Yohana 14:16-18 “Nami nitamwomba Baba, naye
atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli;
ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali
ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. Sitawaacha ninyi
yatima; naja kwenu.”
Utangulizi:
Leo tutachukua Muda tena
kujifunza kwa kina na mapana na marefu, tukikazia tena na tena umuhimu wa Mungu
Roho Mtakatifu katika maisha yetu, Ambaye Bwana Yesu alimuita Msaidizi mwingine,
kanisa ni muhimu sana sana kufahamu na kutoa nafasi kwa Roho Mtakatifu kwa
sababu yeye ni msaada mkubwa sana wa kutuondolea mashaka na kutupa neema ya
kuishi kwa Amani.
Yohana 14:16-18 “Nami nitamwomba Baba, naye
atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli;
ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali
ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. Sitawaacha ninyi
yatima; naja kwenu.”
Wanafunzi wa Bwana wakiwa pamoja
naye katika karamu yake ya mwisho pamoja nao. Yesu anawaeleza kuwa amekamilisha
kazi aliyotumwa na baba na kuwa kilele cha kazi aliyotumwa ni kufa msalabani
kwaajili ya wengi, wanafunzi waliposikia kuwa Yesu anazungumza maswala mengi
yanayohusu kuhitimisha huduma yake duniani, walipata mashaka na huzuni nyingi,
walifadhaika na kujiona kupwaya na kuwa dhaifu, itakuwaje maisha yao bila Yesu?,
nani atakuwa pamoja nao, nani atawasaidia, nani atawashauri, nani atakuwa
karibu nao, nani atawatia moyo, nani atawafundisha na kuwaelekeza, na
wanawezaje kuukabili ulimwengu ambao ni mgumu bila msaada wa Mungu, kukabiliana
na wakuu wa dini za kiyahudi, kukabiliana na upinzani wa kiimani na kidhehebu,
watu wenye kuipinga injili na habari za Mungu, akijua kila kilichokuwa kinaendelea
katika mioyo yao, Yesu aliwathibitishia kuwa atamuomba baba naye atawapa
msaidizi mwingine ili akae nasi milele.
Roho Mtakatifu ndiye Msaidizi
huyo, Roho Mtakatifu ni wa Muhimu sana sana katika maisha yetu, hakuna lugha ya
kuweza kuelezea vya kutosha lakini ikiwa Yesu anasema yafaa au yatufaa au
yawafaa yeye aondoke kwa kuwa asipoondoka msaidizi hatakuja kwetu, maana yake
Msaidizi huyu ni wa Muhimu na msaada ulio karibu zaidi tukinena kiwazimu kuliko
uwepo wa Yesu Kristo duniani, Uwepo wa Yesu Kristo duniani akiwa kama mwanadamu
ulimfunga na kumpa mipaka ya kuwepo katika inchi ya Israel tu, vilevile
kutokuweza kukaa moyoni mwa kila muumini, Lakini uwepo wa Roho Mtakatifu ambaye
hayuko katika mwili, unamuwezesha kuwepo kila mahali na kuwepo ndani ya moyo wa
kila aaminiye na kutimiza mambo makubwa sana katika kiwango kile kile alichokuwa
anakifanya Yesu Duniani kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Ndio maana Yesu akasema
yafaa yeye aende, ili Roho Mtakatifu aweze kuchukua nafsi na kukaa nasi hata
milele unaona ?
Yohana 16:6-7 “Ila kwa sababu nimewaambia
hayo huzuni imejaa mioyoni mwenu. Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa
ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu;
bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.”
Neno yawafaa, au yafaa Katika kiingereza linatumika neno expedient ambalo kwa kiyunani
linasomeka kama Sumpherō ambalo tafasiri yake kwa
kiingereza ni to be good, Be profit, be
profitable, be better yaani kwa Kiswahili, yafaa, ni afadhali, ni faida, ni vema zaidi, ni bora zaidi kwa
hiyo kuondoka kwa Yesu ni bora zaidi, ili aje Roho Mtakatifu kuliko kuendelea
kuweko kwa Yesu Duniani, katika jinsi ya mwili, ikiwa Yesu aliona umuhimu wa
swala hili basi kanisa ni muhimu kwetu kuelewa kuwa Yesu alikuwa Mwalimu bora
zaidi kuliko wote duniani, ni mwafalasafa mkubwa zaidi kuliko wote, ni mtenda
miujiza mikubwa kuliko mtu awaye yote duniani ana sifa ambazo hakuna mwanadamu
awaye yote anazo duniani lakini anasema ni afadhali yeye aende kuliko kubaki
ili aje Roho Mtakatifu ambaye ndiye msaidizi, basi kuna umuhimu mkubwa sana wa
kulizingatia hili, kwa sababu hiyo leo tutachukua muda kujifunza kwa kina na
mapana na marefu somo hili muhimu Msaidizi mwingine kwa kuzingatia vipengele
vitatu vifuatavyo:-
·
Msaidizi
mwingine.
·
Umuhimu
wa kuwa na Msaidizi mwingine.
·
Jinsi ya
kuwa na msaidizi mwingine.
Msaidizi mwingine
Yohana 14:16-18 “Nami nitamwomba Baba, naye
atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli;
ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi
mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. Sitawaacha ninyi
yatima; naja kwenu.”
Msaidizi mwingine anayetajwa
katika maandiko haya ni Roho Mtakatifu, neno Msaidizi mwingine katika
kiingereza linatumika kama neno “Another
Comforter” ambalo kimsingi katika kiyunani linasomeka kama Parakletōs
ambalo katika kiingereza tafasiri zake ni Consoler, an intercessor, advocate, tafasiri zake one called to the side of another for the
purpose of helping him in any way Kwa Kiswahili sasa maana ya Msaidizi
mwingine ni Mfariji, mtetezi,
mwanasheria, wakili, rafiki, na mshauri, Kwa hiyo ni wazi kuwa Yesu
anamuelezea Roho Mtakatifu kama nafsi nyingine itakayosimama kwa niaba ya
kanisa na kuwatetea, kuwafariji, kuwatia nguvu, kuwashauri na kuwapa cha kusema
au kusema kwa niaba yao hata wanapokuwa katika kumbi za kimahakama, au katika
mabaraza na mbele ya maliwali, Roho Mtakatifu atakuwa kama wakili wakati huo.
Na sio wakili atakayehitaji malipo bali anayefanya hivyo kwa sababu ya upendo
wake Mungu, na kuwashauri watu wake kipi cha kutamka na kwa jinsi gani watamke
na kuwashinda wale wanaowashambulia, Biblia ya kiingereza the Amplified Bible
inatumia maneno haya katika kiingereza “And I will ask the Father, and he will give
you another Helper (comforter, Advocate, Intercessor, Counselor, Strengthener,
standby ) to be with you forever ” na Biblia ya kiaramu the Aramaic Bible inasema
hivi katika kiiingereza “ And I shall
request from my Father and he will give you another Redeemer of the accursed,
that he will be with you for eternity” kwa hiyo Roho Mtakatifu ni Mfariji,
ni wakili, ni muombezi, ni kiongozi, ni mtia moyo, ni msaada ulio karibu, Roho
Mtakatifu ni Mkombozi mwingine dhidi ya mshitaki wetu. Kwa hiyo Roho Mtakatifu
ambaye atakaa ndani yetu atatusaidia kutimiliza kile kile ambacho Kristo
angetenda akiwa pembeni yetu.
Mathayo 10:17-20 “Jihadharini na wanadamu;
kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga; nanyi
mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao
na kwa mataifa. Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi
mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. Kwa kuwa si ninyi msemao, bali
ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.”
Matendo 6:8-10 “Na Stefano, akijaa neema na
uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu. Lakini baadhi ya
watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la
Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na
Stefano;lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye.”
Katika lugha ya kiebrania neno
hilo Msaidizi linatajwa kama neno “Ezer”
ambalo maana yake ni Msaada au msaada ulio karibu kwa hiyo Roho Mtakatifu
ni Msaada ulio karibu, ni msaada wa kimwili na kiroho na kihekima na kiushauri na kimuelekeo, na
kiuaffanuzi, na kiualimu, na hutusaidia katika udhaifu wetu, hutusaidia na
kututia nguvu wakati wa mateso na kutuongoza katika kweli yote, Kimsingi Roho wa
Mungu ni msaada kamili kama ule tu ambao ungepatikana kwa Mungu baba na Mungu
mwana yaani Yesu kristo. Roho Mtakatifu ndani yetu katika roho ni muhimu kuliko
Yesu Kristo pembeni yetu katika mwili.
Zaburi 46:1-2 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio
na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa
ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.”
Warumi 8:26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia
udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe
hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.”
Kwa hiyo Roho Mtakatifu ni msaada
wa karibu katika kutoa ushauri wa hekima, ushauri wa nini cha kusema, kipi cha
kufanya, anazungumza kwa niaba yetu, anashughulika kwa niaba yetu, anatutia nguvu,
anatupa wepesi anatusaidia wakati wa majaribu na wakati wa mambo magumu, na
wakati wa mateso, na wakati wa hatari, na wakati wa upinzani, kwa maana nyingine
msaada ule ule aliokuwa akiutoa Yesu Kristo alipokuwa Duniani pamoja na
wanafunzi wake, ndio msaada anaoutoa Roho Mtakatifu kwa kila mwamini kokote
aliko, na msaada ule ule anaoutoa Mungu baba tunaupata kwa Roho Mtakatifu
akaaye ndani yetu, kwa hiyo utaweza kuona umuhimu wake katika maisha yetu
Ni muhimu vile vile kufahamu kuwa
neno Msaidizi mwingine yaani neno mwingine katika kiyunani linatumika neno “Allos” ambalo maana yake, The other, another, more one, yaani
mwingine, tofauti na Yesu lakini akiwa katika kiwango kimoja au sawa na yeye
kwa hiyo lugha hii pia inatufundisha kuwa huyu Msaidizi mwingine yaani Roho
Mtakatifu ni nafsi tofauti na Yesu na ni nafsi nyingine tofauti na Baba lakini
ni watenda kazi pamoja katika kukamilisha kusudi lile lile na hii
inatuthibitishia kuwepo kwa utatu wa Mungu katika maana nyingine angalia maneno
yale “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi
mwingine” hii inathibitisha ukweli kuwa yuko Baba, Mwana na Roho
Mtakatifu kwa hiyo mafundisho kuhusu utatu wa Mungu sio swala la kizushi lakini
ni fundisho jepesi na rahisi la kimaandiko na bwana hajawahi kutukemea au
kutufunulia kuwa hakuna usahihi katika hilo,
Mathayo 28:19-20 “Basi, enendeni,
mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana,
na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na
tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”
Luka 3:21-22 “Ikawa, watu wote walipokwisha
kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka; Roho
Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka
mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.”
Kwa hiyo msaidizi mwingine huyu
ni nafsi nyingine mbali na baba na mwana Huyu ni Roho Mtakatifu, ukweli huu
kuhusu namna Mungu alivyo katika utatu haupingiki kimaandiko kwa sababu neno la
Mungu ndio linavyotuambia na kutuelekeza na kutufundisha, kwa hiyo Msaidizi
mwingine ni Roho Mtakatifu, ni Roho wa Mungu, ni Mungu ndani yetu.
Umuhimu wa kuwa na Msaidizi mwingine
Ni muhimu kufahamu kuwa kuna
umuhimu mkubwa sana wa kila mtu aliyeokolewa kuwa na uhusiano na Msaidizi
mwingine yaani Roho Mtakatifu, Yesu alikuwa na maana pana sana ya kusisitiza kuwa
atamuomba Baba ili atupatie Msaidizi mwingine yaani Roho Mtakatifu ili akae
nasi, Yesu alikuwa anafahamu umuhimu wa Roho wa Mungu katika maisha yetu kwa
sababu Yeye aliishi duniani kama Mwanadamu kwa asilimia 100% na akiwa Mungu kwa asilimia 100% Lakini kama mwanadamu alikuwa anataka kutufundisha namna ya
kuishi na kutenda kama wana wa Mungu tukiwa hapa Duniani, alipokuwa Duniani
Yesu alimtegemea Roho Mtakatifu kwa kila jambo kwa hiyo kila alichokifanya
alikifanya kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Sasa ikiwa Bwana Yesu alimuhitaji Roho
Mtakatifu katika maisha yake ni zaidi sana wewe na mimi tunamuhitaji zaidi. Katika maisha yetu ili aweze kutusaidia katika
kila jambo, Na ni muhimu kuelewa kuwa Roho Mtakatifu sio ushawishi, wala sio nguvu
tu kama watu wengine wanavyofundisha bali ni Mungu kamili, Roho wa Mungu ni
Mungu ona:-
Matendo 5:3-4 “Petro akasema, Anania, kwa
nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa
siri sehemu ya thamani ya kiwanja?Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na
kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje
hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.”
Mathayo 12:22-28 “Wakati ule akaletewa mtu
mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona.
Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi? Lakini
Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa
pepo. Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya
nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya
nafsi yake, haitasimama. Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi
yake; basi ufalme wake utasimamaje? Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je!
Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu. Lakini
mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia.”
Yesu Kristo alitoa kipaumbele kwa
Roho Mtakatifu, alimtegemea Roho Mtakatifu hata kufanya miujiza na kutoa pepo,
Nyakati za kanisa la kwanza walitoa kipaumbele kikubwa kwa Roho Mtakatifu, kwa
msingi huo basi ni muhimu kwetu, kuhakikisha kuwa tunatoa nafasi kwa Roho
Mtakatifu kwa sababu gani yeye anashughulika na maswala yote muhimu yanayohusiana
na maisha yetu mfano:-
1.
Roho
Mtakatifu huuisha Maisha mapya - Roho
Mtakatifu ndiye anayehusika kuweka mfumo wa maisha mapya katika roho zetu, ni
yeye anayehusika katika wokovu wetu, na anakuwa kama anatuzaa upya kwa Roho,
anatufufua kutoka katika hali ya kufa, anatupa uhai anatuhuuisha anaweka ndani
yetu kiu ya kumcha Mungu na kumtafuta Mungu, hatuwezi kupata uamsho wowote
ndani yetu ambao pia unaweza kuwa uamsho wa kanisa zima kama hatutamtii na
kumsikiliza Roho Mtakatifu, mwanadamu anazaliwa akiwa ni mwenye dhambi kwa
sababu ya kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, Dhambi hutufarikisha na Mungu,
mbele za Mungu mtu mwenye dhambi au aliyepotea huhesabiwa kama mfu, kwa sababu
ametengwa mbali na uwepo wa Mungu
Waefeso 2:1-6 “Nanyi
mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa
kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga,
roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi
tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya
mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.
Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu
aliyotupenda;hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu;
alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja
naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;”
Yohana 7:37-39 “Hata
siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake
akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko
yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Na neno hilo alilisema
katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana
Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.”
Uhai wote wa
kimwili na wa kiroho uko katika uweza wa Roho Mtakatifu, bila Roho wa Mungu ni
vigumu kitu chochote kuwa hai na maisha yetu ya kiroho kuwa hai, hatuwezi
kuendelea, hatuwezi kujutia, hatuwezi kutubu, hatuwezi kuomba, hatuwezi kusoma
neno la Mungu endapo Roho Mtakatifu hatahusika katika maisha yetu, kama ilivyo
kwamba Bila Yesu hatuwezi kufanya neno lolote hali kadhalika Bila Roho wa Bwana
sisi nasi hatuwezi kufanya jambo lolote, kwa hiyo Kristo alijua kuwa wanafunzi
wake wamemuamini, lakini wasipokuwa na Roho Mtakatifu ni vigumu kwao kuendelea
na imani ile bila ya msaada ulio karibu na msaada huo ni Roho Mtakatifu ambaye
ndiye anayehuisha Roho zetu, Na kutupa msaada wa kuwa hai katika maswala ya
kiroho.
2.
Roho
Mtakatifu hukaa ndani ya Mwamini – Kuna umuhimu mkubwa sana wa Roho
Mtakatifu kukaa ndani yetu, Katika mstari wa Msingi tunamuona Yesu akisema
atamuomba baba atupe msaidizi mwingine, ili msaidizi huyo akae ndani yetu
Yohana 14:16-18 “Nami
nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala
haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.”
Kukaa ndani yetu
kwa Roho Mtakatifu kuna faida kubwa sana kwa sababu sisi ni hekalu la Roho
Mtakatifu na akiwa ndani yetu tunapata nafasi ya kudumisha uhusiano wetu na
Mungu kwa kuabudu, kuomba, kutafakari na kutuvuta tuwe karibu na yeye, Roho Mtakatifu
anatumika kama daraja linalounganisha mioyo yetu na moyo wa Mungu, huku
akibadilisha tabia zetu kwa kadiri tunavyojitoa kwake kwa kutii anatusababishia
kuzaa matunda ya Roho na kuwa na sifa zinazomfanania Yesu Kristo.
Wagalatia 5:22-23 “Lakini
tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.”
3.
Roho
Mtakatifu hutupa hakika ya wokovu - Tunapa
hakika ya wokovu kwa Imani kupitia Roho wa Mungu ndani yetu, aidha na neno la
Mungu kwa hiyo wokovu wetu hautegemei
hisia zetu namna tunavyojisikia lakini unategemea namna Neno la Mungu
linavyotuambia tukithibitishiwa na Roho wake Mtakatifu
Warumi 8:15-16 “Kwa
kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya
kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Roho mwenyewe
hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;”
4.
Roho
Mtakatifu hubatiza mwamini – Neno la Mungu liliahidi ya kuwa sote
tutabatizwa katika Roho Mtakatifu, Yohana mbatizaji anasema ajaye nyuma yangu
ana nguvu kwa sababu yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu, kwa hiyo ni kazi ya
Mungu kutubatiza kwa Roho wake Mtakatifu, lugha inayofahamika kama kujazwa, kutujaza,
lugha nzuri ya maana sana ni ubatizo wa
Roho Mtakatifu, na hata hivyo, anapotubatiza Roho mwenyewe huusika katika
kutubatiza, tunazamishwa ndani yake na kila kitu mpaka lugha zetu zinaingizwa
katika uwepo wa Roho Mtakatifu bila kutupagaa, “we are filled without possessed”
Mathayo 3:11 “Kweli
mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana
nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza
kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.”
Yohana 1:33 “Wala
mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia,
Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa
Roho Mtakatifu.”
Matendo 1:5 “ya
kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu
baada ya siku hizi chache.”
Matendo 2:4 “Wote
wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho
alivyowajalia kutamka.”
Matendo 10:44-47 “Petro
alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile
neno. Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja
pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho
Mtakatifu.Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu.
Ndipo Petro akajibu, Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu
waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi? ”
Matendo 19:1-6 “Ikawa,
Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika
Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; akawauliza, Je! Mlipokea
Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho
Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema,
Kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba,
akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. Waliposikia
haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono
yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.”
Marko 16:17 “Na
ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema
kwa lugha mpya;”
1Wakorintho 12:13 “Kwa
maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu
Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote
tulinyweshwa Roho mmoja.”
1Wakorintho 14:2 “Maana
yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna
asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.”
1Wakorintho 14:4 “Yeye
anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali ahutubuye hulijenga kanisa.”
5.
Roho
Mtakatifu huzungumza na waamini – Roho Mtakatifu huzungumza, hunena na
kuelekeza wazi wazi, ni jambo la kushangaza wale wanaodhani kuwa Roho Mtakatifu
ni nguvu tu za Mungu na kumuondolea haki ya kuwa nafsi ni muhimu kujikumbusha
kuwa huyu ni Msaidizi mwingine ni nafsi nyingine lakini anafanya kazi moja na Baba
na Mwana na hivyo hutoa maelekezo, huzungumza, na hutoa maonyo.
Matendo 8:27-29 “Naye
akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini
ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa
amekwenda Yerusalemu kuabudu, akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo
cha nabii Isaya. Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili,
ukashikamane nalo.”
Matendo 13:1-2 “Na
huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni
Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa
ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli.Basi hawa walipokuwa wakimfanyia
Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa
kazi ile niliyowaitia.”
1Timotheo 4:1-3 “Basi
Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani,
wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu
wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na
kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani
na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.”
Ufunuo 2:7 “Yeye
aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye
ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.”
Ufunuo 2:11 “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili
ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti
ya pili.”
Ufunuo 2:17 “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili
ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana
iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina
jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.”
Ufunuo 2:29 “Yeye
aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”
6.
Roho
Mtakatifu hujihusisha na uongozi wa kiroho – Wakati wanafunzi wakiwa Pamoja
na Yesu Kristo Duniani yeye ndiye alikuwa kiongozi wao katika maswala yote ya
kiroho na ibada, sasa Yesu anapokuwa Mbinguni huku akiwa pamoja nasi katika
ulimwengu wa Roho, kila wajibu na kazi alizokuwa akizifanya sasa Roho Mtakatifu
hufanya hivyo ndani yetu
Yohana 16:7 “Lakini
mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi
nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu,
nitampeleka kwenu.”
7.
Roho
Mtakatifu hufundisha na Kuongoza katika kweli – Roho Mtakatifu ni Mwalimu
mkuu, ambaye anapokuwa ndani yetu anatufundisha na kutukumbusha wote
tuliomuamini katika neno la Kristo, jambo ambalo ni muhimu sana kwa ukuaji wetu
kiroho na kudumu katika neno la Mungu na kuisimamia Imani, angalia leo wako
watu wanaoukana utatu wazi wazi wakisema kuwa ni jambo lililoingizwa na Warumi
wakati wa utawala wa Mfalme Constantino, wanasahahu kuwa mfalme huyo aliokoka
baada ya kuona alama ya msalaba mbinguni wakati wa usiku na sauti iliyomuambia
kuwa kwa alama hii utashinda na ndipo alipoukubali Ukristo, Mungu alimtumia
kusimamia kweli kadhaa pamoja na wazee wetu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, ni
kweli kuwa kanisa katoliki lina madhaifu kadhaa kama yalivyo makanisa mengine
na kama yalivyokuwa yale makanisa saba ya eneo la Asia ndogo ambayo Yesu aliyakemea
mapungufu yao na kuwatia moyo uwezo wao, hata hivyo pamoja na udhaifu unaoweza
kuuona kwa wakatoliki hawajawahi kufikia ngazi ya kukana uungu wa Yesu au uungu
wa Roho Mtakatifu, kwa hiyo katika wakati huu wa kuishi kwetu tunapaswa kumtegemea sana Roho Mtakatifu
kutuongoza katika kweli badala ya kushiba maharagwe na kuropoka, maandiko yako
wazi kuhusu utatu wa Mungu likiwemo hili ya kuwa Roho Mtakatifu ni Mwalimu kama
vile vile ilivyokuwa kwa Yesu Kristo, na atatukumbusha na kutuongoza na kututia katika kweli yote.
Yohana 14:26 “Lakini
huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu,
atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”
Yohana 16:13-15 “Lakini
yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa
maana hatanena kwa shauri Lake Mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena,
na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa
katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa
hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari”
8.
Roho
Mtakatifu huita watu katika huduma – Roho Mtakatifu huita watu katika
huduma na kuwaongoza katika huduma hiyo sawasawa na Yesu alivyokuwa akiita watu
na wote wanaongoza katika kazi ileile kwa misingi ile ile, mfano unaweza
kumuona Yesu akimuita Sauli kwa kazi yake na unaweza kumuona Roho wa Mungu
akimuita sauli yule yule aliyeitwa na Yesu kwa kazi ile iole iliyokusudiwa na
Bwan Yesu! Ona :-
Matendo 9:1-6 “Lakini
Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani
Mkuu,akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili
akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.Hata
alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote
nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli,
mbona waniudhi?Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu
unayeniudhi wewe. Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo
kutenda.”
Matendo 13:1-4 “Na
huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni
Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa
ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. Basi hawa walipokuwa wakimfanyia
Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa
kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao
juu yao, wakawaacha waende zao Basi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu
wakatelemkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro.”
Matendo 16:6-10 “Wakapita
katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri
lile neno katika Asia. Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia,
lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa, wakapita Misia wakatelemkia Troa. Paulo
akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na
kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. Basi alipokwisha kuyaona yale maono,
mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu
ametuita tuwahubiri Habari Njema.”
9.
Roho
Mtakatifu hutupa uhakika wa uwepo wa Mungu – Roho Mtakatifu anakaa ndani
yetu na anafanya kazi ya kutupa uhakika wa uwepo wa Mungu na uwepo halisi wa
Yesu Kristo na asili zao na zaidi ya yote anatuunga katika ushirika na Mungu
Baba na Mwana na ndio maana maandiko
yana wasiwasi sana na mtu ambaye anaharibu asili ya Mungu baba na Mungu mwana
na wakati mwingine watu wanaofanya hivyo huenda hawana Roho wa Mungu ndani yao kama
maandiko yanavyotuonya wazi wazi
1Yohana 2:22-29 “Ni
nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga
Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana.Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye
Mwana anaye Baba pia.Ninyi basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani
yenu. Ikiwa hilo mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi
mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba. Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia,
yaani, uzima wa milele. Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka
kuwapoteza. Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna
haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za
mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani
yake. Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa,
mwe na ujasiri, wala msiaibike mbele zake katika kuja kwake.Kama mkijua ya kuwa
yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye.”
Warumi 8:9-16 “Lakini
ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata
roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. Na
Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho
yenu i hai, kwa sababu ya haki. Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu
katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu
ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa
ndani yenu. Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa
kufuata mambo ya mwili, kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili,
mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa
wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea
tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo
kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho
zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;”
10.
Roho
Mtakatifu hutia nguvu – Roho wa Mungu hututia nguvu kukamilisha majukumu
yote tuliyopewa na Mungu hapa duniani hasa ya kuhudumia watu, pamoja na kukabiliana
na nguvu zote pinzani zinazotukabili kwa kusudi la kuzuia kusudi la Mungu, na
kutimiza majukumu yote ambayo Mungu anataka tuwatendee watu wake
Luka 4:18-19 “Roho
wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari
njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona
tena, Kuwaacha huru waliosetwa,Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.”
Matendo 1:8 “Lakini
mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa
mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata
mwisho wa nchi.”
11.
Roho
Mtakatifu husaidia katika maombi – Tangu zamani uwezo wa kuomba hauko
katika uweza wa wanadamu, Roho Mtakatifu ndiye anayetuwezesha kuomba kwa kuugua
kusikoweza kutamkwa au kwa kuomboleza, waamini wanapoomba pamoja na Roho
Mtakatifu hawachoki, na sio hivyo tu huomba katika namna iliyo sahihi, Yeye
anaitwa Roho wa neema na kuomba maana yake hutusaidia au kutupa neema ya kuomba,
Maisha ya mtu aliyeokoka yatapata usitawi mkubwa sana endapo watu wake wataomba
wakisaidiwa na Roho Mtakatifu.
Zekaria 12:10 “Nami
nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema
na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama
vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake,
kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.”
Warumi 8:26-28 “Kadhalika
Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo,
lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.Na yeye
aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama
apendavyo Mungu.Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja
na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”
Yuda 1:20 “Bali
ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba
katika Roho Mtakatifu,”
12.
Roho
Mtakatifu huwezesha kuabudu – Mungu ni Roho nao waabuduo halisi wanapaswa
kumuabudu yeye katika Roho na kweli, kimsingi hatuwezi kuabudu vizuri bila
msaada wa Roho Mtakatifu kama tu vile jinsi ambavyo hatuwezi kuomba vizuri bila
Roho Mtakatifu, muunganiko wetu na usikivu wetu katika kumuabudu Mungu na
kupokea kutoka kwake unatuhitaji wakati wa kuabudu tuwe rohoni
Ufunuo 1:9-11 “Mimi
Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na
subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya
Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu. Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana;
nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,ikisema, Haya uyaonayo
uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na
Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.”
Yohana 4:23-24 “Lakini
saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho
na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.Mungu ni Roho, nao
wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”
Wafilipi 3:3 “Maana
sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu,
wala hatuutumainii mwili.”
1Wakorintho 14:15 “Imekuwaje,
basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena
nitaimba kwa akili pia.”
13.
Roho
Mtakatifu hutoa karama – Kwaajili ya kuifanikisha kazi ya Mungu Roho wa
Mungu hutupa karama ambazo kazi yake ni kuujenga mwili wa Kristo na
kulithibitisha neno la Mungu, miujiza yote, uponyaji utoaji wa pepo ni kazi
zinazofanywa na Roho Mtakatifu kupitia karama mbalimbalia anazoziweka kwa
waamini
1Wakorintho 12:7-11 “Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.
Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa,
apendavyo Roho yeye yule; mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine
karama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na
mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na
mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja,
yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.”
Kuna na mambo
mengine mengi sana ambayo msaidizi mwingine huyafanya katika maisha yetu ya
kila siku, hapa nimechagua machache lakini ni msaada kwa wanafunzi wakati wa
mitihani, ni msaada kwa wanajeshi wakiwa vitani, ni msaada kwa usalama wa taifa
na wapelelezi, ni msaada wa wafalme
katika maamuzi, ni msaada kwa wafanya biashara, ni msaada kwa wakulima, ni
msaada kwa wachumi na ni msaada katika michezo na kila eneo ambalo Mtu wa Mungu
analifanyia kazi, ni msaada kwa mafundi wa cherahani na wajenzi alitoa hekima kwa
ujenzi wa hekalu, mavazi ya Haruni, wajenzi wa hema, ujenzi wa Meli wakati wa
Nuhu, ukulima wakati wa Isaka, utawala wakati wa Suleimani, vitani wakati wa
wamaamuzi na Daudi, upelelezi wakati wa Elisha,
kimsingi Roho wa Mungu ni msaada katika maisha yetu hata kitu
kinapopotea Roho Mtakatifu, anahusika kionekane kumbuka habari ya kuelea kwa
chuma cha shoka wakati wa Elisha na matukio mengine chungu nzima muimbaji na
wapigaji kinubi kama Daudi mpaka pepo wanakimbia, vitani ngao zilipakwa mafuta
kupata neema na upako kwaajili ya ushindi na ulinzi, unaweza kuhitaji msaada wa
Roho Mtakatifu katika kila eneo bila kumuwekea Mungu mipaka. Na ni kazi yake kutupa msaada tunaoutaka
Jinsi ya kuwa na msaidizi mwingine.
Roho Mtakatifu ili umpokee ni
lazima uwe umemuamini Bwana Yesu kama mwokozi wako aliyekufa msalabani kwaajili
yako, tendo la kumuamini Bwana Yesu ndilo linalotuunganisha na Mungu na kutufanya
tuwe wana wa Mungu na kwa imani tunajiweka katika nafasi ya kumpokea Roho
Mtakatifu
Matendo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni
mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu,
nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”
Matendo 19:1-6 “Ikawa, Apolo alipokuwa
Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana
na wanafunzi kadha wa kadha huko; akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu
mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.
Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.
Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini
yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina
la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu
akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.”
Yohana 7:38-39 “Aniaminiye mimi, kama vile
maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.Na neno hilo
alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa
maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.”
Ni lazima mtu anayemuhitaji Roho
Mtakatidu awe na shauku, liwe ni hitaji, iwe ni kiu yako na hivyo hua budi kuwa
muhitaji na kumuomba Mungu baada ya kujifunza umuhimu wake unaingia katika
maombi unaomba na Mungu anapoiona shauku yako na kiu yako atakupa Roho
Mtakatifu.
Luka 11:13 “Basi, ikiwa ninyi mlio waovu
mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana
kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?”
Yohana 7:37-39 “Hata siku ya mwisho, siku
ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona
kiu, na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito
ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.Na neno hilo alilisema katika habari ya
Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja,
kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.”
Ni lazima ukae katika neno la
Mungu, Roho Mtakatifu hafanyi kazi nje ya neno lake lililowekwa ndani yetu kwa
hiyo hakikisha unajaa neno na kwa jinsi hii utaruhusu Roho Mtakatifu kufanya
makazi ndani yako na utaiona na kufurahia faida zake zote katika maisha yako
Yohana 15:7-8 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na
maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. Hivyo
hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.”
Utii kwa neno la Mungu husafisha
njia ya Roho Mtakatifi kukaa ndani yetu Zaburi
51:4-11“Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na
kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na
kuwa safi utoapo hukumu.Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu
alinichukua mimba hatiani. Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe
utanijulisha hekima kwa siri, Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi,
Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji Unifanye kusikia furaha na
shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu;
Uzifute hatia zangu zote. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho
iliyotulia ndani yanguUsinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu
usiniondolee.”
Jihadhari usiasi Isaya 63:10 “Lakini
wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui,
akapigana nao.”
Kwa kuwa msaidizi mwingine ni wa
Muhimu na ni zawadi kubwa sana kutoka kwa Mungu wakristo ni lazima tukubali
kuruhusu Mungu atende kazi pamoja nasi kupitia Roho wake Mtakatifu kwaajili ya
utukufu wake, hatuwezi lolote katika maisha haya na bila Mungu hatuwezi kutoboa
kwa sababu hiyo ni muhimu kwetu kuhakikisha kuwa wakati wote tunampa Roho
Mtakatifu kipaumbele katika maisha yetu na tunamtii kwa kila mzigo anaouweka
ndani yetu na tuutimize kwa wakati. Uongezewe neema
Na Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima