Kumbukumbu la torati 26:6-9 “Wamisri wakatuonea, wakatutesa, wakatutumikisha utumwa
mzito. Tukamlilia Bwana, Mungu wa baba
zetu; Bwana akasikia sauti yetu, akaona na taabu yetu, na kazi yetu, na kuonewa
kwetu. Bwana akatutoa kutoka Misri kwa
mkono wa nguvu, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa utisho mwingi, na kwa ishara,
na kwa maajabu; naye ametuingiza mahali hapa, na kutupa nchi hii, nchi ijaayo
maziwa na asali.”
Sinagogi la Kiyahudi huko San Diego, lililoshambuliwa kwa Risasi 28/04/2019
Utangulizi:
Jana tarehe 28 April 2019 sawa na mwezi Nisan 23 5779 kwa kalenda ya
kiyahudi, nilipata habari ya kuuawa kwa Myahudi mmoja kutokana na shambulio la
risasi lililofanyika huko San Diego katika mojawapo ya sinagogi la kiyahudi, na
wengine watatu kujeruhiwa vibaya, nilikuwa bado sijasahau tukio la kuuawa kwa
wakristo wakati wa Pasaka Nchini Sri-lanka nikafikiri na kuwaza kwamba bado
dunia ya leo iliyoendelea kuna watu bado wanafikiri wanaweza kuwepo duniani
peke yao bila kuchanganyika na watu wanaotofautiana nao kimawazo kifikira
kiitikadi na kiimani? Dunia inapaswa kutafakari kwa kina kuhusu ukomavu na
uwezo wa kuchukuliana katika jamii na kupendana bila kujali tofauti zetu,
Biblia inasema katika 1Yohana 4:8 “Yeye
asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.” Hii ni wazi kuwa
bado dunia haijamjua Mungu, na kuwa jamii inapaswa kukumbuka na kuhimiza na
kufundisha kuhusu upendo, ni muhimu kufanya kilalinalowezekana kuing’oa chuki
miongoni mwa wakazi wa dunia, na kukumbuka kuwa Yesu hakuwa mjinga alipokuwa
akifundisha Upendo, alikuwa anajua wazi kuwa dunia itakuja kufikia na kuwa na
matukio haya tunayoyashuhudia leo katika jamii iliyoendelea.
Katika kifungu cha maandiko ya
msingi, Musa alikuwa anawakumbusha wana wa Israel sheria za Mungu na hususani
kwa kizazi kipya ambao wengi waoa walizaliwa Jangwani au na wale waliotoka
Misri wakiwa vijana na waliokuwa wadogo, Musa alikuwa akizungmzia kumtolea
Mungu sadaka za shukurani watakazomtolea Mungu watakapokuwa katika nchi ya
amani nchi iliyojaa maziwa na asali nchi ya Israel aliwalekeza kwamba watakapotoa
wamkumbushe Mungu kuwa walionewa huko Misri, lakini walipomlilia Mungu
akawaokoa na kuwaleta katika inchi hii iliyojaa maziwa na asali
Katika kifungu hiki Kumbukumbu la Torati 26:6 ““Wamisri wakatuonea, wakatutesa, wakatutumikisha utumwa mzito.
.”
Biblia ya kiingereza NIV inasomeka hivi Deuteronomy 26:6 “But the
Egyptians mistreated us and made us suffer, subjecting us to harsh labor.”
Biblia ya
Kiyahudi iitwayo (The Israel Bible) inasomeka hivi Deuteronomy 26:6 “The Egyptians DEALT
HARSHLY WITH US and oppressed us; they imposed heavy labor upon us.”
Musa aliwakumbusha Jambo hili la
msingi walikumbuke watakapokuwa wakiabudu, kwa sadaka ya shukurani, wamkumbushe
Mungu kuwa walitendwa vibaya na wamisri neno kuonewa, kuteswa na kutendwa
vibaya katika lugha ya Kiebrania linatumika neno “VAYAREIU” likimaanisha kuwa lakini
rafiki zetu walitugeuka,walitutenda mabaya, wakatuonea, wakatutesa,
wakatudhulumu kisha wakatugeuza kuwa
watumwa kwa utumwa mbaya na mzito” Hii ilimaanisha kuwa Israel hawakushuka
Misri wakiwa watumwa walikuwa rafiki wa wamisri, walikuwa wapendwa, walikuwa
jamaa na ndugu wa waisrael, lakini hatimaye ukafika wakati wakawageuka,
wakavunja urafiki, wakaanza kuwabagua na kutengeneza sheria za kuwabana, na
kuwaonea na kuwatesa na kuwakandamiza na hatimaye kuwafanya watumwa wao, Ndipo
ulipofika wakati wayahudi wakamlilia Mungu awatoe katika utumwa ule mzito na
Mungu akawaokoa akawapeleka katika nchi ya ahadi, ambako huko npekee ndipo
mahali ambapo Wayahudi watakuwa salama na wakamfurahia Mungu.
Leo hii sio Misri tu ambao
wamewakaribisha Wayahudi kisha wakawaonea baadaye, ziko nchi nyingi tu ambazo
zimewapokea wayahudi wakiwa kama marafiki, kama ilivyotokea Ujerumani na
Uganda, lakini baadaye katika namna isiyoweza kueleweka watu hao waliwageuka nakuwaona
wayahudi kama adui na watu wasiofaa, ili mtahudi aweze kuwa salama ni lazima
popote pale walipo warudi katika nchi yao ya asili nchi yao ya ahadi ili
wamuabudu Mungu pasipo hofu na watoe sadaka ya shukurani na mateso yao yote
yatageuka kuwa historia
Wako watu wengi sana leo
wanateseka lakini chanzo cha mateso yao hakikuwa chuki na majuto na dhuluma
ambazo wanaziona sasa, inawezekana wewe ni House girl ulichukuliwa kama dada wa
kazi kwa nia nzuri, ukaenda mjini kama rafiki na ndugu, na ukapokelewa vema huko
ulikokwenda mama na baba wa nyuma uliyofikia walikataa kuitwa anko walisema
utuite mama au baba, lakini baada ya siku kadhaa hali ilibadilika umeanza
kuitwa hili, limbwa, paka , nyau. Fala na kadhalika.
Inawezekana ulioa au kuolewa kwa
nia nzuri kabisa, wakati unachumbiwa ulikuwa ni rafiki, hukuwa mtumwa mliitana
majina mazuri, sweetie, asali wangu, maua, dear, dally na kadhalika lakini hapa
unaposoma ujumbe huu mambo yamegeuka wewe sasa ni jibwa, fala, lione,
liangalie, sijui nililioa la nini, mlango wa nane, balaa nuksi, mwiba na
kadhalika.
Inawezekana wakati uaajiliwa
ulikaribishwa kwa furaha, bosi aliwataka wenyeji wakupe saada mkubwa
utakaouhitaji, ulidekezwa, ulifanywa kama moja ya wamiliki wa kampuni, ulikuwa
ni wakati wa furaha umepata kazi mpya, lakini baada ya sikukadhaa, Mambo
yamebadilika, unaonekana kama mzigo, unateseka, unapelekeshwa unaonekana hifai
tena.
Kila mahali walikokwenda Wayahudi
walikaribishwa walipokelewa kwa ukarimu lakini leo watu wanawalipua, wanawapiga
risasi, kama majambazi au watu wasiofaa, huko san diego wayahudi wameuawa
katika sabato ya kwanza ya Pasaka walipokuwa katika ibada na mama mmoja mwenye
miaka 60 alifariki na wengine watatu kujeruhiwa vibaya, mmoja akiwa kiongozi wa
kidini Rabbi na mkuu wa sinagogi husika kinawafanya wengine wawe na chuki dhidi
ya wengine, kwa nini wakristo wameuawa Srilanka na kwa nini waqyahudi
wameshambuliwa nani atawasemea
Hujawahi kuona unakaribishwa
mahali vizuri, unapeewa na ofisi, unasifiwa kila mahali unahesabika kama mtu
mwema kisha baada ya muda wewe ndio unaonekana kama mwiba wa kila mmoja pale
ulipo?
Hali hii ndio inayowatokea Israel
Duniani kote, ndio inayoatokea Wakristo, watu wanaona kuwa ni haki kuvaa mabomu
na kuwalipua
Iko siri moja kubwa na ya
kipekee, ni kukaa katika ahadi za Mungu tu, Ili Israel iweze kuwa salama hawana
budi kuungana na kukaa Israel pekee ili wajilinde wakae katika nchi ya ahadi
waliyoahidiwa baba zao Ibrahimu Isaka na Yakobo ndio wanaweza kujithibitishia
usalama wao.
Wako watu wengi leoa hawako
salama kwa sababu walifanya urafiki na shetani, walipokelewa na shetani ,
ibilisi kwa furaha sana wakiwa kama marafiki, Lakini kumbuka kuwa shetani hana
urafiki na mtu awaye yote lazima atakugeuka tu atakutesa atakugeuza kuwa mtumwa
na atakudhulumu, shetani anataka ufanye mambo kwa faida yake na maslahi yake
hakuna mafanikio ya kweli kwa shetani, ili uwe salama huna budi kurudi kwa Yesu
kristo na kujificha kwake, yeye ndio nchi halisi ya ahadi na kwake kuna
usalama, Kwa ibilisi haijalishi kuwa wewe ni mwenye haki au la kwake nifuraha
kubwa ukiangamia yeye na watu wake hawatajali haki yako, wakati umefika wa wewe
kukaa katika uwepo wa Mungu kwa usalama wako, ili amani ipatikane katika ndoa
yako hakikisheni mnamkaribisha Mungu na kujifunza upendo kama yeye alivyoagiza.
Isaya 5:1 Mwenye haki hupotea, wala hakuna
atiaye hayo moyoni; na watu watauwa huondolewa, wala hakuna afikiriye ya kuwa
mwenye haki ameondolewa asipatikane na mabaya”
Hakuna wanaojali kile
kinachowapata wayahudi leo. Lakini Palestina ikiguswa tu dunia itapiga kelele
hata kama wakati mwingine wao ndio wachokozi na ndio wanaoanzisha kurusha
maroketi, Israel ikijibu kama sehemu na wajibu wa kujihami na kujilinda, Israel
ikijilipizia kisasi kwa adui zake dunia inapiga kelele je wadhani Wayahudi sio
watu, nani atawapigia kelele na kuielimsha jamii duniani kuwa nao wanastahili
kutetewa na kuangaliwa kwa maslahi yao duniani, Mimi sisemi kwa sababu nina
asili ya Kiebrania tu hapana bali nataka haki itetendeke duniani ifikie hatua
tujifunze pendo lake Yesu na kuielimisha katika jamii yetu, kila mmoja anapaswa
kujua kuwa kama tunampenda Mungu tutathamini uhai wa watu wake kuliko imani
zetu, Dunia pia inapaswa kuelewa kuwa ili Israel iweze kuwa salama nilazima waelekee katika nchi ya ahadi na
kukaa katika taifa lao wenyewe, ili sisi nasi tuweze kuwa salama turudi katika
uwepo wa Mungu. Tutafanikiwa. Israel walimlilia Mungu, akawasikia akaziona
taabu zao na kuonewa kwao aakawaokoa kwa mkono wa nguvu ulionyooshwa na
wakajiliwa na kipindi cha neema “I stand with Israel.”
Rev. Innocent Kamote.
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima