Alhamisi, 6 Oktoba 2016

Nabii Sefania



ZEPHANIAH: NABII WA HUKUMU YA ULIMWENGU

Ulimwengu wa leo ni kama Babiloni ya kale

A.      Mwandishi wa kitabu cha Zefania na Tarehe ya uandishi

§  Jina zefania maana yake ni “Yehova amemficha
§  Zefania huenda alizaliwa wakati wa Mfalme Manase na inawezekana ni wakati ambapo mfale huyo aliijaza Yerusalemu kwa Damu ya watu wasio na Hatia kwani aliwauwa watu wengi wa Mungu 2Falme 21;16
§  Inawezekana kuwa wazazi wake walimwamini Mungu juu ya ulinzi wa mtoto wao na hivyo kumpa jina Zefania yaani Mungu amemficha
§  Alikuwa ni moja ya vijukuu vya Hezekia kwa ule ukweli kwamba anatoka katika familia ya kifalme na ndugu wa mfalme Yosia hii iliweza kusaidia kufanya ujumbe wake kusikiwa vema siku zote Mungu pia huitumia historia ya mtu kwa utukufu wake ili kuwafikia ndugu na jamaa
§  Inaaminika kwamba Nyumbani kwao ni Yerusalem kwa sababu alifahamu hali halisi ya pale 1;4 Yeye ni maarufu sana kama Muhubiri wa utakatifu au Mwinjilisti anayewakwa
§  Tarehe ya uandishi wa kitabu chake huenda  ni kati ya Mwaka wa 630-625 K.K

B.      Historia ya Nyuma ya mambo 2Falme 21-23,2Nyakati 30-35.
§  Bwana alimtumia Isaya Mika na Hezekia kujaribu kuigeuza Yuda kwa Mungu na hivyo Israel walipokwenda utumwani Yuda ilihifadhiwa
§  Hezekia alifanya kila jitihada kuangamiza ibada za sanamu lakini Mwanae Manase alirejeza kila kitu ambacho baba yake alikiangamiza ,Alijenga tena madhabahu mahali pa juu na madhabahu za miungu ya kipagani miungu kama Kemoshi, miliconi, Baali na Ashera
§  Alimpa hata mtoto wake jina Ammoni kwa ajili ya miungu ya Misri, Mungu alimtia nidhamu kwa kumuachia achukuliwe utumwani na kufungwa huko  Ashuru 2Nyakati 33;1-12 na baadaye Mungu akamrudisha tena katika ufalme na alijaribu kufanya masahihisho kwa uovu alioufanya ingawaje ibada za sanamu alizozianzisha ziliendelea na kukua wakati wa utawala wa mwanae aliyemrithi ambaye alivitiamoyo kuendelea
§  Yosia mwana wa Ammoni  alikuwa mfale mwema  na Zefania alihudumu wakati wa utawala wake  na huenda alimsaidia kufanya mabadiliko huu ulikuwa ni wakati ambapo waashuru wanaanza kuanguka kama taifa kubwa na Babeli ilikuwa inaanza kupata nguvu kumbuka kuwa Mika alikuwa Nabii wa kwanza kitabiri kuhusu kuinuka kwa Babeli

C.      Upekee wa kitabu na ujumbe.
§  Zefania alianza kitabu chake kwa ujumbe wa kutosha kuhusu siku ya bwana na wakati wa hukumu ya mataifa yote Sehemu ya ujumbe wake  ilianza kutimia kuhusu Yuda kuaharibiwa lakini hukumu ilihairishwa mpaka wakati wa Yosia alipofariki kwa kuwa alikuwa mwema na alikuwa na watu waliomgeukia Mungu
§  Zaidi ya hayo unabii utatimizwa wakati wa Dhiki kuu na mwisho ni hukumu ya dunia kuhukumiwa kwa moto
§  Zefania kutabiri kwake kuhusu hukumu ya ulimwengu ilikuwa ni dalili wazi za kuonyesha Mungu ni Bwana wa mataifa yote na kuwa yeye ndiye atawalaye Dunia

D.      Mistari ya Msingi ni
-          1;7 1;14, 2;3.

E.       Siku ya hukumu na Maangamizi 1;1-3;8
1.       Hukumu ya ulimwengu woote 1;1-3,14-18
-          Kiini cha kitabu ni 1;2-3, Na neno siku ya bwana ni wakati wa hukumu
-          Ulimwengu mzima na kila kiumbe kimeathiriwa na dhambi 1;3
-          Kwa ajili ya Yuda Mungu atalitumia  jeshi la Babeli 1;14-18 na siku ya Bwana kwao ilikuwa karibu 1;14 Lakini Paulo anaizungumzia wakati ujao 1Thesalonie 5;2-3
-          Kumbuka matukio ya siku ya Bwana kama yanavyo changauliwa katika kuwa itakuwa ni siku ya;-
a.       Uchungu na kilio 1;14
b.       Kulia kwa mashujaa 1;14
c.        Hasira 1;15
d.       Mgandamizo na kutisha 1;15
e.       Taabu na ukiwa 1;15
f.         Giza na utusitusi 1;15
g.       Mawingu na weusi 1;15
h.       Tarumbeta na kilio cha vita 1;16
i.         Damu kumwagika 1;17
j.         Moto na wivu wake 1;18
k.        Mwanadamu na mnyama kufutiliwa mbali 1;2-3
l.         Dunia nzima kuyeyuka 1;18
m.      Mwisho wa kustukiza kwa ulimwengu 1;18
Kumbuka dalili tatu za mwisho katika k,l,m zitatimia katika mwisho ule uliozungumzwa na Paulo

F.       Hukumu dhidi ya Yuda 1;4-2;3
-          Mashitaka makuu ya Yuda katika kitabu cha Zefania ni kuhusu kuabudu miungu ya uongo
-          Mwanadamu ameumbwa na Mungu kwa kusudi la kuabudu lakini shetani hujaribu kumuharibu mwanadamu kutoka katika kusudi hilo na kuwageuza kuabudu vitu vingine
-          Watu walidai kuwa wanamwabudu Mungu lakini pia waliabudu miungu
-          2falme 23 watu wa Yuda waliabudu kila kitu kinachohusiana na dini za uongo ambayo iliangamizwa na Yosia na wala hawakuogopa 1;18 Mungu aliingiwa na Wivu na hasira yake ikawaka
-          2;1-3 Nabii aliwakumbusha kuwa kama kuna tumaini lolote basi linapatikana katika unyenyekevu na haki na ndipo watu waweza kufaidika katika  katika siku ya hasira ya Bwana.

G.      Hukumu dhidi ya mataifa 2;14-15

-          Hukumu ya Mungu ilikuwa inakuja si kwa Yuda tu bali na kwa mataifa mengine Nebukadreza angeivamia Yuda na mataifa mengine na kustawisha utawala wake Amosi na Zefania walitabiri na ilikuwa inakaribia kutumia

      
        Hukumu ya Mungu kwa mataifa zefania 2;4-15na Amosi 1;6-2;3


Taifa
Hatia
Adhabu
Zefania
Amosi
Ufilisti
Kuchukua mateka na kuuza
Kuharibiwa na ardhi yao kupewa mabaki ya yuda
2;4-7
1;6-8

Moabu

   Na
 Amoni
Ukatili kwa watu wa Mungu,kiburi na kuwacheka
Kuuawa katika vita,kuchukuliwa mateka,kama sodoma na Gomora na ardhi itakuwa kwa mabaki wa Mungu
2;8-11
1;13-2;3
Kushi
Haikuelezwa
Kuuawa kwa upanga
2;12

Ashuru
Kiburi na majivuno
Ninawi uabaki ukiwa na kuchukiwa na watu wote
2;13-15


H.      Hukumu dhidi ya Yerusalemu 3;1-7
-          Katika eneo hili Nabii anawageukia watu wa Yuda na Viongozi huko Yerusalem
-          Wao walikuwa wanawajibika kwa hali ya Taifa na walihukumiwa kutokana na maswala makuu matatu Kugandamiza watu, Uasi na unajisi 3;1 soma 3;1-7
-          Hukumu hizi zingewahusu Viongozi wengi walio madarakani leo
I.         Siku ya wokovu na Furaha 3;8-20
-          Baada ya ujumbe mzito  wa hukumu Zefania anamalizia ujumbe wake  kwa ushindi wa kurejezwa upya wakati wa millennium
-          Ni kweli kuwa hasira zake zitamwagwa lakini 3;8 mabaki kutoka mataifa mbalimbali wataokolewa na kutakaswa 3;9-10
-          Bwana ambaye aliwahukumu atawarudisha nyuma adui zao katika Msalaba na atakuwa pamoja nao 3;15 Bwana ataifanya Israel sifa na furaha.

Mika Nabii


MIKA: NABII WA MASIHI 
A.   Mwandishi
-          Mwandishi wa kitabu cha Mika ni Mika mwenyewe
-          Jina lake maana yake ni “Nani aliye kama Mungu” yeye alitokea Moresheth-Gath mji mdogo kusini magharibi mwa Yerusalem kilomita zipatazo 40 kwa hiyo Tekoa alikoishi Amosi ni Kilomita 27 hivi kutoka kijiji cha Mika
-          Kuna uwezekano ya kuwa Mika ameitembelea Yerusalem mara nyingi na huko aliona jinsi dhambi ilivyosababisha vilio kwa masikini
-          Katika mahubiri yake alikemea dhuluma ya Yerusalem kwa jamii alikemea sana kama Amosi alivyokemea  huko kaskazini
-          Alijulikana kama bingwa wa kuwatetea masikini au Nabii wa uongozi wa haki yaani Nabii wa Masihi alihubiri kabla na baada ya anguko la Samaria huduma yake inakisiwa kuchukua muda wa miaka kati ya  735-700 K.K. kabla kidogo ya Israel kuchukuliwa utumwani na wakati huu Isaya na Hosea walikuwa Manabii sambamba naye Mika alishughulika sana na watu, Isaya alishughulika na Wafalme.

B.      Historia ya hali halisi ya Yuda.

-          Yuda ilikuwa na wakati wa amani na starehe wakati wa utawala wa Yothamu na hivyo watu walijenga ngome na majumba ya kifahari “Kasri” lakini uovu ulikuwa uimepamba moto
-          Wakati wa utawala wa Ahazia Yuda walilazimishwa kulipa kodi kwa Waashuru na kwakweli ulikuwa mzigo mzito sana kwao na hivyo matajiri walichukua mali za masikini
-          Na mpaka wakati wa Hezekia mfalme Yerusalemu ilikuwa ni kitanda cha moto kisicholalika kwa ajili ya uovu, rushwa utapeli na ufisadi- dhuluma

C.      Upekee wa ujumbe na Kitabu cha Mika.

-          Mika alikuwa Nabii wa kwanza kitabiri kuhusu anguko la Yerusalemu na kuchukuliwa utumwani BABELI watu watakuwa walishangazwa kwani Babeli wakati huo ilikuwa bado hata haijajulikana wala kuwadola yenye nguvu Mika 4; 10.
-          Manabii wengi walitabiri pia kuja kwa Masihi akiwemo Isaya lakini Mika alitabiri mpaka mahali atakapozaliwa kuwa ni Bethelehemu Mika 5;5 Mathayo 2;6
-          Mwanzoni Mika alikazia kuhusu utakatifu wa Mungu dhidi ya hali ya uovu wa watu wake, kwani utakatifu wa Mungu unataka utakatifu kwa watu wake, Mika alisisitiza juu ya kumcha Mungu na mahusiano yaliyo mazuri Mika anahitimisha kitabu chake kwa kuonyesha tabia ya Mungu katika Mika 6;8 na kitabu chote kwa ujumla tunaona juu ya tumaini la ujio wa Masihi
-          Na ingawaje atazaliwa Bethelehemu alikuwako tangu milele Mika 5;2 Mika anamwelezea Masihi na kuwa atatawala watu wake Israel kama Mchungaji na kuwalisha  na hii itatimia atakapokuja mara ya pili duniani.

D.      Mstari wa Msingi.

-          Mika 5;2 “Lakini wewe Eeh Bethelehemu Efrata uliye mdogo miongoni mwa Yuda….”
-          Mika 6;8 “Amekuonyesha yaliyo mema…”

E.       Mgawanyo wa kitabu cha Mika

-          Hukumu na haki Sura 1-3
-          Mtawala na mabaki Sura ya 4-5
-          Matakwa na kurejezwa upya Sura 6-7

F.       Uchanganuzi wa kitabu cha Mika.

a.       Hukumu na haki Sura ya 1-3.
-          Soma kwa kulinganisha Mika 1;1, Amosi 1;1 na Obadia 1;1. Manabii hawa woote walipokea ujumbe wao kupitia maono waliyopewa na Mungu
-          Mika hakuwa na mafundisho yoyote kuhusu nini cha kusema, maono ya maangamizi yalimjia na akajazwa Roho Mtakatifu na kupewa Maneno ya kusema Mika 1;1,3;8.
-          Alisisitiza  Umuhimu wa ujumbe wake kwa kuuelekeza kwa watu wote 1;2 alimuona Bwana anashuka kwa hukumu akitembelea mahali pa juu  na milima ikiyeyuka chini ya miguu yake na bonde likagawanyika
-          Kumbuka kuwa Biblia inazungumza kwa mafumbo na wakati mwingine waziwazi mahali pa juu huweza kumaanisha Kiburi au milimani ambako ibada za sanamu zilikuwa zikifanyika 1; 6, 3; 12.
-          Unaposoma Mika 1;3-4 na kulinganisha na 2Petro 3;10-15 na Ufunuo 21;1-5 utagundua kuwa hizi ni nabii mbili kwa Mfululizo yaani
i.                     Kuanguka kwa Samaria na Yerusalemu na
ii.                    Kufanywa upya kwa ulimwengu kwa moto
-          Woote Mika na Petro walisisitiza utakatifu katika mtazamo wa kuja kwa Bwana, na kuyeyuka kwa milima kwa uhalisi kunaweza kuwa wakati wa ujio wa pili.
-          Mika alifanya huduma miaka 13 kabla ya Ashuru kuivamia Samaria na aliishi akaona sehemu ya unabii wake ikitimia. Mika alionyeshwa namna samaria itakavyo haribiwa na Ashuru 1;6-7 
                             
Bethelehemu mahali ambapo wachungaji waliwasikia malaika akiwapa ujumbe wa Kuzaliwa kwa masihi na kisha kundi la malaika wakaimba Ndivyo panavyoonekana leo ni katika mji huu Yesu Masihi alizaliwa Kama alivyotabiri Mika 5;2 miaka 730 K.K, Picha na maelezo kwa Hisani ya maktaba ya Rev.Innocent Kamote, Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

-          Mika alimtumia baadhi ya Maneno kwa baadhi ya miji ambayo ingetekwa na kufanyiwa uharibifu alimtumia mtindo wa Maneno kama au kinyume cha jina halisi la mji kuonyesha kile ambacho kingewapata Mika 1;10-14.
-          Beth- le –afra   nyumba ya vumbi
-          Beth eseli - kuondolea tegemeo
-          Moroth -kuondoa Tegemeo
-          Lakishi - mikanda inayofungwa kwa farasi
-          Moresheth – gath zawadi ya kuagia
-          Akzibu- kijito kidanganyacho wafalme
-          Maresha -  kumilikiwa
-          Zaanani -hutotembea
G.      Hukumu kwa Viongozi pamoja na watu 2-3.
-          Mungu aliamini kuwa Viongozi watasimamia ugawanyaji wa ardhi  kwa familia na kuwa urithi wao wa kudumu lakini kwa sababu ya umasikini familia nyingi zililazimika kuuza mali zao ardhi na ilitakiwa mwaka wa jubilee ambao uliazimishwa kila baada ya miaka 50 ardhi zirudishwe lakini watu wenye tamaa walipanga namna ya kuzidi kuwa matajiri kwa kuendelea kumiliki mali za wengine 2;1-2.Mungu anaitikia mipango yao kwa mpango wake 3-4,Pia tunaona sheria ya kuvuna na kupenda ikifanya kazi soma 2;1;3; 2;2,4;2;2,4-5, 2;8,10, 2;9-10.
-          Hata hivyo bado Mungu alikuwa na mpango na watu wake yaani wokovu kwa wale watakaomfuata 2;12-13 Mungu angewasaidia mabaki ya watu wake huko utumwani na angewarudisha katika nchi yao na ya kuwa Masihi atahusika katika kuwaweka huru watu kutoka katika utumwa wa dhambi Mika 2;13
-          Manabii wa uongo walijaribu kumpinga Mika  na ujumbe wake  wakimuonya kuwa asihubiri mambo hayo 2;6, Linganisha na Amosi 7;10-17 Jaribu kubwa walilokuwa nao Manabii hao katika siku zao ilikuwa ni kuhubiri kile watu wanachokitaka watu ili walipwe na kulishwa 3,5,11 kama watajisahau katika hali hii wataanguka katika giza kubwa la kiroho  alisema Mika 3;6-7
-          Katika sura ya tatu hukumu ya Viongozi  inaonyesha pia tunatakiwa kuwa Viongozi wa aina gani  Viongozi katika Israel walipenda uovu, walijitumikia wenyewe ubinafsi,  na hawakuwa na huruma juu ya watu wengine  3;3. Lakini Mika alikuwa amejazwa nguvu na Roho Mtakatifu 3;8 Matendo 1;8
H.      Unabii kuhusu Utukufu sura ya 4-7
Utawala wa Masihi 4-5
-          Tunamshukuru Mungu kwa kuwepo kwa ufalme wake katika maisha ya mioyo ya watu wake lakini tunatazamia ya kuwa siku moja Kristo atatawala katika ulimwengu huu pale Yerusalemu
-          Mataifa hayatapigana tena na wala hawatajifunza vita tena  4;3
-          Mika 4-5 pia inatuambia baadhi ya matukio yatakayokuwako ambayo yatatukia kabla ya utawala wenye utukufu wa masihi.
-          Katika 4;9-10 Mika anatabiri kuchukuliwa mateka  utumwani Babeli na kurejezwa tena
-          Mika 5;1 si ajabu ni  unabii unaojirudia  kwa ufalme wa Yuda na kwa ajili ya Masihi kwa kupigwa Mathayo 26;67,27;30 wakati mstari wa 2 unaonyesha masihi atazaliwa wapi na ya kuwa ni mtawala wa kimungu na mwenye kudumu milele.
I.         Furaha baada ya mateso Mika 6-7.
-          Sura mbili za mwisho zinaonyesha Israel wakiwa katika kipimo cha Mungu, Mungu aliwaita na kuwahoji kwanini wamemuacha wakati amewaonyesha upendo na wema kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.
-          Israel walifikiri kuwa wanaweza kumpendeza Mungu kwa sadaka zao  6;6-7
-          Mika 6;8 inaeleza kile ambacho Mungu anakitaka kwa mwanadamu yaani Haki, Upendo, Rehema na kutembea kwa Unyenyekevu na Mungu  kwa maana nyingine kulitii neno lake Yakobo 1;22
-          Mungu aliwashitaki Israel kwa ajili ya dhambi ya uongo, uasi, ibada za sanamu, rushwa, uhaini, 6;10-12;16 17;2-6 na hukumu yake ni anguko 6;16
-          Mika 7;18-20 inatoa suluhisho kwa Israel na ni Pendo la Mungu katika kuwasamehe dhambi zao