Alhamisi, 19 Agosti 2021

Huyu mjane masikini ametia zaidi kuliko wote!

Marko 12:41-44Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi. Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa. Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina; maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.”



Utangulizi:

Mara nyingi sana tumewahi kusikia neno kutoa ni moyo, katika semi zetu mbalimbali za Kiswahili, lakini je hivi tumewahi kujiuliza kwa undani maana ya msemo huo na sababu zake? Bila shaka msemo huu una uhusiano mkubwa sana na Mafundisho ya Bwana wetu Yesu Kristo kuhusu Kutoa, hususani kulikotokana na mama mjane kabisa aliyefika Hekaluni na kutoa sadaka katika hazina ya nyumba ya Mungu. Yesu alimsifika kuwa ndiye mtu aliyetoa zaidi kuliko wote katika ibada ile aliyoikusudia!

Kila mmoja wetu anapokuwa amejiandaa kwenda kuabudu na kumtolea Mungu anapaswa kuliweka somo hili moyoni mwake! Kwa sababu Mungu haangalii tu nini tunatoa lakini anaangalia ni kwa sababu gani tunaoa, Mungu hutazama moyo! Hebu tuone tena andiko la Msingi ili tuweze kujifunza kitu kutoka kwa mama huyu! Marko 12:41-44Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi. Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa. Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;  maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.” Tutajifunza somo hili Huyu Mjane masikini ametia zaidi kuliko wote kwa kuzingatia mambo ya msingi yafuatayo:-


·         Maana ya neno masikini:-

·         Huyu Mjane masikini ametia zaidi kuliko wote!

·         Utoaji wa sadaka kama mjane:-

 


Maana ya neno Masikini:-

Neno masikini lililotumika katika andiko hilo kwa lugha ya kiyunani linasomeka kama “PTOCHOS” ambalo linaweza kujumuisha maneno ya tafasiri ya kiingereza kama “Crouching,  and Cringing” sawa kabisa na watu wanaoombaomba na kuchakura majalalani, wakenya wana neno zuri linalokaribiana na hilo la “CHOKORAA” yaani masikini wa kutupwa au ombaomba, ni mtu asiye na kitu kabisa mtu anayeishi maisha ya kuomba omba, kwa maana nyingine wakati sisi wengine tunajidhania kuwa masikini kwa kujilinfanisha na wengine na kuona labda wametuzidi kitu Fulani na ndipo tunapoweza kujifikiri kuwa sisi ni masikini, huyu anayetajwa hapa alikuwa masikini kabisa asiye na lolote! Wala hata mtu wa kujilinganisha naye! Mwanamke huyu hakuwa na kitu lakini sio tu hakuwa na kitu pia tunaambiwa alikuwa mjane, amefiwa na mume wake! Ni Mtu wa namna hii asiye na kitu kabisa ndio Yesu anasema ametoa zaidi kuliko wote jambo hili lina maana gani na linatufundisha nini:-

Huyu Mjane masikini ametia zaidi kuliko wote!

Yesu anajua mioyo yetu na anayajua maisha yetu, lakini pia wakati wa matoleo katika ulimwengu war oho Yesu huketi kuelekea sanduku la hazina, maana yake anafuatilia mwenedno wa utoaji wetu kwake, anajua namna na jinsi na hisia zetu wakati wa kutoa  unaweza kuona wazi tabia yake hapa Marko 12:41 “Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi.” Unaona imani yangu inaniambia kuwa tukio la Yesu kufuatilia utoaji wetu sio tu kuwa lilikuwa katika siku hii HAPANA kila inapofanyika ibada ni wazi kuwa Yesu yupo pamoja nasi katika ulimwengu wa kiroho na anafuatilia kila jambo linalotendeka na namna tunavyofanya katika ibada na uchunguiz wa mioyo yetu Neno la Mungu linasema hivi Mathayo 18:20 “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” Unaona kumbe tunapokusanyika wakati wowote tuwe wawili ama zaidi kwaajili ya kumuabudu yeye mwenyewe anakuwepo katikati yetu na saa ya kutoa maana yake ni kuwa anakuwepo pamoja nasi na kufuatilia kila kitu, bila shaka sasa utakuwa umekubaliana nami. Kwa msingi huo Yesu aliwashuhudia wengi wakitoa na alifanya ufuatiliaji na anafanyi hizi hata sasa, na katika ufuatiliaji huu Yesu alibaini kwamba mwanamke Yule mjane na tena masikini wa kutupwa ALITOA KATIKA KILA KITU ALICHOKUWA NACHO ona Marko 12:44 “maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.” Kumbuka kuwa neno la Mungu halimaanishi kuwa tutoe kila kitu tulichonacho, wala halimaanishi kuwa tusijiwekee akiba hapana Lakini utoaji wa mjane huyu masikini ulimshangaza zaidi Yesu kwa sababu ilikuwa ndio chakula chake yaani hana nyingine zaidi ya ile, lakini kwanini alitoa Mwanamke huyu alitoa kwa sababu aliamini kwamba Mungu atamtunza tu, hata kama ametioa kila alichikuwa nacho mungu atafanya njia kwa namna nyingine, aliamini kuwa kumpa Mungu hakutamfanya apungukiwe na kitu  Wafilipi 4:19 “Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.” Hii ndio kanuni ya Mungu, tunapotoa huwa hatupungukiwi, Mungu hujaziliza kwa namna nyingine mimi na mke wangu huwa tunatabia ya kupunguza nguo zetu na kuzigawa kwa watu wengine, wakati mwingine huwa tunagawa nguo zote ambazo hazitutoshi au hata ambazo huwa hatuzivai mara nyingi tu, huwa tunahakikisha tunapunguza ili zibaki chache tu tunazotumia kwa maisha ya kila sku hapa na pale lakini baada ya miezi kadhaa unashangaa tena Nguo zimekuwa nyingi tena, Mungu wetu ni mchungaji mwema na hukakikisha kuwa kondoo zake hawapungukiwi na kitu Zaburi 23:1 “Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.” Awaye yote anayefanya kitu kwaajili ya Mungu na kwa imani katika Mungu hawezi kupungukiwa na kitu, mjane Yule alitoa kwa imani hii aliamini kuwa Mungu hatamuacha ateseke na njaa hata kidogo ona Zaburi 37:25 “Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.” Mjane huyu aliamini hivyo na liishi hayo katika maisha yake hakuwaza kujilimbikizia alimuamini Mungu kwa asilimia mia moja na alipoukunjua moyo wake katika hili Yesu alimuona na kumtumia kama somo kuu katika maisha ya wanafunzi wake, je ni kitu hani tunaweza kujifunza kutoka katika utoaji wa mjane huyu:-

Utoaji wa sadaka kama mjane:-

Kwa kuwa Bwana Yesu alimfanya mwanamke huyu kuwa kielelezo, ni wazi kuwa kuna maswala ya Muhimy ya kujifuza kutokana na utoaji wa mjane huyu masikini, liko jambo la kujifunza kutoka kwake

a.       Alijitoa yeye mwenyewe kwanza!

 

Utoaji wa mwanamke huyu mjane haukuwa rahisi, na hauwezi kuwa rahisi kama mtoaji huyu angekuwa na ubinafsi, ni wazi kuwa mtoaji huyu alitoa akiwa hana hata chembe ya ubinafsi nah ii maana yake yeye mwenyewe alikuwa tayari amejitoa amejidhabihu kwa Mungu Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” Ni ukweli ulio wazi katika maandiko kuwa kabla hatujamtolea Mungu au hata kumpa mwanadamu sisi ndio sadaka ya kwanza, mwanamke huyu alikuwa ameuua umimi kabisa ukilinganisha na upendo wake kwa Mungu, yeye alikuwa anampenda Mungu kwa dhati, moyo wake na mauisha yake alikuwa ameyatoa kwa Bwana, mtu hawezi kufanya ibada ghali namna hii kama hajajichukia yeye mwenyewe kwanza Luka 9:23-24 “Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.” Unaona huyu mwanamke alitoa kwa kujikana, ni muhimu kufahamu kuwa ibada ni kafara na hakuna kafara isiyogharimu, hatupaswi kumpa Mungu vitu visivyogharimu nafsi zetu, ibada yenye maana zaidi inahusisha kujitoa kwaajili ya Mungu na wengine! Nyakati za kanisa la kwanza katika makanisa yaliyokuwepo Macedonia yaani Ugiriki Bila shaka Kanisa la wafilipi walielewa aina hii ya utoaji katika mapenzi ya Mungu na hivyo japo walikuwa hawana kitu, walitoa tena sio kwa kulazimishwa kwa hiyari, kwa furaha, kwa uwezo na hata zaidi ya uwezo lakini wakitanguliwa na kujitoa kwanza nafsi zao 2Wakoritho 8:1-5 “Tena ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia; maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao. Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao; wakituomba sana pamoja na kutusihi kwa habari ya neema hii, na shirika hili la kuwahudumia watakatifu. Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini tu, bali kwanza walijitoa nafsi zao kwa Bwana; na kwetu pia, kwa mapenzi ya Mungu.” Unaona huu ndio utoaji ambao Yesu aliukusudia wanafunzi wake waelewe, kanisa la leo linapoteza Baraka kwa sababu kwanza wao wenyewe hawajajitoa kwa Mungu na kwa sababu hiyo wanaona taabu kutoa kwa Mungu, wakiwa hawana imani na wamejaa woga kuwa kesho itakuwaje na matokeo yake tuna wakristo wachoyo hata kuliko waislamu na wapagani!, unapooona makanisani kila siku watumishi wa Mungu wanafundisha juu ya kutoa ujue watu hawajitambui na wala somo kuhusu utoaji halijaeleweka kwao!

 

b.      Mjane alitaka kuyatenda mapenzi ya Mungu

 

Mjane Yule hakuenda ibadani kutoa kama maonyesho, alikuwa ameelewa neno la Mungu linataka nini na alikuwa kazini akiyatekeleza mapenzi ya Mungu, akitoa hakuketi chi ni na kufikiri kuhusu ujane wake , wala hakufikiri kuwa Mungu amemtenza mabaya kwa kumuacha katika umasikini wa kutupwa na akiwa hana mtu wa kumsaidia, huenda alikuwa akimshukuru Mungu hata kwa kile alichokipata, na hakusema moyoni ngoja nipate zaidi nitatoa hapana alitaka kuabudu kweli kweli sio kwa mdomo kwa vitendo Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.” Mwanamke huyu mjane na masikini alikuwa kazini, hakuwa kwenye maonyesho, hapiti kutoa sadaka aonekane kuwa kaja ibada, haoiti mkunyesha nguo nzuri wala hapito kuionyesha amekuja ibada hapana yuko kazini kwelikweli ilikuwa saa ya kutoa na alikuwa anakwenda kutoa akijua kwa nini anatoa na tena sio kwa kulazimishwa bali kwa hiyari na uelewa ulio wazi na kwa nia na alikusudia hivyo tangu anatoka nyumbani  2Wakoritho 9:7-8 “Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;” unaiona mwanamke huyu alitoa kwa ukunjufu wa moyo, na Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo na kama sadaka inakukwaza na kukufanya ujisikie huzuni sadaka hiyo haifai, tunapotioa Mungu huangalia nia yetu 2Wakoritho 8:12 “Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.” Haya ndiyo yaliyiompa maksi mjane Yule.

 

c.       Alitoa licha ya umasikini wake!

Pamoja na umasikini mku bwa aliokuwa nao mwanamke Yule mjane, hii haikumfanya aka chini na kujifikiri kuwa kuwa yeye bado sana ! unajua wako watu makanisani ukifika wakati wa sadaka na changizo nyingine za kikanisa wao huwa wanakuwa wapole na wanakaa kimya hawanyooshi mkono kujitoa wanajifikiri wao ni masikini, wanadhani kuwa wako watu maalumu watakaomtolea Mungu lakini wao bado sana nisikilize katika moyo wa Mungu wewe bado sana na tena utaendelea kuwa masikini kwa sababu unajua kutokutoa kwako kwa sababu ya hali yako kunageuka kuwa dua mbaya kwamba ni kama unamwambia Mungu  mimi sitoi kwa sababu hujanipa, unapochangamka na kutoa kama mjane huyu maana yeke ni kuwa unamshawishi Mungu kuona na kukuamini kuwa huyu nikimpa vingi kwa kuwa amekuwa mwaminifu katika madogo atakuwa mwaminifu katika makubwa pia Luka 16:10-12 “Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe? unaona mwanamke huyu mjane na masikini kweli kweli alikuwa mwaminifu katika umasikini wake na kwa sababu hiyo alitoa katika hali hiyo hiyo ya umasikini wake wakati wengine walitoa vilivyowazidi, walitoa wasivyovihitaji, hawakuwa wamejikana katika kutioa kwao, Mwanamke huyu mjane alitoa kwa sababu alimpenda Bwana, alikuwa hana ubinafsi, wala hakutaka kujilimbikizia, hakuwa na muda wa kupiga hesabu, alikuwa akifuarahia ikiwezekana labda hata zawadi ya uhai aliyopewa na Mungu, kutokuugua, kupata nafasi ya kuabudu akiutzama wema wa Mungu kuliko yaliyomkuta huu ndio utoaji usio na ubinafsi


Hitimisho!

Mtu awaye yote anayetaka kupokea kutoka kwa Mungu anapaswa kuelewa kwanini tunatoa, na lazima ieleweke wazi kuwa Mungu huwabariki wale wanaotoa kwa Moyo, utoaji wa kikristo ni hiyari na sio lazima, ni furaha na sio huzuni, ni moyo na sio utajiri, Nyakati za Kanisa la kwanza watu walitoa hata mali zao na kuwagaia wengine na kuifadhili kazi ya Mungu iweze kwenda mbele Barnaba alikuwa mmoja wao ona  Matendo ya Mitume 4:36-37. “Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro,alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume.” Wakristo wanapaswa kujifunza kutoa na wazazi wanapaswa kuwafundisha watoto wao umuhimu wa kutoa tangu wakiwa wadogo, tusisubiri mpaka tumekomaa au kuzeeka tukiwa na tabia ngumu ya choyo Mungu anataka tuwe na tabia hii tangu mwanzo, iwe ni tabia ya maisha yetu na sidhani kama ni sahihi kusubiri wakati tumechoka au umestaafu Muhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.” Kuwafundisha watu wakishakuwa watu wazima ni kuchelewa sana kuwafanya watu hawa kuja kuelewa mapenzi ya Mungu na yanakuwa mmzigo kwao Maombolezo 3:27 “Ni vema mwanadamu aichukue nira Wakati wa ujana wake.” Ni wachache sana wanaweza kuelewa na kujaribu kulitendea kazi somo kama hili lenye kuhusisha kujitoa nasfi lakini wakati wote tukumbuke kutoa kwa moyo pasipo manung’uniko na kuhakikisha kuwa tunatoa kwa sababu nia yetu ni njema na kwa furaha katika kuhakikisha kuwa injili inakwenda mbele na wale wanaoishi kwa injili wanapata mkate wao wa kila siku, kwa kuyajua haya utakuwa umeyatimiza hivyo mapenzi ya Mungu, Muongezewe neema

Na. Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Jumanne, 10 Agosti 2021

Mambo yamtiayo mtu unajisi!

Mathayo 15:17-20 “Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni? Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi. Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano; hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi.”


Utangulizi:-

Mafarisayo na waandishi walitoa shutuma nzito kwa wanafunzi wa Yesu, kwamba hawanawi mikono mpaka kwenye kiwiko wakati wanapokula chakula, na kuwa kwa kufanya hivyo wanayahalifu maagizo ya wazee, Kimsingi hakuna maagizo ya kibiblia yanawataka watu kunawa mpaka kwenye kiwiko cha mkono, lakini mafarisayo walikuwa wameyashika mapokeo hayo kana kwamba ni agizo la kiungu na kutumia kigezo hicho kuwahukumu wengine. Yesu aliwakemea Mafarisayo kwa tabia yao yenye kutoa kipaumbele kwa mambo yasiyo ya msingi na kusahahu mambo ya msingi, kimsingi Yesu hakuwa amedharau kanuni za kiafya kwamba labda watu wasinawe mikono wanapojiandaa kula chakula na kadhalika, Lakini yesu alikuwa anaikemea ile tabia ya kinafiki ya kupuuza mambo ya msingi na kushikilia mambo yasio na msingi ambayo kimsingi hata neno la Mungu halikuwahi kuyaagiza, Yesu alitaka kuonyesha wazi kuwa kula bila kunawa kiwiko cha mkono au kuingiza kitu tumboni kulicho nasisi kunaweza kusiwe na maana sana kwani vinapita tu, lakini alitaka jamii ielewe kuwa kuna mambo ya hatari zaidi ya kuyashughulikia yanayokaa moyoni na kujitikeza hata mdomoni kuliko yale yanayoingia mdomoni kisha yakaenda zake! Kwa mafundisho ya Yesu mambo hayo ndio yamtiayo mtu unajisi! Leo tutachukua muda kuangalia kwa undani mambo yanayomtia mtu unajisi na kumuomba Mungu atuokoe na mambo hayo ili tupate kibali mbele zake!


1.       Mawazo mabaya (evil Thoughts)

 

Ni muhimu kufahamu kuwa kwa mujibu wa Mafundisho ya kibiblia usafi wa Mtu huanzia kwenye moyo wake, yaani kwenye akili na ufahamu, uhusiano wetu na Mungu unategemeana sana na mkao wa moyo, kujibiwa kwetu maombi na kupata thawabu katika kila jambo kunategemeana sana na mkao wa Moyo, hivyo ni muhimu kwetu kuhakikisha kuwa wakati wote tunakuwa safi moyoni kwanza, bila kupuuzia usafi mwingine wanje Neno la Mungu linasema Mathayo 5:8 “Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.” Uhusiano wetu na Mungu haujengwi pekee kwa matendo ya nje bali zaidi hasa na mkao wa mioyo yetu ndani Neno la kiyunani wenye moyo safi husomeka kama “KATHAROS” yaani mtu safi, asiye na hatia asiye na lawama, mtu ambaye hata dhamiri yake haimuhukumu kuwa ana kesi ya kujibu, hakuna hila ndani yake, hakuna unafiki, hakuna kitu kilichojificha, muwazi kwake kwa Mungu na kwa wanadamu mtu mwenye nia ya kumpendeza Mungu, ni ukweli wa kibiblia usiofichika kuwa Mungu haangalii kama wanadamu waangaliavyo, Mungu hutazama moyo, 1Samuel 16;7 “Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.” Kipimo kikubwa cha mtazamo wa Mungu kwa mwanadamu ni Moyo, hii ndio chemichemi ya mambo yote tuyaonayo ulimwenguni, kwa hiyo ili mtu asinajisikie aiwe muovu anapaswa kuhakikisha kuwa anakuwa na mawazo safi, anajilinda sana ndani kusiharibike, Mithali 4:23 “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.” Mtu safi hapimwi kwa kile anachikifanya, mtu safi anapimwa kwa mtazamo wa moyo wake yaani mawazo yake unawaza nini kabla hujatenda, kupata kibali kwa Mungu kunategemeana sana na unawaza nini, yaani nia ya moyo wako Zaburi 19:14 “Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.” Kama tutakuwa safi nje tu lakini katika mawazo yetu tumejaa kila aina ya uovu kamwe Yesu hawezi kutukubali katika viwango vya usafi anaouhitaji Bwana wetu ni ndani kwanza! Mathayo 23:25-28 “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi. Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi.Unaona Bwana Yesu alikemea vikali sana dhambi inayokaa katika mawazo, alikuwa anaelewa wazi kuwa kuwa safi nje lakini ndani hakufai ni unafiki, uhalisia wa Mtu na uzuri na usafi wake huanzia katika mawazo, na mtu akiwa safi ndani nan je yake hupata kuwa safi, kwa msingi huo ni jambo gani linatutia unajisi ili tuweze kulishughulikia ni mawazo yetu kwanza na kwa sababu hiyo hatuna budi kumuomba Mungu mawazo ya mioyo yetu yapate kibali mbele zake yaani tuwaze mema na Mungu awe shahidi wa ule wema ulioko ndani yetu, hapo hatutakuwa najisi, kumbuka kuwa mawazo ndio chemichemi ya kila kitu kiovu!

 

2.       Wivu (envy)

 

Ni muhimu kufahamu kuwa katika maisha haya hatuwezi kuwa na kila kitu, kadiri unavyotembea katika maisha haya ukiwa na fedha unaweza kuwakuta wenzako wana fedha kuliko wewe, una ndoa iliyotulia unaweza kukuita kuna watu wana mahusiano mazuri na matamu kuliko yako, umejenga nyumba unaweza kukutana na wenzako wana Mahekalu makubwa na makasri mazito kuliko wewe, unanunua gari utakutana na wenzako wenye migari, unaweza kuwa u mzuri na ukautana na mtu mzuri kuliko wewe halafu wala hana maringo kama yako, unaweza kuwa na cheo lakini ukakutana na wenzako wenye cheo kikubwa kuliko chako, je unajisikiaje moyoni mwako unahisi wivu? au unaposikia maono na mawazo yamwenzi wako unajiskia kushindana naye, au kumuharibia, au kumuua wivu umewaharibia watu wengi sana maisha na kuwatia unajisi  wazee wetu ndugu wa baba moja wana wa Israel walichukizwa tu na Ndoto za Yusufu ndugu yao na kwaajili ya wivu walifikia hatua ya kutaka kumuua na hata kumuuza Misri ona  ni wivu wao ndio uliozalisha chuki na hata kutaka kumletea uharibifu Mwanzo 37:2-11 “Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu, aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu zake; naye alikuwa kijana pamoja na wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akamletea baba yao habari zao mbaya. Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee wake, akamfanyia kanzu ndefu. Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia, wala hawakuweza kusema naye kwa amani.  Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia; akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake. Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia. Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi? Ndugu zake wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili.” Agano jipya linaweka wazi sababu ya Yusufu kuchukiwa na ndugu zake na hata kutaka kumuua au kuamua kumuuza kule Misri kuwa ilikuwa ni wivu, Matendo 7:9-10 “Wale wazee wetu wakimwonea wivu Yusufu, wakamwuza aende Misri. Mungu akawa pamoja naye, akamtoa katika dhiki zake zote, akampa fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri; naye akamfanya awe mtawala juu ya Misri na nyumba yake yote” wakati wote tukiruhusu roho ya wivu kutawala mioyo yetu na kutkuridhika na kile ambacho Mungu ametubarikia na kukosa shukurani tutajikuta tunajiharibia maisha yetu na kuyatia unajisi, wivu unaweza hata kuleta mauaji, taama pia na ugomvi wa moyoni yakobo anautaja wivu kuwa ni hekima ya kishetani, wako watu wana hekima ya kishetani, wanaweza au wanajua kuleta magomvi, wanajua kuchonganisha hatuna budi kumuomba Mungu atukinge na unajisi wa namna hii ambao Yakobo anauita wivu wenye uchungu Yakobo 3:13-16 “N'nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima. Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.” Hekima ya Mungu haitaki tujilinganishe na wengine wala hairuhusu tujione bora kuliko wengine, namna pekee tunayoweza kujilinda na wiu wenye uchungu ni kufanya mema yatakayotuhakikishia kibali kwa Bwana, kwani Mungu yuko tayari kumbariki kila mmoja na hubariki kila mmoja kwa namna yake kama apendavyo yeye!

 

3.       Tamaa (Greedy).

 

Ni moja ya tabia ambayo imeharibu wengi sana na kuwaletea hasara katika maisha, neno tamaa greedy katika kiingereza ina maana ni ile hali ya kutaka kuwa nacho zaidi, kula zaidi, kuvaa zaidi, kila kitu zaidia ya kile ulicho nacho au unachohitaji, kwa hiyo mtu mwenye tamaa sio kuwa hana isipokuwa ni anahitaji zaidi haridhiki na kile alichonacho! Tamaa inapaswa kudhibitiwa katika hatua za mwanzoni kabisa ili isikomae na kusababisha madhara makubwa Yakobo 1:14-15 “Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.” Watu wengi sana duniani wameharibiwa na tamaa, wanavyo lakini wanataka kuwa navyo zaidi, halii hii ikiuandama moyo wa mwanadamu inapelekea kwenye kuleta madhara makubwa sana na kumtia mtu unajisi, Biblia inatueleza habari ya mfalme mmoja aliyeitwa Ahabu, ambaye ingawa alikuwa mfalme na alikuwa na kila kitu lakini bado alitamani shamba la mtu, ambaye shamba lile lilikuwa la urithi na katika Israel mila zao hazikuruhusu kitu cha urithi kiuzwe au kubadilishwa lakini kwa tamaa jamaa alishindwa hata kula na mkewe aliyeitwa Yezebeli akapanga njama ya kumuua Nabothi ili shamba lile liwe na Ahabu, Mungu liona tulio lile na kutangaza hukumu mbaya sana kwa familia ya Ahabu 1Wafalme 21:1-19 “Ikawa baada ya hayo, Nabothi Myezreeli alikuwa na shamba la mizabibu katika Yezreeli, karibu na nyumba ya kifalme ya Ahabu mfalme wa Samaria. Ahabu akasema na Nabothi, akamwambia, Nipe shamba lako la mizabibu nilifanye shamba la mboga, maana ni karibu na nyumba yangu; nami nitakupa badala yake shamba la mizabibu lililo zuri zaidi; au ukipenda, nitakupa fedha sawasawa na thamani yake. Nabothi akamwambia Ahabu, Bwana apishe mbali nikupe wewe urithi wa baba zangu. Basi Ahabu akaenda nyumbani kwake, ana moyo mzito, tena amekasirika, kwa sababu ya neno lile aliloambiwa na Nabothi Myezreeli, akisema, Sitakupa urithi wa baba zangu. Akajilaza kitandani pake, akageuza uso wake, akakataa kula. Lakini Yezebeli mkewe akamwendea, akamwambia, Kwa nini roho yako ina huzuni hata usile chakula? Akamwambia, Kwa sababu nimesema na Nabothi Myezreeli, nikamwambia, Unipe shamba lako la mizabibu kwa fedha, au, ukipenda, nitakupa shamba la mizabibu lingine badala yake. Akajibu, Sitakupa shamba langu la mizabibu. Yezebeli mkewe akamwambia, Je! Sasa wewe unaumiliki ufalme wa Israeli? Ondoka, ule chakula, moyo wako ufurahi; mimi nitakupa shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli. Basi, akaandika nyaraka kwa jina la Ahabu, akazitia muhuri yake, akazipeleka zile nyaraka kwa wazee, na kwa watu wenye nguvu waliokuwa katika mji wake, waliokaa pamoja na Nabothi. Akaandika katika zile nyaraka, akasema, Pigeni mbiu ya watu kufunga, mkamweke Nabothi juu mbele ya watu, mkainue watu wawili, watu wasiofaa, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe. Wale wazee wa mji wake, na walio wenye nguvu waliokaa mjini mwake, wakafanya kama Yezebeli alivyowaagiza, kama ilivyoandikwa katika nyaraka alizowapelekea. Wakapiga mbiu ya watu kufunga, wakamweka Nabothi juu mbele ya watu. Na hao watu wawili, watu wasiofaa, wakaingia, wakaketi mbele yake; wale watu wasiofaa wakamshuhudia Nabothi mbele ya watu, wakasema, Nabothi amemtukana Mungu na mfalme. Ndipo wakamchukua nje ya mji, wakampiga kwa mawe hata akafa. Wakampelekea Yezebeli habari, wakasema, Nabothi amepigwa kwa mawe, amekufa. Ikawa Yezebeli aliposikia ya kwamba Nabothi amepigwa kwa mawe na kufa, Yezebeli akamwambia Ahabu, Inuka, ulitamalaki shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, alilokataa kukupa kwa fedha, maana Nabothi hako hai, lakini amekufa. Ikawa Ahabu aliposikia ya kwamba Nabothi amekufa, akaondoka, alitelemkie shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, ili alitamalaki.Neno la Bwana likamjia Eliya Mtishbi, kusema, Ondoka, ushuke, ukutane na Ahabu mfalme wa Israeli, akaaye katika Samaria; yuko katika shamba la mizabibu la Nabothi, ndiko alikoshukia ili alitamalaki. Ukamwambie, ukisema, Bwana asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, Bwana asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako.” Ni tamaa inayoweza kusababisha watu wakadhulumu, ni tama inayoweza kusababisha watu wakaua, ni tama inayoweza kusababisha watu wakashindwa kuridhika na kuharibu mioyo yao, Bwana ampe neema kila mmoja wetu kutokuwa na tama katika jina la Yesu Kristo.

 

4.       Kutokujiamini (Insecurity).

 

Kutokujiamini ni moja ya tabia inayonajisi watu wengi sana, wengine wameingia katika mtego wa dhambi kwa sababu tu wamekosa kujiamini, kutokujiamini ni tatizo la kisaikolojia, na kiroho pia, yaani mti haisi usalama kwa sababu anataka kutawala wengine, control au kwa sababu ya kutokujiamini ananyanyapaa wengine au anataka sifa zote ziende kwake, na hataki wengine wasifiwe, wakisifiwa wengine anaponda, uadui kati ya Daudi na Sauli ulianza tkwa sababu wanawake walimsifia Daudi na kumpa sifa kubwa kuliko walizompa Sauli 1Samuel 18:6-8 “Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake. Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme? Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile.” Unaona ni ukweli ulio wazi kuwa Sauli hakujisikia salama kutokana na kusifiwa kwa Daudi, wanawake waliimba kwa kelele za furaha na kumsifia daudi kuwa ameua Makumi elfu na Sauli maelfu, ujumbe huu tu ulileta roho mbaya katika moyo wa sauli aliona wazi kabisa kuwa sasa ufalme ni kama amepewa Daud, wivu uliingia na mipango na vitendo vya kutaka kumua Daudi vilianza tangu wakati ule, Ndugu zangu wako watu, hawataki sifa ziende kwa mwingine, wanajisikia kutokujiamini pale wanapokuwepo watu wenye sifa na uwezo au umahiri kuliko wao, wanadhani wanapoteza nafasi zao na wanaanza kuzitetea kwa nguvu, wakati mwingine unapoona umeandamwa na vita za aina mbalimbali huenda wakati mwingine inasababishwa na watu wasiojihisi kuwa salama, na usalama wao ni mpaka wewe uwe pembeni maana unawazidi kwa kila jambo, jambo la kumshukuru Mungu ni kuwa Daudi hakuuchukua utukufu wa Mungu watu walimsifu yeye na jambo hili lingemfanya kujifikiri mkuwa yeyeni bora zaidi. Angekuwa na kiburi na neema ya Mungu ingemuacha!, Fikiria magomvi mengi yanayojitokeza kati ya wana ndoa kwa sababu tu mmoja ahajiamini, wivu unainuka na kusababisha vita na magombano, hatuna budi kumuomba Mungu atupe kujiamini na kumtegemea Mungu ni njia pekee ya kutuwezesha kujiamini! Unajisikiaje wengine wanaposifiwa?, unajisikiaje unapiokuwa na mtu amekuzidi mabo fulani?  Unajisikiaje mtu Fulani anapofanikiwa? Je inakukwaza au kukuumiza hii ni hali ya kuonyesha wazi kuwa hujiamini, hii ni moja ya tabia ngumu kuibadilisha lazima ukubali kuwa duniani kuna watu wana mambo mazuri kukuzidi na uridhike na kile ulicho nacho na kuwa mwaminifu tu katika talanta uliyokabidhiwa na Mungu! Kutokujiamini vilevile kulimfanya Sara aharibu sifa yake ya kuwa na ukarimu kama mama wa imani ni yeye aliyetoa wazo la Ibrahimu kuingia kwa Hajiri sawa na mila za kiibrania, lakini Hajiri aliposhika ujauzito sara alijihisi kuwa duni na hivyo alianza kumtesa Hajiri mpaka hajiri akakimbia ona Mwanzo 16:1-6 “Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri. Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai. Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe. Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake. Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi na wewe. Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake unaweza kuona kutokujiamini (insecurity) katika maisha ya mtu awaye yote inaweza ikatufanya tusiwe sisi katika uhalisia wake na tukajikuta tunaingia katika uadui au kutesa watu wengine kwa sababu tu za kutokujiamini! Na hivyo kunaweza kutuletea unajisi katika maisha yetu!

 

5.       Kukosa subira (intolerance)

 

Kukosa subira ni mojawapo ya adui mkubwa anayewatia watu wengi unajisi na kuwaacha watunwakashindwa kujitambua, kukosa subira kunaweza kutufanya tushindwe kusamehe, kushindwa kukubali mabadiliko na kujiweka katika ya kutokukubali mabadiliko, Maandiko yanatufundisha sana numuhimu wa kuwa na subira na biblia inatueleza wazi kuwa subira inalipa Yakobo 5:8-11 “Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango. Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu. Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.” Kutokuwa na subira au uvumilivu kumepelekea watu wengi sana kupoteza sifa zao, wakati mwingijne Mungu anaweza kuruhusu mitihani Fulani katika maisha yetu, ili kupima muelekeo wa moyo na utii kwa Mungu, hili suio jambo jepesi kama tunavyoweza kufikiri, wengi, wetu, tunahitaji neema ya Mungu wakati Fulani Sauli aliagizwa na Nabii Samuel, kwamba wamsubiri ilia je kutoa sadaka za kuteteketezwa kabla hawajaenda vitani, Lakini Samuel akachelewa kuja na askari wakaanza kutawanyika badala ya kupigana na wafilisti, kwaajili ya kushindwa kuvumilia Sauli aliamua kutoa sadaka ya kuteteketeza yeye mwenyewe, alipomaliza tu Samuel alitokea na kumwambia kuwa amefanya upumbavu na kuwa hakuitii sauti ya Mungu, kwa sababu agizo la Mungu kupitia Samuel nabii kwa Sauli lilikuwa hivi 1Samuel 10:8 “Nawe utatelemka mbele yangu mpaka Gilgali; nami, angalia, nitakutelemkia huko, ili kutoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja sadaka za amani; siku saba utangoja, hata nitakapokujia, na kukuonyesha yatakayokupasa kuyafanya”. Unaona Sauli alipaswa kusubiri maelekezo kutoka ka Nabii ambaye alikuwa ni msemaji kwa niaba ya Mungu, alipaswa kungoja, huenda kule kupangiwa kusubiri kwa siku saba ilikuwa ni kipimo cha kuona utii kwake lakini hata hivyo alisubiri hata siku ya saba bure, kwani dakika chache tu zilisalia Samuel angewasili, lakini Sauli alishindwa kuvumilia, alishindwa kuwa na subira, Dhambi hii ni yetu wote mara nyingi sana tumeshindwa kumsubiri Mungu au hata kungoja wakati wa Mungu na mara kadhaa tunataka kukabiliana na hali Fulani sisi wenyewe badala ya kufuata maelekezo ya Mungu 1Samuel 13:8-13 “Akangoja siku saba, kwa kadiri ya muhula uliowekwa na Samweli lakini Samweli hakuja Gilgali; na hao watu wakatawanyika mbali naye. Sauli akasema, Nileteeni hapa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani. Akaitoa sadaka ya kuteketezwa. Hata mara alipokwisha kuitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, kumbe! Samweli akatokea. Naye Sauli akatoka kwenda kumlaki na kumsalimu. Samweli akasema, Umefanya nini? Naye Sauli akasema, Ni kwa sababu naliona ya kuwa watu wanatawanyika mbali nami, na wewe hukuja siku zile zilizonenwa; nao Wafilisti wamekusanyika pamoja huko Mikmashi; basi nikasema, Wafilisti watanishukia sasa mpaka Gilgali, kabla sijaomba fadhili za Bwana; kwa hiyo nalijishurutisha, nikatoa sadaka ya kuteketezwa. Naye Samweli akamwambia Sauli, Umefanya upumbavu; hukuishika amri ya Bwana, Mungu wako, aliyokuamuru; kwa maana Bwana angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele.” Mmmh tunaweza kujifunza mambo kadhaa katika mfano huu wa sauliSubira na uvumilivu sio kitu rahisi, lakini ni wazi kabisa kuwa Mungu anatamani sana kuona utii wetu kwake anahitaji kuona uvumilivu wetu katika kuliamini na kulitendea kazi neno lake, lakini pia tunajifunza ya kuwa kuna hasara kubwa sana tunapoamua kufuata njia zetu kuliko njia za Mungu, japo sio rahisi kwa ubinadamu wetu lakini tunahitaji neema ili tumtii yeye na kuchagua njia aliyoichagua yeye lakini vinginevyo watu wengi sana wamejitia unajisi kwa sababu walishindwa au tumeshindwa kuwa na subira.

 

6.        Hasira (Anger)

 

Hasira ni mojawapo ya tabia ya kihisia ambayo inapaswa kuangaliwa kwa umakini na kila mwanadamu, inaonekana kila mwanadamu ana hasira lakini hasira ya kupita kawaida inaweza kutupelekea katika hali ya kutokuona mambo kwa uwazi zaidi, Paulo mtume alifahamu kuwa wakristo wanaweza kuwa na hasira lakini aliwataka waimalize hasira yao mapema na kuiondoa uchungu wote ikiwezekana kabla jua halijachwa ona Waefeso 4:26-27 “Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi.”Kukasirika kupita kawaida kunaweza kuwa nafasi ya shetani kutushambulia na tukajikuta tumefanya upumbavu, watu wengi kwa sababu ya kukasirika kwa haraka na a hata kufanya maamuzi wakiwa wamekasirika wamejikuta wakiharibu mambo maandiko yanatutaka tusifanye haraka kukaririka na lakini vilevile tusiiachie hasira kuleta madhara katika maisha yetu ona Muhubiri 7:9 “Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.” Wengi wetu tumeshuhudia na kuona mara kadhaa migogoro yenye madhara makubwa sana katika nchi yetu na mapigano ya kijinga yakifanyika kati ya wakulima na wafugani, unajua nini vita ya wakulima na wafugani ndio vita ya zamani zaidi kupata kutokea na ndio vita ya kwanza kurekodiwa katika kitabu cha mwanzo nilikuwa nikisoma stori ya Kaini na Abeli, na Roho wa Mungu akataka nichunguze kwanza maana ya majina yao nikaona jina Kaini linasomeka kama “qyn” kwa kiarabu na maana yake ni “metalsmith” au mfua vyuma na kazi yake kubwa ilikuwa ni shughuli za kilimo, na jina Abel “hbl” kwa kiarabu na maana yake ni “herdsman” au mfugaji na kazi yake ilikuwa ni shughuli za ufugaji, na ilikuwa rahisi sana kwa Kaini kumuua Habili kwa sababu Kaini alikuwa mtengenezaji wa silaha vilevile hapa tunapata picha ya mgogoro wa wakulima na wafugaji, lakini zaidi ya yote tunaona jinsi Hasira hasa aliyokuwa nayo Kaini ilivyopelekea kufanya upumbavu na kumtia unajisi, yeye alijaa ghadhabu na hasira na hakua tayari kutenda vizuri ili naye abarikiwe na Mungu ona Mwanzo 4:3-7 “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake; bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.” Unaweza kuona kumbe kila mara tunapokuwa na ghadhabu na kukasirika na uchungu mioyoni mwetu tufahamu kuwa vinaweza kutuletea hasara na tukajikuta tunatenda dhambi na hata kuyatia maisha yetu unajisi mkubwa, watu wengi sana wameharibu maisha yao na ya wengine kwa sababu ya hasira, Bwana ampoe kila moja wetu neema kuishinda hasira na ghadhabu katika maisha yetu katika jina la Yesu amen!

 

7.       Uadui (enmity)

Uadui ni hali ya kutokumpenda mtu au kumchukia mtu au watu kwa muda mrefu katika hali ambayo wakati mwingine sababu zake zinaweza kuwa wazi au zinaweza kutokuwa wazi, watu wanaweza kukuchukia bure tu, wakati mwingine sio kwa sababu unatenda mabaya lakini kwa sababu ya ule wema ulionao unasababisha wengine wajione duni Yesu alichukiwa bure tu bila sababu ona Yohana 15:25 “Lakini litimie lile neno lililoandikwa katika torati yao, Walinichukia bure.” Kwa namna yoyote ile maandiko yanatutaka tuhakikishe kuwa hatuna uadui na mtu, tuhakikishe kuwa tuna amani na watu wote ona Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;” kuwa na uadui katika maisha kunaharibu sana mwenendo wa uhuru wa mtu na kuyafurahia maisha, mtu wa haki anapaswa kuwatendea haki watu wote na bila kubagua kuwa huyu ni adui au laa  na maandika yanakwenda mbali zaidi kiasi cha kututaka kuwatendea mema adui zetu kwa kuwapa mahitaji yao ikiwezekana chakula wakiwa na njaa au maji wakiwa na kiu ona Mithali 25:21-22 “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na Bwana atakupa thawabu.” Hii maana yake ni kuwa hata kama mtu atatutendea vibaya hatupaswi kumlipa mabaya na badala yake hata kama ni kisasi basi hatuna budi kumuachia Mungu alipe  lakini sisi tutende yaliyo mema ona Mithali 20:22 “Usiseme, Mimi nitalipa mabaya; Mngojee Bwana, naye atakuokoa.” Kipimo cha wema wa kiagano jipya kinatutaka kwenda zaidi ya kawaida yaani ikiwa ni pamoja na kuwapenda, na kuwaombea na kuwa kwa kutenda hayo tutakuwa wakamilifu kama baba yetu wa Mbinguni alivyo mkamilifu! Mathayo 5:43-48 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.” Kuendeleza uadui katika maisha yetu na kutokutafuta kuwa na amani na watu wote kumeyaweka na kuyaharibu maisha ya watu wengi pabaya na kusababisha madhara makubwa kwa jamii, Bwana atupe neema na kutusaidia kuwa na utulivu pande zote na tusiwe na roho ya uadui!

8.       Kuhukumu wengine (Prejudice)

 

Kuhukumu wengine kwa kiingereza neno linalotumika ni prejudice ambalo kwa mujibu wa Dictionary ya Oxford maana yake inasomeka – preconceive opinion that is not based on reason or actual experience, giving an opinion about someone which is covered with bias. Kwa tafasiri isiyo rasmi ni kutoa mawazo, au maelezo kuhusu mtu ambayo huna uthibitisho au utafiti wa kina kuwa yana ukweli au usahihi, au kutoa hukumu katika mtazamo wa fikra zako, Kwa mfano mtu anaweza kuwa na tatizo la iana Fulani au ulemavu wa aina Fulani na tukafikiri kuwa amepatwa na ulemavu huo kwa sababu yeye au wazazi wake walifanya dhambi Fulani Yohana 9:1-3 “Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.” Hapa tunaona wazi kuwa kwa mtazamo wa wanafunzi wa Yesu au wayahudi kwa ujumla walikuwa wanadhani ikitokea mtu ana tatizo basi walihesabu kuwa ni laana ya kiungu au ni adhabu inayotokana na dhambi, kwamba huyu alikuwa mlemavu au kipofu tangu kuzaliwa walidhani ni labda huenda wazazi wake au yeye mwenyewe amefanya dhambi, Lakini mtazamo wa Yesu Kristo ulikuwa tofauti sana, hivi ndivyo tulivyo wanadamu, tunahukumu kwa haraka wakati mwingine tukifikiri kuwa tuko sahihi, wakati Fulani nilipiokuwa Korea moja ya wanafunzi nwa chuo cha Biblia cha Methodist aliyekabidhiwa sisi ili kututembeza sehemu mbalibali alikuwa na tattoo kubwa limechorwa mwilini mwake, na kwa haraka sana nilifikiri kuwa huenda mtu huyu hajaokoka na au kama atakuwa ameokoka basi kiwango mcha wokovu wa watu hawa kiko chini, mno wanawezaje kutupa mtu wa aina hii na tena anayeonekana mhuni, na tena yuko chuo cha Biblia? Ukweli ni kuwa mtu yule alikuwa ameokoka na anayeokoa ni yesu Kristo na yhakunamkiwango cha thamani ya wokovu wa mahali Fulani kwani wote tumeokolewa kwa damu ya Yesu, mtu huyu alikuwa ameokolewa na Yesu kutoka katika janga la uhuni uliokuwa umepindukia na sasa alikuwa ni mtu mwema na hata kule kututembeza walikuwa wakiangalia usalama wetu, sio kila mtu aliyechorwa tattoo ni mhuni au ni mtu mbaya kumbe wengine ni watumishi wa Mungu wametolewa huko duniani na wamekuwa kiumbe kipya, kuhukumu wengine au kuwa na mawazo mabaya dhini yaw engine kunaweza kutuweka katika upande usio sahihi wa kimtazamo kuliko vile Mungu anavyotazama mambo,angalia kisa hiki kwa mfano:- Luka 7:36-48Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani. Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu. Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusu-busu miguu yake na kuipaka yale marhamu. Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi. Yesu akajibu akamwambia, Simoni, nina neno nitakalo kukuambia. Akasema, Mwalimu, nena.  Akasema, Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili; mmoja amwia dinari mia tano, na wa pili hamsini. Nao walipokuwa hawana cha kumlipa, aliwasamehe wote wawili. Katika hao wawili ni yupi atakayempenda zaidi? Simoni akajibu akasema, Nadhani ni yule ambaye alimsamehe nyingi. Akamwambia, Umeamua haki. Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, Wamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake. Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu yangu. Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu. Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo. Kisha alimwambia mwanamke, Umesamehewa dhambi zako.” Umeona! Simon alikuwa mtioza ushuru aliyemualika Yesu kwenye karamu ya jioni na mara anaingia mwanamke kahaba anasimama karibu na Yesu, moyoni Simon anajihoji hivi nimealika nabii au chokoraa maana kama huyu jamaa angelikuwa nabii angejua kuwa mwanamke huyu ni wa kufukuza tu maana hafai, Lakini Yesu alitambua kile kilichokuwa kinaendelea katika mawazo ya Simeon, alionyesha wazi kuwa huyu mwenye dhambi nyingi hivi zikisamehewa atampenda Yesu kwa kiwango kikubwa zaidi!, wakati mwingine tumefikiri vibaya kuwa watu wenye dhambi kubwa sana hawawezi kusamehewa na Mungu, au tumefikiri kwa kuwa tumeua hatuwezi kusamehewa ndio maana katika mitazamo ya kiungu biblia inatuonya juu ya kuhukumu wengine kwa haraka Mathayo 7:1-5Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?  Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?  Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.” Unaona maandiko ni kama yanatutaka kujitathimini wenyewe kwa kina zaidi tunapoona shida kwa wenzetu na kujishughulikia sisi zaidi ili ikiwezekana ndipo tuone vema kushughulikia ya wengine kama sisi tuna yetu ya kuyashughulikia na tukaacha na kujihusisha na ya watu wengine huo ni unafiki, kwa hiyo ni lazima tujifunze kuacha kuhukumu wengine, wakati mwingine hata kama kile tunachokihukumu kina ukweli, maandiko yanatuonya kuwa sio kazi yetu kushughulikia hilo kwani Mungu mwenyewe ana njia sahihi ya kushughhulikia mambo ona Warumi 14:4 “Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.”

 

9.       Zinaa/Uasherati (Adulterry and Sexual immorality)

 

Kwa mujibu wa mafundisho ya Yesu Kristo, Zinaa na uasherati ni miongoni mwa mambo yanayomtia mtu unajisi, kwa lugha nyingine yanayoharibu na kumchafua mwanadamu, uasherati na zinaa katika lugha ya kiyunani vinaitwa “PORNEIA” kwa kiingereza sexual immorality , hii inajumuisha maswala ya kufanya ngono nje ya utaratibu unaokusudiwa na Mungu, inajumuisha swala zima la kuangalia picha za ngono kumbuka neno Porneia ndilo mzizi wa neno la kiingereza Pornography, via vya uzazi ni zawadi kutoka kwa Mungu, lakini Mungu alikusudia kuwa vitatumika kwa utaratibu maalumu, nje ya utaratibu maalumu zinaa na uasherati humtia mtu unajisi, na ndio maana torati ilikataza zinaa Kutoka 20:14 “Usizini” Hata hivyo kwa maelezo ya Yesu Kristo zinaa inatoka ndani, inatoka moyoni na isipodhibitiwa huweza kumtia mtu unajisi, na ndio maana Yesu akataka kulishughulikia jambo hili kutoka ndani Mathayo 5:27-28 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” Kwa lugha nyingine Yesu alikuwa anataka kila mmoja ajue kuuweza mwili wake yaani aweze kuidhibiti akili, aweze kuidhibiti tama ili tama hiyo isizae dhambi na kuleta uharibifu ona Yakobo 1: 13-15 “Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.” Unaona Zinaa na uasherati hukaa moyoni, na kwaajili ya hayo, Yesu alitaka kila mmoja ajue namna ya kuudhibiti moyo wake ili asifikie ngazi ya kujitia unajisi, kwa kawaida zinaa huweza kuathiri maeneo matano Muhimu katika maswala ya kimwili na kiroho

a.       Inaharibu uhusiano wetu na Mungu kwa sababu ni Mungu aliyeelekeza katika neno lake kuwa tusizini kwa msingi huo tunapofanya zinaa, maana yake tunaharibu uhusiano wetu na Mungu na kuhesabika kama wavunja sharia au mtu aliyelidharau neno la Mungu 2Samuel 12:9 “Kwa nini umelidharau neno la Bwana, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa wana wa Amoni.” Unaona Daudi alipofanya zinaa nabii alimhoji kwanini umelidharau neno la Bwana, kwa hiyo zinaa na uasherati unapofanyika mtu huathiri uhusiano wake na Mungu

b.      Inaharibu maisha yako ya ndani - 1Wakoritho 6:18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.” Maandiko yanatufundisha kuwa zinaa na uasherati unaharibu maisha yetu ya ndani, andiko hili linazungumzia kuwa mtu akifanya zinaa anatenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe! Neno mwili katika lugha ya kiibrania ni “NEPHES” ambalo maana yake ni nafsikwamba zinaa na uasherati ni dhambi inayoharibu nafsi yaani inakamata akili na kuinajisi akili na kuifanya akili yako kutawaliwa na dhambi hiyo na hivyo kutoa nafasi ya kuirudia tena na tena hivyo kuliharibu Hekalu la Mungu,  kwa hiyo kufanya zinaa ni kuangamiza nafsi yako kabisa ona Mithali 6:32Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.” Unaona maandiko yuako wazi kuwa unaharibu nafsi yako!

c.       Inaharibu uhusiano wetu na wengine – ni muhimu kufahamu kuwa kusudi lingine kubwa la Mungu kukataza zinaa ni kulinda uhusiano wetu na watu wengine, unapofanya zinaa au uasherati unaharibu mahusiano, lakini sio hivyo tu utavunjiwa Heshima watu watakudharau na kukupuuza watakapogundua kuwa huna adabu hujiheshimu na wanaweza kukudhani kuwa wewe ni Malaya au kahaba, Mithali 6:32-33 “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.”

d.      Inaharibu huduma na ushuhuda – Mungu anatarajia kila mtu mwadilifu kuwa ni chumvi ya ulimwengu na nuru ya ulimwengu, kuwa sisi tutauangazia ulimwengu na kuwa kielelezo au mfano wa kuigwa hivyo sisi tunasioma na ulimwengu, ulimwengu unaangalia na kujifunza kutioka kwetu 2Wakoritho 3:2-3 “Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote;” unaweza kuona kwa msingi huo Neno la Mungu halitaki wakristo wasomwe vibaya na wala mambio mabaya yasitajwe kwetu kamwe Waefeso 5:3-5 “Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;  wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru. Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.” Kwa misingi hiyo sasa ni muhimu kwa kila mtu mwenye kupendezwa na uadilifu kujilinda na zinaa na uasherati kwani vinaharibu na kunajisi mioyo yetu nay a watu wengine.

 

10.   Ushirikina “Witchcraft” – Ni hali ya kuacha kumtegemea Mungu na kutegemea vitu vingine, au kuchanganya kati ya mambo ya Mungu na miungu au mashetani, kwa kiingereza witch craft, Sorcery, spiritism, black magic, bad eye, fellowship with demons kwa kiyunani “PHARMAKEIA” kwa mujibu wa maandiko ushirikina pia hupelekea mtu kuharibu maisha yake na kujichafua au kujitia unajisi, maandiko yanatukataza kushirikiana na mashetani 1Wakoritho 10:20-21 “Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.” Kitendo cha kumshirikisha shetani katika mahitaji yako au tamaa zako ndio kinaitwa ushirikina yaani wewe mwanadamu ni mali ya Mungu, lakini badala ya kumtegemea Mungu kukuitana na mahitajhi yako unamtegemea shetani au nguvu za giza, Mungu hapendezwi na watu washirikiana na hivyo kushiriki mambo ya kichawi ni kujitia unajisi katika uhusiano wako na Mungu na wanadamu Walawi 19:31 “Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.” Unaona maandiko yanaonyesha kuwa kuwaendea waganga yaani wenye npepo na wachawi kutaleta unajisi, wataharibu uwezo wako wa kumtegemea Mungu, kuwaendea waganaga na wachawi kwaajili ya kutafuta msaada kunaleta hukumu ya Mungu kwa haraka sana , kunajenga imani bandia ya kinafiki isiyotokana na neema wala nguvu za Mungu, Mungu alitangaza hukumu kwa watu kadhaa na kifo kwa sababu walipokuwa na shida hawakwenda kuutafuta uso wa Mungu bali mashetani ona 2Wafalme 1:2-4 “Na Ahazia akaanguka katika dirisha la chumba chake orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu. Lakini malaika wa Bwana akamwambia Eliya Mtishbi, Ondoka, uende ukaonane na wale wajumbe wa mfalme wa Samaria, ukawaambie, Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Basi sasa, Bwana asema hivi, Hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa. Eliya akaondoka.” Ukweli ni kuwa Mungu alichukizwa na mfalme Ahazia kutokana na moyo wake wa kijinga wa kutokumtegemea Mungu na kutegemea nguvu za giza na hivyo alihukumiwa kufa, Sauli mfalme wa Israel naye alikataliwa na Mungu na kufia vitani kwa sababu moyo wake haukumtii Mungu na hivyo aliamua kwenda kwa mpiga ramli ilimkuuliza huko na aliambiwa kuwa Bwana amekuwa adui yake 1Samuel 28:5-16 “Basi alipowaona hao majeshi ya Wafilisti, huyo Sauli akaogopa, na moyo wake ukatetemeka sana. Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii. Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori. Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako. Yule mwanamke akamwambia, Angalia, unajua alivyofanya Sauli, jinsi alivyowakatilia mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi; mbona basi wanitegea tanzi uhai wangu, ili kuniua? Naye Sauli akamwapia kwa Bwana, akasema, Aishivyo Bwana, haitakupata adhabu yo yote kwa jambo hili. Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli. Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli. Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi. Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia. Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje. Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako? ” Ushirikina ni zinaa ya kiroho, Mungu ameapa katika neno lake kuwa ataukaza uso wake yaani hatakuwa na rehema kwa mtu atakayewaendea wachawi au waganga ona Walawi 20:6 “.Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake.” Unaiona uso wa Mungu utakazwa dhidi ya mtu mshirikina sio hivyo tu mawasiliano yoyote na wenye pepo au waganga ni machukizo kwa Mungu Kumbukumbu la torati 18:10-12 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.” Unaweza kuona ni wazi kabisa kuwa Mungu anachukizwa mno na ushirikina, nani jambo la kushangaza kama mtu ajiita mkristo au hata muislamu kisha akawa mshirikina kwani vitabu vyote vimekataza maswala kama haya, tulisoma kisa cha sauli na maandiko ynaweka wazi kuwa sababu ya kifo chake ilichangiwa pia na kuwaendea waganga 1Nyakati 10:13-14 “Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa Bwana, kwa sababu ya neno la Bwana, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake, asiulize kwa Bwana; kwa hiyo akamwua, na ufalme akamgeuzia Daudi, mwana wa Yese.

 

11.   Dharau au Kutokujali “insensitivity” – Moja ya maswala yanayoweza kuwatia watu unajisi ni pamoja na dharau, au kutokujali insensitivity jambo hili pia huondoa thawabu ya Mungu na kutukosesha neema kama mtu akiwa na Dharau na majivuno ya ndani yenye tabia ya kupuuzia vitu au kitu, mtu mwenye dharau hachukui tahadhari, hajilindi, hafikiri katika kile anachofanya jambo ambalo linaweza kuwa lenye kuleta madhara, Mithali 3:34 “Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema.” Biblia inaonyesha kuwa kwa sababu ya dharau pia watu hujinyima nafasi ya kujifunza na kupokea maarifa na hekima kutoka kwa Mungu Mithali 1:7 “Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.” Watu wengi sana nyakati za Yesu walishindwa kupokea neema ya kumjua Yesu kwa sababu tu walidharau hata kule alikotokea na kwa sababu hiyo Yesu hakufanya miujiza mingi kwa sababu hawakumuamini yaani walimdharau Mathayo 13:54-58. “Na alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii? Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda? Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote? Wakachukizwa naye. Yesu akawaambia, Nabii hakosi kupata heshima, isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake mwenyewe. Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwaomtu mwenye dharau anaweza kukudharau hata kutokana na eneo unalotokea, Yesu alitokea kwenye mji usioheshimika sana na ambao hauna historia ya kutoa nabii, kwa hiyo iliposemekana kwamba anatokea Nazareth watu walipuuza na kudhani kuwa haijawahi kutokea nabii akatokea huko!, Yohana 7:46-52 “Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena. Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika? Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo? Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa. Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao),Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo? Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya! Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.” Dharau ya viongozi wa dini na baadhi ya mafarisayo kuhusu eneo Fulani liliwanyima uwezo wa kumkubali masihi, na hivyo walibaki katika dhambi yao kwa kutokumuamini Yesu, wengi wetu tunaweza kuwadharau wengine kwa sababu ya hali zao, muonekanio wao, upole wao, kabila lao, historia yao na kule wanakotokea! Yohana 1: 45-46 “Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone.” Kwa bahati njema Nathanieli na filipo walimuamini Bwana Yesu lakini jamii yao ilikuwa imeelekezwa wazi kuwa hakuna kitu chema kinaweza kutokea huko hivyo wengi walidharau na kuikosa neema ya kumjua masihi, dharau imewanajisi wengi na kuwafanya wengi kupoteza mahusiano na Mungu au wanadamu wengine hatupaswi kupuuzia au kutokujali, na ndio maana ni muhimu kwetu kumuheshimu na kumsikiliza kila mtu kwa vile hatuwezi kujua nani atakuwa nani siku moja! Kudharau kumetufanya tusiwajali wengine, kumetufanya pia tuache kutioa kipaumbele kwa mambo ya muhimu kwa sababu ya kudhau kwetu!

 

12.   Kutokusamehe (Unforgiveness)

 

Kutokusamehe kunaharibu maisha ya mtu, kunatuweka katika kifungo! kutokusameheni moja ya maswala yanayomtia mtu unajisi, tunajisikia amani na furaha tunaposamehe, na tunaposamehewa, kwa msinmgi huo maandiko yanatufundisha umuhimu wa kusamehe wengine, Ni msamaha ndio unaotupa ufunguo na neema ya kupokea msamaha na sisi kutoka kwa Baba wa Mbinguni  Mathayo 6;14-15 “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.” Kuna shida kubwa sana tusiposamehe Bwana Yesu katika mafundisho yake anatupa stori inayotufundisha umuhimu wa kusamehe,kwa sababu sisi nasi tunahitaji kwa namna Fulani kusamehewa na Mungu baba yetu wa mbinguni, maana kumbuka hakuna mwanadamu aliyemkamilifu, sisi tumemkosea Mungu mara nyingi sana na hivyo ili iweze kuwa rahisi kwetu kusamehewa na Mungu ni muhimu sana na sisi tukasamehe wanaotukosea ona Mathayo 18:23-35 “Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi.Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni. Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia akamkamata,akamshika koo,akisema Nilipe uwiwacho. Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni.  Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake

Kutunza uchungu wa kutokusamehe sio tu kunaendeleza uhasama kati yako na aliyekukosea bali kunakuharibu wewe mwenyewe na kukutia unajisi, kutkusamehe kunakufanya uwe mtumwa wa watu, kutokusamehe kunakufanya uwe chini ya udhibiti wa mtu yaani dunia inakuwa chungu anapotokea mtu unayemchukia usiyempenda na usiyemsamehe, kutokusamehe kunakufanya uwe mfungwa katika gereza lake, unafungwa katika huzuni, unafungwa katika gereza la kukosa amani, unafungwa katika gereza la vita vya moyoni, unafungwa katika gereza la hasira, unafungiwa nje ya furaha na ushirika, uchungu huu ni matokeo ya kiburi na kujihesabia hakli au kutokutaka kupoteza haki zako, na kutaka kulipiza kisasi, kusamehe ni kukubali kupoteza haki zetu, ni kukubali kuachilia ili mtu mwingine asi tu control, na hivyo tutakuwa free kwa mtu huyo na kwa Mungu pia.

               

13.   Choyo (Greed).

 

Moja ya vitu ambavyo pia huutia moyo unajisi ni pamoja na tabia ya kupenda kujilimbikizia kila kitu sisi wenyewe, tabia ya choyo, choyo kinawafungia watu wengi Baraka za Mungu, Yesu amewahi kuonya kuwa uzima wa mtu hauko katika wingi wa vitu anavyomiliki akituonye dhidi ya tabia ya choyo ona Luka 12:15 “Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.” Utoaji na kuwahudumia wengine hutuletea furaha ya kweli, angalia kisa hiki cha tajiri mmoja

 

Bilionea MNigeria Femi Otedola alipoulizwa kwenye interview, ya Simu na Mtangazaji wa Radio, "Sir ni kitu gani unachokumbuka  kilichokufanya uwe na furaha maishani?" Femi alijibu:

"Nimepitia hatua nne za furaha katika maisha yangu na mwishowe nilielewa maana ya furaha ya kweli." Hatua ya Kwanza ilikuwa ni kutafuta Mali na kulimbikiza. Lakini katika hatua hii sikupata furaha niliyoihitaji. Nikaingia hatua ya pili ya kujinunulia vitu vya thamani. Lakini niligundua kuwa vitu vyote hivi vinakupa furaha ya muda tu ambayo haidumu. Nikaingia hatua ya tatu ya kufanya miradi mikubwa. Ni katika hatua hii nilikuwa ninasambaza 95% ya Diesel Nigeria yote na Africa Kwa ujumla. Pia nilikuwa mmiliki mkubwa wa Vessel Africa na Asia. Lakini pia hapa sikupata furaha niliyokuwa nimeifikiria. Hatua ya nne ilikuwa ni kipindi ambacho Rafiki aliniomba kununua Wheelchairs Kwa ajili ya watoto walemavu. Walikuwa kama watoto 200 hivi. Baada ya kuombwa na rafiki yangu nilinunua Wheelchairs 200 mara moja. Lakini pia aliniomba niambatane naye ili nikawakabidhi watoto zile wheelchairs. Nilijiandaa nikaambatana naye.  Nikawagawia zile wheel chairs Kwa mikono yangu mwenyewe. Niliona furaha ikitawala kwenye nyuso za hawa watoto. Nikawaona wamekaa kwenye wheelchairs, wakizunguka na kufurahia. Ilikuwa ni kama wako Picnic wakisherehekea ushindi wa bahati nasibu. NiIihisi furaha ya kweli ndani yangu. Nilipotaka kuondoka mtoto mmoja alinishika miguu yangu. Nilijaribu kujinasua taratibu lakini alinikazia macho akinitazama usoni. Niliinama chini nikamuuliza, kuna kitu kingine unahitaji? Jibu alilolitoa mtoto huyu sio tu kwamba lilinipa furaha bali pia lilinifanya nibadili kabisa mtazamo wangu juu ya maisha. Mtoto huyu alisema:  "Ninakuangalia ili niikumbuke Sura yako, siku nikikukuta mbinguni niweze kukutambua na kukushukuru tena." Maandiko yanasema ni heri kutoa kuliko kupokea

 

 Matendo 20:34-35 “Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami. Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.”            

 

Utoaji unaleta Baraka za kiungu, utoaji ni kuwatangauliza wengine au kumtanguliza Mungu kwanza kabla yetu, kutokutoa ni ubinafsi, tunapotoa Mungu hufungua milango ya Baraka kwetu na kututumia kama bomba la kutiririsha Baraka utoaji ni moyo na sio hali ya kuwa na kitu, wako watu wana moyo na wako tayari hata kile kiduchu alichonacho aweze kushirikiana na wengine ona 1Wafalme 17:8-16Neno la Bwana likamjia, kusema, Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe. Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa.  Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako. Naye akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe. Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao. Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi.  Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi. Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya.”  Tunapomtanguliza Mungu katika utioaji Mungu hatatuacha na kamwe hatutapungukiwa na kitu, utoaji wa kikarimu kama huu aliokuwa nao mjane wa Sarepta umeweza              umeweza kuwekwa Rekodi zake katika maandiko kwa sababu ulikuwa ni utoaji wa namna ya pekee sana utoji unaleta Baraka na kwa sababu hiyo Mungu na atupe neema ya kutokuwa wabinafi na atulinde na choyo katika jina la Yesu amen!

 

14.   Kiburi (Pride)

 

Moja wapo ya maswala ya msingi naya muhimu ambayo katika maisha yetu tunapaswa kujihami nayo siku zote ni kiburi, kiburi ni mojawapo ya tatizo na changamoto ambayo imewatia wengi unajisi, ni ukweli usiopingika kuwa mtu akiwa na majivuno na kiburi moja kwa moja anakuwa adui wa Mungu hata kabla ya kuwa adui wa shetani 1Petro 5:5 “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”  Unaona kiburi kinatutenga na neema ya Mungu, na kwa kawaida kiburi huenda pamoja na maangamizi, kila wakati huwa ninaogopa sanasana ninapoipitia Biblia na kuona jinsi Mungu anavyoonya katika neno lake na nnamuomba sana Mungu anilinde na maangamizi ya aina hii, inaonekana wazi kabisa hakuna neema wala rehema kwa mtu mwenye kiburi, biblia ni kama inatangaza vita na kueleza wazi kuwa kama una kiburi hautatoboa, inaelezea wazi kuwa kuna maangamizi pale kiburi kinapokuwepo ona Mithali 16:18-19 “Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko. Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi.” Unaona kuna uangamivu na maanguko hii inatisha ujue ni lazima kuomba rehema kila wakati kwa sababu Biblia inaonyesha pia kuna kuaibishwa kwamba kijapo kiburi ndipo ijapo aibu ona Mithali 11:2 “Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.” Kwa mujibu wa maelezo ya kibilia ni dhambi hii ilianza kujipenyeza ndani ya moyo wa ibilisi na kwa kweli hukumu yake haikukawia Isaya 14:13-15 “Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.” Unaweza kuona shetani kwa kiburi alijiambia moyoni tendo hili, la kujieleza moyoni Mungu alilichungulia na kuleta hukumu kwa haraka, Luka 14:11 “Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.” Shetani alijiinua kinyume na mamlaka kwa kiburi chake na hivyo aliharibiwa na kushushwa Ezekiel 28:13-18 “Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari. Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako. Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto. Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama. Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.” Mungu alimhukumu shetani na kumtupilia mbali kwa sababu ya moyo wake wa kijiinua moyo wake wa kujivuna na kiburi, kiburi ni tatizo ambalo ni vigumu sana kulijua au kujijua linapokuwa limekuingia lakini kuna dalili chache zinazoweza kutusaidia kujielewa kama kimetuingia

-          Kutokulitetemekea neno la Mungu Isaya 66:1-2 “Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani? Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.”          

-          Kutokubali kushauriwa – Mithali 13:10 “Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.

-          Hujifikiri kuwa yeye ni bora zaidi ya watu wengine – Wafilipi 2:3-11 “Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”

-          Hujawa na maneno ya kujivuna wao tu – 1Samuel 2:3 “Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.”

-          Hujifikiri kuwa wanajua kila kitu 1Wakoritho 8:2 “Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua.”

-          Wana majivuno na ukaidi Mithali 8:13 “Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.”

-          Hawampi Mungu utukufu na hufikiri kila kitu wamefanya kwa uweza wao - Isaya 10:13 “Kwa maana amesema, Kwa nguvu za mkono wangu nimetenda jambo hili, na kwa hekima yangu; maana mimi nina busara; nami nimeiondoa mipaka ya watu, nikaziteka akiba zao, nikawaangusha waketio juu ya viti vya enzi kama afanyavyo shujaa.”

-          Hufikiri kuwa njia yake ni sahihi zaidi – Mithali 16:25 “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti.”

Madhara ya kiburi   Mungu atatoa adhabu – Mithali 16:5 “Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu.”, kiburi kinaleta uharibifu Mithali 18:12 “Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.” Mungu alimshughulikia Mfalme Nebukadreza kwa sababu ya Kiburi Daniel 4:28-33 “Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza. Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu? Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako.  Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng'ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote. Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.”    

Bwana atupe neema kuwa mbali na mambo yote yanayotia unajisi na kutuletea madhara ya aina mbalimbali katika maisha yetu sawa sawa na mapenzi yake na atupe neema ya kuishi maisha matakatifu na ya kumpendeza yeye na kutulinda na kiburi na majivuno na atupe neema ya kuwa wanyenyekevu katika jina la Yesu Kristo amen!

 

Na. Rev. Innocent Kamote

 

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima