Jumatano, 4 Mei 2016

Safari yangu ya Korea ya Kusini.



Kupitia Jomo Kenyatta International Airport 

Jomo Kenyatta International Airport uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenya ambao zamani uliiitwa Embakasi airport ndio uwanja mkubwa wa ndege wa taifa la Kenya ni moja ya viwanja vikubwa kwa Afrika ya Mashariki kutokana na umuhimu wake wa kuhudumia watu sehemu hii, uwanja huu unahudumia watu wapatao 19,000 wengi wao wakiwa ni abiria kutoka Ulaya, Afrika na asia, uwanmja umepewa jina la aliyekuwa Waziri mkuu wa Kwanza na raisi wa kwanza wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta na uko eneo lijulikanalo kama Embakasi kilomita 15 hivi kusini mashariki mwa mji mkuu wa kibiashara wa Kenya Nairobi, uwanja huu unaunganisha Ndege nyingi kutoka nba kuelekea Ulaya, Mashariki ya kati, Mashariki ya mbali na bara la Afrika.
 Nikiwa mjini Nairobi
 Tayari kwa safari ya kuelekea China
 Gari ya kampuni ya Rainbow shutter ilitutoa Arusha mpaka Nairobi kutuwahisha Ndege
 nje ya Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta
 Huyu mhindi alikuwa anapita tu nyuma wanafunzi wa Living Stone wakishusha mizigo yao
 ndani ya uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi
 Tukianza foleni kuonyesha Passport tayari kuelekea Kupanda Ndege


Kupitia Guangzhou China.

Jina Guangzhou maana yake ni mji wa maua, ni mji mkuu wa tatu kwa ukubwa katika taifa la China ukiondoa Beijing, na Shanghai ni mji mkuu wa bandari na una wakazi mara tatu ya wakazi wa Dar es Salaam jumla ya wakazi wa Guangzhou ni 13,080,500 kwa tawkimu za mwaka 2014, jiji hili lina wilaya zipatazo tisa, ni mji muhimu wa kibiashara kwa taifa hilo na una wakai wengi wakiwemo wahamiaji kutoka Arabuni, Afrika na Asia.
 Mwelekeo wa Ndege yetu kutoka Nairobi kuelekea Guangzhou China
 Kufika Uwanja wa ndege wa Guangzhou China
 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guangzhou China
 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guangzhou China
 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guangzhou China
 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guangzhou China


 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guangzhou China

Kutua Incheon International Airport IIA

Incheon International Airport (IIA) ni moja ya viwanja vikubwa sana vya ndege katika inchi ya korea ya Kusini, Mwanzoni ulitumika kama uwanja wa ndege kwaajili ya makao makuu ya mji mkuu wa Korea Soul na moja ya viwanja vikubwa vyandege vya kibiashara, kwa sasa ni uwanja mkubwa sana wa ndege wa kimataifa na kibiashara Duniani hasa tangu mwaka 2005, kwa viwango uliofikia sasa duniani shirika la kimataifa la viwanja vya ndege Airports Council International imekitangaza mara kadhaa kuwa moja ya viwanja bora zaidi vya ndege duniani, pia kwa viwango vya usafi ni moja ya viwanja vya ndege visafi zaidi duniani, na ni moja ya kiwanja bora zaidi duniani maarufu kama skytrax
 
Airport hii ina viwanja vya mazoezi ya golf, sehemu za kulala wageni, vifaa vya kuondolea barafu wakati wa baridi,makasino, Bustani za Ndani, Makumbusho ya Tamaduni za Korea Museum of Korean Culture. Mamlaka ya uwanja huo inadai kuwa abiria wanaowasili wanauwezo wa kuhudnimiwa ndani ya dakika 19 tu na wanaosafiri ndani ya dakika 12 tu, ukilinganisha na viwanja vingine ambapo mtu hutumia lisaa zima  au dakika zaidi ya 45 kukaguliwa na kujiandaa kuondoka jambo linaloifanya Airport hiyo kuwa airport moja wapo za juu kabisa Duniani kwa kusafirisha watu na kuwahudumia kwa haraka, Airport ya Incheon  pia ina kiwango cha asilimia 0.0001% ya upotevu wa mizigo au Baggage mishandling rate 

Incheon International Airport iko kilomita 48 swa na mile 30 Magharibi ya mji mkuu wa Korea Seoul, Incheon international Airport pia ni eneo kubwa sana la makazi ya shirika la Ndege za Korea na ndege za kigeni kama Korean Air, Asiana Airlines, Jeju Air na Polar Air Cargo airport hii inauwezo wa kuhudumia na kusafirisha mizigo ya aina mbalimbali Duniani ikiwa ni pamoja na Mashariki ya asia, ni uwanja wa ndege wa nane duniani kwa kusafirisha watu na uwanja wa ndege wa nne duniani kwa kusafirisha Mizigo. Inasemekana kwa habari ya kusafirisha abiria mwaka 2014 walisafirisha abiria 40,785,953 yaani abiria zaidi ya milioni 40

Ni kupitia fursa ya kiwanja hiki kimoja tu cha ndege unaweza kuona Korea inaingiza kipato cha kiasi gani ukilinganisha na Ardhi kubwa tuliyonayo watanzania na nchi nyingine za Afrika, Korea ya kusini ina ukubwa wa kilomita za Mraba 100,210. Km. wakati Tanzania ina 945,203 km kwa hiyo kijinchi hiki kinaingia mara 9 kwa taifa letu la Tanzania Ee Mungu tusaidie tuondoke hapa tulipo.

 Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Incheon
 Sehemu ya kujichukulia Mizigo Incheon
 Sehemu ya kujichukulia Mizigo Incheon
 Sehemu ya kujichukulia Mizigo Incheon
 Sehemu ya kujichukulia Mizigo Incheon
 Sehemu ya kujichukulia Mizigo Incheon
 Ndani ya Basi lililotupokea basi hili ni la Kanisa la Incheon Presbyterian Church

 Miundo mbinu na madaraka katika jiji la Incheon
 Ndani ya basi lililotupokea
 treni za Umeme nchini Korea ni moja ya usafiri muhimu na wa haraka
 Madaraja
 Ili kutunza Ardhi watu wengi huishi katika Maghorofa apartments
 serikali na mashirika wamejenga nyumba nyingi za makazi ya watu


 Apartments
 Apartments
 daraja refu kuliko yote Nchini Korea lina urefu wa km 21
 daraja refu kuliko yote kuelekea Incheon ukitokea Seoul lina urefu wa Km 21

Kutembelea Myeon-gdong. Ave.

Myeong – dong ni moja ya eneo lililo na shughuli nyingi sana kupita yote katika mitaa ya Jiji la Seoul katika inchi ya Korea Kusini, Eneo hili ni eneo la Maduka kama Ilivyo New York kule Marekani au Kariakoo kule Dar es Salaam, kuna maduka yanayokisiwa kuzidi miliomi moja , wa wachuuzi na wanunuzi hupita katika eneo hili kila siku, eneo hili liko katikati ya mji wa Seoul ndio mahali penye kila kitu cha kisasa kuhusun Korea na kama palivyo katikati ya jiji pia pana chukua historia kubwa sana ya Nchi ya Korea kwa maana maswala ya kiuchumi, kisiasa, na Tamaduni, mahali hapa pia ni eneo muhimu la Matembezi kwa wageni kutoka mataifa mbalimbali, watu kutoka kila pembe ya korea pia huja mahali hapa kwa kununua vitu.

 mitaani katika jiji la Seoul
 mitaani katika jiji la Seoul

 mitaani katika jiji la Seoul
 mitaani katika jiji la Seoul

 mitaani katika jiji la Seoul
 mitaani katika jiji la Seoul
 nikiwa na marafiki nchini Korea

Kutembelea N Tower. 

Ni Mnara mrefu sana ulijengwa mwaka 1969 kwa makadirio ya Dolla za kimarekani milioni mbili na nusu 2.5 Million na ulifunguliwa mwaka 1980, ingawa auliisha mwaka 1971 December 3, aliyeubuni mnara huu ni Mkorea anayeitwa Jangjongryul  ingawa wakati huo vifaa vingi sana vilikuwa havipatikani hadi August 1975, Ghorofa ya tatu kuna makumbusho, hall lililo wazi maduka na mishughuliko mingine, urefu wa mnara huu unakadiriwa kufikia mita 236.7 sawa na futi 777 kwa kitako cha mita 479.7 na hivyo kufanya futi 1574 kutoka usawa wa bahari, Mnara huu maarufu kama N tower au N soul Tower ulinabadilishwa jina mwaka 2015 na kuitwa Namsan tower N ikisimama badala ya Namsan  jina ambalo maana yake ni Nature au asili, mnara huu umegharimu fedha za Kikorea KRW bilioni 15 kwaajili ya kuukarabati na kuufanya upya kila wakati
Licha ya kuwa kivutio kikubwa sana kwa nchi ya korea mnara huu pia unatumika kwa kutuma mawimbi ya  vyombo mbalimbali vya habari nchini humo ikiwemo KBS, MBC, SBS TV, FM, PBC, TBS, CBS na BBS FM, ni moja ya eneo linalotembelewa na watu wengi sana Duniani na pameorodheshwa kama moja ya vivutio 500 vya utafiti duniani.

 Namsan Tower kama minavyoonekana wakati wa Usiku
 Nikiwa na mama yangu wa Kikorea nje ya Namsan Tower
 usiku tuliokwenda kuuangalia mnara wa Namsan
 Baridi ilikuwa kali ukilinganisha na huku tulikotokea Tanzania
 Mji wa Seoul kwambali nyumma ya Namsan Tower
 Picha ya Seoul  na N Tower juu ya Namsan Tower Korea
 Namsan Tower
 Namsan Seoul Korea tower

Kutembelea  Yoido Full Gospel Church.

Yoido Fill Gospel Church ni moja ya Makanisa makubwa yenye kukusanya watu wengi wenye kuabudu mahali pamoja duniani Kanisa hili ni jamii ya makanisa ya Kipentekoste na limeanzishwa na Mchungaji Dr. David Yonngi Cho na mama mkwe wake Choi Ja – Shil wote wakiwa ni wachungaji wa ki Assemblies of God, Mwaka 1958 may 15 kanisa walikuwa wakikutana Nyumbani kwa mkwe wa Mchungaji Cho kwa ibada, na ukiachia wachungaji kulikuwa na mabinti watatu mmoja akiwa mi aliyeolewa na Cho na mwanamke mmoja mtu mzima ambaye aliingia katika ibada kwaajili ya kukimbia mvua. Watumishi hao walianza huduma ya kuhubiri injili wakigonga mlango nyumba kwa nyumba, wakitoa msaada wa kiroho, maombi na misaada ya kibinadamu kama kuombea wagonjwa, baada ya mwezi mmoja tu kanisa lilikua na kufikia watu 50 wengi wakiwa hawatoshi kwa chumba cha sebule  alichopanga Cho na mkwewe, hivyo waliamua kuweka hema nyuma ya nyumba yao, miezi na siku zilipoenda Kanisa lilisonga mbele na kukua na hivyo kuongeza hema hata hema.
Mchungaji cho alikazia mahubiri yake kuhusu Baraka za Roho, mwili na nafsi akikazia kuwa afya njema , mafanikio ya kifedha ni sehemu ya Baraka za Mungu kwa wakristo na wokovu war oho zao, akikazia mahubiri hayo watu wengi zaidi walijiunga na kufikia mwanzoni mwa 1961 kanisa lilifikia idadi ya watu 1000, wakiwa na hema kubwa sasa walinunua eneo lao mahali paitwapo Seodaemun kanisa lilikuwa kwa kasi na mpaka 1964 lilikuwa na waamini 3000 na baadaye likakuwa san asana pamoja na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuugua mara kwa mara kwa Mchungaji Dr. David Yongi Cho sasa Kanisa hili lina washirika wapatao milioni mbili, likiwa na mfumo wa cell ambazo nyingi zinaongozwa na wanawake.

 Jengo la Full Gospel kwa nje picha kwa hisani ya Rev. Innocent Samuel Kamote
 nje ya Kanisa la Full Gospel Church Jijini seoul Korea Maktaba ya Rev. Innocent Kamote
 Rev. Innocent Samuel Kamote
 Rev. Innocent Samuel Kamote
 Ilikuwa furaha kufika mahali hapa kwa kuwa nilisoma sana habari za Mchungaji wa kanisa hili kubwa zaidi kuliko yote duniani Dr, David Yong Cho
 Nikipata picha ya ukumbusho nje ya Yoido Full Gospel Church picha kwa hisani ya Rev. Innocent Kamote

 nje ya Kanisa la Yoido Full Gospel wanafunzi wangu na mwalimu Meirad wakipata kumbukumbu

 Madhari ya ndani ya Kanisa la Yoido Full Gospel Church wakati watu wakiingia kwa ibada
 Rev. Kamote ndani ya Full Gospel jijini seoul Korea
 Rev. Innocent Samuel Kamote Ndani ya Full Gospel Church jijini Seoul Korea
 Nikipiga picha ndani ya Yoido Full Gospel Church
 tukisubiri kuanza kwa ibada ndani ya Kanisa la Yoido Full Gospel Church
 Ndani ya Kanisa la Yoido Full Gospel Church Mjini Seoul Korea nikiwa na wanafunzi
 Nje ya Kanisa la Yoido Full Gospel Church Seoul Korea
 Nje ya Kanisa la Yoido Full Gospel Church Seoul Korea
 Nje ya Kanisa la Yoido Full Gospel Church Seoul Korea
 Nje ya Kanisa la Yoido Full Gospel Church Seoul Korea

Kutembelea Trickeye Museum.

Jina trickeye Museum lina asili ya maneno mawili ya Kiingereza Trick na Eyes  sawa na neno danganya macho kwa Kiswahili mahali hapa ni makumbusho ya kisanii yenye picha na michoro ya aina mbalimbali iliyoumbwa kwa ufundi pamoja na mfumo wa vioo kwa mfumo wa picha ziitwazo kitaalamu 2D au 3D ambazo zinatengeneza mazingira ya kukufanya ujione kama umepotea na hujui wapi pa kutokea, wageni na watu wanaotembelea hapa wanajiona kama sehemu ya michoro hiyo huku picha zako zikiakisi na kujitokeza kila eneo na inaonekana kama kwamba uko pamoja na eneo husika jambo hili linaweza kukufanya wewe na wengine kujicheka au kukucheka kutokana na mazingira yake.
 Kupanda Farasi mweupe trick eye museum
 Kupanda Farasi mweupe trick eye museum
 Kupanda Farasi mweupe trick eye museum
 kama unacheza na samaki hivi
 kama unacheza na samaki hivi
 kama unacheza na samaki hivi
 kama nimesusia kupiga kibodi na ninabembelezwa nipige
 Nimesusa kupiga kinanda sasa

 namwagia mtu maji


 Mchoro ambao ukipiga nao picha inaonekana kama kwamba unammwagia mama huyu maji
 Mchoro ambao ukipiga nao picha inaonekana kama kwamba unammwagia mama huyu maji
 Mchoro ambao ukipiga nao picha inaonekana kama kwamba unammwagia mama huyu maji
 Mchoro ambao ukipiga nao picha inaonekana kama kwamba unammwagia mama huyu maji
 Mchoro ambao ukipiga nao picha inaonekama kama kwamba umekalia mwezi na uko mbinguni
 Mchoro ambao ukipiga nao picha inaonekama kama kwamba umekalia mwezi na uko mbinguni

 Mchoro ambao ukipiga nao picha inaonekama kama kwamba umekalia mwezi na uko mbinguni
 mchoro ambao ukipiga nao picha inaonekana kama umepanda mtumbwi
  mchoro ambao ukipiga nao picha inaonekana kama umepanda mtumbwi
  mchoro ambao ukipiga nao picha inaonekana kama umepanda mtumbwi

Kutembelea National Museum of Korea

Kama ilivyo ada ziara yetu ina makusudi ya kujifunza maswala mbalimbali hapa nchini Korea kwa makusudi ya kuja kuliendeleza Taifa letu katika nyanja mbalimbali, Wakorea kamailivyo kwa Mataifa Mengine hawapendi kusahau Historia na kujikumbusha maswala kadhaa ya Historia na tamaduni  hivyo wanasema Kumbukumbu za matukio mbalimbali
Sisi tulipata Neema ya kutembelea Palace yaani ikulu ya ufalme wa mwisho wa wakorea kabla ya kuharibiwa na wajapani, tulishuhudia uwezo na akili waliyokuwa nayo wazee wa zamani kwamba pamoja na kuishi zamani waliokuwa na ujuzi mkubwawa ujenzi na kukabiliana na mazingira yao walijua namba ya kukabiliana na baridi ushujaa na upambaji wa rangi na kitu cha enzi cha kifalme vilipambwa kwa ustadi wa hali ya Juu unaoashiria kuwa ustaarabu wa binadamu ulianza miaka Mungu na ukiona binadamu hana ustaarabu basi ni kwa sababu amechagua kuwa mjinga tu, na sio kwa sababu ya Kikoea vitendea kazi

Kwa mfano mfalme alikuwa na Jumba ambalo pembeni nilikuwa na Bwawa la kuogelea na walifuga samaki chini nilikuwa na nguzo ndefu na uwazi ambao waliutumia kukokea moto wakati wa baridi na sehemu Mwalimu za kutolea moshi nje ili kuepuka madhara ya kufuta hewa yenye sumu  angalia mfano wa ujenzi huo wa zamani sana katika picha Habari na maelezo yote kwa Hisani ya Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima nikiripoti kutoka Seoul South Korea. 







Nyuma Jengo la zamani la Mfalme wa Korea
Kiti cha Enzi cha Mfalme wa Korea

Ikulu ya wafalme wa Korea
Mbele ya ikulu ya wafalme wa Korea ya Kusini zamani

Kutembelea kiwanda cha Chuma cha POSCO Nchini Korea

Kama ilivyo katika Historia ya maendeleo ya Binadamu uvumbuzi wa chuma una msingi mkubwa na ni mzizi POSCO yaani Pohang Steel Company hapa nchini Korea wamefanya kila liwezekanalo katika kuhakikisha wanabadili uchumi wa Taifa la Korea na kuchangia kwa kiwango kikubwa katika maendekeo ya nyanja zote na maswala ya viwanda, POSCO ni kiwanda kikubwa sana cha Chuma kilichohakikisha kuwa ndoto za Taifa la Kikorea zinafikiwa. Ndoto hii ilianza kufikiwa mnamo miaka ya 1960, Licha ya kutokuwa na mtaji wa kutosha, teknolojia Duni, na hata bila uzoefu, Safari kubwa ya kuelekea katika maendeleo hayo ilianzishwa baada ya uvumbuzi huu wa Matumizi ya Chuma cha pua kwa Kampuni ya POSCO kuanza mnamo miaka ya 1968 Tarehe 1 April.

Wafanyakazi waliamua kufanya kazi kwa bidii, katika eneo la awali lililojulikana kama Rommel House wakiwa hawalali na huku wakila wali uliokuwa na michanga kutokana na kuwa na uwezo duni wakiwa na dhamira thabiti ya kuwa nchi yenye kuzalisha Chuma,
Kwa kuanzia Korea ilizalisha tani milioni 1.3 mpaka 1973, Pohang Steelworks kilikamilika mwaka 1983 baada ya kufikia tani milioni 9.1.

Kwaajili ya kufikia mahitaji makubwa ya China na vyombo vya nyumbani uhitaji wa kuzalisha chuma uliongezeka sana na Uchumi ulikua 

POSCO waliamua kujipanua na kufanya ujenzi mkubwa sana wa kiwanda chao na walianza ujenzi mkubwa kwa kikausha eneo kubwa la la bahari ili kuwa karibu na Bandari, eneo la Yeongilman lilihamwa na kuelekea Gwangyang-man. Ujenzi huo ulianza 1985 na kukamilika 1992 sasa uzalishaji umekuwa mkubwa sana Duniani, na chuma vya aina mbalimbali vinategenezwa kuanzia vyombo vya nyumbani mpaka vya kutengenezea Meli, aidha POSCHO walianzisha Chuo cha utafiti kwa maswala ya Sayansi na ufundi ili kukabiliana na mfumuko wa uhitaji na maendeleo ya uhitaji wa chuma ili kukabiliana na soko, Kitengo hicho kiitwacho POSTECH na RIST (Research Institute of Industrial Science & Technology) Kilianzishwa ili kuendana na utaalamu kitaaluma na kiviwanda. Posco kimekuwa moja ya kiwanda muhimu sana kwa Uchumi wa Korea kusini mpaka kufikia 1998 ilijipanua na kufikia uwezo mkubwa wa kuzalisha na kuuza vyuma , nchi zinazonunua chuma cha POSCO ni pamoja na China, Japan, Marekani na sehemu nyingine Duniani sasa chuma kinazalishwa kwa mitambo maalumu isiyotumia binadamu imeajiri wafanyakazi zaidi ya 2000 wakilipwa mishahara, kusomeshewa watoto na kukaa katika nyumbani za shirika karibu na kazini aidha wafanya kazi huingia kwa zamu na kusababisha uzalishaji kwa masaa 24. 

POSCO Kufuatia Sera za uwekezaji sasa wamejenga kiwanda chao nchini Indonesia na India imeongeza uzalishaji mara dufu na sasa umekuwa kampuni kubwa zaidi ya uzalishaji wa chuma Duniani.

POSCO inaendelea kufanya bidii katika kuzalisha chuma bora zaidi Duniani na katika kukabiliana na uhitaji wa chuma ulimwenguni, unapoiona au kusikia Korea imeendelea kamwe historia hiyo ya Maendeleo haiwezi kuandikika bila POSCO kuhusika, aidha katika kukabiliana na wimbi kubwa la uharibifu wa mazingira Dunia kupitia uzalishwaji wa hewa ya ukaa Carbondioxide POSCO ni kiwanda kinachofanya bidii kubwa sana katika kutunza mazingira.

Ifikapo 2020 POSCO inakisiwa na wataalamu wa uchumi nchini humu kuwa itazalisha Trilioni 100,200 za Kimarekani na kuwa kampuni ya kwanza kwa uzalishaji wa fedha Duniani

Mwanzilishi wa POSCO alisema maneno muhimu ambayo yanakumbukwa hata sasa "Resources are limited but creativity is unlimited " maneno hayo aliyasema wakati upatikanaji wa vizalisha chuma ulipokuwa duni, Korea ya kusini hununua bidhaa za kutengenezea Chuma kutoka Australia kutokana na ukaribu wake wakati POSCO inaongoza kwa uzalishaji wa Chuma na kuinua Uchumi wa Korea watanzania tujiulize tuna viwanda vingapi vya chuma licha ya kuwa tumebarikiwa kuwa na kila aina ya material inayoweza kuzalisha Chuma kumbe chuma ni kila kitu linapokuja swala la Maendeleo jamaa wanajenga reli na madaraja wanaunda magari na meli wanatumia chuma wanachozalisha wenyewe.

Hapa sio Airport ni Station ya Treni iendayo kasi ya Korea iliyoko jijini Pohang Korea ya kusini

kupanda Treni iendayo kasi KM 300 kwa saa kutoka Seoul Kuelekea Pohang
 Kiwanda cha chuma cha POSCO kama kinavyoonekana Mbele

 Mji wa Pohang kama unavyoonekana na kiwanda cha Chuma

Pichani mwanzilishi na Mgunduzi wa Kiwanda cha Magari ya Hyundai


 Rais Park akizindua kiwanda cha Chuma

Gari ya kwanza kabisa ya Korea Hyundai iliyotengenezwa kwa kila kitu na Chuma kutoka Korea

 Nikiwa katika bandari ya Mji wa Pohang nchini Korea
 Jiji La Pohanga kilipo kiwanda cha Chuma hapa ni ufukweli
Pwani ya mji wa Pohang hii ni Bahari ya Pasific
Madaraja katika mji wa Pohang kila kitu kimetengenezwa na Chuma cha Korea na material nyingine

Kutembelea Shirika la Habari la utangazaji la Korea KBS

Kama taifa litakuwa kubwa na likawa halina Uhuru wa habari taifa hilo litakuwa sawa na mnyama twiga. Twiga ni mnyama mkubwa sana lakini hana sauti. Taifa la Korea wana historia kubwa na Maendeleo makubwa pia katika nyanja ya maswala ya Habari. KBS yaani Korean Broadcasting System ni shirika lenye uzoefu wa kutosha lenye kuwathibitishia wakorea kuwa kina uwezo wa kipekee katika kutoa habari kwa weledi na ubora kuliko shirika lolote la habari nchini huko.
KBS wanatumika kama nguzo muhimu kwa jamii ya wakorea katika kuwatimizia wasikilizsji na watazamaji wake mahitaji yao ya kihabari
Wako hurusha habari kwa lugha ya Kikorea na kiingereza
Wako wazi kwa kila MTU kwa wakati wowote
Wanachochea moyo na roho ya kitaifa katika kufikiwa ndoto zao na malengo yao
Wanahakikisha kuwa wanakuwa chombo cha kueneza Upendo na matumaini sio kwa Korea tu Bali Duniani
Kuhakikisha kuwa taifa linakuwa na umoja likijiwakilisha lenyewe kama sehemu ya Duniani
Wanatumika kama walinzi wa nchi na watu wake katika upana wa fikra
Wanakosoa katika mwelekeo chanya kwa matumaini na Upendo KBS wako Barbara ya 13 mtaa wa Yeongdeungpo-gu mjini Seoul karibu na ukumbi wa Bunge Green House Korea kwa uchambuzi wa kina tembelea KBS.co.kr/kbson KBS Wana Jengo la makumbusho na historia ya kutosha katika nyanja ya habari na burudani na ulinzi wa utamaduni. Mimi na wanafunzi wangu tulitembelea hapa na haya ndio yaliyojiri.

Nyuma ya Microphone za miaka ya zamani KBS
Nyuma ya vipaza sauti vya zamani vya KBS
Ndani ya Studio za Majaribio
Studio za Majaribio
Ndani ya Studio za majaribio KBS
Ndani ya Studio za Majaribio KBS
Video ya Majaribio ya Mahojiano studioni KBS
Nje ya shirika la Utangazaji la Korea Kusini KBS
vipaza sauti vya Zamani

Kutembelea Jengo la Bunge la Korea
The national Assembly of the Republic of Korea
                                 Pichani ni Ramani ya Viwanja vya Bunge la Korea ya kusini

Ni Bunge linalotokana na wananchi kwa maana ya kuwa wabunge wa Bunge la Korea wanachaguliwa na wananchi kwa demokrasia huru kila baada ya miaka minne, Mtu anaweza kugombea ubunge akiwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea kila baada ya miaka minne mgombea anaweza kugombe ubunge tena na tena na hakuna kikomo cha kutokugombea tena isipokuwa kwa nafasi ya Uraisi tu
Vyama vikuu vya upinzani nchini Korea ni viwili vikubwa lakini pia viko vyama vingine vidogovidogo kama ilivyo kwa Marekani
Bunge la Korea lina jumla ya wabunge 300 kati yao 246 ni wa kuchaguliwa na wananchi huku 54 wanaingia Bungeni kwa mujibu wa nyadhifa zao kwa miaka minne yakuweko kwako
Wabunge ni walezi wa wananchi, ni wasemaji wao wakuu pia husimamia ukusanywaji wa Kodi katika Majimbo yao wanahusika kukagua mapato,uongozi na utungaji wa sheria sahihi kwa kusudi la kuwatumikia wananchi.

Bunge la Korea lina speaker mmoja na naibu wake. Wabunge wote wa bunge la Korea ukiondoa spika wanakuwa ni wanachama wa kamati mbalimbali za Bunge. Spika wa Bunge hujiuzulu kuwa mwanachama wa chuma chochote mpaka wakati wake utakapoisha spika anapoamua kujiuzulu au kustaafu hupendekeza mtu anayefikiri kuwa anafaa kuwa mrithi wake.
Bunge la Korea Hupiga kura zake kwa kutumia computa IPad zilizoko katika kitu cha kila mbunge na matokea huonyeshwa moja kwa moja katika Screen kubwa mbili zilizoko katika ukumbi wa Bunge hilo,
Bunge la Korea huwa na kazi kubwa muhimu ya kujenja taiga na kuhakikisha watu Wana furaha
Shughuli za Kibunge kwa ujumla ni
1. Kusoma muswada pendekezi
2. Kuuchambua mswada kwa kushirikiana na kamati husika
3. Kuchambua umuhimu wa muswada na kuupa maneno ya kisheria
4. Kufanya maamuzi
5. Kuuwasilisha Serikalini
6.Kuusimamia
Kwa ujumla utendaji wa Kibunge Duniani unafanana kwa kiwango fulani habari kwa Hisani ya Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.

Nje ya Ukumbi wa Bunge la Korea ya Kusini
Nikiwa na Muheshimiwa Spika wa Bunge la Korea ya Kusini
Wanafunzi wa Living Stone Seminary na walimu Tukiwa na Spika wa Bunge la Korea
 Ukumbi wa Bunge la Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge la Korea
 Rev. Innocent Kamote akiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge la Korea

Rev. Innocent Kamote akiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge la Korea
 Rev. Innocent Kamote akiwa ndani ya Maktaba ya Bunge la Korea
 Rev. Innocent Kamote akiwa ndani ya Maktaba ya Bunge la Korea
 Rev. Innocent Kamote akiwa ndani ya Maktaba ya Bunge la Korea
 Rev. Innocent Kamote akiwa ndani ya Maktaba ya Bunge la Korea
 Rev. Innocent Kamote akiwa ndani ya Maktaba ya Bunge la Korea
Rev. Innocent Kamote akiwa ndani ya Maktaba ya Bunge la Korea


KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA VITA VYA KOREA MJINI INCHEON

Utangulizi.

Nilipokuwa Korea hivi karibuni nilipatanafasi pamoja na wanafunzi wangu kutembelea Mji wa Incheon pale Korea ya kusini, pamoja na mambo mengine tulipata nafasi ya kutembelea makumbusho ya vita ya Korea Kaskazini na Korea Ya Kusini mahali hapa ni pazuri na pamejengwa ngome kubwa na ndani kuna makumbusho kuhusu vita hii ni vita ambayo ilikuwa mbaya na historia yake haiwezi kufutika na kizazi kilichopo Korea.

Mimi nilitakakujua historia ya vita hii na sababu zake
Vita ya Korea maarufu kama Korean war ilianza mwaka 1950 June 25, baadaya askari wapatao 75,000 wa Korea ya Kaskazini kuivamia Korea ya kusini na kupita mahali pajulikanapo kama 38 parallel mahali hapa palikuwa na mpaka katiya Korea ya Kaskazini na korea ya kusini, kihistoria taifa hili lilikuwa moja miaka ya zamani lakini liligawanywa kutokana na itikadi za kisiasa zilizokuwako Duniani kwa wakati huo siasa za mregowa kijamaa na mrengo wa kibepari ambao pia unajitambulisha kama mrengo wakidemokrasia na hivyo kuwa na Korea inayoungwa mkono na jumuiyaya Kisoviet na Korea inayoungwa mkono na jumuiya ya mataifa ya Magharibi uvamizi huu ulikuwa ni matokeo ya muda mrefu ya vita baridi kati ya mataifa ya magharibi yenye mrengowa Kidemokrasia na kibepari na mrengowa mataifa ya kimashariki yenyekufuata sera za kijamaa zilizokuwa zikiongozwa na Urusi.
Mwezi mmojatu baadaye Marekani iliingiza vikosivyake kulinda au kujibu uvamizi huodhidi ya Korea kaskazini wakiitetea Korea ya Kusini marabaada ya Marekani kuingilia kati mtazamowa vita hii ulibadilika na kuwa vita yenye mtazamo  wa kupigana na usoshalisti duniani jambo hili lilitia hamasa kwa nchi na mataifa kama Urusi na China namengineyo kuisaidia Korea kaskazini huku Uingereza, Ufaransa, na Marekani. wakiwa na Korea kusini jambo lililoleta picha mbaya na kusababisha kama kinachotokea kufananana vita vya tatu vya Dunia ilikuwa vita mbaya sana kutokea vita hii ilimalizika july mwaka 1953 nakua chamakovu makubwa sana yaliyoko mpaka leo askari wapatao milionitano walikufa katika vita hii mbaya na ndugu wengi kupoteza maisha na kupotea na kumbuka baadhi ya watu wakorea kaskazini na kusini walikuwa ni ndugu wa damu lakini mpaka leo madhara ya vita hii yamewagawa na kuwafanya wabaki na vita baridi hata leo huku mipaka yaoikilindwa na kamera maalumu kali na uzio waumeme na kila upande ukiwa napropaganda dhidiya upande mwingine.
Korea imegawanyika “Katika hali yoyote ile ubora waakili zetu Duniani nilazima uelekezwe katika kuiweka Dunia iwe na uwezo wa kuepuka vita yoyote mbaya kama hii” ~ Dean Acheson (1893~1971), Waziri wa mambo yanje wa Marekani wakati huo alisema kwa bahati mbaya kisiwa peninsula  hii imeangukia katika mikono ya wamarekani na wasovieti hali ilikuwa chini ya wajapani mpaka vita vya pili vya dunia baada ya 1945 peninsula  hii kaskazini ikawa upande wa Urusi na kusini ikawa upandewa Marekani.

Kama ilivyokuwa kwa vita ya pili ya Dunia na vita ya Vietnam vita vya Korea havikupewa kipumbele na vyombovya habarina hivyo kuvifanya visijuli kane sana. Peninsula  iligawanyika vipande viwili kusini kukitawaliwana Dikteta Rhee akiungwa mkono na Marekani1875~1965 na Kaskazini kukitawaliwa na Dikteta Kim ll Sung akiungwa mkono na majamaa waUrusi katika vita hii hakukuwa na mshindi bali wamarekani wanaweza kusema tu kuwa walifanikiwa kuzuia ujamaa usienee kusini na iliwagharimu Maisha na fedha nyingi sana kuijenga Korea kusini na kuifanikisha kuwa tajiri na tunaweza kusema wazi kuwa siri kuu ya maendeleo yataifa la Korea ya kusini nimisaada ya hali na mali isiyo na riba grand.
Eneo hili liligeuka kuwa sehemu muhimu ya vita baridi kati ya Ukomonist na Ubepari na hivyo ilipendekezwa kupewaulinzi katika eneo hilo General Douglas MacArthur alichaguliwa kuwa kiongozi waulinzi wa tishio la ukomonist katika ukanda wa Asia anakumbukwa kwa huhodari wake wa kuukomboa mji wa Seoul wakati wa vita vya Korea kupiti ajiji la Incheon  mahalipalipojengwa makumbusho ya vita vya Korea nilipatanafasi ya kupiga picha na picha ya General MacArthur. zaidi ya askari 40,000 wa Marekani walipoteza maisha katika vita mbaya ya Korea na zaidi ya 100,000 walijeruhiwa. Mpaka sasa kilawakati ziko propaganda zakutishiana kivita katiya Korea ya Kusinina Kaskazini, Korea Kaskazini wamejiendeleza katikau tengenezaji wa Mabomu ya nyuklia na makombora.huku kusini wakijiendeleza katika maswala kadhaa ya sayansi na teknolojia huku vikosi vya kijeshi vya Marekani vikiwa Korea kusini.
 Imani na maombi yangu ni kuwa siku mmoja huenda watamaliza tofautizao na kuwa taifa moja na kubwa na lenyenguvu Duniani.

Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini

 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini

 Rev. Innocent Kamote akiwa na Athor Chikoka  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 silaha zilizotumika wakati wa vita hiyo
 silaha zilizotumika wakati wa vita hiyo
 Picha ya general MacArthur

 Rev. Innocent Kamote akiwa  na Picha ya General MacArthur Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa na Picha ya General MacArthur  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa Sanamu za wapiganaji  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Sanamu za wapiganaji Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
 Ramani ya makumbusho ya vita
 silaha zilizotumika
 silaha zilizotumika
 Rev. Innocent Kamote akiwa  Makumbusho ya vita vya korea Jijini Incheon Korea ya Kusini
silaha na pistol zilizotumika nyakati hizo


Hakuna maoni: