Mstari wa msingi Matendo 2; 46
“Na sikuzote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya Hekalu…….”
Somo la umuhimu wa kuhudhuria
ibada zote ni moja ya masomo muhimu sana , ufahamu kuhusu somo hili kunamfanya
mtu aliyeokoka kupiga hatua kubwa sana katika kukua kiroho na hatimaye yeye naye kuwa mwalimu wa wengine
kwa upesi zaidi,Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu
vifuatavyo;-
Kanisa Mjini Dubai wakristo wanaruhusiwa kuabudu na kujenga makanisa bila kuweka alama ya msalaba juu ya Majengo yao
·
Umuhimu wa kuhudhuria ibada zote
·
Kwanini inatupasa kuhudhuria ibada zote
·
Tuhudhurie ibada katika kanisa lipi?
Umuhimu wa kuhudhuria ibada zote
Moja ya ishara ya muhimu
inayoonyesha kuwa mtu ameokoka ni kuwa na shauku ya kumtafuta Mungu kilka siku
Isaya 58;2 mtu aliyeokoka atapenda kujisomea Biblia na kufanya maombi binafsi nyumbani kila mara anapopata nafasi atakuwa akitafakari na kujifunza neno la
Mungu lakini pia atakuwa akihudhuria ibada
Kuhudhuria Ibada ni amri ya Mungu
kwa kila mtu aliyeokoka Biblia inasema katika Kumbukumbu 12;5 “Lakini mahali
atakapopachagua Bwana Mungu wenu
…..Apaweke jina lake maana ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo nawe wende
huko” Maneno nawe wende huko katika Biblia ya kiingereza ya New International
Version yanasomeka “To that place you must go” kwa msingi huo kwa tafasiri
rahisi tunaweza kusema mahali hapo ni lazima uende unaona kwa hiyo kuhudhuria
ibada ni swala la lazima Mungu anasema lazima uende kanisani Biblia inaagiza
kutokuacha kukusanyika Waebrania 10;25.
Yesu kristo mwenyewe alionyesha
wazi jinsi ilivyo lazima kuwako nyumbani mwa Mungu Luka 2;49 Akawaambia kwani
kunitafuta ? Hamkujua ya kuwa imenipasa
kuwamo nyumbani mwa baba yangu? Yaani imenilazimu Kama kwa Yesu ilikuwa ni lazima basi sisi ni
zaidi sana Biblia inasema Yeye asemaye
ya kuwa anakaandani yake imempasa kuenenda vilevile kama Yeye alivyoenenda 1Yohana 2;6, Watakatifu waliotutangulia kwao
ilikuwa ni furaha walipoambiwa kwenda nyumbani mwa Bwana na waliona siku moja ya kuwamo nyumbani mwa
Bwana ni bora kuliko siku elfu za shughuli za dunia soma Zaburi
122;1,84;1-2,10, ilikuwa ni kawaida kwa manabii na mitume kutunza muda wa
kwenda kusali soma Luka 2;36-37,24;53 Matendo 3;1 sisi nasi kama tunataka
kutumiwa sana na Mungu inatupasa kuiga mfano wao
Watu waliookoka nyakati za kanisa
la kwanza siku zote walidumu kwa moyo mmoja ndani ya hekalu Matendo 2;46 hii
ndio siri kubwa ya mafanikio yao
tusikubali kamwe kwa namna yoyote ile masumbufu ya dunia hii kutunyima
muda wa kwenda kuabudu.
Kwanini inatupasa kuhudhuria ibada zote
Tukiisha kujifunza kuwa neno la
Mungu ni nini na sisi tuliookolewa ni akina nani ufahamu huu utatupa kuelewa
vizuri umuhimu wa kuhudhuria ibada zote
1. Neno
la Mungu ni chakula cha kiroho Yeremia 15;16, Mathayo 4;4, Yohana
6;48-49,57-58, Kumbukumbu 8;3 Ili mtu
apige hatua kubwa ya kiroho katika wokovu inampasa kulipenda Neno la Mungu
kuliko hata chakula cha kimwili Ayubu
23;12 watu wanaokula mara tatu kwa siku pamoja na mapochopocho mengine kwa wiki
wana kula zaidi ya mara 21 kuulisha mwili maana yake na sisi ni muhimu
kuhakikisha kuwa tunazilisha roho zetu kwa kuhudhuria ibada na kuomba na
kuabudu na kujisomea neno n.k.
2. Sisi
ni wanafunzi wa Yesu Baada ya kuwa tumeokolewa tunageuka kuwa wanafunzi wa
Bwana Yesu Mathayo 27;57, Yesu Kristo anakuwa ni mwalimu wetu Yohana 13;13, Naye amelipa kanisa wasaidizi
wa kutusaidia kufundisha neno la Mungu Waefeso 4;11-12 , Mathayo 28;19-20 kwa
msingi huo waliookolewa ni wanafunzi wa Yesu na ili mwanafunzi aweze kufanikiwa
anapaswa kuhudhuria darasani vipindi vyote bila kukosa kama tutalizingatia hili ndipo tutakapokuwa
miongoni mwa hao washindao Ufunuo 2;11.
3. Tuhudhurie
ibada katika kanisa lipi?
Baada ya
kuokolewa Biblia inatupa muongozo wa dhahiri juu ya mahali sahii pa kuabudu
Biblia inasema hatupaswi tena kuyarudia mafundisho yaliyo manyonge Wagalatia
4;9 sasa tunawezaje kujua kuwa mahali hapa ni penye mafundisho manyonge?
Tutachunguza alama zifuatazo na ukigundua moja kati ya hizo basi mahali hapo
hapafai kwa kuabudu
§
Mahali ambapo pana viongozi vipofu Luka 6;39,
Mathayo 15;14 yaani mahali ambapo kuna wachungaji au wainjilisti au wazee wa
kanisa wa dhehebu lolote ambao ulevi, zinaa na uasherati na kila aina ya dhambi
inawatawala hao hawawezi kuwa msaada wa mtu wa kiroho kwa sababu mtu aliyeokoka
amepewa kuona Yohana 9;39-41 hivyo hupaswi kuongozwa na kipofu
§
Mahali ambapo matendo ya giza hayakemewi Waefeso
5;11
§
Mahali ambapo sanamu zinashirikishwa katika
Ibada Isaya 31;7,1Wakoritho 10;14,
1Yohana 5;21
§
Mahali ambapo wanafuata maneno yaliyotungwa na wanadamu
na sio neno la Mungu 2Petro 2;1-3
§
Mahali ambapo hawaamini kuwa Yesu ni mwana wa
Mungu 1Yohana 4;15,5;10-12,Yohana 3;36 .
§
Mahali ambapo Neno la Mungu halihubiriwi bali
zina hubiriwa hadithi tu na hakuna
kukaripiwa kukemewa wala kuonywa Neno siku zote linakuwa ni kufariji tu
2Timotheo 4;1-2,Ayubu 16;1-2,Waebrania 12;5-8.
§
Mahali ambapo kila mtu hata mtoto mchanga
anapewa zamu ya kutoa neno badala ya kukaa chini na kujifunza neno kwanza kwa kukaa chini ya
waalimu 1Koritho 12;28-29 Waebrania 5;11-12
§
Mahali ambapo watu wanafundishwa kushika sheria
ya Musa kwa kutokula aina Fulani ya vyakula kushika sabato n.k. Wakolosai
2;16-17,1wakoritho 10;25-27
§
Mahali ambapo hakuna changamoto bali unakaa tu
na hakuna jipya unaingia ukiwa na kiu ya kujifunza na unatoka ukiwa hajapata
kitu Yohana 7;46
§
Mahali ambapo wanakwepa kuwafundisha watu maneno
magumu ya uzima wa milele Yohana 6;60-61,66-68
Baada ya kuokoka kama utakaa
mahali pa namna hii kwenye mafundisho manyonge ni muhimu kufahamu kuwa wewe
nawe utakuwa mnyonge na hutaweza kuingia mbinguni kwani hakuna kinyonge
kitakachoingia huko Ufunuo 21;27 wala usikubali vyeo au namna yoyote ya
kuwapendeza wanadamu na kukubali kukaa katika unyonge kwa sababu hizo Yeremia
45;5,Wagalatia 1;10, baada ya kuchagua kanisa lisilo na mafundisho
manyonge sasa kaa hapo na uabudu na
kumtumikia Mungu. Mungu akubariki sana
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni