Naitwa Gimpel mjinga au fala, Ingawa sifikiri kabisa
mwenyewe kuwa ni fala au mjinga, kama watu wanavyonifikiri, Lakini ndivyo
wazushi wanavyoniita, walinipa majina tangu nikiwa shuleni, nilipewa majina
kama saba hivi waliniita Jinga, Punda, Bichwa maji, Levi, Mshamba, Wakuja, na
Fala, na jina la mwisho ndio likawa maarufu zaidi, nilikuwa najiuliza kwa nini
naitwa fala? Eti kwa sababu nadanganyika kirahisi, siku moja waliniambia Gimpel
unajua kuwa mke wa Rabbbi amejifungua? Niliondoka shuleni mara moja ili kwenda
kumuangalia, lakini kumbe ulikuwa ni uongo! Nilijiuliza nilipaswa kuangalia
nini je tumbo lake kwamba halikuwa kubwa? au nilipaswa kuangalia nini
ningejuaje kama ana mimba? Je ulikuwa ni ujinga nilioufanya? Aaah sijui lakini
kundi lote la watu walinicheka, waligonga mikono yao na kurukaruka na kunizomea
mpaka saa ya maombi ya usiku, haikunidhoofisha kwa sababu sikuwa mjinga lakini
nafikiri walikuwa wamenipatia siku hiyo, mimi namcha sana Mungu, nikasema
litapiata tu.
Nilipokuwa nikitoka shuleni
kurejea nyumbani nilisikia mbwa wakibweka, kwa vile nilikuwa siogopi mbwa
sikujali, lakini nilifikiri moyoni je kama mbwa hao ni kichaa na wataning’ata
itakuwaje najua madhara ya kung’atwa na mbwa mwenye kichaa, hivyo niliamua
kutimua mbio kama niliyenunua gari, lakini jambo la ajabu nilishangaa watu
waliokuwa sokoni na madukani waliangua kicheko kikubwa sana, kumbe mtu mmoja
aliiigiza mlio kama wa mbwa je ningewezaje kujua kuwa ni mtu? Lakini
nilionekana kuwa mjinga pia.
Watu wengi walipogundua kuwa mimi
ni mtu ambaye ninaweza kudanganyika kirahisi basi kila mmoja alijaribu
anachoweza kukifanya ili mradi kunidanganya, wengine waliniambia Kaisari
anakuja kwenu, wengine mwezi umeanguka huko Turbeen, tumegundua sanduku la
thamani nyuma ya bafuni kwenu, na mengineyo mengi ili mradi tu walijua kuwa
naweza kumuamini kila mmoja, na ndivyo ilivyo nilimuamini kila mtu na niliamini
hakuna lisilowezekana kama ilivyoandikwa katika hekima za mababa, si hivyo tu
niliamini katika wingi wa watu mfano kama kijiji kizima wangeniambia jambo
ningeamini mpaka pale waliponiambia kuwa tunakutania, niliwaamini na nilijua ni
jambo jema kuwaamini watu kuliko kuwa na mashaka nao.
Mimi nilikuwa yatima na bibi
yangu aliyenilea alikuwa amezeeka sana na mwenye kukaribia kufa, hivyo nilipewa
kazi ya kusaidia kuuza mikate kwa mtu mmoja aliyekuwa na baker ya mikate, nilipokuwa
zamu pale karibu kila msichana aliyekuja kuoka mikate aliweza kunidanganya kama
sio mara moja na zaidi, wengine wakiniambia kuna thawabu kubwa mbinguni kama
ukiwa muungwana, wengine waliniambia mke wa kuhani amejifungua dume la ngombe
tangu mwezi july, Ngo’mbe ameruka juu ya dari na kutaga yai, ili mradi tu
wanidanganye, kijana mmoja aliyekuwa mwanafunzi wa Yashiva alikuja na kuniambia
Gimpel ulipokuwa umesimama pale Masihi alikuja na kufufua watu wote makaburini
na baba yako na mama yako wamesimama makaburini wakikuita,
Kusema ukweli nilifahamu wazi
kuwa jambo kama hilo haliwezi kutokea, lakini nilipoambiwa niliingia shaka kuwa
labda huenda kuna kitu na nikashindwa kukishuhudia kwa macho yangu mwenyewe,
lakini wakati wote nilidanganywa dahaa niliamua kuwa sitaamini jambo lolote na
niliweka Nadhiri kutokuamini mtu, lakini hata hivyo walinichanganya sana
nisingeweza kujua mwisho wa jambo kubwa mpaka lililo dogo nimelielewa kwanza.
Niliamua kwenda kwa Rabbi mmoja
ili kupata ushauri, aliniambia “ni afadhali kuwa mjinga siku zote kuliko kuwa
mwovu kwa saa moja” “wewe sio mjinga” alisema “wao ndio wajinga” kwa sababu
yeye anayemsababishia ndugu yake makwazo na aibu Jehanamu inamuhusu, Kama
haitoshi Binti wa rabbi alinichukua mpaka ndani, tukiwa tunaondoka katika
sebule ya Rabbi binti yake aliniambia umeshawahi kubusu ukuta? Nikamwambia
hapana kwanini hasa? Akaniambia ni sheria na unapaswa kuitimiza kila
unapotembelea hapa, daah hilo halikuwa na madhara ati lakini aliangua kicheko
naona alikuwa amenipata tena
Nilitamani sasa kuhamia mji
mwingine, lakini kila mtu alikuwa akijishughulisha kunitafuta mimi,
walinitafuta walinivuta koti langu mpaka wakararibia kulichana walinisemesha
mpaka masikio yangu yalikuwa kama yanataka kulowa mate, alikuwa kama mwenye
kulea mtoto hivi lakini niliambiwa kuwa huyu hakuwa mtoto wake ni mtoto wa
ndugu yake na yeye ni bikira na bado ni msafi hajanajisika, niliwaambia
mnapoteza muda wenu siwezi kumuoa mwanamke huyo, hata hivyo waliniambia
unajiaibisha mwenyewe na kuwa watanipeleka kwa Rabi na kunishitaki kuwa ninataka
kumchafulia jina lake, niliwatazama na kujua kuwa nnaweza kuwakimbia kwa vile
wamenifanya kama mtani wao, waliniambia inaweza kuwa heshima kubwa kwa Mwalimu
wako Rabbi kama tu utamuoa mwanamke huyu aliyelelewa na Rabbi itakujengea heshima, lilikuwa jambo
zuri kidogo kwangu kwa vile nilijihoji kuwa huwezi kuvuka maisha haya pasi na
kupitia hatua hii ya kuoa
Nilimfuata katika nyumba yake ya
udongo iliyokuwa imejengwa eneo kubwa la mchangani na kuingia ndani, kundi
kubwa la watu walinifuata wakiimba nyimbo walikuwa kama nyuki wanaotaka kuingia
mzingani, nilipofika karibu walisimama na kuniacha niingine mwenyewe, niliingia
na kupenya katika kuta nyembaba za nyumba hiyo huku nguo nyingi zikiwa
zimeanikwa, huku nyuma walikaa kimya na waliogopa kumsemesha chochote Elka
maana ndio jina lake, wanamjua kuwa hapendi kuzungumza lakini akizunhgumza ana
maneno makali sana, niliingia ndani na kumkuta akiwa anaosha miguu yake akiwa
hajavaa viatu, alikuwa amevaa nguo ya kitani ambayo ilikuwa imefunuka upande
mmoja, nywele zake zilikuwa nimebanwa vizuri kwa nyuma na chache zikiwa
zinaning’inia usoni, alikuwa ameumbika vizuri, nilivuta pumzi na kukaribia
kuzimia, alikuwa ananijua vema bila shaka, aliniangalia na kuniambia angalia nnani anayekuja kisha? alifuta kiti na kuniamuru nikae
Tuliongea swala zima la kuoana
lakini nilimwambia sikatai lolote lakini ninaomba uniambie ukweli kabisa wewe kweli ni bikira? Na je huyu mtoto kweli
ni wa ndugu yako? Usinidanganye tafadhali kwa sababu mimi ni Yatima
Mimi pia ni yatima alijibu, kila
atakayejaribu kukudanganya na yeye mwishoni na apinde pua yake, ni imani yangu
kuwa watu hawawezi kutuchukulia kwa faida zao, mimi nataka ulipe mahari ya Elfu
Hamsini tu sina makuu, na ngoja nikusanye michango mwenyewe unajua kwa nini
alizungumza kwa uwazi kuwa ni mwanamke ndiye anayelipa mahari na sio wewe, kwa
hiyo usianze kupiga bajeti kuwa nitafanyaje wewe kubali tu tuoane, kisha
aliniambia waweza kurejea ulikotoka
Niliwaza du leo huenda nitaachana
na kazi ya kuoka mikate, na mji wetu haukuwa mji wa watu masikini,waliandaa
kila kitu na kuendelea na maandalizi ya harusi, haikuwa jambo gumu kwa harusi
kuandaliwa wakati ule maandalizi yalifana na siku ya harusi iliwadia kumbuka
harusi yetu ilikuwa ya kiyahudi kwa vile wote tulikuwa wayahudi, siku ya harusi
ilipofika tulijiandaa kama kawaida, Harusi ilifanyika katika geti la uwanja wa
makaburi, watu walifurahi kuimba na kunywa kweli kweli, wakati agano la ndoa
lilipokuwa likifanyika nilisikia Rabbi mkuu aliuliza Bibi harusi ni mjane au
mwanamke aliyeachwa, mwanamke aliyekuwa akimsaidia bi harusi alijibu kwa niaba
yake ni yote mjane na aliyeachika, dah ulikuwa wakati wa giza nene kwangu,
lakini sikuwa na jinsi wakati hu je ningetimua mbio wakati wa shughuli za
harusi? Hali ilikuwa ngumu kwangu.
Watu waliiimba huku wakiwa
wamevaa mavazi meupe na baada ya mahubiri wengine walirusha Maputo meupe juu
wakimsifu Mungu na kwaajili ya kuwakumbuka marehemu, wengine walifurahi na
kucheza mpaka karibu na mimi na wengine walinikumbatia kwaajili ya kunipongeza,
zawadi zilitolewa nyingi sana lakini katika moja ya vitu vilinishangaza vijana
wawili walikuwa wamebeba kijikitanda kidogo cha mtoto, niliuliza je tunahitaji
hii kitu? Ni ya nini hii? Waliniambia usijali wala usiumize ubongo wako kitanda
kitakuwa mikononi mwako, nilijiuliza sana maswali mmh hii nini tena naenda
kupata utani mwingine, lakini nilijipa moyo kuwa mji mzima hawawezi kuwa vichaa
kiasi hiki na haiwezekani mji mzima waamua kunifanya mjinga.
Jioni nilikwenda kugonga katika
chumba cha mke wangu lakini hakuniruhusu kuingia kwake nilisema nini hiki sasa
kwani tuliozwa ili kuja kutazamana? Aliniambia hapana lakini niko katika siku
zangu! Nilimwambia lakini jana ulichukuliwa kwenda kuogeshwa ina maana
hawakuliona hili? Alinijibu jana sio leo, na leo sio jana unaweza kuipiga leo
kama unaiweza mmh kwa kifupi ilibidi nisubiri
Baada ya miezi minne alishikwa na
uchungu wa kujifungua mtoto, kha
wanakijiji walikuwa kimya tu wala hawakunicheka sielewi aina hii ya unafiki,
uchungu ulikuwa umemshika na alikuwa
amejiegemeza katika ukuta na kujaribu kutembea aliita Gimpel nakufa tafhadhali
nisaidie alilia nisamehe, wanawake walikuja na kuingia chumbani mwake na
wengine walianza kuchota maji na kutafuta beiseni la maji ahaa ningefanya nini
nilikwenda kwenye sinagogi na kuanza kuomba nikirudia Zaburi kadhaa
Mji mzima walisikia jambo lile na
habari zilitapakaa, nilisimama kwenye kona nikumuomba Mungu na kuimba zaburi
hilo ndio nililoweza kulifanya katika wakati ule mgumu wa kufikiri mke niliyeoa anajifungua ndani ya miezi minne
Watu waliosikia walisikitika na
kusema maombi maombi maombi, maombi hayawezi kumfanya mwanamke akawa mjamzito,
mmoja alisema maneno mazito kwangu yaani wewe ni sawasawa na Ngo’mbe, kuna
jambo zaidi ya hilo kwa Mungu!
Mke wangu alijifungua mtoto wa
kiume, siku ya ijumaa tuliingia kwenye sinagozi na kiongozi wa sinagogi wakati
wa matangazo alisema kuna sherehe kubwa sana kwa tajiri Gimpel kwani kwake
kumezaliwa mtoto wa kiume, watu wote katika sinagogi waliangua kicheko,
nilijisikia vibaya sana , lakini sikuwa na la kufanya maswala yote ya ibada ya
mtoto na swala la kumtahiri yalikuwa yananihusu mimi
Mji mzima walihudhuria sherehe na
shughuli nzima ya tohara ya mtoto, watu walikuja na vinywaji na zawadi na wengi
walinipongeza na nilitakiwa kutoa jina nilimpa jina la marehemu baba yangu
mzazi roho yake na istarehe kwa amani masikini, dah Baada ya sherehe watu
wote waliondoka na nilibaki peke yangu na mke wangu alichungulia kwenye pazia na
kuniita Gimpel
Mbona uko kimya meli yako
imezama?
Nitasema nini? Umenifanyia jambo
jema sana mara ya pili hii kama mama yangu angelikuwa hai na kulisikia hili
angefariki mara ya pili nilimjibu
We chizi nini? Unawezaje kusema
ujinga kiasi hicho alijibu kwa ukali sana Nilimwambia nani anapaswa kuwa Bwana hapa?
Unanini wewe eeh unawaza nini
kwani? aliuliza tena kwa ukali Nilimwambia wazi kwamba je hii ndio njia sahii ya kumfanyia Yatima?
Umefanya unyama wa hali ya juu nilimwambia
Aliniambia ondoa ujinga huu
kichwani mwako mtoto ni wako!, anawezaje kuwa wangu nilihoji, amezaliwa wiki kama
kumi na nne tu tangu tumeoana?
Aliniambia kuwa amini mtoto huyu
ni wako akanieleza kuwa huyu mtoto alizaliwa akiwa hajatimiza siku zake,
akaniambia nilikuwa na bibi yangu ambaye pia aliwahi kuzaa mtoto ambaye alikuwa
hajatimiza umri wake kwa hiyo maji hufuata mkondo hata huyu hajatimiza umri
wake kabisa na kisha alianza kuapa kwa mwenyezi Mungu kuwa hajaniambia uongo
hata kidogo, sikuweza kumuamini nilimuita Rabbi na tukazungumza siku ya pili na
aliniambia ni jambo la kawaida lilimtokea hata Adamu na Eva walienda kitandani
wawili na wakajikuta wamekuwa wane, je hakuna mwanamke duniani ambaye sio uzao
wa Eva? Walinihoji kiasi cha kuninyamazisha nilinyamaza lakini nani ajuaye mambo
yanavyokuwa? na nilikuwa namuheshimu Rabbi na sikufikiri kama anaweza kunidanganya pia hivyo nilikuwa mpole
Taratibu nilianza kusahau
machungu yangu, nilimlea mtoto kama wangu nilicheza naye alinizoea akitiwa
zongo niliweza kumpeleka haraka wa watoa zongo na kalikuwa kananipokea na
nilifanya kazi kwa bidii sana ili kumtunza mtoto huyu kama unavyoelewa ni
gharama sana swala la malezi, nilifanya kazi kama ngo’mbe au punda na nataka nikwambie
sijawahi kumchukia Elka kutokana na uovu ule, maisha yaliendelea ni kilea
mwanangu na mke wangu kila siku jioni niliwaletea zawadi ya mkate, pia
niliwaletea zawadi mbalimbali na mapocho pocho wakati mwingine niliiba ili
niwaletee zawadi zenye kufaa naamini nitasamehewa kwa wizi huo lakini hii
ilitokana na upendo wangu kwa familia yangu na kuonyesha kuwajali.
Nilikuwa nalazimika kulala mbali
na nyumbani kutokana na kazi zangu na siku za ijumaa nilirudi hata hivyo mke
wangu alikuwa akitoa udhuru wa namna mbalimbali katika kunipatia unyumba akitoa
sababu mara kichwa kinauma, mara kiungulia na mara hivi au vile, kama
mnavyojua wanawake walivyo, nilijisikia uchungu moyoni kwaajili ya hilo, zaidi
ya hilo alikuwa na kaka yake mdogo ambaye alikuwa amekuwa na ni kijana katili
sana aliposikia nikimkoromea aliwasha taa na kunimulika alinionya kuwa anaweza
kunipiga vibaya na kwakuwa alikuwa na nguvu kunizidi nilinyamaza, walinitishia
kunipa talaka pia hali ilikuwa ngumu, Nilihisi kuna mwanaume mwengine anayekula
chakula changu na kuondoka lakini nitafanyaje mimi ni wale watu wanaoachia
kila kitu mikononi mwa Mungu nilisema kama yuko mtu ananiibia Mungu atamlipa!
Siku moja usiku mashine yetu ya
kuokea mikate ilipata shida na hivyo nilitakiwa kurudi nyumbani usiku
nilifurahi kwani nilisema leo nitalala na mimi usingizi japo kidogo na mke
wangu, lakini nilipofika karibu na nyumbani nilisikia kama watu wanaokoroma
zaidi ya mmoja sikufurahi alikuwa mke wangu na mwingine alikuwa anakoroma kama
Ngo’mbe alikuwa ni jamaa amelala na mke wangu nilipotaka kulala ilileta shida
kubwa sana na makelele yalizidi kuwa makubwa kiasi ambacho niliona itakuwa aibu
mji mzima na pia nitamwamsha mtoto hivyo nilirejea Kazini na kuchukua safleti
za magunia nikatandika na kulala, hata hivyo sikupata usingizi nilikuwa
nikijiuliza usiku kucha kuwa uonevuu huu uitaisha lini ni lini mimi nitaendelea
kuwa mjinga, je hata ujinga na wajinga kama mimi hivi hakuna mwisho wao
nilijiwazia Gimpel hataendelea kuwa mjinga nafikiri kuna mwisho wa kila kitu.
Asubuhi nilikwenda kwa Rabbi
kwaajili ya maswala haya kesi hii ilikuwa na mvuto mkubwa sana na hivyo
ilivutia watu wengi Elka aliposikia alikuja akiwa na mtoto, na alikanusha kila
kitu na kusema huenda uko nje ya akili zako umerukwa na akili,Rabi alimkemea na
kusema anajua maswala ya ndoto, maono na kupamabanua mambo, alimkemea huku
akigonga meza, lakini alisimamia msimamo wake kuwa hakufanya jambo hilo ni
uzushi tu alisema Elka.
Wauza nyama na wafanya biashara
ya farasi wote walisimama upande wake na kumtetea, mwanamke mmoja alijitokeza
na kuniambia tumeshakufahamu tabia zako, mara mtoto alianza kujikojolea na
hivyo Elka alitakiwa kuondoka haraka kwa sababu katika sinagogi kuna sanduku la
agano na haipaswi kitendo kile kutendeka katika sinagogi. Hivyo Elka alitolewa,
Nilimwambia Rabii nifenye nini
sasa?
Lazima umpe talaka mara moja
alinijibu Rabbi
Nikamuuliza je akikataa?
Aliniambia lazima utoe talaka
hilo ndio la msingi na si vinginevyo
Nikamwambia sawa Rabbi ngoja
nifikiri
Hakuna cha kufikiri ndugu yangu
vinginevyo utabaki naye katika paa moja na tabia ileile
Je nikitaka kumuona mtoto
niliuliza?
Achana naye huyo kahaba mwache
aendelee na huyo mjinga wake
Alikazia hakikisha unalifanyia
kazi hilo na si vinginevyo maadamu mimi ni hai sitaki kusikia tena
Wakati huo ulikuwa mchana na
nilijiambia kuwa nitahakikisha ninalifanyia kazi.
Usiku nilipokuwa nimejituliza
kwenye magunia nililifikiri jambo hilo kwa uchungu sana, nilimtafakari yeye na
mtoto pia, Hasira zangu zilipanda sana lakini pia nilitafakari kuwa mimi sio
mtu wa kukasirika kiasi kile, niliwaza na kutafakari kuwa wakati mwingine
wanadamu hawawezi kuishi bila kukosea na kwa vile amekataa kabisa kwa kiapo
huenda labda mimi niliona maluweluwe tu yaani unaweza kuona kama mtu halisi
kumbe hakukuwa na mtu na kama ndivyo nitakuwa simtendei haki Elka na
nilipotafakari hilo nilianza kububujikwa na Machozi, kisha asubuhi nilikwenda
kwa Rabbi na kumwambia kuwa huenda nilikosea, Rabi aliniambia kama ni hivyo
sina la kuamua katika kesi yako na unachopaswa kukifanya labda uendelee
kumtunza mkeo lakini usilale naye tena na unapotuma matumizi tumia mtu na
usionane naye tena.
Miezi tisa ilipita kabla marabi
wote hawajafikia muafaka na mwisho walikubaliana na maoni yangu na waliandika
barua sikufahamu kama lingechukua muda mrefu hivyo, hata hivyo baada ya miezi
hii tisa Mke wangu alijifungua mtoto mwingine na sasa alikuwa mtoto wa kike,
siku ya sabato nilimpeleka mtoto kwaajili ya Baraka za kikuhani na
nilikaribishwa karibu na Torati na na kuombwa nitoe jina na nilimpa mtoto jina
la mama mkwe wangu,watu walionifahamu walinitia moyo kuendelea na maswala yangu
kwani walihisi labda nitaelemewa na huzuni wakinicheka, nilijiapiza kuwa sasa
nitaamini kila neno atakaloniambia mke wangu kwani nisipomuamini yeye leo kesho
nitashindwa kumuamini hata Mungu
Niliendelea kuitunza familia
yangu na kuwasaidia chakula na kila kitu kilichowafaa, pia niliendelea
kumsaidia kijana mmoja aliyekuwa jirani yangu na aliyekuwa anajifunza kazi,
siku moja kijana huyu aliniembelea nyumbani na kuniambia Gimpel una mke mzuri
kijana na watoto wawili wazuri sana ambao kwa kweli hustahili lakini kile watu
wanachokisema kuhusu mkeo, kha watu wana midomo mirefu nafikiri unachopaswa
kufanya ni kuwapuuza kama kama ulivyopuuzia msimu wa baridi uliopita.
Siku moja Rabbi alinitumia ujumbe
na kuniuliza una uhakika kuwa uliwaza vibaya kuhusu mkeo? Nilimwambia ndio nina
uhakika, aliniambia kwa nini sasa ulikuja ukishuhudia kuona mwenyewe kwa macho?
Nika mwambia yalikuwa ji maruweruwe tu, aliniambia sasa unaweza kwenda nyumbani
na kuendelea na maisha maana marabi wamekuruhusu nilibusu mkono wa rabi na
kuondoka.
Nilitamani kwenda nyumbani mara
moja sio jambo dogo kuishi mbali na familia, lakini nilijitia moyo kwenda
kazini na kisha nitakwenda nyumbani jioni, jua lilipokuchwa nilifanya
maandalizi na kubeba zawadi kibao na mikate na nikaanza kuelekea nyumbani,
kulikuwa na mbaramwezi ya kutosha siku ile kulikuwa na kabaridi na barafu
zilikuwa zinaanguka, niliona nyota kwa mbali na nilikuwa nikitembea kichwani
kawimbo kalinijia na nilitamani kutembea huku ninaimba lakini nilihofia
kuwaamsha watu waliokuwa wamelala, lakini nilikuwa nauwaza maana ni wimbo
unaofukuza mashetani, niliendelea na safari, nilipokaribia nyumbani moyo wangu
ulianza kudunda kwa kasi kama moyo wa mtu mhalifu, niliingiwa na hofu ya ghafla
moyo wangu ukidunda kwa kasi sana, nilifika na kuona mwangaza ndani kutokana na
Nuru ya mbaramwezi niliweza kuona mtoto mpya aliyezaliwa kakiwa kamelazwa aidha
pia nilimuona mke wangu Elka akiwa amelala na nilipokaribia kabisa nilimuona my
amelala karibu na mke wangu Elka na nilipoangalia vizuri unaweza kuhisi alikuwa
nani? Alikuwa ni yule kijana niliyekuwa ninamsaidia, Ghafla ingawa mbaramwezi
inawaka niliona giza kali,nilitetemeka na meno yalianza kugongana, mikate na
zawadi zilizokuwa mkononi zilianguka ghafla na mke wangu alishituka usingizini
huku akuliza nanii? Kwa sauti Gimpel? Imekuwaje umerudi na uko hapa? Mi nilijua
umekatazwa? Sasa fanya jambo moja tafadhali nenda kaangalie kama mbuzi na
kondoo hapo zizini wako salama maana mmoja alikuwa anaumwa, nilikwenda nilikuwa
nimesahau kama tuna mbuzi na nilipozikia kuwa anaumwa nilimuonea huruma,
nilipofungua mlango wa zizi, mbuzi yule alisimama na inaonekana alikuwa salama
na wengine wote,baada ya hilo nilirejea ndani na kuuliza yuko wapi yule mjinga
mke wangu aliniuliza mjinga gani? Nilimwambia yule kijana akaniambia hizo ndoto
zako inaonekana una mapepo mjinga mkubwa we nitapiga kelele utokezako sasa hivi
tokaa nilipotaka kuleta fujo Yule ndugun yake aliamka na kuja kutaka
kunishambulia alinipiga vibaya kwa nyuma na nikafikiri amevunja shingo yangu
nilitulia na kujiuliza kuna kitu hakiko sawa kwangu, mara yule nduguye
aliniambia usije ukafanya kasfha nyingine hapa na hiyo mikate yako hakuna
atakayekula hapa, Nilitulia
Sawa inatosha sasa Elka alisema na aliniamuru
kulala kimya mpaka asubuhi bila kufanya lolote, asubuhi nilimuona yule kijana
na nilitaka kumuonya lakini alinikemea kwa sauti kubwa kama mbwa na kuniambia
nisikilize inakupasa uende kwa mganga au mtu yeyote mwenye uwezo wa kutibu akutibu
kwa sababu nafikiri kuna misumari kicwani mwako haiku sawasawa duh, jamani
kufupisha hii habari niliishi na mke wangu katika hali hizo kwa miaka 20,
alizaa watoto sita wakiume wawili na wakike wane kwa mtindo huohuo mimi
nikiamini tu kuwa ni wa kwangu, marabi waliniambia endelea kutenda mema kwani
wenye haki huishi kwa imani
Ghafla mke wangu alianza kuugua
kuanzia kwenye maziwa na kushuka chini kadiri siku zilivyoenda hali ilizidi
kuwa mbaya, na ilionekana wazi kuwa hawezi kuishi, nilijaribu kuwaita madaktari
na waganga kumtibu na kila siku walikuja kumwangalia na kumtibu nilimuuguza na
kuacha kwenda kazini wakati huu nilikuwa na Bakeri yangu ya mikate na nilikuwa
mtu tajiri lakini nilikuwa sijamwambia, pamoja na juhudi za kitabibu hakuna
nafuu yoyote mke wangu aliipata hali ilizidi kuwa mbaya kabla hajafa aliniita
kitandani na kuniambia Nisamehe sana Gimpel
Nilimwambia unaomba msamaha kwa
lipi?
Umekuwa mke mwaminifu na mwema
sana
Ole wangu Gimpel alijibu mimi sio
mwema Gimpel nimekudanganya kwa miaka hii yote sasa nataka kupatana na Muumba
na leo nataka nikuweke wazi kuwa watoto hawa wote sio wa kwako, yaani kama
kichwani mwangu ningekuwa ana akili ya mbao ingekuwa vizuri
Nilidakia ni wa nani sasa?
Sijui Gimpel tafadhali nimetembea na wanaume wengi sana na sifahamu
lakini nina uhakika sio wa kwako huna hata mmoja hapa, wakati ninashangaa
aligeuka na kukata roho uso wake ukiwa na tabasamu ni kama alikufa akiwa
ananiambia nimemdanganya Gimpel maisha yangu yote.
Siku moja baada ya kipindi cha
maombolezo kuisha raho chafu ilinijia ikiwa na sura yake ikaniambia Gimpel
mbonma unalala? ulimwengu mzima umekudanganya na ukaamua kuulipa kwa
kuudanganya, nilimuuliza mimi nimeudanganyaje ulimwengu? Unawezaje kubeba mkojo
katika kapu usiku na mchana na kutokuachie uende chooni? Kivipi?
Mimi nilikuwa nakudanganya kuwa
hawa ni watoto wako na nilikuwa nalala na wanaume wengine lakini nawe ulikuwa
unaudanganya ulimwengu kuwa hawa ni watoto wako na mimi ni mkeo
Nilimwambia je hujui kuwa kuna
hukumu ya mwisho?
Aliniambia hakuna hukumu ya
mwisho ulimwengu umekudanganya, umetoa fedha nyingi ukaaminishwa kuwa umenunua
paka tumboni mwako wakati hakuna paka hicho ndio kilichokukuta nikamwambia vipi
kuhusu Mungu?
Akaniambia hakuna Mungu pia
ninachokuambia ni cha kusadikika tu. Nilitamani
kumpiga kwa nguvu lakini nilikuwa nimejaa hofu na nilitaka kupiga kelele kuelezea
kilichotokea, mara yule kijana alikuja niliyekuwa nikimsaidia na baadaye
alilala na mke wangu nilimkamata na kumtupia katika tanuru la moto la mikate
kwa hasira nilimuua na kumzika pamoja na tanuru alisikika akisema leo
umejilipizia kisasi, baada ya tukio hilo niliinamisha kichwa na nilijikaza nikalala usingizi mara tena Elka
akanijia katika ndoto akiwa na sanda akaniambia umefanya nini Gimpel
Nilimwambia ni kwa sababu ya
makosa yako kisha, nikaanza kulia akaniambia we we ni mjinga wewe ni mjinga kwa
sababu mimi nilikuwa muongo kwenye kila kitu cha uongo na nilijidanganya hata
nafsi yangu na sasa ninalipwa yote ukweli sikuwa nimemdanganya yeyote nilikuwa
najidanganya mwenyewe najuta najuta sana, nilimuangalia uso wake na alikuwa
mweusi sana, kwa kuwa alikuwa motoni
lakini aliniambia huna nafasi tena peponi uliyokuwa umewekewa kwa muda mrefu
imefutwa,niliamka na nikakaa nikagundua kuwa kumbe kila kitu kilikuwa kimekaa
sawa anayedanganya anajidanganya khah
Niliharibu kila kitu kwenye bakeri
ya mikate nilikwenda nyumbani na kuchukua mali sehemu Fulani niliwagaia watoto
wote niliwaambia nimemuona mama yenu usiku wa leo ameungua vibaya motoni
niliwaambia kila mmoja asahau kabisa kuwa yuko mtu anaitwa Gimpel na wao
hawakujibu neno lolote walibaki kushangaa
Niliwabussu na kuwatakia maisha
mema na nilivaa mabuti yangu na kuanza kuondoka kila aliyeniona mjini
alinishangaa na kuniuliza unaenda wapi niliwajibu naenda ulimwenguni na
nilihama mji ule kabisa walioniuliza niliwaambia nimedanganywa miaka yote ya
ujana wangu lakini kwa kuishi kwangu sana nimegundua kuwa watu hawa hawakuwa
waongo kwani ndio mtindo wa maisha usipodanganywa leo utadanganywa kesho na
kama sio mwaka huu basi mwaka ujao na kila mtu anaweza kudanganya hata bila
kukusudia
Nilihamia mji mwingine na huko
nilikuwa nikipokelewa na watu kadhaa wa kadha nilikula chakula katika meza
kadhaa isipokuwa usiku nikilala mji nioondoka ulikuwa unanijia na Elka pia
nilijiuliza ulimwengu huu ni ulimwengu wa namna gani, Nilikuwa nikiishi maisha
ya kuwasimulia vijana hadithi mbalimbali katika maisha yangu na nilizisimulia
kiasi ambacho nilikuwa nasahau na kuzirudia zingine na watoto waliokuwa
wakinifuata babu tusimulie khadithi niliwasimulia na wengine waliniiambia haa
babu hii tayari.
Stori hii imeandikwa na Isaack
Bashevis, Mwimbaji na mtunzi wa kiyahudi
Akionyesha maisha ya zamani huko
ulaya miaka ya 1800 hivi wakati jamii ya kiyahudi ilipokuwa inaishi ulaya na
inakuonyesha jinsi Gimpel alivyoweza kuozwa binti wa Kikuhani na rabi, lakini
akidanganywa kuwa ni bikira na jinsi alivyoendelea kudanganywa maisha yake yote
watu wakiitumia nafasi yake ya kumcha Mungu kama njia ya kumhadaa bila kujali kuwa alikuwa yatima pia ulimwengu ni
ulimwengu wa udanganyifu, na ni ulimwengu ambao hauwezi kukuhurumia kwa sababu zozote zile, unaweza kuwa muongo wakati unajaribu kuwa mkweli,
wanadamu ni waongo, makuhani pia ni waongo, hakuna uadilifu, mashetani nao ni
waongo ni nani wa kuaminiwa? Unamuamini sana mkeo, Mumeo? Mchungaji wako? Chagua
wa kumuamini mkweli ni mmoja tu Mungu pekee.
Imetafasiriwa na Rev. Innocent
Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima