Yoeli 3:12-14 “Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la
Yehoshafau; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande
zote. Haya! Utieni mundu, maana mavuno yameiva; njoni, kanyageni; kwa maana
shinikizo limejaa, mapipa nayo yanafurika; kwani uovu wao ni mwingi sana.
Makutano makubwa, makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa
maana siku ya Bwana i karibu, katika bonde la kukata maneno.”
Utangulizi:
Maandiko matakatifu yanatufundisha
kuwa kila mtu na aitii mamlaka iliyokuu, kwa sababu hakuna mamlaka isiyotoka
kwa Mungu na kuwa ile iliyoko imeamriwa na Mungu au imeruhusiwa na Mungu, na
kwa sababu hiyo kuiasi mamlaka ni kumuasi Mungu mwenyewe ona
Warumi 13:1-4 “Kila
mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu;
na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na
agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. Kwa maana watawalao
hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya.
Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake;
kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo
mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu,
amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.”
Maandiko
yanathibitisha wazi kuwa kama mtu atashindana na mwenye mamlaka ni wazi kuwa
anashinda ana agizo la Mungu na sio hivyo tu washindanao na Mungu watajipatia
hukumu! Kanuni ya Mungu siku zote hasimami na muasi, Mungu husimama na mtu wake
au mtumishi wake aliyemuweka, Mungu hajipingi mwenyewe wala hawezi kushindana
kinyume na kusudi lake hivyo atasimama na Mtumishi wake, aliyemuweka kwa kusudi
lake
1Samuel 2:9-10 “Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu
watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda; Washindanao na
Bwana watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; Bwana ataihukumu
miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi
wake.”
Nyakati za agano la kale Mungu katika Hekima yake, alipokuwa
amekusudia kuamua lipi ni lipi au watu walipokuwa wanataka kuamua jambo au
kutafuta suluhu ya kivita mara nyingi maamuzi yao yalifanyika katika bonde,
pande zinazoshindanda zingekaa upande huu wa mlima na upande huu wa mlima na
kisha baada ya uamuzi kufanyika pale bondeni ndipo mahali ambapo watu wangeweza
kufanya maamuzi yao na hapo palijulikana sana kama Bonde la kukata maneno. Vita
ingapiganwa hapo na damu ingemwagika hapo bila kuinajisi nchi, na Mungu angetoa
ushindi kwa mtu husika.
Maana ya Bonde la kukata maneno!
Kama nilivyogusia katika
utangulizi neno Bonde la kukata maneno, limetumika katika maandiko kumaanisha
eneo la kufanya uamuzi, au bonde la kumaliza maneno hususani wakati kuna jambo
linahitaji kufanyiwa uamuzi ikiwemo kumaliza vita, au bonde la kumaliza
migogoro kati ya watu wa Mungu na adui wa watu wa Mungu, Nyakati za biblia watu
walipokuwa na vita kati ya taifa moja na taifa jingine au ufalme mmoja na
ufalme mwingine walikuwa na tabia ya kukaa upande mmoja wa mlima na upande wa
pili wa mlima na kutupiana maneno ya kujigamba, kila mmoja angeweza kusema kile
anachoweza kukisema lakini hatimaye wangeshuka katika Bonde na kumaliza mgogoro
au maneno kwa kuonyeshana umwamba bonde
la kukata maneno lilikuwa kama Mahakama ya usuluhishi au kumaliza ubishi wa
kila mmoja kwa namna yake mfano
1Samuel 17:1-11 “Wakati huo Wafilisti
walikusanya majeshi yao kwa vita, nao wakakusanyika huko Soko, ulio mji wa
Yuda, wakatua kati ya Soko na Azeka, katika Efes-damimu. Naye Sauli na watu wa
Israeli wakakusanyika, wakatua katika bonde la Ela, nao wakapanga vita juu ya
hao Wafilisti. Wafilisti wakasimama juu ya mlima upande huu, na Waisraeli
wakasimama juu ya mlima upande huu, napo palikuwa na hilo bonde katikati. Ndipo
akatoka shujaa katika kambi ya Wafilisti, aliyeitwa Goliathi, wa Gathi, ambaye
urefu wake ulikuwa mikono sita na shibiri moja. Alikuwa na chapeo ya shaba
kichwani, tena amevaa darii ya shaba; na uzani wake ile darii ya shaba ulikuwa
shekeli elfu tano za shaba. Tena amevaa mabamba ya shaba miguuni mwake, naye
alikuwa na mkuki wa shaba kati ya mabega; yake. Na mti wa fumo lake ulikuwa
kama mti wa mfumaji; na kichwa cha mkuki wake kilikuwa shekeli mia sita za
chuma uzito wake; na mtu aliyemchukulia ngao yake akamtangulia. Naye akasimama,
akawapigia kelele majeshi ya Israeli akawaambia, Mbona mmetoka kupanga vita?
Je! Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mtu, akanishukie
mimi. Kama akiweza kupigana nami na kuniua, sisi tutakuwa watumwa wenu; nami
nikimshinda yeye na kumwua, ninyi mtakuwa watumwa wetu, na kututumikia. Yule
Mfilisti akasema, Nayatukana leo majeshi ya Israeli; nipeni mtu tupigane. Basi
Sauli na Israeli wote waliposikia maneno hayo ya Mfilisti, wakafadhaika na
kuogopa sana.”
Kwa hiyo utaweza kuona kuwa
katikati walipokuwa wakitupiana maneno walikaa upande huu wa mlima na upande
huu wa mlima na walitupiana maneno, lakini hapa katikati ya bonde ndio mahali sasa
paliitwa bonde la kukata maneno, kwamba sema utakavyosema na tukana
utakavyotukana tamba utakavyotamba na kunya utakavyo kunya na harisha
uatakavyoharisha toa shombo za kila namna lakini tutakutana katika bonde la
kukata maneno na hapo ndio Mungu ataonyesha kuwa nani ni mbabe? Nani yuko
pamoja naye na ni nani aliyechaguliwa na Mungu, nani anapigana vita vya
kishetani na ni nani anapigana vita vya Bwana!, Bonde la kukata maneno kwa
msingi huo liliitwa bonde la maamuzi, kibiblia pia liliitwa bonde la Yehoshafau
kwa mujibu wa nabii Yoeli, hii ni kwa sababu katika bonde hili Mungu
aliwadhalilisha maadui wa Israel mara kadhaa hususani wakati wa
Yehoshafati mara mbili, lakini pia jina
Yehoshafati maana yake Yehova ndiye muamuzi wangu, kinabii mahali hapa ndipo Mungu atakapokuja
kuuhukumu Mataifa yote yatakayosimama kinyume na Israel na Mungu atawaangamiza
watu wengi sana katika eneo hili hivyo
patakuwa na mauti ya kutisha na kushangaza patakuwa ni mahali pa msiba kwa wale
wote wasiomcha Mungu ona
Ezekiel 39:13-16 “Naam, watu wote wa nchi hiyo watawazika; itakuwa ni sifa
kwao katika siku ile nitakapotukuzwa, asema Bwana MUNGU. Nao watawachagua watu
wa kufanya kazi ya daima, watakaopita kati ya nchi, ili kuwazika waliosalia juu
ya uso wa nchi, ili kuisafisha; miezi saba itakapokwisha kupita watatafuta. Na
hao wapitao kati ya nchi watatafuta; na mtu ye yote aonapo mfupa wa mtu, ndipo
atakapoweka alama karibu nao, hata wazishi watakapouzika katika bonde la
Hamon-Gogu. Tena, Hamona litakuwa jina la mji. Hivyo ndivyo watakavyosafisha
nchi.”
Ezekiel analiona bonde hilo pia
kuwa ni mahali watakapozikwa watu wengi sana walio kinyume na mapenzi ya Mungu,
maiti zao zitazikwa mahali hapo na kumbukumbu lao litapotelea mahali hapo,
Kijiografia eneo hilo linasemekana liko Israel karibu na bonde la Kidron
Mashariki ya Yerusalem, eneo hili kinabii pia ndio litakuja kuwa eneo ambalo
Yesu atabagua Kondoo na Mbuzi na kutoa hukumu kwa mataifa yatakayokuwa kinyume
na Israel
Mathayo 25:31-46 “Hapo atakapokuja Mwana wa
Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo
atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele
zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;atawaweka
kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme
atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu,
urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa
na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni,
mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama;
nalikuwa kifungoni, mkanijia. Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana,
ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni
lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena
tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? Na Mfalme atajibu, akiwaambia,
Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo,
mlinitendea mimi. Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto,
Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari
Ibilisi na malaika zake; kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa
na kiu, msininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike;
nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. Ndipo hao pia watajibu,
wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au
u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? Naye atawajibu, akisema,
Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo,
hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali
wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.” Watu wasiotaka
kutawaliwa na Yesu aidha watachinjwa katika eneo hili Luka 19: 27 “Tena, wale adui zangu,
wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu.”
Msiba katika Bonde la kukata maneno!
Kama tulivyoona maana ya bonde la
kukata maneno kwa kawaida Hapa ndio mwisho wa mabishano yote na mashindano
yote, Mungu anapokuja katika bonde la kukata maneno huwa anaonyesha wazi wazi
nani ni mshindi na ni nani yuko upande wake na kwa kawaida katika Bonde la
kukata maneno huwa ndio mwisho wa maamuzi ya Mungu, kwa kawaida hata kama mahali
hapo hapana bonde Mungu huweza kuifunua ardhi na kufanya bonde popote na
kupoteza watu waliomuasi,
Hesabu 16:1-34
“Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi,
mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na
Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni; nao, pamoja na watu kadha wa
kadha wa wana wa Israeli, watu mia mbili na hamsini, Wakuu wa mkutano,
waliokuwa wateule wa mkutano, watu wenye sifa, wakainuka mbele ya Musa; nao
wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa
kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, Bwana naye yu kati
yao; n'nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa Bwana? Musa aliposikia maneno
haya, akapomoka kifudifudi; kisha
akanena na Kora na mkutano wake wote, akawaambia, Asubuhi Bwana ataonyesha ni
kina nani walio wake, kisha ni nani aliye mtakatifu, tena ni nani
atakayemkaribisha kwake; maana, yeye atakayemchagua ndiye atakayemsongeza
kwake. Fanyeni neno hili; twaeni vyetezo, ninyi Kora na mkutano wake wote;
vitieni na moto, mkaweke na uvumba juu yake mbele za Bwana kesho; kisha itakuwa
ya kwamba mtu Bwana atakayemchagua, yeye atakuwa mtakatifu; inawatosha ninyi,
enyi wana wa Lawi. Musa akamwambia Kora, Sikizeni basi, enyi Wana wa Lawi; Je!
Mwaona kuwa ni jambo dogo kwenu, kuwa Mungu wa Israeli amewatenga ninyi na
mkutano wa Israeli, ili apate kuwakaribisha kwake; ili mfanye utumishi wa
maskani ya Bwana, na kusimama mbele ya mkutano ili kuwatumikia; tena ya kuwa
amekuleta uwe karibu, na ndugu zako wote wana wa Lawi pamoja nawe? Nanyi, je!
Mwataka na ukuhani pia? Kwa sababu hii wewe na mkutano wako wote mmekusanyika
kinyume cha Bwana; na Haruni, je! Yeye ni nani hata mkamnung'unikia? Kisha Musa
akatuma kuwaita Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu; nao wakasema, Hatuji sisi;
je! Ni jambo dogo, wewe kutuleta kutoka nchi iliyojawa na maziwa na asali, ili
kutuua jangwani, lakini pamoja na haya wajikuza mwenyewe uwe mkuu juu yetu
kabisa? Kisha, hukutuleta katika nchi iliyojawa na maziwa na asali, wala
hukutupa urithi wa mashamba, na mashamba ya mizabibu; je! Unataka kuwatoboa
macho watu hawa? Hatuji. Musa akakasirika sana, akamwambia Bwana. Usiikubali
sadaka yao; mimi sikutwaa hata punda mmoja kwao, wala sikumwumiza hata mtu
mmoja miongoni mwao. Kisha Musa akamwambia Kora, Wewe na mkutano wako wote
iweni hapa mbele ya Bwana kesho, wewe, na wao, na Haruni; mkatwae kila mtu
chetezo chake, na kutia uvumba juu yake, mkavilete mbele za Bwana, vyetezo mia
mbili na hamsini; wewe pia, na Haruni, kila mtu na awe na chetezo chake. Basi
wakavitwaa kila mtu chetezo chake, wakatia na moto ndani yake, wakatia na
uvumba juu ya moto, na kusimama pale mlangoni pa hema ya kukutania, pamoja na
Musa na Haruni. Kisha Kora akakutanisha mkutano wote kinyume chao mlangoni pa
hema ya kukutania; na utukufu wa Bwana ukatokea mbele ya mkutano wote. Kisha
Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya
mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja. Nao wakapomoka kifudifudi,
wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya
dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote? Bwana akasema na Musa, na kumwambia,
Nena na mkutano, na kuwaambia, Ondokeni ninyi hapo karibu na maskani ya Kora,
na Dathani, na Abiramu. Basi Musa akainuka na kuwaendea Dathani na Abiramu; na
wazee wa Israeli wakaandamana naye.
Akasema na mkutano, na kuwaambia, Nawasihi, ondokeni penye hema za hawa
watu waovu, wala msiguse kitu chao cho chote, msiangamizwe katika dhambi zao
zote. Basi wakaondoka hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani na Abiramu,
pande zote; nao kina Dathani na Abiramu wakatoka nje wakasimama mlangoni mwa
hema zao, pamoja na wake zao, na wana wao na watoto wao wadogo. Musa akasema,
Kwa jambo hili mtajua ya kwamba Bwana amenituma, ili nifanye kazi hizi zote; kwa
kuwa mimi sikuzifanya kwa akili zangu mwenyewe. Kama watu hawa wakifa kifo cha
sikuzote, kama watu wote wafavyo, au kama wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu
wote; hapo basi Bwana hakunituma mimi. Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo
nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia
shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana Basi
ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao
ikapasuka; nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na
wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote. Basi wao, na wote waliokuwa
nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle
mkutanoni. Nao Israeli wote waliokuwa kando-kando yao wakakimbia kwa ajili ya
kilio chao; kwa kuwa walisema, Nchi isije kutumeza na sisi.”
Haijalishi kuwa wapinzani wako
wana maneno kiasi gani, wana nguvu kiasi gani, wana tisha kiasi gani, lakini
mwisho wa siku wataingia katika bonde la kukata maneno na hapa Mungu ataingilia
kati na kutenda mambo ya ajabu, atamsambaratisha adui na kumfutilia mbali, heri
leo kuwa upande wa Bwana, fungua macho yako uelewe kuwa Mungu yuko upande gani
simama kule aliko Mungu na ushindi utakuwa dhahiri, usipokuwa upande wa Bwana
na usipotaka Bwana akutawale utachinjwa
Goliati alijitamba kwa siku 40
kila siku akiwatisha watu wa Israel lakini alipotokea mtu aliyepakwa mafuta
katika bonde la kukata maneno Daudi mwana wa Yese. Goliathi alizimia na kukatwa
kichwa
1Samuel 17:44-51 “Mfilisti akamwambia
Daudi, Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa
mwituni. Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na
fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa
majeshi ya Israeli uliowatukana. Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu,
nami nitakupiga, na kuku ondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa
angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia
nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli. Nao jamii ya watu wote pia wajue
ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye
atawatia ninyi mikononi mwetu. Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda
akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili
akutane na yule Mfilisti. Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe
moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe
hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi. Hivyo Daudi akamshinda
yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi
hakuwa na upanga mkononi mwake. Ndipo Daudi akapiga mbio, akasimama juu ya
Mfilisti, akautwaa upanga wake, akaufuta alani mwake, akamwua, akamkata kichwa
kwa upanga huo. Nao Wafilisti walipoona ya kuwa shujaa wao amekufa, wakakimbia.”
Kama wako watu wanakushambulia
katika maisha yako wanatangaza vita na wewe usiogope uko mwisho wao katika
Bonde la kukata maneno Mungu ataingilia kati na bonde lako la vita litageuka
kuwa Bonde la Baraka kwako lakini litakuwa bonde la msiba kwa maadui zako
2Nyakati 20:17-27 “Hamtahitaji kupigana
vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa Bwana ulio pamoja nanyi, enyi Yuda
na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa Bwana
yu pamoja nanyi. Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka mbele za
Bwana Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia Bwana.Na Walawi, wa wana wa
Wakohathi na wa wana wa Wakorahi, wakasimama ili wamsifu Bwana, Mungu wa
Israeli, kwa sauti kuu sana. Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika
jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema,
Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini Bwana, Mungu wenu,
ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa. Naye
alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia Bwana, na
kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema,
Mshukuruni Bwana; kwa maana fadhili zake ni za milele. Nao walipoanza kuimba na
kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima
Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa. Kwani wana wa Amoni na wa Moabu
waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali na kuwaharibu; nao
walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia kuharibu kila mtu
mwenziwe. Hata Yuda walipofika mnara wa kulindia wa jangwani, wakalitazama hilo
jeshi; nao, angalia, walikuwa maiti walioanguka nchi, wala hapana aliyeokoka.
Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao
wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko
wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi
sana. Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo
walipombarikia Bwana; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka
hata leo. Kisha wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati mbele
yao, ili kuurudia Yerusalemu kwa furaha; kwa kuwa Bwana amewafurahisha juu ya
adui zao.”
Bonde lilikuwa ni kama ulingo wa
mabondia waliotambiana kwa muda mrefu, afile munu asigale munu, acholile
kachola, show show na kadhalika, Bonde la kukatya maneno ni ikama kiwanja cha
mpira wa soka watu wataingia kati dakika 90 utachezwa na mwamba ataonekana,
watu wataingia ulingoni zitapigwa na mwamba ataonekama
Siku ya leo haijalishi una vita
na nani, haijalishi nani ametangaza vita na wewe kumbuka liko Bonde la kukata
maneno, liko bonde ambalo kwalo Mungu atamaliza migogoro yote atamaliza kesi
zote atafanya maamuzi na mwisho wa siku wale ambao Bwana amewachagua atawaleta
kwake naye ataligeuza Bonde lako kuwa sio la vita tena bali la ushindi na bonde
la Baraka na bonde la kuteka mateka na
bonde la kukusanya nyara na wapinzani wako na maadui zako itakuwa ni msiba
katika bonde la kukata maneno!, Ukiwa na Yesu hutaogopa kama mfalme
Yehoshafati, watu walio na Mungu hawapigani tu vita vya maneno, kama Goliathi
sisi tunalitaja jina la Bwana Mungu wetu yeye ndio tegemeo letu na tumaini letu
hakuna mtu aliyemtumainia akatahayari, hatutatahayarika kamwe, Mungu atamaliza
ngebe za adui zako, Penina alikuwa na maneno sana kuliko Hanna kwa sababu hana
alionekana kuwa tasa na hazai, lakini siku moja mwenye nguvu akaingilia kati na
hana akasema maneno ya ushindi, ona
1Samuel
2:2-9 “Hakuna aliye mtakatifu kama Bwana; Kwa maana
hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu. Msizidi kunena kwa
kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa
maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.Pinde zao mashujaa zimevunjika,
Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu. Walioshiba wamejikodisha ili kupata
chakula, Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha. Naam, huyo aliyekua tasa
amezaa watoto saba, Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika. Bwana huua, naye
hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu. Bwana hufukarisha mtu,
naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. Humwinua mnyonge kutoka
mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu,
Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana,
Naye ameuweka ulimwengu juu yake. Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali
waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;”
Bwana ampe neema kila mmoja wetu
na maisha ya ushindi kwa kila anayemtegemea Bwana na asiyezitegemea akili zake
mwenyewe na tukutane katika bonde la kukata maneno!
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni