Jumapili, 7 Februari 2016

JE MUHAMAD AMETABIRIWA KATIKA BIBLIA?



 Waislamu wanaamini kuwa muhamad ndiye Nabii yule.
       Hoja hii hiliigusia katika kipengele muhimu cha umuhimu wa kukabiliana na changamoto za uislamu,Kwa mujibu wa waislamu nabii muhamad  alitabiriwa katika biblia kuwa yeye ndiye nabii yule hii inatokana na swali ambalo  Yohana aliulizwa na watu waliotumwa na mafarisayo,swali hili lina maeneo makuu matatu ambayo ndiyo yanayoundiwa hoja soma (Yohana 1;12-25).Maswali hayo yaliuliza habari za Kristo,Eliya,na Nabii yule,hoja huundwa katika eneo la Tatu la nabii yule ambapo hapo ndipo hudai kuwa nabii yule ni Muhamad ambaye Yesu mwenyewe alimtabiri katika (Yohana 14;26), kama “ paraklete” kwa kiyunani yaani aliyetukuzwa au Ahmad sawa na muhamad tutajadili hilo huko mbele,Nabii huyu hudaiwa ndiye aliyetabiriwa katika (kumbukumbu la torati 18;15,18),nabii huyu angetoka miongoni mwa ndugu za wayahudi ambao ni waarabu,Mwandishi wa kitabu  kiitwacho uislamu katika Biblia  Ngariba Musa Fundi na Kawemba Mohamed Ali waliamua kujichangamsha katika ukurasa wa 13 wa kitabu hicho wakitoa madai kama hayo kwa kuthibitisha kuwa nabii huyo atakuwa kama Musa hivyo walionyesha jinsi Musa anavyofanana na Muhamad kuliko Masihi



*     Musa alizaliwa akiwa na Baba na mama sawa na Muhamad sivyo ilivyo kwa Yesu.
*     Musa alioa na kuzaa watoto sawa na Muhamad Yesu hakuoa wala kuzaa.
*     Musa alikubalika kwa watu na Muhamad, Yesu alikataliwa.
*     Musa alikuwa nabii na kiongozi wa kisiasa kama Muhamad Yesu alikataa siasa (kufanywa mfalme).
*     Musa alitoa sheria na Muhamad pia Yesu alileta neema na kweli.
*     Warithi wao waliiteka kanaani,warithi wa Yesu walihubiri tu.
*     Musa alikufa na Muhamad na walizikwa,Yesu alipaa mbinguni.
Hivyo nabii kama Musa kwa vyovyote ni Muhamad na si Yesu na hivyo Biblia imemtabiri,Tunaweza kuuweka mpango huu katika jedwali kama ifuatavyo.

         Musa
      Muhamad
       Yesu masihi
Alikuwa na wazazi wote
Alikuwa na wazazi wote
Hakuwa na baba ila mama tu
Alioa na kuzaa watoto
Alioa na kuzaa watoto
Hakuoa wala kuzaa
Alikuwa nabii na kiongozi wa kisiasa
Alikuwa nabii na kiongozi wa kisiasa
Nabii lakini si kiongozi wa kisiasa
Alitoa sheria Torati
Alitoa sheria Quran
Alileta neema injili
Warithi waliiteka kanaani
Warithi waliiteka palestina
Warithi walihubiri tu
Alikufa na kuzikwa
Alikufa na kuzikwa
Alipaa kwenda Mbinguni

Namna ya kutatua Tatizo hili.
     Tukianzia na swala la Muhamad kuwa ndiye nabii Yule kama inavyodaiwa kusemwa na Yohana katika (Yohana 1;12-26).Ni kweli kuwa kuna maswali matatu yanaulizwa katika mazingira ya andiko hili,Nataka kuwakumbusha waislamu tena katika eneo hili kuwa Biblia haitafasiriwi kama quran ambayo hujitegemea kwa kila aya,Biblia ni kitabu cha wanazuoni ni kitabu cha wasomi huwezi kuchukua andiko na kulifasiri kama utakavyo tu , Katika moja ya kanuni za kutafasiri biblia ambazo kwa faida ya wengi nitaziweka kwa mukhtasari katika somo hili huko mwishoni,Kanuni inayopaswa kutumika hapa ni kanuni ya mazingira ya kihistoria na kanuni ya kufasiri unabii, kanuni ya mazingira ya kihistoria “Principle of historical context” inasema ili mtu afasiri Biblia kwa ufasaha anapaswa kujua historia ya andiko au maandiko ili kupata maana halisi ya kile kinachozungumzwa hivyo kihistoria tujiulize ni kwanini wayahudi waliuliza maswali yale matatu?

      Kihistoria Wayahudi walimtofautisha Nabii yule (anayetajwa katika Kumbukumbu 18;15-18) na Masihi ambaye ni mwana waDaudi(Mathayo 22;41-46), wao walifikiri nabii Yule na masihi ni watu wawili tofauti,wakati wa Musa nabii ndiye alikuwa kiongozi,walipoanza kuwa  na Mfalme Mungu alihaidi kupitia Daudi kuleta kiongozi wa kifalme hivyo kimsingi nabii zote hizi zilimhusu Yesu Kristo Yeye ndiye alikuwa nabii mkuu (Luka 7;16b)na Mfalme wa wafalme(Ufunuo 19;11-16).Waislamu hawajui historia hii na wanachanganywa zaidi kwa vile Muhamadi alivyojikinai akitaka kujithibitisha kuwa  ni nabii wa kweli na kuwa naye alitabiriwa alishusha ay  a hii(Al-A-raaf mwinuko 7;157). Ayah ii inadanganya waislamu na kuwafanya watafute katika kwa nguvu katika biblia (Torati)na injili  wakidhani wataona unabii unaomhusu Muhamad,ukweli ni kuwa Yesu ndiye mwisho wa unabii na si zaidi ya hapo kama Muhamad alitabiriwa katika biblia tungelimwamini lakini bahati mbaya hayumo kabisa (Ebrania1;1-4)
Nabii miongoni mwa ndugu zako kama Nilivyo mimi, Nabii mfano wako wewe. (kumbukumbu 18;15,18)
    Mistari hii hutumiwa na wanaharakati wa kiislamu  wakifikiri kuwa inamtabiri Muhamad nabii wa Waislamu,kwa bahati mbaya kama nilivyogusia hapo awali kua Biblia au unabii hautafasiriwi kama apendavyo mtu Fulani (2.Petro 2;20-21),Waislamu hapa hufasiri biblia kama wapendavyo wao wenyewe,Hapa kanuni iliyokiukwa ya kufasiri maandiko  ni sheria au kanuni ya kifungu kizima “The Principle of context” Unaposoma maandiko ya kibiblia  kanuni hii inataka usome kifungu kizima  juu na chini pia kabla ya kunyofoa  aya moja pekee,hivyo unaposoma aya hizi kwa mfano neno “miongoni mwa Ndugu zenu” hii haiwahusu waarabu,kifungu kinaonyesha kuwa Mungu alikuwa anazungumza na  na kabila ya walawi moja kati ya kabila kumi na mbili za Israel, hivyo maneno miongoni mwa ndugu zenu, ilihusu zile kabila kumi na moja nyingine  nje ya walawi soma (Kumbukumbu 18;1-2) mstari wa pili hapo utakutana na neno hili, Wala wasiwe na urithi kati ya Ndugu zao (miongoni mwa).Hapa Mungu anawatenga walawi na zile kabila nyingine zinaitwa ndugu zao lugha kama hii inatumika katika torati (Kumbukumbu 17;14-15) utakutana na Maneno kama haya “….Umweke mmoja katika ndugu zako awe mfalme juu yako

Kwa muundo wa lugha hapo juu je unafikiri Mungu aliwataka wayahudi wakitaka mfalme waweke mwarabu? Ambao ni ndugu wa wayahudi? Jibu ni hapana kwani Mungu hapa anazungumza na wayahudi jamii ya walawi.
     Jambo lingine ambalo wasomaji wa Biblia wanapaswa kulitilia maanani ni kuwa manabii walipozungumza,walizungumza katika namna kuu mbili moja na jamii ya wakati ule (Forthtell) na jamii ya wakati ujao (Foretell),Hivyo unabii huu katika hali ya kawaida ulimhusu nabii anayefuata baada Musa ambae alikuwa anakaribia kufa,nabii aliyemfuata Musa kwa kawaida(Literal) alikuwa ni Yoshua ambae kwa asili hakuwa mlawi alitokea kabila ya Yuda,hivyo Mungu alipozungumza na walawi na kusema atainuliwa nabii miongoni mwa ndugu zenu alimaanisha kiongozi nje ya kabila ya walawi.Hivyo nabii huyu alikuwa Yoshua na kinabii (Foretell)Alikuwa anatabiriwa Masihi ambaye angetokea kabila ya Yuda.

      Kimsingi nabii Musa anafanana na Yesu Kristo kwa mfano tu kwani Yesu halinganishwi na mtu,Yeye yuko juu na nibora zaidi ya Musa(Ebrania 3;1-5)
     1. Musa alikuwa Mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu (Israel)kama walivyojiombea wenyewe (Kumbukumbu 18;16,Hesabu 14;11-19),aliombea wakosaji.SasaYesu kristo ndiye mpatanishi kati ya Myngu na wanadamu kwa ulimwengu mzima (1Timotheo 2;5).
2. Musa alimjua Mungu uso kwa uso;Musa alipataneema ya kuwa na uhusiano na Mungu wa moja kwa moja tofauti na manabii wengine wote (Kutoka 33;11)Jambo ambalo Quran imelikubali(An-Nisaa 4;164) na kuwa inathibitisha ya kuwa hakuna mwanadamu aliyestahili kuongea na Mungu moja kwa moja (Ash-shuura 42;51),Yesu alimjua Mungu uso kwa uso  na alitoka kwake (Yohana 7;29,6;46).Musa alipozungumza na Mungu uso wake uliangaza (kutoka 34;29-30).,Yesu alipozungumza na Mungu uso na mavazi yake yaliangaza kama jua (Mathayo17;2). Hatusomi popote ambapo nabii wa waislamu alipatwa na Hali kama hii.

3. Musa alifanya Ishara na miujiza Mikubwa.
    Musa alifanya miujiza mikubwa sana kwa jina la Mungu kule Misri kulikuwa na ishara kama kumi,jangwani watu walilishwa kwa mana,na miujiza mingine mingi sana,hakuna nabii yoyote atakaedai kuwa anafanana na Musa kama hana muujiza hata mmoja unaofanana na Musa,tunajua kua Muhamad hakuwa na muujiza hata mmoja na ndio maana wapagani wa kiarabu walimuuliza mbona huna muujiza wowote kama wa Musa ?(Al-qasas 28;48)kama Muhamad ndiye nabii aliyefananishwa na Musa mbona hakuna ishara hata moja ya kumlinganishia na Musa? (Kmbukumbu 34;10-11).mistari hii inakazia wazi nabii atakayekuja atakavyokua kama Musa.

4. Yesu pia alifanya miujiza mikubwa.
     Kuna habari za miujiza mingi sana aliyoifanya Yesu alipokuwa duniani ambayo pia inafanana na ile ya Musa wote walikuwa na nguvu dhidi ya Bahari (Kutoka 14;21,Marko 4;39) wako mana bii waliokuwa na nguvu dhidi ya maji ya mito kama Eliye na Elisha (Yoshua 3;13,2Falme 2;14),lakini hakuna hata mmoja aliyekuwa na nguvu dhidi ya bahari,Yesu alitembea juu ya bahari ya galilaya na zaidi ya yoote upepo na bahari vilimtii jambo lililopelekea watu kumuogopa sana (Mathayo 8;27).Musa alilisha watu kwa mikate maarufu kama mana iliyonyesha kila siku juu ya nchi,Yesu alipofanya muujiza wa kulisha watu mikate (wanaume zaidi ya 500) bila kuhesabu wanawake na watoto woote walihisi na kuelewa wazi kuwa huyu bila shaka ndiye nabii yule ajae ulimwenguni (Yohana 6;14) angalia mstari huu kwa makini “.. Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.”muujiza huu alioufanya ulibainisha kuwa yeye ndiye yule aliyetabiriwa na Musa (Torati 18,15,18) kwa msingi huu Kristo anatimiza sifa zinazo tajwa katika (Torati 34;10-11)Mitume wa Kristo walielewa wazi kuwa  unabii huu ulimhusu masihi na katika mahubiri yao mara kwa mara walinukuu  mistari ile ona (Matendo 3;22) na Stefano pia alinukuu katika (Matendo 7;37),Pia ni muhimu kufahamu kama Yesu alikataliwa Musa pia alikataliwa (Matendo7;27).   
                                           
Jinsi maisha ya Musa yanavyofanana na maisha ya Kristo.
Musa
Yesu
Mtoto wa kifalme kwa farao
Mfalme wa wafalme mbinguni
Mrithi wa farao
Mrithi wa Mungu
Aliishi kama mtu maalumu ikulu
Alikuwa na enzi na utukufu mbinguni
Aliishi kama mtu dini jangwani
Aliishi kama mtu duni duniani
Mchungaji wa kondoo jangwani
Mchungaji mwema wa watu woote
Alijinyenyekeza na kuwa mpole
Mnyenyekevu na mpole
Alipata mateso na kuwa mbali na ndugu
Aliteseka Msalabani na akiwa peke yake
Ni mjumbe wa agano la kale
Ni mjumbe wa agano la kale
Mpatanishi wa Israel
Mpatanishi wa ulimwengu mzima
Aklitoa sheria
Alileta Neema na kweli na uzima
Alifanya miujiza mingi mikubwa
Alifanya miujiza mikubwa ya kushangaza
Alimjua Mungu uso kwa uso
Alikuwa Mungu na alitoka kwa Mungu
Kiongozi wa Israel
Ni kiongozi wa kanisa

     Ni muhimu kufahamu kuwa Muhamad hakutabiriwa kabisa katika torati na manabii na injili kwa kweli kama angetabiriwa tungemwamini,sisi tunaamini maandiko sana tusingeweza kukanusha kile ambacho tunakijua lakini hatuwezi kushuhudia uongo labda muhamad mwenyewe angelikuwepo angetusaidia kujua kuwa ametokea wapi bahati mbaya hayuko hai lakini Kristo yu hai leo kaburi lake liko wazi,yeye ni wa kutumainiwa na anastahili kuabudiwa ni vema kumtukuza yule ambaye Mungu amemtukuza,Yeye ni alfa na omega hatuoni mwingine zaidi yake.
    Niwaase tu wanaharakati wa kiislamu waachane na tabia ya kupenda kuyasingizia maandiko kwa kutafuta kama yana mtaja muhamad ukweli ni kuwa Muhamad hayumo katika maandiko yoyote yaani Torati,manabii na injili,yeye yumo katika Quran na khadithi tu hatujui atokako.

Je Muhamad ndiye Msaidizi mwingine? (Yohana 14;26).
     Katika swala zima la kutafuta visingizio kuwa Muhamad alitabiriwa katika Biblia waislam hudai kuwa Yesu alizungumza au kutabiri habari za kuwaletea msaidizi mwingine (Mfariji) mwingine ambaye wao hudai ni Muhamad na quran inathibitisha upotofu huo!
     Madai haya ya waislamu kuwa Muhamad ametabiriwa katika Biblia yanatokana na ahadi ya Yesu kwa wanafunzi wake ambayo ahadi ambayo imekaririwa mara nne katika injili ya Yohana,kuwa baada yake atakuja mwingine atakayetumwa  kutoka kwa Mungu,jina lake ni mfariji(mshauri
/msaidizi) na wanadai huyo ni Muhamad nabii wao jambo ambalo liko wazi hata kwa wakristo wa kawaida kuwa anayezungumzwa hapo ni roho mtakatifu! Hii inatokana na waislamu kudanganyika kupitia aya katika (An- nisaa 4;157)aya hii hudai kuwa nabii wao ametabiriwa ndani ya Torati na Injili,hebu tusome vizuri (Yohana 14;26) unasema hivi
  • “….Lakini atakapokuja huyo msaidizi,huyo Roho Mtakatifu ambaye Baba atampeleka kwa jina langu atawafundisha yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia”
  • Soma pia Aya zifuatazo (Yohana 16;7,14;16,15;26).
   Waislamu hutumia aya hizo na kuzitumia kumthibitisha Muhamad kwa madai kuwa yeye ndiye aliuongoza ulimwengu katika kweli na kwa sababu ya matumizi ya maneno nafsi “Yeye huyo”nk.wanahoji kuwa semi hizi zinamhusu mtu na sio Mungu,pia haimuhusu Roho mtakatifu kwa sababu  kwa sababu yeye amekuwepo tu wakati woote na hata Daudi aliomba kuwa asiondolewe huyo (zaburi 51;11) na Yohana alijazwa tangu utoto akiwa tumboni,(luka 1;15).
     Jibu la maswala haya ni rahisi sana ningependa kuwarudisha tena wahubiri wa kiislam kuwa biblia haisomwi kama Quran au gazeti au kitabu kingine hii (biblia ina kanuni zake kwanza wasome kifungu kizima (Principle of context),Pia wazingatie kanuni ya kulinganisha (Principle of Hermonization),Hii ni kanuni ya ushahidi wa andiko zaidi ya mawili,maandiko yote yaonyesha wazi kuwa Yesu alikuwa ana mzungumzia Roho mtakatifu,yako mambo ambayo yanabainisha wazi kuwa maandiko hayo hayamhusu Muhamadi ambaye alikuja karne sita baada ya Kristo angalia vizuri habari za Roho matakatifu,Roho mtakatifu atakaa nasi hata milele(Yohana 14;16 ).Muhamad alikufa hayuko nasi milele,Roho mtakatifu hatatambuliwa na watu wa dunia hii,wala kupokelewa anakaa ndani yetu (Yohana 14;17)Atatumwa kwa jina la Yesu na kutukumbusha au kutufundisha mambo ya Kristo (Yohana 14;26).Roho mtakatifu atamtukuza Yesu,atanena atakayoyasikia kwa Yesu,(Yohana 16;13-15).Tunasikitika kuwa Muhamad alijitikuza mwenyewe wala hakunena yale aliyoyanena Yesu,Bali yakwake mwenyewe. Hivyo Muhamad sio Msaidizi mwingine,kwani hakai nasi milele na Yuko kaburini amekufa Roho yuko milele,Jana leo na milele.

 Aidha wana harakati wa Kiislamu Katika kutafuta kutetea hoja hii walikwenda kutafuta neno wanalofikiri kwa asili linamhusu Muhamad neno hili la asili la kiyunani ni neno “Paracklutos” ambalo maana yake ni “Praise one” ambalo kwa kiarabu ni Muhamad.Hata hivyo kwa asili neno hilo wamelikosea neno linalotumiwa katika Biblia ya kiyunani ni “Paracletos” ambalo maana yake ni Mfariji,Mshauri,au Msaidizi ambalo hutumika kwa Roho mtakatifu na si kwa Muhamad,hivyo mkristo uwe macho na maneno hayo yanapotumiwa na waislamu kwa lengo la upotoshaji Mungu atupe neeema ya kuugundua uongo wao na kudumu katika kweli katika jina la Yesu.

Je Yesu alikuwa Mwislamu?



Yako madai ya baadhi ya wanaharakati wa kiislamu wanaodai kuwa Eti bwana Yesu alikuwa Muislamu kwa madai kuwa alikuwa akiingia katika Masinagogi (yaani misikiti ya wayahudi) Luka 4;16,Pia kwa sababu alikuwa anaomba akiwa anasujudia (Mathayo 26;38-44) Maandiko haya kwa waislamu ndio kigezo kikuu cha kuwa Yesu ni mwislamu.Madai haya ni ya ajabu sana kwani yanapingana na ile kweli iliyomo katika quran na Khadithi za Kiislamu Kulazimisha kuwa Yesu alikuwa muislamu kunaanza kutufanya tukubali kuwa Qurani ni kweli kuwa si kitabu kinachoongoza katika kweli kwani ni Qurani yenyewe ndiyo inayosema kuwa Muhamad aliamuriwa awe wa kwanza miongoni mwa waliosilimu soma (Surat al-anaam 6;14)……. “Hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu……” ayah ii inathibitisha wazi kuwa Muislamu wa kwanza katika wanaume aliyesilimu alikuwa Muhamadi mwenyewe, aidha katika  kitabu cha cha historia ya Maisha ya nabii muhamad uk 18 kifungu cha pili cha shekh Abdulla Saleh Farsy kinasema ….Basi Mwislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke akimaanishwa bi khadija unaona sasa linakuwa jambo la kushangaza kuona wana mujahidini wakipingana na maulamaa wao au wanazuoni wenzao au hata quran aidha wanaharakati hawa wa kiislamu kumbe wanataka kutuambia kuwa wayahudi nao ni waislamu? Na kama hivyo ndivyo je quran inafundisha nini kuhusu wayahudi? Soma  Surat al maida-5;51 inasema hivi….. “Enyi mlioamini msiwafanye mayahudi na wakristo kuwa rafiki zenu (wa kuwapa siri zenu) wao kwa wao ni marafiki.Na miongoni mwenu atakayefanya urafiki nao basi huyo atakuwa pamoja nao na hakika allah hawaongozi watu madhalimu….” Qurani inaonyesha kuwa Hakuna uhusiano wa waislamu na wayahudi wala wakristo Yesu alikuwa Myahudi na hivyo kuingia katika msikiti wa wayahudi ilikuwa ni desturi yao. Je muhindu akiingia kwenye msikiti wa wahindu ni mwislamu kwa sababu hiyo?

 Musa na Harun pia hawakuwa waislamu wala hawakuanzisha Dini

      Tukumbuke kuwa Yesu alikuja kutafuta  na kuokoa kile kilichopotea hivyo ilikuwa ni lazima aingie kwenye majengo ya watu waliopotea ili apate kuwafundisha Luka 4;17-30, hata hivyo mara nyingi watu hao wa kenye masinagogi walijaa ghadhabu na walimtoa nje ya mji wakimpeleka katika ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa wapate kumtupa chini.Luka 19;45-47 Yesu aliingia katika Hekaluni akaanza kuwatoa nje wale waliokuwa wakifanya biashara akawaambia imeandikwa nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi naye akawa akifundisha kila siku hekaluni je alikuwa dini   gani? Aidha ikumbukwe pia kuwa Paulo mtume pia aliingia katika masinagogi hayo Matendo 17;1-2 na pia ilikuwa ni desturi yake je wanaharakati wa kiislamu wanataka kutuambia kuwa Paulo naye pia alikuwa mwislamu? Kwa kuwa tu aliingia katika sinagogi? Mbona huwa hawadai kuwa Paulo mtume ni mwislamu? Aidha ni Muhimu kukumbuka kuwa mafundisho ya bwana Yesu yalikuwa yakipingana vikali na watu wa Masinagogi Yesu alikemea tabia zao za kupiga panda watoapo sadaka yaani walikuwa wanafiki Mathayo 6;2.,aliwakemea kwa kupenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pande za njia ili waonekane na watu hii nayo ilikuwa tabia ya kinafiki (Mathayo 6;5-15) aidha Bwana Yesu alifundisha kusali kwa kupitia sala ya bwana Baba yetu uliye mbinguni……….  Jambo ambalo waislamu hawalifuati kabisa,Mwishoni watu wa masinagogi walimfukuza Yesu kabisa wakiwa wamejaa ghadhabu ikiwa Yesu alikuwa mwislamu mwenzao iweje walimfukuza? Quran inasema  Wanafiki wamejenga msikiti wa kuleta udhia na kutia nguvu ukafiri……… Hivyo aya hii inathibitisha kwamba misikiti ni ya watu wanafiki,Pia quran  inayataja Masinagogi kuwa ni nyumba tofauti na Misikiti ona Surat al-hajj 22;40 Ambao wametolewa majumba (mjini)mwao pasipo haki ila kwa sababu wanasema  mola wetu ni mwenyezi mungu na kama mwenyezi Mungu asingali wakinga watu baadhi yao kwa wengine bila shaka yangalivunjwa MAHEKALU (Swaamiu) na MAKANISA (Wabiya-unw) na nyumba nyingine za ibada MASINAGOGI (Wasalawatunw) na MISIKITI (Masaajidu) ambamo jina la mwenyezi Mungu hutajwa kwa wingi…….. jambo linalo shangaza ni kuwa Qurani inataja masinagogi tofauti na misikiti kulikoni basi kama sinagogi ni msikiti?

    Biblia haitufundishi kuwa Yesu alikuwa Mwislamu inatuambia Yesu ni mwana wa Mungu soma (Mathayo 3;16-17,Yohana 17;1,8;54,)aidha Tunafundishwa kuwa Bwana Yesu ndiye mwanzilishi wa kanisa katika Mathayo 16;18 anasema  Nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitalishinda”Yesu aliyasema hayo kabla Muhamad hajazaliwa wala uislamu haujaanza aidha ufunuo wa Yohana sura ya pili yoote  Yesu anazungumza na kanisa na anatofautisha na sinagogi. Hivyo Kanisa limeanzishwa na Bwana. Maadui wakubwa wa waislamu ni mayahudi Surat al maida 5;82 na Yesu alikuwa myahudi leo Mujahidina wanasemaje Yesu alikuwa Mwislamu? Na Quran inasema maadui zao ni wayahudi na biblia inasema Yesu alikuwa Myahudi soma (Yohana 4;9).

UPI NI MUONGOZO WA MUNGU WA KWELI QURAN AU BIBLIA?



      Kabla ya Kushughulika na jambo lolote ni muhimu tukafahamu upi ni muongozo kamili wa Mungu,kila dini duniani ina Muongozo wake,lakini sihitaji kupoteza muda kushughulika na miongozo ya watu wengine kwani wao wameridhika na miongozo yao na huwa hawana habari na miongozo ya watu wengine lakini Nitazungumzia zaidi Quran kwani waislamu wana chokochoko hawajatulia na kuridhika na Muongozo wao kama ilivyo kwa Wahindi,Buddha,Shinto,nk. Wala sina shaka na Muongozo wangu yaani Biblia kwa sababu ni Muongozo kamili unaojitegemea na ambao mtu akiufuata atafanikiwa tu ndivyo Mungu alivyomhakikishia Yoshua soma Yoshua (Yoshua 1:7-8)pia Daud alimuhusia Suleman (Ifalme 2;2-3) wala sina wasiwasi na injili kwani ni uongozi kamili wa Mungu kupitia Masihi Yesu hakuna mtu mwenye shaka na Yesu ni mtakatifu na muadilifu alipewa kitabu Ndiyo injili hakuna maswali injili inatosha kabisa kumpeleka mtu mbingini huwezi kutenganisha injili na Yesu yeye ni njia kweli na uzima!


 Lakini nina mashaka na qurani kuwa ni kitabu kisicho jitosheleza kabisa hakiongozi mbinguni hakina nguvu ya kutuokoa na dhambi kuondoa hatia au kutia matumaini ndani ya kurani utakutana na aya zinazo kutia moyo kuendelea kuangalia torati na injili kama Muongozo wa kweli wa Mungu kwa vipi?Quran huiita Tourat na injili “Vitabu vyenye nuru” soma (al Imran 3:184,Fatir 35:25)Aya nyingi za Qurani zinatuambia kwamba torati na injili zimetoka kwa Mungu soma (al-Baqara 2;89 al anam 6:92) humo kuna uongozi na Nuru(al-maida 5;44,46) Wengi wa wafasiri maarufu wa Quran kama Al-Jalalayn,Al-Fakhr,Al-Razi,Al-Tabari na Al-Baydawi woote wanakiri kuwa kulingana na Qurani Torati inaitwa kitabu cha Mwenyezi Mungu (al Imran 3;23)na kitabu kibainishacho kila linalohitajiwa(as saafat 37;117).Hata hivyo tunajua kuwa baadhi ya wanaharakati wa kiislamu wanaamini kuwa Torati na injili zimepotoshwa na zimetiwa mkono hivyo haziaminiki kama hivyo ni kweli uongo huu uliingizwa lini? Quran  inataka watu waiamini torati na injili iweje watu waamini vitu vilivyopotoshwa?hii ina maana mpaka quran inaandikwa vitabu hivyo vilikuwepo na vinaaminika  quran inazidi kutia moyo tuviamini vitabu hivyo ona (al-baqara 2;136,al Imran3;84 an nisaa4;136  )Qurani inawaagiza waislamu kututafuta sisi wenye ujuzi wa torati na injili ikisema hivi Waulizeni wenye kumbukumbu (za vitabu vya mwenyezi Mungu vya kale )ikiwa ninyi hamjui (an nahil 16;43,al-Anbiyaa 21;7) sasa hebu tujiulize Quran ingeelekeza hayo kama vitabu hivi vimepotoshwa?kama haitoshi quran inatuomba sisi watu wa kitabu torati na injili kuvirudia vitabu vyetu soma( al-maida 5;47,68)Kama vitabu hivi vimepotoshwa huoni kuwa kuran inatupoteza zaidi kama inaagiza kuvirudia?Hivyo Vitabu hivi havingeweza kupotoshwa kamwe  baada ya kuandikwa quran,Kuna uthibitisho jinsi maandiko matakatifu  ya siku zetu yanapolinganishwa na torati na injili zilizoandikwa karne nyingi kabla ya Quran zinaonyesha hakuna tofauti wala badiliko wala upotovu na kwabahati nzuri hati hizi za mkono zinapatikana katika maktaba za umma na majumba ya makumbusho,Mtu yeyote anayeamini quran ni lazima akubali kwamba maandiko matakatifu hayajapotoshwa.

 Baadhi ya watu wanaweza kuendelea kupinga wakidai kuwa quran inaonyesha upotovu huo yaani Tahrif kwa kiarabu lakini maulamaa au wasomi wa kiislamu wanasemaje kuhusu hilo? Wanasema hivi upotovu uko wa aina mbili 1. Kuingiza uongo katika maandiko na 2. kupinda au kupotosha maana ya maandishi, Maulamaa hawakubaliani na lile la kwanza ila hili la pili ambalo hata wanaharakati wa kiislamu wanalifanya sana na hukumu yao inawangoja, katika kitabu kinachohusu imani ya Mungu mmoja ambacho ni sehemu ya Sahih, imamAl-bukhari anaeleza maana ya neno tahrif humaanisha ubadilishaji,Hata hivyo hakuna awezaye kubadili herufi yoyote katika kitabu cha Mungu, Katika kitabu chake cha maelezo juu ya an-Nisaa4;46,Imam al-Fakhr Al-raz anasema hivi…. “Maana ya upotovu Tahrif ni kuingiza shaka la kipuuzi na maelezo yenye makosa na kubadili neno liache maanayake ya kweli ili ilete maana isiyo na msingi kwa kutumia hadaa za kimaneno kama vile wazushi wanavyofanya  sasa na zile aya zinazopingana na mafundisho ya madhehebu yao wenyewe hayo ndiyo maoni yalito hakika zaidi” na hiki ndicho wanaharakati wa kiislamu wanavyoifanyia biblia  hii ndiyo Tahrif  hivyo hakuna abadilishaye maneno ya (waadi wa )Mwenyezi Mungu (Surat al anam 6;34),Hivyo quran inathibitisha kuwa Torat na injili (Biblia) ni mwongozo na Nuru, upi ni muongozo wa Mungu wa kweli ni Biblia bila shaka Maswali?................