Wagalatia 4:28-31 “Basi, ndugu zangu, kama
Isaka sisi tu watoto wa ahadi. Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa
mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa. Lakini
lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi
hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. Ndiposa, ndugu zangu, sisi si
watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye mwungwana.”
Utangulizi:
Ni muhimu kuelewa kuwa Paulo
Mtume alikuwa anakamilisha Mafundisho yake kwa Kanisa lililokuwako Galatia
ambao walikuwa wamekumbana na kadhia ya Mateso pamoja na Mafundisho mabaya ya Jamii ya
wayahudi waliokuwa waanaamini katika sheria ya Musa na hata baada ya Injili
kuhubiriwa wao waliwataka wakristo waendelee kuwa chini ya sheria ya Musa
badala ya kuutumia uhuru wao waliokuwa nao katika kristo, Katika kuhitimisha
mafundisho yake anaonyesha kuwa kuna wana wa Muungwana na wana wa Mjakazi. Na anajaribu kuonyesha tofauti zao watoto hao
kwamba Mwana wa Mjakazi alizaliwa kwa mapenzi ya Mwili na yule wa Muungwana alizaliwa kwa kusubiri Ahadi ya
Mungu, sawa tu na tukio la kuzaliwa kwa Ishmael na baadaye Isaka, Ishmael
Alizaliwa kwa mapenzi ya mwili wakati Isaka alizaliwa kutokana na ahadi ya
Mungu ona
Mwanzo
16:1-4 “Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana,
naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri. Sarai akamwambia Abramu,
Basi sasa, BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda
nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai. Sarai mkewe Abramu
akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya
Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe. Basi akamwingilia Hajiri,
naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni
machoni pake.” Kwa hiyo
tunaweza kuona mtoto wa Kwanza wa Abraham anazaliwa kutokana na jitihada za
kibinadamu yaani kwa mapenzi ya mwili na kwa mwanamke aliyekuwa mtumwa (Kijakazi) Na mtoto wa pili alizaliwa kwa uvumilivu na
subira kwa kusubiri ahadi ya Mungu na kupitia mwanamke aliyekuwa mtawala (Huru) Mwanzo 21:1-4 “BWANA akamjia Sara kama
alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema. Sara akapata mimba akamzalia
Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu.
Ibrahimu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara
alimzalia. Ibrahimu akamtahiri Isaka mwanawe, alipokuwa mwenye siku nane, kama
Mungu alivyomwamuru.”
Hawa wote ni watoto wa Ibrahimu,
mmoja alizaliwa kutokana na mawazo na mipango ya kibinadamu na mwingine alizaliwa
kwa kusubiria ahadi ya Mungu, Paulo anajaribu kuunganisha swala hili na hali
halisi waliyokuwa wanaipitia Makanisa ya Galatia, taabu kubwa waliyokuwa
wanaipitia ni Mateso pamoja na Mafundisho potofu ya wayahudi yanayowataka waishike
sheria ya Musa huku wakiwa wamemuamini Yesu Kristo ambaye tayari alikuwa
amekwisha kuwaokoa na laana ya torati, Kitendo cha aalimu hawa wa kiyahudii
kulisumbua kanisa alikifananisha na Ishamael kumdhihaki Isaka, Ishmael akiwa ni
mtoto wa mjakazi na Isaka akiwa ni mtoto wa Muungwana, dhihaka hii haikuweza
kuvumilika kiasi ambacho Sara alitoa wazo la mjakazi na mtoto wake kufukuzwa
kabisa kwani wangemuharibu kabisa Isaka kutokana
na ushawishi wao wa kifisadi
Mwanzo 21:8-12 “Mtoto akakua, akaachishwa
kunyonya; Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.
Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya
dhihaka. Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana
mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka. Na neno hilo lilikuwa
baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe. Mungu akamwambia Ibrahimu,
Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi
wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako
utaitwa.”
Unaweza kuwa na swali moyoni
ambalo hata mimi nilikuwa nalo, kwamba ni aina gani ya dhihaka ilikuwa
inafanyika tena siku ya sherehe hata kumuuzi Sara na kuamuru kuwa mtoto huyo
afukuzwe pamoja na mama yake? Kwa mujibu
wa Marabi wa kiyahudi ni kuwa kijana huyu alikuwa na miaka kama 14 hivi na
tayari alikuwa ameshaonyesha kutokuishi sawa na njia ya baba yake, na kwamba
kulikuweko na dalili nyingi za kukiuka sheria za Mungu ambazo hata Abrahamu
alikuwa anazishika, Sara alikuwa amebaini hilo kwa uwazi kuliko Abrahamu, Sara
aliona kuwa kuna hatari mtoto wa ahadi akasawishika kufuata njia za kaka yake
ambaye kwa siri wayahudi wanaeleza kuwa alikuwa akionekana anaabudu miungu ya
mama yake na kushindana na kijana mdogo wa Ibrahimu. Neno dhihaka kwa waebrania linasomeka kama TSACHAQ kufanya dhihaka
katika mambo muhimu na ya msingi, neno hili pia huumika kumaanisha watu
wasiomcha Mungu au wenye kupuuzia njia za Mungu. Unaweza kuliona katika zaburi
na maandiko mengine ya kiyahudi;-
Zaburi 1:1-2 “Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala
hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na
sheria yake huitafakari mchana na usiku.”
Wakati Abraham na watu wake
wanafanya karamu ya kumshukuru Mungu Ishamel yeye alikuwa anadhihaki kwa msingi
huo kama tungekuwepo kwenye tafrija ile tungebaini kuwa watu wako makini katika
kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyomfanyia Sara na Abraham na kundi la Hajiri
na mwanaye wanapuuzia na kucheka au kuona
kinachofanyika ni upuuzi tu na hawajali kile Mungu alichokifanya wala hawaoni
kuwa ni jambo kubwa. Sara aliona hilo na kubaini kuwa kijana
huyu na mama yake hawana budi kutimuliwa kwani hawangeweza kuishi pamoja, wala
kurithi pamoja na Isaka Mwanzo 21:10 “Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na
mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.”
Paulo anautumia mfano huo sasa
kulifundisha kanisa kuhusu mateso yanayofanywa na wale wanaolitesa kanisa kwa Mateso
na mafundisho yasiyo sahihi ambayo yanalitesa Kanisa Kama Ishamel alivyokuwa
akimdhihaki Isaka waalimu wa uongo walikuwa wakilitesa kanisa kwa kufundisha
kuwa watu wanaweza kukubaliwa na Mungu kwa sababu ya bidii ya mwilini, wakati
kuzaliwa kwa Isaka kulitokana na Mungu kuitimiza ahadi yake na sio juhudi za
kibinadamu, Jamii kubwa ya wayahudi hata pamoja na kuiamini injili waligeuka
kubwa mwiba mkubwa wa mateso katika kanisa na mafundisho yasiyo sahihi aidha wakati wote walihakikisha kuwa
wanapingana na injili na kuwaudhi wahubiri wa injili ona
Matendo 13:48-51 “Mataifa waliposikia hayo
wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa
milele wakaamini. Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote. Lakini Wayahudi
wakawafitinisha wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha
watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao. Nao
wakawakung'utia mavumbi ya miguu yao, wakaenda Ikonio.”
Matendo 17:5-9 “Na Wayahudi wakaona wivu,
wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema, nao
wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya
Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji; na walipowakosa, wakamkokota
Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema,
Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako, na Yasoni amewakaribisha;
na hawa wote wanatenda mambo yaliyo kinyume cha amri za Kaisari, wakisema na
kwamba yupo mfalme mwingine, aitwaye Yesu. Wakafadhaisha ule mkutano na wakubwa
wa mji walipoyasikia hayo. Nao walipokwisha kumtoza dhamana Yasoni na wenziwe
wakawaacha waende zao.”
Matendo 17: 13 “Lakini Wayahudi wa
Thesalonike walipopata habari ya kwamba neno la Mungu linahubiriwa na Paulo
hata katika Beroya, wakaenda huko nako wakawachafua na kuwafadhaisha makutano.”
Unaweza kuona kuwa kanisa sio tu
lilikuwa linapitia mateso ya kawaida na upinzani dhidi ya injili lakini pia
lilipingwa kwa mafundisho yasiyo sahihi Na kanisa la Galatia lilikuwa ni moja
ya kanisa lililoathiriwa na mafundishi hayo
Wagalatia 3:1-9 “Enyi Wagalatia msio na
akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya
macho yenu ya kuwa amesulibiwa? Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je!
Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Je!
Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa
sasa katika mwili? Mmepatikana na mateso makubwa namna hii bure? Ikiwa ni bure
kweli. Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo
kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Kama vile Ibrahimu
alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki. Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa
imani, hao ndio wana wa Ibrahimu. Na andiko,
kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa
imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa
yote watabarikiwa. Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu
aliyekuwa mwenye imani”
Wakristo ni watoto wa Mungu kwa
njia imani na ahadi inayotenda kazi
kupitia uwezo wa Roho Mtakatifu, na kwamba tunapokea wokovu kwa neema na si kwa
juhudi wala kwa matendo ili awaye yote asijisifu:-
Waefeso 2:4-9 “Lakini Mungu, kwa kuwa ni
mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule
tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani,
tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika
ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; ili katika zamani zinazokuja
audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika
Kristo Yesu. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo
haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye
yote asije akajisifu.”
Katika imani ye Kikristo tunapata
kila tunachokipata kwa neema na sio kwa matendo au bidii za kibinadamu hii iko
katika kaisha ya kawaida na katika maisha ya wito wa kumtumikia Mungu hakuna
juhudi wala matakwa ya kibinadamu bali ya Mungu
Warumi 9:14-15 “Maana amwambia Musa,
Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. Basi, kama ni
hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule
arehemuye, yaani, Mungu.”
Hata Mungu anapoita watu katika
utumishi huu anawaita watu kwa neema yake na sio kwa kujipendekeza au kwa
kujidhani ya kuwa ninafaa, wako watu wanaweza kujidhania kuwa wanafaa kuwa
watumishi wa Mungu na wengine hawafai, au mtu akajikinai akifikiri yeye ni
zaidi ya mwingine jambo la namna hii pia liko kinyume na ile dhana ya kiungu,
Mungunhuchagua vile tunavyovidhania kuwa havifai, kumbuka lililotyukuka kwa
mwanadamu ni chukizo kwa Mungu!
1Wakoritho 1:26-29 “Maana, ndugu zangu,
angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi
wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo
mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu
vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya
dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile
vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.”
Tunawezaje kujua kuwa hawa ni
wana wa Muungwana na hawa ni wana wa kijakazi? Maandiko yanaeleza wazi kuwa
wana wa muungwana walizaliwa kwa ahadi na wana wa kijakazi walizaliwa kwa
mapenzi ya mwili na hivyo tunaweza kuwatambua kwa matendo yao, wale waliokuwa
wakiliudhi kanisa na kulitesa ndio wana wa kijakazi na wale waliowapole na
waungwana Paulo ana sema
Wagalatia 4:29 “Lakini kama vile siku zile
yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo
ilivyo na sasa ”
Wana wa kijakzi ni wale
waliozaliwa kwa mwili na wana wa muungwana ni wale waliozaliwa kwa ahadi na
uweza wa Roho Mtakatifu na matunda yao unaweza unaweza kuwatambua
Wagalatia 5:19-21 “Basi matendo ya mwili ni
dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi,
uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na
mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha
kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa
Mungu.”
Wagalatia 5:22-24 “Lakini tunda la Roho ni
upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi;
juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu
wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake”
-
Wana wa
mjakazi hawashindwi kuua mtu, mioyo yao
imejawa na chuki na uchungu ni wakatili na hawana huruma ona Mwanzo 4:1-11 “Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa
Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa BWANA. Akaongeza akamzaa ndugu
yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi,
sadaka kwa BWANA. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu
zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake; bali Kaini
hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake
ukakunjamana. BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso
wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema
dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa
uishinde. Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo
uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua. BWANA akamwambia Kaini,
Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika
ardhi. Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee
damu ya ndugu yako kwa mkono wako; utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake;
utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.”
-
Hawaishi
kuwa na Makundi wala Mafarakano
1Wakoritho 3:1-9 “Lakini, ndugu zangu, mimi
sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu
wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa
sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi,kwa
maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna
husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa
jinsi ya kibinadamu? Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na
mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu?Basi Apolo ni nani? Na Paulo
ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi
nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si
kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. Basi yeye apandaye, na yeye atiaye
maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu
yake mwenyewe.Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la
Mungu, ni jengo la Mungu.”
-
Wanaweza
kupelekana hata mahakamani wala
kudhulumiana 1Wakorintho 6:1-10 “ Je! Mtu wa kwenu
akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si
mbele ya watakatifu?Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na
ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo
ndogo? Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha
haya? Basi, mkiwa na mahali panapohukumiwa mambo ya maisha haya, mwawaweka kuwa
waamuzi hao waliohesabiwa kuwa si kitu; katika kanisa? Nasema hayo nipate
kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima,
awezaye kukata maneno ya ndugu zake? Bali mwashitakiana, ndugu kwa ndugu, tena
mbele yao wasioamini. Basi
imekuwa upungufu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si
afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang'anywa mali zenu? Bali kinyume
cha hayo ninyi wenyewe mwadhulumu watu na kunyang'anya mali zao; naam, hata za ndugu
zenu. Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike;
waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi,
wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala
watukanaji, wala wanyang'anyi.”
Unapoangalia kwa kina na upana na
urefu, watu wenye matendo haya ya mwilini wanaweza kuwapo hata makanisani
katika siku za leo, na wanaweza kuwa na
muda mrefu sana katika wokovu au hata kufikia ngazi Fulani ya kiroho lakini
maandiko yanasema mtawatambua kwa matunda yao, kuwajua wana wa muungwa na wana
wa kijakazi kwa mujibu wa maandiko ni rahisi sana kila mmoja anapaswa kujihoji
na kujichunguza kama ni mwana wa Muuungwana au ni mwana wa kijakazi na kama ni
wa kijakazi au kuna tabia ya kijakazi hatuna budi kutubu na kubadilika ,
tuongeweze neema
Na Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni