MIKA: NABII WA MASIHI
A. Mwandishi
-
Mwandishi wa kitabu cha Mika ni Mika mwenyewe
-
Jina lake maana yake ni “Nani aliye kama Mungu” yeye alitokea Moresheth-Gath mji mdogo
kusini magharibi mwa Yerusalem kilomita zipatazo 40 kwa hiyo Tekoa alikoishi
Amosi ni Kilomita 27 hivi kutoka kijiji cha Mika
-
Kuna uwezekano ya kuwa Mika ameitembelea
Yerusalem mara nyingi na huko aliona jinsi dhambi ilivyosababisha vilio kwa
masikini
-
Katika mahubiri yake alikemea dhuluma ya
Yerusalem kwa jamii alikemea sana kama Amosi alivyokemea huko kaskazini
-
Alijulikana kama bingwa wa kuwatetea masikini
au Nabii wa uongozi wa haki yaani Nabii wa Masihi alihubiri kabla na baada ya
anguko la Samaria huduma yake inakisiwa kuchukua muda wa miaka kati ya 735-700 K.K. kabla kidogo ya Israel
kuchukuliwa utumwani na wakati huu Isaya na Hosea walikuwa Manabii sambamba
naye Mika alishughulika sana na watu, Isaya alishughulika na Wafalme.
B.
Historia
ya hali halisi ya Yuda.
-
Yuda ilikuwa na wakati wa amani na starehe
wakati wa utawala wa Yothamu na hivyo watu walijenga ngome na majumba ya
kifahari “Kasri” lakini uovu ulikuwa uimepamba moto
-
Wakati wa utawala wa Ahazia Yuda
walilazimishwa kulipa kodi kwa Waashuru na kwakweli ulikuwa mzigo mzito sana
kwao na hivyo matajiri walichukua mali za masikini
-
Na mpaka wakati wa Hezekia mfalme Yerusalemu
ilikuwa ni kitanda cha moto kisicholalika kwa ajili ya uovu, rushwa utapeli na
ufisadi- dhuluma
C.
Upekee
wa ujumbe na Kitabu cha Mika.
-
Mika alikuwa Nabii wa kwanza kitabiri kuhusu anguko
la Yerusalemu na kuchukuliwa utumwani BABELI watu watakuwa walishangazwa kwani
Babeli wakati huo ilikuwa bado hata haijajulikana wala kuwadola yenye nguvu Mika
4; 10.
-
Manabii wengi walitabiri pia kuja kwa Masihi
akiwemo Isaya lakini Mika alitabiri mpaka mahali atakapozaliwa kuwa ni
Bethelehemu Mika 5;5 Mathayo 2;6
-
Mwanzoni Mika alikazia kuhusu utakatifu wa Mungu
dhidi ya hali ya uovu wa watu wake, kwani utakatifu wa Mungu unataka utakatifu
kwa watu wake, Mika alisisitiza juu ya kumcha Mungu na mahusiano yaliyo mazuri
Mika anahitimisha kitabu chake kwa kuonyesha tabia ya Mungu katika Mika 6;8 na
kitabu chote kwa ujumla tunaona juu ya tumaini la ujio wa Masihi
-
Na ingawaje atazaliwa Bethelehemu alikuwako
tangu milele Mika 5;2 Mika anamwelezea Masihi na kuwa atatawala watu wake
Israel kama Mchungaji na kuwalisha na
hii itatimia atakapokuja mara ya pili duniani.
D.
Mstari
wa Msingi.
-
Mika 5;2 “Lakini wewe Eeh Bethelehemu Efrata
uliye mdogo miongoni mwa Yuda….”
-
Mika 6;8 “Amekuonyesha yaliyo mema…”
E. Mgawanyo wa kitabu cha Mika
-
Hukumu na haki Sura 1-3
-
Mtawala na mabaki Sura ya 4-5
-
Matakwa na kurejezwa upya Sura 6-7
F. Uchanganuzi wa kitabu cha Mika.
a.
Hukumu
na haki Sura ya 1-3.
-
Soma kwa kulinganisha Mika 1;1, Amosi 1;1 na Obadia
1;1. Manabii hawa woote walipokea ujumbe wao kupitia maono waliyopewa na Mungu
-
Mika hakuwa na mafundisho yoyote kuhusu nini cha
kusema, maono ya maangamizi yalimjia na akajazwa Roho Mtakatifu na kupewa
Maneno ya kusema Mika 1;1,3;8.
-
Alisisitiza
Umuhimu wa ujumbe wake kwa kuuelekeza kwa watu wote 1;2 alimuona Bwana
anashuka kwa hukumu akitembelea mahali pa juu
na milima ikiyeyuka chini ya miguu yake na bonde likagawanyika
-
Kumbuka kuwa Biblia inazungumza kwa mafumbo na
wakati mwingine waziwazi mahali pa juu huweza kumaanisha Kiburi au milimani
ambako ibada za sanamu zilikuwa zikifanyika 1; 6, 3; 12.
-
Unaposoma Mika 1;3-4 na kulinganisha na 2Petro
3;10-15 na Ufunuo 21;1-5 utagundua kuwa hizi ni nabii mbili kwa Mfululizo yaani
i.
Kuanguka kwa Samaria na Yerusalemu na
ii.
Kufanywa upya kwa ulimwengu kwa moto
-
Woote Mika na Petro walisisitiza utakatifu katika
mtazamo wa kuja kwa Bwana, na kuyeyuka kwa milima kwa uhalisi kunaweza kuwa
wakati wa ujio wa pili.
-
Mika alifanya huduma miaka 13 kabla ya Ashuru
kuivamia Samaria na aliishi akaona sehemu ya unabii wake ikitimia. Mika
alionyeshwa namna samaria itakavyo haribiwa na Ashuru 1;6-7
-
Mika alimtumia baadhi ya Maneno kwa baadhi ya miji ambayo
ingetekwa na kufanyiwa uharibifu alimtumia mtindo wa Maneno kama au kinyume cha
jina halisi la mji kuonyesha kile ambacho kingewapata Mika 1;10-14.
-
Beth- le –afra
nyumba ya vumbi
-
Beth eseli - kuondolea tegemeo
-
Moroth -kuondoa Tegemeo
-
Lakishi - mikanda inayofungwa kwa farasi
-
Moresheth – gath zawadi ya kuagia
-
Akzibu- kijito kidanganyacho wafalme
-
Maresha -
kumilikiwa
-
Zaanani -hutotembea
G.
Hukumu
kwa Viongozi pamoja na watu 2-3.
-
Mungu aliamini kuwa Viongozi watasimamia ugawanyaji
wa ardhi kwa familia na kuwa urithi wao
wa kudumu lakini kwa sababu ya umasikini familia nyingi zililazimika kuuza mali
zao ardhi na ilitakiwa mwaka wa jubilee ambao uliazimishwa kila baada ya miaka
50 ardhi zirudishwe lakini watu wenye tamaa walipanga namna ya kuzidi kuwa matajiri
kwa kuendelea kumiliki mali za wengine 2;1-2.Mungu anaitikia mipango yao kwa
mpango wake 3-4,Pia tunaona sheria ya kuvuna na kupenda ikifanya kazi soma
2;1;3; 2;2,4;2;2,4-5, 2;8,10, 2;9-10.
-
Hata hivyo bado Mungu alikuwa na mpango na watu
wake yaani wokovu kwa wale watakaomfuata 2;12-13 Mungu angewasaidia mabaki ya
watu wake huko utumwani na angewarudisha katika nchi yao na ya kuwa Masihi
atahusika katika kuwaweka huru watu kutoka katika utumwa wa dhambi Mika 2;13
-
Manabii wa uongo walijaribu kumpinga Mika na ujumbe wake wakimuonya kuwa asihubiri mambo hayo 2;6, Linganisha
na Amosi 7;10-17 Jaribu kubwa walilokuwa nao Manabii hao katika siku zao
ilikuwa ni kuhubiri kile watu wanachokitaka watu ili walipwe na kulishwa 3,5,11
kama watajisahau katika hali hii wataanguka katika giza kubwa la kiroho alisema Mika 3;6-7
-
Katika sura ya tatu hukumu ya Viongozi inaonyesha pia tunatakiwa kuwa Viongozi wa
aina gani Viongozi katika Israel
walipenda uovu, walijitumikia wenyewe ubinafsi,
na hawakuwa na huruma juu ya watu wengine 3;3. Lakini Mika alikuwa amejazwa nguvu na
Roho Mtakatifu 3;8 Matendo 1;8
H. Unabii kuhusu Utukufu sura ya 4-7
Utawala wa Masihi 4-5
-
Tunamshukuru Mungu kwa kuwepo kwa ufalme wake
katika maisha ya mioyo ya watu wake lakini tunatazamia ya kuwa siku moja Kristo
atatawala katika ulimwengu huu pale Yerusalemu
-
Mataifa hayatapigana tena na wala hawatajifunza
vita tena 4;3
-
Mika 4-5 pia inatuambia baadhi ya matukio
yatakayokuwako ambayo yatatukia kabla ya utawala wenye utukufu wa masihi.
-
Katika 4;9-10 Mika anatabiri kuchukuliwa
mateka utumwani Babeli na kurejezwa tena
-
Mika 5;1 si ajabu ni unabii unaojirudia kwa ufalme wa Yuda na kwa ajili ya Masihi kwa
kupigwa Mathayo 26;67,27;30 wakati mstari wa 2 unaonyesha masihi atazaliwa wapi
na ya kuwa ni mtawala wa kimungu na mwenye kudumu milele.
I.
Furaha
baada ya mateso Mika 6-7.
-
Sura mbili za mwisho zinaonyesha Israel wakiwa
katika kipimo cha Mungu, Mungu aliwaita na kuwahoji kwanini wamemuacha wakati
amewaonyesha upendo na wema kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.
-
Israel walifikiri kuwa wanaweza kumpendeza Mungu
kwa sadaka zao 6;6-7
-
Mika 6;8 inaeleza kile ambacho Mungu anakitaka kwa
mwanadamu yaani Haki, Upendo, Rehema na kutembea kwa Unyenyekevu na Mungu kwa maana nyingine kulitii neno lake Yakobo
1;22
-
Mungu aliwashitaki Israel kwa ajili ya dhambi ya
uongo, uasi, ibada za sanamu, rushwa, uhaini, 6;10-12;16 17;2-6 na hukumu yake
ni anguko 6;16
-
Mika 7;18-20 inatoa suluhisho kwa Israel na ni
Pendo la Mungu katika kuwasamehe dhambi zao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni