Jumatatu, 8 Januari 2024

Kwanini Yesu alijiita Mwana wa Adamu?


Mathayo 16:13-17 “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.”

 

 



Utangulizi:

 

Moja ya njia pekee ya kutambua mtu au kitu kwa kina na mapana na marefu ni pamoja na kuangalia majina ambayo mtu huyo anaitwa au anajiita, katika somo la uungu, unapomzungumzia Mungu baba na mwana na Roho Mtakatifu, moja ya nafsi ambayo inasumbua sana wanazuoni wengi wa Kikristo na zaidi wasio wakristo ni kujua asili ya Kristo, na ni kutokana na kuwepo kwa utata mwingi sana kuhusu asili ya Yesu, kumekuwepo na somo katika vyuo vya Biblia linalojaribu kuchambua kwa undani ili kumjua Yesu ni nani, somo hilo kitaalamu huitwa CHRISTOLOGY  ambalo ni muunganiko wa misamiati miwili ya kiyunani CHRIST na LOGOS ikiwa na maana ya MAARIFA KUHUSU KRISTO – Knowledge about Christ, Somo hilo kimsingi linahusika na kuchambua kwa undani sana kuhusu Yesu Kristo na asili yake, kumjua Yesu na Mungu baba yetu wa Mbinguni yalikuwa ni moja ya sehemu ya muhimu ya maombi ya Yesu Kristo kwetu!.

 

Yohana 17:1-3 “Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe;             kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.”

 

Kumjua Yesu Kristo kwa kawaida sio swala Jepesi kama tunavyofikiri, huwezi kumjua Yesu bila msaada wa Mungu, maandiko au Yesu Mwenyewe na katika maandiko pia wakati mwingine ni mpaka yeye mwenyewe ahusike kukufunulia andiko husika kwa neema yake. Leo tutachukua muda kujifunza somo hili muhimu KWANINI YESU ALIJIITA MWANA WA ADAMU tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-

 

·         Jinsi kuijua asili ya Yesu Kristo kulivyowasumbua wasomi

·         Jinsi ya kumjua Yesu Kristo

·         Kwanini Yesu alijiita mwana wa Adamu

 

Jinsi kuijua asili ya Yesu kulivyowasumbua wasomi

 

Moja ya swala ambalo lilisumbua sana mnamo karne ya kwanza mpaka karne ya tatu kwa wanazuoni wakubwa sana katika kanisa la Mungu, ilikuwa ni pamoja na kuijua nafsi ya Mungu mwana, utata kuhusu Yesu ni nani sio tu ulisumbua vichwa vya wasomi, lakini hata wakati wa Yesu mwenyewe kila mmoja alikuwa akisema lake kuhusu Yesu ni nani ona :-

 

Mathayo 16:13-17 “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.”

 

Katika karne ya tatu swali kuhusu Masihi ni nani bado liliendelea kuwasumbua wasomi na kila mtu alikuwa na maoni yeke kuhusu asili ya Yesu kuwa ikoje na ni nani? Kama tunavyoweza kujionea maoni mbalimbali ya wanazuoni wakiumiza kichwa kumjua Yesu.

 

1.      Waebionite – (Ebionites) – Hili ni kundi la wakristo wa kiyahudi ambao walikuweko karne za mwanzoni wakiishi maisha ya kimasikini wakiwa na Imani kuwa umasikini una uhusiano na maisha matakatifu, waoa walikuwa wakiamini kuwa YESU NI MASIHI LAKINI SIO MUNGU na kuwa kuzaliwa kwake na Mariamu kunasisitiza umuhimu wa kuishika na kuitii Torati ya Musa, Hivyo Yesu ni Mwanadamu aliyetii torati yote ya Musa na kutunukiwa kuwa masihi.

 

2.      Waanostisizim – (Gnosticism) – Hili ni kundi la watu walioamini kuwa Maarifa yanaleta wokovu na dhambi ni ujinga, kundi hili liliamini kuwa YESU ALIKUWA NI ROHO NA HAJAWAHI KUUTWAA MWILI Fundisho la aina hii lilipingwa vikali na Mtume Yohana na alilionya kanisa kuwa makini na aina ya fundisho kama hilo ona

 

 1Yohana 4:1-3 “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.”            

3.      Waariyan – (Arianism) – Ni kundi la Wakristo waliofuata fundisho la Mwanatheolojia aliyeitwa Arius ambaye alikuwa mwangalizi na msomi wa chuo kikuu cha Kikristo huko Alexandria nchini Misri kati ya mwaka 256-336 Baada ya Kristo, wao waliamini kuwa Yesu sio Mungu ni kiumbe cha kwanza kuumbwa na Mungu na hivyo hayuko sawa na Mungu lakini yuko chini kidogo ya Mungu na juu ya malaika, walimuita Yesu Mwanzo wa kuumba kwa Mungu sawa na

 

Ufunuo 3:14c “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, MWANZO WA KUUMBA KWA MUNGU.”

 

Pia wanatumia andiko hili kutoka injili ya Yohana Yesu akisema baba ni Mkubwa kuliko Yeye

 

Yohana 14:28 “Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, KWA MAANA BABA NI MKUU KULIKO MIMI.”

 

4.      Wanestorian – (Nestorianism) – Hili ni kundi lingine la wasomi wa Kikristo, waliokuwa na mtazamo tofauti kuhusu asili ya Yesu, wao waliona kuwa uungu na ubinadamu hauwezi kuwa na muunganiko kwa hiyo Yesu hawezi kuwa Mungu mwanadamu, au kuwa Mungu wakati huo huo na wakati huo huo mwanadamu.

 

5.      Waapolonari – (Apollinarian) – Aplonari alikuwa ni askofu kijana wa kanisa la Laodekia lililokuwako huko Syria mwaka wa 361 baada ya Kristo, yeye aliamini pamoja na watu wake kuwa Yesu alikuwa mwanadamu lakini akili yake ilikuwa akili ya kiungu, kwa hiyo asili hizi mbili hazikuweza kujitokeza kwa pamoja ni kama anataka kusema kuwa kuna wakati Yesu alikuwa mwanadamu na alisema na kundenda kibinadamu na kuna wakati alikuwa Mungu na alitenda na kusema kama Mungu.

 

6.      Waeutiko – ( Eutychians)  - Hili ni kundi la Wakristo waliofuata mafundisho ya Eutychus ambaye aliishi huko Constantinople, kati ya mwaka  380 - 456      baada ya Kristo, wao walikuwa na fundisho kuwa Yesu alikuwa na asili mpya yaani Mungu + Mwanadamu = Asili mpya, kwa hiyo Yesu sio Mungu wala sio Mwanadamu

 

7.      Waorthodox – (Orthodox) – Hili ni Kundi la wakristo wanaoamini kuwa wanafundisho sahihi neno Orthodox maana yake ni Right opinion  wao waliamini kuwa Yesu ni Mungu mwanadamu na kwa sababu hiyo Yeye ni Mwanadamu kwa asilimia 100% na ni Mungu kwa asilimia 100% fundisho hili ndilo lililosalia kuwa fundisho sahihi mpaka sasa kwa mujibu wa kanisa la Mungu  wao wanasimamia andiko la Yohana 1:1-3, 13-14

 

Yohana 1:1-3 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.”

 

Yohana 1:14 “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.”

 

Unaweza kuona makundi hayo yalikuwa na mijadala mikali sana kuhusu Asili ya Kristo, na hii inatufundisha wazi kuwa kumjua Yesu Kristo sio kazi nyepesi kama watu wengi wanavyodhani inahitajika neema maalumu ya kiungu kuweza kumjua Yesu, na ndio maana watu wengi sana huwa wanachanganyikiwa kuhusu, nafsi na asili ya Yesu mpaka leo, Ni muhimu sana tunapoendelea kujifunza somo hili kuwa na maombi ya kutaka kumjua Yesu zaidi, kama mwandishi wa Tenzi za injili namba 92 alivyoimba kuwa anataka kumjua Yesu na azidu kumfahamu, tunahitaji neema ya Mungu kumjua bwana wetu Yesu.

 

Jinsi ya kumjua Yesu Kristo

           

Kumjua Yesu Kristo kamwe hakuwezi kuja kwa akili za kawaida za kibinadamu, wala kwa kujenga hoja za kisomi, maandiko na Yesu Kristo Mwenyewe anaonyesha wazi kuwa kumjua Yesu Kristo kunaweza kuletwa kwetu kwa msaada wa Mungu na ufunuo wa Mungu Baba mwenyewe kwetu kupitia Roho wake Mtakatifu, maandiko au Yesu Kristo mwenyewe moja kwa moja tunaweza kupata ushahidi wa jambo hili kwa kuangalia tena andiko letu la Msingi

 

Mathayo 16:16-17 “Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.”

 

Unaona? Yesu alipouliza swali watu wanasema kuwa mwana wa Adamu ni nani, kulikuwa na majibu mbali mbali kuhusu Masihi, lakini hatimaye Simioni Petro akajibu, wewe ndiwe Kristo Mwana wa Mungu aliye hai, na mara baada ya jibu hili ambalo lilikukuwa jibu sahihi Yesu alijibu kwa kumwambia HERI WEWE SIMONI BAR-YONA; KWA KUWA MWILI NA DAMU HAVIKUKUFUNULIA HILI, BALI BABA YANGU ALIYE MBINGUNI Maneno haya yana maana gani? Rahisi tu huwezi kumjua Yesu bila kufunuliwa na Mungu mwenyewe, na kule kusema mwili na damu havikukufunulia hili, Yesu alikuwa akimaanisha Akili ya kawaida ya kibinadamu na uweza katika uhai wa mwanadamu hauwezi kutambua siri hii ya kuwa Yesu Kristo ni nani, na ndio maana umeweza kuona wasomi wengi walisumbuka kutambua asili ya Kristo na hata leo, watu wa dini nyingine hususani wakiwemo waislamu wanahangaika sana na kutatizwa mno na ukweli kuhusu asili ya Yesu Kristo,  na huwa wanadhani tuna haja ya kumkuza sana au kukufuru kwa kumpa Heshima ambayo wanadhani haistahili, jambo kubwa la Msingi ni kuwa tunamjua Mungu kupitia ufunuo kutoka kwa Mungu mwenyewe! Na neema yake wakati tunapotafakari na kumruhusu yeye atufunulie maandiko!

 

Au wakati mwingine Yesu mwenyewe huwa anahusika kutufunulia yeye mwenyewe ili tuweze kumjua au kutufunulia maandiko ili tuweze kuelewa, jambo hili linadhihirika wazi kuwa hata wanafunzi wa Yesu, waliomuona mubashara alipokuwa hai, alipofufuka ilikuwa ngumu kwao kumjua na hata kujua kile ambacho kimeandikwa kumuhusu, lakini kwa msaada wake yeye mwenyewe waliweza kubaini ukweli uliokuweko na kwa hiyo kwa kupitia ufunuo wake katika maandiko unaweza kumjua kumhusu! Angalia maandiko hapa:-

 

Luka 24:13-32Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. Macho yao yakafumbwa wasimtambue. Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote; tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha. Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo; tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema, wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai. Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona. Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe. Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya kama anataka kuendelea mbele. Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao. Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa. Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao. Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko?      

 

Kwa hiyo hata maandiko kumbe tunaweza tu tukayasoma lakini kama Mungu Baba, au Mwana au Roho Mtakatifu hatakufunulia jambo au utafichwa jambo huwezi kulibaini au kulijua, wanafunzi wa Yesu ni mpaka yalipofumbuliwa macho yao ndio wakaweza kuelewa na macho yao yakafunguliwa wakamtambua, lakini pia alipokuwa akiwafunulia maandiko tena akiwakemea ENYI MSHIOFAHAMU WENYE MIOYO MIZITO YA KUAMINI YOTE WALIYOYASEMA MANABII, ukifungwa ufahamu, ukawa na moyo mzito huwezi kuelewa na kuamini hata kilichoandikwa na manabii, Yesu akikufunulia maandiko utamuelewa kwa undani, na anaweza kufanya hivyo kwa wale waliokuwa pamoja naye n ahata kwa wale wasiokuwa pamoja naye yaani hata sisi leo Yesu yu aweza kutuelekeza kitu kupitia Roho wake Mtakatifu na tukaweza kuelewa yale yaliyofichika ona hii:-

 

Wagalatia 1:11-12 “Kwa maana, ndugu zangu, injili hiyo niliyowahubiri, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu. Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.”

 

Paulo Mtume pia katika kifungu hiki anatuhakikishia kuwa aliihubiri injili ambayo haikuwa ya namna ya kibinadamu kwa sababu aliipokea na kufundishwa na Yesu Kristo mwenyewe kwa ufunuo, kwa hiyo unaweza kukubaliana nami wazi kuwa bila kufunuliwa jambo kuhusu Kristo ni vigumu kwa akili za kawaida kuweza kutambua kitu au jambo kuhusu Yesu Kristo, Hasa kama Bwana amekusudia kulificha au kama hatuna muda wa kusoma na kutafakari na kutaka kumjua. Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuwa na ufunuo kumhusu Kristo ili tuweze kuwa na uelewa mpana kwa kina na mapana na marefu kumuhusu Yesu!, katika somo hili sio nia yangu kumuelezea Yesu Kristo labda nitafanya hivyo wakati mwingine leongo langu kuu ni kujibu swali la Msingi kwanini Yesu alijiita mwana wa Adamu hili tutalitafakari kwa kina katika kipengele kinachofuata:-

 

Kwanini Yesu alijiita mwana wa Adamu

 

Kama umeweza kunifuatilia tangu mwanzo, leo sitaki kujibu swali Yesu ni nani, lakini nataka kujibu na kuweka wazi kwanini Yesu alijiita Mwana wa Adamu, moja  ya njia ya kumjua Yesu ni pamoja na kuyajua maandiko, kwamba yanasema nini Kumuhusu yeye, kwa hiyo katika somo la ufahamu kuhusu Yesu Kristo yaani Christology waalimu wanafanya kazi kubwa sana ya kuchambua majina yoote ya Yesu Kristo yaliyotumika katika maandiko kumuelezea, na moja ya majina hayo ni MWANA WA ADAMU tena inaonekana wazi kuwa jina hili Yesu Kristo mwenyewe ndiye aliyelitumia zaidi kuliko wanafunzi wake wala watu wengine, kwa hiyo kuna swali kubwa sana la msingi la kujiuliza kwanini Yesu alikuwa akijiita mwana wa Adamu? Na kabla ya kuangalia swala hilo tuone sehemu kadhaa katika maandiko Yesu akijiita mwana wa Adamu na tukio hili la kujiita mwana wa Adamu limeonekama mara zaidi ya 82 katika maandiko hususani agano jipya

 

Mathayo 12:31-32 “Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa. Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya MWANA WA ADAMU atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.”            

 

Mathayo 13:37 “Akajibu, akasema, Azipandaye zile mbegu njema ni MWANA WA ADAMU;”

 

Marko 14:62 “Yesu akasema, Mimi ndiye, nanyi mtamwona MWANA WA ADAMU ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija na mawingu ya mbinguni.”

 

Luka 12:8-10 “Nami nawaambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, MWANA WA ADAMU naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu;          na mwenye kunikana mbele ya watu, huyo atakanwa mbele ya malaika wa Mungu. Na kila mtu atakayenena neno juu ya MWANA WA ADAMU atasamehewa, bali aliyemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.”

 

Yohana 1:51 “Akamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya MWANA WA ADAMU.”

 

Yohana 3:13-15 “Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, MWANA WA ADAMU. Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo MWANA WA ADAMU hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.”

 

Mathayo 8:20 “Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota; lakini MWANA WA ADAMU hana pa kulaza kichwa chake.”

Marko 10:45 “Kwa maana MWANA WA ADAMU naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.”

 

Luka 5:24 “Lakini, mpate kujua ya kwamba MWANA WA ADAMU anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (alimwambia yule mwenye kupooza). Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende zako nyumbani kwako.”

 

Mathayo 26:64 “Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona MWANA WA ADAMU ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.”

 

Hayo ni baadhi ya maandiko machache tu ambayo yanamtaja Yesu kama Mwana wa Adamu,  na baadhi ya mikazo hii aliitaja yeye mwenyewe, swali kubwa linabaki kwanini Yesu anajiita Mwana wa Adamu?  Na ni watu wachache sana ambao walimuita Yesu mwana wa Adamu baada ya kumuona akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu ona

 

Matendo 7:55-56 “Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu. Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na MWANA WA ADAMU amesimama mkono wa kuume wa Mungu.”            

 

Kwa mujibu wa utafiti wa kimaandiko na michango ya wanazuoni wengi kuhusu tafasiri ya kwanini Yesu alijiita Mwana wa Adamu kwa mkazo na msisitizo mkubwa? Ziko sababu kadhaa ambazo wanatheolojia wanajaribu kuelezea Kama nitakavoainisha hapa

 

1.      Kusisitiza uhusiano wake na wanadamu

 

Moja ya tafasiri inayoelezwa na wanazuoni ni kwanini Yesu alijiita mwana wa Adamu inasemekana ni kusisitiza uhusiano wake na wanadamu, hii ni kwa sababu neno Mwana wa Katika Kiibrania linasomeka BEN ambalo lina maana kubwa mbili, Mtoto wa, na uhusiano na, Kwamfano watu waliookoka wao huitwa wana wa Ufalme ona

 

Mathayo 8:11-12 “Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni; bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.”        

 

Wakati wale watakaofufuliwa na Bwana wetu Yesu Kristo wanaitwa wana wa Ufufuo

 

Luka 20: 35-36 “lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi; wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo.”

 

Hali kadhalika wale wanaopenda Amani, Yesu aliwaita wana wa Amani unaweza kuona katika

 

Luka 10:5-65. “Na nyumba yo yote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu.”

 

Na mtu ambaye ameandikiwa hukumu ya Mungu, huitwa mwana wa uharibifu mfano ni Yuda ona

 

Yohana 17:12 “Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.”

 

Kwa hiyo Yesu anapotumia neno Mwana wa Adamu anammaanisha kimsingi uhusiano wake na wanadamu, au uhusuano wake na Adamu aliye baba ya wanadamu wote, kwa msingi huo katika mkazo huu Yesu ambaye ni Mungu anataka kuonyesha ushirika wake na wanadamu, anataka kutuonyesha kuwa aliacha enzi na utukufu na kukubali kuwa mwanadamu ambaye kimsingi ni dhaifu na hivyo ni jambo la unyenyekevu sana    

 

Wafilipi 2: 6-8 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.”

 

Kwa msingi huo jina hili Mwana wa Adamu linaunganisha au kuonyesha ubinadamu wote wa Bwana Yesu, akiwa anakula, anachoka, analala, anasalitiwa, anateswa, anadhihakiwa, anateswa na anauawa na hatimaye Mungu anamfufua kutoka kwa wafu, kwa hiyo moja yaw azo la kitheolojia ni kuwa Yesu ambaye ni Mungu alikuwa anafurahia kuushiriki ubinadamu na akawa anaweza mkazo Mwana wa Adamu.

 

2.      Kwaajili ya Kutimiza unabii

 

Jambo lingine linalozungumzwa na wanazuoni kwamba ni kwanini Yesu alijiita Mwana wa Adamu ilikuwa ni kujitambulisha kuwa yeye ndiye Masihi sawa na nabii mbalimbali katika maandiko ukiwemo unabii wa Daniel tunaweza kuliona hilo wazi katika

 

Daniel 7:13-14 “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.”

 

Ni uwazi kuwa unabii huu wa Daniel pamoja na maeneo mengine umesema wazi kuwa masihi atakuwa ni wa namna gani, ni aliye mfano wa Mwanadamu na akapewa Mamlaka na utukufu na ufalme, hivyo ni vya milele, kwa hiyo wanatheolojia wengi wanahisia ya kuwa Yesu alupokuwa akijiita mwana wa Adamu alikuwa pia akijidhihirisha kuwa yeye ni Masihi sawa na namna na jinsi alivyotabiri nabii Daniel.

 

Kwa ujumla kupitia Yesu kuwa mwanadamu, ameweza kufanya kazi kubwa ya kuandaa njia ya ukombozi wa mwanadamu, ukiacha kuja kuwa na Enzi na mamlaka ya utawala wa kiungu duniani lakini Masihi ameweza kufanya mengi kwaajili ya wanadamu, ameweza kuufunua uungu na wema na tabia ya Mungu kupitia uanadamu wake kwa hiyo kuna faida kubwa sana ya Yesu kuwa mwanadamu mfano

 

Kusamehe dhambi wanadamu kwa sababu ameonja unanadamu anajua udhaifu wa mwanadamu – Marko 2:10 “Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza),”

 

Kumtafuta mwanadamu na kumuokoa – Luka 19:9-10 “Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu. Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.”

 

Kushiriki mateso kwa niaba ya wanadamu ili kuleta ukombozi – Marko 8:31  Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupatikana na mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka.”

 

Kumfunua Mungu kwetu – Yesu alipokuwa na mwili wa kibinadamu alisema wazai kuwa kazi ananozifanya na maneno yote aliyokuwa anawafundisha yalikuwa yanafunua matendo ya Mungu kwa wanadamu

 

Yohana 5:19-20 “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; hata na kazi kubwa zaidi kuliko hizo atamwonyesha, ili ninyi mpate kustaajabu.”

 

Kuonyesha shauku ya Mungu kushirikiana na wanadamu – Mathayo 1L22-23 “Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.”           

 

3.      Kwaajili ya Kufunua asili yake ya uungu

 

Tunaelewa wazi kuwa Yesu ni Mungu, kule kuitwa mwana wa Mungu maana yake anashiriki uungu, kwa hiyo Yesu alikuwa akijionea fahari kuushiriki uanadamu, huku yeye akiwa na asili ya uungu, Mungu anamjua mwanadamu kama kiumbe dhaifu na mara kadhaa alilitumia neno mwanadamu akimuita Ezekiel, inasemekana Mungu anamtaja Ezekiel kama mwanadamu mara 93 kwa msingi huo Mungu alikuwa akimaanisha Ezekiel ni mwanadamu lakini sivyo Ilivyo Kwa Kristo. Yesu hakuwa dhaifu Kama Ezekiel Yeye alikuja kumfunua Mungu kwetu, alikuwa Mungu aliyeishi katika ubinadamu

 

Wakolosai 2:9 “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.”

 

Kwaajili ya haya aliweza kusamehe dhambi, aliweza kuonyesha ubwana dhidi ya sabato, aliweza kuonyesha kuwa amekuja kumuokoa mwanadamu, aliweza kuonyesha kuwa ana uwezo wa kufufua wafu, aliweza kuonyesha kuwa anamamlaka ya kuhukumu, na kuonyesha kuwa atarudi tena siku moja duniani, aliweza kuonyesha kuwa ana mamlaka ya kubadili sharia ya Musa kwa kuitimiza na ana mamlaka ya kumuweka huru Mwanadamu na kumkomboa kama mwana wa Mfalme wa Mbinguni

 

Mathayo 26:64 “Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.”

 

Kwa sababu hizi na nyinginezo nyingi wanatheolojia wanazitumia kumuelezea Yesu na kujaribu kujibu kuwa ndio sababu kubwa na za Msingi za Yesu kujiita mwana wa Adamu. Kwa hiyo katika tafiti nyingi na vitabu vingi na wajenga hija wengi wanaishia kwenye jambo hilo na sababu hizo kwanini Yesu alijiita mwana wa Adamu!

 

Hitimisho:

 

Kwa mtazamo wangu mimi ambao ndio umenisukuma kuandaa somo hili, Yesu alipokuwa akijiita Mwana wa Adamu, kuna tofauti kabisa na Mungu alivyokuwa akimuita Ezekiel nabii Mwanadamu, Yesu alikuwa akijiita Mwana wa Adamu, katika mtazamo uleule wa namna anavyojiita au alivyoitwa Mwana wa Abraham, au Mwana wa Daudi, unapoangalia maandiko katika Kitabu za Ezekiel Mungu anapomuita Ezekiel Mwanadamu kuna tofauti na neno Mwana wa Adamu linavyotumika katika Agano jipya tunaweza kuona kwa kitambo kiasi

 

Ezekiel 3:1-4 “Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli. Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo. Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali. Akaniambia, Mwanadamu, haya! Waendee wana wa Israeli ukawaambie maneno yangu.”

 

 

Mathayo 12:31-32 “Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa. Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya MWANA WA ADAMU atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.”

 

Katika kiingereza wakati kwa Ezekiel wanatumia son of man au a son of man kwa Yesu linatumika neno The Son of Man, kwa Ezekiel ikimaanisha mwanadamu, na Kwa Yesu Kristo ikimaanisha Mwana wa Adamu, hii maana yake ni nini?  Huyu ni mwana wa Adamu wa Ahadi ambaye Adamu alikuwa ameahidiwa, kama ilivyokuwa kwa Abrahamu ambaye alikuwa ameahidiwa na Daudi ambaye naye alikuwa ameahidiwa, mwana huyu wa Ahadi aliyeahidiwa Adamu katika kitabu cha Mwanzo:-

 

Mwanzo 3:14-15 “BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.”

 

Ijapokuwa mwana huyu wa ahadi anaitwa uzao wa Mwanamke, lakini kwa uwazi kabisa alikuwa ni mtoto wa Adamu kwa hiyo Tangu wakati huu katika wazo la Adamu na wazo la Mwanamke walikuwa wanafahamu kuwa kuna moja ya mtoto wao ambaye atakuwa suluhisho la mgogoro kati yao na Shetani, Kwa hiyo alikuwa ni mtoto wa ahadi za kinabii, fahamu kuwa katika agano la kale mwanzoni kabisa hakukuwa na nabii na hivyo Mungu baba mwenyewe ndiye aliyekuwa nabii kwa Adamu na Eva na unabii wa kwanza ni Mwanzo 3:15 uzao wa mwanamke,

 

kwa hiyo Yesu alipokuwa akijiita mwana wa Adamu alikuwa akimaanisha mwana wa Ahadi wa Adamu, na Mwana wa Ahadi wa Abraham na mwana wa Ahadi wa Daudi, huyu kwa vyovyote vile angetokea katika mti wa uzao wa Adamu, mti wa uzao wa Ibrahimu na mti wa uzao wa Daudi. Kwa hiyo Yesu alipokuwa akijita Mwana wa Adamu alikuwa anamanisha mwana wa Ahadi wa Adamu ambaye Mungu alikuwa amemkusudia kwa ukombozi, hii ni moja ya sababu ya kujiita mwana wa Adamu, na ni mwana wa adamu ambaye atateseka angalia neno KUPONDA KISIGINO na kupitia maumivu haya ya kupondwa kisigino yeye atakomesha mateso kwa kumaliza uadui kati yetu na shetani angalia neno KUPONDA KICHWA.  Yesu alitumia jina Mwana wa Adamu mara nyingi sana akitaka akili za watu zifunguke na kumwangalia mtoto wa Adamu aliyeahidiwa unaona!

 

Sababu nyingine kubwa ya Msingi ya Yesu kujiita mwana wa Adamu ilikuwa ni maalumu sana akijilinganisha na Mwana wa Adamu aliyeuawa na Ndugu yake, Mwana huyu wa Adamu alikuwa mwenye haki, hakuwa na kosa lolote lakini aliuawa tu kwa sababu alipata kibali kwa Mungu, mwana huyu wa Adamu ni Habili, ambaye aliuawa na kaka yake Kaini,  kwa msingi huo mara kwa mara Yesu alipojiita mwana wa Adamu alikuwa maalumu anajidhihirisha kuwa Yeye ndiye yule Mwenye haki aliyeuawa katika mikono ya watu wabaya, Mwana huyu wa Adamu alimuuma sana Adamu, hasa damu yake ilipomwagika hii ndio picha halisi ambayo wanatheolojia wengi hawajawahi kuizungumzia, lakini Roho Mtakatifu alinifundisha kuwa Yesu anapojiita mwana wa Adamu kwa hakika alikuwa akimaanisha MTOTO WA ADAMU MWENYE HAKI ALIYEUAWA kwa mikono ya ndugu yake na wakati huo huo msisitizo ukiwa katika kuuawa kwake ambako kimsingi kunafanana na kuuawa kwa Habili,  tumeona maswala kadhaa kumuhusu Habili katika maandiko

 

Mtoto huyu wa Adamu alikuwa Mchungaji wa wanyama – Mwanzo 4:2 “Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.”      

 

Mtoto huyu wa Adamu alikubaliwa na Mungu kutokana na Sadaka yake - Mwanzo 4:4 “Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake;”

 

Mtoto huyu wa Adamu alisalitiwa na kuuawa na ndugu yake - Mwanzo 4:8-10 “Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua. BWANA akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.”

 

Mtoto huyu wa Adamu alikuwa mwenye haki - Mathayo 23:32-36 “Kijazeni basi kipimo cha baba zenu. Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji; hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu. Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.”

 

Mtoto huyu wa Adamu Damu yake ilidai haki - Waebrania 12:24 “na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.”

 

Mtoto huyu wa Adamu alikuwa tumaini la ukombozi wa Wazazi wake - Mwanzo 4:25-26 “Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, MUNGU AMENIWEKEA UZAO MWINGINE MAHALI PA HABILI; kwa sababu Kaini alimwua. Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la BWANA.”

 

Mtoto huyu wa Adamu alifanya matendo yake kwa Imani - Waebrania 11:4 “Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.”

 

Jambo hili Muhimu sana linalomuhusu Mwana huyu wa kipekee wa Adamu lina umuhimu mkubwa sana ukiunganisha na matukio yaliyomkuta Bwana wetu Yesu Kristo, Habili alichunga Kondoo, Yesu ndiye Mchungaji mwema, Habili alitoa sadaka iliyokubaliwa na Mungu, Na Yesu mjumbe wa Agano jipya aliyetoa damu inenayo mema kuliko ile ya Habili, Kuuawa kwake kulileta mtoto wa matumaini ambaye baada yake watu walianza kuliitia jina la bwana, ni baada ya kifo cha Yesu Kristo wanadamu wanapata nafasi ya kumfikia Mungu na kumuabudu pasipo hofu, Habili alikuwa mwenye haki, akauawa na ndugu yake, Na Yesu hakuwa na hatia akauawa na ndugu zake kwa hiyo kwa mujibu wa maelekezo niliyopewa mimi kama mkuu wa wajenzi, Mungu alinielekeza niieleze dunia leo, jambo ambalo wanazuoni na wanatheolojia huwa hawalielezei, au hawakuwa wamefunuliwa ya kuwa Yesu anapojiita mwana wa Adamu ni ukweli ulio wazi kuwa katika ubongo wake hakuna na wazo la mtu yule katika Daniel, wala wazo la Mtu yule katika Isaya, wala wazo la kutwaa mwili, wala hakuwa na wazo lingine zaidi ya wazo la mtoto wa Adamu aliyeuawa na ndugu yake akijitaja kama Yeye ambaye atauawa na Nduguze kwaajili ya ukombozi wa ulimwengu!

 

Wanatheolojia wengi wanamtumia Habil kama alama kivuli au unabii kuhusu Kristo na wanakubali kuwa kama Habili alivyouawa na ndugu yake na sababu kubwa ikiwa ni kwa sababu Habili alikuwa mwenye haki, kadhalika Kristo naye aliuawa na Ndugu zake wayahudi akiwa hana hatia, Mungu alimkabili Kaini akihoji Yuko wapi ndugu yako angalia

 

Mwanzo 4:10-11BWANA akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.”

 

Damu ya habili ililia kwaajili ya kutaka kisasi au haki, lakini Damu yake Yesu inalia kwaajili ya rehema na msamaha na wokovu, Waebrania 12:24 “na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.”

 

Waefeso 1:6-7 “Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa. Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.”

 

Kwa msingi huo utakubaliana nami kuwa kama Yesu alivyokuwa akisisitiza ni kwa mauti ya namna gani atauawa na katika dhana hiyo hiyo Yesu alikuwa akijiita Mwana wa Adamu, ni kama Yesu alikuwa akitaka makutano waelewe kuwa YEYE NDIYE HABILI WA PILI, na kama vile kifo hakikuweza kunyamazisha uhai wa Habili, kifo vilevile kimeshindwa kunyamazisha uhai wa Yesu Kristo. Nasisistiza tena na tena Yesu alipokuwa akijiita mwana wa Adamu alikuwa akimuwaza Habili akilini mwaka na kile ambacho wakuu wa makuhani wangemfanyia na kazi ya ukombozi ambayo angeikamilisha kwamkifo chake, aidha masikitiko na maneno ya Adamu alipomzaa Sethi aliposema MUNGU AMENIWEKEA UZAO MWINGINE MAHALI PA HABILI katika mtazamo finyu mtoto huyo ni SETHI na katika mtazamo mpana mtoto huyo ni YESU KRISTO, mtoto wa tumaini la Adamu lililopotea.

 

                       

 

Na Rev. Innocent Samuel Kamote

 

Mkuuu wa wajenzi mwenye Hekima

Jumatatu, 1 Januari 2024

Yesu ni Alpha na Omega !


Ufunuo 1:8 “Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.” Ufunuo 21:6 -7 “Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.” Ufunuo 22:13 “Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.”   



Utangulizi:

Leo ni sikukuu ya Mwaka mpya! Watu wengi sana chini bila kujali Imani yao, wanaungana na jamii kubwa ya watu duniani katika kuadhimisha sikukuu hii ya mwaka mpya, tunaposheherekea sikukuu hii yam waka mpya maana yake ni nini? Tunamshukuru Mungu kwamba tumemaliza siku za mwaka mmoja uliopita wenye, miezi 12, wiki 53, siku 365.25, Masaa 8760, dakika 525,600 na sekunde 31,536,000. Na tunafungua ukurasa wa mwaka mwingine ambao unaweza kuwa na muda unaofanana na huu, kwa kawaida hilo sio jambo dogo na kama tumepenya salama tuna kila sababu za kumshukuru Mungu, lakini vilevile kwa unyenyekevu mkubwa tunamuomba Mungu tena atupe uzima na kutusaidia kwa rehema zake na wema wake kuianza tena safari ndefu yenye wingi wa sekunde, dakika, masaa, masiku, mawiki, na hata miezi, Safari nzima hii hatuwezi kwenda kwa ujanja wetu na tunahitaji neema ya Mungu ya kutuongoza na kutusaidia

Katika siku hii muhimu ya Leo nimechagua kujikumbusha mimi pamoja na wafuatiliaji wangu kujifunza kwa kina na mapana na marefu kwa somo YESU NI ALPHA NA OMEGA tutajifunza somo hili muhimu kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-

·         Maana ya neno Alpha na Omega

·         Yesu Kristo ni Alpha na Omega

·         Jinsi ya kuanza mwaka na kumaliza na Yesu Kristo


Maana ya neno Alpha na Omega

Alpha na Omega ni matamshi ya Herufi ya kwanza na ya mwisho katika lugha ya Kigiriki (Kiyunani) kama vile katika kiswahili tunapotaja A na Z.  Herufi ya kwanza na kiyunani inatamkwa ALPHA na Herufi ya mwisho ya kiyunani inatamkwa OMEGA Ω zinapotajwa kwa pamoja maana yake ni mwanzo na mwisho, Hetrufi hizi zimekuwa maarufu sana, Mkuu w ancho yoyote anapoapishwa kuanza huduma ya utumishi wake Jeshi hujipanga kwa kumkaribisha katika umno la Alpha ambayo ni A na anapohitimisha Jeshi hujipanga kwa kumuaga kwa herufi  Omega  sawa na Herufi Z katika kiingereza na kiswahili na Herufi hizo vilevile zilitumiwa na marabi mbalimbali wa kiyahudi wakimaanisha mwanzo mpaka mwisho wa kitu au jambo Fulani, au jambo zima kuanzia mwanzio mpaka mwisho, Bwana Yesu analitumia neno hilo kujitambulisha kwa kanisa kuwa yeye ni Alfa na Omega akimaanisha mwanzo na mwisho, wakwanza na wa mwisho

Ufunuo 22:13 “Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.”

Hii inamanisha kuwa Yesu alikuwepo tangu mwanzo wa kuumbwa kwa ulimwengu na ataendelea kuwepo mpaka mwisho, yeye ni mwenye kushika majira na nyakati, anajua mwanzo wetu na anajua mwisho wetu, hii ni sawa tu na kusema MIMI NIKO AMBAYE NIKO hii inamaanisha kuwa Yesu ni wa milele na milele

Zaburi 90:1-2 “.Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi. Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.”

Yesu anapojitambulisha kwetu kama Alpha na Omega anamaanisha kuwa alikuweko tangu mwanzo na atakuwepo hata mwisho nah ii maana yake ni kuwa zaidi yake hakuna mwingine

Isaya 41:4 “Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, Bwana, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye.”

Isaya 44:6 “Bwana, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, Bwana wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.”

Isaya 48:11-12 “Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala sitampa mwingine utukufu wangu. Nisikilize mimi, Ee Yakobo; na Israeli, niliyekuita; mimi ndiye. Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho pia.”

Sifa hii ya kuwa mwanzo na mwisho ni sifa ya Mungu peke yake na utukufu huu hakuna mwingine anaweza kujigamba namna hiyo, kwa msingi huo Herufi Alpha na Omega zinafunua ukuu wa Yesu Kristo, mamlaka yake na nguvu zake katika maisha yote ya mwanadamu, anamiliki muda wa mkaisha yetu, na makusudi yote ya maisha yetu, anauwezo wa kuanza nasi na kumaliza nasi, anauwezo na mamlaka ya kuamua kuhusu maisha yetu yalikuwa vipi na yatakuwa vipi, kwa msingi huo tunapokuwa tumeumaliza mwaka uliopita na tunapouanza mwaka huu mpya hatuna budi kuhakikisha kuwa Alpha anakuwa pamoja nasi, na Omega anamaliza pamoja nasi, yawezekana katika mwaka uliopita kuna mambo yaliharibika, kuna mambo hayakwenda sawa lakini kwa kuwa Mungu amekupa neema kuvuka anza mwaka huu na Mungu mwenye mamlaka yote na nguvu zote ili aweze kukufanikisha, kabidhi njia zako zote kwake ili uweze kufanikiwa n ahata kama ulipita katika magumu kiasi gani kwa kuwa hujafa basi Mungu hajamaliza na wewe na hivyo kuna nafasi ya kuanza naye upya wakati huu tyunapoufungua mwaka huu mpya wa 2024 haleluyaaa!

Yesu kristo ndiye aliyeuumba ulimwengu, na kila kitu kilifanyika kwa yeye, na pasipo yeye hakuna kilichofanyika, aidha Yeye ndiye atakayeuhukumu ulimwengu hivyio anaujua mwisho wa Dunia na mwisho wa kila mtu na mwisho wa kila kitu  

Yohana 1:1-3 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.”

2Petro 3:10-13 “Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.”

Yeye ni mwanzo wa Sheria na Mwisho wa sharia, yeye ni kiongozi mkuu wa wokovu wetu, mwanzo na mwisho wa kila kitu na kila jambo katika maisha yetu, kuwa Alpha na Omega kwake Bwana wetu Yesu Kristo kunatupa uhakika ya kuwa hakuna mwanadamu, wala mchawi, wala malaika, wala mwenye mamlaka anayeweza kuamua jambo lolote au kukwamisha jambo lolote wala kuharibu jambo lolote ambalo Mungu amelikusudia katika maisha yetu, Yesu kuwa Alpha na Omega anaonyesha uwezo wake wote wa kushughulika na changamoto zetu zote na kuwa hakuna jambo lolote lililo gumu la kumshinda yeye, tunapoendelea kujifunza na kupata ufafanuzi kuhusu Yesu Kristo hususani mwanzo wa mwaka huu, kunatujengea msingi wa kumtegemea na kumtumaini yeye na kufanikiwa katika kila hatua ya maisha yetu ndani ya  waka huu.

Yesu Kristo ni Alpha na Omega

Yesu kuwa Alpha na Omega kuna maana ya kuwa yeye ni Herufi A mpaka Z, kuna maanisha yeye ana sifa zote zinazoweza kupatikana katika kila Herufi ya maisha za maandishi yetu kwaajili ya faida zetu za kiwmili na kiroho sawasawa na maandiko, katika eneo hili nataka tujifunze kwa kina na mapana na marefu namna na jinsi kila Herufi A mpaka Z zinavyomuelezea Yesu Kristo kwa Faida ya maisha yetu kimwili na kiroho

AYesu ni Alpha  Ni mwanzilishi wa kila kitu kilicho chema katika maisha ya mwanadamu, Ni mwanzilishi wa Imani yetu na mkamilishaji pia Waebrania 12:2 “tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.” Aidha yeye ni Arabuni ya roho zetu Waefeso 1:14 “Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.” Neno Arabuni linalotumika hapa maana yake ni Hakikisho, au garantii, ni kama muhuri wa uhakikisho kuwa sisi ni mali ya Mungu, Mungu anapotuokoa hatuachi hivi hivi anatupa uhakika mioyoni mwetu kupitia roho wake Mtakatifu kuwa sisi ni mali yake 2Wakorintho 1:21-22 “Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu, naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.” Kwa hiyo Mungu anapoianza safari anatupa uhakika na kututhibitishia kuwa atamaliza pamoja nasi Yesu ni A ni Arabuni ya roho zetu, Afya yetu, Imani yetu, safari yetu zitakuwa za uhakika kama tutaanza na Yesu ili tuweze kukamilisha salama pia

Yesu ni A –  Afya ya uso wangu - Zaburi 42:5 “Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.”

Yesu ni A – Afya ya uso wangu – Zaburi 42:11 “Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.”

Yesu ni A – Ahadi ya Uzima – 2Timotheo 1:1 “Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa ajili ya ahadi ya uzima ulio katika Kristo Yesu;”               

Yesu ni A – Aliye juu – Zaburi 46:4 “Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu

Yesu ni A – Aliyeko, Aliyekuwako na Atakayekuja – Ufunuo 1:8 “Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”

B - Yesu ni Bwana wa Mabwana Yeye anatajwa kama Bwana wa Mabwana na Mfalme wa wafalme 

Ufunuo 17:14 “Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu” ,

Yesu ni B – Bwana wa Mabwana - Ufunuo 19:16 “Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.,

Yesu ni B – Bwana Mkubwa Luka 5:5   Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.”

Yesu ni B - Baraka ya Bwana Kumbukumbu 33:23Na Naftali akamnena, Ee Naftali, uliyeshiba fadhili, Uliyejawa na BARAKA YA BWANA; Umiliki magharibi na kusini.”

Yesu ni B – Bwana wa Vita - Bwana wa vita Kutoka 15:3 BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake.”

Yoshua 10:14Haikuwapo siku nyingine mfano wa siku hiyo katika siku zilizotangulia mbele yake wala katika hizo zilizoandama baada yake, hata ikawa yeye Bwana kuisikia sauti ya binadamu; kwa kuwa Bwana alipiga vita kwa ajili ya Israeli.”                

C - Yesu ni Chakula cha uzima – Yohana 6:48-58 “Mimi ndimi chakula cha uzima. Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa. Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife. Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule? Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi. Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele. “

Yesu ni chipukizi la haki – Yeremia 23:5-6 “Tazama siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi. Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu”.

Yesu Kristo ni Chemichemi ya uzima – Zaburi 36:9 “Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima, Katika nuru yako tutaona nuru.”

Yesu Kristo ni Chanda cha Mungu – Kutoka 8:19 “Ndipo wale waganga wakamwambia Farao, Jambo hili ni chanda cha Mungu; na moyo wake Farao ukawa mgumu asiwasikize; vile vile kama BWANA alivyonena.”

Yesu Kristo ni Chapa ya Nafsi ya Mungu – Waebrania 1:3 “Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;”

D - Yesu Kristo anatajwa katika maandiko kuwa dhabihu yetu, kwaajili ya dhambi zetu, ona Waebrania 9:23-26 “Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo. Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu; wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake; kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake.”

Isaya 53:10 “Lakini Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake;”

 

E - Yesu Kristo anatajwa katika maandiko kama Elimu ya utukufu wa Mungu 2Wakorintho 4:6 “Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.”        

Elishadai yaani Mungu mwenye nguvu Mwanzo 17:1-2 “Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, (El Shaddai)  uende mbele yangu, ukawe mkamilifu. Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.”

Mwanzo 35:11 “Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, (El Shaddai) uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako.”      

F - Yesu Kristo ni Faraja Yetu 2Wakorintho 1:3-7 “Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu. Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo. Lakini ikiwa sisi tu katika dhiki, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu; au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu; ambayo hutenda kazi yake kwa kustahimili mateso yale yale tuteswayo na sisi. Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja.”

Yesu ni Fadhili za Mungu – Zaburi 57:3 “Atapeleka toka mbinguni na kuniokoa, Atukanapo yule atakaye kunimeza. Mungu atazipeleka Fadhili zake na kweli yake

Yesu ni Fahari ya Yakobo – Zaburi 47:4 “Atatuchagulia urithi wetu, Fahari ya Yakobo ambaye alimpenda.”

Yesu ni Faraja Yetu, Faraja ya Israel – Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.”

Yesu ni Fimbo ya Mungu – Kutoka 4:20 “Basi Musa akamchukua mkewe na wanawe, na kuwapandisha juu ya punda, naye akarudi mpaka nchi ya Misri; na Musa AKAICHUKUA ILE FIMBO YA MUNGU mkononi mwake.”     

Yesu ni Furaha ya Bwana – Nehemia 8:10 “Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu.”

G  Tumaini lililowekwa ndani yetu linatufanya tuwe na uso wa Imani na matumaini uso mgumu kama gume gume, Yesu alikuwa na Moyo wa gume gume akaweza kuvumilia mateso na dhihaka zote  Isaya 50:7-8  Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya. Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu; ni nani atakayeshindana nami? Na tusimame pamoja; ni nani aliye hasimu yangu? Na anikaribie basi.” 

Ayubu 28:9 “Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake; Huipindua milima hata misingi yake.”

Yeye ni Mwamba wa Gume gume kumbukumbu 32:12-13 “Bwana peke yake alimwongoza, Wala hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye. Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka, Naye akala mazao ya mashamba; Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini, Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume;”

H – Maandiko yanamtaja Yesu kama haki yetu  Yeremia 23:5-6 “Tazama siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi. Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.”

I – Maandiko yanamtaja Yesu kama Immanuel yaani Mungu Pamoja nasi Isaya 7:14  Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.”               

Mathayo 1:21-23. “Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.”   

Yesu ni Ishara Itakayonenwa - Luka 2: 34 “Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa.”

J -  Yesu Kristo ni Jiwe kuu la Pembeni  Isaya 28:16-17 “kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka. Nami nitafanya hukumu kuwa ndiyo kanuni, na haki kuwa ndiyo timazi; na mvua ya mawe itachukulia mbali hilo kimbilio la maneno ya uongo, na maji yatapagharikisha mahali pa kujisitiri.”

1Petro 2:4-6 “Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.”

Pia Yesu ana jina lile lipitalo majina yote Wafilipi 2:9-11 “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”  

Yesu ni Jiwe lililohai – 1Petro 2:4Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.”           

K - Yesu anatajwa kama Kiongozi mkuu wa wokovu wetu – Waebrania 2:10 “Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso.”

Kimbilio letu – Zaburi 46:1-2 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.”

Unapomkimbilia Mungu wetu unakuwa salama Mithali 18:10 “Jina la Bwana ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.”

Yesu ni kichwa cha Kanisa - kichwa cha kanisa Waefeso 5;23 “Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.”

Yesu ni kuhani wetu mkuu - Waebrania 7:17 “Maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki.”; Waebrania 10;21 “na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu;”

Yesu ni Kweli – Yohana 14:6 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”

L – Yesu anatajwa kama lulu moja ya thamani Mathayo 13:45-46 “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua.”             

M – Mchungaji mwema – Yohana 10:11-14 “Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya.Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake.Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;            

Mlango wa kondoo Yohana 10:9 “Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.”

Moto ulao – Waebrania 12:28-29 “Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho; maana Mungu wetu ni moto ulao.”

Mungu mwenye, Nguvu na Msahauri wa Ajabu na Mfalme wa Amani Isaya 9:6-7 “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo.”

Maji ya uzima Yohana 4:10-13 “Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai. Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai? Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake? Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;”

Mkate wa uzima – Yohana 6:35 “Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.”

Mfinyanzi - Yeremia 18;2-6 – “Ondoka, ukashuke mpaka nyumba ya mfinyanzi, na huko nitakusikizisha maneno yangu.Basi nikashuka mpaka nyumba ya mfinyanzi, na tazama, alikuwa akifanya kazi yake kwa magurudumu.Na chombo kile, alichokuwa akikifinyanga, kilipoharibika mkononi mwake yule mfinyanzi, alikifanyiza tena kuwa chombo kingine, kama alivyoona vema yule mfinyanzi kukifanya. Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema, Ee nyumba ya Israeli, je! Siwezi mimi kuwatendea ninyi vile vile kama mfinyanzi huyu alivyotenda? Asema Bwana. Angalieni, kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo mlivyo ninyi katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli.”         

Mungu mkuu - Tito 2;13 “tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;”       

Mwana wa Mungu - Yohana 9;35-37 “Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu? Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini?  Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye.”

Mwana wa Adamu - Mathayo 26;64 “Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.”         

Mwokozi - Tito 1;4,kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tuishirikiyo. Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu.”

Mwalimu Yohana 3:2 “Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.”

Muhukumu wetu siku ya mwisho Yohana 5;22 “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote;”

N – Yesu ni njia na kweli na Uzima  Yohana 14:6 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”

Neno la Mungu – Yohana 1:1-3 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.”

Nabii yule  - Yohana 6;14 “Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni”.    

Nyota ya kung’aa asubuhi - Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.”

Nuru ya ulimwengu - Yohana 8;12 “ Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”              

O – Yesu ni Ondoleo la dhambi zetu tukimuamini, tukitubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha Matendo 2:38-39 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”

P – Yesu ni udhihirisho wa Pendo la Mungu Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”

Pazia la hekalu – Mathayo 27:51-54 “Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi. Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”               

Q – Quail (Kware kutoka Mbinguni) Zaburi 105:40-42 “Walipotaka akaleta kware, Akawashibisha chakula cha mbinguni. Akaufunua mwamba, kukabubujika maji, Yakapita pakavuni kama mto. Maana alilikumbuka neno Lake Takatifu, Na Ibrahimu, mtumishi wake.”             

R – Yesu Kristo ni Rafiki Yohana 15:14-16 “Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.” Tunaweza kuwa na urafiki na Yesu kama Mungu baba alivyokuwa na urafiki na Abrahamu kwa sababu ya utii, yaani kama tutayatenda anayotuamuru na ni rahisi tu Yesu ametuamuru kupenda.

S - Simba wa Kabila la Yuda - Ufunuo 5:4-5 “Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.”

Shahidi mwaminifu – Ufunuo 1:5-6 “tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake, na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina.”

Shina la Daudi - Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.”    

T – Yesu ni Tabibu wa ajabu, amekuja kwaajili ya wale wasio na afya Mathayo 9:11-12 “Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.”

Tumaini letu kuu - Zaburi 71;5 “Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu.”

Taraja letu - Zaburi 71;5 “Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu.”

Tegemeo letu - Yeremia 17;5-8. “Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.”    

U – Upendo wa Mungu 1Yohana 15:13 “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.”

V – Vazi la wokovu wetu Isaya 61:10 “Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.”

W – Yesu ni wokovu wetu ni mwamba wa wokovu wetu Zaburi 95:1-2 “Njoni, tumwimbie Bwana, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu. Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi.”

X – X rays – Mwali wa moto  2Wathesalonike 1:6-8 “Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi; na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu;”

Ufunuo 19:11-13 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.”

Y-  Yesu ni Yeye yule jana leo n ahata milele Waebrania 13:8  Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.”

Z – Zeri ya Gileadi – Dawa isiyoshindwa Yeremia 8:22 “Je! Hapana zeri katika Gileadi? Huko hakuna tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya ya binti ya watu wangu?” yalikuwa ni mafuta maalumu yanayotokana na mmea maalumu unaoitwa zeri ambapo katika nyakati zile matabibu waliutumia kutibu hususani mtu ambaye ameshindikana kutibiwa kwa dawa ya aina nyingine yoyote, Dawa hii kinabii ilikuwa inamtaja Yesu ambaye mtu aliposhindikana kutibiwa na matabibu wengine wote yeye aliweza kutibu, Marko 5:25-29 “Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona. Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule.”

 

Jinsi ya kuanza mwaka na kumaliza na Yesu Kristo

Yesu ni Alpha na Omega maana yake yeye ni mwanzo na mwisho, na pia ana uwezo wa kushughulikia kila jambo katika kila Nyanja ya maisha yetu ya kila siku, Lakini sio hivyo tu tunapokaribia wakati huu wa msimu wa sikukuu yam waka mpya ni muhimu kwetu kukumbuka kuwa sio tu kwamba tunasheherekea mwaka mpya lakini vilevile ni ukweli usiopingika kwamba miaka yetu na siku zetu za kuwepo duniani zinahesabika na kupungua, kwa msingi huo ni lazima tujipange kwa upya na kuhakikisha kuwa TUnashikamana na Yeye aliye Alpha na omega yaani mwamnzo na mwisho wa kila kitu katika maisha yetu na hivyo hatuna budi kumuomba Mungu

1.       Atupe hekima ya kuutumia wakati, yaani sekunde, dakika, saa, siku, wiki, miezi na miaka ijayo kama zawadi ya tahamni sana ili tuweze kuacha alama katika kusudi lile alilotuitia Zaburi 90:12 “Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima.” Muda ni moja ya zawadi kubwa nay a thamani ambayo Mungu ametupa tujifunze kutokupoteza muda, kukemea na kukataa uvivu, umasikini, magonjwa na kila jambo linaloturudisha nyuma kiroho, tusikubali kupoa, tusikubali kurudia makossa, tusikubali kulegea bali tusonge mbele katika wito huu ambao Mungu ametuitia Waefeso 5:15- 16. “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.”

 

2.       Tumia muda wako Mwingi kuwa na Mungu, tunaweza kumkaribia Mungu kwa kujitoa binafsi kwake kwa Maombi, kusoma neno la Mungu, kusikiliza mahubiri, kujumuika katika makusanyiko ya ibada lakini zaidi sana kuutafuta suo wa Mungu kuliko kubwa busy na makundi ya watu Mathayo 14:22-23 “Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano. Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.”

 

 

3.       Mtumaini Bwana – Tumejifunza kuwa Yesu ni Alfa na Omega kwa msingi huo katika mipango yetu yote hatuna budi kuhakikisha kuwa tunamtumaini yeye kwani ni yeye pekee mwenye mwenye uwezo wa kunyoosha mapito yetu yote, Mithali 3:5-6.  Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.”

 

4.       Mfanye Yesu kuwa kiini cha Maisha yako na mipango yako yote – Yesu ni Alfa na Omega tumeweza kujifunza kuwa yeye ni mwamba katika kila Nyanja ya maisha yetu, hatuna budi kuhakikisha kuwa kila jambo tulifanyalo, tunalifanya kwa utukufu wake, tumfanye yeye kuwa kiini kikuu cha maisha yetu na mipango yetu,  hakkisha kuwa unakanyaga mwana na Bwana na kuendelea kuwa na uhusiano naye mwanzo mwisho Mungu atatubariki, linapokusibu lililo gumu kumbuka Alfa na Omega anaweza kuingilia katika katika kila eneo la maisha yetu kulingana na uhitaji wetu.

 

Na. Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima