Kutoka 3:7-10 “BWANA akasema, Hakika
nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa
sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili
niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema,
kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na
Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. Basi, tazama, kilio cha wana wa
Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.
Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana
wa Israeli, katika Misri.”
Utangulizi:
Tuwapo Duniani tunapitia
changamoto za aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mikandamizo ya aina
mbalimbali kutoka kwa Shetani ambaye ndiye adui mkubwa wa maisha ya wanadamu,
Mungu hafurahii uonevu au udhalimu wa aina yoyote ule unaowapata wanadamu, Wana
wa Israel kwa Muda mrefu sana walikuwa wakionewa na wamisri na wakikandamizwa
ili waendelee kuwa watumwa katika nchi ya Misri, hawakuweza kutoka, na adui
hakutaka kuwaachia kwa haraka mpaka Mungu alipoamua kuingilia kati.
Mungu alimtuma Musa kwa mfalme wa
Misri yaani Farao ili amuamuru mfalme huyu awaachie wana wa Israel waende zao
kwa kusudi alilolikusudia Mungu mwenyewe yaani wakamtumikie Mungu na kutimiza
kusudi lake, Ujumbe mkubwa aliopewa Musa ulikuwa ni kumwambia Farao Mungu wa
ewaebrania ameamuru uwaachie watu wake waende, WAACHE WATU WANGU WAENDE hii ilikuwa ni Amri na sio ombi ujumbe huu
umerudiwa tena na tena kwa farao waachie watu wangu waende ona katika maandiko yafuatayo:-
Kutoka 5:1 “Hata baadaye, Musa na Haruni wakaenda wakamwambia Farao,
wakasema, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, WAPE WATU WANGU RUHUSA WAENDE,
ili kunifanyia sikukuu jangwani.”
Unaona sifurahiswi kwa namna fulani
na lugha inayotumika katika Kiswahili kwa sababu yenyewe iko katika mfumo wa
kiungwana nani kama ombi WAPE WATU WANGU RUHUSA WAENDE kimsingi
Mungu hakuwa anaomba ruhusa Mungu alikuwa anaamuru ni amri kwa Farao WAACHIE WATU WANGU WAENDE, Lugha ya
kiingereza katika maeneo yote yanayozungumzia WAPE WATU WANGU RUHUSA WAENDE inatumia AMRI lugha inayotumika kiingereza ni neno
LET MY PEOPLE GO sawa na kuamuru
Waachie watu wangu waende ni aina hii ya lugha ndio inayojirudia rudia kila
mahali kwenye kitabu cha kutoka na
maeneo mengine na unaweza kuona ;-
Kutoka 8:1 “BWANA akamwambia Musa, Ingia
kwa Farao, ukamwambie, BWANA asema hivi, Wape watu wangu ruhusa, ili wapate
kunitumikia.”
Kutoka 8:20 “BWANA akamwambia Musa, Inuka
asubuhi na mapema usimame mbele ya Farao; angalia! Atoka aende majini;
kamwambie, BWANA asema, Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie mimi.”
Kutoka 9:1 “Ndipo BWANA akamwambia Musa,
Ingia wewe kwa Farao, umwambie, BWANA, Mungu wa Waebrania, yuasema, Wape ruhusa
watu wangu ili waende wanitumikie.”
Kutoka 9:16-17 “lakini, nilikusimamisha
wewe kwa sababu hii hii, ili nikuonyeshe uweza wangu, tena kwamba jina langu
litangazwe katika dunia yote. Nawe, je! Hata sasa wajitukuza juu ya watu wangu,
usiwape ruhusa waende zao”?
Unaona ni kwanini Mungu amerudia
mara kwa mara kwa msisitizo waache watu wangu waende? Mungu hafurahii udhalimu,
ukandamizaji na mateso ambayo kwaasili watu wake wanayapitia Mungu aliamua
kuingilia katika hali ya wana wa Israel kwa kuwa walikuwa wanaonewa na wamisri
na wamisri ndio walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko Israel, Mungu hakubaliani na
uonevu wa aina yoyote ile:-
Uonevu ni nini hasa!
1. Ni
kukandamizwa na kuwekwa chini ya mamlaka ya mtu mwingine mwenye nguvu zaidi
yako bila matakwa yako mwenyewe
2. Ni
kuonewa au kuteswa na nguvu Fulani iliyojuu zaidi ya uwezo wako wa kawaida,
bila uhuru kamili
3. Uonevu
hauko katika eneo moja tu, unaweza kuweko katika mwili, katika akili, katika
nafsi, katika ndoa, katika fedha katika Elimu,Biashara, haki na kadhalika na pia uko uonevu wa kiroho au tunaweza kusema
kuwa asili yauonevu wa aina yoyote unaouona ni kutokea rohoni au katika
ulimwengu wa kiroho;
Hatuna budi kugundua na kubaini
ni maeneo gani ya uonevu shetani anatuonelea ili tuweze kuliitia jina la Mungu
atuokoe, kumbuka Israel waliteseka mpaka pale walipolia na kutafuta msaada wa
Mungu ndipo Mungu aliposhuka ili awaokoe ona Zaburi 118:5 “Katika shida yangu nalimwita
BWANA; BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi.” Unaona kila shida
unayoipitia kama mwanadamu hakikisha ya kuwa unamuita Bwana yaani Mungu naye
atakuweka panapo nafasi yaani atakujibu na kutatua tatizo ulilonalo usinyamaze
ukafikiri ya kuwa Mungu amekusahau, HAPANA Mungu anakutaka uwajibike na kufanya
sehemu yako kwa kukataa hali unayoipitia.
Zaburi 42:9 “Nitamwambia Mungu, mwamba
wangu, Kwa nini umenisahau? Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea? ”
Mwandishi wa zaburi aliamua
kuomba Mungu Mwamba wake aliona kama amesahaulika adui alikuwa akimuonea na
hakuwa na furaha alikumbuka kumwambia Mungu, ni lazima tumlilie Mungu atutoe
katika hali zozote za mikandamizo tunazozipitia duniani kumbuka kuwa ni ahadi
ya Mungu kutuweka huru kutoka kwa wale wanaotuonea, Mungu ameahidi kwamba
utakuwa mbali na kunewa ona
Isaya 54:14. “Utathibitika katika haki;
utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana
haitakukaribia.”
Wakati wowote uonevu sio jambo
zuri, maandiko yanasema uonevu humfanya mtu awe kama kichaa, Moja ya sababu ya
kuja kwa Yesu Kristo duniani kama Mwokozi ni pamoja na kufanya kazi ya
kuwafungua walioonewa ona Matendo 10:38
“habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia
mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi
njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja
naye.” Adui yetu mkuu adui wa wanadamu wote na anayetuonea ni
shetani yeye hutuonea katika mazingira mbalimbali na wakati mwingine anawatumia
watu kuleta uonevu, shetani na mapepo na maajenti wake wanaweza kumuonea
mwanadamu katika maeneo zaidi ya kumi na tano:-
·
Unaweza kuonewa Mwili
·
Unaweza kuonewa kwa asili
·
Unaweza kuonewa kiakili
·
Unaweza kuonewa Kiroho
·
Unaweza kuonewa katika Ndoa yako
·
Unaweza kuonewa kiuchumi
·
Unaweza kuonewa Kazini
·
Unaweza kuonewa katika ndoto
·
Unaweza
kuonewa kwa maneno
·
Unaweza kuonewa kihisia/Kisaikolojia/kijinsia.
·
Unaweza kuonewa kichawi
·
Unaweza kuonewa kwa ukoo mzima mnateswa ukoo
wenu wote au familia yenu yote
·
Unaweza kuonewa kwa nguvu na uonevu wa
kukandamizwa
·
Unaweza kuonewa katika haki zako makahamani
·
Unaweza kuonewa bila sababu
·
Unaweza kuonewa kwa sababu
·
Unaweza kuonewa kihuduma
Maandiko yanaonyesha kuwa kila
aina ya uonevu hutoka kwa shetani Yohana
10:10 “Mwivi
haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha
wawe nao tele.” Ni kwa sababu ya kuonewa kwa namna mbalimbali Mungu
alimpaka Yesu Mafuta ili aweze kuwakomboa wanadamu, na Mungu vilevile huwapaka
watumishi wake mafuta ili kuzivunja nira za uonevu ona Luka 4:18-19 “Roho wa Bwana yu juu yangu,
Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma
kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha
huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.” Unaona
Lugha inayotumika hapo kusetwa maana yake ni kuonewa huduma ya kimasihi
ilitolewa na Mungu kwa wanadamu kwa kusudi la kuwaweka watu huru kutoka katika
uonevu wa kila namna, kama Musa ambaye alikuwa na ujumbe waache watu wangu
waende, Yesu ana ujumbe ulio bora zaidi katika ufalme wa ibilisi kumuamuru kwa
jina lake kukuacha uwe huru kutoka katika aina yako ya mgandamizo uliyo nayo!
Tunawezaje basi kutoka katika migandamizo ya shetani.
1.
Kubali
zawadi ya wokovu:
Ni ukweli ulio
wazi kuwa wokovu ni msamaha wa dhambi, nani ukweli ulio wazi kuwa Mungu
anatuhurumia na mgandamizo mkubwa na wa kwanza alionao mwanadamu ni kuwa katika
maisha ya dhambi, dhambi yenyewe ikukutawala inakugeuza kuwa mtumwa
inakukandamiza, wanadamu wengi wanakandamizwa na dhambi hivyo ni watumwa wa
dhambi hawawezi kuimudu na hawawezi kuishinda ona Yohana 8:34 “Yesu akawajibu, Amin, amin,
nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.” Matatizo mengi
ya wanadamu yamesababishwa na dhambi, mtu anayedumu katika dhambi naye ni
mtumwa wa dhambi, dhambi ni mlango mkubwa wa mashambulizi mengi ya adui katika
maisha yetu na uharibifu wa kila namna,
wakati mwingine utaweza kuona mtu aliposamehewa dhambi hapo hapo alipata
na uponyaji wa mwili na akili na roho ona Zaburi
103:3 “Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa
yako yote,” unaona Mungu anaposamehe dhambi katika kifurushi kimoja
hikihiki cha msamaha anatoa na uponyaji kwa hivyo kimaandiko ni dhahiri kwamba
dhambi ikiondoka kwetu ni rahisi sana kuwa huru katika maeneo mengine Yohana 5:14 “Baada
ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima;
usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.” Unaona
yako mateso mengine ambayo yana uhusiano wa moja kwa moja na dhambi japo sio
yote hivyo Mungu anapotusamehe dhambi basi moja kwa moja anatuweka huru vile
vile na kutupa uzima wa maeneo mengine, unapokuwa kwenye dhambi unapoteza haki
zako nyingi ikiwa ni pamoja na ulinzi wa Mungu na hivyo adui anakuwa na mamlaka
ya kukuonea lakini wokovu unapokuja kwetu tunapewa haki yetu
Warumi 6:16-20 “Hamjui
ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii,
mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti,
au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki. Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa
maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya
elimu ambayo mliwekwa chini yake; na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi,
mkawa watumwa wa haki. Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa
miili yenu. Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi
mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate
kutakaswa. Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki.”
Uko uhusiano
mkubwa sana wa mafanikio yetu ya kiroho yaani wokovu na afya yetu Yakobo 5:13-15 “Mtu
wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe
zaburi. Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee,
na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa
mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.”
3Yohana 1:2 “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo
yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo”
Unaona kwa hiyo
kuipokea zawadi ya wokovu ni kwa Muhimu na msingi wa kufunguliwa kwetu kutoka
katika migandamizo ya namna mbalimbali wokovu una uhusiano mkubwa na kusamehewa
dhambi Luka 1:77 “Uwajulishe watu wake wokovu, Katika kusamehewa dhambi zao.”
Na Mafanikio yetu katika mambo yote
asili yake ni mafanikio ya roho zetu, Ni
kwaajili ya ukombozi wa Mwanadamu Mungu alimtuma Yesu duniani ili kila
anayemwamini awe na uzima wa milele kwa hivyo tunapata uzima huu na uzima wa
milele, Yesu alitolewa pale msalabani na kuteswa na kuuawa ili sisi tuweze
kupona katika maeneo yote kama asemavyo nabii Isaya mahali Fulani hivi:-
Isaya 53:3-5 “Alidharauliwa
na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu
ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania
ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa
yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na
kwa kupigwa kwake sisi tumepona.”
Kumbe ni ukweli
ulio wazi kuwa tukimwamini Bwana Yesu kazi yake aliyoifanya pale msalabani na
kuikubali kama zawadi tutaokolewa, Na ndani ya wokovu tutapata raha nyingi sana
nafsini mwetu wokovu huwa na ukombozi mkubwa na wa aina nyingi. Yesu alikuwa
ameahidi tujitie nira yake ili tusilemewe na mizigo yaani utumwa wa namna
mbalimbali Mathayo 11:28-29 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na
mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi
ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;”
2.
Uwe
na ufahamu wa neno la Mungu.
Ufunuo 12:10-11 “Nikasikia
sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu
wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu
zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. Nao wakamshinda
kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha
yao hata kufa.”
Neno la ushuhuda
maana yake ni neno la Mungu, neno la Mungu lina nguvu na mamlaka kubwa sana
kuliko tunavyodhani lenyewe linafananishwa na nyundo ivunjayo mawe vipande
vipande ona Yeremia 23:28-29 “Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye
na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko
ngano? Asema Bwana. Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo
ivunjayo mawe vipande vipande? ”
Unaona iwapo
unataka ushindi katika maisha yako huna budi kujaa neno, Neno linafananishwa na
moto au nyundo ivunjayo mawe vipande vipande, hivyo tukiujaza ufahamu wetu kwa
neno la Mungu kila aina ya utumwa itavunjika haijalishi ni utumwa wa zamani kiasi gani, au ni wenye nguvu kiasi
gani wala haijalishi ni nani ametuweka kwenye utumwa huo, au utumwa huo
unatokea wapi?, kinga kubwa na ya kipekee na silaha ya kumshambulia adui na
kupata ushindi ni neno la Mungu.
Waebrania 4:12-13 “Maana
Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote
ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta
yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala
hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na
kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.”
Kamwe tusilidharau
neno la Mungu wala kulichukulia kama kitu cha kawaida neno la uzima linga nguvu
ya kubadili kila kitu katika maisha yetu neno la Mungu linapotamkwa huwa
haliendi bure ni lazima litatimiza mapenzi ya Mungu ona
Isaya 55:9-11 “Kwa
maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi
juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Maana kama vile
mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha
ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye
chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu;
halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika
mambo yale niliyolituma.”
Neno la Mungu ni
roho tena ni uzima Yohana 6:63 “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo
niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.”
Muda usingeweza
kutosha kupitia maeneo kadhaa wa kadhaa yanayotufundisha kuhusu neno la Mungu
ni ukweli ulio wazi kuwa Yesu alipopandishwa katika mlima wa majaribu alikutana
na shetani na kwa kutumia neno la Mungu aliweza kupata ushindi mkubwa hakuweza
kujitia chini ya ushawishi na majaribu ya yule Muovu, tunaweza kushinda hali
zozote zile endapo tutakuwa na tabia ya kutafuta neno la Mungu linazungumza
nini kutokana na hali yetu na ile hali tunayokumbana nayo na tukajiweka huru!
3.
Omba
kwaajili ya ukombozi.
Mwanadamu
anapokuwa anakandamizwa na ibilisi katika maeneo mbalimbali, kumbuka kuwa
huwezi kujitoa mwenyewe katika maeneo hayo, ni lazima umuombe Mungu aje akupe
msaada wa ukombozi, akukomboe kutoka katika hali unayoipitia, Neno ukombozi
limetajwa mara 147 katika maandiko, Yesu ni mwokozi maana yake vilevile ni
Mkombozi, watu waliokuwa wanatazamia
kuzaliwa kwa Masihi vilevile wanaitwa watu waliokuwa wakiutazamia ukombozi
Luka 2:36-38 “Palikuwa
na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake
ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.
Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu
usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu,
na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari
zake.”
Yesu kwa kuwa ni
Mkombozi ni vema tunapopita taabuni
ni muhimu kuliitia jina lake kwaajili ya ukombozi, kwanini kwa sababu maandiko
yanaonyesha ya kuwa ndani yake yeye tunao ukombozi, Waefeso 1:6-7 “Na usifiwe utukufu wa
neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa. Katika yeye huyo, kwa
damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema
yake.” Kwa hiyo tunakubaliana kuwa kuna ukombozi na huu hufanywa na
Yesu Kristo kwa neema yake, Yeye alijitoa mwenyewe ili atukomboe sisi
Tito 2:13-14 “tukilitazamia
tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na
Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi
yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi
katika matendo mema.”
1Wakorintho 1:30-31 “Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu,
aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;
kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.”
Yesu kama
mkombozi wetu yu aweza kutukomboa nafsi zetu miili yatu na roho zetu, Mungu
alimkomboa Daudi katika shida zake zote na hakusahau jambo hili katika maisha
yake yote, kumbe tunaweza kupitia shida na mateso ya aina mbalimbali lakini
Mungu anaweza kutukomboa na shida zote ona
1Wafalme 1:30 “Naye mfalme akaapa, akasema, Bwana
aishivyo, aliyenikomboa roho yangu katika shida zote” Kristo Yesu
anaweza kutukomboa na shida zetu zote maana yake kila eneo ambalo kwalo adui
anakusudia kutukandamiza au anatukandamiza tayari tunaye mkombozi, tunaweza kukombolewa, familia zetu, maisha
yetu, ndoa zetu, uchumi wetu, na hata
kama tunadhani kuwa tuna laana ya aina yoyote laana hizo zinaweza kukombolewa
kupitia Jina la Yesu, Lakini
vilevile kwa imani katika kazi yake aliyoifanya pale Msalabani
Wagalatia 3:13-14 “Kristo
alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu;
maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; ili kwamba baraka
ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho
kwa njia ya imani.”
Ni wajibu wetu
kama waamini kuutarajia ukombozi Zaburi
130:7-8 “Ee Israeli, umtarajie Bwana; Maana kwa Bwana
kuna fadhili, Na kwake kuna ukombozi mwingi.Yeye atamkomboa Israeli na maovu
yake yote.” Mungu ameahidi
kuwa tumtarajie yeye, kumtarajia maana yake kumsubiria, kumgojea katika njia ya
Maombi, na kumtazamia, tunapaswa kuiamini ahadi hii ya Mungu na kumuomba
ukombozi katika maeneo mbalimbali tunayokandamizwa, Yeye ana uwezo wa kutukomboa
katika taabu zote, tunapomlilia yeye hutuponya na taabu zetu zote na kutukomboa
Zaburi
107:1-6. “Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa
maana fadhili zake ni za milele. Na waseme hivi waliokombolewa na Bwana, Wale
aliowakomboa na mkono wa mtesi. Akawakusanya kutoka nchi zote, Mashariki na
magharibi, kaskazini na kusini. Walitanga-tanga jangwani katika njia ya nyika;
Hawakuona mji wa kukaa. Waliona njaa, waliona na kiu, Nafsi yao ilikuwa
ikizimia ndani yao. Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.”
Tukimlilia Mungu
na kumuomba yeye atatuma ukombozi katika maisha yetu Zaburi 111:9 “Amewapelekea watu wake
ukombozi, Ameamuru agano lake liwe la milele, Jina lake ni takatifu la kuogopwa.”
Hatuna budi
kumuomba Mungu na kumlilia ili atukomboe na kutuachia kila mmoja asiwe chini ya
uonevu na kukandamizwa na ibilisi, Mungu na amuweke huru kila mmoja na familia
yake na ndugu zake na jamaa zake, Mungu atupe kuwa mbali na uonevu, Mungu na
atuthibitishe katika haki!, hatuna budi kumuomba Mungu atukomboe na roho zote
chafu za uharibifu, kiburi, migawanyiko, woga, uzushi, mikandamizo, rushwa,
uchafu, ufisadi, tamaa, mashaka, kutokusamehe, upotoshaji, uvivu, uchawi,
utapeli, uasi, hasira, ulevi, Mauti, maluweluwe, uchungu, zinaa na uasherati,
ulafi, choyo, ubinafsi, na mambo
yanayofanana na hayo!.
4.
Tumia
silaha ya kusifu:
Moja ya silaha
Muhimu ya ukombozi wetu kutoka kwa Mungu kwa mujibu wa maandiko ni pamoja na
kumsifu Mungu, Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kuanza maombi kwa Msingi wa
kumsifia Mungu kumuheshimu na kumtukuza yaani kumsifu Luka 11:1-2 “Ikawa alipokuwa mahali fulani
akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe
sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake. Akawaambia,
Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako
uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]”
Kusifu ni mlango au ufunguo wa kuingilia katika nyua yaani katika ukumbi wa
Mungu kwaajili ya kupokea huduma na majibu ya mahitaji yetu Zaburi 100:1-5 “Mfanyieni
Bwana shangwe, dunia yote; Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa
kuimba; Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake; Kwa kuwa Bwana ndiye
mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi.” Kwa
hiyo tunapoenda mbele za Mungu kwa ibada ya aina yoyote ile ikiwa ni pamoja na
maombi ni muhimu kuanza na kusifu kwa sababu sifa kwa Mungu inafungua mambo
mengi na kumfanya Bwana atujali, na kutusikiliza, Zaburi 29:1-2 “Mpeni Bwana, enyi wana wa
Mungu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu; Mpeni Bwana utukufu wa jina lake;
Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.” Kwa nini maandiko yaaagiza
kuanza ibada au maombi kwa kumsifu Mungu? Ziko sababu kadhaa wa kadhaaa:-
1. Kusifu kunaandaa mioyo yetu kumwangalia
Mungu huku tukiwa tunatambua sifa zake, tunapoaishwa kupelekwa kwenye uwepo
wake na kutusaidia kuelewa ukuu wake pale tunapomuendea lakini sio hivyo tu sifa zina tabia ya
kuufanya uwepo wa Mungu kushuka na kutuhudumia 2Nyakati 5:13 “tena Walawi waimbaji, wote
pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, hali
wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa
mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia na ishirini wakipiga panda;)
hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti
moja ya kumsifu na kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na
matoazi na vinanda, wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana
fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya
Bwana,hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya
lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa Bwana.” Kumbuka
ya kuwa Mungu anakaa katikati ya sifa
Zaburi 22:3 -5 “Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya
sifa za Israeli.Baba zetu walikutumaini Wewe, Walitumaini, na Wewe
ukawaokoa.Walikulilia Wewe wakaokoka, Walikutumaini wasiaibike.”
2. Kusifu kunaharibu vifungo vya adui Kila
kitu ambacho kinakandamiza maisha ya mwanadamu na kututishia katika uonevu
wa aina yoyote ile kimwili na hata kiroho vinaweza kutiishwa na kuharibiwa
kupitia Maombi Matendo 16:23-26 “Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa
gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana. Naye akiisha kupata amri
hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. Lakini
panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia
nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa
tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango
ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.”
3. Kusifu na kuabudu kunamfanya adui
achanganyikiwe na kupoteana, Hakuna silaha ya ajabu kama kumsifu Mungu na
kumuabudu, silaha hii ni ya kipekee inapotumika katika tishio la kivita au
uonevu Bila kujali kuwa jeshi lililojipanga ni kubwa kwa kiwango gani kumsifu
Mungu kutatuletea ushindi wa kushangaza sana angalia 2Nyakati 20:1-4 “Ikawa baadaye, wana wa
Moabu, na wana wa Amoni, na pamoja nao baadhi ya Wameuni, wakaja juu ya
Yehoshafati vitani.Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja
jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng'ambo ya bahari; na tazama, wako
katika Hasason-tamari (ndio En-gedi).Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake
amtafute Bwana; akatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yote.Yuda
wakakusanyika pamoja ili wamtafute Bwana; hata kutoka miji yote ya Yuda wakaja
kumtafuta Bwana.” Wakati majeshi ya wana wa Moabu na wana wa Amoni
na Wameuni walipokuwa wameungana kinyume na mfalme Yeshoshafati, unaweza kuona
pamoja na silaha yote ya kufunga na kumuomba Mungu safari hii maelekezo ya
Mungu namna ya kupigana na kupata ushindi ilikuwa ni kupanga waimbaji ili
wamsifu Mungu ona 2Nyakati 20:14-26 “Ndipo Yahazieli mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana
wa Yeieli, mwana wa Matania, Mlawi, wa wana wa Asafu, akajiliwa na roho ya
Bwana, katikati ya kusanyiko; akasema, Sikieni, Yuda wote, nanyi mkaao
Yerusalemu, na wewe mfalme Yehoshafati; Bwana awaambia hivi, Msiogope, wala
msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; kwani vita si yenu bali ni ya Mungu.
Kesho shukeni juu yao; tazameni, wanakwea kwa kupandia Sisi; nanyi mtawapata
penye mwisho wa bonde, mbele ya jangwa la Yerueli. Hamtahitaji kupigana vita,
jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa Bwana ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na
Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa Bwana yu
pamoja nanyi. Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka mbele za
Bwana Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia Bwana. Na Walawi, wa wana wa
Wakohathi na wa wana wa Wakorahi, wakasimama ili wamsifu Bwana, Mungu wa
Israeli, kwa sauti kuu sana. Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika
jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema,
Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini Bwana, Mungu wenu,
ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa. Naye
alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia Bwana, na
kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka
mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni Bwana; kwa maana fadhili zake ni za
milele. Nao walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa
Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa. Kwani
wana wa Amoni na wa Moabu waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali
na kuwaharibu; nao walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia
kuharibu kila mtu mwenziwe. Hata Yuda walipofika mnara wa kulindia wa jangwani,
wakalitazama hilo jeshi; nao, angalia, walikuwa maiti walioanguka nchi, wala
hapana aliyeokoka. Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao,
wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani,
walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka
nyara, maana zilikuwa nyingi sana.Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde
la Baraka; maana ndipo walipombarikia Bwana; kwa hiyo jina lake mahali pale
pakaitwa Bonde la Baraka hata leo.”
Unaona kumbe hatupaswi kuwa na hofu iko njia nyepesi
sana na silaha nzito ya kutukomboa nayo ni kumsifu Mungu, hii ni silaha kuu ya
kiroho hatupaswi kwa namna yoyote kudhani au kufikiri kuwa wakati wa kumsifu
Mungu ni wakati wa mzaha hapana ni wakati ambapo Mungu yuko kazini hivyo hatuna
budi kumaanisha linapokuja swala la kumsifu Mungu Zaburi 8:2 “Vinywani mwa watoto wachanga
na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe;
Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi.” Watu wanapomsifu Mungu hata kama ni watoto
kunakuwa na misingi ya nguvu na kukomesha adui na kujilipizia kisasi wote
wanaoshindana nasi watatupwa nje kama tutagundua siri iliyoko katika sifa,
kusifu kunatoa nguvu na kibali cha kuwafanyika hukumu dhidi ya adui zetu na
wafalme wao Zaburi 149:5-9 “Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu
vitandani mwao. Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao, Na upanga mkali kuwili
mikononi mwao. Ili kufanya kisasi juu ya mataifa, Na adhabu juu ya kabila za
watu. Wawafunge wafalme wao kwa minyororo, Na wakuu wao kwa pingu za chuma.
Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa; Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote.
Haleluya.”
Unaona kwa msingi huo hatuna budi wakati wote
kukumbuka ya kuwa kumsifu Mungu ni silaha yenye nguvu kubwa na ya ajabu sana
inayoweza kusukuma nyuma majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho na
mwili pia, kumsifu Mungu na kumtukuza hutufanya na kuyanoa mawazo yetu ili
yaweze kumuelekea Mungu na kutambua ukuu wake na uweza wake kila siku kama
ikiwezekana tuwe na Muda wa kumtukuza Mungu na kumsifu Biblia imeeleza hata
vitandani mwetu, unapopita katika wakati Mgumu acha kuogopa mwamini Mungu na
hakikisha kuwa unamuelekea yeye na wakati mwingine jaribu tu kumsifu na utaweza
kuona Mungu atakuweka huru! Hakuna Jeshi la aina yoyote litakaloweza kushindana
nawe kama wewe ni mtu uliyejaa sifa kwa Mungu, Kumsifu Mungu namna hii ndio
siri ya ushindi wa Daudi katika maisha yake
yote yeye alikuwa mtu aliyejaa zaburi za sifa na hivyo hakuwahi kushindwa
vita ya aina yoyote!
Zaburi 27:1-6 “Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani?
Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia,
Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi
lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata
hapo nitatumaini. Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta,
Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana,
Na kutafakari hekaluni mwake. Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya,
Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba. Na sasa
kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu
za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi Bwana.”
5.
Omba
upako wa Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu ni
moja ya mwanachama muhimu katika utatu wa Mungu anajihusisha sana na maeneo
mengi ya ukombozi wetu, yeye ni chanzo cha ushuhuda na ufunuo, anatuongoza
katika maamuzi ya kiulinzi kimwili na kiroho ili tusiiingie hatarini, yeye ni mfariji pia na hivyo anauwezo wa
kutusaidia na kutupa tumaini, Katika nyakati za agano la kale popote pale
ambapo palitokea uonevu na ukahitajika msaada wa kiungu basi Roho wa Mungu
alikuja kwa nguvu juu ya mmoja wapo ya waamuzi au mfalme na mfalme huyo
akawaweka watu huru, uhuru huu ulitokana
na upako wa Roho Mtakatifu, tunaambiwa kuwa Upako unavunja nira ona Isaya
10:27 “Tena
itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake
shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.”
Maandiko yanaonyesha kuwa Upako yaani mafuta ya Roho Mtakatifu huwa yanafanya
kazi ya kuondoa uonevu, Ni kazi ya Roho Mtakatifu kuwatia mafuta watumishi wake
ili wafanye kazi ya kuwatoa watu kutoka katika uonevu wa namna mbalimbali ona Luka 4:18-19 “Roho
wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari
njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona
tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.”
Unaona mafuta yaliyokuwa juu ya Yesu kutokana na Roho Mtakatifu yalifanya
kazi mbalimbali ya kuwafungua watu walioonewa na kukandamizwa na shetani, sio
hivyo tu lakini na kuwaponya na kuwaweka huru, tunaweza kusoma pia katika Matendo 10:38 “habari
za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu
naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na
Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.”
Nyakati za agano
la kale hususani kipindi cha waamuzi na wafalme Mungu Roho Mtakatifu aliwawezesha
wakati wote kufanya matendo ya ukombozi baada ya yeye kuja juu ya watumishi
wake na kuwatia nguvu iliyowawezesha kuwasaidia ndugu zao wasikandamizwe au
waliokuwa wanakandamizwa na maadui na kuwakimbiza adui zao ona maeneo
mblimbali:-
Waamuzi 3:9-11 “Kisha
wana wa Israeli walipomlingana Bwana, Bwana akawainulia wana wa Israeli
mwokozi, aliyewaokoa, yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu.
Roho ya Bwana ikamjilia juu yake, naye akawa mwamuzi wa Israeli; akatoka
kwenenda vitani, naye Bwana akamtia huyo Kushan-rishathaimu, mfalme wa
Mesopotamia, mkononi mwake; na mkono wake ukamshinda Kushan-rishathaimu. Nayo
nchi ikawa na amani muda wa miaka arobaini. Kisha Othnieli, mwana wa Kenazi,
akafa.”
Waamuzi 13:24-25 “Basi
yule mwanamke akamzaa mtoto mwanamume akamwita jina lake Samsoni, mtoto huyu
akakua, Bwana akambarikia. Roho ya Bwana ikaanza kumtaharakisha katika
Mahane-dani, katikati ya Sora na Eshtaoli.”
Waamuzi 14:19 “Roho
ya Bwana ikamjilia juu yake kwa nguvu, naye akatelemkia Ashkeloni, akapiga watu
waume thelathini katika watu hao, na kuzitwaa nyara zao, na kuwapa hao
waliokitambua kitendawili mavao hayo. Hasira zake zikamwaka, naye akakwea
kwenda nyumbani kwa baba yake.”
Waamuzi 11:28-29. “Lakini
mfalme wa wana wa Amoni hakuyasikiza hayo maneno ya Yeftha aliompelekea. Ndipo
roho ya Bwana ikamjilia juu yake Yeftha, naye akapita katika Gileadi na Manase,
akapita na katika Mispa ya Gileadi, na kutoka hapo Mispa ya Gileadi akapita
kuwaendea wana wa Amoni.”
Unaona popote
pale waaamuzi walipowasaidia watu ili kuwaletea ukombozi utaweza kuona Roho
Mtakatifu alikuja juu yao kwanza, Ni Roho huyu huyu Mtakatifu aliyeyainua
maisha ya waamuzi ili kuwatetea watu wake dhidi ya migandamizo ya aina
mbalimbali anaweza kwa uhalisia kutuwezesha na sisi kuondoka katika migandamizo
ya aina mbalimbali, ni mfariji, ni kiongozi kwa awaye yote anayemtegemea
atakuonyesha yakupasayo kufanya na kukupa mbinu unazozihitaji, kila mtu anahitaji, kuwa na maono, hekima,
ujasiri na kukabiliana na changamoto za aina mbalimbali unapotaka kulitumikia
shauri la Bwana au kutimiza kusudi lake duniani, utakuwa kwenye nafasi nzuri ya
kutimiza hilo kama utamruhusu Roho Mtakatifu akutie nguvu, unapojaribu kuongoza
bila Roho Mtakatifu utaanguka lakini ili uweze kufanikiwa tunamuhitaji Roho wa Mungu.
Matendo 11:22-24 “Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa
lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba, aende hata Antiokia. Naye,
alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote
waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo. Maana alikuwa mtu mwema amejaa Roho
Mtakatifu na imani; watu wengi wakaongezeka upande wa Bwana.”
6.
Mkemee
shetani na majeshi yake yote.
Katika maombi
yetu ni muhimu kukumbuka kuwa na maombi ya kufanya vita dhidi ya ibilisi,
kumshughulikia shetani na majeshi yake na maajenti wake wote ni wajibu pekee
tuliopewa na Mungu sio ombi ni amri ona, Mfumo wa kishetani uko katika
protokali za kijeshi, hivyo Ndivyo Mungu alivyowaumba, Mungu anaitwa Bwana wa
Majeshi, Yeye ndio Amiri Jeshi mkuu ana serikali na ana dola Mbinguni, Malaika
waliumbwa kama vyombo vya Dola, hii ikiwa ni pamoja na Malaika walioasi baadaye
yaani majeshi ya Pepo wabaya katika ulimwengu war oho, kwa msingi huo wao
husikiliza amri na mari haitolewi kama ombi inatolewa kwa mamlaka kwa kuamuru
kupitia mairi Jeshi mkuu wa Majeshi ya Bwana yaani Kristo ona Waefeso 6:10-13 “Hatimaye,
mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.Vaeni silaha zote
za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu
sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa
giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.Kwa sababu
hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na
mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.”
Kwa msingi huo
unaweza kugundua kuwa shetani na serikali zake wako katika mfumo wa kijeshi na
ndio maana Yesu aliamuru tumshughulikie alitupa amri sio ombi la kumshughulikia
shetani angalia mfumo wa lugha inayotumika
katika
Luka 10:17-19 “Ndipo
wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa
jina lako. Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.
Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui,
wala hakuna kitu kitakachowadhuru.”
Maandiko wakati
wote yanaonyesha lugha ya kupinga na kukemea linapokuja swala la maombi yetu
dhidi ya kushughulikia kazi za shetani, wakati wote maombi ya kimapambano dhidi
ya ibilisi ni kukemea ni kupigana vita ona
maagizo ya kimaandiko:-
2Wakoritho 10:3-5 “Maana
ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana
silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha
ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu
ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; tena tukiwa tayari
kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia”
1Petro 5: 8-9 “Mwe
na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye,
huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti
katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu
walioko duniani.”
Yakobo 4:7-8 “Basi
mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye
atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha
mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.”
Zekaria 3:2 “Bwana
akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua
Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni? ”
Yuda 1:9 “Lakini
Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya
mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na
akukemee.”
Kwa kuwa shetani
anataka kuwakandamiza watu wetu, sisi wenyewe,familia zetu na hata taifa letu
linapokuja swala la kumtaka aachie huwa ni amri kali, achiaa, toka, nakuamuru,
bwana na akukemee na kadhalika hakuna lugha laini wakati wa kumkemea shetani,
ni kumuamuru aachie haraka na taaachialia
7.
Vunja
madhabahu za uovu
Ni muhimu
kufahamu kuwa mawasiliano yote ya kiroho kati ya Mungu na wanadamu au miungu na
wanadamu hufanyika kupitia madhabahu, kwa msingi huo Mungu aliwaagiza wana wa
Israel watakapoingia katika inchi ya kanaani moja ya jambo muhimu wanalopaswa
kulifanya ni kuzivunja madhabahu zao agizo hili la kuharibu madhabau za uovu
limerudiwa tena na tena katika maandiko ona
Kutoka 34:12-13 “Ujihadhari nafsi yako, usije
ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako.
Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata
maashera yao” Unaona unaweza kuona tena Kumbukumbu la torati 7:1-7 “Bwana, Mungu
wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang'oa mataifa mengi
watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na
Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe; wakati
Bwana, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe
kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao;binti yako
usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake.Kwa kuwa
atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo
itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi. Lakini
watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni
maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga. Kwa maana wewe u
taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu
wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.”
Kwa nini Mungu
aliamuru Madhabau za mataifa yasiyomcha Mungu yaharibiwe? Hii ni kwa sababu
madhabahu ndio ni eneo la kutolea sadaka kwa miungu au kwa shetani ndio eneo la
mwasiliano kati ya miungu na wanadamu, kwa hiyo madhabahu ndizo zinaziotumika
kufanya mawasiliano ya kipepo na kufanya uchawi, kutengeneza hirizi, kupokea
maelekezo ya kipepo, kufanya uaguzi, kufanya utambuzi kwa ramli na mawasiliano yote kati ya miungu na wanadamu
hufanyika kupitia madhabahu, ni madhabahu ndio zinazotumika kuwafunga watu na
kuwaweka katika mahusiano ya kipepo na kusababisha mikandamizo, watu wanapotaka
kukutana na ulimwengu wa kiroho basi pale wanapokutania kwa ibada ndio maagano
ya kipepo yanapofanyika au mahusiano na mapepo ndipo yanapofanyika na ndipo
maisha ya watu wengi yanapoharibiwa
2Wafalme 3:26-27 “Naye
mfalme wa Moabu alipoona ya kwamba ameshindwa vitani, alitwaa pamoja naye watu
mia saba wenye kufuta panga ili wapenye hata kwa mfalme wa Edomu; wala
hawakudiriki. Ndipo akamtwaa mwanawe wa kwanza, yeye ambaye angetawala mahali
pake, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Kukawa hasira kuu juu ya
Israeli; basi wakatoka kwake, wakarudi kwenda nchi yao wenyewe.”
Balaamu
alipokodiwa kuja kuwalaani Israel utaweza kuona jambo la kwanza kulifanya ni kutengeneza
madhabahu unaweza kuona Hesabu 23:1-5 “Balaamu akamwambia Balaki, Nijengee hapa madhabahu saba,
ukaniandalie hapa ng'ombe waume saba, na kondoo waume saba.Balaki akafanya kama
Balaamu alivyonena. Balaki na Balaamu wakatoa sadaka, ng'ombe mume mmoja na
kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu. Balaamu akamwambia Balaki, Simama
karibu na sadaka yako, nami nitakwenda, labda Bwana atakuja kuonana nami; na lo
lote atakalonionyesha nitakuambia. Akaenda hata mahali peupe juu ya kilima.
Mungu akakutana na Balaamu; naye Balaamu akamwambia, Nimetengeneza madhabahu
saba, nami nimetoa sadaka ng'ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila
madhabahu. Bwana akatia neno katika kinywa chake Balaamu, akasema, Umrudie
Balaki; ukaseme maneno haya.”
Kabla ya Mungu
kumtumia Gideoni kama Mwamuzi wa Israel kwa uwezo wake Gideoni alipoisikia
msauti ya Mungu aliye hai aliamua kuivinja kwanza Madhabahu ya baba yake ona Waamuzi 6:24-32 “Ndipo
Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu;
hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri. Ikawa usiku uo huo Bwana
akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba,
ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo
karibu nayo; ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa
taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya
kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata. Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi
miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama Bwana alivyomwambia; lakini ikawa
kwa sababu aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na watu wa mji, hakuweza
kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku. Hata watu wa mji walipoondoka
asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera
iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya
ile madhabahu iliyojengwa. Wakaambiana, Ni nani aliyetenda jambo hili? Hata
walipotafuta habari na kuuliza, wakasema, Gideoni, mwana wa Yoashi, ndiye
aliyetenda jambo hili. Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi Mlete mwanao, afe;
kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali na kwa sababu ameikata ile Ashera
iliyokuwa karibu nayo. Yoashi akawaambia watu wote waliokuwa wakishindana naye,
Je! Mtamtetea Baali? Au mtamwokoa ninyi? Yeye atakayemtetea na auawe hivi
asubuhi; kama yeye ni Mungu, na ajitetee nafsi yake, kwa sababu mtu mmoja
ameibomoa madhabahu yake. Basi akamwita
Yerubaali siku hiyo, akisema, Baali na atete naye kwa ajili ya nafsi yake, kwa
sababu ameibomoa madhabahu yake.”
Unaona kwa
sababu hiyo ni lazima tunapotaka ukombozi kutoka katika maeneo mbalimbali ya
maisha yetu hatuna budi kuharibu kila njia za mawasiliano ya kishetani kwani
hizo ndio madhabahu zenyewe, haribu, hirizi, pembe au vyungu, vimbo au vifaa
vyote vya kiroho ambavyo umepewa na waganga au ambavyo vimezindikwa nyumbani
kwenu, kumbuka kuwa Madhabahu ndio njia ya mawasiliano, na ikiwa madhabahu hiyo
sio ya kiungu, basi itapingana na sheria za kiungu, za Mungu aliye hai,
madhabahu ya miungu migeni itazuia neema ya Mungu wetu kwetu, itaweka mipaka ya
utendaji wa kiungu kwetu, itafungua milango ya roho chafu, itasababisha
matatizo yasiyoweza kupata ufumbuzi, itachelewesha sana upatikananaji wa Baraka
zako, itasababisha matatizo yasiyoisha, inaweza kushababisha talaka, umasikini,
kurudi nyuma, utasa, vifo, aibu na mambo
ya ajabu ajabu, madhabahu zina uwezo wa kusababisha laana au Baraka, Madhabahu
ni ukumbusho kwa wale walioziinua, ili uweze kupata upenyo katika maisha yako
ni lazima uziharibu madhabahu zisizo rasmi na makuhani wake, Madhabahu hugeuka
na kuwa njia (Malango) ya kuvutia viumbe wa kiroho kufanya utembeleo aidha awe
Mungu au miungu yaani mapepo
Mathayo 16:18 . “Nami
nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu;
wala milango ya kuzimu haitalishinda.”
Mwanzo 28:11-19 “Akafika
mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa
jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale
pale.Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake
yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake.
Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu
baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na
uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na
mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa
zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila
uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata
nitakapokufanyia hayo niliyokuambia. Yakobo akaamka katika usingizi wake,
akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Naye akaogopa
akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu,
napo ndipo lango la mbinguni. Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa
lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na
kumimina mafuta juu yake. Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la
mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.”
Unaona kwa
msingi huo hatuna budi kuhakikisha kuwa tunaharibu kila aina ya madhabahu ambayo
iko kinyume na Mungu wetu ili kuzuia sisi kuwa chini ya utumwa wa miungu
mingine kama haya yakifanyika vema basi Ibilisi atatii na kukuacha uende,
waachie watu wangu waende, Wakati
wote unapotaka Mungu awe pamoja nawe na kukukomboa unapotaka mpenyo katika
maisha yako na unapotaka Mungu atembee nawe ni lazima kuhakikisha kuwa njia
zote za mawasiliano na miungu migeni zinahabiwa na kutupwa mbali ili Mungu
atembee katikati yako na familia yako haribu miungu migeni iondoe katika nyumba
yako ichome moto ifukie baki na Mungu akiye hai na uwepo wa Mungu utakuwa
pamoja nawe na hakuna wa kukuonea utaogopwa kila utakakopita
Waefeso 19:19 “Na
watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao,
wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya
kwamba yapata fedha hamsini elfu.”
Mwanzo 35:1-5 “Mungu
akamwambia Yakobo, Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie Mungu
madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau, ndugu yako. Yakobo
akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni
miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu.Tuondoke, tupande
kwenda Betheli, nami nitamfanyia Mungu madhabahu huko; yeye aliyenisikia siku
ya shida yangu, akawa pamoja nami katika njia yote niliyoiendea. Nao wakampa
Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na pete zilizokuwa masikioni
mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu. Wakashika njia,
hofu ya Mungu ikaishika miji iliyowazunguka, wala hawakuwafuata wana wa Yakobo.”
Imani yangu ni
kuwa somo hili ukilifanyia kazi na kuweka yote niliyokufundisha kivitendo
utashangaa kwa miujiza ya ajabu na mpenyo wa ajabu utakaoambatana na maisha
yako kuanzia leo namuomba Mungu kwamba uongezewe neema unapoadhimisha siri za
ukombozi wako kupitia somo hili katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth Mwana wa Mungu aliye hai amen.
Na Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni