Andiko: Ayubu 9: 25 -26 Biblia inasema “ Basi siku zangu
zina mbio kuliko Tarishi; Zakimbia wala hazioni mema, Zimepita kama merikebu
ziendazo mbio; Mfano wa tai ayashukiayemawindo.”
Utangulizi:
Leo
tutachukua muda kutafakari kwa kina somo kuhusu Mfano wa tai ayashukiaye
Mawindo, Ni muhimu kuwa na ufahamu kuwa Mungu aliviumba viumbe vingi duniani
kwa makusudi mbali mbali lakini mojawapo ya kusudi kuu ni kutufunza mambo
mbalimbali ya msingi, Tai ni moja ya Ndege au kiumbe ambaye biblia imezungumza
sifa zake kwa kina na mapana na marefu na tunaweza kujifunza mambo kadhaa ya
muhimu kutoka kwa kiumbe hiki.
Kuna usemi
wa wahenga kuwa ndege wa aina moja huruka pamoja, Usemi huu kwa Tai ni tofauti
tai wanaruka pekeyao na wanafurahia kuruka juu sana, sifa zake zinawekwa katika
Biblia kwa vile ni ndege mwenye sifa za kipakee ni ndege asiyeshindwa na ukubwa
wa mawindo yake.
Kwa nini
Biblia inampa Tai sifa za hali ya juu sana ni muhimu kwetu kujifunza sifa zake
na kuzilinganisha na maisha yetu.
Tai ni wenye uwezo mkubwa wa kuona mbali.
Tai ni wenye uwezo mkubwa wa kuona mbali.
1.
Ayubu 39:27-29 Biblia
inasema hivi “
Je! Tai hupaa juu kwa amri yako, Na kufanya kioto chake mahali pa juu? Hukaa jabalini, ndiko kwenye malazi yake, Juu
ya genge la jabali, na ngomeni. Toka huko yeye huchungulia mawindo; Macho yake
huyaangalia toka mbali.”
Tai kama
utamfanyia uchunguzi na kumchungulia kwa mbali ni ndege makini sana Biblia
inamsifia kuwa “macho yake huyaangalia mawindo toka mbali” ndi ndege hodari
katika kuwinda macho yake amebarikiwa uwezo wa kuona mbali sana na anaona kwa
uwazi kabisa inasemekana anauwezo wa kumuona mwenzake akiwa Maili 50 kwa uwazi
kabisa! Jambo hili linatufundisha nini? Naamini unaweza kupata picha Fulani
Tai huona
kwa uwazi kabisa Maili “50”
I Maili =1.6
km
Maili 50 =
80 km
Mamia ya
watu hodari wamewahi kuishi duniani na kupita wakiwemo watu maarufu sana
duniani na viongozi wakubwa
Ili dunia
iweze kuwa na Mafanikio makubwa sana inahitaji watu na viongozi wenye uwezo wa
kuona mbali sana, Abraham Lincoln rais wa 16 wa Marekani aliongoza katika
wakati mgumu sana wenye matatizo mengi na inchi ikiwa katika vita vya wenyewe
kwa wenyewe, lakini ndiye aliyefanikiwa kuweka misingi ya umoja na kukomesha
utumwa na kuifanya Marekani iwe kama ilivyo leo,
Ili dunia
iweze kuwa na mafanikio ni lazima iwe na watu wenye uwezo wa kuona mbali,
wanaoangalia faida za mbeleni za kwao na za kizazi kinachokuja badala yao
Ili uweze kuwa na mafanikio:-
Ili uweze kuwa na mafanikio:-
·
Ni lazima uwe na uwezo wa kuona mbali Mithali 29:18 “Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana
heri mtu yule aishikaye sheria.”
·
Watu wasio na maono ya mbali wanaweza
kutugawa kupitia dini na ukabila
·
Watu wasioona mbali hawajali kutunza
Mazingira
·
Watu wasioona mbali hawaogopi kuharibu
mahusiano
·
Watu wasioona mbali hawaogopi kuua wanyama
kama tembo kwa faida yao
·
Watu wasioona mbali hawaogopi kufanya Ufisadi
kwa kuifilisi nchi
·
Watu wasioona mbali hawafikiri kujisomea kwa
bidii
·
Watu wasioona mbali hawafikiri kujiwekea
akiba
Mithali 6:6-8 “Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.”
Mithali 6:6-8 “Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.”
·
Watu wasioona mbali hawafikiri kuhusu maisha
yao baada ya kufa duniani Waebrania 11:9-10 “Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya
ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na
Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.Maana alikuwa akiutazamia mji
wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.”
Luka 12:16-21, “Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.”
Yakobo 4:13-15 “Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.”
Luka 12:16-21, “Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.”
Yakobo 4:13-15 “Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.”
·
Kuna majuto kama hatutaweka mipango yenye
kumuhusisha Mungu.
Awaye yote aliye kama tai atakuwa na ujuzi wa kuona mbali na
kuzingatia faida za siku zijazo kuliko kuangalia leo. Unayaona mwindo yako kwa
mbali. Ni lazima tuwe na maono makubwa yaliyopimwa kwa kina na yatakayoleta faida
kubwa na matokeo makubwa katika jamii.
Tai ni ndege wasioogopa Mawindo. wala maadui
2.
Tai ni ndege
asiyeogopa hata kidogo, wakati wote anapambana kuhakikisha anashinda,
atapambana kuhakikisha anapata mawindo yake au anatawala,unapoangalia sinema za
maisha ya tai utaweza kuona hawaogopi
mawindo haijalishi mawindo yao ni makubwa kiasi gani hata kama ni mbuzi ambaye
anaonekana kuwa mkubwa kuliko uwezo wake tai ni lazima atabeba, wana ujuzi
mkubwa wa kuwinda na ni mahodari, tai haogopi
Ni muhimu
kufahamu kuwa kama unataka kufanikiwa katika maisha haya usiogope kufanya jambo
gumu, usiogope kukabiliana na watu wakubwa au waliokuzidi umri, hakikisha kuwa
unakipigania kile unachokipenda,
·
Usiogope kupigania unachokipenda Waamuzi 14:1-7 ”Samsoni
akatelemkia Timna, akaona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti.
Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemwona mwanamke
huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi mnipatie, nimwoe. Ndipo baba
yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu
zako, au katika jamaa zangu zote, hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti
wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana
ananipendeza sana. Lakini baba yake na mama yake hawakujua ya kuwa jambo hili
ni la Bwana; maana alitaka kisa juu ya Wafilisti. Basi wakati ule Wafilisti
walikuwa wakiwatawala Israeli. Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake
wakatelemkia Timna, wakafika mashamba ya mizabibu huko Timna; na tazama,
mwana-simba akamngurumia. Roho ya Bwana ikamjilia kwa nguvu, naye akampasua
kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu cho chote mkononi mwake;
lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya.Basi akatelemka na
kuzungumza na huyo mwanamke; naye akampendeza Samsoni sana.”
·
Usiogope kusimama katika kweli hata kama
itakuletea madhara
·
Usiogope ukubwa wa tatizo unalopambana nalo
pigania mpaka kieleweke Kataa hofu Hesabu 13:25-33 "Wakarejea baada ya kuipeleleza nchi, mwisho wa siku arobaini. Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonyesha matunda ya nchi. Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake. Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko. Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu; na Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima, na Mkanaani anakaa karibu na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani. Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka. Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno. Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi."
·
Usiogope ugumu wa masomo unayosoma
·
Usiogope au kuonea aibu aina ya kazi
unayoifanya
·
Lengo lako kuu ni kuhakikisha unafanikiwa
·
Usiogope mateso utakayoyapata kwaajili ya
imani au kile unachokipigania
·
Usiogope kuanzisha huduma au kufungua kanisa,
usiogope kuwa mmisionary, usiogope kugombea urais kama Mungu anataka ufanye
jambo kwa faida yake lifanye
·
Uisogope kufanya lolote ili kufanikisha
malengo yako, Tai hawaogopi mawindo yao hata kama anachokiwinda ni kikubwa
kuliko umbile lake.
3.
Tai ni Hodari
hawaogopi Dhuruba.
Ukitaka
kujua uhodari wa Tai utaweza kuuona wakati wa dhoruba, wakati huu ndege wengine
wote hukimbia na kujificha kwa kuogopa dhoruba , kwa tai mambo ni tofauti
anafunua mbawa zake na kuzitanua na kupaa kwenda juu zaidi, taia wanatabia ya
kutumia dhoruba kwa faida, wakati ndege wa kawaida wakiogopa, ni muhimu
kufahamu kuwa watu wanaolinganishwa na tai hawakimbii changamoto zozote bali
huzitumia changamoto kusimama na kuongeza viwango, Mungu anataka watu
wasiokimbia changamoto bali wenye uwezo wa kukabiliana nazo huku wakisimama katika
kusudi au kuelekea juu zaidi
Mtu yeyote
anayeogopa Changamoto hawezi kufanikiwa
·
Wakati wa Dhuruba tai Hakimbii kama wengine
·
Tai hupanua mbawa zake na dhuruba humpeleka
juu sana
·
Tai huitumia dhoruba kwa faida
·
Usikimbie changamoto wala usiziogope
·
Tumia changamoto kuongeza viwango au
kujiongeza Matendo 14:21-22, "Hata walipokwisha kuihubiri Injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia,wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi."
1Petro
4:12 " Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho."
4.
Tai wanaruka
juu sana.
Ndege huyu
ndiye anayejulikana kama mfalme wa anga inasemekana tai wanauwezo wa kuruka juu
kiasi cha fiti 10,000, katika
kiwango hicho hutaweza kumuona ndege mwingine na ukimuona ni lazima atakuwa
tai, Tai haruki wala kutafutiza chakula pamoja na njiwa, alisema Dr, Myles Munroe Marehemu, alisema wakati njiwa wakiwa ardhini wanachakuachakua
siku nzima na kulalamika,Tai hawanung’uniki, hawapigi kelele, wanapaa juu sana
wakisubiri mawindo wakisubiri nafasi waweze kuitumia, watu wakuu duniani ni
wale wanaotatua matatizo na sio wanaolalamika, wanatumia nafasi na changamoto
yoyote kama tai dhoruba inapotokea. Ni watu wanaojitunza na kutokuchangamana na
wengine Wakolosai 3:1-2 “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na
Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.”
5.
Tai hawali
kibudu
Ni muhimu
kufahamu kuwa sifa nyingine ya tai ni pamoja na kutokula kibudu tai hawali
wasichokiua wenyewe, siku zote wanakula nyama ya mawindo yao wenyewe, wanakula
nyama safi na mpya hivi ndivyo watu wakuu katika dunia wanavyopaswa kuwa,
Watu wakubwa
duniani hukaa na watu wenye mawazo mpana na wenye kufikiri na wenye uwezo wa
kuamua, watu hodari wasiokata tamaa, hawa ndio watu wanaoweza kuleta mabadiliko
makubwa Duniani, watu wenye uwezo wa kuleta badiliko unapowasikiliza au kukaa
nao karibu, watu wenye ushawishi
Kamwe
usipoteze muda na watu wanaopoteza muda
Kamwe
usipoteze muda na watu wenye kusengenya
Kamwe
usipoteze muda na watu wasio na imani
Kamwe
usipoteze muda na watu wenye kuzungumzia wengine
Walawi 6:9-13 “Haya, mwagize Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya sadaka ya
kuteketezwa ni hii; hiyo sadaka ya kuteketezwa itakuwa pale motoni juu ya
madhabahu usiku wote hata asubuhi; na huo moto wa madhabahu utawaka juu yake
usizimike. Naye kuhani atavaa nguo yake ya kitani, na suruali zake za kitani
atazivaa mwilini mwake; naye atayazoa majivu ambayo huo moto umeiteketezea
sadaka juu ya madhabahu, kisha atayaweka kando ya madhabahu. Kisha atayavua
mavazi yake, na kuvaa mavazi mengine, kisha atayachukua yale majivu kwenda nayo
nje ya marago hata mahali safi. Na huo moto ulio madhabahuni atautunza uwake daima
juu yake, usizimike; naye kuhani atateketeza kuni katika moto huo kila siku
asubuhi; naye ataipanga sadaka ya kuteketezwa juu yake, naye atayateketeza
mafuta ya sadaka za amani juu yake. Moto utatunzwa uwake juu ya madhabahu
daima; usizimike.”
Kamwe usipoteze
muda na watu wenye kupiga majungu na fitina
Kamwe
usipoteze muda na watu ambao kuanguka kwa wengine ndio furaha yao
Kamwe
usipoteze muda na watu wenye kuhukumu
Kamwe
usipoteze muda na watu wenye mitazamo hasi wenye kujihusisha na rushwa na uovu hivyo
ni vibudu, tafuta vya kwako mwenyewe mawindo yako mwenyewe.
Tai anayekula Mizoga!
Tai anayekula Mizoga!
Ni muhimu
kufahamu kuwa tai tunayemzungumzia hapa
mwenye sifa tulizozitaja anaitwa Eagle huyu hali mizoga na taia
anayetajwa katika Mathayo 24:28 huyu
ndiye taia anayekula mizoga huyu anaitwa VULTURE
§ Mathayo 24:28 “ Kwa kuwa popote
ulipo mzoga ndipo watakapokusanyika tai”
§ “Whenever
there is carcass, there the VULTURE will gather” NIV.
§ For
wheresoever' the carcase is there will
eagles be gathered together KJV
Tai
anayekula Mizoga haitwi “Eagle” anaitwa
“Vulture”
Huyu ni aina
nyingine ya tai ambaye hupatikana mashariki ya kati nyikanani na katika mbuga
za wanyama Afrika tai huyu ndiye anayekula mizoga kiingereza sahii anaitwa
VULTURE huyu ndiye ambaye Yesu anazungumza katika injili ya Mathayo
Tai wanauwezo wa kujitia nguvu mpya
6.
Zaburi 103:4-5 “ Akusamehe
maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,
Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema,
Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai;”
Isaya 40:31 “Bali wao
wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai;
watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”
Moja ya
tabia ya tai ya kushangaza sana ni uwezo wake wa kujitia nguvu kwa upya ukiacha
kuwa wanauwezo wa kuona mbali lakini wana maisha marefu inasemekana Tai
anapofikisha miaka 30 anakuwa anachakaa na manyoya yake yanakuwa yamezeeka
hivyo kuathiri uwezo wake wa kiutendaji, inapofikia hivyo tai hakati tamaa ya
kuishi badala yake hutafuta kilele kikubwa cha mlima na kutulia kwa miezi
mitano anagonga mdomo wake katika mawe ya miamba na kungoa ngozi ya juu,
hujinyonyoa manyoa nyake yote wakati huu ajajigomoa na kuanza kuwa na manyoya
mapya mdomo mpya na magamba mapya jambo hili humfanya tai awe na uwezo wa
kurejeza uhai wake kwa miaka mingine 30-40, Ndo maana biblia inasema ujana wako
utarejezwa kama tai
Watu wenye akili ni watu wanaoweza
kujitafakari na kuangalia yote waliyoyafanya katika maisha yao liwe jema au
baya linapokuwa baya unaachana nalo
wanatafuta nini lililo jema na lipi wanaweza kuliendeleza na jipya gani
wanaweza kuenda nalo, na kujifunza jambo jipya la kufanya siku hadi siku. 1Samuel 30:1-8 “Ikawa,
Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki
walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma
moto; nao wamewachukua mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo;
hawakuwaua wo wote, ila wakawachukua, wakaenda zao. Basi Daudi na watu wake
walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao,
waume kwa wake, wamechukuliwa mateka. Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye
wakainua sauti zao na kulia, hata walipokuwa hawana nguvu za kulia tena. Na hao
wake wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na
Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli. Naye Daudi akafadhaika sana; kwa
sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao
watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini
Daudi alijitia nguvu katika Bwana, Mungu wake. Kisha Daudi akamwambia
Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera.
Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko. Daudi akauliza kwa Bwana, akasema,
Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika
utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.”
Kamwe usikubali
kudumaaa
Usikubali
kubaki vilevile siku zote
7.
Tai wanatoa
mafunzo kwa vifaranga vyao
Kumbukumbu la torati 32:10-11 “Alimkuta katika nchi ya ukame, Na katika jangwa tupu
litishalo; Alimzunguka, akamtunza; Akamhifadhi kama mboni ya jicho; Mfano wa tai ataharikishaye kioto chake; Na
kupapatika juu ya makinda yake, Alikunjua mbawa zake, akawatwaa, Akawachukua
juu ya mbawa zake;”
Amini
usiamini tai wanaotoa mafunzo kwa vijana wao, tai wanafikiriwa kuwa ni ndege
katili sana wakati wa kutoa mafunzo na kama hujui makusudi yao unaweza
kukubaliana kuwa ni ndege wakatili, jambo moja la kushangaza kuhusu tai ni
uwezo wake wa kutoa mafunzo kwa vifaranga vyake, utafiti unaonyesha kuwa hakuna
aina ya ndege mwenye mvuto na mpole kama tai kwa watoto wake kushinda tai
Mama wa tai
anapogundua kuwa wakati umefika kwa vifaranga vyake kujifunza kuruka, anawabeba
vifaranga wake mgongoni na kupanua mbawa zake anaruka juu sana kisha anajiondoa
kutoka kifaranga chake na kukiachia kiangukekinapoanguka kinajifunza kuruka
akiona kinaogopa na kinataka kuanguka anakidaka na kukirejeza katika kiota
chake, atafanya hivyo mpaka kimejifunza kuruka.
Watu wakubwa
sana duniani sio mabosi, wakati wote wanawafanya wengine kukua katika jamii na
wanawapa changamoto lakini wanawasaidia kukua na kujiamini na kuendelea kuwapa
maelekezo wengine mpaka wameweza kufanya vilevile kama wao wafanyavyo.
Kumbukumbu 8:1-6 “Amri
hii ninayokuamuru leo mtaishika kuitenda, mpate kuishi na kuongezeka, na
kuingia katika nchi ile ambayo Bwana aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki.
Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii
arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako,
kwamba utashika amri zake, au sivyo. Akakutweza, akakuacha uone njaa,
akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate
kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila
litokalo katika kinywa cha Bwana. Mavazi yako hayakuchakaa, wala mguu wako
haukuvimba, miaka hiyo arobaini. Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile
baba amrudivyo mwanawe, ndivyo Bwana, Mungu wako, akurudivyo. Nawe uzishike
amri za Bwana, Mungu wako, upate kwenda katika njia zake, na kumcha.”
8.
Tai hutoa mafunzo kwa wengine
Amini
usiamini tai wanaotoa mafunzo kwa vijana wao, tai wanafikiriwa kuwa ni ndege
katili sana wakati wa kutoa mafunzo na kama hujui makusudi yao unaweza
kukubaliana kuwa ni ndege wakatili, jambo moja la kushangaza kuhusu tai ni
uwezo wake wa kutoa mafunzo kwa vifaranga vyake, utafiti unaonyesha kuwa hakuna
aina ya ndege mwenye mvuto na mpole kama tai kwa watoto wake kushinda tai
Mama wa tai
anapogundua kuwa wakati umefika kwa vifaranga vyake kujifunza kuruka, anawabeba
vifaranga wake mgongoni na kupanua mbawa zake anaruka juu sana kisha anajiondoa
kutoka kifaranga chake na kukiachia kiangukekinapoanguka kinajifunza kuruka
akiona kinaogopa na kinataka kuanguka anakidaka na kukirejeza katika kiota
chake, atafanya hivyo mpaka kimejifunza kuruka. “2Timotheo 2:2” Ebra 5:
11-14, Math 5:3-4; Ayub 5:11; Zab 91:14).
9. Tai huyatoa
maisha yake kwa ajili ya wengine Eagle do sacrifice
·
Tai anapotaka kuangua vifaranga vyake
·
Hujenga kiota cheke juu sana kwenye miti
mirefu mno
·
Kiota cha tai huwa na vipande vya miti
migumu
·
Kwaajili ya kuwahurumia vifaranga vyake
Tai hujinyofoa manyoya yake mwili mzima ili vifaranga vyake visipate maumivu
wakati huu tai huwa hali vizuri hufunga na kuatamia ili vifarabga vyake
visiumie
·
Ukomavu wa juu kabisa wa kiroho ni mtu
kujitoa kwaajili ya wengine
·
Ukomavu wetu wa juu sana Kiroho
utajulikana pale tunapokuwa tayari kuyatoa maisha yetu kwaajili ya wengine
·
Yuda - Mwanzo 44:1-34,"Akamwamuru yule msimamizi wa nyumba yake akisema, Jaza magunia ya watu hawa chakula kwa kadiri wawezavyo kuchukua, utie na fedha ya kila mtu kinywani mwa gunia lake. Na kikombe changu, kikombe kile cha fedha, ukitie kinywani mwa gunia la yule mdogo pamoja na fedha ya nafaka yake. Akafanya kama vile alivyomwambia Yusufu.Asubuhi kulipopambazuka, hao watu wakapewa ruhusa, wao na punda zao. Na walipotoka mjini, wala hawajaendelea sana, Yusufu akamwambia yule msimamizi wa nyumba yake, Ondoka, uwafuate watu hawa, nawe utakapowapata, waambie, Kwa nini mmelipa mabaya kwa mema? Je! Kikombe hiki, sicho anyweacho bwana wangu? Naye hufanya uaguzi kwa hicho. Mmefanya vibaya kwa kufanya hivi. Akawafuata, akawapata, na kuwaambia maneno hayo. Wakamwambia, Kwa nini bwana wangu anasema maneno kama haya? Hasha! Watumwa wako wasifanye hivi; tazama, hizo fedha mlizoziona kinywani mwa magunia yetu, tumekuletea tena kutoka nchi ya Kanaani. Tuwezeje sisi kuiba nyumbani mwa bwana wako fedha au dhahabu? Atakayeonekana kuwa nacho miongoni mwa watumwa wako, na afe, na sisi nasi tutakuwa watumwa wa bwana wangu. Akasema, Basi na iwe hivyo kama mlivyosema, Mtu atakayeonekana kuwa nacho atakuwa mtumwa wangu, na ninyi mtakuwa hamna hatia. Wakafanya haraka, wakashusha kila mtu gunia lake, na kufungua kila mtu gunia lake. Naye akatafuta, akaanza kwa mkubwa na kuisha kwa mdogo. Kikombe kikaonekana katika gunia la Benyamini. Wakararua nguo zao, wakaweka kila mtu mzigo wake juu ya punda wake, wakarudi mjini. Akaja Yuda na ndugu zake nyumbani kwa Yusufu, naye mwenyewe alikuwamo, nao wakamwangukia kifudifudi. Yusufu akawaambia, Ni tendo gani hili mlilolitenda? Hamkujua ya kwamba mtu kama mimi naweza kufanya uaguzi? Yuda akasema, Tumwambie nini bwana wangu? Tusemeje! Tujivutieje haki? Mungu ameona uovu wa watumwa wako. Tazama, sisi ni watumwa wa bwana wangu, sisi na yeye ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake. Akasema, Hasha! Nisifanye hivi; mtu ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake, ndiye atakayekuwa mtumwa wangu. Nanyi enendeni zenu kwa amani kwa baba yenu. Ndipo Yuda akamkaribia, akasema, Tafadhali, bwana wangu, mtumwa wako na aseme neno moja masikioni mwa bwana wangu, wala hasira yako isimwakie mtumwa wako, maana wewe u kama Farao. Wewe, bwana wangu, ulituuliza watumwa wako, ukisema, Je! Mnaye baba, au ndugu? Tukakuambia wewe, bwana wangu, Tunaye baba, naye ni mzee, na mwana wa uzee wake ni mdogo, na nduguye amekufa; amebaki yeye peke yake wa katika tumbo la mamaye, na baba yake anampenda. Ukatuambia watumwa wako, Mleteni kwangu, ili macho yangu yamwangalie. Tukakuambia, bwana wangu, Kijana hawezi kumwacha babaye, maana akimwacha babaye, babaye atakufa. Ukatuambia watumwa wako, Asiposhuka ndugu yenu mdogo pamoja nanyi, hamtaniona uso wangu tena Ikawa tulipokwenda kwa mtumwa wako, baba yangu, tukamwarifu maneno yako, bwana wangu. Kisha baba yetu akanena, Rudini huko, mkatununulie chakula kidogo. Tukasema, Hatuwezi kwenda; ndugu yetu mdogo akiwapo pamoja nasi, tutashuka, maana hatutaweza kuuona uso wa mtu huyo, ndugu yetu mdogo asipokuwa pamoja nasi. Mtumwa wako, baba yangu, akatuambia, Mnajua ya kuwa mke wangu alinizalia wana wawili;mmoja alitoka kwangu, nikasema, Bila shaka ameraruliwa, wala sikumwona tangu hapo. Na mkiniondolea huyu naye, na madhara yakimpata, mtashusha mvi zangu na msiba kaburini. Basi, nikienda kwa mtumwa wako, baba yangu, na huyu kijana hayupo pamoja nasi, iwapo roho yake imeshikamana na roho ya kijana; itakuwa atakapoona ya kwamba huyu kijana hayuko, atakufa; na watumwa wako watashusha mvi za mtumwa wako, baba yetu, kwa huzuni kaburini.Kwa maana mtumwa wako alijifanya mdhamini wa huyu kijana kwa baba yangu, nikisema, Nisipomrudisha kwako, nitakuwa na hatia kwa baba yangu sikuzote. Basi, sasa nakusihi, uniache mimi mtumwa wako nikae badala ya huyu kijana kuwa mtumwa wa bwana wangu; na huyu kijana umwache aende pamoja na nduguze. Kwa maana nitawezaje kumwendea baba yangu, na huyu kijana hayuko pamoja nami? Nisije nikayaona mabaya yatakayompata baba yangu.
·
Daudi - 2Samuel 18:31-33 "Na tazama, yule Mkushi akafika; Mkushi akasema, Nina habari kwa bwana wangu mfalme; kwa maana Bwana amekulipizia kisasi leo juu ya hao wote walioinuka kupigana nawe. Naye mfalme akamwambia yule Mkushi, Yule kijana, Absalomu, je! Yu salama? Yule Mkushi akajibu, Adui za bwana wangu mfalme, na wote wainukao ili kukudhuru, na wawe kama alivyo yule kijana. Naye mfalme akataabika sana, akapanda juu, akaingia kile chumba kilichokuwa juu ya lango, akalia; na katika kwenda kwake alisema hivi, Mwanangu Absalomu! Ee mwanangu! Mwanangu Absalomu! Laiti ningalikufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu! "
·
Yohana 18: 7-8 " . Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti. Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao."
·
1Yohana 4:10 “Hili
ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi,
akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu” Kuja kwa Yesu Kristo Duniani
ni matokeo ya upendo mkuu wa Mungu kwa mwanadamu, ni matokeo ya juu kabisa ya
upendo usioweza kupimika
·
Yohana 3:16 “Kwa
maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila
mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”
·
Yohana 15:13:- “Hakuna
aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki
zake”.
Ni Muhimu
kufahamu kuwa upendo unaotajwa hapa sio upendo wa kawaida ni upendo wa kimungu
ni upendo wenye huruma za kiungu sio upendo wa kibinadamu kwa kawaida katika
lugha ya kiyunani neno upendo lime gawanyika katika tafasiri kuu nne za upendo
ambazo ni Phileo, Storge, Eros, na Agape au agapan:- aina hizi za upendo
tunaweza kuzichambua kama ifuatavyo:- • PHILEO
aina hii ya upedno kwa kiingereza tunaiita “Companionable love”yaani ni upendo wa Kirafiki, Ni upendo
unaojengeka kutokana na kushirikiana kuzungumza kukubaliana kupeana
zawadi,kuendana na kadhalika huu ni upendo wa kirafiki • STORGE aina hii ya upendo kwa kiingereza tunaiita “Natural affection love” yaani ni upendo
unaotokana na kuweko kwa undugu wa damu, unampenda mtu kwa sababu ni baba, mama,
mwana, mjomba shangazi, dada, kaka na kadhalika katika mahusiano ya kindugu na
damu • EROS aina hii ya upendo kwa kiingereza tunaiita “Erotic love” yaani ni
upendo unaotokana na mvuto wa kimapenzi, ni upendo unaohusu jinsia tofauti na
yako, unampenda mtu kwa sababu ya muonekano wake , umbile lake na uzuri wake
hii husababishwa na mvuto wa kimapenzi, body morphology is concern Muonekana wa
mwili au mvuto unahusika na upendo huu ni wa kihisia. • AGAPE aina hii ya Upendo kwa kiingereza tunaiita “unconditional love” Yaani ni upendo
wenye kupitiliza mipaka ya kibinadamu, ni upendo ambao asili yake ni Mungu ni
upendo unaomtakia mema kila mmoja awe adui au ndugu upendo huunapita mipaka ya
kawaida ya kibinadamu, hauangalii hali ya hewa, unampenda Mungu au mtu bila
kutarajia kitu kutoka kwake, bila kujali mtu huyo ni mwema au mbaya, bila
kujali ni wakati mzuri au mbaya, bila kujali ni wakati wa matatizo au raha
upendo huu unabaki vilevile na haubadilishwi na matukio, Mungu anapoamuru
kupendana au kumpenda Yeye katika maandiko anamaanisha upendo huu wa Agape.
Upendo huu pia hujulikana kama Sacrificial love , upendo wenye kujitoa sadaka
kwaajili ya wengine, ni upendo unaojali kuwahudumia wengine zaidi ya sisi
wenyewe, Huu ndio upendo ulioamriwa katika 1Wakoritho 13 upendo wa kiungu.
1. Daktari mmoja
wa Uingereza aitwaye Will Pooley
alikuwa ni moja ya madaktari waliokuwa mstari wa mbele Nchini “Sierra Leone” huko walikuwa na wenzake
wengi wakipambana na wagonjwa wa EBOLA
na virusi vyake katika harakati hizo Madaktari wengi sana na Manesi wengi sana
wakiwemo wa Afrika Magharibi waliambukizwa virusi vya ebola wakati walipokuwa
wakiwauguza wagonjwa na wengi wao walikufa Ugonjwa utokanao na kirusi cha Ebola
ni ugonjwa hatari wenye uwezo wa kusababisha kifo kwa asilimia 90. Shirika la
afya duniani, WHO katikatovuti yake inasema kwa mara ya kwanza ulibainika mwaka
1976 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Sudan.
Chanzo cha kirusi hiki hadi sasa hakijulikani lakini popo aina ya
(Pteropodidae) wanaonekana kuwa wabebaji wa kirusi hicho, kwa mujibu wa
ushahidi uliopo sasa. Maambukizi hupatikana kwa kila aina ya majimaji
yanayotoka katika mwili wa binadamu ni ugonjwa hatari na unaoua kwa haraka na
hauna tiba Will Pooley alipoupata ugonjwa huu alirejeshwa katika ndege maalumu
na kuanza kutibiwa chini ya uangalizi maalumu huko uingereza Jambo la
kushangaza ni kuwa baada ya kupona kwa bahati tu Will Pooley alitangaza nia
yake ya kurudi tena Sierra Leone kusaidiana na wenzake kupambana na ugonjwa
huo. Mtu huyu aliwashangaza wengi sana na kuwaogopedha wengi sana akiwa amepona
kwa asilimia 100%alisema atarudi Africa kusaidia zaidi maana alizaliwa kwaajili
ya hayo, jambo hili lilimfanya aandikwe kama shujaa na mwanadamu mwenye uwezo
wa kujitoa kwa kiwango cha juu.
2. Maximilian Kolbe alikuwa ni Padre
aliyetokea Poland aliuawa kama mfungwa tarehe 14 August 14,1941, Jeshi la wa NAZI waligundua kuwa baadhi ya
wafungwa wamejaribu kutoroka na hivyo waliamua kuwaua wafungwa kadhaa,
walijaribu kuwaua kwa njia mbalimbali, na hivyo walichagua wafungwa 10 ili
wauawe na kifo chao kiliamuriwa kuwa kifo cha njaa, wafungwa waliamuriwa
kujitoa mmoja mmoja yeye mwenyewe na mfungwa wa kwanza kuchaguliwa alijulikana
kama Franciszek Gajowinczek mfungwa
huyu alipochaguliwa alilia kwa huzuni kubwa akimtaja mkewe, watoto wake na
familia yake na kusikitika kuwa hatowaona tena kutokana na swala hili
Maximillian alisimama na kusogea mbele na kuomba afe yeye kwa niaba ya
Franciszek ombi lake lilikubaliwa, wafungwa waliwekwa kizuizini kwa muda wa
siku kadhaa bila kula wengine walikunywa mikojo yao ili waweze kuishi,
Maximillian alikaa kwa wiki mbili bila kufa huku wengine wote wakiwa wamekufa,
walimchoma sindano ya kufa hakufa na hivyo waliamua kukata kichwa Pope John
Paul II alimtangaza kuwa Mtakatifu kutokana na moyo wake
3. Mifano hii
inatusaidia kujua kile ambacho Bwana wetu Yesu amekifanya Pale alipojibu kuwa
kwaajili ya haya Nalizaliwa alikuwa akimkumbusha Pilato kuwa yeye amekuja
kuwafia wanadamu, amekuja kuwaonyesha upendo wa Mungu jinsi ulivyo
Isaya 53:1-5 “Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” Huu ni upendo mkubwa sana Yesu alikufa kwaajili yetu, Hatuna budi kuhakikisha kuwa tunasimama upande wake siku zote za maisha yetu, tusihesabu damu yake ya thamani kuwa kitu cha hovyo tudumu katika wokovu na kuwa wavumilivu kwaajili ya Mungu wetu.”
Isaya 53:1-5 “Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” Huu ni upendo mkubwa sana Yesu alikufa kwaajili yetu, Hatuna budi kuhakikisha kuwa tunasimama upande wake siku zote za maisha yetu, tusihesabu damu yake ya thamani kuwa kitu cha hovyo tudumu katika wokovu na kuwa wavumilivu kwaajili ya Mungu wetu.”
Mukhtasari:
·
Tai ni wenye uwezo mkubwa wa kuona mbali.
·
Tai ni ndege wasioogopa Mawindo.
·
Tai ni Hodari hawaogopi Dhuruba.
·
Tai wanaruka juu sana.
·
Tai hawali kibudu
·
Tai wanauwezo wa kujitia nguvu mpya
·
Tai wanatoa mafunzo kwa vifaranga vyao
·
Tai hutoa mafunzo kwa wengine
·
Tai huyatoa maisha yake kwa ajili ya wengine
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima
0718990796