Luka 4:18-22
18. Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana
amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia
wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru
waliosetwa, 19. Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. 20. Akakifunga chuo,
akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi
wakamkazia macho. 21. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni
mwenu. 22. Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu?
Moja ya maswala ya msingi namambo
muhimu tunayopaswa kuyafahamu ni pamoja na kufahamu maneno haya ya neema kubwa
yaliyopata kutamkwa na Bwana wetu Yesu Kristo, ni Maneno ambayo hata wale
waliyoyasikia waliyastaajabia maneno hayo ni “KUTANGAZA MWAKA WA BWANA
ULIOKUBALIWA”
Ni muhimu kwetu kufahamu ni nini
maana ya Mwaka wa Bwana uliokubaliwa? Katika kiingereza maneno hayo husomeka
hivi “To proclaim the Year of Lords Favour”
Neno Favour katika Biblia ya Kiyunani yaani Greek linasomeka “Dektos” ambalo
maana yake ni Kukubalika au “Neema”
Kwa kawaida Mungu aliwaamuru wana
wa Israel kuadhimisha sikukuu iliyoitwa Mwaka wa Bwana wa Neema kila Baada ya
miaka 49 mwaka wa 50 Uliitwa mwaka wa Neema au mwaka wa Bwana uliokubaliwa
mwaka huu ulikuwa maalumu na ulikuwa na mafundisho makuu manne yafuatayo
1. Ulikuwa
ni mwaka wa kupuliza tarumbeta yaani mwaka wa kuukaribia mlima au uwepo wa
Mungu
Kutoka 19:10-13 Biblia inasema
hivi;-
10. BWANA
akamwambia Musa, Enenda kwa watu hawa, ukawatakase leo na kesho, wakazifue nguo
zao, 11. wawe tayari kwa siku ya tatu; maana siku ya tatu BWANA atashuka katika
mlima wa Sinai machoni pa watu hawa wote. 12. Nawe utawawekea mipaka watu hawa
pande zote, ukisema, Jihadharini, msipande mlima huu, wala msiuguse, hata
mapambizo yake; kila mtu atakayeugusa mlima huu, bila shaka atauawa. 13. Mkono
wa mtu awaye yote usimguse mtu huyo, ila hakika yake atapigwa kwa mawe, au
kupigwa kwa mkuki; kwamba ni mnyama au kwamba ni mwanadamu, hataishi. Hapo
panda itakapotoa sauti kwa kufuliza ndipo watakapoukaribia mlima.
Ilikuwa ni
vigumu na ni hukumu ya kifo kuukaribia uwepo wa Mungu, lakini ilipopigwa
tarumbeta au panda ndipo watu waliporuhusiwa kuukaribia uwepo wa Bwana, hivyo
mwaka wa Bwana unazungumzia kukaribishwa uweponi mwake
2. Ulikuwa
ni mwaka wa KISABATO yaani mwaka wa MAPUMZIKO Walawi 25:8-17 Biblia inasema hivi: -
8. Nawe
utajihesabia Sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni
siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda. 9. Ndipo
utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi
wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu
yote. 10. Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru
katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile kwenu, nanyi kila
mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake.11.
Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu
hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa. 12.
Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake
yatokayo shambani. 13. Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake. 14.
Tena kama ukimwuzia jirani yako cho chote, au kununua cho chote mkononi mwa
jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe; 15. kwa hesabu ya miaka iliyo
baada ya yubile, ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka
ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe. 16. Kama hesabu ya miaka ilivyo ni nyingi
ndivyo utakavyoongeza bei yake, na kama hesabu ya miaka ilivyo ni chache ndivyo
utakavyopunguza bei yake; kwani yeye akuuzia mavuno kama hesabu yake ilivyo. 17.
Wala msidanganyane; lakini utamcha Mungu wako; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu
wenu.
Mungu alikuwa
anataka watu wake wastarehe wapumzike wafurahi Jubilei, kwa hiyo ulikuwa ni
wakati wa Kustarehe na kuburudika na kupumzika na kurudishiwa milki ya nkila
ulichopoteza
3. Ulikuwa
ni Mwaka wa Kuachia Ardhi (25-38)
“25. Kwamba nduguyo amekuwa maskini, na kuuza sehemu ya milki
yake, ndipo jamaa yake aliye karibu naye atakuja, naye ataikomboa ile aliyoiuza
nduguye. 26. Na kama mtu hana atakayeikomboa, naye mwenyewe amepata mali na kujiona
kuwa anayo ya kutosha kuikomboa; 27. ndipo na aihesabu hiyo miaka ya kuuzwa
kwake, na kilichozidi kumrudishia huyo mtu aliyeinunua; naye atairejea milki
yake. 28. Lakini asipoweza kujipatia mwenyewe, ndipo hiyo iliyouzwa itakaa
mkononi mwake huyo aliyeinunua, hata mwaka wa yubile; na katika yubile itatoka,
naye atairejea milki yake. 29. Tena kwamba mtu anauza nyumba ya kukaa, iliyo
ndani ya mji wenye kuta, ndipo ana ruhusa kuikomboa katika mwaka mmoja mzima
baada ya kuiuza; atakuwa na amri ya kuikomboa muda wa mwaka mzima. 30. Na kama
haikukombolewa katika muda wa mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyo ndani ya mji
wenye kuta itathibitishwa milele kuwa ya huyo aliyeinunua, katika vizazi vyake;
nayo haitatoka katika yubile. 31.Lakini nyumba za vijiji, ambavyo
havikuzingirwa na kuta, zitahesabiwa pamoja na mashamba ya nchi; nazo zina
ruhusa ya kukombolewa, nazo zitatoka katika yubile. 32. Pamoja na hayo, miji ya
Walawi, nyumba za miji ya milki yao, Walawi wana ruhusa ya kuzikomboa majira yo
yote. 33. Tena kama mtu mmoja wa hao Walawi akikomboa, ndipo nyumba iliyouzwa,
na mji wa milki yake, itatoka katika yubile; maana, hizo nyumba za miji ya
Walawi ni milki yao kati ya wana wa Israeli. 34. Lakini konde la malisho ya
miji yao lisiuzwe kwa kuwa ni milki yao ya daima. 35. Na ikiwa ndugu yako
amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe
kama mgeni, na msafiri. 36. Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu
wako, ili ndugu yako akae nawe. 37. Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe
vyakula vyako kwa kujitakia faida. 38. Mimi ndimi BWANA, Mungu wako,
niliyewatoa katika nchi ya Misri ili niwape nchi ya Kanaani, nipate kuwa Mungu
wenu.”
4. Ulikuwa
ni Mwaka wa kuwaachia watumwa uhuru na kila mtu kurejea nyumbani kwao (39-55)
39. Tena kwamba
nduguyo amekuwa maskini pamoja nawe, akajiuza kwako; usimtumikishe mfano wa
mtumwa; 40. kwako wewe atakuwa mfano wa mtumishi aliyeajiriwa, au mfano wa
msafiri; naye atatumika kwako hata mwaka wa yubile; 41. ndipo atakapotoka kwako aende zake, yeye na wanawe
pamoja naye, naye atairejea jamaa yake mwenyewe, tena atairejea milki ya baba
zake. 42. Kwa kuwa hao ni watumishi wangu, niliowaleta watoke nchi ya Misri;
wasiuzwe mfano wa watumwa. 43. Usitawale juu yake kwa nguvu; ila umche Mungu
wako. 44. Tena katika habari za watumwa wako na wajakazi wako, utakaokuwa nao;
mataifa walio kando-kando yenu, katika hao mtanunua watumwa na wajakazi. 45.
Tena katika wana wa wageni wakaao kati yenu mtajinunulia, na katika jamaa zao
walio pamoja nanyi, waliowazaa katika nchi yenu; wao watakuwa milki yenu. 46.
Nanyi mtawafanya kuwa urithi kwa watoto wenu baada yenu, wawe milki yao; siku
zote mtatwaa watumwa wenu katika hao; lakini msitawale kwa nguvu juu ya ndugu
zenu, hao wana wa Israeli, wenyewe kwa wenyewe. 47. Tena kama mgeni au mtu
akaaye nawe akitajirika, na nduguyo amekuwa maskini karibu naye, akajiuza kwa
huyo mgeni, au kwa huyo akaaye kwako, au kwa ukoo wa jamaa ya huyo mgeni; 48.
baada ya kuuzwa aweza kukombolewa; mtu mmoja miongoni mwa ndugu zake ana ruhusa
kumkomboa; 49. au mjomba wake, au mwana wa mjomba wake,
ana ruhusa ya kumkomboa, au mtu awaye yote aliye karibu naye wa jamaa yake, ana
ruhusa ya kumkomboa; au kwamba yeye mwenyewe amepata mali, ana ruhusa ya
kujikomboa mwenyewe. 50. Naye
atafanya hesabu na huyo aliyemnunua, tangu mwaka huo aliojiuza hata mwaka wa
yubile; na ile bei ya kuuzwa kwake itakuwa kama hesabu ya hiyo miaka ilivyo;
atakuwa pamoja naye kama majira ya mtumishi aliyeajiriwa yalivyo. 51. Kwamba ikali
imesalia miaka mingi, kama hesabu yake ilivyo ndivyo atakavyolipa bei ya
ukombozi wake, katika hiyo fedha ambayo alinunuliwa kwayo. 52. Tena kwamba
imesalia miaka michache tu hata mwaka wa yubile, ndipo atafanya hesabu naye,
kama hesabu ya miaka yake ilivyo, ndivyo atakavyolipa tena bei ya ukombozi
wake. 53. Kama mtumishi aliyeajiriwa mwaka hata mwaka, ndivyo atakavyokuwa
pamoja naye; asitawale juu yake kwa nguvu mbele ya macho yako. 54. Tena kwamba
hakukombolewa kwa njia hizi mojawapo, ndipo atatoka katika mwaka wa yubile, yeye,
na watoto wake pamoja naye. 55. Kwa kuwa wana wa Israeli ni watumishi; ni
watumishi wangu niliowaleta watoke katika nchi ya Misri; mimi ndimi BWANA,
Mungu wenu.
Kimsingi katika agano jipya pia
Yesu alipoutangaza alitangaza wakati wa neema ambapo kila alichokisema Yesu,
kilikuwa ni lazima kifanyike , watu wengi katika Israel walijua kuwa mwaka huo
kinabii ulikuwa unahusu ujio wa Masihi na kuwa mwenye uwezo na mamlaka ya
kuutangaza mwaka huo wa Neema alikuwa ni Masihi peke yake ulikuwa ni mwaka
uliokuwa ukisubiriwa ilistaajabisha sana Yesu laliposoma andiko na kutoa hutuba
ya maneno sita tu “LEO MAANDIKO HAYA YAMETIMIA MASIKIONI MWENU”
Ni wazi kuwa Masihi Yesu alikuwa
ametangaza maneno ya neema kubwa sana
kwamba kuanzia wakati ule hata sasa tunaishi ndani ya kipindi cha neema
na ni mwaka wa Bwana ni mwaka ya Jubilei Kristo alitangza wazi kuwa ni mwaka wa
Ø Kukomesha
kila aina ya uonevu
Ø Kuweka
huru waliosetwa na kukandamizwa na shetani
Ø Kutangaza
kuwa kila mtu anaweza kuukaribia uwepo wa Mungu bila kuuawa
Ø Amekuja
kupumzisha watu wenye mizigo na wenye kuelemewa na matatizo mbalimbali
Ø Amekuja
kuweka huru wafungwa wote wa vifungo mbalimbali
Shetani anafahamu wazi kuwa
Tarumbeta imekwisha kupulizwa na kuwa anapaswa kumuachia huru kila mmoja name nakutangazia
msomaji wangu Bwana akuweke huru na kukutoa katika vifungo mbalimbali na kila
aina ya uonevu wa Ibilisi
Huu ni mwaka wa Bwana
uliokubalika, kila kifungu na kikuachie, Roho amanitia mafuta nikutangazie uhuru
uwe Huru sasa katika Jina la Yesu Kristo, Ufunguliwe, kutoka katika vifungo vya
nguvu za giza, uonevu wa Ibilisi, Biashara zisitawi, upandishwe cheo,
waliokufunga wadhoofike na kukuachia huru, kila kifungo nakiharibu na kukivinja
katika jina la yesu Kristo aliye hai Achiaaaaaaaaa haraka Achia wasomaji wangu huna mamlaka ya kuwatesa
nina waweka huru kwa kupakwa mafuta navunja nira zote Katika Jina la yesu
Kristo, Pepo majini na mashetani huna
nafasi ya kumtesa msomaji wangu mwachie sasa hivi katika jina la Yesu Uko huru
sema amen kwa imani
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni