Safari
yangu ya Marekani
Juni 6th -20th
2014 Nilipata nafasi ya Kutembelea taifa kubwa kabisa Duniani yaani Marekani,
kupitia mpango maalumu wa shule yetu Living Stone Boys’ Seminary wa kutembelea
na kupaleka vijana katika Mataifa yaliyoendelea ili kuwaingizia Maono na
mitazamo ya kimataifa kwa kusudi la kuja kuliimarisha taifa letu na kuliletea
maendeleo.
Mpango huu uliandaliwa
na Meneja wa shule na mke wake yaani Rev. Andrew Park na Eunreen Kim Mpango huu
tuliuita USA VISION TRIP. Mchungaji Park Yeye ni Mwanzilishi wa shirika la
Kikristo hapa Nchini liitwalo Mission With Christ ambao ni wamiliki wa Chuo Cha
Biblia kilichopo Kange mjini Tanga kijulikanacho kama Tanga Christian Bible
College (TCBC). Na pia shule ya wavulana ya sekondari iliyoko mjini Muheza
ijulikanayo kama Living Stone Boys’ Seminary
Mchungaji Park alikuwa
na mpango kwamba walimu na wanafunzi wawe na Mwanga wa kutosha kuhusu ujuzi wa
kimataifa ili kujua nini kinapaswa kufanyika katika taifa letu na kuliletea
maendeleo.
Mapema mwezi wa
December 2013 Uongozi wa shule ulinitaka mimi kama mkuu wa shule kuwaandikia
barua wazazi wote ili kwamba waweze kukubaliana na mpango wa kuwaruhusu vijana
wao watakaochaguliwa na shule, kutokana na uadilifu na uwezo mzuri wa kitaaluma
wasaini kwamba watakubaliana na mpango wa shule na kusaini kuwa watakuwa tayari
kukubali endapo watoto wao watateuliwa na uongozi kwaajili ya kwenda Marekani,
wakati huu binafsi nilijua kuwa ni safari itakayowahusu wanafunzi tu.
Niliandaa barua hizo na
wazazi walizijibu, na wengi walikubaliana na wazo hilo, Baadaye uongozi wa
shule tena walinitaka kama mkuu wa shule kuchagua vijana nane walio na nidhamu
na wenye uwezo mzuri kitaaluma nani niliwachagua vijana hao mmoja akiwa ni Rais
wa serikali ya wanafunzi
Vijana waliochaguliwa
walikuwa ni
·
Yohana Martin Komba - Kutoka Korogwe
·
Onstard Mashauri
- Kutoka Arusha
·
Imani Peter Mgazija – Kutoka Tanga
·
William Boniventure. – Kutoka Dar es Salaam
·
Baraka Kolombo. – Kutoka Dar es Salaam
·
Athumani ulimwengu. – Kutoka Muheza
·
Athour Chikoka. – Kutoka Muheza
·
Herbert Gumbo. – Kutoka korogwe
Niliandaa barua za kuwaombea vijana hao Hati za kusafiria na kila
mzazi alihakikisha kuwa anajitahidi kupata Hati ya kusafiria kwa vijana wao,
kupitia ushirikiano uliokuweko kila kijana alifanikiwa kupata hati ya kusafiria
yaani passport, Baada ya zoezi hili kukamilika nilitoa ripoti kwa uongozi wa
shule yaani Meneja kuwa hati za kusafiria kwa vijana ziko tayari.
Katika namna ya kushangaza kabisa nikiwa sina hili wala lile huku
nikishughulikia maswala ya vija na hao kwa moyo mkubwa kabisa Meneja aliniuliza
Mchungaji Una Passport ? yaani una hati ya kusafiria? Jibu lilikuwa Ndiom kwani
niliandaa Passport yangu tangu mwaka 2011 nilipokuwa nimepata Mwaliko wa kwenda
Msumbiji kwa safari za injili, hata ingawaje sikupata neema ya kukanyaga
Msumbiji mpaka sasa. Lakini wakati huu nilipata msisimko mkubwa kwamba hata na
mimi pia nimekuwa miongoni mwa hao wanaokwenda Marekani ? Nilimtikuza Mungu na
kuanza kuwaza juu ya taifa hilo kubwa ambalo kila mmoja alikuwa anatamani
kulitembelea, wakati huu nilijiuliza kuwa ni mwezi December tu 2013 Kaka yangu
alipata Nafasi ya kutembelea Israel Nchi ambayo hata mimi nilitamani sana
niitembelee kutokana na kujihusisha na maswala ya kumtumikia Mungu, Lakini
nilitambua kuwa Mungu alitaka kuonyesha uwezo wake kuwa wakati wa Bwana
kutubariki umefika.
Nilitamani kufika Marekani, nilifurahi niliwaza sana na nilianza
kuushibisha moyo wangu mawazo ya kutosha na ujuzi mkubwa kwa taifa hilo
Nilitambua kuwa marekani ni moja ya mataifa makubwa sana Duniani, ni taifa
ambalo limeendelea, limeendelea katika maswala ya Sayansi na teknolojia pamoja
na uchumi mkubwa, Nilitambua kuwa Marekani ni muunganiko wa Mataifa mengi
makubwa yapatayo 48 yanayounda kwa pamoja sehemu kubwa ya bara la Amerika ya
Kaskazini, nilitambua pia inaunganishja jimbo la Alaska na visiwa maarufu vya
Hawaii na hivyo kufanya nchi zipatazo 50, Ni taifa kubwa sana ndio nilitambua
na nilitamani kwenda ili nijifunze mengi kwa gfaida ya kizazi chetu na
maendeleo ya taifa letu.
Ni kwa sababu hiyo nilitamani sana kuandika maswala mengi nitakayokuwa
nimejifunza huko ili yamkini yaweze kuwa kumbukumbu na kusaidia Maendeleo ya
Taifa letu, Hivyo katika habari hii nataka kuelezea kwa ufupi yale
niliyojifunza, kwa makusudi ya kuwatia moyo wanafunzi na wananchina viongozi wa
Tanzania kufanya kazi kwa bidii na matumaini makubwa kwa imani kuwa kile
ambacho wamarekani wameweza na kukifanya tunaweza na tutafanya naam na makubwa
kuliko ya Marekani tutaweza.
Maandalizi
ya safari
Kama nilivyogusia hapo
awali kuwa maandalizi ya safari yalianza kwa utafutaji wa Hati za kusafiria,
sasa nilikuwa nimetambua wazi kabisa kuwa kuna umuhimu wa kila raia wa Tanzania
hata vijana kuwa na Hati ya kusafiria, nilijifunza kuwa hili linapaswa kuwa
kitu cha kawaida tu, nilikumbuka kuwa kaka alipata shida kiasi katika kuandaa
hati ya kusafiria kwenda Israel, kwa vile kutokea kwa safari na mpaka safari
yenyewe kulikuwa na muda mfupi, Mimi nilikuwa na hati ya kusafiria mapema
zaidi, lakini niliona wazazi na wanafunzi wakihangaika kuipata, na hatiamaye
walizipata hati zao za Kusafiria Passport
Moja ya swala kubwa na
mtazamo mkubwa ambao wengi tunakuwa nao na hata mimi nilifikiri nitakutana nao
ni kuwepo kwa rushwa wakati wa ufuatiliaji wa hati hiyo ya kusafiria, lakini
jambo lililonifurahisha ni kwamba ninaweza kukiri wazi kuwa katika Idara ya
uhamiaji rushwa ilikwishwa kuzikwa miaka mingi, hakukuwa na kudaiwa rushwa,
hakukuwa na mazingira yoyote ya kuhonga ambayo niliyatazamia, zaidi ya malipo
ya kawaida ya 50,000/- ukishakuandaa vielelezo vyote wavitakavyo pamoja na
picha za passport size wazitakazo ukweli ni kuwa hakuna urasimu katika idara
hii. Haya tuliyashuhudia.
Maandalizi yaliendelea
huku kukiwa na mawasiliano ya kudumu na wazazi katika kuhakikisha kuwa vijana
wao wanakuwa salama na safari inafanikiwa, baada ya kila kijana kufanikiwa
kupata hati ya kusafiria, hatua iliyofuata ilikuwa ni ukataji wa Tiketi,
Ukataji huu wa tiketi hufanyika kwa njia ya kielekroniksi kupitia mtandaoni,
unaweza kuangalia mashirika ya ndege ya aina mbalimbali duniani, na usalama
wake na unaweza pia kuangalia unafuu wa bei, tulichagua Ethiopian Airlines na
wote tulipatia tiketi ya Ndege hiyo, na tiketi ilionyesha kuwa tutaondoka Dar kupitia Adds ababa kisha Fiumucino
Italy na kisha Washngton Dulles , tayari tulikuwa na furaha kuwa tutakanyaga
Ethiopia na Ulaya yaani Italy na kisha Marekani kila mmoja alikuwa na moyo wa
Shauku wa kutaka kufika huko.
Baada ya upatikanaji wa
Tiketi tukio lilolofuata lilikuwa ni upatikanaji wa visa ya kimarekani, kwa
mujibu wa Maelekezo tuliyopewa ilikuwa
tunapaswa kufika ubalozi wa Marekani pamoja na hati zetu za kusafiria na wazazi
wa vijana na kuhojiwa maswali kadhaa ndipo baada ya wiki moja tuweze kupatiwa
visa hii ni kama kibali na ruhusa yakuwako katika nchi ya watu, tulijiandaa na
tulimuomba Mungu kwani tuliwahi kusikia na tunafahamu kuwa watu wengi hunyimwa
visa kutokana na kutokutosheleza vigezo husika vinavyotazamiwa na wenye taifa
lao, kwa kweli tulisafiri kwa pamoja na tukafika Dar na kibasi chetu cha shule
tukiwa na wanafunzi wote, tuliamua kutafuta nyumba nyuma ya ubalozi wa Marekani
yaani maeneo ya msasani hivi ili ifikapo asubuhi iwe rahisi kwetu kufika
Ubalozi wa marekani pale Drive in Morroco, asubuhi tulijihami na tukafika
ubalozi wa Marekani, ni mahali panye ulinzi mkali hivi kwa hiyo kihofu cha
kimazingira kilianza kutuingia lakini tulijitia moyo kuwa tuna Mungu, tulifika
nje ya Ubalozi tukiwasubiri wazazi kwani tuliwaambaia kuwa hatutaingia mpaka
wote wamefika tulisubiri njae na walipokuwa wote wamefika tuliingia ndani,
askari wa mlangoni baadaya ukaguzi na kuzuia simu zote za mkononi na vifaa
vingine ambavyo husababisha alamu kulia kama mapene mikanda n.k vibaki na
tuliingia ndani, wazazi waliambiwa wasubiri nje ya ndani ya ubalozi huo,
kulikuwa na foleni watu walikuwa wakikusanya hati zao na kuitwa kwa majina na
kuhojiwa wengine walikuwa wakilia kwa vila walikataliwa, lugha iliyokuwa
ikitumika sasa ni kingereza tuliingiwa na hofu tuliomba Mungu kimoyomoyo
tufanikiwe, shughuli ilikuja tulipopeleka Documents zetu kwa Muhusika huyu
alikuwa dada wa Kitanzania kwa mtazamo wetu, alikuwa mkali na mwenye dharau
alizitupilia mbali hati zetu na kukataa picha zetu kuwa hazifai kwa visa ya
Marekani, hatukuwa tumeelewa, kila mtu alikuwa mgeni na maswala hayo hatuna
uzoefu Missionary Park hakuweko wakati huu, tulifukuzwa bila ya kuelekezwa
lolote tulitoka nje moja kwa moja na tupofika getini tuliitwa tena, nilikuwa
mimi na vijana tu Mama mmoja wa kizungu
alituelewesha sababu za kukataliwa kwetu tulibaini picha zetu zilikuwa mbaya
wamarekani wanataka picha ya kipande Passport size yenye Inchi mbili kwa mbili
yaani two by two na Background yake yaani ukuta wa nyuma unapaswa kuwa mweupe,
tulielekezwa kwenda kupiga picha hizo katika duka moja kubwa pale mikocheni
shipwright alikuweko muhindi mmoja ambaye alikuwa anahusika na kupiga picha
tulielekezwa hapo, wakati tukitoka nje ya Ubalozi punde nilionana na Askofu
Mkuu wa Kanisa la Assemblies Of God Barnabas Mtokambali, tulisalimiana na alinieleza
kuwa amekuja kushughulikia visa yake kwa upya kwamba atakwenda Marekani
karibuni, alinisaidia kunielekeza sehemu hiyo ya kupiga picha za visa,
nilimweleza kusudi la safari yangu na vijana huko marekani alitubariki na
tulikwenda kupiga picha, Roho ilikuwa juu juu kwa vile tulipewa dakika chache
sana za kukamilisha kwa vile siku yenyewe ilikuwa alhamisi na walidai ijumaa
huwa awafanyi kazi na wangefunga muda wa saa tano, tulijitahidi kufanya hivyo
tukisaidiwa na Mzazi wa Williuam Biniventura, zoezi lilifanikiwa na tulirejea
tena Ubalozini, Mungu alikuwa ametusaidia aliondoa hofu zote, watu wengi sana
walikuwa wamepungua kazi ilikuwa imefanyika kwa haraka hivyo ulikuwa ni kama
wakati wetu kuhudumiwa, sikumfurahia kabisa dada Yule wa kitanzania nilimchukia
kwa muda nilishindwa kuelewa alikuwa ana maana gani lakini nilipata somo kwamba
kuna umuhimu wa kukamilisha mambo yote ya watu unayoagizwa kama yalivyo ili
kuepusha usumbufu,
Sasa ulikuwa wakati
wakuitwa kwa mahojiano na niliulizwa maswali mengi sana na afisa ubalozi huyu
alikuwa kaka mnene na mrefu ni mmarekani
alikuwa muelewa sana alihojo kila alichokihoji na nilijibu kwa ujasiri
niliwa na utulivu moyoni vijana walikuwa wakisikiliza mahojiano hayo na tayari
ilikuwa ni kama wana majibu ya kujibu kila nilichoulizwa ndicho walichoulizwa
na wazazi hawakuruhusiwa kuingia ndani, tulishangaa ni kwanini waliwatesa
kuwaito kutoka mbali, lakini visa yam domo ilikuwa imekubaliwa na tuliacha
passport zetu kwaajili ya matengenezo ya visa.
Pichani ndio visa ya
Marekani kama inavyoonekana ikiwa imegongwa katia hati yangu nya kusafiria visa
hii ilituruhusu kutoka 30th April 2014 – 29 April 2015 ilikuwa rhusa
ya Mwaka mzima sisi tulikaa wiki mbil.
Mafanikio ya kupatikana kwa visa
yalitupa ndoto zaidi ya kuiona Marekani , tuliona sasa safari ya Marekani
haikuwa ndoto tu bali sasa ilikuwa ni halisi
Safari ya Marekani Halisi.
Tarehe 05 June 2014 mimi na
wanafunzi na mkurugenzi wa shule tulikuwa tayari tumepatana kuwa tufike mjini
Dar na asubuhi tuwasili uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kwavile mji wa Dar
una foleni kubwa ya magari ingawa saa kumi kamili tulitakiwa kuwa kiwanjani ili
saa 10:45 tuweze kuondoka, ukweli tulifanikiwa kufika uwanjani saa tatu
asubuhi, najua unaweza kuwaza ni kwanini na hata kucheka hatukukubali kumpa
ibilisi nafasi, Biblia inasema wala msimpe ibilisi nafasi, tulijua kuwa foleni
inaweza kutuzuia kufika kiwanjani tuliona ya kazi gani kufika uwanjani
umechelewa uikose Marekani, kila mwanafunzi niliyemhoji hakulala usingizi
vizuri wala hakula vizuri tulikuwa tunaiwaza Marekani na kwangu ilikuwa
hivyohivyo
Mpaka inafika saa sita kila
mwanafunzi wazazi na ndugu walikuwa wamewasili uwanjani meneja na Madam kim
waku wetu walikuwa nao wamefika , walinunua chakula na kila mmoja alikula na
tuliagana na wazazi na kuzamia ndani ya uwanja wa Ndege, sasa kila kitu
nkilitiishwa mioyo ilikuwa inadunda viroho juujuu tukisubiri huku tukisikiliza
kwa makini watangazaji wakitangaza kwa kiingereza watu na ndege zao walizokuwa
wanapaswa kupakia na kuondoka, Madege yalikuwa yakiingia na kuondoka na mioyo
ikitudundadunda kulikuwa na ugumu sasa
kui ilinishika na nilianza kunywa soda sikuwaza hata nikishikwa na haja ndogo
itakuwaje.
Unywaji huu wa soda Katika uwanja
wa Ndege wa Dar haukuwa wa kawaida ulichangiwa na mapigo ya kasi ya moyo na
ukaukaji wa koo kwa sababu tu ya kiherehere cha Safari (Rev. Innocent Kamote)
Ndege yetu sasa ilikuwa imewasili
na tulikuwa tayari kuondoka kwa utaratibu maalumu na ulinzi wa hali ya juu
tulielekezwa geti la kuondokea tiketi zilikaguliwa na hati zetu za kusafiria
sasa nilikuwa nimemkabidhi kila kijana hati yake na nilipofika ndani
nilizipokea tena wakati huu tulizima simu zetu, tulikuwana wasiwasi tutazichaji
wapi na huenda tutashindwa kupiga picha kwa simu zetu kwani ndani ya ndege ilionekana
kama vila simu hazihitajiki hivyo hatukuchukua kumbukumbu yoyote ya ndege yetu
ya Kwanza , ilikuwa ni muda wa masaa kama mawili hivi tuliingia Ethiopia Addis
Ababa hapa tukatoa simu zetu na
kuziwasha , kulikuwa na mapumziko kiasi kusubiri ndege nyingine, hatukuwa na
wasiwasi kuhusu Mizigo yetu, ndege hii tuliyoipanda ilikuwa Boeing 737 kwangu
ilikuwa ya kawaida kwa vile niliipanda nilipokwenda Mtwara kutoka Dar, pia
nilipokuwa Mafia wazazi wangu walitumia ndege kuja Dare s salaam nyakati za
likizo
Tukiwa uwanja wa Ndege wa Ethiopia jijini Addis Ababa ni uwanja wenye Maduka na biashara za aina mnbali mbali eneo hili ni eneo huru kwa shughuli zozote lakini nafikiri shughuli ya kupiga picha nasi tukalitendea haki na vijana wangu kutoka kushoto Mimi Rev. Innocent Kamote, Yohana Komba,Baraka kolombo, William Boniventura,Author Chikoka, wanafunzi wangu waliosimama waliochuchumaa kutoka kushoto ni Imani Mngazija, Onstard Mashauri na Herbet Gumbo. Ethiopia ni moja ya eneo la Afrika lenye vijana watanashati kwa maana ya wembamba na urefu na pia wadada wenye sura nzuri sana na za kuvutia hata hivyo sisi tulikuwa tunapita tu. ndugu Msomaji wangu.
Uwanja wa Ndege wa Addis ababa
Ethiopia tukisubiri Ndege nyingine
Kuelekea Marekani toka Ethiopia
Hatukuwa na muda wa kuchaji simu
zetu tulizima tena na kupanda ndege kubwa zaidi, hii ilikuwa Boeing 777 sasa
hii ilinishangaza kwa vila ilikuwa kubwa sana zaidi ya Boeing 737, tuliruka
kutoka Ethiopia Majira ya saa nne usiku na usiku huo ndege ilikuwa ikionyesha
katika screen yake kwamba tunavuka bahari ya Mediterranean kuelekea Italy
tulifika Fiumucino usiku sana kama saa tisa au kumi usiku wakati huu masaa
yalikuwa yanatuchanganya namna ya kubadili na kuyasoma ndege ilitua na kuongeza
Mafuta na abiria wa Italy waliruhusiwa kushuka, lakini sisi tuliamriwa kusalia
ndani tu, baada ya zoezi la kuongeza mafuta tuliruka tena kuelekea Washington
hapa palikuwa mahali parefu lakini sio kama wakati wa kurudi kwani ndani ya
masaa kama manne hivi tulianza kuona mji
na wakati huu sasa ilikuwa ni asubuhi majira ya saa mbili au saa tatu hivi
asubuhi tuliona misitu mikubwa na nyumba zilizokuwa zimejificha kama zilizokaa
pekee pekee hivi na baada ya nusu saa tulitua katika uwanja wa Dulles mjini
Washington ilikuwa rah asana kwamba sasa tumefika Marekani, nilikumbuka sana
Rome Italy kwani palionekana wazi kuwa mji wenye kuvutia sana na ni mkubwa mmno
kwa vile ilikuwa usiku mataa yalijaa katika jiji lile, tofauti na hapa
Washington mji ulikuwa mpana sana na kwa
vile tulikuwa tunatua ilikuwa ngumu kuona upana wa mji ingawa ni wazi kuwa
Marekani ina miji mikubwa sana, Tuliwasili Uwanjani, hatua za ukaguzi wa hati
za kusafiria ulifanyika, na kulikuwana foleni kubwa kiasi, kwa raia wa marekani
kama Rev Park walivuka haraka na kwa wageni ilikuwa changamoto kubwa sana
niliweza kutambua wageni wengi sana wenye asili ya Ethiopia na wanaigeria ambao
tulikuwa nao ndani ya Ndege, Baada ya kuvuka hatua hii tulekwenda kusubiria
begi zetu na kutokana na kuchelewa kwenye foleni begi nyingi zilikuwa
zimeshafika na ilikuwa rahiri kujichukulia, wenyeji wetu nao walikuwa
wamewasili tayari kutupokea hawa walikuwa Jonathan Park pamoja na Samuel Park
na wazee na Mashemasi wa Open Door Presbyterian Church walikuja ma Magari
mapana kama vibasi kama unavyoweza kufahamu magari ya Marekani ni makubwa
makubwa tu Hapa sasa tulitoa simu zetu na kuanza kupiga picha nilikuwa tayari
sasa kukusanya matukio tangu hatua ya kwanza mpaka ya mwisho ili nipate cha
kuwaelezea Watanzania
Lilikuwa moja ya magari ya
wenyeji wetu ambalo tulilitumia sana kwa mizunguko yetu nchini Marekani Kanisa
la open Door Church walikuwa ndio wafadhili wetu wakubwa kwa kila kitu Malazi,
chakula na mizunguko yoote
Not Suprized! sikuweza kushangaa!
Mara ya kwanza tulipokuwa
tukitokea Dulles Airport kweli sikuweza kushangaa, katika mwezi june
tulipotembelea marekani sasa ni tarehe 6 June 2014 majira ya saa mbili saa tatu
za asubuhi jula lilikuwa linawaka, sikuona magorofa makubwa sana, niliona
barabara ya lami ya kawaida na majengo ya kawaida lakini nilianza kupiga picha
moyoni nilikuwa nashangaa Marekani? Ndo hii mbona mazingira sawa na nyumbani
niliona kawaida na sikushangazwa
Hali hii ya mji tukitokea uwanja
wa ndege ilinifanya nisione tofauti na nyumbani sasa nilipiga picha lakini
nikiwa sina nguvu sana nitaonyesha nini nyumbani mbona kawaida moyoni nikasema
It is not Surprise ! Nilipafananisha na maeneo ya Tazara tu pale Dar es Salaam au makutano ya Mandela na Pugu road au Nyerere road kwa jina la siku hizi.
Taratibu Mazingira yalianza kuwa
na mvuto, na nikajua kwa vyovyote vile ingawa uwanja wa ndege ni mzuri sana na
wa kimataifa huenda majengo yaliyo karibu na Dulles ni ya zamani sana na
yametunzwa tu bila kubadilisha maumbile yake kutokana na uimara wake lakini
sasa nilianza kuona tofaouti, Nilianza kuona gari nzuri zenye rangi nzuri ni
kama mpya hivi, zenye rangi za kung’aa kana kwamba kuna kiwango kuwa gari yako
ikichakaa hairuhusiwi tena kuwako barabarani, kila kitu kilionekana kama kipya,
Magorofa mazuri lakini urefu wa kawaida kama ilivyo Dar es Salaaam na Tanga, Na
mazingira kama Arusha na Kilimanjaro ile kijani yake, Njiani kulikuwa
naBarabara pana zenye kuruhusu magari kwenda kwa kasi Fulani na madaraja
makubwa yenye kamera maalumu zinazofuatilia mwenendo wa Magari njiani sasa moyo
ulianza kuridhika kuwa naam hii ndio Marekani
Mazingira haya yalianza kurudisha
tumaini kuwa kumbe kweli Marekani imeendelea lakini bado sikuona maghorofa
Marefu kama mtazamo wangu ulivyokuwa, lakini wenyeji walisema hii ndio
Washington DC mji ambao ni makao makuu ya serikali ya marekani
Sasa tulifika nyumbani
Tulipelekwa moja kwa moja eneo
linalojulikana kama Virginia Tomas Jeferrson Famer na tulipatiwa nyumba ya
ghorofa yenye vyumba vitatu na jiko ba
sebule nyumba hii inamilikiwa na kanisa la Open Door Church tulikabidhiwa
vyumba na kuweka mizigo na kuelezwa kuwa tutakaa hapo bila muingiliano na
wenyeji isipokuwa kwa muda wanaokuja kutuchukua na kutembeza tu, tulifurahia
kuwa tutakuwa na wakati mzuri Nyumba ile ilikuwa imejengwa kwa matofali ya
kuchoma na mbao ilikuwa nzuri lakini ndogo nje ilikuwa inasomeka namba 2449 tulielekezwa namna ya kufunga kwa
namba na kufungua gari pia liliachwa hapo nje na funguo lakini hakuna aliyekuwa
na ubabe wa kuendesha
Nyumba tuliyofikia
floor ya chini na shughuli ya malaji ikawa kama unavyojionea
Tulielezwa kuwa
tupumzike kwa muda na tutafuatwa baadaye
Eneo la jikoni lilikuwa limesheheni kila aina ya vyakula vinjywaji, mayai, Maziwa mikate, pipoi za aina mbalimbali, maji safi ya kunywa, Nyanya za kusaga, nyama,keki, chocolates, Juisi za aina mbali mbali soda za aina mbali mbali, ilikuwa mtu ushindwemwenyewe kula, Lakini kweli wenyeji wetu na Kanisa la Open door walikuwa wamejiandaa vilivyo kupokea wageni na kuwahudumia kwa ufanisi
sehemu ya stoo iliyoko Jikoni ikiwa Imesheheni mapochopocho ya aina mbalimbali
Friji likiwa limejaa juisi, maziwa, soda na mayai pamoja na sourcege kwa habari ya kula wamarekani wako mstari wa mbele, Haraka sana tulikinai na kuanza kukumbuka vyakula vya nyumbani ambavyo hapa sasa vilikuwa adimu
Nikiwa katika harakati za kutafakari nile nini ili nikalale
Kumbuka
hata hivyo hatukwenda kula tu Marekani kusudi kubwa la safari yetu ilikuwa ni
kujifunza, na kwakweli hatukuwa na muda wa kupumzika tangu tulipofika hata
tulipoondoka, wenyeji wetu walituweka bize (busy) Katika kuhakikisha kuwa
Malengo yetu ya kujifunza yanatimia na kwakweli ndivyo ilivyokuwa safari yangu
nya Marekani ilikuwa ni shule tosha, nataka kuelezea Matukio yote muhmu ya
ziara hii tofauti na namna tulivyotembelea nitaanza kuelezea tukio moja baada
ya jingine kutokana na umuhimu wake nay ale niliyojifunza.
1. Abraham
Lincoln Memorial
Mahali
hapa ni muhimu sana katika kujifunza kupitia Marais wa Marekani wanaoheshimika
sana wenyewe huwaita “The greatest Presidents of America” Mmojawao ni Abraham
Lincolin ambaye tulitembelea makumbusho yake, hapa nilifuatilia kwa Makini Jumba la kumbukumbu za rais huyo na nilitaka kuandika jambo na niliandika swali Abraham Lincoln ni nani na kuanza kuelezea kama unavyoweza kuona katika mada ifuatyo
Hekalu la kumbukumbu ya Rais wa zamani wa Marekani Abraham Lincolin kama linavyoonekana kwa nje, nilitembelea mahali hapa na kujifunza maswala muhimu kupitia kiongozi huyu.
Abraham Lincoln ni
nani?
Mwezi
juni 6-20 mwaka huu nilipata neema ya kutembelea Marekani, ambalo ni moja ya
Mataifa makubwa na Yenye Kuheshimika sana Duniani, katika siku chache
nilizokuweko huko katika program iliyoitwa Vision Trip makusudi yetu makubwa ilikuwa
ni kujifunza Maswala Mbalimbali na kasha kuja na kuyatumia yale yatakayoweza
kutuletea maendeleo makubwakatika taifa letu, Mimi na wanafunzi wangu
tuliotembelea huko tulikuwa tunataka kujua chanzo cha Maendeleo ya wenzetu na
kisha tutumie ujuzi huo kuendeleza Taifa Letu kama viongozi wa sasa na wa
baadaye
Moja
ya maswala Muhimu yaliyosababisha taifa hili kuendelea ni pamoja na kupata
neema ya kuwa na Viongozi Bora! Msingi mkubwa wa Taifa hili uliwekwa na rais wa
Kwanza Mzee George Washington mzee huyu alikuwa anamcha Mungu na Hivyo Mungu
aliwekwa mbele katika taifa hili na ndio msingi wa maendeleo makubwa kwenye
taifa hili, hata hivyo leo nataka kumzungumzia
moja ya viongozi muhimu sana ambaye anawekwa katika orodha ya Maraisi
wakubwa sana wa Marekani wanaoheshimika the Greatest Presidents of United
States Huyu si mwingine bali ni Abraham Lincoln
Abraham Lincoln
Nilianza
kuhisi umuhimu wa Rais huyu wa Marekani hata kabla sijaingia Marekani kwenyewe
kwani tulipokuwa tumeomba Visa na kufanikiwa kuipata nilitamani kuona Visa ya
kimarekani ikoje kwa vile upatikanaji wake nimtihani nilipochungilia visa hiyo
haraka sana niliona Jengo muhimu sana lenye kuashiria makao makuu ya serikali
ya Marekani US Capitol na picha ya Rais huyo wa zamani wa Marekani, licha ya
kuwamo katika mamlaka hayo ya utoaji visa pia Lincon anaonekana katika baadhi
ya fedha za Kimarekani Dollar
Na
tulipofika Marekani pale Washington moja ya maeneo tuliyotembezwa ilikuwa ni
pamoja na Hekalu kubwa lijulikanalo kama Abraham Lincoln Memorial nikataka kujua undani wa Rais huyu na kwa
nini anatukuzwa sana na kusifiwa? Licha ya kutembelea Makumbusho yake pia
nilifika eneo alikouawa na Kupigwa risasi nilikuta watu wengi wanatembelea hapo
who is Abraham Lincoln Huyu jamaa ni nani
Sio sisi tu watu wengi duniani kila sikuwanatembelea mahali hapa na kupiga picha kwa kumbukumbu ya kiongozi huyu mkubwa ukiwafanyia watu mema utakumbukwa milele
Rev. Innocent Samuel Kamote sasa ilikuwa zamu yangu kupata picha ndani ya jengo hilo la kumbukumbu ya Abraham Lincolin, ilikuwa lazima usubiri ili kusudi watalii wapungue upate picha ya utulivu kama hii
Abraham
Lincoln Ni rais wa 16 wa Marekani, alilitumikia taifa hilo mwezi March 1861
mpaka alipouawa April 1865, rais huyu aliongoza Marekani katika wakati mgumu
kwani kulikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilimwaga damu za wengi,
Majimbo saba ya kusini walitangaza kujitenga mara moja mara baada ya kuapishwa
kwa Lincoln wakijua kuwa angekomesha shughuli za watumwa, pamoja na kuwa
aliongoza katika kipindi kifupi sana Rais huyu alifanikiwa kulijenga Taifa hili
Kimaadili, hivyo wamarekani walikuwa na kiwango cha juu sana cha maadili wakati
wake, aliimarisha umoja wa Majimbo yote ya marekani, aliimarisha Katiba na
kumaliza kabisa migogoro ya kisiasa iliyokuweko kwa kufanya hivyo alifanikiwa
sana katika kujenga umoja wa kitaifa wa Taifa la Marekani unayoiona Leo.
Moja
ya Maswala yaliyompa heshima mkubwa huyo pia ni pamoja na kukomesha Biashara ya
Utumwa na ubaguzi Amerika alisema “hatuwezi kuwa na uhuru wa kweli katika taifa
ambalo wengine ni Mabwana na wengine ni watumwa” Hatuwezi kuwana taifa ambalo
wengine wanafurahia uhuru huku wengine wakiwa ni watumwa!”
Licha
ya kupngwa na baadhi ya watu waliokuwa wakiwatumia watumwa kwa faida zao,
Lincoln ni chanzo kikuu cha kuimarika kwa Uchumi wa wamarekani walio nao leo
ndani ya kipindi kifupi alichoonngoza, aliimarisha sekta ya Viwanda,
aliimarisha Mabenki, alijenga Mifereji ya kupita chini kwa chini, alijenga reli
na kuimarisha ukusanyaji wa kodi, Lincoln alikataa pia kupigana vita au kusaini
vita kati ya Marekani na Mexico mnamo mwaka 1846.
Abraham Lincoln
Alizaliwa
mwala 1809 na kuuawa mwaka 1865, alitokea katika Familia masikini nay a kawaida sana Babu yake Samuel
Lincoln alihamia kutoka Uingereza, Baba yake aliitwa Thomas Lincolin Abraham
Lincoln hakuweza kupata hata elimu ya awali katika familia yake na hivyo
alijiendeleza mwenyewe kwa kufanya kazi na kujisomesha, alisoma kwa kutumia taa
ya mafuta ya taa, al;ijiendeleza na kufanikiwa kuwa mwanasheria na baadaye
kujiunga na siasa nyumba aliyoishi na familia yao mwanzoni ilikuwa ya mbao na
yenye chumba kimoja tu, alipojiunga na siasa Lincoln alikuwa na Ushawishi
mkubwa sana kiasi ambacho ukimsikiliza akizungumza unakubali kuwa yaya ni
kiongozi, alikuwa na uwezo wa kujenga hojana mwenye uwezo mkubwa sana wa
Ushawishi, Familia yao ilihamia huko Illinois Jimbo analotokea rais wa Sasa wa
Marekani Barak Obama, alipofanikiwa kuwa rais aliondoka Illinois kuelekea
Washington akitumia Treni jambo ambalo limewahi kuigizwa na Kiongozi wa sasa wa
Marekani.
Aliingia
madarakani akiwa haeshimiki sana lakini amepokea Heshima kubwa na nyingi sana
baada ya kuuawa kwake, Pamoja na Lincolin kuwa mwanademocrasia mkubwa katika
unenaji alikuwa na Madaraka makubwa kuliko raisi yeyote wa marekani
aliyepatakuweko kiasi ambacho kimaamuzi ni kama alikuwa Dikteta. Nanaheshimika
sana kwa kiwango ambacho jamii kubwa hutembelea Makumbusho yake wakiwemo
wayahudi, waasia na watu wa mataifa Mengineyo.
Rev. Innocent Kamote nikiwa mahali alipofia Abraham Lincolin Jijini washingston DC
Lincolin
aliuawa kwa kupigwa risasi na wanaosadikiwa kuwa wapinzani wake hususani wa
sera ya kukataa kumiliki watumwa wa majimbo ya kusini, aliyemuua alijulikana
kwa jina la John Wilkes Booth tarehe 14 April 1865 siku ya Ijumaa kuu wakati
alipokuwa ametembelea Ford Theatre. Washington Booth alikuwa amechukizwa
alipomsikia Lincoln akizungumza na alikuwa amakusudia kumteka lakini
aliposhindwa aliamua kumuua, wakati wa Pasaka hata hivyo lincolin alifariki
asubuhi yake Tarehe 15 April 1865 saa moja na dakika 20. Siku ya kuuawa kwake
mapema alikuwa na Mawaziri wake na aliwaeleza ndoto yake aliyoiota usiku na
wakaitafasiri kuwa ni ya ushindi dhidi ya Sherman na kuwa vita hiyo imefikia
mwisho, siku hiyo Rais Lincoln alionekana mwenye furaha kuliko kawaida hata
waliomuona walisema haijawahi kuonekana akiwa na Furaha kiwango hicho Lincoln
alizikwa nyumbani kwake Springfield kwa Hesmika kubwa za kijeshi, Katika Maraisi
wa Marekani hakuna Rais amabaye amaewahi kuandikwa nn maandishi mengi sana Kama
ilivyo kwa Abraham Lincolin
Mambo ya kujifunza:
1. Kiongozi bora haitaji miaka mingi
sana ili aweze kufanya mambo mazuri Lincoln aliweza kufanya mambo mengi mazuri
huku akiwa na kipindi kidogo cha uongozi.
2. Kuweko kwa matatizo hakuzuii
shughuli za maendeleo Lincolin aliweza kuleta maendeleo licha ya kuweko na
vikwazo na kuwa na wakati mgumu ni vema viongozi wa afrika tukakubali kuwa
Mbaazi zikikosa Mvua husingizia jua, kwa Lincoln changamoto alizokuwa nazo
hazikuzuia yeye kusababsha maendeleo
3. Nguzo ya maadili ni nguzo muhimu
sana kwaajili ya kujenga ufanisi wa kazi
4. Taifa lisilokusanya kodi au kutoa
mianya ya misamaha ya kodi na ubadhirifu kuendelea kwake ni menemene tekeli na
peresi
5. Viongozi wasiojali matumizi
mabaya ya mali za umma matumizi mabaya ya Magari ya serikali watajifunza kwa
Lincoln aliyeamua kwenda ikulu akitumia treni
6. Mwisho nimejifunza kuwa kama
Tukiwatumikia watu kwa moyo wetu wote bila kujali ni vikwazo gani tunakutananavyo
nkatika maisha yetu ama upinzani toka kwa maadui heshima itatufuata siku zote
za maisha yetu hata tujapokufa tutakuwa tungali tunaishi Lincoln anakumbukwa na
kuhesimiwa na watu Milele
Eneo lingine tulilopata nafasi ya kutembelea ilikuwa ni makumbusho ya Rais John F Kennedy, lilikuwa ni eneo zuri na lililoonekana la kisasa, likiwa limepambwa kwa maua mazuri, ya kijani na manjano, eneo hili pia ujulikana kama Kennedy Center ndani ilikuwepo kwaya ambayo ilikuwa ikitumbuiza kwa nyimbo, walikuwa wamevaa suti nyeusi ndefu na sketi nzuri ndefu na za heshima, waimbaji walikuwa wanawake kwa wanaume na walikuwa wakiimba kwa ustadi mkubwa tulielezwa kuwa uimbaji huo hufanyika kila siku kuanzia saa sita mchana, pia wanamuziki hutumbuiza nje na kupiga dansi katika eneo hili,eneo hili hutumika kufundishia na kuimarisha wasanii na wanamuziki wanaoishi Washington na maeneo mengine duniani. Hakukuwa na sananu yoyote ya Kennedy kama ilivyo katika maeneo mengine Lakini nilitaka kujua na kujifunza maswala kadhaa japo machache kuhusu Rais huyu na ndipo nilipojifunza kwamba
John F Kennedy alizaliwa mwaka 1917 na kufariki mwaka 1963, Yeye alikuwa ni rais wa 35 wa marekani, Ndiye aliyekuwa raisi kijana zaidi kuliko wote waliopata kuchaguliwa katika historia ya Marekani, aliingia madarakani mwaka 1961-1963, Bwana Kennedy pia ndiye aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Kikatoliki, kuitawala Marekani na ndiye raisi wa kwanza kuzaliwa katika karne ya 20
Kennedy alikuwa na Urafiki mkubwa sana na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na alikuwa ndiye Rais wa kwanza wa Marekani Kumkaribisha mwalimu Nyerere na kumpokea Ikulu ya marekani kwa heshima kubwa sana kwa namna ambayo haijawahi kutokea Nyerere alipokelewa kwa heshima kubwa ikulu ya marekani na kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride na kuzungumza machache, Heshima aliyomuonyesha Mwalimu Nyerere ilinitia Moyo kuwa mtu huyu alikuwa hana ubaguzi na alikuwa na mtazamo wulio wazi kuwa wanadamu wote ni sawa ni imani yangu kuwa huenda kuuawa kwa raisi huyu kulikuwa na mchango mkubwa wa kumfanya mwalimu kufikiri aina nyingine za kisiasa Mtazamo wao mwanzoni ulikuwa wenye kufanana
Pichani ni video inayoonyesha Jinsi Kennedy alivyompokea Nyerere Jambo hili lilinifanya nimpende Kennedy na kumuona kama ni Mwenzetu katika ulimwengu wa kukomesha ubaguzi na kuwa na mtazamo wa usawa kwa wanadamu wote kwa video hii utakuwa umetambu Moyo wa John F Kennedy ulikuwa ni wa Namna gani, Marekani ilipoteza na Tanganyika pia.
John Kenedy aliuawa Mapema sana kabla hajamalizia miaka yake mitatu ya Utawala, Lakini mambo makubwa ambayo anaweza kukumbukwa kwayo, alikuwa na sera nzuri za Mambo ya ndani na nje ya nchi, na alikuwa mwenye ushawsishi mkubwa sana kwa dunia ya wakati wake, alikuwa mvumilivu na aliweza kuzuia uwezekano wa kuwapo kwa vita kati ya Marekani na Cuba, kwa kuvumilia bila kujibu Mapigo ya rokesti za Cuba dhidi ya Marekani na hivyo kuizuia Marekani isiingie vitani, Alipendwa sana na vijana na walimkubali, inawezekana kuwa ndiye alikuwa Rais Maarufu kuliko wote waliopata kutawala marekani, Alitambua umuhimu wa kutunza Utamaduni na Historia za Wamarekani wa jamii mbalimbali, na alitambua kazi zote za ubunifu na kuzipa kipaumbele, Kutokana na umahiri wake katika kuzungumza na ushawishi, aliweza kupewa umuhimu mkubwa sana katika maswala ya kisiasa utawala na mafanikio makubwa katika karne ya 20 na amekuwa mfano wa kuigwa.
Rev. Innocent Kamote Nikiwa nje ya John F Kennedy Center Jijini Washington DC
kwa Mbali wanamuziki wa Bendi wakijiandaa kutumbuiza hadharani nje ya Ukumbi wa JFK John F Kennedy aliyekuwa Rais wa 35 wa Marekani
Rev. Innocent Kamote Nikiwa nje ya Ukumbi wa John F Kenedy na wanafunzi wa Living Stone Boys walioteuliwa kwenda marekani sasa tulikuwa tumechoka sana tukisubiri wenyeji wetu waje kutuchukua, karibu nami ni Herbert Gumbo, aliyeinama Imani Mhgajiza, aliyeangalia Pembeni Willium Boniventura, anayefuata Onstard Mashauri na baralka kolombo, wawili hawakuonekana vezuri
Hakuna anayeweza kueleza ni kwanini Kennedy aliuawa haijulikani ni kwa sababu gani, inaonekana kama alipigwa risasi na mtu mmoja aliyejulikana kama Lee Harvey Oswald na ni yeye tu anayejua sababu ya kuumuua John F Kennedy maarufu kama JKF Oswald alikuwa ni Baharia aliyeachishwa kazi, huyu alifupia masiha ya Raisi huyo Mpendwa wa Marekani Hata hivyo haikujulikana kuwa ni nani alikuwa pamoja na muuaji, kihistoria inasemekana kuwa Oswald alikuwa na siasa la mrengo wa Kisoviet na mwenye kuunga mkono misimamo ya Cuba na labda sababu hizi zinaweza kuwa zilichangia kuuawa kwa Kennedy lakini nani anaweza kusema chochote kwani kukubali hilo kungemaanisha kuwa wacuba na warusi walifanikiwa katika karata hii waloicheza.
Yote katika yote Burudani na kwaya tulizoziona zilikuwa zinaashiria kuwa Kennedy atakumbukwa kwa kukuza na kulinda Utamaduni wa wamarekani na kusaidia kukuza vipawa kwa wasanii kazi inayofanyika hata leo
Eneo La tatu ambalo tuitembelea na kujifunza maswala mbali mbali ni Jengo maarufu lijulikanalo ka Thomas Jefferson Building, Jengo hili pia linajulikana kama Library of Congress, Jengo hili haliko mbali sana na mlima ujulikanao kama capital hill ambao niytauzungumzia baadaye, inasemekana kuwa jengo hili limejengwa mwaka 1897 hata hivyo lilionekana imara na la kisasa tu, kihistoria jengo hili inasemekana lilijengwa na Rais John Adams na ndipo eneo ambalo aliweka saini ya kuhamishia mji mkuu wa serikali ya marekani kuwa Washington, mahali hapa palikusudiwa kuwa Library ya vitabu vya kisiasa na huenda ilikusudiwa kwa wao tu vitabu vipatavyo 740 hivi vilikusanywa, mwaka 1814 Majeshi ya uingereza yaliharibu jengo hili na kuchoma sehemu hiyo ya Libray ndogo iliyokuweko, Rais Thomas Jefferson aliyekuwa akiishi Monticello baada ya kustaafu alitoa sehemu ya Library yake ili kufidia Library hiyo, Jefferson alikusanya vitabu 6,487 na fedha zipatazo $23,950 zilikusanywa na kuibadilisha Library hiyo kuwa ya kitaifa, rais Jefferson aliamini kuwa kujifunza ni kwa muhimu sana au Elimu ni ya muhimu sana kwa wamarekani kutokana na falsafa yake ya kutaka watu wajisomee ghorofa ya pili ya jengo hili ilipewa jina la Heshima kwa Thomas Jefferson na mwaka 1980 Maktaba hii ilipewa jina la Rasmi kama Thomas Jefferson Building