Ijumaa, 12 Februari 2021

Mungu yule ambaye mimi ni wake!

Matendo 27:23-25Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami, akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.”



Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kwamba ustawi wa nafsi zetu na usalama wa roho zetu ulinzi na muelekeo wa maisha yetu unategemeana sana na Mungu yule Tunayemuabudu!  Hili ninjambo la msingi sana, tunaweza kuwa na mtazamo tofauti, tabia tofauti na mwenendo tofauti, na tukawa tunajiamini sana au tukawa na hofu lakini kwa vyovyote vile kila kitu na kila jambo  matumaini yetu na kujiamini kwetu kwenye kupita kawaida kunategemeana sana na Mungu tunayemuabudu, au kwa lugha nyingine uhusiano wetu na Mungu tunayemuabudu! Angalia maandiko yafuatayo kisha kuna kitu utagundua!

1.      Mwanzo 15:1 ” Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.”

2.      Mwanzo 31:24 “Mungu akamjia Labani, Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.

3.      Matendo 8:9-10 “Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze, kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu.”           

4.      Matendo 23:11 “Usiku ule Bwana akasimama karibu naye, akasema, Uwe na moyo mkuu; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako.

5.      Zaburi 27:1-4 “Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?  Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini. Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.

Maandiko yote hapo Juu pamoja na andiko la msingi yanatufundisha kwamba watakatifu waliotutangulia walikuwa na ujasiri mkubwa sana, walijiamini, walithibitishiwa usalama wao, kwa miili yao nafsi zao, ulinzi na kujaliwa kwa sababu walikuwa na uhusiano wa karibu na Mungu wa kweli aliye hai na mwenye uwezo na nguvu za kuwalinda kuwatetea kuwabariki na kutangaza hatima yao, hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba ustawi wetu katika Nyanja zote za maisha yetu unategemeana sana na Mungu tunayemuabudu!. Paulo mtume alipookuwa safarini Rumi safari ambayo ilikuwa imejawa na misukosuko mingi  na hatari ya kifo, Mungu ambaye Paulo anamuabudu na kumtumikia, Mungu wake alimtuma malaika wake na malaika yule alimthibitishia usalama Paulo pamoja na watu wote aliokuwa nao chomboni ona hii Matendo 27:23-25Kwa maana usiku huu wa leo MALAIKA WA MUNGU YULE AMBAYE MIMI NI WAKE, NAYE NDIYE NIMWABUDUYE, alisimama karibu nami, akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.” Unaona Mtume Paulo ana uhakika wa kile alichoelezwa na malaika wa MUNGU YULE AMBAYE YEYE NI WAKE NAYE NDIYE AMUABUDIYE kwa nini Paulo ansema haya kwa watu wale? Watu wale walikuwa hawamjui Mungu ambaye Paulo  anamuabudu na kumtumikia, walikuwa wanaabudu miungu mingine, kwa hiyo hofu ya kifo na mauti, kuhisi nuksi mikosi na balaa kuliwajaa kwa sababu hawakuwa na ufahamu kwa habari ya Mungu aliye hai ambaye Paulo anamuita Mungu wake, na tena Mungu ambaye yeye anamuabudu na kumtumikia, Mungu huyu sio tu aliyatunza maisha ya Paulo lakini alimpa na maisha ya watu wote waliokuwa pamoja naye na hivyo kwaajili ya Paulo nao walikuwa salama kwa sababu ya uhusiano uliokuwepo kati ya Paulo na Mungu huyo!

Hii maana yake ni nini ? maana yake ni lazima kila mmoja wetu awe na uhakika na Mungu yule anayemuabudu, Maandiko yanakubali kuwa kuna miungu Mingi, Na Mungu mwenyewe amewaonya watu wake kutokuwa na Mungu mwingine zaidi yake ona Kutoka 20:2-3 “Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi.” Unaona kama maandiko yanakiri kuweko kwa miungu mingi,  basi kuna miungu mingi, lakini anayepaswa kuabudiwa ni Mungu mmoja wa kweli, kama mwanadamu awaye yote atakuwa na uhusiano zege yaani uhusiano mzuri na mwema na Mungu huyu wa kweli atakuwa salama katika ulimwengu huu na ule ujao

Je ni kweli Mungu yupo?

Ni muhimu kufahamu kuwa Maandiko hususani neno la Mungu halifanyi kazi ya kuthibitisha kuwa Mungu yupo au hapana, Neno la Mungu linatuhakikishia moja kwa moja kuwa Mungu yupo na neno la Mungu linasema mtu anayewaza kuwa hakuna Mungu ni mpumbavu Zaburi 14:1-2 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.Hakuna jaribio lolote katika maandiko linalojaribu kuithibitisha kuwa Mungu yupo, kila amahali neno la Mungu limethibitisha kuwa Mungu anajulikana labda mtu awaze upumbavu tu moyoni mwake Zaburi 53:1-2 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.

Sasa basi kama Neno la Mungu linaonyesha wazi kuwa asemaye au awazaye moyoni kuwa hakuna Mungu ni mpumbavu tunawezaje kujua sasa ya kuwa Mungu yupo? Neno la Mungu linaweza kutusaidia namna ya kujua uwepo wa Mungu na namna ya kutthibitishia watu kwamba yeye yupo

1.      Kupitia uumbaji

Moja ya vitu ambavyo ninashangaza sana wanadamu hata wale walio wabishi kuhusu uwepo wa Mungu ni uumbaji, uumbaji ni uthibitisho wa wazi kuwa namna ulivyoumbwa na namna ulivyopangiliwa na ustadi wake ni wazi kuwa uumbaji unatangaza uweza nguvu na utukufu wa Mungu  maandiko yanasema Mbingu yaani solar system inatangaza utukufu wa Mungu ona Zaburi 19:1-6 “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake. Mchana husemezana na mchana, Usiku hutolea usiku maarifa. Hakuna lugha wala maneno, Sauti yao haisikilikani. Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu. Katika hizo ameliwekea jua hema, Kama bwana arusi akitoka chumbani mwake, Lafurahi kama mtu aliye hodari Kwenda mbio katika njia yake.Kutoka kwake lautoka mwisho wa mbingu, Na kuzunguka kwake hata miisho yake, Wala kwa hari yake Hakuna kitu kilichositirika.” Mwandishi anataka kutuelezea wazi kuwa mfumo wa jua na mbingu na anga kama ukiuchunguza unaonyesha utukufu wa Mungu, yaani kama vile tunavyoweza kuona na kushangaa vitu vilivyotengenezwa na wanadamu, na tukavihusudu ni wazi kabisa kuwa tunaweza kuhusudu kazi na utendaji wa Mungu wetu namna alivyoumba ulimwengu na hasa maswala ya anga

 


Uumbaji ni wenye kushangaza sana anga pekee limewafanya watafiti kujikuta wakishangaa kwa miaka mingi, Mungu ameweka utaratibu wa ajabu sana mawinguni ambao unawapa wanasayansi wakati mzuri wa kufanya utafiti wa again kujifunza na kujua mwenendo wa kazi na utendaji wa Mungu ambao ni dhahiri kila mtu anakubali kuwa ahuwezi kutokea kwa bahati mbaya tu!, ni wazi kuwa kadiri wanasayansi wanavyofanya uchunguzi wa kina wanabaini na kukubaliana na maneno ya mwandishi wa Zaburi 19:1 kwamba ni kweli Mbingu zinahubiri utukufu wa Mungu!

Watafiti wa kisayansi wa chuo cha Harvard  wanasema mpaka sasa wamegundua na kukubali kuwa kuna zaidi ya Galaxy yaani mfumo wa nyota au majua yaliyoko katika mpangilio ambao unaonekana kama vumbi wa zaidi ya miliono 500 milions

Jua ambalo ni nyota iliyoko karibu na Dunia ina kipenyo kinachokadiriwa kuwa na kilomita 1,392,000  na jua hilo linazunguikwa na sayari zilizothibitishwa zipatazo nane na ya tisa ambayo iko mbali sana na mwenendo wake bado unawachanganya watafiti kuibainisha kuwa ni sayari sayari hizo ni pamoja na

 

Jina la sayari

Umbali kutoka juani

Muda wa kuzunguka jua Revolution

Muda wa siku Rotation

Number of Moons

Mercury


57.9 million km

87.96 siku za dunia

58.7 siku za dunia

0

Venus


108.2 million km

224.68 siku za dunia

243 siku za dunia

0

Earth


149.6 million km

365.26 siku

24 hours

1

Mars


227.9 million km

686.98 siku za dunia

24.6 masaa ya dunia
=1.026 siku ya dunia

2

Jupiter


778.3 million km

11.862 siku za dunia

9.84 saa za dunia

67 (18 named plus many smaller ones)

Saturn


1,427.0 million km

29.456 siku za dunia

10.2 saa za dunia

62 (30 unnamed)

Uranus


2,871.0 million km

84.07 siku za dunia

17.9 saa za dunia

27 (6 unnamed)

Neptune


4,497.1 million km

164.81 siku za dunia

19.1 saa za dunia

13

Pluto 


5,913 million km

247.7 miaka ya dunia

6.39 saa za dunia

4

 

Unaweza kuona itakuwa ni ujinga kama sio upumbavu mkubwa kudhani ya kuwa mfumo huu umejiumba wenyewe  Na ndio maana neno la Mungu linaanza kwa kusema wazi kuwa Hapo mwanzo Mungu aliziumba Mbingu na nchi ona Mwanzo 1:1Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.Hii maana yake ni nini lazima kila mwadamu afikie kwenye hitimisho ya kuwa yuko Mungu aliyeziumba mbingu na nchi, haiwezekani kwa namna yoyote ile kwamba itokee kwamba ulimwengu ulijiumba wenyewe baada ya miaka milioni nyingi sana kama watu Fulani wanavyodhani

Kwa hiyo unaweza kuwaza pale unaposema namwamini Mungu baba mwenyezi muumba wa mbingu na inchi unaweza kupata picha ya Mungu yule tunayemuabudu na kumtumikia na kama una uhusiano naye Mungu yule ambaye mimi/wewe ni wake “THE GOD WHOM I/YOU BELONG TO HIM” kwa hiyo tunaweza kutambua kuwa Mungu yuko kwa kupitia uumbaji wake

2.      Kupitia Historia

Matukio mengo ya kihistoria duniani ni ushahidi ya kuwa nyuma ya kila historia ziko nguvu za Mungu aliyehai, adhai historia yote ya kibiblia imeandikwa kwa ajili ya kufunua nguvu na uweza wa Mungu wa kweli, Mungu wa kweli amejifunua kwetu kupitria taifa la Israel kwa hiyo ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa uwepo wa taifa hili ni ushahidi wa uwepo wa Mungu, kutoka Israel kanisa lilizaliwa na neno la Mungu lilienea duniani kote na ndio maana katika namna yenye kushangaza shetani amewahi kuwashawishi mataifa kadhaa kutaka kujaribu kuiangamiza Israel au kuifuta Israel katika ramani ya dunia, lakini mara kadhaa mataifa hayo yameshuhudia kushindwa vibaya Israel ni kijiti inachowaka moto lakini hakiteketei ona Kutoka 3:2-3 “Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.” Maono haya kitaalamu yalikuwa ni picha ya kinabii pia ya hali ya Israel ambayo inapitia matesio ya aina mbalimbali lakini haiwezi kuteketezwa kwa sababu kile kinazozaniwa kuwa moto, kibinadamu ni kwa sababu Israel imefunikwa na utukufu wa  Mungu;- tuangalie kwa ufupi historia fupi ya vita mbalimbali za anga za Israel ambazo walishinda kwa sababu ya uwepo na ulinzi wa Mungu Mungu amewafanya Israel kuwa hodari kweli kweli unaweza kuona data hizo kutoka (www.israelairforec.org).

*      1948 – wayahudi walipopata uhuru wakiwa kiasi cha wayahudi laki sita hivi kuhesabu wanawake na watoto Waarabu wakiwa milion 80 walikusudia kuwa futilia mbali lakini kwa uweza wa ajabu Israel Iliwapiga vibaya waarabu na kufanikiwa kupanua mipaka yao kutoka Tell Avivi Jaffa mpaka ukanda wa gaza, milima ya Golan, na kuuteka mji wa Yerusalem

*      1950 – Wafaransa walikuwa ndio wafadhili wakubwa wa kuuza ndege za kivita kwa Israel lakini katika vita ya Six days War Israel walionyesha kipigo kikali sana kwa maadui ambacho wafaransa walisema kipigo hicho hakiwezi kusababishwa na ndege zao kwa hivyo uhusiano na Israel kijeshi ulisimama kwani Israel walikuwa wakiziboresha ndege hizo na zikatoa kichapo kikali

*      June 5 1967 – Israel kwa dakika 3 tu walizipiga ndege za maadui 451 zilizokuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kuifuta Israel ndege hizo mpya zilizonunuliwa na wamisri na nyingine za Jordani na Syria  zilitandikwa vibaya na hivyo kupelekea Misri na Jordani kuweka mkataba wa kudumu wa amani na Israel kuwa hawatapigana tena milele, mkataba huu uliwafanya Israel kuipa Misri Jangwa la mlima Sinai, kwa masharti kuwa hawatapigana milele

*      1969-1970 – Ndege 111 za maadui ziliwekwa chini pamoja na msaada wa warusi katika vita hiyo waarabu waliaibika

*      Jeshi la anga la Israel limefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na katika operation mbalimbali waliweza kuwalenga viongozi wa kigaidi wa palestina kwa vipimo vilivyoweza kuwapata na kuwaua mmoja mmoja viongozi hao ni pamoja na Abu ali Mustafa, Ahmed Yasini na Abed al azizi Rant iss aliyeuawa punde akitokea msikitini wakati wa ibada ya ijumaa

*      1976 walifanikiwa kuokoa  wayahudi kadhaa waliokuwa wakitishiwa kuuawa na Iddi amini dikteta aliyetawala Uganda katika operation iliyoitwa operation Entebe

*      1991 – Jeshi la anga la Israel lilifanikiwa kuwaokoa wayahudi wenye asili ya kiafrika huko Ethiopia wanaoshukiwa kuwa ni watoto wa mfalme suleimani  Katika operation iliyoitwa operation Solomon

Hali hiyo inadhihirisha wazi kuwa Mungu yuko nyuma ya mambo, Mungu amewahi kuwapigania Israel katika vita mbalimbali kwa miujiza mikubwa sana, hii yote I nawatokea kwa sababu wanamuamini Mungu aliye hai, aidha unaweza kusoma miujiza 17 ambayo Mungu amewafanyia jeshi la ulinzi la Israel katika https://www.jewishvirtuallibrary.org/  Mungu aidha anahusika pia katika kazi ya kuwekaau kuinua viongozi na kuwashusha maandiko yana ushahidi kuwa hili ni swala pakee ambalo linafanywa na Mungu nyuma ya kura na matakwa ya kawaida ya kibinadamu, Mungu anafanya kazi nyuma ya historia, viongozi wa kisiasa na taasisi zozote duniani wanaonywa kuwa na unyenyekevu na utambuzi ulio wazi kuwa Mungu yuko nyuma ya uwepo wao au kutokuwepo kwao ona  Zaburi ya 75:5-7 “Msiiinue pembe yenu juu, Wala msinene kwa shingo ya kiburi. Maana siko mashariki wala magharibi, Wala nyikani itokako heshima. Bali Mungu ndiye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu.”

Daniel 2:20-22” Danieli akajibu, akasema, Na lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake. Yeye hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa; yeye hufunua mambo ya fumbo na ya siri; huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake.

Daniel 5:18-21 “Kwa habari zako, Ee mfalme, Mungu Aliye juu alimpa Nebukadreza, baba yako, ufalme, na ukuu, na fahari, na utukufu; na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha. Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake. Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng'ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote. Mungu yuko nyuma ya kila Historia, Historia yoyote ile duniani ni Historia ya Mungu.

3.      Tunaweza kumjua Mungu kupitia jina lake!

 

Ni vigumu sana kumuelezea Mungu na tukamuelewa vema bila kwanza kujua kuwa njia pakee ya kumjua Mungu ni kwa njia ya imani Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” Ni ili uweze kuwa na imani maandiko yanatuambia kuwa imani chanzo chake ni kusikia yaani lazima usikilize mafundisho na sio kila mafundisho yanaweza kuwa sahihi bali mafundisho kuhusu Kristo kwa sababu yeye pekee ndiye anayeweza kumfunua Mungu kwetu ona Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Kwa hiyo ni neno la Mungu pekee tena likifundishwa kwa usahihi linaloweza kutusaidia kumfahamu Mungu na kumuamini, Mungu anazo sifa nyingi sana na amajifunua kwa wanadamu kwa namna mbalimbali, na wanadamu walimpa Mungu majina kutokana na ufunuo ambao kwa huo Mungu alijifunua kwao Westminster Catechism inamuelezea Mungu kuwa ni Roho, Aelezeki, habadiliki, anajua yote, ana hekima yote, ana nguvu zote, ni mtakatifu, ni mwema, ni mwenye haki, ni mkweli na kadhalika. Maandiko yanamfunua Mungu kwa majina mbalimbali kutokana na aina ya jambo au kitu au tukio ambalo Mungu alilifanya kwa mwanadamu au wanadamu Fulani kwa wakati huo, nay eye mwenyewe amejidhihirisha kwa jina YAHWH katika maandiko jina ambalo hata Ibrahimu na Isaka na yakobo hawakuwahi kulijua wala kulipata ona

Kutoka 6:2-3 “Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.” Mungu anajifunua kwa mara ya kwanza kwa jina hili kwa Musa kwa sababu hapa alishuka kwa kazi maalumu ya UKOMBOZI hivyo jina hili linadhihirisha kuwa yeye ni Mwokozi na hapa alikuwa ameshuka kuwasaidia mwana wa Israel kukombolewa kutoka katika hali ya utumwa huko Misri Kutoka 3:6-9 “Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu. BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.Ni wazi kuwa Musa alitamani sana kumjua Mungu kwa kina na mapana na Marefu hata pamoja na ufunuo huu aliomba amjue Mungu kwa undani zaidi lakini Mungu alimtangazia jina pana zaidi ona Kutoka 34:5-7” BWANA akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la BWANA. BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.kwa msingi huo ni wazi kuwa katika agano la kale jina la Mungu lilifichwa na ilikuwa ngumu sana kwao kulitaja jina la Mungu au kulitumia bure au kukufuru kwa jina hilo wayahudi waliliogopa na jina hili lilifichwa kwa kuwa Mungu alikuwa anajifunua kwao kidogo kidogo Kutoka 20:7 “Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.

Walawi 18:21 “Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapitisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA.” Walawi 24:16 “Na yeye atakayelikufuru jina la BWANA hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzalia, hapo atakapolikufuru jina la BWANA atauawa

Amri ya kuhakikisha kuwa jina la Mungu linatukuzwa sio wayahudi pekee walioamriwa bali hata wakati wa agano jipya katika mafundisho yake Yesu anataka jina hilo litukuzwe Mathayo 6:9 “Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,”

Jina la Mungu lina uwezo wa kulinda watu wake lima uwezo wa kuinua, lina uwezo wa kubariki Zaburi 20:1-6 “Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue. Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote. Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. Bwana akutimizie matakwa yako yote. Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi wake; Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu.Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu.” Na kwaajili ya jina lake hawezi kuwatupa watu wake 1Samuel 12:21-22 “Wala msigeuke upande, maana, kufuata vitu vya ubatili, visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana Bwana hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza Bwana kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe.”  Kwa msingi huu tunaweza kuona umuhimu wa jina la Bwana Mungu wetu na zaidi ya yote unaweza matumizi ya jina lake kwamba ni lenye nguvu kubwa sana na msaada mkubwa kwa maisha yetu, Maandiko yanaionyesha jinsi watu walibyimuita Mungu majina mbalimbali kwa sababu ya ufunuo aliojifunua kwa watu wake

a.      Elohim – Ni jina ambalo watu walimpa Mungu wakimtambua kama Mungu mwenyezi muumba wa mbingu na ardhi ni jina la Mungu muumba jina hili linatumika kwa wingi likionyesha kuwa Bwana Mungu yu katika wingi na huu ni ufunuo kuhusu utatu wa Mungu elohimu inatumika katika maeneo kadhaa yafuatayo mfano Mwanzo 1:26 “ Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Na limetumika pia katika eneo linguine Mwanzo 11:6-7. “BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao

b.      Yehovah – Ni jina ambalo Mungu mwenyewe alijitambulisha kwa Musa alipokuwa ameshuka katika uwepo maalumu ili kuwasaidia wana wa Israel kutoka utumwani,ukiacha kuwa ni jina la ukombozi pia linaonyesha kuwa ni Mungu ashikaye maagano hasa kwa sababu ya utambulisho wake kama Mungu wa Ibrahimu, Isaka na yakobo, jina hili pia lina maana ya aliyekuwako, aliyeko na atatakayekuwako au niko ambaye niko kuonyesha umilelel wake Kutoka 6:2-3 “Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.” Jina hili Yehovah hata hivyo linasimamam na uaminifu au utendaji wa Mungu katika kutoa neema na msaada kwenye eneo Fulani la maisha pale Mungu anapoleta msaada kwa hivyo lilikuwa ni jina lisiloweza kusimama lenyewe bali lilionyesha ukombozi katika eneo ambalo Mungu anataka kukusaidia au alikusaidia

c.       Yehovah Rapha – Ni jina linalotumika Pale Mungu anapojifunua kwetu kama Mungu mponyaji Kutoka 15:26 “akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.

d.      Yehovah Nissi – Ni jina linalohusiana na uwezo wake wa kutupigania vitani, tunapokabiliwa na maadui au lolote lenye kuzia makusudi ya Mungu kwetu Mungu kama Yehovah Nissi ataingilia kati na kutupigania kwa namna ya kipekee, yeye ameahidi kutupigania milele, awaye yote atakayejifabya adui kwetu Mungu atakuwa adui kwake na atatusaidia katika vita maana yeye ni Bwan wa vita ona Kutoka 17:8-16 “Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu. Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu. Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi; akasema, BWANA ameapa; BWANA atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.

e.      Yehovah Shalom – Ni jina la Mungu lenye uhusiano na kujali kwa mungu na namna Mungu anavyotoa ustawi wa mwanadamu, ni Mungu anapojihusisha na kutupa amani Waamuzi 6:24 “Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.”

f.        Yehovah Ra’ah – Ni jina la Mungu anapojihusisha na kuyalinda maisha yetu, na kujihusisha na utoshelevu wetu Zaburi 23:1 “Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.”

g.      Yehovah tsidkenu – Jina linalotumika pale watu wanapotuhukumu na kutuona kama wenye hatia kwa sababu kadhaa au pale dhamiri zetu zinapohitaji kutiwa moyo kutoka katika hatia Mungu hufanyika kuwa haki yetu Yeremia 23:6 “Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.

h.      Yehovah Yire – Ni jina la Mungu anapojidhihirisha kama Mungu ambaye anakutana na mahitaji yetu Mwanzo 22:14 “Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.”

i.        Yehovah Shammah – Ni jina la Mungu linalodhihirisha uwepo wake BWANA YUPO HAPA Ezekiel 48:35 “Kuuzunguka ni mianzi kumi na nane elfu; na jina la mji huo tangu siku hiyo litakuwa hili, Bwana yupo hapa.”

Ni muhimu kufahamu kuwa pia jina El ambalo pia hutumika kwa utukufu wa Mungu pia ni jina lisiloweza kusimama lenyewe El ni Mungu lakini hutumika na muunganiko wa maneno mengina katika kulikamilisha kama ilivyo kwa jina lile Yehovah

j.        El-Elyon – Mungu aliye juu sana Mwanzo 14:18-20 18. “Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.”

k.      El-Shaddai – Mungu muweza yote mwenye kutekeleza mahitaji ya watu wake Kutoka 6:6-7 “Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa; nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri.        

l.        El-Olam – Mungu wa Milele Mwanzo 21:33 “Ibrahimu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la BWANA Mungu wa milele.” Aidha majina mengine ya Mungu ni pamoja na

m.    Adonai – maana yake Bwana au mttawala Kutoka 23:17 “Mara tatu katika mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele ya BWANA MUNGU.”

n.      Baba – Abba Mwanzilishi wa kila kitu Muumba au sababu ya kuwepo kwetu Matendo 17:28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake. Japo hii haituhakikishii wokovu bila kufuata kanuni ya kumuamini Yohana 1:12-13 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.”

SIFA ZA MUNGU

1.      Mungu anatajwa katika maandiko kuwa ni roho

Yohana 4:24 “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Tunaposema kuwa Mungu ni roho maana yake ni kuwa Mungu Baba hana mwili wa kibinadamu, Lakini mwana wa Mungu Yesu Kristo alikuja Duniani akiwa katika mwili ona Yohana 1:1-2, 14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.Kutokana na tendo hiliLa Mungu mwana kuwa na mwili wa kibinadamu Yeye amejulikana kama Emmanuel yaani Mungu pamoja nasi Mathayo 1:23 “Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi. “          

Mungu anapopewa sifa za kibinadamu hutumika lugha inayoitwa Anthromorphism – ili kusaidia kuleta uelewa kwa wanadamu, kwa msingi huo Biblia inatoa aina Fulani ya matamshi yenye kuashiria au kumfananisha Mungu na utendaji wa kibinadamu!

Mfano Isaya 59:1-“Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;” hapo Munu anatajwa kama ana mkono na ana sikio

2Nyakati 16:9 “Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.” Na pia Kumbukumbu 33:27 “Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza.” Lugha hizi zote ni lufgha zenye kumuelezea Mungu katika namna ya kibinadamu ili kutusaidia kumuelewa Lakini Mungu ni Roho na si mwanadamu!

2.      Mungu hana mipaka “infinite” no limitation

Ni mungu ambaye yuko mahali kote kwa wakati mmoja kwa msingi huo hawezi kutenganishwa na umbali au mahali 1Wafalme 8:27 “Lakini Mungu je? Atakaa kweli kweli juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga!                 Lakini neno hilo pia linatumika kumuelezea Mungu kama Mungu wa milele Muda hauna uwezo wa kumfunga yeye yuko tangu milele na milele ona Kutoka 15:18 “BWANA atatawala milele na milele.” Kumbukumbu 33:27 “Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza.” Zaburi 90:2 “Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.

3.      Mungu ni mwema

-          Ni mwenye upendo na huruma isiyoweza kuelezeka Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”.     

-          Zaburi 69:16 Ee “Bwana, unijibu, maana fadhili zako ni njema, Kwa kadiri ya rehema zako unielekee”.

-          Warumi 8:38-39 “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,  wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

4.      Mungu ni Mtakatifu!

-          Sifa ya utakatifu ni suifa ya Mungu pekee, hakuna mwanadamu mtakatifu wala mkamilifu wanadamu wote wana mapungufu Muhubiri 7:20 “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.”

-          Hakuna mwanadamu mwenye haki hata mmoja mbele za Mungu mpaka kwa neema yake tu ona Warumi 3:10-12, 23-24 “kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja. 23. kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24. wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;” Ni Bwana Mungu wetu tunayemuabudu aliye mtakatiu sana ona Isaya 6:1-4 “Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu. Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka. Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake. Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi.  Ufunuo 15:4 “Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.

-          Maandiko yanatoa wito kwa watu wote kuwa watakatifu kama Baba Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;  1Petro 1:15-16 “bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.”

5.      Mungu ni Mungu mwenye haki (Righteous and Just)

-          Kutokana na haki yake hataruhusu wadhalimu kuingia katika ufalme wake 1Wakoritho 6:9-10 9. “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. 

6.      Mungu ni mkweli na Muaminifu

-          Isaya 25:1 “Ee Bwana, wewe u Mungu wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako; Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.”

-          Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.”

-          Warumi 3:4 “Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu”.

-          Ahadi zake zote ni ndio na kweli Waebrania 10:23 “Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu;”

7.      Mungu ni mtoaji (He is a giving God)

-          Mungu ametupa kila kitu, kila kitu duniani ni chetu, Mwanzo 1:28-31 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo. Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.

-          Ametupa maandiko 2Timotheo 3:16. “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;”

-          Ametupa mwana wake wa pekee Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Ona pia Warumi 8:32”Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?

-          Anatupa Roho wake Mtakatifu Luka 11:13 “Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?    

-          Nguvu za kupata utajiri Kumbukumbu 8:18  Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo”-

-          Anatoa neema kwa wanyenyekevu 1Petro 5:5 “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”      

-          Hutupa Hekima kama tukihitaji Daniel 2:23 “Nakushukuru, nakuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu, uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliyotaka kwako; maana umetujulisha neno lile la mfalme. “

-          Mungu ni mkuu

a.      Anajua yote Omniscient – Warumi 16:27 “        Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amina. 1Samuel 2:3 Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.”

b.      Yu mahali kote Omnipresent – Zaburi 139:7-12 “Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?  Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari; Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika. Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa. “

Yeremia 23:24“Je, mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema Bwana. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema Bwana.”              

c.       Mungu ni mwenye nguvu zote Omnipotent – all powerful     

o   Nguvu za uumbaji Power of Creation Mwanzo 1:1 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.”  Wakolosai 1:16-17 “Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye”.

o   Ana nguvu za kuokoa - Isaya 50:2-3 “ Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu. Mimi nazivika mbingu weusi, nami nafanya nguo ya magunia kuwa kifuniko chao.” Mungu ni mwenye uwezo wa kuokoa na ni mwenye uwezo  wa kutukomboa, anasema katika Isaya kuwa ana uwezo wa kuikemea hata bahari  jambo ambalo liliwatishia sana wanafunzi wa Yesu waliokuwa wanalijua andiko hili vema na kisha Masihi akaikemea bahari mbele yao nayo ikatii ona – Marko 4:39-41 ”Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu. Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado? Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?”

o   Hakuna jambo lolote lililo gumu la Kumshinda yeye Yeremia 32:17 “Aa! Bwana MUNGU, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza;”

d.      Mungu ni wa milele

o   Amekuweko tokea enzi na enzi ona Zaburi 90:1-2 “Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi.Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.”

o   Yeye ni Mwanzo na mwisho Alfa na omega Ufunuo 22:13 ” Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.”

o   Yeye mwenyewe anasema kabla yake na baada yake hakuna mwingine ona Isaya 43:10-11 ”Ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. Mimi, naam, mimi, ni Bwana, zaidi yangu mimi hapana mwokozi.”

e.      Mungu hana kigeugeu

o   Waebrania 13:8 “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.”

o   Yeye sio kama kivuli kinageuka geuka Yakobo 1:17 “ Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. “

8.      Mungu ni Mkamilifu!

Tuwapo duniani kama wanadamu na kutokana na hitilafu ya kuwepo kwa dhambi Duniani kumekuwepo na mapungufu mengi sana wakati mwingine tunaweza kufikiri kuwa labda huenda muumba amekosea au kuna namna anakosa ukamilifu, Lakini sivyo maandiko yanavyotusimulia kuhusu Mungu, Mungu ni mkamilifu katika kazi zake zote na hakuna lolote analoweza kukosea au kujuata, wala hakuna kutokukamilika kokote ambako amekuficha ni mkamilifu katika sifa zako zote

-          Amekamilika katika maarifa na ujuzi wake wote ona Ayubu 37:16 “Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa, Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa?”

-          Hakuna lolote asilolijua ama linaloweza kufichika kwake lolote tulifanyalo hata kwa siri sana anajua yote na anakumbuka vema mno anajua mpaka mawazo yetu na Mapenzi yake ni kamili Warumi 12:2Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

-          Sheria yake pia ni kamilifu haina mapungufu Zaburi 19:7 “Sheria ya Bwana ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia mjinga hekima.

-          Njia zake ni kamilifu Zaburi 18:30 “               Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya Bwana imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia.”

-          Kazi zake ni kamilifu Kumbukumbu 32:4 Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.        

-          Neno Ukamilifu “Perfect katika Kiebrania linatumika neno “TAMIYM” Ambalo maana yake isiyolaumika , isiyo na lawama without Blemish  Katika kiyunani ni “TELIOS”  maana yake Kamilifu sawa na Sadaka ya mnyama ambayo Mungu aliagiza itolewe katika Walawi 23:17-18 17.” Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa BWANA. Nanyi, pamoja na hiyo mikate, mtasongeza wana-kondoo saba, walio wakamilifu, wa mwaka wa kwanza, na ng'ombe mume mmoja, na kondoo waume wawili; watakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA, pamoja na sadaka yao ya unga, na sadaka zao za kinywaji, sadaka ya harufu ya kupendeza iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.”             

Faida za Kumjua Mungu!

Kwa nini tunajifunza kuhusu Mungu? Kuna faida gani ya kujifunza kuhusu Mungu, Nguvu zake na uwezo wake? Ayubu 22:21 “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.” Tunapopata nafasi ya kumtambua Mungu inakuwa rahisi kwetu kustawisha uhusiano wetu na Mungu jambo ambalo litatufanya tuwe na uwezo wa kutambua uwepo wake, kumuheshimu na kumuabudu na kujenga uhusiano mkubwa sana na yeye! Paulo Mtume alikuwa na uhusiano mkubwa sana na Mungu jambo lililopelekea awe na uwezo wa kupata taarifa za usalama wake kutoka kwa Malaika wa Mungu, huku akizungumza wazi kwa wapagani, kuwa mungu huyo ni wake na ndiye anayemtumikia Matendo 27:23-25Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami, akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.”

1.      Kumjua Mungu na kumtumikia kunatupa imani thabiti isiyo na shaka juu ya uwezo wake Daniel 3:16 -18 “Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.

2.      Kumjua Mungu na kumtumikia yeye kunatupa tofauti kati yetu na wapagani au watu wasiomjua Mungu Zaburi 20:7-8 “Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu. Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.” Zaburi 46:1-2 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.”

3.      Uhusiano wetu na Mungu utaimarika atakuwa Mungu wetu na tutakuwa watu wake ona Yeremia 30:19-22 “Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge.Watoto wao nao watakuwa kama zamani, na kusanyiko lao litathibitika mbele zangu, nami nitawaadhibu wote wawaoneao. Na mkuu wao atakuwa mtu wa kwao wenyewe, naye mwenye kuwatawala atakuwa mtu wa jamaa yao; nami nitamkaribisha, naye atanikaribia; maana ni nani aliye na moyo wa kuthubutu kunikaribia? Asema Bwana. Nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.”

4.      Kumjua Mungu kutafungua ukurasa wa maarifa ambayo wengine hawana, ujuzi kuhusu Mungu unauwezo wa kutupa aina ya maarifa ambayo wengine hawana Petro aliwahi kupokea maarifa ya kipekee ambayo kwayo Yesu alijua isingekuwa rahisi kuyajua au kuyapokea Bila kuwa na uhusiano na Mungu ona Mathayo 16:13-17 “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.”

5.      Kumjua Mungu kutatupelekea kufanya mambo makubwa ya ajabu Zaburi 108:12-13 “Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai. Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu” Daniel 11:32 “Na wao wafanyao maovu juu ya hilo agano atawapotosha kwa maneno ya kujipendekeza; lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu.”

6.      Kumjua Mungu na kumtegemea Yeye kunatupa uhakika wa usalama wetu Zaburi 91:1-,7 “Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini. Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo. Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao. Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana, Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri, Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.

7.  Kumjua Mungu na kuwa naye kunatupa ujasiri Yoshua 1:5 “Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha.

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima!

Jumapili, 24 Januari 2021

Nyumba juu ya Mwamba!


Mathayo 7:24-27Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.


Utangulizi:

Kristo Yesu alipokuwa duniani aliishi kama mtenda kazi awaye yote  katika Bwana akiwa na karama na vipawa mbalimbali vya Roho moja ya karama aliyokuwa nayo ilikuwa ni karama ya ualimu,uwezo wake na mamlaka aliyokuwa nayo katika kufundisha iliwafanya wale waliomsikiliza wakubwa kwa wadogo kushangazwa sana na uweza wake wa kufundisha ona

Mathayo 7:28-29 “Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao
”.

Makutano wengi walifurahishwa sana na kukubaliana na mafundisho yake, lakini sio wao tu hata watu wakubwa na wenye cheo na mamlaka walimkubali Yesu kuwa ni Mwalimu wa kweli na kuwa Mungu yuko pamoja naye ona

Yohana 3:1-2 “Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.

Moja ya sifa kubwa sana ya Yesu Katika mafundisho yake ilikuwa ni uwezo wake wa kutumia mifano iliyo hai inayoeleweka vema kama daraja la kuwasaidia wpte waliomzunguka kumuelewa kwa wepesi, Mafundisho ya Yesu yalieleweka kwa watu wa kila Nyanja wakiwemo wasomo na watu wa kawaida, alitumia mifano mbali mbali iliyojumuisha maisha ya kila siku ya jamii yake nay a watu wake mfano alizungumza mifanyo ya Nyanja ya uvuvi, afya, mizabibu, mashamba, mbweha, matajiri na masikini, ndege, maisha ya kawaida, fedha lakini vilevile katika maswala ya ujenzi kama ilivyo katika mfano huu tutakaouchambua leo!

Makusudi makuu ya Yesu kutumia mifano ilikuwa ni kuleta uelewa wa ndani zaidi kwa wasikilizaji wake na kuleta matokeo makubwa ikiwemo kubadilisha maisha yao na kuwasaidia kuelewa makusudi ba mpango wa Mungu kwetu!

Mfano wa Mjenzi mwenye Hekima na Mjenzi mpumbavu.

Mfano huu Yesu aliweza kuuelezea kama kilele cha Mafunisho yake akitaka wale walioyasikia mafundisho yake waweze kuyafanyia kazi, kwa hiyo ulikuwa ni mfano unaosimama kama msumari wa moto kugongelea umuhimu wa kuishi kile ambacho yeye amekifundisha, Yesu alikuwa Carpenter yaani mjenzi alikulia na kujifunza maswala ya ujenzi, na hivyo alifahamu kuwa nyumba imara huwa inajengwa namna gani, uimara wa nyumba ni msingi wake  aidha uende chini sana au ujengwe juu ya Mwamba, lakini sio hivyo tu iwe na uwezo wa kustahimili mikimikiki ya Mafuriko, maji na pepo kali,

Yesu alikuwa akikazia mfano huu kuwataka wote wanaomuamini, wajue kuwa hawajamaliza kazi, Mwanafunzi makini wa Yesu Kristo ni yule anayejifunza kusikia na kutii au kuyafanyia kazi mafundisho ya Yesu Kristo ona

Luka 6:46-49
Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo? Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri. Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa.

Neno la Mungu linatuagiza kuwa watendaji wa neno na sio wasikiaji tu, nykati za leo kumekuwepo na wimbi kubwa sana la wakristo ambao msingi wao hauko katika neno la Mungu, na wahubiri pia msingi wao uko katika miujiza tu na matyokeo yake wameendelea kuwa wachanga wakichukuliwa huku na huko na upepo wa kila namna wa Elimu, Kusudi la kuwepo kwa karama zote tano za huduma ni ili mwili wa Kristo ujengwe watu wakomae wafikie kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo wasiwe watu wa kuyumbishwa huku na kule ona

Waefeso 4:11-15
Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.” Unaona Karama zote za huduma zimetolewa kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, kwa kusudi la kuwajenga watu wakomae, Leo hii watu wengi wamekuwa wakifukuzia miujiza, akiinuka muhubiri huyu na miujiza wanahama huku na kule kwa sababu hawana msingi katika neno, lakini hata wahubiri pia wameshindwa kubalance/ kuweka sawa mzani sikatai kuwa miujiza ni ya muhimu sana na ndio maana hata Yesu aliifanya lakini kulitendea kazi neno la Mungu ni muhimu zaidi kuliko miujiza Biblia inaonya watu wanaofanya muujiza lakini hawayafanyi wala kuyaishi yale Kristo anayoyataka ona  maonyo ya yesu mwenyewe

Mathayo 7:21-23 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”
 

Kipimo kikubwa cha uendeleaji mwema wa Kikristo ni kulitendea kazi neno na sio vinginevyo, watu wanapaswa sasa kuwa na kiu ya kutafuta kujifunza neno la Mungu kuliko kuhangaika huku na kule wakitafuta miujiza ambayo ni ya kitoto tu kwani ni ya Muda mfupi na wale waitendao na hata wanaotenda hufariki dunia, Mkristo mkomavu ni yule anayejifunza neno la Mungu na kukaa katika neno huku akilifanyia kazi kinyume na hapo ni kujidanganya ona


Yakobo 1:22-25 “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.”
  

Unaona neno la Mungu halitaki blaablaa wala unafiki linataka watu walitendee kazi, hiyo ndio akili kinyume cha hapo ni upumbavu, Neno la Mungu linatupa changamoto leo kuwa tusiwe wasikiaji tu bali tuwe watendaji, ni muhimu kujikumbusha kuwa kutoa pepo na kutoa unabii pekee hakutoshi, kwa kuingia katika ufalme wa Mungu wote tunapewa wito wa kulifanyia kazi neno, na kisha wote wenye karama za huduma yaani walimu, wachungaji, wainjilishi, manabii na mitume tumeitwa kuimarisha kanisa na kulijenga na sio kufanya miujiza peke yake, waamini nanyi mnapaswa kujifunza neno la Mungu na kukaa katika hilo, watu wanapaswa kumjua Yesu, huduma zetu zinapaswa kumtambulisha yesu zaidi kuliko sisi wenyewe, huduma zetu ziwaelekeze watu kwa Yesu, tusiwe busy kutafuta umaarufu au kufanya miujiza na hatimaye tukawa maarufu kumshinda Yesu, tunapaswa kuwa makini ili katika huduma zetu tufanyazo kipaumbele kisiwe sisi bali Yesu! Mkazo wetu uwe kuyatendea kazi yale Bwana aliyotuangiza hata kama si kwa ukamilifu lakini huo ndio uwe mwelekeo wetu Kama tunampenda Yesu tutazishika amri zake

Yohana 14:15 “Mkinipenda, mtazishika amri zangu.”
Mfano wa mjenzi ni mfano rahisi kueleweka kwamba mwanafunzi imara ni yule anayesikiliza na kutii walimu wake na kuyatendea kazi yake anayoagizwa, tukiishi hivyo na tukimuomba Mungu then Mungu atafanya sehemu yake na neema yake itakuwa juu yetu, Yohana 13;17 “ Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.”

Mathayo 7:24-27Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!




Jumapili, 17 Januari 2021

Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha!

Zaburi 126:1-6Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto. Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu.  Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi. Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini. Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.”

Utangulizi:

Zaburi ya 126 ni mojawapo ya zaburi zilizoitwa zaburi za kupandia yaani ziliimbwa wakati watu wanapanda kwenda nyumbani mwa bwana Hekaluni aidha pia ni zaburi ya kihistoria inayoelezea maisha  ya wana wa Israel hususani Wayahudi waliorudi kutoka uhamishoni Babeli, Wayahudi hao walichukuliwa mateka wakati wa Mfalme Nebukadreza kwa kusudi la kuwatumikisha hivyo waliishi uhamishoni kama watumwa walifanyishwa kazi kwa faida ya taifa la wakaldayo, Hata hivyo baada ya miaka kadhaa kupita Mungu aliwajia tena watu wake na kuwaletea ukombozi, yaani walirejea katika nchi yao kwa amri ya mfalme Koreshi, makundi matatu ya wayahudi walirejea nyumbani kundi la Kwanza wakati wa Zerubabel na kundi la pili wakati wa Ezra na la tatu wakati wa Nehemia  hivyo inaaminika kuwa zaburi hii inaaminika iliimbwa na wana wa Asafu waliorejea kutoka uhamishoni wakati wa Ezra ona

Ezra 2:1-2, 41. “1. Basi hawa ndio wana wa wilaya, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka mpaka Babeli, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake; 2. ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo hesabu ya wanaume wa watu wa Israeli; 41 Waimbaji; wana wa Asafu, mia moja ishirini na wanane.”


Wimbo huu ulijulikana kama wimbo wa kupandia yaani wayahudi walikuwa wakiuimba kila wakati walipokuwa wakipanda kwenda Yerusalemu kuabudu Hekaluni,  Kumbuka kuwa Nyumba ya Mungu yaani Hekalu lilijengwa juu yam lima yaani sayuni na hivyo mara kwa mara mtu alipoenda nyumbani kwa Bwana ilikuwa ni kama anapanda, Zaburi hii ilitungwa na wana wa Asafu wakati wa Ezara  na wimbo huu ulitumika katika maeneo makuu matatu kushukuru, kuomba na kutia moyo

1.       Kama njia ya kumshukuru Mungu kwa wale waliokuwa wamerejea kutoka utumwani  kwamba Mungu alikuwa amewatendea mambo makubwa sana amewakomboa amewapa uhuru, nyakati za ukoloni wa kizamani mataifa yenye nguvu walipowateka watu waliwachukua kuwa watumwa katika nchi zao, ni watu wa ulaya kama Wayunani na warumi ndio walioanzisha iana ya utumwa au utawala wa kumtawala mtu katika taifa lake lakini wakaldayo na mataifa ya kale waliua watu na wengine waliwahamisha  hivyo kurudi nyumbani hasa wayahudi  kurudi Israel kwao ni Muujiza mkubwa sana ni kurudi katyika uwepo wa Mungu ni jambo la kushangaza mataifa hivyo katika zaburi hii wanashukuru kurejea nyumbani

Zaburi 126:2-3
unaonyesha “Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu. Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi.


2.   Aidha wimbo huu pia ulitumika kuwaombea dua na kuwatia moyo  na kuwataka wale ambao bado walikuwa wamesalia huko utumwani kuendelea kumuomba Mungu ili nao waweze kutoka katika utumwa  walikumbuka kuwa wako ndugu zao ambao bado hawajarejea hivyo walitoa wito na kumsihi Bwana awarejeza ndugu zao walioko kifungoni utumwani nchi ya mbali  ona   

       Zaburi126:4Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini.”

3.  Na eneo la tatu lilitumika kuwatia moyo watu wote waliokuwa wanapitia shida za aina yoyote na changamoto za aina yoyote katika maisha kuwa maisha yao wanayoyapitia ya aina yoyote ile yanafananishwa na maisha ya mkulima na kuwa mtu awaye yote anapopitia taabu na machungu ya aina Fulani ni lazima aelewe kuwa wakati huo katika maandiko unafananishwa na wakati wa kupanda, kupanda kunajumuisha maandalizi ya shamba, kulima na kukatua ardhi  na ujuzi wa nyakati kwamba mvua zitaanza lini? huu ni wakati wa taabu na shida ambayo inahitaji uvumilivu  na kwa kweli wakati wa kuandaa shamba mpaka kupanda ndio wakati Mgumu sana kwa mkulima kuliko wakati wa kuvuna, wakati wa kuandaa shamba na kupanda wakulima wengi hawaonekani mjini wala nyumbani, wanaamka mapema sana kwenda shambani ili walime kabla jua halijawa kali, wakulima hupata taabu sana wanapojiandaa kupanda kwa huku wakijua kuwa uko wakati watafurahia mavuno hivyo kipindi hiki ni kipindi cha machozi.  Wana wa Asafu wanafananisha kipindi cha kupanda kama kipindi cha machozi na wakati wa kuvuna kama wakati wa furaha,  ona

Zaburi 126:5-6 Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.”

Ni muhimu kufahamu hili kuwa maisha ya mwanadamu yana nyakati tofauti tofauti na kila wakati una umuhimu wake na wakati mwingine wakati mmoja una maana sana kwaajili ya wakati mwingine na kila wakati ni muhimu mno  kwa msingi huo ni muhimu kufahamu majira na nyakati ili uweze kujipanda vema kujua kuwa wakatio huu ni wa kupanda au wa kuvuna ukichanganya nyakati utapata tabu sana !  huwezi kuishi maisha ya mavuno wakati wa kipindi cha kupanda ukifanya hivyo utapata hasara kubwa sana ona

Muhubiri 3:1-8 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa; Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga; Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza; Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia; Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa; Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena; Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.”

Maisha yetu yanapofananishwa na nyakati zozote za taabu katika Biblia wakati huo unafananishwa na wakati wa kupanda “it’s a labour time” ni wakati wa taabu ni wakati wa subira ni wakati wa uvumilivu, wakulima huwa wanajitoa muhanga sana wakati wa kupanda yaani kuandaa mashamba kukatua ardhi huku wakivizia wakati sahihi wa kufanya hivyo, sasa wanadamu wenye akili timamu wanapaswa kujua ni namna gani watacheza au wataenenda na mapigo ya huo wakati, huwezi kuishi wakati wa kupanda kama ndio wakati wa kuvuna ni lazima ujue nyakati kwani wakati mmoja hutengeneza wakati mwingine, mtu akiishi kwa anasa wakati wa kupanda atakuwa na msiba wakati wa mavuno, maana wenzake walivumilia wakajitoa kupanda hivyo wakati wa mavuno watafurahi, wakati wa kupanda ni wakati wa subira na uvumilivu wala sio wakati wa kupendeza, maandiko yanavyotuasa wakati wote tutapopitia changamoto zinazotuonyesha kuwa ni kama tuko katika wakati wa kulia, au tuko katika wakati wa kufanya kazi  ni wakati ambao unahitaji uvumilivu kwani hatimaye Mungu ataleta mvua na mazao yatakua na tutavuna kwa furaha kubwa on

Yakobo 5:7-8,,10 -11 “7. Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. 8. Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.10-11 “10. Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu.11. Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.”

Kimsingi neno la Mungu linatujuza kuwa uko wakati Mungu atatutendea mema, jambo kubwa la msingi ni kujua nyakati ni kuwa na hekima na ujuzi kwamba wakati huu ni wakati wa  namna gani na ni jambo gani tunapaswa kulifanya  tusiishi kizemba kumbuka  katika Israel kulikuwa na Kabila moja waliojulikana kama wana wa Isakari hawa waliitwa watu wenye akili sana na kazi yao kubwa walikuwa ni watu wenye kujua nyakati sio tu kujua nyakati bali pia kujua jambo gani linapaswa kutendeka kwa wakati huo ona

1Nyakati 12:32 “Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao
”. 

Kila mmoja wetu anapaswa kujua nyakati na kuwa na akili kama wana wa isakari kujua nini kinatupasa kutenda kwa wakati, mwezi januari mpaka machi ni miezi muhimu sana kwa wanafunzi na walimu kujipanga kufundisha kwa bidii na kujifunza kwa bidii  katika wakati huu wa mwanzo kama hatutajua yatupasayo kufanya tukajifanya tunacheka na kumbe ni wakati wa kulia  tunaweza kujikuta tunakosea, mkulima anapaswa kujua wakati huwezi kupanda wakati wa hari, kama mwanafunzi anataka kustarehe wakati anajua wazi ni wakati wa kujisomea kwa bidii wakati wake wa mavuno utakuwa wakati wa majuto matokeo yatakapotoka anaweza kulia badala ya kufurahi kwa vile hakufahamu ni wakati gani alipaswa kusoma kwa bidii, wote tunajua kuwa ni mbaya sana mwanafunzi kuja na simu shuleni, wazazi pia wanapaswa kufahamu, unampa mtoto simu aje nayo shuleni atasomaje? Hii ni sawa na kuutumia wakati vibaya au kutokujua wakai na jambo la kufanya kwa wakati huo, huwezi kuchanganya masomo na mapenzi, au uvutaji wa bangi na tabia za ajabu ajabu wakati ukiwa mwanafunzi au kutumia ulevi au kufanya biashara ni dhahiri kuwa huo sio wajati wa kufanya hayo kila mmoja anapaswa kufahamu kuwa kuna wakati wa kupanda wakati huu huwa kama wakati mchungu lakini kuna wakati wa kuvuna huu ni wakati ambapo tutayafurahia matunda ya kazi zetu, tunapoanza shughuli za kila aina mwanzoni mwa mwaka huu basi na tufanye kazi kwa bidii sana kama tupandao,lipa ada ya shule kama uliila wakati wa disemba hukujua kuwa kuna januari hukutofautisha wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna? Ahaa ulivuna kabla ya kupanda sisi tutakudai ada ya shule tu!  Wakati ukiwa shuleni mwanafunzi  tujisiomee kwa bidii, tuhudhurie kazini kwa bidii, tuombe na kufanya ibada na  kila lililowajibu wetu kwa bidii tukijua wazi kuwa wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha  na Mungu atatupa wakati wa faraja hatatuacha tuumie tu atakuwa pamoja nasi na tutafurahia uwepo wake kwa nguvu na ushujaa mwingi ataleta mvua yaani neema atayakuza mapando yetu na atatupa wakati wa mavuno, wakati wa matokeo mazuri, wakati wa kuvuna kwa hiyo ni muhimu kwetu tunapoendelea na wiki hii ya kazi ndani ya mwaka huu 2021 tujitoe kwa ngubvu zetu zote tukijua ya kuwa wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha !   .

Wimbo wa Marehemu Fanuel sedekia unatukumbusha umuhimu wa kujua Majira na nyakati na kuzitumia kwa utukufu wa Mungu:-

Nitaimba haleluya asubuhi, nitaimba haleluya Mchana, nitaimba haleluya jioni haleluya na hata usiku X2, Muhubiri anasema kila jambo na wakati wake; wa kupanda na kuvuna wa kulia na kucheka x2  Haleluya nina wimbo; wa kila  wakati na kila majira wimbo wa nyakati zote na marira yote;  wimbo huo ni Haleluya Nitaimba haleluya asubuhi, nitaimba haleluya Mchana, nitaimba haleluya jioni haleluya na hata usiku X2,  – Fanuel Sedekia

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima