Waamuzi 11:1-2 “Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye
alikuwa ni mwana wa mwanamke kahaba; Gileadi akamzaa Yeftha. Mkewe huyo Gileadi
akamzalia wana; na hao wana wa mkewe hapo walipokuwa wamekua wakubwa wakamtoa
Yeftha, na kumwambia, Wewe hutarithi katika nyumba ya babaetu; kwa sababu wewe
u mwana wa mwanamke mwingine.”
Utangulizi:
Wewe u mwana wa mwanamke
mwingine! Yalikuwa ni maneno ya kukatisha tamaa yaliyotolewa kwa kijana shujaa
aliyejulikana kama Yeftha, Mwandishi wa kitabu cha Waebrania katika agano Jipya
anamtaja kama mojawapo wa mashujaa wa imani ona Waebrania 11:32-34 “Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta
habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za
manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata
ahadi, walifunga vinywa vya simba,walizima nguvu za moto, waliokoka na makali
ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita,
walikimbiza majeshi ya wageni.”
Yeftha ni moja ya waamuzi wakubwa
miongoni mwa waamuzi wanaotajwa katika Biblia, waamuzi walikuwa ni viongozi wa
mpito waliotumiwa na Mungu, kuwasaidia Israel walipokuwa hawana mfalme tangu
kufa kwa Yoshua mpaka kupakwa mafuta kwa mfalme wa Kwanza aliyeitwa Sauli, Jina
Yeftha maana yake ni ni Bwana atafanya njia, au Bwana atafungua.
Yeftha alikataliwa na ndugu zake,
baada ya kifo cha baba yake kwa sababu eti alizaliwa na mwanamke Kahaba, sababu
hii inawezekana kabisa ilitokana na sifa zake kuwa alikuwa mtu mwema tene
mwenye ujuzi kuhusu Mungu na hodari sana, alikuwa ni shujaa, kuzaliwa kwake na
mwanamke kahaba haikuwa sababu yay eye kukata tama katika maisha yake,
alijiendeleza kitabia na kuwa mtoto mwema sana kuliko wenzake kwa wivu
walimkataa kwa maneno mabaya ya ubaguzi kuwa yeye ni mwana wa mwanamke mwingine
hii haikuwa sababu ya kumzuia Yeftha ambae aliamua kwenda kuishi katika mji
mwingine ulioitwa Tobu, watu wote hohehahe walimkusanyikia na kuishi Pamoja
naye, Israel walipoonewa na wana wa
Ammoni na kuteswa vibaya walimkumbuka Yeftha na wakatuma wazee kumuomba Yeftha
aje kuwa shujaa wao, naye kwa neema ya Mungu akijazwa Roho Mtakatifu, na
kuonyesha ujuzi wake katika Torati na historia ya wana wa Israel alikubali kuja
na kuwatetea na kuwaokoa dhidi ya wana wa Amoni ona
Waamuzi 11:4-11 “Ikawa baadaye, wana wa
Amoni wakapigana na Israeli. Ikatukia, hapo wana wa Amoni walipopigana na
Israeli, wazee wa Gileadi wakaenda kumtwaa huyo Yeftha katika ile nchi ya Tobu;
wakamwambia Yeftha, Njoo wewe uwe kichwa chetu, ili tupate kupigana na wana wa
Amoni. Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi, Je! Ninyi hamkunichukia mimi na
kunifukuza nitoke katika nyumba ya baba yangu? Basi kwani kunijilia hivi sasa wakati
mlio katika taabu? Wazee wa Gileadi
wakamwambia Yeftha, Kwa ajili ya hayo sasa tumegeuka kukuelekea wewe tena, ili
uende pamoja nasi na kupigana na wana wa Amoni, nawe utakuwa kichwa chetu juu
ya wenyeji wote wa Gileadi. Basi Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi Kwamba
mwanirejeza kwetu tena ili kupigana na wana wa Amoni, naye Bwana akiwatoa mbele
yangu, je! Mimi nitakuwa kichwa chenu? Wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha,
Yeye Bwana atakuwa shahidi kati yetu; hakika yetu tutafanya sawasawa na neno
lako. Ndipo Yeftha akaenda pamoja na wazee wa Gileadi, na hao watu wakamfanya
awe kichwa, tena mkuu, juu yao; naye Yeftha akanena maneno yake yote mbele ya
Bwana huko Mispa.”
Licha ya kufanywa kiongozi na mwamuzi wa Israel
ni wazi kuwa Yefhta aliijua sharia alitenda haki na hata vita yake na namna
alivyokuwa anajenga hoja alijenga kwa haki, akiitumia torati, Yeftha hakuwa na
makosa ni baba yaka ndiye aliyezaa na mwanamke kahaba, lakini kigezo hiki cha
kilitumiwa na ndugu zake kumkataa na kumbagua, huenda jambo hili pia
liliingiliwa na wazee kwa kuwa katika Israel maamuzi yasingelifanyika bila
wazee kuingilia kati wote wakiwa wametiwa upofu na wivu tu, uwezo wa Yeftha
katika kulijua neno la Mungu unaonekana wazi kwa hoja anazozijenga dhidi ya
mfalme wa wana wa Amoni kabla hajampa mkon’goto ona
Waamuzi 11:11-28 “Ndipo Yeftha akaenda
pamoja na wazee wa Gileadi, na hao watu wakamfanya awe kichwa, tena mkuu, juu
yao; naye Yeftha akanena maneno yake yote mbele ya Bwana huko Mispa. Basi
Yeftha akatuma wajumbe waende kwa mfalme wa wana wa Amoni akasema, Je! Wewe una
nini nami, hata umenijilia kupigana juu ya nchi yangu? Mfalme wa wana wa Amoni
akawajibu hao wajumbe wa Yeftha Kwa sababu Israeli waliitwaa nchi yangu, hapo
walipokwea kutoka katika nchi ya Misri, tokea Arnoni mpaka Yaboki, na hata
Yordani; basi sasa rudisha hizo nchi tena pasipo matata. Yeftha akatuma wajumbe
mara ya pili waende kwa huyo mfalme wa wana wa Amoni; akamwambia, Yeftha
akuambia hivi; Israeli hakuitwaa nchi ya Moabu, wala nchi ya wana wa Amoni; lakini
hapo walipokwea kutoka Misri, na Israeli walienenda katika bara hata kuifikilia
Bahari ya Shamu, na kufikilia Kadeshi; ndipo Israeli wakatuma wajumbe waende
kwa mfalme wa Edomu, wakisema, Nakuomba sana unipe ruhusa nipite katika nchi
yako; lakini mfalme wa Edomu hakusikia. Ni vivyo wakampelekea wajumbe mfalme wa
Moabu; wala yeye hakukubali; basi Israeli wakakaa katika Kadeshi. Kisha akaenda
nyikani na kuizunguka hiyo nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu, nao wakapita upande
wa mashariki wa nchi ya Moabu, wakapanga marago upande wa pili wa Arnoni; wala
hawakuingia ndani ya mpaka wa Moabu, kwa maana Arnoni ilikuwa ni mpaka wa
Moabu. Kisha Israeli wakatuma wajumbe waende kwa Sihoni mfalme wa Waamori,
mfalme wa Heshboni: Israeli wakamwambia, Twakuomba utupe ruhusa tupite katika nchi
yako, mpaka mahali pangu. Lakini huyo Sihoni hakuwaamini Israeli ili wapite
ndani ya mpaka wake; bali Sihoni akawakutanisha watu wake wote, nao wakapanga
kambi katika Yahasa, wakapigana na Israeli. Bwana, Mungu wa Israeli, akamtia
Sihoni na watu wake wote mikononi mwa Israeli, nao wakawapiga; basi Israeli
wakaimiliki hiyo nchi ya Waamori, wenye kukaa nchi hiyo. Nao wakaumiliki mpaka
wote wa Waamori, tokea Arnoni hata Yaboki, tokea hiyo bara hata Yordani. Basi
sasa yeye Bwana, Mungu wa Israeli, amewapokonya Waamori watoke mbele ya watu
wake Israeli, na wewe wataka kuwatamalaki? Je! Wewe hutakitamalaki hicho
ambacho huyo Kemoshi mungu wako akupa kukitamalaki? Kadhalika, awaye yote
ambaye Bwana, Mungu wetu, amemfukuza atoke mbele yetu hao ndio
tutakaowatamalaki. Na wewe sasa, je! U mwema kuliko Balaki mwana wa Sipori, huyo
mfalme wa Moabu, kwa lo lote? Je! Yeye alishindana na Israeli, au kupigana nao?
Wakati Israeli waliokuwa wakikaa Heshboni na miji yake, na katika Aroeri na
miji yake, na katika miji hiyo yote iliyo huko kando ya Arnoni, muda wa miaka
mia tatu; mbona ninyi hamkuipata tena katika majira hayo? Basi mimi
sikukufanyia wewe dhambi, lakini wewe unanitenda uovu kwa kupigana nami; yeye
Bwana, yeye Mwamuzi, na awe mwamuzi hivi leo kati ya wana wa Israeli na wana wa
Amoni. Lakini mfalme wa wana wa Amoni hakuyasikiza hayo maneno ya Yeftha
aliompelekea.”
inaonyesha wazi jinsi alivyokuwa mtu wa haki na
mwenye ujuzi wa neno la Mungu, Mungu alimjaza kwa Roho wake na kusikiliza dua
yake na maombi yake akamuwezesha kuwaokowa wana wa Israel kwa kuwapiga wana wa
amoni ona
Waamuzi 11:29-33 “Ndipo roho ya Bwana ikamjilia juu yake Yeftha, naye
akapita katika Gileadi na Manase, akapita na katika Mispa ya Gileadi, na kutoka
hapo Mispa ya Gileadi akapita kuwaendea wana wa Amoni. Naye Yeftha akamwekea
Bwana nadhiri, akasema, Kwamba wewe utawatia wana wa Amoni mkononi mwangu
kweli, ndipo itakuwa ya kwamba, kile kitakachotoka katika milango ya nyumba
yangu kunilaki, hapo nitakaporudi na amani kutoka kwa hao wana wa Amoni, kitu
hicho kitakuwa ni cha Bwana, nami nitakisongeza kiwe sadaka ya kuteketezwa.
Basi Yeftha akavuka kuwaendea wana wa Amoni ili kupigana nao; naye Bwana
akawaua mkononi mwake. Akawapiga kutoka Aroeri hata kufikilia Minithi, miji
ishirini, na mpaka Abel-keramimu, akawapiga kwa machinjo makuu mno. Basi hivyo wana
wa Amoni walishindwa mbele ya wana wa Israeli.”
Ni dhahiri kuwa
Yeftha alikuwa amekubalika na Mungu, sio lazima wakati wote tukubalike kwa
wanadamu, lakini Mungu akikukubali na kuweka mkono wake lazima mlango
uliofungwa na wanadamu utafunguliwa tu , lazima bwana atafanya njia, Kujitoa
kwa Yeftha kwa Mungu na uaminifu wake kwa Mungu hakujawahi kufikiwa na myahudi
wala mkristo awaye yote yeye ni mtuwa pekee aliyeweka nadhiri ngumu sana na
kuitimiza, japokuwa kuna mgogoro mubwa wa kimjadala kuhusu Nadhiri yake, lakini
ni ukweli usiopingika kuwa mwana huyu wa kahaba, mtoto wa mwanamke mwingine
alikuwa vizuri kwa Mungu wake kuliko wana wengine, Ni kitu gani tunaweza
kujifunza kutoka kwake ni kuwa hatupaswi kukata tama katika maisha, kila kikwazo katika maisha yetu tunaweza
kukitumia kuwa nafasi ya kipekee kutupeleka katika hatua nyingine:- Hatupaswi
kukatishwa tamaa na jambo lolote!
Mwanzilishi wa Kampuni ya
kutengeneza injini za aina mbalimbali ikiwemo magari, pikipiki, jenereta na
mashine za pump za kumwagilia na kuoshea magari Chini Japan aliyejulikana kama
SOICHIRO HONDA alizaliwa mwaka 17 November 1906
na alifariki mwaka 5 August 1991 akiwa na miaka 84 Kampuni yake iliitwa
Honda Motor Company ltd. Aliondoka nyumbani akiwa na miaka 15 tu na akaanza
kuwa fundi wa kutengeneza magari na kuuza vifaa nya magari vilivyotumika,
alikuwa nimmtu mchapakazi sana na alipenda sana magari, na kutamani kuwa fundi
wa kuyatengeneza, lakini hata hivyo alikataliwa kwa sababu na mambo yalikuwa
magumu kwa sababu hakuwa na Elimu yeyote, wenzake walimpa kazi ya kuwapikia
chakula na kusafisha duka la spea za magari. Aliamua kujiendeleza mwenyewe ili
kuendeleza kipawa chake alijiunga na timu ya mbio za magari, lakini wakati
Fulani alianguka na kupata ajali ambayo ilimjeruhi mwili wake na hakuweza
kuendelea tena, na akaachana na swala la
mbio za magari, Baada ya kupona Soichiro
alianza kutengeneza Piston rings kwa
uwezo wake, alizipeleka kwa kampuni ya TOYOTA
ili awauzie, lakini walimfukuzilia mbali kwa aibu, walikataa kabia uvumbuzi
wake wakisema ni wa hali ya chini, kukataliwa kwake hakukumfanya ake chini
aliendelea kukazana na kuamua kuanzisha kiwanda chake hatimaye aliweza, leo hii
ndio mtu mwenye pikipiki imara sana kuliko aina nyingine ya pikipiki duniani.
Mungu hamtupi mja wake, Hijalishi
umetiokea katika ukoo gani, au jamii gani au una historia mbaya kiasi gani,
wala haijalishi watu wanasema nini juu yako, jambo kubwa la kuuliangalia ni
Mungu anasema nini juu yako, tunaweza kupitia katika hali ya kukataliwa, Lakini
hilo lisitutishe tumpe Mungu nafasi ya kutuonyesha nini kiko mbele yetu, Na kwa
neema na uweza wa Roho Mtakatifu Bwana atakufanya uwe kimbilio la Ndugu zako na
jamaa zako wote walipokupuuzia na
kukudharau watakuja wakuinamie kumbuka jiwe walilolikataa waashi hilo limekuwa
jiwe kuu la msingi Yeftha aliambiwa wewe u mwana wa mwanmke mwingine, ni kama
wanamwambia wewe sio ndugu yetu halisi, lakini baadaye walikwenda kumuhitaji na
kuhitaji msaada wake!
Na Rev. Innocent Samuel Kamote.
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni