Alhamisi, 25 Machi 2021

Kifo Katika Mpango wa Mungu!

Ayubu 14:5 “Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe, Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;”


Utangulizi:

Kumekuwepo na mijadala mbalimbali, mitazamo na falsafa kuhusu kifo!, Baadhi wakiamini kuwa kila kifo ni mapenzi ya Mungu, wengine wanaamini kama Mungu akiamua usife huwezi kufa na akiamua ufe unakufa, na wengine wakiamini kuwa kila mwanadamu ana siku zake zilizoamriwa kuishi duniani na zikikamilika anaondoka, wengine wanaamini kuwa Mungu huwa anahuzunika sana mtu anapokufa kama sisi  nasi tunapohuzunika matukio ya kifo yanapotokea, lakini kwa sababu tunaishi katika ulimwengu wa dhambi Mungu huruhusu kifo kutokea Ni muhimu kufahamu kuwa ni neno la Mungu pekee yaani Biblia inayoweza kutupa majibu ya maswali yetu kuhusu kifo na maana halisi ya kifo kinapotokea! Lakini ni lazima kwanza tufahamu kuwa Mungu hapendi kuwatesa wanadamu wala kuwahuzunisha ona

 

Maombolezo 3:31-33 “Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.”

Kifo katika mpango wa Mungu!

Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu katika mpango wake hakuwa amekusudia kifo kiwepo katika maisha ya mwanadamu, na ndio maana kwa asili hakuna mwanadamu anayekubali au kukipenda kifo kwa sababu kimsingi sio maumbile ya asili yetu Mungu alimuumba mwanadamu ili aishi milele na ndio maana kifo kimekuwa kinampa taabu sana mwanadamu kwa maana haukuwa mpango wala mapenzi kamili ya Mungu



Muhubiri 3:10-11 “Nimeiona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.” 


Kifo na taabu zake kimekuja kama matokeo ya kuasi kwa mwanadamu, kwa hiyo Mungu alimuwekea mwanadamu uchaguzi kuchagua uzima au mauti kupitia kutii au kuasi na kwa bahati mbaya mwanadamu akaasi na hapo ndipo ilipokuja adhabu ya kifo ambayo Mungu alikuwa amemuonya nayo Adamu ona


Mwanzo 2:15-17 “BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”


Kwa msingi huo kifo kipo Duniani leo kwa sababu ya kuasi kwa mwanadamu mmoja baba yetu Adamu na mama yetu Eva kwa sababu sisi tulikuwa viunoni mwao wakati wana wanaasi na kwa sababu hiyo wanadamu wote wanaonja mauti ona


Warumi 5:12 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;”


kwa hiyo kifo kiliingia ulimwenguni kwa sababu ya dhambi na kikawafikia watu wote kwa nini kwa sababu wote tulikuwa katika viuno vya wazazi hao kwa msingi huo tuwe wema au tuwe waovu ni lazima tutaionja mauti, Kama mwanadamu hangelifanya dhambi, muda wetu wa kutimiza makusudi ya Mungu Duniani ungekuwa kama umekamilika Mungu angetutwaa kwenda mbinguni kukaa naye bila kuonja mauti ona

Mwanzo 5:24 “Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa


.” Huu ndio ulikuwa mpango kamili wa Mungu (Perfect will of God), kwa msingi huo kifo sio mpango kamili wa Mungu bali ni matokeo ya dhambi ambayo yameruhusiwa na Mungu (permissive will of God).sasa kifo kimekuwepo na Mungu aliandaa mpango mwingine wa kukikomesha wakati wa utimilifu wa dahari utakapowadia.

Je kila kifo kinachotokea ni mpango wa Mungu?

Swali hili linaweza kuwa na majibu NDIO na HAPANA kulingana na mazingira ya kifo chenyewe kwa mujibu wa neno la Mungu sio kila kifo kinachotokea ni mpango wa Mungu wala sio mapenzi yake kamili, Maandiko ynashuhudia wazi kuwa Mungu hapendi wala hafurahii kufa kwake mtu mwenye dhambi! Ona

Ezekiel 33:11 “Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, SIKUFURAHII kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?


kwa hiyo kumbe linapokuja swala la Mtu kufa Mungu hapendi afe mtu mwenye dhambi, Mungu hafurahii kufa kwake mtu muovu, Mungu anatamani mtu awe ametubu, awe amegeuka na kuacha njia mbaya kabla ya kifo ili waweze kuungana naye, haya ndio mapenzi kamili kwa kila mwanadamu na ndio maana wakati mwingine Mungu huwaacha waovu kwa kitambo na kuwavumilia ili yamkini ikiwezekana wafikie wakati wa kutubu ona


2Petro 3:9 “. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, Kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana HAPENDI mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba”.


kwa hiyo Mungu hapendi, na hafurahii na hivyo kuna nyakati huwacheklewesha waovu wasife kwa haraka au wasife kabla hawajafikia toba, kwa hiyo kuna mazingira ambayo kwayo Mungu hatafurahia au hafurahii kufa kwa mtu hususani mtu mwenye dhambi. Kwa hiyo Mungu husubiri mtu aifikie toba mtu ageuke na kuiacha njia yake mbaya

Hata hivyo kifo ni kanuni, ni kanuni ya adhabu kwa kitokumtii Mungu, kifo kama kanuni ya adhabu ya kutokumtii Mungu ni hitimisho la hatua kadhaa zisizochukuliwa katika hatua ya dhambi, angalia andiko hili kwa mfano


Yakobo 1:14-15 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.”


Kanuni ya kifo ni dhambi kuna namna ambavyo Mungu katika hekima yake anakiruhusu kifo kwa nafi yenye dhambi, japo kifo sio mapenzi yake kamili lakini ni mshahara wa dhambi kwa hiyo kama nafsi itajaribiwa dhambini na kukawia kufanya toba na kwa bahati mbaya hatuwezi kujua muda ambao Mungu anatupa wa toba kanini ya kifo ambayo ni dhambi ikikomaa inaleta mauti kwa hiyio Mungu pia huruhusu mtu kufa endapo nafsi ya mtu huyo itatenda dhambi ona mfano


Ezekiel 18:20-23 “Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake. Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa. Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi. Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi?” 


Unaona hivyo basi kutokana na kanuni Fulani za dhambi zinapoendelea kutendwa na nafsi basi Mungu huweza kuruhusu Dhambi hiyo kusababisha kifo na kukatiza uhai wa nafsi husika kwa ain azote za uzima huu na ule ujao 


Kutoka 21:14,-16 “Lakini, mtu akimwendea mwenziwe kwa kujikinai, kusudi apate kumwua kwa hila; huyo utamwondoa hata madhabahuni pangu, auawe. Ampigaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.Yeye amwibaye mtu, na kumwuza, au akipatikana mkononi mwake, sharti atauawa huyoKatika mazingira kama kifo kinachotokea hapa ni mpango wa Mungu katika mantiki kwamba uovu umepelekea kufa, tama imepelekea nafsi itendayo dhambi kufa, kwa hiyo sio mapenzi ya Mungu mtu kufia katika dhambi, lakini ni mwanadamu anapokuwa na ukaidi Fulani kinyume na amri za Mungu mungu huruhusu mtu huyo kufa. Kwa hiyo yako mazingira jibu linaweza kuwa ndio na yako mazingira jibu linaweza kuwa sio!

Kwa mfano sio mapenzi ya Mungu kwa watoto wasiowahehimu wazazi wao kufa kabla ya wakati ona Waefeso 6:1-3 “Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.” Kumbe ni mapenzi ya Mungu kwamba watoto wawaheshimu wazazi wao ili siku zao zipate kuwa nyingi tena na za heri duniani, Lakini mtoto ambaye atamlaani baba yake au mama yake Mungu ameamuru apigwe kwa mawe mpaka kufa, kwa lugha nyingine maisha ya mtoto asiyewaheshimu wazazi yatafupishwa 


Kutoka 21:15, 17 “Ampigaye baba yake au mama yake, sharti atauawa. Yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.” kwa hiyo ni wazi kuna mazingira ya aina fulani Mungu hataki mtu afe kwa dhambi na kuna mazingira fulani Mungu huruhusu mtu afe kwa sababu ya dhambi.

Je Mungu hujisikiaje wanapokufa watu wengi?

Swala lingine nyeti ni je Mungu hujisikiaje wanapokufa watu kwa wingi? Kimaandiko bado Mungu huuzunishwa sana wanapokufa watu wengi wakiwa dhambini, Mungu huuzunishwa dhambi inapozidi na hivyo huweza kuruhusu maangamizi mfano 


Mwanzo 6:5-7 “BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.” 


Wakati wa Nuhu Mungu aliufutilia ulimwengu kwa gharika kwa sababu ya kuongezeka kwa maasi, kimsingi Mungu hafurahii udhalimu na uovu unaofanywa na watu, hapendi watu wafe lakini dhambi hupelekea Mungu kuruhusu vifo.


Dunia inaweza kukabiliwa na majanga kama watu hawatatubu, mji au nchi au taifa kama halitamjali Mungu Mungu anaweza kuachilia roho ya mauti ikafanya kazi yake na kuleta madhara kwa watu wema na wabaya wote wakaathirika kutokana na ule ukaidi wa kibinadamu wa kufa kwa dhamiri na kutaka kuendelea kuishi katika maisha ya dhambi ona 


Mwanzo 18:20 “BWANA akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana,” 

Dhuluma na uharibifu wa dhambi uliofanywa na watu wa Sodoma na Gomora ulimsukuma Mungu kuruhusu miji hiyo kuangamizwa kwa wingi wao, Kimsingi watu wengi wa mji au taifa wanapomgeukia Mungu na kuomba rehema zake kwa toba na kuacha njia yao mbaya Mungu huwarehemu watu hao ona 

Yona 3:11-10 “Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru. Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu. Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng'ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe? Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.” 


 Ni wazi kuwa Ninawi ulikuwa mji mkubwa yaani wenye watu wengi na waliishi maisha ya dhambi na dhambi hiyo ilifikia mstari wa kuwaletea mauti lakini walipogeuka na kutubu Mungu aliwasamehe na kifo kikaahirishwa kwao, hii ni ahadi ya Mungu kwa miji yoye, nchi zote na mataifa yote ya kuwa watu wafikilie toba na kuwa watu wakigeuka kuacha njia zao mbaya Rehema za Mungu zitakuwa juu ya watu hao ona 


2Nyakati 7:13-14 “Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.” Kumbe basi yanapotokea majanga ya aina mbalimbali, na matukio yenye kuua watu wengi na matukio mengone ya asili yanayodhuru wanadamu na kuumiza wengi haimaanishi tu kuwa watu wale wanaweza kuwa waovu kuliko wale wanaobaki salama lakini kwa Mungu wakati wote matukio hayo yanakuwa ni wito wa toba kwa watu wote wapate kumgeukia Mungu ona 


Luka 13:1-5 “Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao. Akawajibu akawaambia, Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.” 


Kwahiyo hata yanapotokea majanga katika upande wa Mungu inabaki vilevile Mungu hafurahii kufa kwa wenye dhambi na angepeda wafikie toba lakini ni wazi kwetu kuwa yanapotokea majanga na kuchukua watu wengi, sisi tunaosalia hatuna budi kukaa katika toba na kuacha njia mbaya tukikumbuka kuwa wale walioangamia sio kuwa walikuwa wabaya kuliko sisi.                            

Heri wafu wafao katika Bwana !

Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.”

Kifo ni jambo la kuhuzunisha sana lakini ni tamko la Mungu, kwa hiyo Mungu hawezi kuwa kinyume na neno lake kwa sababu hiyo kifo kitamchukua mtu awaye yote mwema au muovu, kwa wakati wake ambao Mungu ameukusudia chini ya Mbingu, Yesu alipokuwa duniani alidhihirisha kuwa anahuzunishwa na kufa mtu tena hata wale waliokuwa rafiki zake ona Yohana 11:35 “Yesu akalia machozi.” Yesu alilia kwa sababu alihuzunishwa na kifo cha mtu wa karibu na rafiki yake yaani maana yake anahuzunishwa na kila mtu anayemuamini na anayeishi maisha ya haki bila kujali mtu huyo amekufa katika umri wa namna gani. Lakini Maandiko yanaeleza kuwa Heri wafu wafao katika Bwana yaani bila kujali umri au miaka lakini kama mtu huyo amekufa akiwa na imani katima Mungu akiamini kuwa yesu ni Bwana mtu huyo ana Baraka kubwa sana na maandiko yanaonyesha kuwa anapata pumziko baada ya taabu

Kwa sili andiko hilo ni matokeo ya maonyo kwa watu waovu ambao maandiko yanaonyesha kuwa wao wanapokufa hawatakuwa na nafasi ya kupumzika na badala yake watapata taabu sana Ufunuo 14:11 “Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.”


Maandiko hayo yanaonyesha kwa asili wale watakaokufa wakati wa dhiki kuu, na tofauti yake kati ya wale watakaokufa kwa imani na wale watakaokuwa wamemuabudu mpinga kristo, Lakini maandiko hayo kuwa katika muktadha wa nyakati za dhiki kuu, hayaachi uole ukweli ulio wazi wa hata sasa kwamba wale wanaomuamini Yesu watapata raha na wale wasiomuamini watapata taabu sana kwani hayo ni matokeo yanayotokea haraka sana mara mtu anapokufa na aina ya maisha aliyoishi huamua hatima ya maisha yake ya umilele mara moja baada ya kufa ona Waebrania 9:27 “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;” Maandiko ynaonyesha wazi kuwa mara baada ya kufa hukumu hujitokeza pale pale kwa aidha kwenda katika raha au kwenda katika mateso mtu aliyemuamini Bwana Yesu anasamehewa na kuwanywa kuwa kiumbe kipya 2Wakoritho 5:17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.” Watu hawa ambao neema ya Mungu imefunuliwa kwao watapata raha nafsini mwao kama maandiko yasemavyo Mathayo 11:28-29. Kwa hiyo anapokufa mtu mcha Mungu Mungu hufurahia anahuzunika anapoona wale walioko duniani wanalia na wanahuzunika na huhuzunika pamoja nao lakini mtu wa Mungu anapokufa kuna faidha kubwa sana na Mungu hufurahia mauti yake maandiko yanatuambia ina thamani kama nini mauti ya wacha Mungu wake ona Zaburi 116:15 “Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake.” Haijalishi mtu wa Mungu atakufa katika mazingira ya aijna gani vyovyote vile kama Mungu ameruhusu mauti hiyo ina thamani kubwa sana mbele za Mungu aliyekuwa Askofu wa Antiokia aliuawa wakati wa mateso ya Decian askofu huyu ambaye katika historia ya kanisa aliitwa Babylas alikufa akiwa anaimba zaburi hii ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake!, Mtume Paulo aliungana na wazo kama hili kuhusu mauti ya mtu wa Mungu yeye alihesabu hivi kwake yaani kwa mtu kama yeye kuishi ni Kristo na kufa ni faida ona 


Wafilipi 1:21-24 21.Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. Ila ikiwa kuishi katika mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; basi nitakalolichagua silitambui. Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana; bali kudumu katika mwili kwahitajiwa zaidi kwa ajili yenu” kumbe basi kufa katika imani kwa mtu wa Mungu na kwa watu wema ni busara ya Mungu ambaye anakwenda kuwapumzisha na kukaa pamoja na wao, bila kujali ni mazingira gani anakuchukua nani katika umri gani anakuchukua kwa msingi huo kwa uelewa mwembamba kifo ni kupoteza katika akili za kibinadamu na hasa anapokufa mtu mwema lakini kwa uelewa mpana kifo cha mtu mwema kina thamani kubwa sana kwa Mungu, Mara kadhaa wakati mwingine nimeshangazwa na Kocha wa mpira wa miguu anaweza kumtoa mtu ambaye amefunga magoli mengi siku hiyo au mwenye uchu wa kufunga zaidi, na ukatamani aendelee kucheza kwa vile unakuwa na matumaini naye lakini unashangaa kocha anamtoa! Unaweza kumtukana au kumlaumu lakini kwa nini anatolewa kocha ndiye anayejua Katika Biblia kama kuna mtu binafsi nisingelipenda Mungu amchukue Mapema ni Stefano mimi nahizi kuwa angakuwa muhubiri mkubwa na alikuwa ni mtu muhimu, mitume walimtegemea sana na alikuwa na uwezo wa juu sana kulitetea kanisa lakini Mungu kama Mungu aliruhusu Stefano auawe kwa kupigwa mawe na kuwa mtu wa kwanza kuifia Imani, hivyo wakati mwingine Mungu hufanya mambo kama apendavyo yeye na hata hivyo wanatheolojia wanajua faida ya kifo cha Stefano lakini pia tunaijua Furaha ya Yesu aliyesimama kumpokea Stefano!

Je mtu akifa ni kweli kuwa siku yake imefika?

Tumewasikia watu mara kadhaa wakisema mara baada ya mtu kufa kuwa siku yake imefika, au amemaliza kazi iliyokusudiwa au siku yako ikifika bwana hakuna cha kuzia na kadhalika na kadhalika je Mungu amekusudia mwanadamu awe na wakati Fulani muafaka wa kuishi? Je kuna uwezekano wa siku kufupizwa au kuongezwa na nini faida zake na makusudi yake? Maandiko yanatufundisha wazi kuwa kwaajili ya dhambi umri wa kuishi mwanadamu umefupizwa ona Mwanzo 6:1-3 “Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.              


Mwanzoni wanadamu waliweza kuishi hata karne 9 yaani miaka mia tisa na kitu na mwanadamu aliyepata kuishi miaka mingi zaidi aliitwa Methusela yeye aliishi miaka 969 katika rekodi za Biblia ona Mwanzo 5:27 “Siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa.” Kutokana na kuongezeka kwa maasi duniani Mungu aliipunguza miaka ya kuishi mwanadamu na kuwa 120 kama tuonavyo katika maandiko, hivyo 120 ndio kiwango cha wastani wa juu zaidi ambao mwanadamu anaweza kuishi, Wakati wana wa Israel wakiwa Jangwani kutokana na kuasi kwao mara kwa mara Mungu aliwapunguzia wao wana wa Israel Miaka ya kuishi hususani wale walikuwa jangwani wakati wa Musa na miaka yao ikakadiriwa kuwa kati ya 70-80 ona Zaburi 90:10 “Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara.” Musa aliyasema maneno hayo wakati wa hukumu ya wana wa Israel ambao walikuwa wanakufa jangwani kwa sababu ya kutokumuamini Mungu, lakini kibiblia swala la msingi linabakia kuwa wastani wa mwanadamu kuishi ni kati ya miaka “70-120” hata hivyo hii haimaanishi kuwa ni lazima mwanadamu afiikishe miaka hiyo au kwamba anayekufa chini ya umri huo ni muovu hapana hata kidogo bado maisha ya mwanadamu yanabaki kuwa katika mipaka aliyoiweka Mungu! Kama itafikiriwa kuwa mtu akifa chini ya umri huo amekufa kijana basin i vema kuyafikiri maisha ya Yesu ambaye alipokuwa duniani aliishi miaka 33 tu, au kufikiri maisha ya Nabii Yohana mbatizaji ambaye aliishi miaka 30 tu na akauaawa! Ni Mungu tu ndiye anayejua kwanini na lini kifo kitokee kwa mtu kwa sababu zake mwenyewe, siku za mwanadamu za kuishi kwa ujumla sio nyingi kama hata kama mtu ataishi 120 bado ni siku zenye kupita haraka mno. Kwa mujibu wa maandiko 

Ayubu 14:1-2 “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe” mwandishi mwingine wa Biblia anayafananisha maisha ya mwanadamu kama vile maua, maua na majani ndio mfano wa vitu vyenye muda mfuoi sana wa kuishi, ni kama wanasema muda tuliopewa ni mdogo sana ona 

Zaburi 103:15 “Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo.” Pia maisha ya mwanadamu yanafananishwa na kivuli yaani kitu kinachopita na kutoweka kwa haraka sana Zaburi 144:4 “Binadamu amefanana na ubatili, Siku zake ni kama kivuli kipitacho.” 

Katika namna ya kibinadamu wengi tunaweza kufikiri kuwa maisha ya duniani ni matamu sana lakini kwa Mungu katika uwepo wake ndio kuzuri zaidi, Mungu amepangilia na kuweka mipaka katika maisha ya mwanadamu kwamba ukifika wakati huo aliouweka mwanadamu ataondoka tu kwa sababu siku zake zimeamriwa zimeratibiwa ziko programed kwamba huyu zitakuwa hizi tu 


Ayubu 14:5 “Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe, Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;kwa hiyo iko wazi kuwa Mungu ameweka mpaka katika maisha yetu ambao huo hatuwezi kuuvuka iwe tuna pesa kiasi gani, wema kiasi gani na kadhalika aidha pia Mungu huweza kuitimiza ile iliyokusudiwa au kuipunguza maika iliyokusudiwa kwa wanadamu kwa sababu zake na kanuni zake mfano 


Kutoka 23:25-26 “Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.” Aidha Mungu anaweza kuhakikisha kuwa miaka iliyokusudiwa kwa mtu inatimizwa au anaweza kuiongeza lakini pia anaweza kuipunguza kutokana na kanuni mbalimbali za maisha na neno lake mfano Mithali 10:27 “Kumcha Bwana kwaongeza siku za mtu; Bali miaka yao wasio haki itapunguzwa.         


Kila mwanadamu anatamani sana kuishi muda mrefu sana lakini wakati mwingine Mungu hutuepusha na mambo kadhaa na dhiki au mambo mabaya ambayo yeye hangependa ukumbane nayo Hezekia alikuwa moja ya wafalme wazuri ambaye Mungu alitaka kumchukua mapema lakini aliomba Mungu amuongezee muda wa kuishi na Mungu alimuongezea muda wa miaka 15 2Wafalme 20:1-6 “Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana akasema,Nakusihi, Bwana, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la Bwana likamjia, kusema, Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana. Tena, nitazizidisha siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano, nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu.” 


Hata hivyo jambo la kushangaza ni kuwa baada ya miaka hiyo ya nyongeza Hezekia alipata mtoto na ambaye aliwaongoza watu kufanya mambo mabaya sana na kufanya machukizo mabaya zaidi ambayo hata baba yake angalikuwa hai asingeliweza kuyavumilia mauozo hayo ona 2Wafalme 21:9 “Walakini hawakusikia; naye Manase akawakosesha wafanye mabaya, kuliko mataifa Bwana aliowaharibu mbele za wana wa Israeli.” 

Ni kama kusema afadhali Hezekia angelikubali kwenda kwa bwana wakati wake ulipofika kuliko miaka aliyoongezwa. Wakati mwingine Mungu katika hekima yake hufanya mambo kwa manufaa makubwa sana anayoyajua mwenyewe kwaajili ya hayo ni vigumu kumuuliza Mungu kwanini, kwanini hili litokee, lakini tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo na kutokumkufuru Mungu linapofanyika tukio lenmye kushangaza tuendelee kumuamini yeye katika njia zake zote na tusizitegemee akili zetu wenyewe 

Mithali 3:5-6 “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.” Wakati mwingine Mungu anaweza kumchukua mtu mwema akapumzike nyumbani kwa kusudi la kumuepusha na machukizo ya aina Fulani bila kujali njia itakayotumika kwa kuondoka kwake, 


Isaya 57:1 “Mwenye haki hupotea, wala hakuna atiaye hayo moyoni; na watu watauwa huondolewa, wala hakuna afikiriye ya kuwa mwenye haki ameondolewa asipatikane na mabaya.” Mungu anaweza kumchukua mtu ili kumuepusha na mabaya au maumivu makali au ulemavu, au kupooza na maswala mengine mengi,Jambo kubwa la msingi ni kila mmoja kuwa tayari kwa kifo wakati wowote tangu siku unapozaliwa Hata hivyo Yesu Ndiye mwenye funguo yaani mamlaka na kifo na hivyo hutaweza kuondoka mpaka Mungu ameruhusu Shetania anaweza kutujaribu kwa kiwangochochote kile lakini hana ruhusa kuondoa uhai wetu mpaka Mungu mwenyewe afanye hivyo 


Ayubu 2:6 “Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini tunza tu uhai wake” Ufunuo 1:17-18 “Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.”        

Adui wa mwishio atakayeangamizwa ni kifo:

1Wakoritho 15:26  Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mautiHatimaye Yesu Kristo ambaye ana mamlaka dhidi ya kifo na mauti na ambaye alionja mauti ya msalabani na kuishinda kwa kufufuka siku ya tatu mwisho wa dahari atambatilisha adui huyu ambaye amekuwa akisumbua kili zetu na kutuchukulia wapendwa wetu na kutuondolea tumaini duniani na kutufanya tuione dunia kuwa haina maana na ni batili na kutukatisha tamaa na kutufanya tuishi kwa hofu,  habari njema ni kuwa Mungu ataibatilisha mauti yaani kifo na hakitakuwepo tena mjadala wake utafungwa na Mungu mwenyewe kwa kutupa uzima wa milele na kujibu maswali yote ya msingi kuhusu Kifo, kwa sasa kifo ni siri ya ajabu, na Mungu ndiye aijuaye.

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!


Ijumaa, 5 Machi 2021

Kumbuka aliyokufanya Amaleki !


Kumbukumbu 25:17-19 Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri; jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu. Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha Bwana, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.”


Utangulizi:

Moja ya matukio mabaya sana ambayo Israel walitakiwa kuyakumbuka Daima ni pamoja na ukatili mkubwa waliofanyiwa na wana wa amaleki (Amaleki). Musa analikumbuka sana tukio hili baya na la kinyama na anawaandikia Israel na kumkumbusha Joshua kutokulisahau tukio hili baya na la kinyama  lililopata kufanywa na Wamaleki!. Wana wa Israel walikuwa wamefanyiwa mambo ya kikatili sana katika nchi ya Misri, waliteswa na kutumikishwa katika utumwa mkubwa na mzito kwa muda wa zaidi ya miaka 400, waliugua na kulia na kibinadamu haingekuwa rahisi mtu awaye yote kuwaondoa katika utumwa huo mzito isipokuwa tu pale ambapo Mungu alikuja kuingilia kati unawezakuona.


Kutoka 3;7-10 BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa. Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.


Huu ndio ulikuwa mpango wa Mungu na mapenzi kamili ya Mungu, kwamba awakomboe wana wa Israel na kuwafikisha katika nchi ya mkanaani nchi iliyojawa maziwa na asali, aweze kuwafariji na kuwafundisha mapenzi yake ili kwamba kupitia wao jamaa zote za dunia zipate kubarikiwa kupitia mwana wake mpendwa Yesu Kristo ambaye kinabii angetokea Israel na kuwa ishara ya kuaminiwa duniani kote, kwa hiyo Taifa hili lilikuwa limebeba mpango na mapenzi kamili ya Mungu, Mungu aliwapitisha katika jangwa hili zito na la kutisha apate kuwafundisha imani na kumtegemea yeye ili wawe watu wake Lakini wakiwa njiani pamoja na vikwazo vingi walivyokuwa wamekutana navyo walitokewa kabila hili la jangwani waliojulikana kama Amaleki watu hawa walifanya vita na Israel, Kitabu cha kutoka kimetuficha sababu ya vita hii kinaeleza tu walivyotokea na kupigana na Israel na Yoshua akatumwa kuwapiga kwa msaada wa maombi ya Musa unawezakuona katika

Aliyoyafanya Amaleki:-

Kutoka 17:8-14 Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu. Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena

Mungu anakasirishwa sana na tendo la Amaleki kushindana na Israel na akaagiza kuwa Musa ni lazima alihubiri jambo hili kwa Yoshua na  wana wa Israel walikumbuke tukio hili milele, aliambiwa aliweke tukio hili katika kitabu cha kumbukumbu ukumbusho kuwa kizazi cha Amaleki kitashughulikiwa siku zote mpaka kifutike kabisa duniani, sababu kubwa ni kuwa kilikuwa kizazi cha watu katili sana hawakuwa na huruma hawakuwaonea huruma watu waliotoka katika mateso kwa muda mrefu sana waliotakiwa kuhurumiwa waliostahili kuhurumiwa  na waliokuwa wanahitaji msaada, watu waliokuwa wanahitaji msaada na huruma na huduma na kutiwa moyo na msaada wa kibinadamu ambao Mungu alikuwa amefungua mlango kuwatoa katika mateso amaleki walikosa utu kabisa hawakuwahurumia watu ambao walistahili kibinadamu kuhurumiwa, hawakuwahurumia wanyonge, hawakuwahurumia watu waliokuwa wamechoka na kuzimia wala hawakumuhofu Mungu na kwa tukio hili Musa analiweka vizuri katika kitabu cha kumbukumbu la Torati kwamba Amaleki kwamba Israel walikuwa wamewaacha nyuma watu wanyonge wagonjwa na wenye uhitaji wa namna mbalimbali ili labda huenda wapate huduma za kitabibu, maji na huduma nyinginezo lakini Amaleki aliwapiga bila kujali ilihali wakijua kuwa ni watu wanaohitaji huduma na msaada wa kibinadamu ona.

Kumbukumbu 25:18. jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu

 Tukio hili halikuwa tukio lenye kuheshimu ubinadamu, watu wanapokuwa vitani sharia za kivita zinakataza kushambulia maeneo ya kiraia, lakini mbaya zaidi kushambulia hospitali au sehemu zinazotoa huduma za kijamii, wanawake watoto na raia, lakini sio hivyo tu wakati wa vita taifa lile linalopigana linapaswa kuhakikisha kuwa wanajali utu na ndio maana utaweza kuona baadhi ya mataifa wanapokuwa na vita na wananchi wakapata shida ya njaa huwa wanatoa msaada wa chakula na madawa, Katika ulimwengu huu ulio haribika ni dhambi kubwa sana kumuongezea mtu tatizo ilihali yeye mwenyewe ana tatizo au anatoka katika matataizo, kwaajili ya shida zetu, wamekuwepo watu katika jamii ambao matendo yao ni kama waamaleki, badala ya kuwasaidia watu wanyonge wenyewe wamekuwa kikwazo kikubwa sana  kwa watu hao wanyonge, mtu ni mgonjwa anahitaji msaada ana matatizo wanaweza kuwako hata wahubiri au watoa huduma kama hospitalini ambao watadai fedha kutokana na huduma wanayoitoa, mtu anaweza kuwa mlemavu lakini watu wakamuhuzunisha na kumjeruhi roho yake kwa kumuongezea masimango, mtu anaweza kuwa mjamzito akakutana na huduma na maneno ya kukatisha tamaa huko leba wanakojifungulia, mtu anaweza kuwa yatima watu wakawatumia yatima hao kwa manufaa yao, mtu anaweza kuwa mlemavu, kipofu au mwenye ualbino na watu wakawatumia hao kwa manufaa yao wenyewe, mtu anaweza kuwa mjane  anahitaji msaada lakini ujane wake ukatumika kwa manufaa ya wengine, ukatili wa kijinsia, uonevu kwa wanyonge kutokujali, kukosa utu na lugha mbovu sehemu za huduma ni maswala ambayo yanaweza kufanywa na watu ambao wanaweka kwazo kama walivyo Amaleki ambao kwa makusudi kabisa walishindana na kusudi la Mungu la kuwapeleka watu katika nchi ya mkanaani lakini pia kwa kuwaonea wanyinge, jambo hili linahifadhiwa katika kumbukumbu za Mungu na ndipo Mungu hujitakia kisasi, na kuwa na vita na jamii ya watu hao milele, dhuluma na uonevu unawekwa katika kumbukumbu za Mungu na ni lazima vilipiwe ni kwaajili ya haya miaka mingi baadaye Mungu alimtaka mfalme Sauli kuwafutilia mbali Amaleki kwa sababu ya uovu wao lakini hata hivyo Mfalme Sauli alimuudhi sana Mungu kwa sababu alishindwa kuyatii maneno ya Musa mtumishi wake na agizo la Mungu na mapenzi yake ya kutaka kujilipizia kisasi dhidi ya Amaleki

Muhukumu wa ulimwengu lazima atende haki;-

1Samuel 15:1-19 Wakati huo Samweli akamwambia Sauli, Bwana alinipeleka nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na maneno ya Bwana. Bwana wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda. Ndipo Sauli akawaita watu, akawahesabu huko Telemu, askari waliopanda farasi mia mbili elfu, na watu wa Yuda kumi elfu.  Sauli akaufikilia mji wa Amaleki, akauvizia bondeni. Sauli akawaambia Wakeni, Haya! Enendeni zenu, mkashuke ili kujitenga na Waamaleki, nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao; maana mliwatendea wana wa Israeli mema, walipopanda kutoka Misri. Basi hao Wakeni wakaondoka, wakajitenga na Waamaleki. Sauli akawapiga Waamaleki, toka Havila uendapo Shuri, unaokabili Misri. Akamkamata Agagi, mfalme wa Waamaleki, yu hai, akawaangamiza hao watu wote kwa upanga. Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa. Ndipo neno la Bwana likamjia Samweli, kusema, Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia Bwana usiku kucha. Samweli akaondoka asubuhi na mapema ili aonane na Sauli; Samweli akaambiwa ya kwamba, Sauli alifika Karmeli, na tazama, akajisimamishia ukumbusho, akageuka, akapita, akatelemkia Gilgali. Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na Bwana, nimeitimiza amri ya Bwana. Samweli akasema, Maana yake nini, basi, hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu, na huu mlio wa ng'ombe ninaousikia? Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa. Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia neno aliloniambia Bwana usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema. Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha kabila za Israeli? Naye Bwana akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli. Kisha Bwana akakutuma safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hata watakapoangamia. Mbona, basi, hukuitii sauti ya Bwana, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana?

Onyo kwa watu wenye dhukluma:-

Kuwatumiwa wanyonge kwa manufaa yakio mwenyewe ni dhambi kubwa sana, Mungu anachukizwa na udhalimu wa kila namna maandiko yanasema wala wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu, Kitendo cha waameleki kuwazuia Israel wasiende kulitimiza kusudl la Mungu kilikuwa ni kitendo cha kutokujali mpangio wa Mungu, laziki tendo la kuwaonea watu wanyonge na kuwatendea uahlifu liliwekwa katika kumbukumbu za Mungu, lakini tendo la kuwahurumia amaleki na kutiokuangamiza au kumlipizia Bwana kisasi sawasawa na neno lake kulikofanywa na Sauli kulimuudhi sana Mungu, Maana yake ni kuwa Mungu hatakubali mtu awaye yote aliye mnyonge na mnyenyekevu aonewe kupita kawaida, ni lazima ataliweka jambo hilo katika kumbukumbu na kujitakia kisasi milele,

Warumi 12:19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.”

Mungu alitunza uovu wa wana wa Amekeli na alikusudia kujilipizia kisasi, na ole wake mtu yule ambaye atawaacha waameleki, Dhambi yao ilikuwa kubwa , walikuwa waonevu, walikuwa wenye dhuluma, walikuwa wasiojali utu, waliwaonea wanyinge, walishindana na kusudi la Mungu, kuna mambo unaweza kuyafanya kuna ukatili unaweza kuufanya lakini sio kwa watu wanyonge ambao maisha yao yalikuwa ya taabu na Mungu aliwasaidia dhidi ya wamisri,  watu waliohitaji huruma kufarijiwa kuinuliwa na kutiwa moyo, Mungu asingeliweza kupuuzia hata kidogo, Lazima atawangalia wanyonge

Isaya 66:2 Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.”

Mungu ni lazima atatenda haki Mwanzo 18:25b ………. "Hasha: Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?

Mungu atakulipa endapo unaonewa kwa haki na kudhukumiwa hebu mlilie Mungu lalama mbele zake omba na kuliitia jina lake na kisha utaona ukuu wa Mungu katika maisha yako, wale wanaoowatumia wanyionge kwa manufaa yao tubu na achana na unevu wa kila namna Mungu asije akakuhukumu!

Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima

Ijumaa, 12 Februari 2021

Ni Afadhali kukaa katika pembe ya darini!

Mithali 25:24, “Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.” Mithali 21:9 “Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.”


Utangulizi:

Mithali ni mojawapo ya kitabu muhimu katika vitabu vya mashairi ya kiebrania, kama wengi wetu tunavyofahamu kuwa katika tamaduni nyingi kwenye misemo na mashairi au nyimbo, watunzi wengi huifadhi maneno ya maana na yenye uadilifu fulani kwa kusudi la kupeleka mafunzo fulani katika jamii, kama Jinsi ambavyo tumeona hapa katika kitabu cha Mithali, hapo juu, Katika kifungu au vifungu hivyo, Walengwa wa kifungu hiki hasa wanaweza kuwa wanaume na wanawake pia! Na hasa vifungu vinaweza kuwa na kusudi la kutoa ushauri au kuwafundisha wanaume ni mwanamke wa aina gani anaweza kumuoa na wanawake jinsi gani na namna wanaweza kutumia ndimi zao na kutunza hisia zao “TEMPER” zinazoweza kuondoa amani na utulivu katika nyumba na sehemu nyinginezo, Tunapoendelea kujifunza somo hili AFADHALI KAUKAA KATIKA PEMBE YA DARINI, Utagundua kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kila mwanamke kuchunga kauli zake katika mahusiano ya aina yoyote ile! Lakini zaidi sana uhusiano wake katika ndoa. Lakini vilevile kuna maonyo makubwa sana kwa wanaume kuwa kama kuna kitu ukikikosea wakati unakusudia kuoa kuna jambo utakutana nalo. Kwa ufupi matumizi ya ulimi na udhbiti wa hisia zetu una faida na ama hasara kubwa sana katika swala zima la mahusiano. tutajifunza somo hili kwa kuzngatia vipengele kadhaa vifuatacyo:- 

·         Maana ya Pembe ya darini

·         Afadhali kukaa katika Pembe ya darini

·         Mwanamke mgomvi!

·         Umuhimu wa kutunza amani ya moyo!


Maana ya pembe ya darini

Katika tamaduni za ujenzi wa kale hasa katika jamii ya waarabu na wayahudi, walijenga nyumba za ghorofa ambazo juu zilikuwa na dari au sehemu maalumu za kupumzikia, ambayo ilijengwa kwa kusawazishwa juu, Pwani ya Afrika mashariki watakuwa na ufahamu kuhusu aina hii ya ujenzi kwa sababu waarabu walipokuja mapema sana katika miji ya Kilwa, Malindi, Mombasa, Zanzibar, Mafia na Sofala waliacha urithi wa aina hizo za majengo na ambazo wenyeji pia waliigiza, Katika ujenzi huo juu waliweka dari na dari iliweza kuwekwa aina fulani ya lami  na hivyo kupata eneo zuri na salama la kupumzikia, hata hivyo wakati muafaka wa kukaa katika Pembe ya dari ulikuwa ni wakati wa hari yaani wakati wa joto, wakati wa tufani, pepo kali na mvua na radi eneo hilo halingeweza kufaa kwa kupumzikia.

Afadhali kukaa katika Pembe ya Darini

Mwandishi wa kitabu hiki cha Hekima anaona ni heri kukaa katika Pembe ya dari kuliko kukaa na mwanamke mwenye kelele, Yeye mtazamo wake ni kuwa pale kwenye pembe ya darini pana afadhali kukaa wakati wote ikiwa ni pamoja na wakati wa tufani na joto kali na hata wakati wa mvua na radi kuliko kukaa katika nyumba pana na mwanamke mwenye kelele, Nyumba pana  inayozungumzwa hapa ni zile ambazo ni kubwa na zina vyumba vingi na familia kubwa  nyumba ya jamii, nyumba ambayo familia kubwa wanaweza kukaa na kushirikiana nyumba ambayo ina mume mke na watoto yeye anaiona nyumba hiyo kuwa ni nyumba isiyofaa kabisa kama atakuwepo mwanamke mwenye kelele, yaani mwanamke mtawala, mkaidi, kimbelembele asiye na uvumilivu mdadisi, mchunguzi mwenye kushuku, mchoyo, asiye na ushirikiano katika tendo la ndoa mgomvi, mwenye luigha mbaya mwenye matumizi mabaya ya ulimi, kwa mwandishi wa kitabu cha Mithali Mfalme solomoni anaona ni Kheri kukaa katika pemba ya dari kuliko kukaa na aina hii ya mwanamke katika jumba la kifahari  au wakati mwingine ni afhadhali uende nyikani au jangwani kuliko kukaa na mwanamke huyo mgomvui ona

Mithali 21:19 “Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.
Mwandishi pia anaona afadhali kula ukoko wa wali au ukoko wa mkate kuliko kwenye nyumba yenye karamu nyingi lakini haina amani ona

Mithali 17:1 “Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.” aidha katiika

Mithali 19: 13 Biblia inasema hivi “Mwana mpumbavu ni msiba kwa babaye; Na ugomvi wa mke kama kutona-tona daima.”

Mwandishi anazungumzia hapo ugomvi wa mke yaani mwanamke mwenye kelele ni kama kutona tona neno hilo kutona tona katika biblia ya kiingereza ya The Amplified Bible  linatumika neno “continual dripping” hali hii ni ngumu kuielezea kwa kizazi cha leo ambao wanaishi kwenye nyumba nzuri zilizosakafiwa vema kila mahali lakini wale wenye umri wa miaka kadhaa na waliowahi kuishi vijijini wanafahamu taabu ya nyumba inayovuja hasa zile za nyasi au za makuti, unafahamu karaha ya kuishi katika nyumba ambayo hapa panavuja na pale panavuja na kadhalika ile taabu ya kuishi kwenye nyumba inayovuja daima ndio inaitwa kutona tona kwa hiyo kimsingi Sulemani anaonyesha yale maudhi ya kukaa katika nyumba inayovuja ile hali ya kuishi kwa mashaka na wasiwasi katika nyumba inayovuja inalingana kabisa na kuishi na mwanamke mgomvi

Mwanamke mgomvi ni wa namna gani?

Mithali hii ina maswala ya msingi ya kuzingatia sana ona mwanamume aliyeoa hapa anatamani kukaa katika Pembe ya darini au anaona ni afhadhali kukaa katika pembe ya darini juu npeke yake  kuliko kukaa na mwanamke mwenye kelele au mgomvi Mithali inaonekana kuwa yenye kutaka kuchukua ufahamu wetu wote uelekee kwenye kitu kigeni na cha muhimu kwetu kujifunza yaani iweje jamaa aone kuwa kwenye kona ya darini peke yake ni pazuri kuliko kukaa na mwanamke mwenye kelele mgomvi, kuna tatizo kukaa katika kona ya darini ni maisha gani je ni kweli panaweza kuwa na faraja? Bila shaka ni lugha ya kukuza jambo ili kutoa umuhimu kwenye kitu mwandishi anataka kukiwasilisha na hiki si kingine ni mwanamke mgomvi ni mwanamke mwenye kelelel huyu ni mwanamke wa namna gani? Biblia ya kiebrania inatumia neno “MADON” inamaanisha mtu aliyejawa na uchungu Biblia ya kiingereza inatumia neno strife dissension yaani muasi, mwenye uchungu na asiyekubaliana au mwenye mijadala na mpinzani unaweza kuona  kwa hiyo unapokuwa naye  wakati wote kunakuwa na mafuriko ya ugomvi

Mithali 17:14 “Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji; Basi acheni ugomvi kabla haujafurika.
au kunapotokea ugomvi na kutokuelewana yeye hamalizi kwa haraka haachilii hawezi kuacha kubwatuka na kusema na kusengenya  yuko kwaajili ya mashindano yuko kwaajili ya kulipiza kisasi ona

Mithali 18:19 “Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuliko mji wa nguvu; Na mashindano ni kama mapingo ya ngome.”
yaani ni aina ya mwanamke ambaye wakati wote anakwaza au anakuwekea vikwazo na hii inaambatana na ubovu wa moyo alionao na hisia mbaya, acha ya kuwa atakukwaza kiasi ambacho hutakuwa na hamu ya kushirikiana naye hata tendo la ndoa, atajificha katika silaha ya kulia na kujibanza kwenye kuamua kufungasha au kukuletea aibu miongoni mwa watu wanaokuheshimu, atataka akuweke vikao akupeleke kwa wachungaji au wazee wa kanisa au kwa wakwe kule ukasutwe mpaka aonekane yeye ndio mshindi,  ni aina ya mwanamke mwenye wivu mkali sana akikuona umesimama na mwanamke tu hata bila kujali ni wa rika gani na wa aina gani na mnazungumza nini mtajikuta mnaingia katika ugomvi mkubwa , huyu kila kitu ni ugomvi hii ni dhambi mbaya sana ni katika aina hii ya mwanamke ndio inaonekana kuwa ni afadhali kukaa katika pembe ya darini na kuvumilia dhuruba na upepo na upweke kuliko jumba kubwa la karamu na sherehe lakini na aina ya mwanamke kama huyu, aina hii ya mwanamke kwa mujibu wa Sulemani ni msiba ukikaa naye, badala ya kuwa mpole na mwenye kujinyenyekeza na mtii kwa mumewe kama maandiko yanavyoelekeza huyu ni mwanamke mtawala, mwenye hasiram asiye na utulivu hawezi kuzuia hisia zake  amejaa chuki na wakati wowote roho yake iko tayari kwa majibu ya hovyo na kupambana na mumewe, ukiwa na aina hiyo ya mwanamke ni heri kukaa katika pembe ya dari, eneo ambalo utatulia kimyaa na utajisikilizia moyo wako kuliko kuwa na misiba kila wakati na majanga kila wakati!

Mungu alimkusudia mwanamke awe msaada mkubwa wa mumewe MSAIDIZI Neno Msaidizi limetumika pia kuelezea ukaribu wetu na msaada tunaoupata kutoka kwa Mungu ROHO MTAKATIFU  yeye hutusaidia, hujaziliza madhaifu yetu, hutushauri hutuombea na kuleta msaada mwingi, kututeteta na kututia nguvu,  kwa maana nyingine Mwanamke anatakiwa kuwa msaada Mkubwa kama alivyo Roho Mtakatifu katika maisha yetu, kama umeokoka unapojazwa Roho Mtakatifu unakuwa na ujasiri na unapokea nguvu ya ajabu na mambo mengi yanaonekana kurahisishwa hata ukipitia magumu kwa uwepo wa Roho Mtakatifu,  wanaume hawapaswi kufikia hatua ya kuamua kushinda ofisini, au kwenda kunywa kahawa na tangawizi mbali kama watakuwa na mwanamke mwenye kuvutia,  Mithali hii inatufunza kwamba Lugha na matumizi ya ulimi na udhibiti wa hisia kwa mwanamke ni jambo la maana sana mwanamke aliyepewa mume ni muhimu sana kwa mumewe, kwamba mumeo atakuelewa au hata kuelewa maneno yako ni ya muhimu sana na matendo yako pia wakati wote unapomkwaza mumeo na kuzungumza maneno ya kejeli na kumkatisha tamaa unamuharibu mumeo kabisa kabisa na kumbomoa mara 1000 kuliko mtu yeyote yule , sababu ya mtu yule kuona umuhimu wa kutulia katika pembe ya dari ni kwa sababu anajisikia kuumizwa, anajisikia vibaya anajisikia kuvnjika moyo, anakosa faraja ya kweli anaumizwa badala ya kupata faraja kutoka kwa mwanamke, kusema kweli amani katika nyumba na ndoa yoyote ile inaweza kupokea mabadiliko kama wanawake watajua nafasi zao, inawezekana ukawa unasoma hapa halafu ukasema mkuu wa wajenzi anasema tu huyu hajui aina ya mwanaume niliye naye! Angejua ! inawezekana kweli anakuudhi kweli ni kama hakufai lakini alikufaa mpaka mkaoana na kuchumbiana  najua kuwa kuna weza kuwa na maudhi ya hapa na pale lakini hapa Biblia inamtaka mwanamke  awe mtulivu, amtiii amtie moyo na awe na lugyha nzuri hii itamuondoa mumeo katika pembe ya dari, wengi waume zenu wako katika pembe ya dari, hawataki hata kuwasikiliza, wako tayari kusikiliza mpira na kuzungumza na wengine katika magroup ya mitandao ya kijamii wako tayari kuzungumza na wengine kwa lugha ya upole na ubembelezi lakini kwako wanasubiri kufyaua maneno kama risasi ili kujeruhiana, mimi nilikuwa nagombana sana na mke wangu mapaka wakati mwingine nikawa nimezoea maisha ya ugomvi, mpaka nikawa mchokozi nasubiri arushe neno moja tu nimtapikie mpaka anyauke ndio alinizoesha mwenyewe!, Lakini nataka nikuhakikishie mwanamke akibadilika akawa katika nafasi yake ya ulaini wa moyo, ulaini wa lugha ulaini wa ngozi ulaini wa sauti ulaini wa mapishi ulaini wa kujali ulaini wa kukupmkea ulaini wa kila kitu mwanamke akikaa katika uanawake kwelikweli Mwanaume atatoka gerezani, atatoka fgereji atatoka pangoni atatoka kazini atatoka kwenye mpira atatoka kanisani, atatioka kwenye jumuia atatoka kwenye simu na redio na television  ataondoka kwenye pembe ya dari na kuja kutulia na mkewe, haiwezekani nyumba iwe kama ina wanaume wawili ndani haiwezi kuwa nyumba yenye kufaa tafadhali wanawake kuweni wanawake kweli na sisi tutashuka darini na kuwasogelea!

Umuhimu wa kutunza amani ya moyo!

Mithali hii pia inatumika kama mafunzo kwa vijana hasa wale ambao hawajaoa inawakumbusha kuwa ni jambo baya sana kuwa peke yako, Upweke na kuwa mwenyewe ni jambo baya kimaandiko Biblia inasema si vema huyo mtu awe peke yake ona

Mwanzo 2;18 “BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”
ingawa sio vema mtu kuwa mpweke lakini ni mbaya zaidia kama utaona mwanamke mgomvi mwenye kelele, anayetajwa katika mithali hii, kwa hiyo mithali hii inakutaka ujiokoe mwenyewe kuoa mwanamke mgumu kunaweza kuleta huzuni kubwa zaidi kuliko unavyoweza kuwaza, usimkaribie kabisa mwanamke jeuri mwenye mijadala na asiyeweza kuzuia hisia zake, Kuna namna ambayo Mungu ameumba wanakwake na kuna namna neno la Mungu linavyomtarajia mwanamke awe Sulaimani ambaye amewahi kuwa na wanawake wengi aliowaoa anaandika mithali hiii akiwaonya wanaume kujihadhari na mwanamke wa aina hii, wanawake wengi wameharibu huduma za waume zao, maisha ya waume zao, kazi za waume zao heshima za waume zao kwa sababu ya tabia mbaya isiyokuwa ya kimaandiko

Mithali 12:4  Mwanamke mwema ni taji ya mumewe; Bali aaibishaye ni kama kuoza mifupani mwake.“

Mithali 14:1 “Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe”

Mithali 27:15-16  Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi, Na mwanamke mgomvi ni sawasawa; Atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo; Na mkono wake wa kuume hukuta mafuta.”

Mithali 30:21-23 “Kwa ajili ya mambo matatu nchi hutetemeka, Naam, kwa ajili ya manne haiwezi kuvumilia. Mtumwa apatapo kuwa mfalme; Mpumbavu ashibapo chakula;Mwanamke mwenye kuchukiza aolewapo; Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake.”
~
Mithali 31:10-12 “Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani. Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.”

Mfalme Sulemani anaelewa anachokiandika alikuwa na wake 700 na masuria 300,  anajua namna mwanamke mkorofi anavyokua anaonya vijana kuwa makini unapofika wakati wa kufabnya maamuzi ya kuoa siku moja ya majuto na hasira za mwanamke inaweza kukuokoa wewe unayetaka kuoa, Ndoa inaweza kuwa kaburi  na ukajuta na kutamani kutoka na kuwa single tena kuwa na mwanamke mkorofi ni msalaba mkubwa sana  mwanamke mgomvi, mwanamke mwenye kukosoa kila kitu hana jema, mwanamke anayependa kugombana anayependa kukupinga anayependa kushindana nawewe, asiyeridhika na kitu chochote, mwenye maswali ya kila aina, mwenye kukukumbusha makosa ya nyuma, mwenye kisasi asiyesamehe, mwanamke mwenye kumlaani mumewe, asiyetia moyo asiye na adabu, mwenye kiburi mtawala Biblia inatoa maonyo kwamba ni afadhali kukaa kwenye pembe ya dari, mwanamke yeyote utakayeoa na ukagundua kuwa hali yako ya kiroho inaharibika baada ya kumpata, hali yako ya kuomba na kuabudu na upendo unaondoka na kuanza kuwa katili mwanamke anayekufabnya ujute kwanini umeaoa ? huyo ndio mwanamke ambaye biblia inasema hafai, huyu ni mwanamke asiyeweza kuitawala roho yake  anayependa kugombana na kusema leo na mimi nimemkomesha ukizungumza naye anazungumza ukimweleza anakuja juu, sauti yake inapanda kwa kiasi ambacho hata walio nje wanasikia mnavyozozana au anaweza kuwa na kiburi mpaka ukatamani umpige , mwanmake asiyetosheka aliyekinyume na kila kitu, na kila tukio na kuzungumzia vibaya kila kitu, mgumu, hawapendi hata ndugu zako, wakati wote yeye ni kulaumu kila kitu Mwanamke wa namna hiyo Biblia inasema hakufai na kwa vyovyote vila atakupeleka kwenye pembe ya dari,  hawa ni wanawake watawala kama utakuwa umeoa mwanamke wa aina hii utakuwa umechelewa kujiokoa na kifo na hasara vinakuhusu na ndio maana Sulemani anaonya kuwa wanaweza kuionekana kuwa nadhifu na wazuri wakati wa uchumba lakini utakapoingia kwenye agano naye umekwisha hawa kutokana na utawala wao wanaweza kukufanya ukashindwa hata kumudu tendo la ndoa, Maisha yako ni ya muhimu sana jifunze kutokana na maonyo, mke gani anashinda kwenye TV daima , mke gani anashinda anachati tu, simu jmemnunulia wewe, vocha unaweka wewe na simu hiyohiyo na vocha hiyo hiyo inatumika kukutukana jiokoe na maumivu, jiokoe na viumbe wa aina hiyo, ogopa maumivu ya maisha, mwanagalie mama yake ni mwanamke wa namna gani, waulize waliooa , kuwaa mwangalifu na kwanini uishi miaka karibu 50 na mtu atakayeshinda anakuumiza tu tunza amani ya moyo wako!

Mwanamke wa Kikristo anapaswa kujifunza na kuishi kwa upendo, na anapaswa kujua namna ya kujinyenyekeza kwa mumewe anajua nafasi yake kimaandiko

1Wakoritho 11:8-9 “Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume.Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.
” Mwanaume hakuumbwa kwaajili ya mwanamke bali mwanamke kwaajili ya mwanaume hivyo mwanamke wa Kikristo anapaswa kujua wajibu wake anapaswa kuishi maisha ya kumpendeza mumewe ona

1Timotheo 2:13 “Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye
” Mungu alimuumba mwanaume kwaajili yake na wala sio kwaajili ya mwanamke hivyo mwanamke wa kikristo anapaswa kuwa anayejipendekeza nakazia tena anayejipendekeza kwa mumewe, ni lazima wakati wote ahakikishe anajiweka vizuri anajaa neema ili aweze kuwa mwenye mvuto na mwenye kumpendeza mumewe

Mithali 11:16 “ Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; Na watu wakali hushika mali siku zote.
“ mwanamke ni adabu bwana ! mwanamke unyenyekevu jifunze kutoka kwa Abigaili  anajua kubembeleza mpaka mwanaume shujaa mwenye hasira anayetaka kuua anakuwa mpole huu ndio uzuri ambao wanaume wa kweli wanautafuta

1Samuel 25:21-35
Basi Daudi alikuwa amesema, Hakika ni bure nilivyokuwa nikilinda nyikani yote aliyo nayo mtu huyu, asipotewe na kitu cho chote cha mali yake yote; naye amenilipa mabaya badala ya mema. Mungu naye awafanyie hivyo adui za Daudi, na kuzidi, nikimwachia katika wote walio wake hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi. Ndipo hapo Abigaili alipomwona Daudi, alifanya haraka kushuka juu ya punda wake, akamwangukia Daudi kifulifuli, akainama mpaka nchi. Akamwangukia miguuni pake, akasema, Juu yangu, bwana wangu, juu yangu mimi na uwe uovu; tafadhali mjakazi wako na anene masikioni mwako, nawe uyasikilize maneno ya mjakazi wako. Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma. Basi sasa, bwana wangu, aishivyo Bwana, na iishivyo nafsi yako, kwa kuwa Bwana amekuzuia usimwage damu, tena usijilipize kisasi mkono wako mwenyewe, basi sasa adui zako, na hao wamtakiao bwana wangu mabaya, wawe kama Nabali. Na sasa zawadi hii, mjakazi wako aliyomletea bwana wangu, na wapewe vijana wamfuatao bwana wangu. Nakuomba ulisamehe kosa lake mjakazi wako, kwa kuwa hakika Bwana atamfanyia bwana wangu nyumba iliyo imara, kwa sababu bwana wangu anavipiga vita vya Bwana; tena uovu hautaonekana ndani yako siku zako zote. Na hata ijapokuwa binadamu angeinuka akuwinde, na kuitafuta nafsi yako, hiyo nafsi ya bwana wangu itafungwa katika furushi ya uhai pamoja na Bwana, Mungu wako; na nafsi za adui zako ndizo atakazozitupa nje, kama kutoka kati ya teo.Tena itakuwa, hapo Bwana atakapokuwa amemtendea bwana wangu sawasawa na mema yote aliyoyanena juu yako, na kukutawaza juu ya Israeli; hili halitakuwa kwazo, wala chukizo la moyoni kwa bwana wangu, ama ya kuwa umemwaga damu bure, ama ya kuwa bwana wangu amejilipiza kisasi mwenyewe; tena hapo Bwana atakapokuwa amemtendea bwana wangu mema, ndipo umkumbuke mjakazi wako. Naye Daudi akamwambia Abigaili, Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye amekuleta hivi leo kunilaki; na ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe, uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu mwenyewe. Kwa kuwa ni kweli, aishivyo Bwana, Mungu wa Israeli, aliyenizuia nisikudhuru, kwamba hungefanya haraka kuja kunilaki, hakika huyu Nabali asingaliachiwa hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi. Basi Daudi akapokea mkononi mwake vitu vile alivyomletea; akamwambia, Haya! Kwea kwa amani kwenda nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimeukubali uso wako”. Wanawake wacha Mungu sio kuwa wanapendezwa na kufurahishwa na kila kitu kuhusu waume zao hapana wanawatii, wanawanyenyekea, wanawaheshimu wanatumia busara kuishi nao, hawashindani nao ndio biblia inavyoagiza

Waefeso5:22-24
Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo 

Tito 2:3-5  Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.
” Wanawake wacha Mungu sio wagomvi wala jeuri  wanajua kuutumia ulimi wao ona

Mithali 31:26 “Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake.” 1Petro 3:1-4 “Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu
.

Ni wajibu wa kila mzazi wa kikristo na mwenye kupenda uadilifu kumfunza mtoto wake wa kike nawa kiume namna anavyotakiwa kuwa kupitia Mithali za Suleimani kwenye mithali kuna hekina na maarifa na ujuzi utakaosaidia jamii katika maisha ya kawaida na ya kiroho, kila kijana ajifunze kuhusu mke mwema na kujua anapaswa kuoa mwanamke wa namna gani na kila mwanamke anapaswa kujivunza na kujikosoa au kumuiomba Mungu ambadilishe ili asimpeleke mumewe kwenye pembe ya dari kuna faida kubwa sana za kujifunza kupitia mithali za solomon

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima!

Ikawa Mwanzo wa Mwaka Mpya!

2Samuel 11:1-4 “Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Daudi akampeleka Yoabu, na watumishi wake pamoja naye, na Israeli wote; wakawaangamiza wana wa Amoni, wakauhusuru Raba. Lakini Daudi mwenyewe akakaa Yerusalemu. Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti? Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake.




Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa kifungu hiki cha maandiko kina jambo kubwa la msingi la kutufundisha ambalo mwandishi wa kifungu hiki alikuwa anakusyudia kukuileta kwetu! Wengi wetu tunafahamu sana habari ya anguko la Daudi katika zinaa, na tunafahamu madhara makubwa yaliyompata kutokana na dhambi hii, lakini vilevile tunaweza kukubaliana wazi kuwa Daudi alikuwa na udhaifu sawa na ule walionao wanaume wengine, kwamba aliona mwanamke mzuri anaoga akamtamani, na kuzini naye na wengi wameweza kumalumu Daudi kwa sababu mbalimbali hata ikiwa ni pamoja na kujenga Ghorofa lenye dari ya kutembelea na kusababisha kuona mke wa jirani yake ambaye alikuwa anaoga, tunaweza kuwa na sababu lukuki kuhusu anguko la Mfalme Daudi na sababu hizo zikawa na mashiko kadhaa, Lakini mwandishi wa kifungu hiki ana sababu mojawapo ya muhimu zaidi ambayo kimsingi ndio nataka tuiangalie kwa kina katika siku kama hii ya leo!

Ikawa Mwanzo wa Mwaka mpya!

Mwandishi anaanza kwa kueleza Habari ya anguko la Daudi akiwa na sababu nyingine tofauti mno Ikawa Mwanzo wa Mwaka Mpya! Wakati watokapo wafalme kwenda vitani!  Majira ya nchi katika mashariki ya kati yanafanana sana kwa kiwango kikubwa na majira ya Afrika ya mashariki, Mwezi wa Januari na February Mpaka March ndio miezi ambayo tunaweza kuyaita majira ya Mwanzo wa mwaka kunakuwa na Joto kali na ukavu wa aina Fulani, katika majira haya kwa wana wa Israel huangukia kati ya mwezi wa Abibu au mwezi (Nisani) katika majira haya ardhi huwa kame na kavu, na hivyo ndio majira ambayo wafalme wengi waliyatumia kuingia vitani kwa kusudi la kupanua mipaka ya mataifa yao, kuteka nyara, kulipisha kodi wale utakaowashinda au kulinda mipaka yako, wakati huu ulikuwa ni wakati muafaka kwa vita kwa sababu ardhi ilikuwa kavu, na hivyo iliweza kurahisisha vita vya miguu, magari ya kukokotwa na farasi lakini pia kusafirisha silaha na wanajeshi kwa urahisi zaidi kuliko wakati wa baridi na wakati wa mvua ambapo ardhi huwa na matope na vita vinakuwa ni ngumu,  wakati huu pia ilikuwa ni rahisi kuteka nyara vitu na kuvibeba kwa hiyo ilikuwa ni desturi ya Wafalme kutoka kwenda kupigana vita mwanzoni mwa mwaka mpya, Hata Mungu aliwaokoa wana wa Israel kutoka Misri katika majira kama haya.

Kutoka 12;1-2”BWANA akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu”.

Kwa hiyo wataalamu wa nyakati waliweza kuuelewa vema kuwa ulikuwa ni wakati gani na wanapaswa kufanya nini, Mwandishi anataka kutuonyesha kuwa Sababu zilizopelekea Daudi kufanya dhambi au kuanguka dhambini ilikuwa ni  pamoja na:-

1.       Aliudharau wakati – kumbe ilikuwa wazi kabisa na ilikuwa inajulikana kabisa kwamba Mwanzo wa mwaka mpya ni lazima wafalme watoke kwenda kupigana vita, Lakini yeye aliupuuzia wakati  Moja ya tatizo kubwa linaloweza kumleta mwanadamu katika anguko la maisha yake ni kutokujua kuutumia wakati, kuna madhara mengi na majuti makubwa sana kwa kila mwanadamu ambaye hakujua kuutumia wakati, wakati tuliopewa duniani ni mfupi sana na unaenda haraka mno, wastaafu wengi wanajua leo kwa sababu hawakujua kuutumia wakati, vijana wengi wanafikiri wataendelea kuwa vijana tu, wasichana wengi wanadhani wataendelea kuwa wasichana tu, wanafunzi wengi sana wanadhani iko siku watakaa ajipange na kusoma kwa bidii na sasa wengi wanalala na kupoteza muda wakifikiri uko wakati, Hakuna jambo linaumiza sana kama kuja kugundua baadaye kuwa sikuutumia wakati, nilikuwa wapi mimi? Hakuna jambo linaumiza kama kupotezewa wakati!  Kila mmoja wetu anapaswa kufahamu kuwa wakati usipoutumia vema anguko lake ni kubwa  na lenye kuleta madhara makubwa sana duniani, kwa hiyo ni vema kuutumia wakati na kutokuupuuza Yesu alilalamika kwa njia ya kinabii kwa mji wa Yerusalem kwamba utabomolewa na kuharibiwa vibaya sana na Majeshi ya warumi tukio ambalo lilitimizwa mwaka wa 70 baada ya Kristo lakini malalamiko ya Yesu kwa Yerusalem ni kwa sababu tu ya kutokuujua majira na wakati hususani Mwokozi wa ulimwengu alipowatembelea.

 

Luka 19:41-44 “Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.”

 

Daudi alifahamu wazi kuwa ulikuwa ni wakati wa wafalme kwenda vitani lakini yeye hakwenda vitani, alibaki anarandaranda mjini tu na hiki ndio moja ya sababu ambayo mwandishi anaiona kuwa Daud alikosea!

 

2.       Aliudharau wajibu -  Kupigania watu ulikuwa ni moja ya wajibu wa waamuzi na wafalme Daudi alikuwa anawajibika kabisa kwenda vitani, huu ulikuwa ni wajibu wake na wajibu wa wafalme wa mataifa yote, ndio kuna wakati unaweza kumtuma mtu aende, Lakini mwandishi anaonyesha kuwa tatizo hapa lililopelekea habari kuwa nyingine kwa Mfalme Daudi ni kutokwenda vitani yeye alimtuma Yoabu aende, wakati mwingine ili Mungu aweze kuleta ukombozi kwa jamii ni lazima waweko watu watakaokubali kubeba wajibu, kama kila mmoja wetu akibeba wajibu wake kwa ufanisi tutaweza kuona mwanga

 

Luka 1:38 “Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.”

 

Mariam alikubali kuubeba wajibu wa kumzaa Yesu na akaleta faida Kubwa sana Duniani, walimu wakifanya wajibu wao, wanafunzi wakifanya wajibu wao, wanasiasa wakifanya wajibu wao na  wananchi wakifanya wajibu wao hakuna kitakachoshindikana, mke na aafanye wajibu wake na mume naye afanya wajibu wake kila mmoja atimize wajibu Daudi alikwepa na kudharau muda na majira aliyotakiwa kwenda vitani na matokeo yake alipatwa na anguko la kihistoria, hatuwezi kumlaumu yeye kwa sababhu zozote zile kwani kuna kitu cha kujifunza kutoka kwake lakini mwandishi anatuonyesha kuwa moja ya sababu ya anguko lake ni kudharau wajibu, inapotokea kuwa shetani akatutia katika kishawishi cha kutokuzingatia kutimiza wajibu tunaweza kujikuta tunajutia maisha yetu yote na kusema laiti ningelijua kwa msingi huo ni muhimu kwetu tukatimiza wajibu

 

3.       Kupenda rahisi/au uvivu – kupenda rahisi au uvivu kuna madhara makubwa sana katika maisha yetu tunaambiwa kuwa Daudi alikaa tu onaLakini Daudi mwenyewe akakaa Yerusalemu.”Maana yake alikaa tu hakufanya kazi, Daudi aliingiwa na uvivu, mtu akikaa tu bila jambo la Muhimu la kufanya, kinachofuata sasa ni kumpa ibilisi nafasi, “Idlenes gives great adavantage to the temper  Neno la Mungu linapingana vikali sana na swala zima la la uvivu, na wakati wote neno la Mungu linatutaka kupingana na tatizo la uvuvi na linawataka watu wafanye kazi likiwa na mifano mingi sana na maelekezo mengi sana mfano

Mithali 6:6-11 “Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.”
Biblia ina la kusema kuhusu uvivu. Kitabu cha Mithali imejawa na hekima kuhusu uvivu na onyo kwa mtu mvivu. Mithali inatuambia kwamba mtu mvivu anachukia kazi:

Mithali 21:25 "
Matakwa yake mtu mvivu humfisha, kwa maana mikono yake hukataa kufanya kazi." Mithali 26:13-14 “Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani, Simba yuko katika njia kuu. Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake; Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake.“ Mithali 18:9 Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu.

Newton's first law states that, “if a body is at rest or moving at a constant speed in a straight line, it will remain at rest or keep moving in a straight line at constant speed unless it is acted upon by a force”. Mwandishi anaonyesha kuwa taabu nyingine ambayo Daudi ilimpelekea kuingia katika hali hii nzito ya anguko ni kukaa tu bila kufanya shughuli

2 Wathesalonike 3:10 “
Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula”.
Kila mmoja wetu anapaswa kuhakikisha kuwa hatumpi ibilisi nafasi, kila mmoja ahakikishe kuwa anaukomboa wakati na hapotezi muda, muda sio wa kuchezea muda ni mali, lakini wakati huo huo kila mmoja atimize wajibu wake na mwisho tuhakikishe kuwa tunapiga vita uvizu, maswala haya yalipodharauliwa na daudi yalileta anguko kwake ashukuriwe Mungu yeye alianguka katika zinaa lakini anguko baya kuliko yote ni kushindwa maisha hili linaleta majuto makubwa na machungu sana Duniani kuliko naguko la iana nyinguine lolote tunaweza kujiokoa kwa kujituma kwa bidii kwa kutumia nafasi na vipawa tulivyopewa na Mungu na kukamilisha kusudi la Mungu alilolikusudia kwetu Duniani, Neema ya Mungu na ikufunike ikiwa unataka kuishi kama Mfalme katika wakati ujao ni vema ukiyazingatia hayo!

Rev. Innocent Samuel Kamote.

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Mungu yule ambaye mimi ni wake!

Matendo 27:23-25Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami, akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.”



Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kwamba ustawi wa nafsi zetu na usalama wa roho zetu ulinzi na muelekeo wa maisha yetu unategemeana sana na Mungu yule Tunayemuabudu!  Hili ninjambo la msingi sana, tunaweza kuwa na mtazamo tofauti, tabia tofauti na mwenendo tofauti, na tukawa tunajiamini sana au tukawa na hofu lakini kwa vyovyote vile kila kitu na kila jambo  matumaini yetu na kujiamini kwetu kwenye kupita kawaida kunategemeana sana na Mungu tunayemuabudu, au kwa lugha nyingine uhusiano wetu na Mungu tunayemuabudu! Angalia maandiko yafuatayo kisha kuna kitu utagundua!

1.      Mwanzo 15:1 ” Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.”

2.      Mwanzo 31:24 “Mungu akamjia Labani, Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.

3.      Matendo 8:9-10 “Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze, kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu.”           

4.      Matendo 23:11 “Usiku ule Bwana akasimama karibu naye, akasema, Uwe na moyo mkuu; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako.

5.      Zaburi 27:1-4 “Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?  Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini. Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.

Maandiko yote hapo Juu pamoja na andiko la msingi yanatufundisha kwamba watakatifu waliotutangulia walikuwa na ujasiri mkubwa sana, walijiamini, walithibitishiwa usalama wao, kwa miili yao nafsi zao, ulinzi na kujaliwa kwa sababu walikuwa na uhusiano wa karibu na Mungu wa kweli aliye hai na mwenye uwezo na nguvu za kuwalinda kuwatetea kuwabariki na kutangaza hatima yao, hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba ustawi wetu katika Nyanja zote za maisha yetu unategemeana sana na Mungu tunayemuabudu!. Paulo mtume alipookuwa safarini Rumi safari ambayo ilikuwa imejawa na misukosuko mingi  na hatari ya kifo, Mungu ambaye Paulo anamuabudu na kumtumikia, Mungu wake alimtuma malaika wake na malaika yule alimthibitishia usalama Paulo pamoja na watu wote aliokuwa nao chomboni ona hii Matendo 27:23-25Kwa maana usiku huu wa leo MALAIKA WA MUNGU YULE AMBAYE MIMI NI WAKE, NAYE NDIYE NIMWABUDUYE, alisimama karibu nami, akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.” Unaona Mtume Paulo ana uhakika wa kile alichoelezwa na malaika wa MUNGU YULE AMBAYE YEYE NI WAKE NAYE NDIYE AMUABUDIYE kwa nini Paulo ansema haya kwa watu wale? Watu wale walikuwa hawamjui Mungu ambaye Paulo  anamuabudu na kumtumikia, walikuwa wanaabudu miungu mingine, kwa hiyo hofu ya kifo na mauti, kuhisi nuksi mikosi na balaa kuliwajaa kwa sababu hawakuwa na ufahamu kwa habari ya Mungu aliye hai ambaye Paulo anamuita Mungu wake, na tena Mungu ambaye yeye anamuabudu na kumtumikia, Mungu huyu sio tu aliyatunza maisha ya Paulo lakini alimpa na maisha ya watu wote waliokuwa pamoja naye na hivyo kwaajili ya Paulo nao walikuwa salama kwa sababu ya uhusiano uliokuwepo kati ya Paulo na Mungu huyo!

Hii maana yake ni nini ? maana yake ni lazima kila mmoja wetu awe na uhakika na Mungu yule anayemuabudu, Maandiko yanakubali kuwa kuna miungu Mingi, Na Mungu mwenyewe amewaonya watu wake kutokuwa na Mungu mwingine zaidi yake ona Kutoka 20:2-3 “Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi.” Unaona kama maandiko yanakiri kuweko kwa miungu mingi,  basi kuna miungu mingi, lakini anayepaswa kuabudiwa ni Mungu mmoja wa kweli, kama mwanadamu awaye yote atakuwa na uhusiano zege yaani uhusiano mzuri na mwema na Mungu huyu wa kweli atakuwa salama katika ulimwengu huu na ule ujao

Je ni kweli Mungu yupo?

Ni muhimu kufahamu kuwa Maandiko hususani neno la Mungu halifanyi kazi ya kuthibitisha kuwa Mungu yupo au hapana, Neno la Mungu linatuhakikishia moja kwa moja kuwa Mungu yupo na neno la Mungu linasema mtu anayewaza kuwa hakuna Mungu ni mpumbavu Zaburi 14:1-2 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.Hakuna jaribio lolote katika maandiko linalojaribu kuithibitisha kuwa Mungu yupo, kila amahali neno la Mungu limethibitisha kuwa Mungu anajulikana labda mtu awaze upumbavu tu moyoni mwake Zaburi 53:1-2 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.

Sasa basi kama Neno la Mungu linaonyesha wazi kuwa asemaye au awazaye moyoni kuwa hakuna Mungu ni mpumbavu tunawezaje kujua sasa ya kuwa Mungu yupo? Neno la Mungu linaweza kutusaidia namna ya kujua uwepo wa Mungu na namna ya kutthibitishia watu kwamba yeye yupo

1.      Kupitia uumbaji

Moja ya vitu ambavyo ninashangaza sana wanadamu hata wale walio wabishi kuhusu uwepo wa Mungu ni uumbaji, uumbaji ni uthibitisho wa wazi kuwa namna ulivyoumbwa na namna ulivyopangiliwa na ustadi wake ni wazi kuwa uumbaji unatangaza uweza nguvu na utukufu wa Mungu  maandiko yanasema Mbingu yaani solar system inatangaza utukufu wa Mungu ona Zaburi 19:1-6 “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake. Mchana husemezana na mchana, Usiku hutolea usiku maarifa. Hakuna lugha wala maneno, Sauti yao haisikilikani. Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu. Katika hizo ameliwekea jua hema, Kama bwana arusi akitoka chumbani mwake, Lafurahi kama mtu aliye hodari Kwenda mbio katika njia yake.Kutoka kwake lautoka mwisho wa mbingu, Na kuzunguka kwake hata miisho yake, Wala kwa hari yake Hakuna kitu kilichositirika.” Mwandishi anataka kutuelezea wazi kuwa mfumo wa jua na mbingu na anga kama ukiuchunguza unaonyesha utukufu wa Mungu, yaani kama vile tunavyoweza kuona na kushangaa vitu vilivyotengenezwa na wanadamu, na tukavihusudu ni wazi kabisa kuwa tunaweza kuhusudu kazi na utendaji wa Mungu wetu namna alivyoumba ulimwengu na hasa maswala ya anga

 


Uumbaji ni wenye kushangaza sana anga pekee limewafanya watafiti kujikuta wakishangaa kwa miaka mingi, Mungu ameweka utaratibu wa ajabu sana mawinguni ambao unawapa wanasayansi wakati mzuri wa kufanya utafiti wa again kujifunza na kujua mwenendo wa kazi na utendaji wa Mungu ambao ni dhahiri kila mtu anakubali kuwa ahuwezi kutokea kwa bahati mbaya tu!, ni wazi kuwa kadiri wanasayansi wanavyofanya uchunguzi wa kina wanabaini na kukubaliana na maneno ya mwandishi wa Zaburi 19:1 kwamba ni kweli Mbingu zinahubiri utukufu wa Mungu!

Watafiti wa kisayansi wa chuo cha Harvard  wanasema mpaka sasa wamegundua na kukubali kuwa kuna zaidi ya Galaxy yaani mfumo wa nyota au majua yaliyoko katika mpangilio ambao unaonekana kama vumbi wa zaidi ya miliono 500 milions

Jua ambalo ni nyota iliyoko karibu na Dunia ina kipenyo kinachokadiriwa kuwa na kilomita 1,392,000  na jua hilo linazunguikwa na sayari zilizothibitishwa zipatazo nane na ya tisa ambayo iko mbali sana na mwenendo wake bado unawachanganya watafiti kuibainisha kuwa ni sayari sayari hizo ni pamoja na

 

Jina la sayari

Umbali kutoka juani

Muda wa kuzunguka jua Revolution

Muda wa siku Rotation

Number of Moons

Mercury


57.9 million km

87.96 siku za dunia

58.7 siku za dunia

0

Venus


108.2 million km

224.68 siku za dunia

243 siku za dunia

0

Earth


149.6 million km

365.26 siku

24 hours

1

Mars


227.9 million km

686.98 siku za dunia

24.6 masaa ya dunia
=1.026 siku ya dunia

2

Jupiter


778.3 million km

11.862 siku za dunia

9.84 saa za dunia

67 (18 named plus many smaller ones)

Saturn


1,427.0 million km

29.456 siku za dunia

10.2 saa za dunia

62 (30 unnamed)

Uranus


2,871.0 million km

84.07 siku za dunia

17.9 saa za dunia

27 (6 unnamed)

Neptune


4,497.1 million km

164.81 siku za dunia

19.1 saa za dunia

13

Pluto 


5,913 million km

247.7 miaka ya dunia

6.39 saa za dunia

4

 

Unaweza kuona itakuwa ni ujinga kama sio upumbavu mkubwa kudhani ya kuwa mfumo huu umejiumba wenyewe  Na ndio maana neno la Mungu linaanza kwa kusema wazi kuwa Hapo mwanzo Mungu aliziumba Mbingu na nchi ona Mwanzo 1:1Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.Hii maana yake ni nini lazima kila mwadamu afikie kwenye hitimisho ya kuwa yuko Mungu aliyeziumba mbingu na nchi, haiwezekani kwa namna yoyote ile kwamba itokee kwamba ulimwengu ulijiumba wenyewe baada ya miaka milioni nyingi sana kama watu Fulani wanavyodhani

Kwa hiyo unaweza kuwaza pale unaposema namwamini Mungu baba mwenyezi muumba wa mbingu na inchi unaweza kupata picha ya Mungu yule tunayemuabudu na kumtumikia na kama una uhusiano naye Mungu yule ambaye mimi/wewe ni wake “THE GOD WHOM I/YOU BELONG TO HIM” kwa hiyo tunaweza kutambua kuwa Mungu yuko kwa kupitia uumbaji wake

2.      Kupitia Historia

Matukio mengo ya kihistoria duniani ni ushahidi ya kuwa nyuma ya kila historia ziko nguvu za Mungu aliyehai, adhai historia yote ya kibiblia imeandikwa kwa ajili ya kufunua nguvu na uweza wa Mungu wa kweli, Mungu wa kweli amejifunua kwetu kupitria taifa la Israel kwa hiyo ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa uwepo wa taifa hili ni ushahidi wa uwepo wa Mungu, kutoka Israel kanisa lilizaliwa na neno la Mungu lilienea duniani kote na ndio maana katika namna yenye kushangaza shetani amewahi kuwashawishi mataifa kadhaa kutaka kujaribu kuiangamiza Israel au kuifuta Israel katika ramani ya dunia, lakini mara kadhaa mataifa hayo yameshuhudia kushindwa vibaya Israel ni kijiti inachowaka moto lakini hakiteketei ona Kutoka 3:2-3 “Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.” Maono haya kitaalamu yalikuwa ni picha ya kinabii pia ya hali ya Israel ambayo inapitia matesio ya aina mbalimbali lakini haiwezi kuteketezwa kwa sababu kile kinazozaniwa kuwa moto, kibinadamu ni kwa sababu Israel imefunikwa na utukufu wa  Mungu;- tuangalie kwa ufupi historia fupi ya vita mbalimbali za anga za Israel ambazo walishinda kwa sababu ya uwepo na ulinzi wa Mungu Mungu amewafanya Israel kuwa hodari kweli kweli unaweza kuona data hizo kutoka (www.israelairforec.org).

*      1948 – wayahudi walipopata uhuru wakiwa kiasi cha wayahudi laki sita hivi kuhesabu wanawake na watoto Waarabu wakiwa milion 80 walikusudia kuwa futilia mbali lakini kwa uweza wa ajabu Israel Iliwapiga vibaya waarabu na kufanikiwa kupanua mipaka yao kutoka Tell Avivi Jaffa mpaka ukanda wa gaza, milima ya Golan, na kuuteka mji wa Yerusalem

*      1950 – Wafaransa walikuwa ndio wafadhili wakubwa wa kuuza ndege za kivita kwa Israel lakini katika vita ya Six days War Israel walionyesha kipigo kikali sana kwa maadui ambacho wafaransa walisema kipigo hicho hakiwezi kusababishwa na ndege zao kwa hivyo uhusiano na Israel kijeshi ulisimama kwani Israel walikuwa wakiziboresha ndege hizo na zikatoa kichapo kikali

*      June 5 1967 – Israel kwa dakika 3 tu walizipiga ndege za maadui 451 zilizokuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kuifuta Israel ndege hizo mpya zilizonunuliwa na wamisri na nyingine za Jordani na Syria  zilitandikwa vibaya na hivyo kupelekea Misri na Jordani kuweka mkataba wa kudumu wa amani na Israel kuwa hawatapigana tena milele, mkataba huu uliwafanya Israel kuipa Misri Jangwa la mlima Sinai, kwa masharti kuwa hawatapigana milele

*      1969-1970 – Ndege 111 za maadui ziliwekwa chini pamoja na msaada wa warusi katika vita hiyo waarabu waliaibika

*      Jeshi la anga la Israel limefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na katika operation mbalimbali waliweza kuwalenga viongozi wa kigaidi wa palestina kwa vipimo vilivyoweza kuwapata na kuwaua mmoja mmoja viongozi hao ni pamoja na Abu ali Mustafa, Ahmed Yasini na Abed al azizi Rant iss aliyeuawa punde akitokea msikitini wakati wa ibada ya ijumaa

*      1976 walifanikiwa kuokoa  wayahudi kadhaa waliokuwa wakitishiwa kuuawa na Iddi amini dikteta aliyetawala Uganda katika operation iliyoitwa operation Entebe

*      1991 – Jeshi la anga la Israel lilifanikiwa kuwaokoa wayahudi wenye asili ya kiafrika huko Ethiopia wanaoshukiwa kuwa ni watoto wa mfalme suleimani  Katika operation iliyoitwa operation Solomon

Hali hiyo inadhihirisha wazi kuwa Mungu yuko nyuma ya mambo, Mungu amewahi kuwapigania Israel katika vita mbalimbali kwa miujiza mikubwa sana, hii yote I nawatokea kwa sababu wanamuamini Mungu aliye hai, aidha unaweza kusoma miujiza 17 ambayo Mungu amewafanyia jeshi la ulinzi la Israel katika https://www.jewishvirtuallibrary.org/  Mungu aidha anahusika pia katika kazi ya kuwekaau kuinua viongozi na kuwashusha maandiko yana ushahidi kuwa hili ni swala pakee ambalo linafanywa na Mungu nyuma ya kura na matakwa ya kawaida ya kibinadamu, Mungu anafanya kazi nyuma ya historia, viongozi wa kisiasa na taasisi zozote duniani wanaonywa kuwa na unyenyekevu na utambuzi ulio wazi kuwa Mungu yuko nyuma ya uwepo wao au kutokuwepo kwao ona  Zaburi ya 75:5-7 “Msiiinue pembe yenu juu, Wala msinene kwa shingo ya kiburi. Maana siko mashariki wala magharibi, Wala nyikani itokako heshima. Bali Mungu ndiye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu.”

Daniel 2:20-22” Danieli akajibu, akasema, Na lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake. Yeye hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa; yeye hufunua mambo ya fumbo na ya siri; huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake.

Daniel 5:18-21 “Kwa habari zako, Ee mfalme, Mungu Aliye juu alimpa Nebukadreza, baba yako, ufalme, na ukuu, na fahari, na utukufu; na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha. Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake. Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng'ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote. Mungu yuko nyuma ya kila Historia, Historia yoyote ile duniani ni Historia ya Mungu.

3.      Tunaweza kumjua Mungu kupitia jina lake!

 

Ni vigumu sana kumuelezea Mungu na tukamuelewa vema bila kwanza kujua kuwa njia pakee ya kumjua Mungu ni kwa njia ya imani Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” Ni ili uweze kuwa na imani maandiko yanatuambia kuwa imani chanzo chake ni kusikia yaani lazima usikilize mafundisho na sio kila mafundisho yanaweza kuwa sahihi bali mafundisho kuhusu Kristo kwa sababu yeye pekee ndiye anayeweza kumfunua Mungu kwetu ona Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Kwa hiyo ni neno la Mungu pekee tena likifundishwa kwa usahihi linaloweza kutusaidia kumfahamu Mungu na kumuamini, Mungu anazo sifa nyingi sana na amajifunua kwa wanadamu kwa namna mbalimbali, na wanadamu walimpa Mungu majina kutokana na ufunuo ambao kwa huo Mungu alijifunua kwao Westminster Catechism inamuelezea Mungu kuwa ni Roho, Aelezeki, habadiliki, anajua yote, ana hekima yote, ana nguvu zote, ni mtakatifu, ni mwema, ni mwenye haki, ni mkweli na kadhalika. Maandiko yanamfunua Mungu kwa majina mbalimbali kutokana na aina ya jambo au kitu au tukio ambalo Mungu alilifanya kwa mwanadamu au wanadamu Fulani kwa wakati huo, nay eye mwenyewe amejidhihirisha kwa jina YAHWH katika maandiko jina ambalo hata Ibrahimu na Isaka na yakobo hawakuwahi kulijua wala kulipata ona

Kutoka 6:2-3 “Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.” Mungu anajifunua kwa mara ya kwanza kwa jina hili kwa Musa kwa sababu hapa alishuka kwa kazi maalumu ya UKOMBOZI hivyo jina hili linadhihirisha kuwa yeye ni Mwokozi na hapa alikuwa ameshuka kuwasaidia mwana wa Israel kukombolewa kutoka katika hali ya utumwa huko Misri Kutoka 3:6-9 “Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu. BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.Ni wazi kuwa Musa alitamani sana kumjua Mungu kwa kina na mapana na Marefu hata pamoja na ufunuo huu aliomba amjue Mungu kwa undani zaidi lakini Mungu alimtangazia jina pana zaidi ona Kutoka 34:5-7” BWANA akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la BWANA. BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.kwa msingi huo ni wazi kuwa katika agano la kale jina la Mungu lilifichwa na ilikuwa ngumu sana kwao kulitaja jina la Mungu au kulitumia bure au kukufuru kwa jina hilo wayahudi waliliogopa na jina hili lilifichwa kwa kuwa Mungu alikuwa anajifunua kwao kidogo kidogo Kutoka 20:7 “Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.

Walawi 18:21 “Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapitisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA.” Walawi 24:16 “Na yeye atakayelikufuru jina la BWANA hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzalia, hapo atakapolikufuru jina la BWANA atauawa

Amri ya kuhakikisha kuwa jina la Mungu linatukuzwa sio wayahudi pekee walioamriwa bali hata wakati wa agano jipya katika mafundisho yake Yesu anataka jina hilo litukuzwe Mathayo 6:9 “Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,”

Jina la Mungu lina uwezo wa kulinda watu wake lima uwezo wa kuinua, lina uwezo wa kubariki Zaburi 20:1-6 “Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue. Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote. Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. Bwana akutimizie matakwa yako yote. Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi wake; Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu.Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu.” Na kwaajili ya jina lake hawezi kuwatupa watu wake 1Samuel 12:21-22 “Wala msigeuke upande, maana, kufuata vitu vya ubatili, visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana Bwana hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza Bwana kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe.”  Kwa msingi huu tunaweza kuona umuhimu wa jina la Bwana Mungu wetu na zaidi ya yote unaweza matumizi ya jina lake kwamba ni lenye nguvu kubwa sana na msaada mkubwa kwa maisha yetu, Maandiko yanaionyesha jinsi watu walibyimuita Mungu majina mbalimbali kwa sababu ya ufunuo aliojifunua kwa watu wake

a.      Elohim – Ni jina ambalo watu walimpa Mungu wakimtambua kama Mungu mwenyezi muumba wa mbingu na ardhi ni jina la Mungu muumba jina hili linatumika kwa wingi likionyesha kuwa Bwana Mungu yu katika wingi na huu ni ufunuo kuhusu utatu wa Mungu elohimu inatumika katika maeneo kadhaa yafuatayo mfano Mwanzo 1:26 “ Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Na limetumika pia katika eneo linguine Mwanzo 11:6-7. “BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao

b.      Yehovah – Ni jina ambalo Mungu mwenyewe alijitambulisha kwa Musa alipokuwa ameshuka katika uwepo maalumu ili kuwasaidia wana wa Israel kutoka utumwani,ukiacha kuwa ni jina la ukombozi pia linaonyesha kuwa ni Mungu ashikaye maagano hasa kwa sababu ya utambulisho wake kama Mungu wa Ibrahimu, Isaka na yakobo, jina hili pia lina maana ya aliyekuwako, aliyeko na atatakayekuwako au niko ambaye niko kuonyesha umilelel wake Kutoka 6:2-3 “Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.” Jina hili Yehovah hata hivyo linasimamam na uaminifu au utendaji wa Mungu katika kutoa neema na msaada kwenye eneo Fulani la maisha pale Mungu anapoleta msaada kwa hivyo lilikuwa ni jina lisiloweza kusimama lenyewe bali lilionyesha ukombozi katika eneo ambalo Mungu anataka kukusaidia au alikusaidia

c.       Yehovah Rapha – Ni jina linalotumika Pale Mungu anapojifunua kwetu kama Mungu mponyaji Kutoka 15:26 “akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.

d.      Yehovah Nissi – Ni jina linalohusiana na uwezo wake wa kutupigania vitani, tunapokabiliwa na maadui au lolote lenye kuzia makusudi ya Mungu kwetu Mungu kama Yehovah Nissi ataingilia kati na kutupigania kwa namna ya kipekee, yeye ameahidi kutupigania milele, awaye yote atakayejifabya adui kwetu Mungu atakuwa adui kwake na atatusaidia katika vita maana yeye ni Bwan wa vita ona Kutoka 17:8-16 “Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu. Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu. Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi; akasema, BWANA ameapa; BWANA atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.

e.      Yehovah Shalom – Ni jina la Mungu lenye uhusiano na kujali kwa mungu na namna Mungu anavyotoa ustawi wa mwanadamu, ni Mungu anapojihusisha na kutupa amani Waamuzi 6:24 “Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.”

f.        Yehovah Ra’ah – Ni jina la Mungu anapojihusisha na kuyalinda maisha yetu, na kujihusisha na utoshelevu wetu Zaburi 23:1 “Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.”

g.      Yehovah tsidkenu – Jina linalotumika pale watu wanapotuhukumu na kutuona kama wenye hatia kwa sababu kadhaa au pale dhamiri zetu zinapohitaji kutiwa moyo kutoka katika hatia Mungu hufanyika kuwa haki yetu Yeremia 23:6 “Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.

h.      Yehovah Yire – Ni jina la Mungu anapojidhihirisha kama Mungu ambaye anakutana na mahitaji yetu Mwanzo 22:14 “Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.”

i.        Yehovah Shammah – Ni jina la Mungu linalodhihirisha uwepo wake BWANA YUPO HAPA Ezekiel 48:35 “Kuuzunguka ni mianzi kumi na nane elfu; na jina la mji huo tangu siku hiyo litakuwa hili, Bwana yupo hapa.”

Ni muhimu kufahamu kuwa pia jina El ambalo pia hutumika kwa utukufu wa Mungu pia ni jina lisiloweza kusimama lenyewe El ni Mungu lakini hutumika na muunganiko wa maneno mengina katika kulikamilisha kama ilivyo kwa jina lile Yehovah

j.        El-Elyon – Mungu aliye juu sana Mwanzo 14:18-20 18. “Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.”

k.      El-Shaddai – Mungu muweza yote mwenye kutekeleza mahitaji ya watu wake Kutoka 6:6-7 “Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa; nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri.        

l.        El-Olam – Mungu wa Milele Mwanzo 21:33 “Ibrahimu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la BWANA Mungu wa milele.” Aidha majina mengine ya Mungu ni pamoja na

m.    Adonai – maana yake Bwana au mttawala Kutoka 23:17 “Mara tatu katika mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele ya BWANA MUNGU.”

n.      Baba – Abba Mwanzilishi wa kila kitu Muumba au sababu ya kuwepo kwetu Matendo 17:28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake. Japo hii haituhakikishii wokovu bila kufuata kanuni ya kumuamini Yohana 1:12-13 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.”

SIFA ZA MUNGU

1.      Mungu anatajwa katika maandiko kuwa ni roho

Yohana 4:24 “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Tunaposema kuwa Mungu ni roho maana yake ni kuwa Mungu Baba hana mwili wa kibinadamu, Lakini mwana wa Mungu Yesu Kristo alikuja Duniani akiwa katika mwili ona Yohana 1:1-2, 14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.Kutokana na tendo hiliLa Mungu mwana kuwa na mwili wa kibinadamu Yeye amejulikana kama Emmanuel yaani Mungu pamoja nasi Mathayo 1:23 “Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi. “          

Mungu anapopewa sifa za kibinadamu hutumika lugha inayoitwa Anthromorphism – ili kusaidia kuleta uelewa kwa wanadamu, kwa msingi huo Biblia inatoa aina Fulani ya matamshi yenye kuashiria au kumfananisha Mungu na utendaji wa kibinadamu!

Mfano Isaya 59:1-“Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;” hapo Munu anatajwa kama ana mkono na ana sikio

2Nyakati 16:9 “Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.” Na pia Kumbukumbu 33:27 “Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza.” Lugha hizi zote ni lufgha zenye kumuelezea Mungu katika namna ya kibinadamu ili kutusaidia kumuelewa Lakini Mungu ni Roho na si mwanadamu!

2.      Mungu hana mipaka “infinite” no limitation

Ni mungu ambaye yuko mahali kote kwa wakati mmoja kwa msingi huo hawezi kutenganishwa na umbali au mahali 1Wafalme 8:27 “Lakini Mungu je? Atakaa kweli kweli juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga!                 Lakini neno hilo pia linatumika kumuelezea Mungu kama Mungu wa milele Muda hauna uwezo wa kumfunga yeye yuko tangu milele na milele ona Kutoka 15:18 “BWANA atatawala milele na milele.” Kumbukumbu 33:27 “Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza.” Zaburi 90:2 “Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.

3.      Mungu ni mwema

-          Ni mwenye upendo na huruma isiyoweza kuelezeka Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”.     

-          Zaburi 69:16 Ee “Bwana, unijibu, maana fadhili zako ni njema, Kwa kadiri ya rehema zako unielekee”.

-          Warumi 8:38-39 “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,  wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

4.      Mungu ni Mtakatifu!

-          Sifa ya utakatifu ni suifa ya Mungu pekee, hakuna mwanadamu mtakatifu wala mkamilifu wanadamu wote wana mapungufu Muhubiri 7:20 “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.”

-          Hakuna mwanadamu mwenye haki hata mmoja mbele za Mungu mpaka kwa neema yake tu ona Warumi 3:10-12, 23-24 “kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja. 23. kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24. wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;” Ni Bwana Mungu wetu tunayemuabudu aliye mtakatiu sana ona Isaya 6:1-4 “Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu. Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka. Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake. Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi.  Ufunuo 15:4 “Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.

-          Maandiko yanatoa wito kwa watu wote kuwa watakatifu kama Baba Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;  1Petro 1:15-16 “bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.”

5.      Mungu ni Mungu mwenye haki (Righteous and Just)

-          Kutokana na haki yake hataruhusu wadhalimu kuingia katika ufalme wake 1Wakoritho 6:9-10 9. “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. 

6.      Mungu ni mkweli na Muaminifu

-          Isaya 25:1 “Ee Bwana, wewe u Mungu wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako; Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.”

-          Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.”

-          Warumi 3:4 “Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu”.

-          Ahadi zake zote ni ndio na kweli Waebrania 10:23 “Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu;”

7.      Mungu ni mtoaji (He is a giving God)

-          Mungu ametupa kila kitu, kila kitu duniani ni chetu, Mwanzo 1:28-31 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo. Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.

-          Ametupa maandiko 2Timotheo 3:16. “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;”

-          Ametupa mwana wake wa pekee Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Ona pia Warumi 8:32”Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?

-          Anatupa Roho wake Mtakatifu Luka 11:13 “Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?    

-          Nguvu za kupata utajiri Kumbukumbu 8:18  Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo”-

-          Anatoa neema kwa wanyenyekevu 1Petro 5:5 “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”      

-          Hutupa Hekima kama tukihitaji Daniel 2:23 “Nakushukuru, nakuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu, uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliyotaka kwako; maana umetujulisha neno lile la mfalme. “

-          Mungu ni mkuu

a.      Anajua yote Omniscient – Warumi 16:27 “        Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amina. 1Samuel 2:3 Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.”

b.      Yu mahali kote Omnipresent – Zaburi 139:7-12 “Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?  Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari; Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika. Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa. “

Yeremia 23:24“Je, mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema Bwana. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema Bwana.”              

c.       Mungu ni mwenye nguvu zote Omnipotent – all powerful     

o   Nguvu za uumbaji Power of Creation Mwanzo 1:1 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.”  Wakolosai 1:16-17 “Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye”.

o   Ana nguvu za kuokoa - Isaya 50:2-3 “ Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu. Mimi nazivika mbingu weusi, nami nafanya nguo ya magunia kuwa kifuniko chao.” Mungu ni mwenye uwezo wa kuokoa na ni mwenye uwezo  wa kutukomboa, anasema katika Isaya kuwa ana uwezo wa kuikemea hata bahari  jambo ambalo liliwatishia sana wanafunzi wa Yesu waliokuwa wanalijua andiko hili vema na kisha Masihi akaikemea bahari mbele yao nayo ikatii ona – Marko 4:39-41 ”Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu. Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado? Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?”

o   Hakuna jambo lolote lililo gumu la Kumshinda yeye Yeremia 32:17 “Aa! Bwana MUNGU, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza;”

d.      Mungu ni wa milele

o   Amekuweko tokea enzi na enzi ona Zaburi 90:1-2 “Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi.Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.”

o   Yeye ni Mwanzo na mwisho Alfa na omega Ufunuo 22:13 ” Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.”

o   Yeye mwenyewe anasema kabla yake na baada yake hakuna mwingine ona Isaya 43:10-11 ”Ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. Mimi, naam, mimi, ni Bwana, zaidi yangu mimi hapana mwokozi.”

e.      Mungu hana kigeugeu

o   Waebrania 13:8 “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.”

o   Yeye sio kama kivuli kinageuka geuka Yakobo 1:17 “ Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. “

8.      Mungu ni Mkamilifu!

Tuwapo duniani kama wanadamu na kutokana na hitilafu ya kuwepo kwa dhambi Duniani kumekuwepo na mapungufu mengi sana wakati mwingine tunaweza kufikiri kuwa labda huenda muumba amekosea au kuna namna anakosa ukamilifu, Lakini sivyo maandiko yanavyotusimulia kuhusu Mungu, Mungu ni mkamilifu katika kazi zake zote na hakuna lolote analoweza kukosea au kujuata, wala hakuna kutokukamilika kokote ambako amekuficha ni mkamilifu katika sifa zako zote

-          Amekamilika katika maarifa na ujuzi wake wote ona Ayubu 37:16 “Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa, Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa?”

-          Hakuna lolote asilolijua ama linaloweza kufichika kwake lolote tulifanyalo hata kwa siri sana anajua yote na anakumbuka vema mno anajua mpaka mawazo yetu na Mapenzi yake ni kamili Warumi 12:2Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

-          Sheria yake pia ni kamilifu haina mapungufu Zaburi 19:7 “Sheria ya Bwana ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia mjinga hekima.

-          Njia zake ni kamilifu Zaburi 18:30 “               Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya Bwana imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia.”

-          Kazi zake ni kamilifu Kumbukumbu 32:4 Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.        

-          Neno Ukamilifu “Perfect katika Kiebrania linatumika neno “TAMIYM” Ambalo maana yake isiyolaumika , isiyo na lawama without Blemish  Katika kiyunani ni “TELIOS”  maana yake Kamilifu sawa na Sadaka ya mnyama ambayo Mungu aliagiza itolewe katika Walawi 23:17-18 17.” Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa BWANA. Nanyi, pamoja na hiyo mikate, mtasongeza wana-kondoo saba, walio wakamilifu, wa mwaka wa kwanza, na ng'ombe mume mmoja, na kondoo waume wawili; watakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA, pamoja na sadaka yao ya unga, na sadaka zao za kinywaji, sadaka ya harufu ya kupendeza iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.”             

Faida za Kumjua Mungu!

Kwa nini tunajifunza kuhusu Mungu? Kuna faida gani ya kujifunza kuhusu Mungu, Nguvu zake na uwezo wake? Ayubu 22:21 “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.” Tunapopata nafasi ya kumtambua Mungu inakuwa rahisi kwetu kustawisha uhusiano wetu na Mungu jambo ambalo litatufanya tuwe na uwezo wa kutambua uwepo wake, kumuheshimu na kumuabudu na kujenga uhusiano mkubwa sana na yeye! Paulo Mtume alikuwa na uhusiano mkubwa sana na Mungu jambo lililopelekea awe na uwezo wa kupata taarifa za usalama wake kutoka kwa Malaika wa Mungu, huku akizungumza wazi kwa wapagani, kuwa mungu huyo ni wake na ndiye anayemtumikia Matendo 27:23-25Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami, akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.”

1.      Kumjua Mungu na kumtumikia kunatupa imani thabiti isiyo na shaka juu ya uwezo wake Daniel 3:16 -18 “Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.

2.      Kumjua Mungu na kumtumikia yeye kunatupa tofauti kati yetu na wapagani au watu wasiomjua Mungu Zaburi 20:7-8 “Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu. Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.” Zaburi 46:1-2 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.”

3.      Uhusiano wetu na Mungu utaimarika atakuwa Mungu wetu na tutakuwa watu wake ona Yeremia 30:19-22 “Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge.Watoto wao nao watakuwa kama zamani, na kusanyiko lao litathibitika mbele zangu, nami nitawaadhibu wote wawaoneao. Na mkuu wao atakuwa mtu wa kwao wenyewe, naye mwenye kuwatawala atakuwa mtu wa jamaa yao; nami nitamkaribisha, naye atanikaribia; maana ni nani aliye na moyo wa kuthubutu kunikaribia? Asema Bwana. Nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.”

4.      Kumjua Mungu kutafungua ukurasa wa maarifa ambayo wengine hawana, ujuzi kuhusu Mungu unauwezo wa kutupa aina ya maarifa ambayo wengine hawana Petro aliwahi kupokea maarifa ya kipekee ambayo kwayo Yesu alijua isingekuwa rahisi kuyajua au kuyapokea Bila kuwa na uhusiano na Mungu ona Mathayo 16:13-17 “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.”

5.      Kumjua Mungu kutatupelekea kufanya mambo makubwa ya ajabu Zaburi 108:12-13 “Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai. Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu” Daniel 11:32 “Na wao wafanyao maovu juu ya hilo agano atawapotosha kwa maneno ya kujipendekeza; lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu.”

6.      Kumjua Mungu na kumtegemea Yeye kunatupa uhakika wa usalama wetu Zaburi 91:1-,7 “Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini. Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo. Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao. Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana, Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri, Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.

7.  Kumjua Mungu na kuwa naye kunatupa ujasiri Yoshua 1:5 “Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha.

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima!