Alhamisi, 6 Oktoba 2016

Nabii Sefania



ZEPHANIAH: NABII WA HUKUMU YA ULIMWENGU

Ulimwengu wa leo ni kama Babiloni ya kale

A.      Mwandishi wa kitabu cha Zefania na Tarehe ya uandishi

§  Jina zefania maana yake ni “Yehova amemficha
§  Zefania huenda alizaliwa wakati wa Mfalme Manase na inawezekana ni wakati ambapo mfale huyo aliijaza Yerusalemu kwa Damu ya watu wasio na Hatia kwani aliwauwa watu wengi wa Mungu 2Falme 21;16
§  Inawezekana kuwa wazazi wake walimwamini Mungu juu ya ulinzi wa mtoto wao na hivyo kumpa jina Zefania yaani Mungu amemficha
§  Alikuwa ni moja ya vijukuu vya Hezekia kwa ule ukweli kwamba anatoka katika familia ya kifalme na ndugu wa mfalme Yosia hii iliweza kusaidia kufanya ujumbe wake kusikiwa vema siku zote Mungu pia huitumia historia ya mtu kwa utukufu wake ili kuwafikia ndugu na jamaa
§  Inaaminika kwamba Nyumbani kwao ni Yerusalem kwa sababu alifahamu hali halisi ya pale 1;4 Yeye ni maarufu sana kama Muhubiri wa utakatifu au Mwinjilisti anayewakwa
§  Tarehe ya uandishi wa kitabu chake huenda  ni kati ya Mwaka wa 630-625 K.K

B.      Historia ya Nyuma ya mambo 2Falme 21-23,2Nyakati 30-35.
§  Bwana alimtumia Isaya Mika na Hezekia kujaribu kuigeuza Yuda kwa Mungu na hivyo Israel walipokwenda utumwani Yuda ilihifadhiwa
§  Hezekia alifanya kila jitihada kuangamiza ibada za sanamu lakini Mwanae Manase alirejeza kila kitu ambacho baba yake alikiangamiza ,Alijenga tena madhabahu mahali pa juu na madhabahu za miungu ya kipagani miungu kama Kemoshi, miliconi, Baali na Ashera
§  Alimpa hata mtoto wake jina Ammoni kwa ajili ya miungu ya Misri, Mungu alimtia nidhamu kwa kumuachia achukuliwe utumwani na kufungwa huko  Ashuru 2Nyakati 33;1-12 na baadaye Mungu akamrudisha tena katika ufalme na alijaribu kufanya masahihisho kwa uovu alioufanya ingawaje ibada za sanamu alizozianzisha ziliendelea na kukua wakati wa utawala wa mwanae aliyemrithi ambaye alivitiamoyo kuendelea
§  Yosia mwana wa Ammoni  alikuwa mfale mwema  na Zefania alihudumu wakati wa utawala wake  na huenda alimsaidia kufanya mabadiliko huu ulikuwa ni wakati ambapo waashuru wanaanza kuanguka kama taifa kubwa na Babeli ilikuwa inaanza kupata nguvu kumbuka kuwa Mika alikuwa Nabii wa kwanza kitabiri kuhusu kuinuka kwa Babeli

C.      Upekee wa kitabu na ujumbe.
§  Zefania alianza kitabu chake kwa ujumbe wa kutosha kuhusu siku ya bwana na wakati wa hukumu ya mataifa yote Sehemu ya ujumbe wake  ilianza kutimia kuhusu Yuda kuaharibiwa lakini hukumu ilihairishwa mpaka wakati wa Yosia alipofariki kwa kuwa alikuwa mwema na alikuwa na watu waliomgeukia Mungu
§  Zaidi ya hayo unabii utatimizwa wakati wa Dhiki kuu na mwisho ni hukumu ya dunia kuhukumiwa kwa moto
§  Zefania kutabiri kwake kuhusu hukumu ya ulimwengu ilikuwa ni dalili wazi za kuonyesha Mungu ni Bwana wa mataifa yote na kuwa yeye ndiye atawalaye Dunia

D.      Mistari ya Msingi ni
-          1;7 1;14, 2;3.

E.       Siku ya hukumu na Maangamizi 1;1-3;8
1.       Hukumu ya ulimwengu woote 1;1-3,14-18
-          Kiini cha kitabu ni 1;2-3, Na neno siku ya bwana ni wakati wa hukumu
-          Ulimwengu mzima na kila kiumbe kimeathiriwa na dhambi 1;3
-          Kwa ajili ya Yuda Mungu atalitumia  jeshi la Babeli 1;14-18 na siku ya Bwana kwao ilikuwa karibu 1;14 Lakini Paulo anaizungumzia wakati ujao 1Thesalonie 5;2-3
-          Kumbuka matukio ya siku ya Bwana kama yanavyo changauliwa katika kuwa itakuwa ni siku ya;-
a.       Uchungu na kilio 1;14
b.       Kulia kwa mashujaa 1;14
c.        Hasira 1;15
d.       Mgandamizo na kutisha 1;15
e.       Taabu na ukiwa 1;15
f.         Giza na utusitusi 1;15
g.       Mawingu na weusi 1;15
h.       Tarumbeta na kilio cha vita 1;16
i.         Damu kumwagika 1;17
j.         Moto na wivu wake 1;18
k.        Mwanadamu na mnyama kufutiliwa mbali 1;2-3
l.         Dunia nzima kuyeyuka 1;18
m.      Mwisho wa kustukiza kwa ulimwengu 1;18
Kumbuka dalili tatu za mwisho katika k,l,m zitatimia katika mwisho ule uliozungumzwa na Paulo

F.       Hukumu dhidi ya Yuda 1;4-2;3
-          Mashitaka makuu ya Yuda katika kitabu cha Zefania ni kuhusu kuabudu miungu ya uongo
-          Mwanadamu ameumbwa na Mungu kwa kusudi la kuabudu lakini shetani hujaribu kumuharibu mwanadamu kutoka katika kusudi hilo na kuwageuza kuabudu vitu vingine
-          Watu walidai kuwa wanamwabudu Mungu lakini pia waliabudu miungu
-          2falme 23 watu wa Yuda waliabudu kila kitu kinachohusiana na dini za uongo ambayo iliangamizwa na Yosia na wala hawakuogopa 1;18 Mungu aliingiwa na Wivu na hasira yake ikawaka
-          2;1-3 Nabii aliwakumbusha kuwa kama kuna tumaini lolote basi linapatikana katika unyenyekevu na haki na ndipo watu waweza kufaidika katika  katika siku ya hasira ya Bwana.

G.      Hukumu dhidi ya mataifa 2;14-15

-          Hukumu ya Mungu ilikuwa inakuja si kwa Yuda tu bali na kwa mataifa mengine Nebukadreza angeivamia Yuda na mataifa mengine na kustawisha utawala wake Amosi na Zefania walitabiri na ilikuwa inakaribia kutumia

      
        Hukumu ya Mungu kwa mataifa zefania 2;4-15na Amosi 1;6-2;3


Taifa
Hatia
Adhabu
Zefania
Amosi
Ufilisti
Kuchukua mateka na kuuza
Kuharibiwa na ardhi yao kupewa mabaki ya yuda
2;4-7
1;6-8

Moabu

   Na
 Amoni
Ukatili kwa watu wa Mungu,kiburi na kuwacheka
Kuuawa katika vita,kuchukuliwa mateka,kama sodoma na Gomora na ardhi itakuwa kwa mabaki wa Mungu
2;8-11
1;13-2;3
Kushi
Haikuelezwa
Kuuawa kwa upanga
2;12

Ashuru
Kiburi na majivuno
Ninawi uabaki ukiwa na kuchukiwa na watu wote
2;13-15


H.      Hukumu dhidi ya Yerusalemu 3;1-7
-          Katika eneo hili Nabii anawageukia watu wa Yuda na Viongozi huko Yerusalem
-          Wao walikuwa wanawajibika kwa hali ya Taifa na walihukumiwa kutokana na maswala makuu matatu Kugandamiza watu, Uasi na unajisi 3;1 soma 3;1-7
-          Hukumu hizi zingewahusu Viongozi wengi walio madarakani leo
I.         Siku ya wokovu na Furaha 3;8-20
-          Baada ya ujumbe mzito  wa hukumu Zefania anamalizia ujumbe wake  kwa ushindi wa kurejezwa upya wakati wa millennium
-          Ni kweli kuwa hasira zake zitamwagwa lakini 3;8 mabaki kutoka mataifa mbalimbali wataokolewa na kutakaswa 3;9-10
-          Bwana ambaye aliwahukumu atawarudisha nyuma adui zao katika Msalaba na atakuwa pamoja nao 3;15 Bwana ataifanya Israel sifa na furaha.

Hakuna maoni: