Andiko la Msingi: Waebrania 2:1-3 “Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije
tukayakosa. Kwa maana, ikiwa lile neno
lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa
haki, sisi je! Tutapataje kupona,
tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha
ukathibitika kwetu na wale waliosikia;”
Utangulizi:
Yesu Kristo alikuja Duniani kwa
makusudi makubwa mengi, lakini kusudi kubwa ni ili apate kutuokoka! Luka 10:19 “Kwa
kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.”
Na
ndio maana Yesu pia anaitwa mwokozi, ametukomboa katika mambo mengi lakini
kubwa zaidi ametuokoa na adabu ya dhambi
Mathayo
1:21 “Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake
Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.” Kwa hiyo unaweza kuona kuwa kusudi
kubwa la Yesu ni kutuokoa na ametuokoa na mambo mengi lakini zaidi sana
ametuokoa na Dhambi zetu, kwa nini kuokolewa nadhambi ni kwa muhimu sana kwa
sababu kila aina moja ya dhambi tuifanyayo msahara wake ni mauti ona
Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana
wetu” kwa hiyo kutokana na kuweko kwa dhambi katika nasfi zetu
adhabu yake ilikuwa ni kifo, kifo cha mwili huu na kifo cha kiroho ambacho ni
kutengwa na Mungu milele lakini Yesu akaja Duniani akatuelekeza njia kwa
mafundisho yake akaandaa watu watakaotufundisha neno lake kisha Yeye mwenyewe
alikufa kwaajili yetu yaani kwa niaba yetu, ili damu yake itakayomwagika iwe malipo
kwa niaba ya damu zetu na hivyo tukimuamini hukumu hii haina nguvu na
tunasamehewa na huu ndio wokovu mkuu, kwa hiyo sasa kazi yetu ni kumuamini yeye
na kukubali kazi yake aliyoifanya pale msalabani ili tuweze kuwa na uzima wa
milele
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa
Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”
Kwa hiyo wajibu wako mkubwa ni kumuamini yetu, yaani kutambua na kukubali kuwa
alikufa msalabani kwaajili yako na yangu na ukifanya hivyo wewe una uzima wa
milele.
Kwa nini wokovu ni mkuu?
Hakuna
tukio baya duniani au laana mbaya kama kutengwa na uso wa Mungu! Mwanzo 4:13-14.
Kaini akamwambia BWANA, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. Tazama, umenifukuza leo katika uso wa
ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na
kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.”
Mara moja mtu anapokuwa dhambini
anatengwa na uso wa Mungu anakuwa mtoro duniani na kila kitu kinakuwa adui yake
na hata mbu au bacteria wanaweza kukuua ni jambo bay asana kupungukiwa na utukufu
wa Mungu ni hasara ya hali ya juu hata kama una heshima kiasi gani kwaajili ya
hayo basi Neno la Mungu linatuonya kutokuuchezea wokovu, wokovu ni neema tu sio
wote wanaojaliwa kuukubali, sio watu wote watajaliwa kuupata wokovu au hata
kuufahamu, ikiwa wewe umepata neema ya kuufahamu basi usiuchezee wokovu ni mkuu
mno, msamaha wa dhambi ni baraka kubwa mno kuliko kutolewa gerezani, ndio maana
mwandishi wa kitabu cha waebrania ametuonya kwamba tunapaswa kuuangalia sana
kuutunza sana wokovu na tusiuchezee
Waebrania 2:1-3 “Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije
tukayakosa. Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara,
na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki, sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu
mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na
wale waliosikia;”Kwa
nini mwandishi anauona
wokovu kuwa ni mkuu kwa sababu muhimu zifuatazo;-
Ulinenwa na
Bwana mwenyewe, yaani ni zawadi ni mpango wa Mungu mwenyewe tusingeweza kujisamehesha
mbele zake ni yeye mwenyewe kwa hiyari yake aliamua kutusamehe
Umethibitishwa
ndani yetu, yaani unapoukubali kwa imani
unapewa furaha ya dhati moyoni inayokushuhudia kuwa wewe ni wa Mungu tofauti na
jinsi watu wanavyokujua na kukufahamu au kukuangalia
Umethibitishwa
kwa ishara na miujiza na Roho Myakatifu, yaani Mungu
roho Mtakatifu amewaponya wengi na kufanya miujiza mingi kwa kusudi la
kututhiboitishia kuwa kama anaweza kutufanyia ukarimu huumkubwa wa kuiponya
miili yetu anashindwaje kutusamehe dhambi zetu miujiza iko ili tupate kuamini
kuwa Yesu ni mwokozi, kama watu watafurahia miujiza kuliko kuufurahia wokovu na
msamaha wa dhambi watakuwa hawajui thamani ya wokovu Zaburi
103:3 “Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa
yako yote,” Ni msamaha wa dhambi unaoweza kutuletea pia uponyaji wa mwili
na nafsi zetu.
Umegharimu
maisha ya mwana wa Mungu, ni kwaajili ya kutuokoa ilimpasa Yesu kufa
msalabani kwa kifo cha aibu ili mimi na wewe tuweze kuokolewa kuupuuzia wokovu
ni kuidharai kazi ya Yesu aliyoifanya pale msalabani, kurudi nyuma na kuacha
wokovu ni kudharau msalaba Waebrania 6:4-6 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na
kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na
kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya
hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha
Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.”
Tabia ya kuendelea kuukataa na
kuupinga wokovu na kuidharau kazi iliyofanywa na Yesu msalabani inaweza
kutufikisha mahali pabaya sana na huu ndio unaitwa ukengeufu, hii ni dhambi ya
mauti, huku ni kushindana na Roho Mtakatifu, hatujui ni lini na wapi mtu
anaweza kufikia dhambi hii ngumu lakini jnaanza na kudharau wema wa Mungu hivyo
kama hujui wokovu uligharimu nini usiutukane!
Unatupa
Uzima wa milele unatuokoa na dhambi mauti na kuzimu , kama tukiukubali wokovu na kuupokea licha
ya kusamehewa dhambi zetu kila wakati pia tunakuwa na uzima wa milele lakini
Mungu anatulinda na dhambi ya mauti yaani ya kukataa kazi za Roho Mtakatifu na
kuipinga zawadi ya wokovu
Tumeokolewa kwa neema !
Kule kuwa
mbali na Mungu ni kifo, lakini kupitia wokovu kama tumeuamini ni zawadi kubwa
sana kutoka kwa Mungu hivyo hatupaswi kuichezea neema ya Mungu Waefeso 2:1-5 “Nanyi
mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa
kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga,
roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati
yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia,
tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema,
kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu
ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.”
Nimalizie ujumbe
huu kwa stori hii
Mfanya
biashara mmoja alikuwa akifanya biashara ya kuuza chumvi, alisambaza chumvi
yeke sehemu mbalimbali akitumia punda, kila alipoelekea sokoni ilimlazimu
kuvuka mto ili aweze kuelekea sehemu
mbalimbali kwaajili ya kuuza chumvi yake, siku moja punda wake kwa bahati
aliangusha mzigo wa gunia la chumvi kwenye mto, na hivyo chumvi iliyeyuka na
kwenda na maji kutokana na hali hiyo gunia la chumvi likawa Jepesi, hali hii
ilimpa punda yule furaha kubwa mno.
Kwa hiyo
punda yule alianza kuwa na mchezo mbaya ilikuwa kila siku akibeba chumvi
akifika eneo lenye mto aliliangusha gunia kwa makududi yaleyale, Muza chumvi
alijiuliza ni kwanini hali ile inatokea mwisho aliweza kugundua tabia ya punda
wake na akakusudia kumfundisha somo, safari moja alimbebesha gunia la Pamba na
punda bila kujalia amebeba nini alipofika pale aliliangusha tena gunia la
Pamba, akijua kuwa litakuwa jepesi vilevile kama ilivyokua kwa chumvi, lakini
mambo yalikuwa tofauti safari hii, gunia la pamba lilikuwa zito mno kuliko
maelezo na hivyo punda alipata taabu sana na akaacha tabia yake ya mchezomchezo
na mfanya biashara yule akawa na furaha.
Usichezee
neema ya wokovu kwa sababu bahati haiji mara mbili, iko siku unaweza kupoteza
kila ulichojaaliwa na Mungu na ukajikuta unapata tabu , shika sana ulicho
nacho.
Bwana
ampe neema kila mmoja wetu asiuchezee wokovu katika jina la Yesu Kristo amen!
Rev.
Innocent Kamote
Mkuu
wa Wajenzi mwenye hekima.
0718990796
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni