Matthayo 7:6 “Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.”
Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kuwa hapa Yesu
anatumia lugha ya mfano (mficho) iitwayo Metaphor ambapo neno au maneno
yanayotumika katika hali ya kawaida yanaweza kumaanisha matumizi, ya kitu au jambo lingine au linalofanana na
hilo, Yesu anawatumia umbwa na nguruwe hapa akiwaonya wanafunzi wake kuwa na
ufahamu na kuelewa unyeti wa kuwapa vitu vya thamani watu wasio na shukrani,
Wanyama kama mbwa na nguruwe hawawezi kufurahia uadilifu, wala kushukuru kwa
sababu hawajui thamani ya kile wanachofanyiwa
2Petro 2:20-22 “Kwa maana wale waliokwisha
kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama
wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya
kwanza. Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko
kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa. Lakini imetukia kwao
sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na
nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.”
Hali kadhalika wako wanadamu,
ambao kwa namna moja ama nyingine, sio waadilifu, hawana moyo safi, wenye nia
ovu, waliokataa kuwa na Mungu nafsini mwao hawawezi kwa namna yoyote ile kukubaliana na maelekezo mema yanayotolewa
kuhusu injili aidha pia mwisho wa kila kitu wanaweza kuwadhuru hata wale
wanaoihubiri injili, kwa ujumla ujumbe
unahusu wale ambao hawawezi kukubali habari njema lakini sio tu kuikubali
hatimaye kuwakataa wanaoihubiri. Au hata anayehubiriwa !
Kwa muda Mrefu sana wayahudi
walikuwa wakimsubiri Masihi aliyeahidiwa kama mkombozi wao, na zaidi ya yote
walikuwa wamechoshwa na hali ya kuwa watumwa wa mataifa mengine na walikuwa
wkiutazamia uhuru wa kweli chini ya serikali ya kweli ambayo ingeongozwa na
Masihi yaani ufalme wa Mung, Yesu alikuja akiwa anahubiri habari hizo na
kuwathibitia shia kuwa ufalme wa Mungu umekaribia ona Mathayo 4:17 “Tokea wakati huo Yesu alianza
kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.”
Wale waliomuamini na kumkubali walikuwa tayari kuwashirikisha na wengine habari
hii njema, lakini hata hivyo wengi hawakuiamini, badala yake walimuona kuwa
mzushi na mtu ambaye anakufuru
Mark 14:61-65 “Lakini akanyamaza, wala
hakujibu neno. Kuhani Mkuu akamwuliza tena, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo,
Mwana wake Mtukufu? Yesu akasema, Mimi ndiye, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu
ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija na mawingu ya mbinguni. Kuhani Mkuu
akararua nguo zake, akisema, Tuna haja gani tena ya mashahidi? Mmesikia kufuru yake;
mwaonaje ninyi? Wote wakamhukumu kuwa imempasa kuuawa. Wengine wakaanza
kumtemea mate, wakamfunika uso, na kumpiga makonde, na kumwambia, tabiri. Hata
watumishi nao wakampiga makofi.”
Yesu aliyasema haya mapema akiwa
anaelewa kuwa ni watu wa namna gani wanamzunguka nan i mambo gani yatawatokea,
watu wanaolihubiri neno la Mungu hawapendwi, ni vigumu kuwakubali watu
wanaosema kweli, wanaoongoza wengi katika njia ya haki, hivyo japokuwa
wanaifanya kazi iliyo njema lakini matokeo yake ni kuwa watalipwa mabaya
Yohana 16:1-4 “Maneno hayo nimewaambia,
msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila
mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu
hawakumjua Baba wala mimi. Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile
itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo,
kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi.”
Kazi kubwa ya injili pamoja na
mafanikio yake yote ni kuwapa watu uzima wa milele Yohana 10:28 Nami nawapa
uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya
katika mkono wangu. Zawadi hii inatolewa
kwa kuitangaza injili, lakini ni katika namna ya kushangaza sana wahubiri wa
injili mara kadhaa wameonekana kama kitu cha kukataliwa kutupwa na kufanywa kuwa
takataka za dunia, kusema vibaya kama watu waliotolewa wahukumiwe kuuawa ona
1Wakorintho 4:9-13 “Maana nadhani ya kuwa
Mungu ametutoa sisi mitume mwisho, kama watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu
tumekuwa tamasha kwa dunia; kwa malaika na wanadamu. Sisi tu wapumbavu kwa
ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye akili katika Kristo; sisi tu dhaifu,
lakini ninyi mna nguvu; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima. Hata
saa hii ya sasa, tuna njaa na kiu, tu uchi, twapigwa ngumi, tena hatuna makao; kisha
twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki,
tukiudhiwa twastahimili; tukisingiziwa twasihi; tumefanywa kama takataka za
dunia, na tama ya vitu vyote hata sasa.”
Katika tamaduni za kiyahudi Umbwa
na Nguruwe ni alama ya wanyama wachafu na Najisi sawa na wanavyotamkwa katika
maandiko Walawi 11:7-8 “Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu
iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu. Msiile nyama yao, wala
msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu” wanyama hawa wanakula
chochote kile na ni wakali hasa wanapojisikia njaa, wanapotumika kama mfano
katika mithali kuwawakilisha wanadamu, au watu wachafu, baradhuli, wasio na
uadilifu, na wapuuzi, ni ukweli ulio
wazi kuwa ni udhalilishaji wa hali ya juu sana mtu akikutukana au kukuita Mbwa
au nguruwe! Hususani katika jamii ya kiyahudi, lakini hata hivyo Yesu hasiti
kufananisha mtu, umbwa na Nguruwe, akiwalinganisha na watu waliomkataa masihi,
kusudi lake sio kuwadhalilisha, lakini mkazo wake sio watu wengine lakini wale
wanaodhaniwa kuwa watu wa Mungu na kisha wanakataa karama za Mungu, na mwito
wake, Hivyo Yesu anaonya kuwa usipoteze Muda na watu wanaojiita Ndugu lakini
hawayahsiki mafundisho nan i wakristo wa uongo
1Wakoritho 5:11-12 “Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia
kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani
au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii
msikubali hata kula naye.Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi
hamwahukumu hao walio ndani? ”
Neno la Mungu limeagiza kuendelea
kuihubiri injili na hivyo lazima tutakutana na watu mbalimbali katika kuihubiri
injili 1Petro 3:15 “Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari
za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.” Kwa
hiyo hatupaswi kuogopa kuwahubiria watu habari njema, lakini wakati mwingine
hatuna budi kuwa makini kwamba wako mbwa na nguruwe ambao kile unachokitoa
kwao, hakitazaa matunda yanayokusudiwa na badala yake watakurarua kwa sababu
hawaijui thamani ya neno la Mungu, wala hawajui thamani ya Yesu unayemuhubiri
na hivyo hawawezi kukukubali wewe unayebeba mambo yale ya thamani, hii haimaanishi tuwachukie wasioamini
au wale wanaoipinga injili lakini kuwa makini na kutambua kuwa tutakataliwa, na
tusipoteze muda na watu wasioona umuhimu wa injili, zawadi za Mungu na kuwekeza
muda wetu kwa wapinzani wa injili ambao wanaelekea shimoni na wakiishikia
injili au mafundisho wanachukizwa
Mathayo 15:12-14 “Ndipo wanafunzi wake
walipomwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile
walichukizwa? Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni
litang'olewa. Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza
kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.”
Wale ambao wataipinga injili na
mafundisho yetu simple rahisi tu Yesu aliagiza kuwa sio tu tuwache lakini
vilevile tukung’ute mavumbi ya miguuni mwetu
Mathayo 10:14-15 “Na mtu asipowakaribisha
wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule,
kung'uteni mavumbi ya miguuni mwenu. Amin, nawaambia, itakuwa rahisi nchi ya
Sodoma na Gomora kustahimili adhabu ya siku ya hukumu, kuliko mji ule.”
Hata hivyo wahubiri wa injili
hawapaswi kukata tamaa, na wanapaswa kuendelea kuihubiri injili, kwani sio watu
wote wataipinga injili wako wale wanaomcha Mungu ambao Bwana atafungua mioyo
yao ili wayatunze yale tunayoyahubiri;-
Matendo 16:13-15 “Hata siku ya sabato tukatoka
nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa
kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. Mwanamke mmoja, jina
lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu,
akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno
yaliyonenwa na Paulo.Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake,
akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu
mkakae. Akatushurutisha.”
Aidha ikumbukwe kuwa wakati wote
mlango mmoja wa kuihubiri injli ukifungwa Mungu atafungua mlango mwingine,
kwani wako watu wenye kiu ya neno la Mungu ambao Mungu amewaandaa kuipokea
injili na habari njema za Yesu Kristo bila kikwazo japo changamoto zitaendelea
kuwepo ona Matendo 16:6-10 “Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na
Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia. Walipofika kukabili Misia
wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa, wakapita Misia
wakatelemkia Troa. Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia
amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie.Basi
alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa
tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.”
Aidha wahudumu wa injili
wanapaswa kutambua kuwa sio kila wakati watakutana na changamoto kwani iko miji
Mingine ambako Mungu ana wau wake na usalama kwaajili yetu upo Matendo 18:9-10 “Bwana
akamwambia Paulo kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze, kwa
kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa
maana mimi nina watu wengi katika mji huu.”
Ni maombi yangu kuwa Mungu anipe
watu, watakaofunguliwa na Bwana wayatunze ninayoyahubiri na kuyafundisha badala
ya kuturarua, Aidha Roho Mtakatifu aendelee kufungua milango ya injili kwa wale
wenye uhitaji wa kusaidiwa na Mungu atupe kukaa kwa amani pale ambako ana watu
wengi na utisho wake utufunike ili maadui wa injili na ndugu za uongo wasigeuka
na kutusumbua, tuendelee kulinena neno la Mungu kwa ujasiri tukijua wazi kuwa
Yesu yuko Pamoja nasi, lakini tusiache kuwang’utia mavumbi wale wanaoikataa
injili ili Mungu awaletee hukumu kwa haraka, kama yanenavyo maandiko! Awaye
yote atakayejaribu kukupinga kwa sababu yu waihubiri injili Mungu akakutane
naye, Bwana akulinde na Mbwa na Nguruwe wasioelewa utathamani wa kile
ulichikibeba katika jina la Yesu!
Na. Rev. Innocent Samuel Kamote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni