Ufunuo 1:8 “Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo
na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”
Ufunuo 21:6 -7 “Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni
Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya
maji ya uzima, bure. Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake,
naye atakuwa mwanangu.” Ufunuo 22:13 “Mimi
ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.”
Utangulizi:
Leo ni sikukuu ya Mwaka mpya! Watu
wengi sana chini bila kujali Imani yao, wanaungana na jamii kubwa ya watu
duniani katika kuadhimisha sikukuu hii ya mwaka mpya, tunaposheherekea sikukuu
hii yam waka mpya maana yake ni nini? Tunamshukuru Mungu kwamba tumemaliza siku
za mwaka mmoja uliopita wenye, miezi 12,
wiki 53, siku 365.25, Masaa 8760, dakika 525,600 na sekunde 31,536,000. Na
tunafungua ukurasa wa mwaka mwingine ambao unaweza kuwa na muda unaofanana na
huu, kwa kawaida hilo sio jambo dogo na kama tumepenya salama tuna kila sababu
za kumshukuru Mungu, lakini vilevile kwa unyenyekevu mkubwa tunamuomba Mungu
tena atupe uzima na kutusaidia kwa rehema zake na wema wake kuianza tena safari
ndefu yenye wingi wa sekunde, dakika, masaa, masiku, mawiki, na hata miezi,
Safari nzima hii hatuwezi kwenda kwa ujanja wetu na tunahitaji neema ya Mungu
ya kutuongoza na kutusaidia
Katika siku hii muhimu ya Leo
nimechagua kujikumbusha mimi pamoja na wafuatiliaji wangu kujifunza kwa kina na
mapana na marefu kwa somo YESU NI ALPHA
NA OMEGA tutajifunza somo hili muhimu kwa kuzingatia vipengele vitatu
vifuatavyo:-
·
Maana ya
neno Alpha na Omega
·
Yesu
Kristo ni Alpha na Omega
·
Jinsi ya
kuanza mwaka na kumaliza na Yesu Kristo
Maana ya neno Alpha na Omega
Alpha na Omega ni matamshi ya Herufi ya kwanza na ya mwisho katika
lugha ya Kigiriki (Kiyunani) kama
vile katika kiswahili tunapotaja A na
Z. Herufi ya kwanza na kiyunani
inatamkwa ALPHA na Herufi ya mwisho ya kiyunani inatamkwa OMEGA Ω zinapotajwa kwa pamoja maana yake ni mwanzo
na mwisho, Hetrufi hizi zimekuwa maarufu sana, Mkuu w ancho yoyote anapoapishwa
kuanza huduma ya utumishi wake Jeshi hujipanga kwa kumkaribisha katika umno la
Alpha ambayo ni A na anapohitimisha Jeshi hujipanga kwa kumuaga kwa herufi Omega
sawa na Herufi Z katika kiingereza na kiswahili na Herufi hizo
vilevile zilitumiwa na marabi mbalimbali wa kiyahudi wakimaanisha mwanzo mpaka
mwisho wa kitu au jambo Fulani, au jambo zima kuanzia mwanzio mpaka mwisho,
Bwana Yesu analitumia neno hilo kujitambulisha kwa kanisa kuwa yeye ni Alfa na
Omega akimaanisha mwanzo na mwisho, wakwanza na wa mwisho
Ufunuo 22:13 “Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo
na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.”
Hii inamanisha kuwa Yesu
alikuwepo tangu mwanzo wa kuumbwa kwa ulimwengu na ataendelea kuwepo mpaka
mwisho, yeye ni mwenye kushika majira na nyakati, anajua mwanzo wetu na anajua
mwisho wetu, hii ni sawa tu na kusema
MIMI NIKO AMBAYE NIKO hii inamaanisha kuwa Yesu ni wa milele na milele
Zaburi 90:1-2 “.Wewe, Bwana, umekuwa makao
yetu, Kizazi baada ya kizazi. Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia,
Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.”
Yesu anapojitambulisha kwetu kama
Alpha na Omega anamaanisha kuwa
alikuweko tangu mwanzo na atakuwepo hata mwisho nah ii maana yake ni kuwa zaidi
yake hakuna mwingine
Isaya 41:4 “Ni nani aliyetenda na kufanya
jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, Bwana, wa kwanza na wa mwisho,
mimi ndiye.”
Isaya 44:6 “Bwana, Mfalme wa Israeli,
Mkombozi wako, Bwana wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa
mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.”
Isaya 48:11-12 “Kwa ajili ya nafsi yangu,
kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala
sitampa mwingine utukufu wangu. Nisikilize mimi, Ee Yakobo; na Israeli, niliyekuita;
mimi ndiye. Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho pia.”
Sifa hii ya kuwa mwanzo na mwisho
ni sifa ya Mungu peke yake na utukufu huu hakuna mwingine anaweza kujigamba
namna hiyo, kwa msingi huo Herufi Alpha
na Omega zinafunua ukuu wa Yesu Kristo, mamlaka yake na nguvu zake katika
maisha yote ya mwanadamu, anamiliki muda wa mkaisha yetu, na makusudi yote ya
maisha yetu, anauwezo wa kuanza nasi na kumaliza nasi, anauwezo na mamlaka ya
kuamua kuhusu maisha yetu yalikuwa vipi na yatakuwa vipi, kwa msingi huo
tunapokuwa tumeumaliza mwaka uliopita na tunapouanza mwaka huu mpya hatuna budi
kuhakikisha kuwa Alpha anakuwa pamoja nasi, na Omega anamaliza pamoja nasi,
yawezekana katika mwaka uliopita kuna mambo yaliharibika, kuna mambo hayakwenda
sawa lakini kwa kuwa Mungu amekupa neema kuvuka anza mwaka huu na Mungu mwenye
mamlaka yote na nguvu zote ili aweze kukufanikisha, kabidhi njia zako zote
kwake ili uweze kufanikiwa n ahata kama ulipita katika magumu kiasi gani kwa
kuwa hujafa basi Mungu hajamaliza na wewe na hivyo kuna nafasi ya kuanza naye
upya wakati huu tyunapoufungua mwaka huu mpya wa 2024 haleluyaaa!
Yesu kristo ndiye aliyeuumba
ulimwengu, na kila kitu kilifanyika kwa yeye, na pasipo yeye hakuna
kilichofanyika, aidha Yeye ndiye atakayeuhukumu ulimwengu hivyio anaujua mwisho
wa Dunia na mwisho wa kila mtu na mwisho wa kila kitu
Yohana 1:1-3 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno,
naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako
kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote
kilichofanyika.”
2Petro 3:10-13 “Lakini siku ya Bwana
itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na
viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani
yake zitateketea. Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa
ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia
hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu
zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? Lakini,
kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa
ndani yake.”
Yeye ni mwanzo wa Sheria na
Mwisho wa sharia, yeye ni kiongozi mkuu wa wokovu wetu, mwanzo na mwisho wa
kila kitu na kila jambo katika maisha yetu, kuwa Alpha na Omega kwake Bwana
wetu Yesu Kristo kunatupa uhakika ya kuwa hakuna mwanadamu, wala mchawi, wala
malaika, wala mwenye mamlaka anayeweza kuamua jambo lolote au kukwamisha jambo
lolote wala kuharibu jambo lolote ambalo Mungu amelikusudia katika maisha yetu,
Yesu kuwa Alpha na Omega anaonyesha uwezo wake wote wa kushughulika na
changamoto zetu zote na kuwa hakuna jambo lolote lililo gumu la kumshinda yeye,
tunapoendelea kujifunza na kupata ufafanuzi kuhusu Yesu Kristo hususani mwanzo
wa mwaka huu, kunatujengea msingi wa kumtegemea na kumtumaini yeye na
kufanikiwa katika kila hatua ya maisha yetu ndani ya waka huu.
Yesu Kristo ni Alpha na Omega
Yesu kuwa Alpha na Omega kuna
maana ya kuwa yeye ni Herufi A mpaka Z, kuna maanisha yeye ana sifa zote
zinazoweza kupatikana katika kila Herufi ya maisha za maandishi yetu kwaajili
ya faida zetu za kiwmili na kiroho sawasawa na maandiko, katika eneo hili
nataka tujifunze kwa kina na mapana na marefu namna na jinsi kila Herufi A
mpaka Z zinavyomuelezea Yesu Kristo kwa Faida ya maisha yetu kimwili na kiroho
A – Yesu ni Alpha Ni mwanzilishi wa kila kitu kilicho chema
katika maisha ya mwanadamu, Ni mwanzilishi wa Imani yetu na mkamilishaji pia Waebrania 12:2 “tukimtazama
Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya
furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye
ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.” Aidha yeye ni
Arabuni ya roho zetu Waefeso 1:14 “Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi
wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.” Neno Arabuni linalotumika
hapa maana yake ni Hakikisho, au garantii, ni kama muhuri wa uhakikisho kuwa
sisi ni mali ya Mungu, Mungu anapotuokoa hatuachi hivi hivi anatupa uhakika
mioyoni mwetu kupitia roho wake Mtakatifu kuwa sisi ni mali yake 2Wakorintho 1:21-22 “Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na
kututia mafuta, ni Mungu, naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho
mioyoni mwetu.” Kwa hiyo Mungu anapoianza safari anatupa uhakika na
kututhibitishia kuwa atamaliza pamoja nasi Yesu ni A ni Arabuni ya roho zetu,
Afya yetu, Imani yetu, safari yetu zitakuwa za uhakika kama tutaanza na Yesu
ili tuweze kukamilisha salama pia
Yesu ni A – Afya ya uso wangu - Zaburi 42:5 “Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu?
Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu
wangu.”
Yesu ni A – Afya ya uso wangu – Zaburi 42:11
“Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani
yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na
Mungu wangu.”
Yesu ni A – Ahadi ya Uzima – 2Timotheo 1:1 “Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa
ajili ya ahadi ya uzima ulio katika Kristo Yesu;”
Yesu ni A – Aliye juu – Zaburi 46:4 “Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu,
Patakatifu pa maskani zake Aliye juu”
Yesu ni A – Aliyeko, Aliyekuwako na
Atakayekuja – Ufunuo 1:8 “Mimi ni Alfa na Omega,
mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja,
Mwenyezi.”
B - Yesu ni Bwana wa Mabwana Yeye anatajwa kama
Bwana wa Mabwana na Mfalme wa wafalme
Ufunuo 17:14 “Hawa
watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni
Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa,
na wateule, na waaminifu” ,
Yesu ni B – Bwana wa Mabwana - Ufunuo 19:16
“Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja
lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.,”
Yesu ni B – Bwana Mkubwa Luka 5:5 “Simoni akajibu
akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate
kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.”
Yesu ni B - Baraka ya Bwana Kumbukumbu 33:23 “Na Naftali
akamnena, Ee Naftali, uliyeshiba fadhili, Uliyejawa na BARAKA YA BWANA; Umiliki
magharibi na kusini.”
Yesu ni B – Bwana wa Vita - Bwana wa
vita Kutoka 15:3 “BWANA ni mtu wa
vita, BWANA ndilo jina lake.”
Yoshua 10:14 “Haikuwapo siku nyingine mfano wa
siku hiyo katika siku zilizotangulia mbele yake wala katika hizo zilizoandama
baada yake, hata ikawa yeye Bwana kuisikia sauti ya binadamu; kwa kuwa Bwana
alipiga vita kwa ajili ya Israeli.”
C - Yesu ni Chakula cha uzima – Yohana 6:48-58
“Mimi ndimi chakula cha uzima. Baba zenu waliila
mana jangwani; wakafa. Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu
akile wala asife. Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni;
mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili
wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao
wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule? Basi Yesu akawaambia,
Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu
yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao
uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni
chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na
kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Kama vile Baba
aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila
atakuwa hai kwa mimi. Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama
mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele. “
Yesu ni chipukizi la haki – Yeremia 23:5-6
“Tazama siku zinakuja, asema Bwana,
nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa
hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi. Katika siku zake Yuda
ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana
ni haki yetu”.
Yesu Kristo ni Chemichemi ya uzima – Zaburi
36:9 “Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima,
Katika nuru yako tutaona nuru.”
Yesu Kristo ni Chanda cha Mungu – Kutoka 8:19
“Ndipo wale waganga wakamwambia Farao, Jambo hili
ni chanda cha Mungu; na moyo wake Farao ukawa mgumu asiwasikize; vile vile kama
BWANA alivyonena.”
Yesu Kristo ni Chapa ya Nafsi ya Mungu –
Waebrania 1:3 “Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu
wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha
kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;”
D - Yesu Kristo anatajwa katika maandiko kuwa
dhabihu yetu, kwaajili ya dhambi zetu, ona Waebrania 9:23-26 “Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni
zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu
zilizo bora kuliko hizo. Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu
palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia
mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu; wala si kwamba
ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu kila
mwaka kwa damu isiyo yake; kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu
kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa
nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake.”
Isaya 53:10 “Lakini
Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu
kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana
yatafanikiwa mkononi mwake;”
E - Yesu Kristo anatajwa katika maandiko kama
Elimu ya utukufu wa Mungu 2Wakorintho 4:6 “Kwa kuwa
Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu,
atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.”
Elishadai yaani Mungu mwenye nguvu Mwanzo
17:1-2 “Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na
kenda, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, (El
Shaddai) uende mbele yangu, ukawe
mkamilifu. Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha
sana sana.”
Mwanzo 35:11 “Mungu
akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, (El Shaddai) uzidi ukaongezeke. Taifa na
kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako.”
F - Yesu Kristo ni Faraja Yetu 2Wakorintho
1:3-7 “Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu
Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; atufarijiye katika dhiki zetu
zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa
faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu. Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo
yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo. Lakini
ikiwa sisi tu katika dhiki, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu; au
ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu; ambayo hutenda kazi yake kwa
kustahimili mateso yale yale tuteswayo na sisi. Na tumaini letu kwa ajili yenu
ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo
hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja.”
Yesu ni Fadhili za Mungu – Zaburi 57:3 “Atapeleka toka mbinguni na kuniokoa, Atukanapo yule
atakaye kunimeza. Mungu atazipeleka Fadhili zake na kweli yake”
Yesu ni Fahari ya Yakobo – Zaburi 47:4 “Atatuchagulia urithi wetu, Fahari ya Yakobo ambaye
alimpenda.”
Yesu ni Faraja Yetu, Faraja ya Israel –
Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na
mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja
ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.”
Yesu ni Fimbo ya Mungu – Kutoka 4:20 “Basi Musa akamchukua mkewe na wanawe, na kuwapandisha juu
ya punda, naye akarudi mpaka nchi ya Misri; na Musa AKAICHUKUA ILE FIMBO YA
MUNGU mkononi mwake.”
Yesu ni Furaha ya Bwana – Nehemia 8:10 “Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na
kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku
hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni
nguvu zenu.”
G – Tumaini
lililowekwa ndani yetu linatufanya tuwe na uso wa Imani na matumaini uso mgumu
kama gume gume, Yesu alikuwa na Moyo wa gume gume akaweza kuvumilia mateso na
dhihaka zote Isaya 50:7-8
“Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu
hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami najua
ya kuwa sitaona haya. Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu; ni nani
atakayeshindana nami? Na tusimame pamoja; ni nani aliye hasimu yangu? Na
anikaribie basi.”
Ayubu 28:9 “Huunyoshea
mwamba wa gumegume mkono wake; Huipindua milima hata misingi yake.”
Yeye ni Mwamba wa Gume gume kumbukumbu 32:12-13
“Bwana peke yake alimwongoza, Wala hapakuwa na mungu
mgeni pamoja naye. Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka, Naye akala mazao ya
mashamba; Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini, Na mafuta yaliyotoka katika
mwamba wa gumegume;”
H – Maandiko yanamtaja Yesu kama haki yetu Yeremia 23:5-6 “Tazama
siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye
atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika
nchi. Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake
atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.”
I – Maandiko yanamtaja Yesu kama Immanuel yaani
Mungu Pamoja nasi Isaya 7:14 “Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira
atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.”
Mathayo 1:21-23. “Naye
atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa
watu wake na dhambi zao.Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na
Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa
mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.”
Yesu ni Ishara Itakayonenwa - Luka 2: 34 “Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake,
Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na
kuwa ishara itakayonenewa.”
J - Yesu
Kristo ni Jiwe kuu la Pembeni Isaya
28:16-17 “kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema
hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe
la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.
Nami nitafanya hukumu kuwa ndiyo kanuni, na haki kuwa ndiyo timazi; na mvua ya
mawe itachukulia mbali hilo kimbilio la maneno ya uongo, na maji yatapagharikisha
mahali pa kujisitiri.”
1Petro 2:4-6 “Mmwendee
yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule,
lenye heshima. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho,
ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya
Yesu Kristo.Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni
jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.”
Pia Yesu ana jina lile lipitalo majina yote
Wafilipi 2:9-11 “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha
mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti
lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila
ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”
Yesu ni Jiwe lililohai – 1Petro 2:4 “Mmwendee yeye,
jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye
heshima.”
K - Yesu anatajwa kama Kiongozi mkuu wa wokovu
wetu – Waebrania 2:10 “Kwa kuwa ilimpasa yeye,
ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana
wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya
mateso.”
Kimbilio letu – Zaburi 46:1-2 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada
utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,
Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.”
Unapomkimbilia Mungu wetu unakuwa salama
Mithali 18:10 “Jina la Bwana ni ngome imara; Mwenye
haki huikimbilia, akawa salama.”
Yesu ni kichwa cha Kanisa - kichwa cha kanisa Waefeso 5;23 “Kwa
maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni
mwokozi wa mwili.”
Yesu ni kuhani wetu mkuu - Waebrania 7:17 “Maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano
wa Melkizedeki.”; Waebrania 10;21 “na kuwa
na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu;”
Yesu ni Kweli – Yohana 14:6 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu
haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”
L – Yesu anatajwa kama lulu moja ya thamani Mathayo
13:45-46 “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na
mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; naye alipoona lulu moja ya thamani
kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua.”
M – Mchungaji mwema – Yohana 10:11-14 “Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai
wake kwa ajili ya kondoo.Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si
mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na
mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya.Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara;
wala mambo ya kondoo si kitu kwake.Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu
nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; “
Mlango wa kondoo Yohana 10:9 “Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka;
ataingia na kutoka, naye atapata malisho.”
Moto ulao – Waebrania 12:28-29 “Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na
mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na
unyenyekevu na kicho; maana Mungu wetu ni moto ulao.”
Mungu mwenye, Nguvu na Msahauri wa Ajabu na
Mfalme wa Amani Isaya 9:6-7 “Maana kwa ajili yetu
mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani
mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa
milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe,
Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa
hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio
utakaotenda hayo.”
Maji ya uzima Yohana 4:10-13 “Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya
Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye
angalikupa maji yaliyo hai. Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha
kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai? Je!
Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe
akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake? Yesu akajibu, akamwambia,
Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;”
Mkate wa uzima – Yohana 6:35 “Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa
kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.”
Mfinyanzi - Yeremia 18;2-6 – “Ondoka, ukashuke mpaka nyumba ya mfinyanzi, na huko nitakusikizisha
maneno yangu.Basi nikashuka mpaka nyumba ya mfinyanzi, na tazama, alikuwa akifanya
kazi yake kwa magurudumu.Na chombo kile, alichokuwa akikifinyanga,
kilipoharibika mkononi mwake yule mfinyanzi, alikifanyiza tena kuwa chombo
kingine, kama alivyoona vema yule mfinyanzi kukifanya. Ndipo neno la Bwana
likanijia, kusema, Ee nyumba ya Israeli, je! Siwezi mimi kuwatendea ninyi vile
vile kama mfinyanzi huyu alivyotenda? Asema Bwana. Angalieni, kama udongo
ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo mlivyo ninyi katika mkono wangu, Ee
nyumba ya Israeli.”
Mungu mkuu - Tito 2;13 “tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu
wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;”
Mwana wa Mungu - Yohana 9;35-37 “Yesu
akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa
Mungu? Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema
nawe ndiye.”
Mwana wa Adamu - Mathayo 26;64 “Yesu
akamwambia, Wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa
Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.”
Mwokozi - Tito 1;4, “kwa Tito, mwanangu hasa katika
imani tuishirikiyo. Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa
Kristo Yesu Mwokozi wetu.”
Mwalimu Yohana 3:2 “Huyo
alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu;
kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa
Mungu yu pamoja naye.”
Muhukumu wetu siku ya mwisho Yohana 5;22 “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu
yote;”
N – Yesu ni njia na kweli na Uzima Yohana 14:6 “Yesu
akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa
njia ya mimi.”
Neno la Mungu – Yohana 1:1-3 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa
Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote
vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.”
Nabii yule - Yohana 6;14 “Basi
watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule
ajaye ulimwenguni”.
Nyota ya kung’aa asubuhi - Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi
mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota
yenye kung'aa ya asubuhi.”
Nuru ya ulimwengu - Yohana 8;12 “ Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya
ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya
uzima.”
O – Yesu ni Ondoleo la dhambi zetu tukimuamini,
tukitubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha Matendo 2:38-39 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina
lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho
Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa
watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”
P – Yesu ni udhihirisho wa Pendo la Mungu
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali
awe na uzima wa milele.”
Pazia la hekalu – Mathayo 27:51-54 “Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka
juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka;
ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini
mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.
Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona
tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu
alikuwa Mwana wa Mungu.”
Q – Quail (Kware kutoka Mbinguni) Zaburi 105:40-42
“Walipotaka akaleta kware, Akawashibisha chakula
cha mbinguni. Akaufunua mwamba, kukabubujika maji, Yakapita pakavuni kama mto. Maana
alilikumbuka neno Lake Takatifu, Na Ibrahimu, mtumishi wake.”
R – Yesu Kristo ni Rafiki Yohana 15:14-16 “Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. Siwaiti
tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi
nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. Si
ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka
mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote
mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.” Tunaweza kuwa na urafiki na
Yesu kama Mungu baba alivyokuwa na urafiki na Abrahamu kwa sababu ya utii,
yaani kama tutayatenda anayotuamuru na ni rahisi tu Yesu ametuamuru kupenda.
S - Simba wa Kabila la Yuda - Ufunuo 5:4-5 “Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye
kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Na mmojawapo wa wale wazee
akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye
ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.”
Shahidi mwaminifu – Ufunuo 1:5-6 “tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu,
mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na
kutuosha dhambi zetu katika damu yake, na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani
kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele.
Amina.”
Shina la Daudi - Ufunuo
22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu
kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao
wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.”
T – Yesu ni Tabibu wa ajabu, amekuja kwaajili
ya wale wasio na afya Mathayo 9:11-12 “Mafarisayo
walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na
watoza ushuru na wenye dhambi? Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji
tabibu, bali walio hawawezi.”
Tumaini letu kuu - Zaburi 71;5 “Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu
tokea ujana wangu.”
Taraja letu - Zaburi 71;5 “Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu
tokea ujana wangu.”
Tegemeo letu - Yeremia 17;5-8. “Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye
mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa
jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Amebarikiwa
mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.Maana atakuwa kama
mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu
wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa
uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.”
U – Upendo wa Mungu 1Yohana 15:13 “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa
uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.”
V – Vazi la wokovu wetu Isaya 61:10 “Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia
katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki,
kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi
ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.”
W – Yesu ni wokovu wetu ni mwamba wa wokovu
wetu Zaburi 95:1-2 “Njoni, tumwimbie Bwana,
Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu. Tuje mbele zake kwa shukrani,
Tumfanyie shangwe kwa zaburi.”
X – X rays – Mwali wa moto 2Wathesalonike 1:6-8 “Kwa
kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi; na kuwalipa
ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka
mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake katika mwali wa moto; huku akiwalipiza
kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu;”
Ufunuo 19:11-13 “Kisha
nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda,
aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. Na macho
yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye
ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. Naye amevikwa vazi
lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.”
Y- Yesu
ni Yeye yule jana leo n ahata milele Waebrania 13:8 “Yesu Kristo ni
yeye yule, jana na leo na hata milele.”
Z – Zeri ya Gileadi – Dawa isiyoshindwa Yeremia
8:22 “Je! Hapana zeri katika Gileadi? Huko hakuna
tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya ya binti ya watu wangu?” yalikuwa ni mafuta maalumu yanayotokana na
mmea maalumu unaoitwa zeri ambapo katika nyakati zile matabibu waliutumia kutibu
hususani mtu ambaye ameshindikana kutibiwa kwa dawa ya aina nyingine yoyote,
Dawa hii kinabii ilikuwa inamtaja Yesu ambaye mtu aliposhindikana kutibiwa na
matabibu wengine wote yeye aliweza kutibu,
Marko 5:25-29 “Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu
muda wa miaka kumi na miwili, na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi,
amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake
ilizidi kuwa mbaya aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma,
akaligusa vazi lake; maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona. Mara
chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona
msiba ule.”
Jinsi ya kuanza mwaka na kumaliza na Yesu Kristo
Yesu ni Alpha na Omega maana yake
yeye ni mwanzo na mwisho, na pia ana uwezo wa kushughulikia kila jambo katika
kila Nyanja ya maisha yetu ya kila siku, Lakini sio hivyo tu tunapokaribia
wakati huu wa msimu wa sikukuu yam waka mpya ni muhimu kwetu kukumbuka kuwa sio
tu kwamba tunasheherekea mwaka mpya lakini vilevile ni ukweli usiopingika
kwamba miaka yetu na siku zetu za kuwepo duniani zinahesabika na kupungua, kwa
msingi huo ni lazima tujipange kwa upya na kuhakikisha kuwa TUnashikamana na
Yeye aliye Alpha na omega yaani mwamnzo na mwisho wa kila kitu katika maisha
yetu na hivyo hatuna budi kumuomba Mungu
1.
Atupe
hekima ya kuutumia wakati, yaani sekunde, dakika, saa, siku, wiki, miezi na
miaka ijayo kama zawadi ya tahamni sana ili tuweze kuacha alama katika kusudi
lile alilotuitia Zaburi 90:12 “Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa
hekima.” Muda ni moja ya zawadi kubwa nay a thamani ambayo Mungu
ametupa tujifunze kutokupoteza muda, kukemea na kukataa uvivu, umasikini,
magonjwa na kila jambo linaloturudisha nyuma kiroho, tusikubali kupoa,
tusikubali kurudia makossa, tusikubali kulegea bali tusonge mbele katika wito
huu ambao Mungu ametuitia Waefeso 5:15-
16. “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si
kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa
maana zamani hizi ni za uovu.”
2.
Tumia
muda wako Mwingi kuwa na Mungu, tunaweza kumkaribia Mungu kwa kujitoa
binafsi kwake kwa Maombi, kusoma neno la Mungu, kusikiliza mahubiri, kujumuika
katika makusanyiko ya ibada lakini zaidi sana kuutafuta suo wa Mungu kuliko
kubwa busy na makundi ya watu Mathayo
14:22-23 “Mara akawalazimisha wanafunzi wake
wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo, wakati yeye alipokuwa
akiwaaga mkutano. Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani
faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.”
3.
Mtumaini
Bwana – Tumejifunza kuwa Yesu ni Alfa na Omega kwa msingi huo katika
mipango yetu yote hatuna budi kuhakikisha kuwa tunamtumaini yeye kwani ni yeye
pekee mwenye mwenye uwezo wa kunyoosha mapito yetu yote, Mithali 3:5-6. “Mtumaini Bwana
kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako
zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.”
4.
Mfanye
Yesu kuwa kiini cha Maisha yako na mipango yako yote – Yesu ni Alfa na
Omega tumeweza kujifunza kuwa yeye ni mwamba katika kila Nyanja ya maisha yetu,
hatuna budi kuhakikisha kuwa kila jambo tulifanyalo, tunalifanya kwa utukufu
wake, tumfanye yeye kuwa kiini kikuu cha maisha yetu na mipango yetu, hakkisha kuwa unakanyaga mwana na Bwana na
kuendelea kuwa na uhusiano naye mwanzo mwisho Mungu atatubariki, linapokusibu
lililo gumu kumbuka Alfa na Omega anaweza kuingilia katika katika kila eneo la
maisha yetu kulingana na uhitaji wetu.
Na. Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni