezi kuvumilia
kuona unateseka mpaka unalia na kuugua au kuchagua kufa kuliko kuishi, wakati
mateso yako yanapozidi kupita uwezo wako, wakati mateso yako yanapokaribia
kukutupa nje, unapokata tamaa ya kuishi kumbuka kuwa Mungu kupitia mwanaye Yesu
ambaye ni Mwokozi atakutetea atashuka na kuingilia kati na kukurejesha kwenye
furaha yako nawe utasimulia matendo yake makuu nimemuona yeye aonaye.
Na. Rev. Innocent Kamote.
Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima.