Somo
la Saba.
Vijana
na dhambi ya utoaji wa Mimba.
Utoaji
wa Mimba ni moja ya matatizo makubwa yanayokua kwa kasi duniani ni tatizo
linalowakumba hasa vijana na ziko sababu nyingi ambazo huonekana kuwa ni halali
au ni haki kwa watu kujihusisha na utoaji wa Mimba kama ilivyo kwa tatizo kwa
utazamaji wa picha za kingono kama hakutakuwa na njia yoyote ya udhibiti wa
picha za kingono tatizo la utoaji wa mimba litaongezeka kwani ni moja ya
matatizo pacha Hii ni dhambi kubwa kama ilivyo kwa dhambi nyingine Gazeti moja
maarufu nchini Marekani The Washington post
la januari 23, 1983 liliripoti
kuwa kati ya mimba nne zinazotungwa nchini humo moja huishia kutolewa iwapo
jambo hili lilikuwa hivyo 1983 unafikiri hali ikoje sasa hapa nchini ni muhimu
basi sisi nasi tuka liangalia somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu
vifuatavyo;
- Jinsi Mungu anavyouangalia uhai ulioko Tumboni.
- Hukumu ya mungu dhidi ya wale wanaojihusisha na utoaji wa mimba
- Wajibu wa wakristo juu ya utoaji wa mimba.
Jinsi Mungu anavyouangalia uhai
ulioko tumboni.
Ni muhimu kwetu kuwa na ufahamu wakati
ambapo dunia inaona utoaji mamba ni jambo halali kwa sababu zao mbalimbali sisi
tunapaswa kuliangalia jambo hili kama Mungu anavyoliangalia, Mungu hujali sana
uhai ulioko tumboni, Mungu huwa na taarifa za kila kiumbe na hatua za kila
kiumbe vikiwemo vile vilivyoko Tumboni na maandiko yanatufundisha hivyo Isaya 44;24 hapo Biblia inasema
“Bwana,mkombozi wako yeye aliyekuumba tumboni asema hivi mimi ni Bwana
nifanyaye vitu vyote…” Mwandishi wa zaburi anaonyesha jinsi
Mungu alivyokua akijishughulisha na uumbaji wa mwanadamu mfupa kwa mfupa na
kiungo kwa kiungo huku akiamuru miaka ya kuishi kwa mwanadamu huyo hata kabla
ya kuishi hii humaanisha maisha ya tumboni ni maisha kamili na halali kabisa
mbele za Mungu, (Zaburi 139;13-16) wako
watu wanaofikiri kuwa uhai kamili wa mtu huanza mara anapozaliwa lakini
kisayansi na kisaikolojia na kibiblia inakubalika kabisa kuwa Maisha ya
Mwanadamu huanzia tumboni tena siku ya mimba kutungwa,kisayansi inakubalika
kabisa kuwa virithia vya kibinadamu kitaalamu genetic codes za mtu huanza
kuamuliwa na kuwa tayari kuwa mwanadamu huyu atakuaje tangu siku ya kutunga
mamba hizo genetics virithia huamua kuwa mtu huyo atakuaje
kimwili,kiakili,kihisia,na kwa kweli vitaendelea katika maisha ya mwanadamu
huyo vikiboreshwa tu na maswala ya kimazingira,Kibiblia tunazo shuhuda nyingi za Mungu kujihusisha na
viumbe vilivyoko tumboni kama viumbe kamili Malaika Gabriel alitabiri kujazwa
Roho Mtakatifu kwa nabii Yohana tangu akiwa tumboni (Luka 1;15) hii inamaanisha kuwa
kuwa Mungu anahusika na maisha ya viumbe vilivyoko tumboni yakiwemo
maisha ya kiroho,Daudi alipokua akitubia uovu wake alisema kwa asili alikuwa
muovu tangu tumboni mwa mamaye (Zaburi
51;5) Si hivyo tu lakini tunaona jinsi Mungu alivyomchagua nabii Yeremia
alisema maneno haya “Kabla sijakuumba
katika tumbo nalikujua,na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa,nimekuweka kuwa
nabii wa mataifa” (Yeremia 1;5),Unaona
tunawezaje basi kuhalalisha utoaji wa mimba kwa madai kuwa kiumbe hicho
hakijaanza kuishi mbona wako watoto wanaozaliwa wakiwa na miezi 6 au7 au 8 na
wameishi wakiwa wanadamu kamili hebu
tujiulize ni nani ana haki ya kuishi kati ya mtu mwenye umri wa miaka 70 na mimba
ya miezi mitatu au mtoto wa miaka miwili? Uhai ni zawadi kutoka kwa Mungu uwe
ni wa miezi miwili au miaka 30 woote wana haki sawa ya kuishi Mungu atawahukumu
wale woote wanaocheza na uhai, Mimba inaweza kutolewa tu endapo kitaalamu
inahatarisha maisha ya mama au mtoto aliye tumboni yanapotokea matatizo ya moja
aishi moja afe ili kuokoa mojawapo.
Vitoto vingi vinauawa vikiwa tumboni na jamii ya kisasa na kisomi imenyamazia ugaidi huu
Hukumu
ya Mungu dhidi ya wale wanaojihusisha na utoaji wa mimba
Kama
uhai wa viumbe walioko tumboni unathamani kwa Mungu je unafikiri Mungu anawaza
nini kwa watu wanaotoa mimba au wanaojihusisha na kusaidia utoaji wa mimba?
Biblia inasema nini?(Mwanzo 9;5-6) “Hakika damu yenu ya uhai wenu
nitaitaka;na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka na kwa mkono wa mwanadamu
nitaitaka,kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu,Atakayemwaga
damu ya mwanadamu,damu yake mtu huyo itamwagwa na mwanadamu,maana kwa mfano
wake Mungu alimfanya mwanadamu.” Muda usingelitosha kunukuu kila andiko lakini Mungu alikataza kumwaga damu isiyo na hatia (kutoka 23;7) aidha biblia inatamka
laana kwa kila mtu anayemwaga damu isiyo na hatia (Kumbukumbu 27;25 Yerenia 22;17,2;34-35) mtu yeyote anayejihusisha na uuaji wa viumbe walio tumboni ni
muuaji kama wauaji wengine,mimi kama mtumishi wa Mungu na nabii nitoe wito wa
toba kwa woote waliowahi kujihusisha na utoaji wa mimba wawe madaktari ambao
kwa kutumia taaluma zao ambazo hulenga kuokoa maisha ya mwanadamu wao wametumia
kuangamiza uhai watubie dhambi hii aidha wasichana au wanawake waliojihusisha
na utoaji wa mimba watubie aidha nichukue nafasi hii kutoa changamoto kwa
serikali na bunge kutokupitisha sheria zinazohalalisha
vitendo hivi haraamu na pia kuchukua hatua kali kwa wale wenye kujihusisha na
vitendo hivi katili vya mauaji ya Binadamu wadogo wachanga wasioweza kujitetea
ambao vilio vyao huishia kwa Mungu na hivyo kuleta hukumu ya mungu kwa taifa
letu.
Wajibu
wa wakristo juu ya utoaji wa mimba
Kila mkristo anawajibika
kupinga vikali vitendo vya utoaji wa mimba ziko baraka zinazo ambatana na
kulinda viumbe vichanga visivyo na uwezo wa kujitetea juu ya maisha yao wakati
Fulani farao alikuwa ametoa amri kuuawa kwa watoto wote wa kiebrania wakati
walipokuwa wakizalishwa lakini wazalishaji walikataa agizo la farao kwa sababu
walimuhofu Mungu kwakweli Mungu aliwabariki wazalishaji wale na kuwasimamishia
nyumba zao ( Kutoka 1;15-21),Leo hii
wako madaktari wasio mcha Mungu ambao kwa tamaa ya fedha husaidia metendo hayo
ya utoaji mimba hii ni dhambi ni vizuri kutokutoa mimba kwa sababu zozote zile
hata kama umebakwa ukaachiwa ujauzito kaa nao na Mungu atakubariki ni swala la
kimasomo zaa kwanza kisha nenda kaendelee na masomo najua ziko sababu nyingi
ambazo zinaweza kutolewa ili kuhalalisha utoaji huo lakini kwa bahati mbaya
hapa mimi siko katika mdahalo wa kuonyesha inafaa au haifai ila natumia mamlaka
ya juu kabisa neno la Mungu kupiga marufuku swala zima la utoaji wa mimba
nikichukua nafasi hii kulaani aina yoyote ile ya utoaji wa mimba na mjadala
umefungwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni