Jumatatu, 15 Februari 2016

Safari yangu ya Marekani!



Safari yangu ya Marekani

Juni 6th -20th 2014 Nilipata nafasi ya Kutembelea taifa kubwa kabisa Duniani yaani Marekani, kupitia mpango maalumu wa shule yetu Living Stone Boys’ Seminary wa kutembelea na kupaleka vijana katika Mataifa yaliyoendelea ili kuwaingizia Maono na mitazamo ya kimataifa kwa kusudi la kuja kuliimarisha taifa letu na kuliletea maendeleo.

Mpango huu uliandaliwa na Meneja wa shule na mke wake yaani Rev. Andrew Park na Eunreen Kim Mpango huu tuliuita USA VISION TRIP. Mchungaji Park Yeye ni Mwanzilishi wa shirika la Kikristo hapa Nchini liitwalo Mission With Christ ambao ni wamiliki wa Chuo Cha Biblia kilichopo Kange mjini Tanga kijulikanacho kama Tanga Christian Bible College (TCBC). Na pia shule ya wavulana ya sekondari iliyoko mjini Muheza ijulikanayo kama Living Stone Boys’ Seminary
Mchungaji Park alikuwa na mpango kwamba walimu na wanafunzi wawe na Mwanga wa kutosha kuhusu ujuzi wa kimataifa ili kujua nini kinapaswa kufanyika katika taifa letu na kuliletea maendeleo.

Mapema mwezi wa December 2013 Uongozi wa shule ulinitaka mimi kama mkuu wa shule kuwaandikia barua wazazi wote ili kwamba waweze kukubaliana na mpango wa kuwaruhusu vijana wao watakaochaguliwa na shule, kutokana na uadilifu na uwezo mzuri wa kitaaluma wasaini kwamba watakubaliana na mpango wa shule na kusaini kuwa watakuwa tayari kukubali endapo watoto wao watateuliwa na uongozi kwaajili ya kwenda Marekani, wakati huu binafsi nilijua kuwa ni safari itakayowahusu wanafunzi tu.

Niliandaa barua hizo na wazazi walizijibu, na wengi walikubaliana na wazo hilo, Baadaye uongozi wa shule tena walinitaka kama mkuu wa shule kuchagua vijana nane walio na nidhamu na wenye uwezo mzuri kitaaluma nani niliwachagua vijana hao mmoja akiwa ni Rais wa serikali ya wanafunzi
Vijana waliochaguliwa walikuwa ni
·         Yohana Martin Komba - Kutoka Korogwe
·         Onstard Mashauri   - Kutoka Arusha
·         Imani Peter Mgazija – Kutoka Tanga
·         William Boniventure. – Kutoka Dar es Salaam
·         Baraka Kolombo. – Kutoka Dar es Salaam
·         Athumani ulimwengu. – Kutoka Muheza
·         Athour Chikoka. – Kutoka Muheza
·         Herbert Gumbo. – Kutoka korogwe
Niliandaa barua za kuwaombea vijana hao Hati za kusafiria na kila mzazi alihakikisha kuwa anajitahidi kupata Hati ya kusafiria kwa vijana wao, kupitia ushirikiano uliokuweko kila kijana alifanikiwa kupata hati ya kusafiria yaani passport, Baada ya zoezi hili kukamilika nilitoa ripoti kwa uongozi wa shule yaani Meneja kuwa hati za kusafiria kwa vijana ziko tayari.

Katika namna ya kushangaza kabisa nikiwa sina hili wala lile huku nikishughulikia maswala ya vija na hao kwa moyo mkubwa kabisa Meneja aliniuliza Mchungaji Una Passport ? yaani una hati ya kusafiria? Jibu lilikuwa Ndiom kwani niliandaa Passport yangu tangu mwaka 2011 nilipokuwa nimepata Mwaliko wa kwenda Msumbiji kwa safari za injili, hata ingawaje sikupata neema ya kukanyaga Msumbiji mpaka sasa. Lakini wakati huu nilipata msisimko mkubwa kwamba hata na mimi pia nimekuwa miongoni mwa hao wanaokwenda Marekani ? Nilimtikuza Mungu na kuanza kuwaza juu ya taifa hilo kubwa ambalo kila mmoja alikuwa anatamani kulitembelea, wakati huu nilijiuliza kuwa ni mwezi December tu 2013 Kaka yangu alipata Nafasi ya kutembelea Israel Nchi ambayo hata mimi nilitamani sana niitembelee kutokana na kujihusisha na maswala ya kumtumikia Mungu, Lakini nilitambua kuwa Mungu alitaka kuonyesha uwezo wake kuwa wakati wa Bwana kutubariki umefika.

Nilitamani kufika Marekani, nilifurahi niliwaza sana na nilianza kuushibisha moyo wangu mawazo ya kutosha na ujuzi mkubwa kwa taifa hilo Nilitambua kuwa marekani ni moja ya mataifa makubwa sana Duniani, ni taifa ambalo limeendelea, limeendelea katika maswala ya Sayansi na teknolojia pamoja na uchumi mkubwa, Nilitambua kuwa Marekani ni muunganiko wa Mataifa mengi makubwa yapatayo 48 yanayounda kwa pamoja sehemu kubwa ya bara la Amerika ya Kaskazini, nilitambua pia inaunganishja jimbo la Alaska na visiwa maarufu vya Hawaii na hivyo kufanya nchi zipatazo 50, Ni taifa kubwa sana ndio nilitambua na nilitamani kwenda ili nijifunze mengi kwa gfaida ya kizazi chetu na maendeleo ya taifa letu.

Ni kwa sababu hiyo nilitamani sana kuandika maswala mengi nitakayokuwa nimejifunza huko ili yamkini yaweze kuwa kumbukumbu na kusaidia Maendeleo ya Taifa letu, Hivyo katika habari hii nataka kuelezea kwa ufupi yale niliyojifunza, kwa makusudi ya kuwatia moyo wanafunzi na wananchina viongozi wa Tanzania kufanya kazi kwa bidii na matumaini makubwa kwa imani kuwa kile ambacho wamarekani wameweza na kukifanya tunaweza na tutafanya naam na makubwa kuliko ya Marekani tutaweza.

Maandalizi ya safari
Kama nilivyogusia hapo awali kuwa maandalizi ya safari yalianza kwa utafutaji wa Hati za kusafiria, sasa nilikuwa nimetambua wazi kabisa kuwa kuna umuhimu wa kila raia wa Tanzania hata vijana kuwa na Hati ya kusafiria, nilijifunza kuwa hili linapaswa kuwa kitu cha kawaida tu, nilikumbuka kuwa kaka alipata shida kiasi katika kuandaa hati ya kusafiria kwenda Israel, kwa vile kutokea kwa safari na mpaka safari yenyewe kulikuwa na muda mfupi, Mimi nilikuwa na hati ya kusafiria mapema zaidi, lakini niliona wazazi na wanafunzi wakihangaika kuipata, na hatiamaye walizipata hati zao za Kusafiria Passport 

Moja ya swala kubwa na mtazamo mkubwa ambao wengi tunakuwa nao na hata mimi nilifikiri nitakutana nao ni kuwepo kwa rushwa wakati wa ufuatiliaji wa hati hiyo ya kusafiria, lakini jambo lililonifurahisha ni kwamba ninaweza kukiri wazi kuwa katika Idara ya uhamiaji rushwa ilikwishwa kuzikwa miaka mingi, hakukuwa na kudaiwa rushwa, hakukuwa na mazingira yoyote ya kuhonga ambayo niliyatazamia, zaidi ya malipo ya kawaida ya 50,000/- ukishakuandaa vielelezo vyote wavitakavyo pamoja na picha za passport size wazitakazo ukweli ni kuwa hakuna urasimu katika idara hii. Haya tuliyashuhudia.

Maandalizi yaliendelea huku kukiwa na mawasiliano ya kudumu na wazazi katika kuhakikisha kuwa vijana wao wanakuwa salama na safari inafanikiwa, baada ya kila kijana kufanikiwa kupata hati ya kusafiria, hatua iliyofuata ilikuwa ni ukataji wa Tiketi, Ukataji huu wa tiketi hufanyika kwa njia ya kielekroniksi kupitia mtandaoni, unaweza kuangalia mashirika ya ndege ya aina mbalimbali duniani, na usalama wake na unaweza pia kuangalia unafuu wa bei, tulichagua Ethiopian Airlines na wote tulipatia tiketi ya Ndege hiyo, na tiketi ilionyesha kuwa tutaondoka Dar kupitia Adds ababa kisha Fiumucino Italy na kisha Washngton Dulles , tayari tulikuwa na furaha kuwa tutakanyaga Ethiopia na Ulaya yaani Italy na kisha Marekani kila mmoja alikuwa na moyo wa Shauku wa kutaka kufika huko.

Baada ya upatikanaji wa Tiketi tukio lilolofuata lilikuwa ni upatikanaji wa visa ya kimarekani, kwa mujibu  wa Maelekezo tuliyopewa ilikuwa tunapaswa kufika ubalozi wa Marekani pamoja na hati zetu za kusafiria na wazazi wa vijana na kuhojiwa maswali kadhaa ndipo baada ya wiki moja tuweze kupatiwa visa hii ni kama kibali na ruhusa yakuwako katika nchi ya watu, tulijiandaa na tulimuomba Mungu kwani tuliwahi kusikia na tunafahamu kuwa watu wengi hunyimwa visa kutokana na kutokutosheleza vigezo husika vinavyotazamiwa na wenye taifa lao, kwa kweli tulisafiri kwa pamoja na tukafika Dar na kibasi chetu cha shule tukiwa na wanafunzi wote, tuliamua kutafuta nyumba nyuma ya ubalozi wa Marekani yaani maeneo ya msasani hivi ili ifikapo asubuhi iwe rahisi kwetu kufika Ubalozi wa marekani pale Drive in Morroco, asubuhi tulijihami na tukafika ubalozi wa Marekani, ni mahali panye ulinzi mkali hivi kwa hiyo kihofu cha kimazingira kilianza kutuingia lakini tulijitia moyo kuwa tuna Mungu, tulifika nje ya Ubalozi tukiwasubiri wazazi kwani tuliwaambaia kuwa hatutaingia mpaka wote wamefika tulisubiri njae na walipokuwa wote wamefika tuliingia ndani, askari wa mlangoni baadaya ukaguzi na kuzuia simu zote za mkononi na vifaa vingine ambavyo husababisha alamu kulia kama mapene mikanda n.k vibaki na tuliingia ndani, wazazi waliambiwa wasubiri nje ya ndani ya ubalozi huo, kulikuwa na foleni watu walikuwa wakikusanya hati zao na kuitwa kwa majina na kuhojiwa wengine walikuwa wakilia kwa vila walikataliwa, lugha iliyokuwa ikitumika sasa ni kingereza tuliingiwa na hofu tuliomba Mungu kimoyomoyo tufanikiwe, shughuli ilikuja tulipopeleka Documents zetu kwa Muhusika huyu alikuwa dada wa Kitanzania kwa mtazamo wetu, alikuwa mkali na mwenye dharau alizitupilia mbali hati zetu na kukataa picha zetu kuwa hazifai kwa visa ya Marekani, hatukuwa tumeelewa, kila mtu alikuwa mgeni na maswala hayo hatuna uzoefu Missionary Park hakuweko wakati huu, tulifukuzwa bila ya kuelekezwa lolote tulitoka nje moja kwa moja na tupofika getini tuliitwa tena, nilikuwa mimi na vijana tu  Mama mmoja wa kizungu alituelewesha sababu za kukataliwa kwetu tulibaini picha zetu zilikuwa mbaya wamarekani wanataka picha ya kipande Passport size yenye Inchi mbili kwa mbili yaani two by two na Background yake yaani ukuta wa nyuma unapaswa kuwa mweupe, tulielekezwa kwenda kupiga picha hizo katika duka moja kubwa pale mikocheni shipwright alikuweko muhindi mmoja ambaye alikuwa anahusika na kupiga picha tulielekezwa hapo, wakati tukitoka nje ya Ubalozi punde nilionana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Assemblies Of God Barnabas Mtokambali, tulisalimiana na alinieleza kuwa amekuja kushughulikia visa yake kwa upya kwamba atakwenda Marekani karibuni, alinisaidia kunielekeza sehemu hiyo ya kupiga picha za visa, nilimweleza kusudi la safari yangu na vijana huko marekani alitubariki na tulikwenda kupiga picha, Roho ilikuwa juu juu kwa vile tulipewa dakika chache sana za kukamilisha kwa vile siku yenyewe ilikuwa alhamisi na walidai ijumaa huwa awafanyi kazi na wangefunga muda wa saa tano, tulijitahidi kufanya hivyo tukisaidiwa na Mzazi wa Williuam Biniventura, zoezi lilifanikiwa na tulirejea tena Ubalozini, Mungu alikuwa ametusaidia aliondoa hofu zote, watu wengi sana walikuwa wamepungua kazi ilikuwa imefanyika kwa haraka hivyo ulikuwa ni kama wakati wetu kuhudumiwa, sikumfurahia kabisa dada Yule wa kitanzania nilimchukia kwa muda nilishindwa kuelewa alikuwa ana maana gani lakini nilipata somo kwamba kuna umuhimu wa kukamilisha mambo yote ya watu unayoagizwa kama yalivyo ili kuepusha usumbufu,

Sasa ulikuwa wakati wakuitwa kwa mahojiano na niliulizwa maswali mengi sana na afisa ubalozi huyu alikuwa kaka mnene na mrefu ni mmarekani  alikuwa muelewa sana alihojo kila alichokihoji na nilijibu kwa ujasiri niliwa na utulivu moyoni vijana walikuwa wakisikiliza mahojiano hayo na tayari ilikuwa ni kama wana majibu ya kujibu kila nilichoulizwa ndicho walichoulizwa na wazazi hawakuruhusiwa kuingia ndani, tulishangaa ni kwanini waliwatesa kuwaito kutoka mbali, lakini visa yam domo ilikuwa imekubaliwa na tuliacha passport zetu kwaajili ya matengenezo ya visa.


Pichani ndio visa ya Marekani kama inavyoonekana ikiwa imegongwa katia hati yangu nya kusafiria visa hii ilituruhusu kutoka 30th April 2014 – 29 April 2015 ilikuwa rhusa ya Mwaka mzima sisi tulikaa wiki mbil.

Mafanikio ya kupatikana kwa visa yalitupa ndoto zaidi ya kuiona Marekani , tuliona sasa safari ya Marekani haikuwa ndoto tu bali sasa ilikuwa ni halisi

Safari ya Marekani Halisi.
Tarehe 05 June 2014 mimi na wanafunzi na mkurugenzi wa shule tulikuwa tayari tumepatana kuwa tufike mjini Dar na asubuhi tuwasili uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kwavile mji wa Dar una foleni kubwa ya magari ingawa saa kumi kamili tulitakiwa kuwa kiwanjani ili saa 10:45 tuweze kuondoka, ukweli tulifanikiwa kufika uwanjani saa tatu asubuhi, najua unaweza kuwaza ni kwanini na hata kucheka hatukukubali kumpa ibilisi nafasi, Biblia inasema wala msimpe ibilisi nafasi, tulijua kuwa foleni inaweza kutuzuia kufika kiwanjani tuliona ya kazi gani kufika uwanjani umechelewa uikose Marekani, kila mwanafunzi niliyemhoji hakulala usingizi vizuri wala hakula vizuri tulikuwa tunaiwaza Marekani na kwangu ilikuwa hivyohivyo
Mpaka inafika saa sita kila mwanafunzi wazazi na ndugu walikuwa wamewasili uwanjani meneja na Madam kim waku wetu walikuwa nao wamefika , walinunua chakula na kila mmoja alikula na tuliagana na wazazi na kuzamia ndani ya uwanja wa Ndege, sasa kila kitu nkilitiishwa mioyo ilikuwa inadunda viroho juujuu tukisubiri huku tukisikiliza kwa makini watangazaji wakitangaza kwa kiingereza watu na ndege zao walizokuwa wanapaswa kupakia na kuondoka, Madege yalikuwa yakiingia na kuondoka na mioyo ikitudundadunda  kulikuwa na ugumu sasa kui ilinishika na nilianza kunywa soda sikuwaza hata nikishikwa na haja ndogo itakuwaje.


Unywaji huu wa soda Katika uwanja wa Ndege wa Dar haukuwa wa kawaida ulichangiwa na mapigo ya kasi ya moyo na ukaukaji wa koo kwa sababu tu ya kiherehere cha Safari (Rev. Innocent Kamote)
Ndege yetu sasa ilikuwa imewasili na tulikuwa tayari kuondoka kwa utaratibu maalumu na ulinzi wa hali ya juu tulielekezwa geti la kuondokea tiketi zilikaguliwa na hati zetu za kusafiria sasa nilikuwa nimemkabidhi kila kijana hati yake na nilipofika ndani nilizipokea tena wakati huu tulizima simu zetu, tulikuwana wasiwasi tutazichaji wapi na huenda tutashindwa kupiga picha kwa simu zetu kwani ndani ya ndege ilionekana kama vila simu hazihitajiki hivyo hatukuchukua kumbukumbu yoyote ya ndege yetu ya Kwanza , ilikuwa ni muda wa masaa kama mawili hivi tuliingia Ethiopia Addis Ababa  hapa tukatoa simu zetu na kuziwasha , kulikuwa na mapumziko kiasi kusubiri ndege nyingine, hatukuwa na wasiwasi kuhusu Mizigo yetu, ndege hii tuliyoipanda ilikuwa Boeing 737 kwangu ilikuwa ya kawaida kwa vile niliipanda nilipokwenda Mtwara kutoka Dar, pia nilipokuwa Mafia wazazi wangu walitumia ndege kuja Dare s salaam nyakati za likizo


Tukiwa uwanja wa Ndege wa Ethiopia jijini Addis Ababa ni uwanja wenye Maduka na biashara za aina mnbali mbali eneo hili ni eneo huru kwa shughuli zozote lakini nafikiri shughuli ya kupiga picha nasi tukalitendea haki na vijana wangu kutoka kushoto Mimi Rev. Innocent Kamote, Yohana Komba,Baraka kolombo, William Boniventura,Author Chikoka, wanafunzi wangu waliosimama waliochuchumaa kutoka kushoto ni Imani Mngazija, Onstard Mashauri na Herbet Gumbo. Ethiopia ni moja ya eneo la Afrika lenye vijana watanashati kwa maana ya wembamba na urefu na pia wadada wenye sura nzuri sana na za kuvutia hata hivyo sisi tulikuwa tunapita tu. ndugu Msomaji wangu.

Uwanja wa Ndege wa Addis ababa Ethiopia tukisubiri Ndege nyingine

Kuelekea Marekani toka Ethiopia
Hatukuwa na muda wa kuchaji simu zetu tulizima tena na kupanda ndege kubwa zaidi, hii ilikuwa Boeing 777 sasa hii ilinishangaza kwa vila ilikuwa kubwa sana zaidi ya Boeing 737, tuliruka kutoka Ethiopia Majira ya saa nne usiku na usiku huo ndege ilikuwa ikionyesha katika screen yake kwamba tunavuka bahari ya Mediterranean kuelekea Italy tulifika Fiumucino usiku sana kama saa tisa au kumi usiku wakati huu masaa yalikuwa yanatuchanganya namna ya kubadili na kuyasoma ndege ilitua na kuongeza Mafuta na abiria wa Italy waliruhusiwa kushuka, lakini sisi tuliamriwa kusalia ndani tu, baada ya zoezi la kuongeza mafuta tuliruka tena kuelekea Washington hapa palikuwa mahali parefu lakini sio kama wakati wa kurudi kwani ndani ya masaa kama manne hivi  tulianza kuona mji na wakati huu sasa ilikuwa ni asubuhi majira ya saa mbili au saa tatu hivi asubuhi tuliona misitu mikubwa na nyumba zilizokuwa zimejificha kama zilizokaa pekee pekee hivi na baada ya nusu saa tulitua katika uwanja wa Dulles mjini Washington ilikuwa rah asana kwamba sasa tumefika Marekani, nilikumbuka sana Rome Italy kwani palionekana wazi kuwa mji wenye kuvutia sana na ni mkubwa mmno kwa vile ilikuwa usiku mataa yalijaa katika jiji lile, tofauti na hapa Washington mji ulikuwa mpana sana  na kwa vile tulikuwa tunatua ilikuwa ngumu kuona upana wa mji ingawa ni wazi kuwa Marekani ina miji mikubwa sana, Tuliwasili Uwanjani, hatua za ukaguzi wa hati za kusafiria ulifanyika, na kulikuwana foleni kubwa kiasi, kwa raia wa marekani kama Rev Park walivuka haraka na kwa wageni ilikuwa changamoto kubwa sana niliweza kutambua wageni wengi sana wenye asili ya Ethiopia na wanaigeria ambao tulikuwa nao ndani ya Ndege, Baada ya kuvuka hatua hii tulekwenda kusubiria begi zetu na kutokana na kuchelewa kwenye foleni begi nyingi zilikuwa zimeshafika na ilikuwa rahiri kujichukulia, wenyeji wetu nao walikuwa wamewasili tayari kutupokea hawa walikuwa Jonathan Park pamoja na Samuel Park na wazee na Mashemasi wa Open Door Presbyterian Church walikuja ma Magari mapana kama vibasi kama unavyoweza kufahamu magari ya Marekani ni makubwa makubwa tu Hapa sasa tulitoa simu zetu na kuanza kupiga picha nilikuwa tayari sasa kukusanya matukio tangu hatua ya kwanza mpaka ya mwisho ili nipate cha kuwaelezea Watanzania 

Lilikuwa moja ya magari ya wenyeji wetu ambalo tulilitumia sana kwa mizunguko yetu nchini Marekani Kanisa la open Door Church walikuwa ndio wafadhili wetu wakubwa kwa kila kitu Malazi, chakula na mizunguko yoote

Not Suprized! sikuweza kushangaa!
Mara ya kwanza tulipokuwa tukitokea Dulles Airport kweli sikuweza kushangaa, katika mwezi june tulipotembelea marekani sasa ni tarehe 6 June 2014 majira ya saa mbili saa tatu za asubuhi jula lilikuwa linawaka, sikuona magorofa makubwa sana, niliona barabara ya lami ya kawaida na majengo ya kawaida lakini nilianza kupiga picha moyoni nilikuwa nashangaa Marekani? Ndo hii mbona mazingira sawa na nyumbani niliona kawaida na sikushangazwa 


Hali hii ya mji tukitokea uwanja wa ndege ilinifanya nisione tofauti na nyumbani sasa nilipiga picha lakini nikiwa sina nguvu sana nitaonyesha nini nyumbani mbona kawaida moyoni nikasema It is not Surprise ! Nilipafananisha na maeneo ya Tazara tu pale Dar es Salaam au makutano ya Mandela na Pugu road au Nyerere road kwa jina la siku hizi.

Taratibu Mazingira yalianza kuwa na mvuto, na nikajua kwa vyovyote vile ingawa uwanja wa ndege ni mzuri sana na wa kimataifa huenda majengo yaliyo karibu na Dulles ni ya zamani sana na yametunzwa tu bila kubadilisha maumbile yake kutokana na uimara wake lakini sasa nilianza kuona tofaouti, Nilianza kuona gari nzuri zenye rangi nzuri ni kama mpya hivi, zenye rangi za kung’aa kana kwamba kuna kiwango kuwa gari yako ikichakaa hairuhusiwi tena kuwako barabarani, kila kitu kilionekana kama kipya, Magorofa mazuri lakini urefu wa kawaida kama ilivyo Dar es Salaaam na Tanga, Na mazingira kama Arusha na Kilimanjaro ile kijani yake, Njiani kulikuwa naBarabara pana zenye kuruhusu magari kwenda kwa kasi Fulani na madaraja makubwa yenye kamera maalumu zinazofuatilia mwenendo wa Magari njiani sasa moyo ulianza kuridhika kuwa naam hii ndio Marekani

Mazingira haya yalianza kurudisha tumaini kuwa kumbe kweli Marekani imeendelea lakini bado sikuona maghorofa Marefu kama mtazamo wangu ulivyokuwa, lakini wenyeji walisema hii ndio Washington DC mji ambao ni makao makuu ya serikali ya marekani
Sasa tulifika nyumbani
Tulipelekwa moja kwa moja eneo linalojulikana kama Virginia Tomas Jeferrson Famer na tulipatiwa nyumba ya ghorofa yenye  vyumba vitatu na jiko ba sebule nyumba hii inamilikiwa na kanisa la Open Door Church tulikabidhiwa vyumba na kuweka mizigo na kuelezwa kuwa tutakaa hapo bila muingiliano na wenyeji isipokuwa kwa muda wanaokuja kutuchukua na kutembeza tu, tulifurahia kuwa tutakuwa na wakati mzuri Nyumba ile ilikuwa imejengwa kwa matofali ya kuchoma na mbao ilikuwa nzuri lakini ndogo nje ilikuwa inasomeka namba 2449 tulielekezwa namna ya kufunga kwa namba na kufungua gari pia liliachwa hapo nje na funguo lakini hakuna aliyekuwa na ubabe wa kuendesha



Nyumba tuliyofikia floor ya chini na shughuli ya malaji ikawa kama unavyojionea
Tulielezwa kuwa tupumzike kwa muda na tutafuatwa baadaye

 Eneo la jikoni lilikuwa limesheheni kila aina ya vyakula vinjywaji, mayai, Maziwa mikate, pipoi za aina mbalimbali, maji safi ya kunywa, Nyanya za kusaga, nyama,keki, chocolates, Juisi za aina mbali mbali soda za aina mbali mbali, ilikuwa mtu ushindwemwenyewe kula, Lakini kweli wenyeji wetu na Kanisa la Open door walikuwa wamejiandaa vilivyo kupokea wageni na kuwahudumia kwa ufanisi

 sehemu ya stoo iliyoko Jikoni ikiwa Imesheheni mapochopocho ya aina mbalimbali
Friji likiwa limejaa juisi, maziwa, soda na mayai pamoja na sourcege kwa habari ya kula wamarekani wako mstari wa mbele, Haraka sana tulikinai na kuanza kukumbuka vyakula vya nyumbani ambavyo hapa sasa vilikuwa adimu


 Nikiwa katika harakati za kutafakari nile nini ili nikalale



Kumbuka hata hivyo hatukwenda kula tu Marekani kusudi kubwa la safari yetu ilikuwa ni kujifunza, na kwakweli hatukuwa na muda wa kupumzika tangu tulipofika hata tulipoondoka, wenyeji wetu walituweka bize (busy) Katika kuhakikisha kuwa Malengo yetu ya kujifunza yanatimia na kwakweli ndivyo ilivyokuwa safari yangu nya Marekani ilikuwa ni shule tosha, nataka kuelezea Matukio yote muhmu ya ziara hii tofauti na namna tulivyotembelea nitaanza kuelezea tukio moja baada ya jingine kutokana na umuhimu wake nay ale niliyojifunza.

1.      Abraham Lincoln Memorial
Mahali hapa ni muhimu sana katika kujifunza kupitia Marais wa Marekani wanaoheshimika sana wenyewe huwaita “The greatest Presidents of America” Mmojawao ni Abraham Lincolin ambaye tulitembelea makumbusho yake, hapa nilifuatilia kwa Makini Jumba la kumbukumbu za rais huyo na nilitaka kuandika jambo na niliandika swali Abraham Lincoln ni nani na kuanza kuelezea kama unavyoweza kuona katika mada ifuatyo 

 
Hekalu la kumbukumbu ya Rais wa zamani wa Marekani Abraham Lincolin kama linavyoonekana kwa nje, nilitembelea mahali hapa na kujifunza maswala muhimu kupitia kiongozi huyu.

Abraham Lincoln ni nani?

Mwezi juni 6-20 mwaka huu nilipata neema ya kutembelea Marekani, ambalo ni moja ya Mataifa makubwa na Yenye Kuheshimika sana Duniani, katika siku chache nilizokuweko huko katika program iliyoitwa Vision Trip makusudi yetu makubwa ilikuwa ni kujifunza Maswala Mbalimbali na kasha kuja na kuyatumia yale yatakayoweza kutuletea maendeleo makubwakatika taifa letu, Mimi na wanafunzi wangu tuliotembelea huko tulikuwa tunataka kujua chanzo cha Maendeleo ya wenzetu na kisha tutumie ujuzi huo kuendeleza Taifa Letu kama viongozi wa sasa na wa baadaye

Moja ya maswala Muhimu yaliyosababisha taifa hili kuendelea ni pamoja na kupata neema ya kuwa na Viongozi Bora! Msingi mkubwa wa Taifa hili uliwekwa na rais wa Kwanza Mzee George Washington mzee huyu alikuwa anamcha Mungu na Hivyo Mungu aliwekwa mbele katika taifa hili na ndio msingi wa maendeleo makubwa kwenye taifa hili, hata hivyo leo nataka kumzungumzia  moja ya viongozi muhimu sana ambaye anawekwa katika orodha ya Maraisi wakubwa sana wa Marekani wanaoheshimika the Greatest Presidents of United States Huyu si mwingine bali ni Abraham Lincoln

Abraham Lincoln
Nilianza kuhisi umuhimu wa Rais huyu wa Marekani hata kabla sijaingia Marekani kwenyewe kwani tulipokuwa tumeomba Visa na kufanikiwa kuipata nilitamani kuona Visa ya kimarekani ikoje kwa vile upatikanaji wake nimtihani nilipochungilia visa hiyo haraka sana niliona Jengo muhimu sana lenye kuashiria makao makuu ya serikali ya Marekani US Capitol na picha ya Rais huyo wa zamani wa Marekani, licha ya kuwamo katika mamlaka hayo ya utoaji visa pia Lincon anaonekana katika baadhi ya fedha za Kimarekani Dollar 

Na tulipofika Marekani pale Washington moja ya maeneo tuliyotembezwa ilikuwa ni pamoja na Hekalu kubwa lijulikanalo kama Abraham Lincoln Memorial  nikataka kujua undani wa Rais huyu na kwa nini anatukuzwa sana na kusifiwa? Licha ya kutembelea Makumbusho yake pia nilifika eneo alikouawa na Kupigwa risasi nilikuta watu wengi wanatembelea hapo who is Abraham Lincoln Huyu jamaa ni nani
Sio sisi tu watu wengi duniani kila sikuwanatembelea mahali hapa na kupiga picha kwa kumbukumbu ya kiongozi huyu mkubwa ukiwafanyia watu mema utakumbukwa milele

 Rev. Innocent Samuel Kamote sasa ilikuwa zamu yangu kupata picha ndani ya jengo hilo la kumbukumbu ya Abraham Lincolin, ilikuwa lazima usubiri ili kusudi watalii wapungue upate picha ya utulivu kama hii

Abraham Lincoln Ni rais wa 16 wa Marekani, alilitumikia taifa hilo mwezi March 1861 mpaka alipouawa April 1865, rais huyu aliongoza Marekani katika wakati mgumu kwani kulikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilimwaga damu za wengi, Majimbo saba ya kusini walitangaza kujitenga mara moja mara baada ya kuapishwa kwa Lincoln wakijua kuwa angekomesha shughuli za watumwa, pamoja na kuwa aliongoza katika kipindi kifupi sana Rais huyu alifanikiwa kulijenga Taifa hili Kimaadili, hivyo wamarekani walikuwa na kiwango cha juu sana cha maadili wakati wake, aliimarisha umoja wa Majimbo yote ya marekani, aliimarisha Katiba na kumaliza kabisa migogoro ya kisiasa iliyokuweko kwa kufanya hivyo alifanikiwa sana katika kujenga umoja wa kitaifa wa Taifa la Marekani unayoiona Leo. 

Moja ya Maswala yaliyompa heshima mkubwa huyo pia ni pamoja na kukomesha Biashara ya Utumwa na ubaguzi Amerika alisema “hatuwezi kuwa na uhuru wa kweli katika taifa ambalo wengine ni Mabwana na wengine ni watumwa” Hatuwezi kuwana taifa ambalo wengine wanafurahia uhuru huku wengine wakiwa ni watumwa!”

Licha ya kupngwa na baadhi ya watu waliokuwa wakiwatumia watumwa kwa faida zao, Lincoln ni chanzo kikuu cha kuimarika kwa Uchumi wa wamarekani walio nao leo ndani ya kipindi kifupi alichoonngoza, aliimarisha sekta ya Viwanda, aliimarisha Mabenki, alijenga Mifereji ya kupita chini kwa chini, alijenga reli na kuimarisha ukusanyaji wa kodi, Lincoln alikataa pia kupigana vita au kusaini vita kati ya Marekani na Mexico mnamo mwaka 1846.

Abraham Lincoln
Alizaliwa mwala 1809 na kuuawa mwaka 1865, alitokea katika Familia  masikini nay a kawaida sana Babu yake Samuel Lincoln alihamia kutoka Uingereza, Baba yake aliitwa Thomas Lincolin Abraham Lincoln hakuweza kupata hata elimu ya awali katika familia yake na hivyo alijiendeleza mwenyewe kwa kufanya kazi na kujisomesha, alisoma kwa kutumia taa ya mafuta ya taa, al;ijiendeleza na kufanikiwa kuwa mwanasheria na baadaye kujiunga na siasa nyumba aliyoishi na familia yao mwanzoni ilikuwa ya mbao na yenye chumba kimoja tu, alipojiunga na siasa Lincoln alikuwa na Ushawishi mkubwa sana kiasi ambacho ukimsikiliza akizungumza unakubali kuwa yaya ni kiongozi, alikuwa na uwezo wa kujenga hojana mwenye uwezo mkubwa sana wa Ushawishi, Familia yao ilihamia huko Illinois Jimbo analotokea rais wa Sasa wa Marekani Barak Obama, alipofanikiwa kuwa rais aliondoka Illinois kuelekea Washington akitumia Treni jambo ambalo limewahi kuigizwa na Kiongozi wa sasa wa Marekani.

Aliingia madarakani akiwa haeshimiki sana lakini amepokea Heshima kubwa na nyingi sana baada ya kuuawa kwake, Pamoja na Lincolin kuwa mwanademocrasia mkubwa katika unenaji alikuwa na Madaraka makubwa kuliko raisi yeyote wa marekani aliyepatakuweko kiasi ambacho kimaamuzi ni kama alikuwa Dikteta. Nanaheshimika sana kwa kiwango ambacho jamii kubwa hutembelea Makumbusho yake wakiwemo wayahudi, waasia na watu wa mataifa Mengineyo.

 Wema Hawana Maisha wakale walisema nilifika katika mtaa huu katikati ya mji wa Washington hapa palikuwa ni mbali kiasi na mahali pa kumbukumbu yake mbele ya nyumba hii, kuna jengo la sinema mahali hapo karibu na pasaka Lincolin alikuja kuangalia sinema na wasiopenda Maendeleo walimuua, alipigwa risasi na walimuingiza nyumba hii ya jirani kwaajili ya matibabu na akafariki dunia hapa
 Rev. Innocent Kamote nikiwa mahali alipofia Abraham Lincolin Jijini washingston DC

Lincolin aliuawa kwa kupigwa risasi na wanaosadikiwa kuwa wapinzani wake hususani wa sera ya kukataa kumiliki watumwa wa majimbo ya kusini, aliyemuua alijulikana kwa jina la John Wilkes Booth tarehe 14 April 1865 siku ya Ijumaa kuu wakati alipokuwa ametembelea Ford Theatre. Washington Booth alikuwa amechukizwa alipomsikia Lincoln akizungumza na alikuwa amakusudia kumteka lakini aliposhindwa aliamua kumuua, wakati wa Pasaka hata hivyo lincolin alifariki asubuhi yake Tarehe 15 April 1865 saa moja na dakika 20. Siku ya kuuawa kwake mapema alikuwa na Mawaziri wake na aliwaeleza ndoto yake aliyoiota usiku na wakaitafasiri kuwa ni ya ushindi dhidi ya Sherman na kuwa vita hiyo imefikia mwisho, siku hiyo Rais Lincoln alionekana mwenye furaha kuliko kawaida hata waliomuona walisema haijawahi kuonekana akiwa na Furaha kiwango hicho Lincoln alizikwa nyumbani kwake Springfield kwa Hesmika kubwa za kijeshi, Katika Maraisi wa Marekani hakuna Rais amabaye amaewahi kuandikwa nn maandishi mengi sana Kama ilivyo kwa Abraham Lincolin 

Mambo ya kujifunza:
1.      Kiongozi bora haitaji miaka mingi sana ili aweze kufanya mambo mazuri Lincoln aliweza kufanya mambo mengi mazuri huku akiwa na kipindi kidogo cha uongozi.

2.      Kuweko kwa matatizo hakuzuii shughuli za maendeleo Lincolin aliweza kuleta maendeleo licha ya kuweko na vikwazo na kuwa na wakati mgumu ni vema viongozi wa afrika tukakubali kuwa Mbaazi zikikosa Mvua husingizia jua, kwa Lincoln changamoto alizokuwa nazo hazikuzuia yeye kusababsha maendeleo

3.      Nguzo ya maadili ni nguzo muhimu sana kwaajili ya kujenga ufanisi wa kazi
4.      Taifa lisilokusanya kodi au kutoa mianya ya misamaha ya kodi na ubadhirifu kuendelea kwake ni menemene tekeli na peresi

5.      Viongozi wasiojali matumizi mabaya ya mali za umma matumizi mabaya ya Magari ya serikali watajifunza kwa Lincoln aliyeamua kwenda ikulu akitumia treni

6.      Mwisho nimejifunza kuwa kama Tukiwatumikia watu kwa moyo wetu wote bila kujali ni vikwazo gani tunakutananavyo nkatika maisha yetu ama upinzani toka kwa maadui heshima itatufuata siku zote za maisha yetu hata tujapokufa tutakuwa tungali tunaishi Lincoln anakumbukwa na kuhesimiwa na watu Milele

2. John F Kennedy Memorial.
Eneo lingine tulilopata nafasi ya kutembelea ilikuwa ni makumbusho ya Rais John F Kennedy, lilikuwa ni eneo zuri na lililoonekana la kisasa, likiwa limepambwa kwa maua mazuri, ya kijani na manjano, eneo hili pia ujulikana kama Kennedy Center ndani ilikuwepo kwaya ambayo ilikuwa ikitumbuiza kwa nyimbo, walikuwa wamevaa suti nyeusi ndefu na sketi nzuri ndefu na za heshima, waimbaji walikuwa wanawake kwa wanaume na walikuwa wakiimba kwa ustadi mkubwa tulielezwa kuwa uimbaji huo hufanyika kila siku kuanzia saa sita mchana, pia wanamuziki hutumbuiza nje na kupiga dansi katika eneo hili,eneo hili hutumika kufundishia na kuimarisha wasanii na wanamuziki wanaoishi Washington na maeneo mengine duniani. Hakukuwa na sananu yoyote ya Kennedy kama ilivyo katika maeneo mengine Lakini nilitaka kujua na kujifunza maswala kadhaa japo machache kuhusu Rais huyu na ndipo nilipojifunza kwamba 


John F Kennedy alizaliwa mwaka 1917 na kufariki mwaka 1963, Yeye alikuwa ni rais wa 35 wa marekani, Ndiye aliyekuwa raisi kijana zaidi kuliko wote waliopata kuchaguliwa katika historia ya Marekani, aliingia madarakani mwaka 1961-1963, Bwana Kennedy pia ndiye aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Kikatoliki, kuitawala Marekani na ndiye raisi wa kwanza kuzaliwa katika karne ya 20

Kennedy alikuwa na Urafiki mkubwa sana na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na alikuwa ndiye Rais wa kwanza wa Marekani Kumkaribisha mwalimu Nyerere na kumpokea Ikulu ya marekani kwa heshima kubwa sana  kwa namna ambayo haijawahi kutokea Nyerere alipokelewa kwa heshima kubwa ikulu ya marekani na kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride na kuzungumza machache, Heshima aliyomuonyesha Mwalimu Nyerere ilinitia Moyo kuwa mtu huyu alikuwa hana ubaguzi na alikuwa na mtazamo wulio wazi kuwa wanadamu wote ni sawa ni imani yangu kuwa huenda kuuawa kwa raisi huyu kulikuwa na mchango mkubwa wa kumfanya mwalimu kufikiri aina nyingine za kisiasa Mtazamo wao mwanzoni ulikuwa wenye kufanana

Pichani ni video inayoonyesha Jinsi Kennedy alivyompokea Nyerere Jambo hili lilinifanya nimpende Kennedy na kumuona kama ni Mwenzetu katika ulimwengu wa kukomesha ubaguzi na kuwa na mtazamo wa usawa kwa wanadamu wote kwa video hii utakuwa umetambu Moyo wa John F Kennedy ulikuwa ni wa Namna gani, Marekani ilipoteza na Tanganyika pia.

John Kenedy aliuawa Mapema sana kabla hajamalizia miaka yake mitatu ya Utawala, Lakini mambo makubwa ambayo anaweza kukumbukwa kwayo, alikuwa na sera nzuri za Mambo ya ndani na nje ya nchi, na alikuwa mwenye ushawsishi mkubwa sana kwa dunia ya wakati wake, alikuwa mvumilivu na aliweza kuzuia uwezekano wa kuwapo kwa vita kati ya Marekani na Cuba, kwa kuvumilia bila kujibu Mapigo ya rokesti za Cuba dhidi ya Marekani na hivyo kuizuia Marekani isiingie vitani, Alipendwa sana na vijana na walimkubali, inawezekana kuwa ndiye alikuwa Rais Maarufu kuliko wote waliopata kutawala marekani, Alitambua umuhimu wa kutunza Utamaduni na Historia za Wamarekani wa jamii mbalimbali, na alitambua kazi zote za ubunifu na kuzipa kipaumbele, Kutokana na umahiri wake katika kuzungumza na ushawishi, aliweza kupewa umuhimu mkubwa sana katika maswala ya kisiasa utawala na mafanikio makubwa katika karne ya 20 na amekuwa mfano wa kuigwa.

Rev. Innocent Kamote Nikiwa nje ya John F Kennedy Center Jijini Washington DC

kwa Mbali wanamuziki wa Bendi wakijiandaa kutumbuiza hadharani nje ya Ukumbi wa JFK John F Kennedy aliyekuwa Rais wa 35 wa Marekani


Rev. Innocent Kamote Nikiwa nje ya Ukumbi wa John F Kenedy na wanafunzi wa Living Stone Boys walioteuliwa kwenda marekani sasa tulikuwa tumechoka sana tukisubiri wenyeji wetu waje kutuchukua, karibu nami ni Herbert Gumbo, aliyeinama Imani Mhgajiza, aliyeangalia Pembeni Willium Boniventura, anayefuata Onstard Mashauri na baralka kolombo, wawili hawakuonekana vezuri
Hakuna anayeweza kueleza ni kwanini Kennedy aliuawa haijulikani ni kwa sababu gani, inaonekana kama alipigwa risasi na mtu mmoja aliyejulikana kama Lee Harvey Oswald na ni yeye tu anayejua sababu ya kuumuua John F Kennedy maarufu kama JKF Oswald alikuwa ni Baharia aliyeachishwa kazi, huyu alifupia masiha ya Raisi huyo Mpendwa wa Marekani  Hata hivyo haikujulikana kuwa ni nani alikuwa pamoja na muuaji, kihistoria inasemekana kuwa Oswald alikuwa na siasa la mrengo wa Kisoviet na mwenye kuunga mkono misimamo ya Cuba na labda sababu hizi zinaweza kuwa zilichangia kuuawa kwa Kennedy lakini nani anaweza kusema chochote kwani kukubali hilo kungemaanisha kuwa wacuba na warusi walifanikiwa katika karata hii waloicheza.

Yote katika yote Burudani na kwaya tulizoziona zilikuwa zinaashiria kuwa Kennedy atakumbukwa kwa kukuza na kulinda Utamaduni wa wamarekani na kusaidia kukuza vipawa kwa wasanii kazi inayofanyika hata leo  
 
 3.   Thomas Jefferson Building.
Eneo La tatu ambalo tuitembelea na kujifunza maswala mbali mbali ni Jengo maarufu lijulikanalo ka Thomas Jefferson Building, Jengo hili pia linajulikana kama Library of Congress, Jengo hili haliko mbali sana na mlima ujulikanao kama capital hill ambao niytauzungumzia baadaye, inasemekana kuwa jengo hili limejengwa mwaka 1897 hata hivyo lilionekana imara na la kisasa tu, kihistoria jengo hili inasemekana lilijengwa na Rais John Adams na ndipo eneo ambalo aliweka saini ya kuhamishia mji mkuu wa serikali ya marekani kuwa Washington, mahali hapa palikusudiwa kuwa Library ya vitabu vya kisiasa na huenda ilikusudiwa kwa wao tu vitabu vipatavyo 740 hivi vilikusanywa, mwaka 1814 Majeshi ya uingereza yaliharibu jengo hili na kuchoma sehemu hiyo ya Libray ndogo iliyokuweko, Rais Thomas Jefferson aliyekuwa akiishi Monticello baada ya kustaafu alitoa sehemu ya Library yake ili kufidia Library hiyo, Jefferson alikusanya vitabu 6,487 na fedha zipatazo $23,950 zilikusanywa na kuibadilisha Library hiyo kuwa ya kitaifa, rais Jefferson aliamini kuwa kujifunza ni kwa muhimu sana au Elimu ni ya muhimu sana kwa wamarekani kutokana na falsafa yake ya kutaka watu wajisomee ghorofa ya pili ya jengo hili ilipewa jina la Heshima kwa Thomas Jefferson na mwaka 1980 Maktaba hii ilipewa jina la Rasmi kama Thomas Jefferson Building


Library of Congress kwa jinsi ilivyo ndani sasa inajulikana kama Thomas Jefferson BUILDING

Thomas Jefferson Ni nani

sasa nilitaka kujua kuwa Thomas Jefferson ni nani Kule Virginia tulikofikia nyumba tulizokuwa tunakaa zinajulikana kama Thomas Jefferson Farmer na kila mahali iliko tembelea ikiwa ni pamoja na chuo kikuu cha Virginia ambacho nitaeleza habari zake baadaye nilielezwa na wenyeji wetu kuwa pia kilianzishwa na Thomas Jerferson, niliambiwa kuwa katika Orodha ya maraisi wakubwa wa Marekani yeye ni mmoja wao, wenyeji waliniambia kuwa Thomasi Jefferson alikuwa na uwezo wa kuzungumza lugha kubwa Tano zilizoko ulimwenguni, alipenda kusoma na anamchango mkubwa sana katika Elimu na maendeleo ya taifa hili kubwa la Marekani huyu jamaa ni nani hasa 

Thomas Jefferson alizaliwa Apil 13 1743 na alifariki July 4 1826 jumla ya uhai wa maisha yake ni 83 alikuwa raisi wa tatu wa Marekani ni mmoja wa Mababa wa taifa hili au maraisi wajumlishwao katika kundi la "The greatest Presidents of United States of America" aliiongoza Marekani kuanzia 1797 - 1801 akiwa makamu wa rais na aliingia Madarakani kama rais 1801-1809 Thomas Jeferson alikuza sana Demokrasia na Haki za kiraia jambo lililopelekea wamarekani kukataa kushikiliwa mambo yao na waingereza na kujitoa katika ukoloni wa kiingereza na kuwa taifa huru linalojitegemea
 Jeffersona alikuza Biashara na kuweka mikataba na kanuni za kibiashara ili kujikinga na wafanya biashara wa kiingereza waiokuwa wakijipatia faida kwa kujifanyia Biashara Marekani bili mpango, aliingia mkataba na kutafuta kuongeza mipaka mikubwa ya nchi kwa kuliongeza jimbo la Louisiana na kusababisha wafaransa kuingia mkataba wa amani, Alipunguza  Idadi kubwa ya Majeshi, Katika kipindi chake cha pili cha uongozi 1804 Jefferson alikutana na changamoto na upinzani wa ndani toka kwa makamu wake Aaron Bur, hata hivyo Jefferson pia alipingana na maswala ya kusafirisha watumwa na kutokana na umahiri wake na upenda haki Historia inamuweka Jefferson kama kiongozi mwenye mafanikio Makubwa miongoni mwa Maraisi wa Marekani.

Jefferson alikuwa mtu mwenye ujuzi na utaalamu wa maswala mbalimbali alikuwa na ujuzi wa hisabati, tamaduni na maswala ya uvumbuzi, alikuwa pia na shauku katika maswala ya Dini na Falsafa na hivyo alipewa jina la Rais wa Jumuiya ya wanafalsafa wa Marekani Presidency of American Philosophical Society , alijaribu kuzileta Dini pamoja ingawa alivuta na Ukristo lakini pia aliamini katika Imani iitwayo Deism (Deism wanaamini kuwa Mungu alipouumba ulimwengu aliuacha ujiendeshe wenyewe na hashughuliki nao tena) Ukiacha uwezo wake wa kuzungumza kiingereza, Thomas Jefferson alizungumza Kilatini, Kigiriki, Kifaransa, Kiitalia na Kihispania, alianzisha chuo kikuu cha Virginia University of Virginia (UV0, Na alipostaafu aliandika kitabu kirefu sana kiitwacho Notes on The State of Virginia 1785 kitabu hikim kinasadikiwa kuwa moja ya kitabu muhimu sana kilichochapishwa kabla ya maiaka ya 1800 ni ktabu chenyematamko,Lugha ya kiingereza na historia ya marekani, Thomas alimuoa mwanamke ajulikanaye kama Martha Wayles Skelton na kufanikiwa kuzaa naye watoto sita lakini ni mabinti wawili tu walioweza kufikia utu uzima, alikuwa na mashamba makubwa na watumwa wengi sana inasemekana baada ya kifo cha mke wake mwaka 1782 alikuwa na uhusiano na sally Hemings na kuzaa naye baadhi ya watoto alifariki nyumbani kwake  Charlottesville Virginia July 4 1826 akiwa na miaka 83.

Chuo Kikuu cha Virginia (UV) sehemu ya mabweni ni yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi wengi Chuo Hiki kilianzishwa na rais Thomas Jerffeson

Miundo mbinu ya hali ya juu chuoni hapo Hutoa Morali kwa wanafunzi kujisomea

Mabwawa ya kisasa ya kuogelea ni moja ya Maswala muhimu katika kuimarisha mazoezi na ushindani wa Mchezo huo hapo pia ni Chuo kikuu cha Virginia Kilichoanzishwa na rais Thomas Jefferson sasa unaweza kutambua kwanini Rais huyu alikuwa  wa muhimu

 vyumba vya mazoezi ndani ya chuo
Uwanja wa Michezo wa Kisasa chuoni UV baadhi ya wanafunzi wa Living Stone niliokwenda nao wakishangaa

Vyumba vya madarasa ya chuo kikuu cha Virginia

Kumbi nyingine za Lecture yenye miundo mbinu ya Kisasa

 Chumba chenye uwezo wa kukusanya wanafunzi wengi zaidi na kutumia mfumo wa Projecters kufundishia
 Nikipumzika kidogo ndani ya longe ya Chuo kikuu cha Virginia
Tayari kwa kuondoka na kuendelea na Safari


Electronics Libray kitengo cha ICT ni vya Kisasa kweli kweli


Wanafunzi wakifurahia kujisomea chuo kikuu cha Virginia

Ujenzi wake ni wa hali ya juu mahadhi ya Kiitaly na kiyunani yanaonekana wazi kabisa



Chumba kingine cha Kujisomea

Libary ya vitabu vya aina mbalimbali




sehemu za kusomea katika Library ya Virginia

vipande hivi vya ukuta tulivikuta hapa University of Virginia  na wenyeji wetu walituambia kuwa vipande hivyo vya ukuta vilivyohifadhiwa kwenye kioo ni sehemu ya vipande vya ukuta wa Berlin kutoka Ujerumani na vimehifadhiwa kama kumbukumbu katika chuo hiki

 Kanisa Dogo ndani ya Chuo kikuu cha Virginia tulielezwa kuwa sababu kubwa ya Maendeleo na siri kuu ya Maendeleo ya marekani ilikuwa kumcha Mungu japo siku hizi mambo yameparaganyika hata hivyo watu wamchao Mungu ni wengi
Uwanja mkubwa wa wazi eneo la katikati ya chuo kiuu cha Virginia kilichojengwa na Thomas Jefferson kama unavyoonekana hapa 

Rev. Innocent Kamote Nikiwa Chuo Kikuu cha Virginia Nchini Marekani nilipotembelea kujifunza maswala ya Maendelo, Nyuma ni sanamu ya Mwanzilishi wa chuo hiki kikuu Rais wa tatu wa Marekani Muheshimiwa Thomas Jerfferson


4. University of Virginia.
Kama ulivyoweza kuona hapo juu singeliweza kuzungumzia eneo hili la nne  bila kumuhisisha Thomas Jefferson , Kumbuka nilikuwa nikiiielezea Libray of Congres na nikajikuta naelezea Habari za Thomas kwa vile Library hiyo pia inaitwa kwa jina lake Thomas Jerfferson Building, tulipokuwa nchini Marekani tulitembelea pia chuo kikuu cha Virginia chuo hiki kilianzishwa na Rais wa tatu wa Marekani Bwana Thomas Jefferson na huenda hii ikawa ni moja ya sababu ya kuheshimika sana ka kiongozi huyu alijishughulisha na kuwaelimisha watu, chuo hiki kama ulivyojionea katika picha kina madhari nzuri na kikubwa sana pia kina mazingira ya utulivu wa hali ya juu swala linaloruhusu watu kujisomea kwa uhuru
Chuo Hiki kina makaba nyingi sana za fani mbalimbali kwa mfano ziko Library zifuatazo na kuzidi
  • Library ya Science & Enginnering
  • Library ya Astronomy
  • Biology/ Psychology Library
  • Chemistry Library
  • Clemons Library
  • Education Library
  • Fiske Kimball Fine arts Library
  • History and Litereture and Culture 
  • Music Library
  • na special Collection Library
Unaweza kupata picha kuwa watu hawa wamekusudia kwa kiwango kikubwa kusonga mbele na kwa kweli wako Mbele, Library ya Komputa tuliyoitembelea na kitengo cha Kompyuta tulielezwa kuwa kila siku wanafanya utafiri na kugundua jambo jipya katika maendeleo ya teknolojia hiyo, Elimu na kuelimisha watu sio jambo la kuliletea Mchezo, chuo hiki kilijengwa zamani lakini kimetunzwa na kinaonekana kama kipya, nilianza kulinganisha na Taifa letu ambalo huenda labda linafanana na mataifa mengine ya Afrika ambapo vitu vilivyoanzishwa zamani vinakufa au kuuawa kisiasa badala ya kutunzwa, wamarekani wanatunza kila kitu, wanaweka kumbukumbu ya kila kitu, hawaachii kitu chochote kipotee bila shaka wanatambua kuwa hakuwezi kuweko maendeleo bila Mwanadamu kuangalia Historia yake ninapoandika haya naamini ya kuwa utafahamu kuwa kwenda kwetu Marekani hakukuwa kwa kisanii tu ilikuwa tujifunze kitu.
Kwa ujumla wenyeji wetu walitueleza wazi kuwa katika jamii ya waafrika ambao wamewahi kutembelea marekani kuna uwezekano wasiwepo watu waliopata kutembezwa sehemu mbalimbali na nyeti kama ilivyo kwenu, walisema sehemu nyingine tulizotembelea hata wale wenyeji wa Marekani waishio huko hawajawahi kufika kamwe na kuwa ingewagharimu sana sana kutembelea maeneo hayo.

5. Kutembelea Basilica of the shrine of the Immaculate Conception
hili lilikuwa moja ya maeneo muhimu tuliyotembelea Nchini Marekani jijini Washington, ziara yetu ilikuwa ya kitaaluma lakini kwa namna fulani ya kidini pia ilikuwa ni mchanganyiko wa Mambo, Eneo hili ni sehemu ya Kanisa Catholic  ni eneo ambalo watu wengi hutalii na wengine hutoka mbali sana na kufanya hija katikakanisa hili, ni Moja ya makanisa ambayo ujenziwake ni waajabu sana lina michoro mizuri na ya kuvutia na linaonyesha uhodari wa Mafundi katika kuremba na kuliunganisha kuwa moja kama jiwe kanisa hili linaonyesha utajiri wa kitamaduni na ujenzi walio nao Mafundi wa Marekani tulijifunza mambo mengi na kupata nafasi ya kuomba

Kwa Mbali nyuma yangu sasa Unaweza kuliona kanisa hili ambalo limejengwa kitaalamu sana
kanisa hili lilijengwa kutokana na wazo lililotolewa na Askofu Thomas J Shahan aliyekuwa kiongozi wa kanisa hilo na mkuuwa chuo kiitwacho nCatholic University of America , yeye alitoa wazo kuwa lijengwe kanisa la kumbukumbu ya Mariam katika hadhi ya kitaifa , alipeleka mpango wake kwa Pope Pius X mwaka 1913 na wazo lake licha ya kukubaliwa bali liliungwa mkono pamoja na msaada kutoka kwa Pope, Maginnis na Walsh wa Boston walichaguliwa kuwa Mafundi na wabunifu na Kanisa hilo likamaliziwa na James Cadinal Gibbons, askofu Baltimore aliweka jiwe la Msingi mwezi September 23 1920 na kanisa lilimalizika 1926 likiwa kamili Mwaka 1931 Askofu Shahan alifariki na ilikuwa ni miaka ya mambo magumu, miaka ya baadaye maaskofu waKanisa Catholic walifanya bidii ya kumalizia ujenzi kwa kuchangisha fedha za wamarekani wenyewe  na november 20 1959 Kanisa hili la kitaifa liliwekwa wakfu na Pope John Paul wa pili.
 Njia za kanisa hili na madhari yake inavutia na kweli waamini waliamua kuwekeza
 Kamvua kalikuwa kamenyesha ingawa hatukuloa ilikuwa Baraka wakati tunalitembelea Kanisa hili
 Ni mlangoni mwa Kanisa hili zuri lililoungwa na kuwa kama jiwe mlangoni Pameandikwa rejoice in the Lord
 sasa waweza kuona milango ya Pembeni ya Kanisa hili na jinsi lilivyopambwa na kujengwa kitaalamu
 viwanja vya kanisa hili vikiwa safi nashukuru hatukutembelea wakati wa Baridi


 Author Chikoka mwanafunzi wangu akiwa ndani ya kanisa hili
Mimi mwenyewe mkuu wa wajenzi kwa mbali wageni wengine wakiomba dua ndani ya kanisa hili
 


6. Kutembelea Washington National Cathedral
Washington National Cathedral ni moja ya mahali pazuri na pa Muhimumu ambapo nilipata nafasi ya kutembelea na wanafunzi wangu, Kanisa hili nilielezwa kuwa ni Cathedral la mtakatifu Petro na Paulo na liko katika jiji la Washington, Wageni wengi sana hutembelea Kanisa hili kwa ajili ya maombi lakini pia kushangaa ujenzi wake ambao ni wa hali ya juu sana , Kanisa hili limejengwa kwa tamaduni mchanganyiko za majengo ya Waingereza, Ni mahali pazuri sana ni kanisa la Kiaskofu kwa maana anayekuwa askofu mkuu wa Marekani jijini Washington ndiye huendesha ibada zake hapo kama ilivyo kwa St Joseph pale kwetu Dar es Salaam, Viongozi wengi na wakubwa wa kisiasa huabudu katika kanisa hili, inasemekana kuwa lilijengwa kuanzia mwaka 1907 tarehe 29 mwezi wa tisa, Msingi wa Kanisa hili uliwekwa na Rais Theodore Roosevelt na lilikamilika katika mtazamo wa kisasa baada ya miaka 83 na kazi za upambaji zilikamilika wakati wa utawala wa Rais George H.W. Bush mwaka 1990, tulifanya maombi katika kanisa hili kwa vile siku tuliyotembelea sisi hakukuwa na ugeni mwingi wa watu hivyo tulikuwa na Muda mzuri wa kushangaa ufundi huu wa kizamani sana lakini imara wenye kudumu na wenye kuvutia. Kanisa hili lilitumika kama Nyumba ya maombi kwa wanasiasa na wakati wa vita vya pili vya Dunia ilitumika kama sehemu ya uwakilishi ya kuwaombea wamarekani
Washington National Cathedral
 


 Hapa nikiwa nje ya Kanisa la Washington National Cathedral kwa pembeni
 Hapo nikiwa nje ya washington Cathedral kwa upande wa Mbele
Hapo nikiwa nje ya washington Cathedral kwa upande wa Mbele
 Nikiwa Ndani ya Washington National Cathedral

6. Kutembelea Open Door Presbyterian Church

Kwa ujumla hawa ndio walikuwa wenyeji wetu ingawa tulikuwa katika ziara na tulianza kwa kutembelea maeneo mbalimbali wakati sasa ulifika kuhudhuria ibada, ilikuwa jumapili, niliamka mapema sana na vijana wangu tulikuwa tayari tumekwisha jiandaa kwaajili ya Ibada ibada ilikuwa inaanza majira ya saa tatu na nusu mpaka saa tano hivi, hata hivyo kulikuwa na ibada nyingine za vijana zilizotangulia tulifika katika kanisa hili ambalo kwa nje lilikuwa linaonekana kama dogo, lakini kumbe limejengwa sehemu iliyoinuka kwa ustadi mkubwa na chini ni kubwa na lina kumbi nyingi za kutosha, Mbele ya kanisa kulikuwa na screen kubwa kwa ajili ya kuonyesha nyimbo zilizokuwa zinaimbwa na timu ya kusifu na kuabudu, ukumbi ulikuwa unaonekana kama uliojengwa kutoka juu kuelekea chini, na kulikuwa na kama aina ya giza lililodhibitiwa na taa za aina mbalimbali
tulipoingia ibada ilianza kama Kawaida na Rev. Kim alitutambulisha aidha pia tulipata nafasi ya kuimba mimi pamoja na wanafunzi na baada ya ibada nilipiga picha nje ya Kanisa hili kwenye uwanja uliokuwa na nyasi za bandia
 Madhabau ya OPDC open Door Presbyterian Church
 Praise team wakiongoza ibada kwa nyimbo za kuabudu na kusifu

 screen za Open Door pia ziliweza kuonyesha  picha za Maisha ya Living Stone Boys' Seminary
 Na Hapa nje nilipata kumbukumbu ya picha ya Kanisa hilo
Uwanja wa nje wa kanisa la OPDC ukiwa na nyasi za bandia 

7. Kutembelea Ubalozi wa Tanzania Jijini Washington

Katika safari yangu ya Marekani moja ya maeneo ambayo sitweza kuyasahau ni Ubalozi wa Tanzania pale Washington sasa siku kadhaa zilikuwa zimekatika na tayari hamu ya nyumbani ilianza kujitokeza ndimi zetu zilikuwa zimeumia vya kutosha pamoja na ubongo wetu kuzungumza kiingereza kwa muda wote, kuingia ubalozini ilikuwa kama tumefika nyumbani bila shaka hata wenyeji wetu walifurahi sana kwani nao walianza ku floor kiswahili viceko vilitawala kana kwamba sasa tuko nyumbani, Undugu na muunganiko wa upendo wa hali ya juu unajitokeza, Ubalozini maafisa wote wanaona kama wametembelewa na wageni wa Ngazi ya juu sana ilikuwa ni heshima kubwa sana Ubalozi wetu ulikuwa umepambwa vizuri na madhari za mapambo ya kitanzania pia matangazo mbalimbali, Mahali hapa tulipokelewa kwa heshima na Furaha kubwa sana

 Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Washington Marekani tulipotembelea  june 2014

Hapa nikiwa na wanafunzi wangu kutoka Living Stone Boys' Seminary Muheza Mkoani Tanga tukiwa tumetembelea Ubalozi wa Tanzania mjini Washington Marekani Kutoka Kushoto ni Yohana Komba, Onstard Mashauri, Imani Peter, William Boniventure, Baraka Kolombo Author Chikoka, Rev. Innocent Kamote na Hubert Gumbo



 Ndani ya Ukumbi mdogo wa mikutano Ubalozi wa Marekani tukiwa na Mazungumzo na afisa Ubalozi
 Nikakalia kiti kile wanachokalia waheshimiwa wote waendao Ubalozini kwetu
 Nikapiga picha hapa kwenye mapambo ya Matangazo ya vivutio vilivyoko Tanzania ubalozini
Lakini haikuwa vema kutokuacha alama Ubalozini kuwa nilitembelea nikasaini kitabu cha wageni

8. Kutembelea America Air and Space Museum 

hakukuwa na Muda wa kupoteza kwa kweli, tulikwenda darasani, na kusudi ilikuwa ni kujifunza maswala kadhaa kwa faida ya taifa letu, Wenyeji walikuwa wakarimu sana na sasa niligundua kuwa kila mwanadamu anaweza kuwa mkarimu na muungwana bila kujali aanakaa wapi, wenyeji wetu walitupeleka Mahali hapa Air and Space Museum Kubwa tulilojifunza hapa ni kuwa ziko ndege za aina mbalimbali na wenzetu waligundua utengenezaji wa Ndege za aina mbalimbali na teknolojia hii ilianza mapema sana.

America Air and space Museum ni eneo katika jimbo la Virginia jijini Washington kwa kifupi Museum hii inaitwa NASM yaani National Air and Space Museum mahali hapa pana mkusanyiko wa kumbukumbu ya Madege au ndege za aina mbalimbali, Palianzishwa mwaka 1946, watu wengi sana wageni kwawenyeji hutembelea mahali hapa na hivyo kusababisha mamilioni ya watu kutembelea hapo kwa mwaka.

Tulishuhudia Ndege za aina mbali mbali ndogo kwa kubwa na pia za kivita, aidha ndege au vyombo vilivyotumika kupaa mwezini yaani Apolo 15 pia na mavazi yaliyotumiwa na watu waliokwenda mwezini kwa mara ya kwanza yalikuwa yamehifadhiwa hapo, Hakukuwa na mengi ya kufanya kwani baada ya kupata Maelezo ya kina na ya kutosha sasa shughuli ilikuwa ni kupiga mipicha tu na hivi ndivyo ilivyokuwa

 Ndege za aina mbalimbali zikiwa zimehifadhiwa katika makumbusho ya Taifa ya Marekani
 Ndege za aina mbalimbali za kizamani zikiwa hifadhini wamarekani wamejitahidi kutunza kumbukumbu za kila jambo na kila kitu

 Aina za ndege za mwanzoni kabisa ambazo zilitumia nguvu ya upepo kupaa
 Nikiwa nje ya air and space museum Jijini Washngton DC katika jimbo la virginia

 Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima akiwa nje ya Jenzo la air and Space museum jijini Washington june 2014.
 Hapo ni mavazi na vifaa vilivyotumiwa na watu walioshuka mwenzini kwa mara ya kwanza


 Na tukapiga picha na wanafunzi wangu mikononi tukiwa na diary kwaajili nya kuandika maswala kadhaa tuliyokuwa tukijifunza Picha kwa Hisani ya Rev. Innocent Kamote, Mkuu wa wajenzi.


Nje ya Meuseum Magari mengi sana yalikuwa yameegeshwa kuonyesha  idani kuu ya watu wanaohudhuria hapa.

 Juu ni chombo cha kukusanya taarifa kilichoko za maswala ya angani yetu yalikuwa macho tu, ni lazima elimu iwe kigezo kikuu cha kuwapa watoto wetu na kujifunza ili tuweze kufikia huku walikofikia wenzetu

 Ndege nyingine nyingi za kivita na za aina mbalimbali zilikuwa zimehifadhiwa nilipiga nne na kupata picha katika kieneo hiki maalumu kwa shughuli hiyo kama unavyoweza kuona

 Ndege hii iliyoko Nyuma yangu ni Ndege ya kivita ambayo hutengenezwa na Wamarekani ni ya gharama sana na hutengenezwa kwa madini maalumu wenyeji hawakuyataja ambayo husababisha Rada za ndege kutokuwa na uwezo wa kuiona ndege hii hapa ilikuwa imehifadhiwa na nikachukua picha kupata kumbukumbu hii Muhimu


9. Kutembelea Ikulu ya marekani (White House)
wenyeji wetu walituambia kuwa tungeweza kutembelea ikulu ya marekani na hata kuingia ndani, lakini kutokana na kupungua kwa Usalama duniani au kuweko na kutokuaminiana kulikokua kwa kasi an chuki dhidi ya taifa hilo kubwa tungeliweza tu kuruhusiwa kufika karibu na ikulu hiyo na kupiga Picha, palikuwa ni mahlia pazuri na kila mmoja alifurahia kuliona Jengo hilo japo kwa nje, Zilikuwa ni kama ndoto ambazo zinatimia kwa vile mara kwa mara tuliona jengo hilo katika sinema na taarifa za habari, lakini sasa tulipata nafasi ya kufika kwa ukaribu na kupiga picha na mambo yalikuwa namna hii kama unavyoweza kuona katika picha.

Ikulu hii kwa nje inaonekana kama ni jengo Dogo sana lakini ukweli ni kwamba ni jengo kubwa na lina eneo kubwa la utendaji wa kazi za chini ya Ardhi, wenyeji walituambia kuwa katika watu waliopata Kutembelea Marekani kuna uwezekano hakuna waliopata kufika sehemu nyingi kama ninyi

 Ikulu ya Marekani nyuma ya sanamu ya Abraham Lincolin

 Ikulu ya Marekani jijini Washington DC kwa upande wa Mbele watalii hatukuwa wenyewe bali hata wazungu na watu wa mataifa kadhaa hufika mahali hapa na kupiga picha pia nilikutana na wahubiri wa injili ya Mashahidi wa Yehovah Mahali hapa na tukabadilishana nao mawazo.
 nikichukua Picha zaidi za Kumbukumbu

Nikiwa na wanafunzi wangu niliokwenda nao Marekani, kutoka Living Stone Boys'  Seminary Kutoka kushoto, Arthur Chikoka, Mimi Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima Rev. Innocent Kamote, William Boniventure Kifutumo, Yohana Martin Komba, Imani Peter Mngazija, Onstard Mashauri, Hubert Gumbo, na baraka Kolombo june 2014 tulipotembelea Marekani.


10. Kutembelea Capitaol 

Jengo hili ni mahali maalumu kwaajili ya Bunge la Marekani na ni mahali ambapo panmatumika kuapishia maraisi wa marekani, ni jengo zuri sana na kimtazamo linaweza kuzidi lile la Ikulu ya marekani, watu wengi sana hufikiria kuwa Jengo hili ndio ikulu Yenyewe lakini Hapana ni jengo kubwa na limejengwa juu ya Kilima Jengo hilo lilikamilika kujengwa mwaka 1800 lakini mara kwa mara lilifanyiwa ukarabati wa kukamilisha Dome lake kwa kuliiimarisha au kulipanua zaidi, kwa kanuni za Mji wa Washington DC hairuhusiwi kwa mtu yeyote kujenga nyumba ua Ghorofa inayozidi urefu wa Jengo hili na hii ndio sababu iliyopelekea mji wa Washington usiwe na Magorofa makubwa ambayo sisi tuliyatarajia, Jengo hili ni Jeupe lakini majengo mengineyo kati ya mji huu hayaruhusiwi kujipakia rangi unyaotaka bali wanaacha rangi ya tofali au cement yenyewe au marumaru za kizamani tupate picha zaidi za Madhari kamili ya Jengo hilo
Us Capital kama panavyoonekana juu kabisa iko sanamu ya Mwanadamu, hatukuweza kupata maelezo kuwa ni sanamu ya nani, Lakini amevaa Kofia na juu yake ametua Ndege aina ya tai ambaye ni alama kuu na muhimu kwa taifa la Marekani sisi nasi tulitia timu mahali hapa muhimu

Nikiwa katika Jengo hili Muhimu katika Jiji La Washingtone DC Capitol hapa nikiwa nimeikanyaga
 Rev. Innocent Kamote akiwa Jijini Washington Capitol ikionekana kwa Mbali
 Rev. Innocent Kamote akiwa Jijini Washington
 Rev. Innocent Kamote akiwa Jijini Washington
 Rev. Innocent Kamote akiwa Jijini Washington




11. Kutembelewa na Bibi Lucy Mgaya Mkumbukwa
Tukio lingine la furaha ambalo ni vigumu kusahaulika ilikuwa ni pale nilipokuwa nyumbani kabla sijaenda Marekani, Bibi yangu Mzaa mama Yaani Ester Kamote mama yangu, Huyu Bibi mzaa Mama alikuwa amekwenda Marekani yapata miaka nane iliyopita, wakati huu ilikuwa kimya na alipiga simu mara chache, lakini kutokana na kukua kwa teknolojia ya mitandao na simu, niliweza kuwasiliana na Bibi nikiwa nyumbani Tanzania na nilimueleza kuwa nitakuja marekani na nitakaa Virginia wakati ninamueleza Bibi ilikuwa ni taarifa tu, sikufikiri kama Bibi angeliweza kuja kuniona nilijua itakuwa ngumu kumuelekeza niko wapi na haingekuwa rahisi, nilifikiri Bibi yuko mbali sana lakini alinieleza kuwa anakaa Maryland pia sikuwa najua Maryland iko wapi katika majimbo ya marekani, lakini ilikuwa ni mradi nimemjulisha tu kwamba ninakuja huko, Nilipofika Marekani na kwa sabbau tuliweza kutumia simu zetu kupata mawasiliano ya mtandao kama Facebook, Whatsup na vikolombwezo vingine, nilimweleza bibi nilipofikia, aidha nilimjulisha namba ya nyumba tuliyofikia pale virginia, katika namna ya kushangaza Bibi alinipigia simu iliyokuwako mezani, sikuweza kiuamini kuwa ni Bi Lucy Mkubukwa Mgaya kwani Yeye akiwa na Mchngaji wake huyu Msukuma na dada mmoja wa kichaga Oliver Lymo walitinga nyumbani asubuhi kuja kutusalimu, tulifarijika sana sana na tulifurahi, ilikuwa ni kama tunaota lakini kumbe ilikuwa kweli, wote walifurahi na wanafunzi wangu pia tuliungana na kuwa kama familia moja bila kujali kuwa alikuwa bibi yangu mimi mbona aligeuka kuwa bibi wa wote na mchungaji akawa wetu wote na Oliver akawa dada yetu ghafla na mwisho, Bibli alifungua zawadi, alikuwa ametuletea Pilau, na mihogo, mahindi ya kuchemsha na maandazi, siku hii tuliacha kula vyakula vya kimarekani na tilikula vyakula vyenye kufanana na vya kitanzania, nilimuuliza bibi  kuwa alivitoa wapi, alisema kuwa kuna mahali vinapatikana na alisema kila kitu kinapatikana Marekani, nilishangaa lakini kwa vile yeye ni mwenyeji anafahamu ni wapi ametoa hiyo kitu.

 Bibi Lucy Mgaya Mkumbukwa akiwa na wajukuu zake alipotutembelea Virginia

 Rev. Innocent Samuel Kamote nikiwa na Bi Lucy Kushoto na Oliver Lymo Kulia

  Mchungaji wa Bibi na William Boniventura Kifutumo wasukuma hawa walikutana Marekani
 Nikiwa na Bibi ilikuwa furaha kubwa sana
 Rev. Innocent Kamote na Bibi Lucy Mgaya Mkubukwa tukiwa Virginia Marekani
 Nikiwa na Bi Lucy na Oliver Lymo tukiwa na furaha ya kuonana ughaibuni


Nyumbani Virginia Washington Marekani.

 Oliver Lymo akionyesha vituko alikuwa dada mcheshi na utadhani tulionana na kufahamiana miaka mingi

 12. Kushuhudia harusi ya Meneja wetu nchini Marekani.
ukiachia kuwa na ziara ya kipekee Meneja wetu wa Living Stone Boys seminary Rev. Andrew Park alikuwa na wakati wa kufunga Ndoa na Mke wake mpya baada ya mkewe wa kwanza kufariki Dunia nchini Tanzania mjini Tanga kwa ugonjwa wa Kansa ya mapafu, Mchungaji, aliamua baada ya miaka miwili kuoa mke mwingine na katika safari hii tuikiwa Marekani kwa vile Mchungaji park pia ni raia wa Marekani alifunga Ndoa na Kim na sisi tuliishuhudia harusi hiyo na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa
















Matukio wakati wa harusi ya Rev. Andrew Park Meneja wa Living Stone Boys' Seminary na Madam Kim, Kutoka Kushoto Onstard Mashauri, Rev. Innocent Kamote, Ather Chikoka, Park and Kim Maharusi, Yohana komba mwenye mawani, Baraka Kolombo kulia mwishoni, walioketi kutoka kushoto Imani Mngazija, Wiliam Boniventure Kifutumo na Hubert Gumbo picna na maelezo kwa Hisano ya Rev. Innocent Samuel Kamote Home Bible Library.

13. Kutembelea mji mkuu wa Marekani New York 
Ni lazima tutawapeleka New York, ni lazima mkapaone sio mbali sana ni mwendo wa Masaa manne tu kutoka Hapa Washington huko ni kuchangamfu sana ni kama Kariakoo ya Dar es Salaam ndiyo yalikuwa Maneno ya wenyeji wetu walipokuwa wakitutaarifu kuhusu Mji huu wa kimataifa, ni kweli Washington ni mji mtulivu sana na hakuna fujo na makelele ni mji ambao watu hufanya shughuli zao wakiwa na utulivu, Hakuna magorofa marefu sana Washington labda kwaajili ya ile amri ya kutokuruhusiwa kujenga Jengo linalozidi lile la Bunge yaani Capitol, Lakini sivyo ilivyokuwa New York, Ni mji wenye vituko vya kila aina biashara mpaka za barabarani, mchanganyiko wa watu wa aina mbalimbali na maghorofa Marefu sana.

Tuliondoka asubuhi sana siku hiyo Jack Mkorea anayeishi Marekani alikuwa ndiye Dereva wetu, ilikuwa safari ndefu kweli ilitugharimu masaa manne, hatimaye sasa tulipita chini ya bahari, kwa daraja maalumu sana lililojengwa chini ya Bahari kwa ustadi maalumu kuingia katika mji wa New York kwa gari hatimaye tulifika jiji hili, wenyeji walituambia hatuwezi kuumaliza mji huu wote lakini njia rahisi ni kupanda juu ya ghorofa ijulikanayo kama Empire State ni ghorofa refu na liko katikati ya jiji la New York kama ninakumbuka vizuri huenda ghorofa zile zilikuwa zaidi ya mia moja kwani tulielezwa kuwa lina floor 102, tulipanda juu ka lifti na tukapanda gorofa zilizofuata na tukapanda lift nyingine hatimaye tukafika juu kabisa na kuanza kuushangaa mji, watu walikuwa ni wengi sana na wote walikuwa na malengo kama ya kwetu kuuona mji wa New York, Mahali hapa pana ulinzi mkali sana askari walikuwa wengi mno, ni jengo ambalo kama magaidi wakilishambulia linaweza kupoteza watu wengi sana, Jengo hili huwezi kuingia bure tu ili kudhibiti watu, lazima ukate tiketi maalumu za kuruhusu kuingia na tulipanda juu sana na kukaguliwa kisha tulipanda juu zaidi mpaka mwisho, Jengo hili limejengwa mwaka 1930 na kufunguliwa mwaka uliofuata 1931, ni jengo la zamani kwa miaka hii kwa maana lina umri wa miaka 86 hivi lakini ni kama jengo jipya tu na ni imara na limetengenezwa kwa ufundi na utaalamu unaolifanya kuwa kama mnara hivi na ambao kila unavyokwenda juu unakuwa mwembamba zaidi au unaingia ndani na kulifanya likose sababu ya wapi kitakuwa chanzo cha kuanguka kwake.

Baada ya kumaliza shughuli za kuliangalia Jiji sasa tulielekea eneo maarufu kama Zero Ground eneo hilo zamani palikuwa na majengo mawili Marefu sana yaliyojulikana kama International Trade tower lakini yalibomolewa na Osama bin Laden kwa kutumia Ndege na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 3000, eneo hilo sasa lilisafishwa na kuangusha chini na kujengwa vivima vinavyotiririsha maji huku vikiwa na majina ya watu wengi sana wanaokisiwa kupoteza Maisha katika eneo hilo


Hilo ndio Jengo maarufu jijini New York lijulikanalo kama Empire State Building

Jiji la new York likiwa na pilikapila wakati tulipotembelea mwezi June 2014
 watu mbalimbali waliotembelea jiji la New York wakiwa juu Ghorofa 102 wakiliangalia jiji
 Mimi na mwenyeji wetu Jack Lee wa Kanisa la Open Door tukiwa juu kabisa katika jengo la Empire State Building tukiangalia jiji la New York na kisha kuamua kupiga picha ya Kumbukumbu, juu kumewekwa uzio maalumu ili kuzuia watu wasije wakajitupa na kujiua
 New York City kama inavyoonekana kutoka Empire States Building

 Juu kabisa katika jengo la Empire State
 Jiji la new York
 visima vikubwa viwili vimejengwa katika Eneo lijulikanalo kama Zero Ground Jijini New York

 Hapa ni Mchungaji Innocent Kamote nikiwa na wanafunzi wa Living Stone Boys' Seminary  waliochaguliwa kutembelea Marekani, tukiwa juu ya Ghorofa 102 ya Empire State jijini New York Marekani mwezi june 2014
 Hapa ni Mchungaji Innocent Kamote nikiwa na wanafunzi wa Living Stone Boys' Seminary  waliochaguliwa kutembelea Marekani, tukiwa juu ya Ghorofa 102 ya Empire State jijini New York Marekani mwezi june 2014 Hapa ni ndani ya Jengo hilo.
 Hapa ni Mchungaji Innocent Kamote nikiwa na wanafunzi wa Living Stone Boys' Seminary  waliochaguliwa kutembelea Marekani, tukiwa mbele ya visima vya Zero Ground jijini New York Marekani mwezi june 2014.

14. Majumuisho ya ziara yetu ya Marekani.
Ndugu zangu kwa ujumla ni vigumu kumalizia na kuelezea kila kitu ambacho kilifanyika katika ziara yetu, kwani tulitembelea makumbusho ya vita za Vietnam na vita vya Korea na Maryland na sinagogi la kiyahudi, na sehemu nyingine mbalimbali, kwa ujumla ilikuwa ziara ya kipekee sana na hakuna mtu amabaye amewahi kuwa na ziara ya aina hii kwa wageni waliowahi kutembelea Marekani na hata kwa wenyeji pia, kwani Jack Lee alituambia kuwa haijawahi kutokea hata kwa wao wanaoishi huko kutembelea maeneo tuliyowahi kutembelea
Maeneo mbalimbali katika picha
Rev. Innocent Samuel Kamote.
 Makumbusho ya vita ya Vietnam William alichoka kwa matembezi aliamua kukaa chini nyuma ni sanamu za askari walioshiriki vita ya Vietnam
 Mzee huyo wa Kikorea Katikati anamiliki hoteli hii alitukaribisha kwa chakula cha mchana na alituruhusu kula chochote tutakacho kulikuwa na kila kitu na koni za kushushia kisha tukapiga picha
 Maporomoko ya maji huko Maryland
 siku ya Kurudi Nyumbani uwanja wa ndege wa Dulles Jijini Washington Oliver na Mchungaji wa Kisukuma walikuja kutusindikiza, Bibi alikuwa Kazini










 Nje ya Sinagozi la kiyahudi Mjini Washington Marekani
 Eneo fulani hivi Katikati ya mji wa washington DC
 Nikijaribu kupata picha nzima ya mnara na mimi lakini ilishindikana
 Kutembelea Washington Monument mnara mkubwa na mrefu wa kumbukumbu katika mji wa Washington
 Kutembelea chuo cha jeshi la wana maji wa Marekani mjini Maryland Washington DC

Hoteli kubwa ya Kifahari jijini Washington









    
    



Hakuna maoni: