Ijumaa, 5 Februari 2016

Vijana na Magonjwa ya Zinaa !



Somo la nane
Vijana na Magonjwa ya zinaa
Moja ya matatizo makubwa sana duniani hususani barani afrika ni pamoja  na tatizo la magonjwa ya zinaa au magojwa yatokanayo na ngono (yaani Sexually transimitted diseases STd’s)wengi wa wanao athiriwa na matatizo ya magonjwa haya ni vijana hili pia ni tatizo linalochangiwa na kutokutembea katika njia za Mungu na kumtii yeye kabla ya kufikia wakati wa ndoa ambapo mtu huamua kutulia na mmoja,tutajifunza somo hili pia kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo;-

  • Ufahamu kuhusu magonjwa ya zinaa(ngono)
  • Chanzo cha tatizo la maganjwa ya zinaa(ngono)
  • Namna ya kuchukua tahadhari
Ufahamu kuhusu magonjwa ya zinaa (ngono)
   Magonjwa ya ngono yameitwa hivyo kwa sababu huwa hayaambukizi kupitia mbu au hewa n.k.Isipokuwa ni magonjwa yatokanayo na mtum kwenda kwa mtu kupitia tendo la kingono tu, ukimwi ni mojawapo ya magonjwa hayo,Mungu alikwisha toa amri kuhusu zinaa (kutoka 20;14) usizini,kwakweli usipoishi sawa na kanuni hii ya kimungu huwezi kuepuka kukumbana na magonjwa haya ya zinaa magonjwa haya yako kama ifuatavyo;-
                    Magonjwa ya zinaa watu huona aibu kujielezea na yanawamaliza kimya kimya

Ø  Kisonono (Gonorrhea) ni mojawapo ya magonjwa najisi ya ngono,Mtu anapokuwana kisonono nyakati za biblia alitengwa kusudi asiwaambikize wengine lakini ni ugonjwa ambao mtu aliweza kupona (Walawi 15;1-15)kwa kawaida kama ugonjwa huu ataupata mwanamke mja mzito anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa kujifungua.
            Kwa watoto kuanzia umri (0-siku 28)
§  Anakua na usaha machoni usaha wa njano mzito
§  Anavimba sana kope za macho
§  Anakosa raha na hulialia anaweza kuwa kipofu
Kwa wanaume.
§  Anakua na usaha mzito wa manjano kutoka katika uume
§  Maumivu makali wakati wa haja ndogo kukojoa.
§  Kuvimba njia ya haja kubwa au juu ya koo au anaweza asiwe na dalili yoyote (Hii ni mbaya kwani inaweza kukutafuna kwa ndani kimyakimya)
Kwa wanawake
§  Anakuwa na maumivu chini ya tumbo na homa
§  Anatokwa na usaha ukeni na maumivu wakati wa haja ndogo,na maumivu wakati wa kujamiiana,Utasa
§  Kuvimba juu ya koo au njia ya haja kubwa
Ugonjwa huu una aina zake ambazo zinzfanana ambazo nyingine hazijatajwa katika Biblia mfano
Ø  Clamidia” Huu dalili zake haziko wazi lakini zina usaha mweupe unao natanata uumeni au ukeni.
Ø  Chankroid sijapata jina zuri la Kiswahili lakini ugonjwa huu wa zinaa mtu huwa na vidonda sehemu za siri na maumivu makali hususani wakati wa kujisaidia,kuvimba tezi sehemu za siri na wakati mwingine kupasuka na kutoa usaha  na kuwa na utando mweupe mdomoni.
          Kwa wanawake
§  Wanatoka usaha wa kijani au manjano ukeni
§  Usaha huu una harufu mbaya
§  Ugonjwa huambatana na kuwashwa sehemu za siri
§  Kunakuwa na michubuko sehemu za siri
                  Kwa wanaume
§  Kunakuwa na usaha mwepesi sehemu za siri.
§  Wakati mwingine kunakuwa hakuna dalili.
Ø  Kaswende. Ugonjwa huu unakua na hatua kama tatu hivi kwa wanaume na wanawake
1.       Kunakuwa na kidonda kisicho na maumivu ukeni, katika mlango wa ndani wa mfuko wa uzazi(Cervix) au juu ya uume pia kunakuwa na mtoki uisio na maumivu.
  1. Mwezi wa 1-6 tangu kidonda kionekane kunakua na homa,kukosa raha,upele mdogomdogo mwili mzima,kuvimba tezi ukeni sehemu za haja kubwank pamoja na kunyonyoka nywele
  2. Kuanzia mwaka wa 1-2,matatizo ya akili,moyo,nkna tezi kuvimba kwa mtoto aliyeambukizwa dalili huanza kati ya wiki mbili mpaka nane na anaweza kuvimba wengu,ini,viungo,kutoka upele,kuziba pumzi,pua nk.
Athari za magonjwa ya zinaa kwa ujumla
Yanaharibu Mimba,yanachangia kuziba vijifereji vya mayai ya uzazi na hivyo kusababisha kansa,utasa,na kuruhusu maambukizi ya ukimwi kirahisi zaidi,pia huchangia kujifungua mtoto kabla ya wakati,kufunga mamba nje ya mji wa uzazi hii ni kwa wanawake lakini kwa wanaume kuna kuvimba tezi na kutoboka,kuziba njia ya mkojo ,kuvimba sehemu au njia ya kutengenezea mbegu na hivyo kusababisha ugumba,kuchanganyikiwa (Syphilis) kurahisisha maambukizi ya ukimwi na kuvimba kibofu,Kwa watoto upofu ni hatari kubwa kwao uvimbe katika ubongo na uharibifu wa viungo muhimu kama moyo,ini,nk. Na maambukizi ya ukimwi
  • Chanzo cha tatizo la maganjwa ya zinaa(ngono)
Kama magonjwa haya yanavoitwa ni magonjwa ya zinaa ni wazi kuwa chanzo chake  ni zinaa woote tunajua kuwa mungu amekataza zinaa na biblia imeahidi kuwa mungu atawahukumia adhabu waasherati (Waebrania 13;4) ni vizuri kujitunza kama ni kijana subiri mpaka wakati unapooa na baada ya kuwa mumepitia vipimo mbalimbali vya kiafya mungu anapokuwa ametukataza mambo hayaa ametukataza kwa faida yetu ni muhimu basi kwa wanandoa kuzilinda ndoa zao,kwani chanzo kikuu ni zinaa.
  • Namna ya kuchukua tahadhari.
Jifunze kuishi sawa na staid za maisha tulizojifunza mwanzoni, hesabu maisha yako kuwa kitu cha thamani sana na usikubali kuyachezea maisha ni aibu kwako kutibiwa magonjwa ya zinaa ingawa sikuambii kuwa ukiugua usimuone daktari lazima umuone tena wewe nay eye aliyekuambukiza au uliowaambukiza kusudi mtibiwe woote lakini kwa upande mwingine si ni aibu kwa kijana mtanashati kama wewe kubeba magonjwa haya ya aibu? Jilinde basi, hesabu gharama ishi sawa na Mungu anavyotaka usipochukua tahadhari kwa maisha yako mwenyewe unadhani nani ana jukumu la kuyalinda maisha yako? Take care!

Hakuna maoni: