Kabla
ya Kushughulika na jambo lolote ni muhimu tukafahamu upi ni muongozo kamili wa
Mungu,kila dini duniani ina Muongozo wake,lakini sihitaji kupoteza muda
kushughulika na miongozo ya watu wengine kwani wao wameridhika na miongozo yao
na huwa hawana habari na miongozo ya watu wengine lakini Nitazungumzia zaidi
Quran kwani waislamu wana chokochoko hawajatulia na kuridhika na Muongozo wao
kama ilivyo kwa Wahindi,Buddha,Shinto,nk. Wala sina shaka na Muongozo wangu
yaani Biblia kwa sababu ni Muongozo kamili unaojitegemea na ambao mtu akiufuata
atafanikiwa tu ndivyo Mungu alivyomhakikishia Yoshua soma Yoshua (Yoshua 1:7-8)pia Daud alimuhusia
Suleman (Ifalme 2;2-3) wala sina
wasiwasi na injili kwani ni uongozi kamili wa Mungu kupitia Masihi Yesu hakuna
mtu mwenye shaka na Yesu ni mtakatifu na muadilifu alipewa kitabu Ndiyo injili
hakuna maswali injili inatosha kabisa kumpeleka mtu mbingini huwezi
kutenganisha injili na Yesu yeye ni njia kweli na uzima!
Lakini nina mashaka na qurani kuwa ni
kitabu kisicho jitosheleza kabisa hakiongozi mbinguni hakina nguvu ya kutuokoa
na dhambi kuondoa hatia au kutia matumaini ndani ya kurani utakutana na aya
zinazo kutia moyo kuendelea kuangalia torati na injili kama Muongozo wa kweli
wa Mungu kwa vipi?Quran huiita Tourat na injili “Vitabu vyenye nuru” soma (al Imran 3:184,Fatir 35:25)Aya nyingi za Qurani zinatuambia kwamba
torati na injili zimetoka kwa Mungu soma (al-Baqara
2;89 al anam 6:92) humo kuna uongozi na Nuru(al-maida 5;44,46) Wengi wa wafasiri maarufu wa Quran kama
Al-Jalalayn,Al-Fakhr,Al-Razi,Al-Tabari na Al-Baydawi woote wanakiri kuwa
kulingana na Qurani Torati inaitwa kitabu cha Mwenyezi Mungu (al Imran 3;23)na kitabu kibainishacho
kila linalohitajiwa(as saafat 37;117).Hata hivyo tunajua kuwa baadhi
ya wanaharakati wa kiislamu wanaamini kuwa Torati na injili zimepotoshwa na
zimetiwa mkono hivyo haziaminiki kama hivyo ni kweli uongo huu uliingizwa lini?
Quran inataka watu waiamini torati na
injili iweje watu waamini vitu vilivyopotoshwa?hii ina maana mpaka quran
inaandikwa vitabu hivyo vilikuwepo na vinaaminika quran inazidi kutia moyo tuviamini vitabu
hivyo ona (al-baqara 2;136,al Imran3;84
an nisaa4;136 )Qurani inawaagiza
waislamu kututafuta sisi wenye ujuzi wa torati na injili ikisema hivi Waulizeni
wenye kumbukumbu (za vitabu vya mwenyezi Mungu vya kale )ikiwa ninyi hamjui (an nahil 16;43,al-Anbiyaa 21;7) sasa
hebu tujiulize Quran ingeelekeza hayo kama vitabu hivi vimepotoshwa?kama
haitoshi quran inatuomba sisi watu wa kitabu torati na injili kuvirudia vitabu
vyetu soma( al-maida 5;47,68)Kama
vitabu hivi vimepotoshwa huoni kuwa kuran inatupoteza zaidi kama inaagiza
kuvirudia?Hivyo Vitabu hivi havingeweza kupotoshwa kamwe baada ya kuandikwa quran,Kuna uthibitisho
jinsi maandiko matakatifu ya siku zetu
yanapolinganishwa na torati na injili zilizoandikwa karne nyingi kabla ya Quran
zinaonyesha hakuna tofauti wala badiliko wala upotovu na kwabahati nzuri hati
hizi za mkono zinapatikana katika maktaba za umma na majumba ya makumbusho,Mtu
yeyote anayeamini quran ni lazima akubali kwamba maandiko matakatifu
hayajapotoshwa.
Baadhi ya watu wanaweza kuendelea kupinga
wakidai kuwa quran inaonyesha upotovu huo yaani Tahrif kwa kiarabu lakini maulamaa au wasomi wa kiislamu wanasemaje
kuhusu hilo? Wanasema hivi upotovu uko wa aina mbili 1. Kuingiza uongo katika
maandiko na 2. kupinda au kupotosha maana ya maandishi, Maulamaa hawakubaliani
na lile la kwanza ila hili la pili ambalo hata wanaharakati wa kiislamu
wanalifanya sana na hukumu yao inawangoja, katika kitabu kinachohusu imani ya
Mungu mmoja ambacho ni sehemu ya Sahih, imamAl-bukhari anaeleza maana ya neno
tahrif humaanisha ubadilishaji,Hata hivyo hakuna awezaye kubadili herufi yoyote
katika kitabu cha Mungu, Katika kitabu chake cha maelezo juu ya an-Nisaa4;46,Imam al-Fakhr Al-raz anasema
hivi…. “Maana ya upotovu Tahrif ni kuingiza shaka la kipuuzi na maelezo yenye
makosa na kubadili neno liache maanayake ya kweli ili ilete maana isiyo na
msingi kwa kutumia hadaa za kimaneno kama vile wazushi wanavyofanya sasa na zile aya zinazopingana na mafundisho
ya madhehebu yao wenyewe hayo ndiyo maoni yalito hakika zaidi” na hiki ndicho
wanaharakati wa kiislamu wanavyoifanyia biblia
hii ndiyo Tahrif hivyo hakuna
abadilishaye maneno ya (waadi wa )Mwenyezi Mungu (Surat al anam 6;34),Hivyo quran inathibitisha kuwa Torat na injili
(Biblia) ni mwongozo na Nuru, upi ni muongozo wa Mungu wa kweli ni Biblia bila
shaka Maswali?................
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni