UTANGULIZI.
Moja
ya makundi muhimu katika jamii na ambalo linapaswa kupewa kipaumbele na jamii
pamoja na kanisa ni vijana. Si vema kuwapuuzia, vijana ni kundi muhimu ambalo
shetani analitamani sana ili aweze kulitumia Lakini Mungu pia anapenda
kuwatumia vijana, kumbuka Bwana Yesu Mwenyewe aliishi maisha ya ujana tu,
alisulubiwa akiwa na miaka kama 33.5 Lakini kwa kuwa alipata malezi Mazuri ya
kiroho aliweza kusaidia jamii iliyomzunguka na jamii iliyoko leo na hata jamii
ijayo kwa mambo muhimu aliyoyafanya, wewe je unautumiaje ujana wako?
Ni kitu gani unataka jamii ijifunze kutoka
kwako haya yoote yatakuwa na umuhimu endapo utafanya kazi ya ziada ya kuutunza
ujana wako. Kumbuka kuwa ni wewe mwenyewe mwenye jukumu la kujitunza utu wako
na ujana wako. Katika somo hili la Ngome ya vijana Mchungaji Innocent Mkombozi
Kamote atakuwa akishughulikia Maswala muhimu ya vijana kimwili na kiroho ili
waweze kuukulia wokovu huku wakiwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto
mbalimbali katika Maisha Bila kufikia viwango vya kuharibika katika dunia hii
yenye changamoto nyingi.
Mchungaji Kamote ni kijana lakini ameweza
kuutumia ujana wake katika kumtumikia Mungu na hivyo amekuwa mlezi mwema wa
vijana, kati ya mambo anayoyapenda ni kuielimisha jamii katika yale anayodhani
yanaweza kuwasaidia watu Kamote ni Mwandishi wa kitabu Jinsi waislamu
wanavyoweza kujibiwa ambacho ni maarufu sana, pia ni mwandishi wa kitabu Jinsi
ya kuwa na Amani ya kweli katika ndoa na kitabu cha uchambuzi wa waraka wa
waebrania ambacho kinafanyiwa marekebisho kabla ya kutoka!. hiki ni kitabu cha
Nne katika uandishi wake na vyote ni vizuri na vina mvuto mkubwa sana Fuatilia
Mafundisho haya ya muhimu kwa vijana ambayo pia naamini yaweza kuwa Msaada
Mkubwa si kwa vijana tu bali na kila mtu anayependa Kujifunza au kufundisha
maswala kuhusu vijana, kitabu hiki kitakuwa ngao au ilinzi kwa vijana kuhusiana
na maisha yao ndio maana niliamua kukiita Ngao ya vijana.
Mchungaji Kamote pia amekuwa mnnenaji hodari katika semina mbalimbali za
vijana hususani katika makongamano ya Pasaka ya Casfeta kwa miaka mingi
amefundisha masomo kuhusu ujazo wa Roho mtakatifu,Karama za Roho,Maswala ya
vijana na huku akijibu Maswali ambayo
vijana huuliza, na jinsi ya kukabiliana na changamoto za kiislamu fuatilia somo
hili naamini litakuwa baraka kwako kama ilivyokuwa kwa Masomo yale mengine.Kwa
hakika kitabu hiki ni ngome kwa vijana unataka usiharibikiwe soma kitabu hiki
Ngome ya vijana. Hamasisha na wengine kukisoma na fundisha yale unayojifunza
katika kitabu hiki Neema na amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja
nanyi.
Somo la Kwanza;
Vijana na Stadi za Maisha.
Stadi za maisha ni moja ya masomo muhimu
sana kwa vijana kwani huwapa mbinu mbalimbali namna wanavyoweza kukabiliana na
changamoto mbalimbali za maisha ili kutunza uhai na uthamani wa maisha, hususani
ya vijana; Somo hili hufundishwa pia huko duniani katika Elimu nyingine za
kawaida Hapa mchungaji Kamote analifundisha katika Mtazamo wa kibiblia.Stadi za
maisha hujumuisha mbinu, maarifa na akili zinazotusaidia katika maisha yetu, Mungu
husikitishwa tunapoangamia kwa kukosa maarifa (Hosea 4;6) Katika somo hili tutachambua maarifa ambayo kijana au
mtu yeyote anapaswa kuwa nayo ili aishi kwa amani na watu wote na kujiepusha na
mambo ya hatari, pia kujibu kweli kadhaa kuhusu maisha.
Kujitambua;-
Kila mwanadamu mwenye akili timamu anapaswa
kujitambua, Kuna umuhimu mkubwa sana katika kujitambua, Kujitambua ni hali ya
kuelewa uthamani ulionao, wewe ni wa thamani kuliko unavyojifikiri lakini kama
hujitambui huwezi kulinda uthamani huo ulionao, ili mtu ajue uthamani alionao
ni muhimu ujaribu kuwaza kama wewe ungekuwa bidhaa fulani Je thamani yako
ingekuwa ni shilingi ngapi? Na ungependelea uwe bidhaa gani? Maswali hayo
yatakufanya ujitambue, Paulo mtume alitamani Timotheo aliyekuwa kijana
ajitambue uthamani alionao (1Timoth 4;12)
Ni
muhimu kujihoji maswali haya
·
Je? wewe ni nani?
·
Ndoto
zako ni nini katika maisha?
·
Una
umuhimu gani kwa Baba yako, mama yako, wadogo zako, nduguzo, Taifa lako, kijiji
chako, kabila yako n.k?
·
Wajibu
wako katika jamii ni upi?
·
Matarajio
na malengo yako katika jamii ni yapi?
·
Jamii
yako Inatarajia nini kutoka kwako?
·
Kwa
nini ulizaliwa?
·
Je
Ni mambo gani yanadumisha ukamilifu wako kimwili, kijamii, kisaikolojia,
kiuchumi, na kiroho?
Unapokuwa
na majibu ya Maswali hayo hapo juu ndipo unapoweza kutambua uthamani ulio nao
na utakua umejitambua. Mtu anapokuwa amejitambua hawezi kuyafanya maisha yake
kuwa kitu cha kuchezea atayaheshimu maisha, watu wengi hushindwa kujiheshimu kwa
sababu Hajajitambua kuwa yeye ni nani? Na anathamani gani katika dunia hii
hajatambua yeye ni wa Muhimu kiasi gani Kwa Mungu na wanadamu; Mungu atupe
neema kutambua uthamani wetu Kama yeye anavyotutambua akatuumba tofauti Na mtu
yeyote duniani, si unajua kuwa hatufanani kila mmoja ni wa pekee wewe ni wa
thamani. Lolote tulifanyalo tutalifanya kwa ujasiri tukijitambua kuwa sisi ni
nani. Nehemia alijitambua kuwa yeye ni nani na yuko kwa ajili ya nani hii
ilimsaidia kuzikabili changamoto alizokutana nazo katika jamii yake soma. (Nehemia 6; 10-13). Kadiri mtu
anavyojitambua na kujua uthamani alionao au umuhimu alio nao katika jamii
ndivyo maisha yanavyokuwa na thamani kwake, Kwa bahati mbaya watu wengi
wakiwemo vijana hawatambui uthamani walionao na hivyo hujidhulumu nafsi zao au
kusababisha hasara kwa wengine jaribu kuwaza juu ya mfano wa dada huyu ambaye
hakutambua uthamani wake wala kujifikiri kuwa yeye ni nani.
Dada mmoja aliyeitwa jina Sophia (Jina zuri
la kiyunani ambalo maana yake ni Hekima),Sophia alikuwa ni mtoto wa kwanza wa
mkulima mmoja wa matunda wilayani Lushoto,Sophia alilelewa katika maadili
mazuri na wazazi wake na kwa msingi huo alikuwa ni mtoto aliyejitunza yaani
Bikira jambo ambalo ni nadra sana katika jamii ya nyakati za leo kukuta
msichana amejitunza yaani ni bikira asiyejua mume, Binti huyu alisoma masomo
yake ya shule ya msingi wilayani Lushoto na alifanikiwa kufaulu na kuendelea na
masomo ya sekondari na hatimaye alifanikiwa kufaulu na kuendelea na masomo ya
sekondari ya juu A-level kwa bahati nzuri Sophia alifanikiwa kusoma shule
ambazo zilikuwa ni za mchanganyiko yaani zenye wavulana na wasichana,Sophia
alikuwa ni mwenye mvuto mkubwa kwa kweli alikuwa mzuri na hivyo wavulana wengi
walijigonga kwake hata hivyo waliambulia patupu kwani Sophia aliendelea na
msimamo wake wa Elimu kwanza mapenzi baadae moja ya vijana waliomsumbua sana
aliitwa Kelvin kijana huyu naye alikuwa ameumbika hivyo alikuwa Handsome na kwa
kuwa alikuwa mchangamfu alifanikiwa kuwanasa mabinti wengi lakini aligonga
ukuta kwa Sophia jambo hili lilimsumbua sana kwani kila Lugha aliyoitumia
haikuweza kubadili msimamo wa Binti yule wa kisambaa.Jambo hili lilipelekea
wenzake pamoja na Kelvin kutumia njia za maudhi ikiwa ni pamoja na kumuita
Sophia Mshamba! Jambo ambalo lilimuudhi sana Sophia hata hivyo aliendelea kuwa
mgumu.
Siku moja kabla kidogo ya kufanya mtihani
wa kidato cha sita ambapo siku hizi sherehe za mahafali hufanyika mapema kabla
ya Mtihani, katika siku hii wanafunzi walipongezwa kwa tabia mbalimbali
zikiwemo usafi, uwezo wao darasani, nidhamu, ushirikiano n.k Sophia alikuwa
moja ya watu waliopongezwa kwa nidhamu hata hivyo kama ilivyo ada ya siku ya
mahafali siku ile disco lilipigwa usiku kucha na wasichana waliamua kujirusha
kwa furaha huku wakiwa na rafiki zao wa kiume au wa kike yaani washikaji, kujirusha
kulinoga na alikuwa ni Sophia tu aliyeonekana kuwa mpweke kwani kila mtu
alikuwa na wake, moyoni alijihoji kuwa yamkini mimi kweli ni mshamba! yaani
hata siku ya leo ya kuhitimisha masomo wenzangu wanaenjoy mimi nikoniko tu aah!
Alijiuliza moyoni mwake.Kana kwamba Kelvin alijua nini kinaendelea katika
ubongo wa Sophia aliamua kujisogeza karibu naye na kujaribu kumsemesha na
kumnunulia kinywaji kwa mbali sana Sophi alijihisi kuwa naye ni mtu hivi na
kuanza kujisikia vizuri, “Dada Sophie eeh! Hata leo siku yako ya
kuhitimisha masomo bado uko mnyonge njoo basi tucheze japo kidogo masomo si
yamekwisha njoo tujirushe dada umeumbwaje wewe kuinyima raha hata nafsi yako
njoo basi mpendwa eeh” hayo yalikuwa ni baadhi ya maneno kati ya mengi
aliyokuwa akiyarusha Kelvin kwa Sophia maneno yanayoonekana kuwa yaliumba kitu
Fulani katika Moyo wa Soph, Kwa kweli Sophie uzalendo ulimshinda aliamua
kujitosa katika mziki nakupata kilaji kwani alijipa moyo kuwa ni siku yake
baada ya kazi ngumu ya masomo kwanini asijipongeze? Kelvin aliitumia nafasi ya
kucheza mziki kumpapasa Sophie ambaye alikuwa hajui lolote wakati wote huu
katika taa za giza wanafunzi wengine waliendelea na disco huku wakibusiana na
kunyonyana ndimi zao yaani Denda na wengine walionekana kumtia moyo Sophie kwa
kuamua kukamua muziki siku ile akiwa kama mtu aliyechangamka na anayeibuka
kutoka kwenye ulimbukeni kama ilivyo kwa wengine ambao walikuwa wakitoka nje
kwa starehe nyingine zaidi Kelvin aliamua Kumshawishi Sophie ambaye bila
tarshishi alikubali aah! Si ilikuwa siku yake kwa nini aonekane mshamba nao
waliamua kutoka nje ambako wengi walikuwa wakifanya mapenzi katika kona mbalimbali
za ukumbi wa disco gizani huko nje Sophie aliyekuwa bikira naye siku ile kwa
mara ya kwanza alijiruhusu kuingiliwa na Kelvin, Kwa kweli alipoteza ubikira
wake, hata hivyo alijipa moyo kuwa hatarudia tena tabia hiyo na kwakuwa watu
wengi hawajui angejikausha tu bila watu kujua amefanya nini.
Siku za mitihani ziliwadia na wanafunzi
wote walifanya mitihani yao na kumaliza shule, Hata majibu yalipotoka miongoni
mwa watu waliochaguliwa kwenda chuo kikuu Sopjie alikuwa mmoja wao alifaulu
tofauti na wengine yeye alikwenda chuo kikuu sehemu ya Muhimbili kwa ajili ya
kusomea fani ya Udaktari wa maswala ya binadamu huko nako alifaulu na kuanza
kazi katika moja ya hospitali zetu hapa nchini Sophie alibahatika kuolewa na
daktari mwenzake kijana ambaye naye alikuwa na sifa ya kujitunza kama
ilivyokuwa kwa Sophie, Sophie na mumewe huyo walifanikiwa kuishi katika ndoa
kwa muda kama wa mwaka moja hivi wakiwa ni wenye kutumainiwa na wazazi wao kwa
pande zote mbili ndugu zao, kanisani na serikalini na taifa na jamii kwa ujumla
kwani walikuwa ni wenye damu mbichi yaani ni vijana, ndani ya mwaka ule moja wa
ndoa Sophie alifanikiwa kupata ujauzito na kujifungua mtoto wa kiume ambaye
katika hali ya kusikitisha aliugua magonjwa ya ajabu na kufariki, kadhlika hali
ya Sophie na mumewe kiafya haikuwa nzuri tangu wakati ule na kwakuwa wenyewe
walikuwa ni wataalamu wa afya iligundulika kuwa walikuwa wameathirika kwa
virusi na hatimaye ugonjwa wa ukimwi ambao ulipoteza maisha yao wote wawili, Hii
ni habari ya kusikitisha sana kwani wazazi wa kila upande waligharimika
kuwasomesha vijana wao ambao sasa walikuwa wamefikia katika kilele cha maisha
ambapo labda wangejenga familia yao na kuwasaidia wazazi wao au hata ndugu zao
kumbuka pia walikuwa msaada mkubwa kwa jamii kwani wote walikuwa wataalamu!. Je
umejifunza nini?Je unapoitwa mshamba inakupunguzia utu wako? Je unadhani Sophia
alijitambua? Je kutokujitambua kwa Sophie kulileta madhara gani katika jamii je
Sophia alitambua uthamani alio nao katika jamii? Usijiue, usikate tamaa,
usikubali kuyumbishwa katika msimamo wako wewe ni wa thamani kuliko unavyojifikiri
ni kwa sababu tu hujajua Mungu amekusudia nini au uwe nani katika maisha yako
lakini ukiyajua hayo Hutakubali kuyachezea maisha, vijana wengi hawajitambui na
ndio maana huamua Hata kujiua au kunywa sumu eti kwa sababu tu Mchumba amekuacha!
Kwani kuachwa na mchumba ndio mwisho wa dunia? Mimi nakuasa kama Mtumishi wa
Mungu usiharibu maisha yako kwa namna yoyote wala kwa kuvuta sigara au bangi au
kufanya mapenzi holela au kujihusisha na madawa ya kulevya kwani kuna kitu cha
ziada katika maisha yako Mungu amekiweka ni cha kipekee sana kitunze kwani
kinategemea kuishi kwako kwa Muda mrefu ili kijitokeze na dunia ipate kufaidika
na kile kilichomo ndani yako wewe ni wa thamani!.
Katika Maisha yako usikubali chochote
kikutoe katika kusudi ambalo kwalo Mungu amekuumbia, usijali ni hali gani
unazipitia au taifa letu linapitia au familia yako inapitia nani ajuaye labda
wewe ndie mkombozi wa taifa hili au wa familia yako, Kristo alikuja kuwa msaada
kwa Dunia alipofikisha umri wa miaka thelathini hivi unaonaje kama angekata
tamaa mapema? Na alizaliwa katika hali duni na ya kukatisha tamaa baba yake
akiwa ni seremala kama waliokuwa wamefulia hivi lakini hakukata tamaa, Usikate
tamaa tunza ujana wako tambua uthamani wako katika nyanja zote fanya kazi zako
kwa bidii au soma kwa bidii kila ulifanyalo lifanye kwa bidii na Mungu wa
mbinguni atakubarikia.
Mahusiano;-
Kila
mtu anapaswa kujihoji kuwa anahusiana vipi na wenzake katika jamii, Mtu yeyote
aliye bora ni yule ambaye ana mahusiano mazuri na jamii ya watu wanao mzunguka
tunao wafahamu na hata tusio wafahamu.Je una uhusiano mwema na kila mtu? Je
wenzako wanakuonaje katika mahusiano? Jiulize je nyumbani, kanisani, shuleni, barabarani
na majirani zako, bosi wako au watumishi wako wakazi, wafanyakazi wenzio,
wanafunzi wenzio, wapangaji, wanakwaya na wanajamii katika ujumla wake je una
amani nao? Biblia inatufundisha kuwa tutafute kwa bidii kuwa na amani na watu
woote soma (Waebrania 12;14),hii
maana yake hata tunapokuwa tumekosewa ni muhimu kwetu kutafuta amani na wale
tuliowakosea au waliotukosea,Huku wewe ukiwa wa kwanza kutafuta amani hiyo hata
kama wewe ndiwe uliyekosewa hii ndio ishara ya mtu aliye bora! Huwezi kusema
unampenda Mungu huku unamchukia mwenzako unaye muona kwa macho (1Yohana 4;20-21).Je ni lugha gani unayoitumia?Je unaheshimu watu kiasi
gani? Uhusiano wako kwa wakubwa na wadogo ukoje? Wazazi wetu ni marafiki zetu?
Wachungaji na viongozi wako wa dini
kwako ni nani?Ndugu zako wa kike au wa kiume katika bwana na hata nje ya
hapo ni nani kwako? Je unatafasiri vipi uhusiano? Je Kila mwanamume au mwanamke
yaani watu wa jinsia tofauti na wewe ni lazima uwe na uhusiano nao kimapenzi? Je
ngono ni kigezo cha uhusiano kwako? Mahusiano kwako ninini na yanakuongoza
vipi? Je unatarajia watu wakufanyie nini je wewe unafanya Yale unayotaka watu
wakufanyie? Yesu alisema nini angalia (Mathayo
7;12). “Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu nanyi watendeeni vivyo hivyo;
maana hiyo ndiyo torati na manabii.”
Je wewe unawatendea watu Nini? Angalia Mfano huu;-
Dada mmoja aliyekuwa mtanashati
hivi, siku moja alipanda kwenye daladala, Dada huyu aliyekuwa na maringo
aliingia moja kwamoja na kuelekea kukaa kwenye moja ya siti aliyokuwa ameketi
kaka mmoja hivi aliyeonekana wa kawaida tu, Kwa kuwa dada yule mtanashati hivi
alikuwa na maringo na majivuno vijana waleo wanasema ananata! Aliona hakuwa
hata na sababu ya kumsalimia kaka aliyekuwa amemkuta na kukaa naye katika siti
moja, Kwa kweli dada alijiona Sana! na alijiona kuwa yuko salama na safari ikaendelea;,katikati
ya safari kondakta alianza kutoza nauli kama ilivyo ada na mara ndipo ilipofika
zamu ya dada yule,kama unavyojua makondakta wetu hapa nchini wako kikazi zaidi
na hawataki uzuri zaidi ya nauli na unapomletea mzaha anaweza kukukoromea hata
bila kujali nani wanakuzunguka katika gari yeye anajali nini Bwana ahaa si
unajua jioni ndo hesabu anataka fedha tu na ukiweka adabu nyuma yeye alikwisha
imwaga miaka tangu alipokuwa mpiga debe,Dada yule alifungua pochi yake kwa
madaha sana na kumbe kwa bahati mbaya alikuwa amesahau nauli nyumbani hivyo
pochi yake haikuwa na kitu lo! Aibu iliyoje kwani konda hakuwa anaelewa somo
zaidi ya kudai nauli bila adabu huku akinyesha mvua ya matusi “Si
tuko kazini bwana unazani tumekuja kununua sura hapa Nataka nauli” alisisitiza Konda huyu huku akishusha
matusi kedekede abiria wakiwa kimya, Mungu si athumani yule kaka aliyekuwa
karibu na dada yule ambaye alipoingia hata kumsalimu aliona ni kujipotezea muda
aliamua kumpa dada yule nauli ili kumtuliza konda kisha kaka yule alimuuliza
unayo naya kurudia? Dada yule alijivunga kupokea kwa madai kuwa angepitia benk
hivyo swala la nauli ya kurudia halitasumbua, gari lilipofika kituoni dada huyu
ambaye tayari mazingira yalimfundisha adabu alimshukuru yule kaka na kutokomea
mtaani.
Mfano huu unatufundisha nini Je unaweza
kumdharau kila mtu tu? Tunahusiana vipi na wengine Hakuna mtu wa kumpuuzia kila
mtu anastahili heshima bila kuangalia sura heshima haiuzwi ni kitu cha
Bure,Yeyote unaemtendea ubaya leo aweza kuwa msaada wa baadae kwako, Ndio maana
Yesu akasema “Lakini mimi Nawaambia,Wapendeni adui zenu ,Waoombeeni wanaowaudhi”.
(Mathayo 5;44)
Mawasiliano;-
(1koritho 14;26-27). Katika mistari hii kwa ufupi
tunaweza kusema kuwa Paulo mtume hapo alikuwa anashighulikia swala la
Mawasiliano,kwa maana nyingine ili watu waweze kuwasiliana na kuelewana ni lazima kuwepo na utaratibu,Je
umeshawahi kupeleka ujumbe Fulani muhimu na baadae ukagundua kuwa
haukueleweka?Je ulijiuliza ni kwa sababu gani?
Kuwasiliana kunakuwa na maana kama pande zote
mbili zinazohusika zinaelewana,Hivyo ili ueleweke jitahidi kujifunza mbinu za
mawasiliano (Communications skills),Jaribu kutumia mwili wako,Ishara na vitendo
unapowasilisha ujumbe (non- Verbally)Vitendo husaidia kupeleka ujumbe kuliko Maneno
Mkao wako na mvao wako pia unawasilisha ujumbe kuwa wewe ni mtu wa namna
gani.Jaribu kuwaza kuwa unapovaa viguo vya nusu uchi unapeleka ujumbe wa namna
gani?unapozungumza huku unalembua macho au kubana pua kidogo au kama unaeng’ata
kidole unapeleka ujumbe wa namna gani?Unapopeleka ujumbe huku mwili wako uko
tofauti na ujumbe kuna uwezekano ujumbe wako usipokelewe.Angalia kielelezo
kifuatacho;
Nimetoka kwenye uwepo wa Mungu sasa hivi nina
ujumbe Muhimu kwa ajili yako leo na kwa mafanikio yako (Picha na maelezo kwa
hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent
Kamote)
Angalia Muhubiri huyo hapo juu ana
ujumbe muhimu wa mafanikio yako! Je maneno yake na muonekano wake unaweza
kuufanya ujumbe wake wa mafanikio kupokelewa? Ni muhimu kujiangalia kila wakati
na kujitokeza mbele ya hadhira tukiwa na muonekano unaoendana na kile
tunachokikifanya, kukisema kukiamini au kukitetea ili Muonekano wetu uweze
kuhusika katika kupeleka ujumbe. Manabii wengi wakati wa agano la kale
iliwapasa kufanya mambo mengi sana yaliyochangia kufikisha ujumbe ule waliokuwa
wameukusudia kuufikisha kwa jamii husika na wakaeleweka.
Namna
ya kutatua Matatizo ;( 1Falme 3;16-27)
Kutatua
matatizo ni mojawapo ya jambo gumu na linalosumbua watu wengi sana hususani
vijana mtu anayejitambua anapaswa kuwa makini wakati anapojishughulisha na
kutatua matatizo ni muhimu hapa kujiuliza kwanza Tatizo lako ni nini? Au tatizo
uliloletewa ni lipi? Na ni muhimu ukapata muda wa kutafakari na kisha kufikiri
ni njia gani utazitumia baada ya kutafakari njia mbalimbali za kuweza kutatua
tatizo hilo,na kwa kila njia pima kuwa unapoichagua njia hiyo inaleta matokeo
gani (mazuri au mabaya).Baada ya hayo unaweza kuchagua njia ambayo inaleta
matokeo mazuri wakati wote huo ni muhimu kuzingatia maswala yafuatayo
tunapotatua matatizo 1.Angalia kwanza tatizo lenyewe, 2.chagua njia za kutatua
tatizo hususani zisizo na madhara 3. pima matokeo ya namna unavyotatua matatizo
kwa mfano kama u mchungaji si kila wakati kumtenga mshirika kunatatua tatizo
lazima ieleweke kuwa lengo la kumtenga mtu ni kumrejesha awe hai kiroho na sio
kumvunjia heshima kama wafanyavyo watu wengine (Wagalatia 6;1).
Namna
ya Kufanya Maamuzi (Ruthu1;1-22,Mwanzo13;1-13).
(1Falme 12;4-11).Kufanya uamuzi ni moja ya mambo
ya maana sana katika maisha yetu.Ni muhimu kufahamu kuwa uamuzi tunaoufanya leo
ndio utakaoamua maisha yetu ya mbeleni au baadae.wakati wakufanya uamuzi ndio
wakati wakuonyesha upeo na ukomavu alionao mtu.katika ulimwengu wakiroho Mungu
au Shetani huangalia kwa makini sana mtu anapofanya maamuzi ili kila upande
uweze kutekeleza matakwa yake kulingana na uamuzi husika hivyo utaona kuwa kufanya
uamuzi ni jambo la muhimu sana.
Hebu jaribu kuwaza mfano huu “Umeagana na
mpenzi wako kuwa akupitie ili mkatese mjini; anafika na gari yake akiwa amelewa
au amezitwika ze laga kichwani kiasi cha kutosha hivi! Na anataka akuendeshe
kwenye gari yake je utahairisha safari? Au utaenda hapo pana hitaji kufanya
uamuzi na ni mahali pa kufikiri kipi ni cha muhimu woote tunakubali kuwa Uhai
ni mtamu sana utachagua nini? Mtu anayejitambua atajiuliza maswala ya muhimu
yafuatayo;-
- Je unamfahamu vizuri huyo mpenzi wako?
- Akiwa amelewa ana stamina ya kuendesha gari?
- Ikitokea hatari atakuwa na nguvu ya kukutetea?
- Je akilewa hufanya fujo au la?
- Je wewe utaelewekaje?
- Watu wanaokufahamu wakikuona umeongozana na mpenzi anayenesanesa kwa ulevi watakuelewaje?
- Akikuona mtu anayekuheshimu na kukuamini ataathirika vipi?
- Je hali hiyo inakubalika katika jamii yako au kwenu?
- Je wewe unajichukuliaje?
- Jew ewe ni wakuendeshwa na mlevi?
- Je kama unakwenda kutesa utatesa kweli?
- Je kuna kitu unahisi unajihofia?
- Jew ewe unawajibika vipi kwa usalama wako?
- Je kuna njia nyingine yoyote ya kutayua tatizo?
- Je kuna uwezekano wa kuhairisha safari?
- Je ukihairisha safari kutatokea nini?
- Je ni lipi lililo bora kwako
- Je ni lipi La muhimu kwako?
- Je ni maisha?Mpenzi?au Kutesa? lipi la muhimu kwako ukuisha kujiuliza maswali hayo ndipo sa unapoweza kufanya uamuzi je wewe ungechagua nini ?
Namna
ya kuhimili Mihemko; (Mwanzo 39;6-9.2samuel 13;10-15).
Mihemko au mhemko nihisia zote zinazopanda
na kushuka katika maumbile ya mwanadamu,mfano
hasira,jazba,huzuni,aibu,furaha,Nyege, n.k. vijana ndio ambao husumbuliwa zaidi
na tatizo la mihemko kwa sababu ya vichocheo (homonies) zao zinakuwa
zimevurugika wanapokuwa katika hali ya kukuwa na hivyo vichocheo vinakuwa
haviko sawa yaani havija Balance.” Maladjustiment of homonies”kwa msingi huo
iko haja ya kujifunza mapema namna ya kuhimlili mihemko kwa wale waliokoka Roho
mtakatifu hutusaidia kuhimili mihemko,kuhimili mihemko kwa kupiga punyeto au
kujichua hakuwezi kuwa na faida sana kwani kunaweza kuchochea kufanya vitendo
halisi swala hili nitalijadili huko mbeleni, lakini ni muhimu kujihadhari na
hali zozote zinazochangia katika kuchochea mihemko tuliyo nayo ikiwa ni pamoja
na kujihadhari na watu wenye maudhi au wagomvi ili wasiamshe hasira zako au
kujihadhari na vijarida au picha zenye kuchochea maswala ya ngono.Biblia
inasema kila mmoja wenu ajuwe kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima
mwili una nguvu sana unavuta katika maswala matamu ya dunia hii ambayo ndani
yake kuna mauti nani aweza kutusaidia ni Roho wa Mungu pekee (1Thesalonike 4;3-5.7-8soma pia Rumi
7;14-25, 8;5-11).
Namna
ya kuhimili Msongo (mgandamizo wa mawazo).
Watu
wengi sana hupatwa na msongo,hii ni hali ya kuwa na kusongwa na mambo mengi.Mambo mengi
yanayosababisha msongo(Depression)
ni pamoja na kutotimizwa kwa ndoto mbalimbali katika maisha,kubakia
yatima,kulaumiwa,ujane,kufiwa na wazazi,kusakamwa au kunyanyaswa
kazini,nyumbani na wakati mwingine hata kanisani au popote,matarajio
yasiyofikiwa,kufukuzwa kazi,kupatwa na kashfa nk mara nyingi mambo kama haya
husababisha watu kushuka moyo,kutokuona umuhimu wa kuishi,kukata tama,kuwa na
huzuni na kusongwa na mawazo wengi wanaopatwa na haya huamua
kujiua,huchanganyikiwa na kusikika wakizungumza wenyewe barabarani,kutokuweza
kufanya lolote au kujiingiza kwenye ulevi wa kupindukia,wengine kunywa
sumu,kujinyonga n.k. mtu anayejitambua atajifunza namna ya kuhimili msongo hebu
angalia mfano huu;-
Chukulia wewe ni mtu mwaminifu na
unayemcha Mungu sana na katika kumtumikia kwako Mungu unakamatwa na kutiwa
gerezani kwa ajili ya injili kanisa lako linapata taarifa;wanaamua kutuma mtu
mwaminifu sana aje akutie moyo na kukuhudumia ukiwa gerezani,kasha anapofika
huko naye anaugua mahututi sana,kwakuwa wewe ni muhubiri mwenye upako na
umekuwa ukiombea wagonjwa wengi sana unamuombea,baada ya maombi ugonjwa unazidi
kiasi cha kufa na anakua mahututi sana hali inakuwa mbaya je ungekuwa wewe
ungefanya nini? Je unaweza kufikiri kuwa Mungu amekukataa? Au utafikiri kuwa
umefanya dhambi? Je hali hii inaweza kuwapata watu wa Mungu ?je utaamua kuacha
wokovu? Soma (Wafilipi 2;25-30),Hali hii ilimpata Paulo mtume
alipokuwa amefungwa na kanisa la Filipi likamtuma Epafrodito kwa ajili ya
kumtia moyo naye aliugua sana,Lakini Paulo mtume alikuwa amejifunza katika
Mungu kuhimili msongo,Wengi wanaokufa kwa presha au shinikizo la damu ni wale
ambao hawajaweza kuhimili mikikimikiki ya kupokea matatizo mengi kwa wakati
mmoja hali hii ilimpata kuhani Eli katika (1Samuel
30;1-10).tofauti na Ayubu ambaye aliweza kuhimili msongo alipopatwa na
mabaya mengi kwa wakati mmoja (Ayubu 1-2)
jifunze kuhimili misongo wala usizimie moyo wakati wa taabu na umwangalie Mungu
(Mithali 24;10).
Namna
ya kuwa na Fikira Bunifu.
Kuwa na fikira bunifu ni kitendo cha kuwa
na uwezo wa kutatua tatizo kwa haraka, Unatumia akili nili kupambana na tatizo
la ghafla lililotokea bila wewe kutegemea, Mungu ametuumba tofauti wako watu
ambao wamejaliwa uwezo wa kutatua tatizo kwa haraka, lakini walio wengi
wanaposhitukizwa jambo Fulani linalowahitaji kuchukua uamuzi wa haraka huishiwa
nguvu kabisa na kupoteza uwezo wa kufikiri halafu baadae ndipo hupata majibu
lakini mengi huwa ni yenye majuto Ningejua! Biblia inatufundisha jinsi
Daniel,Shedrak na Meshak na Aberdnego walikuwa na fikira bunifu kujiokoa na
kujitia unajisi (Daniel 1;6-16),pia
tunapata taarifa za Raheli ambaye aliiba miungu ya babaye na babaye kuamua
kufanya utafutaji wa miungu yake haraka kwa ubunifu alijifanya yuko katika siku
zake na kujiokoa (Mwanzo 31;19,30-35)
aidha wanawake hawataweza kumsahau mwanamke mwenye akili Abigaili ambaye alikuwa na fikira bunifu na kutatua tatizo la kutaka kuuawa kwa mumewe
na familia yake (1Samuel 25;4-35)Je
unapopatwa na hali zinazo hitaji ubunifu Fulani wa haarkaharaka wewe
unafanyaje? Jaribu kuwaza mfano huu;-
Chukulia kua wewe ni msichana na
umealikwa kwenye pati na rafiki yako inayofanyika mbali na nyumbani kwenu,wewe
humfahamu mtu yeyote yule zaidi ya rafiki yako mnapofika kwenye pati watu woote
uliowakuta wanaonyesha ukarimu na uchangamfu kwako na urafiki,chakula na
vinywaji vinapatikana na mziki mzuri karibu na mwisho wa part usiku mwingi
unagundua kuwa rafiki yako hayupo na unapoulizia unaambiwa kuwa alipatwa na
dharula ya kumpeleka mgeni nyumbani na huenda hatarudi,Kaka wa rafiki yako
ambaye hajaokoka na alikuwa ameshalewa anakuondoa wasiwasi kwamba kwakua ana
gari atakusindikiza nyumbani,kaka huyu ambaye alishaanza kukuzoeazoea tangu
mwanzoni mwa pati,na kwa kuwa saa zile hakuna
daladala wala huwezi kupata hata tax ya kukodi na mfukoni huna fedha je
utafanya nini? Hapo ndipomunapohitaji fikira bunifu.
Namna
ya kuwa na fikira Adilifu.
Biblia inasema katika ( Mathayo 5;8) “Heri
wenye moyo safi maana hao watamuona Mungu” tunapozungumzia fikira
adilifu tunazungumzia ile hali ya moyono kifikira kama je unafikiri kwa
usahihi,hisia zako ni safi? Je unafikiri kwa nia njema,wako watu amabao
wanashida katika kufikiri na wengi wakundi hili ni wale wanaoitwa wameokoka ni
muhimu kufahamu kuwa kama u mtu sahihi utafikiri kwa usahihi si unajua kuwa
Mungu atakapohukumu wanadamu hatahukumu matendo yao tu bali atahukumu na nia
ile iliyopelekea wao kutenda,hivyo kuna faida za muhimu kifikira kama
tutafikiri kiadilifu na kwa moyo safi angalia mfano huu;-
Kijana mmoja mzuri alikuwa amemaliza masomo
yake katika moja ya vyuo vya ustawi wa jamii huko Arusha,baada ya masomo yake
alirudi Daresalaam ambako alikwenda kubangaiza ajira kama unavyojua kuwa siku
hizi ajira ni za shida katika nchi yetu,hasa ukichukulia kuwa mfumo wetu wa
elimu tangu mwanzo ulikuwa umebuniwa kwa namna ya kusoma ili uje uajiriwe na si
kujiajiri,hivyo kaka huyoalifanikiwa kupata ajira katika moja ya vituo vya
kulea watoto yatima kilichoko sinza Daresalaam,Siku ambayo yule kaka alikwenda
kutafuta kazi,mama mmoja mtanashati na mwenye mvuto, alionekana kumtetea sana
yule kijana ili apewe kazi si unajua unaweza kuingia katika ofisi Fulani kasha
ikatokea mtu amekuchunuku tu na kukupenda hata bila ya sababu hili ndilo
lililomtokea kijana huyu mama huyu mweupe wastani aliyekuwa na mwanya na
aliyekuwa mcheshi alifaniukiwa kumshawishi bosi wake kumuajiri kijana hutu,hata
hivyo bosi huyu alisema kijana huyu atakuwachini ya majaribio kwa miezi miwili
hivi (Under probation).kijana alianza kazi na kila mtu alimuonyesha ushirikiano
na kwakuwa mama yule alikuwa mcheshi pale kazini na alionyesha kumchangamkia
kijana yule tangu siku ya kwanza na kwa kadiri walivyozoeana pia walikuwa
wakitaniana katikamaeneo mbalimbali hata hivyo kumbuka kuwa mama yule alikuwa
na mumewe yaani ni mrs. Wakiwa ndani ya miezi miwili ya kuangaliwa siku moja
kama ilivyo ada kijana yule aliyependa kwenda ofisini kwa mama pindi kazi
zinapokuwa zimepungua na kuamua kumtania siku hiyo aliamua kwenda na kumtania
mama yule amabaye pia alikuwa si mwepesi wa kukasirika hata utani unapopita
mipaka siku hiyo kijana aliamua kumpasukia mama yale yaliyokuwa yakimsibu
moyoni kijana alisema “Mama mi leo uvumilivu umenishinda nimeona nipasue jipu
linalonisibu moyoni nimechoka kuugua leo nahitaji dawa yaani kwa ufupi mama mi
nimekuzimia” Mama yule aliangua kicheko na kumuuliza kijana yule “acha utani
wako bwana yaani huko mtaani umekosa dawa kijana mzuri kama wewe uje utafute
dawa ofisini tusidanganyane bwana!”alijibu mama yule Hata hivyo kijana yule
siku ile alikuwa amemaanisha yaani yuko Sirius ,alizidi kujimwaga kwa maeneno
ya kimahaba na kuamua kumsogelea mama yule na kuanza kumpapasapapasa kuanzia
kifuani na maeneo mengine wakati woote hu yule mama alikuwa ametulia tuli
akishangaa jinsi ambavyo utani ule unapitiliza mipaka na kuwa ukicheka na mbwa
basi utaingia naye msikitini!,mwisho mama yule aliamua kuchomoka na kwenda moja
kwa moja katika ofisi ya meneja wa utawala (Admnistrative manager and human
resourses) na kumweleza kilicho msibu meneja aliwaita watuwoote ofisini na
mwishoni alimwagiza askari kumleta kijana yule ambaye punde alipoona watu
wakiwa wamebadilika sura alielewa kuwa leo iko kasheshe kufupisha habari kijana
aliachishwa kazi kwani kumbuka alikuwa katika kipindi cha uangalizi.aibu
ilimpata kijana huyu nini kilimponza? Mara nyingi tunapoona mtu wa jinsia
tofauti akituchangamkia wakati woote huwa himaanishi kuwa anakutaka kimapenzi
wako watu ambao wameumbwa wakiwa wachangamfu tu na mioyoni mwao hawana nia
mbaya je wewe una moyo safi? Unajisikiaje unapoona mtu wajinsia tofauti
wameketi wakiongea mambo yao unadhani kuwa wakati woote wako kwa ajili ya
uzinzi? Si kweli si kila wakati watu wanaweza kuwa na nia hiyo lakini
tunawezaje kuepuka kuwafikiria watu vibaya ni kwa kuwa na mawazo adilifu
tusipende kuwawazia watu kwa upumbavu mtu aweza asiwe karibu na mwanamke na
akawa mzinzi wa kutupwa tu biblia inatufundisha mambo ya kutafakari Hatimaye
ndugu zangu,mambo yoyote yaliyo ya kweli yoyote yaliyo ya staha,yoyote yaliyo
ya haki,yoyote yaliyo safi,yoyote yenye kupendeza yoyote yenye sifa njema
ukiwapo wema wowote,ikiwapo sifa nzuri yoyote yatafakarini hayo.(Wafilipi 4;8), Je wewe umekuwa
ukitafakari mambogani je unahukumu wengine je unafikira adilifu? Mungu atupe
neema kuwa watu wenye fikira adilifu na kuwa watu safi tunaofikiri sawasawa.
Namna
ya kuwa na fikira Yakinifu (Kusimama katika kweli).
Fikira yakinifu ni hali ya kusimama katika
kweli ni uwezo wa kuisimamia kweli hata kama jambo hilo limeamuliwa na mtu
mkubwa au unaye mwamini,mzazi au mtu yeyote,ni uwezo wa kuamua ukwelina
kuuusimamia na wala sikwa mazoea tu, Ni lazima tujifunze kupinga jambo lolote
lisilo sahihi au lisilo la kweli,hakuna jambo linalopendeza kama kuwa mkweli
Shadrak, meshak na Abdednergo waliweza kuisimamia kweli pale mfalme
alipowaamuru mkwa vitisho kuabudu miungu,Daniel hakuacha kuomba pamoja na
sheria iliyopitishwa ili kumtishia asiombe Mungu,Mitume waliendelea kuhubiri
pamoja na amri kutoka kwa viongozi wa dini ya kiyahudi waliowakataza kuhubiri
katika jina la Yesui (Matendo
5;29,4;19). Tunapojifunza kuwa wakweli tangu ujuana tunajiandaa kupata
taifa lenye watu waadilifu na wakweli si wakati woote ni rahisi kuwa wakweli
lakini kumbuka kuwa unaposhindwa kujifunza kuwa mkweli au kusismama katika
kweli unaweza kujikuta unaingia katika madhara Fulani angalia mfano huu;-
“Fikiria kuwa wewe ni dada uliyeokoka na
unapokaribia au kuingia katika siku zako tumbo huwa linakuuma sana, hatimaye
unaamua kwenda hospital na unapoingia katika chumba cha daktari ambaye unaamini
atakusaidia, wakati huu hujaolewa bado, daktari anakuambia kuwa dawa ya tumbo
lako ni kwa sababu hujakutana na mwanaume na ukipata mwanaume tumbo lako
litaacha kasha anaonyesha nia ya kutaka kukusaidia yaani kwa yeye kumaliza
shida yako hiyo kama njia ya matibabu je wewe utafanyaje?”
Vijana wengi wamedanganywa na
kujikuta wakifanywa ngono kwa sababu ya kutokuisimamia kweli kwani maumivu hayo
wakati mwingine hayawezi kuisha kwa kufanya ngono kuwa na mume au kuzaa kwa
wanawake wengine hali hii huendelea,na wengine huacha yenyewe.
Martin Luther King alikuwa na fikira
yakinifu, alisimama katika kweli na kupinga ubaguzi wa rangi waliotendewa weusi
huko Marekani na ingawa aliuawa lakini ndoto zake sasa zinaheshimika,ni vijana
wangapi wanaweza kuisimamia kweli hata kama itagharimu mauti? (Picha na maelezo
kwa hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent
Mkombozi kamote).
Namna
ya kuwa mwenye Ushirikeli (Namna unavyoliona tatizo la mwingine).
Ushirikeli ni hali ya kuwa na huruma ni hali
ya kuona tatizo la mwenzi wako kama vile ni la kwako,ushirikeli pia ni hali ya
kuwajali wengine,namna tunavyowaelewa kikamilifu,na namna tunavyowatendea haki
na namna tunavyo tunavyothamini mawazo na mitazamo yao.Ni katika njia hii
tunaweza kuwatambua wenzetu vilivyo na kuwajali,Yesu nalikuwa na huruma sana
wakati woote aliwahurumia watu alichukua matatizo ya watu kama matatizo yake na
kutafuta utatuzi,mtu bora ni yule ambaye pia hujali wengine,hali hii huboresha
uhusiano na wengine katika somo lijalo tutazungumzia juu ya mahusiano.
Mama Teresa wa Culcuta India (1910-1997)
anaheshimika sana duniani kwa kuwahurumia wengine,alipewa nishani ya Nobel
1979,alianza akiwa masikini lakini alianzisha vituo vya ukarimu kwa ajili ya
kuwasaidia yatima na wajane,wasiojiweza na wenye njaa,leo hii kuna matajiri
wengi sana wasio na huruma kwa wengine wanaongoza kwa dhuluma na ufisadi wewe
utalifanyia nini taifa ushirikeli unaweza kukusaidia kuhisi maumivu ya wengine
(Maelezo na picha Kwa hisani ya makatba
ya Mchungaji Innocent Mkombozi Kamote)
Fikira
achilifu (Mathayo 5;7).
Hii
ni hali ya kuwa na moyo wenye kusamehe,kuachilia kusamehe jambo lolote
lile ambalo ni gumu kuachilika (Mwanzo 45;4-5).hili ni jambo gumu sana
lakini tunapaswa kujifunza kusamehe wako watu ambao huwakwaza wenziwao kiasi
ambacho inakuwa ngumu kuwasamehe hali hii isipodhibitiwa huweza kusababisha
watu kuuana kama ilivyo katika inchi nyingine zilizoendelea vijana huuana sana
kwa sababu ya visa na mikasa ambayo watu hufanyiana kwa kushindwa kusameheana
na kuachilia.
Kabla ya kuwa rais wa kwanza mwafrika
inchini Afrika ya kusini 1994 Nelson Mandela aliteseka gerezani kwa miaka 27
hivi,akipinga sera za kibaguzi za makaburu,aliposhika madaraka haukuwa wakati
kwake kulipiza kisasi na kubagua wazungu bali alisamehe na kuchilia je wewe
ungekuwa Mandela ungefanya nini?(picha na maelezo kwa hisani ya maktaba ya
Mchungaji Innocent Mkombozi Kamote).
Namna
ya kuwa na hali toshelevu.
Hali toshelevu ni hali ya kuridhika,je
unajua kuridhika sio jambo rahisi kama tunavyofikiri,lakini ni muhimu kujifunza
kuridhika.kwa kawaida katika maisha kuna matokeo makuu ya aina mbili kuna
kupanda na kushuka, kwa msingi huo ni muhimu kuwalea vijana kuzijua hali zote
mbili mtuma Paulo alifundishwa na mungu kuhimili hali hizo zote mbili (Wafilipi 4;11-12) hivyo haya ni
maamuzi ambayo mwanadamu aweza kujifunza,Hebu jiulize jinsi ambavyo watu
wanabahatika kupata vyeo vikubwa serikalini na hata katika makanisa lakini
pamoja na mishahara mikubwa wanayoipata angalia rushwa na ufisadi wa kutisha
kumbuka ile kashfa ya Richmond ambayo shirika hili lilikuwa linalipwa milioni 152
hivi kwa siku,watanzania wako kama million 40 hivi hii ni sawa na kusema kila
mtanzania angeweza kupata milioni tatu na ushee hivi kila siku?kama mabo ndivyo
yalivyo ni wachache tena wenywe vyeo na mishahara mikubwa waliofanya haya,kama
hayo hayatoshi wengi wanapoachishwa kazi huchanganyikiwa kwanini kwa sababu
hawako radhi na aina nyingine za maisha ni muhimu kwetu kuwa tayari na aina
zote za maisha,Yesu aliishi maisha ya kuridhika,mitume na wengi lakini hata
mwalimu Nyerere kiongozi wa kwanza wa Tanzania alikuwa mwenye kuridhika hakuwa
na tabia ya kujilimbiklizia mali ili tusiishi maisha yenye maumivu tujifunze
kuridhika
Julius Nyerere hakuwa na makuu
hakujilimbikizia mashamba makubwa wala makampuni makubwa aliishi maisha ya
kuridhika,hakusomesha watoto wake ulaya, walikwenda shule kwa miguu kama
watanzania wengine alilinda rasilimali za taifa hili kwa faida ya vizai vijavyo
leo hii maliasili,wanyama,madini na hata gesi ni dili za wachache na wanainchi
hawafaidiki na lolote kila siku ugumu wa maisha ya kugawana umasikini
unaendelea ni vema mungu akijipatia watu waadilifu,watakaokubali kuridhika na
kuhakikisha kuwa na wengine wanafaidi matunda ya uhuru (Picha na maelezo ni kwa hisani ya Mchungaji Innocent Kamote).
Mali tunazojilimbikizia hatutaweza kuondoka
nazo duniani biblia inasema hivi “Usiogope mtu atakapopata utajiri na fahari
ya nyumba yake itakapozidi,maana atakapo kufa hatachukua chochote utukufu wake
hautashuka ukimfuata” (Zaburi 49;16-17). Jiponye na roho ya tamaa ya
mali vijanawengi wamepoteza maisha kwa kutokuridhika mimi sitaki wewe uwe hivyo
somo hili staid za maisha litakusaidia ukilitendea kazi ubarikiwe.