Somo la sita.
Vijana na Hatari ya mapenzi (Ngono)
Somo hili linatahadharisha tu hatari itokanayo
na ngono au mapenzi, Hakuna jambo zuri kama mapenzi hapa duniani lakini pia
hakuna jambo la hatari duniani kama mapenzi hivyo ni muhimu kuwa tahadharisha
vijana kuhusiana na mapenzi.tutajifunza somo hili kwa kuzingatia maeneo matatu
hivi yafuatayo;
- Tahadhari
ya kufanya mapenzi kabla ya ndoa.
- Madhara
ya kujichua Punyeto.
- Athari za
kuangalia Picha za Ngono.
Tahadhari ya Kufanya mapenzi
kabla ya ndoa.
Kama tulivyoona katika masomo yaliyopita
Biblia ikitahadharisha kutokuyachochea mapenzi kabla ya wakati wake (Wimbo uliobora 3;5). Biblia inakataza
na kukemea vikali maswala ya ukahaba ikiwa na maana ya mapenzi holela nje ya ndoa, huku inatia
moyo kufanya mapenzi ndani ya ndoa (Mithali
7;6-23,5;15-23) kwa msingi huo ni vema vijana wakijitunza na kusubiri
wakati, ujana ni kipindi cha mpito kutoka katika utoto kuelekea katika utu
uzima katika kipindi hiki vijana hupata
mabadiliko ya kimwili na kiakili na kimtazamo,wakati huu mwili na akili
hupevuka na ni kipindi kizuri cha kuweka msingi kwa maisha ya
baadae,kujihusisha na mapenzi wakati huu ni kujiwekea msingi mbaya wa maisha
na kuvuruga shughuli zako za kimaendeleo na mpango wa Mungu alioukusudia
kwako kwa vipi unaweza kujiharibia mtiririko wako wa kimasomo,kazi zako,Mimba
kabla ya wakati au maandalizi,majukumu kabla hujajitegemea,watoto wa
mitaani,magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi na ugumba au kifo,hivyo ukijitambua
kuwa wewe una umuhimu gani au una thamani gani katika maisha haya utajilinda
kujihusisha na ngono kabla ya wakati husika.
Hata hivyo kuna maono mbalimbali
kuhusiana na kushiriki katika ngono kabla ya ndoa na kushiriki ngono ukiwa
ndani ya ndoa kwa wanaounga mkono swala la kuoa au kuolewa ukiwa bikira wana
hoja kuwa bikira anakuwa hajui kile kinachoendelea huko na huko duniani hivyo
ni rahisi kutulia na kuridhika akiwa ndani ya ndoa maana hana ujuzi na wanaume
au wanawake wa nje ambao wanauwezo na
ujuzi tofautitofauti katika utendaji mapenzi.
Kundi jingine ni lile linalounga mkono
kuwa ni vizuri vijana wakiingia katika ndoa huku wakiwa na ujuzi kamili wa
tendo la ndoa kivitendo inadaiwa kuwa wenye ujuzi huu wanakuwa hawana usumbufu
ukilinganisha na wale wasiojua kitu, dhana hizi zote mbili zinaweza kuwa na
ukweli Fulani. Chukulia kuwa una mke uliyemuoa akiwa bikira au mume ambaye ni
bikira na hawana ujuzi wowote kuhusu kinachoendelea kule nje kwa kweli kabisa
jaribu lao kuu litakuwa ni udadisi wa kutaka kujua kinachoendelea upande wa
pili hasa watakapokuwa wakisikia habari mbalimbali za kimapenzi kutoka katika
vyanzo mbalimbali vya huko wasikojua hawa watasumbuka,Rafiki yangu mmoja
aliniuliza swali hili akitetea hoja ya kundi hili la Pili “Kamote hebu fikiria
kama umeoa mke bikira kasha akawa anatoka nje ya ndoa,au umeoa mke aliyekuwa
hana bikira kisha akatulia ndani ya nyumba bila kutoka nje ungechagua yupi?”Dhana
hii inatufundisha situ ubikira ni kitu kingine na uaminifu ni kitu kingine bali
pia inatuonyesha kuwa mwanamke aliyeonja kasha akapata mahali anapoweza
kutulizwa kiu yake barabara hawezi tena kuyatafuta huko nje lakini yule asiye
na ujuzi akijaribiwa na udadisi wake akagundua kuwa kuna jamaa wanaweza mchezo
kuliko jamaa yake kule ndani kuna uwezekano akaamua kuchonga mzinga, Tunaporudi
katika msimamo wa kibiblia tunaona ikiunga mkono sex after marriage yaani ngono
ndani ya ndoa na si vinginevyo.
Madhara
ya kujichua Punyeto.
Vijana wengi wa kike na wa kiume hupitia
tabia ya kupiga punyeto,Punyeto imethibitishwa kuwa haina madhara ya
kiafya,lakini ina madhara ya kisaikolojia na kidhamiri hasa unapokuwa
unalihusisha swala hili na mambo ya kiroho au kiimani basi dhamiri yako inaweza
kukushitaki na ukajihisi kuwa u mwenye dhambi na mwenye kushuka moyo,Tabia ya
kufanya punyeto ina miaka mingi sana duniani lakini Biblia iko kimya kuhusiana
na swala la kufanya punyeto,hata hivyo kama kiongozi wa kiroho nashauri kuwa
tabia hii si nzuri bila kuwahukumu wale wanaolifanya zoezi hili,Mimi mwenewe
nilifanya sana wakati wa umri Fulani wa ujana,(Efeso 4;17-19).Hii ni tabia tuliyojifunza darasani katika somo la
kawaida kama baiolojia tukitiwa moyo kuwa ni njia salama ya kimapenzi na
kupunguza msisimmko na tama za kimapenzi huenda nawe umewahi kusikia au
kujifunza tabia hizi,Katika utafiti uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwa
karibu asilimia 97% ya wanaume wamefanya punyeto na asilimia 87% wanawake
wamefanya punyeto,Muhubiri maarufu duniani amabye kwa sasa ni Marehemu Keneth
Heghine alikuwa akitetea swala zima la ufanyaji Punyeto hata hivyo tendo hili
linaweza kuwa si tatizo endapo anayefanya hatakuwa na picha ya mwanaume au
mwanamke katika mawazo yake afanyapo punyeto jambo ambalo linawezekana kufaulu
kwa asilimia 60% tu za vijana wenye nguvu ya kujidhibiti wasitamani lakini
zaidi ya hayo wengi hufanya tendo hili wakiwa na picha kichwani ya mwanmke au
mwanaume aliyempenda au kumtamani,na wengine hufanya hayao kama matokeo ya tama
endapo jambo hili litafanyika kama matokeo ya tama basi ni wazi kuwa swala hili
kibiblia ni dhambi Biblia inataka tuvitiishe viungo vyetu katika mwili ikiwemo
mawazo mabaya kumbuka kuwa kutamani ni dhambi kamili kama kutenda (Kolosai 3;5,warumi 1;26-27,Mathayo 5;27-28),utafiti
pia unaonyesha kuwa wengi wa waliofanya punyeto waliweza kufanya tendo kamili
la ngono pia.
Hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa punyeto huwa na madhara ya kisaikolojia,vifaa
vingi vinavyotumiwa na wafanya punyeto hasa wanawake vinawatengenezea mazingira
ya kutokutoshelezwa na wanaume zao wa kawaida,kwani vifaa hivi huwa katika hali
ya kusimama kwa Muda mrefu tofauti na uume ambao huwa unasinyaa,kwa sasa dunia
ilivyoendelea kuna vifaa vya kingono vya umeme au mkanda wenye uume bandia
unaoweza kuvaliwa na mwanamke na akafanya ngono na mwanamke mwenzake,au vifaa
vya plastiki wanavyoweza kuvitumia kujiridhisha kimapenzi wenyewe ukiachia njia
za kizamani za kutumia mimea kama karoti tunda kama ndizi,vigongo vya
kuchongesha n.k. Nchi ya Ufaransa ndiyo inayoongoza duniani kwa utengenezaji wa
vifaa bandia vya kujiridhisha kimapenzi na vina soko kubwa sana na inasemekana
hata wajane wengi sana huvitumia. Kwa kweli mwanamke kijana ambaye atakuwa
amejizoeza kujiridhisha kwa vifaa hivi bandia anapoolewa kunakuwa na uwezekano
akaathiriwa na vifaa hivyo na hivyo kuona kuwa haridhishwi na mwanaume wake.
Kwa upande wa pili yaani kwa wanaume pia kunaweza kuwepo na tabia endelevu ya
kujichua kwa kutumia utelezi utokanao na sabuni n.k kwakuwa wanatumia vidole
vya mkono basi msuguano wa mkono unakuwa mkali kuliko ule wa uchi wa kawaida wa
mwanamke kwa msingi huu basi anapooa uchi wa mkewe hautaweza kutosheleza hamu
yake ya kingono na hivyo kuna uwezekano wa kuendelea kwa tabia hiyo hata baada
ya kuoa kwa kuzingatia athari hizi za kimaumbile zinazoweza kujitokeza tunaweza
kuhitimisha kwa kusema kuwa tabia hii si nzuri na ni muhimu kujifunza kuiacha
kwani inapingana na maumbile ya utendaji uliokusudiwa na Muumba, Ili vijana
wajiepushe na tabia hii unaweza kujifunza kutokwenda kitandani mapema kwani
kutakupelekea kufikiri zaidi katika tama ya kufanya punyeto hivyo unapokwenda
kitandani ukiwa umechelewa utalala mapema bila kufikiri hayo,Unapokwewnda
bafuni hakikisha unaoga kwa haraka kama mtu mwenye haraka hivi,shiriki
michezo,Ibada na shughuli nyinginezo,maombi na kufunga n.k ili kujizoeza kutoka
katika hali hizi au anza kupunguza kidogokidogo idadi ya upigaji punyeto kwa
kila wiki au mwezi taratibu hadi sifuri Muombe mungu akuwezeshe kwani
yasiyowezekana kwa wanadamu kwake Yanawezekana.
Athari
za kuangalia picha za ngono
“Mimi ni mtaalamu niliyefanikiwa sana na ni
meneja katika kampuni kubwa isiyo ya kiserekali au iliyobinafsishwa,Nimekuwa
muathirika wa kuangalia picha za ngono kwa zaidi ya miaka 40,sikuzaliwa nikiwa
na tabia hii lakini nilijikitakatika mkumbo tu wa kuziangalia nikiwa na miaka
tisa” ni moja ya shuhuda za mtazamaji wa picha za ngono akishuhudia.Hili ni
tatizo kubwa sana duniani vijana wakubwa kwa wadogo mpaka wabunge na mawaziri
na watu ambao tunaweza kuwapa heshima kubwa sana wakiwemo viongozi wa dini na
hata maaskofu wsamenaswa na picha,mikanda ya video,cd,vcd,dvd,vijarida na story
zilizoandikwa zenye kusisimua sana swala zima lihusulo ngono,Picha hizi za
ngono zina nguvu,zina mvuto zinagusa hisia na akili na zinapenya katika ubongo
wa mwanadamu kuliko hata tabia uliyozaliwa nayo,Nyingine hatuwezi kuziepuka
kwani waandaaji wa matangazo ya bidhaa mbalimbali hutumia wanawake wazuri wenye mvuto wa
kingono wanapotangaza bidhaa zao,wanamuziki wengi huimba nao mivao yao n.k
vinaweza kabisa kufanya usalama wetu kuwa mdogo.
Biashara ya picha za kingono inapesa sana
duniani kuliko biashara yoyote ile hivyo wengi huzitengeneza makusudi kwani
wanataka pesa huko marekani picha za kingono hutengeneaza mapato ya Dollar
billion nane kwa mwaka na hiyo ni takwimu ya mwaka 1985, Picha za kingono
zimeathiri watu wengi sana na kuharibu mitazamo yao angalia ushuhuda huu,;-
“Nilipofikia umri wa miaka 22 hivi nilianza
kuhisi matatizo ya tabia yangu mbaya niliyokuwa nayo,kuna wakati nilishindwa
kufikiri kitu kingine chochote bali mawazo yangu yalijaa picha za kujisisimua
kingono kwa miaka mitatu tu nilikuwa na mikanda,magazeti na vitabu zaidi ya
200”
“Kujiingiza katika utazamaji picha za ngono
ni utumwa wenye kutisha sana ambao mwanadamu hapaswi kuishi nao kwa mtu wa
kiwango chochote kile awe dereva au waziri nahisi kuna mamia ya watu kama mimi
ambao wako kwenye kifungo nilichonacho tena ni wanawake kwa wanaume na idadi
yao inaongezeka”
“Sikuamini kama wanaume kwa wanawake
wanaoangalia picha za ngono kwa muda
mrefu na kutegemea kuwa wanaweza kuwa na uhusiano na wapenzi wengine……Leo
nikiwa na miaka ya arobaini na nane hivi nikiwa na watoto wane….Ninasumbuliwa
kila siku na mawazo na picha na tamaa ya picha za kingono nilizoangalia miaka
hiyo…mawazo haya yanaharibu kabisa uhusiano wangu na mke wangu,na kila mwanamke
ninae mwona hata wale wa kanisani na hata binti zangu nawatamani nafikiri hili
linachangia sana katika uharibifu wa ndoa nyingi na kupelekea kuweko kwa talaka
katika siku za leo”
“Niliangalia picha za ngono kwa zaidi ya
miaka 30 zimeharibu ndoa yangu….Kwakweli zimeniibia penzi langu la kweli na
kuharibu uhusiano na vimeathiri hata watoto wetu ingawa hakujua kuwa
tumeathiriwa na picha za ngono na walishituka tulipotangaza kuwa tunapeana
talaka tulipendana sana lakini sasa najua kuwa picha za ngono zimeharibu ndoa
yangu alisema mama mmoja aliyeachika”
Hizo ni baadhi ya shuhuda ya watu
wanaotibiwa ili kupona katika tatizo la uangaliaji wa picha za ngono na athari
zake kwa kweli zina madhara makubwa na sasa madhara haya yanalikabili bara la
Afrika na inchi yetu ya Tanzania utafiti unaonyesha kuwa hata viongozi wakubwa
wa kidini wamejihusisha kwa namna moja au nyingine katika uangaliaji wa picha
za kingono na kwa sababu hii kumekuwa na maoni yanayotolewa katika kuzitetea au
kuzipinga maoni ya wanaoziona kuwa zinafaa ni kama ifuatavyo;-
Zinachochea nyege na kuongeza hamu ya
kufanya tendo la Ndoa, Zinaongeza nguvu, Zinafurahisha na kukufanya ulipende
tendo la ndoa,Zina sisimua sana,Zinaongeza ujuzi,zinasaidia katika maandalizi
ya kukutana kimwili haya ni baaadhi tu ya maoni ya wenye kutetea picha za
kingono Hebu sasa tuangalie maoni ya wale wenye kuziona kuwa zina Athari
Kwa upande wa wale wenye kuona kuwa zina
athari wao huwa na maoni yafuatayo;-
Zinaharibu mahusiano ya kinyumba,zinaharibu
dhamiri hasa ya Mtu aliyeokoka,zinakufanya uone ni halali kuendelea kuziangalia,zinachochea
kutafuta kutoshelezwa zaidi nje ya ndoa,Hazionyeshi athari za upande wa pili wa
ngono kama magonjwa ya zinaa ukimwi,mamba, ubakaji,zinachochea mazungumzo ya
wazi zaidi kuhusu ngono,zinatoa majaribu ya kuzifanyia kazi au kuigiza,Hazitoi
uhalisi wa mambo zinaingiza imani potofu kuhusu utendaji wa tendo
hilo,zinajenga hali ya kutokuaminiana,zinaleta athari katika mawasiliano
nyumbani,zinaharibu uhusiano wetu na Mungu.
Ni muhimu kufahamu kuwa Kama picha hizi
zinafaa kusingekuwa Na madhara makubwa Kama Yale tuliyoyaona katika shuhuda
hizi Ni wazi kuwa hili Ni tatizo Na Ni lazima kanisa Na serikali ikubali
isikubali linaiharibu jamii, Ni muhimu pia kuangalia Biblia inasemaje kuhusu
kuangalia picha za ngono? Biblia inasema hivi “Sitaweka mbele ya macho yangu
Neno la uovu.Kazi ya waliopotoka naichikia,haitaambatana nami”(Zaburi 101;3).Katika uadilifu wake
Ayubu anasema alifanya agano na macho yake kumwangalia msichana (Ayubu 31;1) hii ilimaanisha kuwa Ayubu
aliyapiga macho yake marufuku kutamani msichana ni wazi kuwa hili
linatukumbusha jinsi ambavyo Daudi aliyekuwa masihi wa Bwana alijikuta akifanya
mambo ya aibu ambayo chanzo chake kilitokana na kuangalia mwanamke aliyekuwa
uchi anaoga na hili liliamsha hisia zilizopelekea kufanya mipango ya kumpata
mwanamke yule ingawa hatujui mipango hiyo ilichukua muda gani lakini tunaweza
kuwa na hakika moja tu kuwa kule kuona na kuangalia kulimjegea picha
isiyofutika ya mwanamke yule Bathsheba na kwa hivyo moyo wa kutamani ulimzidi
nguvu na kuacha kuzitii amri za Mungu, Yesu alionya kule kumwangalia mwanamke
kwa kumtamani kuwa ni sawa na zinaa kamili unaonaje leo Yesu angesemaje kuhusu
Kanda za kingono na picha zilizoenea kila mahali za kingono? Moja ya viungo
ambavyo ni vyenye kiwango cha juu kabisa katika kuhisi kibinadamu macho hupewa
nafasi ya Kwanza, kisha viungo vingine kama sikio,pua, kuonja na kuhisi kwa
ngozi hufuata,Hivyo unaweza kuona umuhimu wa kweka agano na macho Yetu kuwa ni
kwa muhimu kiasi gani kwani kwa mtindo huu watu wanaweza kuwa wazinzi mioyoni
mwao (Mathayo 5;27-28) Kama umenaswa
katika mtego huu kuna njia kuu tatu tu za kukusaidia kutoka katika jaribu hili
nazo ni moja maombi,Kutokuruhusu kuangalia tena na kujilinda kimwili kabisa kuepuka na
kutokujihusisha na jaribu hili la kuangalia picha za ngono lazima ujue kuuweza
mwili wako (1Thesa 4;3-5).Endelea na
zoezi la kukataa kuangalia picha hizi na utaweza kuona wema na fadhili za mungu
zikikufuata siku zote za maisha yako ili kukuleta nyumbani mwa Bwana(zaburi 23;6) hata kama umezama katika
kuangalia picha hizi kiasi gani hii haimaanishi kuwa Mungu hawezi kukutoa huko
mungu yu aweza kukutoa na sisi woote alitutoa katika hali ngumu kama hizi hata
kama hatukuzama katika kuangalia picha za ngono lakini kuna eneo ambalo kila
aliyeokolewa alikuwa amezama na bwana akaweza kukutoa huko Endelea kustahimili
jaribi hilo na utaipokea taji ya uzima (Yakobo
1;12) Toa kipaumbele kulisikia neno la mungu (Mithali 4;20-23) na Ulinde sana Moyo wako kuliko chochote
ukilindacho.