Warumi 12:1-2 “Basi, ndugu zangu,
nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai,
takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe
namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika
mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”
Wote tunafahamu wazi
ya kuwa tunaishi katika ulimwengu, unaoendeshwa kwa viwango, na kwa namna
Fulani hatuwezi kamwe kukwepa kuishi kwa viwango, Dunia ina viwango vyake, na
vingine tunavitumia katika maisha yetu ya kila siku, Lakini neno la Mungu
vilevile linatuelekeza kuishi kwa kiwango kinachokusudiwa, katika maandiko yaani
neno la Mungu, tunasoma hivi katika Warumi 12:1-2 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu,
itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada
yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa
kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya
kumpendeza, na ukamilifu.”Kuna neno muhimu ambalo hatuna
budi kuliangalia kwa undani ili tuweze kupata maana iliyokusudiwa hususani neno
MSIIFUATISHE NAMNA, na tutajifunza somo hili kwa kuzingatia maeneo matatui
yafuatayo:-
·
Maana ya Viwango
·
Umuhimu wa Viwango
·
Jinsi ya kuishi kwa Viwango
Maana ya viwango:-
Warumi 12:2 “Wala msiifuatishe
namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika
mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” Hebu tuliangalie andiko hilo vilevile katika
tafasiri za kiingereza ya New
International Version (NIV) andiko hilo linasiomeka hivi “Do not conform to the pattern of
this world, but be transformed by the renewing of your mind, then you will be
able to test and approve what God’s will is –his good, pleasing and perfect
will.” Unapoangalia sasa tafasiri ya Biblia yetu ya
Kiswahili na kiingereza utaweza kuona neno
“MSIIFUATISHE NAMNA” Na Katika kiingereza cha NIV “DO NOT CONFORM TO THE PATTERN” maneno hayo sasa katika biblia
ya kiyunani yanasomeka kama “PROTYPO” ambalo
sasa maana yake halisi kwa kiingereza ni
Standard, au Pattern, au Norm, au Exemplar, au Archetype, au
Measure, au meter, au Gauge, au measurement, au values. Kwa hiyo utaweza kuona kwa mfano Biblia ya tafasiri ya
kiingereza ya Good News inatumia maneno haya “Do not Conform yourselves to the
STANDARDS of this world, but let God transform you inwardly by a comlete change
of your mind. Then you will be able to know the will of God- what is good and
is pleasing to him and is perfect.” Kwa msingi huo ni kama neno la
Mungu linawataka watu waliookolewa au wanaomcha Mungu kutokuishi sawa na
viwango vya ulimwengu huu, Maana yake ni kuwa kuna aina ya kiwango cha maisha
ambacho Mungu anakikusudia kwetu! Na maandiko yanataka tuishi zawa na viwango
hivyo. Kwa hiyo neno Standard sasa tafasiri yake ni a level of quality or attainment, au Something used as a measure, norm
or model in comparative evaluations, something used or accepted as normal or
average, ni kipimo kinachohusika kupimia ubora wa mambo, wastani wa mambo,
kwa kulinganisha na mengine
Umuhimu wa viwango:-
Katika ulimwengu
tulio nao, viwango vina umuhimu mkubwa sana, na dunia ina vipimo vingi sana vya
kupima ubora wa mambo kwa kina, mapana, na marefu, tunaishi katika ulimwengu
ambao unajua kupima, na thamani ya kitu hupimwa kutokana na kiwango
kinachokusudiwa, wakati mwingine fahari ya kitu Fulani duniani hata kama hakina
maana inaangaliwa sana na ubora wa kiwango chake, sio hivyo tu watu wanaotumia
kitu chenye ubora wa hali ya juu, huweza kujisikia kuwa wao ni maalumu sana na
wakati mwingine hata kujivunia kitu hicho na kuwa na furaha kwa sababu kina
ubora! Kwa hiyo dunia ni dunia ya viwango! Kila kitu duniani kinapimwa kutokana
na kiwango chake!, Mataifa mengi yana mashirika yanayohusika na kupima au
kuangalia viwango vya bidhaa, hapa Tanzania bidhaa huthibitishwa ubora wake
kupitia shirika la (TBS) yaani Tanzania Bureau Standard , wao wakisha
thibitisha kuwa kitu hiki kina ubora huweka neno yao, yako mashirika mengine
pia ya kidini kama ya kislamu, huweka neno Halal au Haram kwa manufaa ya bidhaa
hiyo kutumiwa na imani ya watu hao, Mashirika haya pia hufanya kazi ya
kudhibiti bidhaa fake au zisizo na ubora, kwa hiyo dunia ina utaratibu wake wa
kuweka kitu katika viwango mfano;-
·
Mataifa kwa mfano yako mataifa yanayoitwa yaliyoendelea
na yanayoendelea, Developed and underdevelopment country (nchi zenye uchumi wa
juu, wa wastani wa kati na wa chini)
·
Taaluma kwa mfano kuna Elimu ya juu na Elimu ya
chini, Graduates and undergraduates
·
Matokeo ya mitihani secondary yanapimwa kwa migawanyo
ijulikanayo kama Division I,II,III,IV na 0
·
Matokeo ya vyuoni zile degree ziko za aina saba kwa
waingereza zinapimwa kutokana na viwango vya GPA yaani Grade Point Average,
Marekani wao degree ni degree tu Lakini Waingereza Degree zao wanazigawanya
kwenye maeneo saba mfano:-
Ukipata 70-100 utatunukiwa degree First Class with honours ambayo ina
GPA 4.0
Ukipata 65-69
utatunukiwa degree Upper second Class honours ambayo ina GPA 3.7
Ukipata 60-64
utatunukiwa degree Upper second class honours ambayo ina GPA 3.3
Ukipata 55-59
utatunukiwa degree lower Second class honours ambayo ina GPA 3.0
Ukipata 50-54
unatunukiwa degree lower second class honours ambayo ina GPA 2.7
Ukipata 45-49
unatunukiwa degree Third Class honours ambayo ina GPA 2.3
Ukipata 40-44
unatunukiwa degree Third Class honours ambayo ina GPA 2.0
·
Sio hivyo wote tunafahamu kuwa kuwa aina za simu
tunazomiliki pia zina namna watu wanaziweka katika ubora, i-phone, sumsung,
Nokia, Siemens, Motorola infinix, techno na kadhalika lakini sio hivyo tu
zinatengenezwa wapi
·
Kumbuka hata aina za magari ambazo wazazi wetu
wanamiliki yana ubora, wake, mabati, cement, unga na kila kitu duniani
kinapimwa kutokana na ubora wake
·
Ni katika hali kama hiyo vilevile Mungu atazipima
kazi ya kila mmoja na maisha ya kila mmoja duniani kwa msingi huo basi namna
tunavyomtumikia Mungu duniani katika Nyanja yoyote ile mwisho wa siku Mungu
atazipima kazi zetu kuwa zina thamani ya kiwango gani ona
1Wakoritho 3:12-15 “Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu
au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu
itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika
moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. Kazi
ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. Kazi ya mtu ikiteketea,
atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.”
Viwango ni Muhimu
kwa sababu ndivyo vinavyotofautisha katia ya ubora wa jambo Fulani na lingine
katika maisha yetu Mungu namekusudia sisi tuwe na viwango vya juu sana vya
maisha tukiishi kwa viwango vya juu kabisa vya ubora Mungu atajivunia maisha
yetu, Mungu hujivunia watu wake wanaoishi kwa ubora alioukusudia hapa Duniani
lakini Mungu pia huuzunishwa tunapoishi chini ya kiwango ona
Ayubu 1:1-8 “Palikuwa na mtu
katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu
na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. Kisha walizaliwa
kwake wana saba, na binti watatu. Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba,
na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na
watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko
watu wote wa upande wa mashariki. Nao wanawe huenda na kufanya karamu katika
nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakatuma na kuwaita maumbu yao
watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao. Basi ilikuwa, hapo hizo siku za
karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka
asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote
ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi,
na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote. Ilikuwa,
siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana,
Shetani naye akaenda kati yao. Bwana
akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema,
Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.
Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa
kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye
kumcha Mungu na kuepukana na uovu.”
Tunapoishi kwa
kiwango Mungu hujivunia sana lakini tukiishi chini ya kiwango tutadharaulika,
Paulo Mtume alimtaka Askofu kijana Timotheo kuzingatia kutunza ubora wake katika Nyanja zote za usemi, mwenendo, imani,
upendo na usafi, ili asije akadharaulika
ona
1Timotheo
4:12-14 “Mtu awaye yote asiudharau ujana
wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika
upendo na imani na usafi. Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na
kuonya na kufundisha. Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa
kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee.”
Jinsi ya kuishi kwa viwango:
Warumi 12:1-2 “Basi, ndugu zangu,
nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai,
takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe
namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika
mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”
Mungu anamtarajia
kila mmoja wetu kuishi kwa viwango vya juu ambavyo sio vya ulimwengu huu jambo
hili linawezekana na ndio maana maandiko yanamtia moyo kila mmoja kuishi katika
viwango vya juu, ushindi wetu dhidi ya adui yetu shetani na mafanikio kadhaa ya
ahadi za Mungu kwetu yamewekwa katika kiwango, kila siku kuna kiwango ambacho
Mungu amekusudia ukiishi na ukifikie,
kiwango cha juu cha kuishi maishanyanayompendeza Mungu ni kuishi maisha ya
utakatifu, na kufikia kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo, hilo ndio
lengo letu kuu.
1Petro 1:14-16 “Kama watoto wa kutii
msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye
aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu
wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.”
Tukiishi maisha
matakatifu tutaweza kufurahia kwa kiwango cha juu yale ambayo Mungu
ameyakusudia kwetu katika ahadi zake na katika neno lake ili tuweze kufikia
kiwango ambacho Mungu anakitaka hatuna budi kufanya yafuatayo.
1.
Amua kuishi kwaajili ya Mungu, Mungu ametupa
kuchagua uzima au mauti laana au Baraka Kumbukumbu 30:19-20 “Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo,
kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima,
ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake,
na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate
kukaa katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo,
kuwa atawapa.”
2. Vunja uhusiano na watu wasiomcha
Mungu 2Wakoritho 6:14-18 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi
isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana
shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na
Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana
mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la
Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati
yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo,
Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami
nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na
wa kike”
3.
Acha tabia mabaya zisizofaa na ufanye mwili wako
kuwa Hekalu la Mungu Roho Mtakatifu 1Wakoritho 6:19-20 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho
Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu
wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili
yenu.”
4.
Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha na Mungu
atakupa rehema na neema ya kuishi maisha ya viwango Mithali 28:13 “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa;
Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”
5. Soma neno la Mungu kila siku na
kuliishi Yoshua 1:8 “Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako,
bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa
na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako,
kisha ndipo utakapositawi sana.”
6. Chukia anachochukia Mungu na penda
anachokipenda, usifanye maovu na Mungu atakutumia sana Mungu Daniel
11:32 “Na wao wafanyao maovu juu ya hilo
agano atawapotosha kwa maneno ya kujipendekeza; lakini watu wamjuao Mungu wao
watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu.”
Kumbuka kuwa bidhaa
nyingi zisizokidhi viwango huchomwa moto na kuteketezwa, kabisa, Mungu
hataruhusu chochote kilicho kinyonge yaani kilicho chini ya ubora wake kingie
mbinguni ona Ufunuo 21:27 “Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho
kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika
kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.” Hatuna budi kumuomba Mungu
atuongezee viwango, atpeleke katika kiwango cha juu, na atupe neema ili kwamba
tusiishi sawa na viwango vya watu wa dunia hii, bali sisi tukapate kuishi kwa
kiwango cha juu, tukamtumikie Mungu kwa kiwango cha juu, kila tunachokifanya
tuhakikishe tunakifanya kwa kiwango cha juu, Mungu ni Mungu wa viwango pia.
Na. Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni