Yohana 19:20-22 “Basi anwani hiyo waliisoma
wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulibiwa Yesu palikuwa karibu na
mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani. Basi wakuu wa
makuhani na Wayahudi wakamwambia Pilato, Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; bali ya
kwamba yule alisema, Mimi ni mfalme wa Wayahudi. Pilato akajibu, Niliyoandika nimeyaandika.”
Utangulizi:
Leo tutachukua Muda kujifunza
jambo la muhimu sana kutoka kwa moja ya Mtawala maarufu sana aliyehusika katika
kumuhukumu Yesu Kristo kwenda msalabani na kusulubiwa, Mtawala huyu au Liwali kwa
jina lingine anajulikana kama Pontus Pilatus kiwashili Pilato, Moja ya jambo la
msingi sana tutakaloweza kujifunza ni kuhusu Msimamo wake na mtazamo wake kuhusu Yesu kristo, tutajifunza somo hili kwa
kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo:-
·
Historia
fupi ya Pontius Pilato
·
Niliyoyaandika
nimeyaandika
Historia fupi ya Pontius Pilato *PONTIUS PILATUS*
Ponsyo
Pilato Moja ya watawala vijana
sana kupata kutokea kama anavyoelezewa na Mwanahistoira maarufu wa karne ya
kwanza aliyejulikana kama FLAVIUS
JOSEPHUS aliyekuwa myahudi aliyekuwa na ujuzi wa lugha Kiaramu, Kiebrania
na kigiriki (Aramaic, Latin and Greek) Lugha ambazo zilitumiwa na wasomi wengi
wa nyakati ya karne ya kwanza mtu huyu
Flavius Josephus aliishi kati ya mwaka 37-100 BK na alikuwa kuhani Myahudi, alitekwa na warumi na kuwa Mkalimani wa Kaisari
Vespasian kwa miaka miwili,
Kitabu chake kinapatikana hata kwa ku- download electronic book kama Works of
Flavius Josephus ikitabu chake hicho ni kirefu sana na kinachukua muda mrefu kukisoma.
Yeye anamuelezea
Ponsyo Plato kwa kilatini PONTIUS
PILATUS aliyekuwa liwali wa Kirumi katika inchi ya israel kati ya mwaka
26-36 wakati wa Yesu Kristo, yaani miaka 10 Pilato Anajulikana kutokana na vyanzo mbalimbali,
lakini hasa kwa sababu ya Injili kumtaja
kama hakimu aliyempeleka Yesu kuuawa msalabani. Historia yake
ina0onyesha alipewa utawala akiwa kijana mdogo sana kwa sababu inasemekana
alizaliwa mwaka wa 12 baada ya Yesu, kwa hivyo wakati wa hukumu ya Yesu yeye
alikuwa na umri wa miaka 21 hivi, ukiacha kutajwa katika injili zote nne na
kuelezewa zaidi katika injili ya Yohana pia anatajwa katika
Matendo ya Mitume 3:13 “Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe” utaweza kuona pia
Matendo ya mitume 4:27 27. Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta, ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee.” Na pia anatajwa katika
Matendo 13:28 “Na ijapokuwa hawakuona sababu ya kumfisha wakamwomba Pilato auawe.” Na Paulo mtume alimtaja tena katika kitabu cha
1Timotheo 6:13 ”Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato,”
unaweza kuona namna mtawala huyu anavyotajwa sana katika maandiko, maana yake ni kuwa alikuwa mtu maarufu ambaye wahubiri wa hyakati za kanisa la kwanza hawakuweza kumsahahu! Kwa karne nyingi Pilato amekuwa mtu asiyeweza kusahaulika pilato anatajwa pia katika ukiri wa imani, au imani ya nikea au imani ya mitume au sala ya nasadiki kama “Zamani za Pontio Pilato aliteswa”

Pilato maisha yake ya awali hayajulikani sana japo
viko vyanzo vinavyoeleza kuwa alikuwa ni
Mtot aliyezaliwa nje ya Ndoa ya Mfalme wa Tiro, ambaye alimtuma kwenda Rumi kama muhudumu na
huko aliua mtu na akatumwa kupelekwa Asia ndogo kwa makusudi ya kushughulikia
watu Korofi, kutokana na ukorofi wake mkubwa alipata kibali kwa Warumi alipewa
zawadi ya kutawala kama gavana wa jimbo la Uyahudi (Judea) na Mtawala Tiberio kwaajili ya
kuwashughulikia Weayahudi ambao mara kwa mara waliasi.
Alikuwa mtawala Katili sana aliyeamuru
kuuawa na kusulubiwa kwa wayahudi wengi sana, adiah aliwaudhi wayahudi sana kwa kuleta
desturi za kirumi na hata kukleta habari za miungu migenikwenye hekalu, wakati
mwingine aliweza hata kuchukua kodi za hekaluni na kuzitumia kwa matumizi yasiyofaa
alikuwa muuaji na mtu aliyeweza kuwaua wayahudi vibaya sana moja ya habari za
ukatili wake zilienea wakati wa Yesu ona katika
Luka 13:1” Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.”
Luka 13:1” Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.”
Nilichokiandika
nimekiandika!
Inasemekana makazi makuu ya
Pilato yalikuwa ni Kaisaria hata hivyo Pilato alikuwa na desturi ya kuja
Yerusalem siku za sikukuu kwaajili ya kutuliza Ghasia na kuwadhibiti wayahudi,
wakati wa kukamatwa kwa Yesu, kwa vile yalikuwa ni majira ya Pasaka Pilato alikuwako
Yerusalem, wakuu wa makuhani walipokwisha kumuhukumu Yesu kwa mila na desturi
zao, waliona vema pia kumpeleka kwa Pilato walifahamu tabia zake na hivyo
walijua kuwa kwa ukatili aliokuwa nao Hakuna myahudi anayehusishwa na vurugu
angeweza kusalimika, mambo kadhaa yaliweza kujitokeza wakati wa hukumu ya Bwana
Yesu
Moja ya muujiza mkubwa sana kuwahi
kutokea ni kwa jamaa huyu muuaji na katili kuonekana akinawa mikono na kugoma
kumpeleka Yesu Msalabani kwa sababu
alibaini wazi kuwa Yesu hakuwa na hatia yoyote na alielewa kuwa Wayahudi
wanamleta kwake kwa sababu ya husuda tu hili lilikuwa jambo la kushangaza kwa
vile alikuwa hacheleweshi kesi, na haponyi mtu, kusitasita katika kumuhukumu
Bwana Yesu ilikuwa ni moja ya tabia mpya na ya ajabu iliyowastaabisha wayahudi
kwa sababu walijua wamempeleka penyewe, Aidha Familia yake ilikuwa na taarifa
za Mapema kuwa anakuja mtu mwenye haki na kuwa Pilato anapaswa kuwa na
tahadhari namna atakavyoshughulika na kesi ya mtu huyo ujumbe huu alipewa na
mke wake akimtahadharisha kuhusu hukumu ya siku ile Pamoja na hayo alifanya
kila jitihada kumuokoa Yesu kupitia Mfungwa aliyekuwa hatari na muhaini zaidi
kuliko Yesu lakini hata hivyo wakuu wa dini bado walijaa husuda yaani wivu dhidi
ya Yesu Ona
Mathayo 27: 16-19 “Basi palikuwa na mfungwa mashuhuri siku zile, aitwaye Baraba. Basi walipokutanika, Pilato akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi? Yule Baraba, au Yesu aitwaye Kristo? Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa husuda. Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.”
Pilato pia alikuwa ni mtu pekee aliyeweza kupata nafasi ya kuzungumza na Yesu kipekee na kujua kusudi la kuwepo kwa Yesu Duninani. Yeye alimuelewa wazi Yesu kuwa amekuja kuishuhudia kweli, na kuwa yeye mwenyewe Yesu ndio kweli, aidha alitambua wazi kupitia Yesu kuwa mamlaka aliyonayo yeye imetoka juu yaani imetoka kwa Mungu na pia alipata nafasi ya kujua na kuelewa kuwa Yesu alikuwa mfalme kweli lakini ufalme wake haukuwa wa ulimwengu huu
Yohana n18:33-38a “Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi? Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu? Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini? Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa. Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu. Pilato akamwambia, Kweli ni nini?”
Ni wazi kabisa mpaka wakati Pilato anakuja kutoa hukumu kupitia mashinikizo ya kisiasa kutoka kwa wayahudi tayari kitu Fulani kilikuwa kimejengeka moyoni mwake kuhusu Yesu Kristo na kama isingalikuwa maandiko yatimizwe ni wazi kuwa Pilato angemuachia Yesu huru!

Hapa sasa tunaona wazi kuwa
Maadui wa Yesu Kristo walikuwa wanategemea kuwa kwa kuwa wamemleta Yesu Kwa Pilato
hawezi kusalimika lakini hawakuwa wamejua kuwa Mungu aliandaa kitu katika Moyo wa Pilato na
kuwa hawakujua kuwa Pilato alikuwa anaujua wivu wao na akaandaa aibu kubwa sana na udhalilishaji ambao
wangeupata kuhusu ubaya wao huo, aibu hii yalikuwa ni maneno yaliyowekwa na
Pilato juu ya Msalaba wa Yesu.
Pilato aliandika meneno hayo na
kuyaweka katika msalaba wa Yesu yaliyokuwa yakisomeka “YESU WA NAZARETH MFALME WA WAYAHUDI” Wayahudi wengi sana waliyasoma maneno haya kwa
sababu mahali aliposulubiwa Yesu palikuwa ni karibu na lango la jiji la
Yerusalem na ni mahali ambako wengi walipita, Meneno haya yaliandikwa kwa lugha
kubwa tatu Kiaramu, Kilatini na Kiyunani hivyo yaliweza kusomwa na watu wote
hata wageni waliokuja kutoka sehemu mbalimbali duniani kwaajili ya sikukuu ya
pasaka, wakuu wa makuhani hawakuyafurahia hata kidogo maneno yale kwa hiyo
walimwendea Pilato na kumwambia,
Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; bali ya kwamba yule alisema, Mimi ni mfalme wa
Wayahudi Pilato akajibu, Niliyoandika
nimeyaandika.”
Ilikuwa ni desturi kwa kila
muhalifu anayehukumiwa kusulubiwa na
warumi kuwekewa mashitaka yake juu ya msalaba ili kwamba kila anayepita aweze
kuona ili iwe fundisho kwake, Lakini kwa Kristo ilikuwa kitu cha kushangaza
sana ! hayakuwa mashitaka bali lilikuwa Tangazo halisi kwa ufunuo halisi
Yesu hakuonekana na hatia alikuwa
amehukumiwa kwa sababu ya wivu wa wayahudi tu na Pilato alifahamu, Wayahudi
walikuwa wamechukizwa naye kwa sababu yeye alisema wazi kuwa ni mwana wa Mungu
na pia ndiye mrithi halali wa kiti cha ufalme cha Daudi baba yake, Pamoja na
hayo miujiza mikubwa aliyoitenda na umati mkubwa uliomfuata na kumkubali
ulisababisha wayahudi kupoteza umaarufu wao wa kidini, watu walikuwa
wamemkubali Yesu kuwa ndiye masihi wao, Wayahudi na Viongozi wa kidini wao walijua kwa makosa haya ingeweza
kumshawishi Pilato kutoa hukumu kali kwa kufikiri kuwa Yesu anamuasi kaisari
kwa kujiita Mfalme, Lakini Pilato alielea ukweli Yesu ni mfalme wa namna gani
na kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao
Viongozi wa dini, kwa hivyo hakukuwa na mashitaka zaidi ya hayo Kila ambaye
angeona mashitaka hayo angeweza kueneza habari kuwa Yuko Mfungwa amesulubiwa
msalabani na ni Mfalme wa wayahudi, hana makosa mengine ni mfalme wa wayahudi habari
zingeweza kuenea Rumi, Uyahudi na kila mahali walikotumia lugha zile
alizoandika Pilato, Bila shaka kosa hili la uandishi halikuwa kosa la
kibinadamu, wala Pilato hakuwa amekosea
katika kile alichokiandika ilikuwa wazi kabisa kwamba Pilato alikuwa na ufunuo
sahihi kuwa Yesu alikuwa Mfalme wa Kiroho kwa watu wote walipomwambia ayaondoe maneno yale Pilato
alijibu kwa kiyunani Ho Gegrapha gegrapha! na kilatini Quod scrips scrips, what i have written
I have written yaani Nilichokiandika
nimekiandika Pilato alimaanisha kuwa
ujuzi wake kuhusu Yesu hakuna mtu wa aina yoyote anaweza kuubatilisha ule
ulikuwa ni ukweli uliowazi kabisa ambao Pilato alikuwa ameubaini na ambao
alitaka watu wote watambue, Kila mmoja leo anapaswa kukubali na kutambua Kuwa
Yesu ni Mashihi, Yeye ndiye aliyekusudiwa kwa wayahudi na ulimwengu mzima litakuwa
ni jambo la ajabu sana kwa Mtu mkatili ikama Pilato kubaini ukweli na kujua
kuwa Yesu ni mfalme wa wayahudi na akaanidla kwa lugha tatu kuu za wakati uoe
akitaka kila mtu na kila lugha na kila taifa wajue YESU WA
NAZARETH HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI, Viongozi wa kidini walimsihi
ayaondoe maneno hayo lakini jambo lingine la kushangaza aligoma alisema *NILICHIKIANDIKA NIMEKIANDIKA* Kwa lugha
nyingine Pilato alikuwa anasema amethibitisha, ana uhakika, alichikithibitisha
hakiwezi kutenguliwa milele, Pilato alikuwa gavana alikuwa liwali alikuwa
kiongozi mkubwa alikuwa katili alikuwa muuaji, alikuwa na mamlaka kubwa sana
alihukumu Kesi ya yesu alikuwa kijana alikuwa na akili sana alikuwa katili
lakini alikiri kwa maandiko tena hadharani ya kuwa Yesu ni mfalme wa Wayahudi,
alikuwa anakubali wazi kuwa yesu ni Bwana aluikuwa ameifahamu kweli swali lake
kubwa kwa Yesu Kweli ni nini ? Yesu ndiye njia na kweli na uzima, leo hii kila
mmoja anapaswa kumkiri Yesu kwa utukufu wa Mungu baba haijalishi una cheo gani
haijalishi umefanya dhambi ngapi umwamini Yesu, ukubali kuwa Yesu ni Bwana na
uwe tayari kumtetea Yesu kwamba ulichokiamini umekiamini, ulichiokithibitisha
umekithibitisha ulichokiandika umekiandika Yesu ni Mfalme wa wayahudi!
Kwa mujibu wa kanisa la Orthodox la Ethiopia wanamtambua Pilato
kama Mtakatifu mwenye heri wakiamini kuwa alimkubali Yesu kwa kuokoka na hivyo
ni mtu mwenye kuheshimika sana. Ndio maana anatajwa katika ukiri wa imani ya
Mitume ! NILICHOKIANDIKA NIMEKIANDIKA!
Na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi, mwenye Hekima.
0718990796
0718990796
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni