Alhamisi, 24 Agosti 2023

Usiwape wanawake nguvu zako!


MIthali 31:1-3 “Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake. Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu? Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.”


Utangulizi:

Kitabu cha Mithali ni kitabu kinachotufunza maswala ya muhimu katika maisha na maadili na maonyo ya kila siku pamoja na kutupa hekima jinsi na namna inavyotupasa kuenenda, Moja ya maswala ya msingi tunayojifuza leo ni pamoja na wosia aliopewa Mfalme Lemuel kutoka kwa mama yake ambayo alimfunza ili kutusaidia sisi tuliofikiwa na miisho ya zamani hizi.

Mithali 31:2-3 “Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu? Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme

Mama anaonekana kusisitiza sana kuonyesha namna anavyohitaji  umakini wa jambo ambalo anataka kulileta kwa mwanae ambalo pia analileta kwetu, ambalo kimsingi ingawa lilikuwepo katika siku za zamani sana na leo linaendelea kushika kasi kwa namna mbalimbali, tutajifunza somo hili USIWAPE WANAWAKE NGUVU ZAKO kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:- 

Ø  Maonyo kutoka kwa mama.

Ø  Usiwape wanawake nguvu zako

Ø  Mambo yawapasayo wanaume kufanya! 

Maonyo kutoka kwa mama.

Ni muhimu kufahamu kuwa katika mtazamo wa kale wa mashariki ya kati jukumu kubwa la malezi na makuzi mazima ya mtoto awe wa kiume au wa kike na hata misingi ya imani yake ilisadikiwa kuwa ilitoka kwa mama, Kama mtoto angeonyesha hekima na ubora baba yake angejivunia sana na kama mtoto akionyesha tabia mbaya waliangalia sana kuwa mama yake alikuwa ni mtu wa namna gani ona Mithali 10:1 “Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.” Kwa msingi huo utaweza kuona hata nyakati za utawala wa wafalme wale waliokuwa waovu au waliofanya mema mama zao walitajwa na ubini wao kuonyesha kuwa chanzo cha tatizo au mafanikio ya mfalme husika imechangiwa na  aina ya  mama aliyekuwa naye ona kwa mfano

2Nyakati 29:1-2 “Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka ishirini na kenda; na jina la mamaye aliitwa Abiya binti Zekaria. Akafanya yaliyo ya adili machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyafanya Daudi babaye.”  

Unaona kama mfalme alifanya vizuri maana yake kulikuwa na mama mzuri mwenye tabia nzuri mwenye busara na hekima na mcha Mungu anayetoka katika familia iliyofunzwa vizuri, kadhalika pia wamama walitajwa kulingana na aina ya mfalme kama mfalme huyo alikuwa mwovu utaweza kuona na aina ya mama anatajwa na anakotokea ona kwa mfano

1Wafalme 15:1-3 “Mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya alianza kutawala juu ya Yuda. Miaka mitatu akatawala huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Maaka, binti Absalomu. Akaziendea dhambi zote za babaye, alizozifanya kabla yake; wala moyo wake haukuwa mkamilifu na Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi babaye.”

Ni kwaajili ya mambo kama haya Mungu aliwaelekeza Israel kuhakikisha kuwa wanaoza watoto wao kwa watu sahihi wenye tabia njema ili mioyo yao isikenguke kutoka kwa Bwana ona

Kumbukumbu 7:1-4 “Bwana, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang'oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe; wakati Bwana, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao; binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake. Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi.”

Kwa msingi huo kwa mujibu wa maandiko Mwanamke ana nafasi kubwa sana ya kuambukiza maswala ya kiimani na uadilifu kwa watoto kuliko tunavyoweza kufikiri ukweli huu unathibitishwa pia katika maisha ya Timotheo ambaye baba yake alikuwa myunani na mama yake myahudi na bibi yake alikuwa myahudi pia na imani ilitembea kwa wanawake hao mpaka kwa kijana wao Timotheo ona kile Paulo mtume anakithibitisha hapa

2Timotheo 1:5 “nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.”

Unaona Paulo mtume mkuu wa wajenzi pia alikuwa na imani kuwa imani njema iliyokuwa kwa bibi yake Timotheo, ilikaa wazi pia ndani ya mama yake Eunike na alikuwa na imani kuwa Timotheo ameirithi, ni ukweli ulio wazi kuwa uadilifu, imani,  tabia na mwenendo wetu unaathiriwa kwa kiwango kikubwa na wazazi wetu wa kike kifupi imani inakaa kwa mwanamke.

Ni katika hali kama hiyo Mfalme Lemuel anakumbuka sana mausia aliyopewa na mama yake, yalikuwa ni maelekezo Muhimu sana ambayo mama yake aliyazungumza kwa msisitizo akimtaka kijana wake ayashike ili aweze kufanikiwa katika maisha yake na katika ufalme wake, Mama yake alikuwa anajua mioyo ya wanawake wa ulimwengu huu na alikuwa na ujuzi kuwa watu wengi sana hususani wanaume wamepotezewa Muda, na kupotezewa heshima zao na kuharibikiwa katika uchumi na mafanikio yao kupitia wanawake, ona tena maonyo hayo muhimu

MIthali 31:1-3 “Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake. Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu? Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.”

Usiwape wanawake nguvu zako!

Katika maelekezo hayo muhimu ambayo Lamuel alipewa na Mama yake na ameshirikisha jamii hapa ili wote tuweze kujifunza ni hatari kuhusu wanawake! USIWAPE WANAWAKE NGUVU ZAKO  hili ni moja ya maonyo ya msingi sana ambayo tunataka kujifunza na sisi leo, kila kijana wa kiume anapaswa kulitilia hilo maanani, jambo hili la kuwapa wanawake nguvu zako pia linaendana na linalofuata WAWAHARIBUO WAFALME, kuwapa wanawake nguvu zako na kuwapa wanawake moyo wako kunaleta anguko la mfalme! Kunaangusha, kuonaondoa heshima, kunaharibu mwelekeo wa maisha kunasambaratisha ustawi wa kiuchumi wa mtu, Nafsi yako ikitekwa na uzuri wa wanawake hatima ya kijana wa kiume inakuja kuwa yenye majuto makubwa baadaye jambo hili limeonywa mara kadhaa katika maandiko ona

Mithali 5:1-10 “Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, mzisikie akili zangu; Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa. Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili. Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako; Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;”

Unaweza kuona maonyo ya Mfalme Sulemani yanaenda sambamba na Maonyo ya mama yake Lemuel wote wanaonya Hasara zinazoweza kupatikana kwa Mwanaume kujihusisha na wanawake hususani katika maswala mazima ya kufanya ngono, kufanya zinaa au umalaya au kuwanda wanda katika maisha yetu na uzuri wa wanawake au kutaka kuwaonja wanawake wa aina zote wanaojitokeza katika maisha yetu jambo hili lina madhara kadhaa ambao wenye hekima wameyaainisha hapo, usiwape wanawake nguvu zako!

Nini maana ya KUWAPA WANAWAKE NGUVU ZAKO neno nguvu linalotumika hapo katika kiebrania ni CHAYIL ambalo kimsingi linazungumzia UWEZO, yaani uwezo wako wote kama vile Jeshi au kila kitu ulicho nacho ambacho kinakujenga wewe kuwa wewe, Mfano, HESHIMA, FEDHA, MALI, WATOTO, KAZI, AU NJIA ZAKO ZOTE ZA UCHUMI, MAISHA YAKO, AU MUDA, Kwa hiyo neno CHAYIL ni mjumuisho wa maswala kadhaa muhimu kama kazi, heshima, cheo, muda nguvu na uwekezaji wako wote.  Kwa mujibu wa wenye hekima hapo ni kuwa unapojitoa katika maisha ya kuwapenda wanawake na umalaya  utafutilia mbali kila ambacho umesumbuka kukijenga kwa miaka kadhaa ya maisha yako neno WAHARIBUO  katika Kiebrania ni DEREK  ambalo maana yake ni kufutuilia mbali,  wanaume wengi hutumia nguvu zao na  na muda wao kujijenga kitaaluma, kiuchumi, kiroho na kadhalika lakini moja ya changamoto kubwa sana kibinadamu inayowapata wanaume ni kuwa wanapokuwa na mafanikio makubwa na kuwa maarufu na kuwa na nguvu kubwa kiuchumi, na hata kimwili na kujipatia umaarufu basi adui mkubwa sana wa mafanikio yao au anguko lao kubwa sana linalowakabili ni WANAWAKE, kila mwanamke anavutiwa sana na mwanaume aliyejijenga, Mwenye fedha, mwenye six Park, aliye ha umaarufu, mwenye uchumi mzuri, mwenye tabia nzuri, mwenye nyumba, gari na mafanikio mbalimbali katika maisha, Mama wa Lemuel alikuwa na ufahamu huo na akamuonya mwanaye kuwa asitoe moyo wake kwa hawa wanaoangusha wafalme sikiliza; wafalme hapa sio lazima wawe watu walioko kwenye mamlaka za kiserikali au rais na kadhalika Ufalme hapa unazungumzia kufikia kiwango Fulani cha utukufu ni kiwango Fulani cha mafanikio, kilele Fulani cha mafanikio na heshima unapokifikia hicho wewe ni mfalme na unaweza kuharibikiwa kama moyo wako hautajali kujilinda na wanawake, na kumbuka vilevile Mama wa Lamuel Hakusema Mwanamke bali amesema wanawake maana yake ile hali ya kupenda kumiliki au kutembea na wanawake wengi baada ya mafanikio, kitabu hicho hicho kumbuka kuwa kina imani kuwa mtu muadilifu anaweza kutafuta mke mmoja tu na akatulia naye Mithali 31:10 “Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.” Kwa hiyo tatizo sio mke tatizo ni wanawake hawa wanaleta uharibifu na neno la Mungu linathibitisha hayo kama tutakavyoona mbeleni:-

-          Kiuchumi – Maandiko yanatufundisha kuwa tangu siku za zamani limekuwa ni jambo la kawaida kuwa kunapokuwa na mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanamke na Mwanaume fedha au mali huusika katika kuwapa wanawake, wanaume wameumbiwa kutoa na wanawake wamaumbiwa kupokea, hivyo linaweza kuwa jambo la kawaida wanawake kutaka malipo katika mahusiano,

 

Mwanzo 38:14-18Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, wala hakuozwa awe mkewe. Yuda alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba, maana amejifunika uso.  Akamgeukia kando ya njia, akasema, Niruhusu niingie kwako. Maana hakujua ya kuwa ni mkwewe. Akamwuliza, Utanipa nini, ukiingia kwangu? Akasema, Nitakuletea mwana-mbuzi wa kundini. Naye akamwuliza, Je! Utanipa rehani hata utakapomleta? Akasema, Nikupe rehani gani? Akamjibu, Pete yako ya muhuri, na kamba yake, na fimbo yako iliyo mkononi mwako. Basi akampa, akaingia kwake, naye akapata mimba.”

 

Ni kifungu cha zamani sana japo kinaweza kuwa na mafunzo mengine mengi tofauti lakini moja ya kitu tunajifunza hapo ni kuwa tangu zamani wanawake walipenda kupokea kitu kutoka kwa wanaume na wanaume walihonga, mwanamke aliuliza utanipa nini ukiingia kwangu? Na mwanaume alisema nitakupa mwanambuzi, katika nyakati za leo wanawawake wameharibika zaidi, hali ya kutaka kuhongwa imepanuka katika kiwango ambacho leo kinaitwa kuchunwa, wanaume wamepewa majina ya mabuzi na wanawake ni wachunaji, kuna utapeli mwingi na mkao mkubwa wa wanawake kuhitaji fedha kama malipo ya ngono, lakini sio kwa malipo ya ngono tu ila watawekeza mioyo yao katika kuwaelemea wanaume kwa sababu mbalimbali mojawapo ikiwa ni ugumu wa maisha lakini vilevile na kwa moyo wa ubinafsi hata kama hawauzi mapenzi au kufanya biashara ya mapenzi, lakini vyovyote vile hali hii inachangia katika kudhooficha uchumi wa mwanaume, wanawake wa leo ambao wengi wao wana mikopo wanayotakiwa kurejesha mawazo yao makubwa yamekuwa katika fedha zaidi kuliko kwenye penzi lenyewe kuwaendekeza Malaya kutakueletea anguko la kiuchumi, na kufilisi uwezo wako, katika maeneo mbalimbali likiwemo hili la uchumi.

 

-          Nguvu – Huu ni uwezo wa kimwili na Kiroho, kisaikolojia wanawake wanavutiwa sana na Mwanaume mwenye nguvu, hili sio jambo la ajabu kiasili, kwani hata wanyama katika ulimwengu wao majike huwa hayavutiwi na mwanaume mnyonge, kama mwanaume atakuwa hana nguvu anapoteza heshima kwa mwanamke, lakini hata hivyo kujihusisha katika ngono kulikokithiri kwa wanawake wa aina mbalimbali pia hupelekea kupoteza nguvu za kimiwli, na kiroho na nguvu za uzazi au hata nguvu za kiume 

 

Zaburi 127:3-5 “Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu. Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo wana wa ujanani. Heri mtu yule Aliyelijaza podo Lake hivyo. Naam, hawataona aibu Wanaposema na adui langoni

 

Maandiko yanazungumzia umuhimu wa watoto, Nguvu ya familia yoyote ni watoto wake tabia ya kujaribu kujifurahisha na kila mwanamke inaweza kuathiri uzao wako au unaweza kupoteza mbegu zako na watoto wako wakawa wa mtu mwingine, wako watu wengi leo wamezaa hovyo hovyo  na wamezaa mpaka na wake za watu na ni ngumu kwenda kudai watoto katika familia isiyokuwa yako, watoto wanajenga jamii ni thawabu kutoka kwa Mungu lazima wazaliwe katika utaratibu na mpangilio maalumu ili uzao wako usipotee kama mishale mkononi mwa shujaa ndivyo walivyo watoto wa ujanani, Heri mtu yule aliyelijaza podo lake, yaani heri mtu mwenye mishale mingi, kuwa na watoto wengi lilikuwa moja ya jambo lenye heshima kubwa sana nyakati za Biblia. Lakini sio watoto waliotawanyika ni watoto wanaolelewa katika boma moja (Podo) ni chombo maalumu cha kuhifadhia mishale ambayo unaweza kuitumia wakati wa mapambano, shujaa hawezi kutumia mshale ambao hauko kwenye podo lake!, Uzaaji wa watoto hovyo hovyo pia unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuharibu uchumi na uadilifu wa kitabia unaoukusudia uwe kwa watoto wako!

 

Aidha pia nguvu zako za kiume zinaweza kuharibiwa kupitia tabia ya kulala hovyo na wanawake, asili ya nguvu zako za kiuchumi, kimwili na kiroho pia inaweza kuharibiwa kama hutakuwa na tahadhari na wanawake hasa unapokuwa na mahusiano ya kingono na wao.

 

Waamuzi 16:13-18 “Delila akamwambia Samsoni, Hata sasa umenidhihaki, umeniambia maneno ya uongo; niambie sasa, waweza kufungwa kwa kitu gani? Akamwambia, Ukivifuma hivi vishungi saba vya nywele za kichwa changu katika mtande wa nguo. Basi akazifunga kwa msumari, akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Naye akaamka usingizini, akaung'oa ule msumari, na ule mtande. Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi. Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa. Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.”

 

-          Heshima – Daudi alikuwa ni Mfalme aliyeheshimika sana mbele za Mungu na wanadamu kwa ujumla ndiye mtu anayetajwa katika maandiko kuwa aliupendeza moyo wa Mungu, jambo hili lilimpa heshima kubwa sana lakini aliposhiriki ngono na mke wa Mtu alipoteza mamlaka yake na heshima, jambo hili lilimletea aibu kubwa sana ona

 

 2Samuel 11:4 “Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake.

 

Unaona kitendo hiki hata Nathan nabii alimweleza wazi kuwa kwa jambo hili umewapa adui za Bwana nafasi kubwa ya kukufuru ona

 

2Samuel 12:14 “Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za Bwana nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika yake atakufa.”  

 

Nguvu na heshima aliyokuwa anapewa Daudi iliingia shidani kupitia zinaa alijivunjia heshima japo alitubu na aliendelea kuuelekeza moyo wake kwa Mungu, Lakini aliitia daosari karatasimyake ya kuwa mfalme muadilifu

 

Mwanaye Sulemani vilevile anajieleza mwenyewe kuwa wanawake ndio sababu ya anguko lake kubwa na anaeleza wazi kuwa anguko lake lilisababishwa na upenzi wake mkubwa kwa wanawake na kutokusikiliza mausia ya mama yake Lemuel anayejitaja hapa ni mwandishi wa kitabu hiki Jina Lemuel kwa Kiibrania maana yake ni “ALIYEJITOA KWA MUNGU” au “KWAAJILI YA MUNGU FOR GOD OR DEVOTED TO GOD  jina hilo halijulikani katika orodha nya wafalme wa Yuda na Israel ni huenda ni jina ambalo Sulemani aliitwa na mama yake Bathsheba au ni jina analoamua kulitumia katika utunzi wa stori hii au shairi hili kwa ni ni  anatumia jina hili nadhani anatumia jina la fumbo kwa kusudi tu la kutuletea somo husika katika Israel, kwa msingi huo mwandihi wa Mithali hizi ni Suleimani na hapa anaonyesha hekima yake aliyiojifunza kutoka kwa mama yake mwenye hekima na uadilifu kwa hiyo  hakujawahi kuwa na historia ya kuwepo mfalme aliyeitwa Lemuel, na hivyo tunaamini Lemuel ni Suleimani nanamamam yake ni Bathsheba. Sasa Pamoja na heshima kubwa sana aliyokuwa nayo na hekima aliyopewa na Mungu Sulemani aliharibikiwa kwa kutokufuata maonyo  na mafundisho ya mama yake na hapa anataka kutumia uzoefu alioupata kutufunza sis nasi tusiharibikiwe!.

 

1Wafalme 4:4-6. “Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni. Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.”

 

Anguko hili la Sulemani la kufikia hatua ya kuabudu miungi mingine ndilo kwa namna Fulani limechangiwa na moyo wake wa kuwapenda wanawake wengi ona

 

1Wafalme 4:1-3 “Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda. Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.”

 

Akiwa katika hali hii ya majuto baadaye ndio anatuasa kama Lemuel akionya kuwa tusikilize hekima sio lazima sana Mwalimu awe mama Lakini katika mafunzo ya Hekima wakati wowote chanzo cha mafunzo kinaitwa mama, kama mtu alikuwa na hekima kubwa sana na mali nyingi na muda na mafanikio mengi sana akapata hata anguko la kuabudu miungu ni sawa na kupoteza muda wake na kuharibikiwa katika kila kitu, Suleimani alikuwa na akili moyoni mwake hangeweza kuzungumza habari za baba yake na mama yake Bathsheba kama sisi tunavyoweza kuzungumza lakini akilini alikuwa na ujuzi kujihusu kuhusu na kupitia uzoefu alioupata ni uwazi kuwa Sheria ya Mungu pia ilikuwa imewaonya wafalme kutokujitwalia wake wengi Kumbukumbu 17: 17 “Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno.” Lakini yeye hakusikiliza wala kujali jambo lililopelekea kuleta madhara makubwa katika maisha yake!

 

-          Nguvu za kiroho – Kupenda wanawake licha ya kuharibu nguvu za uchumi, heshima na mali pia wanawake wanaharibu hali ya Msimamo wa kiroho, Kupenda wanawake husababisha kuwapenda wao zaidi kuliko kumpenda Mungu, Ni swala lililowazi kuwa Baba Yetu Adamu angeweza kutokukubaliana na Mwanamke katika kula lile tunda na angeweza kutoa ripoti kwa Mungu kwa kile kilichotokea na pia kuwa na toba au kuomba msamaha kwa tukio lile hii inawezekana ya kuwa ilichangiwa kwa kiwango kikubwa na upendo wake kwa mkewe na Mungu akimsomea hukumu anaanza kwa kusema Kwakuwa umeisikiliza sauti ya mkeo …. Ona

 

Mwanzo 3:17-19 “Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.”

 

Muda usingeweza kutosha kurejea hali ya Mwamuzi maarufu Samsoni, na Mfalme maarufu Daudi na mtu mwenye hekima Sulemani, hasa Sulemani tunaona kuwa aligeuzwa moyo kuabudu Miungu mingine, hapa tunajifunza kuwa ukiacha shetani na ushawishi mwingine wa Dunia wanawake wana nafasi kubwa sana ya kugeuza mwelekeo wa Moyo wa Mwanaume,

 

Mambo yawapasayo wanaume kufanya!

 

Luka 10:27. “Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.”

 

Ni muhimu kufahamu kuwa wanaume wanawajibika katika kila hali itakayotokea katika maisha yao, wanaume wanatakiwa kutumia nguvu zao, akili zao, fedha zao na hisia zao zote ambazo Mungu amewapa kuhakikisha kuwa wanalinda usalama wao na baraka ambazo Mungu amezikusudia kwao, Kama wanaume wanampenda Mungu basi nivema akili zao, na moyo wao na roho zao zikaelekezwa kwa Mungu na kulitiii neno lake.

 

Moja ya adhabu iliyotangazwa na Mungu katika bustani ya Edeni kama mgogoro kati ya mwanamke na mwanaume ni pamoja na ugomvi dhidi ya nguvu, yaaani mamlaka na utawala ona Mwanzo 3:16 “Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.”

 

Kimsingi sehemu muhimu ambayo nataka kila mtu msomaji wangu na wasikilizaji wangu waweze kunielewa ni eneo ambalo maandiko yanasema TAMAA YAKO ITAKUWA KWA MUME NAYE ATAKUTAWALA, katika maandiko ya kiibrania neno NENO tamaa linatajwa kama neno TESHUQAH Katika kiibrania kwa kiingereza ni STRETCHING OUT AFTER  ambalo maana yake ni kujaribu kujitutumua dhidi ya  na Mungu anapotangaza mgogoro huu anaoshesha na matokeo ni kutawaliwa neno naye ATAKUTAWALA – linasomeka kama MASHAL ambalo hapa linatumika kama kuzidiwa, kutawaliwa, au kuwa na nguvu juu yako, kwa tafasiri nzuri maana yake ni kuwa wanawake watakuwa na tamaa ya kutaka kuwatawala wanaume lakini hatimaye watatawaliwa unaweza kuona

 

Kwa hiyo kinachotokea ni kuwa mwanaume anapojitoa katika mapenzi, kwa haraka sana Mwanamke atajinyoosha kwenye utawala, atatawala hisia zako, mwili wako, tama yako, uchumi wako, roho yako na kuiteka nafsi yako na usipoweza kujinasua katika hilo maana yake UMEWAPA WANAWAKE NGUVU ZAKO  na uwezo wako wa kutawala mambo mengine unakuwa umeishia hapo, akiweka msingi wa maongozi katika kanisa Paulo mtume katika nafsi yake analiweka hili wazi kuwa kama kiongozi hawezi kuitawala nyumba yake hataweza kufaa kuwa mtawala katika kanisa ona 1Timotheo 3:4-5 “mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)

 

Kwa msingi huo ili mwanaume ajikwamue ni lazima ajui kujitawala na kutawala na akiweza hicho hatawekwa chini ya uweza wa kitu chochote,aidha kabla ya kujiingiza katika mahusiano mwanaume anatakiwa kupiga hesabu kama mtu aendaye vitani ajue kuwa anajiingiza katika gharama kubwa sana Luka 14:31 “Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?

 

Kila mwanaume ana nguvu ya kutubu na kufanya mabadiliko katika maisha yake, kama mapenzi yanachukua nafasi kubwa sana katika kazi zetu, na kutupa kupuuzia maswala ya msingi kama Familia na ibada kwa Mungu wetu tunazo nguvu za kutengeneza mambio ya nyumba zetu na kuwa watulivu, wote tunauwezo wa kushinda, wanaume wote kwa namna moja ama nyingine tuna udhaifu wote ukiacha Yesu Kristo, lakini iko nguvu katika maamuzi ambazo tunaweza kufanya, tunaweza kutubu, neno toba katiika kiyunani ni Mtanoia ambalo maana yake ni kugeuka kuna nguvu ya kufanya maamuzi ya kugeuka na kuacha njia zetu mbaya na tukajikuta tunafanikiwa badala ya kuzitumia nguvu zetu na kupotea tunaweza kuzitumia nguvu zetu katika kumtii Mungu  

 

Na Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!     



Jumapili, 20 Agosti 2023

Biblia na Umisheni!


Mathayo 28:18-19 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”





Utangulizi:

Mojawapo ya jambo kubwa na Muhimu sana katika kuyatenda mapenzi ya Mungu ni pamoja na kufanya kazi ya umisheni, Kazi ya umisheni ndio mapenzi halisi ya Mungu, wakati wote kanisa linapaswa kukumbuka kuwa mojawapo ya sehemu muhimu ya utekelezaji wa agizo kuu ni pamoja na kazi ya umisheni na haya ndio mapenzi ya Mungu kwetu! Kusudi kubwa mataifa yote wamjue Mungu na kumwamini mwana wa Mungu Yesu Kristo ili wawe na uzima wa milele

Yohana 17:3 “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.”

UMUHIMU WA KUFIKIRI KUHUSU ULIMWENGU.

ü  Mpango wa Mungu wa Wokovu hauhusu tu Utamaduni mmoja au taifa moja pekee. 

ü  Mungu hajawahi kufikiri kuhusu Mtu mmoja tu au taifa moja pekee 

ü  Mpango wa Mungu wa wokovu unahusu Ulimwengu mzima, na unaanza na mtu mmoja, Familia, taifa na ulimwengu mzima 

ü  Mungu anapokuita wewe na kukubariki kumbuka sio kwaajili yako tu na Familia yako, au watu wako na taifa lako tu bali ni  kwaajili ya ulimwengu mzima 

ü  Kwa hiyo lolote ambalo Mungu amekuita kulifanya na kulitenda ni kwaajili ya Ulimwengu mzima

 

MUNGU ALIPOMUITA IBRAHIMU.

Mwanzo 12:1-3 BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za DUNIA watabarikiwa.

MUNGU ALIPOMUITA YEREMIA.

Yeremia 1:4-5 Neno la Bwana lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

MUNGU ALIPOTUPA YESU KRISTO.

Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ULIMWENGU, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

BIBLIA NA UMISHENI

ü  Biblia inazungumzia kuhusu Umisheni

ü  Umisheni ni nini?

ü  Umisheni ni agizo muhimu analopewa mtu au watu, linalohusiana na kutoka au kuwaendea watu wa utamaduni tofauti kwa kiyunani “APOSTOLOS” AU APOSTELLO yaani Utume

ü  Ni Sauti ya wito wa kiimani au kidini au kimaandiko, au kidhehebu hususani Wakristo kutoka na kwenda kutimiza Agizo kuu Duniani kwa kusambaza na Kuhubiri Habari njema za Bwana Yesu

ANGALIA AGIZO KUU

Mathayo 28:18-20Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye MATAIFA yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;  na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

UMUHIMU WA UMISHENI

ü  Kwa sababu wanadamu wote Wamepotea  

ü  Luka 19:10 “Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea” 

ü  Umisheni ndio mapenzi kamili ya Mungu 

ü  Ni Agizo kuu kuhubiri injili Mathayo 28:18-20 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” 

ü  Kutakuwa na kuwajibika kwaajili ya damu ya mtu mwovu kama hatutafanya sehemu yetu

 

Ezekieli 33:8-9 “Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako.”     

 

ZABURI 14:1-3

Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja. 

WATU WOTE WAMEFANYA DHAMBI

WARUMI 3:10-12, 23

kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja. 23.kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;

 

YESU NI KIELELEZO.

ü  Akizungumza juu ya Huduma aliyokuja kuifanya Duniani Yesu yeye mwenyewe alisema wazi kwanini amekuja Ulimwenguni 


ü  Luka 19:10 - Alikuja kuokoa na kutafuta kilichopotea 


ü  Mathayo 18:11- Alikuja kutafuta kilichopotea 


ü  Mathayo 18:14 – Mungu hataki awaye yote apotee 


ü  Mathayo 18:12-13 Mtu mmoja atubuye ni muhimu kuliko 99 wasio na hitaji la toba 


ü  Luka 15:7,10,32 – Kuna furaha kubwa mbinguni kwaajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye

 

MUNGU NDIYE MWANZILISHI WA UMISHENI.

 

ü  Mpango wa Ukombozi uliandaliwa na Mungu ni yeye ndiye aliyemtafuta mwanadamu Mwanzo 3:8-9 “Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone. BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? ” 


ü  Mungu hataki mtu yeyote apotee Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” 


ü  Alishuka Wajati wana wa Israel wanaonewa Kutoka 3:7-10 “BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa. Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.”   

      

ü  Anataka watu wote wafikilie Toba – 2Petro 3:9 “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” 


ü  Baba wa Mbinguni hafurahii awaye yote apotee Mathayo 18:12-14 “Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je! Hawaachi wale tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea? Hata akipata kumwona, amin, nawaambia, amfurahia huyo zaidi, kuliko wale tisa na tisini wasiopotea. Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee.” 

WITO WA UMISHENI

 



Yesu ni Mfano wa Umisheni

  1. Utii
  2. Kujikana nafsi
  3. Huruma
  4. Kusudi

 

 

















Matendo 16:9-10

Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema

UMISHENI UNAHITAJI UTII 

Yesu alikuwa mtii katika mapenzi ya Mungu yote 

 

Zaburi 40:7-8 Ndipo niliposema, Tazama nimekuja, (Katika gombo la chuo nimeandikiwa,) Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.” 

 

Waebrania 10:5-7 Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari; Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu

 

UMISHENI UNAHITAJI KUJIKANA NAFSI

 

ü  Yesu alijikana nafsi 

ü  Hakuna mahali popote ambapo Yesu alitumikia umimi au kuonyesha au kunena kuhusu mambo yake 

ü  Kila alichokifanya ilikuwa ni kwaajili ya kumpendeza Mungu baba yake na kuwahudumia watu 

ü  Majaribu yote yaliyomjia Yesu Kristo kutoka kwa Shetani ilikuwa yalilenga kujihurumia yeye 

ü  Matthew 4:1-11, “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.” 

ü  Mark 1:12-13, “Mara Roho akamtoa aende nyikani. Akawako huko jangwani siku arobaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu, na malaika walikuwa wakimhudumia.” 

ü   Luke 4:1-13 “Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa. Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate. Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde; na ya kwamba,mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda.” 

ü  Huu ni ushahidi wa majaribu ambayo Yesu aliyashinda  

 

UMISHENI UNAHITAJI HURUMA  

 

ü  Yesu aliongozwa na huruma kubwa kwa wanaoteseka na wanaopotea 

ü  Wakati wote alisukumwa na huruma kwa wanadamu Mathayo 9:36-38 “Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji. Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.” 

ü  Alivuka mipaka na kwenda kuwahudumia watu waliokataliwa na waliokuwa na dhambi Yohana 4:3-10. aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya. Naye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria. Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe. Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita. Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe. Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula. Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.) Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai.”  
           

ü  Mtu wa huzuni nyingi ajuaye sikitiko aliyechukua mateso yetu Isaya 53:3-4 “Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.”  

 

UMISHENI UNAHITAJI KUKAA KWENYE KUSUDI LA MUNGU  

 

ü  Yesu alihakikisha anakaa katika kusudi wakati wote 

ü  Mara kadhaa Yesu alijaribiwa na watu ili atoke katika kusudi 

ü  Kuna wakati watu walitaka kumfanya yeye kuwa mfalme Yohana 6:15 “Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.” 

ü  Na kuna wakati Shetani alimtumia moja ya wanafunzi wake Kumzuia asiende msalabani Mathayo 16:22-23 “Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.” 
         

ü  Ndugu zake pia hawakumuelewa Mathayo 12:46-50 “Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye. Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe. Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani? Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu! Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.”              

John 7:3-9. “Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. Kwa maana hakuna mtu afanyaye neno kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhihirishe kwa ulimwengu. Maana hata nduguze hawakumwamini. Basi Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote upo. Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. Kweeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sikwei bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa haujatimia wakati wangu. Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alikaa vivi hivi huko Galilaya.”            

 

UMISHENI UNAHITAJI NGUVU ZA MUNGU

 

ü  Umisheni sio rahisi bila kuwa na nguvu za Mungu 

ü  Musa hakuenda Misri bila nguvu za Mungu, alikabiliana na Yane na Yambre wachawi wakubwa waliomsaidia Farao 2Timotheo 3:8, “Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.” 

ü  Kutoka 7:20-22 “Musa na Haruni wakafanya hivyo, kama BWANA alivyowaambia; naye akaiinua ile fimbo, na kuyapiga maji yaliyokuwa mtoni, mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake; na hayo maji yote yaliyokuwa katika mto yakageuzwa kuwa damu. Hao samaki waliokuwa mtoni nao wakafa; na ule mto ukatoa uvundo, Wamisri wasipate kunywa maji ya mtoni; na ile damu ilikuwa katika nchi yote na Misri. Lakini waganga wa Misri wakafanya mfano wa hayo kwa uganga wao; na moyo wake Farao ukawa mgumu, wala hakuwasikiza, kama BWANA alivyonena.” 
     

ü  Filipo alipambana na Simon Mchawi Matendo 8:5-21 “Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiri Kristo. Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa. Ikawa furaha kubwa katika mji ule. Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa. Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu. Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake. Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka. Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana; ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu. Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema, Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu. Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.”  

            

ü  Paulo mtume alipambana na Elima yule Mchawi Matendo 13:6-12 “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu; mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,  akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.” 


ü  Samsoni dhidi ya wafilisti Waamuzi 15:14-16 “Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo roho ya Bwana ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake. Naye akaona mfupa mbichi wa taya ya punda, akautwaa, akapiga watu elfu kwa mfupa huo; Samsoni akasema, Kwa taya ya punda chungu juu ya chungu, Kwa taya ya punda nimepiga watu elfu.”    

        

ü  Eliya dhidi ya Manabii wa baali 1Wafalme 18:21-40 “Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini? Bwana akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno. Ndipo Eliya akawaambia watu, Mimi nimesalia, mimi peke yangu, nabii wa Bwana; lakini manabii wa Baali ni watu mia nne na hamsini. Kwa hiyo na watutolee ng'ombe wawili; wao na wajichagulie ng'ombe mmoja, wamkate-kate na kumweka juu ya kuni, wasitie moto chini; nami nitamtengeza huyo ng'ombe wa pili, na kumweka juu ya kuni, wala sitatia moto chini. Nanyi ombeni kwa jina la mungu wenu, nami nitaomba kwa jina la Bwana; na Mungu yule ajibuye kwa moto, na awe ndiye Mungu. Watu wote wakajibu wakasema, Maneno haya ni mazuri. Eliya akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng'ombe mmoja, mkamtengeze kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini. Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya madhabahu waliyoifanya.  Ikawa, wakati wa adhuhuri, Eliya akawafanyia dhihaka, akasema, Mwiteni kwa sauti kuu; maana ni mungu huyo; labda anazungumza, au ana shughuli, au anasafiri, au labda amelala, sharti aamshwe. Wakapiga kelele, wakajikata-kata kwa visu na vyembe kama ilivyo desturi yao, hata damu ikawachuruzika. Ikawa, wakati wa adhuhuri ulipopita, walitabiri hata wakati wa kutoa dhabihu ya jioni; lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu, wala aliyeangalia. Kisha Eliya akawaambia watu wote, Nikaribieni mimi. Watu wote wakamkaribia. Akaitengeneza madhabahu ya Bwana iliyovunjika. Eliya akatwaa mawe kumi na mawili, kwa hesabu ya kabila za wana wa Yakobo, aliyejiliwa na neno la Bwana na kuambiwa, Jina lako litakuwa Israeli. Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la Bwana; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu. Kisha akazipanga zile kuni, akamkata yule ng'ombe vipande vipande, akaviweka juu ya kuni. Akasema, Jazeni mapipa manne maji, mkayamwage juu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya kuni.  Akasema, Fanyeni mara ya pili. Wakafanya mara ya pili. Akasema, Fanyeni mara ya tatu. Wakafanya mara ya tatu.  Yale maji yakaizunguka madhabahu; akaujaza mfereji maji. Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. Unisikie, Ee Bwana, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, Bwana, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie. Ndipo moto wa Bwana ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji. Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, Bwana ndiye Mungu, Bwana ndiye Mungu. Eliya akawaambia, Wakamateni hao manabii wa Baali, asiokoke hata mmoja. Wakawakamata; na Eliya akawachukua mpaka kijito cha Kishoni, akawaua huko.”    

           

ü  Tunapotumwa katika umisheni tutakutana na watu, na serikali zinazotegemea nguzu za giza na sio Mungu Mwanzo 41:1-8 “Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. Na tazama, ng'ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini. Na tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto. Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu. Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.” 


ü  Huwezi kuigiza nguvu za Mungu Matendo 19:11-20 “Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida; hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka. Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa. Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa. Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao. Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha hamsini elfu.Hivyo ndivyo neno la Bwana lilivyozidi na kushinda kwa nguvu.” 


ü  Ni lazima tuwe na Nguvu za Mungu Waefeso 6:12, “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” 

ü  2Wakorintho 10:4, (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)     
            

ü  Matendo 1:8, “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” 

ü  Luka 24:49 “Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.”

 

UMISHENI UNAHITAJI FEDHA

 

ü  Kazi ya umisheni inahitaji watu watakaoifadhili Warumi 10:13-15 “kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!” 

ü  Yesu alikuwa na watu waliokuwa wakiifadhili huduma yake Luka 8:1-3 “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye, na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba, na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.” Kama sisi hatuendi tunaweza kwenda kwa njia ya maombi na ufadhili 

ü  2 Wakorinthio8:9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.”

 

MAVUNO YAKO TAYARI

 

Yohana 4:35 “Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno.”

 

INUENI MACHO YENU MASHAMBA YAKO TAYARI

 


 

UMISHENI UNAWEZA KUFANYIKA KATIKA KILA HALI

 

Binti aliyekuwa kijakazi huko Shamu 2Wafalme 5:1-14 “Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake Bwana alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma. Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani. Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake. Mtu mmoja akaingia, akamwambia bwana wake, akasema, Yule kijana mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi na hivi. Mfalme wa Shamu akasema, Haya! Basi, mimi nitampelekea mfalme wa Israeli waraka. Basi akaenda zake, akachukua mikononi mwake talanta kumi za fedha, na vipande vya dhahabu elfu sita, na mavazi kumi. Akampelekea mfalme wa Israeli waraka ule, kusema, Waraka huu utakapokuwasilia, tazama, nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, ili upate kumponya ukoma wake. Ikawa, mfalme wa Israeli alipousoma waraka, alirarua mavazi yake, akasema, Je! Mimi ni Mungu, niue na kuhuisha, hata mtu huyu akanipelekea mtu nimponye ukoma wake? Fahamuni, basi, nakusihini, mwone ya kuwa mtu huyu anataka kugombana nami. Ikawa, Elisha, yule mtu wa Mungu, aliposikia kwamba mfalme wa Israeli ameyararua mavazi yake, ndipo akatuma mtu kwa mfalme, akisema, Mbona umeyararua mavazi yako? Na aje sasa kwangu mimi, naye atajua ya kuwa yuko nabii katika Israeli. Basi Naamani akaja na farasi wake na magari yake, akasimama mlangoni pa nyumba ya Elisha. Naye Elisha akampelekea mjumbe, akisema, Enenda ukaoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi. Lakini Naamani akakasirika, akaondoka, akasema, Tazama, nalidhania, Bila shaka atatoka kwangu, na kusimama, na kuomba kwa jina la Bwana, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma. Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! Siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi? Akageuka, akaondoka kwa hasira. Watumishi wake wakamkaribia, wakamwambia, wakasema, Baba yangu, kama yule nabii angalikuambia kutenda jambo kubwa, usingalilitenda? Je! Si zaidi basi, akikuambia, Jioshe, uwe safi? Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi.” 

 

ü  Alikuwa ni binti kijana na mtumwa tu

ü  Alikuwa na busara na alionyesha upendo

ü  Alikumbuka Nguvu za Mungu wa Israel 

ü  Alihubiri habari za uweza wa Mungu wa Israel kwa mkuu wa Majeshi ya Syria 

ü  Mkuu wa majeshi ya Syria alimuamini Mungu wa Israel 2Wafalme – 5:14-15 “Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi. Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako.”

ü   Ni kupitia Binti Mtumwa mjakazi mwenye ujasiri na Busara mtu mkubwa sana mkuu wa majeshi wa Syria alimuamini Mungu wa Israel na kuponywa ukoma wake

 

Mfano wa vijana watatu utumwani 

 

Daniel 3:16-18 “Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”          

Hanania, na Mishaeli, na Azaria, ni vijana waliochukuliwa utumwani kule Babeli, tamaduni yao lugha yao majina yao yalibadilishwa Daniel 1:2-7 “Bwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika mkono wake, pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu; naye akavichukua mpaka nchi ya Shinari, mpaka nyumba ya mungu wake; akaviingiza vile vyombo katika nyumba ya hazina ya mungu wake.Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana; vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao. Huyo mfalme akawaagizia posho ya chakula cha mfalme, na ya divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme. Basi katika hao walikuwapo baadhi ya wana wa Yuda, Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria. Mkuu wa matowashi akawapa majina; alimwita Danieli, Belteshaza; na Hanania akamwita Shadraka; na Mishaeli akamwita Meshaki; na Azaria akamwita Abednego.”

      

Walilazimishwa kuabudu miungu ya huko, lakini kwa ujasiri mkubwa walishuhudia kuwa yuko Mungu wa kweli Duniani Daniel 3:16-18 “Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”       

    

Kupitia ujasiri wao na imani yao Waliweza kumshawishi Mfalme kumuabudu Mungu wa Israel ona Daniel 3:28-29 Nebukadreza akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe. Basi mimi naweka amri ya kuwa kila kabila ya watu, na kila taifa, na kila lugha, watakaonena neno lo lote lisilopasa juu ya huyo Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watakatwa vipande vipande, na nyumba zao zitafanywa jaa; kwa kuwa hakuna Mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii.”               

 

Mfano wa Daniel Kupitia Tundu la Simba 

 

Daniel 6:1-28 “Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote; na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara. Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote. Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake. Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake. Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele. Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba. Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika. Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku. Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo. Basi watu hao wakakusanyika pamoja, wakamwona Danieli akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu wake. Ndipo wakakaribia, wakasema mbele ya mfalme katika habari ya ile marufuku ya mfalme; Je! Hukuitia sahihi ile marufuku, ya kwamba kila mtu atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme, atatupwa katika tundu la simba? Mfalme akajibu, akasema, Neno hili ni kweli, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi isiyoweza kubadilika. Basi wakajibu, wakasema mbele ya mfalme, Yule Danieli, aliye mmoja wa wana wa wale waliohamishwa wa Yuda, hakujali wewe, Ee mfalme, wala ile marufuku uliyoitia sahihi, bali aomba dua mara tatu kila siku. Basi mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danieli; akajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa. Ndipo watu wale wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya kuwa ni sheria ya Wamedi na Waajemi, lisibadilike neno lo lote lililo marufuku, wala amri yo yote iliyowekwa na mfalme. Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya. Likaletwa jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia muhuri kwa muhuri yake mwenyewe, na kwa muhuri ya wakuu wake, lisibadilike neno lo lote katika habari za Danieli. Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa. Asubuhi mfalme akaondoka mapema, akaenda kwa haraka mpaka penye lile tundu la simba. Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa? Ndipo Danieli akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele. Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno. Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile tundu. Ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake. Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu. Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, waliokaa juu ya uso wa dunia; Amani na iongezeke kwenu. Mimi naweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho. Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara na maajabu mbinguni na duniani, ndiye aliyemponya Danieli na nguvu za simba. Basi Danieli huyo akafanikiwa katika enzi ya Dario, na katika enzi ya Koreshi, Mwajemi.”

Alikuwa bora kuliko mawaziri wote 120 

Alihudumu Katika utawala wa Dario mmedi Daniel 6:1-3 “Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote; na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara. Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.”
       

Wenzake walitafuta namna ya kupata sababu za kumshitaki Daniel 6:4-9 “Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake. Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake. Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele. Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba. Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika. Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku.” 

Daniel Hakuacha kuomba Daniel 6:10-16, “Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo. Basi watu hao wakakusanyika pamoja, wakamwona Danieli akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu wake. Ndipo wakakaribia, wakasema mbele ya mfalme katika habari ya ile marufuku ya mfalme; Je! Hukuitia sahihi ile marufuku, ya kwamba kila mtu atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme, atatupwa katika tundu la simba? Mfalme akajibu, akasema, Neno hili ni kweli, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi isiyoweza kubadilika. Basi wakajibu, wakasema mbele ya mfalme, Yule Danieli, aliye mmoja wa wana wa wale waliohamishwa wa Yuda, hakujali wewe, Ee mfalme, wala ile marufuku uliyoitia sahihi, bali aomba dua mara tatu kila siku. Basi mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danieli; akajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa. Ndipo watu wale wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya kuwa ni sheria ya Wamedi na Waajemi, lisibadilike neno lo lote lililo marufuku, wala amri yo yote iliyowekwa na mfalme. Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.”  na kwaajili hiyo alitupwa katikamtundu la Simba 

Mungu alimuokoa Daniel na kuwa ushuhuda kwa mfalme na taifa zima Daniel 6:20-27 “Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa? Ndipo Danieli akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele.Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno. Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile tundu. Ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake. Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu. Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, waliokaa juu ya uso wa dunia; Amani na iongezeke kwenu. Mimi naweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho.  Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara na maajabu mbinguni na duniani, ndiye aliyemponya Danieli na nguvu za simba.”



Mfano wa Nabii Yona huko Ninawi

 

Aliitwa na Mungu kwenda katika jiji la Ninawi  – Yona 1:1 “Basi neno la Bwana lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema,” 

Yona aliamua kukimbia kwenda nchi ya mbali zaidi Yona 1:3 “Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa Bwana; akatelemka hata Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa Bwana.” 

Mungu alisababisha tatizo kubwa lililopelekea yona kutupwa baharini Yona 1:4-10 “Lakini Bwana alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwa baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika. Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi. Basi nahodha akamwendea, akamwambia, Una nini, Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee. Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na mpige kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona. Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani? Akawaambia, Mimi ni Mwebrania; nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi kavu. Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha.” 

Yona alitupwa baharini , na kumezwa na nyangumi Yona 1:12 “Naye akawaambia, Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itatulia; kwa maana najua ya kuwa ni kwa ajili yangu tufani hii imewapata.” 

Mungu alimuamuru Samaki mkubwa kumtapika Yona na kumuita mara ya pili, alitii na kuhubiri mji wa Ninawi na mfalme na watu wote wakamgeukia Mungu  Yona 3:4-10 “Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng'ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe? Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.”       

 

Mfano wa Mfalme Suleimani na Hekima yake 

 

Mungu alimpa Mfalme Suleimani Hekima kubwa sana 1Wafalme 10:1-5 “Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Sulemani juu ya jina la Bwana, alikuja ili amjaribu kwa maswali ya fumbo. Akaingia Yerusalemu na wafuasi wengi sana, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikilia Sulemani, akazungumza naye mambo yote aliyokuwa nayo moyoni. Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala hakukuwa na neno alilofichiwa mfalme asimwambie. Naye malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Sulemani, na nyumba aliyokuwa ameijenga, na chakula cha mezani pake, na watumishi wake walivyokaa, na kusimamia kwao wangoje wake, na mavazi yao, na wanyweshaji wake, na daraja yake ya kupandia mpaka nyumba ya Bwana, roho yake ilizimia.” 

Suleimani Mwana wa Daudi aliweka wazi kuwa mpango wa Mungu ulikuwa ni kwa mataifa yote

Alijenga Nyumba ya Mungu ambayo ilikuwa na utikufu mkubwa sana uliovutia watu wa dunia nzima

Wafalme wengi maarufu walikuja kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuisikia hekima ya suleimani na kuona nyumba ya kifahari aliyoijenga, maalumu sana Malikia wa Sheba (Ethiopia) alisema wazi kuwa habari alizosikia kuhusu Suleimani ni za kweli na zaidi hata ya kile alichokisikia 1Wafalme 10:6-7“Akamwambia mfalme, Ndizo kweli habari zile nilizozisikia katika nchi yangu za mambo yako na za hekima yako. Lakini mimi sikuzisadiki habari hizo, hata nilipokuja na kuona kwa macho yangu; tena, tazama, sikuambiwa nusu; wewe umezidi kwa hekima na kufanikiwa kuliko habari nilizozisikia.”

 

Mfano wa Hekalu la Mfalme Sulamani

 


Nyumba ya Mungu yenye Mvuto Mkubwa sana

 

1Wafalme 8: 41 - 43 “Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako; (maana watasikia habari za jina lako kuu, na za mkono wako ulio hodari, na za mkono wako ulionyoshwa); atakapokuja na kuomba kuielekea nyumba hii; basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukatende kwa kadiri ya yote atakayokuomba mgeni huyo; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe kama watu wako Israeli, nao wajue ya kuwa nyumba hii, niliyoijenga, imeitwa kwa jina lako.”

 


Sehemu ya mabaki ya ukuta wa Hekalu imekuwa na mvuto mpaka leo

Kwa wayahudi wenyewe


Kwa wanasiasa na viongozi maarufu duniani



Donald Trump



 


 Brack Obama


 

William Ruto Rais wa Kenya 


Shinzo Abe aliyewahi kuwa waziri mkuu maarufu wa Japan

Waziri mkuu wa Israel Mwenyewe Benjamin Netanyahu


 

Pope Benedict wa 16


 

 

Pope Francis

 

Mfano wa Paulo na sila

 

Walikuwa katika kazi ya umisheni wakafungwa – Matendo 16:23-31 “Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana. Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.  Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa. Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia. Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa. Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila; kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.”  
          

Walishambuliwa na kupigwa kwaajili ya injili na wakatupwa gerezani, lakini waliitumia hali hiyo Kuomba na kumuimbia Mungu wa Kweli, Mungu alisababisha Magereza kutikisiaka Matendo 16:25-26 “Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.”  
  

Hali ilimalizika kwa mkuu wa gereza kumuamini Yesu kuwa ni Bwana na mwokozi na yeye na nyumba yake kubatizwa Matendo 16:30-33 “kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake. Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo.”

 

Mfano wa Mtumwa aliyemkimbia Bwana wake

 

Onesmo mtumwa wa Philemon alimkimbia bwana wake  na kufungwa Gerezani - Philemoni 1:1-9 “Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yetu, kwa Filemoni mpendwa wetu, mtenda kazi pamoja nasi, na kwa Afia, ndugu yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo. Namshukuru Mungu wangu sikuzote, nikikukumbuka katika maombi yangu; nikisikia habari za upendo wako na imani uliyo nayo kwa Bwana Yesu na kwa watakatifu wote; ili kwamba ushirika wa imani yako ufanye kazi yake, katika ujuzi wa kila kitu chema kilicho kwetu, katika Kristo. Maana nalikuwa na furaha nyingi na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu imeburudishwa nawe, ndugu yangu. Kwa hiyo, nijapokuwa nina ujasiri katika Kristo kukuagiza likupasalo; lakini, kwa ajili ya upendo nakusihi, kwa kuwa ni kama nilivyo, Paulo mzee, na sasa mfungwa wa Kristo Yesu pia.” 

Wakati huo Paulo Mtume alikuwa amefungwa Gerezani, ndani ya gereza alikutana na Onesmo aliyemkimbia Bwana wake ambaye ni Mwanafunzi wa Paulo mtume, Mwanafunzi huyo ni Filemoni 

Paulo mtume alimuhubiri Onesmo ambaye aliiamini injili, na alipokuwa anaachiwa paulo akliandika waraka wa kumuombea Msamaha na kuwapatanisha Onesmo na Filemoni 

Kwa kuwa sasa amebadilika kupitia injili na mafundisho ya Mtume Paulo akiwa kifungoni Philemoni  Philemon 1:10-18 “Nakusihi kwa ajili ya mtoto wangu niliyemzaa katika vifungo vyangu, yaani, Onesimo; ambaye zamani alikuwa hakufai, bali sasa akufaa sana, wewe na mimi pia; niliyemtuma kwako, yeye mwenyewe, maana ni moyo wangu hasa; ambaye mimi nalitaka akae kwangu, apate kunitumikia badala yako katika vifungo vya Injili. Lakini sikutaka kutenda neno lo lote isipokuwa kwa shauri lako, ili kwamba wema wako usiwe kama kwa lazima, bali kwa hiari. Maana, labda ndiyo sababu alitengwa nawe kwa muda, ili uwe naye tena milele; tokea sasa, si kama mtumwa, bali zaidi ya mtumwa, ndugu mpendwa; kwangu mimi sana, na kwako wewe zaidi sana, katika mwili na katika Bwana. Basi kama ukiniona mimi kuwa mshirika nawe, mpokee huyu kama mimi mwenyewe. Na kama amekudhulumu, au unamwia kitu, ukiandike hicho juu yangu.”

 

Mfano wa Filipo na Towashi wa Kushi (Ethiopia)

 

Filipo aqlielekezwa na Roho Mtakatifu kwa mtu huyu Muhimu kutoka Ethiopia Matendo 8:26-40 alimshuhudia habari za Kristo na injili ikafika nchini Ethiopia na bara la afrika mapema mnamo Karne ya Kwanza. 

Matendo 8:26-30 Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa. Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu, akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma?”

 

WITO KATIMA UMISHENI

 

Tunapopitia maandiko tunagundua kuwa bado Mungu anaita watu katika kazi ya umisheni 

Na pia tunagundua kuwa kwa njia yoyote na katika hali yoyote ile bado tunaweza kuihubiri habari njema kwa wengine, tunaweza kuwahubiri watu habari njema kwa maneno yetu na matendo yetu kwa njia yoyote 

Mungu ametuita ili tuwe baraka kwa wengine, katika hali yoyote ile tunaweza kumtumikia Mungu au tunamtumikia Mungu, popote tulipo sisi ni mabalozi wa Yesu 2Wakorintho 5:20 “Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.”

 

Mathayo 28:18-20

 

Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”

 

Matendo 1:8

 

Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”

 

1Nyakati 16:24

 

Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake.”

 

Yohana 20:21

Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.”


Warumi 10:13-15

 

kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!”

 

Isaya 52:7

 

Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!”

 

Marko 16:15

 

Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.”

Yeremia 1:7-8

 

Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru. Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana.”

 

Isaya 6:8

 

Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.”

 

2Timotheo 2:2

Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.”

 

Matendo 13:47

 

Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.”

 

Mathayo 24:14

 

Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.”

 

SWALI KWA KANISA LAKO

 

Ø  Je injili inahubiriwa ? 

Ø  Je ni kanisa ambalo watu wanaamini katika wokovu 

Ø  Biblia inatambuliwa kama mamlaka ya mwisho na neno la Mungu? 

Ø  Waamini au washirika wanajazwa Roho Mtakatifu? 

Ø  Je mnatazamia kurudi kwa Yesu Kristo mara ya Pili? 

Ø  Je Kanisa linapaleka wamishionari? 

Ø  Je wewe mwenyewe unajitathimini vipi?

 

RAMANI YA UMISHENI

 

Matendo 1:8

Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”

 

YERUSALEM 

-          Kuimarisha kanisa la mahali pamoja, kanisa litakaa katika mafundisho, watu watashuhudiwa, watu wataokoka na kubatizwa, watu watazaliana watafundishwa chini ya walimu na wachungaji ili waweze kuimarika na watamuomba Roho Mtakatifu kulizidisha kila wakati kwa idadi ya watu wanaookolewa, ukuaji kibailojia, kiidadi na kiroho 

-          Matendo 2:41-42 “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.”                

 

-          Matendo 5:28 “akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.”

 

-          Matendo 2:47 “wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.”

 

YUDEA

 

-          Kuhubiri nje ya kanisa la mahali pamoja

-          Kufungua matawi katika maeneo mengine

-          kupanda kanisa jipya

-          Kuwafikiwa watu wa tamaduni tofauti kidogo mfano Kenya na Tanzania

-          Kuwapelekea wachungaji na walimu kuwahudumia

-          Matendo 8:4 “Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno.”

 

SAMARIA NA HATA MWISHO WA NCHI

 

-          Hapa ndio Umisheni wenyewe

-          Hapa ni kuwafikiwa watu wa tamaduni tofauti

-          Hapa ni kuwafikia watu wa mabara tofauti

-          Kuwafikiwa watu wa dunia nzima

-          Kuwafikiwa watu wa Asia, watu wa Afrika, Ulaya na America na sehemu zote duniani

 

Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!