Mithali 27:17 “Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake”
Utangulizi:
Chuma hunoa chuma ni moja ya
andiko maarufu na lenye hekima sana katika utumishi tulioitiwa hapa duniani,
biblia ya Kiswahili inatumia neno chuma hunoa chuma ndivyo mtu aunoavyo uso wa
rafiki yake lakini katika kiingereza andiko hilo linasomeka “As Iron sharpens Iron, so one person sharpens
another”, kwa hiyo tungeweza kusema
hivi kwa lugha ya Kiswahili changu kama chuma kinavyonoa chuma ndivyo ilivyo
kwa kila mtu na jirani yake.
Usemi huu unatusaidia kujitambua
kuwa tunategemeana na hakuna mtu anaweza kutoboa peke yake, yaani ili kwamba
wewe uweze kuwa mtu mwema zaidi, unaweza kuwa mzuri zaidi kwa kuwafanya wengine
kuwa wazuri zaidi. Au unaweza kuwa mzuri
zaidi kwa kujifunza kutoka kwa wengine, sisi peke yetu hatutoshi, lakini tuko
hivi tulivyo kwa sababu tulijifunza kutoka kwa wengine, tulikubali kuongozwa,
na tulipokea hekima na maonyo kutoka kwa wengine, Biblia inasema enenda pamoja
na wenye hekima nawe utakuwa na hiyo hekima! Ona
Mithali 13:20 “Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima;
Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.”
Chuma kunoa chuma katika hali ya
kawaida maana yake kuna manufaa ya ajabu sana inapotokea vyuma vikasuguana kwa
pamoja, inatengeneza makali ambayo yana uwezo mkubwa sana wa kukata kitu kwa
urahisi, chuma kinaweza kubaki na makali yake ya kawaida, na kikapoteza ufanisi
au kubaki hali ileile kwa utendaji uleule au kuwa butu, lakini kinaponolewa au kugongwa na chuma kingine kinakuwa tofauti
kabisa, kwa msingi huo kwa kadiri chuma hicho kinavyozidi kunolewa au kugongwa
au kufuliwa ndio kinavyozidi kuwa na makali zaidi, chuma hunoa chuma humaanisha
au inamaanisha ni kumchonga mtu kitabia, mwenendo, maisha, kitaaluma, kihekima,
uzoefu na kadhalika, kwa msingi huo kunakuwa na faida pande zote mbili na
matokeo yake ni kuwa pande zote mbili huwa kali na hatimaye wote hufanya vizuri
katika kazi zao, kama ni kukatua au kukata vitu vipande vipande. Au kufanikisha wajibu ule uliokusudiwa na
mwenye chuma. Mwanadamu hakuumbwa awe peke yake tunasema kwa kiingereza “human being is a social being” kwa hiyo
tunahitajiana katika mazingira mbalimbali ili tuweze kufika
Mwanzo 2:18 “BWANA Mungu akasema, Si vema
huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”
Wataalamu wa Elimu ya jamii
katika ukristo Christian sociology wanakubaliana kuwa andiko hilo licha ya kuwa
kwaasili lilimuhusu Adam na Eva, lakini kwa upana linahusu ile hali ya mty kuwa
peke yake haikuwa njema katika uumbaji wa Mungu, na kuwa Mungu aliona kuwa mtu
anahitaji watu, wenzake wengine, na ndio maana aliwabariki ili waongezeke na
kuitawala Dunia so its absolutely that human being is a social being
Na ndio maana nyakati za kanisa
la kwanza walionywa kutokuacha kukusanyika ili watu waendelee kuonyana kwa
kadiri siku ile ilivyokuwa inakaribia, tunaweza kusali peke yetum, tunaweza
kumuabudu Munghu tukiwa wenyewe lakini kwanini tunahitaji kwenda ibadani
kwanini tunahitaji kujumuika na wenzetu katika ibada kwa sababu tunahitajiana
pia hata kama tumeokolewa
Waebrania 10:24-25 “tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo
na kazi nzuri; wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya
wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile
kuwa inakaribia.”
Kwa msingi huo basi jni wazi kuwa
usemi huu chuma hunoa chuma unamaana pana sana kwetu na kwa jamii nzima na kuna
mambo mengi mno ya kujifunza tunayoweza kuyapata kutokana na usemi huu kama
ifuatavyo:-
1.
Chuma
hunoa chuma ni usemi unaotufundisha kuwa na umoja
Tumeona kuwa
usemi unasema chuma hunoa chuma ina maana ya pia mtu wa aina Fulani anaweza
kumsaidia au kusaidiwa au kusaidiana na mwingine kuwa wa aina Fulani kwa hiyo
kanuni hii ya biblia inatufundisha nguvu ya umoja katika kanuni za kiroho umoja
una nguvu sana, biblia inaeleza wazi kuwa umoja ni wa thamani sana popote pale
unapotaka mafanikio kama ni ya kitaasisi au serikali au taifa lazima kwanza
watu wawe na umoja hilo ni la msingi sana.
Muhubiri 4:9-10 “Afadhali
kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana
wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake
aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua! ”
Maandiko
yanaonyesha kuwa ni afadhali au ni heri kuwa wawili kwa sababu kuna kuinuliwa
kuliko mtu akiwa peke yake, lakini kazi yao pia huwa kubwa kuliko kazi ya mtu
mmoja sio hivyo tu, watu wapoomba wakiwa wawili au watatu Mungu hufanya au
hujibu maombi yao kwa urahisi zaidi kwa msingi huo umoja au kuwa zaidi ya mmoja
kuna uwepesi unaoweza kupatikana kwa kusaidiana na kwa kutegemeana na kwa
kuwekana sawa na kuna faida kubwa sana za kimwili, kiroho, kiuchumi,
kisaikolojia, kisiasa, na kijamaa na kadhalika
Mathayo 18:19-20 “Tena
nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote
watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo
wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”
Maombi ya watu
wawili waliopatana yana nguvu kubwa sana na Mungu huyajibu lakini sio hivyo tu
Mungu anakuwepo katikati ya watu wanapokusanyika kwa jina lake, maandiko
yanasema watu wanapokaa kwa umoja Mungu huachilia upako wake kwa namna ya
kushangaza kutoka kwa kluhani mkuu Yesu Kristo
Zaburi 133:1-3 “Tazama,
jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja. Ni kama mafuta
mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa
mavazi yake. Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko
Bwana alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.”
Kwa hiyo katika
ulimwengu war oho Mungu anafahamu sana umuhimu wa umoja, kama kuna jambo
mojawapo muhimu ambalo Yesu aliliombea kanisa na wanafunzi wake ni kuwa na
umoja ona
Yohana 17:20-22 “Wala
si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.
Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao
nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe
uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama
sisi tulivyo umoja.”
Hakuna taasisi
yoyote ile inayoweza kusimama kama tasisi hiyo haina umoja, shetani anajua kuwa
ili aweze kuwaharibia watu atamwaga roho ya mafarakano ili kuwe na makundi nah
ii ndio dalili mbaya sana ya kuanguka kwa taasisi au taifa au hata ndoa.ni pale
umoja unapokuwa umeondoka. Lazima tuwe na nia moja, tupendane inapotokea kila
mtu anaangalia maslahi yake, moyo wa ubinafsi na kujiona bora kuliko wengine
hapo ndipo mambo huanza kuharibika
Wafilipi 2:1-4 “Basi
ikiwako faraja yo yote katika Kristo, yakiwako matulizo yo yote ya mapenzi,
ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema, ijalizeni
furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja,
mkinia mamoja.Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa
unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila
mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine”
kwa msingi huo
kanuni ya chuma kunoa chuma ina maanisha kuwa na umoja kushikamana kwa nyenzo
zinazofanana ili kujenga na kufanikisha kazi ya Mungu au ujenzi wa jamii au
taifa kwa mshikamano unaokubaliana na kuelekezana, kwa msingi huo kujitenga na
jamii au kutiokukubali kuchangamana na wenzako kunaweza kuwa na mchango mbaya
sana katika makuzi na ufanisi wa mtu mmoja mmoja.
2.
Chuma
hunoa chuma ni usemi unaotufundisha pia kutoambatana na watu wenye tabia mbaya.
Chuma hunoa
chuma ni msemo pia unaotufundisha kuambatana na watu wenye tabia njema
1Wakoritho 15:33 “Msidanganyike;
Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.” Ni vema kuuangalia mstari
huu kwa kiingereza unasema hivi
1Corinthians 15:33 “Do not be misled, Bad Company
corrupts good character” usemi huu umetokana na usemi wa kiyunani
unaotafasirika hivi “DO NOT BE FOOLED, DECEIVED, MISLED, BAD
FRIEND, COMPANY WILL RUIN GOOD HABITS, OR CHARACTER, OR MORALS, Imenukuliwa
kutoka katika mashairi ya zamani sana ya kigiriki kati ya mwaka 342-291 KK., Yaani
kama chuma hunoa chuma basi chuma hicho vilevile kikiwa kiovu kitakufanya uwe
muovu zaidi, kwa msingi huo maandiko yanatufundisha kujihadhari na watu waovu,
au kuacha kuwa na mahusianio na watu wabaya, huwezi kuwa na tabia njema kama u
nashikamana na watu wenye tabia mbaya mafundishio ya yesu Kristo ya na ukatili
mikubw zaidi wakati masihi alipokuwa akitahadharisha mambo ya kukosesha
Mathayo 18:7-9 “Ole
ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo
ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha! Basi mkono
wako au mguu wako ukikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe; ni afadhali kuingia
katika uzima hali umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili
au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele. Na jicho lako likikukosesha,
ling'oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo,
kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto.”
Yesu alitumia
maneno haya kumaanisha kuvunja uhusiano na mtu anayesababisha wewe ukosee,
anazungumzia kuacha kuambatana na watu waovu wanaokuharibia ambao badala ya
kukunoa uwe mzuri wanakunoa uwe mbaya, badala ya kukuongoza katika mkema
wanakuongoza kufanya uovu, utaharibikiwa lugha ya Paulo mtume inanyoosha pia
moja kwa moja katika tahadhari ya swala hili ona
2Wakoritho 6:14-18 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa
maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya
nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye
aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani
kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai;
kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea,
nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao,
Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,”
maandiko yako
wazi na yanatutaka tuwe makini na wale tunaoambatana nao, wana ushawishi wa ina
gani je ni chuma cha aina gani usije ukanolewa kuwa muovu zaidi hivyo ni muhimu
ukawa makini na kuchagua mtu wa kuambatana naye asiwe mvuta bangi, asiyetumia
madawa ya kulevya, walevi, wazinzi, makahaba, majambazi, wezi, waongo,
matepeli, watu wa misheni town, wenye tama, wasengenyaji, watukanajim wasagaji, mashoga, wavuta sigara, waasi
maandiko yanatuasa kuachana na makutano wa aina hii hawa tukiambatana nao
watatunoa na tutakuwa waovu zaidi, Musa anasema mtu akikushawishi katika uovu
muue
Kumbukumbu la Torati 13:6-10 “Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mamaako,
au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye
kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala
baba zako; katika miungu ya mataifa yaliyo kando-kando yenu karibu nawe au
mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya dunia; usimkubalie
wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala
usimfiche;mwue kweli; mkono wako na uwe wa kwanza juu yake katika kumwua, na
baadaye mikono ya watu wote. Nawe mtupie mawe hata afe; kwa kuwa alitaka
kukupotoa na Bwana, Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba
ya utumwa.”
Maandiko
yanatuonya kuacha kuandamana na mkutano katika kutenda maovu, kwa sababu hiyo
hata kama utaona kuwa kuna kundi au watu wanakusudia kufanya jambo baya ni
muhimu wewe ukajihadhari kama lengo la umoja wao ni kwenda kufanya maovu, pima
wewe mwenyewe lolote lile iwe ni maandamanio, migomo uasi au lolote ambalo
unaona liko kinyume na Mapenzi ya Mungu au neno lake wewe usiambatane nao hata
kama wako wengi
Kutoka 23:2 “Usiandamane
na mkutano kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lo lote kwa
kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu;”
Neno la Mungu
liko makini sana kuhusu kuambukizwa kutenda uovu, na lina msimamo mkalisana
kuhusu kujiunga na jamii isiyotaka kutenda mema, kwa msingi huo kama ni chuma
hunoa chuma basi kama chuma hicho ni cha uovu waovu hunoa waovu wenzao na hivyo
utakua uemambatana na wapumbavu na wala sio wenye hekima na biblia inaonyesha
matokeo kuwa utaumia.
3.
Chuma
hunoa chuma ni usemi unatufundisha kuwa na tabia ya kutiana moyo.
Chuma hunoa
chuma maana yake pia kuna watu wanaoweza kututia moyo, tunachohitaji sisi ni
kutiwa moyo, kuna watu wakitiwa moyo tu wanafanya vizuri chuma hunoa chuma
humaanisha ni kupata mtu anayeweza kujua hali yako na ni nini unachohitaji
kukifanya kisha akakutia moyo kufanya vizuri, Mungu mwenyewe amefanya kazi ya
kututia moyo kwa neno lake akitutaka tusigope kabisa anajua kuwa wako watu
wakitiwa moyo hufanya vizuri. imani yao hupanda na Mungu ametuhakikishia
ushindi mkubwa usiokuwa wa kawaida watu wanapotiwa moyo ona mifano ya kutiana
moyo katika maandiko:-
Isaya 41:6-13 “Wakasaidiana,
kila mtu na mwenzake, kila mtu akamwambia ndugu yake; Uwe na moyo mkuu.
Seremala akamtia moyo mfua dhahabu, na yeye alainishaye kwa nyundo akamhimiza
yule apigaye fuawe, akiisifu kazi ya kuunga, akisema, Ni kazi njema; naye
akaikaza kwa misumari isitikisike. Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo,
niliyekuchagua; mzao wa Ibrahimu, rafiki yangu;
wewe niliyekushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake,
nikikuambia, Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua wala sikukutupa; usiogope, kwa
maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia
nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu
washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia. Utawatafuta wala hutawaona
wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale
waliofanya vita juu yako. Kwa maana mimi, Bwana, Mungu wako, nitakushika mkono
wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.”
Wakati mwingine
sio tu kungoja kutiwa moyo lakini unaweza kujitia moyo mwenyewe kama chuma
kwelikweli kwa kuuthibitishia ulimwengu kuwa wewe sio dhaifu na wewe ni hodari
jikabidhi kwa Mungu na Bwana Mungu yeye hatajali hata kama uko peke yako
atakusaidia yeye ni sehemu yetu ya kujitia moyo hivyo wakati unapokuwa katika
halia inayokuhusu wewe pekee hakikisha kuwa unajitia moyo mwenyewe .
Yoeli 3:9-10 “Tangazeni
haya kati ya mataifa; takaseni vita; waamsheni mashujaa; watu wa vita na
wakaribie; na wapande juu. Yafueni majembe yenu yawe panga, na miundu yenu iwe
mikuki; aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari.”
Watu wawapo
duniani wanahitaji kutiwa moyo, ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa tunawatia moyo
wengine, lakini wako watu ambao kazi yao ni kuvunja moyo, lakini usikubali kwa namna
yoyote ile kuvunjika moyo Maandiko yanatutaka pia tujitie moyo, ukijitia moyo
mwenyewe unakuwa chuma na baadaye utawasaidia watu wanaovunjika moyo!
Nehemia
alipokuwa anaujenga ukuta wa Yerusalem alikutana na changamoto za wapinzani
ambao walikuwa ni wakatishaji tamaa na walikuwa wanatoa maneno ya kejeli
kuhusiana na ukuta wa jiji la Yerusalem alilokuwa analijenga Nehemia kama
msimamizi, ni ukweli usiopingika kuwa kama Nehemia hangekuwa shupavu yeye
angekata tama na hivyo watu wengine neo wangekata tama! Ona
Nehemia
4:1-3 “Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba
tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana,
akawadhihaki Wayahudi. Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria,
akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa
dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu
hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto? Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa
karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa
ukuta wao wa mawe.”
Nehemia
alitishiwa na hata kutumiwa manabii wa uongo, lakini hata hivyo hakukata tama
na matokeo yake kazi ilisonga mbele kupitia yeye na wale aliokuwa akiwaongoza
ona matisho aliyokutana nayo na namna alivyoweza kustahimili:-
Nehemia 6:11-13 “Nami
nikasema, Je! Mtu kama mimi nikimbie? Naye ni nani, akiwa kama nilivyo mimi,
atakayeingia hekaluni ili kuponya maisha yake? Sitaingia. Nikatambua, na
tazama, siye Mungu aliyemtuma; lakini amefanya unabii huu kinyume changu; nao
Tobia na Sanbalati ndio waliomwajiri. Kwa sababu hii aliajiriwa, ili mimi
niogope, nikafanye hivyo na kutenda dhambi, kisha wao wawe nazo habari mbaya,
ili wanishutumie.”
Chuma kuona
chuma kunamaanisha kusaidiana kuinuana kutiana moyo ambako mwisho wa yote
kutakuwa na faida kwa watu wote, sio mtu mmoja kila mmoja anahitaji kutiwa moyo
au kujitoa moyo ili hatimaye aweze kuwa Baraka kwa wengine, kwa eneo lake ili
mambo yaweze kuwa mema.
4.
Chuma
hunoa chuma ni usemi unatufundisha kuwa tayari kubadilika:-
Chuma kunoa
chuma maana yake vilevile ni kukubali kubadilika, vile vyuma vinaposuguana
kunatokea mabadiliko chanya, lakini wakati mwingine chuma kunoa chuma
humaanisha unaweza kuchoma moto chuma kimojawapo kikaiva katika moto kisha
ukatumia nyundo kugonga kile chuma kingine mpaka kikanyooka, chuma kinachogongwa
kinabadilika na kuwa katika umbile lililokusudiwa na mhunzi, kwa hiyo unapogongwa
badilika usipobadilika utagongwa zaidi au utaondolewa, Mungu anaweza kutuinulia marafiki wazuri
ambao wanaweza kutusaidia kukua na kukomaa wao wanaweza kuwa wakweli kwetu na
wanaweza kutuambia ukweli, kutushauri au kutukemea na kutujenga, na kutukosoa,
kosoa zao zinaweza kuwa za kutusaidia hivyo kuna umuhimu kwetu kukubali kubadilika na kufuata mashauri yao ama kufuata ushauri
wa neno la Mungu, ni Baraka kuwa na watu wanaotunyoosha japo tunaweza
tusijisikie vizuri kwa wakati Fulani, kibinadamu iko wazi kuwa wanadamu
wachache sana wanaopenda kuambiwa ukweli, na wanaokubali kukemewa lakini lazima tukubali kukemewa kuna watu
hawakubali maonyo, hawataki kukemewa hawataki kuambiwa ukweli, tabia ya aina
hii ni sawa na chuma kukataa kunolewa na anguko linaweza kutokea kwa watu
wasiokubali maonyo.
Mithali 29:1 “Aonywaye
mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa.”
Neno la Mungu
linatutahadharia kwamba ni muhimu kukubali maonyo wako watu hawataki kuonywa
wakiguswa tu wanavimba wanageuka wanakuwa jeuri wanajibu wanajitetea
wanajigamba wanajiona kuwa hawastahili kuguswa maandiko yanasema hao wamekuwa
wana haramu kama sisi ni wana wa
halali basin i muhimu kwetu tukawa watu tunaokubali maonyo
Waebrania 12:5-11 “tena
mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu,
usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye; Maana yeye
ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili
ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi
asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote,
ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.Na pamoja na hayo
tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali
sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? Maana ni hakika, hao kwa
siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu,
ili tuushiriki utakatifu wake. Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha
furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda
ya haki yenye amani.” Maandiko
aidha yanawataka viongozi wa kiroho kukaripia na kuonya na kukemea
2Timotheo 4:2-4 “lihubiri
neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya
kwa uvumilivu wote na mafundisho. Maana utakuja wakati watakapoyakataa
mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu
makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie
yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.”
Watu
waliyakubali maonyo baadaye walikuja kuwa viongozi wazuri sana Petro ndiye
mwanafunzi nwa Yesu aliyekemewa mara nyingi sana, lakini alikuwa na uelewa
mkubwa sana kuwa kwa Yesu kuna maneno ya uzima wa milele,
Mathayo 16:21-23 “Tangu
wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda
Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na
waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Petro akamchukua, akaanza
kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. Akageuka, akamwambia Petro,
Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali
ya wanadamu.”
Petro pamoja na
makemeo makali sana hakumwacha Yesu aliendelea kushikamana naye Yohana 6:66-68 “Kwa
ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane
naye tena. Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka
kuondoka? Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno
ya uzima wa milele.”
Petro alikuwa na
uelewa kuwa kukemewa kule kungekuja kumleta katika nafasi ya kuwa kiongozi na
kufanya vizuri, Nyakati za kanisa la kwanza watu waliokuja kuwa viongzi wazuri
ni wale ambao waliwahi kukemewa hadharani mbele ya wote na wakiwa wanajua
umuhimu wa maonyo waliyapokea na kubadilika na kuja kuwa viongozi wazuri sana
akiwemo Tizo aliyekuja kuwa askofu wa makanisa, Mungu aklimuinua sana na kuja
kuwa kiongozi mkubwa sana na Paulo mtume alijivunia baadaye kwa sababu
alikubali maonyo
2Wakoritho
8:16-23 “Lakini
ahimidiwe Mungu atiaye bidii ile ile kwa ajili yenu katika moyo wa Tito. Maana
aliyapokea kweli yale maonyo; tena, huku akizidi kuwa na bidii, alisafiri
kwenda kwenu kwa hiari yake mwenyewe. Na pamoja naye tukamtuma ndugu yule
ambaye sifa zake katika Injili zimeenea makanisani mwote. Wala si hivyo tu,
bali alichaguliwa na makanisa asafiri pamoja nasi katika jambo la neema hii,
tunayoitumikia, ili Bwana atukuzwe, ukadhihirike utayari wetu. Tukijiepusha na
neno hili, mtu asije akatulaumu kwa habari ya karama hii tunayoitumikia;
tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya
wanadamu.Nasi pamoja nao tumemtuma ndugu yetu tuliyemwona mara nyingi katika
mambo mengi kuwa ana bidii, na sasa ana bidii zaidi sana kwa sababu ya tumaini
kuu alilo nalo kwenu. Basi mtu akitaka
habari za Tito, yeye ni mshirika wangu, na mtenda kazi pamoja nami kwa ajili
yenu; tena akitaka habari za ndugu zetu, wao ni mitume wa makanisa, na utukufu
wa Kristo.” Baadaye sifa zake zilienea makanisani kote alikuwa ni
mtu mwema mtendakazi pamoja na Paulo mtume
na mtume wa makanisa unapokuwa kanisani, shuleni kazini na kila mahali
ili uweze kuwa mzuri na kufiti kwa kazi basin i vema ukakubali kunolewa.
5.
Chuma
huona chuma ni usemi unaotukumbusha kujifunza kutoka kwa wengine
Wakati mwingine
Mungu hutumia watu, kujifunza kutoka kwa mtu mwingine hii ni kanuni pia ya
chuma kunoa chuma training
2Timotheo 2:2 “Na
mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu
waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.”
Paulo mtume hapa
anaonyesha kuwa Timotheo alijifunza vitu kutoka kwake na anataka Timotheo ayatumie yale
aliyiojifunza kutoka kwake awakabidhi watu waamini fu watakaofaa kuwafundisha
na wengine, kujifunza kutoka kwa wengine ni njia sahihi ya kujinoa, chuma
kinapokinoa chuma kingine husaidia kukifanya chuma kilichonolewa kutumika kama
jinsi chuma kile kilivyokusudiwa na aliyekinoa, Maandiko yanaionyesha wazi kuwa
wale waliojifunza kutoka kwa Yesu Kristo walitambulika kwa namna walivyokuwa na
ujasiri mkubwa sawasawa na ule aliokuwa nao Yesu Kristo, hii ilisababishwa na yule aliyewanoa namna
alivyo ona
Matendo 4:13 “Basi
walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na
elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja
na Yesu.”
Viongozi wa dini
walishangazwa sana na uwezo mkubwa wa Petro na Yohana, ujasiri, uwezo wa
kujieleza na kujiamini na miujiza waliyoifanya walitaka kujua kuwa watu hawa ni
watu wa namna gani wamesomea wapi, wengi wa viongozi wa dini ya kiyahudi
walikuwa walimu waliwafunza watu lakini walishangaa neno watu wasio na Elimu na
Maarifa lina maana ya (watu wasiokuwa na
ujuzi wa Torati maamuma, hawakupitia darasa lolote la viongozi wa kidini
wanaotambulika lakini wasio na maarifa unlearned and ignorant kwa kiyunani
(Idiotai) watu walioibuka tu,
wasiojulikana wanatokea wapi) walikuja kubaini kuwa watu hawa ni ni wazi
kuwa mafunzo yao waliyapata kwa Yesu, Yesu alipochagua wanafunzi wake hakwenda
kwenye madarasa ya watu maalumu alichukua watu wa kawaida tu wasio na Elimu na
kuwanoa wakawa vile anavyotaka
Mathayo 4:18-22 “Naye
alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni
aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa
wavuvi. Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Mara
wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine
wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwamo chomboni pamoja
na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita. Mara wakakiacha
chombo na baba yao, wakamfuata.”
Hawa walikuwa
watu walionolewa na Yesu mwenyewe, walikuwa mashujaa, walikuwa majasiri,
walikuwa na uwezo wa kunena, walikuwa na uwezo wa kujenga hoja za kimaandiko na
kuthibitisha wazi kuwa Yesu ni Bwana, jambo lililopelekea wajiulize hawa
wametokea wapi ni ukweli ulio wazi kuwa wao walikuwa wamejifunza kila kitu
kutoka kwa Yesu Kristo,
Wakati Paulo
mtume yeye alikuwa mtu aliyejifunza kutoka katika shule za viongozi wa kiyahudi
waliokuwa maarufu sana wakati huo,
Matendo 22:3-5 “Mimi
ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji
huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi,
nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi; nikawaudhi
watu wa Njia hii hata kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na
wanawake. Kama Kuhani Mkuu naye anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia,
ambao nalipokea barua kwao kuwapelekea ndugu wale, nikaenda Dameski, ili
niwalete wale waliokuwa huko hata Yerusalemu, hali wamefungwa, ili waadhibiwe.”
Sasa unaweza
kuona kuwa Paulo mtume tofauti na Petro na Yohana yeye alikuwa amepitia shule
za kiyahudi na aliweza kujitambulisha hivyo na hawa wazee walikuwa wanamjua na
Gamaliel alikuwa ni Rabbi aliyeheshimika sana ona
Matendo 5:34-35 “Lakini
mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamalieli, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa
na watu wote, akasimama katika baraza, akaamuru mitume wawekwe nje kitambo
kidogo, akawaambia, Enyi waume wa Israeli, jihadharini jinsi mtakavyowatenda
watu hawa.”
Unaona Gamaliel
anatajwa kama Mwalimu wa Torati aliyeheshimika sana alikuwa rabbi wanahistoria
wa nyakati za kanisa la kwanza wanaeleza kuwa rabbi huyu alifundisha kati ya
mwaka wa 22-55 Baada ya Kristo, na hivyo kuna uwezekano mkubwa alimfundisha
Paulo aliyekuwa na umri wa miaka kama 16 hivi, gamaliel alikuwa ni farisayo
aliyebobea kutika katika shule ya Rabbi Hillel, wa kizazi kabla kidogo ya Yesu
kristo, wakati huo kulikuwa na marabbi maarufu sana Rabi Hillel na rabbi
Shammai, hawa walihusika kwa kiwango kikubwa kuwanoa wayahudi wengi katika
maswala ya sharia na mitazamo mikubwa miwili yay a Reberal na conservative, kwa msingi huo kila mmoja
alinolewa kwa namna Fulani kutoka kwa mwingine, Muda usingeliweza kutosha
kuonyesha kuwaona wengi waliopata mafunzo kutoka vyanzo mbalimbali
Musa alipata
Elimu ya kimisri ona Matendo 7:22-25 “Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa
maneno na matendo. Umri wake ulipopata kama miaka arobaini akaazimu moyoni
mwake kwenda kuwatazama ndugu zake Waisraeli.Akamwona mmoja akidhulumiwa, akamtetea,
akamlipia kisasi yule aliyekuwa akionewa, akampiga huyo Mmisri. Alidhani kwamba
ndugu zake watafahamu ya kuwa Mungu anawapa wokovu kwa mkono wake, lakini
hawakufahamu.” Ni Elimu hii aliyoipata na elimu ya dini aliyoipata
kule Midian kwa Yethro mkwewe vilimuwezesha kuwa mwanzilishi na kiongozi mkubwa
na wa kwanza au baba wa Taifa la Israel na kulijengea ustaarabu mwingi sana,
tukubali kumbe basi kujifunza kutoka kwa wengine na hasa wale wakali kweli
kweli ili watunoe na tuwafuate Waebrania
13:7 “Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza,
waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao,
iigeni imani yao.”
Kwa hiyo hapa
usemi unatukumbusha wazi kwamba ili tuweze kuwa wazuri sana kuna manufaa ya
kujifunza kutoka kwa wengine na kuwasaidia wengine kuwa wazuri zaidi, kumbuka
hakuna mtu nanaweza kuwa mtu peke yake na
hivi tulivyo ni matokeo ya kujifunza kutoka kwa wengine!
6.
Chuma
hunoa chuma ni usemi unaotukumbusha umuhimu wa neno la Mungu
Kwa karne nyingi
sana imethibitika wazi kuwa neno la Mungu limekuwa na nguvu kubwa sana ya
kubadilisha maisha ya mwanadamu kuliko namna nyingine zozote, kama mtu anataka
kunolewa vema kunyooshwa na kuwa mwema awe tayari kunyenyekea kwa neno la Mungu
Biblia inalisifia neno la Mungu kama upanga ukatao kuwili ona
Waebrania 4:12-13 “Maana
Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote
ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta
yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala
hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na
kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.”
Lenyewe lina
uwezo wa kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo, na limekuwa na sifa za
kubadilisha maisha ya watu wa makabila
mbalimbali na kuwapa utamaduni wa kibiblia lenyewe kama nyndo vilevile
linauwezo wa kuvunja vunja na kulainisha
Yeremia 23:28-29 “Nabii
aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno
langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema Bwana. Je! Neno
langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande? ”
Neno la Mungu
lina nguvu ya kuumba Mwanzo 1:1-31 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi
ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji;
Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu
akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku
moja. Mungu akasema, Na liwe anga
katikati ya maji, likayatenge maji na maji. Mungu akalifanya anga, akayatenga
yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.
Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili. Mungu
akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu
paonekane; ikawa hivyo. Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji
akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mungu akasema, Nchi na itoe
majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao
mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. Nchi ikatoa majani, mche
utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani
yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Ikawa jioni ikawa asubuhi,
siku ya tatu. Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge
kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka; tena
iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo.
Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo
utawale usiku; akafanya na nyota pia. Mungu akaiweka katika anga la mbingu,
itie nuru juu ya nchi na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza;
Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne. Mungu
akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege
waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na
kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa
jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni
vyema. Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya
baharini, ndege na wazidi katika nchi. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.
Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho
kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. Mungu akafanya
mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila
kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki
wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye
kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano
wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.Mungu akawabarikia, Mungu
akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki
wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya
nchi. Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa
nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo
chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani,
na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche,
ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo. Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na
tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.”
Neno la Mungu lina nguvu ya kuhekimisha
2Timotheo 3:14-17 “Bali wewe ukae katika mambo yale
uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza
kwao; na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza
kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa
mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha
katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila
tendo jema.”
Neno la Mungu lina nguvu ya kuleta
mabadiliko Isaya 55:10-11 “Maana kama vile mvua
ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha
ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye
chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu;
halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika
mambo yale niliyolituma.”
Neno la Mungu lina uwezo wa kutusaidia
kuzishinda dhambi Zaburi 119:9-11 “Jinsi gani
kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. Kwa moyo wangu
wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.Moyoni mwangu
nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.”
Mtu awaye yote anayetaka
kunolewa katika maisha yake basi na ajifunze kunyenyekea na kukaa katika neno
la Mungu, Mungu analiheshimu sana neno lake lakini sio hivyo tu anawaangalia
watu waliopondeka watetemekao wasikiapo neno lake Isaya 66:2 “Maana mkono wangu ndio uliofanya
hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu
ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka,
atetemekaye asikiapo neno langu.”
Muda
usingeliweza kutosha kuona namna na jinsi neno la Mungu linavyofanya kazi
katika mazingira mbali mbali lakini lenyewe ni chuma ni nyundo ivunjayo mawe
vipande vipande lina uwezo wa kuzalisha nguvu za aina yoyote ile tuitakayo,
lina uwezo wa kutunoa na kutufanya upa na kututakasa na kutuweka sawa!
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni