Jumapili, 7 Juni 2020

Nilichokiandika Nimekiandika!



Yohana 19:20-22 “Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulibiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani. Basi wakuu wa makuhani na Wayahudi wakamwambia Pilato, Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; bali ya kwamba yule alisema, Mimi ni mfalme wa Wayahudi.  Pilato akajibu, Niliyoandika nimeyaandika.



Utangulizi:


Leo tutachukua Muda kujifunza jambo la muhimu sana kutoka kwa moja ya Mtawala maarufu sana aliyehusika katika kumuhukumu Yesu Kristo kwenda msalabani na kusulubiwa, Mtawala huyu au Liwali kwa jina lingine anajulikana kama Pontus Pilatus kiwashili Pilato, Moja ya jambo la msingi sana tutakaloweza kujifunza ni kuhusu Msimamo wake na mtazamo wake  kuhusu Yesu kristo, tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo:-

·         Historia fupi ya Pontius Pilato
·         Niliyoyaandika nimeyaandika


Historia fupi ya Pontius Pilato *PONTIUS PILATUS*
Ponsyo Pilato  Moja ya watawala vijana sana kupata kutokea kama anavyoelezewa na Mwanahistoira maarufu wa karne ya kwanza aliyejulikana kama FLAVIUS JOSEPHUS aliyekuwa myahudi aliyekuwa na ujuzi wa lugha Kiaramu, Kiebrania na kigiriki (Aramaic, Latin and Greek) Lugha ambazo zilitumiwa na wasomi wengi wa nyakati ya karne ya kwanza  mtu huyu Flavius Josephus aliishi kati ya mwaka  37-100 BK na alikuwa kuhani Myahudi, alitekwa na warumi na kuwa Mkalimani wa Kaisari Vespasian kwa miaka miwili, Kitabu chake kinapatikana hata kwa ku- download electronic book kama Works of Flavius Josephus  ikitabu chake hicho ni  kirefu sana na kinachukua muda mrefu kukisoma.


Yeye anamuelezea Ponsyo Plato kwa kilatini PONTIUS PILATUS aliyekuwa liwali wa Kirumi katika inchi ya israel kati ya mwaka 26-36 wakati wa Yesu Kristo, yaani miaka 10 Pilato  Anajulikana kutokana na vyanzo mbalimbali, lakini hasa kwa sababu ya  Injili kumtaja kama hakimu aliyempeleka Yesu kuuawa msalabani. Historia yake ina0onyesha alipewa utawala akiwa kijana mdogo sana kwa sababu inasemekana alizaliwa mwaka wa 12 baada ya Yesu, kwa hivyo wakati wa hukumu ya Yesu yeye alikuwa na umri wa miaka 21 hivi, ukiacha kutajwa katika injili zote nne na kuelezewa zaidi katika injili ya Yohana pia anatajwa katika


Matendo ya
Mitume 3:13 “Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe utaweza kuona pia


Matendo ya mitume 4:27 27. Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta, ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee.”
Na pia anatajwa katika


Matendo 13:28 “Na ijapokuwa hawakuona sababu ya kumfisha wakamwomba Pilato auawe.”
Na Paulo mtume alimtaja tena katika kitabu cha

1Timotheo 6:13 ”Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato,”
unaweza kuona namna mtawala huyu anavyotajwa sana katika maandiko, maana yake ni kuwa alikuwa mtu maarufu ambaye wahubiri wa hyakati za kanisa la kwanza hawakuweza kumsahahu! Kwa karne nyingi Pilato amekuwa mtu asiyeweza kusahaulika pilato anatajwa pia katika ukiri wa imani, au imani ya nikea au imani ya mitume au sala ya nasadiki kama “Zamani za Pontio Pilato aliteswa


Pilato  maisha yake ya awali hayajulikani sana japo viko vyanzo vinavyoeleza kuwa alikuwa ni  Mtot aliyezaliwa nje ya Ndoa ya Mfalme wa Tiro,  ambaye alimtuma kwenda Rumi kama muhudumu na huko aliua mtu na akatumwa kupelekwa Asia ndogo kwa makusudi ya kushughulikia watu Korofi, kutokana na ukorofi wake mkubwa alipata kibali kwa Warumi alipewa zawadi ya kutawala kama gavana wa jimbo la Uyahudi (Judea)  na Mtawala Tiberio kwaajili ya kuwashughulikia Weayahudi ambao mara kwa mara waliasi.


Alikuwa mtawala Katili sana aliyeamuru kuuawa na kusulubiwa kwa wayahudi wengi sana,  adiah aliwaudhi wayahudi sana kwa kuleta desturi za kirumi na hata kukleta habari za miungu migenikwenye hekalu, wakati mwingine aliweza hata kuchukua kodi za hekaluni na kuzitumia kwa matumizi yasiyofaa alikuwa muuaji na mtu aliyeweza kuwaua wayahudi vibaya sana moja ya habari za ukatili wake zilienea wakati wa Yesu ona katika 

Luka 13:1
Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.”

Nilichokiandika nimekiandika!

Inasemekana makazi makuu ya Pilato yalikuwa ni Kaisaria hata hivyo Pilato alikuwa na desturi ya kuja Yerusalem siku za sikukuu kwaajili ya kutuliza Ghasia na kuwadhibiti wayahudi, wakati wa kukamatwa kwa Yesu, kwa vile yalikuwa ni majira ya Pasaka Pilato alikuwako Yerusalem, wakuu wa makuhani walipokwisha kumuhukumu Yesu kwa mila na desturi zao, waliona vema pia kumpeleka kwa Pilato walifahamu tabia zake na hivyo walijua kuwa kwa ukatili aliokuwa nao Hakuna myahudi anayehusishwa na vurugu angeweza kusalimika, mambo kadhaa yaliweza kujitokeza wakati wa hukumu ya Bwana Yesu

Moja ya muujiza mkubwa sana kuwahi kutokea ni kwa jamaa huyu muuaji na katili kuonekana akinawa mikono na kugoma kumpeleka Yesu Msalabani  kwa sababu alibaini wazi kuwa Yesu hakuwa na hatia yoyote na alielewa kuwa Wayahudi wanamleta kwake kwa sababu ya husuda tu hili lilikuwa jambo la kushangaza kwa vile alikuwa hacheleweshi kesi, na haponyi mtu, kusitasita katika kumuhukumu Bwana Yesu ilikuwa ni moja ya tabia mpya na ya ajabu iliyowastaabisha wayahudi kwa sababu walijua wamempeleka penyewe, Aidha Familia yake ilikuwa na taarifa za Mapema kuwa anakuja mtu mwenye haki na kuwa Pilato anapaswa kuwa na tahadhari namna atakavyoshughulika na kesi ya mtu huyo ujumbe huu alipewa na mke wake akimtahadharisha kuhusu hukumu ya siku ile Pamoja na hayo alifanya kila jitihada kumuokoa Yesu kupitia Mfungwa aliyekuwa hatari na muhaini zaidi kuliko Yesu lakini hata hivyo wakuu wa dini bado walijaa husuda yaani wivu dhidi ya Yesu Ona


Mathayo 27: 16-19 “Basi palikuwa na mfungwa mashuhuri siku zile, aitwaye Baraba. Basi walipokutanika, Pilato akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi? Yule Baraba, au Yesu aitwaye Kristo? Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa husuda. Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.”  


Pilato pia alikuwa ni mtu pekee aliyeweza kupata nafasi ya kuzungumza na Yesu kipekee na kujua kusudi la kuwepo kwa Yesu Duninani. Yeye alimuelewa wazi Yesu kuwa amekuja kuishuhudia kweli, na kuwa yeye mwenyewe Yesu ndio kweli, aidha alitambua wazi kupitia Yesu kuwa mamlaka aliyonayo yeye imetoka juu yaani imetoka kwa Mungu na pia alipata nafasi ya kujua na kuelewa kuwa Yesu alikuwa mfalme kweli lakini ufalme wake haukuwa wa ulimwengu huu


Yohana n18:33-38a “Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi? Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu? Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini? Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa. Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu. Pilato akamwambia, Kweli ni nini?


Ni wazi kabisa mpaka wakati Pilato anakuja kutoa hukumu kupitia mashinikizo ya kisiasa kutoka kwa wayahudi tayari kitu Fulani kilikuwa kimejengeka moyoni mwake kuhusu Yesu Kristo na kama isingalikuwa maandiko yatimizwe ni wazi kuwa Pilato angemuachia Yesu huru!


Hapa sasa tunaona wazi kuwa Maadui wa Yesu Kristo walikuwa wanategemea kuwa kwa kuwa wamemleta Yesu Kwa Pilato hawezi kusalimika lakini hawakuwa wamejua kuwa  Mungu aliandaa kitu katika Moyo wa Pilato na kuwa hawakujua kuwa Pilato alikuwa anaujua wivu wao na akaandaa  aibu kubwa sana na udhalilishaji ambao wangeupata kuhusu ubaya wao huo, aibu hii yalikuwa ni maneno yaliyowekwa na Pilato juu ya Msalaba wa Yesu.

Pilato aliandika meneno hayo na kuyaweka katika msalaba wa Yesu yaliyokuwa yakisomeka “YESU WA NAZARETH MFALME WA WAYAHUDI Wayahudi wengi sana waliyasoma maneno haya kwa sababu mahali aliposulubiwa Yesu palikuwa ni karibu na lango la jiji la Yerusalem na ni mahali ambako wengi walipita, Meneno haya yaliandikwa kwa lugha kubwa tatu Kiaramu, Kilatini na Kiyunani hivyo yaliweza kusomwa na watu wote hata wageni waliokuja kutoka sehemu mbalimbali duniani kwaajili ya sikukuu ya pasaka, wakuu wa makuhani hawakuyafurahia hata kidogo maneno yale kwa hiyo walimwendea Pilato na  kumwambia, Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; bali ya kwamba yule alisema, Mimi ni mfalme wa Wayahudi Pilato akajibu, Niliyoandika nimeyaandika.”
Ilikuwa ni desturi kwa kila muhalifu anayehukumiwa kusulubiwa  na warumi kuwekewa mashitaka yake juu ya msalaba ili kwamba kila anayepita aweze kuona ili iwe fundisho kwake, Lakini kwa Kristo ilikuwa kitu cha kushangaza sana ! hayakuwa mashitaka bali lilikuwa Tangazo halisi kwa ufunuo halisi

Yesu hakuonekana na hatia alikuwa amehukumiwa kwa sababu ya wivu wa wayahudi tu na Pilato alifahamu, Wayahudi walikuwa wamechukizwa naye kwa sababu yeye alisema wazi kuwa ni mwana wa Mungu na pia ndiye mrithi halali wa kiti cha ufalme cha Daudi baba yake, Pamoja na hayo miujiza mikubwa aliyoitenda na umati mkubwa uliomfuata na kumkubali ulisababisha wayahudi kupoteza umaarufu wao wa kidini, watu walikuwa wamemkubali Yesu kuwa ndiye masihi wao, Wayahudi na Viongozi wa kidini  wao walijua kwa makosa haya ingeweza kumshawishi Pilato kutoa hukumu kali kwa kufikiri kuwa Yesu anamuasi kaisari kwa kujiita Mfalme, Lakini Pilato alielea ukweli Yesu ni mfalme wa namna gani na  kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao Viongozi wa dini, kwa hivyo hakukuwa na mashitaka zaidi ya hayo Kila ambaye angeona mashitaka hayo angeweza kueneza habari kuwa Yuko Mfungwa amesulubiwa msalabani na ni Mfalme wa wayahudi, hana makosa mengine ni mfalme wa wayahudi habari zingeweza kuenea Rumi, Uyahudi na kila mahali walikotumia lugha zile alizoandika Pilato, Bila shaka kosa hili la uandishi halikuwa kosa la kibinadamu,  wala Pilato hakuwa amekosea katika kile alichokiandika ilikuwa wazi kabisa kwamba Pilato alikuwa na ufunuo sahihi kuwa Yesu alikuwa Mfalme wa Kiroho kwa watu wote  walipomwambia ayaondoe maneno yale Pilato alijibu  kwa kiyunani Ho Gegrapha gegrapha! na kilatini Quod scrips scrips, what i have written I have written yaani Nilichokiandika nimekiandika  Pilato alimaanisha kuwa ujuzi wake kuhusu Yesu hakuna mtu wa aina yoyote anaweza kuubatilisha ule ulikuwa ni ukweli uliowazi kabisa ambao Pilato alikuwa ameubaini na ambao alitaka watu wote watambue, Kila mmoja leo anapaswa kukubali na kutambua Kuwa Yesu ni Mashihi, Yeye ndiye aliyekusudiwa kwa wayahudi na ulimwengu mzima litakuwa ni jambo la ajabu sana kwa Mtu mkatili ikama Pilato kubaini ukweli na kujua kuwa Yesu ni mfalme wa wayahudi na akaanidla kwa lugha tatu kuu za wakati uoe akitaka kila mtu na kila lugha na kila taifa wajue  YESU WA NAZARETH HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI, Viongozi wa kidini walimsihi ayaondoe maneno hayo lakini jambo lingine la kushangaza aligoma alisema *NILICHIKIANDIKA NIMEKIANDIKA* Kwa lugha nyingine Pilato alikuwa anasema amethibitisha, ana uhakika, alichikithibitisha hakiwezi kutenguliwa milele, Pilato alikuwa gavana alikuwa liwali alikuwa kiongozi mkubwa alikuwa katili alikuwa muuaji, alikuwa na mamlaka kubwa sana alihukumu Kesi ya yesu alikuwa kijana alikuwa na akili sana alikuwa katili lakini alikiri kwa maandiko tena hadharani ya kuwa Yesu ni mfalme wa Wayahudi, alikuwa anakubali wazi kuwa yesu ni Bwana aluikuwa ameifahamu kweli swali lake kubwa kwa Yesu Kweli ni nini ? Yesu ndiye njia na kweli na uzima, leo hii kila mmoja anapaswa kumkiri Yesu kwa utukufu wa Mungu baba haijalishi una cheo gani haijalishi umefanya dhambi ngapi umwamini Yesu, ukubali kuwa Yesu ni Bwana na uwe tayari kumtetea Yesu kwamba ulichokiamini umekiamini, ulichiokithibitisha umekithibitisha ulichokiandika umekiandika Yesu ni Mfalme wa wayahudi!

Kwa mujibu wa kanisa la Orthodox la Ethiopia wanamtambua Pilato kama Mtakatifu mwenye heri wakiamini kuwa alimkubali Yesu kwa kuokoka na hivyo ni mtu mwenye kuheshimika sana. Ndio maana anatajwa katika ukiri wa imani ya Mitume ! NILICHOKIANDIKA NIMEKIANDIKA!

Na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi, mwenye Hekima.
0718990796

Mkristo na Mitandao ya kijami



Luka 13:1-5Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.  Akawajibu akawaambia, Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.” 







Utangulizi:


Ni muhimu kufahamu kuwa taarifa (Habari) ni moja ya nyenzo yenye kubwa sana yenye kubeba maana zinazoweza kujenga au kubomoa jamii, taarifa zina nguvu, zina nguvu zote mbili za kujenga au kubomoa, Mungu ndiye mwanzilishi wa taarifa, Alipomuumba mwanadamu alimpa taarifa ya namna na jinsi ya kuutawala ulimwengu alimweleza kama mtu huru namna anavyoweza kuutumia ulimwengu na alimuelekeza namna nzuri ya kuutumia ulimwengu lakini pia alimuonya kuwa kama atautumia ulimwengu vibaya angeweza kuleta madhara makubwa kwa maisha yake na jamii yake yaani kifo. Taarifa inaweza kuwa ndogo lakini kama ikitumika vibaya inaweza kuleta madhara makubwa sana kwa jamii kama njiti ya kiberiti inavyoweza kuchoma msitu mzima! 


Ni muhimu kufahamu kuwa nyakati za Biblia pia kulikuwa na namna ambavyo watu waliweza kupokea na kutoa taarifa kama unavyoweza kuona katika kifungu hiki


Luka 13:1-5Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.  Akawajibu akawaambia, Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.” 


Yesu alikuwa amepokea taarifa au habari kuhusu Wagalilaya waliouawa vibaya na Pilato, na baada ya kupokea taarifa hizi tunaona namna Yesu alivyozitumia taarifa hizo sasa kuwafundisha watu wake somo kuhusu toba na pia akiunganisha na taarifa nyingine ya watu kumi walioangukiwa na mnara huko siloamu, Kutoa na kupokea taarifa ni haki ya kila jamii, Yesu aliitumia taarifa hii kwa sababu huenda aliamini au kulikuwa na namna ya uthibitisho kuwa chanzo cha taarifa alichokipokea kilikuwa ni chanzo cha kuaminika na kwa sababu hiyo taarifa alizozipokea zilikuwa na ukweli, na hivyo alizitumia kufundisha kama mfano kwa jamii iliyomzunguka, Unapochunguza kwa kina mafundisho ya Yesu Kristo utaweza kuona alikuwa na mifano mingi sana na alikuwa na stori nyingi sana na khadithi nyingi sana na nyingi alizitumia katika kuielimisha jamii na kuijenga kama jinsi Mungu anavyotaka.


Kutokana na kupanuka kwa technolojia leo hii kumekuweko na vyanzo vingi sana vya kupokea na kutoa habari, lakini ni jambo la kusikitisha sana kuwa jamii ya leo haizingatii uadilifu katika swala zima la kupokea na kutoa habari, Mfano mzuri ni tukio la hivi karibuni ambapo watangazaji/ waandishi wa habari wa TBC walifariki, lakini wakati huo huo kulikuwa na taarifa za kufariki kwa Mtangazaji wa shirika hilo wa habari za biashatra aliyeitwa “Gloria Maiko” aidha kabla ya kuenea kwa taarifa hii kuhusu kufa kwake ilienea taarifa kuwa Gloria anaumwa sana tena ana ugonjwa wa Corona, Mimi napenda habari, mimi ni mwana habari, mimi nimesoma Introduction to jounalism, napenda kupata taarifa kwa sababu huwa pia natoa taarifa yaani nazitumia kuijenga jamii, sio hivyo tu unaposoma chuo cha Biblia kwaajili ya kazi ya uchungaji hausomei Biblia pekee unaandaliwa pia kuwa mwana habari kwa sababu kanisa linaweza kuwa na gazeti, Kanisa linaweza kuandika vitabu, kanisa linaweza kuwa na televisheni, kanisa linaweza kuwa na radio, kanisa linaweza kuwa na ukurasa wa faceboo, instagram, blog na nyenzo nyingine za utoaji wa taarifa kwa hiyo lazima watu wa Mungu wawe na angalau ufahamu mdogo tu kuhusu upokeaji na utoaji wa habari, wakati huu nilisoma chanzo kingine kuhusu Gloria kinasema hivi ngoja nikinukuu


 TBC1 tuliwaonya kukusanyika siku ya msiba wa Marini Hassan hamkusikia! Haya leo Joseph Kambangwa mfanyakazi wenu kafa kwa corona na maziko ni kesho saa 4 huko huko Mloganzila! **Gloria Maiko (anatangazaga habari za biashara) yuko hoi ana dalili zote za corona! RIP Kambangwa  


mwisho wa kunukuu, angalia huyu ni mtu mwenye akili timamu, ni mtu ambaye jamii inamtegemea, jamii inaamini labda katika hiki alichokisema lakini je habari hii ilikuwa na malengo gani kwa jamii, ilikusudia nini kwa Gloria? Na kwa familia yake, je ilikuwa inajenga au inabomoa? Kwa sababu baada ya kuenea kwa Taarifa hii Gloria Maiko alijitokeza kwenye mitandao ya kijamii akithibitisha kuwa yeye yuko hai na wala haumwi! Lakini mwandishi anajisikiaje? Baada ya Gloria mwenyewe kutokea je wale walioeneza katika mitandao ya kijamii na kutoa salamu za astarehe kwa amani wanajisikiaje katika mioyo yao baada ya mtu mliyemzushia kifo kujitokeza na kuonyesha yuko hai, nimetoa tu mfano huu lakini Jambo hili limewahi kuwatokea wengi, hapa nchini hata Mheshimiwa Augustin Lyatonga Mrema alizushiwa mara kadhaa mpaka alipojitokeza na kuionya jamii kuwa yeye ni mzima na kuwa kuanzia sasa atawafungulia mashtaka watu wanaoanzisha uzushi huu, Huko ulaya mambo ya aina hii yako sana lakini kwa mujibu wa tamaduni zao, Lakini sisi ni Watanzania na wana Afrika Mashariki je mambo haya ni sawasawa? Je wale waliosomea uandishi wa habari jambo hili ni sawa katika utoaji wa taarifa na upokeaji, Je wale wanaozushia wenzao hujitokeza kuomba radhi? Je wanachukuliwa hatua gani je ni aina gani ya jamii tunaijenga ya watu wanaosema ukweli au jamii ya waongo? Mungu ametupa hekima na akili na maendeleo makubwa ya nyenzo za utoaji wa taarifa lakini ni muhimu zikatumika kwaajili ya utukufu wa Mungu, kwa wakristo tunaambiwa katika maandiko kwamba lolote tulifanyalo kwa neno au kwa tendo tulifanye kwa utukufu wa Mungu ona


 Wakolosai 3:17 “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.” 


Swali kubwa ambalo kila mwana jamii anapaswa kujiuliza na kuhoji ni kuwa kama Yesu angekuwepo Duniani leo ni habari gani angeikubali na habari gani angeikataa na je angetumiaje mitandai ya kijamii, na sisi vilevile tujiulize je tunapopata habari ambazo hazina uhakika haziko sahihi, hazina utu, zina mitazamo hasi, zinaupendeleo, na kama ni za uongo wanaozitoa hawawajibishwi, habari hazina kiasi, na ziko kinyume na uadilifu je tungejisikiaje? Nafikiri wote tuna namna ambavyo tunatarajia jinsi habari au taarifa inavyopaswa kuwa! Mkurugenzi wa Maadili ya uandishi wa habari aitwaye Aidan White anasema ziko kanuni 400 ambazo wanahabari wanapaswa kuzizingatia lakini ziko kanuni 5 Muhimu zaidi ambazo kila mwandishi na mtoa habari anapaswa kuzifuata bila kushindwa 


1.       Ukweli na Uhakika (Accuracy) – “the quality or state of being correct or precise” Maana yake kila mtoa habari na mpokea habari na mtawanya habari au taarifa anapaswa kuhakikisha kuwa taarifa anayoitoa ina UKWELI na pia IMEHAKIKISHWA. Lakini pia kuzinagatia kuwa habari inaweza kuwa ya ukweli na imehakikishwa lakini swali je ni wakati muafaka kuitoa? Kwa sababu inaweza kuwa kweli na ya uhakika lakini wakati ukawa hauruhusu kuisema au mazingira yakawa hayaruhusu kusema !, tunapohubiri injili watu wa Mungu huwa hatuleti maneno ya kushawishi,  watu wanapaswa kuziamini habari njema na za kweli ili wapate kuamini na kuokolewa.


Isaya 53:1 ”Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?  wale yenye ufundi wa kibinadamu tunapopeleka habari njema tunapeleka habari ambazo ni za kweli na zinathibitishwa na Roho Mtakatifu, ile Nguvu ya ukweli pekee inauwezo wa kuwaweka watu huru na kuiponya jamii. Nyakati za Biblia watu waliwahi kueneza habari za uongo kwaajili ya faida zao na hivyo ikafikiriwa kuwa Yesu aliibiwa na hakufufuka ona. 


Mathayo 28:12-15 “Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi, wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala.Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi.Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo”. Waandishi wa habari ni kama manabii wanapaswa kutia habari za ukweli na uhakika ona Kumbukumbu la Torati 18:22 “Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope” 


Biblia liagiza kuwa kama nabii atatia taarifa na akadai taarifa hiyo imetoka kwa Mungu na kumbe sivyo yaani haikutimia yaani haina ukweli asiogopwe maana yake achukuliwe hatua, kwa hiyo kama watu wanaotoa habari na habari zao zikawa sio za uhakika torati inashauri wachukuliwe hatua katika agano la kale waliuawa, katika agano jipya  wanapaswa kuchukuliwa hatua, Yesu angelikuwepo leo hangeweza kukubalia habari ambayo haijathibitishwa haina ukweli na haijahakikishwa!  Habari zisizo za kweli zinaumiza mioyo ya watu na kubadili mtizamo wa mtu Habari za uongo zinasumbua na kuiumiza jamii Yakobo alilia na kuomboleza kwa miaka mingi sana baada ya kueletewa habari kuwa yusufu mwanae amekufa ona 


Mwanzo 37:31-35 “Wakaitwaa kanzu ya Yusufu, wakachinja mwana-mbuzi, na kuichovya kanzu katika damu. Wakaenda nayo ile kanzu ndefu, wakamletea baba yao, wakasema, Tumeona hii; basi, utambue kama kanzu hii ni ya mwanao, ama siyo. Akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa.Yakobo akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi. Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia” 



Yusufu hakuwa amekufa kweli lakini wana wa israel walimdanganya baba yao naye akaamini kuwa mwanaye Yusufu amekufa lakini kumbe habari hii haikuwa sahihi Yakobo aliishi kwa huzuni kwa miaka 13 akiwa na mtazamo kuwa mwanaye amekufa, Ni mpaka watoto wake tena walipomletea habari kuwa mwanao Yusufu yuko hai ndipo Roho ya Yakobo ilipofufuka kwa furaha



Mwanzo 45: 25-28 . “Wakatoka Misri, wakafika nchi ya Kanaani kwa Yakobo, baba yao. Wakampasha habari, wakisema, Yusufu angali hai; naye ndiye mtawala katika nchi yote ya Misri. Moyo wake ukazimia, kwa sababu hakuwasadiki. Wakamwambia maneno yote ya Yusufu, aliyowaambia; na alipoona magari aliyoyapeleka Yusufu, ili kumchukua, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka. Israeli akasema, Yatosha! Yusufu mwanangu angali hai; nitakwenda, nionane naye kabla sijafa.” 



Kumbe sasa tunaweza kufahamu kuwa habari inaweza kuhuisha au kuua kwa msingi huo ni vema wakristo wawe makini katika kutoa na kupeleka taarifa, Taarifa inauwezo wa kuua, Habari inaweza kuwa ya kweli lakini lazima pia inagaliwe namna unavyoipeleka kwa sababu ina nguvu inaweza kuua au kupoteza maisha ya mtu ona 


1Samuel 4:10-17 “Wafilisti wakapigana nao, Israeli wakapigwa, wakakimbia kila mtu hemani kwake; wakauawa watu wengi sana; maana katika Israeli walianguka watu thelathini elfu wenye kwenda vitani kwa miguu.Hilo sanduku la Mungu Likatwaliwa; na Hofni na Finehasi, wale wana wawili wa Eli, wakauawa. Basi, mtu mmoja wa Benyamini akapiga mbio kutoka mle jeshini akafika Shilo siku ile ile, hali nguo zake zimeraruliwa, na mavumbi kichwani mwake.  Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia, akingojea; maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule mtu alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia. Naye Eli aliposikia kelele za kile kilio, akasema, Maana yake nini kelele za kishindo hiki? Yule mtu akafanya haraka, akaenda, akamwambia Eli. Basi Eli umri wake umepata miaka tisini na minane; na macho yake yamepofuka hata asiweze kuona. Yule mtu akamwambia Eli, Mimi ndimi niliyetoka jeshini, nami leo hivi nimekimbia toka jeshini. Naye akasema, Yalikwendaje, mwanangu? Yeye aliyeleta habari akajibu, akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi sana wameuawa, hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na sanduku la Mungu limetwaliwa.” 


2.       Huru – Independence – yaani taarifa inapaswa kuwa ya haki isiyopendelea upande wowote, Kila mtoa habari na mpokea habari anapaswa kuwa na mtizamo wa haki, hapaswi kuwa mwenye kupendelea upande fulani, mfano kama ni kwa habari ya vyama vya siasa ni vema mtoa habari na mpokea habari wakawa hawana mtazamo wa kisiasa au mtazamo wa siasa zinazofungamana na upande fulani, taarifa itolewe kwa uwazi na kwa haki na ihaririwe kwa uwazi na kwa haki, Maandiko yanatufundisha wale wanaomuamini Yesu kuwa imani yetu katika Kristo isiwe kwaajili ya kupendelea watu 


Yakobo 2:1 “Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu unaona Yesu angelikuwepo leo hangeweza kupokea au kutoa habari inayomkandamiza mtu fulani haki ingesimama, Wako watu ambao wanaweza kutoa taarifa lakini kwaajili ya maslahi yao, kwa hiyo kanuni za kiandishi zinataka watu wasipeleka taarifa kwaajili ya faida yao ona pia 


Yuda 1:16 “Watu hawa ni wenye kunung'unika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.”  Kila mpokea habari na mtuma habari hapaswi kuwa na upendeleo anapaswa kutenda haki kama hakimu Mambo ya walawi 19:15 “Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.” Maandiko yanamtaka kila mmoja kutenda haki kuhukumu kwa haki agizo hili sio kwa mahakimu pekee bali na kwa wanaotoa taarifa na kupokea taarifa au kusambaza taarifa na 


Kumbukumbu la Torati 1:16-17 “Nikawaagiza wakati ule waamuzi wenu, nikawaambia, Sikizeni ninyi maneno kati ya ndugu zenu, mkaamue kwa haki kati ya mtu na nduguye, na mgeni aliye pamoja naye. Msitazame nafsi za watu katika hukumu; mwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu awaye yote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza.         


3.      Usiyo na Masalahi nayo – Impartiality kwa kiingereza neno hili maana yake “Impartiality is a principle of justice holding that decisions should be based on objective criteria, rather than on the basis of bias, prejudice, or preferring the benefit to one person over another for improper reasons“ yaani kanuni ya haki inayotaka maamuzi yafanyike kwa mujibu wa vigezo na sio kwa sababu mtu una masalahi fulani, au ukungu fulani unaotaka mtu mmoja anufaike dhidi ya mwingine kwa sababu zisizo sahihi, unapopokea au kutoa habari kwa makusudi maovu au kwa uependeleo kwa Mungu hufai kuwa mtu wa haki, Yesu angekuwepo leo kwa habari ya kupokea na kutoa habari angehukumu kwa haki Isaya 11:1-5Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda. Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana; na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia” Mtoa habari au mpokea habari anapaswa kuwa mwaminifu na kuwa mtu wa haki, wakati mwingine kwa sababu ya mitazamo fulani na hata kwaajili ya kupokea rushwa tumepokea au kutoa habari kwa maslahi ya upande fulani kwa sababu tunaletu jambo, Mungu hapendezwi na utaratibu huo na ndio maana hatua kali sana zinapaswa kuchukuliwa endapo itabainika mwandishi kuwa ana dalili za kupokea rushwa.


Nyakati za Kanisa la Kwanza stephano aliuawa kwa sababu ya maslahi ya watu, na sio kwa sababu alisema uongo Matendo 6:9-15 “Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;  lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye. Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu. Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza. Wakasimamisha mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati; maana tumemsikia akisema kwamba Yesu huyo Mnazareti atapaharibu mahali hapa, na kuzibadili desturi tulizopewa na Musa. Watu wote walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao, wakamwona uso wake kuwa kama uso wa malaika.” Stephano alihukumiwa na kuuawa kwa sababu ya taarifa za uongo kwa masalahi ya watu wa dini kwa sababu hawakutaia kuambiwa ukweli, kila mpokea taarifa na mtuma taarifa anapaswa kyuhakikisha kuwa anatoa taarifa yenye kujenga jamii na sio kuua au kwa sababu ana maslahi nayo.


4.       Taarifa yenye kujali utu –  Sence of Humanity Ni muhimu kufahamu kuwa biblia inasema usiue kuua kuko kwa namna nyingi sana unaweza kuua kwa kutumia maneno, unamuua mtu kisiasa, umamuharibia mtu au unamchafua mtu huku ni kuua mpokea habari au mtoa habari anapaswa kuhakikisha kuwa anajali utu, ni dhambi kuandika, kupokea au kutoa habari yenye kudhuru, yenye kuharibu ubinadamu wa mtu, au yenye kumvunjia mtu heshima hatupaswi kutoa habari wala kusambaza habari au habari picha yenye kuharibu maisha ya wengine au kudhalilisha, watu wasiojua kutumia mitandao ya kijamii wanapiga picha hata za watu waliopata ajali mbaya na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii, katika nchi nyingi zilizoendelea hata mwili wa Marehemu anapoagwa haupigwi picha, Picha ya marehemu inayoruhusiwa kuonekana ni ile ambayo wanafamilia wataiweka juu ya jeneza kwaajili ya kumbukumbu yake, nchi nyingi zawatu wasiostaraabika utaona mtu aliyepasuka kichwa kwa ajali, waliovunjika miguu, mtu mwenye ulemavu wa jabu na picha za kutisha sana zinarushwa kwenye mitandao ya kijamii, je umewahi kujiuliza kwanini mtu akipata ajali watu hutoa nguo zao na kuufunika mwili wa marehemu?  Ni kwaajili ya kujali utu, Mungu hawezi kukubali na kufurahia utu wa mtu udhalilishwe, kwa msingi huo kila mtoa habari na mpokea habari namsambazaji anapaswa mno sana kuzingatia utu, Yesu alikubali kifo cha aibu pale msalabani ili kutunza heshima ya mwanadamu, natarajia kuona jamii iliyostaarabika ambayo haitarusha picha ya marehemu yoyote akiwa na pamba puani, wala hata jeneza ikiwezekana na kama umefiwa weka picha ya aliyefariki ikiwa katika hali ya ubora na usiiwekee “X” muonyehse mtu enzi za ubora wake, sikitika kwa kumpoteza mtu huyo lakini usimdhalilishe nduguyo, aidha usisambaze wala usizikubali picha za watu walio katika hali mbaya za ajali, mwanadamu ameumbwa kwa sura na utukufu wa Mungu na lazima utu wa kila mtu uheshimiwe, hali kadhalika picha za ngono na zenye kuonyesha uchi ni mwiko kwa watu waadilifu, Mtu wa haki huwa hadhalilishi mtu mwingine. Mathayo 1:18-19Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.” Mtu wa haki huwa hafanyi mambo kwa kusudi la kumuaibisha mtu mwingine hata kama mtu huyo ni kweli amefanya jambo hilo Yesu angekuwepo leo hangekubali kupokea au kutoa taarifa zinazodhalilisha utu wa mwanadamu ambao ni uumbaji wake.


5.       Kuwajibika – accountability - In ethics and governance, accountability is answerability, Maana yake kila mtoa habari na mpokea habari na msambaza habari wanapaswa kujua na kukubali kuwa wanawajibika kwa habari wanazotoa au kusambaza, kwa msingi huo kama utatoa habari na ikasababisha madhara au hata isiposababisha madhara ufahamu kuwa unatakiwa kuwa na utayari wa kuijibia kuitolea maelezo na kuwa tayari kuomba radhi ikiwa umekosea,  au kukubali kukosoelewa na kupokea maoni ya jamii kuhusiana na ulichokitoa au kukisema na ikiwezekana kuwa tayari kushitakiwa mahakamani na hata kufungwa na au hata kuuawa na wale watakaochukizwa na habari ulizozitoa Mfano 2Samuel 1:2-15 “hata siku ya tatu ikawa, tazama! Akaja mtu kutoka kambi ya Sauli, nguo zake zimeraruliwa, tena ana mavumbi kichwani mwake; basi, ikawa alipomfikia Daudi, akaanguka chini, akamsujudia. Daudi akamwambia, Umetoka wapi? Akamwambia, Nimeokoka katika kambi ya Israeli. Daudi akamwambia, Yalikwendaje? Tafadhali uniambie. Akajibu, Watu wamekimbia vitani, tena watu wengi wameanguka wamekufa; hata Sauli naye na Yonathani, mwanawe, wamekufa.Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Umejuaje ya kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?  Yule kijana aliyempa habari akasema, Nalikuwapo kwa nasibu juu ya kilima cha Gilboa, na tazama, Sauli alikuwa ameegemea fumo lake; na tazama, magari na wapanda farasi wanamfuatia kwa kasi. Naye alipotazama nyuma, akaniona, akaniita. Nikajibu, Mimi hapa. Akaniambia, U nani wewe? Nikamjibu, Mimi ni Mwamaleki. Akaniambia, Tafadhali simama karibu nami, ukaniue, maana shida imenipata; kwa sababu roho yangu ingali hai ndani yangu. Basi, nikasimama karibu naye, nikamwua, kwa sababu nalijua hakika ya kuwa hawezi kupona baada ya kuanguka; kisha nikaitwaa ile taji iliyokuwa kichwani mwake, na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, nami nimevileta hapa kwa bwana wangu. Ndipo Daudi akashika nguo zake akazirarua na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja naye; wakaomboleza, wakalia, wakafunga hata jioni, kwa ajili ya Sauli, na kwa ajili ya Yonathani mwanawe, na kwa ajili ya watu wa Bwana na kwa ajili ya nyumba ya Israeli; kwa sababu wameanguka kwa upanga. Naye Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Watoka wapi wewe? Akajibu, Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki. Daudi akamwambia, Jinsi gani hukuogopa kuunyosha mkono wako umwangamize masihi wa BWANA? Ndipo Daudi akamwita mmoja wa vijana, akamwambia, Mwendee, ukamwangukie. Basi akampiga hata akafa.”, kila habari unayoitoa ni muhimu kufahamu kuwa itakugharimu, Kijana huyu alitoa habari iliyoweza kudhuru maisha yake, yeye alifikiri atapata sifa kwa Daud lakini kifo cha Sauli na Jonathan haikuwa habari njema kwa Daud na hivyo kijana huyu aliuawa, habari zinaweza kugharimu maisha yetu mbele za Mungu na wanadamu, Yesu alisema kila neno lisilo na maana atakalolinena mwanadamu atatoa hesabu yake Mathayo 12:36-37Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwaYesu atakapokuja atawahukumu wazushi wote hapa aliwaonya watu waliokuwa wakitoa habari zisizo sahihi kuhusu utendaji wa Yesu Kristo, Yesu anatoa pepo kwa Roho wa Mungu wapotoshaji wakesema anatumia nguvu za mkuu wa pepo Baalzebub, lazima ieleweke wazi kuwa watoa habari watawajibika sio mbele za wanadamu tu na mbele za Mungu! Wote tunakumbuka kuwa Sababu ya kifo cha Yohana Mbatizaji na kuwekwa kwake gerezani kulitokana na kupokea habari na kuzitumia habari hizo kumkemea Mfalme Herode ona Mathayo 14:3-10 “Maana Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodia, mke wa Filipo nduguye. Kwa sababu Yohana alimwambia, Si halali kwako kuwa naye. Naye alipotaka kumwua, aliwaogopa watu, maana walimwona Yohana kuwa nabii. Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode. Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lo lote atakaloliomba.  Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.  Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe; akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani.Watoa habari wengi sana wameuawa na kupotezwa na kufunguliwa mashitaka duniani kwa sababu ya utoaji habari, habari inaweza kuwa ya kweli na imethibitishwa lakini kama haikuzingatia kanuni hii ya kuwajibika basi inaweza pia kugharimu maisha yetu, mtoa habari mpokea habari na msambaza habari wanapaswa kuwa na uangalifu mkubwa sana namna wanavyopeleka habari


Hitimisho! 

Biola shaka kuna kitu umejifunza hapo sisi kama wakristo ndio chumvi ya ulimwengu napenda kila mmoja wetu aelimike na kukubalia kujifunza kuwa katika wakati huu wa utandawazi wakati ambapo kila mwanadamu anauwezo wa kutoa taarifa, kupokea taarifa na kusambaza taarifa ni Muhuhimu kwetu tukaacha kujisahau na kukumbuka kuwa ziko kanuni za neno la Mungu ambazo zinatuongoza jinsi na namna ya kuitumia mitandao hii ya kijamii, ninapohitimisha nataka kukukumbusha mambo kadhaa ya msingi yafuatayo:- 

a.       Tumia mitandao ya kijamii kuhudumu kwa neno la Mungu na kusambaza habri njema za Yesu

b.      Kumbuka kujitenga kwa muda na mitandao ya kijamii na kwenda kuomba, Yesu wakati mwingine aliacha makutano wengi sana na akajitenda kwenda kuomba.

c.       Kumbuka kuwakumbusha watu kutubu na kuishi maisha yanayompendeza Mungu, jitambue kuwa wewe ni mjenzi wa jamii na hivyo kabla ya kutoa habari tulizozipokea hakikisha kuwa zitakuwa zenye kujenga, kuonya kukemea kuelekeza na kukaribia kwa kusudi la mkujenga.

d.      Kumbuka kutia moyo mambo yaliyo mema kwa ku like na kuweka maoni yako na kukosoa vikali maovu na kuonyesha wazi jambo au kitu usichopendezwa nacho tumia neno la Mungu

e.      Tumia mitandao ya kijamii kudumisha uhusiano na kutafuta amani na watu wote na sio kuharibu, hakikisha nkuwa huondoki katika kusudi lako la matumizi ya mitandao, kama ni injili injili,

f.        Tumia mitandao ya kijamii kuonyesha semina, mikutano ya neno la Mungu na maswala muhimu ya kijamii onya karipia fundisha na jihadhari na matapeli, uwe makini na taarifa zako, maadui wanaweza kutumia taarifa zako kukudhuru wewe mwenyewe.

g.       Zingatia kanuni husika tulizojifunza na muombe Mungu ziwe kanuni muhimu katika maisha yako, asomaye na afahamu, ukiyajua hayo heri wewe ukiyatenda,

Na. Mchungaji Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima
0718990796

Mungu kwetu sisi ni Kimbilio na Nguvu!


Zaburi 46:1-3Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.  Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.”




Utangulizi:


Moja ya matukio muhimu sana ambayo Dunia inaweza kuwa imejifunza katika wakati huu wa Corona ni pamoja na kukubaliana na Neno la Mungu kuwa Mungu ndio asili kuu ya usalama wa mwanadamu; kukitokea vita, au serikali zetu zote zenye nguvu duniani zikashindwa, au kukitokea matukio mabaya ya kutisha ambayo hata wenye nguvu duniani wanaogopa, sisi tunapaswa kuelewa kuwa kiko chanzo kimoja kikubwa cha usalama ambacho ni Mungu!

Watu wenye uwezo wa kufikiri Duniani kama alivyo rais wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli walikaa na kutafakari kwa kina na kugundua kuwa, hakuna kinachoweza kutuponya iwe ni maendeleo makubwa duniani, iwe ni elimu, iwe ni sayansi na technolojia, vyote haviwezi kuwa na majibu ya usalama wa kweli leo isipokuwa Mungu, Tumejifunza leo kuwa lolote linaweza kutokea hata kwa sekunde moja tu na likaondoa usalama na vyote vikashindwa kutusaidia isipokuwa maombi na kumtegemea Mungu  vina uwezo mkubwa sana!

Rais wetu alifunga siku kadhaa kule Dodoma, maombi yake binafsi, lakini vilevile alitangaza maombi ya kitaifa kwa siku tatu, na akayaona majibu ya maombi na kisha akatoa muongozo na kisha akatangaza shukurani na Tanzania ikawa na utulivu wa hali ya juu! Kwa nini kwa sababu yeye kama rais ana serikali ana nguvu na ni mwana sayansi, lakini alitambua kuwa msaada wa kweli unatoka kwa Mungu! Hakuna ulinzi mwingine wowote isipokuwa kumgeukia Mungu tu  na kumtegemea ona


Zaburi 46:8-10 “Njoni myatazame matendo ya Bwana, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi. Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari. Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi. Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.


Mungu tu ndiye wa kutumainiwa Na ni Mungu tu ndiye Mlinzi wa kweli, Niliposikia habari wakati wa tatizo la Corona mwanzoni zilikuwa na utishio mkubwa sana hasa niliposikia Prince Charles yaani mtoto wa malikia naye ameugua corona unajua nini? Hawa ndio watu wanaolindwa zaidi Duniani kuliko mru yeyote Kikosi cha kumlinda malikia  kinaitwa SCOTLAND YARD SQUARD Kikosi hiki kinamlinda malikia na familia yake kwa masaa 24 na kina makomandoo waliofuzu mafunzo mbalimbali wapatao 185,  wao pia wana jina lingine maarufu kama RPS yaani ROYAL PROTECTION SQUAD ukiacha kuwa wanalindwa, watoto na wajukuu wa malikia wenywe ni askari waliofuzu na kushiriki vita za aina mbalimbali, Gharama za ulinzi wa wajukuu wa malkia Prince William na Prince Harry pekee unagharimu paundi laki tano 500.000.  Paundi moja kwa sasa ni sawa na shilingi za kitanzania 2900 hivi 500,000 X 2900 = 1,450,000,000 kwa mwaka wanalindwa na vifaa vya kisasa zaidi, Hapo hatujaeleza gharama za ulinzi wa malikia na mwanae mkubwa Prince Charles, Ikiwa mtu mkubwa kama huyu anaweza kupata virusi vya Corona  sembuse wewe mbwa mfu tu!  Je unadhani unakula vizuri kuliko yeye? Je unadhani unachekiwa afya vizuri kuliko yeye? Je unadhani una madaktari bingwa na hodari kuliko yeye?

Huwezi kuponyoka bila Mungu, Daudi alielewa kuwa kuna siri ya ziada katika Mungu, ni Mungu pekee ndiye anayeweza kutulinda na sio kinginecho


Zaburi 20:6-8 “Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi wake;Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu. Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu.Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.


Mungu anatusubiri tu tuuitie msaada wake tutambue kuwa yeye atatujibu na hatutategemea mbinu za kibinadamu pekee bali Mungu atatokeza msaada katika kila hatari inayotukabili katika siku zetu duniani, Tunapomkimbilia yeye hatupaswi kuogopa chochote tunapaswa kusimama kwa imani na kutambua ya kuwa Bwana atakaa imara katika kiti chake cha enzi na kudhibiti kila kinachoinuka mbele yetu!

Zaburi 46:1-3Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.  Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.”
Ulinzi wetu na usalama wetu unapatikana kwa imani kutoka kwa Mungu na sio mazingira yanayotuzunguka, yeye Bwana ni mwenye nguvu yeye ndio Ngome, imani yetu inapaswa kumsadiki yeye kuwa yuko mahali kote na ndiye anayetupa tumaini ni Mungu aliyejitambulisha kwetu kwa Israel yaani Mungu wa Yakobo

Zaburi 46:7, “Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.” Tana mstari wa 11 “Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. 

Mungu anataka tumtegemee yeye tumtumaini yeye na hapendi tutegemee vitu na mambo mengine, yeye hutupa amani hata wakati wa hofu kubwa inayoikumba dunia yeye humwaga Baraka kwa watu wote wanaomtegemea

Yeremia 17:5-7 “Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake”.

Mungu atupe imani thabiti sana wakati huu, tumtegemee yeye  na hata wakati wa hatari na majanga tumkumbuke yeye, tuendelee kuutegemea uwepo wake na ulinzi wake kwa sababu uwepo wake ni amani kubwa sana bila kujali nini kinatokea, Ayubu alipoteza kila kitu lakini alisimama imara kwa sababu alimtegemea Mungu, Wamtumainio Bwana ni kama Mlima sayuni hautatikisika wakaa milele, Zaburi 125:1 wengi wamepoteza uhai na kufa katika wakati huu wa Corona kwa sababu ya hofu na kutokuwa na imani kwa Mungu, hapa Tanzania watu wengi pia waliogopa lakini ashukuriwe Mungu kwamba tuna Rais anayemcha Mungu, na amekuwa sio rais tu bali ni mlezi wa kiroho wa taifa. Alisimama katika imani kuliko hata viongozi wa kiroho wengine, na aliwakosoa vikali hata wale waliofunga nyumba za ibada ! na kuwakumbusha kuwa imara kama Daniel Shadrack meshak na Abednego.
Mungu wetu habadiliki na kanuni zake ni zilezile, Mungu yuleyule aliyetenda kazi nyakati za agano la kale ndiye anayetenda kazi hata sasa, Biblia inasema hivi

Zaburi 105:5 “Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi inasema

Tukimtegemea Mungu tutakuwa salama katika ulimwengu usio salama, tuendelee kutegemea yeye na kusimama katika nafasi yetu, tunapoiangalia hali halisi leo tutaweza kukubaliana kabisa kuwa ulimwenguni sio mahali salama lakini imani yetu ikisimama katika neno la Mungu na ahadi zake na wote tukasimama imara katika imani na kuondoa hofu na kuwa na ujasriri  hakuna kitu kitakuja kututikisa duniani.

1Wakoritho 16:13 “Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari.” Biblia inasema

Isaya 26:3 “Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.”

Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima!
0718990796

Jumatano, 20 Mei 2020

Vita kali dhidi ya ndoa katika Mpango wa Mungu!


Malaki 2:14-16 “Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako. Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.”



Utangulizi:
Mojawapo ya changamoto kubwa zinazoukumba ulimwengu wa leo ni pamoja na changamoto kali katika ndoa, kila kunapokucha na katika kila mazungumzo, mafundisho na mijadala swala la ndoa na changamoto zake haliwezi kukosekana swala hili linasumbua wengi katika jamii masikini kwa matajiri, wenye cheo kwa wasio na cheo, wenye elimu na wasio na elimu wakristo na wasio wakristo na kadhalika; Kuna tatizo kubwa sana katika swala la ndoa, hata kwa wataalamu wa saikolojia, walimu na hata watumishi wa Mungu wenye kuzijua ndoa kwa kina na mapana na marefu bado linapokuja swala la ndoa watu wote huingia katika malalamiko ya changamoto hii! Walimu wengi wa Ndoa na mahusiano wamejaribu kutoa ufahamu wa aina mbalimbali katika ndoa ili ndoa ziweze kuwa na amani na zinaweza kufanya kazi kwa kiwango flani lakini huwa wanasahau kuzungumzia swala moja la muhimu kuhusu VITA VYA KIROHO DHIDI YA NDOA! Wengi watafundisha kuhusu ndoa, majukumu ya mwanamke na mwanaume, wajibu wa mke na mume, maswala ya mahaba na staili na mitindo, vyakula muhimu vya wana ndoa sijui nini sijui nini lakini wanasahau kuzungumzia kwamba kuna vita vya kiroho dhidi ya ndoa hili ni muhimu kujulikana kwa kila mwana ndoa vinginevyo hakuna kitakachoweza kufabnya kazi, masomo yote ni ya muhimu lakini kama changamoto bado ziko hapa linabaki swala la mapambano ya kiroho kwa ajili ya ndoa yako! Ndoa ina vita zake hii ni muhimu kufahamu.

2Wakoritho 2:11.”Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.” Ni muhimu kufahamu kuwa ziko mbinu za utendaji wa ibilisi zinazopambana na ndoa sahihi ili isiweze kufanya kazi, na shetani anaweza kukupa amani ambayo unaweza kudhani kuwa ni amani ya kweli kwa kukubali kuweko kwenye ndoa bandia baada ya kushindwa vita katika ndoa Halisi, watu wengi sana wanadhani kuwa wana amani sasa kwa kuweko kwenye ndoa ambazo sio mpango wa Mungu na huko wanaweza kusema kuwa ndoa ile sio mpango wa Mungu, labda mwanzoni nilikosea au pale nimeingia cha kike swali kubwa la kujiuliza kwanini ile ndoa yako ya awali ilikuwa na vita kiasi kile ? na sasa je unadhani una amani ya kweli kwa kuwa sasa uko katika ndao ya pili? Je hujawahi kujiuliza kuwa amani hiyo sio ya Kristo? Imetokana na kuwa shetani hawezi kukupiga vita tena kwa sababu umeshashindwa vita na umekuwa mateka wake ukijifariji katika ndoa isiyokuwa ya halali hata kama imefungwa na mchungaji flani! Angalia!

Shetani anaitwa mungu wa dunia hii  na moja ya kazi yake ni kupofusha fikra uwezo wa kufikiri au kumgundua na kupata upenyo, anapofusha fikra za watu wa ulimwengu huu wasiijue kweli ambayo itawaweka huru 2Wakoritho 4:4 “ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.” Yeye ni muongo ni mwenye hila na kwa kutumia hila zake anauwezo mkubwa sana wa kuudanganya ulimwengu ona pia Ufunuo 12:9 “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Unaona maandiko yanamuita shetani joka Mkubwa, joka la zamani anaujuzi wa kupanga mambo, ana ujuzi wa kushambulia ana ujuzi wa kutenda kwa hila ili audanganye ulimwengu ana vita dhidi ya kanisa ana vita dhidi ya taasisi inayoitwa ndoa, kabla ya kupigana na kanisa zamani sana alianza kupigana na ndoa, ndo ndio taasisi yake ya kwanza kupambana nayo, fikiria leo alivyofanikiwa kusambaratisha maneno ya Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai leo ynaonekana kama maneno yasiyotekelezeka na yaliyojaa uongo je ni ili shetani aonekane kuwa mkweli? Tujikumbushe maandiko kuhusu kile alisema Yesu hapa Mathayo 19:3-10 “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.  Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.” Kutokana na uongo wa ibilisi kifungu hiki kimewashinda wengi kukitii na kukifanyia kazi katika ulimwengu wa leo, kumbuka hata Dunia na mataifa makubwa na makanisa makubwa yanapofikia ngazi ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja leo hii ni muhimu kwetu kukumbuka kuwa hii ni mojawapo ya dalili ya kiwango cha juu cha shetani kupambana na kitu kinaitwa ndoa, wengi wamekivunjilia mbali kifungu hicho cha maandiko wakijihalalishia ndoa zisizo sahihi chini ya amani ya muda mfupi ya shetani, Sheatani anachukizwa na ndoa shetani anachukizwa zaidi na ndoa ya Kikristo, shetani anapiga vita ndoa sahihi, kwa sababu anajua kuwa kwa kufanya hivyo anaizuia injili isiwafikie walengwa na watu hao wakakokolewa kwa sababu kwenye ndoa kuna siri kubwa sana inayofananana na siri ya kuwepo kwa kanisa Waefeso  5:32-33 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.Ni kwaajili ya jambo hili ni muhimu kwetu kuangalia kwa undani kuhusu vita vya kiroho katika ndoa ili kujiepusha na kuangalia upande mmoja wa shilingi ikiwemo swala la mahusiano, mawasiliano, taili, uongozi, wajibu na majukumu,  malezi  na kadhalika na tusisahau kuwa pamoja na umuhimu wa haya yote ndoa inapigwa vita kali sana !

Ndoa katika mpango wa Mungu!

Mungu alimuumba mwanadamu katika sura na mfano wake Mwanzo 1;27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” Mwanamke na mwanaume wanapofunga ndoa wanafunua mpango maalumu wa Mungu neno kuumbwa kwa Mfano wa Mungu kwa kiyunani linatumika neno “imago dei”  ambalo kwa kiingereza ni intellectual ability, Moroal decision and the ability to make wilful choice, purity and ruling, uwezo wa kiakili, maamuzi ya kimaadili, uwezo wa kuchagua usafi na utawala kwa hiyo mwanadamu aliumbwa awe mwakilishi wa Mungu na Mungu alimuamuru mwanamke na mwanaume kuitawala Dunia kueneza utukufu wake kumfanya yeye asifiwe huu ndio ulikuwa msingi wa mwanzo kabisa wa Ndoa Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Kuzaa na kuongezeka hapa ni kuendeleza uzao wa Mungu duniani kwa jamii ya watu wanaomtii na kumuheshimu Mungu na kutangaza utukufu wake Kwa kupitia ndao hii ya kwanza tunauona wazi kabisa Mpango wa Mungu ni kuzalisha watu watakaomtukuza yeye Duniani, watu watakaodhihirisha uhodari wa kutembea na uwepo wa Mungu na Biblia katika fundisho hili inaonyesha wazi kupitia uumbaji huu Mungu alikusudia kwamba

·         Ndoa iwe ya mke mmoja Mume mmoja
·         Ushirikiano wa tendo la Ndoa uwe ni wa jinsia ya kiume na ya kike
·         Kiongozi katika ndoa aliwajibika kuwa Mwanaume kutokana na kuumbwa kwanza
·         Ndoa ilikusudiwa iwe ya kudumu na yenye umoja usioweza kutenganishwa maneno ya Adamu huyu ni Mfupa katika mfupa wangu na nyama katika nyama yangu yanatumika kuonyesha umoja usioweza kutenganishwa yaani Adamu na Eva walikuwa kitu kimoja na umoja wao ulikuwa wa kudumu na msikamano wao ulikuwa ukitenganishwa ni kifo ndio kingetokea kwao wote Neno Mfupa wangu na nyama yangu katika agano la kale lilitumika kumaanisha Undugu ambao kwa namna yoyote ile hauwezi kukanushika ona Mwanzo 29:14 “Labani akamwambia, Ndiwe kweli mfupa wangu na nyama yangu. Naye akakaa kwake muda wa mwezi mmoja.” Ona pia Waamuzi 9:2 “Haya, neneni tafadhali masikioni mwa waume wote wa Shekemu, mkaulize, Je! Ni lipi lililo jema kwenu, kwamba hao wana wa Yerubaali wote, ambao ni watu sabini, watawale juu yenu, au kwamba mtu mmoja atawale juu yenu? Tena kumbukeni ya kwamba mimi ni mfupa na nyama yenu.” Linganisha pia 2Samuel 5:1 “Ndipo kabila zote za Israeli wakamwendea Daudi huko Hebroni, wakasema naye, wakinena, Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako.” Tungalie pia 2Samuel 19:12 “Ninyi ni ndugu zangu, ninyi ni mfupa wangu na nyama yangu; mbona basi ninyi mmekuwa wa mwisho wa kumrudisha tena mfalme. 1Nyakati 11:1 “Ndipo Israeli wote wakamkusanyikia Daudi huko Hebroni, wakisema, Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako.” Unaona neno Mfupa wangu na Nyama yangu lilitumika kumaanisha umoja usioweza kutenganishwa kamwe, muunguno usioweza kukanushwa sasa ukaribau anaokuwa nao mke na Mume na muungano wao wa kimapenzi na uwezo wao wa kushirikiana tendo la ndoa na Baraka za Mungu huwafanya wao wawe karibu zaidi kuliko ndugu wa kawaida kwa lugha nyingine unapoacha mumeo aende au mkeo aende zake yaani mnapoachana unaacha uchi wako uende zake, mwili wako uende zake, mifupa yako iende zake, na mwili wako uende zake, na kuanza kutumiwa na watu wengine, Mungu alikusudia Ndoa ibebe huduma ya kuongezeka duniani na kuitawala dunia chini ya mamlaka ya uungu kwa kumtii, kwa kulitambua kusudi hili kila ndoa iliyo sahihi iliyo katika mapenzi na mpango wa Mungu itaanza kupigwa vita kali na ibilisi kwa sababu Shetani anajua wanando wasichokijua kwa hiyo anawataka wasumbuke wapigane wagombane wafarakane waachane watendane mambo ya hiyana wasemane vibaya wanyimane unyumba wasimtii Mungu atawasumbua mpaka wakimbie na atawapa nafuu wanapokuwa katika ndoa ya pili isiyokuwa mapenzi ya Mungu

Shetani atafanya hivi kwa sababu yupo na yuko tayari kupingana na Muumba wake, atawadanganya wanadamu atawavuruga ili wamuasi Mungu wasitii neno lake akitumia hila na ujanja mwingi sana hatimaye aweze kuharibu na atakupa amani bandia kwa sababu anajua umeshaasi na kifo kinakuhusu yaani utakwenda katika ziwa la moto wa milele kwa sababu sasa unazini milele wewe ni mali yake hawezi kukuvuruga tena amefanikiwa kukupata na ndio maana utaona wale walioachana na wake zao na waume zao wa awali unaweza kukuta sasa wanaamani ya kutosha huko UZINZINI kwa mtu asiye Mfupa wake wala nyama yake kwa sababu amekuwa mtumwa wa dhambi na chombo cha ibilisi hata kama mambo yanakwenda “smoothly” yaani shwari usifikiri wewe ni mjanja kwamba umeshinda vita hapana umeshindwa vita wewe ni mali ya ibilisi hii ndio mbinu yake tangu awali ona Mwanzo 3:1 anasifiwa kwa uhodari wake ujanja na udanganyifu au werevu Mwanzo 3;1 “Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?neno mwerevu hapo katika kiingereza linatumika neno “crafty” ambalo maana yake ni Clever at achieving one’s aims by indirect or deceitful methods  Yaani mwerevu ni mwenye ujanja wa kufikia malengo yake kwa kutumia njia isiyo ya wazi moja kwa moja au kwa kutumia njia za udanganyifu kwa kutumia hila hizo sasa Shetani alifanikiwa kumdanganya Eva na kisha kummalizia Adam na kuwafanya waasi na kwa njia hii kufanikiwa kuleta mauti duniani na uharibifu mkubwa na kupitia wao wanadamu wote wamekuwa wavunjifu wa sheria ya Mungu namaanisha neno lake kama ilivyokuwa kwa Adamu Hosea 6;7 “Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu; huko wamenitenda mambo ya hiana.” Ona pia Warumi 5:12-21 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja. Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi. Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki. Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.  Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.  Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi; ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.” Unaona sasa hasara kubwa sana imaupata ulimwengu mzima kutokana na kazi ya ibilisi kwa Adamu na Eva na nikwambie kuwa hasara kubwa inaupata ulimwengu kupitia wewe na mimi kwa kuasi kwetu na kuvunja amri na maagano na Mungu wetu, ndoa sasa haiwezi kuwa kamilifu duniani na ikiwa ni ya watu wa Mungu inakuwa na vita kubwa sana na wapiganaji wakiwa hawaelewi zitavunjika sana na watapewa ndoa ambazo zina amani ya muda mfupi lakini zinawapeleka Motoni kimya kimya vita ilitangazwa kati ya shetani na uzao wa mwanamke  kwa mtazamo mpana uzao wa mwanamke ni Yesu Kristo lakini kwa mtazamo rahisi sisi wanadamu wote ni uza wa mwanamke kwa hiyo mafarakano katika ndoa ni vita ileile alioianza shtani katika bustani ya Edeni, kwa hiyo kama vile mtu akiokoka tunamfundisha kuwa imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi yaani vita nyingi ni muhimu vile vile wana ndoa wakaelewa kuwa pamoja na sarakasi zote mtakazofanikiwa au mtakazojifunza iwe uwazi katika maswala ya fedha, mahusiano, ndugu, staili, kujituma, vyakula, majukumu ya mke na mume, malezi na kuchekeana na kadhalika lazima ujue shetani na mapepo yako kazini kuhakikisha kuwa yanapambana na ndoa yako mpaka mwisho wa dahari kwa hiyo 1Petro 5:8 “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.“ shetani anazunguka zunguka popote palipo na kusudi la Mungu ili awaharibu wana ndoa.

Ndoa katika mpango wa Ibilisi

Unapoyachunguza maandiko utaweza kuona sasa Shetani kama mpinzani wa Mpango wa Mungu naye ana mipango yake inayolenga kuleta uharibifu katika ndoa, Ni muhimu kukumbuka sasa wakati dhambi inaingia ulimwenguni kupitia kazi za shetani taasisi ya kwanza kushambuliwa na vita ya ibilisi ilikuwa ni ndoa kwa haraka sana tunaona sasa katika kitabu cha Mwanzo wanadamu wakiondoka katika mapenzi ya Mungu kuhusu ndoa na kujiingiza katika mapenzi ya ibilisi na matakwa yao au tamaa zao.  Hapa ziko aina nyingi za uharibifu wa ndoa ambao maandiko yanaonyesha kuwa shetani aliufanya kwa ulimwengu hatua kwa hatua na kuwapeleka wanadamu kwenye uharibifu mkubwa sana wa ndoa iliyokusudiwa na Mungu, Dalili zifuatazo ni Ishara ya kazi za shetani kutokomeza mapenzi ya Mungu katika ndoa.

1.      Ndoa ya mke zaidi ya mmoja.

Moja ya dalili kubwa kabisa ya matokeo ya dhambi ilikuwa ni ndoa ya wake wengi ona katika Mwanzo 4:19 “Lameki akajitwalia wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila.Wakati huu kutoka katika ndoa ya mke mmoja ambaye ni mfupa katika mfupa na nyama katika nyama kuelekea kwenye wanadamu kutekeleza tamaa zao kuoa wake wengi ilikuwa ni sihara ya uharibifu wa uadilifu katika ndoa, ndoa hizi zimeonyesha na kuashiria kutokuwepo kwa haki, kuwepo kwa mafarakano, visa na mikasa katika biblia tumeona kuwa hata pale ndugu wa familia moja walipoolewa na mtu mmoja kama Leah na Raheli bado mapungufu makubwa yaliashiria kuwa ndoa hizi hazikuwa mpango wa Mungu, sio hivyo tu wanadamu waliondoka katika ndoa ya mke mmoja kuelekea wake wengi, shetani aliendelea kuwatoa wanadamu kutoka hatua ya kuoa wanawake kwa kujitakia bila kufuata utaratibu.

2.      Ndoa za watu wasiofuata utaratibu.

Ukiyachunguza maandiko hapo katika Mwanzo 4:19 kuna neno KUJITWALIA neno hili laonyesha wazi kuwa Lameki alikuwa mtu wa kwanza wa uzao ule wa Kaini ambao ulijitenga na uso wa Mungu na kwa matakwa yake mwenyewe alijitwalia wake zaidi ya mmoja tofauti na mpango wa kwanza wa Mungu ambao ulikuwa mke mmoja na mume mmoja Mwanzo 2:24 “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.Tabia hii ya lameki baadaye ilienea hata miongoni mwa uzao wa watu waliokuwa wanamcha Mungu na hivyo watu walianza kujiolea bila kufuata utaratibu ona Mwanzo 6:1-2 “Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.” Unaweza kuna maana yake sasa watu waliingia katika kujitwalia wake wowote waliowachagua neno kujitwalia maana yake ni bila kufuata utaratibu, uchafu wa tendo la ndoa na kutokuheshimiwa kwake na watu kujifanyia vyovyote watakavyo bila kufuata utaratibu ulikuwa ni mpango wa ibilisi kuvuruga mpango wa Mungu kadiri dunia inavyoharibika leo, hizi vurugu za shetani zitaonekana ni kitu cha kawaida katika jamii, watu hawatafuata utaratibu, kwa nini Mungu anataka utaratibu ufuatwe? Tusipofuata mpango wake itafikia hatua watu watazaa watoto wakiwa hawajui baba wa watoto hao ni nani, wanaume watakanusha watoto kwa nsababu hawana uhakika kuwa mimba hiyo ni yake au ya mwanaume mwingine ni jambo la kusikitisha Mungu alihukumu kizazi hiki cha watu wasiofuata utaratibu

3.      Ndoa ya watu wa jinsia moja.

Baada ya ndoa za watu wasiofuata utaratibu biblia inatuonyesha uharibifu mwingine huu ni wa ndoa za jinsia moja  yaani wanaume kwa wanaume na au wanawake kwa wanawake  mifano ikiwa ni miji ya Sodmoma na Gomora  ona Mwanzo 19: 1-25 “Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi. Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha. Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala. Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote. Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua. Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake. Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi. Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu. Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje mlango. Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango. Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango. Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa; maana tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za BWANA; naye BWANA ametupeleka tupaharibu. Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze. Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu. Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi BWANA alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji. Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea. Lutu akawaambia, Sivyo, bwana wangu! Tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha rehema zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia mlimani nisipatwe na yale mabaya, nikafa. Basi mji huu u karibu, niukimbilie, nao ni mdogo, nijiponye sasa huko, sio mdogo huu? Na nafsi yangu itaishi. Akamwambia, Tazama, nimekukubali hata kwa neno hili, kwamba sitauangamiza mji huo uliounena. Hima, ujiponye huko, maana siwezi kufanya neno lo lote, hata uingiapo humo. Kwa hiyo jina la mji ule likaitwa Soari. Jua lilikuwa limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari. Ndipo BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa BWANA. Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile.Ndoa zinapofikia kuwa ni za jinsia moja hapo ndio huwa ni kilele cha juu kabisa cha uharibifu wa ndoa katika mipango ya shetani, Shetani alifanikiwa kuharibu Ndoa kwa kiwango hiki Mungu alitaka Ibrahimu alishuhudie tukio hili ili iwe fundisho kwa wana wa Israel na wale wote wanaomuamini Mungu wa Ibrahimu kuwa wasifanye mambo kwa mfano wa watu wa Sodoma.

4.      Ndoa ya Ndugu wa damu au ndugu wa karibu sana.

Muda mfupi sana mara baada ya tukio hili la kuangamizwa kwa miji nya Sodoma na Gomora  Biblia inatupa kisa kingine tena namna na jinsi shetani alivyoendelea na jitihada zake za kuhakikisha kuwa kila aina ya uchafu na mambo yanayovuruga na kuleta uharibifu  katika ndoa yanastawi sasa hata tunaona Lutu na binti zake wakilala na kuzaa hii ni aina nyingine ya mipango ya ibilisi katika kuchafua na kuharibu ndoa angalia sasa Mwanzo 19:30-38 “Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili. Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote. Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao. Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena usiku huu, ukaingie ukalale naye. Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo. Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo.” Hili lilikuwa ni tukio la kushangaza sana namna na jinsi shetani alivyoweza kuharibu Familia hii ambao walikuwa wameokolewa kutoka Sodoma sasa wanaingia katika uchafu huu, dhambi ya aina kama hii inaonekana kufanyika pia katika kanisa la Koritho wakati wa kanisa la Kwanza 1Wakoritho 5:1-2 “Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo.Unaweza kuona kuwa tabia za uchafu wa aina hii unaweza kufanywa hata na watu walioko kanisani kama hawatasimama na kushindana na ibilisi katika kupingana na uharibifu anaokusudia kuufanya katika ndoa ni kwaajili ya haya Musa alitangaza laana kubwa sana kwa watu wanaoweza au kuthubutu kutaka kufanya mapenzi ngono au tendo la ndoa na jamii ya watu waliokaribu nao na ambao ni ndugu zao ona Mambo ya walawi 18:1-24 “BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena wewe na wana wa Israeli, uwaambie, Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mliyokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msiende katika amri zao hao. Mtazifanya hukumu zangu, nanyi mtazishika amri zangu, ili mwenende katika hizo; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi BWANA. Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi BWANA. Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake.  Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako. Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue. Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe. Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake. Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu. Usifunue utupu wa umbu la mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya karibu.Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi lako. Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo. Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo.  Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu. Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu hai. Nawe usimkaribie mwanamke kufunua utupu wake wakati wa kutengwa kwa ajili ya unajisi wake. Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye. Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapitisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA. Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko. Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote;Mungu aliweka sheria hizi zote kwa kusudi la kulinda uadilifu na kuweka utaratibu miongoni mwa watu wake kwa sababu mataifa na dini zile za kanaani zilifanya haya hawakuishi kwa utaratibu wa kimungu bali wa kishetani na Mungu akliwataka watu wake kutunza uadilifu, Hata hivyo sheatani aliendelea na vita byake dhidi ya ndoa hata kufikia utaratibu wa ndoa kuwa utaratibu wa mikataba yaani ndoa zenye talaka, Mpango wa talaka ni ishara nyingine ya kuharibiwa kiuadilifu kwa ndoa je inawezekanaje mtu ambaye ni mfupa wako na nyama yako sasa ikafikia ngazi ya kuachana kwa karatasi na wino?

5.      Ndoa ya mikataba kupeana talaka.

Talaka haina tofauti na ndoa za mikataba tu, watu wanaingia makubaliano wanaishi kwa muda flani halafu wanaachana huu haukuwa mpango wa Mungu, Kisheria Musa aliruhusu hati ya talaka katika torati, hii ni kwaajili ya maswala ya kimahakama au kimaamuzi kwa vile Musa pia alikuwa mwamuzi wa Israel Judge, Lakini katika uadilifu na mpango wa Mungu, Mfupa wako na Nyama yako haviwezi kutenganishwa kamwe, watu ambao wamekuwa mwili mmoja wanatenganishwaje ? lakini kutokana na uharibifu wa kimaadili hati ya talaka ilikubalika ona maandiko Kumbukumbu 24:1-4 “Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake.  Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine. Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe; yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za Bwana; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi. Yesu Kristo nabii mkuu au mkuu wa manabii au mwenye kutuma manabii ambaye manabii wote walizungumza habari zake yeye ndio kiongozi mkuu wa wokobvu wetu alipokuja Duniani katika mafundisho yake hakukubaliana na swala zima la hati ya talaka, kwani hili halikuwa msingi wa mwanzo wa mpango wa Mungu kupeana talaka ni kutoka nje ya mapenzi ya Mungu Mungu alonyesha wazi kuchukizwa na tabia ya kuachana na hata kunyimana unyumba ambako kuliitwa kutendana mambo ya hiyana ona Malaki 2:14-16 “Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako. Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.” Ni wazi kuwa Mungu anachukia kuachana Yesu alionyesha wazi kuwa watu waadilifu na wale wanaomfuata yeye wanapaswa kukubali kuwa kutoa talaka ni ngazi ya juu kabisa ya ugumu wa moyo uliokosa msamaha mapenzi ya Mungu kamili kwetu ni kuwa ndoa zidumu mpaka kifo kiitenganishe ona Mathayo 19:3-10 “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?  Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?  Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.  Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.” Kutokana na kifungu hiki ndio maana utasikia usemi kama ule Ndoa ni pingu za maisha, au utasikiwa wamefunga pingu za maisha usemi huu una maana gani? Wanafunzi wa Yesu (Mitume) walimuelewa sana  Yesu alipozungumzia  Maswala ya ndoa hasa pale alipokuwa akijibu maswali ya mafarisayo kuhusu ndoa, Mafarisayo walimuuuliza Yesu kwa kumjaribu kama Ni halali mtu kumuacha mkewe kwa kila Sababu,Majibu ya Yesu yalionyesha kuwa hakuna sababu  ya mtu kumuacha mkewe hata kama mmojawapo wa wanandoa amefanya zinaa! Wanafunzi kwa kulielewa hili walisema mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivi haifai kuoa.

Najua utakuwa umeshitushwa sana na Mtazamo huu hapo juu lakini nataka nikupeleke katika msingi wa mafundisho ya Kristo kuhusu ndoa na Kuachana, Ni muhimu ikaeleweka wazi kuwa wakati mafarisayo wakimuuliza Yesu maneno hayo walikuwa tayari wameathiriwa na shule kuu Mbili za marabi maarufu waliofundisha theolojia za kiyahudi Rabi wa kwanza aliitwa Rabi Shimney huyu alikuwa na msimamo mkali alipinga Kuachana akisimamia vilivyo mafundisho ya Musa na rabi wa pili aliitwa Rabi Hilel huyu alikuwa na mrengo wa kushoto na msimamo wa wastani yeye alikazia kuwa waweza kumuacha mkeo kwa sababu zozote na ukaoa mwingine akisimamia Sheria ya Musa, Kimsingi Mafarisayo wengi walipendezwa na msimamo wa Hilel katika maswala ya ndoa na kwakuwa walimuona Yesu kuwa Kama rabi mwenye msimamo wa wastani  walitaka kujua kuwa angelielemea katika Eneo gani kati ya haya Mawili;  katika namna ya kushangaza sana Yesu alionekana kuwa na Msimamo mkali katika Eneo la ndoa kuliko Hilel, Shimney na Hata Musa Mwenyewe Yeye alionyesha kuwa hakuna sababu yoyote ambayo inakubalika katika Mungu kuwa Inaruhusu Mtu kumuacha mkewe au kuachana na ya kuwa hata Musa aliruhusu talaka kama matokeo ya ugumu wa mioyo waliyokuwa nayo wayahudi kwa vyovyote ugumu huu ni ile hali ya kutokusamehe.

Watu wengi sana leo wamewaacha wake zao au hata waume zao kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao ugumu wa kutokusamehe wamekuwa wakiwaona kuwa wenye dhambi sana ni wangapi ambao wamefanyiana mambo ya hiyana lakini leo wako pamoja inashangaza leo hii kuona hata wapendwa (watu waliookoka) wakiingia katika  hali hizi za kuvunja ndoa na kushindwa na watu wasio mjua Mungu na huku wakiungwa mkono na viongozi wao wa dini kwa nini watu waachane kama Yesu yupo? Yeye alikuwa na msimamo thabiti wa kutokupenda watu waachane je leo tunamfuata Yesu au tunaona kuwa alipitwa na wakati maana wakati wake hakukuwa na Magonjwa na changamoto kama hizi zilizoko leo? Kuachana ni kumvunjia Mungu Heshima na kudhalilisha mafundisho mazuri ya Kristo na kuvunja kanuni zake za uumbaji na utaratibu wake tangu mwanzo acha mawazo ya kuachana katika jina la Yesu, tafuta kutengeneza nyumba yako na sio kuibomoa Yesu alionyesha wazi kuwa hakuna sababu za kuachana. Hii ina maana gani?  Hakuna sababu ya Kuachana. Kifungu kile tulichosoma katika Mathayo 19;3-10. Kimsingi katika mistari hii Yesu alifafanua kuwa hakuna sababu ya Kuachana isipokuwa kifo tu  ni muhimu kufahamu msingi wa Mungu kuwa Yeye anachukizwa na kuachana tangu zamani Kama tulivyoona pia katika kitabu cha nabii malaki hapo juu Malaki 2;16. Hata hivyo kuna utata wa kitheolojia kuhusu Mathayo 19;3-10 kwamba Yesu alisema Mtu anaweza kumuacha mkewe kwa sababu ya Uasherati ni muhimu kuchambua Maana halisi ya Mistari hii ili kupata maana halisi ya kile anachokisema Bwana Yesu, Kwanza ni muhimu kwetu kuchanganua Maneno haya Mawili Uzinzi na Uasherati huku ukitilia maanani kuwa Yesu alitumia neno uasherati.

Tofauti ya Uzinzi na Uasherati;

Katika tafasiri za kawaida za Kiswahili uasherati ni tendo la kujamiiana linalofanyika nje ya watu waliooana au tendo la ngono linalofanywa na watu au mtu ambaye hajaoa au kuolewa mtu wa jinsi hii anapofanya hayo huitwa Muasherati, Uzinzi ni tendo la ndoa linalofanywa na wanandoa nje ya ndoa.
Kwa msingi huu Yesu alipotumia neno Uasherati alimaanisha watu ambao hawajaoana bado isipokuwa wana uhusiano wa kutaka kuoana yaani ni wachumba, hii ni kwa sababu katika jamii ya Kiyahudi hawakuwa na neno mchumba kama tulilonalo sisi, Hivyo Binti bikira ambaye anatarajiwa kuolewa au amelipiwa mahari huyu aliitwa mke na huyu angeweza kuachwa kama angebainika kuwa amefanya uasherati kabla ya ndoa basi uhusiano huu ungevunjika, Mfano mzuri ni ule wa Yusuphu na Mariam walikuwa ni Mtu na mchumba wake ambaye alikuwa amemposa, Hivyo kwa tendo la Yusuphu kumuona Mariam akiwa na Mimba alikusudia kumuacha kwa siri Hata hivyo katika Kumuasa asimuache Malaika na Biblia  inatumia Neno  Usimuache Mkeo” Unaona! Mathayo 1;18-25 “Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.  Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.  Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe; asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.kwa Msingi huu basi Yesu alimaanisha kuwa anayeweza kuachika ni Mchumba na si mke, Yesu anasemaje kwa Wanandoa? Kwa wanandoa endapo wataachana kwa sababu ya zinaa wote aliyeacha na aliyeachwa watakaa bila kuoa au kuolewa tena, na endapo watafanya hivyo yaani mume ataoa na mke ataolewa tena “Remarried” watakuwa wanazini milele yaani wanaishi katika maisha ya dhambi. Yesu anatoa ushauri gani? Wanaweza kumaliza tofauti zao na kupatana tena na kurudiana angalia 1Wakoritho 7; 10 “Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;” kwa nini kwa sababu watu wanapooana wanakuwa mwili mmoja na kinachoweza kuwatenganisha ni kifo tu kama vile ambavyo ndugu wanakuwa ndugu siku zote za maisha yao duniani mpaka ndugu huyo anapofariki Dunia ona   Warumi 7;2-3 “ Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume. Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.” Unaona kwa hivyo ni kifo tu ndicho kinachoruhusiwa kutoa upenyo wa mtu kuoa au kuolewa tena!  Na hakuna kosa lolote linalohalalisha ndoa kuvunjwa na kama ikitokea wanandoa wakaachana wanapaswa kukaa hivyo hivyo maisha yao yote au kurudiana kinyuime cha hapo wanafanya uzinzi  Ni kwa sababu hii wanafunzi wa Yesu walisema Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivi haifai kuoa, Kimsingi Yesu alionyesha wazi kuwa wale walioachana wakati wa Musa waliachana au Musa aliruhusu wafanye hivyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yaani hali ya kutokutaka kusameheana, Hakuna dhambi isiyosameheka hivyo kimsingi kama tunashindwa kusamehe ni Ngumu nasi kupokea msamaha kutoka kwa Mungu. Aidha katika agano la kale wazinzi walipigwa kwa mawe hata kufa na jambo hili lilimfanya mtu mwenye haki awe mume au mke aliyebaki kuoa au kuolewa tena hivyo kanuni inabaki vilevile kuwa kifo tu ndicho kingetenganisha wanandoa Adamu angeamua kumuacha Hawa ingekuwa sawa na kujiharibu mwenyewe je mtu aweaza kujikata sehemu ya mwili wake na kujitupa? Kama watu wakioana wanakua mwili mmoja unadhani kuna usalama watu wanapoachana rudi kwenye msingi wa neno, sasa tunapoona watu wanaachana leo na wanaolewa tena tujue kuwa shetani yuko kazini anafanikisha kazi yake ya kuharibu mpango wa Mungu kwa wanadamu na wote waliotengana na kuamua kuolewa tena wameshindwa vita na kama wana amani ni amani ya bandia, na kama wanamtumikia Mungu sijui ni kwa Biblia gani lakini msimamo wa bwana Yesu uko wazi zaidi ndoa nyingi sana zimepigwa leo, na watu wameoa tena na wengine ni wachungaji kama msimamo huu umekushinda ni vema ukauza nyanya, kwa sababu kama ndoa imekushinda unapoteza sifa ya kusimamia ndoa nyingi zilizoko kanisani, kama ndoa imekushinda huna sifa ya kuhubiri msamaha, huna sifa ya kuhubiri uvumilivu, huna sifa ya kufungisha ndoa, huna sifa ya kuwa kiongozi, maana umeshindwa hata kujisimamia mwenyewe!, huna sifa ya kuwa kiongozi wa maombi na mapambano ya kiroho kwa sababu umeshindwa vita na mapambano dhidi ya ndioa yako mwenyewe!

6.      Ndoa ya binadamu na mnyama.

Kama maswala ya uharibifu wa ndoa kwa talaka na mikataba hautoshi shetani ameshambulia sana ndoa na kuifikisha katika hatua ya wanadamu kutokutamani kuwa na binadamu wenzao sasa watu wanahangaika na kuzini na wanyama, katika karne hizi maswala haya yamezidi watu wanafikia hatua hata ya kufanya ngono na farasi, mbwa, nguruwe na kadhalika haya pia ni machukizo na machafuko ambayo Mungu aliyakemea ona Kutoka 22:19 “Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa.” Kwa nini haya yote yanatokea huu ndio mpango wa ibilisi katika kutaka kuharibu kabisa mpango wa Mungu kuhusu Ndoa, Muda usingeweza kutosha kuelezea kila kitu kibaya ambacho kinaashiria uharibifu mkubwa wa ndoa kwa aina binadamu, lakini hili ndio kusudi kubwa la shetani kuharibu na kushindana na kupambana na kupigana na ndoa kwa wanadamu wote, ndoa hizi zote za aina hii ni mpango wa ibilisi katika kushambulia na kuharibu kusudi kubwa la Mungu kutukuzwa kupitia uadilifu wa watu wake na ndoa zao.

7.      Ndoa ya watu wa Imani tofauti.

Mpango mwingine wa ibilisi katika kuharibu kusudi la Mungu katika ndoa yeye pamoja na majeshi yake ya pepo katika ulimwengu wa roho watataka watu waoane na watu wa imani tofauti kumbuka hapa sio kabila bali imani tofauti, Mungu alipowakataza wayahudi kuolewa na au kuoa mataifa wengine sababu kubwa haikuwa kabila zao bali imani zao, walikuwa wanaabudu miungu mingine na hivyo mpango na makusudi ya Mungu yangeharibika kwa shetani kulazimisha watu wa Mungu waolewe au waoe watu wasiokuwa na imani au wasioamini katika Mungu wa Ibrahim na Isaka na Yakobo  mtego mkubwa wa ibilisi kwa watu wa mungu ni kuwa wao na watoto wao waabudu miungu mingine jambo ambalo ni machukizo kwa Mungu Kumbukumbu 32:16 “Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa machukizo”.  Imani hizi ni mbaya na zina ushetani mwingi na uovu mkubwa sana Zaburi 106:37 “Naam, walitoa wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani.” Mungu hataki kwa namna yoyote watu wake kushirikiana na mashetani 1Wakoritho 10:20-21 “Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.Mungu alipowakataza wana wa Israel wasioane na watu wa mataifa yale yanayowazunguka sababu kubwa ilikuwa ni kuzilinda imani zao, kuwalinda wasiingie kwenye wimbi kubwa la kuabudu miungu na kushiriki ibada za kishetani, Mungu aliwaonya kuwa ndoa ni moja ya kwa watu hao wa imani tofauti ni moja ya mtego wa ibilisi atakaoutumia kuwaingiza katika ibada hizo na tabia mbaya isiyo ya kiadilifu na itakayoharibu utukufu wa Mungu duniani Kutoka 34:11-16 “Liangalie neno hili ninalokuamuru leo; tazama, mbele yako namtoa Mwamori, na Mkanaani, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.  Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako. Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao. Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa BWANA, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu. Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake. Ukawaoza wana wako binti zao, nao binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakawavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao.”  Unaona hakuna hekima unaweza kuitumia hapa kuwavuta wao kwa Mungu, wewe ndio utakayevutwa kuelekea upande wao na kujikuta ukiingia katika mtego wa ibilisi ni kwa kutumia ndoa shetani atajitahidi kuwanasa watu wa Mungu waingie katika mtego wa ibilisi ndoa na watu wa imani tofauti nay a Mungu wa kweli iko mifano kadhaa katika biblia ambapo muda usingeweza kutosha kuiona ya watu ambao walioa wanawake wa aina hiyo na baadaye wakajikuta wanaabudu miungu moja ya mifano hii ni Mfalme Sulemani aliyegeuzwa moyo na kumuacha Mungu wa baba yake kwa sababu ya kuoa binti za wanawake wa falme za kipagani 1Wafalme 11:1-6 “Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda. Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni. Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.Wewe huwezi kudai kuwa una hekima kama Suleimani lakini hata pamoja na kupewa hekima kubwa aligauzwa moyo na kuabudu miungu kwa sababu ya mtego wa ndoa, wakristo hawana budi kuvumilia na kusubiri kuolewa na mtu mcha Mungu wa jamii ya Kikristo, usikubali kuingia katika mtego wa ibilisi na kusukumwa kuoa au kuolewa na mtu wa imani tofauti na yako, unaweza kudhani kuwa mtazamo huu ni wa gano la kale tu hapana katika agano jipya pia Paulo mtume alikazia vikali kutokufungiwa nira na watu wasioamini ona 2Wakoritho 6:14-18 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.  Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,” andiko hili linakataza sio tu kuoana lakini hata kushirikiana katika maagano au vutu vyenye kutufunga pamoja na wasioamini, kwa kuwa tunazungumzia ndoa hapa nataka kukazia kuwa Mungu hajaruhusu ujiolee tu mtu wa imani tofauti  na ya Mungu wa kweli n ukioana na mtu awaye yote ambaye yuko nje ya ushirika na Yesu umeingia katika mtego wa ibilisi katika ndoa yako wewe na watoto wako, unapooa mtu wa imani tofauti na yako maana yake unaunganisha mwili wako na mtu anayetokea katika chanzo kingine cha kiroho jambo hili litazuia kuendelea kuenezwa kwa utukufu wa Mungu duniani Kumbukumbu 22:10 . “Usilime kwa ng'ombe na punda wakikokota jembe pamojamwenye masikio ya kusikia na asikie

8.      Ndoa ya watu waovu.

Ni muhimu kufahamu kuwa shetani akitaka kuleta uharibifu katika kanisa hutumia ndoa mbovu ya watu waovu, kama katika kanisa kutakuwa na ndoa mbovu ni rahisi kuwa na kanisa bovu au kuwa na viongozi waovu, Tangu kanisa lilipoanza kwa nguvu siku ya Pentecost tunaona Shetani hajawahi kutajwa tena mpaka katika Matendo 5:1-11 1. “Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali, akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?  Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya. Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika. Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo.Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe. Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe. Hofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya.Hapa shetani anatajwa kwa mara ya kwanza katika kanisa la kwanza akiwa amewatumia wana ndoa Anania na Safira wao ni wana ndoa walioshindwa kumpinga shetani ili kusudi wasitumbukie katika mtego wa dhambi, kutokana na tabia yao na mwenendo wao waliliathiri kanisa kwa kumpa ibilisi nafasi na wakapatana pamoja ili walidanganye kanisa hii inatufundisha nini kwamba Shetani anaweza kuzitumia ndoa kupinga mpango wa injili, kuna wanadoa wengi wanaotaka kujitoa kwaajili ya kanisa lakini shetani anaweza kuwazuia wenzi wao wasitoe, kuna wahubiri wengi wazuri wameanguka na kushindwa kuwa Baraka kwa kanisa kwa sababu ya ndoa mbovu, unasikia muhubiri mkubwa sana anayetumiwa na Mungu kwa mamlaka ya ajabu sana, mkewe anavunja maagizo ya neno la Mungu la kutokunyimana agizi ambalio liko wazi msinyimane wao wanawabania waume zao na kuharibu huduma zao katika karne hii haya tumeyaona sana Petro aliona ni afadhali hawa wafe lakini Kanisa liendelee, watu wengi kwaajili ya ubinafsi, choyo, ujinga na kutokuelewa hawafikiri kuwa wao ni wa muhimu sana katika huduma za kanisa kupitia ndoa zao, kupitia uovu wa wana ndoa kazi ya Mungu inakataliwa, mabinti wengi na wamama wamekwaza katika huduma zao kwaajili ya mama wachungaji wenye wivu mkali wa kimapenzi, eti mumewe anapofanya huduma yeye anawaza kuwa mumewe ataibiwa, mabinti wanapotaka kumtumikia Mungu wao wanawaza ujinga, shetani amepata nafasi sana ya kulishambulia kanisa kupitia ndoa za watu waovu. Watu wengi wameingia katika mtego wa ibilisi kupitia wake zao akiwemo Adam kwa msingi huo ni muhimu kwa kila mwanandoa kujua na kutambua kuwa usafi wake wa moyo una umuhimu mkubwa kwa kanisa na kuwa tabia zao zina umuhimu mkubwa kwa kanisa fikiria kama Mariamu na yusufu wangekuwa hawana msimamo katika ndoa yao Je wangeweza kuwa Baraka kwa ulimwengu kwa kumlea Masihi!

9.      Kukataza watu wasioe wala kuolewa.

Paulo alimuonya Mwangalizi askofu Timotheo kuwa awe makini kwa sababu wengine watamfuata shetani na kufuata roho zidanganyazo nyakati za mwisho kutakuwako na aina nyingi sana za mafundisho na ni mafundisho ya mashetani na yatakuwa na nguvu sana katika kanisa na hivyo watu wa Mungu wanapaswa kuwa makini katika maonyo hayo yote utaweza kuona shetani hataacha kutumia ndoa angalia katika 1Timotheo 4:1-3 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.Unaona hapa shetani analishambulia kanisa kwa njia muhimu, halishambulii kanisa kwa kukanusha kuwa hakuna utatu, au Kuwa Yesu sio Mungu hapa shetani anaingiza kwa werevu mafundisho yenye kukataza watu kuoa au kuolewa, katika nyakati hizi kulikuwa na mafundisho kuwa kutokuoa ndio kujitoa kwa viwango vya juu sana katika maswala ya wokovu na huko Coritho walifundisha wazi kuwa unaweza kuoa lakini tendo la ndoa ni najisi na hivyo kujiepusha nalo ni kwa muhimu sana katika kujitoa kwako kwa Mungu kiasi ambacho wakristo walinyimana sikiliza nikuambie ni wazi kabisa haya ni mashambulizi ya nshetani na ni muhimu ikaeleweka wazi kuwa kukataza Wakristo kuoa au kuolewa ni sawa na kukataza injili isihubiriwe.

10.  Ndoa ya watu Kunyimana unyumba

Ndoa inaimarika kwa kushirikiana kwenye tendo la ndoa la mara kwa mara au ikiwezekana kila siku na kila saa nafasi ipatikanapo na kama afya zinaruhusu, 1Wakoritho 7:2-5 “Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.”        

Kushirikiana katika tendo la Ndoa kwa wana ndoa mara kwa mara ni jambo zuri na linakubalika sana mbele za Mungu, katika kanisa la Koritho kulikuwa na tatizo la watu kufikiri kuwa huenda tendo hili ni dhambi, kwa hiyo watu walikosa kiasi na kujitoa kwa Mungu katika kufunga na kuomba wakishindwa kuwa na kiasi katika kukumbuka ndoa zao, Paulo mtume aliwakumbusha wajibu wa kila mwana ndoa kuhakikisha kuwa wanashirikiana tendo la ndoa 1Wathesalonike 4:3  Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;” jambo au wazo la kufikiri kuwa tendo la ndoa ni dhambi lingeharibu hali ya utakatifu wao lakini tendo hili linapofanyika ndio linaimarisha utakatifu miongoni mwa wanandoa, swala la kujinyima tendo la ndoa kwa kufikiri kuwa ndio kujitoa kwa Mungu yalikuwa ni mafundisho potofu kwa kanisa la Korintho, Paulo mtume alieleza kwa uwazi kwamba mke na mume wanapaswa kushirikiana tendo la ndoa bila vikwazo kwa hiyo aliwaamuru wasinyimane (Mst5) Kumpa mwenzi wako tendo la ndoa ilikuwa ni moja ya wajibu ambao uliamuriwa katika Torati Kutoka 21:10 “Kwamba ajitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia.” Kumpa mkeo ngono au mumeo ngono ni wajibu kwa kuwa ni haki ya mwenzi wako iwapo mtu hatatoa haki hiyo kimaandiko Mungu atakuja kumuhukumu kwa kosa la kutokutoa haki na kutokumuogopa yeye angalia Malaki 3:5 “Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi.Lugha aliyoitumia Paulo mtume kuhusu kupena haki inafanana na lugha inayotumika kudhulumu au kutoa haki kwa mtu aliyeajiriwa na kutokumpa au kumpa  haki yake au ujira wake au mshahara wake ona katika Yakobo 5:4 “Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi.” Kwa msingi huo kitendo cha kumnyima mwezi wako kinafanana na kuzuia haki ya mtu au mshahara wa mtu au kumdhulumu kwa hiyo kilio cha mwezi wako kuhusu tendo la ndoa au kunyimwa hali yake kitaingia masikioni mwa Bwana na Bwana atahukumu! Sasa Paulo mtume sio tu anaonya na kuwataka wanandoa kupeana haki lakini vilevile anaonya kuwa kunyimana huko kutampa ibilisi nafasi yaani watu wanaonyimana tendo la ndoa au kukosa kiasi kwa visingizio vya kujitoa kwa Mungu na kumnyima mwezi wako tendo la ndoa ni kumkaribisha shetani kuingilia ndoa yenu, shetani akifanikiwa kuwaangusha au kumuangusha mwanandoa mmoja mnakuwa mmewapa nafasi maadui wa Yesu Kristo kukufuru 2Samuel 12:14a “Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za Bwana nafasi kubwa ya kukufuru,  kwa hiyo jina la Bwana litadhaulika watu wanaofundishwa na kuhubiriwa injili watakuwa na moyo mgumu na unasababisha kikwazo kwa injili ya Mungu kusambaa ulimwenguni kote, njia sahihi ya kutatua tatizo hili ni kuhakikisha kuwa wana ndoa wanapeana tendao la ndoa kila wakati, na wote mnalifurahia tendo hilo, kinyume cha hayo mnakaribisha mashambulizi ya shetani kwenye maisha yenu na huduma zenu. Baraka kubwa na mafanikio makubwa ya mwanadamu yamefungwa katika ndoa kama wanadamu wataharibu ndoa wataondoa baraka zote ambazo Mungu amezikusudia acha kuzuia baraka zako, acha kuharibu mpango na kusudi la Mungu kwa mwenzi wako kwa kumnyima au kwa kunyimana kumbuka shetani yuko kazini kukuharibia ndoa yako na ndoa yako ikiharibika umeingia dosari.

Jedwali hapa chini linaonyesha ndoa katika mpango wa Mungu na ndoa katika mpango wa ibilisi

NDOA KATIKA MPANGO WA MUNGU
NDOA KATIKA MPANGO WA IBILISI
Mwili mmoja
Iwe njema
Mke na mume
Mke mmoja
Enye utaratibu
Bila zinaa
Hakuna kuachana
Ya kudumu
Yenye amani na utulivu
Yenye utakatifu
Yenye kupeana
Imani moja
Binadamu kwa binadamu
Nnia sahihi

Mali ya kila mmoja
Watu wanyimane
Jinsia moja
Wake wengi
Isiyo ya utaratibu
Enye zinaa
Yenye talaka
Ya mikataba
Mafarakano na kero
Yenye uchafu
Yenye kunyimana
Imani ya mashetani
Binadamu na wanyama
Njia isiyosahihi

Jinsi ya kupambana na kuitetea ndoa yako
Sheatani pia ataishambulia ndoa ya Kikristo kwa mashambulizi ya aina mbalimbali yakiwemo magonjwa na  mateso mengine yakiwa na uhusiano na uzazi au viungo vya uzazi moja kwa moja ili Ndoa ya Wakristo iweze kuwa imara na yenye kusimama kama lilivyo kanisa wanandoa wanapaswa kuvaa silaha zote za Mungu ili waweze kuzipinga hila za shetani
Waefeso 6:10-20 10. “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.  Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu
kitabu cha waefeso ndio kimezungumzia kwa undani zaidi mapambano ya vita vilivyopo katika ya shetani na kanisa kuliko kitabu kingine chochote, ni kweli tunafahamu kuwa shetani ameshindwa pale Msalabani, lakini ni muhimu kukumbuka sehemu ya hukumu yake haijalkamilika mpaka mwisho wa dahari kwa msingi huo akiwa bado ni mungu wa dunia hii yeye na majeshi yake anapambana na kanisa lakini vilevile anapambana na wana ndoa kwa msingi huo basi ni muhimu kwa wanandoa kusimama imara na kupambana kiume dhidi yake ili waweze kushinda kama ningekuwa natumia English ningeweza kutumia neno  you must be very aggressive” ndio maana biblia inasema tuwe Hodari hii ni lugha ya kivita tuwe hodari katia uweza wa nguvu zake, wanandoa wana nguvu kubwa sana ya kumsabaratisha shetani kama ndoa yao itasimama imara  Kumbukumbu la torati 32:230 “Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana asingaliwatoa?unaweza kuona pia katika Muhubiri 4:9-12 “9. “Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!  Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto? Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.” Biblia inaonyesha kuwa wawili hii ni wale walioshikamana walio na umoja wana nguvu kubwa sana wana uwezo mkubwa sana wa kusambaratisha adui katika ulimwengu wa roho na ndio maana shetani hupigana na wana ndoa ili kuondoa umoja na mshikamano na wakati mwingine ugomvi vita na mafarakano, kinyongo na kutokusameheana ili yamkini hata wana ndoa wasiweze kuomba pamoja  na kama wana ndoa wakifarakana kisha mmoja aakaomba peke yake hawezi kufanikiwa na kupenya 1Petro 3:7 “Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

Ili wanandoa waweze kuwa na ushindi dhidi ya vita kali dhidi ya Shetani wanapaswa kuishi kwa amani wanapaswa kuitafuta sana amani ili kusudi maombi yao yasizuiliwe, kumbuka tunapambana na shetani hivyo tunapaswa kuwa makini sana tunapaswa kuvaa silaha zote za Mungu ili tuweze kuzipinga hila zake asili ya vita yetu hii ni ya kiroho lakini matokeo yake ni ya kimwili, shetani atataka kutushambulia na kutuvuruga akitaka kuhakikisha kuwa mke anakuwa kinyume na mumewe na mume anakuwa kinyuma na mkewe au watoto kinyume na wazazi, aidha vita hii itaathiri wote wanaowazunguka likiwemo kanisa.

Mkiyajua hayo heri ninyi mkiyatenda!

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!