Utangulizi
Siku
za hivi karibuni kumezuka mjadala mkubwa sana kuhusu umuhimu wa ubikira katika
imani, wote tunafahamu kuwa Maandiko katika Agano la kale na Agano jipya kwa
ujumla yalisisitiza sana umuhimu wa kuoa mwanamke bikira!, Mila nyingi na
tamaduni nyingi pia zinathamini sana umuhimu wa mume kuoa au kupata mwanamke
Bikira, Bikira ni nini na ina umuhimu gani kiimani? Je kuna ulazima wa kuoa
mwanamke Bikira? Kwa nini Mungu aliiweka bikira na kwa nini alisisitiza mwanamwali
kuolewa bikira kuna jambo gani katika ulimwengu wa kiroho kuhusu ubikira, je
kuoa mwanamke ambaye hakuwa na bikira kuna faida gani au hasara gani? Maswala
haya yote yote yanatufikisha mahali hapa ambapo tunapaswa kuliangalia swala
hili kwa kina na mapana na marefu.
Mabinti Bikira Uko Afrika ya Kusini hupewa uthamani mkubwa sana katika tamaduni zao
Maana ya Neno Bikira kimaandiko!
Kwa
mujibu wa tafasiri za Agano la kale neno bikira lilitumika kumaanisha
Mwanamwali yaani mwanamke kijana asiyejua Mume au ambaye hajawahi kushiriki
tendo la Ndoa, na kuna maneno kadhaa ya kiebrania yaliyotumika kuwataja
wanawake hao, yaani BETULAH
mwanamwali bikira asiyejua mwanaume au ambaye hajaingiliwa na uume bado kwa
kiarabu BATULI, na BAHUR mwanamke au mwanamwali kijana na ALMAH mwanamwali bikira aliyetolewa
mahari au ambaye yuko karibu kuolewa, Almah pia ilitumika kumaanisha mwanamke
safi ambaye hakuna maswali katika kuthibitisha usafi wake, Neno hili ALMAH ndilo analolitumia Isaya Nabii
katika Unabii unaohusu Mwanamwali atakayemzaa Masihi Isaya 7: 14. “Tazama Bikira (ALMAH)
atachukua Mimba!.” Kwa hiyo kibiblia hii ilikuwa ndio maana ya neno Bikira.
Hata hivyo Neno la Mungu lilikuwa na maana ya ndani zaidi kama tutakavyoiona
baadaye.
Umuhimu wa Ubikira katika Ndoa.
Ni
ukweli usiopingika kabisa kuwa kwa mujibu wa mafundisho ya kibiblia yaani Agano
la kale na Agano jipya na katika mtazamo wa Mungu, Ndoa ilithibitika kuwa ni
halali na takatifu endapo alama za ubikira zingeonekana katika tendo la kwanza
la ndoa, Damu ambayo ingemwagika kwa mara ya kwanza ingeweza kuthibitisha kuwa
mwanamke huyu ameingiliwa kwa mara ya kwanza, Damu hii ilihusianishwa kama damu
ya agano lililo wazi kabisa kuwa ndoa hiyo ni ya halali na ni safi na kwa mume
na kwa sababu hiyo huyo ndio angekuwa mkeo halali na mwenye kumuingilia ndio
mmiliki halali wa Mume huyo:-
Walawi
21: 1,7 Biblia inasema hivi “ Kisha Bwana akamwambia Musa Nena na hao makuhani
wana wa Haruni kuwaambia, Mtu ASIJINAJISI……. Wasimumwoe mwanamke aliye Kahaba,
au huyo aliye mwenye UNAJISI, wala wasimuoe mwanamke aliyeachwa na mumewe: kwa
kuwa yeye ni kuhani ni mtakatifu kwa bwana Mungu wake” ni wazi kuwa hapa BIBLIA
iliwakatza Makuhani kuoa wanawake wenye UNAJISI yaani ambao sio safi yaani
ambao wameshabikiriwa hivyo kwa ufupi walitakiwa kuoa mwanamke Bikira! Yaani
ASIYENAJISIWA!
Ubikira
katika agano la kale na wakati wa sheria uliinua sana thamani ya mwanamke,
licha ya kuweko kwa mahari maalumu (Waebrania waliita Mohar Betulot) kiarabu (Mahar
al Batul) sawa na “bride price for virgin”
Mahari maalumu ya Ubikira, kwa sababu ya kukutwa Bikira, heshima kwa
wazazi kwa matunzo mazuri ya binti yao, heshima kwa binti kwa kujitunza lakini
pia ilithibitisha uwezo na kiwango cha juu cha uadilifu.
Katika
Torati ya Musa mwanaume alipolala na mwanamwali aliyeposwa “ALMAH” na kuharibu uanawali wake
alitakiwa kumuoa yeye, na kama Baba yake angekataa asimuoze binti yake kwa mtu
aliyembikiri, mwanaume huyo alipaswa kulipa mahari sawa tu na ile ya muoaji wa
mwanamke Bikira “Kutoka 22:16-17”
Kama
mwanamume angembaka mwanamke Bikira alipaswa kwa mujibu wa torati kulipa shekel
50 sawa na mahari ya mwanamwali bikira na alilazimika kumuoa na hakupaswa
kumuacha maisha yake yote Kumbukumbu
22:28-29
Kumbukumbu 22: 13-22
Biblia inasema hivi “13.Mtu akitwaa mke, akamwingilia na kumchukia, 14. kisha
akamshitaki mambo ya aibu kumzushia jina baya, akasema, Nimemtwaa mwanamke
huyu, nami nilipomkaribia sikuona kwake alama za ubikira; 15. ndipo babaye yule
kijana na mamaye watakapotwaa alama za yule kijana za ubikira, wawatolee wazee
wa mji langoni; 16. na baba yake yule kijana awaambie wazee, Mwanamume huyu
nilimpa binti yangu awe mkewe, naye amchukia; 17. angalieni, amemwekea mambo ya
aibu, asema, Sikuona kwa binti yako alama za ubikira, nazo hizi ndizo alama za
binti yangu za ubikira. Na wayakunjue yale mavazi mbele ya wazee wa mji. 18.
Basi wazee wa mji ule na wamtwae yule mtu mume na kumrudi, 19. wamtoze shekeli
mia za fedha, wampe babaye yule kijana, kwa kuwa amemzulia jina baya mwanamwali
wa Israeli; naye awe mkewe; hana ruhusa ya kumwacha siku zake zote. 20. Lakini
likiwa ni kweli neno hili, la kutoonekana kwake yule kijana alama za ubikira;
21. na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na waume wa mji
wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israeli,
kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondoa uovu
katikati yako.
Kupoteza
ubikira kungegharimu adhabu ya kifo kwa kijana wa kike na, kuondoa bikira ya
mwanamwali kulilazimu kulipa mahari na kumuao hii ilikuwa sheria nzima ya
uanawali au ubikira katika agano la kale au torati ya Musa
Katika
agano jipya pia mwanzoni Ubikira ulichukuliwa kuwa ni sehemu ya Maisha ya
kujitoa na kumtumikia Mungu, mtu alipaswa kuishi maisha ya uanawali siku zote
za maisha yake ni hii ingekuwa ni sadaka Sacrifice kuwa ameyatoa maisha yake
kwa Yesu na hataki kuruhusu Unajisi katika maisha yake hivyo wazee wengi
nyakati za Kanisa la kwanza waliwatunza binti zao, wasiolewe waishi maisha ya
kumtumikia Mungu, jambo hili lilifanywa kwa usimamizi wa mzazi vilevile kama
ilivyokuwa katika agano la Kale kwa vile kama binti angenajisiwa au kubikiriwa
aibu ingekuwa kwa familia nzima, lakini ingekuwaje sasa kama binti anajisikia
kutaka kuolewa Paulo mtume akashauri
1Wakoritho
7: 8-9 Lakini nawaambia wale wasiooa bado na wajane Ni heri wakae Kama mimi
nilivyo, Lakini kama hawawezi kujizuia na waoe; maana ni afhadhali kuoa kuliko
kuwaka tamaa”
1Wakoritho
7: 25-28 “ Kwa habari za wanawali sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri
langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za Bwana kuwa mwaminifu. Basi, naona hili
kuwa jema, kwa ajili ya shida iliyopo, kwamba ni vema mtu akae kama alivyo. Je!
Umefungwa kwa mke? Usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? Usitafute mke. Lakini,
kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama
hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.
Wanawali
wanaotajwa hapo ni vijana wa kike walio bikira kwamba kwa mujibu wa Paulo kama
wanaamua kujitoa na kuishi maisha hayo ya utawa ni vema na kama wanaamua
kuolewa hawana hatia yaani sio dhambi
Kwa
hiyo katika falsafa za agano jipya kuishi maisha ya ubikira ilikuwa ni aina ya
sadaka Sacrifice ambayo madada wengi wanaishi maisha ya utawa hulazimika kuwa
bikira na hawasumbuki katika maisha yao kwa vile hawajui lolote
HAWAJANAJISIKA!.
Umuhimu wa Ubikira kwa mujibu wa Tamaduni za kiyahudi.
Kwa
mujibu wa tamaduni za Kiyahudi na katika vitabu vya tamaduni zao vijulikanavyo
kama Talmud, Halakhah na Hagadah Marabi
wakuu kama Gamaliel na Eliezer na Joshua bin Hananiah wanatoa maoni yao kuwa kulikuweko na utata
kadhaa katika kuziangalia alama za ubikira kwani wakati mwingine alama za Damu
hazikuonekana kabisa katika harusi kadhaa huku kikiwa na uhakika kuwa mabinti
hao walikuwa safi na hawakuwa wamenajisiwa ugumu wa uume kuingia katika uke
ulionekana na ulisumbua katika hatua za awali za ndoa au tendo la ndoa hii
ilipelekea kuondoa umuhimu wa Damu katika kuthibitisha ubikira wa mwanamke hata
ingawa damu ya ubikira ina kiherehere na humwagika kwa wingi tu katika mtindo
ulio wazi kuwa mwanamke huyu ni bikira lakini sio wote wanakuwa na alama hiyo
na hivyo labda kungekuweko uwezekano wa kuhukumiwa kwa mabinti wasio na hatia
ambao ubikira wao uliweza kutokuthibitika katika mazingira mengine
Mkazo
mkubwa wa ubikira unapochunguzwa vyema Katika maandiko ulimaanisha
KUTOKUNAJISIKA, ASIYENAJISIKA, UNAJISI ni lazima kujiuliza unajisi ni nini
kunajisika kunakozungumzwa hapo ni nini? Neno unajisi kwa urahisi ni kuchafuka,
kuchafuliwa n.k. kuingiliwa kwa mwanamke katika tendo la ndoa kungepeleka
taarifa ya uzuri au ubaya wa tendo hilo katika Ubongo na ungerekodiwa mara
moja, taarifa ya utamu wa tendo la ndoa ingekuwa imeingizwa kwa mwanamwali
ambaye hakuna mtu wa kumuoa bado, uhitaji wa tendo ungeingizwa mapema kwa binti
katika ubongo wake, angeanza kuwakwa tamaa ya kutaka mume huku hakuna wa kumuoa
na hivyo roho ya ukahaba ingeingia kichwani na hivyo kumbikiri mwanamke
kungeitwa kumnajisi au kumfanya kuwa kahaba, na kama binti aneshindwa kujitunza
angeitwa mpumbavu kwa hiyo maana kubwa ya kiroho kuhusu UBIKIRA ni KUTOKUNAJISIKA.
Mwanamke anaweza kuwa Bikira lakini akawa amenajisika
Kama
maana ya kiroho ya Ubikira ni kunajisika uko uwezekano wa mwanamke kuwa na
ubongo au nafsi iliyonajisika na huku akaendelea kuwa Bikira!, Katika Tamaduni
za kiarabu ambako hukazia sana maswala ya Ubikira huku wanawake wakiwa ni adimu
sana ziko shuhuda kuwa baadhi ya wanawake Uarabuni, na Jordani na mataifa
mengine yenye tamaduni hizi, wanawali walionajisika bongo zao kimapenzi
walikuwa auwamekuwa tayari kutunza heshima ya ubikira wana na heshina ya
familia zao kwa kutunza ubikira wa uke huku wakitoa maumbile yao ya Nyuma na
kuwafurahisha wanaume waliowahitaji kwa nyuma eti ili kutunza mbele je kuna
umuhimu gani wa kuoa mwanamke ambaye ametunza bikira ya mbele huku bikira ya
kichwani imeharibiwa? Amenajisika
Biblia
inaonyesha wazi kuwa Binti wawili wa LUTU walikuwa Bikira yaani walikuwa
wanawali lakini kutokana na historia ya kuishi katika mazingira ya Sodoma na
Gomora mabinti wa Lutu walibaki na bikira za uke wao lakini walikuwa
wamebikiriwa akili zao na uchafu wa Sodoma na Gomora na hivyo hatima yake hawakuona
tija kulala na Baba yao baada ya kumlevya na kupokea ujauzito, kwa nini
walimlevya kwa sababu walielewa wazi kuwa baba yao katika akili nza kawaida
hangelikubali kuzaa na binti zake Angalia Mwanzo 19: 8 “Tazama ninao binti
wawili ambao hawajajua mtu mume nawasihi nitawalotea kwenu…” andiko hilo
lathibitisha wazi kuwa mabinti wa Lutu walikuwa Bikira hawakujua Mume, lakini
pamoja na haya binti za Lutu walikuwa waovu mioyoni mwao Mwanzo 19:30-38 Biblia
inasema hivi “
Lutu
akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa
sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake
wawili. Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume
katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote. Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo,
tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao.
Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule,
akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala
alipoondoka. Ikawa siku ya pili, mkubwa
akamwambia mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena
usiku huu, ukaingie ukalale naye. Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule,
akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.
Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. Yule mkubwa
akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo.
Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa
Waamoni hata leo.
Unaweza
kuona je ulimwengu tulionao leo unaruhusu watu kuendelea kuwa Bikira? Je watu
wamenajisika au la? Leo hii kuna vifaa maalumu ambavyo vinawawezesha watu
kushiriki ngono hata bila mwanamke au mwanaume “sex toys” zimeenea kila mahali
duniani, maendeleo ya sayansi na teknolojia yenye kuruhusu watu kunajisika
yameenea kila mahali unaweza kumpata bikira katika dunia ya sasa ambaye
hajabikiriwa uke lakini amebikiriwa Ubongo! Lipi lilolo jema ASIYENAJISIKA,
kama unataka bikira maana yake tafuta mtu ambaye ubongo wake umetakaswa na
kusafishwa na damu ya Yesu asomaye na afahamu
Ubikira na uhalali wa Ndoa.
Biblia
inapozungumzia ubikira haizungumzii sehemu moja ya kiungo cha mwili
inazungumzia usafi wa nafsi, mwili na roho. Ndio maana kanisa huitwa bikira
mbele za Mungu, hivyo neno ALMAH alilolitumia Isaya kuhusu Mariam ndio neno
zuri lenye kufaa kwa mtu mwenye sifa ya kumbeba masihim Mariamu hakuwa bikira
wa uke tu, mabikira wa uke tu katika Israel walikuwa wengi, Mariam alikuwa safi
Mwili nafsi na Roho na hakukuwa na maswali katika habari ya maisha yake”
Hakuna
mwalimu yeyote wa ndoa Duniani ambaye amewahi kufafanua kuwa uhalali wa ndoa
unasababishwa na bikira hata kidogo, ilivyo ni kwamba hata Biblia haisemi kuwa
ubikira unaifanya ndoa iwe halali, biblia inaonya kuwa TENDO LA NDOA lenyewe
ndio linaloifanya ndoa iwe halali kuwe na damu ya ubikira au isiweko, yaani
katika Ulimwengu wa kiroho unaunganishwa na mwanamke au mwanamume hata kama ni
kahaba hana bikira kuwa mwili mmoja kwa tendo la ndoa
1Wakoritho
6:16 “ Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana
asema wale wawili watakuwa mwili mmoja”
Chunguza
andiko hilo hapo juu nini kinaunganisha ndoa? Sio bikira ni tendo la ndoa hata
kama utalifanya na kahaba unakuwa mwili mmoja naye
Hivyo
bikira haijawahi kutumika na wanatheolojia wa aina yoyote kama sehemu halali ya
kuunganisha ndoa
Je ni mambo gani yanayoifanya ndoa kuwa halali?
Ndoa halali haimaanishi
kuwa ni ile iliyofungwa kanisani tu ndoa inaweza kufungwa kanisani nabado ikawa
si halali au batili, Cheti cha ndoa si ndicho kinachoifanya ndoa kuwa halali,
Machoni pa Mungu, Adamu na Hawa babu na bibi zetu walizaliwa zamani kabla ya
kuwepo kwa vyeti, lakini ndoa zao zilikuwa halali na zilidumu kwa Muda wa
kutosha Je nini basi kinaifanya ndoa iwe halali? Maswala yafuatayo huifanya
ndoa kuwa halali;-
RUHUSA YA WAZAZI.
Ndoa inakua halali
kwanza pale ambapo wazazi hasa wa mwanamke (Mwanamwali),wanapokuwa wametoa
ruhusa ya binti yao kuolewa na kijana, Baada ya kijana kuomba kibali hicho na kuruhusiwa aidha kwa kupitia
yeye au mshenga wake, (Mwanzo
34;8,11-12, Samuel 13;11-13,1Koritho 7;36) baada ya Ruhusa hiyo hata kama
kuna taratibu nyingine zitafuata kama
mahari, kitakachofuata hapo hakiifanyi ndoa kutokua halali iwe ni taratibu za
kimila au desturi, dini au dhehebu, Fulani, Mchungaji, shekhe, Padree au ofisi
ya DC. Machoni pa Mungu hiyo ndoa ni halali na haitenganishwi (Malaki 2;13-16).Hivyo ni lazima ndoa
hizo ziheshimike na talaka si ruksa (Ebrania
13;4,Math 19;3-4,6) Kumbuka kuwa Mungu huzieshimu ndoa zote hizi hivyo watu
wa namna hii wanapookoka kuja kanisani kama wameyazingatia haya watapokelewa
kama wanandoa halali isipokuwa kama ana mke zaidi ya mmoja mkewe halali atakuwa
ni yule wa kwanza katika kuwaoa hivyo atabakia na yule mkewe wa kwanza kama mke halali na jambo hili
litafanyika kwa hiyari baada ya kujifunza Biblia na kuielewa wala si kwa
shinikizo la kichungaji.
SWALA LA KISHERIA
Swala lingine linaloifanya ndoa iwe
halali ni swala la kisheria au swala la
kiserekali kwa mfano hapa Tanzania Unapokaa na mwanamke au mwanamume kinyumba
kwa Muda unaozidi miezi mitatu mfululizo na kuzidi, Kisheria serikali
inawatambua kama mke na mume walio halali hata kama mahari haijatolewa. Kwa
sheria hii mwanamume anapo pokonywa mke kwa sababu yoyote ile ana haki ya
kufungua kesi mahakamani na kudai haki ya kurejeshewa mkewe na endapo mwanamke
atafukuzwa bila sababu za msingi ana haki ya kudai mahakamani yaliyo haki yake jambo la msingi au ushauri wa bure kwa
wanandoa wa jinsi hii ni kuzisajili ndoa zao serikalini hii itasaidia ndoa
kutambuliwa rasmi na kuepuka usumbufu wakati yanapotokea Matatizo kama
kuachana, madai ya mirathi au kifo, hili litawafanya watu hao kuwa salama, Wanapookolewa
watu wa namna hii ni muhimu mkwa watumishi wa Mungu kuwasaidia watu hao
kujisajili na kutokutia moyo ndoa hizi kuvunjika hii ni kwa sababu kanisa ni
msimamizi wa utaratibu duniani na serikali pia hivyo ni muhimu kwa kanisa
kusaidiana na serikali katika kuhakikisha watu wanaishi kwa utaratibu na si
vinginevyo (Warumi 13;1)
SWALA LA UZIMA WA VIA
AU VIUNGO VYA UZAZI (MITAMBO).
Hili ni mojawapo ya swala gumu na lenye utata sana na huwa lina leta maaamuzi magumu endapo linatokea hususani
katika ndoa zetu za kikristo katika swala hili wako wale wanaounga mkono kuwa endapo ndoa itafungwa na baada ya kufungwa ikabainika
kuwa mmoja wa wanandoa hana uwezo wa kufanya tendo la ndoa yaani mitambo yake ya kike au kiume haifanyi
kazi basi ndoa hiyo ni batili na hasa pale itakapo bainika kuwa mmoja hawezi
kabisa kufanya hivyo tangu walipooana ndoa hiyo inabatilishwa swala hili
linategemea na mtazamo wa kichungaji na mazingira. Wengine huliona jambo hili
kuwa ni halali na wengine huliona kuwa si halali lakini kwa mujibu wa serikali
watu wa namna hii hutenganishawa na mahakama.
SWALA LA AGANO (KIAPO)
CHA NDOA.
Ndoa ni swala nyeti
linalogusa jamii, Dini, Serikali na Mungu, pia hugusa Maisha ya kiroho ya Wahusika, Hivyo ni muhimu kuelewa kuwa Mungu
ni muhusika mkuu hasa pale wanandoa wanapoapa
kwa Mungu humuhusisha yeye Moja kwa moja
na kule kumhusisha Mungu huifanya ndoa kuwa AGANO, Agano ni nini? Neno agano kwa ufupi ni Patano, Ahadi au
nadhiri inayofanywa baina ya pande mbili huku zikimuhusisha Mungu, Patano
linapofanywa bila kumuhusisha Mungu huitwa
“Mkataba” na Mungu anapinga vikali sana Ndoa za mkataba ndoa za mkataba zinazo ibuka duniani hivi karibuni ni kinyume
na mapenzi ya Mungu, Mkataba unaweza kuvunjika, lakini sivyo lilivyo Agano,
Agano linapokuwa limefanyika huwa limefanyika
(Yoshua 9;14, Kumbukumbu
20;10,Samuel 21;1-9) Agano huwa
halivunjiki hata kama mmojawapo atakuwa amedanganya kwa namna yoyote hiwezi
kubatilisha Agano.Kwa mtazamo huu basi sababu ya via vya uzazi kutokufanya kazi
inaweza isikubalike kibiblia.
Ubikira
haujawahi kutajwa kokote kule kama jambo linaloifanya ndoa kuwa halali, kwa
sababu hiyo binti napobikiriwa yuile aliyembikiri anakuwa ameinajisi akili ya
binti na hivyo alipaswa amchukue asimuache kwa vile kufanya hivyo kungeharibu
maisha ya binti na kumfanya aishai maisha yasiyo yenye kujitunza, Mke wa mtu
pia aweza kunajisiwa, kama mtu aliolewa na hajawahi kutoka nje ya ndoa yake pia
anakuwa safi na mwaminifu kwa mumewe, anapojaribu kufanya tendo la ndoa na
mwanamume mwingine kinachotokea ni uwezekano wa kunajisika kiakili, kwa vila
wanawake na wanaume hutofautiana katika utendaji wao washughuli za kimapenzi
kila mmoja ana namna yake na hivyo kujaribu sehemu nyingine kunaweza kukuumbia
ulevi mwingine wa kimapenzi nakukufanya uhesabike kuwa kahaba au Malaya jambo
hili pia hutokea kwa wanaume wanawake hutofautiana miitikio yao kimapenzi na
kimahaba na maumbile yao na kadhalika huweza kukufanya uonje tofauti na hivyo
kujikuta unaharibu maisha yako ya uadilifu na hivyo kuharibu ubikira wako hata
sasa
Ubikira
ilikuwa ni alama kivuli ya kibiblia yenye kuzungumzia maswala yafuatayo
1.
Mungu hakutuita katika uchafu
(UNAJISI)
Biblia inasema hivi 1Thesalonike 4: 3-7 “3. Maana haya ndiyo
mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue
kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya,
kama Mataifa wasiomjua Mungu. Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika
jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama
tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana. Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali
tuwe katika utakaso.
2.
Zinaa inakaa katika akili inakamata
akili
Ikimbieni zinaa 1 Wakorotho 6: 18-20 “Ikimbieni zinaa. Kila
dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa
hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni
hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si
mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu
katika miili yenu”.
Biblia ya kiingereza haisemi ikimbieni zinaa inasema flee
from from
sexual immorality yaani kukimbia uchafu wa kingono hii ni zaidi ya zinaa na
inahusu kujinajisi na sehemu nyingine muhimu inasema “yeye afanyaye zinaa
hutenda dhambi juu ya mwili wake” ni muhimu kupafahamu mahali hapa muhimu
ambapo pamesumbua wanatheolojia wengi kwa miaka kutotafasiri kwa usahii eneo
hilo neno juu ya mwili wake “against their own body” kiibrania ni neno NEPHES
ambalo maana yake NAFSI ambayo tafasiri yake AKILI au UBONGO dhambi ya zinaa au
uchafu wa kingono unatawala mawazo sana kuliko dhambi nyingine zambi nyingine
zote hazikai akilini Ni nje ya mwili wake lakini dhambi za kingono zinakamata
akili Juu ya mwili wake hii ndio tafasiri kwamba zinaa inatia UNAJISI
3.
Uhusiano wa Mungu na watu wake Efeso
5:31 wawili kuwa mwili mmoja kisaikolojia ni kuunganisha nafsi na hisia, si
vema kuunagnisha nafsi na hisia na mtu ambaye hujaamua kuwa naye, Mungu
nanapenda watu committed na wanaume wameumbwa kwa mafano wa Mungu pia wanawake
hivyo kila mmoja anapenda uaminifu, Mungu anataka kanisa aminifu mume anataka
mke mwaminifu na mke anataka mume mwaminifu hili ndo swala la msingi katika
uhusiano Damu aliyoimwaga Yesu kwaajili yetu ilikuwa ni uthibitisho wa upendo
na kujitoa kwake kwetu, damu ya ubikira ni uthibitisho wa uvumilivu uaminifu na
upendo kwa Yule atakayekuwa mwenzi wako lakini kwa sasa damu hii haina msingi
tena si kwa maana kuwa watu wasijitunze bali kwa maana ya kufanya uhalali wa
ndoa uaminifu ni msingi na kutokuruhusu akili yetu kunajisika
4.
Kila mmoja anapaswa kufanya kila
aliwezalo kuhakikisha kuwa anamfurahisha mwenzi wake kisaikolojia ili kumjenga
awe wake, kama hujaolewa unaporuhusu chuchu zako kunyonywa na makalio kupapaswa
na mdomo wako kuliwa denda mwanamume huyo anakuteka kisaikolojia na kukufanya
umtegemee na kumuhitaji, miitikio yako kama unalegea ua unatoa milio au
unalegeza macho nk inamnfanya mwanamme huyu kukukumbuka na kutekwa kisaikolojia
na ndoo maana kumfikisha mtu kileleni katika mapenzi kunaweza kuwa hatua ya juu
kabisa ya kuunganisha nafsi kuliko kuondoa bikira na ndio maana ndoa huwa
halali kwa tendo la ndoa zaidi kuliko Ubikira
Ukiyajua hayo heri wewe ukiyatenda
Makala na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.
Maoni 9 :
kwanini watu hawayapati masomo haya? naona wanakosa mengi sana
Ubarikiwe na Mungu, Kiukweli kuna Jambo lililo niathiri kisaikolojia, nilikua na Mchumba wangu tulie juana akiwa bado ni bikra, nilikua nipo katk imani skupenda kabsa kumwingilia, lakini nilimwacha nyumbani kwa ahadi kali,,
''Nakuomba uzidi kua katka uaminifu kama ulio nao" alinipa ahadi za kutosha,
Nilielekea Masomoni Chuoni Dodoma (UDOM) Nilipo rudi nilihitaj kuanza nae maisha, lakn alionekana know badilika kimaumbile kama ameharibiwa,
Siku moja nililazmika kubunja ukimya na kumbana hapo ndipo alip nambia ukweli, niliumia sana, Kiukweli nimeshindwa kumwacha ila naumia hasa napo mwon na kumkumbuka mtu alie mharibu, nimemwoa lakn hamu hutoeka gafla nkikumbuka kua ameharibiwa na kidume fulani,,
Napata wakati mgumu sana, naomba msaada wako nifanye nn sioni umuhm wake, namwona kana kwamba hana utam wowote inaniuma
Unaweza tumia simu 0759021034
Email danielzachason25@gmail.com
Naomba ushauri
kwa ninavyo ona ndoa na mahusiano mengi huvunjika kutokana kwamba watu wengi hususani wanawake kwenye mahusiano wamekua na wanazidi kuwa watumwa wa wanaume waobwa zamani hvyo hata ukiwa nae kama mke ni sawa na kuwa unaishi ma mke wa watu tu kwa sababu akitafutwa na mwanaume wake wa zamani hawezi kukataa kutokana na agano la damu aliotoka kipindi anatolewa bikira..na hii ni kwa wasichana ambao hawajaokolewa yaani kuzaliwa mara ya pili kiroho nandio maana shetani anatumia huo mwanya kuharibu ndoa za watu kwa kuwakumbushaa mambo ya zamani
kwa ninavyo ona ndoa na mahusiano mengi huvunjika kutokana kwamba watu wengi hususani wanawake kwenye mahusiano wamekua na wanazidi kuwa watumwa wa wanaume waobwa zamani hvyo hata ukiwa nae kama mke ni sawa na kuwa unaishi ma mke wa watu tu kwa sababu akitafutwa na mwanaume wake wa zamani hawezi kukataa kutokana na agano la damu aliotoka kipindi anatolewa bikira..na hii ni kwa wasichana ambao hawajaokolewa yaani kuzaliwa mara ya pili kiroho nandio maana shetani anatumia huo mwanya kuharibu ndoa za watu kwa kuwakumbushaa mambo ya zamani
Ingiza maoni yako...yatulazimu tuoe bikira ili tusihishi kwa wasiwasi maana anakuwa wa kwako peke yako
Ni kweli kabisa ni tatizo tunaloishi nalo kwa sasa wanawake wengi wapo hivyo na ndio maana kumekua na ile misemo kama mtalaka hatongozwi! msemo huu hutumika hata kama mwanamke hakuolewa ila tu kama alishakutana na mwanaume sababu akikutana nae basi mwanaume hatumii nguvu nyingi kumshawishi tena huenda akaanza yeye! kiukweli tunaishi na wake za watu! Kungelua na uwezekano taratibu hizi zirudi na zikaziwe zingesaidia sana hata mimba zisizo na baba zisinge kuwepo
hili jambo ni la muhimu sana ndugu zangu oa mwanamke bikira utapunguza matatizo kwenye familia yako hata watoto wako utaweza kuwalea kwa mfano wa mama yao.
(a) Kukosa Hofu na Kutii Sheria ya Mungu
(b) Kuacha Mira na Tamaduni za Mababu
(c) Elimu na Utandawazi wa Kishetwani ndio chanzo cha ngono zembe
hili andiko ni zuri na limejitosheleza vyema kwa kugusia maeneo yote muhimu.
Chapisha Maoni